Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46379 articles
Browse latest View live

RAIS MSTAAFU DKT. KIKWETE ATEMBELEA KIWANDA KINACHOSHONA MASHATI YAKE

$
0
0
Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii 

Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ametembelea Kiwanda cha Ubunifu wa Nguo cha Binti Africa ambacho kimemshonea Nguo zake tangu alipokuwa Rais wa Tanzania.

Akizungumza na Michuzi TV, Dkt. Kiwete amesema kuwa Binti Afrika imemshonea nguo muda mrefu kwa ubunifu wa hali juu, amepongeza kwa kuwa nguo hizo za aina ya Batiki zina viwango vya ubora zinazoweza kuuzika kokote duniani.

Dkt. Kikwete amepongeza Mkurugenzi wa Kiwanda hicho, Johari Sadiq licha ya mchango kutoka kwa Mama yake mzazi, kwa kujituma na ubunifu huo ambapo unaweza kutengeza mazingira yoyote kujipatia kipato. "Watu wakumbuke Wabunifu wapo hapa nchini, wasifikirie vitu vya nje peke yake hapa ndani (Tanzania) wanaweza kupata vitu vyenye ubora wa hali ya juu",amesema Dkt. Kikwete.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kiwanda cha Uzalishaji Nguo, Johari Sadiq amesema wamepata heshima kubwa kupata ugeni wa Dkt. Kikwete katika Kiwanda hiko amesema hatua hiyo imetokana na ubora na ubunifu walionao hivyo imepelekea kuwa mteja wao muda mrefu. 

"Dkt. Kikwete amekuwa mteja wetu toka alipokuwa Rais wa nchi hii, tumeanza kuvalisha nguo zetu toka mwaka 2013, alinikuta kwenye Maonyesho nikiwa na bidhaa zangu akazipenda ubora wake, akajaribu kwa kuagiza Shati mbili", amesema Johari

Johari amesema kuwa amekuwa akijifunza muda mrefu kwa watu wengine ambapo wamefanya kazi hiyo ya ubunifu kwa muda mrefu.Ametoa wito kwa Wabunifu kutofautisha ubunifu wa majukwaani na uzalishaji nguo kuweka msingi wa uzalishaji wakuvaa nguo za kila siku, ametoa wito kwa Wabunifu kujikita zaidi kwenye uzalishaji zaidi wa nguo. Amesema miaka mitano anataka kuwa na 'Brand' ambayo itatambulika zaidi nchini kwa kuvalisha viongozi na watu wakawaida. 
 Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya  kutembelea Kiwanda cha Ubunifu wa Nguo cha Binti Africa ambacho kimemshonea Nguo zake tangu alipokuwa Rais wa Tanzania, leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
 Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia nguo zinazo tengenezwa na  Kiwanda cha Ubunifu wa Nguo cha Binti Africa ambacho kimemshonea Nguo zake tangu alipokuwa Rais wa Tanzania. kulia ni MKurungezi wa kiwanda hicho, Johari Amour Sadiq.
 Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia mashine mbalimbali  katika Kiwanda cha Ubunifu wa Nguo cha Binti Africa ambacho kimemshonea Nguo zake tangu alipokuwa Rais wa Tanzania, leo jijini Dar es Salaam.
Mafundi wa  Kiwanda cha Ubunifu wa Nguo cha Binti Africa wakiendelea na kazi.
Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa kiwanda  cha nguo cha Binti Africa leo jijini Dar es Salaam.

WABUNGE WA EALA WATOA ELIMU YA MTANGAMANO WA EAC

$
0
0
Waheshimiwa Wabunge wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari kuwaeleza zoezi walilopanga la kuelimisha wadau kuhusu Mtangamano wa Jumuiya ya AAfrika Mashariki.
Mwenyekiti wa Wabunge wa Tanzania katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Abdallah Makame na Katibu wake, Mhe. Josephene Sabastian wakiwa katika kikao na Wbunge wenzzao wa Tanzania, maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bunge la EALA na Trade Mark East Africa katika Hoteli ya Serena. Mkutano huo ni maandalizi ya zoezi la siku nne la kutoa elimu kwa wadau mbalimbali kuhusu fursa za Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuanzaia tarehe 04 hadi 07 Februari 2019 jijini Dar Es Salaam. 
Mhe. Habib Mnyaa, Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe. Marym Ussi wakishiriki kikoa cha maandalizi ya zoezi la kutoa elimu kuhusu Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. 
Mhe. Pamela Maasay (kulia) na Mhe. Happiness Legiko wakifjiandaa kukutana na wadau mbalimbali kwa ajili ya kutoa elimu ya Mtangamano. 
Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambao Wizara yao ndio mratibu w mauala ya Mtangamano wakiwa katika kikao cha maandalizi cha kutoa elimu ya Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. 
Maafisa kutoka Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika kikao cha maandalizi ya zoezi la kutoa elimu kuhusu Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. 
Mhe. Dkt. Abdallah Makame akitoa maelekezo kwa Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa dawati la Bunge. 
Kikao kinaendelea Mkutano wa Waandishi wa Habari 
Waandishi wamefurika kusikiliza Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu zoezi la kuelimisha wadau kuhusu Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. 
Waheshimiw wabunge (kushoto) na wandihi w habari wkiendelea na mkutano wao. 
Bandari ya Dar Es Salam 
Kaimu Mkurugenzi wa Bandari ya Dar Es Salaam akiwakaribisha Wabunge wa EALA katika Bandari ya Dar Es Salaam. Waheshimiwa Wabunge walienda Bandari ya Dar Es Salaam kuona maboresho yanayofanywa na bandari hiyo pamoja na kusikiliza wadau wanotumia bandari hiyo changamoto wanaokutana nazo. 
Waheshimiwa Wabunge walienda kutembelea gati namba moja ambalo ni moja ya mageti ynayofnyiwa maboresho makubwa. 
Mheshimiwa Maryam akisherehekea Siku yake ya kuzaliwa tarehe 04 Februari kwa kuwalisha keki Wabunge wenzake. 
Happy Birthday kwa Mhe. Maryam Ussi kutoka kwa Mhe. Fancy Nkuhi.

ILANI YA CCM INAVYOTEKELEZWA WILAYA YA HAI

$
0
0
Serikali imetoa kiasi cha shilingi 5,558,604,325.95 kwa ajili ya kugharamia elimu bila malipo kwa Wilaya ya Hai kuanzia Desemba 2015 ambapo kati ya fedha hizo shilingi 1,633,980,574.16zimetumika kugharamia elimu bila malipo kwa shule za msingi na 3,924,623,751.79 kwa ajili ya kugharamia elimu bila malipo kwa kidato cha kwanza hadi cha nne.

Hali hiyo imesababisha ongezeko la uandikishaji wanafunzi ngazi ya awali kutoka 3,843 mwaka 2015 hadi kufikia 4,127 mwaka 2018 na msingi kutoka 4,201 mwaka 2015hadi kufikia 4,758 mwaka 2018.

Akisoma taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi kwa miaka mitatu katika wilaya ya Hai, Mkuu wa Wilaya hiyo Lengai Ole Sabaya amesema sera ya elimu bila malipo kwa watoto wenye umri kwenda shule imefanya watoto wengi kutoka kwenye familia duni kupata fursa hiyo muhimu kwa ajili ya maendelo ya taifa.

Alisema serikali imeendelea kuboresha mazingira ya ufundishaji na ufuatiliaji wa shule ambapo kwa mwaka 2018 Wilaya ilikabidhiwa pikipiki 17 kwa ajili wa waratibu elimu kata ikiwa ni sambamba na uboreshaji wa miundo mbinu ya elimu ikiwemo ujenzi wa vyumba 35madarasa ya elimu msingi, matundu 120 ya vyoo.

Aliongeza kuwa Wilaya imepokea walimu 22 wa masomo ya sayansi na kuongeza idadi ya walimu kutoka 118 hadi walimu 140 katika juhudi za kuimarisha masomo ya sayansi shuleni.

