Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1810 | 1811 | (Page 1812) | 1813 | 1814 | .... | 1897 | newer

  0 0

  WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema Taifa limepoteza kijana aliyekuwa msatari wa mbele kuwahamasisha vijana wajitambue wawe wazalendo kwa nchi yao na watambue fursa za maendeleo zilizopo na wasiwe walalamikaji.

  Ameyasema hayo leo (Jumatano, Februari 27, alipokwenda kuhani msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba kwa niaba ya Serikali, nyumbani kwa wazazi wa marehemu Mikocheni jijini Dar es Salaam.

  Waziri Mkuu amesema vijana nchini walikuwa na kiongozi aliyekuwa akiwaongoza kwa kuwafungua kimawazo na kuwaonesha fursa mbalimbali zitakazowawezesha kuwakwamua kifikra na kiuchumi ili waweze kujitegemea.

  Waziri Mkuu amesema msiba huo ni wa wote kwani marehemu amefanya kazi kubwa ya kushirikiana na Serikali kuhamasisha vijana kujitambua na kutambua fursa zilizpo na kuzifanyia kazi. “Ruge ametoa mchango mkubwa kwa Taifa

  Amesema marehemu Ruge katika kipindi cha uhai wake amefanya kazi kubwa kwa upande wa Serikali, kuanzia awamu ya nne hadi ya tano hususani katika suala la kuhamasisha vijana kujikwamua na kutokuwa wategemezi.

  Pia, Waziri Mkuu amesema historia yake inaeleza namna alivyozunguka nchi nzima na kukutana na makundi ya vijana mbalimbali na kuwaelimisha namna ya kutambua fursa zilizopo nchini huku akiwahamasisha wawe wazalendo.

  "Marehemu alikuwa akitoa hadi fedha zake binafsi kwa ajili ya kuwawezesha vijana hasa wale ambao hawakuwa na uwezo wa kiuchumi ili nao washiriki katika shughuli mbalimbali za ujasiriamali na hatimaye waondokane na utegemezi.”

  Kadhalika, Waziri Mkuu ametoa wito kwa wazazi, watoto wa marehemu pamoja na wananchi kwa ujumla waendelee kuwa na subira na watulivu katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao. 


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMATANO, FEBRUARI 27, 2019.
  WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza mbele ya waandishi wa habari mapema leo alipokwenda kuhani msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba kwa niaba ya Serikali, nyumbani kwa wazazi wa marehemu Mikocheni jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe akizungumza na Maafisa Utamaduni wa Mikoa na Halmashauri zote nchini (hawapo katika picha) katika Kikao Kazi cha 11 kilichoandaliwa na Wizara yake chenye lengo la kujadili changamoto na fursa zilizopo katika Sekta hiyo kinachoongozwa na Kauli Mbiu “Umoja Upendo na Kazi Asili ya Utamaduni wetu”Kinachofanyika leo na kesho Jijini Dodoma. Wa Kwanza Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi.Susan Mlawi na Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Bw.Boniface Kadili. 

  Na.Shamimu Nyaki -WHUSM 

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe amewaagiza Maafisa Utamaduni wa Mikoa na Halmashauri nchini kusimamia na kutekeleza Sera ya Utamaduni ya Mwaka 1997 kwakua ni ndio muongozo wa kukuza na kuendeleza Utamaduni wa Nchi yetu. 

  Mhe. Waziri ameyasema hayo leo Jijini Dodoma alipokuwa akifungua Kikao Kazi cha 11 cha Maafisa Utamaduni wa Mikoa na Halmashauri zote nchini kilichoandaliwa na Wizara yake ambapo amesema kuwa Kikao kazi hicho kitasaidia kuibua changamoto na kutafuta namna ya kuzikabili pamoja na kubuni fursa zilizopo katika Sekta hiyo. 
  Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi. Susan Mlawi akizungumza na Maafisa Utamaduni wa Mikoa na Halmashauri zote nchini (hawapo katika picha) katika Kikao Kazi cha 11 kilichoandaliwa na Wizara yake chenye lengo la kujadili changamoto na fursa zilizopo katika Sekta hiyo kinachoongozwa na Kauli Mbiu “Umoja Upendo na Kazi Asili ya Utamaduni wetu”Kinachofanyika leo na kesho Jijini Dodoma. 
  Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Boniface Kadili akizungumza katika Kikao Kazi cha 11 cha Maafisa Utamaduni chenye lengo la kujadili changamoto na fursa zilizopo katika Sekta hiyo kinachoongozwa na Kauli Mbiu “Umoja Upendo na Kazi Asili ya Utamaduni wetu”Kinachofanyika leo na kesho Jijini Dodoma. 

  “Naamini kikao kazi hiki kitatoka na maadhimio mazuri yanayoelezea namna bora ya kuondoa mmomonyoko wa maadili unaotokana na kudharau, kupuuza na kudidimiza mila na desturi za nchi yetu na kufuata tamaduni za nje zisizofaa.” Amesema Dkt Mwakyembe. 

  Aidha Mhe. Mwakyembe amewataka maafisa Utamaduni hao kutumia falsafa ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere inayosema, “Utamaduni ni kielelezo cha uhai na Utashi wa Taifa lolote lile, hivyo Taifa lisilo na Utamaduni ni Taifa mfu”. Hivyo amewataka Maafisa hao kutumia taaluma yao kuwahimiza Watanzania kujivunia Utamaduni wetu. 

  Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi. Susan Mlawi ameeleza kuwa kikao hicho kitakumbusha Maafisa Utamaduni kujadili mambo mbalimbali ya msingi, kubaini fursa pamoja na kuweka maazimio yatakayosaidia kuendeleza Utamaduni wa nchi yetu. 
  Baadhi ya Maaafisa Utamaduni wa Mikoa na Halmashauri zote Nchini wakiwa katika Kikao kazi cha 11 kilichoandaliwa na Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo chenye chenye lengo la kujadili changamoto na fursa zilizopo katika Sekta hiyo kinachoongozwa na Kauli Mbiu “Umoja Upendo na Kazi Asili ya Utamaduni wetu”Kinachofanyika leo na kesho Jijini Dodoma. 
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya Viongozi wa Wizara yake na Maafisa Utamaduni wa Mikoa na Halmashauri zote nchini baada ya kufungua Kikao Kazi cha 11 kilichoandaliwa na Wizara yake chenye lengo la kujadili changamoto na fursa zilizopo katika Sekta hiyo kinachoongozwa na Kauli Mbiu “Umoja Upendo na Kazi Asili ya Utamaduni wetu”Kinachofanyika leo na kesho Jijini Dodoma. 

  Kikao kazi hicho kinaongozwa na kauli mbiu isemayo “Umoja Upendo na Kazi Asili ya Utamaduni wetu” 

  Mbali na hayo Waziri, Dkt.Mwakyembe ametoa salamu za pole kwa Uongozi na Wafanyakazi wa Clouds Media Group, ndugu jamaa na marafiki kufuatia kifo cha aliyekuwa Muanzilishi na Mkurugenzi wa Uzalishaji Vipindi Clouds Media Group Bw. Ruge Mutahaba ambaye alifariki jana Nchini Afrika Kusini. 

  Katika hatua nyingine Mhe.Waziri Mwakyembe ameliagiza Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kushirikiana na Jeshi la Polisi nchini kumchukilia hatua za kinidhamu Msanii wa muziki wa kizazi kipya Godfrey Tumaini maarufu kama Dudu Baya kutokana na maneno aliyoyatoa ya kumdhihaki marehemu Ruge Mutahaba aliyekuwa Muanzilishi na Mkurugenzi wa Uzalishaji Vipindi Clouds Media Group ambaye alifariki jana Nchini Afrika Kusini

  0 0

  Waziri wa Elimu, Sanyansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako(kulia) na Waziri wa Elimu na Mafunzo wa Serikali ya Jamhuri ya Sudan Kusini, Mhe. Deng Deng Hoc Yai wakiweka saini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano katika Sekta ya Elimu hususan katika lugha ya Kiswahili jana jijini Dodoma. 
  Waziri wa Elimu, Sanyansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako(kulia) akifurahia wakati Waziri wa Elimu na Mafunzo wa Serikali ya Jamhuri ya Sudani Kusini, Mhe. Deng Deng Hoc Yai akionyesha hati ya mkataba wa makubaliano ya ushirikiano katika Sekta ya Elimu baina ya Tanzania na Sudan Kusini mara baada ya kuweka saini jana jijini Dodoma. (Picha na: Frank Shija – MAELEZO, Dodoma)
  Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiwasili katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Elimu jana kwa ajili ya kutiliana saini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano katika Sekta ya Elimu hususan katika Lugha ya Kiswahili na Waziri wa Elimu na Mafunzo wa Serikali ya Jamhuri ya Sudani Kusini, Mhe. Deng Deng Hoc Yai (kulia) jana jijini Dodoma. Kushoto ni Balozi wa Sudan Kusini nchini Tanzania, Mhe.Mariano Deng Ngor. 
  Waziri wa Elimu, Sanyansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako akizungumza wakati wa hafla ya kutiliana saini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano katika Sekta ya Elimu hususan katika lugha ya Kiswahili na Waziri wa Elimu na Mafunzo wa Serikali ya Jamhuri ya Sudani Kusini, Mhe. Deng Deng Hoc Yai (kushoto) jana jijini Dodoma. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Ave Maria Semakafu. 
  Waziri wa Elimu, Sanyansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako akisisitiza jambo wakati wa hafla ya kutiliana saini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano katika Sekta ya Elimu hususan katika lugha ya Kiswahili na Waziri wa Elimu na Mafunzo wa Serikali ya Jamhuri ya Sudani Kusini, Mhe. Deng Deng Hoc Yai (kushoto) jana jijini Dodoma. 
  Waziri wa Elimu na Mafunzo wa Serikali ya Jamhuri ya Sudan Kusini, Mhe. Deng Deng Hoc Yai wakati wa hafla ya kutiliana saini mkataba wa makubalina ya ushirikiano katika sekta ya elimu baina ya Tanzania na Sudan Kusini jana jijini Dodoma. Kushoto kwake ni Waziri wa Elimu, Sanyansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako 
  Balozi wa Sudan Kusini nchini Tanzania, Mhe.Mariano Deng Ngor akitoa neno la shukrani wakati wa hafla ya kutiliana saini mkataba wa makubalina ya ushirikiano katika sekta ya elimu baina ya Tanzania na Sudan Kusini jana jijini Dodoma. Kulia ni Waziri wa Elimu, Sanyansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako na Waziri wa Elimu na Mafunzo wa Serikali ya Jamhuri ya Sudan Kusini, Mhe. Deng Deng Hoc Yai(katikati).

