Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1787 | 1788 | (Page 1789) | 1790 | 1791 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba wamefanya kikao kati yao na wataalam kutoka Taasisi mbalimbali nchini Tanzania walio katika Timu ya Kitaifa ya Majadiliano ya Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Uganda hadi Tanzania.

  Kikao hicho kinachofanyika Kampala – Uganda ni cha maandalizi kabla ya kufanyika kikao na Mawaziri wa Uganda wanaohusika na mradi huo baadaye leo.

  Kikao cha Mawaziri wa Tanzania na Uganda wanaohusika na mradi huo kinafanyika kufuatia majadiliano ya wataalam wa nchi hizi mbili yaliyoanza tarehe 21/1/2019 na kufuatiwa na Kikao cha Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali zinazosimamia mradi kutoka Tanzania na Uganda kilichofanyika tarehe 24/1/2019 Kutoka kushoto ni Januari Makamba Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, William Lukuvi Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk.Merdad Kalemani Waziri wa Nishati, Profesa Paramagamba Kabudi Waziri wa Sheria na Katiba Mawaziri kutoka Jamhuri ya Muungano ya Tanzania wanaohudhuria kikao kuhusu maandalizi ya ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda mpaka Tanga nchini Tanzania kinaofanyika leo nchini Uganda.

  Mawaziri kutoka Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Jahuri ya Uganda wakiwa katika mkutano kuhusu maandalizi ya ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda mpaka Tanga nchini Tanzania unaofanyika leo nchini Uganda.
  Baadhi ya wataalam wakiwa katika mkutano huo.
  Makatibu wakuu wa wizara mbalimbali kutoka nchini Tanzania wakihudhuria mkutano huo.
  Baadhi ya maofisa kutoka Tanzania wakihudhuria mkutano huo.

  0 0

  Na Amisa Mussa

  MKUU  wa  Mkoa  wa  Tabora  Aggrey Mwanri ameahidi kuwashughulikia wataalam wa afya wanaowatoza fedha  wajawazito wakati kutaka kujifungua.

   Pamoja na mambo mengine amesema kwa sasa wanaendelea kuboresha upatikanaji wa huduma za afya pamoja na kupunguza vifo vya mama na mtoto mkoani humo.

  Akizungumza katika kampeni za  Bima ya Afya ya Jamii(CHF) iliyoboreshwa pamoja na Kampeni ya  Jiongeze Tuwavushe salama ,Mwanri ametumia kampeni hizo kuwanyooshea vidole baadhi ya watoa huduma za afya ambao wanawatoza fedha wanawake wajazito wanakwenda kujifungua katika vituo vya afya na zahanati.

  Mwanri amesema hatosita kumchukulia hatua za kinidhamu mtumishi wa afya atakayebainika kumtoza fedha mama mjamzito.

  Katika hatua nyingine Mwanri ametoa onyo kwa wakurugenzi wa  Halmashauri  za  Wilaya  mkoani humo ambao  wamezembea  kuwasajili  wazee  na  kufungua  madirisha  maalum ya  kuwahudumia  katika hospitali  na zahanati zilizopo kwenye maeneo yao.

  Kuhusu uzinduzi  wa  kampeni  hizo  imekwenda  pamoja na  Serikali ya  Mkoa  wa  Tabora  kupokea  magari  madogo  nanne ya kubeba wagonjwa kutoka Shirika  Care  International kupitia  mradi  wa  Tamani yenye  thamani  ya zaidi ya Sh.Milioni 184.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Kulia) akichangia Mjadala wa Changamoto za Usalama na uhaba wa Chakula Duniani tarehe 24 Januari 2019 Davos, Uswisi
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine akizungumza na Rais wa WEF, Mhe. Borge Brende tarehe 25 Januari 2019 Davos, Uswisi
  Mhe. Waziri Mahiga akifanya mazungumzo na  Bi. Rachel Samren, Makamu wa Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Millicom (Millicom International Cellular S.A) tarehe 25 Januari 2019 Davos, Uswisi.  Tanzania imesisitiza umuhimu wa kukabili uhaba wa chakula kwa kuzalisha mazao kwa kutumia utalaamu wa kisasa kwa kuwpatia wakulima pembejeo na masoko ya uhakika ya chakula cha ziada.

  Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb) wakati wa kuchangia mjadala unaohusu uhakika wa chakula na changamoto za uhaba wa chakula duniani katika mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani (World Economic Forum-WEF) unaofanyika Davos, Uswisi kuanzia tarehe 22 hadi 25 Januari 2019.

  Mhe. Mahiga alimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika jukwaa hilo ambalo kaulimbiu ya mwaka huu ni Kutengeneza Mazingira ya Utandawazi wa Dunia kwa ajili ya Mapinduzi ya Kisasa ya Nne ya Viwanda “Shaping a Global Architecture in the Age of the Fourth Industrial Revolution”.

  Katika mkutano huo, ajenda kuu zilizojadiliwa ni pamoja na Mapinduzi ya Nne ya Viwanda, Agenda ya Afrika ya Maendeleo, Hali ya Ulinzi na Usalama Pembe ya Afrika, changamoto za biashara ya kimataifa, ushirikiano wa Bara la Ulaya na Afrika katika ajenda mpya ya maendeleo.

  Tanzania ilialikwa kuchangia mjadala unaohusu uhakika wa chakula na changamoto za uhaba wa chakula duniani pamoja na ajenda ya uwezeshaji wa mawasiliano ya simu za mkononi. Katika ajenda hiyo, Tanzania ilitoa wito wa umuhimu wa teknolojia katika kuboresha utaalamu katika sekta ya kilimo kwa ajili ya kuwawezesha wakulima wadogo waliopo vijijini.

  Hili ni Jukwaa la pekee ambalo linakutanisha kwa pamoja Viongozi wa Serikali kutoka mabara yote duniani, Taasisi na Mashirika ya Kimataifa, Viongozi wa Makampuni Makubwa ya Kibiashara kwa ajili ya kujadili maendeleo na mwelekeo wa uchumi duniani.

  Kando ya Mkutano huo, Mhe. Dkt. Mahiga alikutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa mashirika na makampuni ambayo yapo Tanzania na yanayohitaji kupanua wigo kama vile Tigo na General Electric na makampuni yanayotafuta fursa za kuwekeza Tanzania. Aidha, alikutana na Rais wa WEF, Mhe. Borge Brende ambapo aliahidi kushawishi wawekezaji kuwekeza Tanzania na kuandaa Jukwaa la wawekezaji wa kimataifa la Tanzania ili waweze kuwekeza Tanzania.

  Viongozi wengine waliokutana na Waziri Mahiga ni pamoja na; Bw. Scott Strazik, Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Gesi yenye Makao makuu yake Atlanta, Georgia- Marekani; Bw. Richard Hatchett, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kupambana na magonjwa ya Mlipuko (Coalition for Epidermic Preparedness Innovations); Bi. Rachel Samren, Makamu wa Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Millicom ambayo TIGO ni Tawi la Kampuni hiyo, na Bw. Mohamed Al-Beity, Mtanzania aliyetambuliwa na Jukwaa la Uchumi Duniani kwa mradi wa kutangaza Utalii wa Tanzania kwa njia ya Mtandao (Tanzania Digital Tourism).


  Imetolewa na:
  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
  Dodoma
   26 Januari 2019


  0 0

   Waziri Ummy Mwalimu baada ya kutoa tamko la maadhimisho ya siku ya ukoma Duniani ambayo itafanyika kesho akiwakabidhi waathirika wa ukoma chakula kwenye makazi yaliyopo Nunge wilayani Kigamboni.Siku ya ukoma Kitaifa itafanyika kesho makazi ya watu waishio na ukoma Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro
   Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,,Jinsia Wazee na Watoto akiwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni Rachel Mhando,Viongozi wa wizara pamoja na wazee hao wakitoa ujumbe wa kuashiria kuondoa unyanyapaa dhidi ya waathirika wa ukoma.
   Waziri  wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwapa mikono waathirika wa ugonjwa wa mikono wanaoishi makazi ya Nunge wilayani Kigamboni ikiwa ni ishara ya kuondoa unyanyapaa kwa waathirika wa ukoma
   Waziri  wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwapa mikono waathirika wa ugonjwa wa mikono wanaoishi makazi ya Nunge wilayani Kigamboni ikiwa ni ishara ya kuondoa unyanyapaa kwa waathirika wa ukoma

   Waziri Ummy Mwalimu akitoa tamko la siku ya ukoma Duniani ambapo aliwasisitiza wananchi kujenga tabia ya kuchunguza miili yao pamoja na watoto kama kuna mabaka rangi ya shaba  yasiyo na hisia na kuwahi hospitalini mara waonapo dalili hizo.
   Mwaathirika wa ugonjwa wa Ukoma Vumilia Chambuso akitoa Shukrani kwa Waziri wa Afya,Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu mara baada ya kutoa tamko la maadhimisho ya Siku ya Ukoma katika makazi ya Ninge Jijini Dar es Salaam.
   Askari akimuongoza mtuhumiwa anayedaiwa kuuza maeneo katika makazi ya Nunge baada ya kutajwa na mmoja ya mkazi wa makazi ya Nunge. 
  Kamishina Msaidizi wa Idara ya Ustawi wa Jamii Rabikila Mushi akitoa taarifa kwa Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katika makazi ya Nunge.


  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

  Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema jamii imekuwa na mtazamo hasi na kufanya wagogonjwa wa ukoma umekuwa kuogopwa na kuweka unyanyapaa na kufanya wagonjwa hao kuogopwa kuwa tegemezi na kutothaminiwa.

  Ummy ameyasema hayo wakati akitoa tamko la maadhimisho ya siku ya Ukoma Duniani ambayo hufanyika Jumapili ya mwisho ya Januari iliyofanyika katika makazi ya Nunge Kigamboni jijini Dar es Salaam.

