Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

UJUMBE WA ALEX MSAMA KWA WASANII KUELEKEA KUANZA KWA TAMASHA LA PASAKA

$
0
0
WAKATI Tamasha la Pasaka likijiandaa kuwasha moto katika Jiji la Dar es Salaam, Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion na muandaaji wa Tamasha la Pasaka  Alex Msama ametoa mwito kwa wasanii mbalimbali nchini wakiwamo wa muziki wa Injili kuhakikisha wanafuata na kuheshimu Sheria za Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA).

Msama amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumzia msimu mpya wa Tamasha la Pasaka ambalo linatarajia kuanza Aprili 21,2019.Amefafanua tamasha hilo litaanzia Katika Jiji la Dar es Salaam na kauli mbiu ya tamasha hilo inasema Umoja na upendo huduma amani ya nchi yetu.

Kuhusu wasanii kufuata Sheria za BASATA, Msama ametoa mwito kwa wasanii kuiheshimu Baraza hilo na kwamba wasanii ambao watashiriki ni wale ambao wamejisajili na kutambuliwa kisheria.

Kuhusu tamasha hilo amesema BASATA tayari wametoa  maelekezo yenye lengo kuhakikisha tamasha hilo linafanikiwa. "Siku zote usipokuwa na msimamizi huwezi kufanya vizuri, Wasanii wengi wanakuwa na dharau, bila BASATA tamasha hili lingekuwa limekufa siku nyingi", amesema Msama

Katika hatua nyingine, Msama amesema kuwa wapo kwenye mazungumzo na wasanii kutoka mataifa ya nje, kuhakikisha nao wanapata mualiko ili  washiriki tamasha hilo.

"Wasanii wote ambao watashiriki ni wale wanaoiheshimu BASATA, ni vema wasanii wakahakikisha wanafuata sheria katika kufanya kazi zao za sanaa", amesema Msama .Msama muda si mrefu wataanza kutaja majina ya wasanii ambao watashiri tamasha hilo na kueleza kwa mwaka huu tamasha hilo litafanyika pia katika Jiji la Dodoma.

Wakati huo huo Msama amesema katika kipindi cha tamasha la Pasaka watatumia pia nafasi hiyo kuendelea kumuombea Rais  Dk.John Magufuli, Makamu wa  Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na viongozi wa ngazi mbalimbali wa Serikali ya Awamu ya Tano.
 Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotions na muandaaji wa Tamasha la Pasaka Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari leo alipokuwa akifafanua mambo mbalimbali kuhusu maendeleo ya Tamasha la Pasaka jijini Dar es salaam,ambalo linatarajiwa kuanza kurindima Aprili 21,2019.
 Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion na muandaaji wa Tamasha la Pasaka Alex Msama akitoa ufafanuzi zaidi kuhusiana na wasanii watakaoshiriki kwenye tamasha hilo ambalo kwa kawaida hufanyika kila mwaka,mbele ya waandishi wa habari leo, jijini Dar es salaam kushoto ni Mratibu wa Tamasha hilo Jimmy Charles.
Waandishi wa Habari wakimsikiliza  Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion na muandaaji wa Tamasha la Pasaka Alex Msama alipokuwa akizungumza nao leo jijini Dar kuhusu maendeleo ya maandalishi ya tamasha la pasaka na ujumbe muhimu kwa wasanii/waimbaji watakaoshiriki tamasha hilo.

RAIS DKT.MAGUFULI AWAAPISHA MAJAJI 6 WA MAHAKAMA YA RUFANI NA MAJAJI 15 WA MAHAKAMA KUU TANZANIA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Jaji Winnie Korosso Kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania. Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini  Dar es Salaam. Januari 29, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Jaji Sahel Barke Kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania. Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini  Dar es Salaam. Januari 29, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Jaji Lugano Samson Mwandambo Kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania. Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini  Dar es Salaam Januari 29, 2019.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Jaji Dkt. Mary Levira Kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania. Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini  Dar es salaam. Januari 29, 2019.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Jaji Ignus Paul Kitusi Kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania. Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini  Dar es salaam. Januari 29, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Jaji Rehema Kerefu Sameji Kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania. Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini  Dar es salaam Januari 29, 2019.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapish Bw. John Rugalema Kahyoza Kuwa Jaji wa Mahakama ya Kuu . Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini  Dar es salaam Januari 29, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapish Bi. Susan Bernard Mkapa Kuwa Jaji wa Mahakama ya Kuu . Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini  Dar es salaam Januari 29, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapish Bw. Fahamu Hamidu Mtulya Kuwa Jaji wa Mahakama ya Kuu . Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini  Dar es salaam Januari 29, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapish Bw. Cyprian Phocas Mkeha Kuwa Jaji wa Mahakama ya Kuu . Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini  Dar es salaam Januari 29, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapish Bw. Willbard Richard Mashauri Kuwa Jaji wa Mahakama ya Kuu . Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini  Dar es salaam. Januari 29, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapish Bw. Dunstan Beda Ndunguru Kuwa Jaji wa Mahakama ya Kuu . Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini  Dar es salaam Januari 29, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapish Bw. Seif Mwinshehe Kulita Kuwa Jaji wa Mahakama ya Kuu . Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini  Dar es salaam Januari 29, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapish Bi. Upendo Elly Madeha Kuwa Jaji wa Mahakama ya Kuu . Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini  Dar es salaam Januari 29, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapish Bw. Yohane Bokobora Masara Kuwa Jaji wa Mahakama ya Kuu . Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini  Dar es salaam. Januari 29,2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapish Bw. Mustapha Kambona Ismail Kuwa Jaji wa Mahakama ya Kuu . Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini  Dar es salaam. Januari 29,2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapish Bw. Athumani Matuma Kirati Kuwa Jaji wa Mahakama ya Kuu . Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini  Dar es salaam. Januari 29,2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapish Bw. Zepherine Nyalugenda Galeba Kuwa Jaji wa Mahakama ya Kuu . Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini  Dar es salaam. Januari 29,2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapish Bw. Dkt. Ntemi Nimilwa Kilikamajenga Kuwa Jaji wa Mahakama ya Kuu . Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini  Dar es salaam. Januari 29,2019.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapish Bi. Dkt. Juliana Laurent MasaboKuwa Jaji wa Mahakama ya Kuu . Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini  Dar es salaam. Januari 29,2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapish Dkt. Lilian Mihayo Mongella Kuwa Jaji wa Mahakama ya Kuu . Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini  Dar es salaam. Januari 29,2019.
 Majaji wapya wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu Wakiapa kiapo cha uadilifu kwa Viongozi wa Umma mbele ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwaapisha  Ikulu Jijini  Dar es salaam. Januari 29,2019.
 Wakuu wa Wilaya  wapya 2 wa Wilaya ya Mwanga  na Tarime pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri 10 Wakiapa kiapo cha uadilifu kwa Viongozi wa Umma mbele ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwaapisha Majaji wapya 6 wa Mahakama ya Rufani na  Majaji 15 Mahakama Kuu Ikulu Jijini  Dar es salaam. Januari 29,201
Majaji wapya wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu Wakitia saini hati za  kiapo cha uadilifu kwa Viongozi wa Umma mbele ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwaapisha  Ikulu Jijini  Dar es salaam. Januari 29,2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kuwaapisha  Majaji wapya 6 wa Mahakama ya Rufani na Majaji wapya 15 wa Mahakama Kuu ,Ikulu Jijini  Dar es salaam. Januari 29,2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. John Kijazi, Waziri wa Sheria Profesa Palamagamba Kabudi, Waziri wa TAMISEMI Seleman JaffO, Jaji Kiongozi Dkt. Eliezer Fereshi pamoja na Majaji wapya 6 wa Mahakama ya Rufani  mara baada ya kuwaapisha Majaji hao na Majaji wapya 15 wa Mahakama Kuu ,Ikulu Jijini  Dar es salaam. Januari 29,2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. John Kijazi, Waziri wa Sheria Profesa Palamagamba Kabudi,Waziri wa TAMISEMI Seleman JaffO, Jaji Kiongozi Dkt. Eliezer Fereshi pamoja na Majaji wapya 6 wa Mahakama ya Rufani Majaji wapya 15 wa Mahakama Kuu,Watumishi mbalimbali wa Mahakama mara baada ya kuwaapisha Majaji hao. Ikulu Jijini  Dar es salaam. Januari 29,2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. John Kijazi, Waziri wa Sheria Profesa Palamagamba Kabudi,Waziri wa TAMISEMI Seleman JaffO, Jaji Kiongozi Dkt. Eliezer Fereshi pamoja na Majaji wapya 6 wa Mahakama ya Rufani Majaji wapya 15 wa Mahakama Kuu na Viongozi wa Madhehebu mbalimbali ya Dini  mara baada ya kuwaapisha Majaji hao. Ikulu Jijini  Dar es salaam. Januari 29,2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. John Kijazi, Waziri wa Sheria Profesa Palamagamba Kabudi,Waziri wa TAMISEMI Seleman JaffO, Jaji Kiongozi Dkt. Eliezer Fereshi pamoja na Majaji wapya 6 wa Mahakama ya Rufani Majaji wapya 15 wa Mahakama Kuu, Wakuu wa Wilaya 2 na Wakurugenzi 10 wa Halmashauri, Mara baada ya kuwaapisha Majaji. Ikulu Jijini  Dar es salaam. Januari 29,2019.
Wakuu wa Wilaya  wapya 2 wa Wilaya ya Mwanga  na Tarime pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri 10 wakiwa katika hafla ya uwaapisho wa Majaji 6 wa Mahakama ya Rufani na Majaji 15 wa Mahakama Kuu .Ikulu Jijini  Dar es Salaam Januari 29,2019.
PICHA NA IKULU