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wakuu wa Idara za Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke wakati alipotembelea hospitali hiyo, Februari 27, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwafariji wanawake waliolazwa kwenye wodi ya wazazi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke wakati alipotembelea hospitali hiyo, Februari 27, 2019. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa amempakata mototo Natasha Chriswell wakati alipotembelea Kliniki ya Methadone katika hospitali ya Mwananyamala wilayani Kinondoni, Februari 27, 2019. Kulia ni mama wa mtoto huyo, Zaynab Hamisi ambaye miaka saba iliyopita alikuwa ni muathirika wa dawa za kulevya na amepatiwa matibabu katika Kiliniki hiyo,  hivi sasa ni mzima, ameolewa na amebahatika kupata mtoto huyo.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wakuu wa Idara za Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke wakati alipotembelea hospitali hiyo, Februari 27, 2019.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa amempakata mototo Natasha Chriswell wakati alipotembelea Kliniki ya Methadone katika hospitali ya Mwananyamala wilayani Kinondoni, Februari 27, 2019. Kulia ni mama wa mtoto huyo, Zaynab Hamisi ambaye miaka saba iliyopita alikuwa ni muathirika wa dawa za kulevya na amepatiwa matibabu katika Kiliniki hiyo,  hivi sasa ni mzima, ameolewa na amebahatika kupata mtooto huyo. Wa tatu kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Dar es alaam, Paul Makonda na wa pili kulia ni Mkuu wa kitengo cha Methadone hospitalini hapo, Dkt. Sosthenes Hongo.
   
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapa pole wagonjwa wakati alipotembelea wodi ya watoto katika Hospitali ya Mwayamala wilayani Kinondoni, Februari 27, 2019.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu


  *Wananchi waipongeza kwa kuwa umeimarisha utoaji wa huduma za afya

  WANANCHI wameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli kwa kuwabana watumishi wa umma, kwa sababu uamuzi huo umezaa matunda na sasa hali ya utoaji wa huduma katika maeneo mbalimbali nchini yakiwemo ya hospitali yameimarika.

  Kauli hiyo imetolewa leo (Jumatano, Februari 27, 2019) na wagonjwa waliolazwa katika wodi ya wazazi kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa hospitali hapo.

  “Huduma zimeimarishwa dawa tunapata, hakuna lugha chafu wala kuombwa rushwa. Tunahudumiwa vizuri na kuna wakati hadi tunabembelezwa kunywa dawa mambo ambayo hapo nyuma hayakuwepo, hivyo tunaishikuru Serikali.”

  Mmoja wa wagonjwa hao ambaye amelazwa katika wodi ya wazazi hospitalini hapo baada ya kujifungua, Mwajuma Mohammed amesema baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kuingia madarakani na kuwabana watumishi wa umma sasa kuna mabadiliko makubwa sana ya kiutendaji.

  Amesema zamani baadhi ya wauguzi hususani wanaofanyakazi kwenye wodi ya wazazi hawakuwa na lugha nzuri walikuwa wakiwatukana na kuwakashifu jambo ambalo kwa sasa halipo, kwani wakifika wapokelewa vizuri.

  Mama mwingine aliyelazwa kwenye wodi hiyo, Crista Moyo amemuomba Waziri Mkuu kuisadia hospitali hiyo kwa kuiongezea watumishi kwa kuwa walipo ni wachache ukilinganisha na idadi ya wagonjwa wanaofika hospitalini hapo kila siku.

  Crista ameishauri Serikali ikiwezekana iajiri hata watu wasiokuwa na taaluma ya udaktari au uuguzi ili wakafanyekazi ambazo hazihitaji ujuzi kama za kuwasaidia wagojwa kutoka eneo moja kwenda lingine.

  Kwa upande wake, Waziri Mkuu amezishauri Halmashauri jijini Dar es Salaam zihakikishe zinaendelea kuimarisha vituo vya afya na kuongeza vingine ili utoaji kupunguza msongamano wa wagonjwa kwenye hospitali za rufaa.Pia ameshauri ianzishwe miradi ya ujenzi wa nyumba za watumishi katika hospitali hizo kwa lengo ya kuwezesha utoaji wa huduma mbalimbali zikiwemo za dharura kwa wakati.

  “Rais Dkt. Magufuli anataka wananchi wapate huduma za afya karibu na makazi yao ili kuwaondolea adha ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma hizo. Ndio maana tunajenga vituo vya afya vilivyokamilika vinavyotoa huduma zote muhimu kama maabara, upasuaji na mama na mtoto.”

  Waziri Mkuu amesema lengo la ziara hiyo ni kukagua utoaji wa huduma za afya zinazotolewa katika hospitali hizo na kubaini kama kuna changamoto ili Serikali iweze kuzitambua na kuzitafutia ufumbuzi.“Tumesikia changamoto zinazowakabili madaktari, tumezichukua na tutazifanyia kazi ikiwepo ya upungufu wa watumishi mbalimbali kama madaktari na wauguzi ili kuboresha zaidi utoaji wa huduma kwa wananchi.”

  Waziri Mkuu amesema dhamira ya dhati ya Serikali kwao ni ya kuwatumikia wananchi wote bila ya ubaguzi wa aina yoyote, hivyo waendelee kuwa wazalendo na washirikiane na Serikali yao. Wafanye kazi kwa bidii.Naye,Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Dkt. Amaani Malima amesema hospitali hiyo inahudumia wagonjwa wa nje 1,800 hadi 2,000 kwa siku na wagonjwa wa ndani 250 hadi 300. Wagonjwa hao watoka wilaya mbalimbali.

  Dkt. Malima amesema hospitali hiyo ina jumla ya watumishi 439 kati yao madaktari bingwa ni 16, madaktari 76 na wauguzi 209 na watumishi wengine 138. “Idadi hii ni ndogo kulingana na mahitaji ya hospitali kwani tuna upungufu wa watumishi 278 sawa na asilimia 39.”

  Akizungumzia hali ya upatikanaji wa dawa muhimu kwenye hospitali hiyo, Dkt. Malima amesema kwa kipindi cha Januari upatikanaji ulikuwa wa kuridhisha kwa asilimia 85 ya kiasi cha dawa na vifaa tiba vilivyohitajika.

  Awali, Waziri Mkuu alitembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala ambapo alikagua mradi wa ujenzi wa jengo la kuhudumia wagonjwa mashuhuri ambalo lilianza tangu mwaka 2014 na bado halijakamilika.

  Hivyo, ameishauri Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kuangalia namna ya kuweza kusaidia ujenzi wa jengo hilo ili mradi huo uweze kukamilika na hatimaye huduma zilizokusudiwa kutolewa katika jengo ziweze kufanyika.Pia, Waziri Mkuu amewataka Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dkt. Daniel Nkungu na Kiongozi wa Wauguzi, Wambura wahakikishe wanaimarisha ushirikiano wao na hata wanapotoa maagizo kwa wasaidizi wao wawe wanataarifiana.

  Kwa upande wa watumishi wanaofanya kazi katika idara za maabara amewataka wawe wanawahi kutoa huduma kwa sababu kuna malalamiko ya ucheleweshwaji wa huduma katika eneo hilo.

  Kadhalika, Waziri Mkuu amewataka watumishi wanaofanya kazi katika kitengo cha radiolojia kwenye hospitali za Rufaa za Mkoa za Mwananyamala na Temeke jijini Dar es Salaam waache urasimu na wafanye kazi kwa kuzingatia maadili ya taaluma zao.

  0 0

  Mkuu wa Huduma za T- PESA, Moses Alponce (wa pili kushoto) pamoja na Naibu Mkurugenzi wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), Bi Khadija Shamte (wa kwanza kulia) wakisaini mkataba wa makubaliano kibiashara leo mjini Zanzibar kati ya pande zote mbili. 
  Mkuu wa Huduma za T- PESA, Moses Alponce (wa pili kushoto) pamoja na Naibu Mkurugenzi wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), Bi Khadija Shamte (wa pili kulia) wakibadilishana nakala za mkataba wa makubaliano kibiashara leo mjini Zanzibar mara baada ya kutiliana saini. 
  Mkuu wa Huduma za T- PESA, Moses Alponce (wa pili kushoto) pamoja na Naibu Mkurugenzi wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), Bi Khadija Shamte (wa pili kulia) wakionesha nakala za mkataba wa makubaliano kufanya kazi kwa ushirikiano kibiashara leo mjini Zanzibar mara baada ya kutiliana saini. 
  Mkuu wa Huduma za T- PESA, Moses Alponce (kushoto) akizungumza kwenye hafla ya kutiliana saini makubaliano ya kufanya kazi kiushirikiano kibiashara. Kulia ni Naibu Mkurugenzi wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), Bi Khadija Shamte akiwa katika hafla hiyo. 
  Picha ya pamoja kati ya wafanyakazi wa PBZ na TTCL (T PESA) walioshiriki katika hafla ya kuingia makubaliano hayo ya ushirikiano kibiashara. 


  SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kupitia kampuni yake tanzu ya T-PESA imesaini makubaliano ya kufanya kazi na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), ambapo mawakala wa T-PESA watahudumiwa na benki hiyo.

  Makubaliano hayo ya ushirikiano kibiashara kati ya PBZ na T-PESA yamefanyika leo mjini Zanzibar, ambapo Mkuu wa Huduma za T- PESA, Moses Alponce amesema yatawawezesha mawakala wao kupata huduma za kifedha kupitia PBZ.

  Alisema T-PESA wanajivunia kufanikiwa katika ushirikiano huo kibiashara kwani utaiwezesha huduma zao kuenea kwa kasi zaidi, hasa ukizinga kuwa PBZ ni taasisi kubwa ya kifedha inayotoa huduma Zanzibar, Pemba na hata Tanzania Bara.

  Miongoni mwa maeneo ambayo yamo katika mkataba wa ushirikiano huo kibiashara, mbali na PBZ kutoa huduma kwa mawakala wa T-PESA ya kutoa na kupokea fedha pia itakuwa ikitumia sehemu ya huduma za TTCL kama huduma za sauti na vifurushi, pamoja na huduma za simu.

  Kwa upande wake, Naibu Mkurugenzi wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), Bi Khadija Shamte alisema benki hiyo inamtawanyiko mkubwa wa matawi yake kuanzia mjini na vijijini huku wakiwa na uzoefu mkubwa katika kutoa huduma za fedha kupitia simu za viganjani.Kupitia mtawanyiko huo mkubwa kihuduma, tunapenda kuwahakikishia ushirikiano mzuri katika makubaliano hayo na jamii kwa ujumla watanufaika na kufurahia huduma zetu.