“Kutokana na juhudi za serikali kuboresha sekta ya elimu pamoja na usimamizi na ufuatiliaji unaofanywa na viongozi wa ngazi zote, Wilaya ya Hai ilishika nafasi ya pili kimkoa na nafasi ya nane kitaifa katika matokeo ya darasa la saba mwaka jana” Alisisitiza Sabaya.

Mbali na elimu; Sabaya alisema pia serikali imeendela kutoa fedha kupitia mfuko wa maendeleo ya Jamii (TASAF) katika mpango wa kunusuru kaya masikini ambapo hadi Desemba 2018 jumla ya shilingi 3,049,467,299.98 zimetolewa kwa kaya 3,890 walizotumia kuanzisha miradi midogomidogo inayowapatia kipato ikiwemo kufuga kuku, kilimo cha bustani za mbogamboga na biashara mbalimbali.

Akizungumzia sekta ya Afya; Dc Sabaya alisema kiasi cha shilingi 1,496,355,495.00 zimetumika kununua dawa na kufanya kiwango cha upatikanaji wa dawa kufikia asilimia 90.57 ukilinganisha na asilimia 73.59 ya mwaka 2014.

“Tunaendelea kuboresha sekta hii muhimu na tumejenga duka la dawa linalotoa huduma kwa gharama nafuu saa 24 kwa wananchi wa kutoka maeneo mbalimbali nadni na nje ya wilaya” alisema.

“Tumekamilisha wodi ya wanawake katika hospitali ya wilaya, kukamilika kwa miundo mbinu hii muhimu kumewapunguzia wananchi adha ya kutembea umbali mrefu kwa ajili ya kutafuta huduma na kupunguza idadi ya wagonjwa waliokuwa wanalazimika kwenda Hospitali ya Mkoa Mawenzi’alisisitiza Sabaya.

Katika kuboresha sekta ya umwagiliaji; serikali kwa kipindi hicho imetoa shilingi 844,000,000 kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa mifereji 3 ya umwagiliaji ili kuongeza eneo la umwagiliaji kwa lengo la kuimarisha uzalishaji.

Aidha wilaya ya Hai imeanzisha kilimo cha mazao mawili ya biashara ambayo ni Korosho na vanilla kwa lengo la kuinua uchumi wa mkulima.

Akizungumia huduma ya maji Sabaya alisema serikali imetoa kiasi cha shilingi 4,062,951,699.35 kuimarisha usambazaji wa maji ambazo zimetumika kufanya ujenzi na upanuzi wa mradi wa maji wa Losaa-Kia, kujenga vituo 58 vya kutolea huduma kwenye vijiji 10 vya Mkalama, Mijongweni, Ngosero, Mbatakero, Mungushi, Kimashuku, Sanya Station, Tindigani, Mtakuja na Chemka.

Naye mgeni wa heshima Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Ndugu Kheri James alipongeza ushirikiano ulipo kati ya viongozi wa Wilaya ya Hai na kutaka hali hiyo iendelezwe.
Kheri alisema kuwa juhudi zilizoonyeshwa na waatalamu kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya na Kamati ya ulinzi na usalama imeifanya Wilaya kuwa ya kwanza Kimkoa na ya kumi kitaifa katika ukusanyaji wa mapato na kwamba hali hiyo itaboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
 Aliyekuwa mhandisi wa Ujenzi, Msangi akibadhiwa zawadi kutokana na usimamizi bora ya miradi ya ujenzi

 Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi akipokea mkono wa pongezi kutoka kwa mgeni wa heshma kutokana na usimamizi na ufuatiliaji bora uliofanya wilaya kushika nafasi ya kumi kitaifa.
 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa,  Ndugu Kheri James  akinyoosha juu ngao aliyokabidhiwa na wananchi wa Wilaya ya Hai kumpelekea Mhe. RAis wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli,kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya 
  Viongozi wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa,  Ndugu Kheri James  (hayupo pichani). Kutoka kushoto ni Katibu wa CCM Wilaya ya Hai, Kumotola Kumotola; Mbunge wa Jimbo la Siha Mhe. Godwin Mollel; Mkuu wa Wilaya ya Hai, Mhe. Lengai Ole Sabaya  na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Hai Mhe. Wang’uba Maganda.

CCM PWANI YAPOKEA WANACHAMA WAPYA 250 MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA MIAKA 42

$
0
0
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) MKOA WA Pwani Kimepokea Wanachama 250 kutoka vyama vya upinzani katika maadhimisho ya sherehe za miaka 42 ya kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi (CCM) Kwa Mkoa wa Pwani ambapo shughuli hiyo kimkoa imefanyika wilayani Mkuranga.

 Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo pamoja na kuwapokea wanachama hao wapya Mwenyekiti wa CCM MKOA Wa Pwani Ramadhani Maneno amewapongeza na kuwakaribisha wanachama hao wapya kuwa CCM ni chama bora nchini hivyo hawakukosea kufanya maamuzi ya kujiunga na chama hicho.

Waziri wa Tamisemi na Mbunge wa Kisarawe,Mh.Suleiman Jafo akizungumza na wananchi wa mkoa wa Pwani kuhusu changamoto zote zinazohusiana na wizara yake yeye akishirikiana na Naibu Waziri Wake Mwita Waitara watahakikisha wanatatua matatizo yote na kuwaomba watanzania wawaombee wao na Rais Magufuli Wawe na Afya njema watekeleze majukumu yao kwa asilimia 100%. 

"Ndugu zangu wanaccm wapya nawapongeza kwa kujiunga na chama dume chama tawala cha CCM na tena msijutie kujiunga na chama hiki kwa kuwa tunaye Mwenyekiti wetu wa CCM Taifa na Rais wa Jamburi ya Muungano wa Tanzania,Cde Dk.John Magufuli ambaye tangu aliposhika hatamu mambo mengi mazuri ameyafanya tena yanaonekana hivyo karibuni tuijenge Pwani yetu" Alisema Mwenyekiti Maneno.

 Pia Mwenyekiti Maneno Amewataka Wanachama wote wa chama hicho kuacha tabia ya kujipitisha pitisha kutaka nafasi ya udiwani na ubunge na kuwataka mara moja kuacha tabia hiyo mara moja na kuwasisistiza muda wa wao kutembea kwa wanananchi na wanachama kujinadi bado akasema kwa mwanachama yeyote wa CCM anayejipitisha na kujinadi kutaka nafasi yeyote kati ya hizo alizozisema anafanya makosa na hatua stahiki zitachukuliwa dhidi yake.

 Naye Naibu Waziri wa Nishati Subirá Mgalu amesema kuwa Serikali ya Dk. John Magufuli kupitia wizara yake inahakikisha inasambaza umeme nchi nzima katika mkoa wa Pwani mradi mkubwa wa uzalishaji wa umeme stigle gorge umezinduliwa utakapokamilika pale Rufiji utafanikisha maeneo mengi nchini kuwa na umeme wa uhakika. 

Hata Hivyo Waziri wa Tamisemi na Mbunge wa Kisarawe,Mh.Suleiman Jafo amewahakikishia wanapwani na nchi kwa ujumla kuhusu changamoto zote zinazohusiana na wizara yake yeye akishirikiana na Naibu Waziri Wake Mwita Waitara watahakikisha wanatatua matatizo yote na kuwaomba watanzania wawaombee wao na Rais Magufuli Wawe na Afya njema watekeleze majukumu yao kwa asilimia 100%. 

Akizungumza wakati akisoma risala ya wilaya ya Mkuranga Katibu wa CCM wilaya hiyo,Hakimu Jackson alisema kuwa kutokana na utaratibu wa kila wilaya,kata na matawi kuwa na vitega uchumi ili chama kiondokane na mfumo wa kuombaomba amemshukuru mbunge wa jimbo lá Mkuranga na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega na família yake kwa kuisaidia chama wilaya kwa kujenga vibanda vya fremu 11,ukuta na ukumbi wa kisasa ambao utaiwezesha chama kuongeza mapato yake. 

