Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1802 | 1803 | (Page 1804) | 1805 | 1806 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Wafanyakazi wa kiwanda cha Global Packaging (T) Ltd cha Kibaha mkoani Pwani wakiendelea na kazi ya kuzalisha vifungashio vya aina mbalimbali. Kiwanda hicho kinazalisha tani 150 za vifungashio kwa mwezi na kutoa ajira kwa mamia ya watanzania na pia kuondoa changamoto ya upatikanaji wa vifungashio hapa nchini.

  Mitambo ya wa kiwanda cha Global Packaging (T) Ltd cha Kibaha mkoani Pwani kama inavyoonekana katika picha, hiki ni moja ya kiwanda kinachozalisha vifungashio hapa nchini ikiwa ni matokeo ya dhana ya ujenzi wa uchumi wa viwanda inayosisistizwa na Serikali ya Awamu ya Tano.
  Wafanyakazi wa kiwanda cha Global Packaging (T) Ltd cha Kibaha mkoani Pwani wakiendelea na kazi ya uzalishaji vifungashio kwa kutumia mitambo ya kisasa. Kiwanda hicho kinazalisha tani 150 za vifungashio kwa mwezi na kutoa ajira kwa mamia ya watanzania na pia kuondoa changamoto ya upatikanaji wa vifungashio hapa nchini.


  Sehemu ya mitambo ya kuzalisha vifungashio katika Kiwanda cha Global Packaging (T) Ltd cha Kibaha mkoani Pwani.
  (Picha zote na MAELEZO)

  Na Lilian Lundo – MAELEZO


  Kiwanda cha Global Packaging (T) Limited kilichopo Halmashauri ya Mji wa Kibaha, Mkoa wa Pwani kimepunguza kwa kiasi kikubwa uagizaji wa vifungashio nje ya nchi.

  Hayo yameelezwa mapema wiki hii na Meneja Mradi wa kiwanda hicho, Hatibu Njuwila wakati wa mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii.“Kiwanda kilianza uzalishaji Januari, 2017 na kuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli , kinazalisha tani 150 za mifuko au vifungashio kwa mwezi,” amesema Njuwila.

  Ameendelea kusema, wateja wakubwa wa kiwanda hicho ni wakulima wanaozalisha bidhaa za nafaka kama vile mahindi, mtama na mchele, bidhaa zinazotokana na madini na mazao mengine yanayohitaji vifungashio.Amesema, lengo la uanzishwaji wa kiwanda hicho ni kupunguza uagizaji wa vifungashio nje ya nchi kutokana na kuwepo na uigizaji mkubwa wa vifungashio kutoka nje ya nchi kwa gharama kubwa.

  Aidha amesema, mafanikio waliyoyapata katika kipindi cha miaka miwili tangu kuanza kwa uzalishaji wa kiwanda hicho ni pamoja na kuajili wafanyakazi 98 ambao wote ni Watanzania, ambapo kwa asilimia kubwa ni kutoka Halmashauri ya Kibaha.Mafanikio mengine ni kupunguza kwa kiasi kikubwa uagizaji wa vifungashio kutoka nje ya nchi, kulipa kodi mbalimbali za Serikali Kuu pamoja na Halmashauri ambapo imeongezea Serikali mapato.

  Matarajio ya kiwanda hicho ni kuzalisha vifungashio vyenye ubora na ambavyo vinakidhi mahitaji ya wateja ambayo itaongeza thamani ya mazao na uhifadhi na kupata masoko ya uhakika ndani na nje ya nchi.Global Packaging (T) Limited imejipanga vyema kutekeleza sera ya Serikali ya viwanda kwanza kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025, inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

  0 0


  Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa akisalimiana na Viongozi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa mara baada ya kuwasili ofisini hapo katika ziara yake ya kukagua utekelezaji wa masuala ya watu wenye Ulemavu Mkoa wa Dodoma.
  Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa (kushoto) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma.
  Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa akipitia kwa makini taarifa ya utekelezaji wa masuala ya watu wenye ulemavu ya Mkoa wa Dodoma. (Kushoto) ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Bi. Germana Orota.
  Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Bilinith Mahenge akimweleza jambo Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa (Kushoto) jinsi Mkoa wa Dodoma umekuwa ukitekeleza na kuhudumia watu wenye ulemavu.
  Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa akizungumza na viongozi wa Mkoa na Vyama vya Watu wenye Ulemavu wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa masuala ya watu wenye ulemavu katika Mkoa wa Dodoma. (Kushoto) ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Dodoma Mjini Bw. Edward Mpogolo (Kulia) ni Afisa Ustawi wa Jamii, Bi. Felisiana Mboya
  Mkalimani wa lugha za alama Bw. Adrian Chiyenje (aliyesimama) akumfafanulia Mwenyekiti Chama cha Viziwi Mkoa wa Dodoma, Bw. Mazengo Kusentha (wenye uziwi) maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu), Mhe. Stella Ikupa (hayupo pichani).
  Afisa Ustawi wa Jamii Jiji la Dodoma, Bi. Rebeka Ndaki akieleza utekelezaji wa shughuli za watu wenye ulemavu kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa (hayupo pichani).
  Katibu wa SHIVYAWATA Mkoa wa Dodoma, Bw. Justus Ng’wantalima akiwasilisha taarifa ya Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia (Watu wenye Ulemavu), Mhe. Stella Ikupa (hayupo pichani) walipokutana kwenye ukumbi mpya wa Ofisi za Jiji la Dodoma.

  Katibu Chama cha Watu Wenye Ualbino Dodoma, Bw. Hudson Seme akichangia mada kuhusu masuala ya Watu wenye Ualbino wakati wa mkutano na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa (hayupo pichani).


  Baadhi ya washiriki wakisikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu), Mhe. Stella Ikupa (hayupo pichani) wakati wa ziara yake alipokuwa akikagua utekelezaji wa masuala ya watu wenye Ulemavu.
  PICHA ZOTE NA OFISI NA OFISI YA WAZIRI MKUU
  (KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)


  Na; OWM (KVAU) – Dodoma

  Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa ameviasa Vyama vya Watu wenye Ulemavu nchini kuhakikisha wanashirikiana na Serikali katika kuendeleza ustawi wa Watu wenye Ulemavu.

  Naibu Waziri Ikupa ameyasema hayo alipofanya ziara Mkoani Dodoma kukagua utekelezaji wa masuala ya Watu wenye Ulemavu ndani ya mkoa huo, ambapo alikutana na viongozi Mkoa na Vyama vya Watu wenye Ulemavu.

  Mhe. Ikupa alieleza kuwa ushirikiano baina ya Serikali na vyama vya watu wenye ulemavu ni muhimu katika kuhakisha haki na masilahi ya watu wenye ulemavu yanalidwa kwa kuzingatia Sera, Sheria na Miongozo mbalimbali.

  “Serikali imeendelea kuchukua hatua na kutekeleza jukumu lake la kuhamasisha na kuwalinda watu wenye ulemavu nchini kwa kuhakikisha haki za kundi hilo maalumu zinatekelezwa,” alisema Ikupa .Aidha, alisisitiza uongozi wa Mkoa kuhakikisha unahusisha mahitaji maalumu ya wenye ulemavu katika bajeti wanazozitenga, kutoa elimu na taarifa juu ya upatikanaji wa dawa, mafuta ya watu wenye ualbino na vifaa saidizi, na uundwaji wa kamati za kuhudumia wenye ulemavu.

  Aliongezea kuwa, ni vyema Maafisa Maendeleo ya Jamii pamoja na maafisa ustawi wa jamii wakahakikisha wanawasaidia watu wenye ulemavu wanapokabiliana na changamoto kwenye uandikaji wa maandiko ya kuomba mikopo. “Unakuta kikundi cha watu wenye ulemavu wanakuwa wabunifu na wanawazo zuri la kuanzisha mradi au biashara lakini wanakumbana na changamoto ya kuaandaa andiko la miradi yao na hivyo kuwafanya wakate tamaa mapema,” alisema Ikupa

  Pia, aliwasii Maafisa Ustawi wa Jamii kuwa na takwimu sahihi za idadi ya watu wenye ulemavu na kuendelea kuweka mifumo mizuri ya kutunza taarifa hizo. Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Bw. Edward Mpogolo aliunga mkono na kuyapokea maelekezo yote ya Naibu Waziri na kumhakikishia kuwa Mkoa wa Dodoma utakuwa mstari wa mbele katika kutekeleza maagizo aliyoyatoa.

  “Tutafanya kazi kwa ushirikiano mzuri na Vyama vya Watu wenye Ulemavu ili kuangalia namna bora ya kuwahudumia kwa kuzingatia mahitaji yao,” alisema Mpogolo. Naye Katibu wa SHIVYAWATA Mkoa wa Dodoma, Bw. Justus Ng’wantalima alimpongeza Naibu Waziri kwa jitihada ambazo amekuwa akizifanya katika kutetea Watu wenye Ulemavu.