  Aidha aliongeza kuwa Benki ya PBZ ni moja ya taasisi za fedha kongwe nchini Tanzania, ambayo inamilikiwa kwa asilimia 100 na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ). PBZ inalimiliki soko kwa takribani asilimia 50 huku ikiwa na wateja zaidi ya milioni 1.0.

  0 0

  Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Vifaa vya Kielekroniki vya Wateja wa Jumia, Sandeep Narayanan, Makamu Mkuu wa Rais wa Jumia, Bw. Romain Christodoulou, Makamu Mkuu wa Rais wa kampuni ya Xiaomi, Bw. Wang Xiang, pamoja na Makamu wa Rais wa Xiaomi, Wang Lingming wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuingia makubaliano katika Kongomano Kuu la Simu Duniani lililofanyika jijini Barcelona, Hispania mnamo Februari 27, 2019.
   Kushoto ni Makamu Mkuu wa Rais wa Jumia, Bw. Romain Christodoulou pamoja na Bw. Wang Xiang (kulia), Makamu Mkuu wa Rais wa kampuni ya Xiaomi wakiweka sahihi wakati wa makubaliano ya biashara katika Kongomano Kuu la Simu Duniani lililofanyika jijini Barcelona, Hispania mnamo Februari 27, 2019.  · Ushirikiano huu unaifanya Xiaomi kuingia rasmi kwenye soko la mtandaoni barani Afrika kupitia Jumia, na kuwapatia fursa ya kipekee mamilioni ya wateja kuzifikia bidhaa za Xiaomi.

  kampuni inayoongoza barani Afrika kwa kuuza bidhaa mtandaoni, imesaini mkataba muhimu wa ushirikiano wa kibiashara na kampuni inayoongoza kiteknolojia ya Xiaomi katika Kongamano Kuu la Simu Duniani (the Mobile World Congress) jijini Barcelona nchini Hispania, na kuwapatia fursa ya kipekee mamilioni ya Waafrika kuzifikia kwa urahisi bidhaa za Xiaomi.

  Kupitia ushirikiano huu, Jumia itafungua duka maalum la Mi mtandaoni kwake na kuipatia Xiaomi fursa ya kuwafikia mamilioni ya wateja walioko mtandaoni katika nchi takribani 14 barani kote, wakati huo huo Jumia itaitambulisha rasmi simu aina ya Redmi Go (1GB + 8GB) mahsusi kwa Afrika na bidhaa nyinginezo nyingi ndani ya mwaka huu. Ushirikiano huu utapewa nguvu na juhudi za pamoja baina ya pande mbili za shughuli za kimasoko kwa mwaka wote wa 2019, kwa kutumia uwezo wa Jumia kwa kidigitali pamoja na wa kimasoko wa Xiaomi, ikijumuisha jamii ya mashabiki wa Mi. Hii ni hatua ya kwanza muhimu yenye kutia matumaini katika ushirikiano wa karibu baina ya makampuni haya mawili kwa miaka mingi ijayo.

  “Ushirikiano huu ni muhimu sana kwetu, kwa kuwa ni dhahiri utakuza matumizi ya simu janja Afrika na kusaidia kuenea kwa manunuzi ya njia ya mtandaoni. Jumia na Xiaomi zote zina vinasaba sawa vya mtandao wa intaneti hivyo basi zitakuwa na kusudio moja: kutoa simu za kisasa zenye ubora wa hali ya juu na gharama nafuu huku ikiwapatia wateja namna ya kipekee ya kufanya manunuzi. Hii itazinufaisha kampuni zote mbili na zaidi ni wateja wote barani Afrika,” amesema Afisa Mtendaji Mkuu wa Jumia Tanzania, Bw. Zadok Prescott, akielezea juu ya ushirikiano huo.

  “Tunaamini kwenye kufanya kazi na makampuni ambayo yana maadili sawa nasi na tunayofuraha kushirikiana na Jumia kuwafikia mashabiki wengi zaidi wa Mi Afrika nzima,” amesema Wang Xiang, Makamu Mkuu wa Rais wa Xiaomi. “Mfumo wa kuuza bidhaa kwa njia ya mtandaoni ni sehemu ya Xiaomi na tunaamini ya kwamba kufanya kazi na Jumia kutatusaidia kuleta ubunifu kwa kila mtu barani Afrika.” 

  Afrika imeshuhudia kukua kwa kuingia bidhaa za kiwango cha gharama nafuu kutoka kwa makampuni ambayo yamejikita zaidi katika bei hususani kutokea China, kitu pekee ambacho ni muhimu katika kukuza matumizi ya simu za kisasa barani. Takwimu zinaonyesha kuwa ueneaji

  wa simu za kisasa Afrika ulikuwa 36% kwa mwaka 2018, huku idadi hiyo inatarajiwa kufikia 66% kufikia mwaka 2025.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais Mtendaji Mwandamizi wa Shirika la Kimataifa la Ushirikiano la Japan (JICA) Bw. Kazuhiko Koshikawa (wa tatu Kushoto) na ujumbe wake walipokutana  Ikulu jijini Dar es salaa leo Februari 28, 2019. Wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Damas Ndumbaro.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpa zawadi ya picha ya kuchora ya wanyama wakuu watano (Big Five)  Makamu wa Rais Mtendaji Mwandamizi wa Shirika la Kimataifa la Ushirikiano la Japan (JICA) Bw. Kazuhiko Koshikawa alipokutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaa leo Februari 28, 2019. Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Damas Ndumbaro.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpa zawadi ya kinyago ja UJAMAA  Makamu wa Rais Mtendaji Mwandamizi wa Shirika la Kimataifa la Ushirikiano la Japan (JICA) Bw. Kazuhiko Koshikawa alipokutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaa leo Februari 28, 2019. Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Damas Ndumbaro.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na  Makamu wa Rais Mtendaji Mwandamizi wa Shirika la Kimataifa la Ushirikiano la Japan (JICA) Bw. Kazuhiko Koshikawa (wa tatu Kushoto) na ujumbe wake baada ya kukukutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaa leo Februari 28, 2019. Wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Damas Ndumbaro.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na Makamu wa Rais Mtendaji Mwandamizi wa Shirika la Kimataifa la Ushirikiano la Japan (JICA) Bw. Kazuhiko Koshikawa (wa tatu Kushoto) na ujumbe wake baada ya kukukutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaa leo Februari 28, 2019. Wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Damas Ndumbaro.
  PICHA NA IKULU

  0 0


  Washindi hao Enstern Ngao (wa pili kushoto), pamoja na Simon Chacha (wa pili kulia) wakikabidhiwa mfano wa tiketi zao za ndege kwenda na kurudi Dubai baada ya kujishindia bahati nasibu ya Benki ya NMB iliyojulikana kama MASTABATA hivi karibuni. Wanao wakabidhi wa kwanza kulia ni Philbert Casmir na Manfredy Kayala (kushoto) maofisa NMB kutoka kitengo cha huduma za kadi.
  Meneja Huduma za Kadi wa Benki ya NMB, Bw. Manfredy Kayala (katikati) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) kabla ya kuwakabidhi tiketi hizo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Simon Chacha (kushoto) na Mfamasia wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Enstern Ngao (kulia) baada ya kujishindia bahati nasibu ya MASTABATA iliyokuwa inaendeshwa na Benki ya NMB hivi karibuni.
  Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Simon Chacha (katikati) akifurahia tiketi yake mara baada ya kukabidhiwa. 
  Mfamasia wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Enstern Ngao (katikati), akikabidhiwa mfano wa tiketi ya ndege ya kwenda na kurudi Dubai baada ya kujishindia bahati nasibu ya Benki ya NMB ya MASTA BATA hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Wanao mkabidhi kulia ni Philbert Casmir na Manfredy Kayala maofisa wa NMB kitengo cha huduma za kadi.
  Meneja Huduma za Kadi wa Benki ya NMB, Bw. Philbert Casmir (kulia) akikabidhiwa mfano wa tiketi ya ndege ya kwenda na kurudi Dubai Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Simon Chacha (kushoto) baada ya kujishindia bahati nasibu ya MASTABATA iliyokuwa inaendeshwa na Benki ya NMB hivi karibuni. 


  0 0

  Nahodha wa Kanda ya Magereza Sajini Tausi Abdul akipambana na Private Ester Lisu wa Ngome wakati wa Mchezo wao katika Michauano ya BAMMATA kuwania nafasi ya pili katika Mchezo huo Ngome ilishinda Magereza vikapu 68 kwa 60 . Picha na Luteni Selemani Semunyu.

  Mchezaji wa Kanda ya Magereza Sajini Mary Kimiti akipambana na Private Ester Lisu wa Ngome wakati wa Mchezo wao katika Michauano ya BAMMATA kuwania nafasi ya pili katika Mchezo huo Ngome ilishinda Magereza vikapu 68 kwa 60 . Picha na Luteni Selemani Semunyu.


  Wachezaji wa Mpira wa Wavu kutoka Magereza na JKT wakichuana wakatika wa Michuano ya Majeshi BAMMATA katika Mchezo huo Magereza walishinda Seti tatu kwa moja Picha na Luteni Selemani Sem unyu.

  …………………………………………………………………………….

  Na Luteni Selemani Semunyu

  Mashindano ya Majeshi Tanzania BAMMATA yameendelea kushika kasi huku timu ya Soka ya JKT ikiaga mashindano hayo kwa mwaka 2019 kwa kishindo baada ya kuifunga Zimamoto magoli 10 kwa Moja.

  Matokeo hayo yamejitokeza katika mchezo wa kufunga Dimba uliochezwa katika Dimba la Uhuru licha ya Timu hizo zote hazikuwa na nafasi ya kuingia katika Hatua ya Nusu Fainali.

  Katika Soka sasa Mchezo kati ya Ngome na Magereza unaotarajiwa kuchezwa kesho katika Dimba la Uhuru utaamua nani wa kucheza na Polisi na nani kucheza na SMZ katika hatua ya Nusu Fainali.

  Katika Ridha atika mchezo mwingine Mpira wa Kikapu Wanawake mchezo uliokuwa ukiamua mcshindi wa Pili Ngome wameibuka na Ushindi kwa Vikapu 68 kwa 60.

  Katika Mpira wa Wavu wanawake Magereza wameifunga JKT kwa seti tatu kwa Moja huku kwa Upande wa Wanaume Ngome wameifunga Polisi Seti tatu bila.

  Katika Shabaha pistor wanawake mshindi wa Kwanza Pc Pili Mkama wa pili PC Salvina Mhiche na PC Bertha Jonathan wote wa Polisi.

