Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel Catalog



Channel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1809 | 1810 | (Page 1811) | 1812 | 1813 | .... | 1897 | newer

  0 0





  Na Lucas Mboje, Dar es Salaam
  MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya NBC,Theobald Sabi leo amekutana na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Phaustine Kasike na kufanya mazungumzo yaenye lengo la kuangalia njia bora zaidi za kudumisha na kuboresha uhusiano baina ya pande zote mbili.

  Akizungumza katika mkutano huo ambao pia ulijumuisha maafisa waandamizi kutoka Benki ya NBC na Jeshi la Magereza, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi alilishukuru Jeshi hilo kwa kuwa mdau mkubwa wa Benki kupitia mikopo, akaunti za mishahara za askari na pamoja na Shirika Magereza ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikitoa huduma kwa askari wa Jeshi hilo.

  “Nichukue fursa hii kulishukuru Jeshi la Magereza kwa mahusiano ya kibiashara ambayo limekuwa likitupatia, nilipongeze Shirika la Magereza kwa kuendelea, kuwa mdau muhimu katika huduma zetu za kibenki pamoja na Maafisa na askari wa Jeshi la Magereza”. Alisema Mkurugenzi Sabi.

  Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Phaustine Kasike alimshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi kwa kutembelea Jeshi hilo na kuipongeza Benki ya NBC kwa maboresho mbalimbali katika huduma zake za kibenki.

  Jenerali Kasike amesema kuwa Jeshi la Magereza litaendelea kushirikiana na Benki ya NBC katika miradi yake ya kiuwekezaji na huduma mbalimbali ili kuongeza ufanisi wa Jeshi hilo.

  “Nikuombe Mkurugenzi Sabi na uongozi mzima wa Benki ya NBC kuona uwezekano wa kusaidiana katika huduma mbalimbali za kijamii magerezani kwani Jeshi la Magereza ni watoa huduma kwa jamii hususani huduma ya urekebishaji wa wahalifu ambao ni zao la jamii yenyewe”. Alisema Jenerali Kasike.


  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Phaustine Kasike akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi(kushoto) alipotembelea ofinisi za Makao Makuu ya Magereza jijini Dar es salaam, leo Februari 25, 2019.


  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Phaustine Kasike akizungumza katika kikao na uongozi wa Benki ya NBC, uliomtembelea ofinisi kwake, Makao Makuu ya Magereza jijini Dar es Salaam Februari 25, 2019.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi(kushoto) akizungumza na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Phaustine Kasike alipokutananaye kwa mazungumzo juu ya kuangalia njia bora za kudumisha uhusiano baina ya Benki ya NBC na Jeshi la Magereza nchini, katika Makao Makuu wa Magereza, jijini Dar es Salaam, Februari 25, 2019. Wengine kulia ni Maafisa Waandamizi wa Bendi hiyo.

  Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Uwesu Ngarama(kulia) pamoja na Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Mhandisi, Tusekile Mwaisabila9kushoto) wakifuatilia mazungumzo hayo katika Ofisi ya Kamishna Jenerali wa Magereza nchini.

  Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(wa tatu toka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi(wa tatu toka kushoto) pamoja na Maafisa waandamizi wa Jeshi la Magereza na Benki ya NBC katika Makao Makuu wa Magereza, jijini Dar es Salaam, Februari 25, 2019(Picha na Jeshi la Magereza).

  0 0


  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ambae amepewa jukumu la kuwa Mwenyekiti wa kuongoza Kamati ya kuisaidia timu ya Taifa (Taifa Stars) kufuzu fainali za mataifa ya Africa (AFCON) leo amezindua rasmi kamati hiyo yenye wajumbe 14 ambapo amewaomba wananchi kuwa kitu kimoja katika kuisapoti timu hiyo.

  RC Makonda amesema majukumu makubwa 3 watakayoanza nayo Kama kamati ni Kuirudisha timu kwa wananchi, kuweka maandalizi mazuri ya timu na uwezeshaji wa timu. 

  Aidha RC Makonda amesema katika kikao cha Leo kamati imepanga kukutana na watu wa makundi mbalimbali wakiwemo Viongozi wa Dini, Wasanii, Wanasiasa, Wamiliki wa Vyombo vya Habari na wadau mbalimbali ili kwa pamoja tuiunge mkono timu ya Taifa. 

  Hata hivyo RC Makonda amesema kwa sasa timu ipo katika mikakati ya maandalizi ya Mechi ya mwisho dhidi ya Uganda itakayochezwa Machi 24.

  Kamati hiyo inaongozwa na RC Makonda ambae ni Mwenyekiti, Katibu wake akiwa ni Mhandisi Hersi Said ambapo Wajumbe wa kamati hiyo ni Mohamed Dewji, Haji Manara, Jerry Muro, Farouk Barhoza, Salim Abdallah, Mohamed Nassor, Patrick Kahemele, Abdallah Bin Kleb, Tedy Mapunda, Philimon Ntaihaja, Farid Nahid na Faraji Asas.

  TAIFA STARS TUNA KILA SABABU YA KUSHINDA.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu jukumu la kuwa Mwenyekiti wa kuongoza Kamati ya kuisaidia timu ya Taifa (Taifa Stars) kufuzu fainali za mataifa ya Africa (AFCON) ,ambapo leo amezindua rasmi kamati hiyo yenye wajumbe 14 ambapo amewaomba wananchi kuwa kitu kimoja katika kuisapoti timu hiyo.

  0 0

  Na Stella Kalinga, Simiyu
  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia  masuala ya watu wenye  ulemavu, Mhe.Stella Ikupa  ametoa wito kwa viongozi wa vyama vya watu wenye  ulemavu, kuwahamasisha wanachama wao kujiunga na  mfuko  wa afya ya jamii (CHF )ulioboreshwa ili waweze kupata uhakika wa matibabu.

  IKUPA ametoa wito huo  wilayani Itilima  katika ziara yake wakati akizungumza na viongozi wa Wilaya, Viongozi wa Vyama vya wenye ulemavu na  baadhi ya wenye ulemavu wenyewe wakati wa ziara yake wilayani humo Februari 25, 2019, ambayo ililenga kukagua utekelezaji wa maelekezo ya Serikali ikiwa ni pamoja na mradi wa Kitalu nyumba na masuala mbalimbali yahusuyo wenye walemavu.

  Amesema ni vema viongozi wa vyama na wenye ulemavu wakapena taarifa na kuhamasishani kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii(CHF) ulioboreshwa, ili wapewe vitambulisho waweze kutibiwa kirahisi.

  “Mkijiunga na CHF iliyoboreshwa mkapata kadi mtakuwa na uwezo wa kutibiwa muda wowote, kwa hiyo peaneni hizo taarifa mjiunge watu mnaofahamiana muweze kupewa hivyo vitambulisho mpate kutibiwa kirahisi wakati tukiwa tunasubiri ile bima ya afya kwa kila Mtanzania” alisema Mhe. Ikupa.

