Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live

KAMISHNA JENERALI WA UHAMIAJI ATEMBELEA KAMBI YA WANAMICHEZO UHAMIAJI CHUO CHA MAGEREZA UKONGA JIJINI DAR ES SALAAM.

0
0
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala leo tarehe 22 Februari, 2019 amefanya ziara ya kuwatembela Wachezaji wa Timu za Mpira wa Miguu na Kikapu walioweka kambi katika Chuo cha Magereza Ukonga jijini Dar es salaam. 

Lengo la ziara hiyo ni kupata taarifa ya maandalizi, kukagua timu hizo na kuwatia hamasa katika kuelekea katika Mashindano ya Majeshi yatakayoanza kutimua vumbi kesho Jumamosi Februari 23. Michezo hiyo ya Majeshi hufanyika kila mwaka na huandaliwa na Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA). 

Akitoa taarifa ya Maandalizi na hali za wachezaji, Mwenyekiti wa BAMMATA Kanda ya Uhamiaji Naibu Kamishna wa Uhamiaji Nasra Jumaa alimweleza Kamishna Jenerali kuwa wachezaji wote wako katika hali nzuri na wana ari ya kushindana. 

“Afande Kamishna Jenerali tunashukuru kwa ujio wako hapa na napenda kukujulisha kuwa wachezaji wako katika hali nzuri, wana ari kubwa na wako tayari kuiletea ushindi na heshima idara yetu ya uhamiaji. Tunakuahidi ushindi tu” Alisema Naibu Kamishna Nasra. 

Naye Mwalimu wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Uhamiaji maarufu kama Kimbunga FC, Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji Wahid Mmanga akitoa taarifa kuhusu timu yake alisema kwamba wako tayari kupambana na kuleta ushindi dhidi ya timu nyingine za Majeshi kwani safari hii hawatokubali kuwa wasindikizaji. 

“Afande sie tumekuja kucheza ili tushinde, miaka iliyopita timu kutoka majeshi mengine walikuwa wakitumia wachezaji wa Timu zao ambazo ziko Ligi Kuu lakini kwa utaratibu mpya mwaka huu hakuna kutumia wachezaji wa timu za majeshi zilizo Ligi Kuu ya soka Tanzania hivyo tuna uhakika wa kuchukua kikombe” Alieleza Naibu Kamishna Mmanga. 

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Makakala alieleza kuridhishwa na maandalizi ya timu na kuwatakia wachezaji kila la kheri kwenye Mashindano hayo. “Nimefurahishwa na maandalizi, mnaonekana kweli mna ari na hamasa ya ushindi. Naomba mkacheze ili kuiletea heshima idara yetu, mimi na watumishi wote wa Uhamiaji tuko pamoja nanyi na tutawashangilia kila mnapocheza. Hii michezo inasaidia sisi kama jeshi la uhamiaji kujenga mahusiano mazuri na majeshi mengine ya nchi yetu, pia ni faida kwenu wachezaji kwani inawajengea afya bora kwa mazoezi mnayofanya. Niwatakie kila la kheri” . 

Michezo ya Majeshi kwa mwaka huu itashirikisha timu za wachezaji wa Mpira wa Miguu, Kikapu, Kuvuta Kamba, Kulenga shabaha na Riadha. Michezo hiyo itafunguliwa rasmi kesho Jumamosi saa nne asubuhi katika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es salaam.





RAIA WA ETHIOPIA AHUKUMIWA KIFUNGO MIAKA MIWILI JELA TABORA

0
0
Na Amisa Mussa
Mahakama Ya Hakimu  Mkazi  Mkoa  Wa  Tabora  Imemuhukumu  Kutumikia  Kifungo  Cha Miaka  Miwili Jela Au  Kulipa Faini Ya  Shilingi  Laki  Tano  Raia  Wa Ethiopia  Anayefahamika  Kwa  Jina  La  Gashahuni  Degu  Mwenye  Umri  Wa Miaka 21 Baada  Ya Kupatikana  Na Hatia  Ya  Kuingia  Nchini  Bila Kibali  Halali Kinyume  Cha  Sheria  Ya Uhamiaji  Sura  Ya 54 Iliyofanyiwa  Marejeo  Mwaka 2016.
Mwendesha  Mashitaka  Upande  Wa  Idara Ya Uhamiaji  Octavian  Kilatu Akisoma  Maelezo  Ya  Kosa Ameieleza  Mahakama Kuwa  Mtuhumiwa  Gashahuni  Alikamatwa Tarehe 21 Februari  Mwaka  Huu  Stend Kuu Ya Mabasi  Mjini  Tabora  Akisafiri  Kutoka  Mkoani  Mara  Kuelekea Mbeya  Hadi  Afrika  Ya  Kusini  Mahali  Ambako Alieleza  Alikuwa Anakwenda Kutafuta  Ajira.
Aidha Kutokana Na Hukumu Iliyotolewa  Na Hakimu  Mkazi  Mkoa  Wa  Tabora  Jocktan Rushwela  Ilifanya  Raia  Huyo  Wa Kigeni  Gashahuni  Degu  Kuangua   Kilio Hadharani  Katika  Viwanja  Vya  Mahakama  Akidai  Kuomba  Msamaha.

SERIKALI YAAGIZA WABADHIRIFU KWENYE VYAMA VYA MSINGI KUTUMBULIWA

0
0
Kaimu Mrajisi kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Wizara ya KilimoCharles Malunde amewataka warajisi wa kila mkoa kuwaondoa mara moja kwenye nafasi zao viongozi wa vyama vya msingi ambao watabainika kujihusisha na ubadhirifu wa fedha za ushirika huku akibainisha kuwa muda wakupiga dili umeshapita.

Hayo ameyasema leo Februari 22,2019 Mjini Shinyanga kwenye kikao cha Wadau wa Pamba kilichofanyika kwenye ukumbi wa SHIRECU,ambacho kimejumuisha mikoa sita ukiwemo mkoawaMwanza,Geita,Simiyu,Mara,Shinyanga na Tabora ambapo amesema ushirika wa sasa siyo kama ule wa zamani wa kupiga dili na kuongeza kuwa watahakikisha kila fedha ya vyama vya msingi inatumika ipasavyo. 

  Alisema suala la uchaguzi ndani ya vyama vya ushirika halina msimu na kuwataka warajisi wasaidizi wa kila mkoa kuchukua hatua haraka, iwapo kiongozi akienda kinyume na taratibu aondolewe mara moja katika nafasi yake kwani wanahitaji kuleta mabadiliko kwenye ushirika ambao utakuwa unaweza kujitegemea. 

“Tunahitaji mtu anayeingia kwenye ushirika ajitathimini kwanza mwenyewe ,tunahitaji kujenga ushirika na mahali popote pale mkigundua kuna shida chukueni hatua,najua hata nyinyi viongozi kama mngekuwa na shida leo hii tusingekuwa nanyi hapa kwenye kikao hiki ninachowasihi simamieni vizuri ushirika”,alisema kaimu mrajisi. 

  Kwa upande wake Meneja wa Bodi ya Pamba Kanda ya Ziwa Jones Bwahama alisema changamoto kubwa waliyokumbana nayo vijijini ni baadhi ya wakulima kutonyunyizia dawa pamba yao kwa hofu kuwa itakauka kutokana na mvua kutonyesha jambo ambalo ni upotoshaji mkubwa na kuwatakakupulizia ili kuzuia wadudu wasiendelee kuharibu. 

Alisema wakulima wasipopulizia viuadudu pamba inaendelea kuharibika kwani kuna wadudu wanaofyonza na wanaokula vitumba ambapo majani yanaanza kujikunja ,ambapo aliwaondoa hofu wakulima na kuwataka kupulizia pamba yao isiendelee kuharibika kwani haiwezi kukauka.Kikao hicho cha wadau wa pamba kimejumuisha warajisi wasaidizi wa mikoa,maafisa ushirika,viongozi wa vyama vya msingi na wadau wa zao la pamba,ambao wanatoka katika mikoa sita ambayo yote inajihusisha na kilimo cha pamba licha ya mikoa kufikia kwa sasa 17 lakini kikao hicho kimehusisha mikoa sita.  Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) Luhende Richard Luhende akifungua mkutano huo wa wadau wa zao la Pamba - Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blogKaimu Mrajisi kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Wizara ya Kilimo Charles Malunde akizungumza kwenye kikao hicho cha wadau wa zao la Pamba, na kuzitaka AMCOS kuacha kufanya kazi kimazoea.Wajumbe wa wakiwa kwenye mkutano.Wajumbe wakiwa kwenye mkutano wakisikiliza nasaha za viongozi.Meneja wa Bodi ya Pamba kutoka Kanda ya Ziwa Jones Bwahama akiwasilisha taarifa ya usambazaji wa Viatilivu pamoja na Maandalizi ya Msimu wa ununuzi wa Pamba katika msimu ujayo, na kuwataka wakulima wapulizie dawa na siyo kusubili hadi mvua zianze kunyesha.Nicodemas Sicilima ambaye ni meneja wa Mashirikiano wa mikoa na wilaya akiwasilisha taarifa ya mikakati ya kuendeleza zao la Pamba na vyama vya msingi vya ushirika Amcos.Anjelina Lukas ambaye ni Kaimu mafunzo kutoka chuo cha Ushirika Moshi Tawali la Kizumbi- Shinyanga, akiwasilisha mpango wa mafunzo kwa wajumbe wa Bodi na watendaji wa vyama, ili waweze kuwa na uwezo wa namna ya uandishi wa vitabu vya Amcos.Meneja wa Bank ya CRDB Tawi la Shinyanga Mjini Said Pamui akichangia mada namna taasisi hiyo ya fedha inavyoweza kushiriki kikamilifu katika kuchangia kutatua changamoto inavyovikabili vyama hivyo vya Ushirika, ikiwamo ukopeshaji wa fedha pamoja na kufungua akaunti za wakulima.Wajumbe wakiendelea na kikao.Meneja wa chama kikuu cha Ushirika Chato Joseph Masingiri akichangia mada kwenye kikao hicho.Kaimu Meneja wa chama cha ushirika Mbongwe na Bukombe Elikana Kagoma akichangia mada kwenye kikao hicho, ili kuboresha uzalishaji wa zao la Pamba.Meneja mkuu wa chama cha ushirika Igembensabo- Tabora Emmanule Malunde akichangia mada kwenye kikao hicho na kulalamikia kuwepo na baadhi ya vyama vya msingi vya Ushirika Amcos mkoani Tabora kutafuna fedha za ushuru wa zao la Pamba Milioni 122.Mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika mkoani Geita (GCU) Zainabu Shabani, akichangia mada kwenye kikao hicho na kulalamikia kuwepo na upungufu wa viatilifu vya kuulia wadudu pamoja na kutokwenda kwa wakati kwa wakulima.Joseph Mihangwa ambaye alikuwa mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) naye akichangia mada kwa lengo la kuboresha zaidi kilimo cha zao hilo la Pamba.Wajumbe wakiwa mkutanoni.Mkutano ukiendelea. Wajumbe wakisikiliza kwa makini uwasilishwaji wa mada pamoja na majibu ambayo wameuliza ili kuboresha zao hilo la Pamba.Mkutano ukiendelea.Wajumbe wakiwa mkutanoni.Awali mrajisi msaidizi kutoka mkoa wa Mwanza Saulo Paulo Lunyeka akisoma ajenda za kikao hicho cha wadau wa zao la Pamba.Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog

WAZIRI MBARAWA AAGIZA TAASISI ZA SERIKALI ZIFUNGIWE MITA ZA LUKU

0
0

WAZIRI wa Maji Proffesa Makame Mbarawa akizungumza baada ya kupokea taarifa ya mkoa wa Tanga wakati wa ziara yake leo
WAZIRI wa Maji Proffesa Makame Mbarawa kushoto akimsikiliza kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi wakati akielezea hali ya upatikanaji wa maji kwa mkoa wa Tanga wakati wa ziara yake
WAZIRI wa Maji Proffesa Makame Mbarawa kulia akisaini kitabu cha wageni wakati alipofika Ofisi za Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) kushoto ni Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Mhandisi Geofrey Hilly



WAZIRI wa Maji Proffesa Makame Mbarawa ameagiza taasisi zote za serikali zifungiwe mita za luku ili ziweze kwenda na matumizi mazuri ya maji ili kupunguza changamoto za kutokulipa kwa wakati bili za maji na kujikuta zikiingia kwenye madeni makubwa.

Proffesa Mbarawa aliyasema hayo leo wakati wa ziara yake mkoani Tanga ambapo alisema mita za luku litasaidia kuweza kuondokana na kasumba za watu kumwaga maji hivyo na hivyo kuweza kusimamia matumizi ya maji kwenye maeneo yao.

“Ndugu zangu mita za luku msiwapelee wateja sugu bali wapelekeeni hata wale watu wengine ambao wapo kwenye maeneo mbalimbali lakini pia Jeshi la Polisi sio wabaya wanalipa bili lakini wawekeeni mita za luko isipokuwa ndani ya kituo cha Polisi msiweke”Alisema Waziri Mbarawa.

“Lakini hatupelekei wateja sugu tunakosea kwa sababu hii inaweza kupelekwa kukote kwa sababu inaweza kusimamia matumizi ya maji ndani ya mwezi husika…..nirudir Jeshi la Polisi sio wabaya wanalipa bili zao lakini wawekeni mita sio mwanzo maeneo mengi Mtwara,,Iringa nao wanatumiakwenye kota zao wawekeeni mita hizo”Alisema Waziri Mbarawa.Aidha pia mita hizo la luku zitaweza kusaidia kuweka matumizi mazuri ya maji na mambo ya kuanza kulalamika hawalipi tuwafungie traasisi zio nyingi mita moja laki mbili ukchukua wateja 20 karibuni milioni nne na mapato yatakayopatikana ni makubwa.

Hata hivyo alsema serikali imejipanga kuhakikisha changamoto ya huduma ya maji hapa nchini inatatuliwa ili wananweza waweze kunufaika na huduma hiyo muhimu kwa ukuaji wa uchumi na maendeleo.Katika ziara hiyo Waziri Mbarawa alitembelea maeneo mbalimbali ikiwemo kwenye chanzo cha Maji cha Mabayani,Mtambo wa kusafirishia maji eneo la Mowe na eneo la Horohoro wilayani Mkinga.

MAKAMU WA RAIS AZITAKA HALMASHAURI ZOTE NCHINI KUHAKIKISHA ZINATOA ASILIMIA 10% YA MAPATO YAKE KWA WANAWAKE,VIJANA NA WAZEEibu wa sheria.

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi wa vikundi vya ujasiriamali ambayo vimekabidhiwa hundi ya shilingi milioni 40 kama sehemu ya 10%ya mapato ya Halmashauri ambapo vikundi 11 vimefaidika na mkopo huo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Sikonge ambaye pia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Joseph Kakunda(kulia) mara baada ya kuwasili Sikonge mkoani Tabora ikiwa sehemu ya ziara yake ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  akimwagilia mei wa kumbukumbu alioupanda mara baada ya kuweka  jiwe la msingi  la ujenzi wa Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora.
 Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe. Joseph Kakunda akihutubia wananchi katika uwanja wa TASAF Sikonge mkoani Tabora.
 Sehemu ya Wananchi wa Sikonge, mkoani Tabora waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara ambao Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alikuwa mgeni rasmi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya TASAF wilayani Sikonge mkoani Tabora
 
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amezitaka Halmashauri zote nchini kuhakikisha zinatoa asilimia 10% ya mapato yake kwa Wanawake, Vijana na Walemavu kwa mujibu wa sheria.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati akihutubia wananchi katika Viwanja vya TASAF wilaya ya Sikonge mkoani Tabora ikiwa ni siku ya tatu ya ziara yake ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo.

“Niagize Halmashauri zote kuhakikisha zinatoa fedha hizo kama ilivyopangwa bila riba yeyote kwani fedha hizi zipo kisheria na kwa kutozitoa ni kuvunja sheria”alisema Makamu wa Rais.

Aidha, amesisitiza Halmashauri kuweka utaratibu mzuri kuhakikisha fedha zinazokopeswa kwa vikundi zinarejeshwa kwa kuwa lengo la fedha hizo ni kuwanufaishwa walengwa zaidi huku akishauri kuwepo na makundi yenye mradi unaoleta tija kwa manufaa ya wengi.

Makamu wa Rais ametoa wito kwa wakulima wa tumbaku mkoani Tabora kutoharibu mazingira kwa kukata miti kwani hasara ya kukata mti ni kubwa kulikoni faida wanayoipata hivyo amewashauri kutumia teknolojia mpya ya Solar na Umeme kama ilivyoshauriwa na wataalamu.

Wakati huohuo Mbunge wa Jimbo la Sikonge ambaye pia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Joseph Kakunda amesema mpaka 2021 kwa mara ya kwanza vijiji vyote wilayani Sikonge vitapata umeme wa uhakika.

Mheshimiwa Kakunda ameleeza namna wananchi wa Jimbo lake walivyoridhishwa na kasi ya maendeleo ambapo Serikali imetoa pesa katika miradi ya afya, miradi ya elimu na kuboresha miundombinu ya barabara.

Pia alielezea Vipaumbele ambavyo wamejiwekea jimboni kwake katika kukuza fursa za kimaendeleo, vipaumbele hivyo ni kuanzisha viwanda vya usindikaji mazao ya kilimo, pili viwanda vya vifaa vya majumbani na ujenzi na tatu ni viwanda vitakavyoajiri watu wengi kwa wakati mmoja.

Kwa upande mwingine Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko amesema Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kurudisha uchumi wa madini kwa Watanzania.“Wananchi changamkieni kuwekeza kwenye uchumi wa madini, lipeni kodi kwa maendeleo ya Taifa letu”. alisema Waziri huyo.

Katika ziara hiyo Makamu wa Rais aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la Halmashauri ya wilaya hiyo,alikabidhi hundi ya shilingi milioni 40 kwa vikundi 11 vya ujasiriamali na kuzungumza na wananchi.

Makamu wa Rais ameongozana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba, Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko, Naibu Waziri Maji Mhe. Juma Aweso, Naibu Waziri Ujenzi Mhe. Elias Kwandikwa, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelline Mabula na Naibu Waziri TAMISEMI Mhe. Mwita Waitara.

HOSPITALI ZOTE NCHINI ZATAKIWA KUWA NA ICU YA WATOTO WACHANGA

0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiongea na mama Mjamzito wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akieleza Waandishi wa Habari (hawapo kwenye picha) umuhimu wa kifaa kinacho rekodi mahudhurio na muda wa watumishi kufika ofisini (Biometric) wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akimjulia hali mama aliyetoka kujifungua, wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akimtazama mtoto njiti, aliyepakatwa na mamaye, wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na Madaktari Bingwa wa Hospitali teule ya Mkoa wa Pwani Tumbi, baada ya kumaliza ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali hiyo.


……………………….


NA WAMJW – PWANI


WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ameziagiza Hospitali za rufaa zote nchini kuwa na ICU kwaajili ya watoto wachanga ili kupunguza vifo vifo vyao.

Waziri Ummy amesema hayo wakati wa ziara yake ya kukagua hali ya utoaji wa huduma za Afya katika Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi.

Waziri Ummy ameagiza hayo kupitia kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo kuwa ahakikishe watoto wachanga lazima wawe na ICU yao ili kuhakikisha vifo vya Watoto wachanga vinapungua nchini.

“Watoto wachanga wagonjwa, wawe na ICU yao, lengo letu kama Serikali ni kupunguza Vifo vya Watoto wachanga, kwasababu tukipunguza vifo vya Watoto wachanga, tutakuwa tumepunguza vifo vya Watoto wanye umri wa chini ya miaka mitano” alisema Waziri Ummy.

Waziri Ummy aliendelea kusema kuwa karibu 40% ya vifo vya watoto ni watoto wachanga na katika kila Watoto 100, Watoto 40% ni Wachanga, hivyo Serikali inaendelea kuchukua jitihada za makusudi ili kupunguza vifo hivi, ikiwemo kusisitiza kila Hospitali nchini kuwa na ICU.

“Karibu 40% ya vifo vya watoto ni watoto wachanga na katika kila Watoto 100, Watoto 40% ni Wachanga, kwahiyo Daktari ni lazima tulifanyie kazi agizo hilo” alisema Waziri Ummy.Licha ya changamoto alizokutana nazo Waziri Ummy amesema kuwa Serikali inatarajia kujenga jengo mahususi kwaajili ya huduma za Dharura katika Hospitali zote za Rufaa za Mikoa nchini ili kuokoa maisha ya wagonjwa, hasa waliopata ajali.

