Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1788 | 1789 | (Page 1790) | 1791 | 1792 | .... | 1904 | newer

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo Januari 27 kwa kushirikiana na Benki ya NMB, wametoa Vifaa Tiba vya kujifungulia katika wodi ya Mama na Mtoto, pamoja na vifaa tiba hivyo aliwazawadia  watoto 36 waliozaliwa siku ya  katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro .

  Makamu wa Rais aliwakilishwa na Katibu wake Bw. Juma S. Mkomi ambaye amesema kuwa Makamu wa Rais amekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha huduma ya afya ya mama na mtoto inaboreshwa.

  “Suala la kuboresha huduma ya mama na mtoto limeelezewa kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020 lakini Makamu wa Rais kwa upekee amelipa kipaumbele kwa sabau ni moja kati ya ahadi zake kuu wakati kampeni” alisema Katibu huyo wa Makamu wa Rais.

  Akizungumza wakati wa hafla hiyo Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Dkt. Rita Lyamuya amemshukuru Makamu wa Rais kwa kuwakumbuka watoto waliozaliwa hospitalini hapo ambapo alisema kuwa watoto 36 wamezaliwa katika siku ya leo na kwa kipindi cha robo mwaka watoto  1779 walizaliwa  kati ya hao waliozaliwa kwa upasuaji ni 586.

  Aidha, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Mashariki Aikansia Muro amesema Benki ya NMB inaunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya tano katika kuboresha huduma zote za kijamii hususani sula zima la  afya na elimu na wataendelea kushirikiana na Serikali katika kuboresha huduma za kijamii ambapo leo wamemuunga mkono Mhe. Makamu wa Rais kwa kutoa Vitanda vinne vya kujifungulia, Vifaa vya kumsaidia mama kujifungulia (delivery kit) 8, pamoja na vifaa vingine ambavyo kwa ujumla vinagharimu shilingi milioni 5.

  Kwa Upande mwingine Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro Bw. Clifford Tandari ameishukuru Serikali kwa kutenga shilingi bilioni 8.5 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali 3 na vituo vya afya 11 katika mkoa wa Morogoro.
    Katibu wa Makamu wa Rais Bw. Juma S. Mkomi akimkabidhi Bi. Apendae Mohamed (kushoto) beseni yenye mahitaji muhimu kwa mtoto wake  ikiwa zawadi kutoka kwa  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa watoto 36 waliozaliwa leo tarehe 27, Januari kama kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa katika hospitali ya Rufaa ya Morogoro. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
   Katibu wa Makamu wa Rais Bw. Juma S. Mkomi akimkabidhi Bi. Apendae Mohamed (kushoto) akipokea kadi kwa niaba ya   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan mara baada ya kukabidhi zawadi  kwa watoto 36 waliozaliwa leo tarehe 27, Januari kama kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa kwa Makamu wa Rais katika hospitali ya Rufaa ya Morogoro. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
   Katibu wa Makamu wa Rais Bw. Juma S. Mkomi akipokea Vifaa Tiba vya kujifungulia wakina mama kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kutoka kwa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Mashariki Bi. Aikansia Muro ikiwa sehemu ya Benki hiyo kuunga mkono juhudi za Makamu wa Rais katika kuboresha huduma ya afya ya Mama na Mtoto leo katika hospitali ya rufaa ya Morogoro ambapo Makamu wa Rais alitoa zawadi kwa watoto 36 waliozaliwa tarehe 27, Januari kama kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
    Katibu wa Makamu wa Rais Bw. Juma S. Mkomi akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Rufaa ya Morogoro Dkt. Lucy Nkya moja ya mabeseni yenye mahitaji muhimu kwa watoto waliozaliwa leo ikiwa zawadi kutoka kwa  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa watoto 36 waliozaliwa leo tarehe 27, Januari kama kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
   Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Rufaa ya Morogoro Dkt. Lucy Nkya akionyesha juu moja ya mabeseni yenye mahitaji muhimu kwa watoto waliozaliwa leo kama ishara ya kumshukuru Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuwakumbuka  watoto 36 waliozaliwa leo tarehe 27, Januari ikiwa ni kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)   0 0


  Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu kushoto akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa UWT Taifa Jesca Mbogo katikati ni Katibu wa CCM wilaya ya Muheza Moyo

  Naibu Katibu Mkuu wa UWT Taifa Jesca Mbogo kushoto akiingia shuleni hapo kwa ajili ya kushiriki ujenzi wa bweni la w katika shule ya msingi mbaramo yenye watoto wenye mahitaji maalum.

  Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu akishiriki ujenzi huo

  msingi ukiwa umechimbwa
  sehemu ya wanafunzi wa shule hiyo wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa UWT Taifa Jesca Mbogo


  WAZAZI na walezi wilayani Muheza wametakiwa kusimamia nidhamu za watoto wao ili kuepukana na suala la mmomonyoko wa maadili ambalo lina wakabili baadhi ya watoto hapa nchini.

  Wito huo ulitolewa hivi karibuni na Naibu Katibu Mkuu wa UWT Taifa Jesca Mbogo ametoa kauli hiyo wakati wa ziara yake wilayani humo ambapo pamoja na mambo mengine ametembelea eneo la ujenzi wa mabweni katika shule ya msingi mbaramo yenye watoto wenye mahitaji maalum.

  Alisema iwapo wazazi watawajibika ipasavyo kuhakikisha wanasimamia maadili hayo watawasaidia vijana wao kuweza kuepukana na tabia ambazo sio nzuri ambazo wanaweza kuzipata kutokana na makundi mengine. Hata hivyo pia alisema serikali ya Awamu ya Tano inafanya jitihada kubwa ya kuboresha miundo mbinu ya watoto kujisomea hivyo wazazi wanapaswa kusimamia suala zima la nidham kwa wototo wao .

  Kwa Mkuu wa wilaya ya Muheza Mwanaasha Tumbo amesema kuwa kupitia kampeni ustawi wao ni wajibu watajenga madarasa na mabweni kwa ajili ya watoto walemavu ambayo wameshaanza kuitekeleza katika shule ya msingi mbaramo. Katika kuunga mkono jitihada hizo mbunge wa Jimbo la Muheza Balozi Adadi Rajab pamoja na mambo mengine ameahidi kutoa mifuko Saruji ili kuhakikisha mabweni hayo yanakamilika kwa wakati ili kutoa fursa kwa wanafunzi kusoma bila kuwepo kwa vikwazo

  0 0

  Kuwahudumia Wakimbizi ni jukumu la Wote sio la Nchi moja
  Kazi ya kuwahudumia wakimbizi ni Ubinadamu na ni jukumu la kimataifa na ni kitu cha kushangaza kuona nchi zilizoendelea zinaziachia nchi masikini kubeba mzigo wa kugharamia wakimbizi.

  Kauli hiyo ilitolewa na Rais Mstaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti mwenza wa Baraza la Wakimbizi Duniani (World Refugees Council-WRC), Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa kuwasilisha ripoti ya Baraza hilo kwenye Umoja wa Mataifa New York, Marekani tarehe 24 Januari 2019.

  Rais Mstaafu alitanabainisha kwamba Baraza lao lilipokea msimamo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa kukataa mpango wa kukopa Benki ya Dunia ili kuwahudumia wakimbizi wakati yenyewe inadaiwa mikopo ya kimaendeleo iliyonayo. Serikali inaamini kazi ya kuhudumia wakimbizi ni ya kibinadamu kwa kushirikiana na Jumuiya ya Kimataifa badala ya kuibebesha nchi moja mzigo wa madeni.

  Taarifa hiyo imebainisha kuwa tatizo la wakimbizi limekuwa kubwa sana duniani wakati huu kuliko wakati wowote ule tangu vita vya Pili vya Dunia. Mathalan, kuna idadi ya watu milioni 68.5 waliopoteza makwao (Internally displaced persons) mwaka 2017 na kati yao, milioni tatu wamepoteza makwao kwa sababu ya mabadiliko ya hali ya hewa na uchafuzi wa mazingira. 

  Ripoti inaeleza kuwa, kumekuwa na ongezeko kubwa la wakimbizi na wanaopoteza makwao kusini mwa jangwa la Sahara ambao walifikia milioni 18.4 mwaka 2017 ukilinganisha na idadi ya milioni 14.1 mwaka 2015. Ripoti inabainisha kuwa ongezeko hilo limetokana na sababu mbalimbali zikwemo upvotevu wa amani katika nchi zao.

  Ripoti inazidi kubainisha kuwa asilimia 30 ya watu wote duniani mwaka 2017 walikuwa wakimbizi na waliopoteza makwao ukilinganisha na asilimia 23 ya mwaka 2015. Kati ya idadi hiyo, wanaotoka Afrika, asilimia 79% wanatoka katika nchi za Somalia, Nigeria, Sudan kusini na Jamhuri ya Afrika ya Kati. 

