Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live

MADIWANI WA MANISPAA YA MUSOMA WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO MKOANI RUKWA

0
0
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Albinus Mugonya akiwakaribisha Madiwani 12 wa Manispaa  ya Musoma (kulia) waliongozana na baadhi ya watumishi sita kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya. Msafara huo umefika Mkoani Rukwa kwa ziara ya kujifunza mambo mbalimbali ya kiuongozi kutoka kwa madiwani wenzao wa Manispaa ya Sumbawanga na Serikali ya Mkoa kwa ujumla.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Sumbawanga Sabas Katepa akiwatambulisha madiwani mbalimbali kutoka Manispaa ya Musoma Mkoani Mara walipofika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kwa ajili ya utambulisho katika ziara yao ya mafunzo Mkoani Rukwa. 
Madiwani hao walipata fursa ya kutembelea ukumbi wa kurushia mawasiliano ya moja kwa moja (Video Conference) ambayo yanauwezo wa kuziunganisha ofisi mbalimbali za Serikali katika kikao kimoja. Pichani Mchambuzi wa mifumo ya Kompyuta Galus Ouma akitoa maelezo mafupi na namna mtandao huo unavyofanya kazi.
Madiwani hao walitembelea pia makumbusho ndogo ya Mkoa iliyopo katika jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa. Makumbusho hii imesimama kwa nguvu kubwa iliyowekwa na Mkuu wa Mkoa wa huo Injinia Stella Manyanya ambapo taarifa mbalimbali za kimkoa na taifa zinapatikana.
Baadhi ya tuzo mbalimbali ambazo Mkoa wa Rukwa umewahi kuzipata pia zinapatikana katika makumbusho hii.
Baadhi ya zana za asili ya jamii ya watu wa Rukwa zinapatikana katika makumbusho hii. 
Picha za Wakuu wa Mikoa waliowahi kuungoza Mkoa wa Rukwa tangu ulipoanzishwa mwaka 1974 zinapatikana katika makumbushi hii.
Picha ya Pamoja.
(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)

RAIS KIKWETE AKIWA MGENI RASMI SHEREHE YA SIKU YA WATU WENYE ULEMAVU DUNIANI

0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua rasmi alama mpya za barabarani kwa watu wenye ulemavu wakati wa sherehe ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo Novemba 3, 2013. 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea tuzo toka kwa Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu, Bi. Lupi Maswanya wakati wa sherehe ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo Novemba 3, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Usalama barabarani ya Watu wenye Ulemavu (NCPDRS) na mbunifu wa alama za barabarani kwa watu wenye ulemavu ,Bw. Jutoram Kabatelle,kabla ya kuzindua rasmi alama mpya kwa watu wenye ulemavu wakati wa sherehe ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo Novemba 3, 2013. 
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wadau wa SHIVIWATA wakati wa sherehe ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo Novemba 3, 2013
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembelea mabanda ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na watu wenye ulemavu wakati wa sherehe ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo Novemba 3, 2013 .PICHA NA IKULU.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipongeza baada ya kupokea risala toka kwa Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu (SHIRYAWATA) akisoma risala kwa kutumia Braille huku mkalimani wa lugha ya alama akifanya kazi hiyo (kulia) katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo Novemba 3, 2013 kuwa mgeni rasmi kwenye sherehe ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo Novemba 3, 2013 akiwa  mgeni rasmi kwenye sherehe ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani.


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na  Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu (SHIRYAWATA) akiwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Hussein Mwinyi pamoja na Mwenyekiti wa (SHIVWATA) baada ya kuhutubia  katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo Novemba 3, 2013 kwenye sherehe ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akitoa cheti kwa  Bw. Frederick Msigallah wa CCBRT katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo Novemba 3, 2013 kwenye sherehe ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi hati mwakilishi na Mtangazaji wa ITV i katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo Novemba 3, 2013 kwenye sherehe ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani. 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa cheti kwa niaba ya TBC Mtangazaji mahiri wa stesheni hiyo ya Taifa Bi. Amina Mollel  katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo Novemba 3, 2013 kwenye sherehe ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani.PICHA NA IKULU.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokewa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Hussein Mwinyi alipowasili katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo Novemba 3, 2013 kuwa mgeni rasmi kwenye sherehe ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani
 Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu (SHIVYAWATA) Bw. Amon Anastaz akisoma risala kwa kutumia braille katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo Novemba 3, 2013 kwenye sherehe ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipongeza baada ya kupokea risala toka kwa Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu (SHIRYAWATA) akisoma risala kwa kutumia Braille huku mkalimani wa lugha ya alama akifanya kazi hiyo (kulia) katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo Novemba 3, 2013 kuwa mgeni rasmi kwenye sherehe ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani

DK MIGIRO APONGEZWA NA WENGI KWA KUTEULIWA NA RAIS KUWA MBUNGE

0
0
 Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akipongezwa na Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye kwa kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa Mbunge, jioni mjini Mbalizi, jijini Mbeya. Viongozi hao wamo kwenye ziara ya kuimarisha chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM.

Akizungumzia uteuzi huo, mjini Mbalizi jioni hii,
Dk. Migiro amemshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa uteuzi huo ambao ameupokea kwa furaha, na kueleza kuwa kitendo hicho kinadhihirisha jinsi Rais Kikwete alivyo na imani naye pamoja na imani kwa Wanawake wa Tanzania.
 Dk. Migiro (kulia), akipongezwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwa uteuzi wake huo.
 Dk. Migiro akizungumza na vyombo vya habari, jinsi alivyopokea kwa furaha uteuzi wake huo.
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro akimpongeza Dk. Migiro kwa kuteuliwa na Rais Kikwete kuwa Mbunge.

DR ASHAROSE MIGIRO AZUNGUMZIA KUTEULIWA KWAKE KUWA MBUNGE.

0
0

HUYU NA YULE: Mahojiano na waTanzania Evans Mhando na Fatuma Matulanga wakiwa CHINA

0
0
WaTanzania Evans Mhando (L) na Fatuma Matulanga (M) walipokutana jijini Beijing nchini China. Wiki hii walikuwa wageni katika kipindi cha HUYU NA YULE kinachotayarishwa na Mubelwa Bandio (R) wa Jamii Production.

Katika huyu na yule wiki hii, nimepata nafasi ya kuzungumza na vijawa wawili wa kiTanzania wanaosoma nchini China. Nao ni Fatuma Matulanga aliyeko Beijing na Evans Mhando aliyeko Nanchang ambao kwa pamoja tumejadili mambo kadhaa na zaidi kuhusu vijana
Wameeleza mengi wakioanisha kijana na maisha ya China na Tanzania ikiwemo
1: TOFAUTI KATI YA KIJANA WA CHINA NA TANZANIA
2:TOFAUTI KATI YA ELIMU YA CHINA NA KWINGINE. Ni kweli kuwa China haifunzi ubunifu na ndio maana wanasifika kwa kuendeleza kuliko kubuni?
3: MALALAMIKO KUWA BIDHAA ZA CHINA HAZINA UBORA, YANATAZAMWA VIPI HUKO CHINA?
4: NI KIPI WANACHOJUA SASA KUHUSU CHINA AMBACHO HAWAKUJUA KABLA HAWAKWENDA CHINA?
5: MABADILIKO YA SERA YA MTOTO MMOJA MNAONA IMEPOKELEWA VIPI HAPO?
6: NI KIPI WANACHOTAMANI KINGETOKA CHINA KWENDA TANZANIA (HASA KATIKA TASNIA YA HABARI?)
Na mengine mengi

Ni huyu na Yule ya Mubelwa Bandio wa Jamii Production akihojiana na Fatuma Matulanga na Evans Mhando, wanahabari wa shirika la utangazaji la Tanzania (TBC) wanaojiendeleza kielimu nchini China
Kwa maoni ama ushauri, usisite kutuandikia kupitia jamiiproduction@gmail.com

KATIBU MKUU WA CHADEMA ZIARANI, SHINYANGA, KIGOMA, TABORA na SINGIDA

0
0

ZIARA YA KATIBU MKUU DKT. WILLIBROD SLAA


Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willibrod Slaa ataanza ziara ya siku 20 katika mikoa ya Shinyanga, Kigoma, Tabora na Singida kuanzia Desemba 4-23, mwaka huu.  


Lengo la ziara hiyo ambayo imetokana na maombi ya muda mrefu ya viongozi wa chama katika maeneo husika, ni kuimarisha na kukagua uhai wa chama katika ngazi za chini hususan kata na majimbo mikoa hiyo.


Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu Dkt. Slaa atakutana na wananchi katika mikutano ya hadhara ambapo atazungumzia masuala mbalimbali ya kitaifa na eneo husika, kisha atafanya vikao vya ndani vya kichama.


Ziara hiyo itaanzia mkoani Shinyanga ambapo siku ya Jumatano Desemba 4, mwaka huu, Katibu Mkuu Dkt. Slaa atakuwa Wilaya ya Kahama, siku inayofuata Desemba 5, atakuwa Wilaya ya Kakonko, Jimbo la Buyungu na Desemba 6, atakuwa Jimbo la Muhambwe.


Ratiba ya siku zinazofuata itaendelea kutolewa kwa vyombo vya habari.


Imetolewa leo Jumanne, Desemba 3, 2013, Dar es Salaam na;

Tumaini Makene


Ofisa Mwandamizi wa Habari CHADEMA

HIKI NDIO CHANZO CHA BINTI HUYU KUPATA UJAUZITO.

0
0

KINANA MA UJUMBE WAKE WAWASILI MBEYA MJINI,AKUTANA NA WAFANYAKAZI WA TAZARA,KUUNGURUMA JIONI MKUTANO WA HADHARA.

0
0
katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na ujumbe wake wakizungumza na Wafanyakazi wa TAZARA-Iyunga,Wilayani Mbeya mjini Mkoani Mbeya mapema leo,kuhusiana na matatizo mbalimbali yanayoikabiri shirika hilo nchini.

Kinana alisikiliza changamoto mbalimbali kutoka kwa Uongozi wa Shirikia hilo ikiwemo suala la Uchakavu wa mitambo na vitendea kazi,Upatikanaji wa Mafuta ya kuendeshea mitambo,Upungufu wa wafanyakazi,Kutolipwa Mishaharaya Wafanyakazi kwa wakati,Makato ya malimbikizo Michango ya Wafanyakazi kupeleka NSSF,Mafao kuchukua mda mrefu,Hujuma mbalimbali ndani ya shirika hilo, ukosefu wa magari na changamoto nyinginezo.

Ndugu Kinana katika kujibu na kutoa ufafanuzi wa changamoto hizo,alizipokea na kuomba kuzifanyika kazi ipasavyo na kuhakikisha TAZARA inaimarika.Aidha aliongeza kwa kusema kuwa kuna baadhi ya Changamoto zinatokana na baadhi ya wenye Malori kufanya hujuma mbalimbali kuhakikisha TAZARA inaendelea kudidimika kila kukicha,kwamba hawapendi TAZARA ifufuke,Kwa hivyo tutafute namna ya kuimarisha TAZARA
 Wafanyakazi wa Shirika la TAZARA wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipozungumza nao mapema leo,kwenye ukumbi wa mikutano wa shirika hilo mara alipowasili na ujumbe wake kutokea Mbeya Vijijini katika ziara ya kukiimarisha chama cha CCM.
 Mmoja wa wafanyakazi wa TAZARA,aliyejitambulisha kwa jina la Maulid Said  akzizungumza kuhusiana na hujuma mbalimbali zinazofanywa na baadhi ya watu ya kuhakikisha shirika hilo haliendelei,aidha ameitupia lawama Serikali kwa kuacha barabara zetu zikiharibika kila kukicha na Malori ya Mizigo kwa kuzidisha uzito huku ikishindwa kuliimarisha shirika la TAZARA ambalo lingeweza kupunguza ama kuliondoa kabisa tatizo hilo.
 Mfanyakazi wa TAZARA,aliyejitambulisha kwa jina la Seif Rashid akiuliza swali kuhusu suala la Mafao katika shirika hilo la TAZARA,akibainisha kuwa limekuwa tatizo sugu kwa Wafanyakazi wastaafu.
 Mmwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wilaya (Mbeya) TAZARA,Ali Mkami akisoma hotuba fupi mbele ya Katibu Mkuu wa CCM na Ujumbe wake uliofika kwenye shirika hilo na kuzisikiliza kero na changamoto mbalimbali zilizopo.
 Mbunge wa Viti Maalum Mkoani Mbeya Mary Mwanjelwa akiwasalimia Wafanyakazi wa TAZARA waliofika kuzungumza na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Ujumbe wake,akiwemo Katika wa NEC,Itikadi na Uenezi Nape Nnauye,Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt.Asharose Migiro.Ndugu Kinana na Ujumbe wake leo wako Mbeya mjini kuhitimiza ziara yao ya Kuimarisha chama cha CCM,Ziara hiyo ilianzia Mkoa wa Ruvuma na Mbeya na Njombe.
 Wafanyakazi wa TAZARA wakisikiliza kwa makini
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na uongozi wa TAZARA,Pichani kati Mkuu wa Wilaya ya Mbeya ,Mh.Norman Sigalla na shoto ni Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt.Asharose Migiro.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Ujumbe wake,Katika wa NEC,Itikadi na Uenezi Nape Nnauye,Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt.Asharose Migiro walipokuwa wakiwasili katika kijiji cha Iwambi kata ya Iwambi,Wilaya Mbeya mjini,mkoani Mbeya katika ziara ya Kukiimarisha chama chao.
Vijana na mambo yao wakimkaribisha Ndugu Kinana na ujumbe wake.