OFISA TRA AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA KUPOKEA RUSHWA YA SHILINGI MILIONI 10

$
0
0
Na Karama Kenyunko globu ya Jamii

OFISA Msaidizi wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Kituo cha Gerezani Kariakoo, Dar es Salaam, Charles Kapongo  amefikishwa katika Mahakama ya Wilayaya Ilala akikabiliwa na tuhuma za kupokea rushwa ya Sh. milioni 10.

Akisoma hati ya mashtaka wakili wa serikali kutoka Takukuru, Dumas Muganyizi amedai  mbele ya Hakimu Mkazi, Flora Haule kuwa,  Januari 25, mwaka huu katika maeneo ya ofisi za TRA zilizopo Gerezani Kariakoo ndani ya Wilaya ya Ilala,  mshtakiwa alitenda kosa. 

Imedaiwa siku hiyo mshtakiwa Kapongo akiwa mwajiriwa na TRA, alipokea rushwa ya USD ,4200 Ambazo ni Sawa na Sh.  milioni 10, kutika kwa Naibu Magala ambaye ni mwajiriwa wa kampuni ya Ushauri  ya Hakha Business Accounting.

Wakili Flora Anaendeleaje kudai kuwa,  fedha hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya kushawishi kupunguza makadirio ya kodi ya kampuni hiyo,  kutoka Sh 45,571,664 kwenda Sh.  milioni nane kitendo ambacho ni kinyume na maadili yake ya kazi.

Hata hivyo,  mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo na yuko nje kwa dhamana baada ya kufanikiwa kukamilisha masharti yaliyowekwa Na Mahakama ambapo alitakiwa kuwa na wadhamini kati yao mmoja atoke kwenye taasisi yoyote inayotambulika Na wote wametakiwa kusaini bondi ya Sh.  Milioni tano.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi bado haujakamilika na kesi hiyo itatajwa Februari 11.2019
 FISA Msaidizi wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Kituo cha Gerezani Kariakoo, Dar es Salaam, Charles Kapongo akifishwa katika Mahakama ya Wilayaya Ilala akikabiliwa na tuhuma za kupokea rushwa ya Sh. milioni 10.
 

Kampuni ya Utalii ya Wengert Windrose Safari yatoa mamilioni kwa vijiji 12 Longido

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Longido Frank Mwaisumbe akiwa na baadhi ya viongozi wa vijiji na wafanyakazi wa kampuni ya Wingert Windrose Safaris baada ya kukabidhiwa hundi.

Na Ripota Wetu,Arusha.

Arusha.Kampuni ya uwindaji wa kitalii ya Wengert Windrose Safaris imetoa kiasi cha sh 36 milioni kwa Vijiji 12 vinavyozunguka kitalu cha uwindaji cha Lake Natron North wilayani Longido ili kuchangia huduma na miradi ya maendeleo.

Meneja mahusiano ya kampuni hiyo, Clarence Msafiri alimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Longido,Frank Mwaisumbe mfano wa hundi kwa niaba ya vijiji hivyo kisha kukabidhi hundi halisi yenye thamani ya Sh 3 milioni kwa kila kijiji.

Vijiji vilivyonufaika na fedha hizo ni Mairowa,Magadini,Gelai,Wosiwosi,Ngoswaki na Matale A, Origrai,Matele B,Lumbwa ,Ilnjakitsapukin ,Kimwati na Alaililai ambapo pia kampuni hiyo imetoa fedha nyingine kiasi cha dola 5000 zaidi ya sh 11 milioni kuchangia huduma za jamii kupitia ada ya kitalu chake cha uwindaji.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa hundi hiyo, Mkuu huyo wa Wilaya, Mwaisumbe aliwataka viongozi wa vijiji kusimamia vizuri matumizi ya fedha hizo hasa katika kipindi hiki ambacho ujenzi wa madarasa unaendelea kwa kasi ili kutoa nafasi kwa watoto wa jamii hiyo ya wafugaji kupata fursa ya elimu.

Mwaisumbe alisema anaishukuru sana, Kampuni ya Wengert kwa kuwa mdau mkubwa wa maendeleo katika wilaya hiyo, kutokana na kujitoa kuchangia shughuli nyingi za maendeleo katika wilaya hiyo.“Naishukuru kampuni hii kwa kuonesha uzalendo na kuheshimu makubaliano kusaidia vijiji na naamini mtaendelea kushirikiana katika kuhakikisha Longido tunakua na uhifadhi endelevu unaozingatia ustawi wa jamii inazunguka maliasili zetu,”alisema Mwaisumbe

Meneja Mahusiano wa kampuni ya Wenget Windrose Safaris Limited,Clarence Msafiri alisema wataendelea kushirikiana na vijiji vinavyowazunguka kuchangia huduma za jamii.Msafiri alisema licha ya fedha hizo, kampuni hiyo pia itaendelea kutoa ajira kwa vijana wa jamii inayowazunguka lakini pia tayari wametoa kiasi cha dola 5000 sawa ni Sh 11.5 milioni ambayo ni malipo kwaajili ya kila kitalu kila mwaka.

Msafiri alitaja vijiji vilivyonufaika kuwa ni Mairowa,Magadini,Gelai,Wosiwosi,Ngoswaki na Matale A,vijiji vingine ni Origra,Matele B,Lumbwa ,Ilnjakitsapukin ,Kimwati na Alaililai.Akizungumza kwa niaba ya vijiji hivyo, Diwani wa Kata ya Mundarara ,Alais Mushao alisema mchango wa uhifadhi ni muhimu katika kuinua na kuchangia shughuli za maendeleo na kuitaka kampuni hiyo kufanya kazi zake kwa kutunza mazingira ili rasilimali hizo zinufaishe vizazi vijavyo.


Kampuni ya Wingert Windrose Safaris ni kati ya kampuni zinazomilikiwa na taasisi ya Friedkin Conservation Fund(FCF) ambayo pia inamiliki kampuni ya Mwiba Holdings iliyowekeza hifadhi ya Makao na Kampuni ya Game Tracking Safaris(TGTS) ambayo imewekeza maeneo kadhaa nchini.

ALIYEKUWA MKURUGENZI MKUU NIDA DICKSON MAIMU SASA AFUNGULIWA MASHTAKA 100,APANDISHWA KIZIMBANI

$
0
0
Na Karama Kenyunko globu ya Jamii, 
BAADA ya kuachiwa huru na kukamatwa tena jana mchana,  aliyekuwa  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho (NIDA), Dickson Maimu na wenzake watano wamepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka 100 mapya yakiwemo mashtaka 25 ya utakatishaji fedha.

Wakili wa Serikali Wankyo Saimon akisaidiana na Wakili kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai amewataja washtakiwa wengine mbali na Maimu kuwa ni Meneja Biashara wa (NIDA), Aveln Momburi,
Mkurugenzi wa Kampuni ya Aste Insurance Brokers,  Astery Ndege, Ofisa Usafirishaji, George Ntalima, Mkurugenzi wa Sheria, Sabina Raymond na Xavery Kayombo.


Katika mashtaka hayo ambayo yamesomwa mbele ya Hakimu Mkazi Salum Ally,  washtakiwa wanakabiliw Na mashtaka 22 ya kughushi, mashtaka 43 ya kutumia nyaraka kwa lengo la kumdanganya mwajiri, mashtaka mawili ya kula njama, mashtaka 25 ya kutakatisha fedha na mashtaka matano ya kuisababishia hasara NIDA.

