Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1808 | 1809 | (Page 1810) | 1811 | 1812 | .... | 1897 | newer

  0 0

    Katibu wa Kikosi Kazi cha Kuratibu Zoezi la Serikali Kuhamia Dodoma Bw.Meshach Bandawe akionesha hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa tenki la maji ndani ya mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mji wa Serikali.
   Katibu wa Kikosi Kazi cha Kuratibu Zoezi la Serikali Kuhamia Dodoma Bw.Meshach Bandawe akionesha hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa jengo la Wizara ya Nishati linalojengwa ndani ya mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma wakati wa ziara yakukagua maendeleo ya ujenzi wa mji wa Serikali.
   Katibu wa Kikosi Kazi cha Kuratibu Zoezi la Serikali Kuhamia Dodoma Bw.Meshach Bandawe akionesha hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa jengo la Wizara ya Fedha na Mipango linalojengwa ndani ya mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma wakati wa ziara yakukagua maendeleo ya ujenzi wa mji wa Serikali.
   Muonekano wa hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa jengo la Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora katika mji wa Serikali Ihumwa jijini Dodoma. 
    Katibu wa Kikosi Kazi cha Kuratibu Zoezi la Serikali Kuhamia Dodoma Bw.Meshach Bandawe akiongea na mafundi katika jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais linalojengwa ndani ya mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma wakati wa ziara yakukagua maendeleo ya ujenzi wa mji wa Serikali.
   Katibu wa Kikosi Kazi cha Kuratibu Zoezi la Serikali Kuhamia Dodoma Bw.Meshach Bandawe akiongea na Mkandarasi na Mshitiri katika jengo la Wizara ya Kilimo linalojengwa ndani ya mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma wakati wa ziara yakukagua maendeleo ya ujenzi wa mji wa Serikali.

  0 0

  Vijana wametakiwa kutokata tamaa,kuondoa hofu na kuwa makini katika maisha licha ya changamoto mbalimbali wanazokutana nazo ili waweze kufikia ndoto zao za maisha. 


  Ushauri huo umetolewa Februari 23,2019 na Muuguzi mkunga mstaafu aliyebobea katika fani ya ushauri nasaha, Gladness Olotu wakati wa Bonanza la Michezo lililokutanisha vijana kutoka kwenye klabu za vijana kutoka halmashauri za wilaya za Misungwi,Nyamagana,Sengerema na Kwimba mkoani Mwanza. 

  Klabu hizo zinasimamiwa na asasi ya kitaifa inayolenga kutokomeza UKIMWI kwa watoto na familia ya Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) kwa ufadhili wa Watu wa Marekani kupitia Centres for Disease Control (CDC). 

  Akifungua Bonanza hilo,lililofanyika katika Viwanja vya Lessa Garden Hotel jijini Mwanza, Olotu aliwashauri vijana kujiamini na kutokubali kukata tamaa lakini pia kuwa wasikivu wanapoelekezwa mambo ya msingi katika maisha. 

  “Kupitia michezo hii mmefurahi pamoja, mmefahamiana,mmepata marafiki wapya na kujifunza mambo kadha wa kadhaa kupitia michezo,naomba muendelee kujiamini na kuzingatia ushauri mnaopewa ili mtimize ndoto zenu, ni vyema pia kuwa wamoja na kuendelea kushirikiana”,aliongeza Olotu. 

  Kwa upande wake, Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza,Cecilia Yona alisema AGPAHI imekuwa ikiandaa michezo kwa watoto na vijana ili kuwapa msaada wa kisaikolojia kwani asasi hiyo inajali watoto ili wakue na kuishi katika matumaini chanya. 

  Alisema bonanza hilo limeshirikisha vijana balehe zaidi ya 50 kutoka kwenye vituo vya tiba na matunzo kwenye halmashauri za wilaya mkoani Mwanza lengo likiwa ni kujifunza kwa njia ya michezo kuimarisha afya zao. 

  Miongoni mwa michezo iliyofanyika wakati wa bonanza hilo ni kukimbia mita 100,mbio za magunia,kabute,landrover na mchezo wa kufunga vitambaa usoni. 
  Muuguzi mstaafu aliyebobea katika fani ya ushauri nasaha, Gladness Olotu akifungua bonanza la michezo lililokutanisha vijana kutoka kwenye klabu za vijana kutoka halmashauri za wilaya za Misungwi,Nyamagana,Sengerema na Kwimba mkoani Mwanza - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog.
  Muuguzi mkunga mstaafu aliyebobea katika fani ya ushauri nasaha, Gladness Olotu akiwahamasisha vijana kuwa wamoja na kushirikiana sambamba na kutokata tamaa ili wafikie ndoto zao za maisha. Kushoto ni Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza,Cecilia Yona.Wa kwanza kushoto ni Pudensia Mbwiliza na Joan John ambao ni Walimu wa vijana kutoka Hospitali ya Rufaa Bugando Jijini Mwanza.
  Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza,Cecilia Yona akielezea malengo ya bonanza la michezo ambayo ni kuburudika na kujifunza kwa njia ya michezo. 
  Vijana wakicheza kwa kushika vichwa wakati wa bonanza hilo. 
  Mchezo wa Landrover ukiendelea. 
  Vijana wakiunga mstari kumfuata mshindi katika mchezo wa karatasi,jiwe na mkasi. 
  Vijana wa kike wakichuana kwenye mbio za mita 100. 
  Mchezo wa mbio za mita 100 ukiendelea kwa vijana wa kiume. 
  Mbio za magunia zikiendelea.
  Mchezo wa kuvuka vikwazo ili kuweza kufikia malengo : Kulia ni Mwalimu wa vijana Douglas Renatus kutoka hospitali ya rufaa Bugando akitoa maelekezo kwa washiriki juu ya mambo ya kufanya huku wamefungwa vitambaa usoni. 
  Washiriki wa mchezo wa kuvuka vikwazo ili kuweza kufikia malengo wakiendelea kutembea huku wakipewa maelekezo kutoka kwa vijana waliowazunguka. 
  Mshiriki wa mchezo wa kuvuka vikwazo ili kuweza kufikia malengo baada ya kuvuka kikwazo namba mbili akichukua zawadi ya limao.  Watu wazima nao hawakubaki nyuma katika michezo hiyo ili kuwatia moyo vijana. 
  Mwalimu wa vijana Pudensia Mbwiliza akiwasisitiza vijana kutokata tamaa na kuepuka hofu katika maisha.
  Mwalimu wa vijana Joan John akiwafurahisha vijana.
  Vijana wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea. 
  Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza,Cecilia Yona akitoa mwongozo wa kugawa zawadi kwa washindi wa michezo mbalimbali iliyofanyika pamoja na zawadi za jumla kwa washiriki. Wa kwanza kushoto ni Nicholaus Michael na Douglas Renatus ambao ni walimu wa vijana kutoka hospitali ya rufaa Bugando. Kulia ni Muuguzi mkunga mstaafu aliyebobea katika fani ya ushauri nasaha, Gladness Olotu. 
  Mshindi wa mbio za mita 100 kwa vijana wa kike akipokea zawadi ya saa kutoka kwa mgeni rasmi Muuguzi mkunga mstaafu aliyebobea katika fani ya ushauri nasaha, Gladness Olotu. Wa kwanza kulia ni Mwalimu wa vijana kutoka Hospitali ya Rufaa Bugando Jijini Mwanza,Joan John akitaja majina ya washindi katika michezo.Wa pili kutoka kulia ni Mwalimu wa vijana kutoka Hospitali ya Rufaa Bugando Jijini Mwanza, John Shayo. 
  Muuguzi mkunga mstaafu aliyebobea katika fani ya ushauri nasaha, Gladness Olotu akikabidhi zawadi ya saa kwa mshindi wa mbio za mita 100 kwa kundi la vijana wa kiume. 
  Kijana akiangalia zawadi ya saa baada ya kukabidhiwa. 
  Kijana akishikana mkono na Muuguzi mkunga mstaafu aliyebobea katika fani ya ushauri nasaha, Gladness Olotu wakati wa zoezi la kugawa zawadi za jumla kwa washiriki wa bonanza. 
  Vijana wakiendelea kupokea zawadi za chupa za maji. 
  Picha ya pamoja washiriki wa bonanza la michezo. 
  Washiriki wa bonanza la michezo wakiwa katika picha za vurugu. 


  Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya namna ya kutengeneza sabuni bora kutoka kwa Mwenyekiti wa kikundi cha Wazalendo Ndugu Imani Matabula wakati wa maonyesho yua wajasiriamali katika viwanja vya Kolimba wilaya ya Kaliua mkoa wa Tabora. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mbunge wa Zamani wa Jimbo la Kaliua na Waziri wa Zamani katika Wizara mbali mbali Profesa Juma Kapuya(kushoto) mara baada ya kumaliza kuhutubia wananchi katika uwanja wa Kolimba wilaya ya Kaliua mkoani Tabora. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Naibu Waziri TAMISEMI Mhe. Mwita Waitara (kushoto) kabla ya kuhutubia  wa mkutano wa hadhara katika uwanja wa Kolimba wilaya ya Kaliua mkoani Tabora. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

   

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua kwa kuwa mstari wa mbele katika suala zima la kuwainua Wanawake, Vijana na Walemavu ambapo zaidi ya milioni 450 zimetolewa katika makundi hayo ndani ya kipindi cha 2017 – 2018.

  Makamu wa Rais ametoa pongezi hizo leo wakati akihutubia wananchi kwenye uwanja wa Kolimba, Kaliua moani Tabora.