  Katika ziara hiyo Naibu Waziri Ikupa, alitembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Chama cha Walemavu Sulungai kinachojishughulisha na ushonaji wa viatu vya wazi (kobasi) na utengenezaji wa majiko. Vilevile Mhe. Ikupa alitembelea shule ya Viziwi iliyopo Jijini Dodoma.

  0 0


  0 0

  NAIBU Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuuchunguza ujenzi wa kibanda cha kuhifadhia jenereta ya kuvuta maji katika mradi wa maji wa Ruaha Mbuyuni, wilayani Kilolo mkoani Iringa kinachodaiwa kujengwa kwa zaidi ya Sh Milioni 20.
  Mbunge wa jimbo la kilolo vennance Mwamoto akimuelezea Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso juu ya mradi huo wa maji unavyoleta changamoto kwa wananchi wa jimbo la kilolo
  Hichi ndio kibanda cha kuhifadhia jenereta ya kuvuta maji katika mradi wa maji wa Ruaha Mbuyuni, wilayani Kilolo mkoani Iringa kinachodaiwa kujengwa kwa zaidi ya Sh Milioni 20.  NA FREDY MGUNDA,IRINGA

  NAIBU Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuuchunguza ujenzi wa kibanda cha kuhifadhia jenereta ya kuvuta maji katika mradi wa maji wa Ruaha Mbuyuni, wilayani Kilolo mkoani Iringa kinachodaiwa kujengwa kwa zaidi ya Sh Milioni 20.

  Aliyasema hayo juzi katika ziara yake ya siku moja wilayani humo kukagua miradi mbalimbali ya maji, ikiwemo ile inayosuasua kwasababu mbalimbali.

  “Nimepata taarifa eti kibanda hiki kimejengwa kwa zaidi ya Sh Milioni 20,” alisema na kuuliza ukweli wa taarifa hizo kwa mhandisi wa maji wa halmashauri ya wilaya hiyo, Enock Basyagire aliyesema hakuwepo katika halmashauri hiyo wakati kikijengwa na kuomba akapitie nyaraka ili kujiridhisha. 

  Aliwahimiza Takukuru kulifuatilia jambo hilo kwa haraka na kama kutakuwa na kile alichoita “matumizi mabaya ya fedha za umma” wahusika wakamatwe na kufikishwa mbele ya mkono wa sheria. Wakati huo huo, waziri Aweso ameoneshwa kusikitishwa kwake kuona katika mradi huo, tenki kubwa la kuhifadhi maji limejengwa katika eneo lisilo na chanzo cha maji; ambalo kwa mujibu wa taarifa ya mhandisi wa halmashauri hiyo, gharama yake ni zaidi ya Sh Milioni 45. 

  “Huu ni uhuni, mmejenga tenki la Sh Milioni 45 na halijawahi kuwa na maji; mimi sio mtaalamu wa maji lakini najua, huwezi kujenga tenki katika eneo lisilo na chanzo cha uhakika cha maji, ni bora hapa mngechimba kisima kirefu huenda mngepata maji kwa ajili ya wananchi hawa wakati mkisubiri mradi mkubwa,” alisema. 

  Akitoa onyo kwa wahandisi wa maji kuacha kucheza na fedha za umma huku akiwataka wataalamu wa maji kutoka Bonde la Rufiji kufanya utafiti kujua eneo linaloweza kuwa na maji yatakayonusuru mradi huo ambao utekelezaji wake ulianza awamu ya nne ya Dk Jakaya Kikwete, Aweso alisema: 

  “Serikali haipo tayari kuona wataalamu wanaotakiwa kuwasaidia wananchi kupata maji, wanatengeneza mazingira ya kula fedha za umma. Alimuita mhandisi huyo mbele ya wananchi waliokuwepo wakati akikagua tenki hilo na kumtaka kuwaomba radhi kwa ujenzi huo ulioshindwa kuzingatia mambo ya kitaalamu; ombi lililopokelewa vizuri na wananchi hao. 

  Katika kukabiliana na changamoto za matumizi mabaya ya fedha za miradi ya maji inayosimamiwa na halmashauri, alisema Wizara imeamua kuanzisha Wakala wa Maji Vijijini hatua inayotarajiwa kusaidia kukomesha tabia hiyo. 

  Alisema wakala hiyo itakapoanza itasaidia kupunguza au kumaliza ulaji wa fedha za miradi ya maji na wahandisi wasio na nia njema katika kushughulikia kwa weledi changamoto za maji katika maeneo yao, wataondolewa na nafasi zao watapewa wengine. 

  Awali Mbunge wa Jimbo la Kilolo, Venance Mwamoto alimwambia naibu waziri huyo kwamba kata ya Ruaha Mbuyuni ni moja ya maeneo yenye changamoto ya muda mrefu ya upatikanaji wa maji safi na salama katika jimbo hilo. Mwamoto alisema ukosefu wa maji safi na salama katika kata hiyo umewaweka wananchi wake katika mazingira hatari ya kupata magonjwa ya mlipuko kikiwemo kipundupindu ambacho hutokea mara kwa mara. 

  “Leo umekuja mwenyewe, umejionea na umesikia kutoka kwa baadhi ya wananchi, naomba uwaondoe hofu wananchi hawa,” alisema huku naibu waziri akiahidi kuishughulikia changamoto hiyo kwa kasi kubwa. Mwenyekiti wa Kijiji cha Ruaha Mbuyuni, Adam Danando alisema sehemu kubwa ya wananchi wa kijiji na kata hiyo wamekuwa wakitegemea maji ya bonde la mto Lukosi yenye chumvi na bakteria ambao ni hatari kwa afya zao.

  0 0

  Mwenyekiti wa bodi ya wakaguzi akiwa amesimama na baadhi ya wajumbe wa bodi kujadili maendeleo mazuri ya ujenzi unaoendelea katika eneo hilo la lemuguru kata ya kisongo,nakupewa maelekezo na Mratibu wa mradi wa ujenzi Mhandisi Peter Kagady
  Mwenyekiti wa bodi ya wakaguzi nchini mhandisi Alexander kyaruzi(Alievaa miwani) akipewa muongozo wa ujenzi utakaoendelea katika eneo hilo la legumuru kata ya kisongo na mratibu wa mradi mhandisi peter kigadya( alievaa koti la langi ya chungwa) mbele ya wajumbe ya bodi
  Mwenyekiti wa bodi ya wakaguzi nchini Mhandisi alexander kyaruzi kati kati akikakagua moja ya mashimo yanguzo aliochimbwa kwaajili ya kusimamisha minara mikubwa ya umeme.
  Baadhi ya vijana wanaojishughurisha na ujenzi wa upandishwaji wa nguzo kubwa za umeme wilayani monduli , ikiwa ni moja ya mradi unaondelea katika njia za usambazaji wa umeme vijijini.
  Mwenyekiti wa bodi ya ukaguzi nchini Mhandisi Alexander Kyaruzi pamoja na wajumbe wa bodi ya ukaguzi wakijadilianana kupeana maelekezo pamoja na waratibu wa ujenzi wa kituo cha kupooza na kusambasa umeme lemuguru kata ya kisongo mkoani arusha.
  Eneo la ujenzi utakaofanyika wa kupooza na usambazaji umeme uliopo lemuguru kata ya kisongo mkoani arusha ambapo magari yanabeba udongo usiofaa kwa ujenzi na kuweka udongo unaofa kwa ujenzi
  Na. Vero Ignatus Arusha


  Mwenyekiti wa bodi ya Tanesco nchini Mhandishi Alexander Kyaruzi kwa kushirikiana na wajumbe wa bodi hiyo wamefanya ukaguzi katika kituo kikubwa cha kupoza na kusambaza umeme uliopo Lemguru Kata ya Kisongo mkoani Arusha

  Akizungumza wakati walipotembelea mradi huo Mhandisi Kyaruzi amesema lengo la ziara hiyo ni kujionea maendeleo, hali ya usimamizi ya miradi, ambapo hadi sasa vipo vituo viwili ambacho cha Lemguru wanaongeza kilovet 400 - 420 eneo lingine linaloboreshwa ni kutoka Iringa mpaka Shinyanga lenye msongo wa kilovet 400 

  Kwa mujibu wa Mhandisi Kyaruzi mradi huo mkubwa wa kupooza na kusambaza umeme unaunganisha nchi za Zambia, Kenya, Uganda na wenyeji Tanzania, ambapo utaweza kuleta uhakika wa umeme unatokea katika mikondo mbali mbali ya maji,kama vile Uganda unatumia mto ambao unasambaza umeme katika nchi nyingine za Africa ikiwemo Tanzania