Pia washtakiwa wanakabiliwa Na mashtaka mawili ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na shtaka moja la matumizi mabaya ya madara lipo moja ambalo linamkabili  Maimu na Sabina. 

Katika shtaka la kwanza la kula njama Maimu, Ndege na Ntalima wanadaiwa, kati ya Julai 19, 2011 na Agosti 31,2015 wakiwa maeneo tofauti tofauti ndani ya Jiji la Dar es Salaam walikula njama ya kufanya udanganyifu wa Sh bilioni 1.175 dhidi ya NIDA.

Pia Maimu anatuhumiwa kutakatisha fedha kiasi cha sh bilioni 1,175,785,600.93  kati Julai 19,2011 na Agosti 31, 2015  ambapo anadaiwa kujihusisha moja kwa moja kuhamisha fedha hizo huku akijua ni zao la kosa la kughushi.
Katika shtaka jingine,  Maimu na  Raymond wanatuhumiwa November 7, 2011 wakiwa Makao Makuu ya NIDA, Kinondoni jijini Dar es Salama walitumia madaraka yao vibaya na kusababisha  huo cha sheria  (Law School) Dar es Salaam na Kampuni ya Gotham International Ltd kupata faida ya Sh .899,935,494.

Imedaiwa kati ya Novemba 12, 2011 na Mei 12, 2015, Maimu na Momburi wakiwa makao makuu ya NIDA, Kinondoni akiwa Mkurugenzi na Meneja wa biashara walishindwa kusimamia ujenzi wa jengo lililopo plonti namba 39A na kuikuisababishia mamlaka hiyo hasara ya Sh 402,210,885.02.

Aidha imeendelea kudaiwa kuwa kati ya Julai 19,2011 na Agosti 12, 2011,  washtakiwa Maimu na Ntalima wakiwa Makao Makuu ya NIDA walitumia nyaraka ya uongo kwa nia ya kumdanganya mwajiri wao kuwa walitumia stakabadhi ya malipo namba 0034 na namba 0035 kuilipa Kampuni ya Aste Insurance Brokers Ltd dola za Marekani 10,300.00.

Hata hivyo, washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama ya Kisutu haina Mamlaka ya kusikiliza kesi za Uhujumu uchumi,  hadi Mahakama Kuu kwa kupata kibali kutoka kwa DPP. 

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo umeshakamilika na tayari wamewasalisha maelezo ya mashahidi Mahakama Kuu.

Katika kesi hiyo washtakiwa, Momburi na Raymond wao hawajapatikana na kosa la kutakatisha fedha, kwa hiyo mashtaka yao yanadhaminika, hivyo upande wa utetezi uliiomba mahakama kuwapatia washtakiwa hao dhamana. 

upande wa mashtaka ulieleza kuwa dhamana iko wazi kwa washtakiwa hao, lakini si hapa ni Mahakama Kuu kama wanataka wanaweza kupeleka maombi ya dhamana Mahakama Kuu.

"Njia pekee ni wapeleke maombi yao Mahakama Kuu yakasikilizwe na kutolewa uamuzi kwa sababu sisi hatuna Mamlaka ya kusikiliza kesi hii," amsema hakimu Ally 

Kesi hiyo imeahirishwa hadi February 12 mwaka huu, ambapo washtakiwa watasomewa maelezo ya mashahidi (Committal)

Mchango wa biashara za mtandaoni katika ukuaji wa biashara Afrika

$
0
0
Mchango wa biashara za mtandaoni katika ukuaji wa biashara Afrika

Waafrika milioni 400 wanatumia intaneti.

Mahitaji ya Waafrika ni sawa na kwingineko duniani kote. Wanahitaji bidhaa nzuri, bora na zenye bei nafuu.

Licha ya kutazamwa kwa mitazamo tofauti na mataifa mengi yaliyoendelea duniani, Afrika imeonyesha kuwa shughuli nyingi zinaweza kufanyika na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa. Kwa miaka kadhaa sasa makampuni makubwa kutoka Ulaya, Marekani na Asia yamefungua matawi ya biashara zao na kufanikiwa. Vilevile, maelfu ya biashara mpya zimekuwa zikianzishwa na kufungua fursa nyingi katika sekta mbalimbali.

Afrika ni ya pili kwa kuwa na watumiaji wengi wa mtandao wa intaneti ukiachana na China, ambapo kwa sasa ina watumiaji wa mtandao wa intaneti takribani milioni 400, ambapo idadi ya Waafrika wote ni zaidi ya bilioni 1.2.
Idadi hiyo kubwa ya Waafrika wanaotumia intaneti imekuja na fursa ya biashara ya mtandaoni ambayo imekuwa ikifanyika kwa miaka takribani 20 sasa katika nchi za Marekani na Ulaya. Aina hii ya biashara inahusisha uuzaji na ununuzi wa bidhaa kutoka kwa wauzaji tofuati kwa njia ya mtandao katika sehemu moja.

Katika mahojiano yaliyofanywa hivi karibuni baina ya mmojawapo wa waanzilishi na Afisa Mtendaji Mkuu wa Jumia, Bw. Sacha Poignonnec na kampuni ya McKinsey & Company ameelezea kuwa mwanzoni ilikuwa ni vigumu kufanya uamuzi wa kufanya biashara Afrika kutokana na changamoto na ugumu ambao waliambiwa wangekutana nao.

“Wakati tunaanza shughuli zetu kwa mara ya kwanza kabisa jijini Lagos nchini Nigeria, tulifungua tovuti yetu hakuna aliyekuwa anatujua lakini wateja walinunua simu za mkononi. Nilishangazwa sana na ile shauku ya wateja kununua bidhaa, tena za gharama ya juu. Cha kustaajabisha zaidi tulifanikiwa kuuza bidhaa na kuzipeleka mpaka walipo wateja. Kwa kweli, ilitia moyo kuona mambo mazuri yakitokea kuliko mabaya tuliyoyasikia,” alielezea Bw. Poignonnec.

“Nina matumaini makubwa na biashara ya mtandaoni Afrika kwasababu kitu cha upekee kuhusiana na bara hili ni kwamba tayari nusu ya idadi ya watu wake wameunganishwa. Kati ya watu zaidi ya bilioni 1.2, milioni 400 wanatumia mtandao wa intaneti. Idadi hii ni ya pili duniani ukiachana na China. Hata hivyo, mbali na idadi hiyo bado kuna mazingira magumu ya usambazaji wa bidhaa na huduma. Hii imekuwa ni changamoto kubwa kwa wateja pale wanapohitaji kufanya manunuzi. Lakini, kwa sababu ya matumizi ya simu za mkononi na intaneti, wateja hivi sasa wanao uwezo wa kuzifikia huduma katika njia iliyo rahisi zaidi,” aliongezea.

Bw. Poignonnec aliendelea mbele zaidi kwa kuelezea kuwa tabia za wateja wanaopatikana Afrika hazitofautiani na sehemu zingine. Mahitaji ni yaleyale. Wanahitaji bidhaa nzuri na bora ambazo zinapatikana kwa bei nafuu. Siku zote wateja wanahitaji kuokoa muda na gharama. Katika maeneo mengi ambayo tunafanya shughuli zetu tunawasaidia wateja kuwa na machaguo mengi ya kununua bidhaa kitu ambacho hakipo katika maeneo wanayoishi.

Katika kipindi cha miaka takribani sita tangu Jumia ianze kufanya shughuli zake barani Afrika changamoto kubwa iliyokumbana nayo ni mfumo wa uendeshaji.

Ameelezea kuwa kwa anayeifahamu Afrika vizuri ni kwamba haina mfumo mzuri wa anwani za makazi katika majiji yake mengi. Hivyo basi kwa watoa huduma kama wao ili kuwafikia wateja vizuri ni lazima washirikiane na wauzaji wa nyumbani ambao ndiyo wanayafahamu vizuri maeneo yao. Kwa mfano, mteja anaweza kuagiza bidhaa lakini anwani ya mahali anapoishi inaweza kuwa ni kwa kuelezea majengo yanayopatikana karibu au shughuli maarufu zinazopatikana eneo alilopo.

Kwa hiyo, endapo ukishirikiana na wauzaji sahihi wanaopatikana kwenye eneo hilo na wenye ufahamu sahihi wa maeneo yao utaweza kuwafikia wateja wote kwa urahisi. Lakini mfumo huu pia nao changamoto zake, vingenevyo uwe na mfumo mzuri wa uendeshaji ambao tumeutengeneza. Tunatumia nyenzo na mifumo ya kiteknolojia ambayo tunawapatia ili waweze kuendesha shughuli zao kwa ufanisi, kama vile malipo baada ya bidhaa kufika pamoja na huduma mpaka alipo mteja.