  Aidha katika hatua nyingine Makamu wa Rais ameridhia kuondolewa mara moja kwa Mhandisi wa Maji wa Wilaya ya Kaliua Mhandisi Fikiri Samadi baada ya kushindwa kutekeleza mradi wa maji wa shilingi bilioni 1.5.

  “Ziara hizi ni ziara za kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo na serikali imekuwa mstari wa mbele kuweka pesa nyingi kwenye miradi ya maendeleo hivyo yeyote atakayekwamisha atachukuliwa hatua mara moja”alisema Makamu wa Rais.

  Makamu wa Rais amesema wilaya ya Kaliua ni mfano wa kuigwa kwa kujenga jingo la upasuaji pamoja na wodi ya wazazi yenye uwezo wa kuchukua vitanda 24 katika kituo cha afya Kaliua kwa mapato yao ya ndani pamoja na michango kutoka chama cha msingi Nsungwa ambapo mpaka kukamilika wametumia shilingi 159,703,199.98.

  Kwa upande mwingine Naibu Waziri TAMISEMI amesema vikundi vinavyopewa mikopo na Halmashauri lazima virejeshe mikopo hiyo ili iweze kuwasaidia watu wengine akizungumzia kwa wilaya ya Kaliua peke yake ambapo zaidi ya milioni 450 zimetolewa mpaka sasa zimerudishwa milioni 89 tu.

  Akizungumzia suala la uchaguzi katika kata 3 za Igombe Mkuluu, Mirambo na Kanindo zilizopo katika jimbo la Ulyankulu, Naibu Waziri TAMISEMI Mhe. Waitara amesema lazima usalama wa Taifa uzingatiwe na upewe kipaumbeke kwani kwenye maeneo hayo kuna waliopewa uraia na kuna wakimbizi hivyo Serikali itakapojiridhisha wanaweza shiriki katika uchaguzi ujao.

  0 0
  0 0

  Na Veronica Simba – Lindi

  Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amekemea vikali utendaji kazi mbovu wa Mkandarasi State Grid, anayetekeleza mradi wa umeme vijijini Mkoa wa Lindi, kutokana na kufanya kazi chini ya kiwango na kutokamilisha wigo wake kwa wakati kama mkataba unavyoelekeza.

  Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nangambi Naipuli, Kata ya Mingumbi, wilayani Kilwa, Mkoa wa Lindi, jana Februari 24, mwaka huu, Naibu Waziri alisema Serikali imemvumilia kwa muda mrefu Mkandarasi huyo, ambaye pia anatekeleza mradi huo katika Mkoa wa Morogoro.

  Kufuatia utendaji huo duni wa mkandarasi husika, Naibu Waziri alikataa kuwasha umeme katika kijiji hicho, kama ilivyokuwa imepangwa, na kuelekeza kuwa atafanya zoezi hilo pale ambapo idadi ya wananchi waliounganishiwa umeme itakapokuwa ya kuridhisha, tofauti na idadi ndogo ya waliounganishiwa sasa ambayo ni watano tu.

  “Huu ni utapeli mtupu, mimi sitafanya kazi hii. Siwashi umeme na naenda kutoa taarifa kwenye mamlaka zinazohusika kwamba mkandarasi anababaisha.”

  Akifafanua, Naibu Waziri alieleza kuwa Mkandarasi huyo amekuwa mwenye kiburi na asiyejirekebisha na kwamba taarifa za utendaji wake mbovu tayari zinafahamika hadi wizarani hivyo hakuna haja ya kuendelea kumvumilia, bali ni lazima hatua stahiki zichukuliwe dhidi yake.

  Kufuatia hali hiyo, Afisa Tawala wa Wilaya ya Kilwa, ambaye alimwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo, Christopher Ngubiagai, alimtaka Mkandarasi husika kuripoti ofisini kwake siku ya Jumatano, Februari 27 mwaka huu, akiwa na Hadidu za Rejea ili pamoja na mambo mengine, akaeleze amejipanga vipi kukamilisha kazi husika ndani ya muda wa makubaliano.

  Awali, Naibu Waziri Mgalu alitembelea na kukagua Kituo cha kufua umeme kwa kutumia gesi asilia cha Somanga kilichopo wilayani Kilwa, ambapo alieleza kwamba Serikali imedhamiria kupeleka umeme wa uhakika na wa kutosha katika mikoa yote ya Kusini.

  Aidha, Naibu Waziri alitembelea pia vijiji vya Kisangi na Mkwanyule pamoja na Kilwa Kisiwani ambapo alizungumza na wananchi kuhusu masuala mbalimbali ya umeme pamoja na kupokea kero zao.

  Akiwa Kilwa Kisiwani, alimsisitiza Mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Umeme Jua mahala hapo, ambaye ni Kampuni ya Green Leaf, kuhakikisha anakamilisha kazi hiyo kwa wakati, kabla ya Juni 30 mwaka huu, ambapo Mkataba wake utakwisha.

  Naibu Waziri yuko katika ziara ya kazi ya siku Nne mkoani Lindi, ambayo aliianza jana, Februari 24, mwaka huu. Katika ziara hiyo, amefuatana na wataalamu mbalimbali kutoka wizarani, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) pamoja na kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
   Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu (mwenye kinasa sauti), akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nangambi Naipuli, Kata ya Mingumbi, wilayani Kilwa, Mkoa wa Lindi, jana Februari 24, mwaka huu, akiwa katika ziara ya kazi.
   Mkazi wa kijiji cha Mkwanyule, Kata ya Masoko, wilayani Kilwa, Rehema Sudi (kulia), akitoa maoni yake kuhusu masuala ya umeme, kwa Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (mwenye kilemba), wakati wa ziara yake eneo hilo jana, Februari 24, mwaka huu.
   Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (mwenye kilemba – katikati), akiwa katika usafiri wa Boti ndogo pamoja na Ujumbe wake, kuelekea Kilwa kisiwani, mkoani Lindi, jana Februari 24, mwaka huu akiwa katika ziara ya kazi.
  Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (mwenye kilemba cha kijani), akiwasili Kilwa kisiwani, mkoani Lindi, kwa ajili ya kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme na kuzungumza na wananchi, akiwa katika ziara ya kazi, jana Februari 24, mwaka huu.

  0 0

  WAKATI Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk. John Magufuli, ikidhamiria kuinua uchumi kwa kutumia miundombinu ya usafirishaji, wadau wa maendeleo wamekuwa wakitumia fursa zilizopo kunufaisha watanzania.

  Miongoni mwao ni Mkurugenzi wa Makampuni ya Kiluwa Group, Mohamed Kiluwa ambaye amedhamiria kuanzisha kiwanda cha kutengeneza mabehewa ya treni yaliyochakaa kwa kutumia reli ya kisasa na ya zamani.

  Akiwa katika hafla ya kubadilishana nyaraka za makubaliano hayo aliyoingia na Kampuni ya Africa Jambo Group ya nchini Afrika Kusini, katika Jiji la Johannesburg hivi karibuni Kiluwa alisema anataka kufanya kitu cha kipekee katika ardhi ya Tanzania kinyume na matarajio ya wengi.

  “Hiki tunachotaka kukifanya hakijawahi kufikiriwa na wengi lakini kitaleta tija katika uchumi wa nchi, tunafahamu tunapoelekea ni Tanzania ya viwanda na uchumi wa kati. Tutahitaji mbinu bora za usafirishaji malighafi na bidhaa, reli ni njia rahisi na salama kusafirishia mizigo,” alisema Kilua.

  Alibainisha,  kiwanda hicho kitakuwepo katika eneo la uwekezaji Kiluwa Free Processing Zone mkoani Pwani, ambapo taarifa ya awali ya utekelezaji wa mradi huo inabainisha utakuwa katika awamu tatu.

  Kila awamu itatoa ajira kwa watu  wapatao 980, mradi huo unalenga katika soko la ndani ya Tanzania na Afrika kwa ujumla. Vilevile wakazi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki watakuwa sehemu ya wanufaika kwa kuwa baadhi ya mizigo itakwenda katika nchi jirani za Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi hadi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) pamoja na nchi za ukanda wa kusini mwa Afrika.

  “Ifahamike tumetenga kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 150, kwa ajili ya kukamilisha mradi huu ambao utaleta mapinduzi makubwa katika sekta ya viwanda nchini pamoja na usafirishaji,” alisema Kiluwa.

  Naye, mwakilishi wa Kampuni ya Africa Jambo Group, Marthinus Christian Landman alisema wameamua kuwekeza Tanzania kwa sababu wanajua ni eneo muhimu linalokua kwa kasi kiuchumi kutokana na malengo makubwa yaliyowekwa na serikali iliyopo madarakani.