"Ndugu Mgeni Rasmi Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani Ramadhani Maneno vibanda hivi vyote,fremu 11 na uzio hivi vyote kwa pamoja vimejengwa kwa thamani ya Sh. Milioni 34,686,500 kwa fedha yake Mwenyewe mh.Mbunge Ulega bila kusaidiwa na mtu yeyote" Alisema Katibu Jackson Aidha Katibu Jackson aliongeza kwa kusema kuwa pamoja na kujenga ukuta na vibanda vya fremu pia mh.Ulega anaendelea na ujenzi wa ujenzi wa ofisi za kata 19 Kátia ya kata 25 ambapo ametumia Sh.Milioni 20,930,000 ukijumlisha fedha alizotoa kata na wilaya jumla ni Sh.Milioni 55,616,500 kitendo hiki anachokifanya mbunge ulega kinapaswa kuigwa na wabunge wengine wa CCM nchi nzima.

Kwaupande wake mbunge wa jimbo la Mkuranga ambaye pia ni naibu waziri wa Mifugo na uvuvi Abdalah Ulega ambaye amechangia gharama za ujenzi wa ukuta na fremu katika jengo la ccm amesema ujenzi huo utasaidia kukuinua chama hicho kiuchumi.Ulega amesema jengo hilo lililogharimu zaidi ya milion hamsini,amelijenga kwa mapenzi yake na chama cha Mapinduzi CCM.

Hata hivyo amewashukuru viongozi wote wa wilaya ya Mkuranga akiwemo Mkurungenzi wa halmashauri na diwani wa Mkuranga kwa ushirikiano mkubwa katika kufanikisha ujenzi huyo.Sherehe za kumbuku za kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi kutimiza miaka 42 kwa mkoa wa Pwani,imebeba kaulimbiu isemayo kazi ni kipimo cha utu, kazi,tulinde uhuru wetu.nae,Ahmed Salum kada wa chama cha Mapinduzi amempongeza mbunge kwa jitihada kubwa anzozifanya za kuendelea ilani ya chama hicho ameahidi kumuunga mukono katika miladi mbalimbali ya unjezi wa ofisi za chama. Mwenyekiti wa CCM, mkoa wa Pwani,Ramadhani Maneno akiwahutubia wakazi wa Pwani na vitongoji vyake ndani ya uwanja wa (CCM) Mkuranga,wakati wa sherehe za miaka 42 ya kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi (CCM) Kwa Mkoa wa Pwani, ambapo shughuli hiyo kimkoa imefanyika wilayani Mkuranga. Sherehe hizo zimehudhuriwa na viongozi Mbalimbali wa Kitaifa. Mwenyekiti wa CCM, mkoa wa Pwani,Ramadhani Maneno akiwaongoza wakazi wa mkoa Pwani kufyeka majani eneo la Hospital ya wilaya ya Mkuranga wakati wa sherehe za miaka 42 ya kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi (CCM) Kwa Mkoa wa Pwani ambapo shughuli hiyo kimkoa imefanyika wilayani Mkuranga.  Semu ya viongozi mbalimbai wakiwa meza kuu. Sehemu ya wananchi walio hudhuria wakati wa sherehe za miaka 42 ya kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi (CCM) Kwa Mkoa wa Pwani ambapo shughuli hiyo kimkoa imefanyika wilayani Mkuranga. (Picha zote na Emmanuel Massaka,MMG) Naibu Waziri wa Nishati Subirá Mgalu akizungumza na wananchi wa mkoa Pwani kuhusu mradi mkubwa wa uzalishaji wa umeme Stigle Gorge utakapokamilika utanufaisha maeneo mengi nchini kuwa na umeme wa uhakika.   Ahmed salum kada wa chama cha Mapinduzi akimpongeza mbunge kwa jitihada kubwa anzozifanya za kuendelezaa Ilani ya chama hicho,aidha ameahidi kumuunga mkono katika miradi mbalimbali ya ujezi wa ofisi za chama.  Maandamano yakiendelea sambamba na ubebaji wa mabango yenye Ujumbe wa mbalimbali.(Picha zote na Emmanuel Massaka,MMG) Sehemu ya wananchi walio hudhuria wakati wa sherehe za miaka 42 ya kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi (CCM) Kwa Mkoa wa Pwani ambapo shughuli hiyo kimkoa imefanyika wilayani Mkuranga.      Semu ya viongozi mbalimbali wakiwa meza kuu.

CHANJO YA MLANGO WA KIZAZI HAIHUSIANI NA UZAZI WA MPANGO

$
0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akisisitiza jambo leo wakati akiongea na Waandishi wa Habari katika siku ya Saratani Duniani, iliyofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari Bunge jijini Dodoma, 
Mkurugenzi wa Ubora ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Mohammed Mohammed akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya Dkt. Grace Maghembe leo katika tamko la siku ya Saratani Duniani lililofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari Bunge jijini Dodoma. 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiteta jambo na Mkurugenzi wa Ubora kutoka Wizara ya Afya Dkt. Mohammed Mohammed ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Afya. 
Waandishi wa Habari wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu wakati akitoa tamko la siku ya Saratani Duniani, leo jijini Dodoma 
Mkurugenzi wa Ubora kutoka Wizara ya Afya Dkt. Mohammed Mohammed. ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Afya leo katika tamko la siku ya Saratani Duniani lililofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari Bunge jijini Dodoma.
…………………………………………………………………………………. 

Na WAMJW – DOM 

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu amewatoa hofu Wananchi kwa kusisitiza kuwa chanjo ya kuwakinga wasichana na Saratani ya Mlango wa kizazi haihusiani na uzazi wa mpango wala kumzuia msichana kuja kupata uja uzito baadae. 

Ameyasema hayo leo wakati akiongea na Waandishi wa Habari katika siku ya Saratani Duniani, iliyofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari Bunge jijini Dodoma, huku kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni “NITAFANYA JITIHADA ZOTE KUPUNGUZA JANGA LA SARATANI DUNIANI”. 

Waziri Ummy amesema kuwa Chanjo ya Mlango wa kizazi ni salama na imethibitishwa na Shirima la Afya Duniani kwaajili yakuwakinga Wasichana dhidi ya maambulizi ya Saratani ya Mlango wa kizazi. 

” Chanjo ya kuwakinga wasichana na saratani ya mlango wa kizazi haihusiani na uzazi wa mpango, ni chanjo ambayo imethibitishwa na Shirika la Afya Duniani kwaajili yakuwakinga wasichana dhidi ya maambukizi ya Saratani ya mlango wa Kizazi” Alisema Waziri Ummy 

Waziri Ummy amesema kuwa katika kila wagonjwa wa Saratani 100, takribani wagonjwa 31 ni wanawake wa Saratani ya Mlango wa kizazi, hivyo amewahasa wazazi na walezi nchini kuhakikisha wasichana wanaostahili kupata chanjo hii, wanaipata bila vikwazo vyovyote ili kutokomeza kabisa Saratani hii nchini. 

“Katika kila wagonjwa wa Saratani 100, Wagonjwa takribani 31 ni wanawake wa Saratani hii ya Mlango wa kizazi, kwahiyo hatuna haja ya kuiogopa chanjo hii kwasababu ndio itayowakinga watoto wetu na maambukizi ya Saratani ya mlango wa kizazi” alisema Waziri Ummy. 

Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Tafiti za Saratani (IARC), zinaonyesha kwamba kwa Tanzania kunatokea mgonjwa 1 wa Saratani kwa kila watu 1000, hivyo Tanzania inakua na wagonjwa wapya wa Saratani 55,000 kwa mwaka na takribani wagonjwa 28,610 hufariki kwa mwaka, ambapo ni vifo asilimia 52 ya wagonjwa wapya. 

Aliendelea kusema kuwa Taarifa kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road zinaonesha kwamba kumekuwa na ongezeko la wagonjwa wa Saratani mwaka hadi mwaka, huku akisema kuwa Mwaka 2015 wagonjwa wapya 5,764, huku mwaka 2016 wagonjwa wapya 6,338, na mwaka 2017 wagonjwa wapya 7,091, pia mwaka 2018 wagonjwa wapya 7,649. 