  Ripoti imeeleza nchi zinazopokea wakimbizi wengi kuwa ni pamoja na Uganda, wakimbizi milioni moja na laki nne; Ethiopia, laki Tisa; Tanzania laki tatu na ishirini na Sita elfu; na Rwanda elfu 84. Baadhi ya nchi zimechukua wakimbizi hao ikiwemo Marekani, Canada, Australia na Finland ingawa idadi yao ni ndogo mno. 

  Katika ripoti hiyo, baraza limetoa mependekezo mbalimbali ya kukabiliana na tatizo la wakimbizi duniani. Mapendekezo makubwa ni pamoja na kudhibiti nchi ambazo zinachochea au kuanzisha migogoro kwa kuweka mfumo thabiti wa kimataifa, kuongeza usuluhishi wa migogoro, kutowanyanyapaa wakimbizi kwa kujenga ukuta na kusaidia juhudi za kutafuta amani katika maeneo yenye migogoro. 

  Baraza la Wakimbizi duniani ni chombo kilichoundwa na wataalamu mbalimbali wakiwemo wanasiasa, watafiti na watunga sera kwa lengo la kufanya utafiti wa kina utakaosaidia kubuni njia na mbinu za kitaalamu na za ubunifu zitakazosaidia kukabiliana na kumaliza kabisa tatizo la wakimbizi duniani. 

  Imetolewa na:
  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
  Dodoma 
  27 Januari 2019 
  Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti Mwenza wa Baraza la Wakimbizi Duniani (World Refugees Council, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete (mstari wa mbele wa kwanza kushoto) akiwa na viongozi mbalimbali jijini New York baada ya Baraza hilo kuwasilisha ripoti kwenye Umoja wa Mataifa ya namna ya kukabiliana na tatizo la wakimbizi duniani. Picha inaonesha kitabu cha ripoti iliyowasilishwa. 
  Mheshimiwa Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Mhe. Balozi Modest J. Mero (kushoto) na viongozi wengine wa Baraza la Wakimbizi Duniani.

  0 0


  Yah: Ziara ya Kampuni kubwa za uwekezaji kutoka Austria na India

  Ujumbe wa Makampuni 16 makubwa ya uwekezaji kutoka Austria utafanya ziara ya kikazi hapa nchini kuanzia tarehe 28 hadi 30 Januari, 2019. 

  Ziara ya ujumbe huo nchini ni mwendelezo wa jitihada za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani ambao unawakilisha pia nchini Austria na wadau mbalimbali katika kutekeleza diplomasia ya uchumi. Pamoja na mambo mengine, diplomasia ya uchumi inalenga kwenye kutafuta na kuleta wawekezaji wenye nia ili wawekeze katika maeneo mbalimbali hapa nchini kwa lengo la kukuza uchumi na kuinua kipato cha wananchi. 

  Makampuni hayo ya Austria yana nia ya kuangalia fursa za uwekezaji hapa nchini katika sekta mbalimbali ikiwemo afya, mawasiliano ya simu, umeme wa kutumia maji na usafirishaji. 

  Ukiwa nchini, ujumbe wa Kampuni 8 umeomba kuonana na kufanya majadiliano na viongozi wa Wizara mbalimbali tarehe 29 Januari, 2019 jijini Dodoma akiwemo Mhe. Japhet Ngailonga Hasunga (Mb.), Waziri wa Kilimo; Mhe. Dkt. Medard Kalemani (Mb.), Waziri wa Nishati; Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb.), Waziri wa Fedha na Mipango; Mhe. Ummy Mwalimu (Mb.), Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Watoto na Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. 

  Lengo la ujumbe huo kukutana na Mawaziri hao ni kutaka kufahamu kuhusu kazi na miradi mbalimbali inayosimamiwa na kutekelezwa na wizara hizo ili waone namna ya kuwekeza katika maeneo hayo. Aidha, ujumbe huo utashiriki kwenye Kongamano la Biashara lililoandaliwa kwa ushirikiano kati ya Chama cha Wafanyabiashara, Wakulima na Wenyeviwanda Tanzania (TCCIA) na Ubalozi wa Austria. Kongamano hilo litafanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam tarehe 28 Januari 2019. 

  Serikali ya Tanzania na Austria zina mahusiano ya kidiplomasia ya muda mrefu tangu uhuru ambapo Austria imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali kupitia mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) hapa nchini hususan katika sekta ya kilimo, afya na kuwajengea uwezo wanawake. Ziara ya ujumbe wa makampuni hayo ni dalili njema za kuanza kuimarika zaidi kwa mahusiano kati ya Tanzania na Austria. 

  Wakati huohuo, Ujumbe wa wawekezaji kutoka Kampuni ya Bureau Facility Services Pvt Ltd (CISB) ya India utafanya ziara hapa nchini kuanzia tarehe 29 Januari hadi 05 Februari 2019. Ziara hiyo ina lengo la kukamilisha utaratibu wa kuwekeza katika maeneo kadhaa ikiwemo ujenzi wa kiwanda cha madawa, kutafuta fursa ya kuwekeza kwenye miundombinu kama vile barabara na madaraja na ujenzi wa nyumba na hoteli. Wajumbe hao wanatarajia kukutana na kufanya mazungumzo na Mawaziri na Viongozi Wakuu Waandamizi wa sekta husika. 

  Ujumbe huo wa watu watatu utaongozwa na Bw. Alban Rodricks kutoka CISB ambaye alishafanya ziara hapa nchini mara kadhaa. Aidha, Ujumbe huo unatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Hamisi Kigwangala (Mb.), Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Ummy A. Mwalimu (Mb.), Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto na Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe (Mb.), Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano pamoja na Mhe. Angellah Kairuki (Mb), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji. 


  Katika ziara yao hiyo fursa mbalimbali za kiuwekezaji zinatarajia kuibuliwa pamoja na kujadiliana namna bora ya kushirikiana kati ya Tanzania na India. 

  Imetolewa na: 
  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, 
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, 
  Dodoma. 
  27 Januari 2019

  0 0

  Februari 15 wawe wamekamilisha uhakiki na malipo kwa wakulima wa korosho

  WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Kilimo pamoja na Bodi ya Mazao Mchanganyiko wahakikishe hadi Februari 15 mwaka huu wawe wamekamilisha uhakiki na kuwalipa wakulima wote wa zao la korosho.

  Pia amesema Serikali inaendelea kufuatilia mwenendo wa mazao makuu ya biashara kuanzia hatua ya uzalishaji hadi masoko yake likiwemo zao la korosho kwa lengo la kuwapatia tija wakulima.

  Amesema zao la korosho ambalo awali soko lake halikwenda vizuri kutokana na utaratibu uliokuwa ukitumiwa na wafanyabiashara kwa kutenda bei ndogo na wakulima wenyewe kugomea bei hiyo.

  Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumapili, Januari 27, 2019) wakati akizungumza na wadau wa zao la korosho mkoani Mtwara, lengo likiwa ni kupata taarifa juu ya mwenendo mzima wa bidhaa hiyo kwa msimu wa mwaka 2018/2019.

  Amesema Serikali ilitoa nafasi kwa wafanyabishara kufanya marekebisho ili waweze kununua bidhaa hiyo kwa bei nzuri bila mafanikia hali iliyopelekea Serikali kuamua kununua korosho zote ili wakulima wapate tija.

  Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mgumba amesema kuwa, taarifa iliyotolewa na timu ya uhakiki ilisema msimu wa 2018/2019 matarajia yalikuwa ni kuvuna tani 150,000 kutokana na kushuka kwa uzalishali.“Lakini kwa kazi nzuri iliyofanywa na timu nzima ya Wizara, wilaya na mkoa na timu ya uhakiki hadi sasa korosho tulizozipokea ambazo ziko katika maghala ni zaidi ya tani laki mbili.”

  Amesema zoezi hilo limewapa tija kubwa katika zao hilo tofauti na taarifa zilizowafikia hapo awali, ambapo wanatarajia baada ya zoezi hilo kumalizika watafikisha zaidi ya tani 200,000 ikiwa ni nyongeza zaidi ya tani 100,000.

  Amesema, Wilaya inayoongoza kwa uzalishaji mkubwa hapa nchini ni Tandahimba amabpo wamefikia asilimia 96 ya uhakiki hadi kufikia jana huku zoezi la malipo kwa korosho zote zilizohakikiwa kwa mkoa wa Mtwara yamefikia asilimia 83.

  Hata hivyo, Waziri huyo amesema kuwa fedha za kununulia korosho hizo zipo kwa kuwa Serikali imejipanga vizuri. Jumla ya sh bilioni 700 zimetengwa kwa ajili ya zoezi hilo ambapo hadi sasa zaidi ya sh. bilioni 400 zimeshalipwa wakulima waliohakikiwa hadi juzi.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  S. L. P. 980,
  41193 – Dodoma, 
  JUMAPILI, JANUARI 27, 2019. 
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika  kikao alichokiitisha cha wadau wa zao la korosho kilichofanyika mjini Mtwara, Januari  27, 2019. Kulia ni Naibu Waziri wa Kilimo, Omary Mgumba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
  Baadhi ya washiriki wa kIkao cha wadau wa zao la korosho wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakati alipozungumza katika kikao hicho alichokiitisha mjini Mtwara, Januari 27, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa mkoa wa Mtwara wakati alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Mtwara ambako aliongoza kikao cha wadau wa zao la korosho, Januari 27, 2019. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa mkoa wa Mtwara wakati alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Mtwara ambako aliongoza kikao cha wadau wa zao la korosho, Januari 27, 2019. 
   Baadhi ya washiriki wa kIkao cha wadau wa zao la korosho wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakati alipozungumza katika kikao hicho alichokiitisha mjini Mtwara, Januari 27, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  0 0

  Na WAMJW -Mvomero, Morogoro.

