Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1806 | 1807 | (Page 1808) | 1809 | 1810 | .... | 1898 | newer

  0 0

   Bei za bidhaa mbalimbali katika soko  la Kiwalani wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam,kamazinavyo onekana katika picha.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)

   Bei za mchele katika soko la Kiwalani wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam  kama inavyo onekana katika vibao.
  Bei ya Nazi  katika soko la Kiwalani wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam kama inavyo onekana katika vibao.

  0 0

  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo, Alex Msama akizungumza jijini Dar es Salaam leo ofisini kwakwe Kinondoni kuhusu maandalizi wa tamasha hilo litakalofanyika Aprili 21 jijini Dar es salaam.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo, Alex Msama akimsikiliza mmoja wa waratibu wa tamasha hilo Saleh Ali wakati akifafanua zaidi kuhusu maandalizi ya tamasha hilo litakalofanyika Aprili 21 jijini Dar es salaam.

  0 0

   Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Simon Anange akipokea Dhana za kufundishia Masuala ya Familia na Malezi ya Mtoto kutoka kwa Mkurugenzi  Msaidizi Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Idara ya Watoto Sehemu Familia na Malezi Bi. Grace Mwangwa   wakati wa kufunga mafunzo kwa maafisa hao kuhusu mafunzo ya uelimishaji Jamii  kwa kutumia Kitini cha Familia na Malezi ya Mtoto.
   Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Simon Anange akikabidhi Dhana za kufundishia Masuala ya Familia na Malezi kwa Afisa Maendeleo ya Jamii aliyewakilisha Mkoa wa Shinyanga wakati wa kufunga mafunzo kwa maafisa hao kuhusu mafunzo ya uelimishaji Jamii  kwa kutumia Kitini cha Familia na Malezi ya Mtoto. 
   Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Simon Anange akiongea na Maafisa Maendeleo ya Jamii pamoja na Maafisa Ustawi wa Jamii kutoka Mikoa ya Kigoma, Shinyanga na Katavi wakati wa kufunga mafunzo kwa maafisa hao kuhusu mafunzo ya uelimishaji Jamii  kwa kutumia Kitini cha Familia na Malezi ya Mtoto.
   Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya uelimishaji Jamii  kwa kutumia Kitini cha Familia na Malezi ya Mtoto wakiwa katika kazi ya vikundi kujadiliana namna bora ya kuwasiligsha mafunzo hayo kwa Jamii kabla ya kufungwa kwa mafunzo hayo mapema leo Katika mji mdogo wa Kasulu. 
  Mkurugenzi  Msaidizi Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Idara ya Watoto Sehemu Familia na Malezi Bi. Grace Mwangwa akiongea na Maafisa Maendeleo ya Jamii pamoja na Maafisa ustawi wa Jamii   wakati wa kufunga mafunzo kwa maafisa hao kuhusu mafunzo ya uelimishaji Jamii  kwa kutumia Kitini cha Familia na Malezi ya Mtoto.

  Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma Kanali Simon Anange amesikitishwa na watoto kufanyiwa vitendo vya ukatili na ndugu na watu walioaminiwa kuwalea au kuwatunza iwe nje au manyumbani kwao.
  Akifunga Mafunzo ya siku nne kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii pamoja na Maafisa Ustawi wa Jamii kuhusu matumizi ya Kitini cha Malezi ya Mtoto na Familia yalitolewa na Wizara ya Afya Idara Kuu Maendelep ya Jamii  Kanali Anange amesema amesema asilimia 40 ya vitendo vya ukatili inafanyika mashuleni ikiwemo utani wa kumdhalilisha mtu na kufanya watoto kuichukia shule.
  Akiutaja unaofanyika mashuleni Kanali Anange amesema ni ukatili wa kunyanyasa mtu kwa kumtania jambo ambalo limechangia baadhi ya watoto wanaokumbwa na kadhia hiyo kugoma kwenda shule.
  Aidha Mkuu wa Wilaya hiyo amelitaja tatizo la kibinafsi kuwa linachangiwa na wazazi wa siku hizi kuwalea watoto katika mazingira ya kujitenga tofauti na hapo awali ambapo mtoto kimsingi alikuwa ni mtoto wa Jamii nzima.
  Amesema tatizo tulilonalo la watoto wa mitaani linatokana na malezi mabaya kwani katika Jamii ya watu wa Zanzibar hakuna watoto wa mitaani akiitaja Tanzania bara kukosa upendo kwani Jamii yetu inayojiita imeendelea imezidisha ubinafsi kwa kuwa na upendo tu kwa watoto walio wazaa tu bila kuangalia watoto wengine walipokosa upendo na kukimbilia mitaani.
  Ameitaja jamii kuanagalia kile tunachokiita kuendelea kama kinaleta tija kwani maendeleo ya sasa ya mtoto kula katika saani peke yake kinamfanya kufikili kuwa cha kwake ni cha kwake matokeo yake ni kuwa na jamii yenye ubinafsi na maendeleo ya sasa yanakiuka misingi muhimu kama zamani kwa kisingizio cha maendeleo na kuongeza kuwa wakati mwingine maendeleo ya sasa yanaipeleka jamii kuendekeza mambo yasiyokuwa ya razima.
  Wakati huohuo Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Familia kutoka Wizara ya Afya, Idara  Kuu Maendeleo ya Jamii Bi. Grace Mwangwa amesema ili kuweza kuendeleza Jamii zetu Serikali kupitia Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto imejipanga kutokomeza mila mbaya katika Jamii na kuenzi mila nzuri lakini pia kuitaka jamii kutambua kuwa kuna tofauti kati ya kutunza na kulea watoto.
  Aidha Bi. Mwangwa amesema kuwa Serikali imejiwekea malengo kupitia mpango kazi huo kuwa ifikapo mwaka 2022 serikali iwe imetokomeza vitendo vya ukatili katika Jamii na kuongeza kuwa mpango huu pia unaangalia mazingira salama ya mtoto akiwa shuleni lakini pia katika Jamii.
  Mafunzo haya kuhusiana na malezi ya mtoto na familia yamefanyika kwa wataalamu wa maendeleo ya Jamii kutoka Mikoa ya Shinyanga, Kigoma na Katavi na mikoa hii kwa kiasi kikubwa ina changamoto ya uwapo wa mimba na ndoa za utotoni lakini yanafanyika huku Taifa likuwa linakumbwa na kitisho kipya cha mauaji ya watoto.


  0 0

  Na Andrew Chale

  Viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwemo Mawaziri pamoja na viongozi wengine wamejitokeza kuhani msiba wa mtoto wa Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia Mbunge wa Nzega Vijijini  Dk.Hamisi Andrea  Kigwangalla  marehemu Zulqarinain  aliyefariki jana February 21,2019 majira ya Saa nne asubuhi  JAKAYA KIKWETE CARDIAC INSTITUTE - MUHIMBILI.

  Viongozi hao pamoja na ndugu na jamaa na marafiki wamejumuika kwa pamoja nyumbani kwake Mikocheni A katika Kota za Mawaziri jirani na kituo cha mafuta cha Victoria.

  Baadhi ya viongozi hao akiwemo Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Paramagamba Kabudi,Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii  Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu,Waziri wa Kilimo  Japhet Hasunga

  Wengine ni Naibu Waziri wa Afya  Dk Faustine Ndugulile, Naibu waziri mambo ya ndani Masauni, Naibu Waziri Madini, Naibu Waziri mambo ya Nje  na wengine wengineo.

  Pia wengine Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda pamoja na wengine wakiwemo Wabunge,  ndugu  jamaa na Marafiki.

  Awali  Msemaji wa Familia Bwana  Lumola alieleza  kuwa mwili utasafirishwa 22 Februari kwa  ndege na Mazishi yanatarajiwa kufanyika saa Kumi jioni Nzega Vijijini  Jimboni kwa Waziri Dk Kigwangalla.

  #R.I.P. Zul.

  Inna lillahi wainna illaihi rajiuun
  0 0


  Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

  SERIKALI nchini kupitia Wizara  ya Mifugo  na Uvuvi imewahakikishia wafugaji kuwa hakuna mifugo itakayopotea  kutokana na magonjwa  mbalimbali.

  Haya yameelezwa na Naibu  Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdullah Ulega wakati akizungumza na wafugaji wa Wilaya ya Kibaha mkoani  Pwani, wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja alioifanya mkoani humo kwa lengo la  kukagua miradi iliyoko chini  ya wizara hiyo.

  Amesema Serikali  ilibinafsisha sekta  hiyo  kwa watu binafsi,lakini kwa sasa imerejeshwa serikalini  ili kuwasaidia  wafugaji wa aina zote.

  "Kwa sasa  tunazalisha chanjo  ya mdondo zaidi ya milioni 100 kwa mwaka,lengo ni kuwafanya  wafugaji wa kuku na hasa akinamama  waweze kuondokana na umasikini,"amesema Ulega.

  Ameongeza  madhumuni ya Serikali ya Awamu ya tano  ni kuhakikisha nchi inakuwa  na mifugo mizuri yenye kuleta tija kwa wafugaji na wawekezaji wa nyama,hivyo amewataka wafugaji kuamini serikali kwa jinsi inavyowapambania katika kuhakikisha soko la bidhaa hiyo  inakuwa kubwa  na yenye tija kwao.