Airtel Money yaongeza kiwango cha kutoa pesa hadi shilingi milioni 3 kwa siku BURE

0
0
Meneja huduma ya Airtel Money Asupya Nalingigwa akiongelea ongezeko la kiwango cha kutoa pesa mpaka shilingi  milioni  3 kwa siku kupitia huduma ya Airtel Money wakati kampeni ya kutuma na kutoa pesa BURE ya hakatwi mtu hapa ikiendelea.Vilevile wateja wa Airtel wanaweza kuweka mpaka kiwango cha shilingi Milioni 5 kwa siku kwenye akaunti zao za Airtel Money.
-------------------------------------------------------------
 Kampuni ya mitandao ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania, imetangaza ongezeko la kiwango cha kuweka na kutoa pesa kupitia huduma ya Airtel Money.

Kampuni hiyo sasa inawawezesha wateja wa Airtel kote nchini kutoa mpaka kiasi cha shilingi milioni 3 kwa wateja waliosajili laini zao kikamilifu kwa kila siku anapotaka kutoa pesa kwa siku. Vilevile wateja hao wanaweza kuweka mpaka kiwango cha shilingi Milioni 5 kwa siku.

Akiongea wakati wa kutangaza ongezeko hilo, Meneja wa Airtel Money Asupya Nalingingwa alisema kwa sasa wateja watakuwa na uwezo wa kutoa na kuweka kiasi kikubwa cha fedha na kuepuka usumbufu wa kutoa au kuweka pesa mara nyingi.

“Wateja wa Airtel Money na wateja wote wa simu za mkononi wataweza kunufaika kwa kiasi kikubwa.  Wataepuka usumbufu na kujihakikishia usalama wakutosafiri na pesa nyingi kwa kuwa Airtel Money inaliwezesha hilo ambapo kwa sasa watatoa na kuweka kiasi kikubwa cha fedha tofauti na ilivyokuwa awali,” alisema Bw, Nalingigwa.

Aliongeza kwa kusema wateja wa Airtel Money ambao wameweshwa kwa muda mrefu kutuma na kupokea pesa bure kupitia huduma ya ‘Hakatwi Mtu hapa’ wanapata faida kwa kuokoa  kiasi cha shilingi elfu 20 kila wanapotuma  Milioni 3 Tzs na hivyo inasaidia kupunguza makali ya maisha na kurahisisha shughuli mbalimbali zikiwemo za kibiashara.

“Kama ningekuwa mfanyabiashara au mtu mwingine ambaye natumia pesa kwenye mzunguko kila siku, kupitia ongezeko hili ningejihisi mwenye faraja sana kwani shughuli zangu zingeenda vyema,” alimalizia Bw, Nalingigwa.
Kupitia ongezeko hilo kila mwananchi anaweza kutuma na kuweka kiasi cha fedha kulingana na mahitaji yake katika muda wowote unaomfaa.

HISIA ENTERS THE 6 FINALIST - 4 DAYS TO GO TO THE FINALE!

0
0

TANZANIANS THANKS FOR YOUR VOTES – 4 DAYS TO GO TO THE FINALE!
now
HISIA is among the 6 finalists!

5 DAYS to go before East Africa’s favorite music reality show produces an East African star for the 6th time through Tusker.

You have a say on who takes the grand price home.  Our Tanzanian representative HISIA depends on your votes to win.

EVERY SINGLE VOTE COUNTS!