  Katika hatua nyingine amewaagiza maafisa Ustawi wa jamii na maendeleo ya jamii kutoa elimu vijijini kwa  watu wenye  ulemavu kuhusiana na  uundwaji wa vikundi na namna ya kutekeleza miradi mbalimbali.
  Mkuu wa Wilaya ya Itilima,Mhe.  Benson Kilangi  akizungumzia utekelezaji wa mradi wa kitalu nyumba amesema katika awamu ya kwanza jumla ya vijana 20 wamepata mafunzo ya utengenezaji wa vitalu nyumba na kufundishwa stadi mbalimbali za kuendesha kilimo biashara na kuongeza mnyororo wa thamani.
  Naye Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Festo Kiswaga amesema  miradi ya vitalu katika Mkoa wa Simiyu itatekelezwa kwa viwango na kwa malengo yaliyokusudiwa, huku akibainisha kuwa vitasaidia kuongeza kipato kwa wananchi katika mkoa  na kuwa sehemu ya wananchi kujifunza kilimo bora.
  Kwa upande wao viongozi pamoja na watu wenye ulemavu walioshiriki katika ziara hiyo wamemwomba Mhe. Naibu Waziri kushughulikia baadhi ya changamoto zinazowakabili katika maeneo yao.
  “Ninaomba Serikali itusaidie tuweze kupata wakalimani wa lugha ya alama ili na sisi walemavu wa kusikia tuweze kupata ujumbe unaokuwa unawasilishwa na viongozi wetu kwenye mikutano na ziara kama hii ya leo hii itatusaidia sana” alisema Mhandi Ntobi Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu wasiosikia Mkoa wa Simiyu.
  “NaombaWataalam waje watutembelee kwenye vijiji vyetu na kwenye vyama vyetu watusaidie kutupa elimu ya namna ya kuunda vikundi na namna ya kufanya shughuli zinazoweza kutuongezea kipato” Bw. Seni Jitabo mlemavu wa viungo Mkazi wa Zagayu wilayani Itilima.
  Naibu Waziri Ikupa, anaendelea na ziara yake Mkoani Simiyu ambayo itahitimishwa 27 Februari 2019, akiwa wilayani Itilima Naibu waziri ametembelea kitalu nyumba kilichopo Lagangabilili na kituo cha maarifa ya jamii Kanadi, ambako amejionea shughuli mbalimbali za uzalishaji zinazofanywa na vijana.
    Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi,Ajira na Wenye Ulemavu anayeshughulikia walemavu, Mhe. Stella Ikupa akizungumza jambo na Bw. Mhandi Ntobi ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Watu wasiosikia Mkoa wa Simiyu, wakati akiwa katika ziara yake Wilayani Itilima Mkoani Simiyu, Februari 25, 2019.
   Mbunge wa Jimbo la Bariadi, Mhe. Andrew Chenge akimweleza jambo Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi,Ajira na Wenye Ulemavu anayeshughulikia walemavu, Mhe. Stella Ikupa( wa pili kulia) alipotembea Ofisi za CCM Mkoa wa Simiyu wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu, Februari 25, 2019.
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi,Ajira na Wenye Ulemavu anayeshughulikia walemavu, Mhe. Stella Ikupa( katikati kwa walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu na watumishi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Mkoani Simiyu(NSSF na PSSSF) mara baada ya kutembelea ofisi za mifuko hiyo wakati wa ziara yake mkoani Simiyu , Februari 25, 2019.
   Bw. Seni Jitabo ambaye ni mlemavu wa Viungo akiwasilisha baadhi ya changamoto kwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi,Ajira na Wenye Ulemavu anayeshughulikia walemavu, Mhe. Stella Ikupa(hayupo pichani) wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu, Februari 25, 2019
   Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi,Ajira na Wenye Ulemavu anayeshughulikia walemavu, Mhe. Stella Ikupa akipokea zawadi ya sabuni kutoka kwa Afisa Vijana wa Wilaya ya Itilima ambaye alimkabidhi kwa niaba ya viongozi wa Wilaya hiyo wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu, Februari 25, 2019
  Moja ya Kitalu nyumba(green house) ikatika kata ya Lagangabilili wilayani Itilima, kilichotembelewa na  Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi,Ajira na Wenye Ulemavu anayeshughulikia walemavu, Mhe. Stella Ikupa wakati wa ziara yake.

  0 0

  NA LUSUNGU HELELA-WMU


  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ameshauri itungwe sheria ya kuhakikisha kila Halmashauri nchini inapanda miti milioni 1.5 kila mwaka ili kukabiliana na tatizo la uharibifu wa mazingira nchini

  Hatua hiyo inakuja baada ya agizo la Makamu wa Rais, Mhe.Samia Suluhu Hassan alilolitoa wakati alipokuwa akizindua kampeni ya kuifanya Dodoma kuwa ya kijani mwezi Disemba 2018 kuwa kila Halmashauri ihakikishe inapanda miti milioni 1.5 kila mwaka.

  Amesema hata hivyo tangu agizo hilo lilipotolewa hakuna Halmashauri hata moja iliyoweza kulitekeleza agizo hilo badala yake Halmashauri zilizo nyingi zimekuwa zikitaja takwimu za uongo.

  Akizungumza mbele ya Makamu wa Rais, Mhe.Samia Suluhu Hassan kwenye kongamano la kulinda Mazingira lililofanyika kitaifa mkoani Tabora, Mhe.Kanyasu ameshauri itungwe sheria itakayowabana Wakurugenzi kutekeleza agizo hilo.

  Amesema endapo agizo hilo likapitishwa na bunge na baadaye kuwa sheria Wakurugenzi watalazimika kupanda idadi hiyo ya miti badala ya ilivyo sasa kila Mkurugenzi kutekeleza agizo hilo kama hiyari.

  Ameeleza kuwa Halmashauri zilizo nyingi zimekuwa zikitaja takwimu kubwa za miti iliyopandwa lakini anapokwenda kwa ajili ya kuiona wmiti hiyo imekuwa haionekani na huku wengine wamekuwa wakiibuka na visingizio kwa vile hakuna idadi hiyo ya miti waliyoipanda.

  Amesema idadi ya miti ambayo imekuwa ikitajwa na Halmashauri kupandwa imekuwa ya vitabuni isiyo na uhalisia wa aina yoyote.Ameongeza kuwa hata zile Halmashauri ambazo zimekuwa zikijaribu kupanda zimekuwa hazifikishi idadi hiyo hata zikishapanda zimekuwa hazijishughulishi na kufuatia maendeleo ya miti hiyo.

  Amesema hali hiyo imepelekea miti iliyo mingi kufa kwa kukosa uangalizi huku mengine kuliwa na mifugo wakati Halmashauri hizo zimekuwa zikibaki na takwimu zile zile za miti waliyoipanda.

  Akizungumza Makamu wa Rais, Mhe.Samia Suluhu Hassani amesema agizo lake lililenga kila Halmashauri ipande miti milioni 1.5 ikiwa ni lazima na sio hiyari kama Halmashauri zinavyotekeleza.

  Hata hivyo, Mhe. Samia ameeleza kuwa katika agizo hilo lilikuwa wazi liikitaka kila Halmashauri ihakikishe inapanda miti ya aina yoyote ile akitolea mfano mizabibu, miti ya matunda ili mradi tu uwe mti bila kujali miti ya aina gani.

  Ameongeza kuwa kutokana na uharibifu mkubwa wa mazingira unaoendelea nchini, Ofisi yake itahakikisha taratibu zinafuatwa za kulifanya agizo hilo liwe sheria.
  Makamu wa Rais, Mhe.Samia Suluhu Hassan akimwagilia miti mara baada ya kuupanda mara baada ya kumalizika kwa kongamano la mazingira lililofanyika mkoani Tabora.
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akizungumza mbele ya Makamu wa Rais, Mhe.Samia Suluhu Hassan kuhusu umuhimu wa kutunga sheria ya kuzibana Halmashauri kupanda miti 1.5 kila mwaka ili kukabiliana na tatizo la uharibifu wa mazingira
  Makamu wa Rais, Mhe.Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Mawaziri na Manaibu Waziri pamoja na viongozi mbalimbali mara baada ya kongamano la mazingira lililofanyika mkoani Tabora.
  Makamu wa Rais, Mhe.Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja wananchi waliohudhuria kongamano la mazingira mkoani Tabora
  Miongoni mwa wachangiaji katika kongamano la Mazingira, Juma Elias akitoa mchango wa mawazo wa namna ya kulinda mazingira kutokana na uharibifu mkubwa wa mazingira unaotokana na ukataji miti ovyo mkoani Tabora.( PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA- MNRT)

  0 0


  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

  KATIBU Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Hassan Mwinyimvua ametembelea Kituo cha kufua umeme wa Gesi Asilia Kinyerezi I na Kinyerezi II jijini Dar es Salaam.