  Kwa Upande wa Wanaume Sajini Kenya Kiula wa Polisi wa pili ni Sajini Jumanne Wambura wa Ngome na watatu ni PC Joseph Mwenda Polisi.

  Kwa Upande wa Rifle Wanawake ni Private Elizabeth Kibondo Ngome wa pili ni Mteule Daraja la Pili Sophia Ramadhani wa Ngome na PC Sharifa Kibwana Ally wa Polisi huku kwenye Riadha relay wanaume Mita 400 Timu ya Ngome imeibuka na Ushindi.

  0 0

  *Mwenyewe asema ametafakari na kuamua kurudi nyumbani

  *Rais Dk. Magufuli atoa neno, CCM wachekelea kila kona


  Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

  WAZIRI Mkuu mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne Edward Lowassa ametangaza rasmi kurudi Chama Cha Mapinduzi(CCM) kuanzia leo Machi 1,2019. 
  Lowassa aliondoka CCM na kwenda upinzani katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) wakati wa mchakato wa kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.Aliondoka CCM na kwenda upinzani baada ya jina lake kukatwa katika kugombea urais kupitia Chama hicho.

  Hivyo  alipata ridhaa ya kugombea nafasi ya Urais kupitia Chadema waliokuwa wameunganisha nguvu na vyama vingine vinne vya siasa vilivyokuwa vimeunda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

  Akiwa upinzani Lowassa aliteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema lakini kuna kipindi aliamua kwenda Ikulu kufanya mazungumzo na Rais Dk.Magufuli ambapo baada ya kukutana na Rais alisema amevutiwa na utendaji kazi wake na anampongeza.

  Akizungumza leo katika Ofisi za ndogo za CCM zilizopo Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam,Lowassa hakuwa na maneno mengi ya kueleza zaidi ya kuwaambia Watanzania kuwa ameamua kurudi nyumbani (CCM).

  "Nimetafakari na sasa nimeamua kurudi nyumbani CCM ambako sehemu kubwa ya maisha yangu nimekuwa huko,"amesema Lowassa huku mamia ya wananchi wakiwamo wanachama na wapenzi wa CCM walikuwa wanamshangilia.

  Wakati Lowassa anatangaza kurejea CCM alikuwa amesikindikizwa na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Igunga ambaye pia aliwahi kuwa Mtunza wa fedha wa CCM Rostam Aziz.

  Akizungumza baada ya Lowassa kurudi CCM, Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Magufuli amesema wamempokea Lowassa na katika kuthibitisha hilo waliona ni vema uamuzi wake akautangazia Ofisi za CCM Lumumba kama sehemu ya uthibitisho.

  "Kama ambavyo amezungumza kwa kifupi mwenye Mzee Lowassa kwamba amerudi nyumbani ambako ni huku CCM, tumempokea.Amekuja kutangazia hapa Lumumba kama sehemu ya kutoa shuhuda.

  "Kwa upande wetu tumekaa, tumefakari na kujiridhisha Lowassa amekaa kwenye Chama kwa muda mrefu na kwa bahati mbaya zilizojotokeza aliamua kwenda upinanzani.Tumemsikiliza mawazo yake kwamba amekaaa kwenye Chama Cha Mapinduzi sehemu kubwa ya maisha yake na kwamba kutokana na sababu ambazo amezieleza aliamua kwenda upinzani na leo hii amerudi nyumbani,"amesema Rais Magufuli.

  Hata hivyo kabla ya Rais Magufuli kuzungumza aliamua kuwatania watu waliokuwa wamejitokeza Lumumba na kuwaambia imekuaje wako hapo au wanamaono na hivyo walijua kitakachotokea.

  Wakati huo huo Katibu Mkuu wa CCM Dk.Bashiru Ally amesema Lowassa amefikia uamuzi wa busara kwa kurudi nyumbani kwa ajili ya kushirikiana katika kuleta maendeleo ya wananchi wote.

  "Amerudi nyumbani, kwa hiyo tunaanza kazi ya kujenga Taifa letu na kujenga utu wetu, Lowassa ni kiongozi ambaye ametoa mchango mkubwa katika nchi yetu.Kwa niaba ya Mwenyekiti wa Chama chetu tumepanga kumpokea na yupo tayari kushirikiana nasi kuwatumikia wananchi,"amesema Dk.Bashiru.

  Hata hivyo uamuzi  huo wa Lowassa umeonekana kuwakosha wana-CCM kwani baadhi yao wameonesha kufurahia uamuzi huo.


  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa heshima zake za mwisho kwa Marehemu Ruge Mutahaba alipoongoza maelfu ya waombolezaji kuuaga mwili wa marehemu ambaye aliyekuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi wa Clouds Entertainment kwenye hafla iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumamosi March 2, 2019
   Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa heshima zao  za mwisho kwa Marehemu Ruge Mutahaba  kwenye hafla ya kuuaga mwili wa marehemu ambaye aliyekuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi wa Clouds Entertainment  katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumamosi March 2, 2019
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa mkono wa pole kwa ndugu na familia ya Marehemu Ruge Mutahaba alipoongoza maelfu ya waombolezaji kuuaga mwili wa marehemu aliyekuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi wa Clouds Entertainment kwenye hafla iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumamosi March 2, 2019

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa pole kwa baadhi wananchi waliofikika kutoa heshima zao kwa Marehemu Ruge Mutahaba alipoongoza maelfu ya waombolezaji kuuaga mwili wa marehemu aliyekuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi wa Clouds Entertainment kwenye hafla iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumamosi March 2, 2019
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi wengine alipoongoza maelfu ya waombolezaji kuuaga mwili wa marehemu ambaye aliyekuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi wa Clouds Entertainment kwenye hafla iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumamosi March 2, 2019  
  : Sehemu ya waombolezaji waliofika kuuaga mwili wa marehemu ambaye aliyekuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi wa Clouds Entertainment kwenye hafla iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumamosi March 2, 2019 .

  0 0

  Na Maryam Kidiko  - Maelezo.                                   
  Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda Hassan  Khamis Hafidh amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itachukuwa hatuwa kali kwa Mfanyabiashara yoyote atakaeingiza bidhaa isiyokuwa na kiwango kwa ajili ya matumizi ya wananchi.
   Aliyasema hayo Bandari ya Malindi Zanzibar alipofika kuangalia zoezi la kuhamisha tani 520 za sukari kwenda kuangamizwa kwenye mashimo ya mchango katika kijiji cha Zingwezingwe baada ya kugundulika kukosa kiwango kwa matumizi ya binaadamu.
  Alisema kuwa Serikali ipo makini kulinda afya za Wananchi wake hivyo haitakubali kuingizwa bidhaa yoyote isiyofaa kwa matumizi ya wananchi  ili kuwaepusha na maradhi.
  Aidha alisema ulinzi mkali wa vikosi vya ulinzi na usalama umeandaliwa kwa ajili ya kusimamia sukari hiyo ili kuhakikisha hakuna mtu atakaefanya mbinu ya kuipata mpaka zoezi zima la kuiangamiza limalizike.
  Aliwataka Wafanyabiashara kuendesha biashara zao kwa njia za halali na kuacha tabia ya kununua bidhaa za gharama nafuu bila ya kuangali ubora wake kwa lengo la kutafuta faida kubwa.
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wakala wa Chakula na Dawa Dk. Khamis Ali Omar alisema Makontena 20 ya sukari isiyo na kiwango yenye uzito wa Tani 520 ya Kampuni ya Rashid Ali Trader yaliingizwa Zanzibar mwaka uliopita kwa awamu mbili na alipewa tahadhari kuhusu tatizo la sukari hiyo alipoingiza kwa mara ya kwanza lakini aliendelea kuiingiza.
  Alisema baada ya sukari hiyo kufanyiwa uchunguzi ilionekana haina kiwango na kuchukuwa hatua za kisheria ili isiweze kufika kwa wananchi kwa matumizi mbali mbali.Alisema baada ya kugundulika kasoro hiyo, mmilikiwa huyo Rashid Ali  alishauriwa kuirejesha ilikonunua ama kuiingamiza lakini mashauri yote mawili aliyakataa.
  Katika siku ya kwanza ya zoezi la kuangamiza sukari hiyo katika mashimo ya mchanga ya Zingwezingwe makontena matatu kati ya 20 yaliharibiwa chini ya ulinzi mkali wa vikosi vya ulinzi na usalama
  Kwa Upande wake Mrakibu Muandamizi wa Jeshi la Polisi Khamis Ramadhan alisema zoezi la kusafirisha sukari hiyo kutoka Bandari ya Malindi na kufika katika sehemu ya kuangamizwa limeenda vizuri na hakuna tatizo lolote lililojitokeza hadi lilipomalizika kwa siku ya kwanza.
  Alisema zoezi hilo lililoongozwa na maafisa wa Bodi ya Chakula na Dawa Zanzibar limeshirikisha Vikosi vya Ulinzi na Usalama na wafanyakazi wa kitengo cha Mazingira Zanzibar.
   Wafanyakazi wa Bodi ya Chakula na Dawa wakimwaga sukari katika mashimo ya mchanga ya Zingwezingwe Wilaya ya Kaskazini B wakiwa katika zoezi la kuiangamiza sukari   tani 520 baada ya kugundulika kukosa kiwango kwa matumizi ya binaadamu.     iliyokosa kiwango kwa matumizi ya binadamu. 
   Gari aina ya kijiko ikiangamiza sukari katika mashimo ya mchanga ya Zingwezingwe Wilaya Kaskazini B baada ya kugundulika kukosa kiwango kwa matumizi ya wananchi.
   Gari zikiwa zimepakia sehemu ya tani 520 za sukari bandarini Malindi zikisubiri kupelekwa mashimo ya mchanga Zingwezingwe, Wilaya Kaskazini B, kwa ajili ya kuangamizwa baada ya kugundulika kukosa kiwango kwa matumizi ya wananchi.
   Shehena ya sukari ikiwa imemwagwa katika mashimo ya mchanga ya Zingwezingwe Wilaya Kaskazini B ikisubiri kuangamizwa baada ya kukosa kiwango kwa matumizi ya wananchi.
   Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Chakula na Dawa Zanzibar Dk. Khamis Ali akizungumza na waandishi wa habari kwenye mashimo ya mchanga Zingwezingwe wakati wa kuangamiza sehemu ya tani 520 za sukari iliyoingizwa nchini ikiwa haina kiwango kwa matumizi ya wananchi.PICHA NA RAMADHANI ALI MAELEZO ZANZIBAR.