HOW TO VOTE
a)      Create your account on https://tusker.mobi/register to have a say on who wins the grand price ( ONE VOTE PER DAY)

Or

b)      SMS the words Tusker12 to the number 15324 ( 5 SMS PER PERSON PER DAY)

Weruweru Alumni Meeting of Dec 08

0
0

MSIKILIZE MKONGWE WA UTANGAZAJI MASOUD MASOUD NDANI YA MKASI WA SALAMA.

0
0

Homa yapanda Uhuru Marathon

0
0
ZIKIWA zimebaki siku chache kwa ajili ya shindano la mbio ndefu za Uhuru, Uhuru Marathon, kufanyika, tayari wanariadha mbalimbali wameapa kufanyika katika mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam Desemba 8, mwaka huu.
 
Katibu wa Kamati ya Uhuru Marathon, Innocent Melleck alisema, homa ya mbio hizo imepanda, hasa baada ya kujitokeza kwa wanariadha wengi wa mataifa mbalimbali.
 
Melleck alisema, mbali na wengi kujitokeza bado anaamini wengi wataendelea kujiandikisha ili kufanikisha lengo lake. Mpaka sasa tayari kuna wanariadhaa maarufu waliojiandikisha kutoka Tanzania, Uganda, Kenya, Afrika Kusini, Ethiopia, Angola, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Malawi na Marekani.
 
Wengine wanatoka Ujerumani, Jamaica, Urusi, China, Japan, Venezuela, Comoro, Nigeria, Italia, Canada, Madagascar na Uturuki.  Mmoja wa wanariadha hao ni bingwa wa dunia wa marathon kwa upande wa wanawake, Edna Kiplagat wa Kenya anayetarajiwa kuwasili nchini Jumamosi.
 
“Hii ni faraja kubwa kwetu, kwani inaonyesha kwa kiwango kikubwa lengo letu la kupigania amani, umoja na mshikamano miongoni mwetu linakubalika na watu wengi duniani,” alisema.
 
Aidha Melleck alisema usajili bado unaendelea kwa wale wanaotaka kushiriki ambapo fomu zitakazotolewa kwa mshiriki wa kilomita 3 atalipa Sh 100,000 yule wa kilomita 5 Sh 2,000 na washiriki wa kilomita 21 na 42 watalipia Sh 6,000.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AMUAGA BALOZI MPYA NCHINI NIGERIA OLE NJOLAY

0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na kumkaribisha Balozi mpya nchini Nigeri, Ole Njolay, wakati alipofika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo mchana kwa ajili ya kumuaga akielekea kuanza kazi rasmi. Picha na OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Balozi mpya nchini Nigeri, Ole Njolay, wakati alipofika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo mchana kwa ajili ya kumuaga akielekea kuanza kazi rasmi. 

WAFANYAKAZI WA TAZARA WAOMBA TAZARA ICHUKULIWE NA WACHINA..!

0
0

MBUNGE WA IRINGA MJINI,MCH.MSIGWA AKANA TUHUMA ZA KUTOKABIDTHI FEDHA ZA RAMBI RAMBI ZA DAUDI MWANGOZI

0
0
Mbunge wa jimbo la Iringa mjini kupitia chama cha CHADEMA,Mch. PETER MSIGWA, amekanusha kuhusiana na tuhuma zinazomkabili juu ya kutokabidhi fedha za rambirambi kiasi cha shilingi milioni moja kwa mjane wa aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha wandishi wa habari mkoa wa Iringa marehemu DAUDI MWANGOSI, ambazo zilitolewa na wanachama wa CHADEMA waliopo nchini Uingereza na kusema kuwa tuhuma hizo si za ukweli, ni mambo ya uzushi na kwamba watu wanasema hivyo ili kumchafua  .


Akizungumza na na kituo cha redio ya Nuru fm ya Iringa,kupitia kipindi cha sunrise power,Mh. MSIGWA amesema kuwa ni kweli pesa hizo alipokea kupitia kwa MAJID MGENGWA na baada ya kupokea fedha hizo alichangisha tena fedha kwa wananchi wa jimbo la Iringa mjini kupitia mkutano, ambapo walichangia kiasi cha laki tatu  pamoja na yeye mwenyewe aliongezea kiasi cha shiringi laki tano ,hivyo kupelekea kufikia kiasi cha shiringi milioni moja na laki nane na sitini na nane na kumkabidhi mjane wa marehemu  DAUDI MWANGOSI.