  Aidha Mhandisi Alexander Kyaruzi amefurahishwa, na kuwapongeza wasimamizi wa mradi huo kwa juhudi zinazofanywa,katika kusimamia vyema pamoja na kuwapa vijana nafasi za ajira katika maeneo hayo huku akiwatakaa kuzidisha kasi ya uendeshaji wa mradi hadi kufikia mwaka 2020

  ‘‘Tulivyo kuja hapa kwanza tulifurahi pamoja na kwamba ni mwanzo na kwenye mwanzo mzuri unaoneka,lakini hapa tunaona wanaondoa kwanza udongo na kubadilisha udongo ambao haufai kwa ujenzi na kuweka udongo kwa ajili ya ujenzi ndipo waaanze ujenzi maana ujenzi huu wa mradi tumeweka mikakati mpaka mwaka ujao uwe umekamilika,na ukitoka hapa unaelekea Singida mpaka Namanga’’ Alisema

  Alisema mradi unategemea mpaka kufikia mwaka 2020 uwe umekamilika na mradi utaleta faida za umeme katika vijiji vyote nchini,na pia utaleta manufaa kwa vijana wasio na ajira na wanaokaa vijiweni kupata fursa za ajira

  Hata hivyo mratibu wa mradi wa njia za kusafirisha umeme wa msongo wa kilovet 400 Afrika ya Mashariki katika nchi za Zambia,Kenya,Uganda na Tanzania Mhandisi Peter Kigadya amesema mpaka sasa maendeleo ya mradi yamefikia pazuri na mradi umeunganishwa kutokea Kenya mpaka Arusha na kuelekea Singida.

  Amesema mradi mzima wa una sehemu kubwa tatu ujenzi wa njia za umeme na njia kuu za kupoozea umeme,pamoja na usafirishaji wa umeme katika vijiji,sehemu ya kwanza kwanza Iinatoka Singida mpaka babati,na sehemu ya pili ni babati mpaka arusha, na sehemu ya tatu arusha mpaka namanga na njia zote tatu zipo katika ujenzi na mpaka sasa njia hizo wameziwekea msingi.

  0 0

  Mwanafunzi kutoka Shule ya Kata Nkololo aliyefanya vizuri kwa kupata daraja la kwanza (pointi saba) na kushika nafasi ya kwanza kimkoa katika mtihani wa Taifa wa Kidato cha nne mwaka 2018 Ibrahimu Buyungumya(kushoto) na Mwanafunzi wa Kike Kwandu Maduhu kutoka Shule ya Sekondari Biashara aliyefanya vizuri kwa kupata daraja la kwanza (pointi 11) katika mtihani huo na kuongoza kimkoa (wasichana), wakionesha kadi zao za akaunti ambazo wamekabidhiwa (katika hafla maalum ya kuwapongeza iliyofanyika shule ya Sekondari Nkololo wilayani Bariadi Februari13, 2019 ) baada ya kufunguliwa akaunti na kuwekewa zawadi hizo.
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(katikati) akizungumza jambo na Mwanafunzi kutoka Shule ya Kata Nkololo aliyeongoza kimkoa katika mtihani wa Taifa wa Kidato cha nne mwaka 2018 kwa kupata daraja la kwanza(pointi saba) ,Ibrahimu Buyungumya(kushoto) na Mwanafunzi wa Kike Kwandu Maduhu kutoka Shule ya Sekondari Biashara aliyeongoza kwa upande wa wasichana kwa kupata daraja la kwanza (pointi 11) katika mtihani huo, baada ya hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri kimkoa, iliyofanyika katika shule ya sekondari Nkololo wilayani Bariadi Februari 13, 2019.
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(mwenye suti kulia) akishuhudia wanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Nkololo wilayani Bariadi wakifanya mazoezi kwa vitendo wakati wa hafla ya kuwapongeza walimu waliofanikisha na wanafunzi waliofanya vizuri katika Mtihani wa Kidato cha nne mwaka 2018 iliyofanyika kimkoa shuleni hapo, Februari 13, 2019.
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(kushoto) akiteta jambo na Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju, wakati wa hafla ya kuwapongeza walimu waliofanikisha na wanafunzi waliofanya vizuri katika Mtihani wa Kidato cha nne mwaka 2018 iliyofanyika kimkoa, katika shule ya sekondari Nkololo wilayani Bariadi Februari 13, 2019.
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(wa pili kushoto) akiwakabidhi zawadi ya ngao viongozi wa Halmashauri ya mji wa Bariadi ambayo iliongoza kimkoa na kushika nafasi ya tisa kati ya halmashauri zaidi ya 185 nchini katika mtihani wa Taifa wa Kidato cha nne mwaka 2018, (kushoto na wa pili kushoto) ni wanafunzi walifanya vizuri Kimkoa kutoka shule za Serikali), wakati wa hafla ya kuwapongeza walimu waliofanikisha na wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani huo iliyofanyika kimkoa katika shule ya sekondari Nkololo wilayani Bariadi Februari 13, 2019.
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (wa nne kushoto mbele) katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa mkoa na Halmashauri ya Mji wa Bariadi , walimu wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, wanafunzi walawili walioongoza katika matokeo ya mtihani wa Taifa wa kidato cha nne mwaka 2018 Kimkoa na wazazi wao, baada ya hafla ya kuwapongeza walimu waliofanikisha na wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani huo iliyofanyika kimkoa katika shule ya sekondari Nkololo wilayani Bariadi Februari 13, 2019.
  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo akizungumza na viongozi, walimu, wazazi na wanafunzi katika hafla ya kuwapongeza walimu waliofanikisha na wanafunzi waliofanya vizuri katika Mtihani wa Kidato cha nne mwaka 2018 iliyofanyika kimkoa, katika shule ya sekondari Nkololo wilayani Bariadi Februari 13, 2019.
  Mkuu wa Shule ya Sekondari Biashara Mwalimu Mathias Joseph akionesha zawadi ya shilingi 460,000/= iliyotolewa kama motisha kwa walimu wa shule hiyo waliofanikisha kutoa jumla ya alama A 23 katika Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha nne mwaka 2018, wakati wa hafla ya kuwapongeza walimu waliofanikisha na wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani huo iliyofanyika kimkoa katika shule ya sekondari Nkololo wilayani Bariadi Februari 13, 2019.  Na Stella Kalinga, Simiyu

  Wanafunzi wa shule za Serikali (kata) Wilayani Bariadi, Ibrahim Buyungumya kutoka Shule ya Sekondari Nkololo , aliyepata daraja la kwanza alama (points) saba na Kwandu Maduhu wa Biashara Sekondari aliyepata daraja la kwanza alama kumi na moja, wamekiri kuwa kambi za kitaaluma zimechangia kuongeza ufaulu wao katika Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2018.

  Wanafunzi hao wameyasema hayo katika hafla ya kuwapongeza walimu waliofanikisha na wanafunzi waliofanya vizuri katika Matokeo ya mtihani wa Taifa wa Kidato cha nne mwaka 2018 Kimkoa na kuufanya mkoa kushika nafasi ya Tisa Kitaifa, iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Nkololo wilayani Bariadi, Februari 13, 2019.

  Wanafunzi hao wamesema pamoja na kumuomba Mungu, juhudi zao binafsi za kujisomea, jitihada za walimu, malezi kutoka kwa wazazi wanakiri kambi za kitaaluma zilizofanyika mkoani Simiyu kwa madarasa yote ya mitihani ziliwasaidia kuwaandaa na mtihani huo wa Taifa, huku wakisisitiza kambi hizo ziwe endelevu na wakapendekeza kuwa kwa mwaka 2019 ziongezewe muda na zianze mapema zaidi.

  “ Namshukuru Mungu kunifanikisha kupata daraja la kwanza alama saba, nawashukuru walimu wangu, wazazi wangu kwa namna walivyokuwa msaada kwangu; pia kipekee namshukuru Mkuu wetu wa Mkoa kwa kutuletea kambi, zimetusaidia sana maana tulipata nafasi ya kukutana na wanafunzi wenzetu na walimu mahiri kutoka shule mbalimbali na zilitusaidia kuelewa masomo kwa mawanda mapana zaidi” alisema Ibrahimu Buyungumya.

  “Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kupata daraja la kwanza alama 11, nawashukuru wazazi, walimu pia nashukuru uwepo wa kambi za kitaaluma ambazo zilitusaidia sana kujiandaa vema na mtihani wetu, nashauri kambi hizi zianze mapema na muda uongezwe ili ziwasaidie wadogo zetu wafaulu vizuri zaidi yetu sisi” alisema Kwandu Maduhu.