  “Ugonjwa wa ukoma hausababishwi na imani za kishirika bali ni vimelea vya magonjwa ambavyo huingia ndani ya mwili na kusababisha ukoma”

  Hiyo ni kauli ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alipokuwa akizungumza na waathirika wa ugonjwa wa ukoma pamoja na wananchi katika maadhimisho ya siku ya Ukoma Duniani, wilayani Mvomero, katika Mkoa waMorogoro.

  Dkt. Ndugulile amewaasa wananchi kuachana na imani za kishirikina kwa kuamini kuwa ya kwamba ugonjwa huo unahusika moja kwa moja na imani hizo za giza.

  “Dhana ya kwamba ugonjwa huu ni wa kurogwa siyo kweli, ugonjwa wa ukoma hausababishwi na mtu kulogwa wala kutupiwa jini bali ni vimelea ambavyo huingia mwilini na kusababisha ugonjwa wa ukoma, ni watu kama mimi na wewe” anasema Dkt Ndugulile.

  Aidha Dkt Ndugulile ametumia nafasi hiyo kuwaelimisha wananchi kuwa ugonjwa wa ukoma unatibika na kusema kuwa dawa za kutibu ugonjwa huo zipo na kuwaondolea hofu ya kuwa ugonjwa huo kutotibika. Hata hivyo Dkt. Ndugulile ametoa rai kwa wananchi wote kujitokeza mapema katika vituo vya kutolea huduma za afya kupata huduma za matibabu pindi wanapohisi kuwa na dalili za ugonjwa wa ukoma.

  “Mtu yeyote ambaye anaanza kuona mabadiliko kwenye ngozi yake, anapata mabaka ambayo hayaelewi au kupoteza hisia pindi unapojigusa ni muda wa kwenda hospitalini kufanya uchunguzi na kama utagundulika kuwa na vimelea vya ugonjwa wa ukoma utapewa matibabu” alisisitiza Dkt. Ndugulile.

  Dkt. Ndugulile amewataka wananchi kuwa mabalozi wa kuwaelimisha watu wengine juu ya dalili na athari za ugonjwa wa ukoma. “Niwaombe ndugu wananchi tuendelee kutoa elimu kuhusiana na ugonjwa huu ni ugonjwa ambao tunaweza tukauzuia na tusiwe na athari kwenye jamii na tusingependa kuona kwenye zama hizi watu wanapata athari za kudumu na wanapoteza viungo, hisia katika sehemu za miili yao au kuharibika ngozi kwa sababu ya kutopata matibabu mapema” alifafanua Dkt Ndugulile.

  Naibu Waziri huyo wa Afya amesema kuwa Serikali ipo katika hatua nzuri za kutokomeza ugonjwa wa ukoma nchini licha ya changamoto ambazo zipo katika baadhi ya maeneo sugu ambayo ugonjwa huo umeonekana kuwa ni tatizo. “Takwimu zinaonyesha kuwa takribani watu 1993 huugua ugonjwa wa ukoma kila mwaka huku mikoa ya Lindi, Rukwa, Mtwara, Pwani, Tanga, Geita, Dodoma, Tabora, Kigoma na Mkoa wa Morogoro ikiwa na idadi kubwa ya wagonjwa” alisema Dkt. Ndugulile.

  Sasa hivi tumepiga hatua kubwa, tunajua jinsi gani ugonjwa unaambukizwa, na namna ya kuutibu pamoja na kujikinga dhidi ya maambukizi mapya, naamini kwa mikakati iliyopo tunaweza kuutokomeza ugonjwa huu.

  Akizungumiza mikakati iliyopo Dkt Ndugulile amesema kuwa pamoja na elimu ambayo wamekuwa wakiitoa, Serikali imehamishia nguvu kwenda kwenye jamii moja kwa moja kuwabaini wagonjwa wa ukoma. “Hatusubiri watu watufate, tumewekeza nguvu nyingi kwenye jamii na kuwafikia huko huko maeneo wanayoishi” alisema Dkt Ndugulile.

  Kwa upande mwingine, Dkt Ndugulile amezindua Mpango wa Kingatiba ya Ugonjwa wa Ukoma mahususi kwa wale ambao wamekuwa wakiishi na wagonjwa wa ukoma ili waweze kujikinga kutopata ugonjwa huo na kutoa rai kwa wananchi wote ambao wamekuwa wakiishi na wagonjwa wa ukoma kujitokeza katika vituo vya huduma za afya kumeza dawa hizo za kujikinga na ukoma.

  “Mtu mwenye ukoma na ambaye amekunywa dawa za kingatiba hawezi kusambaza ugonjwa huu na tunaweza kuishi na kushirikiana naye kufanya shughuli mbalimbali kimaendeleo” alisema Dkt Ndugulile na kuwaasa wananchi kuacha tabia za kuwanyanyapaa wenye ukoma.

  Dkt Ndugulile ameipongeza taasisi ya GLRA kutoka Ujerumani inayojihusisha na kuwatunza watu wenye ukoma kwa kuwaanzishia miradi ya ujasiriamali na kuwaunganisha wahanga wa ugonjwa huo na jamii pamoja na kuwapongeza pia wagonjwa wa ukoma kujishughulisha na shughuli za uzalishaji kipato kuliko kuwa omba omba barabarani.

  Awali akitoa salamu zake Rais wa Taasisi ya GLRA Bw. Patric Meisen amesema kuwa anafuraha kuona Tanzania na Ujerumani zikiwa na mahusiano mazuri na kuahidi kuendelea kuwasaida waathirika wa ugonjwa ukoma nchini.

  “Tumekuwa tukifanya kazi na wataalam wa afya katika kuwatunza waathirika waugonjwa wa ukoma, hatujaishia hapo tuu, tumewasaidia waathirika wa ugonjwa huu kwa kuwapatia mitaji itakayowasaidia kujiongezea kipato ambacho kitawasaidia” alisema Bw. Meisen.

  Siku ya Ukoma Duniani huadhimishiwa kila jumapili ya mwisho wa mwezi Januari, ambapo kwa mwaka huu 2019, maadhimisho hayo kitaifa yamefanyika Wilayani Mvomero, Mkoa wa Morogoro yakiwahusisha wadau mbalimbali wa Sekta ya afya huku kauli mbiu ikiwa ni “Tutokomeze Ubaguzi, Unyanyapaa na Chuki dhidi ya Waathirika wa Ukoma”  Picha ya pamoja, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulike (wa nne kutoka kushoto, walioketi) akiwa na wadau wa Sekta ya Afya nchini.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (kulia)akisalimiana na Mzee Anthony Martin (kushoto) wakati alipotembelea makazi ya wasiojiweza ya Chazi, Katika Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (kushoto) akisalimiana na Rais wa Taasisi ya GLRA bw. Patric Meisen kutoka Ujerumani inayowahudumia waathrika wa ukoma nchini.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (kushoto) akisalimiana na Bi. Christina Mohammed (kulia) mhanga wa ugonjwa wa ukoma katika makazi ya watu wasiojiweza ya Chazi yaliyopo Wilayani Mvomero, Morogoro.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (kulia) akisalimiana na wazee waliopata msaaada wa viatu vya kutembelea toka Taasisi ya GLRA inayowasaidai watu wenye ugonjwa wa ukoma nchini.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (kushoto) akitoa kingatiba kwa mtoto aliyekuwa akiishi na mgonjwa wa ukoma. Kingtiba hiyo itamlinda dhidi ya ugonjwa wa ukoma imezinduliwa na Dkt. Ndugulile katika maadhimisho ya siku ya Ukoma Duniani yaliyofanyika Wilayani Mvomero, Morogoro.