“Nafurahi kusema, Serikali imeahapata fedha kwahiyo tutakuwa na jengo mahususi kwaajili ya huduma za Dharura na wagonjwa wa ajali, na hii tunataka iwe katika Hospitali za Rufaa za Mikoa zote ili mgonjwa aweze kuokolewa maisha muda mfupi anapofika Hospitali” alisema Waziri Ummy.

Pia, Waziri Ummy ameridhishwa kwa kiasi kikubwa juu ya hali ya upatikanaji wa dawa nchini, huku akiwatoa hofu Mwananchi kuwa Serikali kupitia Bohari ya Dawa (MSD) ina dawa zakutosha.

Aliendelea kusema kuwa Serikali imeainisha fani nane nane za kipaumbele ili kuwa na madaktari Bingwa wawili katika kila fani ikiwemo, Daktari Bingwa wa Watoto, Daktari Bingwa wa magonjwa yakina mama na uzazi, Daktari Bingwa wa upasuaji wajumla, Bingwa wa upasuaji wa mifupa, Daktari Bingwa wa magonjwa ya ndani (Physician) n.k

Mbali na hayo Waziri Ummy amesema kuwa katika Mkoa wa Pwani Serikali imejenga na kuboresha vituo vya Afya zaidi ya 16, Hospitali za Wilaya 3, na kuboresha Hospitali ya Mikoa ili kuwa na huduma za wagonjwa mahututi na wagonjwa wa Dharura.

Mbali na hayo Waziri Ummy amewahasa Mwananchi kujiunga na mfuko wa Bima ya Afyà ili kujihakikishia matibabu wakati wa ugonjwa, jambo litalosaidia kuokoa gharama kubwa za matibabu pindi Mwananchi anapopata ugonjwa.

“Nitoe Wito kwa Wananchi kujenga utaratibu wakujiunga na Bima ya Afya, kwasababu ndio njia ya uhakika yakujihakikishia matibabu kabla hawajaugua” alisema Waziri Ummy.

WAZIRI MKUU ATOA SIKU 16 KWA MKURUGENZI ROMBO

0
0

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ametoa siku 16 kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo, Magreth John awe amepeleka asilimia 20 sawa na sh milioni 114 ya kijiji cha Holili kabla ya Machi 10 mwaka huu, fedha hizo zinatokana na mauzo ya madini ya pozolana.

Ametoa maagizo hayo leo (Jumamosi, Februari 23, 2019) wakati akizungumza na watumishi wa Kituo cha Pamoja cha Forodha cha Holili pamoja na wananchi wa kijiji cha Holili, akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Kilimanjaro. Kituo hicho kipo katika mpaka wa Tanzania na Kenya.

Waziri Mkuu alitoa maagizo hayo baada ya wananchi wa kijiji cha Holili kuwasilisha malalamiko yao kupitia mabango wakimuomba awasaidie ili Halmashauri hiyo iweze kulipa fedha zao zinazotokana na mapato ya mauzo ya madini hayo yanayochimbwa kijijini kwao.

“Mkuu wa wilaya (Agness Hokororo) simamia kuhakikisha kiasi hicho cha fedha kinakwenda kwa wananchi na Mkuu wa Mkoa (Dkt. Anna Mgwira) nataka nipate taarifa kuwa fedha hizo zimeshalipwa kwa uongozi wa kijiji husika.”

Kadhalika, Waziri Mkuu amewataka watendaji katika maeneo mbalimbali nchini kuwa wamepelekwa huko kwa ajili ya kuwahudumia wananchi, hivyo hawana budi kutenga muda wa siku tatu kwa wiki na kwenda maeneo ya vijijini kusikiliza kero zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amesema hali ulinzi na usalama katika mpaka huo si nzuri, Serikali imeamua kuimarisha ulinzi kwenye mpaka huo, hivyo ni muhimu kwa wananchi washirikiane katika kuulinda mpaka huo.

Hivyo, Waziri Mkuu ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuwakamata na kuwachukulia hatua watu wote watakaokamatwa wakipita au kuingiza mizigo kupitia njia zisizo rasmi kwa sababu hao ndio wanaopitisha silaha.

Waziri Mkuu amesema wananchi wa Tanzania na Kenya hawajazuiwa kufanya biashara upande wowote bali wanatakiwa wafuate sheria, kanuni na taratibu zilizopo katika nchi husika ikiwa ni pamoja na kutumia njia rasmi.

Amewataka viongozi na watendaji waliopo maeneo ya mipaka huo wa Holili wawe makini kwa sababu mpaka huo hauko salama na kuna mambo mengi yanayoendelea ambayo yapo kinyume cha sheria.

DKT. MWANJELWA AMPA ONYO KALI AFISA UTUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBAHA KWA KUMTOLEA LUGHA CHAFU MSTAAFU

0
0



Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Mji Kibaha na Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi hao chenye lengo la  kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi hao, kabla kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri hizo mkoani Pwani.
IMG_2001
Baadhi ya watumishi wa umma wa Halmashauri ya Mji Kibaha na Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha  wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani), wakati wa kikao kazi cha watumishi hao na Naibu Waziri huyo chenye  lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi hao, kabla ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri hizo mkoani Pwani.
IMG_2003
Katibu Tawala Mkoa wa Pwani, Bi. Theresia Mbando akitoa neno la utangulizi kumkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) kuzungumza na watumishi wa Halmashauri ya Mji Kibaha na Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi hao  chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi hao, kabla kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri hizo mkoani Pwani.
IMG_2004
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akitoa onyo kwa Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, Bi. Ruth Mwelo ambaye ni Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu  wa Halmashauri hiyo kwa kumtolea lugha chafu mstaafu aliyekuwa akidai haki yake, onyo hilo amelitoa wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi hao.

……………………
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) amempa onyo kali Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, Bi. Ruth Mwelo ambaye ni Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu  wa Halmashauri hiyo kwa kumtolea lugha chafu mstaafu aliyekuwa akidai haki yake na kumtaka afisa huyo ajirekebishe haraka iwezekanavyo.

Onyo hilo amelitoa wilayani Kibaha, wakati wa kikao kazi na watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha na Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji, kabla ya kutembelea wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika wilaya hizo ili kujiridhisha na utekelezaji wake.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema, haiwezekani afisa huyo mwenye dhamana ya kusimamia Sheria, Kanuni na Taratibu za kiutumishi ndio awe kikwazo cha utendaji kazi katika Halmashauri hiyo kwa kutoa lugha chafu dhidi ya wanaofuta huduma ofisini kwake, na kuongeza kuwa, afisa huyo ndiye anayestahili kuwa kwenye Kamati ya Maadili ili kutoa miongozo ya uadilifu na kusimamia maadili ya watumishi kwa ujumla katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amemtaka afisa huyo kutotumia cheo chake vibaya na badala yake asimamie vema nidhamu na masilahi ya watumishi wa umma.
Sanjari na hilo, Mhe. Dkt. Mwanjelwa amemtaka afisa huyo kuacha tabia ya kutoa siri za ofisi na kutokuwa mchonganishi miongoni mwa watumishi wenzie kwani matendo hayo hayapaswi kufanywa na mtumishi yeyote nchini.

Aidha, Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema ameamua kuweka bayana  mapungufu ya afisa huyo mbele ya watumishi wenzie ili ajifunze kutokana na matendo yake yasiyoridhisha na aweze kubadili mwenendo wake mbaya wa kimaadili.
Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) ameendelea kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma nchini, kwa kutoa onyo kwa watumishi wote wanaobainika  kukiuka Kanuni za Maadili ya Utendaji Kazi katika Utumishi wa Umma.

MSAMA PROMOTIONS YATOA MSAADA WA VYAKULA VITUO SITA VYA YATIMA NA WASIOJIWEZA

0
0
Kuelekea Tamasha la Kihistoria la Pasaka kwa mwaka 2019, Kampuni ya Msama Promotions imetoa msaada katika vituo Sita vya Watoto wasiojiweza  ili kujikimu kimaisha.

Msama Promotions imetoa msaada huo kwenye vituo vya Sifa (Bunju), Zaidia (Sinza), Maunga (Mkwajuni), Honoratha (Temeke), Watoto Wetu Tanzania na Mwandaliwa (Boko).

Akizungumza na Waandishi wa Habari baaada ya kutoa msaada huo, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Alex Msama amesema Tamasha hilo linafanya kazi yake pamoja na kuisaidia jamii isiyojiweza.

"Kama kawaida yetu Kampuni ya Msama Promotions kujali Watoto Yatima, kuwasaidia kwa kiwasomesha kuwapa mambo mbalimbali ikiwemo Chakula na Malazi", amesema Msama.

Pia, Msama ametoa wito kwa Kampuni nyingine kuwasaidia Watoto hao wasiojiweza ili kujikimu kimaisha kama ilivyo kwa Watoto wengine waliokuwa na wazazi wao.

Tamasha hilo la Kihistoria linatarajiwa kufanyika April 21, 2019 katika jiji la Dar es Salaam ambapo linatarajiwa kuzunguka mikoa 10, likiwa na lengo la kuombea Taifa pamoja na Viongozi wake akiwemo Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Mkurugenzi wa Kampuni  ya Msama Promotions , Alex Msama akijiandaa kugawa msaada wa vyakula katika vituo sita ambavyo ni Sifa (Bunju), Zaidia (Sinza), Maunga (Mkwajuni), Honoratha (Temeke), Watoto Wetu Tanzania pamoja na Mwandaliwa (Boko).
Mkurugenzi wa Kampuni  ya Msama Promotions , Alex Msama akikabidhi msaada wa vyakula kwa baadhi ya vituo vya watoto wasiojiweza,Msama ametoa msaada huo kwa vituo sita ambavyo ni Sifa (Bunju), Zaidia (Sinza), Maunga (Mkwajuni), Honoratha (Temeke), Watoto Wetu Tanzania pamoja na Mwandaliwa (Boko).
Mkurugenzi wa Kampuni  ya Msama Promotions , Alex Msama akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari mara baada ya kutoa msaada kwa vituo sita vya jijini Dar,ikiwa ni sehemu ya fedha zilizokuwa zikipatikana katika tamasha la pasaka,ambalo hufanyika kila mwaka,likianzia jijini Dar na kuendelea katika mikoa zaidi ya 10
Mkurugenzi wa Kampuni  ya Msama Promotions , Alex Msama akifurahia jambo na mmoja wa watoto mara baada ya  kutoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo vyakula  kwa vituo sita vya jijini Dar,ikiwa ni sehemu ya fedha zilizokuwa zikipatikana katika tamasha la pasaka,ambalo hufanyika kila mwaka,likianzia jijini Dar na kuendelea katika mikoa zaidi ya 10
Mara baada ya kutoa msaada wa vyakula na vitu mbalimbali,Mkurugenzi wa Kampuni  ya Msama Promotions , Alex Msama pia alipata wasaa wa kula chakula cha pamoja na baadhi ya watoto hao waishio katika mazingira magumu.