  Amesema tunaadhimisha miaka 60 ya uwepo wa Shirika la Ujerumani linaloshughulikia masuala ya Kifua kikuu na Ukoma (GLRA). Shirika hili limekuwa mstari wa mbele katika kuisaidia serikali kuhakikisha Ukoma unatokomezwa kwa kufadhili shughuli mbali mbali ikiwa ni pamoja na kutoa vyombo vya usafiri kwa waratibu wa Kifua kikuu na Ukoma nchi nzima.


  Ummy Siku ya Ukoma Duniani inatupa fursa ya kutathmini mwelekeo wa jitihada zetu nchini na zile za kimataifa katika kupambana na ugonjwa huu kwa kauli mbiu katika maadhimisho ya mwaka huu ni “Tutokomeze Ubaguzi, Unyanyapaa na Chuki dhidi ya Waathirika wa Ukoma.

  Aidha amesema waathirika wengi wa Ukoma wananyanyapaliwa na kubaguliwa katika maeneo mengi, takriban asilimia 50 ya wagonjwa wa Ukoma hupatwa na sonona na huishi maisha ya huzuni na wasi wasi mkubwa.

  Amsema wadau na wananchi wote wanahimizwa kuungana na kuongeza nguvu katika kupinga matukio vyote vya ubaguzi na unyanyapaa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha hakuna sheria kandamizi kwa watu walioathirika na ugonjwa wa Ukoma. Kwa kufanya kazi pamoja na kupinga kwa nguvu zote vitendo hivi itatusaidia kupiga hatua mbele kuelekea kutokomeza Ukoma.

  Ummu amesema nchi imefikia viwango vya utokomezaji wa Ukoma kitaifa mwaka 2006 kwa kiwango cha chini cha mgonjwa mmoja (1) kati ya watu 10,000, na kwa mujibu wa takwimu za Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua kikuu na Ukoma (NTLP) za mwaka 2017, jumla ya wagonjwa wapya 1,933 waligunduliwa na hivyo kufanya kiwango cha ugunduzi kuwa watu wane (4) kwa kila watu 100,000 na nchi kuwa . miongoni mwa nchi 22 zenye wagonjwa wengi wa Ukoma duniani nchi nyingine ni pamoja na India, Indonesia, Brazil, Ethiopia, Msumbiji, Nigeria na DRC Kongo.

  Amesema mikoa 10 iliyogundulika na wagonjwa wapya wa Ukoma wengi zaidi kila mwaka na kuchangia karibia 80% ya wagonjwa wote ni Mikoaya Lindi, Rukwa, Mtwara, Morogoro,Pwani,Tanga,Geita,Dodoma,Tabora na Kigoma na Wilaya 20 ambazo hazijafikia lengo la utokomezaji ugonjwa ni Liwale, Lindi vijijini, Nachingwea, Ruangwa, Nanyumbu, Masasi mjini, Pangani, Mkinga, Korogwe, Mvomero, Kilombero, Morogoro vijijini, Ulanga, Shinyanga Manispaa, Mafia, Rufiji, Kilwa, Chato, Nkasi, na Mpanda.

  Ametoa rai kwa jamii, wazazi na walezi kuwa sote tujenge tabia ya kuchunguza miili yetu na ya watoto wetu endapo utaona mojawapo ya dalili za Ukoma ambazo ni baka au mabaka mwilini yenye rangi ya shaba na hayana hisia, vijinudu kwenye ngozi au mishipa ya fahamu kuvimba na dalili zingine nyingine ni ganzi kwenye mikono na miguu unashauriwa kwenda kwenye kituo cha tiba kilicho karibu nawe kwa uchunguzi bila kuchelewa.

  Ugonjwa wa Ukoma unatibika. Mgonjwa aliyeanza tiba hawezi kuambukiza mtu mwingine na hivyo hakuna sababu ya kumtenga na anaweza kuendelea na shughuli za kawaida za maisha.

  "Nachukua nafasi hii kwa niaba ya serikali ya awamu ya tano ya Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuyashukuru mashirika mbali mbali ya ndani na nje yanayounga mkono juhudi zetu za kutokomeza Ukoma nchini”amesema Ummy

  0 0  Waziri wa Maji na Umwangiliaji Profesa Makame Mbarawa (mwenye kofia nyeusi) akiwa ameongozana na msimamizi wa miradi alipofanya ziara katika Kata ya Goba, Manispaa ya Ubungo manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na kuwahakikishia wakazi hao kupatiwa maji ifikapo Februari Mosi mwaka huu. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

  Waziri wa Maji na Umwangiliaji Profesa Makame Mbarawa (mwenye kofia nyeusi) akipata maelezo toka kwa msimamizi wa miradi mara alipofanya ziara katika Kata ya Goba, Manispaa ya Ubungo manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Moja ya mita za maji ambazo zimeshasafungwa kwa wakazi wa Goba Kinzudi jijini Dar es Salam.  
  Ziara ikiendelea...

  Waziri wa Maji na Umwangiliaji Profesa Makame Mbarawa (kulia) akijibu hoja za mkazi wa Goba Kinzudi jijini Dar es Salaam Waziri wakati alipofanya ziara katika Kata ya Goba, Manispaa ya Ubungo manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na kuwahakikishia wakazi hao kupatiwa maji ifikapo Februari Mosi mwaka huu.

  Mkazi wa Goba Kizudi jijini Dar es Salaam Waziri akitoa shukrani zake za pekee mbele ya wanahabari kwa Serikali jinsi ambavyo imepanga kuwapatia maji.
  Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS)
  Waziri wa Maji na Umwangiliaji Profesa Makame Mbarawa (kulia) akijibu hoja za mkazi wa Goba Kinzudi jijini Dar es Salaam Waziri wakati alipofanya ziara katika Kata ya Goba, Manispaa ya Ubungo manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na kuwahakikishia wakazi hao kupatiwa maji ifikapo Februari Mosi mwaka huu.


  Mkazi wa Goba Kinzudi akimshukuru waziri kufika eneo lao na kusikiliza changamoto zao. 
   
  Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 
   
  Serikali imewathibitishia wakazi wa kata ya Goba, Manispaa ya Ubungo manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam uhakika wa kupata maji safi na salama kuanzia Februari mosi Mwaka huu. Akizungungumza baada ya kufanya ziara katika maeneo hayo, Waziri wa Maji na Umwangiliaji Profesa Makame Mbarawa amesema Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA ) imepeleka vijana wapatao 50 kukamilisha mradi wa usambazaji maji katika maeneo hayo.
   
   Amesema vifaa vyote vimefikishwa katika eneo hilo na vijana wameanza kazi rasmi. "Kuanzia Ijumaa Februari mosi maji katika maeneo haya yataanza kutoka na kila mwananchi atapata maji safi na salama hivyo naomba muendelee kuwa wavumilivu wakati shughuli ya uunganishwaji mabomba inaendelea," amesema Profesa Mbarawa. 
   
  Amesema katika mitaa ya Kinzudi na kwa Ubarikio zilizopo katika kata hizo wanatarajia kuunganisha wateja wapya mia saba (700) ambao wanatarajia kuongeza mapato ya DAWASA. "Tunakiri kukosea kwa kuwa hakukuwa na haja ya mradi huo kuchelewa kutokana na kutekeleza miradi mingi kwa wakati mmoja na sasa tumekubaliana kuwekeza nguvu katika mradi mmoja na utakapokamilika tunahamia mwingine kwa wingi," amesema. 
   
  Kwa upande wao wakazi wa Mtaa hiyo wameishukuru serikali kwa kuwaahidi kupata maji kwani wamekuwa wakiteseka kwa kutumia muda mrefu kutafuta maji. Mmoja wa wakazi hayo Juma Saidi amesema wamechimba mitaro ili wapatiwe huduma hiyo ambapo kwa sasa wanaishukuru DAWASA kuwatua mzigo huo. "Huku kwetu maji yamekuwa ni lulu maana yanauzwa shilingi 500 kwa ndoo jambo linalotufanya kuhangaike hata kuyapata," amesema.

  0 0

  Na Ahmed Mahmoud Arusha

  Wananchama na viongozi wa Umoja wa Wanawake nchini (UWT) wametakiwa kujenga mshikamano na umoja sanjari na kuhamasisha wenzao kuungana kwa pamoja kujenga maendeleo na kuibua kero mbali mbali ili ziweze kupatiwa ufumbuzi na serikali.

  Akiongea kwenye kikao cha majumuisho kilichoshirikisha mikoa ya Singida,Manyara,Tanga,Kilimanjaro na wenyeji Arusha Katibu mkuu wa umoja huo Queen Mlonzi amewaambia kuwa upendo ndio silaha kuu ya wanawake katika kukabiliana na majukumu ya ujenzi wa taifa na Familia hivyo mafunzo waliotoa ni shemu ya kujenga jamii.

  Amewataka wanawake kujenga na kuacha kupeleka maneno huko na huko kwani wao ni sehemu ya taifa na wanamchango mkubwa wa kuisaidia nchi kufikia malengo tarajiwa ya uchumi wa kati mbali na changamoto mbali mbali wanazokutana nazo.

  “Kwenye ziara hii tumekutana na changamoto mbali mbali za migogoro ya wananchi ikiwemo lishe duni,elimu,ukekektaji na ndoa za utotoni haya tumeyafundisha kwenye semina zetu kote tulipo pita nyie viongozi mkawe mabalozi wazuri wa kuhubiri na kuyafanyia kazi hizi changamoto kwenye jamii zenu zinazowazunguka”alisisitiza Mlonzi.

  Kwa Upande wake Naibu Katibu mkuu wa umoja huo Jesca Mbogo amesema kuwa wanawake Kote nchini wanawajibu wa kuhakikisha lishe duni inakuwa historia ndani ya mikoa yetu hadi ngazi za familia kwa kuishi kwa upendo na kuwajali wenzetu pindi tunapoona wana matatizo tuwasaidie kwa hali na mali.

  Amesema kuwa tukiishi kwa mshikamano na umoja tutafikia kwenye malengo ya uzalendo utakaopelekea kuona mchango wa maendeleo kwenye taifa letu tuishi kwa kuhubiri upendo ili kuweza kuitunza amani yetu na umoja wetu kama wanawake na mwisho wa siku taifa liendelee.