  0 0

   Askofu Jimbo Katoliki la Musoma Mhashamu Michael Msongazila (kulia) akimweleza jambo Mkuu wa  Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika Siku ya maombi ya Dunia yaliyofanyika Machi Mosi, 2019 katika Viwanja vya Parokia ya Yohana Mbatizaji Nyamiongo Musoma kwa kujumuisha wanawake wa madhehebu ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania(CCT) na Wanawake WaKatoliki Tanzania(WAWATA)  .
   Mkuu wa  Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akiimba pamoja na Kwaya ya Upendo kutoka Kanisa la Anglikana Musoma katika Siku ya maombi ya Dunia yaliyofanyika Machi Mosi, 2019 katika Viwanja vya Parokia ya Yohana Mbatizaji Nyamiongo Musoma kwa kujumuisha wanawake wa madhehebu ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania(CCT) na Wanawake WaKatoliki Tanzania(WAWATA)  . 
   Mkuu wa  Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) na Askofu Jimbo Katoliki la Musoma Mhashamu Michael Msongazila wakifurahia jambo katika Siku ya maombi ya Dunia yaliyofanyika katika Viwanja vya Parokia ya Yohana Mbatizaji Nyamiongo Musoma kwa kujumuisha wanawake wa madhehebu ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania(CCT) na Wanawake WaKatoliki Tanzania(WAWATA)  , Machi Mosi, 2019.
   Kwaya kutoka Kanisa Katoliki Parokia ya Yohana Mbatizaji Nyamiongo Musoma ikiimba katika ibada ya siku ya maombi ya Dunia yaliyofanyika katika Viwanja vya Parokia ya Yohana Mbatizaji Nyamiongo Musoma kwa kujumuisha wanawake wa madhehebu ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania(CCT) na Wanawake Wakatoliki Tanzania(WAWATA)  , Machi Mosi, 2019.
   Mkuu wa  Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka( wa pili kushoto), viongozi wa Kanisa na baadhi ya viongozi wa wanawake wakiwa  ibada ya siku ya maombi ya Dunia yaliyofanyika Machi Mosi, 2019 katika Viwanja vya Parokia ya Yohana Mbatizaji Nyamiongo Musoma na  kujumuisha wanawake wa madhehebu ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania(CCT) na Wanawake Wakatoliki Tanzania(WAWATA) .
   Baadhi ya wanawake wa madhehebu ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania(CCT) na Wanawake Wakatoliki Tanzania(WAWATA)wakiwa katika ibada ya siku ya maombi ya Dunia yaliyofanyika Machi Mosi katika Viwanja vya Parokia ya Yohana Mbatizaji Nyamiongo Musoma.

  Na Stella Kalinga, Mara.

  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa wito kwa wanawake, kuwa mstari wa mbele kuhimiza jamii juu ya umuhimu wa kuwasomesha watoto, ili kuondokana mila potofu  zilizopitwa na wakati, ukiwemo ubaguzi wa kijinsia na mfumo dume.

  Mtaka ametoa wito huo, wakati wa siku ya maombi ya Dunia yaliyofanyika Nyamiongo  Manispaa ya Musoma Mkoani Mara ambako alikuwa mgeni rasmi, ambayo yaliwahusisha wanawake kutoka katika madhehebu ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania(CCT) na Wanawake Wakatoliki Tanzania(WAWATA).

  Amesema suluhisho la mila potofu zilizopitwa na wakati kama mfumo dume, ubaguzi wa kijinsia na kuona watoto wa kiume ni bora kuliko wa kike ni kuwasomesha watoto wote pasipo kujali kuwa ni wa kike au wa kiume.
  “Ukisomesha watoto wako vizuri wakafanikiwa kwenye hiyo nyumba hakuna atakayesema yeye ni bora zaidi ya mwenziye, hakuna atakayesema mimi ndiye mwanaume kwenye hii nyumba na huyu ni  mwanamke, somesheni watoto hayo mambo yote yaliyopitwa na wakati yataisha” alisema Mtaka.
  Aidha, Mtaka amewaomba wanawake na waumini wote wa ujumla kuendelea kuliombea Taifa, Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine, ili nchi iendelee kuwa na amani na viongozi waweze kufanya mazuri yaliyokusudiwa kwa ajili ya Watanzania wote.
  Katika hatua nyingine Mtaka ametoa wito kwa viongozi wa madhehebu ya dini pamoja na kusimamia kiroho wawe msaada kwa makundi mbalimbali yaliyomo makanisani hususani vijana na wanawake, ili yaweze kuendesha miradi ya maendeleo itakayowasaidia kubadilisha maisha yao kiuchumi.
  Baadhi ya wanawake walioshiriki katika Maombi ya dunia baada ya kusikia hotuba ya Mkuu  wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ambaye alikuwa mgeni rasmi wamesema watahakikisha wanasimamia vema malezi ya watoto wao na kuhakikisha wanasoma huku wakiunga mkono wazo la vikundi kuwa na miradi ya maendeleo.
  “ Kama mama nimejifunza mengi; moja ni kuwa tukiwasomesha watoto wetu hakutakuwa na unyanyasaji, mfano kama kuna watu wanafanya ukeketaji kwa watoto wa kike, jamii ikielimika haya hayatakuwepo na tutahakikisha wanasoma mpaka vyuo vikuu; ujasiriamali nao tutafanya ili tujikwamue kwenye umaskini” Devotha Charles mshiriki kutoka Mwisenge
  “Baadhi ya wanawake katika makanisa yetu tulikuwa hatua miradi na wengine waliokuwa nayo  ilikuwa  inaenda kwa kusuasua, lakini baada ya ujumbe tulioupokea leo nina hakika utaleta mwamko kwa wanawake wengi kuanzisha miradi ya kuwasaidia kupata kipato” Jackline Cheche mshiriki kutoka Parokia ya Nyamiongo Musoma.
  Kwa upande wake Askofu wa Jimbo Katoliki la Musoma Mhashamu Michael Msongazila amesema maombezi kwa ulimwengu yaendelee kufanyika ili watu waweze kuheshimu uhai wa mwanadamu.
  “Ombeeni ulimwengu uheshimu uhai wa mwanadamu tumeumbwa katika sura na mfano wa Mungu, tumekabidhiwa dhamana hiyo ya uumbaji, uhai huu tuulinde tuutetee na tuukuze kwa ajili ya kujenga ulimwengu, maisha yetu yana nafasi ya pekee yanapokuwa na Mungu” alisema Askofu Mlonganzila.
  Maombi ya Dunia kwa wanawake wa madhehebu ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania(CCT) na Wanawake Wakatoliki Tanzania(WAWATA) hufanyika kila mwaka Machi Mosi yakiwa na lengo la kuombea familia, Taifa na Dunia kwa ujumla juu ya amani na mahitaji mengine.

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tigo Tanzania Simon Karikari (wa pili kulia) akikata utepe kuashiria kumkabidhi rasmi nyumba mzee Joram Mollel (93) ambaye amekuwa akishiriki mbio za Tigo Kili Half Marathon kwa miaka minne mfululizo. Kulia kwake ni mzee Mollell akifautiwa na mwanaye Elibarik Mollel pamoja na Afisa Biashara Mkuu wa Tigo Tarik Boudiaf. Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika eneo la Mushono jijini Arusha. Kulia ni kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Aidan Komba
   Babu Joram Molle (93)  akitoa neno la shukrani muda mfupi baada ya kukabidhiwa nyumba na Kampuni ya Tigo kutokana na ushiriki wake wa mbio za Tigo Kili Half Marathon kwa miaka minne mfululizo. Wanaomsikiliza kushoto ni  Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo Simon Karikari akifuatiwa na Afisa Biashara Mkuu Tarik Boudiaf, na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini Aidan Komba. Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika eneo la Mushono jijini Arusha.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tigo Tanzania Simon Karikari, akimkabidhi fungua za nyumba mzee Joram Mollel ikiwa ni kama zawadi na kukubali mchango wake kwa mbio za Tigo Kili Half Marathon kwa miaka minne mfululizo pamoja na umri mkubwa. Anayeshuhudia ni Kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini Aidan Komba. Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika eneo la Mushono jijini Arusha.
   Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Tigo Tanzania wakiwa katika picha ya Pamoja muda mfupi baada ya Kampuni hiyo kumzawadia nyumba mzee Joram Mollel mkazi wa Jijini Arusha ikiwa ni kutambua mchango wake katika mbio za Tigo Kili Half Marathon ambazo mzuee huyo ameshiriki kwa miaka minne mfululizo. Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika eneo la Mushono jijini Arusha.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Tigo Simon Karikari akizungumza na wahabari hawapo pichani wakati wa hafla ya kumkabidhi nyumba Mzee Joram Mollel (93), aliyekuwa akikimbia mbio za Tigo Kili Half Marathoni kwa miaka minne mfululizo, kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini Aidan Komba. Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika eneo la Mushono jijini Arusha.  KAMPUNI ya Mawasiliano ya Tigo imemkabidhi nyumba ya vyumba 17 ikiwa na samani zote za ndani Babu Joram Mollel (93), kutokana na ushiriki wake wenye mafanikio katika mbio za Tigo Kili Half Marathon kwa miaka mine mfululizo.

  Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika eneo la Mushono nje kidogo ya Jiji la Arusha, ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo Simon Karikari pamona na Afisa Biashara mkuu Tarik Boudiaf 

  Akizungumza kwenye hafla hiyo Karikari alisema, nyumba hiyo ilinunuliwa na kukarabatiwa kisha kumkabidhi Babu Mollel kama ishara ya shukrani kwa kujituma na umahiri wake katika riadha.

  'Babu Mollel amekuwa akishiriki mashindano ya Tigo Kili Half Marathoni kwa miaka mingi sasa. Tulipoona hali ya makazi yake si nzuri Tigo tuliona njia sahihi ni kuwezesha apate nyumba yake mwenyewe,"alisema Karikari.

  “Katika nyumba yake hii ya hapa Mushono, Babu atakuwa anakaa katika nyumba ya kisasa, iliyo tayari na samani pamoja na vyombo vyote muhimu vya ndani. Nyumba hii pia imeunganishwa na umeme na maji. Hati ya nyumba pia ipo kwa jina lake, hivyo yeye ndiye mmiliki halali wa nyumba hii,” aliongeza Karikari. 

  Aidan Komba, ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini alisema kwamba nyumba imegawanyika sehemu tatu na kuongeza kuwa Babu Mollel atakaa katika nyumba moja na mbili zilizobaki ataweza kuzipangisha na kujipatia kipato cha kuendeshea maisha yake ya kila siku. 