  Lengo la ziara yake alisema ni kuangalia maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya Kinyerezi II na ule wa upanuzi wa Kinyerezi I (Kinyerezi I expansion)

  Mradi wa Kinyerezi II ambao unazalisha kiasi cha Megawati 240 tayari umekamilika na umeme umekwishaingizwa kwenye Gridi ya Taifa, wakati ule.

  “Tunashukuru kwamba tunaenda vizuri hasa Kinyerezi II ambayo kiukweli mradi umeshamalizika sasa hivi tunapata umeme kilichobaki ni masuala ya kuweka kila kitunsawa baina ya Mkandarasi na wataalamu wetu.” Alisema Dkt. Mwinyimvua baada ya kupokea taarifa ya miradi hiyo miwili toka kwa Meneja Miradi wa Shirika la Umeme Nchini TANESCO, Mhandisi Stephene Manda.

  Alisema kwa upande wa mradi wa upanuzi Kinyerezi I, (Kinyerezi I extension) kazi imeanza ingawa kulikuwepo na ucheleweshwaji wa vifaa bandarini na kuagiza uongozi wa TANESCO kukutana na taasisi zinazohusika na masuala ya kodi na utoaji mizigo bandarini ili kupanga utaratibu wa jinsi ya kulipa kodi mbalimbali bila ya kuathiri utoaji wa mizigo hiyo (vifaa na mitambo) bandarini.

  “Nakumbuka mlipewa wito na Mheshimiwa Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akiwataka mjitahidi isifike mwezi wa nane, ikiwezekana hata mwezi wa tano muwe mmemaliza kazi.” Alisema.

  Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu alifuatana na Kamishna wa Nishati kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Innocent Luoga wakati kwa upande wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO, waliongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Dkt. Tito Mwinuka.

  Akitoa taarifa kwa Katibu Mkuu na ujumbe wake, Meneja Miradi wa TANESCO, Mhandisi Stephene Manda, alisema wakati Mradi wa Kinyerezi II Megawati 240 ambao umekamilika tangu Desemba mwaka jana (2018), mradi wa Kinyerezi I ambao unafanya kazi una Megawati 150 na ule wa kufanya upanuzi (Kinyeerzi I extension) utakuwa na Megawati 185 na kazi tayari imefikia asilimia 76%

  “Tunategemea mtambo wa kwanza wa mradi huu wa upanuzi tutakuwa tumeuwasha ifikapo mwezi Mei, 2019 na kukamilika kabisa kwa mradi mzima itakuwa Agosti 2019.” Alibainisha Mhandisi Manda na kuongeza Jumla ya umeme utakaokuwa unazalishwa hapa Kinyerezi kufikia Agosti mwaka huu itakuwa Megawati 575.” Alisema

  Akifafanua zaidi alisema kutoka pale Kinyerezi I Extension tutakuwa na extension ndogo ya kutoa umeme kwa ajili ya mradi wa SGR.
  Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Hassan Mwinyimvua (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Dkt. Tito Mwinuka (kulia), wakiongozwa na Meneja Miradi wa Shirika hilo. Mhandisi Stephene Manda (kushoto), wakati Katibu Mkuu akikagua maendeleo ya mradi wa upanuzi wa kituo cha kufua umeme wa Gesi Kinyerezi I (Kinyerezi I expansion), jijini Dar es Salaam, Februari 25, 2019.
  Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Hassan Mwinyimvua (watatu kulia), Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga, (watano kulia), na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Dkt. Tito Mwinuka (wapili kulia), wakiongozwa na Meneja Miradi wa Shirika hilo. Mhandisi Stephene Manda (aliyenyoosha mikono) wakati Katibu Mkuu akikagua maendeleo ya mradi wa upanuzi wa kituo cha kufua umeme wa Gesi Kinyerezi I (Kinyerezi I expansion), jijini Dar es Salaam, Februari 25, 2019. 
  Katibu Mkuu pia alijionea kituo cha kupokelea gesi kikiwa tayari kwenye eneo la mradi huo. 
  KATIBU Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Hassan Mwinyimvua, akipatiwa maelezo.
  Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga(kushoto), akiwa na Mkandarasi eneo la mradi.
  Katibu Mkuu Dkt. Mwinyimvua na ujumbe wake wakimsikiliza mkandarasi anayetekeleza mradi wa upanuzi Kinyerezi I, kuhusu mwenendo wa mradi huo.
  Kiongozi wa zamu wa chumba cha udhibiti mitambo, kwenye mradi wa umeme wa gesi Kinyerezi II, Mhandisi Chidololo Enzi, (kulia) akitoa maelezo mbele ya Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Hamisi Hassan Mwinyimvua (katikati), alipotembelea kujihakikishia kukamilika kwa mradi huo unaozalisha Megawati 240.
  Kiongozi wa zamu wa chumba cha udhibiti mitambo, kwenye mradi wa umeme wa gesi Kinyerezi II, Mhandisi Chidololo Enzi, (kulia) akitoa maelezo mbele ya Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Hamisi Hassan Mwinyimvua(kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Dkt. Tito Mwinuka (wapili kushoto).
  Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Hassan Mwinyimvua (wapili kushoto), Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga, (wakwanza kushoto), na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Dkt. Tito Mwinuka (wapili kulia), wakiongozwa na Meneja Miradi wa Shirika hilo. Mhandisi Stephene Manda (aliyenyoosha mkono) wakati Katibu Mkuu akikagua maendeleo ya mradi wa Kinyerezi II jijini Dar es Salaam Februari 25, 2019 ambapo alielezwa kuwa tayari umekamilika.



  Hii ndiyo Kinyerezi II kama inavyoonekana Februari 25, 2019 wakati wa ziara ya Katibu Mkuu Nishati, Dkt. Mwinyimvua.













  0 0

  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina akifungua mkutano wa Jukwaa la Kimataifa la Maziwa uliofanyika jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Serena. Mkutano huo ulishirikisha wadau wakubwa wa sekta ya maziwa kutoka nje na ndani ya nchi. 
  Meneja Mwandamizi Biashara ya Kilimo, Huduma ya Ushauri na Utafiti wa Benki ya NMB akizungumza kwenye mkutano wa Jukwaa la Kimataifa la Maziwa uliofanyika jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Serena. 
  Baadhi ya viongozi wa Jukwaa la Kimataifa la Maziwa wakiwasilisha mada kwenye mkutano huo ulishirikisha wadau wakubwa wa sekta ya maziwa kutoka nje na ndani ya nchi. 
  Baadhi ya viongozi wa Jukwaa la Kimataifa la Maziwa wakiwasilisha mada kwenye mkutano huo ulishirikisha wadau wakubwa wa sekta ya maziwa kutoka nje na ndani ya nchi. 


  BENKI ya NMB kwa kushirikiana na Jukwaa la Kimataifa la Maziwa na wadau wengine wameungana kukutanisha wadau wa sekta ya maziwa ili kuangalia namna ya kukuza uzalishaji, uchakataji na matumizi maziwa hususani nchini Tanzania.

  Wadau hao zaidi ya 150 kutoka nchi mbalimbali na Tanzania wanakutana kwa siku mbili mfululizo kuangalia namna bora ya kuifanya sekta ya maziwa kufanya vizuri zaidi na kushiriki katika kupunguza umasikini kwa jamii zinazozalisha bidhaa hiyo.

  Benki ya NMB imetumia zaidi ya shilingi bilioni 100 kwa ajili ya mikopo kwa wakulima mbalimbali ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali kuinua kilimo ikiwemo sekta ya maziwa nchini.

  Kwa upande wake Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina akizindua mkutano huo leo jijini Dar es Salaam, aliishukuru NMB kwa kukutanisha wadau hao kujadili namna bora ya kuinua sekta hiyo nchini Tanzania.
  Baadhi ya wadau wa sekta ya maziwa kutoka nchini Tanzania wakizungumza katika mkutano huo. 
  Sehemu ya wadau wakubwa wa sekta ya maziwa kutoka nje na ndani ya nchi wakishiriki katika mkutano huo. 
  Sehemu ya wadau wakubwa wa sekta ya maziwa kutoka nje na ndani ya nchi wakishiriki katika mkutano huo.