  0 0
  0 0


  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akiwasili kwa ajili ya hafla ndogo ya chakula na vinywaji kwa wateja na wadau wa DTB Tanzania iliyofanyika katika hoteli ya Nashera mjini Dodoma hivi karibuni. Pamoja nae kutoka kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu ya TTCL Waziri Kindamba, Mwakilishi wa hoteli hiyo Phoebe Geoffrey na Meneja Maendeleo na Biashara wa DTB Tanzania Magusa Nhende. 
  Baadhi ya wageni waalikwa, maafisa wa Serikali na wateja wa DTB Tanzania katika hafla ndogo ya chakula na vinywaji kwa wateja na wadau wa DTB Tanzania iliyofanyika katika hoteli ya Nashera mjini Dodoma hivi karibuni.
  Mgeni ramsi, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akitoa hotuba fupi katika hafla ndogo ya chakula na vinywaji kwa wateja na wadau wa DTB Tanzania iliyofanyika katika hoteli ya Nashera mjini Dodoma hivi karibuni.
  Mkuu wa kitengo cha TEHAMA wa DTB Tanzania, Bi. Stella Masha (mwenye mtandio wa pinki) akimkaribisha Mgeni rasmi, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dk. Harrison Mwakyembe kuhudhuria hafla ndogo ya chakula na vinywaji kwa wateja na wadau wa DTB Tanzania iliyofanyika katika hoteli ya Nashera mjini Dodoma hivi karibuni. Kutoka kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu ya TTCL Waziri Kindamba na Katibu wa Waziri Andrew Magombana.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akisalimiana na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Omary Mgumba wakati wa hafla ndogo ya chakula na vinywaji kwa wateja na wadau wa DTB Tanzania iliyofanyika katika hoteli ya Nashera mjini Dodoma hivi karibuni.

  Meneja Maendeleo na Biashara wa DTB Tanzania, Magusa Nhende akizungumza na wateja wenye biashara ndogondogo na wadau wa benki hiyo kutoka mji wa Dodoma na vitongoji vyake katika semina ya siku moja iliyojadili kwa kina kanuni za uendeshaji wa biashara na udhibiti wa mapato, sharia ya kazi na mwenendo wa Uchumi Tanzania. Warsha hiyo iliandaliwa na DTB Tanzania kwa kushirikiana na PKF Associates jijini Dodoma hivi karibuni.


  Mtendaji wa Kampuni ya PKF Associates, Muntansir Gulamhussein akizungumza na wateja wenye biashara ndogondogo na wadau wa DTB Tanzania kutoka mji wa Dodoma na vitongoji vyake katika semina ya siku moja iliyojadili kwa kina kanuni za uendeshaji wa biashara na udhibiti wa mapato, sharia ya kazi na mwenendo wa Uchumi Tanzania. Warsha hiyo iliandaliwa na DTB Tanzania kwa kushirikiana na PKF Associates jijini Dodoma hivi karibuni. Kulia ni Meneja wa Maendeleo na Biashara wa DTB Tanzania, Magusa Nhende.

   
  Benki ya DTB-Tanzania, leo imeendesha warsha ya siku moja kwa wateja wake wenye biashara ndogondogo na kati waliopo katika mji wa Dodoma na vitongoji vyake. Warsha hii ya siku moja iliyofanyika katika hoteli ya Nashera, iliandaliwa kwa ushirikiano na kampuni ya PKF Associates; ambao ni wataalam wa utunzaji mahesabu, kodi na uendeshaji wa biashara.

  Maswali yaliyojadiliwa kwa kinaga ubaga ni kanuni za uendeshaji wa biashara na udhibiti wa mapato, sharia ya kazi na mwenendo wa Uchumi Tanzani na dunia kwa ujumla.

  Waendesha warsha kutoka PKF Associates walichanganua kwa undani marekebisho mbalimbali na miongozo katika ulipaji wa kodi na mambo mbali mbali yanayohusisha sheria za kazi nchini. Wageni waalikwa (wateja wa Benki ya Diamond Trsut) walipata kujua bidhaa na huduma mbalimbali zitolewazo na benki, zikiwemo dhamana za benki, mikopo mbalimbali, mikopo ya bima, huduma za kutuma na kupokea fedha ndani na nje ya nchi.

  Akiongea na waandishi wa habari katika warsha hiyo, Mkurugenzi mtendaji na Meneja mkuu wa DTB Tanzania, Ndugu Viju Cherian, alisema “Tumeweka lengo la kufanya warsha kama hii katika miji yote tuliyo na matawi ili kuzungumza na wafanyabiashara wadogo na wa kati mikakati mizuri ya biashara bora: kuweka rekodi za biashara, kanuni za biashara na upangiliaji wa matumizi ya mikopo ya kibenki, ambazo ni vitu muhimu katika uendeshaji wa biashara”.

  Wageni waalikwa katika warsha hiyo walipata nafasi ya kuzungumza na viongozi kutoka DTB-Tanzania na kubadilishana ujuzi wa kazi pamoja na ubunifu wa biashara katika sekta mbalimbali kwa mfano Biashara, Viwanda, Usafirishaji, Ujenzi. “Warsha hii ni sehemu muhimu sana katika kukuza uchumi na sekta ya biashara ndogondogo na kati na inahitaji kupewa kipaumbele.Tumetoa mikopo zaidi ya Shs. bilioni 285 kwa biashara ndogondogo na kati. Hii ni asilimia 40% ya mikopo yote iliyotolewa na benki yetu”. Ndugu Viju aliongeza.

  DTB Tanzania kwa sasa ina matawi 28 nchini, 14 kati ya hayo yakiwa jijini Dar es Salaam kama ifuatavyo (Mtaa wa Jamaat, Masaki, Morocco, Magomeni, Mbezi, Mbagala, Nyerere, Kariakoo, Tawi la Nelson Mandela, Upanga lililo barabara ya Umoja wa Mataifa na Tawi la CBD lililo kwenye makutano ya barabara za Samora na Mirambo) jingine ni Tawi Mbezi Chini lililo Kata ya Kawe na tawi jipya kabisa la Mlimani City. Matawi mengine yakiwemo matawi mawili kwa miji ya Mwanza na Arusha na tawi moja katika miji ya Dodoma, Kahama, Mbeya, Morogoro, Moshi, Mtwara, Mwanza, Tabora, Tanga na visiwa vya Zanzibar.

  DTB Tanzania ni kampuni tanzu ya makampuni ya DTB (DTB Group) yanayoendesha shughuli za kibiashara katika ukanda wa Africa Mashariki nchini Kenya, Uganda na Burundi. DTB Tanzania pia ni kampuni tanzu ya Mfuko wa Aga Khan wa Maendeleo ya Kiuchumi (The Aga Khan Fund for Economic Development – AKFED) ambayo ni tawi la Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan (Aga Khan Development Network -AKDN)

  0 0

  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Nalika Said Masudi kulia,akikabidhi shlingi milioni 15 kwa mkuu wa wilay ya Tunduru mkoani Ruvuma Juma Homera ili kusaidia ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule za sekondari Namwinyu,Ligunga na Matemanga,katikati ni mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Tunduru Gaspar Balyomi na mwenyekiti wa halmashauri hiyo Mkwanda Sudi

  0 0

  Muandaaji wa michuano ya riadha ya Mirerani Tanzanite Marathon, Charles Mligo (Mnyalu) akizungumza kwenye uzinduzi wa mashindano hayo.
  Muandaaji wa michuano ya riadha ya Mirerani Tanzanite Marathon, Charles Mligo (Mnyalu) akizungumza kwenye uzinduzi wa mashindano hayo
  Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, mhandisi Zephania Chaula akimkaribisha Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza ili kuzindua michuano ya riadha ya Mirerani Tanzanite Marathon. 
  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza akizindua mashindano ya riadha ya Mirerani Tanzanite Marathon yaliyofanyika mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara. 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Yefred Myenzi akionyesha medali ya shaba baada ya kuwa miongoni mwa washindi wa kilomita tano katika michuano ya Mirerani Tanzanite Marathon. 
  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza akiongoza mbio za kilomita tano katika michuano ya riadha ya Mirerani Tanzanite Marathon yaliyofanyika mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.
  Baadhi ya wakazi wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakishuhudia mbio za Mirerani Tanzanite Marathon zikitaka kuanza. 
  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza akiwa na baadhi ya wanariadha walioshiriki mbio za Mirerani Tanzanite Marathon yaliyofanyika mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara. 

  …………………………….

  MWANARIADHA mwanajeshi wa JWTZ Faraja Damas ameng’ara kwenye mbio za Mirerani Tanzanite Marathon kilomita 21 zilizozinduliwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza, baada ya kushika nafasi ya kwanza kwa kutumia muda wa saa 1:14.

  Katika mbio hizo zilizofanyika mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Michael Joseph alishika nafasi ya pili kwa kutumia saa 1:34.

  Mshindi wa tatu alikuwa Stephano Huche aliyetumia muda wa saa 1:34 huku Failuna Mtanga akishika nafasi ya kwanza kwa wanawake katika kilomita 21 kwa kutumia saa 1:09. 

  Angelina Daniel alishika nafasi ya pili kwa wanawake kilomita 21 kwa saa 1:14 na nafasi ya tatu ni Rosalina Fabian kwa saa 1:16 na mbio za watoto kilomita tano wanafunzi wa shule ya awali na msingi ya Blue Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani, Sarah Barakael, Clara Flavian na Shangwe Isack, walingara kwa kuongoza michuano hiyo. 

  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza akizungumza wakati akizindua mbio hizo aliwataka maofisa michezo wa mikoa na wilaya kufuatilia vipaji vya michezo mashuleni na kutokaa maofisini. 

  Shonza alisema vipaji vingi vipo kwenye ngazi za shule hivyo maofisa michezo wa wilaya na mikoa wafuatilie hilo kwa manufaa ya sekta ya michezo nchini. 