  “Napenda kuwashukuru sana Tigo kwa zawadi hii ya kipekee. Maneno yangu hayawezi kuelezea furaha niliyonayo. Ktendo hiki kina maana kubwa sana kwangu. Maana hivi sasa ninaweza nikasema sasa nina mahali pakuita kwangu,” alisema Babu Mollel. 

  Ushiriki wa Babu Mollel katika mashindano ya Kilimarathon ni wa zaidi ya miaka 15, ambapo amekuwa akiwavutia watu wengi kumshangilia wakati akishiriki mbio za marathon, pamoja na uzee wake. Katika miaka minne mfululizo iliyopita, Tigo imekuwa mlezi na mdhamini mkuu wa mbio za kilometa 21 zinayojulikana kama ‘Tigo Kili Half-Marathon’, ambayo ni nusu ya mbio kamili ya kilometa 42 za marathon ambayo hufanyika katika vilima vya Mlima Kilimanjaro, mlima mrefu kuliko wote barani Afrika. 

  “Babu Mollel ni taswira halisi ya uanamichezo, ujasiri na jitihada. Yeye ni mfano aliye hai kwamba kama binadamu tunaweza tukafanikiwa katika lolote lile ambacho tukiamua kukifanya kwa dhati, na kuondoa dhana nzima kwamba umri au changamoto zingine zozote zinaweza zikawa sababu ya kutokufanikiwa kwetu. Leo, tunamsheherekea yeye,” alieleza Karikari kuhusu mzee huyo wa miaka 93.

  Mwaka jana, Tigo ilishirikiana na Babu Mollel katika kampeni maalum ya Tigo Kili Half-Marathon iliyoitwa ‘Tisha kama Babu’. Kampeni hiyo ilikuwa na lengo kubwa la kuhamasisha Watanzania kuweza kuishi maisha ya kujali afya zao. Wakati huo huo, Tigo pia ilisitisha rasmi namba ya mbio aliyokuwa akiitumia Babu Mollel ‘1040’ na alitambuliwa rasmi kama mwanamichezo wa heshima ‘Hall of Fame’.

  0 0

  Anaandika Abdullatif. Yunus

  Siku ya Jumamosi Bado Masaa machache kabla ya kumpokea Mpambanaji, Shujaa, Muongoza njia Marehemu Ruge Mutahaba Nyumbani kwao Kiziru, Kabale - Bukoba. Hali ni shwari nyonyo za waombolezaji zikiwa zimejaa simanzi na masikitiko kwa kuondokewa na kipenzi chao Ruge, Kamati ya Maandalizi chini ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa inazidi kujipanga kuupokea ugeni Mkubwa uliobeba zawadi ya Mpendwa wao, kiu ikiwa kubwa zaidi kwa ndugu jamaa na marafiki kutaka kushuhudia kwani wengi hawajaamini kile wanachokiona na kukisikia Dar es salaam. 

  Kufuatia Msiba huo tayari Sheikh wa Mkoa Kagera Alhaj Haruna Kichwabuta amefika msibani kutoa pole kwa wafiwa, Mara baada ya kurejea akitokea Zanzibar akiwa ameambatana na Sheikh wa Mkoa wa madhehebu ya Ijumaa na Adhuhuri Alhaji Kamugunda.

  Kutokana na Shughuli za siku ya Jumatatu (siku ya mazishi) kuhamishiwa Viwanja vya Gymkhana Kamati ipo katika mipango ya kuratibu eneo kwa ajili ya mpangilio wa majukwaa, maegesho na huduma nyingine, pia katika kuheshimu ukubwa wa Msiba huu tayari barabara ya kuelekea Kijijini Kiziru Kabale Nyumbani kwao Marehemu imeanza kukarabatiwa ili kuhakikisha kila jambo linakwenda sawa upande wa usafirishaji wa watu watakaokwenda msibani.

  Hali ilivyo sasa Nyumbani tayari kaburi limekamilika likingoja kwa heshima Mwili wa Shujaa, upande mwingine maandalizi yanaendelea baada ya kufungwa Turubai (tents) waombolezaji sasa wanaendelea kufika hapa kwa ajili ya kutoa pole.
  Kaburi likingoja Kumsitiri Shujaa
  Sheikh wa Mkoa Kagera (BAKWATA) Haruna Kichwabuta alievaa Koti, pamoja na Sheikh wa Mkoa madhehebu ya Ijumaa na Adhuhuri Alhaji Kamugunda wakiwa Nyumbani kwa Profesa Mutahaba Kiziru Kabale.
  Sheikh Haruna Kichwabuta akiwa na Mzee Revelian Rwabyo mmoja wa waasisi wa Familia ya Mzee Mutahaba, Mara baada ya kuwasili Nyumbani kwao Marehemu Ruge Kutoa pole.
  Pichani ni marekebisho na ukarabati unaoendelea katika barabara ya kuelekea kijijini Kiziru Kabale Bukoba, katika kusawazisha mashimo na baadhi ya maeneo korofi ili ipitike kiurahisi.
  Pichani Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti akijadiliana jambo na Katibu wake Ndg. Salala Katika viwanja vya Gymkhana wakati Kamati hiyo ilipofika viwanjani hapo kuendelea kuratibu shughuli ya kuupokea ugeni wa Msibani wa Ruge.
  Pichani ni Askofu TZA wa Clouds (mwenye kofia) akitoa ufafanuzi kuhusu jukwaa litakalofungwa eneo hilo kwa ajili ya shughuli ya kuaga.
  Pichani ni viwanja vya Gymkhana ambapo shughuli nzima ya Ibada na Kuaga itakapofanyika, kama unavyoona Kamati chini ya Mkuu wa Mkoa Kagera Tayari imefika Kuendelea kuratibu tukio.

  0 0

  Picha hii Ilipigwa 15/August/2018, ni dhahiri ni picha ya Mwisho Ruge kuonekana Public,alikua na nafuu,alikuja ofisini, juzi yake nilikua nimepokea ujumbe kuachana na Clouds kuuanza Utumishi wa Umma na mtu wa kwanza kumpigia kabla hata ya baba yangu mzazi alikua ni Ruge si kwa nia mbaya ila nilitaka mwongozo wa Haraka.

  Alifurahia na hapo hapo Aliwapigia simu viongozi mbalimbali kwa wito wangu na direct hasa Katibu mkuu Utumishi Dk.Ndumbaro akimuomba anipokee kijana wake serikalini na akimsisitiza kua “ni kijana niliemlea kwa nguvu sana na nimewekeza sana kwake, mtumie vizuri, nimeumia kumpoteza ila ni kazi yangu kuandaa vijana wakaitumikie nchi yao,alimwambia huyu ni azina kwa taifa hili na atawasaidia”,aliyasema haya akiwa kitandani anaumwa.

  Baada ya kuripoti siku hii pichani alipata nafu akaenda ofisini akanisihi nije Dar niondoke Dodoma haraka anataka anipe baraka zake na kunikutanisha na Mwalim wangu wa Sayansi ya Siasa Ndugu Bashiru Katibu Mkuu wa CCM Taifa ofisini kwa Clouds ambae pia alifanya kipindi Clouds360 siku hiyo, alimwambia Katibu “kijana wangu huyu Serikali imeninyang’anya anaenda Pangani kuitumikia nchi,ni kijana ninaemuamini sana na ana uwezo mkubwa sana” baada ya hapo tuliongea mengi na baadae kumsindikiza katibu mkuu chama na kupiga picha ya ukumbusho na kumbe ni picha ya mwisho na akaniita tena ofisini na kunambia “nenda usiniangushe na usiisahau Clouds na THT ,utafika mbali”.

  Ulilalamika kuwa naondoka huku unaniitaji sana na umeniandaa ili nije kuuinua Clouds Media mimi na vijana wengine unaowatengeneza maana unataka kupumzika mambo ya Clouds hivo utatuachia sisi sikuelewa kupumzika kwa maana gani?

  Picha hii imenikumbusha mafundisho ulionipa mara zote, ni kila wakati naada ya kazi ungenpigia kila mmoja aliefanikisha kumwambia “Im proud of you” ,ulikua mtu wa kutoa moyo sana na kushukuru kila jambo, lililofanikiwa kwenye project zako

  Ruge nadhani tunapaswa kuandika KITABU juu yako na natoa rai tuungane kufanya hili..!tukisema mengi tutawachanganya watu, wengine hawaelewi wanahisi tunaongeza chumvi ila ni wazi kwetu ulikuna kama NABII..!
  Sisi nasi tuna mioyo ya namba gani tusikulilie kwa kilio cha uchungu na machozi ya damu.?
  #shujaamwogozanjia


  Na Gibson George Bayona Ruge.

  0 0

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu akisema jambo wakati wa kikao na watendaji wa Hospitali ya Wilaya ya Kilosa (hawapo pichani)
  aziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu (kushoto) akiteta jambo na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Dkt Halima Mangiri.

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu ( kulia) akiwasalimia mama na mtoto katika wodi ya mama na mtoto katika Hospitali ya Wilaya ya Kilosa
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu akisoma nyaraka za dawa katika chumba cha dawa cha Hospitali ya Wilaya ya Kilosa. 
   


  Na WAMJW – Kilosa, MOROGORO.

  Wananchi wametakiwa kujiunga na mfuko wa Bima ya Afya ili kuwa na uhakika wa kupata matibabu wanapofika kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini.

  Waziri Ummy Mwalimu ameyasema hayo leo alipokuwa ziarani Wilaya ya Kilosa Mkoa wa Morogoro akikagua hali ya utoaji wa huduma za afya katika Hospitali ya Wilaya ya Kilosa. “Ni muhimu kwa wananchi kuwa na bima ya afya ili waweze kuwa na uhakika wa kupata matibabu ikiwemo dawa bila ya kikwazo cha fedha” amesema Waziri Ummy.

  Waziri Ummy amesema kuwa matarajio ya wananchi mara baada ya kujiunga na bima ya afya ni kupata huduma bora za afya bila usumbufu huku wakiwa na uhakika wa kupata dawa kwa makundi yote ikihusishwa wale wa Bima ya Afya pamoja na Mfuko wa Bima ya Afya Ngazi ya Jamii (CHF) iliyoboreshwa.

  “Mwananchi yeyote ambaye amekuja na bima ya afya, CHF iliyoboreshwa wanapaswa kupata huduma zote, kumwona daktari bure, vipimo bure, na dawa bure” amesema Waziri Ummy na kuongezea “Bila ya kufanya hivyo hakuna umuhimu wa kuwaambia wananchi kukata bima za afya.