  0 0

   Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kihuwe, Wilaya ya Nachingwea, Mkoa wa Lindi, Februari 25, 2019, akiwa katika ziara ya kazi, ambapo pia aliwasha rasmi umeme katika kijiji hicho.

   Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (mwenye kinasa sauti) akifurahi pamoja na wananchi wa kijiji cha Kihuwe, Wilaya ya Nachingwea, Mkoa wa Lindi, Februari 25, 2019, mara baada ya kuwasha rasmi umeme katika kijiji hicho.

   Sehemu ya umati wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Namatula, iliyopo wilayani Nachingwea, Mkoa wa Lindi, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani), alipokuwa akizungumza nao, kabla ya kuwasha rasmi umeme katika shule hiyo, Februari 25, 2019.

   Baadhi ya wataalamu kutoka Wizara ya Nishati, TANESCO na REA wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Muungano, wilayani Nachingwea, Mkoa wa Lindi, Februari 25, alipokuwa katika ziara ya kazi ambapo aliwasha rasmi umeme katika kijiji hicho.

   Mmoja wa wakazi wa Kijiji cha Kihuwe, wilayani Nachingwea, Mkoa wa Lindi, Samwel Ndungo akiuliza swali na kueleza changamoto kwa Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani), alipofika katika kijiji hicho kuwasha rasmi umeme na kuzungumza na wananchi, akiwa katika ziara ya kazi, Februari 25, 2019.

   Mmoja wa wakazi wa Kijiji cha Kihuwe, wilayani Nachingwea, Mkoa wa Lindi, William Hassan akiuliza swali na kueleza changamoto kwa Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani), alipofika katika kijiji hicho kuwasha rasmi umeme na kuzungumza na wananchi, akiwa katika ziara ya kazi, Februari 25, 2019.
   Mmoja wa wakazi wa Kijiji cha Kihuwe, wilayani Nachingwea, Mkoa wa Lindi, Matthew Ntunga akiuliza swali na kueleza changamoto kwa Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani), alipofika katika kijiji hicho kuwasha rasmi umeme na kuzungumza na wananchi, akiwa katika ziara ya kazi, Februari 25, 2019.

   Sehemu ya umati wa wananchi wa kijiji cha Mapochelo, Wilaya ya Nachingwea, Mkoa wa Lindi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji hicho, Februari 25, 2019 alipokuwa katika ziara ya kazi ambapo pia aliwasha rasmi umeme katika kijiji hicho.



  Na Veronica Simba – Nachingwea
  Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amewataka wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini kutumia busara katika kazi hiyo ili iwaongoze kufanya maamuzi sahihi hususan uunganishaji umeme katika taasisi na miradi ya umma.
  Alitoa wito huo kwa nyakati tofauti jana, Februari 25 mwaka huu, akiwa katika ziara ya kazi wilayani Nachingwea, Mkoa wa Lindi.
  Akizungumza ofisini kwa Mkuu wa Mkoa na baadaye katika vijiji vya Kihuwe, Muungano na Mapochero, ambavyo aliviwashia umeme rasmi; Naibu Waziri alisisitiza kuwa pamoja na kila mkandarasi kuwa na wigo wa eneo analopaswa kuunganisha umeme, lakini siyo busara kwake kuruka taasisi za umma na miradi muhimu kama vile ya maji, afya na mingineyo kwa sababu tu iko nje ya wigo.
  “Unafika eneo, unaona Zahanati ile pale, akina mama wanajifungua gizani; Shule ile pale, kuna hosteli, unaziachaje bila umeme sababu tu hazipo ndani ya wigo! Mkandarasi unapaswa kutumia busara, ikibidi tuandikie sisi Serikali, tuone namna gani gharama husika zitalipwa ili maeneo kama hayo yasikose umeme,” alisema.
  Katika hatua nyingine, Naibu Waziri alisema kuwa serikali inaendelea kujivunia kugundulika kwa gesi katika mikoa ya kusini na kwamba watanzania wanapaswa kufahamu kwamba serikali imedhamiria kuitumia ipasavyo.
  Akifafanua, alisema gesi inapaswa itumike katika viwanda vya mbolea, majumbani na katika kuzalisha umeme. Hivyo, aliwataka wananchi kupuuza maneno yanayosemwa na baadhi ya watu kuwa serikali haitoi tena kipaumbele kwa gesi iliyogunduliwa mikoa ya kusini.
  Naibu Waziri alifafanua zaidi kuwa, ili kupata umeme mwingi, wenye bei nafuu na wa uhakika; ni lazima serikali ihakikishe inatumia vyanzo mbalimbali vya kuzalisha umeme ikiwemo maji, upepo, jua, gesi, tungamotaka na vinginevyo.
  “Ndiyo maana tunaanzisha miradi mbalimbali ya kuzalisha umeme ambayo inatumia vyanzo mbalimbali, siyo gesi peke yake. Ni muhimu mkalitambua hilo kwamba, kama nchi, hatuwezi kutumia gesi peke yake katika kuzalisha umeme, tukaacha vyanzo vingine. Inabidi tutumie vyanzo vyetu vyote tulivyojaaliwa na Mungu.”
  Akizungumzia utekelezaji wa miradi ya kupeleka umeme maeneo mbalimbali ya nchi hususan vijijini, Naibu Waziri alisema kazi hiyo inaendelea kufanyika  kwa ufanisi ambapo sasa serikali imewaelekeza wakandarasi wa miradi hiyo kuhakikisha wanawasha umeme katika vijiji vitatu kila wiki kwa kila mkandarasi.
  Hata hivyo, aliwataka wananchi kuwa na subirá kwani kazi ya kuunganisha umeme inatekelezwa hatua kwa hatua.
  Naibu Waziri anaendelea na ziara yake mkoani Lindi ambapo amefuatana na wataalamu mbalimbali kutoka wizarani, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

  0 0


  Jumla ya  wanafunzi 52  wa stashahada ya ualimu kutoka katika chuo cha ualimu cha Monduli wamefika   katika ofisi za  Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania, Makao Makuu Njiro Arusha  kwa lengo la kujifunza kwa vitendo masuala mbali mbali ya kisayansi ambayo wamekuwa wakiyasoma katika nadharia.

  Lengo la ziara hii ya siku moja kwa wanafunzi hawa ni kujifunza ili kufahamu dhana nzima ya juu ya matumizi salama ya mionzi na namna udhibiti unavyofanyika na wao kuwa mabalozi wazuri katika uhamasishaji wa matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia.

  Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Profesa Lazaro Busagala amewaeleza wanafunzi hao kuwa elimu waliyoipata katika ziara hii ya mafunzo itawawezesha kuelewa matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia na kujilinda na mionzi pindi watakapokuwa wakitekeleza majukumu yao ya kikazi hapo baadaye.

  Kiongozi wa wanafunzi hao Mwalimu  Sikana Menard ameeleza kuwa ziara hiyo imewasaidia wanafunzi hao ambao ni walimu watarajiwa hapo baadae katika masomo ya sayansi kuwa wamepata  elimu kubwa kuhusiana na masuala ya mionzi.

  Amesema wamekuwa wakiwafundisha wananfunzi kwa njia ya nadharia tu hivyo kwa kutembelea kwenye Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania kutawasaidia sana kujionea teknolojia mbali mbali katika maabara za TAEC zenye ubora wa hali ya juu kwa ajili ya mafunzo.

  Aidha TAEC inaendelea kuwakaribisha wananchi, wanafunzi na wadau mbalimbali ili kujipatia elimu na kujifunza masuala tofauti tofauti yanayohusu udhibiti salama wa mionzi na  matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia  hapa nchini.