  Mkuu wa Shule ya sekondari Biashara, Mwl. Mathias Joseph ambaye shule yake ilifanya vzuri kwa kupata alama A 23 na alama B 79 amesema pamoja na kambi za kitaaluma siri nyingine ya kufanya vizuri ni jitihada zilizofanywa na walimu pamoja na usimamizi mzuri wa mikakati iliyowekwa na idara ya Elimu na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi na mitihani ya mara kwa mara.

  Akizungumza katika hafla ya kuwapongeza walimu waliofanikisha na wanafunzi waliofanya vizuri katika Matokeo ya mtihani wa Taifa wa Kidato cha nne mwaka 2018 katika mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amewapongeza viongozi, walimu, wanafunzi, wazazi na wadau wote wa elimu mkoani humo, kwa jitihada walizofanya katika kuongeza ufaulu.

  Aidha, Mtaka ameelekeza kamati zote za shule zikutane na wazazi wa wanafunzi wa madarasa ya mtihani ili wakubaliane juu ya wanafunzi hao kuanza kambi za kitaaluma na wazazi hao wachangie chakula ambacho watoto wao wangekula wakiwa majumbani kwao kitumike wakiwa kambini.

  “Nilishatoa maelekezo na nayarudia; kamati za shule zikae na wazazi wakubaliane madarasa yote ya mtihani watoto waanze kambi za kitaaluma na wazazi wachangie chakula kile kile ambacho watoto wangekula wakiwa nyumbani, ili watoto wapate nafasi nzuri ya kusoma na kujiandaa na mtihani wa Taifa” alisema Mtaka.

  Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu, Enock Yakobo ametoa wito kwa wazazi mkoani humo kuhimiza watoto kusoma ili waweze kufikia ndoto zao akakemea tabia ya baadhi ya wazazi kuwaachisha masomo watoto wa kike na kuwaozesha.

  Jumla ya wanafunzi 7094 kati yao wavulana ni 4224 na wasichana 2875 walifanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne mwaka 2018 mkoani Simiyu na kuwezesha mkoa kushika nafasi ya tisa Kitaifa kati ya mikoa 31, ambapo umepanda kwa nafasi mbili ikilinganishwa na mwaka 2017 ambapo ulishika nafasi ya 11 Kitaifa.

  Katika pongezi zilizotolewa kwa walimu na wanafunzi mwanafunzi wa kiume aliyeongoza Kimkoa amezawadiwa shilingi milioni Moja, mwanafunzi bora wa kike shilingi laki tano (wote wamefunguliwa akaunti) na kuahidiwa kupewa mahitaji yote muhimu watakapochaguliwa kidato cha tano, huku walimu sitini kila mwalimu akipewa shilingi elfu ishirini kwa kila alama A iliyopatikana kwenye somo lake.

  0 0

  Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii

  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema uamuzi wa Mahakama ya rufaa dhidi dhamana ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko utatolewa na Mahakama ya Rufaa.

  Hakimu Mkazi Mfawidhi, Kelvin Mhina amesema hayo leo Februari 14, 2019 wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa mahakamani hapo ambapo amesema mpaka sasa kesi hiyo haijaaanza kusikilizwa, mpaka watakapopata majalada ya maamuzi kutoka Mahakama ya Rufaa.

  Mapema,  Wakili wa Serikali, Ester Martin amedai kesi hiyo leo imekuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba wanasubiri uamuzi wa Mahakama ya Rufaa. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 28, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa wakati wakisubiri Rufaa  yao Ambayo tasikilizwa Februari 18, mwaka huu.Novemba 23, mwaka jana,Jaji Mashauri akiwa Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, alifuta dhamana kwa Mbowe na Matiko kutokana na kukiuka  masharti ya dhamana.

  Baada ya uamuzi huo , washitakiwa hao wakiwakilishwa na Wakili Peter Kibatala walikata rufaa Mahakama Kuu kupinga maamuzi ya mahakama hiyo ya kufuta dhamana.Hata hivyo, baada ya mahakama Kuu chini ya Jaji Sam Rumanyika kusikiliza mapingamizi ya pande zote iliamua kuanza usikilizaji wa rufaa hiyo.

  Upande wa Serikali ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Paul Kadushi alidai kuwa wamekata rufaa katika Mahakama ya Rufani kupinga maamuzi yaliyotolewa na kuiomba mahakama hiyo kuacha kuendelea kusikiliza rufaa hiyo kwa sababu haina mamlaka.

  Hata hivyo, baada ya upande wa serikali kuwasilisha rufaa yao,  kuliibuka malumbano ya kisheria baina ya mawakili wa pande zote, huku mawakili wa kina Mbowe wakiongozwa na Wakili Peter Kibatala, walipinga uhalali wa taarifa ya serikali ya kusudio la kukata rufaa kwa madai hawajafahamishwa na Msajili wa Mahakama Kuu kuhusu kuwepo kwa taarifa hiyo.

  Jaji Rumanyika alisema kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP) anapewa mamlaka ya kukata rufaa kwa uamuzi mdogo chini ya kifungu cha 6 cha Sheria ya Mamlaka ya Rufaa na kwamba kunapokuwepo taarifa ya kusudio la kukata rufaa Mahakama ya Rufani, mahakama ya chini haiwezi kuendelea na shauri.

  Jaji  Rumanyika alisema mahakama yake imefungwa mikono hivyo anasitisha usikilizwaji wa rufani hiyo hadi hapo itakapotolewa uamuzi katika Mahakama ya Rufani.Mbali na Mbowe na Matiko, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Katibu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji, Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu ambao wote walikuwepo mahakamani.

  Katika kesi ya msingi, washitakiwa wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 13, ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai kati ya Februari Mosi na 16, mwaka  2018 maeneo ya Dar es Salaam.  Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko wakitoka kwenye viunga vya mahakama leo.


  0 0


  Na Khadija Seif,Globu ya jamii
  MSANII wa muziki kutoka nchini Nigeria  Enitimi Alfred a.k.a Timaya ameamua kufungua kwa kuweka wazi sababu za kumshirikisha mkali wa Bongofleva nchini Tanzania Alikiba kwenye album yake mpya.

  Timaya ambaye amejijengea umaarufu kutokana na staili yake ya uimbaji, amesema kuwa ndoto yake ya muda mrefu ilikuwa ni kuhakikisha siku moja anafanya kazi na Alikiba kwani pamoja na uwezo wake mkubwa pia ni shabiki wake amekuwa akimfatilia kwa muda mrefu sana.

  "Nilikutana nae kwa mara ya kwanza kwenye kazi iliyokutanisha wasanii wa nchi mbalimbali kama amani wa Kenya,R.kelly,Navio na wengine wengi lengo ni kuleta karibu mataifa hayo mawili Afrika na Amerika pamoja na kudumisha amani,furaha na upendo ," amesema Timaya

  .Hata hivyo amefafanua katika album yake mpya iitwayo Chulo vibes amemshirikisha Alikiba pamoja na Msanii Burnaboy kutoka Nigeria ambaye kwa sasa anafanya vizuri na kwamba Burnaboy ni msanii anayedumisha utamaduni wa kiafrika kwa ujumla na ni mfano mzuri wa kuigwa kutokana na nyimbo zake kama YE,On the low na Gbona zenye mahadhi na midundo ya kiafrika zaidi na hata video zake zinahamasisha utamaduni wa kiafrika kuanzia mavazi na washiriki wa video hizo.

  "Matarajio yangu ni kufanya ngoma na wasanii wa Afrika mashariki kwa nchi za Kenya,uganda na Burundi maana wasanii wa nchi hizo nao wanafanya vizuri," amesema Timaya.Ameongeza kuwa anataka kufanya kazi na wasanii ambao hajawahi kufanya nao kazi na ndio maana ndani ya albamu hiyo mpya ameshirikisha wasanii tofauti kabisa na anafurahia kuona muitikio umekua mzuri,hivyo basi anategemea kufika mbali zaidi kimuziki na ndio maana ndani ya albamu hiyo mpya ameshirikisha wasanii tofauti kabisa ambao hakuwahi kufanya kazi nao.