Kwa upande mwingine Waziri Ummy amedai kuwa Serikali imeanzisha huduma kwenye vituo 624 vilivyopo katika Halmashauri mbalimbali nchini ambapo jumla ya wanawake 375,522 walifanyiwa uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi na saratani ya matiti mnamo mwaka 2017, ukilinganisha na wanawake 416,841 waliofanyiwa uchunguzi huo mwaka 2018. Kati ya hao, wanawake 16,147 waligundulika kuwa na mabadiliko ya awali mwaka 2017, na wanawake 18,341 mwaka 2018.

WAZIRI MKUU AKITETA JAMBO NA SPIKA BUNGENI LEO

$
0
0
Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa akizungumza na Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai Katika Ukumbi wa Spika Jijini Dodoma leo Februari 4, 2019. PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

HYATT HOTEL’S LUXURY SKY BAR CELEBRATES AUSTRALIA DAY WITH AUSTRALIA’S FAVOURITE SPREADS

$
0
0
General Manager of Hyatt Regency Dar es Salaam Mr. Garry Friend awarding one of the invited guests on Australian National Day at Hyatt Which also they went to Zanzibar ( Mazizini Orphanage Centre) and helped on fundraising some amount to orphanage.

…………………………………………………………………..

Hyatt Regency Dar es Salaam has today unveiled the national pride of Australia to the Tanzanian community at the hotel’s luxury rooftop.

Across the nation and around the world on Australia day, citizens reflect on what it means to be Australian and recall the birth of a new nation, marked in history with the arrival of the first British ships and the raising of the flag of Great Britain at Sydney Cove.

“We are pleased to fly the national flag in the most prominent place in the city, which offers the best music entertainment, food and drinks for local Tanzanians and the Australian community to enjoy together,” said Mr. Garry Friend, General Manager of Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kilimanjaro.

“We are here to create a truly memorable experience, and we plan to hold different events every year to help make a difference in society. Today we will raise some money and offer tickets to Zanzibar as a prize, as a means of helping orphanage centers in Zanzibar.” He added

About Hyatt Regency.

The Hyatt Regency brand prides itself on connecting travellers to who and what matters most to them. More than 160 conveniently located Hyatt Regency urban and resort locations in over 30 countries around the world serve as the go-to gathering space for every occasion – from efficient business meetings to memorable
Family vacations. The brand offers a one-stop experience that puts everything guests need right at their fingertips. Hyatt Regency hotels and resorts offer a full range of services and amenities, including the space to work, engage or relax, notable culinary experiences, technology-enabled ways to collaborate and expert event planners that can take care of every detail.

MAKATIBU WA WABUNGE MAJIMBONI WAPATIWA MAFUNZO

$
0
0

Mtaalamu kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma , Ndugu Dorah Chenyambuga akitoa mada kuhusu utunzaji wa nyaraka, uendeshaji wa ofisi, ufuatiliaji na tathimini kwa makatibu wa waheshimiwa wabunge majimboni. Mafunzo hayo yametolewa na Ofisi ya Bunge chini ya mradi wa kulijengea Bunge Uwezo (LSP II) unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)
Baadhi ya makatibu wa waheshimiwa wabunge majimboni wakipatiwa mafunzo ya kujengewa uwezo.mafunzo hayo yaliyofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma yametolewa na Ofisi ya Bunge chini ya mradi wa kulijengea Bunge Uwezo (LSP II) unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu kutoka Ofisi ya Bunge Ndugu Jane Kajiru akifungua mafunzo kwa makatibu wa waheshimiwa wabunge majimboni kwa ajili ya kujengewa uwezo wa kutekeleza majukumu yao.mafunzo hayo yametolewa na Ofisi ya Bunge chini ya mradi wa kulijengea Bunge Uwezo (LSP II) unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), kushoto kwake ni Mratibu wa Mradi wa LSP II Ndugu Mary Lasway .
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu kutoka Ofisi ya Bunge Ndugu Jane Kajiru akifungua mafunzo kwa makatibu wa waheshimiwa wabunge majimboni kwa ajili ya kujengewa uwezo wa kutekeleza majukumu yao.mafunzo hayo yametolewa na Ofisi ya Bunge chini ya mradi wa kulijengea Bunge Uwezo (LSP II) unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), kushoto kwake ni Mratibu wa Mradi wa LSP II Ndugu Mary Lasway

Ommy Dimpoz - Ni Wewe (Official Music Video)

MAGAZETI YA LEO JUMANNE ,FEBRUARI 5 2019.

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA, PHAUSTINE KASIKE ATEMBELEA GEREZA KUU LA WANAWAKE TANZANIA - KINGOLWIRA, MOROGORO

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Gereza Kuu la Wanawake Tanzania - Kingolwira, ACP. Loyce Ruhembe alipotembelea alipotembelea Gereza hilo jana februari 4, 2019 katika ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro.
. Mkuu wa Gereza Kuu la Wanawake Tanzania, Kingolwira, ACP. Loyce Ruhembe akitoa taarifa fupi ya uendeshaji wa Gereza Kuu la Wanawake Tanzania – Kingolwira kwa Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(kushoto meza kuu) jana februari 4, 2019 alipotembelea Gereza hilo.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(katikati) akikagua maeneo mbalimbali ya Gereza Kuu la Wananwake(kulia) ni Mkuu wa Gereza Kuu la Wanawake Tanzania, Kingolwira, ACP. Loyce Ruhembe. Kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Udereva cha Magereza – Kingolwira, ACP. Lazaro Nyanga.
Askari wa Gereza Kuu la Wanawake Kingolwira wakiwa timamu kazini wakati Kamishna Jenerali wa Magereza nchini(hayupo pichani) akizungumza na Wafungwa wa Gereza hilo jana februari 4, 2019 alipotembelea Gereza hilo.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(kulia) akiangalia mradi wa kuku wa mayai katika Gereza Kuu la Wanawake Tanzania – Kingolwira alipotembelea jana februari 4, 2019.
Ujenzi wa nyumba kwa njia ya ubunifu katika Kambi mojawapo ya Gereza Mtego wa Simba, Morogoro ukiendelea katika hatua awali za ujenzi.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akiangalia mashine kufunga majani ya malisho ya mifugo katika mradi wa ng’ombe wa maziwa Gereza Mtego wa Simba
Mkuu wa Chuo cha Udereva cha Magereza – Kingolwira, ACP. Lazaro Nyanga akimuongoza Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(kushoto) kukagua majenego mbalimbali yanayokarabatiwa katika chuo hicho kwa kutumia ubunifu(Picha na Jeshi la Magereza).

MAHAKAMA YAANZISHA MPANGO WA KUWALEA WANAFUNZI KIMAADILI

$
0
0


Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Latifa Mansoor akizungumza na wanafunzi leo Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dodoma
Mwanafunzi kutoka shule ya Sekondari Kilakala akizungumza. Lydia Churi Ntambi

Wanafunzi wa vyuo na shule za sekondari wakiwa tayari kuzungumza na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Latifa Mansoor leo Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dodoma
Wanafunzi wa vyuo na shule za sekondari wakiwa tayari kuzungumza na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Latifa Mansoor leo Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dodoma


Na Lydia Churi-Mahakama, Dodoma

Mahakama ya Tanzania imeanzisha mpango wa kushirikiana na vyuo na shule za sekondari katika kuwalea na kuwatambua wanafunzi wenye vipawa, tabia na maadili mema ambapo huwafuatilia na kuwafanyia tathmini ili baadaye waje kufanya kazi na Mahakama pamoja na maeneo mengine katika sekta ya Sheria

Katika wiki ya utoaji wa elimu ya Sheria inayoendele jijini Dodoma, wanafunzi kutoka baadhi ya vyuo vikuu na shule za sekondari nchini wanashiriki kwa kujifunza masuala ya mbambali yanayohusu sheria pamoja na taratibu za kimahakama jijini.

Akizungumza na Wanafunzi, Waalimu na Washauri wa wanafunzi hao, kwa niaba ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Dodoma, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Latifa Mansoor amesema kupitia Mpango huo wa Mahakama, watumishi watakaoajiriwa na Mahakama ni wale tu wenye tabia na maadili mema na wenye uwezo uliothibitika ili waweze kutoa huduma bora hapo baadaye.