  Imetolewa na;


  Peter G. Ngamilo
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
  Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu Profesa Zhao Yuanil kutoka Hospitali ya Kimataifa ya Chuo Kikuu cha Peking cha Beijing nchini China mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika Mazungumzo na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu Profesa Zhao Yuanil kutoka Hospitali ya Kimataifa ya Chuo Kikuu cha Peking cha Beijing nchini China aliyeambatana na ujumbe wake pamoja na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Profesa Lawrence Maseru na Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Respicious Boniface Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu Profesa Zhao Yuanil kutoka Hospitali ya Kimataifa ya Chuo Kikuu cha Peking cha Beijing nchini China wanne kutoka kulia, Balozi wa China hapa nchini Wang Ke watatu kutoka kulia pamoja Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Respicious Boniface. Wengine katika picha ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, Balozi Zuhura Bundala pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Profesa Lawrence Maseru.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu Profesa Zhao Yuanil kutoka Hospitali ya Kimataifa ya Chuo Kikuu cha Peking cha Beijing China wanne kutoka kulia mara baada ya kumaliza kupiga picha ya kumbukumbu Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi zawadi ya Kinyago Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo  na Mishipa ya Fahamu Profesa Zhao Yuanil kutoka Hospitali ya Kimataifa ya Chuo Kikuu cha Peking cha Beijing China mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Balozi wa China hapa nchini Wang Ke akishuhudia.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa China hapa nchini Wang Ke mara baada ya kumaliza mazungumzo na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo  na Mishipa ya Fahamu Profesa Zhao Yuanil kutoka Hospitali ya Kimataifa ya Chuo Kikuu cha Peking cha Beijing China. PICHA NA IKULU

  0 0



  Na; OWM (KVAU) - SONGWE

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amewataka vijana nchini kuchangamkia fursa zilizopo kwenye maeneo yao kwa kuanzisha vijiwe vya kiuchumi.

  Kauli hiyo ameitoa na Waziri Mhagama wakati akiwa kwenye ziara ya kukagua maendeleo na miradi ya vijana iliyopo katika Kituo cha Maendeleo ya Vijana, Sasanda kilichopo Kata ya Nyimbili, Mkoani Songwe.

  Akiwa katika ziara hiyo Mhe. Mhagama alieleza kuwa, Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli imeendelea kutimiza azima yake ya ujenzi wa uchumi wa viwanda, hivyo vijana watumie fursa hiyo kujifunza mambo muhimu na kuanzisha viwanda vidogo vidogo ambavyo vitawafanya wabadilishe vijiwe wanavyokaa kuwa vya kiuchumi.

  “Tunataka kuona vijana watakapo jifunza kilimo bora, ufugaji wa ng’ombe au nyuki wataweza kuboresha thamani mazao na bidhaa kwa kuanzisha viwanda vidogo ndani ya Mkoa wa Songwe, mkakati wetu katika kituo hiki ni kutoa mafunzo yatakayowawezesha vijana kuongeza thamani ya mazao na bidhaa watakazozalisha ambazo zitakuwa ni kichocheo muhimu katika kufikia maendeleo yao” alisema Mhagama

  Aliongeza kuwa, Takribani vijana 500 kwenye kituo hicho wamejifunza stadi za maisha, ufundi na elimu mbalimbali zinazotolewa kwenye kituo ambazo zitawawezesha kujipatia kipato.

  Sambamba na hilo, Mhe. Mhagama aliwahimiza Viongozi wa Mkoa kushirikiana na Ofisi yake ili waweze kuwasaidia vijana ambao wamekwisha anzisha viwanda vidogo vidogo ndani ya mkoa huo kwa kuwawezesha kuzalisha bidhaa zenye ubora na kuwatafutia soko la uhakika ndani na nje ya nchi.

  Aidha, Waziri Mhagama alitoa rai kwa vijana kujiunga kwenye vikundi ambavyo ni endelevu na vyenye muelekeo wa kuanzisha viwanda vidogo vitakavyowawezesha kujiajiri na kuajiri wenzao na pelekea kufikia uchumi wa kati kama mpango wa maendeleo wa taifa unavyoelekeza.

  Pia, aliwaelezea juu ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru ambazo zitafanyika katika Mkoa huo na kuwataka vijana na wanawake kutumia fursa hiyo kuutangaza vyema mkoa wa Songwe.

  Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana, Bw. James Kajugusi alieleza kuwa kituo cha Maendeleo ya Vijana cha Sasanda kimewawezesha vijana kujitambua na kujiwekea malengo ya maisha na kuyatekeleza kwa faida yao, jamii na taifa kwa ujumla.

  “Tunatarajia kuanzisha mafunzo na programu zitakazowaelekeza vijana masuala ya kilimo biashara ambacho kitasaidia upatikanaji wa malighafi zitakazokuwa zinahitajika kwenye viwanda vilivyopo nchini,” alisema Kajugusi

  Naye Bw. Silia Kibona ambaye ni mnufaika kupitia kituo hicho, aliishukuru Serikali kwa kuwajengea mazingira ya kujifunzia ambayo yamewasaidia kupata mafunzo muhimu na aliwahamasisha vijana wenzie kuhudhuria mafunzo yanayotolewa kwenye kituo hicho.

  Kituo cha Maendeleo ya Vijana – Sasanda kilianzishwa mwaka 1979 kwa ushirikiano wa Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni wa Taifa, Vijana na Michezo iliyopo wakati huo pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya. Uanzishaji wa Kituo hicho ulifuatia kuanzishwa kwa mpango wa kuunda vikundi vya vijana vya uzalishaji mali, uliolenga kuwawezesha vijana wasio na ajira kuweza kujiunga na kufanya kazi za kujitegemea hasa katika sekta ya kilimo. 

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na vijana wanaopata mafunzo ya kilimo bora na ufugaji wa kisasa katika kituo cha Maendeleo ya Vijana – Sasanda kilichopo Kata ya Nyimbili, Mkoani Songwe alipofanya ziara kukagua maendeleo na miradi ya vijana katika kituo hicho.


  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (katikati) akimwagilia maji mti alioupanda katika kituo hiko cha Sasanda alipofanya ziara katika kituo hicho kukagua maendeleo na miradi ya vijana. (Kushoto) ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe Bi.  Tusubileghe Benjamin na (Kulia) ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi.

  Bw. Zawadi Mdolo akimueleza jambo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama kuhusu mafunzo wanayopatiwa katika shamba darasa juu ya kulima bora na upatikanaji mazao mengi. (Mwenye miwani) ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Brigedia Jenerali (Mst.), Nicodemus Mwangela.

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akioneshwa na kupata maelezo ya vifaa vinavyotumiwa na vijana wa kituo cha Sasanda katika shughuli ya kuvua samaki.

  Bw. Lusekelo Mbukwa akimueleza jambo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama kuhusu majani wanayotumia kwa ajili ya malisho ya ng’ombe yanayosaidia ukuaji bora wa mifugo hiyo na upatikanaji wa maziwa mengi.

  Bi. Oliveta Mwashilindi akimueleza jambo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama kuhusu bidhaa ya asali inayotengenezwa na kikundi cha vijana cha Maisha Daily kilichopata mafunzo ya ufugaji nyuki katika kituo cha Sasanda.

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wanakikundi cha Rasupashoma Group, Bw. Ibrahim Malabela jinsi wanavyotengeneza viatu bora na vyenye kudumu kwa muda mrefu. (Mwenye miwani ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Brigedia Jenerali (Mst.), Nicodemus Mwangela na (Kulia) ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi.

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na vijana walionufaika kupitia kituo cha maendelo ya vijana, Sasanda alipotembelea kuona mradi walioanzisha katika Kata ya Nyimbili. (Wenye miwani) ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Brigedia Jenerali (Mst.), Nicodemus Mwangela.
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Brigedia Jenerali (Mst.), Nicodemus Mwangela mara baada ya kumaliza ziara yake ya kukagua maendeleo na miradi ya vijana katika kituo cha Sasanda.
   Muonekano wa shamba darasa moja wapo lililopo katika Kituo cha Maendeleo ya Vijana cha Sasanda Mkoani Songwe.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewasili mkoani Shinyanga tayari kwa ziara ya kikazi ya siku 5. Makamu wa Rais ambaye amesafiri kwa njia ya barabara akitokea mkoani Tabora ambapo napo alikuwa na ziara yenye lengo la kuhamasisha na kukagua shughuli za kimaendeleo.