  Kwa upande mwingine, Waziri Ummy amewataka watoa huduma za afya nchini kutoa huduma bora kwa kuzingatia Mwogozo wa Taifa wa Matibabu na orodha ya dawa muhimu huku akiwataka kutoa huduma bora za matibabu kwa kutoa dawa kulingana na mwogonzo unavyobainisha. “Badala ya kumwandikia unayoitaka wewe au mgonjwa, tumeweka utaratibu weka dawa ambayo ipo kwa mujibu wa mwongozo” alisema Waziri Ummy.

  Waziri Ummy amesema kuwa lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha wananchi wanapata dawa katika vituo vya kutolea huduma kwani kumekuwa na malalamiko hapo zamani wagonjwa wakisema madaktari walikuwa waki waambia dawa hakuna huku ili hali dawa zipo.

  “Hatutaki kuona wananchi wanalalamika dawa hakuna na kutuona tunadanganya wakati dawa zipo, na mwongozo unasema wazi kama hakuna dawa A mpe dawa B. Alisikika akisema Waziri Ummy. Ka upande mwingine Waziri Ummy ameupongeza Uongozi wa Hospitali ya Wilaya ya Kilosa kwa kuhakikisha dawa zinapatikana kwa ufanisi muda wote na kuwataka mafanikio ambayo wameyapata wahakikishe waharudi chini.

  “Serikali itaendela kuhakikisha inaboresha Sekta ya afya ili Taifa liweze kuwa na nguvu kazi yenye afya bora kazi yenu nyinyi ni kuhakikisha mnaendelea kutoa huduma bora na kuhakikisha dawa zinapatikana muda wote” amesema Waziri Ummy. Naye Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Dkt. Halima Mangiri ameishukuru Serikali kwa kuuongeza bajeti ya dawa wilayani humo.

  Dkt. Mangiri amesema kuwa bajeti ya dawa imekuwa ikiongezeka maradufu mwaka hadi mwaka huku akitolea mfano wa mwaka 2017/18 hali ya upatikanaji wa dawa ilikuwa ni asilimia 86, huku kwa mwaka 2018/19 hali ya upatikanaji dawa ikiongezeka na kufikia asilimia 96.

  “Tunaishukuru Serikali, Kwa kweli hali sasa sii kama zamani, tunapata dawa na hali inaridhisha” alisema Dkt Mangiri.

  0 0

  Daktari Bingwa wa Upasuaji Magonjwa ya Masikio, Pua na Koo, Dkt. Godlove Mfuko wa Hospitali ya Taifa Muhimbili –Mloganzila akimpima mgonjwa kiwango cha usikivu katika zoezi la upimaji wa usikivu linalofanyika leo hospitalini hapo leo na kesho.
  002
  Katika picha baadhi ya wananchi waliojitokeza kupima kiwango cha usikivu hospitalini hapo.
  003
  Wazazi wakiwa na watoto kabla ya kwenda kuwaona wataalam wa magonjwa ya masikio, pua na koo wa Hospitali ya Muhimbili Upanga na Mloganzila.
  004 A004 B
  Wananchi wakisubiri kupata huduma ya upimaji ya usikivu katika Hospitali ya Mloganzila.
  005
  Mtaalam wa magonjwa ya masikio, pua na koo wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Teddy Uisso akimpima mgonjwa kiwango cha kusikia.

  006
  Mratibu wa Usikivu kutoka Mfuko wa Usikivu wa Starkey akitoa elimu kwa wananchi wanaosubiri kuwaona wataalam wa magonjwa ya masikio, pua na koo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila.

  ………………………..
  Wingi wa watu waliojitokeza leo kupima usikivu wao umeonyesha ni jinsi gani wananchi wanajali afya zao, huku wakipewa sababu zinazosababisha baadhi ya watu kupoteza uwezo wa kusikia na jinsi ya kuzuia upotevu wa kusikia.
  Upimaji wa usikivu bila malipo umeanza leo Machi 2, 2019 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila ambapo kauli mbiu ni “Chunguza Usikivu Wako (Check Your Hearing” yenye lengo la kuhamasisha kila mmoja kuchukua hatua ya kufanyiwa uchunguzi wa usikivu wake.

  Huduma ambazo zimeanza kutolewa leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila ni; upimaji wa kuona kiwango cha kusikia na rufaa ya kupata matibabu Muhimbili kwa watakaobainika kuwa na tatizo. Pia elimu ambayo imetolewa ni dalili na vyanzo vya kupoteza usikivu, kutoa takwimu za ongezeko la upotevu wa usikivu duniani na hatua zinazochukuliwa nchini.

  Katika shughuli ya upimaji huo, wananchi wameelezwa sababu zinazosababisha mtu au watu kupoteza uwezo wa kusikia. Zifuatazo ni sababu zinazosababisha watoto wachanga kupoteza uwezo wa kusikia. Kwanza familia kuwa na watu wenye matatizo ya kutokusikia, maambukizi ya magonjwa kutoka kwa mama wakati akiwa mjamzito, mtoto kuzaliwa kabla ya wakati, mtoto kukosa hewa wakati wa kuzaliwa na kupata homa ya manjano baada ya kuzaliwa.

  Kwa upande wa watoto na watu wazima, sababu zinazosababisha kupoteza uwezo wa kusikia ni; kuugua surua, uti wa mgongo au sikio kupata maambukizi na uchafu kutoka sikioni, matumizi yasiyo sahihi ya dawa mbalimbali, kuumia sikio au kichwa, kukaa sehemu zenye kelele au zenye sauti kubwa sana, kusikiliza sauti kupitia vifaa mbalimbali kabla ya umri unaofaa na nta au kitu kisichokuwa cha kawaida kuziba mfumo wa njia ya sikio.

  Wazee nao wamekuwa wakipoteza uwezo wa kusikia kutokana umri wao hivyo uwezo wao wa kusikia hupungua, kukaa sehemu zenye kelele au zenye sauti kubwa sana, kupata shinikizo la damu, kuugua sukari na wengine kutumia dawa mbalimbali.

  Wataalam wa magonjwa ya masikio, pua na koo wanaeleza kuwa njia za kuzuia upotevu wa kusikia kwa mtu mzima ni kuweka kifaa au kitu chochote ndani ya sikio, anashauriwa kutumia pamba laini au kifaa maalumu cha kuziba masikio kwenye sehemu zenye sauti kubwa, endapo ana shida ya sikio au masikio anatakiwa kumuona daktari, anatakiwa kuchunguza dawa anazotumia kama zinaweza kuathiri usikivu wake na pia, anashauriwa kutumia vifaa salama vya masikio kama ulivyoelekezwa na daktari.

  Kwa upande wa watoto; mzazi anashauriwa asimweke mtoto kifaa au kitu chochote ndani ya sikio labda kama unamsafisha sikio, watoto wanapaswa kufundishwa kutokuweka kifaa au kitu chochote ndani ya sikio, endapo  sikio la mtoto linauma, limeumia, kukatika au linatoka uchafu  ndani mpeleke kwa daktari, usiwaruhusu watoto kuogelea kwenye maji machafu, mzazi usimpige mtoto sehemu za sikio, mkinge mtoto katika sehemu zenye sauti au kelele kubwa na wafundishe watoto kusikiliza kwa kutumia vifaa salama.

  Katika hatua hii, mzazi au mlezi anawezaje kuhisi mtoto wake amepoteza uwezo wa kusikia? Mtoto anaweza kuwa na matatizo ya kutokusikia ikiwa hatojibu jambo kwa sauti, kutokuelewa kitu gani kinazungumzwa au kushindwa kuongea kwa ufasaha, kuchelewa kuongea kwa ufasaha, kutokwa na uchafu sikioni, na kuumwa sikio mara kwa mara au sikio kuziba.

  Kwa upande wa mtu mzima atakuwa amepoteza uwezo wa kusikia endapo;  atauliza mara kwa mara watu warudie walichoongea, kuwa na tabia ya kuongeza sauti ya redio na runinga, kukosa baadhi ya maneno katika maongezi, kuwa na kelele katika sikio na wakati mwingine watu wanakwambia unaongea kwa sauti kubwa sana.

  Upimaji wa usikivu bila malipo umeanza leo Machi 02,2019 na utamalizika Kesho Machi 03,2019.

  0 0


  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akifungua kikao cha Ushauri cha Mkoa (RCC) kilichofanyika Machi Mosi, 2019 katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu cha Morogoro
  Wajumbe wa Kikao cha RCC wakiwa katika Ukumbi tayari kwa majadiliano.
  Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Clifford Tandari (aliyesimama)akimkaribisha Mwenyekiti wa Kikao cha RCC kufungua kikao hicho kilichofanyika Machi Mosi, 2019 katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu cha Morogoro
  Mbunge wa Jimbo la Malinyi Mkoani Morogoro Mhe. Haji Mponda akichangia hoja wakati wa kikao cha RCC kilichofanyika Machi Mosi, 2019 katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu cha Morogoro
  Wajumbewa Kamati ya RCC wakisikiliza kwa makini mawasilisho ya sekta mbalimbali zilizowasilishwa kwenye kikao hicho kilichofanyika Machi Mosi, 2019 katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu cha Morogoro  …………………..

  Na. Andrew Chimesela – Morogoro

  Mkoa wa Morogoro umepanga kutumia zaidi ya shilingi 355Bil. katika Bajeti yake ya makadirio ya mwaka wa fedha 2019/2020 ambazo fedha hizo zitatumika katika matumizi mbalimbali ikiwemo mishahara ya watumishi wake, Maendeleo na matumizi mengine.

  Hayo yalibainishwa katika kikao cha Ushauri cha Mkoa kilichofanyika Machi Mosi mwaka huu katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu cha Mjini Morogoro ambapo wajumbe wake waliridhia makadirio ya Bajeti hiyo Kutumika.

  Akiwasilisha Bajeti hiyo, Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Uratibu na Utawala Bw. Diaz Ndomba kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa huo Bw. Clifford Tandari alisema bajeti hiyo imezingatia mwongozo wa Maandalizi ya Mpango wa Bajeti ya mwaka 2019/2020 na Ilani ya Uchaguzi ya chama cha Mapinduzi (2015).

  Aidha, amesema Bajeti hiyo imezingatia pia Dira ya Maendeleo ya Taifa (2020/2025), malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa (2030) pamoja na malengo ya Mpango wa kufanya mageuzi ya kiuchumi wa Viwanda hapa nchini.

  “kipaumbele kimeendelea kuwekwa katika kuimarisha mazingira wezeshi ya Ujenzi wa Viwanda vidogo, vya kati na vikubwa” alisisitiza Bw. Ndomba.