  Aidha  ameongeza kuwa kipindi hiki wafugaji nchini wamekuwa  wakinyanyaswa na wafanya biashara kwa kuuza chanjo hizo kwa bei  ya Sh.35,000  mpaka Sh. 45,000 kutokana na hali hiyo Serikali imeamua kusambaza dawa  hizo za chanjo kwa bei ya Sh.20,000, hivyo itawasaidia watanzania  wengi na kuondoa vifo  vya  mifugo.  

  Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa wlWakala maabara ya vetenari Tanzania,Dk. Furaha Mramba  amesema chanjo zinazozalishwa katika maabara hiyo zinaubora uliothibitishwa na mamlaka za maabara za Mifugo Africa na itakapokamilika itatosheleza mahitaji ya ndani  na nyingine kuuzwa nje ya nchini.

  Katika ziara hiyo  Ulega pia ametembelea chamba la  kuzalisha malisho ya mifugo lililopo Vikuge wilayani Kibaha, pamoja Halmashuri ya Chalinze wilayani Bagamoyo kisha kuhutubia mkutano wa hadhara  kata ya Pangani na kuwaomba wakazi wa kata hiyo kuacha tabia ya kuvamia maeneo yaliotengwa na serikali kwa ajili ya miradi mbalimbali ya Maendeleo.
   Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na watumishi mbalimbali wa kampuni ya Ranchi ya Taifa ya Mlandizi wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani.
    Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akifafanua jambo kwenye mkutano wa hadhara  kata ya Pangani,ambapo amewaomba wakazi wa kata hiyo kuacha tabia ya kuvamia maeneo yaliotengwa na serikali kwa ajili ya miradi mbalimbali ya Maendeleo.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)

     Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega  (alienyosha mkono) akiwa ameambatana na watendaji mbalimbali wakikagua upanuzi mkubwa wa maabara ya  kutengenezea chanjo za kudhibiti magonjwa ya mifugo  iliyopo  mji wa Kibaha mkoa wa Pwani.


    Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na wafugaji ambapo aliwahakikishia kuwa hakuna Mifugo itakayopotea  kutokana na ugonjwa  wowote.
  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega(katikati) akiwa katika picha ya pamoja. 
  Muonekano  wa Kiwanda cha chanjo ya Hester Biosciences  kinachojengwa kata ya Tangini wilaya ya Kibaha mkoa wa Pwani.(Picha zote na Emmanuel Massaka,MMG)  0 0

  Na Estom Sanga-Nachingwea 

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Mheshimiwa George Mkuchika amekumbana na kilio cha Wananchi wa wilaya za Liwale na Nachingwea Mkoani Lindi cha kuomba serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF kuwajumuisha kwenye huduma za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ili nao waweze kunufaika na huduma za Mpango huo. 

  Wakitoa taarifa za Utekelezaji wa Mpango huo kwa Waziri Mkuchika ambaye yuko katika ziara ya kikazi mkoani Lindi,viongozi wa serikali za vijiji na wilaya hizo wamesema mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa Mpango huo yameibua hamasa ya Wananchi kujiletea maendeleo na hivyo kupunguza kero ya umaskini. 

  “Mheshimiwa Waziri,Mpango huo unatekelezwa katika takribani nusu ya vijiji vya wilaya yetu na kuacha sehemu kubwa ya wananchi bila huduma hiyo muhimu iliyoanzishwa na serikali yetu,tunaomba wananchi wenye sifa za kujumuishwa kwenye Mpango huo wapate fursa hiyo muhimu” amesisitiza Mbunge wa Nachingwea Mwl……… 

  Wananchi ambao hawajajumuishwa kwenye Mpango wa Kunusuru Kaya maskini wamemweleza Mheshimiwa Mkuchika kuwa wao pia wanastahili kupata huduma za Mpango huo kwani pia wanakabiliwa na umaskini na kuwa wako tayari kutekeleza masharti ya Mpango kwani kwa sasa wameona faida zake kutoka kwa Walengwa ambao wameboresha maisha yao kwa kiwango kikubwa. 

  Akihutubia mikutano mbalimbali ya Wananchi katika Wilaya za Liwale na Nachingwea ,Mhe. Mkuchika ameweka bayana mipango ya Serikali Kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF –kuwa sehemu ya pili ya Awamu ya Tatu ya Mapngo huo ambayo inatarajiwa kuanza hivi karibuni itahakikisha kuwa vijiji /shehia ambazo hazikujumuishwa katika sehemu ya kwanza ambazo ni asilimia 30 nchini kote zinapata pia fursa hiyo. 

  “tutahakikisha kuwa tunawaandikisha Wananchi wote wenye sifa za kunufaika na huduma za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa na serikali kupitia TASAF ili vita dhidi ya umaskini iwe endelevu na yenye kasi ya kuridhisha” amesisitiza Mheshimiwa Mkuchika. 

  Aidha Waziri huo wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora amekuwa akisisitiza juu ya umuhimu wa viongozi katika ngazi za vijiji,kata,wilaya na hata mkoa kuhakikisha kuwa wanakuwa karibu zaidi na Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini na kutoa hamasa kwa Walengwa hao kutumia ruzuku wanayopata kujiletea maendeleo kwani suala la kupambana na umaskini limebainishwa kwa ufasaha kwenye Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015. 

  Katika hatua nyingine Mheshimiwa Mkuchika ameridhishwa na hatua ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF kuendelea kujenga miundombinu katika sekta ya elimu,afya na maji katika maeneo mbalimbali ya utekelezaji wa Mpango na hivyo kupunguza adha ya kufuata huduma hizo mbali na maeneo yao kwa Walengwa na Wananchi wengine kwenye maeneo hayo. 

  Ameyasema hayo alipokagua madarasa yaliyojengwa na TASAF katika Shule ya Msingi Kongo wilayani Nachingwea ambako pia TASAF imejenga tanki la maji,vyoo,madawati, meza ,makabati na kuweka umeme wa jua(solar panel) katika shule hiyo ya msingi kwa kuwashirikisha walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kupitia utaratibu wa Ajira za Muda.
  Waziri Mkuchika akifurahia zawadiya kuku aliyopewa na Walengwa wa TASAF wilayani Nachingwea Mkoani Lindi baada ya kuwahutubia wananchi na walengwa hao.

   Waziri Mkuchika akikagua madarasa yaliyojengwa na TASAF katika shule ya msingi Kongo wilayani Nachingwea mkoani Lindi akiwa kwenye ziara ya kikazi wilayani humo.
   Waziri Mkuchika akizungumza na wanafunzi katika shule ya msingi Kongo wilayani Nachingwea ambako TASAF imejenga madarasa,vyoo,tanki la maji na mfumo wa umeme jua (solar )

  0 0  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Maulidi Banyani akisisitiza jambo katika mkutano huo.
   Kaimu Mkurugenzi wa Hazina na Uendelezaji Biashara, William Genya akijadiliana jambo na Meneja wa Wakala wa Majengo wa Serikali (TBA) mkoa wa Geita, Glagys Jeffta wanaoshuhudia ni maafisa uendelezaji biashara, Clara Lumbanga, Olivia Musanga Zoka na Phoibe Keu.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Eliud Mwaiteleke akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Maulidi Banyani leo jioni.
  Eneo lililopimwa la Rubambangwe linavyoonekana kwa picha ya Drone,
  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Eliud Mwaiteleke, Mkuu wa Wilaya ya Chato Mtemi Simioni na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Maulidi Banyani wakijadiliana jambo jioni ya leo baada ya uzinduzi wa mauzo ya viwanja Chato.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Eliud Mwaiteleke akijadiliana jambo na Mkuu wa Wilaya ya Geita Josephat Maganga.
   Mazungumzo yakiendelea baada ya uzinduzi wa mauzo ya viwanja.

   Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Eliud Mwaiteleke akijadiliana jambo na  na Kaimu Mkurugenzi wa Masoko wa NHC, Itandula Gambalagi.

  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Maulidi Banyani akizungumza kutoa neno la shukurani katika uzinduzi huo kulia kwake ni Mkuu wa Mkuu wa Wilaya ya Chato Injinia Msafiri Mtemi Simioni na kushoto kwake ni Waziri wa Nishati na mbunge wa jimbo hilo, Dk. Medard Kalemani.
  Waziri wa Nishati na mbunge wa jimbo hilo, Dk. Medard Kalemani akimshukuru Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Maulidi Banyani kwa mchango wake katika upimaji wa viwanja hivyo vilivyozinduliwa mauzo.


   Hadhira ikifuatilia hafla hiyo ya uzinduzi.
   Hadhira ikifuatilia hafla hiyo ya uzinduzi.
  Mkuu wa Wilaya ya Chato Injinia Msafiri Mtemi Simioni  akizunguma katika uzinduzi huo kushoto kwake ni  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Maulidi Banyani na Waziri wa Nishati na mbunge wa jimbo hilo, Dk. Medard Kalemani. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Halmashauri na Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya hiyo, Philip Shoni.
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Maulidi Banyani akijadiliana jambo na Waziri wa Nishati na mbunge wa jimbo hilo, Dk. Medard Kalemani.

  Waziri wa Nishati na mbunge wa jimbo hilo, Dk. Medard Kalemani akizungumza katika hafla hiyo na kulia kwake ni  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Maulidi Banyani.