  Mara baada ya kuwasili mkoani Shinyanga Makamu wa Rais alitembelea kituo cha Afya cha Samuye na kupata nafasi ya kuzungumza na wananchi wa eneo hilo. “Serikali ina kila nia ya kusogeza huduma za afya bora kwa wananchi”alisema Makamu wa Rais.

  Aidha aliwaambia wananchi hao kuwa Serikali inakuja na sheria ya mpango wa bima za afya kwa wote ambayo itamuhitaji kila mtanzania kuwa na bima ya afya. Makamu wa Rais amewataka wakazi wa kata ya Samuye kushirikiana katika kuzuia mimba za utotoni kwani kwa kiasi kikubwa zinahatarisha maisha ya watoto wa kike.

  Kwa upande wake Naibu Waziri TAMISEMI Mwita Waitara amesisitiza Halmashuri kutenga asilimia 40 kwa ajili ya miradi ya maendeleo na kuzitaka halmashauri zote kumalizia maboma ya zahanati wakati serikali kuu inaleta pesa za kumalizia maboma ya shule na madawati.

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Telack (kulia) mara baada ya kuwasili katika kituo cha afya Samuye mkoani Shinyanga. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko (kulia) mara baada ya kuwasili katika kituo cha afya Samuye mkoani Shinyanga. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa Kata ya Samuye mara baada ya kutembelea na kukagua  kituo cha afya Samuye mkoani Shinyanga, kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Telack na kushoto ni Naibu Waziri TAMISEMI Mwita Waitara. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wananchi wa kata ya Tinde waliojitokeza kumlaki wakati akiwasili mkoani Shinyanga akitokea mkoani Tabora. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)


  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kabla ya mazungumzo, Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Februari 26, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (katikati) na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga, Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Februari 26, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Mshindi wa sh milioni tano kutoka kwenye kinyang'iro cha babati nasibu ya Biko anayejulikana kama Felista Fabian Halagi wa Mbulu, mkoani Manyara, akiwa bank katika makabidhiano ya fedha zake alizoshinda kutoka Biko, mchezo wa kubahatisha unaotamba katika viunga mbalimbali vya nchi yetu huku washindi sita kila jumatano na Jumapili wakipatikana na kushinda mamilioni na bodaboda kila siku. Picha na Mpigapicha Wetu.
  Mshindi wa sh milioni tano wa Biko kutoka Mbulu, mkoani Manyara, Felista Fabian amekabidhiwa fedha zake baada ya kushinda kutoka Biko.


  0 0

  Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga (wa pili kushoto) akikata utepe kuzindua rasmi moja kati ya Matrekta mapya ya ya Sonalika, yanayosambazwa na Kampuni ya Rellance, wakati wa hafla fupi ya uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam, leojana. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo (kulia) ni Meneja Masoko, Sajal Bagga na Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Stephen Mloshi. Picha na Mafoto Media.
  Furaha baada ya uzinduzi huo....
  WAZIRI wa Kilimo, Japhet Hasunga, akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi huo.
  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo, akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo.
  Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Stephen Mloshi, akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo.




  Sehemu ya washiriki katika hafla ya uzinduzi huo.

  Wawakilishi wa benki ya CRDB waliohudhuria hafla hiyo wakitambulishwa.

  Waziri akimpongeza mmoja wa wakulima walionufaika na Matrekta hayo.... kutoka Mbinga
  Waziri akionyesha zawadi aliyokabidhiwa na mkurugenzi wa kampuni hiyo (kushoto).
  Picha ya pamoja baada ya uzinduzi


  Waziri katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo.

  0 0

  Na Sylvester Raphael
  Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti amemaliza mgogoro wa wakulima na wafugaji uliodumu kwa zaidi ya miaka kumi na moja katika Kijiji cha Kahundwe kata Chanika Tarafa Kituntu Wilayani Karagwe,baada ya kukutana nwa wananchi wa kijiji hicho na kutoa msimao wa Serikali na kuonya juu ya uvunjifu wa amani uliowahi kutokana na mgogoro huo mwaka 2008.
  Awali kabla ya kwenda Kijijini Kahundwe Februari 26, 2019 kuwasikiliza wananchi hao wakulima (wavamizi) na Wafugaji na kumaliza mgogoro huo Mkuu wa Mkoa Gaguti aliunda timu ya wataalam kupitia nyaraka mbalimbali kuhusu kijiji hicho na kuwasikiliza wananchi pande zote mbili ili kubaini ukweli na chanzo cha mgogoro ambapo timu hiyo ilifanya kazi yake na kuwasilisha majibu kwake.
  Mkuu wa Mkoa Gaguti baada ya kupitia taarifa ya timu aliyoiunda na kuwasili Kijijini Kahundwe na kusikiliza pande zote mbili za Wakulima (Wavamizi) na wafugaji aliwaeleza wananchi hao kuwa tayari Serikali ilishabaini ukweli wa ni nani mmiliki halali wa eneo hilo la Kijiji cha Kahundwe kati ya Wakulima na Wafugaji.
  “Mwaka 1987 mamlaka za vijiji vinne zilikaa na kukubaliana kutenga eneo la kufugia  mifugo yao na lilitengwa eneo la Kijiji Kahundwe kuwa eneo la wafugaji na kusajiliwa kisheria, lakini kuanzia mwaka 2008 hadi 2015 baadhi ya wananchi kutoka maeneno mengine walivamia eneo hilo na wavamizi sita walikamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria na kupatikana na hatia na kufungwa jera miezi sita kila mmoja.” Alieleze Mkuu wa Mkoa Gaguti.
  Mkuu wa Mkoa Gaguti aliendelea kuwaeleza wananchi kuwa tangu wakati huo kumekuwa na uvamizi wa wakulima kutoka nje ya Kijiji hicho na kuleta mgogogro mkubwa kati yao na wafugaji. Aidha, alisema kuwa Serikali tayari imebaini ukweli wa uhalali wa nani anatakiwa kuwa katika eneo hilo na itasimamia ukweli huo wa mwaka 1987  na kama kutakuwa kuna wananchi wanataka mabadiliko wafuate sheria kama wenzao walivyofanya katika kutenga eneo hilo kuwa la wafugaji.
  “Hapa hakuna mgogoro wa ardhi bali ni uvunjifu wa sheria tu, nitahakikisha namaliza uvunjifu huu kuanzia sasa na sitaki kusikia jambo hili linaendelea. Lengo la kuja hapa ni kusimsmia msimamo wa Serikali kwa njia ya amani na utulivu. Natambua kuwa kuna wakazi au wafugaji 200 lakini 43 kati ya hao ni wavamizi si wenyeji nataka jambo hilo liishe mara moja.” Alitoa msimamo wa Serikali Mkuu wa Mkoa Gaguti.
  MAAGIZO
  Mkuu wa Mkoa Gaguti alimwagiza na kumpa wiki moja  Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Godfrey Mheluka kuanzia tarehe 27/02/2019  kufanya uhakiki na utambuzi wa wafugaji wadogo ambao walisajiliwa katika Kijiji hicho cha Kahundwe na kuwaondoa wavamizi ambao ni wakulima na wafugaji wakubwa waliotoka maeneo mengine.
  Pili Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Godfrey Mheluka na timu yake wafanye uhakiki wa mifugo ili kubaini wafugaji ambao kwanza si raia wa Tanzania na pili kubaini wingi wa mifugo kusudi kama kuna wafugaji wakubwa wenye mifugo mingi waondolewe ili wafuate sheria za kuomba vitalu vya kufugia kama wafugaji wakubwa au wawekezaji katika vitalu.
  Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Kahundwe walimweleza Mkuu wa Mkoa wa Kagera kuwa mgogoro huo unachochewa na Diwani wa Kata ya Chanika kwasababu wakati wa Kampeini ya mwaka 2015 aliwahidi baadhi ya wananchi hao wavamizi kuwa akipata madaraka atahakikisha wanalichukua eneo la Kijiji cha Kahundwe kama eneo lao la kilimo.
  Naye Bw. Bernard Sau Afisa Ardhi Wilaya ya Karagwe akitoa maelezo mbele ya Mkuu wa Mkoa Gaguti alisema kuwa kijiji cha Kahundwe kilisajiliwa mwaka 1987 kwa GN namba 620 kama Kijiji cha wafugaji na wakati huo ilikuwa Wilaya moja ya Karagwe kabla ya kutengwa Wilaya mbili za (Karagwe na Kyerwa) na baada ya kutenga Wilaya mbili kijiji cha Kaundwe kilibaki Wilaya ya Karagwe na kijiji hicho kina jumla ya Hekta 20,000 za kufugia. 