  “Siku zote mfanyabiashara anaangalia eneo ambalo atanufaika, tunaangalia zaidi faida kabla ya kukamilisha mikataba, tumejiridhisha kwa sasa Tanzania ni sehemu sahihi na salama kiuewekezaji kwa sababu Rais Dk. John Magufuli amedhamiria kuona watu wanafanya kazi, hakuna kona kona wala rushwa,” alisema Landman.  
    Mkurugenzi wa Makampuni ya Kiluwa Group ,Mohamed Kiluwa (kulia) na Mwakilishi wa Kampuni ya Africa Jambo Group ya nchini Afrika Kusini,Marthinus Christiaan LandMan wakibadilishana nyaraka za mkataba wa makubaliano ya mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza mabehewa ya treni ya zamani (Analogy) na ya Kisasa (Standard Gauge) nchini Tanzania. Makubaliano hayo yamefanyika nchini Afrika Kusini mwishoni mwa wiki,na kwamba mradi huo utakuwa na awamu tatu,ambapo kila awamu itatoa ajira ya Wafanyakazi  wapatao 980,mradi huo ukifanikiwa utalenga soko la ndani na nje.
   Mkurugenzi wa Makampuni ya Kiluwa Group ,Mohamed Kiluwa na Mwakilishi wa Kampuni ya Africa Jambo Group ya nchini Afrika Kusini,Marthinus Christiaan LandMan wakisaini nyaraka za mkataba wa makubaliano ya mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza mabehewa ya treni ya zamani (Analogy) na ya Kisasa (Standard Gauge) nchini Tanzania. Makubaliano hayo yamefanyika nchini Afrika Kusini hivi karibuni,na kwamba mradi huo utakuwa na awamu tatu,ambapo kila awamu itatoa ajira ya Wafanyakazi  wapatao 980,mradi huo ukifanikiwa utalenga soko la ndani na nje.

  0 0


  "I hope a free Africa will remember the little I did for this continent. I am a satisfied man because I played my part".
  HASHIM MBITA, 24.8.2014.


  1. Introduction:

  CAMARADA, Rt. Brig. Gen. HASHIM IDD MBITA, chose to sleep forever on 26.4.2015 at the Lugalo Millitary hospital, Dsm after a long illness. Brig. Gen. MBITA did not die, to borrow an English catchphrase, "Soldiers never die, they simply fade away". Brig. Gen. MBITA simply faded away. He chose to fade away on the date that Tanganyika and Zanzibar were united to create the United Republic of Tanzania. Thus, in my humble view, UNITY is the message he left behind.

  President JAKAYA MRISHO KIKWETE stated:

  "There are very few people that have served the country the way Mzee MBITA has served this nation. He also led the liberation efforts of our brethren in the Southern African countries for 20 years until they all achieved their independence. There is not a freedom fighter in Mozambique, Angola, Zimbabwe, Namibia and South Africa who did not know the contribution made by Mzee MBITA. His death has robbed us of a true son of the African soil. He was a man of his own kind"

  There are certain individuals life and fate make us stumble upon not to learn from them as they breath, but rather that we may marvel at their collossal nature when they are no longer with us. Such is the case with Brig. Gen. MBITA.

  The Dot.com generation knows very little or nothing about this Big man. Currently, one can hear a story here and there of what this fallen hero did. With the passing of time and if no effort is made towards writing his Big Story, then Brig. Gen. MBITA could be just a smoke that just passed over the sky!.

  The Billion-dollar question is who was this Unique Tanzanian who served his country with honour and distinction?

  2. Birth of a Jewel:

  HASHIM IDD MBITA was born on 2.11.1933 at Songoro, Gongoni, Tabora.

  3. Primary Education:

  MBITA studied at Town primary school and passed his exams with flying colours.

  4. Secondary Education:

  MBITA joined Tabora boyz secondary school, known for nurturing luminaries for post-independence government, in 1950 and he completed his A Leve studies in 1957.

  5. MBITA Joins the Cooperatives Department:

  MBITA joined the Cooperatives Department in Mwanza in 1957.

  6. MBITA Joins TANU:

  MBITA joined the Tanganyika African National Union (TANU) in 1958 and was always a humble party cadre before moving to public relations as a journalist.

  7. MBITA Joins the Ministry of Information:

  MBITA, a journalist by profession, worked with the Department of Information, Ministry of Information as the Director of Information.

  8. MBITA Attends Millitary Training in the UK:

  Given Mwalimu NYERERE's overhaul and re-branding of the army after the 1964 mutiny, MBITA was sent to UK for millitary training and then was appointed political commissar in the army.

  9. MBITA Becomes Press Secretary to Mwalimu NYERERE:

  MBITA, thereafter, moved to the State House to become Press Secretary to Mwalimu NYERERE and was later TANU's Secretary General.

  10. MBITA Becomes TANU's Secretary General:

  In 1970, MBITA was appointed TANU Secretary General.

  11. MBITA Appointed Executive Secretary of OAU in 1972:

  In 1972, MBITA was appointed Executive Secretary of the the OAU Coordinating Committee for the liberation of Africa.

  MBITA's work was guarded by the 9-nation Committee with a Non-Executive Chairman. He had to link up and work with the OAU Secretary General and occassionally with the rotating chairmen.

  Nurturing these relationships and balancing between the demands from Addis and from the Committee of Nine was not easy.

  MBITA mobilized materials and training for the liberation forces of the remaining countries still under colonial rule, all of whom gained independence during his tenure including Guinea-Bissau 1974, Cape Verde 1975, Angola 1975, Zimbabwe 1980, Namibia 1990 and South Africa 1994.

  As Committee Administrative Chief, Brig. Gen. MBITA was singulary the person most hated by the likes of Ian Smith in Rhodesia and F.W De Clerk of South Africa. As such, the regimes considered Brig. Gen. MBITA the Trouble-maker Numero Uno! His life was thus in great danger and in fact several schemes hatched to illiminate him unsuccesfully.

  12. MBITA: Mission Accomplished, 1994!

  The Liberation Committee closed down in August 1994 with MBITA submitting a Final Report under the title: "MISSION ACCOMPLISHED"

  At the final meeting of the OAU Liberation Committee in Arusha, Mwalimu NYERERE heaped praises on Brig. Gen. MBITA for his outstsnding contribution for liberation of the continent.

  A 9-Volume history of Southern Africa Liberation struggles known as the HASHIM MBITA PROJECT was published in his honour in Dsm in 2014 as Southern African Liberation Struggles: Contemporaneous documents(1960-1964).

  13. MBITA Appointed TZ Ambassador to Zimbabwe:

  Once Brig. Gen. MBITA was done with the libetation mission, he was assigned to several other tasks including being a diplomat.

  Thus, when relations between TZ and Zimbabwe deteriorated over a Tanzanian envoy's stance over the seizure of white farms, Brig. Gen. MBITA was dispatched by president BEN MKAPA as High Commissioner to smoothen relations. He served as Ambassador from 2003 to 2006 and did a commendable job.

  14. Brig. Gen. MBITA Fades Away, 2015:

  That Brig. Gen. MBITA faded away on 26.4.2015, a day of significant proportions to TZ is an unblemished indicator of the impact this Great man had on African politics and its quest for freedom from colonial rule. He was one of the last remaining African heroes.

  15. MBITA: Showered with Praise & Awards

  The late Brig. Gen. MBITA was one of the heroes of African Liberation. His heart belonged not only to TZ but also to Africa, his motherland:

  15.1 Zimbabwe:

  Zimbabwe awarded Brig. Gen. MBITA the highest national honour that could be given to a foreigner- "THE ROYAL ORDER OF MUNHUMUTAPA", in recognition of his outstanding role, during the SADC summit at Victoria Falls.

  Brig. Gen. MBITA was represented by his beautiful daughter, Ms SHEILLA MBITA, a BOT employee. It read:

  "We in Zimbabwe are glad that Hon. MBITA was able to appreciate this honour although he was not feeling well. His daughter came to receive the honour".
  SIMBARASHE MUMBENGWEGI, Foreign Minister.

  15.2 South Africa:

  President JACOB ZUMA, on 8.12.2015, bestowed MBITA with the Order of the Companions of Oliver Tambo in Gold, during the 2018 National Orders Awards ceremony:

  "For his exceptional and gallant support of African liberation movements and his tireless efforts in ensuring that the struggle for freedom throughout the African continent bore fruit".


  15. 3 Joachim Chissano:

  Former president JOACHIM CHISSANO who was MBITA's close friend and who had once visited and stayed with MBITA in his house in Tabora for a couple of days, said:

  "During his prime, Camarada MBITA was outwardly a good natured man, but in the job, he was tough, no-nonsense, results demanding, high discipline-enforcement army officer. He was a Millitary per excellence".

  15.4 Keneth Kaunda:

  "Brig. Gen. HASHIM MBITA was the Headmaster of the Africa Liberation movement's Highest school".

  15.5 Sam Nujoma

  SAM NUJOMA, Namibian founding President, described Brig. Gen. MBITA as "courageous" and "symbol of freedom from colonialism and occupation".

  15.6 Joseph Kabila:

  "The late HASHIM MBITA was not only a national of his mother country, Tanzania, but also a denizen of the African continent".

  15.7 AU:

  On 30.1.2016, President ROBERT GABRIEL MUGABE of Zimbabwe, the then outgoing chairperson of SADC and AU, presented "THE HASHIM MBITA PROJECT" to the African Union.

  The Publication is composed of 10 Volumes which document the history of the Liberation struggles in Southern Africa to be accessible to all citizens of the continent.

  15.8 SADC

  "This Award is for the important role Brigedier General MBITA played in regional liberation during his 20 year tenure as the Executive Secretary of the Liberation Committee of the OAU".

  16. Journeying with MBITA:

  As a Milambo High School Form 5 student, back in the day, I once had the privilege of travelling with Hon. MBITA in the Central Line train First Class Compartment from Dsm to Tabora. Though it was a 24 hour journey but it felt like a two hour journey as the Big man told me a lot of stories such as how he was executing his duties, criss-crossing the continent to foresee liberation struggles and various challenges he was facing. It was simply, the best journey of my life!.

  17. Conclusion:

  Very unfortunately, Tanzania has been drowsed with that heavy blanket of sleepness as despite having several universities, none has awarded Brig. Gen. MBITA with an honourary doctorate for his invaluable contribution to Africa.

  Brig. Gen. MBITA's story has to be written. We should not allow this unique history slip through our fingers!
   