  Alisema ana wapongeza waandaaji wa mashindano hayo ambayo japokuwa ni mara ya kwanza lakini wamejitahidi kuepuka changamoto mbalimbali ambazo huwa zinajitokeza kwenye michezo mbalimbali. 

  Mkuu wa wilaya ya Simanjiro mhandisi Zephania Chaula alisema mashindano hayo yametumika kuweka historia ya mashindano makubwa ya riadha kufanyika kwenye eneo la mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro. 

  Mhandisi Chaula alisema katika wilaya hiyo hakujawahi kufanyika mashindano ya riadha ila kupitia Mirerani Tanzanite Marathon jina la Simanjiro linaingia kwenye historia ya kufanyika mashindano makubwa. 

  Katibu wa shirikisho la riadha Tanzania, Wilhelim Gidabuday alisema baadhi ya wakenya walizuiwa kushiriki michuano hiyo baada ya kukosa vibali. Gidabuday alisema hawana nia mbaya ya kuwazuia wakimbiaji hao wanne wa Kenya ila kutokana na kutokuwa na vibali hivyo hawakuruhusiwa kushiriki. 

  Muandaji wa mashindano hayo ya Tanzanite Mirerani Marathon, Charles Mligo (Mnyalu) alisema lengo la mashindano hayo ni kuunga mkono jitihada za Rais John Magufuli kwa kutangaza utalii wa madini ya Tanzanite. 

  Mnyalu alisema baada ya Rais Magufuli kuagiza ukuta unaozunguka migodi ya madini ya Tanzanite kujengwa nao wakaamua kuanzisha mashindano hayo ili kutangaza madini ya Tanzanite ambayo hapa duniani yanapatikana mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara pekee

  0 0

  MKURUGENZI wa Mfuko wa ‘KhalifaFund’ Naizar Cheniour, amesema mfuko huo umeazimia kuwawezesha vijana wa Zanzibar katika nyanja mbali mbali za kiuchumi ili kuweza kujiajiri na kuinua hali zao za maisha.

  Mkurugenzi huyo amesema hayo leo wakati alipozungumza na waandishi wa habari, mara baada ya ujumbe wa Mfuko huo ulipowasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume.

  Ujumbe huo upo nchini kwa ziara maalum, ikiwa ni muendelezo wa mazungumzo na Serikali, yenye lengo la kufanikisha utekelezaji wa programu mbali mbali katika sekta za biashara, ujasiriamali, miundombinu na nyenginezo.

  Alisema Mfuko umelenga kuwawezesha vijana wa Zanzibar katika upatikanaji wa rasilimali fedha, utaalamu na masuala ya kiufundi ili waweze kujiajiri kupitia shughuli za ujasiriamali na hivyo kuweza kujitegemea.Aliwataka vijana na Wazanzibari kwa ujumla kutarajia mafinikio makubwa kutokana na program mbali mbali zitakazotekelezwa kupitia Mfuko huo.

  Alisema mfuko wa KhalifaFund, una uzoefu mkubwa katika utekelezaji wa programu za maendeleo na shughuli za kiuchumi, ambapo umekuwa ukifanya kazi hizo katika nchi mbali mbakli duniani.Mapema, Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Viwanda, Dk. Juma Ali Juma alisema ujio wa Viongozi wa Mfuko wa’ KhalifaFund’ umelenga kukamilisha mazungumzo yaliofikiwa katika kikao kilichopita ili kuwa tayari kwa utekelezaji wa yale yalioafikiwa.

  Alisema mfuko huo wa kifedha, wenye makao makuu yake Abu Dhabi ,UAE utatowa msukumo mkubwa katika utekelezaji wa program mbali mbali za kimaendeleo na kiuchumi, sambamba na kuwawazesha vijana kupitia kazi za ujasiriamali.Alisema wakati ukiwa nchini utakutana na kufanya mazungumzo na taasisi mbali mbali za Serikali pamoja na kutembelea maeneo tofauti.

  Hii ni mara ya pili kwa viongozi wa Mfuko wa ‘KhalifaFund’ kuja nchini kwa ajili hiyo, ambapo kabla ulipata fursa ya kutembelea sekta tofauti za maendeleo na kiuchumi Unguja na Pemba.Aidha, ujio wa mfuko huo unafutia ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein aliyoifanya Umoja wa nchi za Falme ya Kiarabu (UAE) Januari mwaka uliopita.
  KATIBU Mkuu Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar Ndg.Juma Ali Juma, akisalimiana na Afisa wa Mfuko wa Khalifa Fund for Enterprise Development Ndg. Abdulah Al Jarwani, wakati wakiwa sili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, kwa ziara ya siku tatu kutembelea Miradi mbalimbali Zanzibar.(Picha na Ikulu)
  KATIBU Mkuu Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar Ndg Juma Ali Juma, akizungumza na Ujumbe wa Mfuko wa Khalifa Fund for Enterprise Development ya Abudha Dhabi UAE, ulipowasili Zanzibar kwa ziara ya Siku Tatu ukiongozwa na Mkurugenzi Nizar Cheniour, mwenye fula nyeusi. wakiwa katika ukumbi wa VIP uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, baada ya kuwasili kwa ziara ya siku tatu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
  KIONGOZI wa Mfuko wa Khalifa Fund for Enterprise Development wa Abu Dhabi UAE, ukiongozwa na Mkurugenzi Ndg. Nazar Cheniour, akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, kutembelea Miradi mbalimbali ya Maendeleo Zanzibar.(Picha na Ikulu)
  AFISA wa Mfuko wa Khalifa Fund for Enterprise Development Ndg. Ali Al Saad, akipata maelezo ya kutoka kwa Mkurugenzi wa Ushirika wa Fakirice Milling Enterprises wa Kisongoni Ndg. Yussuf Faki Yussuf, akitowa maelezo ya usagaji wa mpuga katika ushirika wao wakati walipotembelea ushirika huo leo.(Picha na Ikulu)
  KATIBU Mkuu Wizara ya Biashara na Viwanda Ndg Juma Ali Juma, akitowa maelezo kwa Kiongozi wa Ujumbe wa Mfuko wa Khalifa Fund for Enterprise Development Ndg. Nizar Cheniour, walipotembelea Ushirika wa Fakirice Milling Enterprises Kisongoni,unaojishughulisha na kukoboa mpunga.(Picha na Ikulu)

  0 0
  0 0

  SERIKALI Imefuta kodi ya pango la ardhi kwa Taasisi na Madhehebu ya dini nchini kuanzia mwaka wa fedha wa 2018/2019.

  Hatua hiyo imetangazwa jana Jumapili Januari 27, 2019 na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi jijini Mbeya wakati wa ibada ya kuwaweka wakfu viongozi wa Jumuiya Kuu ya Kanisa la Kibaptisti Tanzania (BCT).

  Lukuvi amesema Rais Magufuli ameiagiza wizara hiyo kutoyatoza kodi madhehebu ya dini kwa sehemu ambazo zimeandaliwa kwa ajili ya kufanyia ibada.

  "Rais ameagiza kuanzia Julai mosi mwaka huu wa fedha madhehebu ya dini yasilipe kodi ya ardhi kwa maeneo ambayo huduma za maombi na ibada zinatolewa, hata hivyo msamaha huu hauhusu maeneo ambayo kuna miradi ya kuingiza fedha ambayo tunajua madhehebu mengi yameanzisha," amesema Lukuvi.

  Lukuvi amefafanua maagizo hayo tayari yametolewa kwa makamishna wa ardhi wa kanda na mikoa pamoja na maofisa ardhi wa majiji, manispaa na halmashauri nchi nzima.Hata hivyo, Lukuvi ametoa nafasi ya kukutana na viongozi wa dini ambao wana migogoro ya ardhi kwenye maeneo ambayo wanatoa huduma.

  "Najua kuna migogoro mingi kwenye maeneo ambayo mnatoa huduma hivyo nawakaribisha ofisini kwangu Dodoma na kama migogoro itakuwa mikubwa nitafika mpaka eneo la mgogoro," amesema Lukuvi.

  “Wizara yangu imepewa jukumu la kutatua migogoro ya ardhi kabla ya mwaka 2020 na tusipotatua migogoro ya dini inaweza kupelekea uvunjifu wa amani nchini hivyo hatutaki kuifuga migogoro iliyopo,” amesema.

  Awali, askofu wa kanisa la Baptisti nchini, Arnold Manase amesema kanisa lake ni moja ya madhehebu yanayoongoza kuwa na migogoro ya ardhi na baadhi ya waumini wa kanisa hilo.

  "Kwa kuwa waziri mwenye dhamana upo naomba nafasi nije ofisini kwako nikueleze migogoro iliyopo ndani ya kanisa langu ili uangalie namna ya kuitatua maana migogoro imekithiri mpaka kufikia hatua ya kujenga makundi miongoni mwa waumini," amesema Manase.