  Mkuu wa Wilaya ya Chato Injinia Msafiri Mtemi Simioni akijadiliana jambo na  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Maulidi Banyani na Waziri wa Nishati na mbunge wa jimbo hilo, Dk. Medard Kalemani.
   Wakifuatilia hafla hiyo.

  Mkuu wa Wilaya ya Chato Injinia Msafiri Mtemi Simioni akijadiliana jambo na  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Maulidi Banyani na Waziri wa Nishati na mbunge wa jimbo hilo, Dk. Medard Kalemani.
  Wakiagana mara baada ya kuhitimisha hafla ya uzinduzi wa mauzo ya viwanja.


  Halmashauri ya Wilaya ya Chato ikishirikiana na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) inautangazia umma juu ya uuzaji wa viwanja 1,035 vilivyopimwa na kuwekewa barabara katika eneo la Mlimani na Rubambangwe kata ya Muungano. Mauzo ya viwanja yanaanza wiki ijayo.

  Wananchi wote mnakaribishwa kununua viwanja vyenye matumizi mbalimbali kama vile makazi, makazi na biashara, viwanja vya biashara, maeneo ya kumpumzikia, viwanja vya michezo na huduma mbalimbali za kijamii kama zahanati, Shule, Vituo vya Mafuta kwa bei ya kuanzia Tsh 1,300 kwa mita ya mraba.

  Viwanja vipo mita chache kutoka katikati ya mji wa Chato. Vipo mkabala na barabara kuu iendayo Bukoba. Pembezoni mwa Ziwa Victoria.

  Viwanja vilivyopimwa na kupangwa kwa ajili ya makazi vina ukubwa kama ifuatavyo:
  1. Ujazo wa juu (High density)
  2. Ujazo wa kati (Medium density)
   3. Ujazo wa chini (Low density) 

  VIWANGO VYA GHARAMA YA VIWANJA KWA MATUMIZI MBALIMBALI

  1. Makazi –Bei ya kiwanja kwa mita moja ya mraba ni Shilingi 1,300/=
  2. Makazi na biashara- Bei ya kiwanja kwa mita moja ya mraba ni Shilingi 1,700/=
  3. Biashara (Hotel, Vituo vya mafuta, maduka makubwa)- Bei ya kiwanja kwa mita moja ya mraba ni Shilingi 2,200/=
  4. Huduma za jamii (Zahanati, shule ya awali, sekondari) Bei ya kiwanja kwa mita moja ya mraba ni Shilingi 2,200/=
  5. Ibada/kuabudu- Bei ya kiwanja kwa mita moja ya mraba ni Shilingi 2,200/=

  UTARATIBU WA KUNUNUA KIWANJA

  Chukua fomu ya maombi kutoka o­fisi za Halmashauri ya Wilaya ya Chato au Ofi­si ya NHC iliyo karibu nawe.
  Lipia angalau asilimia 30 ya thamani ya kiwanja unachonunua na kiasi kinachobaki kilipwe ndani ya siku 90.
  Malipo yote yafanyike kwenye akaunti ya benki ifuatayo: Jina la Akaunti : MRADI WA VIWANJA CHATO Nambari ya akaunti : 327 100 116 07 Benki: NMB Tawi la Chato
  Rejesha fomu ya maombi uliyojaza kwa usahihi ukiambatanisha pamoja na vielelezo vinavyohitajika ikiwemo nakala ya malipo (deposit slip) kutoka benki.
  Utapatiwa barua ya uthibitisho (Offer Letter) mara tu ombi lako litakapokubaliwa, pamoja na masharti ya kukamilisha malipo ya kiwanja unachochagua.
  Kwa maelezo zaidi tembelea ofisi za Idara ya ardhi ya Halmashauri ya Wilaya ya Chato.

  Au KAMBARAGE House, 1 Mtaa wa Ufukoni, Dar es Salaam, Tanzania. Kwa Mawasiliano piga namba  +255 282 228 007/ +255 754 444 333.

  PHILIP SHONI
  KWA NIABA YA MKURUGENZI MTENDAJI
  HALMASHAURI YA WILAYA YA CHATO
  21/02/2019


  0 0

  Na Khadija Seif,Globu ya jamii

  KIJANA Khamis Salum mwenye ulemavu wa miguu awapongeza wasanii wa Bongomovie kwa kumtembelea na kumpatia baadhi ya mahitaji nyumbani kwake Yombo jijini Dar es salaam.

  Akizungumza na waandishi wa habari Salum amesema ni faraja kubwa ameipata na hakutegemea kama wasanii wangeweza kumkumbuka na kumpelekea baadhi ya mahitaji kama vile mchele,magodoro pamoja na fedha.

  Hata hivyo ameomba apatiwe msaada wa kitabibu kutokana na maumivu makali anayoyapata siku hadi siku na kumsababishia kushindwa kutimiza ndoto zake kama kijana .

  "Naamini nitaweza kusimama tena naomba Rais wetu wa wanyonge Dk.John  Magufuli pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda  wasikie kilio changu kwani nateseka sana, ukizingatia mimi kiumri bado mdogo nahitaji kusoma na kutimiza malengo yangu," amesema Salum.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Nitete Frola Rauo amesema Salum anahitaji kupendwa,kuthaminiwa na kutunzwa na watu wote kwani ni kijana mdogo sana na anahitaji msaada wa hali na mali.

  Rauo amesema kupitia shirika la Nitetee ambalo lipo kwa ajili ya kusaidia watu waliweza kufanya mikakati ya kuhakikisha wanamtoa Salum pale Kariakoo na kumtafutia sehemu ya kuishi ambayo ni yombo kwa sasa

  "Tulimpeleka  hospital kwa ajili ya vipimo mbalimbali na kugundua tatizo lake la miguu kuvimba linazidi kukua siku hadi siku tofauti na hapo awali," amesema Rauo

  Hata hivyo kiongozi wa Msafara huo ambae ni Msanii wa Bongomovie Steven Mengere a.k.a Stive Nyerere amesema Salum ni watoto kama watoto wengine wanahitaji kutazamwa kwa jicho la kipekee kwa sasa kutokana na maradhi yanayomsumbua ya miguu kuwa mikubwa na kumlazimu kukaa ndani na kuwa tegemezi kwa kila kitu.

  "Sisi wasanii tujitathimini na kulichukua jukumu la kumsaidia mtoto huyo kwa sasa na kuwahamasisha jamii inayotuzunguka na taifa kwa ujumla kuhakikisha Khamis anasimama," amesema Steve Nyerere.

  Pia ameeleza kuwa mahitaji madogo waliyompatia hayataishia hapo bali watarudi kujipanga upya na kuhakikisha wanampatia vitu vingine ikiwemo kumlipia chumba,fedha pamoja na vingine.
  Kijana mwenye tatizo la miguu kujaa Khamis salum akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wasanii baada ya kumtembelea anapoishi kwa sasa yombo jijini Dar es salaam.
  Msanii wa Bongomovie Steven Nyerere akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wasanii waliofika kumtembelea mtoto Khamis salum  na  kuwasilisha mahitaji yake  salum  jijini Dar es salaam

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha Maombolezo, Victoria Jijini Dar es salaam nyumbani kwa Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala, kufuatia kifo cha Mtoto wake aitwaye Zul Hamis Kigwangala Kilichotokea Februari 21,2019 katika Hospitali ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (Muhimbili)  Jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Watoto Hk Junior ,Sheila na Hawa ambao ni watoto wa Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala alipoambata na mkewe Mama Janeth Magufuli kutoa pole kwa Familia ya Waziri huyo nyumbani kwake Victoria Jijini Dar es salaam, kufuatia kifo cha Mtoto wake aitwaye Zul Hamis Kigwangala Kilichotokea Februari 21,2019 katika Hospitali ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (Muhimbili)  Jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika Dua maalum na mkewe Mama Janeth Magufuli ,Dkt. Bayoum Kigwangala (Mke wa Dkt. Kigwangala), Hk Junior , Sheila, Hawa (Watoto wa Waziri Kigwangwala) pamoja na Bi Hawa Mushi na Bi. Bagaile Bakari nyumbani kwa Waziri huyo Victoria Jijini Dar es salaam, kufuatia kifo cha Mtoto wake aitwaye Zul Hamis Kigwangala Kilichotokea Februari 21,2019 katika Hospitali ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (Muhimbili)  Jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
  0 0  0 0

  Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Azza Hilal Hamad
  Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) ameipongeza serikali ya awamu tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli kwa kuzipatia fedha shule zenye msongamano mkubwa wa wanafunzi katika halmashauri ya Shinyanga. 
  Azza ametoa pongezi hizo jana Februari 21,2019 kwenye Mkutano wa hadhara wa wananchi wa kata ya Tinde iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga uliohudhuriwa pia na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko. 

  Alizitaja shule zilizopokea pesa kutoka serikalini kwa ajili ya ujenzi wa madarasa,vyoo na nyumba za walimu kuwa ni Shule ya Msingi Masunula (Milioni 146.6),Mwasingu (milioni 46.6),Tinde A (milioni 46.6) na Tinde B (milioni 46.6). 