Akizungumzia utekelezaji wa mpango huo, Jaji Mansoor amesema baadhi ya mambo ambayo Mahakama inashirikiana na vyuo na shule hizo ni kuwa na mahusiano ya karibu na kuwa na fomu za ufuatiliaji wa mienendo ya maadili na taaluma za wanafunzi ambazo hujazwa na kutumwa kwa Mahakama ya Tanzania mara mbili kwa mwaka.

Aliyataja mambo mengine ya ushirikiano kuwa ni pamoja na uanzishwaji wa klabu na utoaji wa elimu ya sheria mashuleni pamoja na mpango wa kuwazawadia fursa za masomo na zawadi nyingine wanafunzi wenye vipaji na maadili mema.

Aidha, Jaji Mansoor pia aliwataka Waalimu na washauri wa shule hizo kuwalea na kuhakikisha kuwa wanafunzi hao wanakuwa na ubora katika taaluma, tabia na maadili. Aliongeza kuwa wanafunzi wa vyuo hufuatiliwa na kumbulkumbu zao huhifadhiwa kwa mahitaji ya baadaye ikiwemo ajira kwa watumishi wa Mahakama na Sekta ya Sheria kwa ujumla.

Aliwataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii na kuwa na tabia na maadili mema kwa manufaa yao na ya taifa kwa ujumla.” Tunawaalika katika maadhimisho haya ili kubadilishana uzoefu na pia mjifunze masuala mbalimbali ya sheria ili muwe na ufahamu zaidi”, alisema.

Kufuatia Mpango huu wa ushirikiano, Mahakama ya Tanzania inatarajia kuwa na huduma zilizoimarika, watumishi kufanya kazi kwa ubora wa hali ya juu na kwa kuzingatia utawala wa sheria, na vitendo vya rushwa na ukiukwaji wa maadili kupungua.

Vyuo ambavyo mpaka sasa vimeingia kwenye ushirikiano na Mahakama ya Tanzania ni vyuo vikuu vya Dar es salaam, Mzumbe, Dodoma, Ruaha, Iringa na chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto.

Shule za sekondari ni pamoja na Maua Seminari. Kisimiri, Shule ya Wavulana Ilboru, Shule ya sekondari Kilakala, Shule za Sekondari za Wavulana za Feza, Marian na Tabora. Nyingine ni Shule ya sekondari Msalato na Mazinde Juu.

Mawaziri wa Tanzania, Rwanda na Burundi wakagua kazi ya ujenzi wa mradi wa umeme wa Rusumo

$
0
0
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa tatu kushoto) pamoja na Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga (wa pili kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Lt. Col. Michael Mntenjele (wa nne kushoto) wakitoka kukagua eneo kutakapojengwa mitambo ya kuzalisha umeme wa megawati 80 katika eneo la Rusumo mkoani Kagera.
Maporomoko ya maji ya Mto Kagera, yatakayotumika kuzalisha umeme wa megawati 80 kwa ajili ya nchi za Tanzania, Rwanda na Burundi.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa pili kulia), Waziri wa Nishati na Migodi wa Burundi, Come Manirakiza (wa kwanza kushoto) na Waziri wa Miundombinu wa Rwanda, Claver Gatete (wa Tatu kulia mstari wa pili) wakitoka kukagua eneo kutakapojengwa mitambo itakayozalisha umeme wa megawati 80 katika eneo la Rusumo lililopo mpakani mwa nchi ya Rwanda na Tanzania.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (katikati), Waziri wa Nishati na Migodi wa Burundi, Come Manirakiza (kushoto kwa Dkt. Kalemani) na Waziri wa Miundombinu wa Rwanda, Claver Gatete (kulia kwa Dkt Kalemani) wakiwa katika kikao chao na wataalam mbalimbali wanaosimamia mradi wa umeme wa Rusumo kilichofanyika Rusumo mkoani Kagera.
Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga (katikati) akifuatilia kikao cha Mawaziri wa Rwanda, Tanzania na Burundi kilichohusu utekelezaji wa mradi wa umeme wa maji wa Rusumo.


Na Teresia Mhagama,

Mawaziri wanaohusika na utekelezaji wa mradi wa umeme wa maji wa Rusumo (MW 80) kutoka Tanzania, Rwanda na Burundi wamekagua kazi ya ujenzi wa mradi huo wilayani Ngara mkoa wa Kagera na kutoa maelekezo mbalimbali yatakayowezesha kasi ya utekelezaji wa mradi huo kuongezeka.

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani ndiye aliyewaongoza, Waziri wa Nishati na Migodi wa Burundi, Come Manirakiza na Waziri wa Miundombinu wa Rwanda, Claver Gatete katika kukagua kazi mbalimbali zinazoendelea kufanyika ikiwemo ujenzi wa eneo itakapojengwa mitambo ya kuzalishia umeme na ujenzi nyumba za wafanyakazi.

Baada ya kukagua kazi zinazoendelea kufanyika, Mawaziri hao walifanya kikao chini ya uenyekiti wa Dkt Medard Kalemani na kuiagiza Bodi ya Wakurugenzi ya mradi huo kusimamia ipasavyo kazi mbalimbali za ujenzi ili mradi huo ukamilike mwaka 2020 kama ilivyo katika makubaliano.

Dkt. Kalemani alisema kuwa, kazi ya ujenzi wa mradi huo ilianza mwezi Februari mwaka 2017 na inapaswa kukamilika ndani ya miezi 36 hivyo Bodi hiyo yenye wajumbe kutoka nchi zote Tatu ihakikishe kuwa mkandarasi anakamilisha kazi kwa wakati.

“ Pia tumeiagiza Bodi na wataalam walioko katika mradi huu, wahakikishe kuwa wanashirikisha Mamlaka na Taasisi mbalimbali zilizopo katika maeneo ya mradi katika nchi zote Tatu hasa katika masuala yanayohusu jamii zinazozunguka mradi na stahili za wafanyakazi ili kutokuwa na vikwazo katika utekelezaji,” alisema Dkt Kalemani.

Kuhusu faida za mradi huo, alisema kuwa, kila nchi itapata megawati 27 na kujenga miundombinu ya usafirishaji umeme wa kV 220 ambapo kwa upande wa Tanzania, itajengwa miundombinu hiyo kutoka Rusumo kwenda Nyakanazi kwa umbali wa kilometa 98.

Aliongeza kuwa, miundombinu hiyo ya usafirishaji umeme, kwa upande wa Tanzania, itaingiza umeme katika gridi ya Taifa kupitia njia ya umeme inayotoka Geita na kwamba, vijiji 13 vinavyopitiwa na mradi wa Rusumo vitasambaziwa nishati hiyo.

Kuhusu gharama za mradi, alisema kuwa, kila nchi imegharamia mradi huo kupitia wadau wa maendeleo ambao ni Benki ya Maendeleo Afrika (AfdB) na Benki ya Dunia (WB) ambapo kwa ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme kila nchi imechangia takribani Dola za Marekani milioni 113.

Kwa upande wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme, alisema kuwa kila nchi imechangia kiasi cha Dola za Marekani milioni 36.7.

Kwa ujumla, alisema kuwa, Mawaziri wa nchi hizo Tatu wameazimia kuwa, mradi huo utekelezwe kwa kasi usiku na mchana bila kuwa na visingizio na kama kuna muda uliopotezwa na mkandarasi wa mradi, ufidiwe kwa njia mbalimbali ikiwemo kuongeza nguvu kazi.

Aidha, ili kuongeza usimamizi katika mradi huo, Mawaziri hao ambao kwa kawaida hukutana kila baada ya miezi Sita, wameamua kufanya vikao vya dharura kila itakapohitajika ili kuhakikisha kuwa yale wanayoaagiza yanatekelezwa kwa ufanisi.