  0 0


  Mgeni rasmi wa uzinduzi wa Usajili wa vyeti vya Ndoa na safari za Ibada ya Hijja Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela wa pili kutoka kushoto, kaimu sheikhe wa Mkoa huo alhaji sheikhe Hasan Kabeke wakiomba dua iliyoongozwa na Mjumbe wa Baraza la Ulamaa Ali Hamis Ngeruko (kulia) baada ya Mkuu huyo wa Mkoa kuzindua mkakati huo juzi

  ………………….

  NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA

  IBADA ya Hijja nchini Saudi Arabia imeibua fursa za kibiashara kwa Watanzania hivyo wanatakiwa kuchangamkia ili wanufaike kiuchumi.

  Hayo yalielezwa juzi jijini Mwanza na Mjumbe wa Baraza la Ulamaa la Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Ali Hamis Ngeruko wakati wa uzinduzi wa elimu ya Hijja na Usajili wa Vyeti vya Ndoa kwa waumini wa dini ya kiislamu uliofanyika kitaifa jijini humu.

  Alisema Ibada hiyo ya Hijja ni jambo linalohitaji elimu kwa kuwa giza haliwezi kuongoza jambo, hivyo ufinyu wa elimu husababisha watu wengi kuharibu mengi ukiwemo uhusiano wao kwa ujinga na wengine huendelea kuharibu.

  Alieleza kuwa soko hilo lililopo Mina huko Makka kuna fursa ya soko la kimataifa la mifugo, vyakula, mikeka na tasbihia lakini bado Watanzania hawajalitambua wala kufikiria kutumia fursa hizo kibiashara zilizopo kwenye mji huo Mtakatifu wakati wa Ibada ya Hijja na kunufaika kiuchumi.

  “BAKWATA Taifa imeona izindue elimu ya Ibada ya Hijja Mwanza na kila mkoa utafanya kazi hiyo , utasimamia na kuelimisha waumini.Pia Uhusiano na ushirikiano wa Serikali na BAKWATA upo kwenye mambo mbalimbali japo baadhi ya watu wanaweza kuona uzinduzi wa elimu ya Hijja una uhusiano gani au hauna uhusiano,” alisema.

  Nguruko alieleza zaidi kuwa Tanzania imejaaliwa madini na vito yanayotumika kutegeneza tasbihi, wana mifugo na nguo (vitenge) hivyo Watanzania wakiitumia fursa hiyo wataingiza fedha nyingi za kigeni kutokana na kuuza bidhaa za aina hiyo Makka lakini wamelalia soko hilo.

  “Watanzania tutanufaika na mengi kwani Makka si ibada tu, kuna biashara inafanyika pia na kwa kuwa tunayo mikeka, vitenge, madini na mifugo na mchele bado soko hilo hatujaliona na haliwezi kutambuliwa bila kutambulishwa.Hivyo watu wawe na maarifa na hijja yao pamoja na neema watumie fursa zilizopo Makka,”alisema mjumbe huyo wa baraza la Ulamaa.

  Kwa mujibu wa Nguruko waumini wanaokwenda kuhiji wanatakiwa kuchangamkia fursa za soko la Makka ambalo raia wengi wa nchi za Afrika Magharibi (Nigeria, Cameroon na Senegal) ndio pekee wamelitumia kwa uchumi wa nchi zao na mtu mmoja mmoja kunufanika nalo kwa kupeleka na kuuza bidhaa zao huko.

  Kwamba tasbihi , mikufu, mikeka na vitenge ni ubunifu wa watu wa mataifa hayo ambao umewanaingizia vipato vizuri kupitia Makka huku biashara ya mifugo na mchele ikifanywa na raia wa kutoka Thailand na Australia na kuhoji “ sidhani kama Watanzania tunalitambua soko hilo , tumelala na mifugo yetu na mchele.”a

  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela ambaye mgeni rasmi alisema hakuwahi kufikiria fursa za kiuchumi kwenye Hijja hivyo Watanzania wazione, wajue watanufaika nazo vipi iwe kwa Waislamu na wasio Waislamu.

  Alisema jambo hilo serikali italibeba na BAKWATA taifa kwa upande wao walichukue na kuwataka waumini wa dini ya kiislamu waliowekeza nchini waone watakavyoshiriki kwenye fursa hizo ingawa kinachoangaliwa zaidi ni ubora wa bidhaa na mifugo.

  Mongela alipongeza utaratibu huo unaofanywa ndani ya BAKWATA kuwa ni mapinduzi na migogoro iliyokuwepo wakati Hijja itakwisha na kuifanya serikali itapate ahuweni kwa kuwa nchi yetu haina dini ila wananchi wake wana dini.

  Naye kaimu Sheikh wa Mkoa wa Mwanza Alhaji Hasan Kabeke alisema BAKWATA kutoa elimu hiyo ya safari ya Ibada ya Hijja inalenga kuwazindua Waislamu ikiwa ni pamoja na kutumiza majukumu yake kwa mujibu wa katiba ya baraza hilo.

  Alifafanua kuwa Tanzania imetengewa nafasi za mahujaji 23,000 lakini wanaojaaliwa kwenda ni 2,500 hadi 3,000 kulinganisha na Kenya inayopeleka mahujaji 4,500 hivyo Waislamu wanayo fursa bado ya kwenda kuhiji kwa gharama ya sh. 10,105,000 sawa na Dola 4300 za Marekani