   

  0 0


  BENKI ya NMB imewatangaza wateja watatu ambao wameibuka washindi katika droo ya mwisho ya kampeni ya matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' maarufu kwa jina la 'MastaBata'.

  Wateja hao watatu katika shindano hilo, EINSTEIN STEPHEN MAGEBO, SIMON CHACHA, pamoja na NUIS PAUL KASAMBALA wakiwa na wenza wao wanatarajia kusafirishwa na Benki ya NMB kwenda nchini Dubai kula Bata kwa siku nne mfululisho safari iliyogharamiwa na NMB kila kitu.

  Akizungumza katika tukio hilo, Meneja Mwandamizi Huduma za Kadi wa Benki ya NMB, Bw. Stephen Jilala alisema washindi hao wamepatikana baada ya kuchezeshwa kwa droo ya mwisho ya Shindano la MastaBata lililoendeshwa kuhamasisha matumizi ya mfumo wa 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' kwa wateja wao.

  Aliongeza kuwa mbali na washindi hao wateja kibao wa NMB waliotumia mfumo huo wa malipo pia wamejishindia shilingi 100,000/- kila mmoja na wengine wengi kujishindia simu janja za kisasa aina ya 'Samsung S9+'.
  Meneja Mwandamizi Huduma za Kadi wa Benki ya NMB, Bw. Stephen Jilala (katikati) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kupatikana kwa washindi watatu wa NMB kwenye shindano la MastaBata ambao pamoja na wenza wao watasafiri kwenda Dubai kwa siku nne kula 'Bata'. Kulia ni Meneja Huduma za Kadi NMB, Bw. Philbert Casmir pamoja na Meneja Mwandamizi kitengo cha kadi NMB, Bw. Manfredy Kayala (kushoto) wakifuatilia tukio hilo. 

  Mtangazaji kutoka kituo cha EFM, Emmanuel Kapanga (katikati) akizungumza kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa Shindano la MastaBata lililoendeshwa na Benki ya NMB ambaye amejishindia safari ya mapumziko kwenda Dubai kwa siku nne kula 'Bata' na mwenza wake. Jumla ya washindi watatu pamoja na wenza wao wataambatana katika safari hiyo iliyolipiwa kila kitu na Benki ya NMB. Kulia ni Ofisa Mwandamizi kutoka Bodi ya Taifa ya Michezo ya Kubahatisha, Abdallah Hemed akisimamia droo hiyo. Kushoto ni Bi. Saumu Rajabu kutoka Selcom. 


  Meneja Mwandamizi Huduma za Kadi wa Benki ya NMB, Bw. Stephen Jilala akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kupatikana kwa washindi watatu wa NMB kwenye shindano la MastaBata ambao pamoja na wenza wao watasafiri kwenda Dubai kwa siku nne kula 'Bata'. Kulia ni Meneja Huduma za Kadi NMB, Bw. Philbert Casmir akifuatilia tukio hilo.

  Watangazaji wa kituo cha EFM radio na TV, Emmanuel Kapanga (katikati) na Tunu Hussein (kushoto waliokaa), wakizungumza kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa Shindano la MastaBata lililoendeshwa na Benki ya NMB ambaye amejishindia safari ya mapumziko kwenda Dubai kwa siku nne kula 'Bata' na mwenza wake. Jumla ya washindi watatu pamoja na wenza wao wataambatana katika safari hiyo iliyolipiwa kila kitu na Benki ya NMB. Kulia ni Ofisa Mwandamizi kutoka Bodi ya Taifa ya Michezo ya Kubahatisha, Abdallah Hemed akisimamia droo hiyo.
  Sehemu ya wafanyakazi wa Benki ya NMB pamoja na wageni waalikwa wakishuhudia kutangazwa kwa washindi watatu wa droo ya mwisho ya shindano la MastaBata. Washindi wa mejishindia safari ya mapumziko kwenda Dubai kwa siku nne kula 'Bata' na mwenza wake. Jumla ya washindi watatu pamoja na wenza wao wataambatana katika safari hiyo iliyolipiwa kila kitu na Benki ya NMB. 

  0 0

  WAZIRI wa Maji Proffesa Makame Mbarawa akizungumza mara baada ya kutembelea chanzo cha Maji cha Amani wilayani Muheza wakati wa ziara yake mkoani Tanga
   WAZIRI wa Maji Proffesa Makame Mbarawa kushoto akimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu
  MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza wakati wa ziara hiyo


   WAZIRI wa Maji Proffesa Makame Mbarawa akishuka kwenye tanki kubwa la kuhifadhia maji eneo la Kilapula Jijini Tanga ambayo yatatoka eneo la Pongwe kuelekea wilayani Muheza kupunguza changamoto ya uhaba wa maji kwenye wilaya hiyo
   Mabomba yakiwa yameweka eneo hilo mradi huo mkubwa ukiendelea kutekelezwa
   Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly kushoto akiwa na katibu wa Mbunge wa Jimbo la Muheza kulia kushoto ni PRO wa Mamlaka hiyo Dorrah Killoh
   WAZIRI wa Maji Proffesa Makame Mbarawa kulia akionyeshwa kitu kwenye ramani na Mhifadhi wa Misitu ya Amani wilayani Muheza Mwanaidi Kijazi katika wakati alipotembelea chanzo kikubwa cha Maji wilayani Muheza cha Amani kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo  kulia ni Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly
  WAZIRI wa Maji Proffesa Makame Mbarawa katikati akisisitiza jambo kwa viongozi wa wilaya ya Muheza mara baada ya kutembelea chanzo hicho

  WAZIRI wa Maji Proffesa Makame Mbarawa amesema serikali kupitia mamlaka za maji watahakikisha wanapeleka huduma ya maji safi na salama kwenye vijiji vilivyopo karibu na vyanzo vya maji ili waendelee kuvitunza viweze kusaidia vizazi vya sasa na vijavyo.

  Mbarawa aliyasema hayo wakati alipotembelea chanzo cha Maji cha Amani wilayani Muheza mkoani Tanga ikiwa ni ziara yake ya siku ya pili mkoani hapa ambapo aliwataka wananchi kulinda vyanzo

  Alisema haitakuwa na maana iwapo wananchi hao wanaendelea kuvitunza vyanzo vya maji lakini hawana maji safi na salama hivyo watahakikisha nao wanapata huduma hiyo muhimu kwa ustawi wa maisha yao na jamii zao.

  Alieleza kwa sababu mwaka 1962 maji yaliyo yakipatikana kwa mtu mmoja yalikuwa mita za ujazo 7862 hivi sasa mtu mmoja kwa mwaka anaweza kutumia maji yaliyopo mita za ujazo 1800 lakini siku hizo kulikuwa na watu milioni 10.6 lakini leo hii watu zaidi ya milioni 50 na watu wanazidi kuongezeka.

  “Ndugu zangu Serikali kupitia mamlaka za Maji tutahakikisha wananchi wanaoishi karibu na vyanzo vya maji wanapata huduma ya maji safi kwa maana haitakuwa na maana kama wataendelea kuvitunza vyanzo hivyo wakati wao hawapati maji safi na salama “

  “Lakini pia nisisitize kwamba tuhakikishe vyanzo vya maji vilivyopo tunavilinda kwa nguvu zote kwani vinazidi kupungua kutokana na uharibifu wa mazingira pia wananchi wakielimishwa wanaweza kuvitunza, “Alisema.

  Aidha aliwataka wananchi hao kuhakikisha wanaendelea kuvitunza vyanzo vya maji ili viweze kusaidia vizazi vya sasa na baadae kwani bila kufanya hivyo chanzo hicho kinaweza kukauka.

  “Lakini kitakapokauka watu watafikiria kwenda mto Pangani na huko kunaweza pia kukauka hivyo kuna umuhimu wa kuhakikisha vyanzo hivyo vinatunzwa kwa lengo la kuendelea kuwepo “Alisema.

  Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo katika taarifa yake alimueleza Waziri Mbarawa kwamba hali ya upatikani maji wilayani humo eneo la mjini ni asilimia 35 kwa mjini na kipindi cha kiangazi asilimia 18.

  Alisema kwa upande wa vijiji upatikanaji wa maji ni asilimia 65 inakuwa ni nafuu kwa sababu baadhi ya maeneo kuna maji yanatiririka sehemu ambazo kumejengwa vyanzo vya maji na hivyo kuyapata kirahisi.

  “Mradi wa maji eneo la Muheza mjini ulijengwa mwaka 1977 ukitumia chanzo cha Mkurumuzi kilichopo Magoroto huku kililenga kuwapata huduma hiyo wakazi 8000 lakini kwa sasa sasa wapo wakazi 32000.

  Mkuu huyo wa wilaya alimueleza waziri huyo kwamba mpango wao kwa sasa ni kuhakikisha wanapata chanzo cha uhakika ili kupata maji ili kuondosha changamoto kubwa ya wilaya hiyo.

  “Kwani mh Waziri wakati wa kiangazi wananchi wananua ndoo moja ya maji kwa sh.1000 jambo ambalo ni changamoto kubwa na hilo linaweza kupatiwa ufumbuzi kwa miradi mikubwa “Alisema

  Naye kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu alisema eneo hilo la chanzo lilikuwa kwenye hali mbaya baada ya kuvamiwa na watu waliokuwa wakitafuta madini kabla ya kushirikiana na watu wa maliasili na serikali ya wilaya kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na kulirudisha kwenye hadhi yake.