  0 0

  Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na wanafunzi na walimu wa Shule Maalum ya Msingi Pongwe pamoja na wakazi wa mtaa wa Pongwe Kaskazini, jijini Tanga, alipotembelea shule hiyo kwa lengo la kukagua, kujionea na kujiridhisha na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa uzio katika Shule hiyo, ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi mkoani humo yenye lengo la kukagua miradi ya TASAF na kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma.
  Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, Bi. Zena Said akimkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) kuzungumza na wanafunzi na walimu wa Shule Maalum ya Msingi Pongwe pamoja na wakazi wa mtaa wa Pongwe Kaskazini, jijini Tanga, katika siku ya kwanza ya ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo mkoani humo yenye lengo la kukagua miradi ya TASAF na kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma.
  Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akishiriki kuimba wimbo na wanafunzi wenye mahitaji maalum wa Shule Maalum ya Msingi Pongwe ya jijini Tanga, alipotembelea shule hiyo kwa lengo la kukagua, kujionea na kujiridhisha na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa uzio katika Shule hiyo wenye lengo la kuimarisha ulinzi na usalama wa wanafunzi wa jamii ya albino katika shule hiyo. 
  Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akimuagiza Mkurugenzi wa Jiji la Tanga, Bw. Daudi Mayeji (hayupo pichani) kuwasilisha mchanganuo wa matumizi ya fedha zilizotolewa na TASAF kwa lengo la kujenga uzio ili kuimarisha usalama wa wanafunzi wa jamii ya albino katika Shule Maalum ya Msingi Pongwe jijini Tanga.
  Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akifurahia jambo na wanafunzi wenye mahitaji maalum wa Shule Maalum ya Msingi Pongwe ya jijini Tanga, alipotembelea shule hiyo kwa lengo la kukagua, kujionea na kujiridhisha na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa uzio katika Shule hiyo wenye lengo la kuimarisha ulinzi na usalama wa wanafunzi wa jamii ya albino katika shule hiyo. 
  Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb), amemtaka Mkurugenzi wa Jiji la Tanga, Bw. Daudi Mayeji kuwasilisha mchanganuo wa shilingi 101, 089,736.65/= zilizotolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kujenga uzio wa Shule Maalum ya Msingi Pongwe kwa lengo la kuimarisha ulinzi na usalama wa wanafunzi wa jamii ya albino katika shule hiyo. 

  Agizo hilo amelitoa jijini Tanga, alipotembelea mradi wa ujenzi wa uzio katika shule hiyo maalum ili kujionea na kujiridhisha na utekelezaji wa mradi huo, ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi mkoani humo yenye lengo la kukagua miradi ya TASAF na kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma mkoani Tanga. 

  Mhe. Dkt. Mwanjelwa amefafanua kuwa, licha ya kuridhika na kazi nzuri iliyofanywa na Mkurugenzi huyo pamoja na wasaidizi wake ya ujenzi wenye viwango, lakini anataka maelezo ya kina ya matumizi ya fedha hizo baada ya kuangalia uzio uliojengwa na kiwango cha fedha kilichotolewa na TASAF ambapo ameelezwa kwamba gharama za uzio huo ni shilingi milioni 75 hivyo, anataka kujua kiasi kilichobakia kimetumikaje. 

  Mhe. Dkt. Mwanjelwa ameongeza kuwa fedha iliyotolewa na TASAF imefanya kazi nzuri na kusisitiza kuwa, fedha iliyotolewa kutekeleza mradi wa ujenzi wa uzio huo ni lazima kazi yake iwe ya kiuhalisia kulingana na fedha iliyotolewa na sio vinginevyo. 

  Awali, akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa uzio huo, Kaimu Mtendaji, Mtaa wa Pongwe, Bi. Dorah Senkondo amesema, ujenzi wa uzio wa mita 738 katika Shule Maalum ya Msingi Pongwe utaimarisha ulinzi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum ambao ni walemavu wa ngozi kutokana na changamoto ya kiusalama iliyopo kwa jamii ya albino. 

  Bi. Senkondo ameainisha kuwa, serikali kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini nchini, imetoa kiasi cha shilingi 101, 089,736.65/= ikiwa ni fedha za awamu ya kwanza ili kutekeleza ujenzi wa mradi huo, ambapo jumla ya mita 496 zimejengwa hadi hivi sasa, hivyo kubakiza ujenzi wa uzio wa mita 242 utakaokamilika kupitia fedha za awamu ya pili zitakazotolewa. 

  Ujenzi wa uzio huo unahusisha mchango wa jamii na usimamizi kutoka katika Halmashauri ya jiji la Tanga ili kuweza kufikia lengo la kuimarisha ulinzi na usalama kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum wa Shule ya Msingi Pongwe iliyopo mtaa wa Pongwe Kaskazini jijini Tanga. 


  IMETOLEWA NA; 
  KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI 
  OFISI YA RAIS (UTUMISHI) 
  TAREHE 14 FEBRUARI, 2019

  0 0


  The African Union (AU), at a top level summit meeting in the Ethiopian capital of Addis Ababa this week, formally launched 2019 as the “Year of Refugees, Returnees and IDPs: Towards Durable Solutions to Forced Displacement in Africa.” 

  The launch of the 2019 theme at the 32nd AU Summit comes at a time when forced displacement remains a major issue confronting the African continent. More than a third of the world’s forcibly displaced people are in Africa, including 6.3 million refugees and asylum-seekers and 14.5 million internally displaced people. 

  But the AU heads of state and government attending the gathering noted that there has also been progress in tackling forced displacement. UN Secretary-General António Guterres praised Africa’s approach and noted that the AU and UN are working together across the continent to tackle the scourge. 

  “Africa hosts nearly a third of the world’s refugees and internally displaced people. Despite the continent’s own social, economic and security challenges, Africa’s governments and people have kept borders, doors and hearts open to millions in need,” Guterres, former head of UNHCR, the UN Refugee Agency, for 10 years. 

  In his closing remarks, Egypt’s President Abdul Fattah Al-Sisi, the new chairperson of the African Union called for a focusing of efforts “to solve the problem of refugees, IDPs and migrants in a comprehensive manner along with post construction and development plans and programmes.” 

  The AU’s 2019 focus on the forcibly displaced comes at a particularly appropriate time. This year marks the 50th anniversary of the adoption of the 1969 Organization of African Unity Convention on Refugees and the 10th anniversary of the 2009 AU Convention on IDPs in Africa (Kampala Convention). The AU and its partners, including UNHCR, plan several commemorative events across the continent during the year. 

  Over the weekend, the AU and the UN Refugee Agency co-organised a roundtable conference aimed at tackling the root causes of forced displacement in Africa and achieving durable solutions. UN High Commissioner Filippo Grandi addressed the meeting and also attended the AU Summit. He also held productive bilateral meetings in Addis Ababa with the leaders of several African countries that are faced with the problem of forced displacement. 

  The AU and UNHCR also organised a high-level dialogue on the theme of the year. Speakers included the African Union Commission chairperson Moussa Faki Mahamat; UNHCR’s Filippo Grandi; UN Emergency Relief Coordinator Mark Lowcock; and Director General of the International Organization for Migration Antonio Vitorino. Others were the Executive Director of UNAIDS Michel Sidibe; Secretary General of the International Federation of the Red Cross Elhadj As Sy; the United Nations High Commissioner for Human Rights Michelle Bachelet Jeria, and UNDP’s Administrator Achim Steiner. 

  For more information, please contact: Sulaiman Momodu momodu@unhcr.org (+251930470524) or Suleyman Ali alisul@unhcr.org (+251911079548).
  Heads of State and Government at the closing ceremony of the AU Summit

  0 0

  NAIBU Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye(Mb) amelitaka Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL Corporation kuongeza juhudi katika kusambaza Huduma za Mawasiliano ili kuwafikia Wananchi wote katika pembe zote za Nchi,

  Akizungumza na Menejimenti ya Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL katika ziara yake ya siku moja kukagua utekelezaji wa majukumu ya Shirika hilo, Mhe Nditiye amesema, Serikali inathamini mchango mkubwa wa Shirika hilo na inataka kuona jitihada zaidi zikichukuliwa katika kuboresha ufanisi wa Shirika na Sekta ya Mawasiliano Nchini.

  “TTCL ni Shirika la Umma, Nawapongeza kwa yote mazuri mnayoyafanya na hasa kwa ubunifu wa huduma na gharama nafuu za huduma hizo kwa Wananchi, Huduma ya Video Conference imetoa matokeo mazuri sana, itaokoa muda na gharama kwa kuwawezesha Watendaji wa Serikali kuwasiliana bila kusafiri kutoka eneo moja kwenda jingine. Napongeza pia huduma ya malipo kwa kadi inayotarajia kuanza hivi karibuni, hizi ni juhudi ambazo Serikali inaziunga mkono.”

  Pamoja na kupongeza juhudi za TTCL zilizowezesha Shirika hilo kuongeza mapato, idadi ya Wateja wake na wigo wa upatikanaji wa huduma Nchi nzima, Mhe Nditiye ametoa Siku 30 kwa Menejimenti ya Shirika hilo kuhakikisha kuwa linaondoa kero ya upatikanaji wa Vocha na Laini za simu(Simcards) katika maeneo mbalimbali Nchini.

  Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL Corporation Mhandisi Omari Nundu amesema, baada ya kufanya vyema katika mwaka 2018, TTCL imejipanga vyema kufanikisha malengo yake kwa mwaka 2019 ambapo limekusudia kuimarisha Idara na Vitengo vyake ili kuongeza viwango vya ubora wa huduma kwa Wateja sambamba na kutekeleza majukumu ya Shirika kwa Umma.

  “Ripoti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA kwa mwaka unaoishia Desemba 2018 inaonesha TTCL kuwa Shirika linalokuwa kwa kasi na kuongeza idadi ya Wateja na wigo wa huduma zake huku huduma za T PESA nazo zikistawi kwa kasi kubwa. Hadi kufikia Januari mwaka huu, T PESA ina Wateja zaidi ya laki tatu, Mawakala elfu kumi na moja na miamala ya takribani Tsh bilioni nne. Nikuhakikishie Mhe Naibu Waziri kwamba mwaka huu 2019 tutapata mafanikio zaidi kwa kuwa tuna mikakati thabiti itakayotupa matokeo mazuri”, amesema Mwenyekiti Nundu. 
  Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (Sekta ya Mawasiliano) akizungumza jambo na Menejimenti ya Shirikika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Corporation alipotembelea shirika hilo leo jijini Dar es Salaam.
  Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (Sekta ya Mawasiliano) akisisitiza jambo kwa Menejimenti ya Shirikika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Corporation (hawapo pichani) alipotembelea shirika hilo leo jijini Dar es Salaam.
  Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati mbele) anayesimamia sekta ya Mawasiliano akisisitiza jambo kwa Menejimenti ya Shirikika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Corporation (hawapo pichani) alipotembelea shirika hilo leo jijini Dar es Salaam.
  Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye anayesimamia Sekta ya Mawasiliano (mbele kushoto) pamoja na Menejimenti ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Corporation wakitoka kutembelea miundombinu ya mkongo wa taifa wa mawasiliano unaosimamiwa na Shirika la TTCL. Kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo Sekta ya Mawasiliano, Dk. Jim Yonaz, Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Mhandisi Omary Nundu na Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa TTCL, Ndugu Ally Mbega wakiongozana na naibu waziri. 
  Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye anayesimamia Sekta ya Mawasiliano (mbele kushoto) pamoja na Menejimenti ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Corporation wakiwa na Naibu Waziri Nditiye mara baada ya kutembelea miundombinu ya mkongo wa taifa wa mawasiliano unaosimamiwa na Shirika la TTCL.
  Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (kulia mbele) akiwa na Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa TTCL, Ndugu Ally Mbega pamoja na Menejimenti ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Corporation alipotembelea miundombinu ya mkongo wa taifa wa mawasiliano inayosimamiwa na Shirika la TTCL.

  0 0

  Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

  MBUNGE wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde amewatembelea wakina mama wajawazito katika vituo vya afya na zahanati katika Jiji la Dodoma na kutoa msaada wa vifaa vya kujifungulia.

  Baadhi ya vifaa hivyo ni Delivery Pack 350 yenye thamani ya Sh.milioni saba, mashuka 100 yenye thamani ya Sh.milioni 1.1, pakiti 40 za dawa aina ya Dinoprostone zenye thamani ya Sh.milioni moja, na Carton 30 za Maji ya Kunywa ambapo msaada huo umesababisha uwepo wa furaha kubwa kwa wakina mama wajawazito na kushindwa kuficha hisia zao na kudondosha machozi ya furaha.

  Akizungumza leo baada ya kukabidhi msaada huo Mavunde amesema ameamua kutumia siku ya leo ya Februari 14,2019 kuonesha upendo kwa wakina mama hao wa Dodoma kwa kusaidia vifaa hivyo muhimu wakati wa kujifungua na hiyo ni  shukrani anayoirudisha kwa mama zake hao kutokana na upendo wao mkuu.

  Akimshukuru Mbunge Mavunde kwa msaada huo mkubwa,Mganga Mkuu wa Jiji la Dodoma Dk.Gatete Mahava amemuomba Mbunge Mavunde kuendelea kusaidiana na Serikali kutatua changamoto katika sekta ya Afya hasa katika kituo cha Afya cha Makole ambacho kimefanyiwa upanuzi mskubwa baada ya kukamilika ujenzi wa wodi ya wakina mama kupitia fedha kiasi cha Sh.milioni 500 zilizotolewa na Serikali ya Rais Magufuli katika Ujenzi wa Zahanati na Vituo vya Afya.

  Katika tukio hilo Mavunde aliambatana na viongozi wa CCM Wilaya,Mbunge wa Viti Maalum Bura, madiwani wa Kata,Wasaniii na Mama Lishe wa Soko kuu Majengo.
  Pichani kulia ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde leo akikabidhi baadhi ya vitu kwa mmoja wa akina mama mara baada kuwatembelea akina mama hao wajawazito katika vituo vya Afya na Zahanati Jijini Dodoma na kutoa Msaada wa Mifuko ya Vifaa vya kujifungulia (Delivery Pack) 350 yenye thamani ya Tsh 7m,Mashuka 100 yenye thamani ya Tsh 1.1m ,Pakiti 40 za Dawa aina ya Dinoprostone zenye thamani ya Tsh 1m na Carton 30 za Maji ya Kunywa.
  Baadhiya vifaa mbali mbali vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde kwa akina mama Waja wazito katika vituo vya Afya na Zahanati Jijini Dodoma
  Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde na ujumbe wake akiwasili kwenye moja ya zahanati jijini Dodoma kukabidhi baadhi ya vitu kwa akina Mama wajawazito katika vituo vya Afya na Zahanati Jijini Dodoma na kutoa Msaada wa Mifuko ya Vifaa vya kujifungulia (Delivery Pack)350 yenye thamani ya Tsh 7m,Mashuka 100 yenye thamani ya Tsh 1.1m ,Pakiti 40 za Dawa aina ya Dinoprostone zenye thamani ya Tsh 1m na Carton 30 za Maji ya Kunywa. 
  Pichani kulia ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde leo akikabidhi baadhi ya vifaa mmoja wa akina mama mara baada kuwatembelea akina mama hao wajawazito katika vituo vya Afya na Zahanati Jijini Dodoma na kutoa Msaada wa Mifuko ya Vifaa vya kujifungulia*(Delivery Pack) 350 yenye thamani ya Tsh 7m,Mashuka 100 yenye thamani ya Tsh 1.1m ,Pakiti 40 za Dawa aina ya Dinoprostone zenye thamani ya Tsh 1m na Carton 30 za Maji ya Kunywa.
  Picha ya pamoja

  0 0  0 0

  Na WAMJW – DSM

  NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile ameziagiza Halmashsuri zote nchini kuhakikisha zinaweka mikakati thabiti ili kutokomeza Magonjwa ya Matende na Mabusha nchini.

  Ameyasema hayo leo wakati wa Uzinduzi wa kambi ya upasuaji kwa watu wenye tatizo la ugonjwa wa Mabusha na kuangalia hali ya utoaji Huduma za Afya katika Hospitali ya Vijibweni Manispaa ya Kigamboni Mkoa wa Dar es salaam.

  Dkt. Ndugulile amesema kuwa Halmashsuri zote nchini wakati zinaandaa Vipaumbele ni lazima watenge bajeti kwaajili ya mipango endelevu ili kuhakikisha kwamba zinaweza kupambana na Magonjwa haya yaliyokuwa hayapewi kipaumbele bila kuwategemea Wafadhili.

  “Niwaombe sana, Wakati mnaandaa Mipango hii, tusiweke masuala mengi ya Semina, tuelekeze nguvu katika intervention, tuweke vitu ambavyo vitaleta mabadiliko, tutenge fedha kwaajili ya mipango endelevu, kwaajili yakuhakikisha kwamba tunaanza kujisimamia katika Magonjwa haya, haipendezi kama nchi kwenda kulia kwa Wafadhili kwa mambo ambayo tunaweza kuyafanya” Alisema Dkt. Ndugulile.

  Mbali na hayo, Dkt. Ndugulile amesema kuwa, kati ya Wilaya 120 ambazo zilikuwa na uambukizo wa magonjwa haya, Wilaya  96 zimeweza kupunguza maambukizi kwa asilimia 80, hivyo kufikia kiwango cha kusimamisha ugawaji wa Kingatiba kwa jamii katika Wilaya hizo.

  Dkt ndugulile aliendelea kuwahasa wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam kushiriki kikamilifu pindi yanapotokea mazoezi kama haya ili tuweze kutokomeza ugonjwa wa Matende na Mabusha, kwani bado Mkoa wa Dar es Salaam, maambukizi yapo juu kwa kiwango cha asilimia 10. 