  Ameinyooshea kidole baadhi ya halmashauri kushindwa kutoa mikopo kwa kina mama kwa wakati hali inayowafanya kushindwa kuzichangamkia fursa za kimaendeleo hivyo kuwataka kuwapatia mikopo wakinamama na vijana kwa wakati na kuwafuta huko walipo 

  “Ziara hizi ambazo tumefanya semina mbali mbali kuhusiana na masuala ya Ukeketaji,Elimu,Lishe duni na Ndoa za utotoni ambazo zipo kwenye jamii yetu ili kuondoa changamoto na kuweza kuisaidia serikali kufikia malengo ya maendeleo kwani ukimueleimisha mwanamke ambaye ana usawishi mkubwa kwenye jamii utakuwa umeielimisha jamii nzima”alisema Mbogo.

  Awali mbunge wa viti maalum Catherine Mgige alitoa Pikipiki Saba kwa viongozi wa umoja huo kwa lengo la kuwawezesha viongozi hao kuwafikia wananchini na wananchama hadi vijijini ambao ndio malengo ya serikali kuwafikia wananchi wa hali ya chini kuweza kuwainua kiuchumi.

  Amesema kuwa pikipiki hizo ziwe chachu ya ushindi wa chama hicho kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mapema mwishoni mwa mwaka huu wakitanguliza mshikamano kama wanachama wa chama cha mapinduzi kwani umoja ni ushindi na mshikamano unahitajika bila kuyapa nafasi makundi kutugawanya.

  Nae mwenyekiti wa Umoja huo mkoani hapa Jasmin Bachu amewataka wanachama wa umoja huo kutembea vifua mbele kwa kazi inayofanywa na serikali ya Awamu ya tano chini ya Dkt.John Magufuli na kujipanga kuisaidia katika kuhakikisha malengo ya serikali yanatimia na wao kama mkoa na umoja huo wamejipanga kuyasemea yote yanayofanywa na serikali hii.

  Amesema kuwa wanawake wa mkoa wa Arusha wamejipanga kutekeleza maagizo yote yaliotolewa na viongzo wao wa ngazi ya taifa na kuyafanyia kazi kwa umoja wao na mshikamano na kuacha kusemana kwa kupeleka maneno upande huu na huu ambapo aliwaomba wenzao wa mikoa mingine kuja kujifunza Arusha na wao pia wataenda kujifunza kwao kwa lengo la kufikia kwenye umoja.

  “Kwa dhati nisema kuwa wanawake wenzangu wa mkoa wa Arusha tumejipanga kuhakikisha umoja na mshikamano utakaopelekea ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi ujao wa serikali za mitaa ili yote mlio yasema kwenye ziara yenu viongozi wangu tutyafanyia kazi kwa vitendo na tutayaishi katika maisha yetu”alisema Bachu

  0 0

   Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(aliyevaa miwani) akikagua mashamba ya mahindi katika Gereza la Kilimo Mollo, Mkoani Rukwa mara baada ya kuwasili leo januari 26, 2019(wa kwanza kulia) ni Mkuu wa Gereza Mollo, SSP. Francis Nkurushi  akimuongoza Mkuu wa Jeshi hilo kujionea mashamba ya kimkakati katika mpango wa kuelekea kujitosheleza kwa chakula cha wafungwa magerezani.
   Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(aliyevaa miwani) akitoa maelekezo kwa watendaji wa Jeshi hilo wakati akikagua moja ya mashamba ya mahindi ya Gereza Mollo, Mkoani Rukwa alipofanya ziara ya kikazi katika Gereza hilo leo januari 26, 2019.
   Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(kulia) akikagua moja ya ghala la kuhifadhia mahindi yanayozalishwa katika Gereza Mollo.
  Mashamba ya mahindi katika Gereza la Kilimo Mollo yakiwa yamestawi kama inavyoonekana katika picha. Gereza hilo katika msimu wa kilimo wa mwaka 2018/2019 limelima jumla ya hekari 825 za zao la mahindi.
  . Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akiteta jambo na Mkuu wa Magereza Mkoani Rukwa, ACP. Jail Mwamgunda alipotembelea Gereza Mollo leo Januari 26, 2019.
  Maafisa na askari wa Gereza Mollo wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(hayupo pichani)alipotembelea Gereza hilo leo januari 26, 2019(Picha zote na Jeshi la Magereza).

  0 0

   Meneja Mahusiano wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Anjela Mziray akisisitiza jambo kwenye kikao kazi cha wanachama wa vyama vya waandishi wa habari mikoa ya Mtwara na Lindi.
   Meneja Uhusiano wa NHIF, Anjela Mziray akifafanua jambo, kulia kwake ni Kaimu Meneja wa Mkoa wa Mtwara, Gidion Katondo na Meneja wa Mkoa wa Lindi Bw. Emmanuel Mwikwabe, Kulia ni Wenyeviti wa Mtwara, Martina Ngulumbi na Christopher Lilai.
   Washiriki wa kikao kazi wakifuatilia mada juu ya shughuli zinazofanywa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
   Wanachama wa vyama vya waandishi wa habari mikoa ya Lindi na Mtwara wakifuatilia ufafanuzi wa     hoja mbalimbali.
   Sehemu ya wanachama hao wakifuatilia mada.
  Meneja wa Mkoa wa Lindi Bw. Emmanuel Mwikwabe akiwasilisha mada ya maboresho yaliyofanywa na Mfuko.


  Na Grace Michael, Mtwara 

  Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umewahimiza waandishi wa habari kushirikiana nao katika kuendelea kuelimisha na kuhamasisha wananchi kuhusu umuhimu wa bima ya afya pamoja na kushiriki kuulinda Mfuko huo ili uweze kudumu na kunufaisha wengi. 

  Rai hiyo imetolewa na Meneja Mahusiano wa NHIF, Anjela Mziray wakati wa kikao kazi kilichofanyika mkoani Mtwara kikihusisha wanachama wa vyama vya waandishi wa habari katika Mikoa ya Lindi na Mtwara. 

  “Nawaomba sana ndugu zangu tuendelee kushirikiana katika kuhakikisha tunahamasisha wananchi kupitia vyombo vyetu ili waelewe na kutumia huduma za Mfuko huu ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za matibabu lakini pia ili Mfuko uendelee kuwa imara tuendelee kuunganisha nguvu katika kuulinda Mfuko wetu,” alisema Mziray. 

  Alisema kuwa endapo wanahabari watashiriki vyema juhudi za Mfuko za kufikisha taarifa kwa wananchi zinazohusiana na umuhimu wa kutumia huduma za matibabu kwa mfumo wa bima, wananchi wengi wataweza kujiunga na hatimaye kuwa na uhakika wa kupata matibabu. 

  “Kwa sasa bima ya afya ndio suluhisho kwa huduma za matibabu kwa wananchi wetu na ili wafanikiwe kujiunga ni lazima tuhakikishe tunawafikia kwa njia mbalimbali ikiwemo ya elimu na uhamasishaji hivyo kama ambavyo mmekuwa wadau wazuri wa Mfuko tangu mwanzo tuendelee kuwafikia wananchi wetu kupitia program mbalimbali za uelimishaji,” alisema Bi. Mziray. 

  Kwa upande wa wanachama wa vyama vya waandishi wa habari katika Mikoa ya Lindi na Mtwara, wameupongeza Mfuko kwa juhudi kubwa ambazo umefanya hususan za kuanzisha mpango wa Ushirika Afya ambao utawasaidia kwa kiwango kikubwa wakulima ambao awali hawakuwa na fursa hiyo. 

  “Mfuko umekuwa ni mkombozi mkubwa kwa afya za wananchi wengi tukiwemo na sisi waandishi wa habari, mfano mzuri sisi wa Mkoa wa Lindi na Mtwara ni wanufaika na tumeweka kipaumbele sana katika suala hili kwa kuwa tunafahamu kabisa kuwa gharama za matibabu ni kubwa na bila bima ya afya ni ngumu mtu kumudu gharama hizo, hivyo niendelee pia kuwahamasisha wanahabari wa mikoa mingine kuhakikisha wanajiunga na Mfuko lakini pia kuendelea na uhamasishaji,” alisema Katibu wa Chama cha Waandishi wa Mkoa wa Lindi Bw. Christopher Lilai. 

  Mfuko umesema unaendelea na maboresho mbalimbali ya huduma zake ikiwemo kuongeza wigo wa wanachama kupitia makundi mbalimbali lakini pia upatikanaji wa huduma za matibabu kirahisi kupitia uimarishaji wa mifumo wa TEHAMA.


  0 0

  Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na Mtandao wa Wabunge wa kupambana na Rushwa (APNAC) pamoja na wawezeshaji wa semina (hawapo kwenye picha), wakati wa semina ya mafanikio na changamoto katika utekelezaji wa sheria ya wakala wa vipimo na mizani iliyofanyika leo tarehe 26 Januari, 2019 katika hoteli ya Dodoma Jijini Dodoma. 
  Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akifungua semina ya mafanikio na changamoto katika utekelezaji wa sheria ya wakala wa vipimo na mizani iliyofanyika leo tarehe 26 Januari, 2019 katika hoteli ya Dodoma Jijini Dodoma.
  Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa pili kulia) akimsikiliza Mwenyekiti wa Mtandao wa Wabunge wa kupambana na Rushwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Mkuchika (wa pili kushoto) wakati wa semina ya mafanikio na changamoto katika utekelezaji wa sheria ya wakala wa vipimo na mizani iliyofanyika leo tarehe 26 Januari, 2019 katika hoteli ya Dodoma Jijini Dodoma. Kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Joseph kakunda na kushoto ni Katibu wa Mtandao wa Wabunge wa kupambana na Rushwa, Mhe. Daniel Mtuka
  Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akiteta jambo na Mwenyekiti wa Mtandao wa Wabunge wa kupambana na Rushwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Cpt. George Mkuchika wakati wa semina ya mafanikio na changamoto katika utekelezaji wa sheria ya wakala wa vipimo na mizani iliyofanyika leo tarehe 26 Januari, 2019 katika hoteli ya Dodoma Jijini Dodoma. 
  Afisa Mtendaji Mkuu wa wakala wa vipimo na mizani, Dkt. Ludovick Manenge akizungumza na wajumbe wa Mtandao wa Wabunge wa kupambana na Rushwa (APNAC) wakati wa semina ya mafanikio na changamoto katika utekelezaji wa sheria ya wakala wa vipimo na mizani iliyofanyika leo tarehe 26 Januari, 2019 katika hoteli ya Dodoma Jijini Dodoma. 
  Mjumbe wa Mtandao wa Wabunge wa kupambana na Rushwa (APNAC) na Mbunge wa Mufundi, Mhe. Cosato Chumi akizungumza jambo wakati wa semina ya mafanikio na changamoto katika utekelezaji wa sheria ya wakala wa vipimo na mizani iliyofanyika leo tarehe 26 Januari, 2019 katika hoteli ya Dodoma Jijini Dodoma. 
   