  Alisema pia waliwapeleka wataalamu ili kuangalia kama kweli kuna mamdini kwenye eno hilo ili kama wanaweza kuruhusu uchumbaji wa madini ufanyike bila kuathiri chanzo cha maji hivho hivyo taarifa yao bado tunaisubiri.

  “Lakini pia niwashukuru Tanga Uwasa wameanza mikakati ya kuwapa maji vijiji vyote vinavyozunguka chanzo hicho kuhakikisha nao wananufaika na hduuma hiyo muhimu badala ya kutumia maji yanayo tiririka “Alisema.
  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera akimsikiliza Mfanyakazi wa kiwanda cha kubangua Korosho cha Korosho Africa Ltd Tunduru Mkoani Ruvuma Issa Kahesa kulia alipokuwa akimueleza kazi ya ubanguaji wa korosho za Serikali inavyoendelea katika kiwanda hicho.
  Baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha kubangua korosho cha Korosho Africa Ltd wakiendelea na kazi kiwandani hapo ambapo hadi kufikia jana zaidi ya wananchi 200 wamepata ajira.
  Mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera aliyeinama akiangalia ubora wa korosho za Serikali zinazobanguliwa katika kiwanda cha kubangua korosho cha Korosho Africa Ltd kilichopo Tunduru Mkoani Ruvuma.
  Mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera akiangalia korosho zilizobanguliwa katika kiwanda cha Korosho Africa Ltd ambacho kimeingia mkataba na Serikali kwa ajili ya kubangua korosho za Serikali zilizonunuliwa katika msimu wa 2018/2019 kutoka kwa wakulima wa wilaya ya Tunduru,kulia ni mfanyakazi wa kiwanda hicho Issa Kahesa

  0 0

  Mkurugenzi Mkazi wa Repssi Tanzania, Edwick Mapalala akiongea na vijana kijiweni kuhusu athali za mimbaMkurugenzi Mkazi wa Repssi Tanzania, Edwick Mapalala akiongea na vijana kijiweni kuhusu athali za mimba
  Baadhi ya wanafunzi wakimsikiliza Mkurugenzi Mkazi wa Repssi Tanzania, Edwick Mapalala


  Mwandishi wetu, Pwani.

  Shirika linalojihusisha na masuala ya kijamii na kisaikolojia kwa watoto (REPPSI) limeendelea kufanya kampeni ya kutokomeza tatizo la ndoa na mimba za utotoni mkoani Pwani.

  Kampeni hiyo inafanyika ili kuhakikisha watoto wa kike wanatimiza ndoto zao za kielimu ili kushiriki katika mkakati wa Serikali wa Tanzania ya viwanda.

  Akizungumza na wakazi wa Kibiti Mkoani Pwani, Mkurugenzi Mkazi wa REPSI Tanzania, Edwick Mapalala alisema tatizo la mimba na ndoa za utotoni bado kubwa na kwamba linahitaji jitihada za pamoja kupambana nalo.

  “Mfano ni hizi kampeni za kutoa elimu na kuihamasisha jamii kumthamini mtoto wa kike zinasaidia kwa hiyo kama tutaendelea nazo jamii itaelewa, watoto watatimiza ndoto zao,” alisema.

  Mapalala alisema katika kampeni hizo wanazoshirikiana na Shirika la Pasada linalojihusisha na masuala ya Ukimwi chini ya Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam na Pwani, vijana hasa madereva bodaboda wamefikishiwa elimu kuhusu thamani ya mtoto wa kike.

  Baadhi ya viongozi wa vijiji na kata walikiri kuwa ndoa za utotoni ni changamoto kubwa lakini wanaendelea kupambana nayo.Mratibu wa Elimu Kata ya Salala, Wilayani Kibiti Erasmus Assenga alisema kwa mwaka huu tu wanafunzi wawili wa Sekondari katika kata hiyo wameacha masomo kwa mimba.

  “Kwa hiyo kampeni hii ni muhimu kwa sababu watoto wa kike wenyewe wanafikishiwa elimu, jamii hasa wanaume wanaelezwa na wanajua umuhimu wa kuwathamini,” alisisitiza.

  Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii wa Pasada Ester Mbwana alisema anaamini kuwa baada ya kampeni hizo kutakuwa na mafanikio makubwa kwa sababu, jamii inaelewa na imekubali kusaidia katika ulinzi wa mtoto.

  0 0

  Februari 25, 2019

  Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawaomba radhi Wateja wake wa Mkoa wa Dar es salaam kwa kukosa huduma ya umeme kwa siku za hivi karibuni kutokana na maboresho makubwa yanayohusisha matengenezo kinga ya mashine 3 za Kituo cha Ubungo II, pamoja na uwekaji wa transfoma kubwa la MVA 300 kwenye Kituo cha kupoza umeme cha Ubungo ili kukiongezea uwezo na kwenda sambamba na ukuaji wa mahitaji ya jiji la Dar es Salaam.

   Kabla ya matengenezo kuanza mnamo Januari 2019 Kituo hiki cha kupoza umeme cha Ubungo kimekuwa kinapokea umeme kutoka katika vituo vya Uzalishaji umeme vilivyopo upande wa msongo wa kilovolti 220 kupitia transfoma mbili zenye uwezo wa MVA 150 kila moja, zenye kupokea umeme wa msongo wa Kilovolti  220 na kuushusha hadi kuwa msongo wa Kilovolti 132  katika transforma namba sita na namba  saba za kituo cha Ubungo na  vituo vya uzalishaji umeme vilivyoungwa kwenye msongo wa kilovolti 132 ambavyo vimeungwa moja kwa moja kwenye mfumo mkuu wa usambazaji umeme  kwa Dar es Salaam na Zanzibar.

  Kutokana na matengenezo yanayoendelea vituo vya uzalishaji umeme vilivyoungwa kwenye msongo wa kilovoti 132 na 33 vimekuwa nguzo kubwa ya upatikanaji wa umeme. Vituo hivyo ni Ubungo II na Tegeta.

  Shirika kupitia wataalamu wake tayari limefanya jitihada kubwa za kupunguza athari za upungufu wa upatikanaji wa umeme kwa wakaazi wa Dar es salaam na Zanzibar kwa kufanya yafuatayo: 

  Mosi, Kufungua laini ya msongo wa kilovoti 132 kati ya Kilimanjaro na Hale: Hili hufanyika ili kutoruhusu umeme wa kutoka Dar es Salaam na Morogoro kwenda Kilimanjaro hivyo Mkoa huu kuchukulia kwenye upande wa msongo wa kilovolti 220 kutoka Arusha.

  Pili , Kuwezesha upatikanaji wa umeme katika baadhi ya  maeneo ya Mkoa wa Dar es salaam, kwa kuunga baadhi ya njia za Usafirishaji  umeme kutoka Kituo cha Kinyerezi, Gongolamboto hadi Mbagala ili kuwezesha maeneo hayo kupata umeme bila kupitia kituo cha Ubungo  ambacho kipo katika matengenezo.

  Tatu, Kufungua njia ya umeme ya kilovolti 132 itokayo Kituo cha Kunduchi   hadi Mlandizi na kuunga maeneo hayo katika njia ya umeme ya kilovolti 132 itokayo Morogoro ili kuwezesha jiji la Dar es salaam kuwa na umeme wa uhakika.

  Nne, Kufungua laini ya msongo wa kilovolti 132 kati ya Ubungo na Chalinze upande wa Ubungo ili kutozihusisha transfoma za Ubungo kwenye mzigo wa mikoa mingine na hivyo kutumika kuhudumia  wateja wa  Dar es Salaam na Zanzibar pekee.

   Tunatarajia matengenezo haya yanayokwenda kwa awamu yatakamilika ifikapo mwezi Juni 2019.

  TANESCO itaendelea kutoa taarifa ya Maendeleo ya kazi ya matengenezo ya kituo cha Ubungo yenye lengo la kuwezesha upatikanaji wa umeme wa uhakika Dar es salaam na Zanzibar kwa siku zijazo 

  Kituo cha miito ya simu 2194400 na 0768 985100

  Tovuti: www.tanesco.co.tz, 

  Mitandao ya kijamii

  Twitter, www.twitter.com/tanescoyetu,

   Facebook https://www.facebook.com/tanescoyetultd/

  IMETOLEWA NA:

  OFISI YA UHUSIANO
  TANESCO MAKAO MAKUU

  0 0

  Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha.

  SHULE ya msingi Maendeleo ,kata ya Mailmoja Kibaha, mkoani Pwani, inakabiliwa na msongamano mkubwa wa wanafunzi ambapo darasa moja lina wanafunzi 284.

  Changamoto hiyo aliitaja ,mwalimu mkuu wa shule hiyo Miriam Mkama wakati mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kata ya Maili Moja Mathayo Mkayala alipofanya ziara kutembelea miradi ya elimu na barabara akiwa na kamati ya siasa ya kata hiyo .

  Alisema ,shule hiyo ina wanafunzi wengi ikiwemo wa awali wanafunzi 153, la kwanza wako 284 la pili wako 209, tatu wako 210, la nne wako 171, la tano wako 177, la sita wako 175, saba 158 na memkwa wako sita.

  Alitaja changamoto nyingine ,ni upungufu wa vyoo ambapo wavulana 792 wanatumia vyoo vitano mapungufu 26 upande wa wasichana 756 wanatumia vyoo vinne .

  Nae mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Maili Moja ,Mathayo Mkayala alisema ,kutokana na hali hiyo kuna kila sababu ya wananchi wa kata ya maili Moja kusaidia ujenzi wa madarasa mapya ili kupunguza msongamano huo ambao unahatarisha wanafunzi kutoweza kusoma vizuri.