  0 0

  Mkuu wa Gereza Kitete – Nkasi, SP. Job Lwesya(katikati) akimuongoza Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(kushoto) kukagua mashamba ya maharage ya Gereza Kitete – Nkasi alipofanya ziara ya kikazi katika Gereza hilo leo januari 27, 2019.
  Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akiangalia moja ya jembe la trekta la Gereza hilo alipotembelea Gereza Kitete – Nkasi leo Januari 27, 2019.
  Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(katikati) akizungumza na Maafisa na askari wa Gereza Kitete – Nkasi alipofanya ziara ya kikazi yenye lengo la kukagua shughuli mbalimbali za uzalishaji mali katika Gereza hilo.
  Maafisa na askari wa Gereza Kitete – Nkasi wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(hayupo pichani)alipotembelea Gereza hilo leo januari 27, 2019 (Picha zote na Jeshi la Magereza).  Na ASP. Lucas Mboje, Nkasi

  KATIKA kuelekea kwenye mpango wa kujitosheleza kwa chakula cha wafungwa magerezani Gereza la Kilimo Kitete – Nkasi limeanza uzalishaji wa maharage ambapo katika msimu huu wa mwaka 2018/2019 tayari limelima zao hilo.

  Akizungumza leo mara baada ya kutembelea Gereza hilo, Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike amesema kuwa ameridhishwa na hatua mbalimbali zinazoendelea katika kufanikisha mpango mkakati wa uzalishaji wa chakula kwa wingi katika maeneo yakimkakati pamoja na uwepo wa changamoto mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya hali ya hewa na vitendea kazi.

  “Ni lazima tuhakikishe kuwa jukumu hili tulilopewa linatekelezwa ipasavyo hivyo, Mkuu wa Gereza pamoja na timu yako hakikisheni mnaongeza bidii ya kazi kwa kutumia rasilimali zilizopo ikiwemo nguvu kazi ya wafungwa ili kufikia malengo ya hekari 300 za zao la maharge mlizopewa kwani msimu bado unaruhusu”. Alisema Kamishna Jenerali Kasike.

  Aidha, Kamishna Jenerali Kasike amesema kuwa Jeshi litaangalia uwezekano wa kuliwezesha Gereza Kitete zana mbalimbali za kilimo kama vile trekta, ambazo zitarahisisha kufanikisha malengo ya kimkakati ili kuongeza uzalishaji wa chakula cha wafungwa.

  Ameongeza kuwa Gereza Kitete – Nkasi ni miongoni mwa magereza 10 ya kimkakati ambayo tayari yameainishwa katika mpango mkakati wa Jeshi la Magereza katika kujitosheleza kwa chakula cha wafungwa. Magereza mengine ni Songwe, Mollo, Arusha, Idete, Kiberege, Kitengule, Pawaga, Kitai na Gereza Ludewa.

  Katika hatua nyingine, Kamishna Jenerali Kasike amewaasa viongozi wa Jeshi hilo pamoja na watendaji waliopewa dhamana ya kusimamia vitengo(Ugavi na Uhasibu) katika vituo vyao kuzingatia suala la uadilifu na amewataka kujiepushe na vitendo vyote vya ubadhilifu wa mali za umma ili kuwezesha kufikia malengo yaliyokusudiwa.

  Kwa upande wake, Mkuu wa Gereza Kitete, SP. Job Lwesya alisema kuwa katika msimu wa Kilimo wa mwaka 2018/2019 gereza hilo limelima ekari 114 za maharage na kwa sasa linaendelea na maandalizi ya mashamba mengine ili kufikia malengo waliyopewa ya kulima hekari 300 za maharage.

  Aidha, aliongeza kuwa gereza hilo linayo ardhi ya kutosha na yenye rutuba hivyo wamejipanga kimkakati katika kuhakikisha kuwa wanazalisha mazao mbalimbali kwa wingi kwa ajili ya chakula wafungwa.

  Gereza Kitete – Nkasi lina eneo lenye ukubwa wa ekari 3,742 ambazo zinafaa kwa kilimo cha mazao mbalimbali ya chakula ikiwemo zao la maharage, mahindi na Arizeti. Gereza hilo lilianzishwa rasmi mwaka 1989 kwa lengo la kuwahifadhi wahalifu pamoja na kuwapatia wafungwa programu za urekebishaji ili wamalizapo vifungo vyao waweze kuwa raia wema.

  0 0

   
  Meneja Mwandamizi wa NMB, Bidhaa za Amana - Stephen Adili (kulia) akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Akaunti na Malipo - Michael Mungure na kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha huduma kwa Wateja - Abella Tarimo.
  Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja - Abella Tarimo (kushoto) wa Benki ya NMB akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Akaunti na Malipo - Michael Mundure na kulia ni Meneaja Mwandamizi wa Bidhaa za Amana wa Benki ya NMB - Stephen Adili.


  Meneja Mwandamizi wa NMB, Bidhaa za Amana - Stephen Adili (kulia) akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Akaunti na Malipo - Michael Mungure na kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha huduma kwa Wateja - Abella Tarimo.


  NA SALUM MKANDEMBA

  KATIKA kuharakisha kasi ya maendeleo ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla, ikiwemo kuchagiza idadi ya Watanzania wanaotumia huduma za kibenki, Benki ya NMB imetangaza kufuta tozo mbalimbali kuanzia Februari mwaka huu.

  Kufutwa kwa tozo hizo na kufungua milango ya huduma bure za kibenki ‘free banking,’ kumetangazwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Kitengo cha Malipo na Akaunti wa NMB, Michael Mungure, alipoongea na wanahabari.

  Mungure alibainisha kuwa, baada ya tafiti za kina, zilizojikita katika kujua kiini cha kutoongezeka kwa idadi ya Watanzania wanaotumia huduma za kibenki, hivyo kuachwa na kasi ya maendeleo kuelekea Uchumi wa Kati, wameamua kuja na ‘free banking.’

  Alizitaja baadhi ya tozo zilizofutwa kuwa ni pamoja na ile ya kufungua akaunti kwa mteja mmoja mmoja (Individuals Account), ada ya kila mwezi (monthly maintenance fees), makato ya miamala (transactions fees) na kufufua akaunti ya zamani (dormant account).

  “Hii tozo ya miamala tuliyofuta na ambayo itatumika kuanzia Februari mwaka huu ni ya kuhamisha fedha kutoka akaunti moja ya NMB kwenda akaunti nyingine ya NMB, lakini pia kutakuwa na huduma bure zilizotajwa hapo juu, pamoja kuuliza salio,” alisema Mungure.

  Kwa upande wake, Meneja Mwandamizi wa Bidhaa za Amana wa NMB. Stephen Adili, aliwataka Watanzania kuchangamkia fursa ya kufutwa kwa tozo hizo kwa kufungua na kutumia huduma za NMB, ambazo zinapatikana kirahisi kidijitali pia.

  “Kuanzia sasa tunataka wateja wetu na Watanzania kwa ujumla, waje wafungue akaunti kwa wingi na hakutakuwa na makato kama tulivyoainisha, fursa ambayo itaharakisha ustawi wa maendeleo ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla,” alisema Adili.

  0 0  0 0

   *Asema ndoto yake ni kuona TANESCO inajiendesha kwa faida,kutoa gawio kwa Serikali


  *Aelezea mkakati wao ni kuendelea kuboresha huduma ya umeme, agusia miundombinu

  *Akerwa na tabia ya kuchoma moto katika maeneo ambayo miundombinu yao inapita


  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii


  MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO), Dk.Tito Mwinuka amewahimiza watumishi wote wa shirika hilo kutoa huduma bora ,sahihi na kwa wakati kwa wateja wao huku akieleza ndoto yake ni kuona shirika hilo linajiendesha kwa faida na kutoa gawio kwa Serikali.

  Dk.Mwinuka ameeleza hayo mjini Arusha, wakati anazungumza na wahariri wa vyombo vya habari nchini baada ya kukamilika kwa ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya umeme inayotokelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi mahiri wa Rais Dk.John Magufuli .

  Ziara hiyo imefanyika katika mkoa wa Arusha na Kilimanjaro na miongoni mwa miradi ambayo wahariri wameona ilivyotekelezwa ni ile iloyopo kwenye TEDAP.

  Akifafanua zaidi wakati anajibu baadhi ya maswali ya wahariri hao.Dk.Mwinuka amesema pamoja na kuwepo kwa pongezi nyingi zinatokana na kuwepo kwa huduma bora zinazotolewa na shirika hilo lakini bado amesisitiza kwa watumishi wote wa TANESCO kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wateja.

  "Tunataka kuona TANESCO inatoa huduma nzuri na hiyo iwe kwa nchi nzima.Tunataka mteja anapokwenda TANESCO au kokote ambako tunatoa huduma basi apate huduma nzuri,sahihi na kwa wakati pamoja na kuheshimiwa.Hivyo niendelee kutoa rai kwa watumishi wa ngazi zote tuliyopo tutoe huduma nzuri,"amesisitiza.