  Wajumbe wa Mtandao wa Wabunge wa kupambana na Rushwa wakiwa katika semina ya mafanikio na changamoto katika utekelezaji wa sheria ya wakala wa vipimo na mizani iliyofanyika leo tarehe 26 Januari, 2019 katika hoteli ya Dodoma Jijini Dodoma.PICHA NA OFISI YA BUNGE)


  Na.Alex Sonna,Dodoma

  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano La Tanzania Job Ndugai amesema bado kuna tatizo kubwa katika vipimo sahihi wakati wa ununuzi wa mazao kutoka kwa wakulima licha ya kuwepo kwa Sheria ya vipimo.

  Hayo ameyasema leo jijini Dodoma alipokuwa akifungua Semina ya wabunge juu ya changamoto na mafanikio ya sheria ya vipimo ikiwa ni pamoja na wabunge hao kutoa michango yao katika semina hiyo jinsi ya kupambana na rushwa katika vipimo.

  Wabunge hao ni wanachama wa hiari wa chama cha kupambana na vitendo vya rushwa APNAC ambao hutoa michango juu ya kupambana na rushwa na kuifikisha panapo husika.Spika amesema kuwa wakulima wamekuwa wakinyonywa sana na baadhi ya wafanyabisha kwa kutumia vipimo ambavyo si sahihi ikiwemo ufungaji wa mazao kwa njia ya lumbesa.

  “Rasilimali nyingi zimekuwa zikipotea kutokana na ufungashaji kwa njia ya lumbesa , na nyinginezo ambazo si rasmi tufikie wakati tuwe na sheria kali zaidi kwani wakulima wetu wamenyonywa na kupunjwa vya kutosha” amesema Ndugai

  Akitolea ufafanuzi kuhusiana na vipimo vya magari ya mizigo Spika alishangazwa kuona kuwa magari hayo licha ya kupita katika mizani mbalimbali lakini bado yanzuiwa sehemu Fulani kwa sababu ya kutakiwa kupimwa tena.

  Aidha amesema kuwa hali hiyo imekuwa ikiwakera wananchi kwani hawaelewi nini tatizo mpaka kuwepo kwa vipimo kila sehemu na kufanya msururu wa magari kuwa mkubwa kusubiri kupimwa.“Kama ni magari ya mizigo inawezekana wakaongeza njiani lakini kama wale wanaosafirisha mafuta kweli jamani tuliangalie na hilo tuliangalie” amesisitiza

  Spika Ndugai amesema kuwa hali hiyo ni chimbuko la rushwa kwani kama mfanyabishara anayesafirisha mafuta ameshapima vituo vyote hakuna sababu ya kumzuiakwani uwezekano wa kuongeza ujazo wa mafuta njiani ni mdogo.

  Awali akitoa taarifa ya awali kwa wabunge wanachama wa chama cha wabunge wanapambana na rushwa (APNAC) Katibu wa APNAC Daniel Mtuka alisema APNEC iliundwa mwaka 2000.Hata hivyo amesema kuwa madhumuni ya kuundwa kwake ni kupambana na rushwa mara baada ya kuona vitendo vya rushwa vinazidi.

  Pia amesema kuwa wabunge waliokuwepo kipindi hicho waliona kuna umuhimu wa kuanzisha kikundi cha wabunge ambao watapambana na rushwa.Spika Ndugai amesema kuwa APNAC ilifanikiwa mwaka 2007 kushiriki kuandaa sheria namba 11 ya TAKUKURU ambapo sheria hiyo ilikuwa na vifungu vine tu lakini sasa vipo 24

  Amesema kuwa bado Sheria ya Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa inahitaji marekebisho zaidi. Alisema kutokana na hali hiyo APNAC ilita mawazo wakati wa mchakato wa Bunge la katiba ambao alisema ungewabana zaidi wanaokamatwa na vitendo vya rushwa.

  “Tumeweza kutoa marekebisho mengi juu ya Sheria ya TAKUKURU na mengi yameweza kusaidia nchi yetu lakini bado tunaona ipo haja ya kuendelea kutoa mawazo yetu.Kwa upande wa vipimo Waziri wa Biashara na Viwanda Josph Kakunda amesema kuwa bado kuna changamoto kubwa katika suala la vipimo.Hata hivyo amesema kuwa kumekuwa na udanganyifu mkubwa kwa wafanyabiashara na madalali wanunuapo amzao toka kwa wakulima .

  “Vipimo kama vya Lumbesa, Madebe na hata vikopo bado vimekuwa vikitumika katika sehemu nyingi hapa nchini ingawa tunavikataa” amesema
  Amesema kuwa Wizara yake imeweza kujenga vituo vya msoko katika mipaka ili wakulima waweze kuuza mazao yao kihalali na uzito unaotakiwa.

  0 0

  *Lengo ni kujua changamoto zao, kuzitatua haraka

  Na Said Mwishehe-Blog ya Jamii-Arusha

  SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limeweka mfumo maalumu wa kutumia magurupu ya WhatsApp (Jukwaa), kwa lengo la kutoa na pokea taarifa za nishati ya umeme kwa wateja wao wa kada mbalimbali nchini.

  Akizungumza na leo jijini Arusha Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji, amesema kuanzishwa kwa magroup ya WhatsApp lengo ni kutoa taarifa kwa wateja wao nchini kote umetokana na maagizo ya bodi ya shirika hilo ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha wateja wanapata taarifa ya kila kinachoendelea kuhusu nishati ya umeme.

  “Tunatambua nguvu ya magurupu ya WhatsApp katika kufikisha taarifa kwa jamii, hivyo TANESCO tumeona hili na hivyo kupitia Bodi yakatoka maagizo maalumu kwa wilaya zote na mikoa nchini kuwahakikisha yanaanzishwa magurupu hayo.

  “Hivyo mameneja wa TANESCO kwa ngazi ya Wilaya na Mkoa yato nchini wameanzisha magurupu hayo kwa ajili ya kuwasiliana na wateja. Kupitia magurupu mbali ya kuwa na wateja wapo viongozi wa ngazi mbalimbali wa TANESCO na lengo ni kuhakikisha changamoto yoyote inayohusu umeme inatolewa kwa wakati ili wateja wetu wajue,” amesema Muhaji.

  Amesema tangu kuanzishwa kwa magurupu hayo kumeleta faida kubwa kwani hivi sasa wateja wa shirika hilo wanao uhakika wa kupata taarifa ya kila kinachoendelea na wakati huo huo wateja nao wanayo fursa ya kuwalisha changamoto iwapo zitajitokeza.

  Ameongeza katika kuhakikisha magurupu hayo yanaleta tija zaidi kwa ngazi ya Wilaya na Mkoa walichokifanya ni kuweka magurupu kulina na aina ya wateja, hivyo yapo magurupu kwa ajili ya wateja wakubwa ambapo miongoni mwao wamo wawekezaji.

  “Kuna magurupu ya wateja wa kati na magurupu ya wateja wa kawaida kuanzia ngazi ya mtaa hadi mkoa.“Tuliamua pia kwenye magurupu hayo wamo na viongozi wa ngazi mbalimbali wa Serikali ya mtaa, wakuu wa wilaya, wabunge na viongozi wengine wa Serikali ambao ni sehemu ya wadau muhimu katika kuhakikisha tunatatua changamoto za umeme.

  “Kwa maana hiyo hata Mkurugenzi Mtendaji wa shirika letu katika mtaa anaoishi ameunganishwa kama mteja wa TANESCO kwenye grupu la WhatsApp na wakati huo kama kiongozi,” amesema

  Alisema kupitia mfumo huo wamepata faraja kuona yamekuwa msaada mkubwa wa kufikisha taarifa zao kwa wateja huku akisisitiza kwa sasa wanahimiza wilaya zote za TANESCO kuhakikisha wanaanzisha magrupu hayo kwa wale ambao bado.

  Amesema kwa Dar es Salaam kupitia magurupu hayo wamekuwa wakipata taarifa kutoka wa wateja wao kwa haraka zaidi na watendaji wa Shirika wanatafuta ufumbuzi kwa haraka.Ukweli njia hii ya mawasiliano imekuwa na tija kubwa kwetu na tutaendelea kuitumia.

  Leila ambaye yupo kwenye ziara ya wahariri wa vyombo vya habari mkoani Arusha yenye lengo la kuangalia miradi mbalimbali ya umeme inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano amesisitiza umuhimu wa magurupu hayo ambapo wawekezaji wa mkoa huo wamekiri kuwa sasa imekuwa rahisi kwao kupata taarifa mara kwa mara.

  Wakizungumza na Blog ya Jamii baadhi ya wamiliki wa viwanda waliopo mkoani Arusha , wamesema kwa sasa wanajiona wenye thamani kutokana na namna ambavyo TANESCO imeamua kuwaweka karibu kupitia njia hiyo ya kuwasiliana.