  0 0

  Na Peter Haule, WFM, Morogoro
  Halmashauri zote nchini zimetakiwa kujifunza kutekeleza miradi ya Kimakakati inayopatiwa ruzuku na Serikali, katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kwa kuwa thamani halisi ya mradi wa Soko la kisasa utakaogharimu Sh. bilioni 17 hadi kukamilika kwake inaonekana.
  Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, alipofanya ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua mradi wa kimkakati wa ujenzi wa Soko la Kisasa katika Manispaa ya Morogoro Mkoani Morogoro wenye lengo la kuzifanya Mamlaka za Serikali za Mitaa ziweze kujitegemea kimapato.
  Dkt. Kijaji alisema kuwa Kama ipo halmashauri iliyopewa fedha za kutekeleza miradi ya kimkakati kwa kuwekeana mkataba na Serikali na bado inashindwa kufuata makubaliano ya mkataba ijifunze kutoka Manispaa ya Morogoro.
  “Ukilinganisha na miradi mingine ya kimkakati niliyoikagua katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, huu ni wa mfano, zipo halmashauri ambazo zimepewa fedha halafu zinarudi tena kuangalia upya mikataba ambayo waliwekeana saini na Serikali jambo ambalo linatia mashaka, tuje tujifunze kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro kwa nini ameweza kwenda na wakati ulio katika mkataba”alisema Dkt. Kijaji.
  Alipongeza hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi huo ambao umefikia asilimia 30 japo walitakiwa kufikia asilimia 40 katika kipindi hiki kutokana na changamoto ya kujaa maji na kuutaka uongozi wa Manispaa hiyo kukamilisha ujenzi ndani ya kipindi cha miezi mitano ili wafanyabiashara waanze kulitumia soko hilo.
  "Mapato ya Soko hili yataongezeka kutoka Shilingi bilioni moja, kwa mwaka hadi Sh. bilioni 4 kwa kuwa idadi ya wafanyabiashara itaongezeka kutoka 400 kwa sasa hadi 900 na huduma zingine zitatolewa kama Benki" alieleza Dkt. Kijaji.
  Dkt. Kijaji alisema kuwa dhamira ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, ya kuanzisha miradi ya kimkakati kwa manufaa ya watanzania itatimia kupitia mradi wa Soko la Kisasa la Manispaa ya Morogoro.
  Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Bi. Regina Chonjo, ameishukuru Serikali kwa kupeleka mradi huo Wilayani kwake, kwa kuwa soko lililokuwepo lilijengwa mwaka 1953 hivyo kuwa na miundombinu mibovu iliyosababisha wananchi kuwa na magonjwa ya mlipuko kikiwemo kipindupindu, hivyo mradi huo si tu utaongeza mapato na kuweka mandhari nzuri, lakini pia utaimarisha afya za wananchi.
  Naye Meya ya Manispaa ya Morogoro  Bw. Pascal Kihanga, alisema kuwa waliwaahidi wananachi kusimamia ujenzi wa Soko hilo jambo ambalo linatekelezwa kwa juhudi kubwa, hivyo kufikia mwezi Septemba mwaka huu mradi utakabidhiwa kwa Serikali na wafanyabiashara wote walioondolewa kupisha mradi na  wengine watarudi.
  Mhandisi wa Mradi huo Antonio Mkinga, amesema kuwa mradi huo utakamilika katika muda uliopangwa, kwa kuwa mpaka sasa hakuna vikwazo ambavyo vinaweza kuzuia utekelezaji wake.
  Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ni miongoni mwa Halmashauri 17 zilizokidhi vigezo vya kutekeleza jumla ya miradi 22 ya kimkakati nchini kwa mwaka wa fedha 2018/2019 kwa gharama ya shilingi bilioni 147 ambapo Manispaa hiyo ilipata mradi huo wa soko la kisasa litakalogharimu shilingi bilioni 17.
   Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto) akiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Bi. Regina Chonjo, wakati akikagua ujenzi wa Soko la Kisasa la Kimkakati la Manispaa ya Morogoro, ambalo ndilo la mfano katika miradi ya kuziwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa kujitegemea kimapato. 
   Muonekano wa Soko la Kisasa la Kimkakati la Manispaa ya Morogoro, ambalo limekamilika kwa asilimia 30 na linatarajiwa kukabidhiwa kwa Serikali Septemba mwaka huu na kuhudumia wafanyabiashara zaidi ya 900.
  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa nne kushoto) akietendelea na ukaguzi wa ujenzi wa Soko la Kisasa la Kimkakati la Manispaa ya Morogoro  Mkoani Morogoro .(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango)

  0 0

  *Asema Serikali inatumia fedha nyingi kujenga miundombinu
  *Awataka wananchi kulinda barabara zinazojengwa nchini

  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  WANANCHI wenye tabia ya kutupa takataka katika mitaro iliyopo pembezoni mwa barabara na kusababisha kuziba na kujaa taka imeonekana kumkera Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa(TAMISEMI)Selemani Jafo kutoa onyo kali.

  Jafo ametoa onyo hilo leo Februari 26 ,mwaka 2019 wakati ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Dar es Salaam ambapo akiwa
  katika barabara ya Kijichi Toangoma ameshuhudia baadhi mitaro ya barabara hiyo ikiwa imeanza kujaa taka.

  "Serikali inatumia fedha nyingi kutengeneza miundombinu ya barabara ,hivyo lazima wananchi nao waitunze ili iwe salama.Wenye tabia ya kutupa taka waache na hii tabia hatuwezi kuacha iendelee,viongozi wa wilaya hakikisheni usafi wa mitaro unapewa kipaumbele," amesema Waziri Jafo.

  Wakati huo huo amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam Felix Lianiva kuanzisha kampeni ya usafi katika maeneo yote ya miundombonu ya barabara ili ibaki salama."Nitoa maagizo kwa Mkuu wa Wilaya ukiwemo Mkuu wa wilaya ya Temeke kuanzisha kampeni ya usafi.Nataka mitaro yote iwe
  safi,"amefafanua.

  Akizungumzia utekelezaji wa miradi ya DMDP ,Waziri Jafo amesema jumla ya Sh.Bilioni 660 zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo na kwa Mkoa wa Dar es Salaam na kwa sasa kuna mabadiliko makubwa ambayo yametokana na kukamilika kwa miradi na maeneo mengine bado inaendelea na ipo hatua mbalimbali za utekelezaji.

  Waziri Jafo amepata nafasi ya kutembelea ujenzi wa kituo cha afya Buza ambacho
  kinajengwa kisasa na lengo ni kuondoa adha ambayo wananchi wa Buza na maeneo jirani wamekuwa wakiipata.Amefafanua kuwa ujenzi huo wa kituo cha afya unafanyika chini ya ufadhili wa fedha za miradi ya DMDP na kwamba kabla ya kuanza ujenzi huo ilikuwa ni zahanati lakini kwa namna ambavyo kitakuwa kitakapokamilika kitakuwa kituo cha afya.

  "Serikali ya Awamu ya tano chini ya uongozi mahiri wa Rais Dk.John Magufuli kuna mambo makubwa yanaendelea kufanyika nchini ya kuboresha huduma mbalimbali ikiwemo sekta ya afya.Wananchi wa Buza ni mashahidi kupitia ujenzi huu wenye lengo la kuboresha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi," amesema Waziri Jafo.

  Amewahakikishia wananchi wa Buza kuwa baada ya ujenzi kukamilika Serikali itapeleka vifaa tiba vyote ambavyo vinahitajika kuhakikisha huduma zinazotolewa zinakuwa bora.Pia amesem Serikali itapeleka Gari mpya ya kubeba wagonjwa( Ambulance).

  "Tutaleta Ambulance mpya kabisa kwa ajili ya kituo cha afya Buza,lengo ni kuhakikisha mnakuwa mnakuwa na kila kitu ambacho kinahitajika hapa.Hii yote inatokana na dhamira njema ya Rais wetu ya kupeleka huduma muhimu kwa
  wananchi wote," amesema Waziri Jafo.

  Waziri Jafo ameendelea kutoa shukrani kwa Benki ya Dunia kutokana na misaada ya fedha ambayo wanaitoa kwa Serikali ya Tanzania na kufafanua kupitia fedha hizo katika Majiji,Manispaa na Halmashauri kote nchini miradi ya maendeleo inaendelea kutekelezwa na mingine imekamilika.

  "Kuna zaidi ya Sh.Trilioni mbili ambazo zinatumika kuboresha miji yote nchini.Na
  kwa Dar es Salaam zimetengwa fedha hizo Sh.Bilioni 660 kuendeleza Jiji na ukweli kuna mabadiliko makubwa hata maeneo ambayo yalikuwa hayapitiki, hivi sasa
  yanapitika vizuri," amesisitiza Waziri Jafo.

  0 0












  0 0

  Mkurugenzi wa Idara ya  Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dkt Hassan Abbas akizungumza na waandishi habari wakati alipokwenda kutoa pole ya Msiba wa Aliyekuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji Vipindi wa Clouds Ruge Mutahaba aliyefariki Jana nchini Afrika Kusini. Dkt Abbas amesema Ruge alikuwa kijana wa pekee aliyetoa mchango wake ambao umeweza kuonekana katika kusaidia vijana wengi nchini.Amesema kuwa vijana waliobaki nao waoneshe njia zilizoachwa na Ruge kwa kuamini katika kusaidia wengine. Amesema Ruge ametutoka lakini tulikuwa na muhitaji lakini kazi ya Mungu haina makosa.

older | 1 | .... | 1809 | 1810 | (Page 1811) | 1812 | 1813 | .... | 1897 | newer