  "Wanafunzi wamejazana hata namna ya kufundishwa inakuwa ni ngumu hili ni tatizo hivyo wananchi wanapaswa kuliangalia suala hili kwa upekee kwa kujenga madarasa mengine,” alisema Mkayala.

  Awali, diwani wa Kata ya Maili Moja ,Ramadhan Lutambi alisema ,changamoto ni kubwa na wameanza mchakato wa kuwaomba wazazi na wananchi kujitolea matofali matatu yamefika 980 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ambapo kwa sasa wameanza darasa moja linalojengwa na wananchi.

  Kamati hiyo ya siasa ya kata ya Maiali Moja ilitembelea baadhi ya miradi ya ujenzi wa shule ya msingi Muheza, ujenzi wa madarasa matatu shule ya msingi maendeleo, ujenzi wa vyoo shule ya sekondari Bundikani na ujenzi wa barabara toka shule ya Bundikani kwenda Mpakani.

  0 0


  Jumla ya Tani 106 za Bidhaa mbali mbali ikiwemo Mchele zimeteketezwa na Wakala wa Chakula Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDA) baada ya kubainika hazifai kwa matumizi ya Binadamu.
  Zoezi la kuteketeza bidhaa hizo limefanyika Jaa la Kibele Mkoa wa Kusini Uguja na kusimamiwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ZFDA Dkt. Kahamis Ali Omar.
  Akizungumza na Wanahabari wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo Dkt. Khamis alisema lengo la uteketezaji wa bidhaa hizo ni kuzizuia zisiingie katika mzunguko wa Soko na kwenda kuathiri Wananchi ambao wangezitumia.
  Amezitaja bidhaa hizo kutoka Makampuni tofauti kuwa ni pamoja na Mchele, Juice, Tomato, Maziwa, Dawa za Mbu na Pempus za Watoto ambazo zote ziliingizwa kutoka nje ya nchi.
  “Kiujumla bidhaa nyingi zimeharibika kutokana na mzungungo wa usafiri ambazo zingine ziliingia maji chunvi ikiwemo Mchele, Juice na Maziwa na baadhi ndio zimepitwa na muda” alisema Dkt. Khamis
  Dkt. Khamis amesema wapo Wafanyabiashara ambao wameanza kuelewa umuhimu wa mashirikiano na ZFDA na hivyo kuitaarifu ofisi yao pale bidhaa zao zinapopata hitilafu kwa ajili ya kuchukuliwa hatua.
  Ametoa wito kwa Wafanyabiashara wengine kutoa ushirikiano na ZFDA ili kuendelea kuingiza bidhaa ambazo zinaviwango kwa faida ya Wananchi na Taifa kwa ujumla.
  “Ushauri wangu kwa wafanyabiashara pale bidhaa zao zinapoharibika basi waje moja kwa moja ofisini kwetu ili tuchukue hatua za kuziangamiza kwa ushirikiano” alinasihi Dkt. Khamis
  Hata hivyo alisisitiza kuwa watashirikiana vyema na Wafanyabishara waaminifu lakini wale ambao watakua wanakiuka taratibu ZFDA itawachukulia hatua za kisheria.
  Amefafanua kuwa katika kuhakikisha zoezi hilo linafanyika kwa ufanisi mkubwa hushirikina na wadau mbali mbali ikiwemo Maafisa kutoka Idara ya mazingira.
  Kaimu Mkurugenzi huyo wa ZFDA alitoa wito kwa Wananchi kuwafichua wafanyabishara wanaouza bidhaa zilizopitwa na wakati na wale wote wenye Ghala za kinyemela ili kuwachukulia hatua za kisheria.
  Wakala wa Chakula Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDA) umekuwa ukifanya juhudi mbalimbali ikiwemo kuwasimamia Wafanyabishara ili kuingiza Bidhaa nchini zenye ubora ambazo zitakuwa hazina madhara kwa watumiaji.
   Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ZFDA Dkt. Kahamis Ali Omar akizungumza na Wanahabari hawapo pichani kuhusu zoezi la kuteketeza bidhaa mbali mbali zilizoharibika huko Kibele Mkoa wa kusini Unguja.
   Wafanyakazi wa ZFDA wakipasua vipolo vya Mchele kwa ajili ya kuuteketeza, katika zoezi lililofanyika Jaa la Kibele Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
   Mchele usiofaa kwa matumizi ya Binaadamu ukiwa umemwaga tayari kuteketezwa katika Jaa la Kibele Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
   Gari la Katapila likiuteketeza Mchele usiofaa kwa matumizi ya Binadamu katika Jaa la Kibele.
   Shehena za Tomato zikiwa katika magari zikisubiri kuteketezwa huko katika Jaa la Kibele.
  Shehena za Maziwa na Juis zisizofaa kwa matumizi ya Binadamu zikianza kushushwa katika gari ili kuteketezwa. Picha na Abdalla Omar-Maelezo Zanzibar


  0 0

  Anna Sangai (katikati) kutoka TGNP Mtandao akizungumza na wanahabari leo (hawapo pichani) kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Lilian Liundi kuhusiana na uzinduzi wa kampeni ya ulinzi wa mtoto iitwayo 1-5-5 Namlinda itakayozinduliwa Februari 27. Kulia ni Muibuaji na Mfuatiliaji Miradi, Janeth Mawinza akiwa katika mkutano huo.
  Anna Sangai (katikati) kutoka TGNP Mtandao akizungumza na wanahabari leo (hawapo pichani) kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Lilian Liundi kuhusiana na uzinduzi wa kampeni ya ulinzi wa mtoto iitwayo 1-5-5 Namlinda itakayozinduliwa Februari 27. Kulia ni Muibuaji na Mfuatiliaji Miradi, Janeth Mawinza akiwa katika mkutano huo.
  Muibuaji na Mfuatiliaji Miradi, Janeth Mawinza (katikati) akifafanua jambo kwa wanahabari leo (hawapo pichani) kuhusiana na uzinduzi wa kampeni ya ulinzi wa mtoto iitwayo 1-5-5 Namlinda itakayozinduliwa Februari 27. Kulia ni Rehema Mwateba mwanachama wa TGNP akiwa katika mkutano huo pamoja na Anna Sangai kushoto.  “Mlinde mtoto afurahie utoto wake, ujana wake na uzee wake”

  Ukatili dhidi ya watoto umekuwa ni sehemu ya maisha ya watoto wengi nchini. Mojawapo ya aina za ukatili unaokumba kundi hili ni ukatili wa kingono.

  Mnamo mwaka 2011, nchi yetu ilitoa taarifa ya utafiti uliofanyika kuhusu ukatili dhidi ya wanawake na watoto, utafiti huo uligundua kuwa karibia mmoja kati ya wasichana watatu na mmoja kati ya wavulana saba wamekutana na ukatili wa kingono kabla ya kutimiza miaka 18.

  Hata hivyo, kulingana na utafiti huo, wengi wa watoto hawatoi taarifa juu ya vitendo hivyo, wachache wanatafuta huduma na wachache zaidi wanafanikiwa kupata matibabu au msaada wanapotoa taarifa ya matukio hayo. Pia, ripoti iliyotolewa na Kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) zinaonyesha kuwa matukio ya ukatili wa kingono miongoni mwa watoto yanaongezeka nchini.

  Kulingana na ripoti hiyo iliyotolewa Juni 2018, wastani wa watoto 394 wamebakwa kila mwezi katika maeneo mbalimbali Tanzania bara, huku ulawiti wa watoto ukiongezeka kutoka matukio 12 kwa kipindi cha Januari hadi Juni 2017 hadi matukio 533 kwa kipindi cha Januari hadi Juni 2018, na mikoa inayoongoza kwa matukio hayo ni Dar es salaam na Iringa.

  Vitendo hivi havikubaliki katika jamii kwani ni kinyume cha haki za binadamu na mikataba mbalimbali ya kimataifa, na kikanda iliyoridhiwa na serikali juu ya ulinzi wa mtoto dhidi ya aina zote za ukatili wa kijinsia. Mikataba hiyo ni pamoja na Mkataba wa haki za mtoto wa mwaka 1989, tamko la Afrika juu ya haki na ustawi wa mtoto la mwaka 1990.

  Vitendo hivi vinarudisha nyuma maendeleo ya mtoto na taifa kwa ujumla. Miongoni mwa athari zitokanazo na ukatili wa kingono dhidi ya watoto ni pamoja na watoto kuathirika kisaikolojia, maambukizi ya magonjwa ya zinaa na UKIMWI, mimba za utotoni, na kubwa zaidi ni kuhatarisha ustawi wa taifa na kuchochea uongezeko la vitendo hivi katika jamii.

  Kutokana na takwimu hizo, hali ya tatizo ni kubwa sana, jambo ambalo limesukuma TGNP Mtandao kuja na kampeni ya ulinzi wa mtoto iitwayo 1-5-5 Namlinda. Kampeni hii inachangia katika jitihada za serikali kutokomeza aina zote za ukatili dhidi ya watoto kupitia Mpango wa Taifa wa Kutokomeza dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) unaolenga kupunguza ukatili dhidi ya wanawake na watoti kwa asilimia 50 ifikapo 2022.

  Kampeni hii inalenga kuendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya athari za ukatili wa kingono kwa watoto na umuhimu wa kuwalinda dhidi aina hiyo ya ukatili, kutathmini na kuibua mijadala katika jamii juu ya hali halisi ya ukatili wa kingono, kuhamasisha jamii kuzuia vitendo hivi visitokee na kutoa taarifa mara waonapo matukio hayo ya ukatili wa kingono kwa watoto ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua stahiki.