Kuna fursa nyingi endapo waafrika wataamua kuitumia ipasavyo fursa ya biashara kwa njia ya mtandaoni. Tofauti na nchi za Marekani na Ulaya ambapo biashara nyingi huanzia madukani na kuhamia mtandaoni, kwa Afrika wafanyabiashara wengi wanaanzia mtandaoni na kisha hufungua maduka. Sababu kubwa ni kwamba hakuna gharama kufanya biashara mtandaoni.

Ili kujiunga na Jumia kuifanya biashara yako iwepo mtandaoni hauhitaji gharama yoyote kujiunga, hakuna malipo ya kila mwezi au pango la duka, fursa ya kujitangaza na kutafuta masoko ni bure, kuna fursa kubwa ya kuwafikia wateja wengi waliopo maeneo mbalimbali ndani ya muda mfupi pamoja na uhakika wa bidhaa kuwafikia wateja mpaka pale walipo.

Hivyo basi kama mfanyabiashara unaweza ukaanza kidogokidogo mtandaoni, ukawekeza ile faida ndogo unayoipata, baada ya hapo unakua kiasi ambacho unaweza kufungua duka kubwa na kuajiri watu wengi zaidi.

MAGAZETI YA LEO JUMATANO JANUARI 30,2019

KATIBU MKUU WA MAMBO YA NJE AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KWENYE KIKAO CHA MAKATIBU WAKUU WA EAC

$
0
0
Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe (aliyekaa mbele), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye kikao cha maandalizi kabla ya kushiriki kikao cha Makatibu Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kilichofanyika jijini Arusha tarehe 29 Januari 2019. Pamoja na mambo mengine kikao cha Makatibu Wakuu kilipokea na kujadili taarifa mbalimbali zilizowasilishwa kwao na wajumbe wa ngazi ya Wataalam. Kikao cha Makatibu Wakuu kitafuatiwa na kikao cha Baraza la Mawaziri kitakachofanyika tarehe 30 Januari 2019 kwa ajili ya kuandaa Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika tarehe 1 Februari 2019. 
Bw. Stephen Mbundi (katikati), Kiongozi wa kikao cha ngazi ya wataalam ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akitoa taarifa kwa Makatibu Wakuu. Wengine katika picha ni Dkt. Yamungu Kayandabila (kushoto), Naibu Gavana na Bw. Bernard Haule, Kaimu Mkurugenzi, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Evaristo Longopa (wa pili kulia) akichangia jambo wakati wa kikao cha maandalizi ya ushiriki wa Tanzania kwenye kikao cha Makatibu Wakuu kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Wengine katika picha ni Prof. Sifuni Mchome (wa kwanza kulia), Katibu Mkuu, Wizara ya Katiba na Sheria, Prof. Joseph Buchweshaija, Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda na Biashara na Prof. Siza Tumbo, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo. 
Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Aziz Mlima (kulia) akifuatilia kikao hicho akiwa pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina KH. Shaaban 
Wajumbe ambao ni Wataalam kutoka Wizara, Idara na Taasisi mbalimbali za Serikali wakifuatilia kikao 
Kikao kikiendelea 
Wajumbe wengine wakiwa kwenye kikao 
Wajumbe wa kikao wakifuatilia kikao 
Wajumbe kutoak Wizara, Idara na Taasisi za Serikali walioshiriki kikao 
Wajumbe wengine nao wakifuatilia kikao 
Wataalam wa masuala mbalimbali kutoka Wizara, Idara na Taasisi za Serikali wakiwa kwenye kikao 
Wataalam wakinukuu masuala mbalimbali yaliyokuwa yanajadiliwa kwenye kikao hicho 
Kikao kikiendelea 
Kikao kikiendelea

WAKENYA WATUA NCHINI KUJIFUNZA MIRADI YA MAJI TAKA

$
0
0


Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na masuala ya Kijamii nchini (CCI) Tim Ndezi akiwakaribisha wageni kutoka nchini Kenya waliofika Tanzania kwa ajili ya kujifunza masuala mbali mbali yanayohusu Maji Taka kupitia Shirika la CCI na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA). 


Ujumbe huo ulilenga kutembelea na kujionea miradi ya majitaka maeneo ya Vingunguti na Toangoma, Kigamboni jijini Dar es Salaam kwenye miradi maalum ya Maji Taka inayotekelezwa katika maeneo yasiyopimwa na yenye msongamano. Wageni hao ni maofisa wa Serikali ya Kenya kutoka Kampuni ya majisafi na majitaka Nairobi (NCWSC) na Huduma za jamii, Mashirika binafsi na viongozi wa vikundi vya jamii wapo nchini kwa siku 5 wakitembelea Dar es Salaam na Mwanza. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mji Mpya, Kata ya Vingunguti Rahimu Seif Gassi (kulia) kiwakaribisha wageni kutoka nchini Kenya waliofika Tanzania kwa ajili ya kujifunza masuala mbali mbali yanayohusu Maji Taka kupitia Shirika la CCI na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) huku wakiwa wamelenga eneo la Vingunguti na Toangoma jijini Dar es Salaam kwenye miradi ya maji Taka. Wageni hao ni maofisa wa Serikali ya Kenya kutokea upande wa Maji na Huduma za jamii, Mashirika binafsi na viongozi wa vikundu vya jami wapo nchini kwa siku 5 wakitembelea Dar es Salaam na Mwanza.

Mhandisi wa Maji na Usafi wa Mazingira wa Shirika lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na masuala ya Kijamii nchini (CCI), Festo Dominick Makoba ambaye ndiye msimamizi wa eneo la Vingunguti jijini Dar es Salaam.
Moja ya Choo cha kisasa vinavyojenga na Shirika la CCI kwa kusaidiana na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) ili kuwawezesha wananchi wanaoishi katika maeneo yasiyo rasmi.
Moja ya chemba za vyoo vya kisasa.
Muonekano wa Choo cha zamani ambacho wakazi wa Vingunguti walivyokuwa wakitumia.
Mhandisi wa Maji na Usafi wa Mazingira wa Shirika lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na masuala ya Kijamii nchini (CCI), Festo Dominick Makoba ambaye ndiye msimamizi wa eneo la Vingunguti jijini Dar es Salaam akionyesha namna mabomba ya vyoo yalivyopita.
Wageni wakiendelea na ziara.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mji Mpya, Kata ya Vingunguti jijini Dar es Salaam, Rahimu Seif Gassi (kulia) kutoka nchini Kenya waliofika Tanzania kwa ajili ya kujifunza masuala mbali mbali yanayohusu Maji Taka kupitia Shirika la CCI na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) huku wakiwa wamelenga eneo la Vingunguti na Toangoma, Kigamboni jijini Dar es Salaam kwenye miradi ya maji Taka.
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na masuala ya Kijamii nchini (CCI) Tim Ndezi akiwakaribisha wageni kutoka nchini Kenya waliofika Tanzania kwa ajili ya kujifunza masuala mbali mbali yanayohusu Maji Taka kupitia Shirika la CCI na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) huku wakiwa wamelenga eneo la Vingunguti na Toangoma, Kigamboni jijini Dar es Salaam kwenye miradi ya maji Taka.
Wananchi wa Vingunguti jijini Dar es Salaam akiwakaribisha wageni kutoka nchini Kenya waliofika Tanzania kwa ajili ya kujifunza masuala mbali mbali yanayohusu Maji Taka kupitia Shirika la CCI na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) huku wakiwa wamelenga eneo la Vingunguti na Toangoma, Kigamboni jijini Dar es Salaam kwenye miradi ya maji Taka.
Wananchi wakimsikiliza mwenyekiti.
Bi Kellen Muchira kutoka Shirika la Caritas Switzerland lililopo nchini Kenya akizungumza machache juu ya jinsi walivyoweza kufika Tanzania kujifunza namna ya Shirika la CCI na DAWASA wanavyoweza kushirikiana kuwasaidia wakazi wanaoishi katika makazi yasiyo rasmi kukusanya Maji Taka.
Afisa Miradi wa Akiba Mahirani Trust ya nchini Kenya, Patriki Njoroge akieleza machache mbele ya wakazi wa Vinguti jijini Dar es Salaam wakati walipofika Tanzania kujifunza namna ya Shirika la CCI na DAWASA wanavyoweza kushirikiana kuwasaidia wakazi wanaoishi katika makazi yasiyo rasmi kukusanya Maji Taka.
Makazi wa Vingunguti akisoma risara mbele ya wageni.
Msimamizi wa Miradi ya Majitaka Wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) Mhandisi Charles Makoye akiwaelezea juu ya mradi wa kuchakata maji Taka uliopo Toangoma wageni kutoka nchini Kenya waliofika Tanzania kwa ajili ya kujifunza masuala mbali mbali yanayohusu Maji Taka kupitia Shirika la CCI na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) huku wakiwa wamelenga eneo la Vingunguti na Toangoma, Kigamboni jijini Dar es Salaam kwenye miradi ya maji Taka.
Msimamizi wa Miradi ya Majitaka Wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) (mwenye shati jeupe) akiwaonyesha chemba ya mradi wa kuchataka Maji Taka iliopo Toangoma jijini Dar es Salaam.
Msimamizi wa Miradi ya Majitaka Mhandisi Charles Makoye (Kulia) akiendelea kutoa maelezo.
Wageni wakiwa katika picha ya pamoja.