  Aidha, Dkt ndugulile amesema kuwa Watu wapatao 206,708 sawa na asilimia 87.47 katika Manispaa ya Kigamboni walipatiwa Kingatiba, na kwa Manispaa ya Ubungo Watu wapatao 997,632 sawa na asilimia 87.36 walipatiwa Kingatiba, huku manispaa zote za Mkoa wa Dar es Salaam, jumla ya watu wapatao 5,127, 596 sawa na asilimia 87.63 walipatiwa Kingatiba hiyo. 

  Kwa upande mwingine Dkt. Ndugulile amesema kuwa Serikali kupitia uhisani wa CNTD, inatarajia kuwafanyia upasuaji watu 400 wakazi wa Manispaa za Kigamboni na Ubungo huku akiwaomba Wananchi wa Manispaa hizo kujitokeza ili kutumia vizuri fursa hii adimu.

  Nae Mratibu Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Dkt. Upendo Mwingira amesema kuwa Serikali kupitia Mpango huu kwa kushirikiana na Wadau  inatoa huduma hii ya upasuaji kwa wagonjwa hawa bila malipo, hivyo kuwahasa watu wenye ugonjwa huu kujitokeza ili kupata huduma hii.

  Nae Shuhuda aliyepata huduma hii ya upasuaji Bw. Ahmed Abrahaman amewahasa Watu wengine walio na ugonjwa huu kujitokeza kupata huduma hii ya upasuaji ili kuondokana na aibu hii kwa jamii, huku akisisitiza kuwa upasuaji huu unafanyiwa kwa njia za kisasa na wa muda mfupi sana.
   Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikata utepe, ishara ya ufunguzi rasmi wa uzinduzi wa kambi ya upasuaji kwa watu wenye ugonjwa wa Mabusha, uliofanyika katika Hospitali ya Vijibweni Kigamboni, wakwanza kushoto ni Mkurugenzi wa NIMRI Prof. Yunus Mgaya.
  Madaktari kutoka Hospitali ya Vijibweni Kigamboni wakifanya upasua wa kutoa busha leo, katika uzinduzi wa kambi ya upasuaji kwa watu wenye ugonjwa wa Mabusha, uliofanywa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile (Hayupo kwenye Picha)
   Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwajulia hali wagonjwa waliokwisha fanyiwa upasuaji wa Mabusha baada ya kufanya uzinduzi wa kambi ya upasuaji kwa watu wenye ugonjwa wa Mabusha, uliofanyika katika Hospitali ya Vijibweni Kigamboni.
  Wananchi waliojitokeza kumsikiliza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (jayupo kwenye picha) wakati wa uzinduzi wa kambi ya upasuaji kwa watu wenye ugonjwa wa Mabusha, uliofanyika katika Hospitali ya Vijibweni Kigamboni.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo mbele ya Wananchi waliojitokeza kumsikiliza (hawapo kwenye picha) wakati wa uzinduzi wa kambi ya upasuaji kwa watu wenye ugonjwa wa Mabusha, uliofanyika katika Hospitali ya Vijibweni Kigamboni.
  Mratibu wa Mpango wa taifa wa kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Upendo Mungila akitabasamu, baada yakupata pongezi kutoka kwa Naibu Waziri wa Afya Dkt Faustine Ndugulile, kwa  kazi nzuri anayoifanya ya kutokomeza Matende na Mabusha.(P icha na Emmanuel Massaka,MMG)

  0 0

  Na WAMJW-DAR

  Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetangaza nia ya kuanza kujenga vituo vya utengamao kwa watoto wenye ulemavu nchini (Rehabilitation Centers).

  Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa ufunguzi wa kituo kipya cha utengamano wa watoto wenye ulemavu cha Kila Siku( Community Based Rehabilitation Centre) kilichopo Kawe Jijini Dar Es Salaam.

  “Ninaahidi kwenye kila kituo cha afya cha serikali ni lazima tuanze kujenga majengo ya utengamao kwa ajili ya watoto wenye ulemavu, tuna takribani vituo vya afya 510 nchini tunaweza tusijenge kwenye vituo vyote kwa wakati mmoja lakini naamini tunaweza tukaanza na vituo vya afya 50”. Amesema Waziri Ummy.

  Waziri Ummy amesema kuna changamoto za kupata takwimu sahihi za watu wenye ulemavu ambapo kupitia sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 inaonesha watu wenye ulemavu nchini ni asilimia 5.8 na kati ya hao asilimia 60 ni watoto chini ya miaka 18.

  Kufuatia hali hiyo Waziri Ummy ameomba wadau mbalimbali wa Afya waweze kusaidiana na Serikali katika kutekeleza azma ya kujenga vituo hivyo, lengo likiwa ni kuwafikia wanawake na walezi wengi wenye watoto wenye ulemavu nchini. 

  Waziri Ummy amesema kuna uhaba mkubwa wa vituo vya Utengamao nchini huku akitoa mfano wa Jiji la Dar Es Salaam lenye vituo visivyozidi 6 lakini idadi ya watu ikiwa ni zaidi ya Milioni 5. Hata hivyo Waziri Ummy ameupongeza uongozi wa Kituo hicho cha Kila Siku Community Based Rehabilitation kwa kuanzisha huduma za utengamao kwa watoto wenye ulemavu na kuwataka wazazi na walezi kuwapeleka watoto wenye ulemavu kwenye vituo hivyo kuliko kuwafungia ndani.

  Aidha, Waziri Ummy ameagiza Maafisa Ustawi wa Jamii kuhakikisha wanatoa elimu kwa wazazi na walezi wenye watoto wenye ulemavu kwenye maeneo yao ili kuondoa dhana potofu ya kufungia ndani watoto na kuwanyima haki zao za msingi.

  Kwa upande wake Mkuu wa Shirika la Comunita Solidali nel Mondo kutoka nchini Italia Bw. Michelangelo Chiurchiu amesema lengo la kuanzishwa kituo hicho ni ujumuishwaji kwa wote wenye lengo la kuboresha maisha ya watu wenye ulemavu kupitia uboreshaji wa huduma za utengamao kijamii, kujenga uwezo wa kiuchumi kwa watu wenye ulemavu pamoja na ujumuishwaji wa watoto wenye ulemavu katika elimu ndani ya mkoa wa Dar Es Salaam.
   Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akifungua jiwe la msingi lililowekwa katika ujenzi wa kituo kipya cha utengamao wa watoto wenye ulemavu kilichopo Kawe Jijini Dar Es Salaam. Kushoto ni Balozi wa Italia nchini Tanzania Bw. Roberto Mengoni na katikati ni Mkuu wa Shirika la Comunita Solidali nel Mondo Bw. Michelangelo Chiurchiu

   Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akisalimiwa na mmoja wa watoto wenye ulemavu wakati alipotembelea maeneo wanapofundishwa utengamao katika kituo cha utengamao cha Kila Siku kilichopo Kawe Jijini Dar Es Salaam.
   Baadhi ya wazazi na walezi wa watoto wenye ulemavu wakifuatilia hotuba mbalimbali zilizotolewa katika ufunguzi wa kituo kipya cha utengamao wa watoto wenye ulemavu cha Kila Siku kilichopo Kawe Jijini Dar Es Salaam.
   Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akikata utepe kuashiria ufunguzi wa kituo kipya cha utengamao wa watoto wenye ulemavu cha Kila Siku kilichopo Kawe Jijini Dar. Kushoto ni Mkuu wa Shirika la Comunita Solidali nel Mondo Bw. Michelangelo Chiurchiu na Kulia ni Balozi wa Italia nchini Tanzania Bw. Roberto Mengoni.
   Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akisikiliza jambo alilokua akielezwa na Mkuu wa Shirika la Comunita Solidali nel Mondo Bw. Michelangelo Chiurchiu wakati wa ufunguzi wa kituo kipya cha Utengamao wa Watoto wenye ulemavu kilichopo Kawe Jijini Dar Es Salaam.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akihutubia wananchi na wazazi, na walezi wa watoto wenye ulemavu (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa kituo kipya cha utengamao wa watoto wenye ulemavu cha Kila Siku kilichopo Kawe Jijini Dar Es Salaam.

  0 0

  KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amekutana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola na kumpongeza kwa kazi nzuri kwa kuunganisha wananchi na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). 

  Lugola ambaye utembea na Ilani ya CCM katika mazingira tofauti ikiwemo ofisini na pamoja na mikutano yake ya kikazi, kitendo hicho kinamfurahisha kiongozi huyo wa CCM na kumtaka achape kazi zaidi. 

  Polepole alikutana na Lugola Ofisi za CCM Mkoa wa Arusha, leo wakati Waziri huyo alipokua anatoka katika kikao chake na Kamati ya Siasa ya Mkoa ya Chama hicho, alipofanya ziara katika ofisi hizo. 