  Mbunge huyo aliishukuru serikali kwa kazi nzuri iliyofanya tena kwa muda mfupi kusikia kilio cha wananchi wa Shinyanga huku akibainisha kuwa aliombea shule nyingi za mkoani Shinyanga zilizopata sasa ni hizo shule nne. 
  “Mheshimiwa DC upo hapa kwa niaba ya Mheshimiwa Rais,nitumie fursa hii kuishukuru sana serikali ya Dkt. John Pombe Magufuli,serikali inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi,serikali sikivu,nimesema wamenisikiliza kwa muda mfupi,nifikishie salamu hizi”. 

  “Tunashukuru sana kwa kutusikiliza Wana Tinde,Jukumu langu kama Kiongozi ni kubeba kero zenu na kuhakikisha nawasemea na kuzitatua ninaamini lile goti mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa nikazisemea shule zenye msongamano mkubwa wa wanafunzi,Mwezi Julai 2018 alipopita Tinde lilikuwa linatoka ndani ya moyo wangu na ndiyo maana tumepata majibu haraka iwezekanavyo mwezi Januari mwaka huu”,aliongeza. 

  Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko alisema “Ni wajibu wetu sasa kuhakisha kwamba,hizi pesa tulizopewa kwa ajili ya madarasa mawili na vyoo sita kwa kila shule,tuhakikishe hatuishii madarasa mawili pekee bali tujenge madarasa matatu,tuhakikishe tunaweka nguvu kazi zetu ikiwemo sisi wenyewe kuchimba misingi”. 

  Hata hivyo wananchi walisema wapo tayari kuchangia nguvu kazi zao kwenye ujenzi wa madarasa na vyoo vya shule na ili kuonesha utayari walianzisha harambee kwenye mkutano ambapo shilingi 140,500 zilipatikana papo hapo,ahadi ya tripu 21 za mchanga, maji tripu 10 pamoja na mifuko 9 ya saruji.
  Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kata ya Tinde na kuwahamasisha wananchi kushiriki katika shughuli za maendeo - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
  Wakazi wa Tinde wakimsikiliza mbunge wao Azza Hilal.  Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akizungumza na wakazi wa Tinde.  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko akizungumza na wakazi wa Tinde.
  Wakazi wa Tinde wakiwa kwenye mkutano.
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko akiwasisitiza wananchi kushiriki kwenye shughuli za maendeleo.
  Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akielezea kuhusu mchango wake wa mabati 23 kwa ajili ya ujenzi wa vyoo katika shule za msingi Tinde A na Tinde B.
  Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akikabidhi mabati 23 kwa ajili ya ujenzi wa vyoo katika shule za msingi Tinde A na Tinde B.
  Mwananchi akitoa mchango wake wakati wa harambee iliyoanzishwa na wananchi kuchangia ujenzi wa vyoo vya shule na madarasa katika shule za Tinde A na B.
  Mwenyekiti wa kijiji cha Jomu George Masele akionesha eneo ambapo panajengwa vyoo katika shule ya msingi Tinde B.
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko akizungumza wakati akikagua maeneo ya ujenzi wa madarasa katika shule za msingi Tinde A na Tinde  B. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

  0 0


  Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Dodoma na mjumbe wa bodi ya TAPANET Mh Fatuma Toufiq aikichangia hoja , katika mkutano wa mwanzo wa mwaka unaowakutanisha washiriki kutoka katika mikoa yote ya Tanzania bara na Zanzibar kwa lengo la kutadhimini mafanikio ya mradi changamoto na mikakati ya kutoa msaada wa huduma za kisheria baada ya 2020
  Meneja uwezeshaji (capacity development ) wa LSF, Bwn Bryceson Munuo akiongea na wakuu wa bodi na mashirika yanayotoa huduma za msaada wa kisheria yanayofadhiliwa na LSF, katika mkutano wa mwanzo wa mwaka unaowakutanisha washiriki kutoka katika mikoa yote ya Tanzania bara na Zanzibar kwa lengo la kutadhimini mafanikio ya mradi changamoto na mikakati ya kutoa msaada wa huduma za kisheria baada ya 2020
  Ofisa Mkuu wa LSF , Kees Groenendijk akitoa cheti cha utendaji bora kwa mwakilishi wa kibondo Paralegal kutoka mkoa wa Kigoma bwana Japhet kufatia utendaji bora katika maeneo mbalimbali ya utekelezaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa mwaka 2018. Akishuhudia ni Meneja uwezeshaji (capacity development ) wa LSF, Bwn Bryceson Munuo
  Ofisa Mkuu wa LSF , Kees Groenendijk akitoa cheti cha utendaji bora kwa Mkurugenzi wa CCT Cotrida Ndezi Kwa niaba ya Paralegal kutoka mkoa wa Dodoma, Katuka Paralegal Organisation Chamwino, kufatia utendaji bora katika maeneo mbalimbali ya utekelezaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa mwaka 2018. Akishuhudia ni paralegal kutoka katuka Chamwino bi Shida Andrea Sasine Meneja uwezeshaji (capacity development ) wa LSF, Bwn Bryceson Munuo.


  ************************

  Wakuu wa Mashirika yanayojishughulisha na utoaji wa msaada wa kisheria wanakutana Dodoma kujadili mbinu stahiki za kupanua wigo wa utoaji wa huduma za kisheria nchini---lengo kuu likiwa ni kuwakwamua watanzania maskini kutoka katika matatizo mbalimbali ya kisheria na kuwasaidia kupata haki zao.

  Kongamano hili inawakutanisha pamoja wakurugenzi na wajumbe wa bodi kutoka katika mashirika ya msaada wa kisheria yanayotekeleza miradi ya huduma za kisheria maeneo mbalimbali nchini chini ya ufadhili wa Shirika la Legal Services Facility (LSF).

  “Mkutano huu unatoa fursa kwa wadau wa utoaji wa huduma za kisheria, hasa wale wanafadhliwa na LSF, kujadili mafanikio, changamoto mbalimbali na njia bora za katika utoaji wa huduma za kisheria na namna na kufikisha huduma za kisheria kwa watanzania wengi wahitaji, hasa waishio vijijini,” kwa mwaka 2018 tumeweza kufikia watu zaidi ya million 3 kulinganisha na mwaka 2017 ambapo watu milioni 1 na laki 4 walifikiwa katika kupata elimu ya sheria. 

  Na kwa upande wa msaada wa kisheria mwaka 2018 tumefikia idadi ya watu 76,000 kulinganisha na mwaka 2017 ambapo 65000 walifikiwa, ni wazi kabisa kumekuwa na ongezeko katika kuwafikia na kubadili mtazamo,maisha ya wananchi kwa kuwawezesha kupata stahiki zao kwa maendeleo bora ya kijamii na kiuchumi kila mwaka amesema Meneja Mradi wa LSF-Ramadhan Maselle, wakati wa ufunguzi Mkutano huu.

  Lengo kuu la Kangamano, kwa mujibu wa Maselle, ni kuhakikisha huduma za kisheria na wasaidizi wa kisheria zinawafikia watanzania wengi wenye matatizo ya kisheria, mpaka chini kabisa katika ngazi za vijiji.

  Washiriki wa mkutano pia watapata nafasi kujadili kwa mapana na marefu mrradi wa LSF, mbinu za kufanya miradi/shughuli inayotekelezwa na vituo vya msaada wa kisheria, mashirika na wadau mbalimbali chini ya ufadhili wa LSF, iwe enderevu.

  “Uenderevu wa miradi ni jambo la msingi sana, ndo maana kauli mbiu ya Kangamano hili la 2019 ni ‘LSF Grantees beyond 2020; Strengths and Challenges—maana yake Mashirika yanayofadhiliwa na LSF baada ya 2020; Uwezo na Changamoto. Kauli mbiu hii inatatoa fursa kwa LSF, mashirika yanayofadhiliwa na LSF na wadau wengine, kujadili mbinu mbadala za kuhakikisha shughuli na miradi ya usaidizi wa kisheria na utoaji wa huduma za kisheria, inakuwa enderevu hata kama ufadhili wa LSF hautakuwepo,” kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na LSF.

  “Mijadala na mikakati utokanayo na Mkutano huu yataisaidia LSF, mashirika yanayofadhiliwa na LSF na wadau wengine kupata uelewa mpana kuhusu mbinu mbadala zitakazosaidia kupata fedha na raslimali fedha kutoka katika vyanzo mbalimbali mbadala kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya usaidizi wa kisheria na hatimae kuwakwamua watanzania maskini kutoka katika matatizo mbalimbaili ya kisheria yanayowakabili,” alisisitiza Masele

  Aidha katika Kangamano LSF itatoa vyeti vya utendaji bora kwa vituo 8 vya watoa huduma za msaada wa kisheria ambao wamefanya vizuri katika mwaka 2018. Vitu hivyo ni pamoja na Kibondo Kigoma , Makete Njombe, katuka Dodoma, toje tanga, kyela Mbeya, ukerewe Mwanza, Serengeti mara na Micheweni Zanzibar

  Mkutano huu unatarajia kuudhuriwa na washiriki wapatao 106, ikiwa ni pamoja na viongozi wa mashirika yanayofadhiliwa na LSF, wajumbe wa bodi wa mashirika husika, viongozi wa serikali kutoka katika wizara mbalilimbali--TAMISEMI, Wizara ya Sheria na Katiba, Wizara ya Afya, Wizara ya Ardhi, na waandishi wa habari.