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA, PHAUSTINE KASIKE AHITIMISHA ZIARA YAKE MIKOA YA NYANDA ZA JUU KUSINI, MKOANI RUVUMA

$
0
0




Mkuu wa Magereza Mkoani Ruvuma, ACP. Alexander Nyefwe akimwelezea Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(aliyevaa miwani) juu ya wadudu wanaoshambulia mahindi katika shamba hilo hata hivyo tayari wamekwishapiga dawa za kuzuia wadudu hao.
Askari wa Gereza Kitai, Sajini Edga Mwakibinga akiimarisha ulinzi ndani ya mashamba ya mahindi wakati wafungwa wakiendelea na kazi ya palizi katika mashamba hayo ya Gereza, januari 29, 2019.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(aliyevaa miwani) akizungumza na Wafungwa wa Gereza la Kitai waliokuwa wakiendelea na kazi ya palizi katika mashamba ya mahindi baada ya kumaliza kukagua mashamba hayo, januari 29, 2019.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(aliyevaa miwani)akiangalia miundombinu inayotarajiwa kutumika katika kilimo cha umwagiliaji katika mashamba ya gereza Kitai ili kufikia malengo ya mpango mkakati wa kujitosheleza kwa chakula cha wafungwa.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike mashine ya kuzalisha nishati ya umeme wa maji katika Gereza la Kitai ambapo kwa sasa mashine hiyo haifanyi kazi kutokana na baadhi ya vifaa kuungua.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Songea, Mhe. Pololeti Kamando(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(wa pili toka kushoto) alipotembelea Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, januari 29, 2019. Wengine ni Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa huo(Picha na Jeshi la Magereza).
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(kushoto) akipokea taarifa ya Magereza Mkoa kwa Mkuu wa Magereza Mkoani Ruvuma, ACP. Alexander Nyefwe kabla ya kutembelea Gereza Mahabusu Songea na Gereza la Kilimo na Mifugo Kitai lililopo Wilaya ya Mbinga, januari 29, 2019.
Mkuu wa Gereza Kitai – Nkasi, SSP Sylivester Shija akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike alipowasili gerezani hapo katika ziara ya kikazi yenye lengo la kukagua mashamba ya mahindi ya Gereza hilo, januari 29, 2019.

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AKUTANA NA UONGOZI WIZARA YA KILIMO MALIASILI MIFUGO NA UVUVI ZANZIBAR

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Zanzibar,kuhusiana na maendeleo ya Miradi mbalimbali ya Wizara hiyo,kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi na kulia Mshauri wa Rais Masuala ya Uwekezaji na Uwezeshaji Mhe. Abdulrahman Mwinyijumbe, mkutano huo umefanyika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Kilimo Maliasi, Mifugo na Uvuvi Zanzibar,kuhusiana na Maendeleo ya Miradi mbalimbali ya Wizara hiyo,kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, Waziri wa Kilimo Maliasili,Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Rashid Ali Juma, wakiwa katika ukumbi wa mikutano Ikulu Zanzibar.
WAZIRI wa Kilimo, Maliasili,Mifugo na Uvuvi Zanzibar. Mhe. Rashid Ali Juma, akiwasilisha ripoti ya Maendeleo ya Miradi mbalimbali ya Wizara yake ,wakati wa mkutano na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, hayuko pichani na kulia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi.(Picha na Ikulu)
VIONGOZI wa Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Zanzibar, wakifuatilia taarifa ya maendeleo ya Miradi ya Wizara hiyo, wakati ikiwasilishwa na Waziri wa Kilimo Maliasi, Mifugo na Uvuvi.Mhe. Rashid Ali Juma, wakati wa mkutano na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
KATIBU Mkuu Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Zanzibar Bi. Maryam Juma Sadalla, akichangia wakati wa mkutano na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein,kuzungumzia maendeleo ya Miradi ya Wizara hiyo, mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu) 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Viongozi wa Wizara ya Kilimo Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, katika ukumbi wa mikutano Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)

Korosho Yaingiza Serikali fedha za Kigeni Zaidi ya Tsh. Trilioni Moja

$
0
0

Zao la Korosho katika kipindi kilichoishia Januari 2018 liliingizia Taifa fedha za kigeni shilingi 1,136,609,586,722 ikilinganishwa na mazo mengine ya biashara.

Akijibu swali la Mbunge wa Mtwara Mjini, Mhe. Maftaha Abdallah Nachuma, Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omari Mgumba, amesema licha mchango huo katika uchumi wa Taifa, zao la korosho limekuwa likikabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo Serikali imekuwa ikizitafutia ufumbuzi ikiwemo kuongeza bei ya korosho na kutafuta masoko ya uhakika.

Mhe. Mgumba amezitaja changamoto hizo kuwa ni kuyumba kwa bei ya korosho katika soko la dunia kutokana na zao hilo kuuzwa likiwa ghafi yaani bila kuongezwa thamani, tija ndogo katika uzalishaji, baadhi ya wakulima kutotumia miche bora na matumizi hafifu ya pembejeo ikiwemo viuadudu kama salfa na wakulima kutozingatia kanuni bora za kilimo katika uzalishaji.

Aidha, Mhe. Mgumba amezitaja changamoto nyingine kuwa uvunaji na uhifadhi hafifu wa korosho, uwezo mdogo wa maghala ya kuhifadhia korosho na baadhi ya wakulima kuchanganya zao hilo na mawe na mchanga kwa ajili ya kuongeza uzito wakati wa mavuno.

“Katika kukabiliana na changamoto hizo, Serikali imeboresha mfumo wa uuzaji wa korosho kwa kuimarisha usimamaizi na ukaguzi kuanzia ngazi ya vyama vya msingi, maghala makuu, maghala aya hifadhi na kutoa elimu, kurejesha kwa kiwanda cha BUCCO cha mkoani Lindi cha ubanguaji wa korosho, ujenzi wa maghala matatu ya kuhifadhia korosho katika mikoa ya Lindi, Pwani na Tanga ili kuongeza kiwango cha uhifadhi na ubora wa korosho pamoja na kuzalisha miche bora 10,000,000 na kuisambaza kwa wakulima bure,”alisema Mgumba.

Naibu Waziri Mgumba ameongeza kuwa mikakati mingine ni pamoja na kuimarisha mnyororo wa thamani katika zao la korosho ili kuongeza uzalishaji, kuimarisha usambazaji wa pembejeo za kilimo kwa wakati, kutoa huduma za ugani pamoja na kuweka mazingira wezeshi na kuwajengea uwezo wabanguaji wa ndani kwa lengo la kuongeza thamani ya korosho inayozalishwa nchini.

Akijibu swali la nyongeza kutoka kwa Mbunge wa Mtama, Mhe. Nape Nnauye aliyetaka kujua hatua zilichukuliwa na Serikali kuhusu vitendo vya rushwa katika kuhakiki ununuzi wa Korosho, Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga alisema kuwa wote waliojihusisha na vitendo hivyo hatua kali zilichukuliwa dhidi yao ikiwemo kusimamishwa kazi.

Serikali ya Awamu ya Tano imekuwa na dhamira ya dhati ya kuwainua wakulima nchini ikiwemo wa korosho kwa kuongeza bei ya korosho na kusimamia ununuzi wake. Jambo ambalo limekuwa kichocheo kwa wakulima wengi katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani na Tanga kujikita katika kilimo hicho.

Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli mwishoni mwaka 2018 alisema Serikali itanunua korosho kwa bei ya shilingi 3,300 kwa kilo. Jambo ambalo lilifanyiwa kazi na wakulima wa zao hilo wanafurahia bei hiyo na kutambua kuwa Serikali inawajali.