Msigwa amesema kuwa ni wanasiasa tu wanaojaribu kuwachafua baada ya kuona kuwa wameshindwa na tayari amewasiliana na uongozi wa chama chake ili kuweza kulichukulia hatua gazeti ambalo limeandika tuhuma hiyo.


Wazazi na walezi waaswa kuwapeleka watoto kupata matone ya Vitamin A.

0
0

Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Lishe toka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Vincent Assey akieleza kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu mpango wa utoaji matone ya vitamin A ya nyongeza kwa watoto walio katika umri wa Miezi 6 hadi mitano, wakati wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Leo Jijini Dar es Salaam.

(Picha na Hassan Silayo)

Na Fatma Salum.
Wazazi na Walezi wamesisitizwa kuwapeleka watoto wenye umri wa Miezi sita hadi miaka Mitano kupata matone ya vitamin A yanayotolewa kwenye vituo vya Huduma za afya Kote nchini.

Msisitizo huo umetolewa na Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Lishe toka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Vincent Assey wakati wa Mkutano na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam.

Dkt. Assey alisema  kuwa zoezi la utoaji matone ya vitamin A kwa watoto linalofayika mara mbili kwa mwaka kila mwezi juni na disemba huenda sanjari na utoaji wa dawa za Minyoo kwa watoto wenye umri wa mwaka mmoja hadi miaka mitano.

Dkt. Assey alisisitiza kuwa matone hayo ni Muhimu kwa watoto kwani yanasaidia katika ukuaji,maendelezo ya afya na uhai wa mtoto.

“Ni muhimu kwa wazazi na walezi wafahamu kuwa, vyakula tunavyokula havikidhi mahitaji ya vitamin A mwilini kwa Mtoto, kwani mahitaji yao ni makubwa hivyo watoto hawana budi kupewa matone ya vitamin A mara mbili kila mwaka ili kukidi mahitaji hayo” Alisema Dkt. Assey.

Naye Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sayansi ya Chakula na Lishe kutoka Taasisi a Chakula na Lishe (TFNC) Dkt. Elifatio Towo alisema kuwa watoto walio katika umri wa Miaka Mitano wanapaswa kupewa vyakula vyenye Vitami A kwa Wingi kama Mboga za Majani ,Matunda, Dagaa, mafuta ya Mawese na Maini ili kuwaongezea vitamin hiyo isiyotengenezwa na Mwili hivyo ni lazima itokane na vyakula.

Aidha Dkt. Towo aliongeza kuwa madhara yatokanayo na upungufu wa vitamin A mwilini ni pamoja na kutokuona vizuri kwenye Mwanga hafifu, upofu, maradhi ya Mara kwa Mara na Vifo vya watoto, hivyo ili kupambana na tatizo hilo yapaswa kuzigatia unyonyeshaji sahihi wa watoto,ulaji wa vyakula vyenye virutubisho na watoto kupatiwa matone ya vitamin A.


Takwimu za kitaifa juu ya demografia na afya ya jamii (Demographic and Health Survey) za mwaka 2010 zinaonesha kuwa hapa nchini upugufu wa Vitamin A unaathiri asilimia 33 ya watoto walio chini ya Umri wa miaka 5 na Asilimia 37 ya wanawake walio katika Umri wa Kuzaa.

Taasisi ya Elimu Tanzania yadhamiria kuendelea kuinua kiwago cha elimu nchini

0
0
Kaimu Mkurugezi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt. Leonard Akwilapo akieleza kwa waandishi wa Habari(Hawapo Pichani) Kuhusu utekelezaji wa Majukumu ya Taasisi hiyo ikiwamo uendeshaji wa Mafunzo ya Mitaala kwa walimu nchini, wakati wa Mkutano Uliofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Leo Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Ubunifu na Uboreshaji wa Mitaala Bi. Angela Katabaro.
(Picha na Hassan Silayo)


Na Kiza Sungura

Taasisi ya Elimu Tanzania  [TET]imedhamiria kuendelea kuboresha utendaji wake ili kuinua kiwango cha elimu nchini. 

Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wataasisi hiyo Dr.Leonard Akwilapo wakati akizungumza na waandishi wahabari jijini Dar es Salaam.