  Alipoulizwa kuhusu ndoto yake ,Dk.Mwinuka amejibu kuwa ndoto yake ni kuona TANESCO inajiendesha na kufanya kazi zake kwa faida na kwamba wanakwenda vizuri huku akifafanua kwa miaka miwili sasa shirika hilo linajiendesha bila kupewa ruzuki.

  " Malengo yetu ni kuhakikishia TANESCO tunafanya kazi zetu na kutengeneza faida na hii imeanza kuleta tija,ni mwaka wa pili tunajiendesha bila ruzuku ya Serikali na hiki ndicho tunachosisitiza tuwe shirika ambalo linapata faida na hatimaye tutoe gawio kwa Serikali," amefafanua Dk.Mwinuka.

  Kuhusu madeni ,Dk.Mwinuka ameweka wazi TANESCO ilikuwa inadaiwa madeni makubwa ambayo yaliionekana sugu lakini kupitia mikakati yao wamedhamiria kulipa madeni hayo na kwamba kwa sasa wamefanikiwa kwani deni haliongezeki na hivyo wanatarajia kuyamaliza.

  "Kutokana na hali iliyokuwepo miaka ya nyuma TANESCO ilijikuta inadaiwa ,hivyo tunaendelea kulipa madeni ya nyuma," amesema na kusisitiza pamoja na muelekeo mzuri wa shirika hilo bado wamejipanga kutoa huduma ikiwemo ya kuhakikisha nchi yetu inakuwa na umeme wa uhakika na kuendelea kutatua changamoto zilizopo.

  Kuhusu miradi ya Miradi ya Kuimarisha mifumo ya Usambazaji Umeme nchini(TEDAP) Dk.Mwinuka amesema wamefanikiwa kuitekeleza miradi hiyo kwa mikoa ya Arusha,Kimanjaro na Dar es Salaam na kwamba uwepo wa miradi hiyo imeleta tija kubwa.Alipoulizwa iwapo TANESCO itapeleka mradi wa TEDAP katika mikoa mingine ,Dk.Mwinuka amesema kuwa "Ni kweli tunatamani kuipeleka miradi hiyo nchi nzima maana tumeona faida yake kwa mikoa ambayo tuimeitekeleza.

  "Pamoja na kutamani TEDAP itekelezwe na kwenye mikoa mingine lakini changamoto kubwa ni fedha.Hata hivyo pamoja na changamoto hiyo TANESCO tumejiongeza kwani kwa kutumia fedha zetu za ndani tumeutekeleza mradi wa TEDAP eneo la Dege Kigamboni.Hivyo tutaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuimarisha upatikanaji wa umeme," amesema Dk.Mwinuka.

  Pamoja na mambo mengine wahariri walitaka kufahamu kuhusu uchomwaji moto maeneo ambayo imepita miundombinu ya TANESCO,amejibu kuwa ni kweli kuna mikoa uchomaji moto umeshika kasi na kuitaja baadhi ya mikoa hiyo ni Lindi,Mtwara na Songea ambako huko ndiko mto unaonekana kuwaka sana.

  " Wananchi wasichome moto katika maeneo ambayo miundombinu ya umeme, ni jukumu letu sote kuhakikisha tunailinda na kuitunza miundombinu yetu ya umeme ambayo uwekezaji wake katika kutekeleza miradi ya umeme inatumia gharama kubwa.Tuitunze miundombinu yetu,"amesema Dk.Mwinuka.

  Wakati huo huo Dk.Mwinuka amezungumzia namna ambavyo wakati mwingine TANESCO inatupiwa lawama katika jambo ambalo huenda halikusababishwa na Shirika hilo.Ametoa mfano unapotokea moto lawama mara nyingi zinaelekezwa TANESCO hata kama chanzo cha moto ni mteja wao.

  "Mtu anaweka pasi kwenye umeme,halafu anapomaliza kunyoosha nguo hazimi swichi ya umeme,ikitokea bahati mbaya kukatokea moto lawama zinakwenda TANESCO wakati sababu za moto ni mteja.Hata hivyo hatuwezi kukwepa moja kwa moja ,hivyo sote tunaotumia umeme kuchukua tahadhari kuondoa hizi lawama," amesema Dk. Mwinuka na kuwaomba wateja wao kuwa sehemu ya kuondoa tatizo la moto.

  Kuhusu TANESCO kutumia magrupu ya WhatsApp kutoa taarifa kuhusu umeme kwa wateja wao,amesema magrupu hayo yanasaidia sana kutoa taarifa kwa haraka na uhakika.Ametoa rai kwa TANESCO kwa wilaya na mikoa yote nchini kuhakikisha kunakuwa na magrupu hayo na kuhakikisha wananchi wengi wanajiunga nayo kwa lengo la kutoa na kupokea taarifa zinazohusu umeme nchini.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, TANESCO Dkt. Tito Mwinuka (kushoto), akiwa na Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Shirika hilo anayeshughhulikia usambazaji na huduma kwa wateja, Mhandisi Raymond Seya, (wakwanza kulia), Meneja Mwandamizi wa TANESCO anayeshughulikia Miradi, Mhandisi Emmanuel G. Manirabona, wakati akizungumza kwenye majumuisho ya ziara ya wahariri wa vyombo vya habari waliokuwa wakitembelea mradi wa ukarabati na uimarishaji miundombinu ya umeme, TEDAP, na ule wa Kenya-Tanzania Power Interconnection Project (KTPIP) TII jijini Arusha.
  Dkt. Mwinuka na wasaidizi wake, wakiwa na wahariri.
  Dkt, Mwinuka akisikilzia kwa makini maoni na maswali kutoka kwa wahariri
  Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, akifungua kikao hicho.

  Meneja Mwandamizi wa TANESCO Kanda ya Kaskazini, Mhandisi Stella Hiza, akijitambulisha. Picha na
  K-VIS BLOG/Khalfan Said, Arusha

  0 0


  Na Rhoda Ezekiel,Kigoma

  WANAFUNZI wa Shule ya Msingi Kichacha katika Kijiji cha Kichacha Kata ya Kasanda wilayani Kakonko mkoani Kigoma wameipongeza Serikali kwa kuwajengea madarasa na kuwatoa chini ya mti walikokuwa wakisomea awali.

  Pongezi hizo wamezitoa jana baada ya Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala kutembelea shule hiyo na kukuta watoto wakiwa katika vyumba vya madarasa tofauti na awali walipokuwa wakisomea katika nyumba ya miti.

  Mwanafunzi wa darasa la tano katika shule hiyo Kulwa Anania amesema walikuwa wakipata wakati mgumu pindi mvua zilipokuwa zikinyesha kwani walikuwa hawaendi shule kwa kuwa walikuwa hawana eneo zuri la kusomea na ilikuwa ikisababisha kushuka kwa ufaulu katika masomo.

  Amesema wanaipongeza Serikali kwa kutatua changamoto yao waliokuwa nayo na sasa wanaendelea kusoma vizuri katika mazingira mazuri na wanaipongeza serikali kwa jitihada wanazo zifanya.Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Msingi Kichacha Emanuel Siwija amesema kwa mwaka 2017/2018 walipokea jumla ya Sh. milioni 42 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa na vyoo matundu manne na ofisi moja, ambapo mpaka sasa ujenzi huo umekamilika na wanafunzi wanatumia vyumba hivyo.

  Amesema awali wanafunzi hao walianza kusomea chini ya mti ,na baadae wakajenga kijumba cha miti kwa ajili ya kujihifadhi na 2018 ndipo walipopata madarasa na mpaka sasa upungufu ni mdogo.Ameongeza kwa mwaka jana wao kama shule kwa matokeo ya darasa la nne wameshika nafasi ya pili katika Wilaya na wanaendelea kupambana kuhakikisha wanafunzi wote wanafaulu kwa kuwa nyenzo za kufundishia wanazo na Serikali imetoa madawati kupitia Mkuu wa Wilaya.

  Akiwa katika ziara ya kukagua shughuli za maendeleo Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala, amesema wao kama Serikali wamejitahidi sana kuhakikisha suala la upungufu wa vyumba vya darasa linapungua na kuhakikisha Wanafunzi wanapata elimu na katika mazingira bora ya kusomea .

  Amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wananchi kuhakikisha watoto wote wanapata elimu, na kuwaomba wananchi kuendelea kushirikiana na Serikali kuchangia shughuli za maendeleo bila kujali itikadi zao.

  Aidha Mkuu huyo alitoa mwito kwa Wananchi wa Wilaya hiyo kuwapuuza Wale wote wanaowashawishi wananchi kuacha kujitolea katika shughuli za maendeleo kwa kuwa maendeleo yote yanaletwa na Wananchi kwa kushirikiana na Serikali.
  Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kichacha katika Kijiji cha Kichacha Kata ya Kasanda wilayani Kakonko mkoani Kigoma,Kanali Ndagala ametembeea shule hiyo na kukuta watoto wakiwa katika vyumba vya madarasa tofauti na awali walipokuwa wakisomea katika nyumba ya miti.
  Shule ya msingi Kichacha ilivyo sasa

  Shule ya msingi Kichacha ilivyokuwa mwaka 2017

  0 0

  Muasisi na mwenyekiti wa  taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi amezindua Maktaba ya Shule ya Msingi Tandale Magharibi na kutoa wito kwa wanafunzi kuitumia vyema maktaba hiyo kujenga maarifa.
  Aidha amewataka wanafunzi kuilinda maktaba hiyo kama chanzo cha maarifa na weledi.