WAZIRI MHAGAMA AWASILISHA RASMI BUBGENI MUSWADA WA VYAMA VYA SIASA

$
0
0

*Wabunge waanza kuuchambua,Halima Mdee ataka Bunge kuchukua tahadhari


Na Said Mwishehe,Globu ya jamii


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi ,Vijana na Ajira amewasilisha rasmi Bungeni Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa ambapo baada ya kuwasilisha wabunge mbalimbali wameuchambua na kutoa maoni yao.

Hata hivyo baadhi ya wabunge hasa wa Vyama vya Upinzani ambao wamechangia mjadala kuhusu muswada huo wametilia shaka baadhi ua vipengele na kuomba Bunge kuviangalia kwa umakini mkubwa.

Wakati anawasilisha Muswada huo wa Marekebisho ya Sheria vya Vyama vya Siasa Waziri Mhaga ameliambia Bunge leo mjini Dodoma na lengo la muswada huo ni kuwa na sheria ya vyama vya siasa ambayo itamuwezesha Msajili wa Vyama vya Siasa kutekeleza majukumu yake vuzuri.

Amefafanua baadhi ya vipengele vilivyopo kwenye muswada huo ambapo kabla ya hapo aliweka wazi mchakato wa muswada huo ulianza rasmi mwaka 2013 na ilipofika mwaka 2014 ulisimama kupisha mchakato wa Katiba Mpya na mwaka 2015 mchakato ukasimamishwa kupisha uchaguzi Mkuu.

"Muswada wa marebisho ya  Sheria ya Vyama vya Siasa wa mwaka 2018 unalenga kufanya mabadiliko mbalimbali kwa lengo la kumuwezesha Msajili wa Vyama vya siasa kufanya shughuli zake kwa ufanisi." Kama nilivyotangulia kueleza awali mchakato ulianza mwaka 2013 wakati ukusanyaji wa maoni na ilipofika mwaka 2014 ulisimama kwa ajili ya mchakato wa Katiba mpya na mwaka 2015 ulisimama kupisha uchaguzi mkuu.Muswada huu ninaouwasilisha leo hii umegawanyika sehemu kuu mbili,"amesema Waziri Mhagama.

Amefafanua muswada huo unampa nafasi Msajili wa Vyama vya Siasa kutekeleza majukumu yake ambapo akatumia nafasi hiyo kuelezea hatua kwa hatua vipengele vilivyomo kwenye muswada huo kikiwemo kipengele kinachovitaka vyama vya siasa kuheshimu Katiba ya nchi pamoja na alama kuu za Taifa.

Pia kuna vipengele ambavyo vinatoa maelekezo ya vyama vya siasa namna ya kupata viongozi wake pamoja na hatua zinazotakiwa kufuatwa kwa anayetaka kuanzisha chama cha siasa.

 Katika kipengele cha kuanzisha chama cha siasa moja ya sharti ni kwa anayeanzisha kuwa raia wa kuzaliwa wa Tanzania ambacho kinakwenda sambamba na uraia wa wazazi.Kipengele hicho kimeonekana kuibuq mjadala Bungeni.
 
Pamoja na mambo mengine muswada huo kwa mujibu wa Waziri Mhagama amesema  unaweka maelekezo ya jina la chama cha siasa kutofafana na chama kingine ili kuepuka migongano kati ya chama na chama.
Pia amesema muswada unaweka maelekezo ya jina la chama cha siasa kutofafana na chama kingine.Pia muswada huo una kipengele ambacho kinataka vyama vya siasa kuwasilisha orodha ya majina ya viongozi wa ngazi mbalimbali pamoja na kuwepo orodha ya wanachama kwa lengo la kumuwezesha msajili kuwa na kumbukumbu ya vyama husika.

Waziri Mhagama pia amesema muswada huo una kipengele ambacho kinaeleza kuwa  ni marufuku kwa vyama vya siasa kuwa na vikundi vya ulinzi ambapo kipengele hicho nacho kimeibua mjadala kwani wakati Mbunge wa Kawe Halima Mdee(Chadema) wakati anachangia ameonesha kutoridhishwa na uwepo wa kipengele hicho na kuomba Bunge na Kamati ya Katiba na Sheria kuangalia upya kipengele hicho.
Wakati huo huo Mdee wakati anacgangia muswada huo amesema si kweli kwamba wabunge wa vyama vya upinzani pamoja na vyama vya siasa nchini vinaukataa muswada huo kwani mwaka 2009 walipeleka muswada Bungeni kutaka sheria ya vyama vya siasa kufanyiwa marekebisho.

"Kambi ya upinzani bungeni mwaka 2009 tulipeleka muswada bungeni ili kuhakikisha sheria ya vyama siasa inafanyiwa marekebisho lakini ikakataliwa.Hatujawahi kuogopa kukaguliwa jana,leo na kesho,tuache kutumia propaganda katika jambo la Nchi.

"Watu hapa wanasema tusijadili mambo madogo,hivi kujadili jambo linalovunja Katiba ni dogo?Ibara ya 8 C ya muswada huu kinavunja Katiba," amesema Mdee na kufafanua kuna vipengele ambavyo vinaleta ubaguzi na hilo ni huko ni kuvunja Katiba ya nchi.

Amezungumzia pia kipengele ambacho kinataka kuwepo na orodha ya viongozi wa ngazi mbalimbali kwa kupeleka orodha hiyo kwa Msajili sambamba na kuorodhesha majina ya wanachama jambo ambalo ni gumu hasa kwa kuzingatia mwanachama anaweza kujiunga leo na kesho akatoka kwenye chama husika.

Pia ameonesha mashaka na kipengele cha kuzuia vyama vya siasa kuwa na vikundi vya ulinzi ambapo anasema kipengele hicho hakubaliani nacho .

OPERESHENI YA JESHI LA POLISI KILIMANJARO YAKAMATA KILO 400 YA MIRUNGI NDANI YA SIKU SITA.

$
0
0
Anaandika Dixon Busagaga, Moshi.

OPERESHENI ya kukamata Dawa za kulevya inayoendelea mkoani Kilimanjaro imefanikiwa kukamata kilogramu 320 na Dawa za kulevya aina ya Mirungi zikiwa kwenye gari aina ya Toyota Alphasad lenye namba za usajili T 308 DMC ikisafirishwa kuelekea mkoani Arusha.

Hili ni tukio la pili ndani ya siku sita kwa Jeshi la Polisi kufanikiwa kukamata kiasi kikubwa cha Dawa za Kulevya aina ya Mirungi ambapo tukio la karibuni kikosi cha Pikipiki cha jeshi hilo kilifanikiwa kunasa kilogramu 80 za Mirungi iliyokuwa ikisafirishwa kwa kutumia pikipiki kutoka nchi jirani ya Kenya.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,Kamishna Msaidizi wa Polisi,Hamis Issah alithibitisha kukamatwa kwa Dawa hizo za kulevya katika eneo la KIA zikiwa njiani kusafirishwa kuelekea Arusha kutokea nchi jirani ya Kenya .

“Tulipata taarifa uwepo wa gari nyeusi ambayo mwendo wake ulitiliwa shaka na askari wetu ,na kila walipokuta askari ilikuwa ikiwasha taa huku ikiwa mwendo wa kasi,ndipo katika kituo cha KIA askari walizuia magari yote na kufanikiwa kuikamata hiyo gari”alisema Kamanda Issah.

“Wale watu waliokuwa kwenye hii gari baada ya kuona askari wanawafuata walikimbia na kupanda pikipiki zilizokuwa pembeni yake na kutokomea kwa uelekeo wa Arusha na hata hii gari inaonekana uelekeo wake ulikuwa ni huko huko Arusha na tumefanikiwa kuikamata.”aliongeza Kamanda Issah.

Alisema gari lililokuwa limebeba mzigo huo wa dawa zakulevya litakuwa chini ya jeshi la Polisi huku akitoa wito kwa mmiliki wa gari hilo kujitokeza mwenyewe kabla hatua za kufuatilia katika vyombo vingine vya dola kuanza .

Katika tukio la hivi karibuni Polisi walikamata Majani ya Miringi yaliyokuwa yamefungwa katika vifurushi vidogo vidogo zaidi ya 50 na kisha kuwekwa kwenye mfuko mmmoja mkubwa maarufu kama Kiroba huku wahusika wakitumia pikipiki maarufu kama Bodaboda.

Alisema kundi la wasafirishaji wa Dawa hizo za kulevya ambao wamekuwa wakisafirisha kutoka nchi ya Kenya kupitia mpaka wa Holili pindi linapoingia barabarani limeonekana kuwa tishio na hatari kwa usalama wa watu wengine barabarani kwa namna wanavyoendesha pikipiki zao.
 Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Hamis Issah akiwa ameshikilia dawa za kulevya aina ya mitungi baada ya kukamatwa katika eneo la KIA.
 Magunia yenye Dawa za kulevya aina ya Mirungi yakipimwa katika mzani mara baada ya kukamatwa yakisafirishwa kuelekea mkoani Arusha.
 Gari aina ya Toyota Alphasad lenye namba za s usajili T 308 DMC lilikuwa kumbeba dawa hizo aina ya Mitungi kilogramu 380.