  “Mheshimiwa Waziri nakupongeza kwa kuunganisha wananchi na ilani ya CCM, endelea kuchapa kazi,” alisema Polepole. Hata hivyo, Waziri Lugola alimshukuru Polepole kwa kumpa pongezi hiyo na kuahidi kufanya kazi zaidi kwa ajili ya kumsaidia Rais Dkt John Magufuli katika uongozi wake. 

  Waziri Lugola yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi akifuatilia maagizo yake aliyoyatoa kwa vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo ndani ya Wizara yake. 
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akimsalimia Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole, Ofisi ya CCM Mkoa wa Arusha, leo. Waziri Lugola alikutana na Polepole mara baada ya kumaliza Kikao chake na Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa ambapo Waziri huyo ufanya hivyo kila anapofanya ziara zake mikoani, Polepole alimpongeza Waziri huyo kwa kuunganisha Wananchi na Ilani ya CCM, alitaka azidi kuchapa kazi. Picha na Mpiga Picha Wetu.

  0 0
  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akizungumza na viongozi wa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kuhusu madaktari kuimarisha mawasiliano na wagonjwa ili kuwapa fursa ya kujua mwendendo wa matibabu yao.
  Baadhi ya wakurugenzi wa Muhimbili na JKCI wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Museru leo kuhusu uboreshaji wa huduma za matibabu kwa wagonjwa wanaotibwa katika taasisi hizo.
  Baadhi ya wakurugenzi wa Muhimbili, MOI na Muhimbili-Mloganzila wakiwa kwenye mkutano huo leo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Prof. Mohamed Janabi akichangia mada kwenye mkutano huo.
  Mkutano ukiendelea leo katika ukumbi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo.   Viongozi wa taasisi nne; Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila zimekutana leo kujadiliana jinsi ya kuboresha huduma za matibabu kwa wagonjwa wanaotibiwa katika taasisi hizo.

  Katika mkutano huo, wakurugenzi na wakuu wa idara wamekubaliana kuimarisha mawasiliano katika taasisi hizo ili kuhakikisha wagonjwa wanaendelea kuonwa na wataalam kwa wakati.

  Akizungumza na viongozi hao, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru ambaye amekuwa Mwenyekiti wa mkutano huo, amewaomba wakurugenzi wenzake kuendelea kuimarisha ushirikiano na kuandaa mikutano ya mara kwa mara baina ya taasisi hizo.

  “Sisi kama wakurugenzi tuendelee kuwahimiza madaktari na watalaamu wengine kuimarisha mawasiliano yao na wagonjwa ili kuwapa fursa ya kujua mwendendo wa matibabu yao,” alisisitiza Prof. Museru.

  Alisema uwepo wa mawasiliano mazuri baina ya watoa huduma na wananchi wanaohudumiwa utapunguza malalamiko yanayojitokeza mara kwa mara kuhusu mwenendo wa matibabu kwa wagonjwa.

  Pia, katika mkutano huo, taasisi hizo zimekubaliana kutumia miundombinu iliyopo kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa endapo taasisi moja itakua imeelemewa.

  “Kwa mfano, MOI au Muhimbili inaweza kulaza wagonjwa wa ICU wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwa muda kama ICU yao imejaa huku wakisubiri kupata nafasi ya kitanda katika taasisi hiyo ya Moyo,” amesema Mkurugenzi huyo.

  Taasisi hizo zitakuwa zikikutana mara kwa mara ili kujadiliana changamoto mbalimbali zinazojitokeza, huku lengo kubwa likiwa ni kuboresha huduma za matibabu zinazotolewa MNH, MOI, JKCI na Muhimbili- Mloganzila.

  0 0

  WACHIMBAJI na wadau wa madini wa Mkoa wa Manyara, wanatarajia kuandamana kesho jumamosi kwa lengo la kumshukuru Rais John Magufuli kwa kukubali kusaini muswaada wa dharura wa marekebisho ya sheria za fedha, kupunguza na kufuta kodi zilizolalamikiwa. 

  Maandamano hayo ya kilomita tatu yataanzia kwenye lango la Magufuli la kuingia ndani ya ukuta unaozunguka migodi ya madini ya Tanzanite hadi kwenye uwanja wa Barafu wa CCM mji mdogo wa Mirerani. 

  Kaimu Mwenyekiti wa chama cha wachimbaji madini mkoa wa Manyara (Marema) Tawi la Mirerani, Shwaibu Mushi (Bahati) alisema maandalizi ya maandamano hayo yatakayopokelewa na mkuu wa mkoa huo Alexander Mnyeti yanaendelea vizuri. 

  Mushi alisema Maandamano hayo yatawahusisha wachimbaji wote wa madini wa mkoa wa Manyara, kutoka wilaya zote za Simanjiro, Kiteto, Babati, Hanang' na Mbulu. Alisema wanampongeza Rais Magufuli kwa kuwakubalia ombi hadi wabunge wakapitisha sheria hiyo baada ya mkutano wa kisekta wa wadau wa madini uliofanyika hivi karibuni jijini Dar es salaam. 

  Alisema kauli mbiu ya maandamano hayo ni 'Rais wetu, madini yetu, uchumi wetu' ambapo wadau mbalimbali wa madini wakiwemo wachimbaji, wamiliki wa migodi na wazamiaji (WanaApolo) watashiriki. "Pia wadau wengine wanaonufaika na madini wakiwemo wafanyabiashara, madalali na wanunuzi wa madini mbalimbali watashiriki maandamano hayo ya kumpongeza Rais Magufuli," alisema Mushi. 

  Alisema wanaandamana kumpongeza Rais Magufuli baada ya kupita siku 17 tangu mkutano wake na wadau wa madini kufanyika na kisha kupitishwa kuwa sheria na bunge. Alisema wao wenyewe kama wadau wa madini hawana cha kumpa Rais Magufuli hivyo wanatumia maandamano hayo kwa lengo la kumuunga mkono na kuonyesha kuwa wapo naye pamoja katika uongozi wake. 

  "Maandamano hayo yanatarajia kuanzia saa mbili asubuhi na kumalizika saa nne asubuhi ambapo itasomwa risala ya kumpongeza Rais Magufuli kudhibiti utoroshwaji madini, ulipaji kodi na kumuunga mkono," alisema Mushi. Hata hivyo, kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara Agostino Senga alisema maandamano kama hayo huwa yanaruhusiwa kufanyika mradi wahusika wawe na kibali kutoka kwa mkuu wa polisi wa wilaya husika. 

  Kamanda Senga alisema hivi karibuni yalifanyika maandamano kama hayo ya wafugaji na wakulima kumpongeza Rais Magufuli kwa kuwatetea hivyo hata hayo ya wadau wa madini watayaruhusu wakiomba kibali. 
   Kaimu Mwenyekiti wa Marema Tawi la Mirerani, Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Shwaibu Mushi (Bahati) akizungumza na waandishi wa habari juu ya maandamano ya kumpongeza Rais John Magufuli kesho jumamosi. 
   Wazamiaji wa migodi ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara (WanaApolo) wakipanga viroba vilivyotolewa mgodini, ambapo kesho jumamosi wanaandamana kwa ajili ya kumuunga mkono Rais John Magufuli kwa kuwajali na kuwatetea. 
  Baadhi ya wanaApolo wa mgodi wa madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakisomoa viroba mgodini, huku wakijiandaa kwa ajili ya kuandamana kesho jumamosi ili kumuunga mkono Rais John Magufuli kwa kuwajali wachimbaji madini. 

  0 0

   Kaimu Balozi wa Marekani Dkt. Inmi Patterson  akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bw. John Mongella wakati Dkt. Patterson alipomtembelea ofisini kwake hivi karibuni. Dkt. Patterson yupo katika ziara ya kikazi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa kujionea miradi mbalimbali ya maendeleo inayofadhiliwa na Serikali ya Marekani. (Picha: Ubalozi na Ubalozi wa Marekani)
  Kaimu Balozi wa Marekani Dkt. Inmi Patterson (aliyenyanyua mkono) akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini Tanzania (Union of Tanzania Press Clubs Tanzania - UTPC), Bw. Abubakar Karsan (mwenye Tai) wakati Dkt. Patterson alipotembelea ofisi hizo hivi karibuni. Dkt. Patterson yupo katika ziara ya kikazi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa kujionea miradi mbalimbali ya maendeleo inayofadhiliwa na Serikali ya Marekani.  (Picha: Ubalozi na Ubalozi wa Marekani).

older | 1 | .... | 1802 | 1803 | (Page 1804) | 1805 | 1806 | .... | 1897 | newer