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke John Bwana amewataka maafisa maendeleo wa wilaya hiyo kuwaangalia kwa jicho la pili wanafunzi waliohitimu mafunzo VETA.

  Ameyasema hayo katika mahafali ya wanafunzi 49 waliohitimu mafunzo ya Kozi ya Hotelia jana Jijini Dar es Salaam.Bwana amesema kuwa maafisa maendeleo wanatakiwa kuwaingiza wanafunzi hao katika vikundi ili wapate mikopo na kujiendeleza kiuchumi.

  Amesema kuwa, wanafunzi hawa wameweza kupata mafuno hayo kupitia Kanisa la Jeshi la l wokovu na haina budi kupata fursa za mikopo kwani ni msingi mzuri kwa maendeleo yao ya baadae.

  Askofu Mkuu wa Kanisa la Jeshi la Wokovu Colonel Wayne Bungay amewapongeza wanafunzi hao na kuwataka waende wakajiendeleze kupitia mafunzo hayo waliyoyapata kwani wao ni tegemeo kubwa kwa maendeleo ya taifa hili.Colonel Bungay amesema, mradi huu umesaidiwa na watu wa Kanisa la Jeshi la wokovu Uholanzi, Kanisa la Jeshi la Wokovu Norway sambamba na Serikali ya Norway kuunga mkono na kusaidiana kwenye mradi huo.

  Kwa upande wa Mkuu wa Chuo cha VETA Violet Fumbo amesema kuwa wanafunzi hawa wamepata mafunzo hayo na wameweza kufany vizuri na aanamini hawataufanyia mzaha na kuishia kuweka vyeti ndani.Amewataka wanafunzi hao kujiajiri na kuonyesha ujuzi wao ili jamii waweze kufahamu kuwa Chuo cha VETA kinatoa mafunzo bora na yenye weledi. 

  Mbali na kukabidhiwa vyeti wanafunzi waliofanya vizuri waliweza kukabidhiwa zawadi na Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke.Wanafunzi hao ni Damian Francis katika upande wa Food Production, Najat Mgaja kwa upande wa House Keeping, Hotel Management ni Turuki Mansour, Bakery ni Edna Msabi.

  Mafunzo haya yatamalizika 2021, kwa jumla ya wanafunzi 300 kutoka kata 5 za Wilaya ya Temeke kuchaguliwa katika vipindi tofauti ili kuweza kusoma katika Chuo cha Veta.Wanafunzi hao wanatoka katika kata za Miburani, Chamazi, Toangoma, Makangarawe na Kilakala.
  Askofu Mkuu wa Kanisa la Jeshi la Wokovu Colonel Wayne Bungay akizungumza na wahitimu waliomaliza mafunzo ya Hotelia kwenye Chuo cha VETA yakiwa ndani ya mradi wa Kanisa hilo, Kulia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeka John Bwana na Kushoto ni Rais wa vyama vya wanawake wa Jeshi la Wokovu Tanzania Colonel Deborah Bungay
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke John Bwana akizungumza na wahitimu na kuwapongeza kwa hatua waliyofikia ya kumaliza mafunzo ya Hotelia na kuwataka waende kujiendeleza ikiwemo na kuomba mikopo kutoka kwa Manispaa ili wajiajiri na kuacha kusubiri kuajiriwa
  Mkuu wa Chuo cha VETA Violet Fumbo amewashukuru Kanisa la Jeshi la Wokovu kwa kuona na kuthamini mchango wa vijana kwenye nchi kwa kuamua kuwapatia fursa ya kupata mafunzo ndani ya Chuo chake, jumla ya wanafunzi 49 wamemaliza mafunzo hayo na kukabidhiwa vyeti vya VETA leo Jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke John Bwana akikabidhi vyeti kwa baadhi ya wahitimu wa Kozi ya Hotelia kwenye mahafali jana Jijini Dar es Salaam, jumla ya wanafunzi 49 wamehitimu mafunzo hayo
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke John Bwana akikabidhi vyeti kwa baadhi ya wahitimu wa Kozi ya Hotelia kwenye mahafali   jana Jijini Dar es Salaam, jumla ya wanafunzi 49 wamehitimu mafunzo hayo
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke akitoa zawadi kwa mwanafunzi bora Damian Francis wakati wa mahafali ya wahitimu wa Mafunzo ya Hotelia walio katika mradi wa Kanisa la Jeshi la wokovu wakisoma katika chuo cha VETA leo Jijini Dar es Salaam.
  Picha ya Pamoja na wanafunzi waliohitimu

  0 0
 • 01/26/19--20:50: Article 2
 • * Aonya wanasiasa wanaotukana viongozi wa dini

  * Moja ya barabara kupewa jina la Kardinali Pengo,heshima ya kutambua mchango wake kwa taifa.

  Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

  MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amewataka maafisa elimu wa Halmashauri na Wilaya za Mkoa wa Dar es salaam kuhakikisha vipindi vya dini vinafundishwa katika shule zote ili kujenga maadili mema.

  Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa bweni, ukumbi pamoja na gari la shule katika shule ya sekondari ya Mtakatifu Joseph Millenium Goba jijini Dar es salaam, Makonda amesema kuwa shule nyingi zimekuwa zikitumia muda wa vipindi vya dini kufanya mambo mengine na kusisitiza kuwa walimu wakuu wasiofuata utaratibu huo watachukuliwa hatua kali. 

  Aidha Makonda amewaonya wanasiasa wanaotukana viongozi wa dini kuchukua tahadhari, hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayetukana kiongozi wa dini.

  Amesema kuwa viongozi wa dini wamekuwa na mchango mkubwa katika kutetea uzalendo na kuhimiza maadili na amemshukuru kwa namna ya pekee Askofu Mwadhama Cardinali Polycarp Pengo Askofu wa Jimbo kuu la Dar es salaam kwa kuwa mmoja wa viongozi wazalendo kwa taifa na amehaidi moja ya barabara kubwa zinazojengwa jijini Dar es salaam zitapewa jina lake katika kutambua mchango wake na kumuenzi.

  Vilevile amewataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii na kuwa nidhamu na sio kushinda katika mitandao ya kijamii ambayo imekuwa ikipotosha.Kwa upande wake Mwadhama Pengo amemshukuru Makonda kwa mchango wake  na kuahidi kuiombea barabara itakayopewa jina lake pia amemshukuru Mbunge wa Hanang' Dkt. Mary Nagu kwa kuanzisha harambee ambayo imefanikisha kununua basi kwa ajili ya wanafunzi.

  Shule ya Sekondari ya Mtakatifu Joseph Millenium inapatikana Goba jijini Dar es salaam na harambee ya kuchangia ujenzi huo ilianza mwaka 2016 ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda alichangia mifuko ya saruji na magodoro yapatayo 400 ili kuweka hali nzuri ya ujifunzaji shuleni hapo.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda (kushoto) akizindua ukumbi wa mikutano na shughuli za kitaaluma katika shule ya Mtakatifu Joseph Millenium, kulia ni Askofu Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda (kulia) akiteta jambo na Askofu Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo wakati wa hafla ya uzinduzi wa bweni, ukumbi pamoja na gari la wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Mtakatifu Joseph Millenium, jana jijini Dar es salaam.
  Viongozi wa dini na serikali wakiimba wimbo wa taifa katika hafla  ya uzinduzi wa bweni, ukumbi na gari la shule ya Mtakatifu Joseph Millenium ,Goba jiji Dar es salaam.Pichani kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, akifuatiwa na Askofu Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo, na Mkuu wa shule hiyo Sista. Caroline Kokutekana,kushoto ni Mbunge wa jimbo la Hanang' Dkt. Mary Nagu.

  0 0

  Na Ramadhani Ali -Maelezo.
   
   Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mmanga Mjengo Mjawiri amesema ili kupata matokeo mazuri ya wanafunzi katika mitihani ya elimu ya juu na vyuo, juhudi kubwa inahitajika katika kuimarisha elimu ya maandalizi na msingi.

  Amesema Maafisa Elimu na Walimu wakuu wa skuli za msingi wanapaswa kuwa wasimamizi na wafuatiliaji wa karibu wa kazi za kila siku za walimu wao ili malengo yaliyowekwa ya elimu yaweze kufikiwa.

  Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali alieleza hayo alipokuwa akizindua Mradi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Walimu wa masomo ya Sayansi, Kiingereza na Hesabu wa darasa la tano na sita wa skuli za Unguja ili waweze kutoa msaada kwa wanafunzi na kuongeza ufaulu wao.

  Alisema imebainika kuwa pamoja na juhudi zinazochukuliwa za kuwapatia walimu mafunzo ya mara kwa mara suala la ufuatiliaji na ufuatiliaji limekuwa ni tatizo kubwa kwa skuli nyingi za Zanzibar.Aliweka wazi kuwa msimamo wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kuwa kuanzia sasa inataka kuona mafunzo yanayotolewa kwa walimu wa skuli yanaleta mabadiliko na kuongeza ufanisi katika skuli zao

  Aliwataka walimu wakuu kuwa wabunifu katika kuongoza na kushirikiana na Maafisa Elimu na viongozi wa Halmashauri, hasa wakati huu wa wa ugatuzi, kubuni mbinu mpya za kuendeleza mbele skuli zao.Aidha aliwataka walimu wakuu kujitambua na kuthamini nafasi waliyopata huku wakijenga upendo kwa walimu, wanafunzi na kujiepusha kufanya makosa ambayo yanaweza kuwavunjia heshma mbele ya jamii.

  Akizungumza katika uzinduzi wa Mradi huo katika Kempasi ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar Kempasi ya Nkrumah, Mkurugenzi wa Idara ya Mafunzo ya Walimu Maimuna Fadhil Abass alisema kwa vile elimu ya msingi imeingizwa katika ugatuzi, viongozi wa Wilaya wanatakiwa kuipokea na kuifanyia kazi huku Wizara ya elimu ikiendelea na wajibu wa kusimamia sera.