Ni Mkeka na Mvinyo Maadhimisho ya Valentine Dar

$
0
0
Wadau mbalimbali wa uzalishaji wa mvinyo hapa nchini pamoja na watumiaji wa kinywaji hicho wanatarajia kufurahia pamoja Siku ya wapendanao yaani Valentine Day katika hafla ya maalum inayofahamika kama ‘Mkeka na Mvinyo’ itakayofanyika usiku wa Februari 14 katika hoteli ya Whitesands jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Mratibu wa hafla hiyo kutoka kampuni ya Real PR Solutions (RPR), Bi Calorine Kirwanda amesema mbali na kuwakutanisha wadau muhimu wa kinywaji hicho, hafla hiyo inalenga kutoa fursa kwa watumiaji wa mvinyo hapa nchini kufurahia vinywaji tofauti vya aina hiyo vinavyozalishwa hapa nchini huku wakiwa wamekaa kwenye mikeka.

“Pamoja na kutoa fursa kwa watumiaji wa mvinyo siku hiyo kufurahia pamoja na wapendwa wao, usiku wa Mkeka na Mvinyo unalenga kuunga mkono jitihada za serikali katika kutangaza utalii na kukuza viwanda vya ndani kupitia uhamasishaji wa matumizi ya bidhaa zinazozalishwa hapa nchini ikiwemo aina tofauti ya mvinyo bora kabisa unaozalishwa hapa nchini,’’

“Upekee wa hafla hii unaanzia kwenye jina lake ‘ Mkeka na Mvinyo’. Hivyo basi itahusisha matumizi ya mikeka ambapo wageni wetu watapata fursa ya kuketi kwenye mikeka huku wakifurahi mvinyo bora unaozalishwa hapa nchini pamoja na nyama choma kadili ya matakwa yao,’’ alisema.

Aliwataja baadhi ya wadau muhimu katika kufanikisha hafla hiyo kuwa ni pamoja na Hoteli ya Whitesands, Bodi ya Utalii Tanzania, (TTB), GS 1, pamoja na kampuni ya magazeti ya TSN wazalishaji wa magazeti ya Daily News pamoja na Habari Leo.

Bi Kirwanda aliongeza kuwa hafla hiyo ni sehemu ya mkakati wa kampuni hiyo utakaozinduliwa hivi karibuni unaolenga kutangaza utalii wa ndani pamoja kuvumbua fursa mbalimbali za kibiashara ndani ya nchini kwa lengo la kukuza uchumi unaofahamika kwa jina la ‘Domestic Tourism Promotion Initiative’ (DTPI).

“Tunahitaji kuhamasisha zaidi matumizi ya bidhaa za ndani ili kukuza uchumi wetu kama taifa,’’ aliongeza bi Kirwanda huku akitaja baadhi ya maeneo ambayo tiketi za hafla hiyo zinapatikana kuwa ni pamoja na Hoteli ya Whitesands na Shamo Tower Mbezi Beach.

Alisema, tofauti na mtu mmoja mmoja au kwa wale ambao watakuwa na wapendwa wao, Mkeka na Mvinyo inatoa fursa kwa mashirika na taasisi mbalimbali kufurahia pamoja katika dhana nzima ya kuonesha upendo, shukrani na pongezi baina yao na wadau wao katika shughuli zao za kila siku huku wakifurahia mvinyo na chakula kizuri katika viunga vya hoteli ya Whitesands.

“Ifahamike kwamba siku ya wapendanao sio kwa ajili ya wale wenye mahusiano ya kimapenzi tu bali pia inaweza kutumiwa na mashirika au taasisi mbalimbali lengo likiwa ni kuonesha upendo, shukrani na pongezi kwa wafanyakazi, na wadau mbalimbali wanaoshirikiana nao katika shughuli zao za kila siku,’’ alifafanua.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Meneja Mauzo na Masoko wa kampuni ya magazeti ya TSN, Januarius Maganga alisema kampuni hiyo imeaamua kuunga mkono mpango huo kutokana na kuguswa kwake na namna unavyolenga kuchochea harakati za masoko kwa bidhaa za ndani sambamba na kuunga mkono agenda ya serikali ya uchumi wa viwanda.

Kwa upande wake Afisa Uhusiano Mwandamizi kutoka Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bw Geofrey Tengeneza alisema kupitia mpango huo mbali na kutangaza utalii wa fukwe pia utatangaza utalii wa asili kwa kuwa utahusisha mvinyo unaozalishwa hapa nchini huku watumiaji wakiwa wameketi kwenye mikeka ya asili.


Afisa Uhusiano wa kampuni ya GS 1, Bi Clementine Kahamba (kushoto) akizungumza kuhusiana na hafla hiyo. akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na hafla hiyo itakayohusisha adau mbalimbali wa uzalishaji wa mvinyo hapa nchini pamoja na watumiaji wa kinywaji hicho itakayofanyika siku ya wapendanao yaani Valentine Day Februari 14 katika hoteli ya Whitesands jijini Dar es Salaam. Wengine ni pamoja na Mratibu wa hafla hiyo kutoka kampuni ya Real PR Solutions (RPR), Bi Calorine Kirwanda (wa pili kushoto), Meneja Mauzo na Masoko wa kampuni ya magazeti ya TSN, Januarius Maganga (wa pili kulia), pamoja na Meneja Uendeshaji wa Hotel ya Whitesands Bw Ali Hilika.
Mratibu wa hafla ya ‘Mkeka na Mvinyo’ kutoka kampuni ya Real PR Solutions (RPR), Bi Calorine Kirwanda (wa pili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na hafla hiyo itakayohusisha adau mbalimbali wa uzalishaji wa mvinyo hapa nchini pamoja na watumiaji wa kinywaji hicho itakayofanyika siku ya wapendanao yaani Valentine Day Februari 14 katika hoteli ya Whitesands jijini Dar es Salaam. Wengine ni pamoja na Meneja Mauzo na Masoko wa kampuni ya magazeti ya TSN, Januarius Maganga (wa pili kulia), Afisa Uhusiano wa kampuni ya GS 1, Bi Clementine Kahamba (kushoto) pamoja na Meneja Uendeshaji wa Hotel ya Whitesands Bw Ali Hilika.

RAIS MAGUFULI ATOA MILIONI 200 KWAJILI YA UNUNUZI WA VIFAA VYA KISASA KITUO CHA CHANEL 10 NA AFRICAN MEDIA GROUP

$
0
0
 Rais Dkt Magufuli.
 
Na. Vero Ignatus

Katika kushehereke miaka 42 ya kuzaliwa chama cha mapinduzi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametembelea kituo cha Luninga cha Chanel ten sambamba African group na kuzungumza na wafanyakazi na kusikiliza changamoto zao

Katika ziara hiyo Rais ameahidi shilingi milioni 200 kwaajili ya kununua vifaa vipya kwaajili ya kurushia matangazo ambapo amesema kupitia chombo hicho Watanzania watanufaika kwa kupata taarifa na watajifunza mambo mengi ,

Rais Magufuli amezungumzia pia kuhusu Uhuru wa vyombo vya habari ambapo amesema kuwa kila mtanzania anayohaki ya kuzungumza, kupata habari na kuelewa mambo yanayoendelea katika nchi yake

Ametoa angalizo kwa wanahabari kuwa wazingatie Maadili pale wanapotoa habari katika vyombo vyao na wahakikishe kuwa habari hizo zinaukweli ndani yake.'' Wanahabari mnatakiwa mzingatie maadili wakati mnatoa habari zenu, unaweza kutoa habari amabayo haina uhakika ukahatibu maisha ya mtu kabisa, kisha baadae unakuja kugundua siyo jambo la ukweli italeta picha mbaya kayika jamii''Amesisitiza Rais Magufuli

Rais amesisitiza kuwa Vyombo vya habari vinatakiwa vizungumze kwani vinaibua mambo mengi ambayo ni msaada kwa viongozi na watanzania kwa ujumla hivyo mnahitaji vinahitajika umakini mkubwa.

Amewataka wanahabari kufanya kazi huku wakitanguliza Uzalendo wa Taifa la Tanzania mbele kwani watakapo kwenda kinyume wataharibu Amani iliyopo na mataifa jirani wataitazama nchi kwa mtazamo mwingine

'' Hakuna mtu mwingine atakayetoka nje ya nchi kuja kutusaidia kujenga nchi ni sisi wenyewe tutangulize maslahi ya Taifa zungumzeni mambo mema kwaajili ya nchi yenu'' Alisema Rais. Amesema katika nchi ya Tanzania vyombo vya habari vilivyopo vinatakiwa kuizungumzia nchi vyema hivyo wanahabari wote
Wanao wajibu wa kuzungumza mambo chanya bila kupindisha ukweli wala kumuonea mtu yeyote.