  Maktaba hiyo imewezeshwa na taasisi hiyo kufuatia shindano la Andika Chalenge kwa shule za serikali nchini.Aliwataka pia wazazi kutekeleza jukumu lao la kushawishi watoto kusoma vitabu na kutumia maktaba na kuwa weledi katika masomo kwa kujisomea.

  Akizindua maktaba hiyo ambayo Taasisi iliikarabati, kuweka mashubaka pamoja na vitabu vya aina mbalimbali, Mwenyekiti wa Taasisi, Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi amesema amejisikia furaha kutimiza ahadi ya kukabidhi maktaba kwa shule hiyo iliyotoa mshindi.

  Katika  shindano hilo la uandishi la Andika Challenge ambalo linafanyika mikoa yote Tanzania na kushirikisha wanafunzi wote wa shule za msingi za serikali kuanzia darasa la 4 mpaka la 7 ambapo wanafunzi huandika hadithi na kutuma kwa sanduku la posta 163 Dar es salaam, washindi huzawadiwa tuzo na shule aliyotoka husaidiwa kuwa na maktaba.

  Shule ya Msingi Tandale Magharibi imepata maktaba hiyo baada ya mwanafunzi wake Nuurat Venance kushinda shindano la kutunga hadithi lililowashindanisha wanafunzi wa shule za msingi za manispaa za Kinondoni na Ubungo, jijini Dar es salaam.  Hivi sasa shindano hilo linawashindanisha wanafunzi  wote wa shule za msingi hapa nchini.

  Alisema baada ya mshindi kupatikana mwaka jana ambaye alitoka katika shule hiyo, taasisi ilibaki na changamoto ya kuwezesha kupatikana kwa maktaba, na anapoifungua maktaba hiyo anafurahishwa kuwa taasisi imetekeleza ahadi yake kwa mshindi wa shindano hilo.

  Jacqueline Mengi akizungumza katika makabidhiano hayo alisema kwamba nia kubwa wa shindano hilo ni kusaidia watoto kujua kusoma na kuandika na pia kuwa wabunifu na kutumia ubunifu wao kusonga mbele.Alisema pamoja na serikali kuwezesha elimu bure, wao kama taasisi wanatoa mchango wao ambao utasaidia kuimarishwa kwa tabia ya kusoma na kujipatia maarifa kutoka katika maktaba.

  Alisema taasisi ya Dk Ntuyabaliwe iliyoanzishwa kwa ajili ya kumuenzi baba yake ambaye alikuwa anapenda sana kujisomea vitabu na kuwahimiza watoto wake akiwemo yeye kujifunza kusoma,  kwa sasa inaendesha shindano hilo la Andika Challenge ili kuhakikisha kwamba wanafunzi wanajijenga katika ubunifu na matumizi wa lugha ya Kiswahili kwa kutunga hadithi zao wenyewe.

  Anasema kwa msimu huu mashindano hayo yanaendelea na kwamba vigezo vinavyostahili kufanywa na wanafunzi kuanzia darasa la 4 hadi la 7.
  Ikiamini kwamba kusoma na kuandika ndio njia pekee ya kukabiliana na wanafunzi wanaomaliza shule bila kujua kuandika Jacquline alisema kwa sasa wamewezesha shule 7 kuwa na maktaba, wanafunzi 4,406 kusaidia mambo mbalimbali na vitabu takaribani 20,827 kuwafikia wanafunzi.

  Mapema Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Grace Mtesigwa alisema kitendo cha kukabidhi maktaba kwa shule hiyo, Taasisi ya Dk Mtuyabaliwe imekuwa ikiunga mkono kwa vitendo jitihada za Rais John Magufuli za kuboresha elimu nchini.

  Wakitoa shukrani kwa niaba ya shule, Mwalimu Mkuu Doris Msigalo na Mwakilishi wa Wazazi  Sudi Makamba wameishukuru Taasisi na kusisitiza kuwa wataitumia na kuitunza vizuri maktaba hiyo.
  Muasisi na mwenyekiti wa  taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi akisalimiana na Mwakilishi wa Wazazi na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa,  Sudi Makamba mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Shule ya Msingi Tandale Magharibi kwa ajili ya tukio la kuzindua maktaba mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam.
  Muasisi na mwenyekiti wa  taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Tandale Magharibi mara baada ya kuwasili shuleni hapo kwa ajili ya tukio la kuzindua maktaba lililofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam.
  Muasisi na mwenyekiti wa  taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi akiuliza maswali kwa wanafunzi wa shule ya msingi Tandale Magharibi mara baada ya kuwasili shuleni hapo kwa ajili ya tukio la kuzindua maktaba lililofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam.
  Muasisi na mwenyekiti wa  taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi akiimba pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi Tandale Magharibi mara baada ya kuwasili shuleni hapo kwa ajili ya tukio la kuzindua maktaba  lililofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam.
  Muasisi na mwenyekiti wa  taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Tandale Magharibi mara baada ya kuwasili shuleni hapo kwa ajili ya tukio la kuzindua maktaba  lililofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam.
  Muasisi na mwenyekiti wa  taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi akikata utepe kufungua maktaba mpya ya shule ya msingi Tandale Magharibi iliyojengwa na taasisi hiyo jijini Dar es Salaam katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa juma. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mwalimu Mkuu  wa shule hiyo, Doris Msigalo (katikati), Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Grace Mtesigwa (wa kwanza kulia) pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo.
  Muasisi na mwenyekiti wa  taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi akikata utepe kufungua maktaba mpya ya shule ya msingi Tandale Magharibi iliyojengwa na taasisi hiyo katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Grace Mtesigwa, Mwakilishi wa Wazazi  Sudi Makamba, viongozi wa bodi ya shule pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo.
  Muasisi na mwenyekiti wa  taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Grace Mtesigwa wakipitia baadhi ya vitabu vilivyotolewa na taasisi hiyo kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya msingi Tandale Magharibi kujisomea na kuongeza maarifa.
  Muasisi na mwenyekiti wa  taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi akimkabidhi moja ya kitabu mwanafunzi  Nuurat Venance aliyeshinda shindano la kutunga hadithi “Andika Challenge” lililowashindanisha wanafunzi wa shule za msingi za manispaa za Kinondoni na Ubungo, jijini Dar es salaam na kupelekea shule yake kujengewa maktaba na taasisi hiyo.
  Muasisi na mwenyekiti wa  taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi akipewa mkono wa pongezi na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Grace Mtesigwa mara baada ya kuonyesha picha za muonekano wa jengo la maktaba ya shule ya msingi Tandale Magharibi lilivyokuwa awali.
  Muasisi na mwenyekiti wa  taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi akimkumbatia mwanafunzi  Nuurat Venance aliyeshinda shindano la kutunga hadithi “Andika Challenge” lililowashindanisha wanafunzi wa shule za msingi za manispaa za Kinondoni na Ubungo, jijini Dar es salaam na kupelekea shule yake kujengewa maktaba na taasisi hiyo.
   Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Tandale Magharibi, Doris Msigalo akitoa neno la shukrani Muasisi na mwenyekiti wa taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi mara baada ya kuwakabidhi jengo jipya la maktaba shuleni hapo.
  Muasisi na mwenyekiti wa  taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi  katika picha ya pamoja na uongozi wa Shule ya msingi Tandale Magharibi na baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo mara baada ya kufungua maktaba mpya iliyojengwa na taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.
  Muasisi na mwenyekiti wa taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi  akisalimiana na Mama mzazi wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Bi. Sandrah aliyemwakilisha mtoto wake aliyesoma shule ya msingi Tandale Magharibi kushiriki halfa ya uzinduzi wa maktaba mpya shuleni hapo.Katikati ni Dj wa Diamond Platnumz Romy Jones.
  Muasisi na mwenyekiti wa taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi  katika picha ya pamoja na Mama mzazi wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Bi. Sandrah (wa pili kulia), Dj wa Diamond Platnumz Romy Jones (wa pili kushoto), Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Grace Mtesigwa (kulia) pamoja na dada wa Diamond Patnumz, Esma Platnumz.
  Baadhi ya walimu wa Shule ya Msingi Tandale Magharibi wakipiga ‘Selfie’ na Muasisi na mwenyekiti wa taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi  mara baada ya kufungua maktaba mpya shuleni hapo.

  0 0
 • 01/28/19--03:24: GARI INAUZWA.
 •  Make : Toyota Allion
  Mileage : 58,800Km
  Condition : Good condition,Original Seats ,Ac,New Tyres.
  Price : 9.5M
  Location : Makumbusho
  Engine : CC1790
  Contacts : 076 61 12445
   


older | 1 | .... | 1788 | 1789 | (Page 1790) | 1791 | 1792 | .... | 1904 | newer