Dr. Akwilapo alisema kuwa kwa kuzingatia mpango mkakati wamaendeleo wamiaka mitano (2011- 2016), taasisi hiyo inatarajia kufanya maboresho katika majukumu yake mbalimbali kwa lengo la kuleta tija katika sekta ya elimu nchini.

Akitaja mipango ya taasisi hiyo Dr. Akwilapo alifafanua kuwa ni pamoja na kufanya tahakiki ya mitaala katika ngazi zote, kuandaa vifaa vya kujifunzia nakufundishia vikiwemo vitabu, vifaa vya kielektroniki na vipindi vya redio na televisheni.

Aidha TET inatarajia kukamilisha andiko la Mwongozo wa Taifa wa Ukuzaji Mitaala, kufanya tathmini ya utekelezaji wa mitaala ya elimu ya awali hadi sekondari na kuendesha makongamano ya kitaifa na kimataifa kuhusu mitaala.

Pia Dr. Akwilapo aliongeza kuwa wana mpango wakujenga kituo cha kisasa cha mafunzo ya ukuzaji mitaala eneo la Mikocheni jijini Dar es Salaam, kuandika sera ya utafiti na uelekezi wa kitaalam pamoja na kuendesha mafunzo elekezi kwa walimu na watekelezaji wa mitaala.

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Ubunifu naUboreshaji Mitaala ya taasisi hiyo Bi Angela Katabaro alisema kuwa katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita taasisi imeweza kuboresha mihtasari ya masomo 26 ya ualimu ngazi ya cheti kwa elimu ya awali na msingi.

Pia Bi Katabaro aliongeza kuwa taasisi hiyo kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu- TAMISEMI ilichapisha na kusambaza mihtasari na miongozo ya masomo yote ya shule za msingi.

Kwa upande waelimu ya sekondari taasisi iliweza kuboresha mihtasari 25 ya kufundishia kidato cha tano na sita na kuendesha mafunzo ya utekelezaji wa mtaala wa sekondari kwa walimu wa shule mbalimbali za sekondari hapa nchini.

RAIS KIKWETE ATEUA KAMISHNA MPYA WA UHAMIAJI ZANZIBAR

0
0

CHINA WATILIANA SAINI NA WIZARA YA AFYA ZANZIBAR LEO

0
0
Waziri wa Afya wa Zanzibar Juma Duni Haji na Naibu Mkurugenzi Mambo ya Afya kutoka jimbo la Changzhou Dk. Chen Jiangua wakitia saini makubaliano ya ujenzi wa kituo cha maradhi ya Mifupa Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani na magonjwa ya tumbo Hospitali Kuu ya Mnazimmoja katika sherehe zilizofanyika Wizara ya Afya Mjini Zanzibar.
Waziri wa Afya wa Zanzibar Juma Duni Haji akibadilishana hati ya makubaliano na Naibu Mkurugenzi wa Mambo ya Afya wa Jimbo la Changzhou baada ya kutiliana saini makubaliano ya ujenzi wa kituo cha maradhi ya mifupa Hospitali ya Abdalla Mzee na Kituo cha magonjwa ya tumbo Hospitali kuu ya Mnazimmoja katika sherehe zilizofanyika Wizara ya Afya Mjini Zanzibar.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk. Muhammed Dahoma akiukaribisha ujumbe wa Madktari kutoka Jimbo la Changzhou katika sherehe za utiaji saini makubaliano ya ujenzi wa kituo cha maradhi ya mifupa na magonjwa ya tumbo katika Hospitali ya Abdalla Mzee, Mkoani Pemba na Hospitali Kuu ya Mnazimmoja katika sherehe zilizofanyika leo Wizara ya Afya Mjini Zanzibar.
Picha ya pamoja ya viongozi wa Wizara ya Afya ya Zanzibar wakiongozwa na Waziri wa Afya Juma Duni Haji na Ujumbe wa madaktari kutoka Jimbo la Changzhou ulioongozwa na Naibu Mkurugenzi wa Mambo ya Afya wa Jimbo hilo baada ya kutiliana saina makubaliano ya ujenzi wa kituo cha maradhi ya mifupa Hospitali ya Abdalla Mzee na kituo cha maradhi ya matumbo Hospitali ya Mnazimmoja. Sherehe hiyo ilifanyika Wizara ya Afya Mjini Zanzibar (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live




Latest Images