  0 0
 • 02/22/19--11:28: USHINDI LAZIMA-NAMUNGO
 • JOSEPH MPANGALA, RUANGWA/LINDI

  Kocha wa Timu ya namungo FCBakari malima kutoka wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi amejigamba kuondoka na Uchindi dhidi ya Timu ya yanga SC ya Jijini Dar es salaam katika Kombe la Shirikisho la Azam ASFC.

  Timu ya Namungo ambayo inaongoza katika msimamo wa ligi daraja la kwanza inatarajia kucheza na Yanga siku ya jumapili wiki hii wakiwa katika mwendelezo wa kusaka tiketi ya kwenda robo fainali.

  Bakari malima anasema anaifaham Timu ya yanga Vizuri hivyo anauhakika wa kupata ushindi akiwa katika kiwanja cha nyumbani.

  “Mimi Yanga nawafaham Nje ndani sidhani kama watapata mteremko kama wanaotarajia na uhakikia kwa kuwa gem yenyewe tunachezea hapa nyumbani tunauwezo wa kufanya Vizuri”amesema kocha Malima.

  Licha ya kujiandaaa vizuri timu hiyo inamajeruhi wanne wa kikosi cha kwanza ambapo kocha tayari ameanza kuandaa vijana wengine ili kuweza kuziba pengo la wachezaji hao.

  ‘’tatizo lililopo kwenye timu yangu sasa hivi kunamajeruhi kama wanne wa kikosi cha kwanza na niwachezaji tunaowategemea lakini tayari kuna vijana tunawanadaa kuchukua nafasi”

  Hata hivyo Malima amewaomba mashabiki wa mikoa ya kusini kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu ya namungo kama moja ya Timu inayowakilisha Mikoa ya Kusini.

  Tayari kikosi cha Timu ya Yanga SC kinachojumuisha wachezaji 20 kimeondoka jijini Dares salaam Ijumaa asubuhi ya kuelekea wilaya ya Ruangwa Mkaoni Lindi tayari kucheza na timu ya Namungo.

  0 0

  Mtaalam wa Tiba Radiolojia (Interventional Radiology) wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Erick Mbuguje (kulia) akitoa usaha kwenye jibu lililopo ndani ya ini la mgonjwa, huku akiongozwa na Dkt. Troy Koch kutoka Chuo Kikuu cha Utah nchini Marekani. Wengine ni wataalam wa tiba radiolojia wakishiriki kwenye huduma hiyo
  Wataalam wa tiba radiolojia wakiendelea kutoa tiba kwa mgonjwa mwenye usaha kwenye jibu lilipo ndani ya ini la mgonjwa huyo.
  Mkuu wa Idara ya Radiolojia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Flora Lwakatare akizungumza na waandishi wa habari kuhusu huduma ya kibingwa ya tiba radiolojia (interventional radiology) inayofanyika katika hospitali hiyo. Kushoto ni Daktari Bingwa wa Radiolojia, Dkt. Frank Minja kutoka Chuo Kikuu cha Yale nchini Marekani.
  Kutoka kushoto ni Daktari Bingwa wa Radiolojia, Dkt. Troy Koch kutoka Chuo Kikuu cha Utah nchini Marekani akiwa na wataalam wenzake kwenye mkutano huo leo.
  Daktari Bingwa wa Radiolojia, Dkt. Frank Minja kutoka Chuo Kikuu cha Yale nchini Marekani akiwaeleza waandishi wa habari jinsi vyuo vikuu vya Yale, Indiana, Utah na Emory nchini Marekani vinavyoshiriki kutoa mafunzo na huduma ya kibingwa ya tiba radiolojia kwa wataalam wa Muhimbili.Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)


  Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imesema kwamba asilimia 99 ya wagonjwa wenye vivimbe vya kinywa (dental ehemngiomas) hivi sasa wanapatiwa huduma ya kibingwa ya tiba radiolojia (interventional radiology) badala ya kupelekwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu zaidi. A


  Awali, wagonjwa wenye matatizo ya vivimbe vya kinywa walikuwa wanapewa rufaa ya kwenda kutibiwa nchini India, lakini hivi sasa wanatibiwa Muhimbili baada ya huduma hiyo kuanza kutolewa katika hospitali hiyo.Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mkuu wa Idara ya Radiolojia, Dkt. Flora Lwakatare wa hospitali hiyo amesema wagonjwa ambao tayari wamepatiwa huduma hiyo wamekuwa wakipata matokeo mazuri katika tiba zao.

  Dkt. Lwakatare amesema kuwa tiba hiyo inafanywa na wataalam wa Muhimbili akiwamo Daktari Bingwa wa Radiolojia, Dkt. Gerald Mpemba na Fundi Sanifu wa Radiolojia, Fabian Maha kwa kushirikiana na wenzao kutoka vyuo vikuu vya Yale, Indiana na Emory nchini Marekani wakiongozwa na Dkt. Frank Minja na Dkt. Troy Koch ambaye anatoka Chuo Kikuu cha Utah, Marekani.

  “Tiba hii ni mwendelezo wa mafunzo yalioanza Novemba, mwaka jana. Huduma ambazo zimetolewa na zinazoendelea kutolewa ni utoaji wa sampuli kutoka kwenye vivimbe kutoka sehemu mbalimbali za mwili ambazo si rahisi kufikiwa bila kufanyika upasuaji mkubwa na kuzibua mirija ya nyongo (percutaneous biliary drainage),” amesema Dkt. Lwakatare.

  Amesema huduma nyingine ni kuvyonya vivimbe vyenye maji au usaha (percutaneous drainage) na kuweka mirija kwenye figo ambazo mirija ya mkojo imeziba (nephrostomy tube placement).

  Amesema tiba hiyo ina faida kubwa kwa kuwa inamuepusha mgonjwa kufanyiwa upasuaji mkubwa ambao ni hatarishi na kwamba mgonjwa anayepatiwa tiba radiolojia anaruhusiwa kurejea nyumbani siku hiyo hiyo na hivyo kupunguza gharama endapo angelazwa kwa ajili ya kuendelea na matibabu.

  “Tumeweza kuokoa fedha za kuwatibia wagonjwa waliokuwa wanapata huduma hizi nje ya nchi hasa wale wenye vivimbe vya kinywa. Kwa sasa wagonjwa hawa tunawatibu kwa Tshs. 2 milioni kila mmoja katika hatua nne ili kukamilisha tiba yake na mgonjwa huyo endapo angepelekwa kutibiwa nje ya nchi matibabu yake yangegharimu Tsh. 96 milioni kwa mgomjwa mmoja katika hatua zote nne,” amesema Dkt. Lwakatare.

  Pia, Dkt. Lwakatare aliwashukuru wataalam kutoka Marekani kwa kujitolea kuendesha mafunzo hayo pamoja na kuleta vifaa kwa ajili ya kutoa huduma hiyo.“Tunapenda kutoa shukrani zetu kwa serikali kwa uwekezaji mkubwa wa kununua vifaa tiba katika hospitali yetu jambo ambalo limewezesha kuimarisha huduma za kibingwa ikiwamo tiba radiolojia.

  Katika hatua nyingine, Dkt. Troy Koch ambaye anatokea Chuo Kikuu cha Utah nchini Marekani amewashukuru wataalam wa Muhimbili kwa ushirikiano waliouonyesha tangu walipofika kwa ajili ya kutoa huduma ya kibingwa ya tiba radiolojia.Tiba radiolojia ni tiba maalum ambayo inahusisha vifaa vya radiolojia kama vile X-ray, fluoroscopy, CT-scan na ultrasound kutibu moja kwa moja au kuchukua sampuli kwa ajili ya uchunguzi.Huduma hiyo ikijumuisha mafunzo ilianza ilianza Februari 4, mwaka huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila ambako kinamama wenye vivimbe kwenye matiti walitibiwa na kwamba mafunzo hayo pamoja na tiba yataendelea hadi Machi 9, mwaka huu.

  Tangu kuanzishwa kwa huduma hiyo Novemba, mwaka 2017, wagonjwa 220 wamepatiwa huduma ya kibingwa ya tiba radiolojia wengi wao wakiwa wagonjwa wenye vivimbe vya kinywa. Katika kambi hii, wagonjwa 50 wanatarajiwa kupatiwa huduma hiyo.

  0 0


   
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) akipokelewa na mwenyeji wake, Waziri wa Ulaya na Mambo ya Nje wa Ufaransa, Mhe. Jean- Yves Le Drian jijini Paris. Dkt. Mahiga yupo nchini Ufaransa kwa ziara ya siku mbili tarehe 21 na 22 Februari 2019. 
   
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) akiwa katika mazungumzo na mwenyeji wake, Waziri wa Ulaya na Mambo ya Nje wa Ufaransa, Mhe. Jean- Yves Le Drian .

  Tanzania na Ufaransa zimeahidi kuimarisha ushirikiano wa kimaendeleo; kuongeza uwekezaji na biashara; na kutafuta ufumbuzi wa migogoro inayozikabili nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu, Ukanda wa Bahari ya Hindi na changamoto nyingine za kiusalama katika maeneo hayo.