RAIS DK. SHEIN AWATAKA WAZAZI, WALEZI KUWEKA MAZINGIRA BORA KWA WATOTO KUPATA ELIMU

0
0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiangalia moja ya meza mpya zilizoagiziwa kwa ajili ya matumizi ya Skuli za Sekondari na Msingi Zanzibar, baada ya kufungua madarasa manne ya Skuli ya Sekondari ya Mchanga Mdogo Wilaya ya Wete Pemba akiwa katika ziara yake kutembelea Miradi ya Maendeleo.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiangalia moja ya meza mpya zilizoagiziwa kwa ajili ya matumizi ya Skuli za Sekondari na Msingi Zanzibar, baada ya kufungua madarasa manne ya Skuli ya Sekondari ya Mchanga Mdogo Wilaya ya Wete Pemba akiwa katika ziara yake kutembelea Miradi ya Maendeleo.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akikata utepe kuashiria kufungua jengo jipya la Skuli ya Sekondari ya Mchanga Mdogo Wilaya ya Wete Pemba leo.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akiwasili katika viwanja vya Skuli ya Mchanga Mdogo akiwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Riziki Pembe Juma kushoto, wakielekea katika jengo ljipya la Madarasa ya Skuli ya Sekondari ya Mchanga Mdogo kwa ajili ya uwekaji jiwe la msingi, akiwa katika ziara yake Kisiwani Pemba.(Picha na Ikulu)
WANAFUNZI wa Skuli ya Sekondari na Msingi ya Mchanga Mdogo Wilaya ya Wete Pemba, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwahutubia wakati wa hafla ya ufunguzi wa Madarasa ya Skuli ya Sekondari Mchanga Mdogo Pemba.
WANANCHI wa Kijiji cha Mchanga Mdogo Wilaya ya Wete Pemba wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia baada ya hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi Skuli ya Sekondari ya Mchanga Mdogo Pemba.

WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Riziki Pembe Juma akihutubia kabla ya kumkaribisha mgeni rasmin kuwahutubia Wananchi wa Kijiji cha Mchanga Mdogo Wilaya ya Wete Pemba, wakati wa hafla ya ufunguzi wa Jengo la Skuli ya Sekondari Mchanga Mdogo
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Madarasa Mapya ya Skuli ya Sekondari Mchanga Mdogo Wilaya ya Wete Pemba, akiwa katika ziara yake kutembelea Miradi ya Maendeleo Kisiwani Pemba.
WANAFUNZI wa Skuli ya Msingi Mchanga Mdogo Wilaya ya Wete Pemba wakiimba Wimbo wa Sisi Sote Tumengomboka wakati wa hafla ya ufunguzi wa majengo ya Skuli ya Sekondari Mchanga Mdogo Kisiwani Pemba leo.
 
……………………………………………………………………………………..
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amewataka wazazi na walezi kote nchini kuwasaidia na kuwatengenezea mazingira bora watoto wao ili waweze kusoma bila taabu.

Kwa nyakati tofauti, Dk. Shein amesema hayo leo wakati alipofungua jengo la madarasa manne katika skuli ya sekondari Mchangamdogo pamoja na kuweka jiwe la msingi la jengo la madarasa manne katika skuli ya msingi Bopwe, Wilaya ya Wete Pemba.

Huo ni muendelezo wa ziara zake za kukaguwa miradi mbali mbali ya maendeleo pamoja na utekelezaji wa Ilani ya CCM. Dk. Shein aliwataka wazazi an walezi kuepuka kuwatuma watoto kupita kiasi katika masuala yasio na mnasaba wa elimu, kwa msingi kuwa hayaendani na umri walionao, hususan katika suala zima la kujiendeleza kitaaluma.

Alisema wapo baadhi ya wazazi na walezi wanaowatumikisha vibaya watoto wao katika kazi za kujikimu kimaisha ikiwemo biashara, hivyo kuwatwisha mzigo usioendana na wakati wao. Aidha, aliwataka walimu kufanikisha dhana ya ulezi wa wanafunzi kwa kuwabidisha kitaaluma, sambamba na kuwataka kuondokana na vitendo vyote vya uharibifu dhidi ya wanafunzi, ikiwemo udhalilishaji wa kijinsia.

“Mwalimu na mwanafunzi ni mtu na mzee wake mnapaswa kujenga urafiki na sio uadui’, alisema. Vile vile Dk. Shein aliwataka walimu kufanyakazi zao kwa misingi ya taaluma ya ualimu pamoja na kuzingatia maadili ya kazi hiyo, akiweka wazi azma ya Serikali ya kuwachukulia hatua walimu wote watakaobainika kukiuka miongozo na sheria za kazi.

Katika hatua nyengine, Dk. Shein aliwataka wanafunzi kusoma kwa bidii na jitihada zote, akibainisha kutokuwepo kwa sababu zozote zile zitakazomfanya mwanafunzi kushindwa kusoma vizuri kutokana na mazingira bora yaliowekwa na Serikali.

Alisema Serikali itaendelea kuimarisha sekta ya elimu, kwa kukamilisha madarasa saba yanayohitajika katika skuli ya Sekondari Mchangamdogo ili kukidhia mahitaji ya wnaafunzi, sambamba na mahitaji ya skuli zote nchini, kw akuyapatia vifaa vya kufundishia pamoja na samani.

Dk. Shein alirudia kauli yake kwa kusema lengo la Serikali ni kuwajengea mazingira bora wanafunzi ili kuhakikisha inapata wataalamu katika fani zote, akibainisha kuwa wataalamu ndio chachu ya maendeleo ya taifa lolote Duniani.

Alisema Serikali ya awamu ya saba itaendelea kusimamia upatikanaji bora wa elimu bila malipo katika skuli za maandalizi, msingi na sekondari na kubainisha jukumu la Serikali la kuwaondolea dhima wazazi katika uchangiaji wa vifaa.

Dk. Shein aliwahakikishia wazazi na wanafunzi kuwa serikali itaendelea kutekeleza ahadi ya upatikanaji wa elimu na taaluma yenyewe kwa kuimarisha miundombinu na upatikanaji wa samani zote ili kuwawekea mazingira bora ya kielimu wanafunzi. Aidha, alisema pamoja na serikali kukosa uwezo wa kutosha wa kutoa elimu bure katika masomo ya Vyuo Vikuu, itaendleea kutoa mikopo kwa wanafunzi wote wa elimu ya juu.

Nae, Waziri wa Nchi, (OR), Serikali za Mitaa, Tawala za Mikoa na Idara maalum za SMZ, Haji Omar Kheir, alisema Wizara yake itatimiza jukumu la kusimamia sekta ya elimu katika ngazi ya maandalizi na msingi, akibainisha madarasa manne ya Skuli ya msingi Bopwe (yaliowekewa jiwe la msingi) kuwa ni miongoni mwa madarasa 60 yalioendelezwa na Wizara hiyo kupitia mfumo wa Ugatuzi.

Aidha, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Riziki Pembe Juma aliipongeza Serikali katika kusimamia vyema sekta ya elimu pamoja na kuwajengea mazingira mazuri wanafunzi ya kupata elimu.

Mapema, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Madina Majaka , alisema ujenzi wa jengo la madarasa manne katika skuli ya Sekondari Mchangamdogo umegharimu zaidi ya shilingi Milioni 34.4, ambapo utapunguza mlundikano wa wanafunzi madarasani, akibainisha haja ya kupatikana madarasa mengine saba ili kuondokana kabisa na kadhia hiyo.

Aidha, Katibu Mkuu, Wizara nchi (OR), Serikali za mitaa, Tawala za Mikoa na Idara maalum za SMZ, Radhia Rashid alisema ujenzi wa jengo la madarasa manne katika skuli ya msingi Bopwe utagharimu shilingi Milioni 53.6 hadi utakapokamilika, fedha zinatokana na Bajeti ya serikali pamoja na michango ya wananchi.

WAKATI HUO HUO, RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein alisema Serikali imefanya kazi kubwa na ngumu katika kuliimarisha zao la karafuu na hatimae kuleta tija kwa wananchi, hususan wa kisiwa cha Pemba. Alisema bado zao hilo lina umuhimu mkubwa katika uchumi wa Zanzibar , na kusisitiza azma ya serikali katika kuliendleeza kibiashara.

Dk. Shein alisema hayo katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete, alipozungumza na Viongozi na wanachama wa CCM, pamoja na kupokea taarifa ya Utekelezaji wa kazi za Maendeleeo Wilaya Wete kwa kipindi cha Agosti 2017 hadi Disemba, 2018. Alisema amefurahishwa sana na hali ya amani na utulivu iliyopo katika Wilaya hiyo na Mkoa wa Kaskazini Pemba kwa ujumla, hatua iliyotoa fursa kwa wananchi kufanya shughuli zao za maendeleo bila vikwazo.

Aidha, alilipongeza Baraza la Mji wa Wete kwa kukusanya vyema mapato hadi kufikia asilimia 96.6 ya malengo lililopangiwa. Sambamba na hilo Dk. Shein alisema ameridhishwa na hatua za Wilaya hiyo kusajili wanafunzi katika skuli za msingi na maandalizi, kwa kigezo kuwa huo ndio msingi bora wa elimu kuelekea ngazi za elimu ya sekondari.

Alisema changamoto za maji katika maeneo ya Uvinje na Kiuyu Mjini yatapatiwa ufumbuzi, na kuonya tabia ya ubinafsi iliopo kwa baadhi ya watendaji wa Mamlaka ya Maji (ZAWA), Wilayani humo inayodhoofisha upatikanaji wa huduma hiyo. Aidha, Dk. Shein akaukumbusha uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, kukamilisha ujenzi wa Chuo cha Amali Mtamwe ambapo ujenzi wake ulianza takriban miaka minane iliyopita, ukiwa umesita.