Pia amewataka Watanzania kila mmojawapo anapoingia ofisini kwake afanye kazi kwa ajili yake na kwa maslahi ya Taifa lake akitanguliza uzalendo ,'' Miaka ijayo tunataka kuwa na mabilionea, wanyabiashara wakubwa, wakulima na wafugaji katika nchi yetu wanaofanya kazi na kulipa kodi ya serikali watakaotambuliwa kimataifa kwamba wanatoka Tanzania'' Amesema Magufuli.


Kituo cha Luninga cha Chanel ten na African Media group, vya Jijini Dar es salaam, vyote hivyo vinamilikiwa na Chama cha Mapinduzi(CCM) nchini

TRC YAWAPA SHAVU WASANII KUTEMBELEA MRADI WA RELI YA KISASA YA STARDARD GAUGE

$
0
0
*Wasanii wapewa fursa adhim kutembelea mradi wa standard garge

Na Khadija Seif, Globu ya Jamii.

Shirika la reli nchini (TRC) limetoa nafasi kwa wasanii kutembelea mradi wa reli ya kisasa ya Standard Gauge ili kujionea unavyoendelea. Mradi huo wa reli ya Kisasa ya Standard Gauge umeanzia jijini Dar es Salaam na kuelekea Morogoro utarahishisha usafiri wa abiria na mizigo, pia inatarajia kukuza biashara kati ya Tanzania na nchi Jirani kama vile Burundi, Rwanda na DRC kwa kuwa baadaye itaendelezwa kwenda hadi nchi zote zilizoko mpakani mwa Tanzania. Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Mtendaji Mkuu wa shirika la reli nchini (TRC) Jamila Mbarouk amesema ni fursa adhimu kwa wasanii pamoja na waandishi wa habari kwa pamoja kupanda treni hiyo kwa lengo la kuangalia mradi huo uliweza kujengwa kwa awamu mbali mbali.

Mbarouk amesema Safari hiyo itasaidia kutangaza utalii uliopo ndani hasa kuwepo kwa treni hiyo ya umeme ikiwa na uwezo wa kubeba mizigo ya tani elfu 10 huku iikiwa na spidi ya kilomita 160 kwa saa. "Shirika la reli (TRC) limewapa kipaumbele wasanii, wachoraji, wacheza mpira, Washehereshaji (MC), Waimbaji watakuwa mabalozi wazuri katika kuutangazia umma treni hiyo kukagua Standard Garge mpya itakayotoka Dar es salaam hadi Morogoro" alisema Mbarouk.

Aidha ameeleza treni hiyo imeitengeneza kwa pesa za watanzania kutokana na kodi zilizokusanywa. Mbarouk ametoa wito kwa wananchi na wafanyabiashara kulipa kodi ili iweze kusaidia uchumi wa Tanzania maana bila kodi hakuna maendeleo. Kwa upande wake Msanii wa filamu nchini Steve Nyerere amepongeza uongozi wa Shirika la Reli (TRC) kwa kuwapa fursa wasanii na kutambua mchango wao katika jamii.

"Mkuu wa mkoa Paul Makonda anakaribisha kwa wote wanaohitaji mikopo aliyohaidi wakati wa Mkutano wa wasanii wote nchini kuweza kupata mkopo huo utakaowezesha kufanya kazi kwa weledi mzuri ili kukuza tasnia zote nchini." alisema Nyerere. Ameongeza kuwa ni vyema wasanii kuendelea kutangaza mema yote yanayofanywa na rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kuwaletea maendeleo Watanzania kwa kuwa wao ni vioo vya jamii na wananguvu kweli kuleta mabadiriko.
  Kiongozi wa Wasanii, Steve Nyerere akuongea na wanahabari kuwaelezea madhumuni ya Safari ya wasanii wote katika wote Februari 7, 2019 kutembelea mradi wa Reli ya Kisasa ya reli ya Kisasa ya Standard Gauge inayoanzia Dar es Salaam na kuelekea Morogoro. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.   Kaimu Mtendaji Mkuu wa shirika la reli nchini (TRC) Jamila Mbarouk (kulia) akiongea na wanahabari jinsi walivyoweza kudhamini wasanii hao kutembelea Mradi wa mradi wa Reli ya Kisasa ya reli ya kisasa ya Standard Gauge inayoanzia Dar es Salaam na kuelekea Morogoro ambapo amesema kuwa wametoa nafasi hiyo ili wasanii wakienda, warudi na watoe ushuhuda wa kweli kwa wananchi maana wao ni kioo cha jamii.
Kiongozi wa Bendi ya Twanga Pepeta Asha Baraka ambaye ni mwakilishi wa wamiliki na wasanii wa bendi za muziki wa Dance akitoa machache mbele ya wanahabari.
Msanii wa Muziki wa Taarabu Khadija Kopa akitoa msisitizo wa wasanii kuendelea kumuunga mkono rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutangaza yale mazuri ambayo amekuwa akiyafanya katika kusukuma kurudumu la maendeleo Tanzania.

IGP SIMON SIRRO AMEFANYA MABADILIKO YA MAKAMANDA WA POLISI WA MIKOA

WAZIRI WA KILIMO AKUTANA NA BALOZI WA UINGEREZA NCHINI

$
0
0
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akizungumza na mgeni wake Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Sarah Cooke alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dodoma, Jana tarehe 4 Januari 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga, Naibu Mawaziri wa kilimo Mhe Innocent Bashungwa na Mhe Omary Mgumba, pamoja na wataalamu wa wizara ya kilimo wakizungumza na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Sarah Cooke alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dodoma, Jana tarehe 4 Januari 2019.
Pichani ni Naibu mawaziri wa kilimo Mhe Innocent Bashungwa (Kulia) na Mhe Omary Mgumba, wakifatilia kikao kazi kilichoongozwa na Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga wakizungumza na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Sarah Cooke alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dodoma, Jana tarehe 4 Januari 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akimsikiliza mgeni wake Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Sarah Cooke akizungumza kwenye kikao kazi wakati alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dodoma, Jana tarehe 4 Januari 2019.

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma

Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. SARAH COOKE, jana tarehe 4 Januari 2019 amemtembelea Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga na kufanya nae mazungumzo yenye lengo la kuongeza na kuimarisha Ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na Uingereza katika sekta ya kilimo.

Katika mazungumzo hao, Mhe Hasunga na Bi. COOKE wamekubaliana kuongeza kasi ya Ushirikiano baina ya nchi hizo mbili, makubaliano ambayo yatasaidia uwezekano wa kasi ya ukuaji wa sekta ya kilimo kwa nchi zote mbili.

Katika kikao kazi hicho Waziri Hasunga amemueleza Balozi huyo kuwa serikali ya Tanzania imeanza zoezi la utambuzi wa wakulima nchini kwa kuwaandikisha ambapo mpaka sasa wakulima wa zao la Tumbaku wamekwisha andikishwa.

Hasunga alisema kuwa lengo la zoezi hilo la uandikishaji ni kuimarisha utambuzi wa wakulima ili serikali iweze kuwahudumia kwa weledi wakulima kote nchini kupitia pembejeo mbalimbali za kilimo ili kuondokana na wakulima hewa ambao wanatumia mwanya huo kuiibia serikali.

Vilevile amemueleza Balozi huyo kuwa serikali imejipanga kuimarisha sekta ya utafiti wa kilimo nchini jambo litakaloongeza tija na manufaa makubwa kwa wakulima nchini.

Katika mazungumzo hayo, Mhe Hasunga amemueleza Bi COOKE namna ambavyo serikali ya Tanzania imejipanga kuimarisha masoko ya ndani na nje ya nchi kwa wakulima.

Bi. COOKE, kwa upande  wake amefurahishwa na jinsi ambavyo Waziri wa Kilimo pamoja na wasaidizi wake wanapambana kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli katika kuimarisha sekta ya kilimo sambamba na kuboresha masoko ya wakulima nchini.