  Ahadi hiyo ilitolewa na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi hizo jijini Paris leo walipokutana kwa ajili ya mazungumzo. Mhe. Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki yupo nchini Ufaransa kwa ziara ya kikazi siku siku mbili 21 na 22 Februari 2019 kufuatia mwaliko wa Waziri wa Ulaya na Mambo ya Nje wa Ufaransa, Mhe. Jean- Yves Le Drian ambaye ameahidi pia kufanya ziara ya kikazi nchini Tanzania hivi karibuni.

  Kabla ya mazungumzo hayo, Mheshimiwa Balozi Mahiga alikutana na kufanya mazungumzo na kundi la Maseneta wa Ufaransa ambao ni marafiki wa Tanzania wakiongozwa na Seneta Ronan Dantec ambaye ni Mwenyekiti wa Maseneta hao. Maseneta hao walipendekeza kuanzishwa kwa ushirikiano dada kati ya jiji la Paris na Dodoma. Ushirikiano huo ujikite zaidi katika matumizi bora ya ardhi, mipango miji na kutekeleza miradi mbalimbali ya kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi.

  Vilevile, Maseneta hao wameelezea dhamira yao ya kutaka kushirikiana na Serikali ya Tanzania kuibua vipaji vya mchezo wa mpira wa miguu katika shule mbalimbali nchini.

  Wakati huo huo, Mhe. Mahiga alifanya mazungumzo na Bibi Marie Audouard, Naibu Mshauri wa Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa anayeshughulikia masuala ya Afrika. Katika mazungumzo yao, Bibi Audouard aliainisha maeneo ya kipaumbele ya Mhe. Rais Emmanuel Macron katika mahusiano yake na nchi za Afrika.

  Vipaumbele hivyo ni pamoja na kuimarisha zaidi mahusiano na nchi zinazoongea lugha ya kiingereza na kireno; kuendelea kushirikiana katika usuluhishi wa migogoro ya kikanda na kimataifa; kuhamasisha sekta binafsi ya Ufaransa kwenda kuwekeza Afrika; na kubadilishana uzoefu katika nyanja za utamaduni hasa kwa vijana.

  Viongozi wengine aliofanya nao mazungumzo Mhe. Waziri ni pamoja na Bibi Audrey Azoulay, Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO; na Bw. Bertrand Walckenaer, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD).

  Katika mazungumzo na Mkurugenzi wa UNESCO, Waziri Mahiga alilishukuru Shirika hilo kwa kuwa mshirika wa Tanzania kwa miaka mingi kwenye masuala ya elimu, sayansi na utamaduni na kuahidi kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana katika masuala mbalimbali yanayohusu elimu, sayansi na utamaduni.

  Kwa upande wa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa AFD, Mkurugenzi huyo alieleza kuwa, kutokana na ushirikiano mzuri uliopo wameongeza mara mbili kiwango cha fedha za maendeleo nchini Tanzania ambazo zitatumika kufadhili miradi katika sekta za uchukuzi, nishati, maji safi na taka, kilimo, afya na mabadiliko ya tabianchi.

  Mheshimiwa Waziri anahitimisha ziara yake leo kwa kukutana na Jumuiya ya Wawekezaji na wafanyabiashara wa Ufaransa (MEDEF) na Bi. Luise Mushikiwabo, Mtendaji Mkuu wa Jumuiya ya nchi zinazozungumza Kifaransa (IOF).


  Imetolewa na:
  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
  Dodoma.
  22 Februari 2019 

  0 0

  Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania Jaji Mstaafu Thomas Mihayo akitia saini kwenye karatasi ya makubaliano ya ushirikiano wa maandalizi ya maonesho ya ngumi ya kimataifa yatakayoambatana na Mkutano wa Wafanyabiashara na Watalii kutoka katika mataifa 75 Duniani utakaofanyika mwanzoni mwa mwezi Julai mwaka huu 2019,kushoto kwake ni Makamu wa Rais wa Kampuni ya Rejoy ya China inayoandaa mashindano hayo Bw. Andrew Lu 
  Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania Jaji Mstaafu Thomas Mihayo na Makamu wa Rais wa Kampuni ya kimataifa ya Rejoy ya nchini china wakionyesha karatasi za makubaliano ya ushirikiano wa maandalizi ya mchezo wa ngumi wa kimataifa utakaofanyika Jijini Arusha mapema mwezi Julai mwaka huu 


  Na Grace Semfuko-MAELEZO


  Bodi ya Utalii Tanzania TTB imetiliana saini mkataba wa ushirikiano na Taasisi ya Rejoy ya Beijing Nchini China ya maandalizi ya mikutano mikubwa ya siku mbili ya wafanyabiashara wa sekta mbalimbali wa nchi hizo wakati wa msimu wa maonesho ya kimataifa ya mchezo wa ngumi yanayotarajiwa kufanyika Jijini Arusha mwanzoni mwa mwezi Julai mwaka huu. 

  Mkataba huo unahusisha maandalizi ya mikutano ya washiriki wa maonesho hayo, ambapo wafanyabiashara na Watalii kutoka katika Nchi zaidi ya nchi 75 Duniani wanatarajiwa kushiriki maonesho hayo yatakayoambatana na kutembelea vivutio vya utalii pamoja na kubadilishana uzoefu wa kibiashara baina ya watu wa mataifa hayo.

  Akizungumza mara baada ya kutiliana saini makubaliano hayo, Mwenyekiti wa Bodi ya TTB Jaji Mstaafu Thomas Mihayo, alisema ni hatua muhimu kwa Tanzania ya kupokea ugeni huo ambao pamoja na kunufaisha Taifa kiuchumi lakini pia utatangaza Tanzania katika utalii.

  “Sisi Bodi ya Utalii Tanzania ni furaha yetu kuona tumefikia makubaliano haya ambayo yataleta tija kwa Taifa letu, Kampuni ya Rejoy ni ya kimataifa ambayo imepewa idhini ya kuandaa mchezo wa ngumi Duniani, ni kampuni kubwa, maarufu na yenye uzoefu wa kutosha katika mchezo huo, hivyo kuja kwao Tanzania ni hatua kubwa sana,pia Ukumbi wa mikutano Arusha AICC wanahusika katika makubaliano haya” alisema Jaji Mstaafu Thomas Mihayo Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB

  Makamu wa Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Rejoy, Bw. Andrew Lu, ambayo wemekuwepo nchinikwaa wiki sasa, alisema makubaliano hayo yanalenga kuwaweka karibu TTB na Kampuni yake na kwamba watahakikisha maandalizi ya mikutano na mchezo huo wa ngumi yatafanikiwa kwani wameweka hamasa kubwa kwenye nchi zilizoonyesha nia ya kushiriki.

  “Tunautangaza mchezo huo kwa hapa Tanzania, watu wengi watakuja kushiriki na kuuona, pia tunatangaza utalii wa Tanzania ili watu hao wakija waweze pia kutembelea hifadhi za utalii na vivutio vya Taifa la Tanzania, tuna uzoefu wa miaka 15 katika kazi hii na tutafanikiwa” alisema Andrew Lu Makamu wa Rais wa Kampuni ya kimataifa ya mchezo wa ngumi.

  Makubaliano hayo ambayo mchakato wake unaanza February 22 na kutarajiwa kukamilika machi mwishoni, utekelezaji wake utaanza mwezi April kwa maandalizi ya kupokea ugeni huo mkubwa huku mwezi julai mwanzoni Tanzania ikitarajiwa kupokea ugeni huo kutoka katika mataifa mbalimbali, zaidi ya 70 duniani.

  Katika tukio kubwa hilo la ngumi za uzito wote ambalo litarushwa mubashara nchi nying duniani litatizamwa na maelfu ya wahudhuriaji toka china na nchi mbalimbali wakiwaa ni watalii na wafanya baishara kama wasafirishaji na wahudumiaji katika sekta ya utalii lengo likiwa ni kutangaza sekta ya utalii duniani.

  0 0  Mh. Ester Bulaya ameendelea na ziara yake jimboni na siku ya Jana ameshiriki kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo inayofadhiriwa mfuko wa jimbo kwa mwaka wa fedha 2017/2018 na kuzungumza na wananchi pamoja na Wanafunzi.

  Mapema majira ya 5:00 asubuhi Mh. Mbunge alifika katika shule ya Msingi Kilimani kwaajili ya ukaguzi wa mradi wa Ujenzi wa Choo chenye jumla ya matundu 12 yaani me 6 na ke 6 ambapo mh. Mbunge kupitia fedha ya mfuko wa jimbo alichangia tsh milioni nne (4,000,000/=) ili kuwapunguzia wazazi michango ambayo ilionekana kuwa kero kwa wananchi wa maeneo ya Nyasura.

  Aidha mh. Mbunge baada ya kusomewa taarifa ya ujenzi wa choo husika kupitia mwl. mkuu wa shule akawiwa na usimamizi mzuri wa fedha husika na kuamua kutoa tsh 800,000/= fedha toka mfukoni kwaajili ya umaliziaji wa choo husika kwa kupaka langi na uwekaji wa milango ili choo hicho kianze kutumika kwa uharaka kwani nikweli kuwa wanafunzi wamekuwa wakipata adha kwa muda mrefu.