  Kampeni hii pia inalenga kujenga nguvu za pamoja na wadau mbalimbali nchini katika kuweka mikakati ya pamoja ya ulinzi wa mtoto dhidi ya ukatili wa kingono na kuhakikisha kila mtu katika jamii anajisikia kuwajibika kumlinda mtoto.

  Hivyo, kampeni hii imelenga kuwafikia wanawake, wasichana, wavulana, wanaume, viongozi wa dini, serikali, jamii, vyombo vya habari, madawati ya jinsia polisi, asasi za kiraia, wadau wa maendeleo, makungwi, watoa huduma za afya,wanaharakati, watoa huduma za usafiri wa umma kama bodabodaa na daladala pamoja na wabunge, na wanasiasa.

  Kampeni hii inatarajiwa kuzinduliwa rasmi tarehe 27 Februari 2019 ambapo wawakilishi wa wadau mbalimbali ambao ni walengwa wa kampeni watashiriki ili kupitishwa katika kampeni hii na kujadiliana kwa pamoja wajibu wa kila kundi katika ulinzi wa mtoto. Kampeni hii inatarajiwa kuzinduliwa rasmi na mkuu wa jeshi la polisi Tanzania-IGP Saimoni Sirro.

  Jamii inawajibu wa kuwalinda watoto dhidi ya vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia. Hii ni kwa mujibu wa sheria ya mtoto na. 21 ya mwaka 2009 na mpango kazi wa taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

  TGNP Mtandao, inaamini kuwa ikiwa kila mtu katika jamii atatimiza wajibu wake vizuri wa kumlinda mtoto, Tanzania billa ukatili wa kingono kwa watoto inawezekana. Pia, TGNP inaamini kuwa ikiwa watoto watakuwa huru dhidi ya aina zote za ukatili wa kijinsia, tutakuwa na taifa imara lenye viongozi bora, nguvukazi iliyo na afya njema na tutaweza kufikia malengo ya dunia ya maendeleo endelevu. Madai yetu katika kampeni hii ni pamoja na:-

  Kuitaka jamii kuguswa na tatizo la ukatili wa kigono kwa watoto wakiwa nje na ndani ya shule Jamii ichukue hatua za kumlinda mtoto popote alipo. Kila mmoja alipo asimamie ulinzi wa mtoto vyombo vya habari vitoe elimu kwa wingi juu ya athari za ukatili wa kingono kwa watoto, faida ya kuwalinda watoto na kuendelea kukemea vitendo hivyo vya ukatili dhidi ya watoto.

  Serikali kuu, serikali za mitaa na vyombo vya dola visimamie kikamilifu sheria ya kudhibiti uchawi na. 12 ya mwaka 1998(The Witchcraft Act). Ambayo imeainisha adhabu kwa watu wanaoendesha vitendo vya kishirikiana vinavyoweza kuwadhuru watoto na kuongeza vitendo vya ukatili wa kingono kama ubakaji.

  Tunatoa rai kwa jeshi la polisi na vyombo vingine vya dola kama wadau wa kutekeleza MTAKUWAA (NPA) kuhakikisha watoto wanakuwa salama kwa kuimarisha ulinzi katika maeneo yote yanayotajwa kuwa sio salama kwa watoto nchini.

  Kupitia kampeni hii jamii yote, kupitia mtu mmoja mmoja na kikundi inapaswa kumlinda na kuhakikisha ustawi wa mtoto. Tunaitaka serikali na wadau kuzijengea uwezo kamati za ulinzi wa watoto ili waweze kutimiza majukumu yao ikiwemo kubaini maeneo hatarishi katika kijiji/ mtaa na kupanga mikakati ya kupunguza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

  0 0

    Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Musoma Bi. Vicky Mbunde akifungua kikao cha Kamati ya Ulinzi wa Wanawake na Watoto ya Mkoa wa Mara kilichofanyika leo Mjini Musoma.
   Katibu Tawala msaidizi Utawala na Rasilimali Watu mkoa wa Mara Bi. Clothilde Komba akilezea umuhimu wa kikao cha Kamati ya Mkoa ya ulinzi wa Wanawake na  Watoto kilichofanyika leo Mjini Musoma.
    Mkurugenzi Msaidizi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Sebastian Kitiku akielezea umuhimu wa jumbe katika kuleta hamasa kwa jamii katika kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto katika kikao kilichofanyika leo mjini Musoma.  
   Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Mara Bi. Neema Ibamba akieleza mikakti ya mkoa wa Mara katika kutekelza Mpango wa Kitaifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto katika kikao kilichowakutanisha kamati ya Ulinzi wa Wanawake na Watoto mkoa wa Mara.
   Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Mathias Haule akielezea umuhimu wa uwepo wa Kamati ya Ulinzi kwa Wanawake na Watoto kwa Kamati ya Mkoa wa Mara katika kikaokilichofanyika leo mjini Musoma.
  Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi kwa Wanawake na  Watoto mkoa wa Mara wakifuatilia mada ,balimbali zizilokuwa zikitolewa katika kikao hicho kilichofanyika mkoani humo.Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

  Na Mwandishi Wetu Mara
  Mkoa wa Mara umeweka Mipango dhatiti katika kuhakikisha wanapambana na vitendo vya kikatili dhidi ya Wanawake na Watoto kwa kuhakikisha wanaifikia jamii katika kutoa ujumbe sahihi wa kuaondokana na vitendo vya kikatili hasa vitendo vya ukeketaji vilivyoshamiri mkoani humo.
  Hayo yamebainika leo mkoani Mara wakati wa kikoa cha wadau kutoka Kamati ya Ulinzi ya Wanawake na Watoto pamoja na wawakilishi wa Wakuu wa Wilaya zote za Mkoa wa Mara kwa lengo la kupokea jumbe mbalimbali zitakazosaidia kuelimisha jamii ya mkoa huo kuondokana na mila potofu zinozopelekea vitendo vya kikatili kwa wanawake na watoto.
  Akifungua kikao hicho Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Musoma Bi. Vicky Mbunde amesema kuwa kwa Mkoa wa Mara kuanzia mwaka 2010 mpaka 2013 vitendo vya ukatili wa kijinsia vilikuwa asilimia 72 na vimepungua kufikia asilimia 66 mwaka 2015/2016.
  Ameongeza kuwa tatizo la vitendo ya ukatili mkoa wa Mara sio vya kutengenzwa bali kwa kiasi kikubwa matatizo hayo husababishwa na mila potofu zinazochangiwa na uwepo wa mfumo dume ambayo inaathiri ustawi wa wanawake na watoto mkoani humo.
  Bi. Vicky asema kuwa Serikali ya Mkoa wa Mara imejipanga katika kuhakikisha inatokomeza vitendo vya kikatili dhidi ya wanawake na watoto ikiwemo utoaji wa elimu kwa kutumia jumbe zilizoandaliwa na mkoa kwa kutumia redio, magazeti na mikutano ili kuipa jamii uelewa wa juu ya madhara ya vitendo vya kikatili.
  Ameutaja mkakati mwingine kuwa ni kampeni ya kila mwisho wa mwaka ambapo vitendo vya ukeketaji hufanyika ili kuihamasisha jamii kuachana na mila porofu zinazomgandamiza mwanamke na mtoto.
  Akiwasilisha malengo ya kikao hicho Mwenyekiti wa Kamati hiyo kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa Clothilde Komba amesema kuwa lengo la kikao hicho ni kujadiliana na kupata namana bora ya kupambana na vitendo vya ukatili mkoani humo.
  Akiwasilisha jumbe katika kikao hicho Mkurugenzi Msaidizi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Sebastian Kitiku amesema kuwa jumbe hizo muhimu sana katika kuhakikisha jamii inabadilika na kuondokana na vitendo vya ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto.

  0 0

   Mshindi wa bodaboda ya biko na sh milioni moja, Deogratius Ngunyale, wa Kinondoni jijini Dar es Salaam ambaye pia ni daktari wa Hospitali ya Muhimbili, (katikati) akiwa na watu wake wa karibu katika makabidhiano ya bodaboda hiyo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam. Droo nyingine kubwa ya biko hufanyika kila Jumatano na Jumapili. Picha na mpigapicha wetu.
  Daktari wa Hospitali ya Muhimbili, Dkt Deogratius Patrick Ngunyale, amefanikiwa kukabidhiwa bodaboda yake na sh milioni moja aliyoshinda kutoka kwenye bahati nasibu ya biko iliyochezeshwa jana jumapili, jijini Dar es Salaam na daktari huyo mwenye maskani yake Kinondoni, jijini hapa akiibuka kidedea katika droo hiyo.

  Makabidhiano hayo yamefanyika leo jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Mratibu Msaidizi wa Matukio wa biko, Hassan Ahmed.

  Akizungumzia ushindi wake huo, dokta Patrick alisema kushinda bodaboda ya biko kutarahisisha maisha yake kwa kuhakikisha kuwa anaitumia katika mambo mbalimbali ya kukuza uchumi wake.

  Kucheza Biko ni kuanzia sh 500 na sh 1000 na kuendelea, huku ushindi wake ukianzia sh 1000 hadi sh 100000 kwa watakaocheza sh 500 hadi sh 9500 wakati watakaocheza kwa sh 1000 na kuendelea, mchezaji anaweza kujishindia zawadi ya papo kwa hapo kuanzia sh 5000 hadi sh milioni moja bila kusahau wote kuingia kwenye droo kubwa ya Jumatano na Jumapili.