Balozi huyo amemueleza waziri wa kilimo kuwa Uingereza itaendeleza maradufu ushirikiano na Tanzania kwani ni nchi yenye Amani na utulivu mwingi kwa wananchi wake.

MADIWANI MOSHI KUCHUNGUZA TUHUMA ZA UBADHILIFU WA FEDHA KITUO CHA AFYA PASUA

$
0
0
 Mstahiki Meya wa manispaa ya Moshi,RAymond Mboya akiwa aameongozana na Madiwani wa Halmashauri hiyo kukagua shughuli za ukarabati unaoendelea katika kituo cha Afya cha Pasua mjini Moshi.
 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi,Raymond Mboya akijaribu kuzungusha moja ya vitanda vilivyowekwa katika wodi ya wazazi katika kituo hicho. 
 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi ,Raymond Mboya akizungumza mara baada ya kutembelea kituo cha Afya cha Pasua kujionea shughuli za ukarabati wa kituo hicho zinavyoendelea. 
 Baadhi ya wanachama wa chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) wakiwa katika kituo hicho kuunga mkono shughuli za maendeleo . 
 Diwani wa kata ya Bomambuzi ,Juma Raibu kilipo kituo hicho cha Afya akizungumza mara baada ya ukaguzi . 
 Moja ya jengo la kituo hicho likiwa katika hatua za mwisho kukamilika. 
 Shughuli za upakaji rangi ikiendelea kwa baadhi ya majengo katika kituo hicho. 
 Baadhi ya majengo mapya yaliyoongezwa katika kituo hicho cha Afya Pasua .


Na Dixon Busagaga,wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.


BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi limeeleza kufanyia kazi tuhuma za ukiukwaji wa taratibu katika mradi wa ukarabati wa Kituo cha Afya cha Pasua unaotajwa kupelekea upotevu wa fedha .

Kauli hiyo imetolewa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi,Raymond Mboya wakati wa ziara ya Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi walipotembelea kituo cha Afya cha Pasua kujionea ukarabati unavyoendelea.

“Kuna matatizo na hayo matatizo nimesema nije kwanza kuangalia ,kwa kuwa bado hili swala liko kwenye vikao vya ndani tutatoa taarifa yakikamilika kwenye vikao kwanza, ni kwamba kuna taratibu hazijakaa vizuri kwenye mchakato mzima wa ukarabati wa kituo cha afya.”alisema Mstahiki Mboya .

Alisema fedha zilizotumika katika ukarabati wa kituo hicho ni fedha za serikali zinazotokana na kodi inayokusanywa kutoka kwa wananchi na kwamba zinapotumika ni lazima baraza la Madiwani kufuatilia na kujiridhisha kama zimetumika kwa utaratibu uliokusudiwa.

“Hizi fedha ni kodi zetu ,ambazo wakati mwingine zinaitwa fedha za serikali sasa zinapotumika hapa ni lazima tuhakikishe zinatumika kwa utaratibu uliokusudiwa na kwa utaratbu ambao hauta leta mashaka wala tatizo kwa hiyo tusubiri mchakato na taratibu za vikao zitakapo kamilika tutawajulisheni”alisema Mboya 

Akizungumzia kuhusu ukarabati wa Kituo hicho ,Mstahiki Mboya alisema hakuna mradi unaofanyika mahala popote bila ya kupitishwa katika vikao halali vya baraza la Madiwani na kwamba hadi kuanza kwa ukarabati kwa kituo hicho taratibu zilifuatwa.

“Tangu mwaka 2013 tulikuwa tunatenga fedha kwenye Bajeti ya ujenzi wa vituo vya Afya kikiwemo kituo cha Afya cha Pasua ,na ilikua ni sehemu ya upasuaji ,wodi ya kujifungulia kina mama,chumba cha mionzi ya X-ray na chumba cha kuhifadhi maiti”alisema Mboya .

“Tumekuwa tukitenga na kwa kuwa ukarabati ulitakiwa uwe mkubwa ,tumeendelea kutenga miaka yote na ilivyoingia serikali ya awamu ya tano ikaingia na mkakati wa kuboresha vituo vya Afya na manispaa ya Moshi tulifanikiwa kwa sababu ilikuwa kwenye mpango”alisema Mboya.

Alisema katika ukarabati huo serikali imetoa kiasi cha Sh Mil 400 ikiwa ni mchango wake huku fedha nyingine zikitakiwa kutolewa na Halmashauri hali iliyowalazimu kubadilisha matumizi ya fedha kwa baadhi ya vifungu ili zikamalizie maeneo ambayo bado hayajakamilika katika kituo hicho.

“Kukamilika kwa kituo hichi kutawezesha wananchi wa maeneo ya kata ya Bomambuzi ,Pasua ,Matindigani na Kaloleni waweze kupata huduma ambayo ni ya kiwango na hasa tuilenga kwe nye eneo la wodi ya wazazi.”alisema Mboya .

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Pasua ,Juma Raibu alisema ukarabati wa vituo vya Afya ni mpngo mkakati wa taifa kwa ajili ya kuwasaidia wananchi na kupunguza changamoto zilizokuwa zikiikabili sekta ya Afya nchini.

“Mimi kama Diwani nilipewa maelekezo kwa barua kwamba niunde kamati mbalimbali za kuweza kusaidia ukarabati wa kituo hiki uweze kuendelea ,kamati ya kwanza niliambiwa niunde ya manunuzi,kamati ya mapokezi na kamati ya ujenzi ili wazawa wa eneo hili wawe ni sehemu ya wasiamamizi wa mradi huu”alisema Raibu.

Katika ziara hiyo Globu ya Jamii ilishuhudia wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakiwa wamoja katika kukagua maeneo mbalimbali ya kituo hicho .

Mstahiki Meya ,Raymond Mboya(Chadema) akazungumzia hali hiyo na kuungwa mkono na Diwani wa kata ya Kilimanjaro ,Priscus Tarimo wakieleza kuwa linapofika suala la maendeleo itikadi za kisiasa huwekwa pembeni.

“Hii inaashiria Moshi tumekomaa ,nah ii inaashiria kwamba kwa nini inaitwa Moshi ,kwamba baada ya uchaguzi kauli yetu ni maendeleo ,anayeleta siasa huwa hatumpia nafasi ,na ndio maana mimi kama Meya kwenye baraza nawaambia tunaongea lugha ya maendeleo”alisema Mboya.

Naye Diwani Tarimo akaeleza juu ya hali hiyo “Mazingira ya ya kisiasa katika mkoa wa Kilimanjaro hasa katika manispaa ya Moshi ni tofauti sana kutokana na uelewa mkubwa wa watu na inawezekana kabisa madiwani wa pande zetu tukakaa pamoja na jambo linalohusu maendeleo tukalisimamia kwa pamoja.

TANESCO,ABB WAENDELEA KUFUNGA TRANSFOMA YA MEGAWATI 240 KITUO KIKUU CHA UBUNGO

$
0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

TIMU ya wataalamu wa Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) kwa kushirikiana na Mkandarasi ABB wa nchini Switzerland, wameendelea na kazi ya kufunga transfoma yenye uwezo wa Megawati 240 katika Kituo Kikuu cha Kupoza na Kusambaza umeme cha Ubungo jijini Dar es Salaam.
 
Kwa mujibu wa taarifa ya TANESCO iliyoitoa leo imesema transfoma hiyo iliingia hapa nchini Januari 28, 2019 na lengo ni kuendelea kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme wa uhakika na kuleta ufanisi katika usambazaji wa umeme katika jiji la Dar es Salaam na Pwani.

Akielezea uwezo wa Transfoma hiyo, Mkuu wa Kituo cha Kupoza na Kusambaza umeme Ubungo, Mhandisi Joseph Msumali amesema transfoma hiyo yenye uwezo wa kusukuma takribani Megawati 240 kutoka kwenye msongo wa kilovoti 220 kuelekea Msongo wa kilovoti 132 kwa ajili ya usambazaji na matumizi ya nishati ya umeme katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.
 Ufungaji wa Transfoma ukiendelea

 
Viewing all 46379 articles
Browse latest View live




Latest Images