  Akimkaribisha Naibu Waziri kuzindua Mradi huo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Maalim Abdulla Mzee alisema zipo baadhi ya skuli zinawalimu wazuri lakini zimeshindwa kutoa mwanafunzi hata mmoja kwenda michepuo jambo linaloashiria uwajibika mdogo kwa skuli hizo.

  Alisema lengo la Wizara ya Elimu ni kuona kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa michepuo kinaongeza kila mwaka na wameandaa zawadi maalum kwa skuli itakayo ongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wao kwa kila mwaka.
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Maalim Abdulla Mzee akiwaeleza walimu wa Skuli za Sekondari walioshiriki uzinduzi wa Mradi wa Mafunzo ya kutoa msaada kwa wanafunzi wa Skuli za Msingi (TESS) katika Kempasi ya SUZA Nkrumah.
  Baadhi ya Walimu, Maafisa Elimu na Wakurugenzi wa Halmashauri walioshiriki Mafunzo ya kutoa msaada kwa wanafunzi wa Skuli za Msingi (TESS) wakifuatilia uzinduzi wa Mradi huo katika Kempasi ya SUZA Nkrumah.
  Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mmanga Mjengo Mjawiri akizungumza na walimu, Maafisa Elimu na Wakurugenzi wa Halmashauri katika uzinduzi wa Mradi wa Mafunzo ya kutoa msaada kwa wanafunzi wa Skuli za Msingi (TESS) katika Kempasi ya SUZA Nkrumah
  Picha ya pamoja ya Naibu Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Amali Mmanga Mjengo Mjawiri na baadhi ya washiriki wa mafunzo ya kutoa msaada kwa wanafunzi wa Skuli za Msingi (TESS) katika Kempasi ya SUZA Nkrumah.
   

  0 0

   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Waziri wa Madini, Dotto Biteko, wakati akiwasili kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma Januari 26, 2019, kufungua mkutano wa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
    Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Binilith Mahenge, wakati akiwasili kwenye mkutano wa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara, katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma Januari 26, 2019, katikati ni Waziri wa Madini, Dotto Biteko
   Wakuu wa Mikoa wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wakati akiwahutubia kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Januari 26, 2019.
   Wakuu wa Mikoa wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wakati akiwahutubia kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Januari 26, 2019.
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwahutubia Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara, wakati akifungua mkutano kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma Januari 26, 2019. 
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwahutubia Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara, wakati akifungua mkutano kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma Januari 26, 2019. 
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwahutubia Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara, wakati akifungua mkutano kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma Januari 26, 2019. 
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiteta jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI Suleiman Jafo, kabla ya kufunguamkutano wa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara, uliofanyika katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma Januari 26, 2019.
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka, mara baada ya kufunguamkutano wa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara, katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma Januari 26, 2019. Katikati ni Waziri wa Madini, Doto Biteko
   Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Constantine Kanyasu (kulia), akimsikiliza  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, baada ya kufungua mkutano wa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara jijini Dodoma Januari 26, 2019. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima, baada ya kufungua mkutano wa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara, nje ya  ukumbi wa Hazina jijini Dodoma Januari 26, 2019.  *Ataka maagizo ya Rais kuhusu masoko ya madini yatekelezwe haraka


  WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameuagiza uongozi wa Wizara ya Madini uhakikishe kanuni za uendeshaji wa masoko ya madini katika mikoa yote nchini zinakamilika na kuanza kutumika kwa wakati huku lengo likiwa ni kuongeza tija kwenye sekta hiyo.

  Katika kukabiliana na changamoto ya utoroshwaji wa madini nchini, Rais Dkt. John Magufuli aliagiza kuanzishwa kwa masoko ya madini kwenye mikoa yote, hivyo Waziri Mkuu ameitaka Wizara ya Madini na wakuu wote wa mikoa watekeleze maagizo hayo haraka.

  Ameyasema hayo leo (Jumamosi, Januari 26, 2019) wakati akifungua mkutano kuhusu uanzishwaji wa masoko ya madini katika mikoa yote nchini. Mkutano huo umefanyika kwenye ukumbi wa Kambarage, Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dodoma.

  Mkutano huo wa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa umehudhuriwa na Mawaziri, Manaibu Waziri, Makatibu Wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu pamoja na watendaji wa Wizara ya Madini pamoja na watendaji wa Tume ya Madini.

  Waziri Mkuu amesema katika kuanzishwa kwa masoko hayo, rasimu ya kanuni imeandaliwa na hivyo ni vema wakazielewa vizuri kwa sababu wao ndiyo watakaozitekeleza kwenye maeneo yao ili Serikali iweze kufikia lengo ililojiwekea katika kuimarisha sekta ya madini.

  ”Kutokana na umuhimu wa masoko hayo naagiza kanuni hizo zikamilishwe haraka iwezekanavyo ili kuwasaidia watu wetu kupata masoko ya uhakika ya madini na Serikali itanufaika na mrabaha na tozo mbalimbali zitakazokuwa zikitozwa kwa mujibu wa sheria.”

  Kadhalika, Waziri Mkuu ameagiza pindi kanuni hizo zitakapokamilika, Wizara ya Madini ihakikishe zinafikishwa kwa Wakurugenzi wa Majiji, Manispaa na Halmashauri za wilaya, maeneo ya machimbo, wachimbaji na wafanyabiashara wa madini ili kuondoa migogoro.

  Hata hivyo, Waziri Mkuu ameongeza kuwa OR-TAMISEMI kupitia wakuu wa Mikoa na Maafisa Tawala wa Mikoa wakishirikiana na Wizara na Tume ya Madini waandae taratibu zitakazowezesha Wakurugenzi wa halmashauri kutoa maoni katika kuanzisha masoko.

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka wakuu wa mikoa wakasimamie kikamilifu masuala ya ulinzi na usalama kwenye masoko hayo ili kuwahakikishia wafanyabiashara, wachimbaji na wananchi usalama wa kutosha wakati wa kuuza madini hayo.

  Amesema kwa muda mrefu Rais Dkt. Magufuli amekuwa akisisitiza kuhusu sekta ya madini kuchangia ipasavyo katika pato la Taifa na hivyo kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijami kwa wananchi, lakini sekta hiyo imekuwa na matatizo ikiwemo utoroshwaji wa madini na migogoro kwa wachimbaji hususani wachimbaji wadogo.

  ”Jitihada mbalimbali zimekuwa zikichukuliwa kuhakikisha changamoto hizo zinaondolewa kwa lengo la kuongeza tija kwenye sekta ya madini. Napenda mfahamu kuwa mna nafasi muhimu katika kuifanya sekta hii iweze kuleta manufaa yanayotarajiwa kwa Taifa.”

  Kwa upande wake, Waziri wa Madini, Doto Biteko amesema mkutano muhimu kwa sababu linalenga kumaliza changamoto ya masoko ya madini nchini, hivyo amewataka wakuu wa mikoa wahakikisha walipa kipaumbele jambo hilo kwa kuwa linamanufaa kwa Taifa.

  Amesema kwa sasa wachimbaji na wafanyabiashara wa madini hawana maeneo maalum wanayoweza kufanyia biashara ya madini hali ambayo inachangia kuwepo kwa utoroshwaji wa madini, jambo ambalo linasababisha Serikali kukosa mapato.

  Waziri Biteko ameongeza kuwa ili kukabiliana na changamoto ya masoko ya madini, Wizara iliunda kamati iliyojumuisha wajumbe kutoka katika taasisi mbalimbali za Serikali zikiwemo Ofisi ya Rais Ikulu, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wizara ya Madini, Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Viwanda na Biashara, Benki Kuu na Tume ya Madini. 

  Amesema kamati hiyo iliundwa ili kuandaa rasimu ya Kanuni za kuanzisha na kusimamia Masoko ya Madini Nchini. “Katika kuandaa kanuni hizo, jina la kanuni linapondekezwa liwe The Mining ( Mineral and Gem House) Regulations, 2019," amesema Waziri Biteko.

  0 0

  Na Ripota Wetu, Globu ya jamii

  MKUU wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Juma Homera amesema moja ya kipaumbele chake kwa sasa ni kutatua changamoto ya uhaba wa upatikanaji wa maji safi na salama ambapo kupitia mikakati iliyopo wamefanikiwa kuchimba zaidi ya 210.

  Akizungumza leo na Michuzi Blog, Homera amesema mikakati ya Wilaya ya Namtumbo ni kuboresha huduma mbalimbali za kijamii na kwake yeye maji safi na salama ni kipaumbele chake namba mbili ni maji.

  Amefafanua kutokana na malengo ambayo wamejiwekea wamefanikiwa kuchimba visima hivyo 210 ambavyo kwa sehemu kubwa vimechimbwa kwa ufadhili wa wadau mbalimbali wakiwamo Alfridaus na Istiqaama waliochimba visima 106 vifupi.

  Pia amesema Anglican chini ya mradi wa boresha afya ya mama na mtoto wamechimba visima 25,kupitia mapato ya ndani wamechimba visima viwili, Help for Underderserved community wamechimba visima 57 na Mei mwaka huu wa 2019 kunatarajiwa kuchimbwa visima virefu 60 katika Jimbo la Tunduru Kaskazini 60 na visima zaidi ya 40 vitachimbwa Jimbo la Tunduru Kusini.

  Ameongeza kuwa kisima kimoja kimechimbwa chini ya ufadhili wa Kanisa Katoliki Parokia ya Namiungo na wanaendelea na uchimbaji kwa kata nzima, pia visima 20 kati ya 25 vimejengwa upya kwa fedha za Serikali chini ya program ya lipa kwa matokeo.