 
 

HALOTEL YAREJESHA FAIDA KWA JAMII

$
0
0
KATIKA kuhakikisha inatekeleza agizo la Serikali ya kurejesha faida kwa jamii Kampuni ya Simu ya Halotel imemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kiasi cha zaidi ya Sh Milioni 20 kwa ajili ya kuwawezesha vijana wa mkoa huo kujiajiri kupitia sekta ya ujenzi.

Mbali na fedha hizo, Halotel pia imekabidhi vifaa mbalimbali vya hospitali kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa vikiwemo vitanda, neti, mashuka na aproni vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni sita katika Hospitali ya Makole iliyopo Dodoma mkoani humo.

Akikabidhi misaada hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilithi Mahenge mbele ya Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Atashasta Nditiye, Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel, Tanzania Nguyen Van Son alisema pamoja na mambo mengine, misaada hiyo imelenga kuunga mkono juhudi mbalimbali za maendeleo zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano.

Son alisema katika kuhakikisha inaunga mkono jitihada hizo za Serikali, Kampuni hiyo ya simu ya Halotel imekuwa mstari wa mbele kurudisha faida kwa kile inachokipata kwa kuisaidia jamii mambo mbalimbali kwa lengo la kukabiliana na changamoto zinazowazunguka.

Alisema hatua hiyo imelenga kutoa shukrani kwa wananchi kwa hatua yao ya kuwaunga mkono kwa kutumia huduma za kampuni hiyo iliyosambaa nchi nzima ikitoa huduma mbalimbali na hasa katika maeneo na hasa vijijini.“Tunaamini misaada hii itakwenda kuwa chachu ya maendeleo katika sekta ya afya na ujenzi, hususani kwa kuwawezesha vijana kujiajri katika sekta za ujenzi unaoendana na kukua kwa mji wa Dodoma” alisema Son.

Aidha aliishukuru Serikali kwa kuweka mazingira wezeshi na rafiki yaliyowavutia kuweza kwenye Sekta ya Mawasiliano nchini na kuongeza kuwa dhamira yao ni kuendeleza ushirikiano na kuhakikisha kuwa huduma za mawasiliano zinakuwa za viwango, ubora na gharama nafuu kwa mtumiaji.

Aidha akizungumza wakati wa makabidhiano ya misaada hiyo, mbali na kuipongeza Halotel kwa hatua hiyo, alizitaka kampuni zingine kuiga mfano huo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Serikali linayozitaka kampuni za simu kurejesha sehamu ya faida kwa jamii.

“Nitoe wito kwa kampuni zingine za simu za mkononi ziige mfano wa Halotel wa kurudisha shukrani kwa wananchi” alisema Nditiye na kuwataka wananchi kuthamini mchango wa mawasiliano katika maisha yao ya kila siku kwa uchumi na maendeleo ya Taifa.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilithi Mahenge, pamoja na kuipongeza Halotel alisema msaada huo umekuja wakati muafaka hususani wakati huu ambao mkoa huo unaendelea na mikakati yake ya kuwasaidia vijana.
“Vijana wa Dodoma mtanufaika na Serikali kuhamia Dodoma, kupitia fedha hizi tumeona tuanzishe kikundi cha vijana ili waweze kuanzisha kiwanda cha kufyatua matofali na mradi huo utakuwa na vijana wa kutoka Jeshi la Kujenga Taifa ili wawasaidie ili baadae vijana waweze kuanzisha na kuendeleza viwanda vyao,” amesema Dkt. Mahenge.

Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Makole Dkt Geogre Matiko, aliishukuru Halotel kwa msaada huo na kwamba kutokana na mahitaji mbalimbali yaliyopo katika hospitali hiyo ya Makole huku akizitaka taasisi zingine kuiga mfano huo.
Alisema pamoja na jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali kuinua sekta ya afya, bado kuna changamoto baadhi ambazo kama wadau watajitokeza na kusaidia kama ambavyo Halotel imefanya, zitaweza kupungua ama kuisha kabisa.


Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) akikabidhi vifaa mbali mbali vya hospitali vilivyotolewa na kampuni ya Halotel kwa Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Makole, Dodoma Dkt. George Matiko ( wa pili kushoto) Mkurugenzi wa kampuni ya Halotel, Nguyen Van Son (wa pili kulia) kwa niaba ya Serikali kutoka kwa kampuni ya Halotel kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa. Wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa Mawasiliano, Wizarani Mhandisi Dkt. Maria Sasabo

Mkurugenzi wa kampuni ya Halotel, Nguyen Van Son(wa kwanza kushoto) akikabidhi hundi ya shilingi milioni 20.6 kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilithi Mahenge (wa kwanza kulia) kwa ajili ya kuanzisha kiwanda cha kufyatua matofali cha kikundi cha vijana wa Dodoma, akishuhudia makabidhiano ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati).


TAMASHA SAUTI ZA BUSARA YATOA OFFA MAALUM KWA WATANZANIA

$
0
0
Zikiwa zimesalia siku chache kabla ya tamasha la Sauti za Busara kuanza, Mwenyekiti wa Busara Promotions Simai Mohammed Said amewataka watanzania na wakaazi wa Zanzibar kwa ujumla kuchangamkia fursa zinazo tokana na tamasha hilo. 

“Kuna offa maalum kwa ajili ya watanzania ambayo ni ya chini kabisa ukilinganisha na kile wanacholipa wageni kutoka sehemu zingine kuingia kwenye tamasha,” alisema Simai. 

Alisema fursa zinazo tokana tamasha hili haipatikani mahali popote na wanaofaidika zaidi ni wakazi wa mitaa ambao bado wanashindwa kutumia hizo fursa kikamilifu . 

"Kuna nyakati ambazo watu wanauliza maswali mengi kuhusu tamasha laSauti za Busara na wengine wanakwenda mbali hadi kusema kuwa ni tamasha kwa watalii wakati wao ndio wenyeji," alisema Bw Simai .Mwenyekiti wa Bodi zaidi aliongeza: 'Hakika hakuna haja ya kuangalia mbali sana kupata majibu ya maswali kama hayo; Kwa miaka 16 iliyopita muda huu umekuwa msimu wa juu kwa biashara ya utalii kulingana idadi ya wageni wanaokuja Zanzibar’. 

Kulingana na yeye kuna dalili kwamba hoteli zote za Zanzibar zimejaa kikamilifu na Jiji la Zanzibar kwa ujumla ipo katika hali ya matarajio.Balozi wa Norway nchini Tanzania, Elizabeth Jacobsen kwa upande wake atakuwa akihudhuria tamasha kwa mara ya kwanza na anatarajia mengi kutoka kwenye tamasha hilo hususan fursa zinazopatikana kwenye tamasha. 

“Tunaendelea kusaidia shughuli za kitamaduni kama Sauti za Busara kwa sababu tunaelewa thamani ya shughuli hizo. Tunaona hii ni jukwaa muhimu la kujieleza bure, kukuza tamaduni zetu, weledi na utaalamu katika sekta ya kitamaduni ya Tanzania "alisema Balozi huyo wa Norway, ambaye alianza majikumu yake la kidiplomasia mnamo Septemba 2018. 

Pia aliwahimiza wafanyabiashara ambao ni walengwa wakuu wa tamasha kuunga mkono tukio hilo kwa namna ya uwajibikaji kwa jamii.Julia Bishop ambaye ni makamu wa Mwenyekiti kwa upande wake alisema amejionea mwenyewe jinsi tamansha la Sauti za Busara linavyo badilisha maisha ya wasanii hususan wale chipukizi wasiojulikana kabisa. 

“Kwa mtu ambaye hajawahi kufika Zanzibar kabla ni vigumu kufikiria ukubwa wa tukio hili, ubora wa maonyesho, utaalamu na msisimko ambayo hupatikana ndani ya Stone Town, "alisema.Kulingana na yeye, ukweli kwamba makundi madogo ambayo haijulikani sana kupata fursa sawa na nyota wa muziki kwenye jukwa moja yenyewe ni hatua ya kubadili maisha. 