  Bahati nasibu ya Biko inachezwa kwa mitandao ya simu minne ambayo ni Tigo Pesa, M-Pesa, Artel Money na HaloPesa, ambapo namba ya Kampuni ni 505050 na kumbukumbu namba 2456, huku Watanzania wakiweza kujishindia zawadi kubwa katika droo kubwa za Jumatano na Jumapili.

  0 0

   Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula akisema jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wataalam wa udhibiti ubora wa Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA na Wakala wa Chakula, Dawa na vipodozi Zanzibar (ZDFA) Jijini Dar Es Salaam.
  Picha ya Pamoja wajumbe wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula (aliyeketi wa tatu kulia)
   
   
  Na WAMJW- Dar es Salaam

  TANZANIA yatajwa miongoni mwa nchi 50 kati ya 194 duniani zenye mifumo imara na madhubuti ya udhibiti wa ubora wa bidhaa za vyakula, dawa na vipodozi.

  Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Zainab Chaula leo wakati alipokuwa akifungua mafunzo ya siku tano kwa wataalam wa udhibiti ubora wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi (ZDFA) na wenzao kutoka nchi ya Malawi.

  Mafunzo hayo maalum yameandaliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO-Tanzania) kwa lengo la kuwaongezea mbinu mbalimbali zitakazowasaidia kuimarisha nchi hizo kuongeza nguvu ya udhibiti wa bidhaa hizo.

  “WHO imetutambua na imetupa level (daraja) la tatu, hii ni hatua nzuri, TFDA imefanya kazi kubwa, hii inamaanisha mifumo ya udhibiti tanzania inatambulika duniani kote na kwamba misingi ya udhibiti ya mamlaka yetu imefikia ngazi ya kimataifa". Amesema Dkt. Chaula na kuongeza “Lakini pamoja na hatua hiyo lazima iendelee kujiimarisha ili ikiwezekana tupande daraja tufikie level 4 ambayo ndiyo kiwango cha juu zaidi".

  “Ili tuweze kuhakikisha tunafanya vizuri zaidi, mamlaka yetu inapaswa kutengeneza mifumo ya ufuatiliaji ubora na usalama wa bidhaa kuanzia viwandani hadi kwa mtumiaji, ili kuhakikisha hakuna dawa bandia zinaingia nchini mwetu”.

  Akiwasilisha mada Dkt. Alireza Khadem Broojerdi kutoka WHO amesema ili kuongeza nguvu ya udhibiti nchi zinapaswa kushirikiana kwa ukaribu.

  “Tunayo malengo 17 ya kidunia (SDGs), lengo namba tatu linasisitiza juu ya afya bora kwa wote, tunayo pia malengo ya mwaka 2019- 2030, mpaka sasa nchi 50 ikiwamo Tanzania sawa na asilimia 26 zimefikia daraja la tatu na nne. Nchi 45 sawa na asilimia 23 zipo daraja la pili, nchi 96 zimefikia daraja la kwanza na zingine zilizobaki bado hazijafikia viwango hivyo,” amesema Dkt. Khademu.

  Awali akizungumza Kaimu Mkurugenzi wa TFDA, Dkt. Candida Shirima amesema kupitia semina hiyo iliyoandaliwa na WHO watajifunza mbinu mbalimbali zitakazowasaidia kuweza kufikia malengo waliyojiwekea katika kuendelea kuimarisha mifumo ya udhibiti wa bidhaa hizo.

  0 0

  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa pili kushoto) akitoa maelekezo kwa viongozi wa Shule Kongwe ya Sekondari ya Wasichana Ruvu Mkoani Pwani, kuhakikisha maboresho ya shule hiyo yanakwenda sambamba na ufanisi katika utoaji taaluma, wakati alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua uboreshaji huo. Kulia ni Mbunge wa Kibaha Vijijini Mhe. Hamoud Juma na kushoto ni Mkuu wa Shule hiyo Bi. Juliana Chimazi.
  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa pili kulia), akikagua maboresho ya Shule Kongwe ya Sekondari ya Wasichana Ruvu, Mkoani Pwani, wa pili kushoto ni Afisa Elimu Sekondari wa Wilaya ya Kibaha Bi. Fatuma Kisanazo, watatu kushoto ni Mbunge wa Kibaha Vijijini Mhe. Hamoud Juma na kulia ni Mkuu wa Shule hiyo Bi. Juliana Chimazi.
  Muonekano wa Bweni la wanafunzi wa Shule Kongwe ya Sekondari ya Wasichana Ruvu, Mkoani Pwani, ambapo Mkuu wa Shule hiyo Bi. Juliana Chimazi, aliomba Serikali isaidie katika kuboresha miundombinu ya nyumba 6 za walimu ambayo haijakarabariwa baada ya fedha sh. milioni 990 kumalizika kabla ya kazi hiyo kukamilika.
  Afisa Elimu Sekondari wa Wilaya ya Kibaha Bi. Fatuma Kisanazo, akitoa ufafanuzi wa namna walivyosimamia fedha za Serikali zilizotolewa kwa ajili ya kuboresha Shule Kongwe ya Sekondari ya Wasichana Ruvu, Mkoani Pwani, wakati wa ziara yua kikazi ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (hayupo pichani) wilayani Kibaha Mkoani Pwani.
  Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Ruvu, Mkoani Pwani Bw. Shaibu Mangalu, akielezea namna Shule hiyo ilivyotumia utaratibu wa shule hiyo kwa njia ya Force Account uliogharimu takribani Sh. milioni 992, wakati Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipotembelea na kukagua maboresho hayo.
  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa sita kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Mbunge wa Kibaha Vijijini, Viongozi na walimu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Ruvu, Mkoani Pwani, ,baada ya kukagua uboreshaji wa miundombinu ya shule hiyo .Picha na Peter Haule, Wizara ya Fedha na Mipango).

  0 0

  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Lindi Bw. Shaibu Ndemanga mara baaya ya kufanya ziara ya kukagua dampo la Manispaa hiyo ili kujionea uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira. Katika dampo hilo lililopo eneo la Machole Manispaa ya Lindi Naibu Waziri Sima ameuagiza uongozi wa Mkoa kusitisha umwagaji wa maji taka katika eneo hilo.
  Naibu Waziri Mussa Sima akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Wilaya na Halmashauri ya Mkoa wa Lindi mara baada ya kukamilika kwa kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi. Pamoja na mambo mengine, kikao hicho kimeweka mikakati ya kuhifadhi ikolojia ya vyanzo vya maji vinanvyochangia maji katika bonde la Rufiji
   
   
  Na Lulu Mussa,LINDI .

  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima ameuagiza Uongozi wa Mkoa wa Lindi kusitisha mara moja hatua ya kumwaga maji taka katika dampo la Halmashauri hiyo.Agizo hilo limetolewa hii leo Mkoani Lindi mara baada ya kufanya ziara ya kikazi ya kukagua uzingatiaji na Usimaimizi wa Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004. 
   
  Akiwa katika Halmashauri hiyo Mhe. Sima amejione uchafuzi mkubwa mazingira kwa Halmashauri ya Lindi kuchanganya taka ngumu na maji taka katika dampo moja na kuagiza uongozi wa Mkoa huo kusitisha mara moja utaratibu huo na kupiga marufuku wananchi kuingia kiholela katika dampo hilo.“Utaratibu wa kutofautisha taka uanzie nyumbani na katika sehemu za kukusanyia taka, taka zikiletwa hapa dampo ziwe zimeshachambuliwa, huu utaratibu wa watu kuingia hapa dampo kuokota chupa za plastiki usitishwe mara moja” Alisisitiza Naibu Waziri Sima.
   
  Waziri Sima amesema kuwa kuna uwezekano mkubwa wa taka hatarishi kutupwa dampo kwakuwa hakuna mkakati madhubuti wa kutenganisha taka hizo toka kwenye vyanzo vya uzalishaji.Ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake katika Mkoa wa Lindi Naibu Waziri Sima pia amepata fursa ya kuongea na Viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi wakiwemo madiwani na viongozi wa Serikali za Mitaa kuweka mikakati madhubuti ya kutunza Ikolojia ya Vyanzo vya Maji ambavyo ni mto Njenje na Parang’andu ambavyo hutirisha maji yake katika Mto Luwengu ambao humwaga maji yake kati katika Mto Rufiji.
   
  “Ndugu zangu sote tunafahamu umuhimu wa hifadhi ya Mazingira na umuhimu wa Bonde la Mto Rufiji katika uzalishaji wa Umeme wa Uhakika, sisi watu wa Mazingira hii kwetu ni fursa, maana uzalishaji wa umeme utasaidia kuhifadhi mazingira kwa kupunguza matumizi ya kuni na mkaa. Nawasihi wote tuwe mstari wa mbele katika kuhakikisha sisi tunakuwa mfano wa kulinda vyanzo vya maji.” Sima alisisitiza.
   
  Aidha, Naibu Waziri Sima pia amepata fursa ya kutembelea Hospitali ya Mkoa wa Lindi na kuridhishwa na Mtambo maalumu wa kuteketeza taka ulipo Hospitalini hapo na kuagiza majengo yayojengwa katika Sekta ya Afya kuweka miundombinu ya kuvuna maji.Naibu Waziri Sima yuko katika ziara ya kukagua changamoto za kimazingira pamoja na kuweka mikakati ya kuzipatia ufumbuzi na pia kuhimizi usimamizi endelevu wa Mazingira kwenye ikolojia ya vyanzo vya maji vinavyochangia maji katika Bonde la Rufiji.

older | 1 | .... | 1808 | 1809 | (Page 1810) | 1811 | 1812 | .... | 1897 | newer