Mapema, Waziri wa Nchi (OR), Serikali za mitaa, Tawala za Mikoa na Idara maalum za SMZ, Haji Omar Kheir aliwataka wananchi wanaojishughulisha na biashara za magendo, ikiwemo ya zao la karafuu kuacha mara moja, akibainisha kuwa Serikali itachukuwa hatua za kisheria pamoja na kutaisha mali za wahusika.

Nae, Mkuu wa Wilaya ya Wete, Abeid Juma Ali, alisema miongoni mwa changamoto zilizoikabili Wilaya hiyo atika kipindi hicho ni pamoja na upungufu wa wafanyakazi katika sekta ya Afya, upungufu wa madarasa na walimu katika skuli za msingi na sekondari.

Abdi Shamna, Ikulu Zanzibar

TANZANIA INAUMWA KWA AJILI YAKO RUGE

0
0
Ruge Mutahaba.

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

MAISHA yangu ya uandishi wa habari kwa miaka 19 sasa, hakuna siku hata moja nimewahi kuandika makala, maelezo, maoni au ushauri kuhusu Mtanzania ambaye anasumbuliwa na maradhi.

Nimekuwa na utamaduni wa kutoa pole au kushiriki kwenye maombi ya kuhakikisha mwenzetu anayeumwa, Mwenyezi Mungu ampe unafuu na apone haraka. Nimekuwa nikifanya hivyo kadiri ninapopata taarifa. Ila sijawaji kuandika maelezo mareeefu kumzungumzia mgonjwa!

Kwa mara ya kwanza leo naomba nivunje mwiko huo. Iwapo nitakuwa nakosea naomba nisamehewe. Nimeshindwa kuvumilia, nimeshindwa kukaa kimya. Nimeshindwa kuzungumza na moyo wangu na kisha kubaki nayo kichwani. Hapana nimeshindwa. Naomba ruhusa niandike kuhusu Ruge Mutahaba.

Ndio! Nataka kumzunguzia Ruge Mutahaba. Huyu huyu Bosi Ruge, ni huyu huyu Ruge ambaye wengi wamefanikiwa kupitia kwenye mikono yake. Ruge ambaye ukisikia atazungumza na Watanzania kupitia vyombo vya habari vya Clouds Media Group wote tunasubiri. Tunaka kufahamu anazungumza kuhusu nini. Ruge ambaye tunamuita Scofield wa Tanzania.

Mungu Muumba wa mbingu na ardhi, nipe ujasiri wa kuandika maelezo ambayo yatanyooka na kueleweka kwa haraka. Unapotaka kumzungumzia Ruge Mutahaba lazima kichwa kitulie, lazima uwe na hakika ya kile ambacho unataka kukisema.

Najua na Watanzania wanajua kwa sasa Bosi Ruge yupo kitandani. Ruge anaumwa. Pole kaka. Natoa pole kwako bosi Ruge. Nina hakika Mungu atakunyanyua na kusimama tena. Mungu atakuponya, Watanzania kila mmoja kwa imani yake wanakuombea Ruge upone haraka. Pole kaka, pole rafiki, pole swahiba wa Watanzania.

Taarifa za kuumwa kwako nimezipata kupitia taarifa mbalimbali ambazo zimekuwa zikitolewa kuhusu wewe. Sebastian Maganga alitoa taarifa rasmi kuhusu kuumwa kwako.

Na juzi hapa nimemsikia mdogo wako Mbaki Mutahaba, aliyetoa maelezo kuhusu hali yako. Nimemsikia akitoa taarifa ya gharama ya fedha ambayo inatumika kila siku kwa ajili ya matibababu yako.

Ruge narudia tena, sina shaka hata kidogo, afya yako itaimarika na kurejea kwenye majukumu yako ya kila siku. Nikiri sijawahi kukutana na wewe 'Live' tukazungumza au kujadili chochote. Huo ndio ukweli. Hata hivyo kukua kwa teknolojia ya habari na mawasiliano, nimekuwa nikikutana na wewe kupitia vyombo vya habari mbalimbali na hasa vile ambavyo unavisimamia vya Clouds Media Group.

Kaka kupitia wewe umenibadilisha kwenye mambo mengi. Umenifundisha maisha ni nini? Ili uishi unatakiwa kufanya nini? Unatakiwa kufanya mambo ya aina gani kufikia mafanikio. Ruge Mutahaba pole kaka. Katika maisha kuna watu ambao najua umekutana nao na kuzungumza nao.

Najua ni wengi lakini idadi yao haizidi wale ambao umewafikia kupitia vyombo vya habari. Sitaki kuzungumzia wasanii wa fani mbalimbali. Sisemi uliokutana nao kwenye jukwaa la fursa ambalo huambatana na tamasha la Fiesta.

Ruge wewe ni mwalimu wa kila kitu. Mwenyezi Mungu aliamua kuweka vitu ndani yako kwa ajili ya wengine. Leo unaumwa, mioyo yetu inaumizwa na kuumwa kwako. Pona kaka. Tunaumia kwa sababu kukosekana kwako katika kipindi hiki yapo baadhi ya mambo hayaendi sawa. Kuna kitu tunaona kinakosekana. Tunamuomba Mungu akupe afya njema na urejee nyumbani.Tunakuhitaji sana.

Amka Ruge wetu, amka Bosi Ruge, amka Scofield wa Tanzania. Najua umekaa kwa muda mrefu kitandani lakini huu ni wakati sahihi kwako kumka tena.Tunakusubiri kaka, tunakusubiri kaka mkubwa. Njoo tuendelee na maisha ya kuijenga Tanzania yetu.

Uwezo wako, maarifa yako, akili yako na ubunifu wako umechangia kwa kiasi kikubwa nchi yetu kupiga hatua kimaendeleo. Unaweza usione moja kwa moja lakini namna ambavyo umetengeneza fursa na Watanzania wakazitumia vema wengi wao wamebadilika. Wamepiga hatua kubwa za kimaendeleo.

Muangalie Nasibu Abdul a.k.a Diamond. Amepita kwenye mikono yako. Wapo wengi ambao wamenufaika kimaisha kupitia akili yako. Njoo kaka tunakusubiri nyumbani Tanzania. Kama binadamu najua huwezi kufanya kila kitu kikafurahisha watu wote lakini ukweli utabaki kuwa wengi wamenufaika kupitia wewe.

Naandika huku nikikumbuka ile kauli mbiu 'Fungulia Dunia kuwa unachotoka'. Kaka Ruge binafsi nimekuwa ninachotaka. Nikwambie kaka Ruge kuumwa kwako, tunaumwa wengi. Huo ndio ukweli.

Mungu amekupa akili ya kujua ufanye nini na kwenye jambo gani. Umekuwa msaada mkubwa kwa Watanzania wengi. Hakuna kampeni ambayo ulianzisha ikakwama. Nimekumbuka wimbo wa Tuulinde na Amani ambao uliishirikisha wasanii mbalimbali.

Kaka Ruge tumekuzoea kukuona unaumiza kichwa kuhakikisha mambo yanakwenda. Rudi brother tuijenge nchi yetu. Sioni mahali ambapo Ruge ulitaka kufika ukakwama. Kila mahali ambako ulitamani kufika ulifanya hivyo.

Ruge ni wewe ambaye ukiamua jambo liwe linakuwa. Kikubwa zaidi ambacho najifunza kutoka kwako ni uwezo wako mkubwa wa kuchuja kipi uzungumze sasa na kipi uzungumze baadaye.

Tanzania imesimama, inakusuburi uamke kitandani. Inakusubiri urudi. Rudi kaka Ruge, Rudi Bosi Ruge. Njoo tuungane kwenye harakati za maisha yetu ya kila siku.

Kukuzungumzia wewe unaweza kutumia siku, wiki, mwezi na hata mwaka bila kumaliza. Umefanya mengi na natamani kuona ukiendelea kufanya mengi zaidi. Moyo wangu unaumia, machozi yanatoka. Ugonjwa wako unatuliza wengi. Amka ndugu yetu, amka Mzee wa vipaji lukuki.

Nikiri nimefarijika kuona kuna kampeni maalumu ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia matibabu yako. Tumeambiwa kwa siku gharama ni kati ya Sh5 mpaka 6 milioni kila siku.

Ruge Mutahaba (kulia) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mh.Paul Makonda
 
Ni wakati wetu Watanzania kuungana kuchangia matibabu yako. Ni matumaini yangu Watanzania tutaendelea kukuombea na kukuchangia kadiri ya uwezo wetu. Familia kwa nafasi yake imeendelea kutimiza majukumu ya kuhakikisha mwanafamilia wao anapata matibabu.

Rais Dk. John Magufuli alikuwa wa kwanza kutoa fedha kwa ajili ya matibabu ya Ruge.

Kaka Ruge siku zote umekuwa mstari wa mbele kuchangia wengine, hivyo nasi tunayo nafasi ya kukuchangia. Nia yetu ni kuona afya yako inakuwa imara. Ulitumia nafasi yako kuwashika mkono Watanzania waliopoteza matumaini, ni wakati wetu nasi kukushika mkono. 

Uliwapa faraja waliokosa faraja, ni wakati wetu kukupa faraja.Tanzania All Stars uliwatumia mara kwa mara pale ulipoona iko haja ya kusaidia jamii iliyo kwenye mataabiko. Ni matumaini yangu Tanzania All Stars nao watakushika mkono.

Kaka Ruge wewe ni bonge la binadamu. Mungu amekupa utu na ubinadamu. Vyote unavyo. Nitakuombea kwa Mungu akuponye maradhi yanayokusibu. Nitakuombea kila sekunde, kila dakika na kila saa.

Nihitimishe kaka Ruge pole kwa kuumwa. Watanzania tunakuombea. Ukiupata ujumbe huu naomba utambue bado tunakupenda na tuko pamoja nawe.

Hata hivyo nikiri tu naumia sana ninaposikia baadhi ya watu wakiwamo wasanii ambao umewajenga kupitia vyombo vyako vya habari, wakitoa lugha za kejeli, dharau na kiburi dhidi yako. Inaumiza sana. Nawasikiliza wee kisha nasema Mungu wahurumie. Bosi Ruge pole. Pole kaka.

Simu: 0713833822.