Tamasha la Sauti za Busara linadhaminiwa na Ubalozi wa Norway, Ubalozi wa Uswisi nchini Tanzania na Zambia, Umoja wa Ulaya, Africalia, Ubalozi wa Ufaransa, Ubalozi wa Ujerumani, Pro Helvetia, Zanlink, Mozeti, Shirika la Ndege la Ethiopia, African Movie Channel, Zanzibar Media Corporation, TV-E, E-FM, Madinat Al Bahaar, Golden Tulip na wengine wengi. 

Sauti za Busara ni tamasha la muziki la Kiafrika linalofanyika kila mwaka, mwezi Februari mjini Zanzibar, Tanzania katika eneo la Ngome Kongwe (Old Fort) sambamba na matukio mengine ya kuvutia yanayofanyika kwa wakati mmoja maeneo ya Stone Town- ikiwemo Carnival Street Parade, Swahili Encounters, Movers & Shakers na Busara Xtra.

MKUU OPERESHENI MAALUM JESHI LA POLISI NCHINI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA KIKOSI CHA KUPAMBANA NA UHALIFU MKOA WA MTWARA

$
0
0
Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Nchini Naibu Kamishna DCP Liberatus Sabas, akizungumza na kikosi Maalum cha kupambana na uhalifu katika viwanja vya Kikosi cha kutuliza Ghasia Mkoa wa Mtwara, baada ya kuwasili katika ziara yake ya kikazi akitokea mkoani Ruvuma. (Picha na Jeshi la Polisi) 
Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Nchini Naibu Kamishna DCP Liberatus Sabas, akishiriki mazoezi ya pamoja na kikosi maalum cha kupambana na uhalifu Mkoa wa Mtwara baada ya kuwasili katika ziara yake  mkoani humo.
Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Nchini Naibu Kamishna DCP Liberatus Sabas aliesimama katikati, akimsikiliza Mkaguzi wa Polisi INSP, Idd Kimia wa kushoto kwake wakati akiangalia utayali wa kikosi cha kupambana na uhalifu Mkoa wa Mtwara  ambacho hakipo pichani. 
Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Nchini Naibu Kamishna DCP Liberatus Sabas katikati na kulia kwake ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara ACP Joseph M.Konyo wakiwa katika picha ya pamoja na kikosi maalum cha kupambana na Uhalifu mkoani humo. (Picha na Jeshi la Polisi).

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KAIMU BALOZI WA MAREKANI, BALOZI WA SWEDEN JIJINI DODOMA

$
0
0
 Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Balozi wa Sweden nchini, Anders Sjoberg alipomtembelea leo tarehe 30 Januari, 2019 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Balozi wa Sweden nchini, Anders Sjoberg alipomtembelea na kufanya nae mazungumzo leo tarehe 30 Januari, 2019 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
pika wa Bunge, Job Ndugai (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Sweden nchini, Anders Sjoberg baada ya kumtembelea na kufanya nae mazungumzo leo tarehe 30 Januari, 2019 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

BIKOSPORTS YABIDHI TUZO KWA KOCHA ZAHERA NA MAKAMBO KUTOKA YANGA

$
0
0

Kampuni ya michezo ya kubashiri ya BikoSports  kupitia kwa afisa uhusiano wao Geof Lea,leo  imekabidhi tuzo kwa kocha wa Yanga Mwinyi Zahera na mshambuliaji wa timu hiyo Heritier Makambo ambao walikuwa wameshinda tuzo hizo.

Makambo na alifanikiwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Disemba 2018 wakati kocha Mwinyi Zahera alifanikiwa kushinda tuzo ya Kocha Bora wa mwezi huo huo Disemba ikiwa ni mara ya tatu anashinda tuzo hiyo.

Shirikisho la soka Tanzania TFF liliingia mkataba wa udhamini na kampuni ya BikoSports kwa ajili ya kutoa zawadi na tuzo kwa washindi wa mchezaji bora wa mwezi na kocha bora sambamba na zawadi ya Tsh Milioni 1 kila mmoja kwa kipindi chote cha msimu wa Ligi Kuu 2018/2019 kilichosalia.

Msemaji wa bikosports Tanzania, Geoffrey Lea akimkabidhi tuzo kocha bora wa mwezi Desemba,Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera zinazodhaminiwa na Bikosports.

Msemaji wa bikosports Tanzania, Geoffrey Lea picha ya kwanza akikabidhi tuzo kwa mchezaji bora wa mwezi Desemba Elichia Makambo. 


Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera (kulia) na mchezaji bora wa mwezi Desemba Elichia Makambo wakiwa katika picha ya pamoja.
Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera akifanya mahojiano na baadhi ya waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa tuzo yake kama kocha bora wa mwezi Desemba zinazodhaminiwa na Bikosports.

MKUTANO MAALUM WA 38 WA BARAZA LA MAWAZIRI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUFANYIKA JIJINI ARUSHA

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza kama kiongozi wa ujumbe wa Tanzania kwenye Kikao Maalum cha 38 cha Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kinachofanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 30 Januari 2019 ikiwa ni maandalizi ya Mkutano wa 20 wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika tarehe 1 Februari 2019. Wengine katika picha ni Kapt. Mstaafu, Mhe. George Mkuchika (kushoto), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Maejimenti ya Utumishi wa Umma na Mhe. Dkt. Philip Mpango, Waziri wa Fedha na Mipango. Anayeonekana nyuma ya Mhe. Mkuchika ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe. 
Mawaziri hao wakipitia nyaraka mbalimbali wakati wa kikao hicho 
Mwenyekiti wa Kikao Maalum cha 38 cha Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Uganda, Mhe. Kirunda Kivejinja (wa pili kulia), ambaye pia ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha Baraza hilo. 
Ujumbe wa Burundi ukiwa kwenye kikao hicho cha Baraza la Mawaziri 
Ujumbe wa Kenya nao ukifuatilia kikao 
Mjumbe kutoka Sudan Kusini (kushoto) akiwa katika meza moja na ujumbe wa Rwanda wakati wa kikao cha Baraza la Mawaziri 
Ujumbe wa Uganda nao ukifuatilia kikao 
Wajumbe wa Tanzania wakiongozwa na Mawaziri wakifuatilia kikao. Kulia ni Naibuu katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bibi Amina KH. Shaaban 
Dkt, Aloyce Nzuki, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii akiwa na Bw. Stephen Mbundi, Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki 
Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Dkt. Aziz Mlima (kushoto) kwa pamoja na Kaimu Mkurugenzi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia kikao cha Baraza la Mawaziri 

Wajumbe wengine wa Tanzania


====================================================




KUHUSU MKUTANO MAALUM WA 38 WA BARAZA LA MAWAZIRI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

Mkutano Maalum wa 38 wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unafanyika jijini Arusha kwa lengo la kujadili na kukubabaliana na agenda mbalimbali zitakazowasilishwa kwenye Mkutano wa 20 wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya hiyo utakaofanyika tarehe 1 Februari, 2019.

Mkutano huo ambao unaongozwa na Mwenyekiti kutoka Jamhuri ya Uganda ambaye pia ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Kirunda Kivejinja utajadili agenda mbalimbali muhimu ambazo ni pamoja na ripoti ya utekelezaji wa maamuzi mbalimbali yaliyofikiwa na Baraza hilo kwenye vikao vilivyopita; taarifa kutoka Ofisi ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, taarifa kuhusu masuala ya miundombinu, forodha na biashara na ripoti ya kamati ya utawala na fedha.

Agenda zingine ni taarifa ya Baraza kwa Wakuu wa Nchi kuhusu utekelezaji wa maamuzi mbalimbali yanayofiwa kwenye mikutano ya Wakuu hao wa Nchi na Kalenda ya Matukio ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Juni 2019.

Mkutano huo wa Mawaziri ulitanguliwa na vikao vya Maafisa Waandamizi kutoka nchi wanachama kilichofanyika tarehe 28 Januari kikifuatiwa na kikao cha Kamati ya Uratibu chini ya Makatibu Wakuu kutoka nchi wanachama kilichofanyika tarehe 29 Januri 2019.

Ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano huo unaongozwa na Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na kuwahusisha pia Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (Mb), Waziri wa , Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), Waziri Fedha na Mipango, Mhe. Kapt. Mstaafu George Mkuchika (Mb), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Mhe. Joseph Kakunda (Mb), Waziri wa Viwanda na Biashara na Mhe. Innocent Bashungwa, Naibu Waziri wa Kilimo. 

Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo inaundwa na nchi sita za Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda na Sudan Kusini imeendelea kuhakikisha wananchi katika nchi hizo wananufaika na Jumuiya hiyo hususan katika nyanja za biashara, ulinzi na usalama, viwanda, kilimo, miundombinu na huduma za kijamii. 


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Arusha.
30 Januari 2019


Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images