  Mh. Mbunge alitoa nafasi kwa wanafunzi kwaajili ya kutoa changamoto zinazowakabili ndipo alisimama mwanafunzi mmoja kwa niaba ya wanafunzi wenziwe na kutoa changamoto ya kutokuwa na mpira wa miguu ambapo mh. Mbunge akatoa tsh 50,000/= kwaajili ya ununuzi wa mpira na kuhaidi kuleta jezi kwa upande wa football na Netball ili wanafunzi wazitumie wakati wa michezo.

  Nae mwl. mkuu wa shule ya msingi Kilimani akishukru kwa niaba ya kamati ya shule alisema anashukru sana kwa ujio wa mh. Mbunge kukagua fedha zake zinatumikaje lakini pia anashukru kwa kukumbukwa tena kwa kupewa fedha awamu ya pili katika shule hiyo kwani mwaka wa fedha 2016/17 shule hiyo pia ilipewa fedha kwaajili ya uezekaji Darasa na 2017/18 ujenzi wa choo hivyo mh. Mbunge aendelee kuwaunga mkono tena na tena.

  Mh. Mbunge akiambatana na mh. Diwani wa kata ya Nyasura aliendelea na ziara ya kukagua ujenzi wa darasa katika Shule ya msingi Nyasura ambapo kupitia fedha ya Mfuko wa jimbo kwa mwaka wa fedha 2017/18 aliombwa kuchangia tsh 910,000/= kwaajili ya kumalizia upauaji wa Darasa husika na sasa Darasa limemalizika kwa hatua ya upauaji na linatumika kutokana na upungufu wa Madarasa uliopa shuleni hapo.

  Baadae jioni mh. Mbunge alielekea katika Kata ya Nyatwali ambapo alizungumza wananchi na kupokea kero za wananchi na hatimae kutoa mrejesho kwa wananchi juu ya shughuli mbali mbali za maendeleo katika Kata ya Nyatwali.

  Aidha wakati mh. Mbunge akipokea kero za wananchi ilizuka kero ya wananchi kuhamishwa ndipo mh. Mbunge akaamua kuwauliza kwa kauli moja kuwa anaomba ajue wanaotaka kulipwa na kuhamishwa wanyooshe mikono na wanaotaka kubaki pia, wananchi wote kwa pamoja walikubaliana kuwa hawako tayari kuhamishwa na kumuomba mh. Mbunge awasaidie kuwawakilisha ili wasihamishwe katika makazi yao waliyoyazoea.

  Mh. Mbunge Leo ataendelea na ziara katika kijiji cha Bukore, Tairo, Sazira na baadae kijiji cha bitaraguru kwa kuzungumza na wananchi na kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo inayofadhiriwa na fedha ya mfuko wa jimbo

  0 0


  Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (katikati), akifafanua jambo wakati alipofanya ziara katika Kiwanda cha Madawa cha Vista Pharma Ltd.
  Mhandisi Basem Khader kutoka Kampuni ya Petra Construction waonajenga Kiwanda cha Vista Pharma akitoa maelezo kwa waziri wa afya juu changamoto wanazokabiliana nazo wakati wa ujenzi wa kiwanda hicho.
  Moja ya majengo ya ofisi katika kiwanda cha Vista Pharma.
  Kiwanda cha Vista Pharm kikiwa katika hatua za awali za ujenzi wake.

  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kiwanda cha Madawa cha Vista Pharm, Churchil Katwaza, akisoma taarifa za kiwanda hicho kwa Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.
  Msafara wa Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, ukiwasiri katika eneo la uwekezaji la Kiwanda cha Madawa cha Kairuki Pharmaceutical Industrial Limited (KPIL).
  Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, akiangalia ramani ya ujenzi wa Kiwanda cha Kairuki Pharmaceutical Industrial Limited (KPIL).
  Msimamizi wa Kiwanda cha Madawa cha KPIL, kilichopo Kibaha mkoani Pwani, Dk. Muganyizi Kairuki, akitoa maelezo juu ya junzi wa kiwanda hicho kwa Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.
  Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akiwa katika ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Kiwanda cha Madawa cha Kairuki, kilichopo Kibaha mkoani Pwani.
  Waziri akipata maelezo ya ujenzi wa Kiwanda cha Madawa cha KPIL.
  Msimamizi wa Kiwanda cha Madawa cha Kairuki, kilichopo Kibaha mkoani Pwani, Dk. Muganyizi Kairuki, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (katikati), kutembelea na kuangalia maendeleo ya ujenzi wa viwanda vya dawa vya Kairuki Pharmaceutical Industrial Ltd (KPIL) na Vista Pharma Ltd.
  Kutembelea eneo la kiwanda.
  Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, akisaini kitabu cha wageni alipofika katika Kiwanda cha Madawa cha Kairuki Pharmaceutical Industrial Ltd.
  Msimamizi wa Kiwanda cha Madawa cha Kairuki Pharmaceutical Industrial Ltd (KPIL), Dk. Muganyizi Kairuki akitoa taarifa ya ujenzi wa kiwanda hicho kwa Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy, alipofanya ziara katika kiwanda hicho.
  Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Pwani akizungumza wakati akimkaribisha waziri wa afya kuzungumza.
  Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy, akitoa majumuhisho baada ya kutembelea viwanda vya kutengeneza madawa vya Kairuki Pharmaceutical Industrial Ltd na Vista Pharma mkoani Kibaha.
  Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy, akitoa majumuhisho baada ya kutembelea viwanda vya kutengeneza madawa vya Kairuki Pharmaceutical Industrial Ltd na Vista Pharma mkoani Kibaha.
  Mbunge wa Kibaha Mjini akitoa neno kwa wawekezaji wa viwanda vya madawa.
  Waziri Ummy akitoka katika moja ya majengo katika eneo la kiwanda cha Kairuki Pharmaceutical Industrial Ltd.
  Eneo la ujenzi wa kiwanda cha Kairuki Pharmaceutical Industrial Ltd.
  Waziri akiagana na Dk. Muganyizi Kairuki.
  Waziri Ummy akiagana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Vista Pharma.
  Waziri Ummy akitoka katika kiwanda cha Kairuki Pharmaceutical Industrial Ltd baada ya kumaliza ziara yake.
  Picha ya pamoja.


  Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akisaini kitabu cha wageni alipofika katika eneo linapojengwa Kiwanda cha Madawa cha Vista Pharma Ltd kilichopo Kibaha mkoani Pwani. (Picha na Francis Dande).
  Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, akisalimiana na mwekezaji wa Kiwanda cha Madawa cha Vista Pharma Ltd wakati wa ziara yake ya kuangalia maendeleo ya viwanda vya kutengeneza dawa mkoani Kibaha.


  WAZIRI wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amesema katika kila Sh. 100 ambayo Serikali inatumia kununua dawa nchini, Sh. 94 inapelekwa nje ya nchi kwa ajili ya ununuzi wa dawa hizo.

  Waziri Ummy alisema hayo jana wilayani Kibaha, Pwani wakati wa ziara yake ya kutembelea na kuangalia maendeleo ya ujenzi wa Viwanda vya dawa ambavyo ni Kampuni ya Kairuki Pharmaceutical Industrial Limited (KPIL) na Vista Pharma Ltd.

  Alisema fedha hiyo inayokwenda nje kwa ajili ya ununuzi wa dawa ni kubwa na ili kuikoa ni muhumu kwa wawekezaji kuendelea kuwekeza nchini hasa katika ujenzi wa viwanda vikiwemo vya dawa na vifaa tiba ambavyo ndivyo vinapewa kipaumbele na serikali.

  "Changamoto tunayopitia Serikali mbali na kwamba tunatumia fedha nyingi katika uagizaji wa dawa, bado dawa hizi zinachelewa kufika, Bohari ya Dawa (MSD) imekuwa ikiagiza dawa nje ya nchi na dawa hizo hukaa takribani zaidi ya miezi sita ndio zinaingia nchini, jambo hili ufanya upatikanaji wa dawa usiwe rahisi.

  “Hivyo tunaposema upo umuhimu wa ujenzi wa viwanda vya dawa tunamaanisha," alisema.Alisema ujenzi wa viwanda nchini utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza gharama za uagizaji wa dawa hizo nje ya nchi, gharama za upatikanaji wa dawa nchini kushuka na kuokoa fedha zinazonunulia dawa hizo.

  "Kati ya wadau 72 wa masuala ya afya nchini walioomba kujenga viwanda vya dawa hapa nchini, ni nane mpaka sasa ndio wameanza kujenga na kati ya hao sita viwanda vipo Kibaha.“Hii inaonyesha ni kwa namna gani viwanda hivi vikikamilika vitakavyozalisha dawa zenye ubora zaidi na kuhakikisha tunaokokoa fedha za nje tunazozitumia katika kununua dawa," alisema na kuongeza "Kwa mwaka huu wa fedha serikali imetenga Sh. Bilioni 270 katika wizara yangu kutoka Sh. Bilioni 30, hivyo fedha za kununua dawa zipo wawekezaji wakazane wamalize haraka viwanda hivyo ili fedha hizi zibaki hapa nchini, " alisema.

  Hata hivyo, alisema serikali itahakikisha inatengenza mazingira mazuri ya kurahisisha ujenzi wa viwanda unaenda sambamba na uimarishaji wa miundombinu ya umeme, maji na barabara. Kwa Upande wake, Msimamizi wa Kiwanda cha Kairuki, Dk.Mganyizi Kairuki, alisema kiwanda chao kinatarajia kuanza uzalishaji wa dawa za maumivu na nyingine aina 10 ambazo ni za maji ifikapo mwakani.