Bluefins yataja ‘jeshi’ la waogeleaji 29 kwa ajili ya mashindano ya Mwanza

0
0
Dar es Salaam. Klabu inayokuja juu kwa kasi katika mchezo wa kuogelea nchini, Bluefins imetangaza kikosi cha waogeleaji 29 kwa ajili ya kushindana katika mashindano ya Isamilo yaliyopangwa kuanza ijuu mkoani Mwanza.
Muasisi na Kocha Mkuu wa timu hiyo, Rahim Alidina aliwataja waogeleaji  wa kile kuwa ni Alexis Misabo, Filbertha Demello, Maryam Ipilinga, Viva Pujari, Sarah Shariff, Aminaz Kachra, Fatema Manji, Muskan Gaikwad, Aliyana Kachra, Zainab Moosajee na Lina Goyayi.
Waogeleaji wa kiume ni Moiz Kaderbhai, Idris Zavery, Sahal Harunani, Isaac Mukani, Enrico Barretto, Zac Okumu, Hassan Harunani, Mohamedhussein Imran, Husain Hassanali, Burhanuddin Mustansir na Ayaan Shariff.
Wengine ni Kaysan Kachra, Parth Motichand, Shuneal Bharwani, Sahil Chudasama, Salman Yasser, Christian Fernandes na Revocatus Josephat.
 Alidina alisema kuwa wamewajumuisha waogeleaji wenye umri wa miaka  saba (7) kwa lengo la kuwapa uzoefu wa mashindano kabla ya kushindana katika mashindano ya Taifa yaliyopangwa kufanyika  mwezi Aprili.
Alisema kuwa waogeleaji hao wapo katika maandalizi ya mwisho na wanatarajia kuondoka jijini kabla ya Ijumaa ya wiki hii kwenda kuonyesha uwezo wao.
“Haya ni mashindano ya tatu kwa mwaka huu, tulianza na Morogoro na baadaye Taliss-IST. Yote hayo tumefanya vizuri,” alisema.
Alisema kuwa wanatarajia kufanya vyema katika mashindano hayo pamoja na waogeleaji wao kuweka muda mpya wa kuogelea (PBS).
"Timu yetu imekuwa ikifanya vizuri katika mashindano hayo ambayo yanaandaliwa na klabu ya kuogelea ya Mwanza (MSC). Tulishinda mwaka 2016 na mwaka 2017 na 2018 tulimaliza katika nafasi ya pili. Mikakati yetu ni kuweka historia mwaka huu,” alisema.

KATIBU WA ACT WAZALENDO NA WENZAKE 162 WAJIUNGA NA CCM WILYANI MUFINDI ,WASEMA JPM ANATOSHA

0
0

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi ccm Mkoa wa Iringa,Dkt.Abel Nyamahanga akipokea bendera ya chama cha ACT wazalendo kutoka kwa Ambi Daudi ambae ni Katibu wa ACT wazalendo wilaya ya Mufindi aliyejiunga na ccm leo hii katika maadhimisho ya miaka 42 ya kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi ccm.

……………………………………………………………

Maadhimisho hayo yamefanyika kwa wilayani Mufindi kwa kushiriki katika shughuli za kijamii huku Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa akishirikiana na Kaimu katibu wa CCM Mkoa Marco Mbaga,Mkuu wa wilaya ya Mfindi Jamhuri David pamoja,Wabunge pamoja na viongozi wa ccm wilaya ya Mufindi,wanachama na wananchi,wameshiriki madhimisho hayo kwa kuchimba msingi wa ujenzi wa vyoo mbora katika shule ya sekondari Upendo,kujenga daraja,kukabidhi mifuko 49 ya saruji kwa kikundi cha vijana wajasilimali wanaojishughuliisha na utengenezaji wa tofali katika eneo la soko la Mafinga Mjini na shule ya sekondari upendo kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa vyoo pamoja pia wamezungumza na walimu wa wilaya ya Mufindi.

Katika maadhimisho hayo jumla ya wanachama wapya 162 wamejiunga na chama cha mapiduzi ccm,na kusema kuwa wamekunwa na utendaji mzuri wa Rais Magufuli.PICHA NA ESTA MALIBICHE
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Dkt. Abel Nyamahanga akivalishwa skafu mara baada ya kuwasili katika ofisi za CCM wilaya ya Mufindi leo asubuhi.

Badhi ya wanachama wapya waliojiunga na chama cha mapinduzi CCM leo katika maadhimisho ya miaka 42 ya kuzaliwa CCMm,yaliyoadhimishwa wilayani humo.


Kiongozi wa soko la Mafinga akipokea mifuko ya saruji kwa ajili ya kikundi cha vijana wajasiliamali wanaojishughulisha na utengenezaji wa tofali.

Mwenyekiti wa ccm Mkoa wa Iringa Dkt.Abel Nyamahanga pamoja na Mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri Wilium wakichimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa vyoo bora katika shule ya sekondari Upendo iliyopo Mafinga Mjini.

Mbunge wa Mufindi Kusini Mendrad Kigola akichimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa vyoo bora katika shule ya sekondari Upendo iliyopo Mafinga Mjini.





Ujenzi wa daraja katika kata ya Upendo Mfinga mjini zikiendelea









DOKTA MPANGO AZIONYA TAASISI ZA SERIKALI ZISIZOTUMIA MFUMO WA KIELETRONIKI KUKUSANYA MAPATO

0
0

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akitoa ufafanunuzi wa kero zilizowasilishwa na Wafanyabiashara wa Sekta mbalimbali wakati wa kikao na Wafanyabiashara hao, kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC mkoani Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo akiwakaribisha Waheshimiwa Mawaziri, Wakuu wa Taasisi za Serikali na Wafanyabiashara wa Sekta mbalimbali (hawapo pichani), waliohudhuria kikao kilicholenga kutatua kero mbalimbali zinazokwamisha biashara mkoani humo kilichofanyika Jijini Arusha.


Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akisalimiana na Wenyeviti wa Taasisi Binafsi waliohudhuria mkutano uliowakutanisha Mawaziri mbalimbali, Wakuu wa Taasisi za Serikali na Wafanyabiashara uliolenga kukuza biashara mkoani humo, kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC mkoani Arusha.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akiorodhesha baadhi ya hoja zilizowasilishwa na Wafanyabiashara wa Sekta mbalimbali wakati wa kikao na Wafanyabiashara hao, kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC mkoani Arusha, Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Uwekezaji Mhe. Angela Kairuki.
Viongozi mbalimbali wakijadili jambo kabla ya kuanza kwa kikao kilichowajumuisha viongozi hao, Wakuu wa Taasisi za Serikali, Wafanyabiashara wa Sekta mbalimbali kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC mkoani Arusha.

…………………………………………………………………………..

Na Josephine Majura na Ramadhani Kissimba, WFM, Arusha

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.Dkt. Philip Isdor Mpango amezitaka Taasisi zote za Serikali kutumia kikamilifu mfumo wa malipo wa Serikali wa kielektroniki (GePG), ili kutimiza azma ya Serikali ya kudhibiti mianya ya upotevu wa fedha za Umma.

Dkt. Mpango ameyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa kikao cha wafanyabiashara wa sekta ya madini, utalii, mahotel na viwanda wa Mkoa wa Arusha kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC).

Akijibu hoja na kutolea ufafanunuzi wa kero mbalimbali zilizowasilishwa na Wafanyabiashara hao, Dkt. Mpango alisema Serikali ilishatoa maagizo kwa Taasisi zote za Serikali kuwa malipo yote yafanyike kwa kutumia mfumo wa malipo ya Serikali, na endapo itatokea Taasisi yoyote itashindwa kufanya hivyo itachukuliwa hatua za kisheria.

“Serikali iliziagiza Taasisi zote kuanza kutumia mfumo wa malipo ya Serikali ifikapo mwezi Juni, 2019, na nina agiza kuanzia leo mwananchi yeyote asikubali kulipa malipo yoyote yasiyotumia mfumo huu” alisisitiza Dkt. Mpango.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Uwekezaji Mhe. Angela Kairuki alisema Serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na Sekta Binafsi katika kukuza uchumi wa nchi, hivyo Serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali kuhakikisha kwamba inaboresha mazingira ya ufanyaji biashara hapa nchini.

Mkutano huo uliandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo, kwa lengo la kutatua kero mbalimbali za Wafanyabiashara wa Mkoa huo, na kuhudhuriwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Joseph Kakunda, Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mhe. Kangi Lugola, Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu ya Rais Mazingira Mhe. Januari Makamba, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Eng. Isack Kamwele, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu, na Naibu Waziri wa Vijana, Kazi na Ajira, Mhe.Anthony Mavunde.

ATCL ILIPOZINDUA SAFARI ZAKE ZA ZAMBIA NA ZIMBABWE

0
0
Wageni wakisubiriwa kushuka katika ndege hiyo ya ATCL 
Waziri wa uchukuzi na mawasiliano wa Serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhandisi Isack Kamwele akisalimiana na Waziri wa mazingira na utalii wa Zimbabwe Prisca Mupfumira, mara baada ya ndege aina ya air bus A220-300 kutua kwa mara ya kwanza katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Robert Gabriel Mugabe kuashiria uzinduzi rasmi wa kuanza safari katika nchi za Zambia na Zimbabwe.
Kaimu waziri wa uchukuzi wa Zambia Mutolwe Kafwaya akikata keki maalum juzi katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Kenneth Kaunda Lusaka Zambia wakati wa uzinduzi rasmi wa safari za ndege za Air Tanzania katika nchi hiyo kuanzia Feb.22,kulia ni waziri wa Uchukuzi na mawasiliano wa Tanzania mhandisi Izack Kamwelwe,na kushoto ni balozi wa Zambia nchini Tanzania Benson Chali. 
Waziri wa Mazingira na utalii wa Zimbabwe Prisca Mupfumira akizungumza na wageni mbalimbali waliohudhurua hafla ya uzinduzi wa safari ya ya shirika la ndege la Tanzania aina ya Airbus A220-300 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Robert Gabriel Mugabe Harare Zimbambwe juzi kulia ni baadhi ya viongozi mbalimbali waliohudhuria halfa hiyo akiwemo waziri wa uchukuzi na mawasiliano wa Tanzania mhandisi Isack Kamwele.