  Mchanganuo wa bajeti hiyo ambayo ni ongezeko la asilimia 16 ukilinganisha na Bajeti ya mwaka 2018/2019 ni za matumizi ya kawaida ambapo Sh. 267,398,052,000 zitatumika kwa ajili ya mishahara huku matumizi mengineyo zitatumika Sh. 36,075524,000 na kufanya jumla yake kuwa Sh. 303,473,576,000.

  Kwa upande wa Matumizi ya miradi ya Maendeleo Mkoa huo umepanga kutumia Sh. 37,817,411,000 ikiwa ni fedha za ndani na Sh. 13,953,937,000 zitakuwa ni fedha za nje na kufanya jumla 51,771,348,000 hivyo jumla kuu kufikia Sh. 355,244,924,000.

  Mwisho wa mawasilisho hayo Mkoa ulitoa Ombi kwa Serikali kuu hususan Wizara ya Fedha na Mipango kuendelea kutoa kwa wakati fedha zilizopangwa na kupitishwa kama ilivyoainishwa kwenye mpango kazi wa Mkoa.

  Akifungua kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe aliendelea kuwaagiza Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Mkoa huo kusimamia rasilimali fedha zinazopatikana ikiwa ni pamoja na kukusanya mapato ya ndani kwa kutumia mashine za kiilektroniki na kuzipeleka Bank kwa wakati.

  Aidha, aliwaonya watumishi wa umma wenye tabia ya kutumia vibaya fedha za Serikali kuacha tabia hiyo mara moja la sheria itawafuata huku akiwataka Wenyeviti wa Halmashauri hizo kuwachukulia hatua kali za kisheria na za kinidhamu watumishi hao watakaokiuka katika kutumia vibaya rasilimali fedha za Serikali.

  “Ila tu ukivunja utaratibu ndio mambo mengine yanajitokeza kwa bahati nzuri Wenye viti wa Halmashauri mpo, kama hayo yanatokea msisite kuchukua hatua, kwa sababu miongozo ipo na wataalamu wapo muwape taarifa sahihi kwa ajili ya kuchukua hatua.”alisisitiza Dkt. Kebwe

  Katika kipindi cha kujadili yatokanayo suala la Kijiji cha Ngombo kilichopo Wilaya ya Malinyi Mkoani humo liliibuka huku baadhi ya wajumbe wakitaka ufafanuzi zaidi ambapo Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Omari Mgumba (MB) aliwaka wajumbe pamoja na wananchi wa Kijiji cha Ngombo kuendelea na kazi zao kama kawaida kama Serikali ilivyoagiza lakini bila kufanya uendelezaji mwingine katika maeneo hayo hadi hapo Serikali itakapotoa kauli nyingine.

  Aidha, Naibu Waziri huyo wa Kilimo alishauri kuwa ili Mkoa uwe na mipango sahihi juu ya kilimo ni lazima Mkoa kuwa na mpango Mkakati kuhusu kilimo na kusimamia kwa karibu zoezi la kupata takwimu sahihi za wakulima hususan wa mazao ya kimkakati kwa kuwasajili ili kujua idadi yao, mahali walipo, kiasi cha eneo wanalolima, mazao wanayolima pamoja na mahitaji yao ya msingi.

  0 0

   Shirika lisilo la Kiserikali la Agape AIDS Control Programme (AACP) la mkoani Shinyanga linalotetea haki za watoto limeunda Mabaraza ya Watoto ngazi ya vijiji katika kata ya Didia halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, kwa lengo la kuwajengea uwezo watoto kupaza sauti dhidi ya vitendo ya vya ukatili ambayo huwa wanafanyiwa, ikiwemo kupewa ujauzito na kuozeshwa ndoa za utotoni.

  Zoezi la uundaji wa Mabaraza ya watoto limeendeshwa leo Machi 2, 2019  na Ofisa Maendeleo ya Jamii wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Aisha Omari kwa kushirikiana na Shirika la Agape, ambapo jumla ya mabaraza matano yameundwa katika kijiji cha Chembeli, Mwanono, Didia, Mwamalulu na Bukumbi. Akizungumza wakati wa uundaji wa Mabaraza hayo, Meneja Mradi wa Kuzuia Mimba na Ndoa za Utotoni kutoka Shirika la AGAPE Mustapha Isabuda, amesema Mabaraza hayo ya watoto yatakuwa chachu kubwa ya kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya watoto. 

  Alisema watoto wanapokuwa wanakutana kwa pamoja wao wenyewe kupitia mabaraza hayo, huwa wanakuwa wawazi kuelezea changamoto za matukio ya kikatili ambayo huwa wanatendewa na baada ya hapo viongozi wao huziwasilisha kwenye mamlaka husika akiwemo mtendaji wa kijiji na hatimaye kutatuliwa. 

  “Tumeunda Mabaraza haya ya watoto ngazi ya vijiji katika kata ya Didia ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wetu wa kupinga mimba na ndoa za utotoni, ambao unafadhiliwa na Shirika la kimataifa la FireLight Foundation kutoka nchini Marekani ambapo kwenye kata hii kuna matukio mengi ya ukatili dhidi ya watoto,”alisema Isabuda. 

  Naye Ofisa Maendeleo ya Jamii halmashauri ya Shinyanga Aisha Omari alipongeza uundaji wa mabaraza hayo ya watoto na kutoa wito kwa watoto wayatumie vizuri ili kujikomboa na kupata haki zao za msingi, ikiwemo kutobaguliwa, kupewa elimu hasa kwa watoto wa kike na kutoozeshwa wangali watoto. Kwa upande wao watoto hao akiwemo Nyamisi Singu ambaye alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la watoto katika kijiji cha Bukumbi alisema mabaraza hayo yatakuwa msaada mkubwa sana kwao kwani  idadi kubwa ya watoto huwa wanaogopa kuelezea changamoto zao kwa watu wakubwa, na mwisho wa siku wanaambulia ujauzito ama kuozeshwa ndoa za utotoni. 

  Wenyeviti waliochaguliwa kuongoza wenzao katika Mabaraza ya watoto, ni  Yusuf Sita (kijiji cha Mwanono), Aloyce Masele (Chembeli), Ashraf Salumu (Didia), Paschal Maganga (Mwamalulu) na Nyamisi Singu (Bukumbi).Wengine ni Karoline Issaya ambaye amechaguliwa kuwa Makamu mwenyekiti baraza la watoto kijiji cha Mwanono ,katibu ni Ramadhani Frank, Chembeli Makamu mwenyekiti ni Milembe Maila ,katibu ni Sofia Sudi, Didia Makamu mwenyekiti ni Mwanne Emmanuel ,katibu Sundy Mayala, Mwamalulu Makamu mwenyekiti ni Scholastika Kidaha, katibu Pendo Hassani, Bukumbi Makamu mwenyekiti ni Elivida Kabuga, katibu akiwa ni Ramadhani Mrisho. Meneja Mradi wa Kuzuia Mimba na Ndoa za utotoni kutoka Shirika la Agape la kutetea haki za watoto mkoani Shhinyanga Mustapha Isabuda ,akizungumza na watoto juu ya umuhimu wa Mabaraza ya watoto namna yatakavyoweza kuwasaidia kutokomeza matukio ya ukatili dhidi yao na kuweza kupata haki zao za msingi ikiwemo elimu, pia kutokomeza mimba na ndoa za utotoni.Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog Ofisa Maendeleo ya Jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Aisha Omari akiwataka watoto kuyatumia vizuri Mabaraza ya watoto katika kupaza sauti juu ya matukio ya ukatili dhidi yao ili yapate kufanyiwa kazi kabla ya kuwaletea madhara. Ofisa Maendeleo ya jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Aisha Omari, akiwasisitiza watoto kuacha kuficha matukio ya ukatili wanayofanyiwa bali wayafichue ili wawe salama na kuweza kutimiza ndoto zao. Ofisa Maendeleo ya jamii Kata ya Didia wilaya ya Shinyanga Felista Mell, akielezea hali ya matukio ya ukatili kwenye kata hiyo ikiwemo utekelezaji wa watoto pamoja na kupewa wanafunzi kupewa mimba, ambapo kwa mwaka huu tayari wanafunzi watatu wa shule za msingi wana ujauzito na wameshaachishwa masomo, na kuwataka watoto hao wavunje ukimya watoe taarifa mapema ya matukio ya ukatili.  Afisa Mtendaji wa Kata ya Didia halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Jackson Majenga, akiwataka watoto hao kupitia viongozi wa mabaraza yao, kumpelekea pia taarifa za matukio ya kikatili ili ayafanyie kazi, ambapo mpaka sasa wameshamkamata mtuhumiwa mmoja wapo ambaye amempachika mimba mwanafunzi huku wengine wawili wakiendelea kutafutwa. Watoto wakiwa kwenye mkutano wa kuunda Mabaraza yao, wakisikiliza nasaha kutoka kwa viongozi wa serikali na Shirika la Agape juu ya kuyatumia mabaraza kupaza sauti na kupata haki zao za msingi.  Watoto wakiendelea kusikiliza nasaha za viongozi kabla ya kuanza uchaguzi wa kuunda mabaraza yao ambayo yatakuwa msaada mkubwa kutokomeza matukio ya ukatili dhidi yao likiwemo na suala la mimba na ndoa za utotoni na hatimaye kutimiza ndoto zao. Watoto wakiendelea kusikiliza kwa makini namna ya kutumia Mabaraza yao kutoa taarifa za matukio ya kikatili dhidi yao, ikiwemo fursa ya kupata elimu hasa kwa watoto wa kike na kutoozeshwa ndoa za utotoni kwa tamaa ya wazazi kutaka mifugo. Viongozi wa Baraza la watoto katika kijiji cha Chembeli ambao wamechaguliwa wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa baraza hilo Aloyce Masele katikati ni Makamu mwenyekiti Milembe Maila, akifuatiwa na katibu Sofia Sudi. Ashraf Salum (kulia) amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa Baraza la watoto katika kijiji cha Didia akiwa na makamu wake Mwanne Emmanuel. Nyamisi Singu (wa kwanza kulia) amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa Baraza la watoto katika kijiji cha Bukumbi, katikati ni Makamu wake Elivida Kabuga na wa kwanza  kushoto ni Katibu Ramadhani Mrisho. Watoto wakifurahi pamoja na Ofisa Maendeleo ya jamii halmashauri ya wilaya Aisha Omari, mara baada ya kumaliza kuunda Mabaraza na kuchagua viongozi ambao watakuwa wakiwaongoza katika mikutano ya kujadili changamoto ambazo huwa zinawakabili juu ya matukio ya ukatili dhidi yao ili  yatatuliwe. Na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

older | 1 | .... | 1810 | 1811 | (Page 1812) | 1813 | 1814 | .... | 1897 | newer