  Alisema mbali na uzalishaji wa dawa, kiwanda hicho pindi kitakapokamilika kinatarajia kutoa ajira za moja kwa moja 200 na zisizo za moja kwa moja 1,000."Zaidi ya Sh. Bilioni 38 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa kiwanda hiki fedha ambazo ni mikopo kutoka benki, hivyo tunazidi kuziomba baadhi ya benki kukopesha maana suala hili limekuwa ni changamoto," alisema.

  Naye Mwenyekiti wa Kampuni ya Bandari Pharmacy inayojenga kiwanda cha Vista Pharmacy, Churchill Katwaza, alisema kiwanda chao kinatarajia kuzalisha dawa sita ikiwemo ya kutuliza maumivu ya tumbo, kuongeza damu kwa wajawazito pamoja na inayotibu ushambulizi wa vidudu vya bakteria mwilini.

  "Tutazalisha jumla ya vidonge milioni 702 kwa mwaka na takribani chupa milioni 32 za dawa ya maji zenye ujazo wa milimita 100,"alisema Katwaza.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpa mkono wa pole  JR Hamisi Kigwangalla kufuatia kifo cha mdogo wake Zul, kulia ni Baba wa Marehemu Zul, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt Hamisi Kigwangalla muda mfupi kabla ya mazishi yaliofanyika Puge wilayani Nzega mkoa wa Tabora. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpa mkono wa pole Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt Hamisi Kigwangalla kufuatia kifo cha mtoto wake mdogo wa kiume Zul muda mfupi kabla ya mazishi Puge wilayani Nzega mkoa wa Tabora. 
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini Mhe. Hussein Bashe mara baada ya kuweka jiwe la msingi la uzinduzi wa kiwanda cha kuchakata gesi, kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Aggrey Mwanri (kulia)Makamu wa Rais yupo kwenye ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Tabora. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Naibu Waziri TAMISEMI Mhe. Mwita Waitara,  Mbunge wa Igalula Mhe. Mussa Ntimizi (kulia) na Mkuu Mkoa wa Tabora Mhe. Aggrey Mwanri, Mkuu wa Wilaya ya Uyui Bi. Gift Msuya (kushoto) mara baada ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa kituo cha Afya Igalula, wilayani Uyui mkoa wa Tabora. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).


  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo akijibu akizungumza na waraghabishi kutoka mikoa mbalimbali katika mkutano wa Digitali kwa maendeleo ulioandaliwa na Shirika la OxfamTanzani na kufanyika Katika ukumbi wa  African Dreams Jijini Dodoma
  Naibu waziri wa Elimu William  Olenasha akizungumza katika mkutano wa Waraghabishi wa Digitali kwa Maendeleo ulioandaliwa na Shirika la. OXFAM Tanzani Jijini Dodoma
  Naibu Waziri wa Elimu  Sayansi na Teknolojia na Mbunge wa Ngorongoro William Olenasha akipita taarifa kupitia simu yake ya mkononi katika mkutano wa Digitali kwa Maendeleo ulioandaliwa na Shirika la Oxfam Jijini Dodoma
  Sabore Ngarusi Kutoka wilayani Ngorongoro akiuliza swali kwa Katibu Mkuu wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo kwamba wizara hiyo imejipangaje kuondoa taizo la maji wilayani humo.
   Mbunge wa Viti maalum Dodoma Mhe. Fatuma Tawfiq akifuatilia mjadala  katika mkutano huo wa Digitali kwa Maendeleo Jijini Dodoma
   Mbunge wa Mbogwe mkoa wa Geita  Mhe. Maselle akifuatilia mjadala kwa makini
   Mbunge wa Mtwara vijijini Mhe. Hawa Ghasia akichangia mjadala katika Mkutano wa Digitali kwa Maendeleo ulioandaliwa na Shirika la Oxfam Nchini Jijini Dodoma
   Mbunge wa Viti maalum Dodoma Mhe. Fatuma Tawfiq akichangia mada katika mkutano huo wa Digitali kwa Maendeleo Jijini Dodoma
   Katibu mkuu Wizara ya maji Profesa Kitila Mkumbo akifuatilia mjadala Digitali kwa Maendeleo kwa makini Jijini Dodoma
  Jimmy Luhende Kutoka Shirika la ADLG. akichangia mada katika mkutano wa waraghabishi wa Digital Kwa maendeleo ulioandaliwa na Shirika la Oxfam Tanzania. 
  Naibu Waziri wa Elimu Williwm Olenasha akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi kutoka katika Shirika la Oxfam Tanzania
  Naibu waziri wa Elimu Willium Tate Ollenasha akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali na Waandishi wa habari za mtandaoni Jijini Dodoma katika Mkutano wawaraghabishi Digitali kwa maendeleo

  Na. Vero Ignatus, Dodoma

  Zaidi ya 30% ya miradi ya maji iliyokamilika vijijini haifanyi kazi kwasababu imekabidhiwa kwa jamii kwani ni tofailuti na ile ya mijini ambayo inakabidhiwa kwa Wahandisi au kwa wataalamu wa maji

  Hayo yamesemwa na Katibu mkuu Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo alipokuwa katika mkutano wa waraghabishi Digitali kwa maendeleo Jijini Dodoma ulioandaliwa na Shirika la Oxfam Nchini ambapo amesema miradi hiyo inapokabidhiwa kwa wananchi haina uangalizi wa kutosha

  Profesa Mkumbo amesema Kituo kimoja Cha maji kinapaswa kuhudumia watu 250 hadi kufikia January 2019 tayari wameshajenga  vituo 130,000 vijijini na vinavyofanya kazi,83,000 takribani wananchi 60 mpaka 65 wanapata maji.

  Amesema kuwa Madhumuni ya Sheria Mpya ya Rasilimali za Maji Na. 11/2009 ni kuhakikisha kuwa Rasilimali za Maji hapa nchini zinatunzwa, zinatumiwa, zinaendelezwa, zinaboreshwa, zinasimamiwa na kudhibitiwa kwa kuzingatia kanuni

  Amesema kuwa Sheria mpya ya Maji iliyo pitishwa inagusia vipengele viwili uanzishwaji wa wakala wa maji vijijini adhabu kwa watu wanao haribu miundombinu ya maji

  Amezitaja Wilaya ya Ngorongoro iliyopo mkoani Arusha  kuwa ni  mojawapo  yenye changamoto kubwa ya kufikiwa kutokana na Jiografia yake ila hadi sasa (Mb)Mh.William Ollenasha Ameshafanya usanifu vijiji 8 vitanufaika na mradi  wa maji

  Akijibu swali lililoulizwa na mmoja wa Waraghabishi kuhisiana na  uondoshwaji wa bei za maji Profesa Mkumbo amesema Mchakato wa kupandisha bei ya maji ni shiriki, linaanza na mamlaka ya maji na mara nyingi upandaji wa bei ya maji inategemeana na gharama za uendeshwaji wa mamlaka za maji

  Vilevile ameainisha Takwimu za upatikanaji wa maji kwamba zinazipata kwa aina mbili ambazo ni Miundombinu ya maji ilivyo sambazwa, Kutumia water system kwenye mtandao wa EWURA ambapo Tafiti yake hufanyika kwa kuwapigia wananchi na kuwauliza maswali

  '' Kwa mujibu wa Takwimu za mwaka 2017 za NBS zinaonesha 66% ya wananchi wa Tanzania wanapata maji'' Alisema Mkumbo

  Kwa upande wake Naibu waziri wa Elimu Sayansi na Yeknolojia na mbunge wa Ngorongoro Willium Olenasha amelishukuru Shirika la Oxfam kwa kutoa mafunzo kwa wananchi namna ya kutumia nyenzo za digitali ili kuleta maendeleo kwa jamii inayowazunguka.

  Naibu Waziri wa wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Olenasha amesema kuwa Serikali ipo pamoja na Oxfam pamoja na Waraghabishi katika kuhakikisha kwamba changamoto zinazoibuliwa na wananchi zinatatuliwa na viongozi husika kwa haraka na kwa wakati.

  Ameongeza kuwa Nchi nyingi zimesonga mbele kwa kasi kwa sababu ya kutumia teknolojia ya dijitali hivyo Oxfam imekua ikishirikiana na serikali katika shughuli za maendeleo ikiwemo mradi huo wa Dijitali Kwa Maendeleo

  Wakishukuru Shirika la Oxfam kwa mafunzo ya kutumia nyenzo za Digitali kwa maendeleo Lucy Samweli, Diwani viti Maalumu Kata ya Nyasato Geita amesema Kwa kutumia mitandao ya kijamii amepata ushauri kutoka kwa watu mbalimbali wanaosoma anachokituma katika mitandao hiyo na hivyo kuboresha utendaji kazi yake

  Na Bi Royce Jumanne, Mraghabishi kutoka Kigoma amesema kuwa  Kupitia simu zao za mkononi waraghabishi wamefanikiwa kuhamasisha jamii kuchangia madawati ili kuwezesha wanafunzi kusoma katika mazingira mazuri.


older | 1 | .... | 1806 | 1807 | (Page 1808) | 1809 | 1810 | .... | 1898 | newer