************

Shirika la ndege la Tanzania ATCL limezindua rasmi safari za ndege katika nchi za kusini mwa bara la afrika zikiwemo Zambia na Zimbabwe ambapo imeelezwa kuwa itachangia kuchagiza maendeleo ya kiuchumi, baina ya nchi hizo tatu na itafungua milango ya biashara lakini pia kupunguza gharama,muda na usumbufu ambao abiria kutoka katika nchi hizo walikuwa wakiupata kwani walilazimika kuzunguka mpaka nchi jirani ili wafike Zambia au Zimbabwe.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati ndege aina AIRBUS A 220-300 ikiruka kwa mara ya kwanza kutoka kiwanja cha ndege cha kimataifa cha JKN Dar es salaam kuelekea katika nchi hizo na kutua nchini Zimbabwe na Zambia.

Uzinduzi rasmi wa ndege hiyo umefanyika katika viwanja viwili tofauti kikiwemo kile cha Robert Gabriel Mugabe Harare- Zimbabwe na baadae uwanja wa Kenneth Kaunda Lusaka- Zambia, huku abiria hao wakipongeza serikali ya awamu ya tano kwa kuwekeza katika sekta ya anga ambayo zaidi ya miaka ishirini ilionekana kuyumba.

Baadhi ya abiria Mahenye Muya mfanyabiashara wa pembejeo za kilimo kutoka Arusha alisema kuwa kuzinduliwa kwa ndege hiyo kumewasaidia kupunguza gharama na mzunguko usiokuwa wa lazima ambao awali ili kufika Lusaka walilazimika kupitia Ethiopia. 

“Kutoka Tanzania mpaka Harare ni kama saa 1.dakika 50 na Lusaka ni saa 1.dakika 45 muda wa safari umepungua kwa saa tano,unajua sisi wafanyabiashara muda ni pesa kwa kutumia ATCL nimesave muda na pesa”alisema Muya

Waziri wa uchukuzi na mawasiliano mhandisi Izak Kamwelwe amesema shirika hilo limedhamiria kujiimarusha katika sekta hiyo kwa kuongeza idadi ya ndege lakini pia kuhakikisha linafika katika nchi mbalimbali barani Afrika na bara la Asia.

“hivi karibuni tutaanza kwenda India ambayo ni mwisho wa mwezi Machi,na mwezi April mwishoni au Mei tutaanza kusafiri kwenda China kwa sababu tupo katika hatua nzuri ya mazungumzo.”alisema Kamwelwe.

Alisema serikali itaendeleza na wimbi la kununua ndege ambapo mwezi November itapokea ndege nyingine aina ya Dreamliner na Bombadier hivyo kufanya serikali ya Jamhuri ya muungano kuwa na ndege 11.

Akizungumzia namna shirika hilo lilivyojipanga katika kutoa huduma hiyo ya anga karika nchi mbalimbali barani Afrika Mkurugenzi mtendaji wa shirika la ndege nchini Mhandisi Ladislaus Matindi alisema ATCL imejipanga kutoa huduma safi na ndege zake ni za uhakika.“ATC imejipanga kulihudumia soko hilo kwa hiyo hatufanyi majaribio wala hatufanyi kitu tusichokuwa na uhakika nacho tunahakika na hili soko”alisema Matindi

Kwa upande wake waziri wa mazingira na utalii wa Zimbabwe Prisca Mupfumira na kaimu waziri wa uchukuzi na mawasiliano wa Zambia Kafwaya Mutotwe wamesema kuanza kwa safari hizo kutaendeleza kuimarisha uhusiano uliopo wa muda mrefu uliowekwa na waasisi wa mataifa hayo katika Nyanja mbalimbali.

“Leo historia inaandikwa tena baada ya miaka ishirini ndege za Tanzania kugusa ardhi ya Zimbabwe naamini uzinduzi huu unatarajiwa kufungua furs azote kuanzia kiuchumi,na raia wetu kufurahia mawasiliano ya uhakika kufikia vivutio vya utalii na biashara”alisema Mupfumira

Ndege hiyo aina ya AIRBUS A 220-300 ya Shirika la ndege la Tanzania itakuwa ikisafiri mara tatu kwa wiki kuelekea katika nchi za Zambia na Zimbabwe ambapo mpaka sasa ndege hizo zitakuwa zikifika katika nchi nne za Afrika ikiwemo Uganda na Burundi.

MAKAMU WA RAIS ASEMA UPATIKANAJI WA MAJI KALIUA KUFIKIA ASILIMIA 50 MWAKA 2020

0
0
NA TIGANYA VINCENT

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itahakikisha tatizo la maji wilayani Kaliua linatafutiwa ufumbuzi ili kuwatua ndoa kichwani wakinamama.

Alisema ifikapo mwaka 2020 hali ya upatikanaji wa maji katika Wilaya ya Kaliua utaongezeka kutoka asilimia 25 za sasa na kufikia asilimia 50

Makamu wa Rais alitoa kauli hiyo kwenye mkutano wa hadhara katika uwanja wa Kolimba wilayani Kaliua ikiwa ni siku nne ya ziara yake mkoani Tabora .

Alisema Serikali itahakikisha inachimba visima na kujenga mabwawa katika maeneo ambayo maji kutoka Ziwa Victoria yatakaposhindwa kufika ili kuwaondelea shida na upatikanaji wa maji safi na salama wananchi.

Katika hatua nyingine Makamu wa Rais ametoa onyo kwa watu ambao wameanza kuingia katika hifadhi za mistu na kuendesha uharibifu ikiwa ni pamoja na ukataji wa miti na kuendesha kilimo ndani ya hifadhi.

Alisema tamko la Rais wa Jamhuri ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli lilihusu vijiji ambavyo vilikuwa tayari ndani ya maeneo ya hifadhi na vilivyo ainishwa na sio kuanzisha makazi mapya ndani ya hifadhi.

Makamu wa Rais alisema mtu akayeingia katika Hifadhi atachukuliwa hatua za kisheria na kuwataka Watendaji mbalimbali kuhakikisha wanawaondoa watu ambao wameanza kuvamilia mistu na kuongeza kuwa Rais Magufuli hakusema watu waanze kuingia katika hifadhi ya mistu.

Wakati huo huo Makamu wa Rais alisema ifikapo mwaka 2023 vijiji vyote nchini vitakuwa na umeme. Aliwataka wananchi kutumia upatikanaji wa umeme katika masuala ya maendeleo ya viwanda vya kati na vikubwa.


SERIKALI HAITOMUACHA SALAMA MTUMISHI YEYOTE ATAKAEKULA FEDHA ZA UMMA KWA MASILAHI BINAFSI

0
0

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi hao, mara baada ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF Wilayani Bagamoyo.
Baadhi ya watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani), wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji, mara baada ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF Wilayani Bagamoyo.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Mhe. Zainab R. Kawawa akimueleza Dkt. Mwanjelwa hatua alizochukua dhidi ya changamoto ya ubadhirifu wa fedha za umma wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi wa Halmashauri hiyo chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji, mara baada ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF Wilayani Bagamoyo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Mhe. Zainab R. Kawawa wakisikiliza maelezo ya kiutumishi toka kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, Bw. Shabani Milao wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi wa Halmashauri hiyo chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akisisitiza nidhamu katika matumizi ya fedha za umma kwa watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.

…………………..

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) amesema Serikali haitosita kumchukulia hatua kali za kinidhamu na kisheria mtumishi wa umma yeyote atakaebainika kula fedha za umma ambazo zinatolewa na Serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri huyo wakati wa kikao kazi na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji, mara baada ya kutembelea wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wilayani humo ili kujiridhisha na utekelezaji wa mpango huo.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amewataka watumishi wa umma wote nchini kuwa waaminifu na waadilifu katika kutumia vema fedha za umma ambazo malengo yake ni kuwaletea maendeleo wananchi hususani wanaoishi katika maeneo ya vijijini.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa ametoa wito kwa watumishi wa umma kubadilika na kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha za Serikali kwa kuzingatia Kanuni, Sheria na Taratibu, akitoa mfano wa fedha zaidi ya shilingi milioni 457 ambazo zilitolewa na Serikali kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze ambazo zilitumika kinyume na utaratibu, na kuongeza kuwa, halmashauri hiyo ililazimika kuzirejesha baada ya Serikali kubaini ubadhirifu huo na kuamuru zirejeshwe.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Mhe. Zainab R. Kawawa amemueleza Dkt. Mwanjelwa kuwa, baada ya kuwachukulia hatua watumishi wabadhirifu katika Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, mapato ya Halmashauri hiyo yaliongezeka kutoka milioni 400 kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Septemba, 2018 na kufikia milioni 760 kwa kipindi cha mwezi Oktoba hadi Desemba, 2018 na kuongeza kuwa, kutokana na hatua iliyochukuliwa anaamini mapato ya Halmashauri hiyo yataongezeka na inawezekana yakafikia bilioni moja katika kipindi hiki cha kuanzia mwezi Januari hadi Machi, 2019.

Mhe. Kawawa ameahidi kuendelea kuwashughulikia ipasavyo watumishi wote wanaohujumu mapato ya Serikali katika wilaya yake kwani atahakikisha mapato yanaongeza, na kufafanua kuwa pasipo shaka wapo watumishi wachache wanaohujumu vyanzo vya mapato na kufanya ubadhirifu hivyo amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo kuendelea kuchukua hatua stahiki za kinidhamu na kisheria kwa watumishi wote waliobainika kujihusisha na kuhujumu mapato na kushiriki katika ubadhirifu wa fedha.

Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) anaendelea na ziara ya kikazi kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma Mkoani Pwani, mpaka sasa ameshakutana na watumishi katika Halmashauri ya Mji Kibaha, Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo na Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze ambapo amewataka watumishi hao kuwa waadilifu, kufanya kazi kwa bidii, maarifa na kuzingatia weledi katika utendaji kazi.