  "Tumeamua kutatua changamoto ya uhaba wa maji ndani ya wilaya yetu, kupitia mipango sahihi ya Serikali ya kutatua changamoto za wananchi pamoja na kushirikiana na wadau wa maendeleo, leo hii tunajivunia kwani tumeanza vizuri kwenye hili la upatikanaji wa maji safi na salama kwa kuchimba visima na kazi hiyo inaendelea,"amesema Homera.
   Mkuu wa Wilaya ya Tunduru,Mh.Juma Homera akiwa sambamba na wananchi wake wakishuhudia kukamilia kwa Kisima cha maji kijiji cha pacha nne kata ya Namiungo  kilichochimbwa kwa ufadhili wa Roman catholic Parokia ya Namiungo.Mh Homera amesema moja ya kipaumbele chake kwa sasa ni kutatua changamoto ya uhaba wa upatikanaji wa maji safi na salama ambapo kupitia mikakati iliyopo wamefanikiwa kuchimba zaidi ya 210.
    DC Homera akimtwisha Ndoo ya maji  na kumtua Mwenyekiti wa kijiji hicho cha pachanne.
   DC Homera akikabidhi kisima kwa wananchi ,ambapo amesema moja ya kipaumbele chake kwa sasa ni kutatua changamoto ya uhaba wa upatikanaji wa maji safi na salama ambapo kupitia mikakati iliyopo wamefanikiwa kuchimba zaidi ya 210.

  DC Homera akiwashukuru wataalamu wakiwa sambamba na mitambo inayotumika kuchimbia visima vya maji, ambayo ni ya shirika lisilo la kiserikali la Marekani 'Help for Underderserved community (HUC) ',ambao mpaka sasa wamechimba visima zaidi ya 57 awamu ya kwanza,bado awamu ya pili Mei mwaka huu 2019 wanatarajia kukamilisha  kuchimba visima 100.
  Baadhi ya Wananchi wakichota maji kwa miongoni mwa visima vilivyochimbwa na Alfirdaus na Istiqama kijiji cha mchekeni kata ya marumba wilayani Tunduru

  0 0


  Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amemtaka mkuu wa wilaya ya Karatu kuwatafuta wataalam wa serikali, pamoja na wakandarasi waliopata zabuni za kutekeleza miradi ya maji wilayani Karatu kufika wilayani hapo bila kukosa ndani baada ya siku 14. Wito huo ni kuanzia Tarehe 28 Januari, 2019 ili kufanyika kikao na wahusika kueleza jinsi walivyosimamia na kutekeleza miradi ya maji wilayani Karatu.

  Naibu Waziri Aweso amesema katika kikao hicho asitumwe mwakilishi, bali wahusika wenyewe, na atashiriki kikao hicho ili kubaini changamoto zote za miradi ya maji wilayani Karatu na kutafuta jibu ili maji safi na salama yawafikie wananchi na wadau wengine kwa wakati kama serikali ilivyopanga.

  Waziri Aweso katika ziara ya ukaguzi amesema imebainika baadhi ya miradi ya maji imekabidhiwa ikiwa na mapungufu na makosa mbalimbali hali ambayo haikubaliki, pia kutowatendea haki wananchi wanaohitaji maji kwa shughuli mbalimbali za maendeleo.

  Awali, Mkuu wa wilaya ya Karatu Mhe. Theresia Mahongo amesema kuwa miongoni mwa changamoto za miradi ya maji wilayani hapo ni mapungufu ya kiusanifu. Amesema hali hiyo imetokana na miradi ilipoanza kutekelezwa mwaka 2012/2013 haikufanyiwa mapitio ya usanifu upya baada ya mtaalam mshauri kampuni ya Tanplanet Njegimi Express kuachishwa kazi kwa kutokidhi viwango.

  Halmashauri ya wilaya ya Karatu ilipangiwa kutekeleza miradi ya maji katika vijiji 10 na katika halmashauri hiyo miradi ilipangwa kuhudumia vijiji 13 kwa kutekelezwa katika vijiji vya Getamock/Mahhahha, Khusumay, Kansay, Buger, Endonyawet, Matala, Endamaghang/Mikocheni, Laja/Umbangw, Mang’ola Juu na Makhoromba.

  Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiangali mtambo wa kunyonya maji chini ya ardhi umbali wa kina cha mita 180 eneo la Bwawani Karatu. Maji yanayopatikana hapo yanasambazwa kwa wakazi wa mji wa Karatu
  Naibu Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso (Mb) akiangalia mfumo wa mabomba katika tenki katika mradi wa maji wa kwa Tom, Karatu mjini. Utekelezaji wa mradi huo umefika asilimia 33 na utakapokamilika utahudumia zaidi ya wakazi elfu 10 na kuongeza upatikanaji maji wilayani Karatu kutoka asilimia 33 hadi asilimia 53. Mwenye miwani ni Mkuu wa wilaya ya Karatu Mhe. Theresia Mahongo.
  Naibu Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso (Mb) akitoa maelezo katika moja ya mradi wa maji, wilayani Babati eneo la Eyalabe. 
  . Naibu Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso (Mb) pamoja na viongozi wa wafugaji baada ya ukaguzi wa miradi ya maji na kuwahakikishia maji safi na salama yatapatikana, yakutosheleza majumbani na mifugo yao, eneo la Makuyuni, Monduli.


  0 0

  Abdullatif Yunus - Kagera

  Shirika la World Vision Tanzania limekabidhi majengo yaliyojengwa na mradi wa World Vision(Izigo AP) kwa kushirikiana na wananchi wa kijiji Kabuleme, Kata Izigo, Wilaya ya Muleba.

  Akizungumza katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika shule ya Msingi Kabuleme, Meneja Kanda ya Kagera Bi. Juliana Charles ameeleza kuwa mnamo mwaka 2017 mradi wa maendeleo Izigo ulipokea barua kutoka shule ya msingi Kabuleme iliyoainisha matatizo makubwa yanayoikumba shule hiyo, likiwemo tatizo kubwa la uhaba wa madarasa, choo cha wanafunzi na walimu pamoja na madawati. 

  Baada ya mradi kupokea taarifa hiyo walifika shuleni hapo na kuona hali halisi ya mazingira ya shule na ufundishaji kwa ujumla. Ndipo walipoandikia andiko na kupitia wafadhiliwa wa nchi ya Ujerumani, andiko liliweza kupata Tzs. 76,000,000.00 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa, matundu 5 ya vyoo vya wanafunzi, tanki la maji ya kunawa mikono lenye ujazo wa lita elfu tano, madawati 60 na mipira 6 ya michezo.

  Akipokea majengo hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba, Ndg. Emmanuel Sherembi ameendelea kushukuru sana shirika la World Vision Tanzania kwa kuendelea kufadhili miradi mbalimbali iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa wilayani Muleba ikiwemo ujenzi na ukarabati wa zahanati ya Bushekya, ujenzi wa zahanati Bugasha, ujenzi wa miundombinu shule ya msingi Kabuleme na ujenzi wa jengo la mama na mtoto kituo cha afya Izigo.

  "Msichoke kutufadhili katika sekta za Elimu na Afya kwani Wilaya ya Muleba ina uhaba mkubwa sana wa miundombinu ya Elimu na Afya hali inayopelekea jamii kukosa huduma hizo za muhimu. Serikali imekuwa ikijitahidi kuboresha miundombinu hiyo lakini bado uhitaji ni mkubwa", ameeleza Ndg. Emmanuel Sherembi.

  Majengo yaliyokabidhiwa ni pamoja na vyumba vitatu vya madarasa vyenye thamani ya Tzs. 60,132,210.00 ambapo Shirika la World Vision limechangia Tzs. 54,512,210.00 na jamii imechangia Tzs. 5,620,000.00, ujenzi wa matundu matano ya vyoo na ununuzi wa tanki la maji wenye thamani ya Tzs. 14,693,360.00, ununuzi wa madawati 60 kwa jumla ya Tzs. 5,160,000.00 na ununuzi wa mipira 6 ya michezo yenye thamani ya Tzs. 435,000.00. Jumla ya gharama za ujenzi na vifaa ni Tzs.80,420,560.00.

  Meneja wa Shirika la World Vision Kanda ya Kagera, Bi Juliana Charles akisoma Taarifa ya Mradi kabla ya Kuukabidhi rasmi.
  Pichani ni Meneja Bi Juliana Charles na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muleba Ndg. Emmanuel Sherembi kwa pamoja wakishirikiana kukata utepe wa jengo la madarasa matatu kama ishara ya Uzinduzi.
  Sehemu ya Madawati yaliyokabidhiwa World Vision Kagera kwa Shule ya Msingi Kabuleme iliyopo Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera.
  Picha ya Tanki la Maji lililokabidhiwa.
  Jengo la Vyoo vya Matundu matano vilivyokajengwa na World Vision Kanda ya Kagera kwa kushirikiana na Wananchi.
  Jengo la Vyumba vitatu vya madarasa vilivyotokana na Mradi wa World Vision - Kagera kwa kushirikiana na Wananchi wa Izigo Muleba.
  Picha ya Pamoja, Viongozi wa Halmashauri ya Muleba, World Vision, Kamati ya Shule, walimu na wanafunzi baada ya kukabidhiwa Mradi.
  Pichani Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muleba Ndg. Emmanuel Sherembi akizungumza na Wananchi na wanafunzi (hawapo pichani), baada ya kuzindua majengo hayo yaliyojengwa kwa Hisani ya shirika la World Vision.