WAZIRI MHAGAMA AKAGUA MAANDALIZI YA UZINDUZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU MKOANI SONGWE

0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akitoa maelezo kwa walimu wa halaiki mara baada ya kukagua na kujionea hatua za awali za maandalizi ya vijana wa halaiki.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana, Bw. James Kajugusi (wa pili kutoka kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipotembea Uwanja wa Mlowo kujionea hali ya maandalizi. (Kushoto) ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza.
Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi, Mhandisi Tanu Deule akitoa maelezo kuhusu Uwanja kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (watano kutoka kushoto) alipotembelea na kukagua hali ya Uwanja na miundombinu mbalimbali katika uwanja wa Mlowo zitakapofanyika Sherehe hizo(mwenye miwani) ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Brigedia Jenerali (Mst.), Nicodemus Mwangela. (Wa tatu kutoka kushoto) ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza. PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)






Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na Viongozi na watendaji wa Mkoa wa Songwe mara baada ya kuwasili Mkoani hapo wakati wa ziara yake ya kukagua maandalizi hayo Mkoani humo. (Kushoto) ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Brigedia Jenerali (Mst.), Nicodemus Mwangela akitoa taarifa ya Mkoa wa Songwe kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipowasili mkoani humo kukagua maandalizi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akipitia kwa makini ripoti ya maandalizi ya Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru alipowasili kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe kupokea taarifa hiyo. (Kulia) ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Songwe Bw. Elinico Mkola.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza jambo mara baada ya kupokea taarifa ya maandalizi alipofanya kikao kifupi na baadhi ya Wanakamati ya Maandalizi ya Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoani Songwe. (Kushoto) ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Brigedia Jenerali (Mst.), Nicodemus Mwangela. (Kulia) ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Songwe Bw. Elinico Mkola.
Baadhi ya Viongozi na Watendaji wa Mkoa wa Songwe wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao kuhusu maandalizi ya Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Ofisi za Chama cha Mapinduzi (CCM) zilizopo Vwawa, Mkoani Songwe.
Vijana wa Halaiki wakitengeneza umbo la Mlima Kilimanjaro kuashiria kupandisha Bendera ya Taifa katika mlima Kilimanjaro wakati Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipotembea vijana hao katika shule ya msingi ya Ichenjezya ambapo vijana hao wa halaiki wanafanya maandalizi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na vijana wa halaiki mara baada ya kuwasili shule ya msingi ya Ichenjezya iliyopo Vwawa kujionea maandalizi ya Vijana hao.


……………………….

Na; OWM (KVAU) – Songwe

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama amefanya ziara na kukagua maandalizi ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru zinazotarajiwa kufanyika tarehe 2 Aprili, 2019 Mkoani Songwe.

Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa kutoka kwenye kamati ya Maandalizi, Waziri Mhagama alieleza kuridhishwa na hatua za awali za maandalizi na kuipongeza kamati ya Mkoa kwa kusimamia vyema na kuratibu shughuli za maandalizi hayo.

“Niwapongeze kwa hatua hizi mlizofikia katika kuhakikisha shughuli hii ya kitaifa inafana, maana maandalizi bora yataleta heshima kwa Mkoa katika kufanikisha jukumu hilo muhimu, hivyo mzingatie masuala yote ya msingi na kufanya uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Songwe una kuwa wa kihistoria,” alisema Waziri Mhagama

Aliongeza kuwa, Mbio za Mwenge wa Uhuru zinahistoria kubwa katika Taifa letu, ikiwa ni mwaka wa 55 sasa tunaadhimisha mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa na ni mwaka wa 27 toka kuanzishwa mfumo wa vyama vingi ikiwa ni kielelezo tosha cha kukua kwa demokrasia nchini.

Vilevile ni miaka 20 ya kumbukizi ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere hivyo ni vyema vijana wakatambua historia ya Taifa na kujifunza falsafa za Baba wa Taifa kwa kuwa na umoja, mshikamano, uzalendo, kujitolea na zaidi kuchochea maendeleo ya nchi.

“Kupitia shughuli hii ya kitaifa vijana wanapaswa kutumia fursa hiyo kuelewa historia ya Taifa lao pamoja na Mwenge wa Uhuru kama kielelezo muhimu cha Utaifa,” alisisitiza Mhagama

Hata hivyo, Mhe. Mhagama aliusihi uongozi wa Mkoa kutumia nafasi hiyo kutangaza vivutio vya utalii, fursa za kiuchumi na shughuli mbalimbali zilizopo ndani ya mkoa wa Songwe. Pia aliwataka waendelee kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya uzinduzi.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali (Mst.), Nicodemus Mwangela, alipokea maelezo yaliyotolewa na kuahidi kusimamia shughuli zote za maandalizi kwa ufanisi na kukamilisha ndani ya muda uliopangwa.

“Nikuhakikishie maandalizi yataendelea kwa kasi na yatakamilika kwa wakati ili kuwawezesha wananchi wa Mkoa wa Songwe wanashiriki katika tukio hilo muhimu na kuitumia fursa hiyo ya Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kujitangaza kama Mkoa,” alisisitiza Mhe. Mwangela

SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI MCHANGO WA WATUMISHI WA UMMA KATIKA KULETA MAENDELEO YA NCHI

0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb), akisalimiana na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi kabla ya kuingia katika ukumbi wa halmashauri hiyo kuzungumza na watumishi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb), akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi (hawapo pichani) katika kikao kazi kilichofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri hiyo. Kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Bi. Rehema Madenge na kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Mhe. Shaibu Ndemanga.
Baadhi ya Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya Manispaa ya Lindi.
Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Mhe. Shaibu Ndemanga akitoa neno la shukrani baada ya kikao kazi kati ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) na watumishi wa halmashauri ya Manispaa ya Lindi kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo.

Urasimishaji Ardhi ni Kichocheo cha Maendeleo Endelevu -MKURABITA

0
0
Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania ( MKURABITA) Bi Seraphia Mgembe akionesha hati milki ya kimila ya kumiliki ardhi na kusisitiza umuhimu wa wananchi Wilayani Chamwino mkoani Dodoma kuchukua hati milki hizo baada ya kurasimisha mashamba yao ili waweze kujiletea maendeleo.
Meneja Urasimishaji Ardhi Vijijini kutoka Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) Bw. Antony Temu akisisitiza umuhimu wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wananchi waliorasimisha mashamba yao katika kijiji cha Membe Wilayani Chamwino mkoani Dodoma.



Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Chamwino Bi Juliana Mtolera akisisitiza jambo wakati wa mafunzo kwa wakulima zaidi ya 100 katika kijiji cha Membe Wilayani humo wakati wa mafunzo yakuwajengea uwezo ili waweze kuzalisha kwa tija, mafunzo hayo yameandaliwa na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania ( MKURABITA) kwa kushirikiana na Halmshauri ya Wilaya hiyo.



Sehemu ya wakulima zaidi ya 100 wa kijiji cha Membe Wilayani Chamwino wakifuatilia mafunzo ya kuwajengea uwezo ili waweze kuzalisha kwa tija baada ya kurasimisha mashamba yao.

……………………………………………………………………………………………………

Na; Frank Mvungi, Dodoma

Serikali ya Awamu ya Tano imejikita katika kuwezesha wananchi kiuchumi kupitia Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA ) kwa kuwawezesha wananchi kurasimisha ardhi wanazomiliki yakiwemo mashamba na kupatiwa hati za kimila za kumiliki ardhi.

Ni vyema wananchi Wilayanis Chamwino na maeneo mengine ambayo ymeshanufaika na urasimishaji wakatambua kuwa jukumu lao sasa ni kutumia fursa zitokanazo na urasimishaji kujiletea maendeleo.

Sasa wananchi wote mlionufaika na urasimishaji tambueni kuwa Serikali imewekeza kwenu kwa kuwajengea uwezo hali inayowawezesha kujikwamua na kujiletea maendeleo ikiwemo kupata mikopo katika Taasisi za fedha kama mabenki kupitia hati za kimila za kumiliki ardhi.

Dhamira hii safi ya Serikali inapaswa kuungwa mkono na wananchi wote ambao wameshanufaika na urasimishaji uwe wa ardhi au biashara, nalisema hili kwa kuwa nimeshudia hivi karibuni Mratibu wa MKURABITA Bi Seraphia Mgembe akihamasisha wananchi wa Wilaya ya Chamwino na maeneo mengine hapa nchini kujitokeza kuchukua hati zao ambazo ni ukombozi wa kiuchumi na mwarobaini wa umasikini kwa wananchi wanyonge.

Uhamasishaji huu nimeushuhudia ukifanyika mara kwa mara na hata wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wakulima zaidi ya 100 na viongozi 10 wa Kijiji cha Membe, Wilayani Chamwino Bi Mgembe alionekana kuguswa na suala la wananchi kuchelewa kuchukua hati zao za kimila baada kurasimishiwa mashamba yao, akionesha shauku yake ya kutaka kuona wananchi wanajikwamua kiuchumi kupitia hati hizo.

Kutokana na urasimishaji huo ambao umefanyika katika Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma jumla ya mashamba 1145 yalipimwa katika Kijiji cha Membe ambapo hatimiliki 1000 zimeweza kuandaliwa na sehemu kubwa ya hati hizo hazijachukuliwa na wananchi na kuzitumia katika suala zima la kujenga uchumi na kupanua wigo wa uzalishaji wa mazao mbalimbali ikiwemo alizeti.

Dhamira hii njema ya Serikali inatekelezwa na Ofisi ya Rais- MKURABITA ambayo imejipambanua kwa vitendo kutokana na kutekeleza dhana yakujenga uchumi shirikishi au jumuishi unalenga kuwawezesha wananchi kupitia rasilimali zilizopo katika maeneo yao ikiwemo ardhi.

Hati hizo ziwe chachu kwa wananchi kujikwamua kiuchumi na kuunga mkono nia hii njema ya Serikali ya kuwaletea maendeleo; katika hili ni wazi kuwa wananchi wa Wilaya ya Chamwino wamepata ukombozi wa kiuchumi ambapo sasa wanapaswa kuunga mkono juhudi hizi kwa kuchukua hati hizi.

Aidha, jambo jingine muhimu ni wananchi wote ambao tayari maeneo yao yamepimwa na kupatiwa hati ni kuongeza bidii katika uzalishaji ili kuendana na dhana ya ujenzi wa viwanda ambavyo vinategemea malighafi kutoka katika sekta ya kilimo.

Aidha, faida za urasimishaji ni kama ; kuhakikisha usalama wa milki kwa kuiongezea thamani ardhi husika, Kuweza kujipatia mikopo na kuwawezesha wamiliki kuingia ubia katika uwekezaji kwenye ardhi na kilimo kupitia wadau mbalimbali.

MKURABITA imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa dhamira ya Serikali kuwezesha wananchi kiuchumi inatimia kwa wakati kutokana na mkazo inaouweka katika kuwezesha wananchi kurasimisha mashamba yao, viwanja na biashara zao katika maeneo mbalimbali yaliyofikiwa na mpango huu.
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live




Latest Images