  0 0

  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, ,Maliasili na Utalii, Nape Nnauye akiwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo akiwaonesha kundi la tembo mara baada ya kamati hiyo kufanya utalii nyakati za jioni mwishoni mwa wiki wakati Kamati hiyo ilipomaliza kufanya kikao cha kujadili mradi wa kukuza na kuendeleza utalii Kusini katika Hifadhi ya taifa ya Ruaha koani Iringa. (Picha na Lusungu Helela-MNRT)
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Constantine Kanyasu (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja kwenye jabali ambalo watalii hupanda katika jiwe hilo kwa ajili ya kuona makundi ya wanyama aina ya kiboko wakiwa wanakunywa maji katika mto wa Ruaha Mkuu katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha mkoani Iringa mwisho ni wa wiki wakati kamati hiyo ilipofanya utalii wakati Kamati hiyo ilipomaliza kikao cha kujadili mradi wa kukuza na kuendeleza utalii Kusini . (Picha na Lusungu Helela-MNRT)
  Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Maliasili na Utalii, Neema Mgaya akiwa ameongoza na Mwenyekiti wa Kamati nhiyo, Nape Nnajuye pamoja na wajumbe wengine wakitelemka katika eneo la kuonea wanyama aina ya viboko nyakati za jioni wanapokunywa maji mto wa Ruaha Mkuu katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha mkoani Iringa mwisho ni wa wiki wakati kamati hiyo ilipofanya utalii wakati Kamati hiyo ilipomaliza kikao cha kujadili mradi wa kukuza na kuendeleza utalii Kusini . (Picha na Lusungu Helela-MNRT)
  Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Maliasili na Utalii, Mwita Getere akiwa ameongozana na wajumbe wengine wakipanda ngazi juu ya sehemu ya kuonea wanyama aina ya viboko nyakati za jioni wanapokunywa maji mto wa Ruaha Mkuu katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha mkoani Iringa mwisho ni wa wiki wakati kamati hiyo ilipofanya utalii wakati Kamati hiyo ilipomaliza kikao cha kujadili mradi wa kukuza na kuendeleza utalii Kusini . (Picha na Lusungu Helela-MNRT)  NA LUSUNGU HELELA-IRINGA

  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu amewataka Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa chachu ya kuhamasisha utalii wa ndani kwa wananchi wanawaongoza kwa kutenga muda wa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini.

  Imeelezwa kuwa hamasa ya wananchi ya kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini imekuwa na mwitikio mdogo ukilinganisha na idadi ya watalii wa kutoka nje.

  Kauli hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu akiwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara ya siku mbili ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa mradi wa kukuza na kuendeleza utalii Kusini katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha mkoani Iringa.

  Amesema endapo kila Mbunge kwa nafasi yake ataweza kuhamasisha wananchi kutembelea vivutio vya utalii mapato yataweza kuongeza maradufu kupitia Utalii wa ndani tofauti na ilivyo sasa."Tengeni muda wa kupumzika baada ya pilikapilika ya kuwahudumia wapiga kura wenu, unakuja huku Ruaha unapumzisha akili huku ukijipanga mwaka 2020 kwa ajili ya uchaguzi Mkuu" alisema.

  " Tusisubiri tuje kikazi kama tulivyokuja hivi, Panga njoo na familia yako ufurahie maisha mara moja moja sio mbaya" Alisisitiza Kanyasu.Pia, Kanyasu aliwaomba Wabunge hao kila wanapopata nafasi ya kukutana na wananchi majimboni mwao wawahamasishe kutembelea vivutio vya utalii ili kumuunga mkono Rais John Magufuli kwa jitihada anazofanya za kutaka kuongeza mapato yatokanayo na sekta ya utalii.

  Amesema ufufuaji wa kampuni la usafiri wa ndege nchini (ATCL) kwa kununua ndege saba achilia mbali mradi wa reli ya Standard Garge ni juhudi wazi za Rais John Magufuli kuona sekta ya utalii inagusa maisha ya kila wananchi kimapato.Katika hatua nyingine, Kanyasu aliwaomba Wabunge hao wawahamasishe wananchi kuchangamkia fursa za utalii kwa kujenga Hoteli au kwa kuanzishavituo vya utalii wa kiutamaduni ambao umekuwa ukipendwa sana na watalii wengi wa kutoka nje.

  Aidha, Mhe.Kanyasu aliwaeleza Wabunge hao kuwa baada ya kufungua utalii Kusini, Serikali inakusudia kufungua utalii katika kanda nyingine ikiwemo ya kanda ya ziwa na kanda ya Kaskazini Magharibi, Hivyo wawaandae wananchi wao kuchangamkia fursa za utalii badala ya kubaki walalamikaji.

  Kwa upande wake, Mbunge wa Mtama ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Nape Nnauye alisema kufunguliwa mapema kwa utalii Kusini kutatoa picha halisi kwa wananchi katika kunufaika kiuchumi kupitia sekta hiyo katika kanda nyingine

  Pia, Mhe, Nape aliishauri Serikali kulifanyia kazi suala la tozo ya kuingia ndani ya hifadhi (single entry) kutokana na malalamiko ya muda mrefu wanayoyatoa wananchi kwanaoishi Katibu na Hifadhi kuwa imekuwa ikiwabana watalii kutoka nje ya Hifadhi kuwatembelea wananchi hao.

  0 0

  MKUU wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti ameagiza wachimbaji wadogo wa madini ya Tanzanite (WanaApolo) wapite bila kulipa kwenye lango la kuingia ndani ya ukuta unaozunguka migodi ya madini hayo hadi hapo utaratibu wa kulipia sh70,000 ili wapatiwe vitambulisho vya kupita utakapofanyika. 

  Uamuzi huo umepokelewa kwa mikono miwili na wananchi wa mji mdogo wa Mirerani kwani awali waliokuwa wanaruhusiwa ni wale wenye mkataba wa kulipwa mshahara pekee. 

  Mnyeti akizungumza na wadau wa madini alisema wanaApolo watapita bila kulipa chochote kwenye lango hilo hadi hapo vitambulisho maalum vitakapoandaliwa ambavyo watalipia kila mmoja sh70,000 kwa mwaka mmoja. Alisema wamekubaliana kwenye kikao cha wamiliki wa migodi na wanaApolo kuwa suala la malipo ya mishahara au asilimia 10 pindi madini yakitoka wataamua wao wenyewe. 

  "Baada ya serikali kukubaliana na pendekezo lenu la kuachana na suala la mishahara ambalo lipo kisheria inabidi ikusanye kodi ya mshahara na tozo ya uendelezaji ufundi stadi," alisema Mnyeti. Mbunge wa jimbo la Simanjiro James Ole Millya alisema wanamshukuru Mnyeti kwa uamuzi huo kwani utawanufaisha watu wengi. 

  Aliwataka wamiliki wa migodi na wachimbaji wote kutimiza wajibu wao huku wakitilia mkazo suala la ulipaji wa kodi kwa ajili ya maendeleo.Mwenyekiti wa chama cha wachimbaji madini mkoa wa Manyara, (Marema) Justin Nyari alisema Mnyeti ameweka historia kwa tamko hilo kwani baadhi ya wachimbaji waliondoka ila sasa watarudi. 

  Nyari alisema wao kama viongozi wa wachimbaji watakutana na makundi yote yanayojihusisha na madini hayo ili kuweka utaratibu mzuri wa kufanya shughuli hiyo na wanaApolo kutohama hama. Katibu wa Marema tawi la Mirerani, Omary Mandari alisema wanampongeza Rais John Magufuli kwa kujenga ukuta huo na mkuu wa mkoa kwa uamuzi wake wa kuruhusu watu kupita. 

  Mandari alisema utaratibu huo wa kuingia bila malipo wakati huu ikisubiriwa vitambulisho maalum ni mzuri tofauti na hapo awali ambapo wanaApolo ilitakiwa waingie kwa kutumia mikataba ya mishahara. Makamu Mwenyekiti wa usalama, afya na mazingira wa shirikisho la wachimbaji madini nchini (Femata) Dk Bernard Joseph alisema wamejipanga kuhakikisha utunzaji mazingira na afya za wafanyakazi. 

  Dk Joseph alisema wameweka utaratibu wa wafanyakazi wanaofanya shughuli migodini ikiwemo kuumia, uokoaji na kufukiwa tukishirikiana na wachimbaji wazoefu na Wizara ya Madini. 
  Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti akipokelewa na askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na polisi kwenye geti la Magufuli la kuingia ndani ya ukuta unaozunguka migodi ya madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro. 
   Mwenyekiti wa chama cha wachimbaji madini Mkoa wa Manyara (Marema) Justin Nyari akizungumza kwenye kikao cha wadau wa madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro. 
   Mkuu wa kituo cha polisi Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, ASP Evarest Makala akielezea mikakati ya ulinzi na usalama. 
  Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Pastory Mnyeti akizungumza kwenye kikao cha wadau wa madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro.

  0 0


   Katibu wa Makamu wa Rais Bw. Juma S. Mkomi akipokea Vifaa Tiba vya kujifungulia wakina mama kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kutoka kwa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Mashariki Bi. Aikansia Muro ikiwa sehemu ya Benki hiyo kuunga mkono juhudi za Makamu wa Rais katika kuboresha huduma ya afya ya Mama na Mtoto leo katika hospitali ya rufaa ya Morogoro ambapo Makamu wa Rais alitoa zawadi kwa watoto 36 waliozaliwa tarehe 27, Januari kama kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa.
    Katibu wa Makamu wa Rais Bw. Juma S. Mkomi akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Rufaa ya Morogoro Dkt. Lucy Nkya moja ya mabeseni yenye mahitaji muhimu kwa watoto waliozaliwa leo ikiwa zawadi kutoka kwa  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa watoto 36 waliozaliwa leo tarehe 27, Januari kama kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa.
   Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Rufaa ya Morogoro Dkt. Lucy Nkya akionyesha juu moja ya mabeseni yenye mahitaji muhimu kwa watoto waliozaliwa leo kama ishara ya kumshukuru Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuwakumbuka  watoto 36 waliozaliwa leo tarehe 27, Januari ikiwa ni kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa.


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo Januari 27 kwa kushirikiana na Benki ya NMB, wametoa Vifaa Tiba vya kujifungulia katika wodi ya Mama na Mtoto, pamoja na vifaa tiba hivyo aliwazawadia  watoto 36 waliozaliwa siku ya  katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro .

  Makamu wa Rais aliwakilishwa na Katibu wake Bw. Juma S. Mkomi ambaye amesema kuwa Makamu wa Rais amekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha huduma ya afya ya mama na mtoto inaboreshwa.

  “Suala la kuboresha huduma ya mama na mtoto limeelezewa kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020 lakini Makamu wa Rais kwa upekee amelipa kipaumbele kwa sabau ni moja kati ya ahadi zake kuu wakati kampeni” alisema Katibu huyo wa Makamu wa Rais.

  Akizungumza wakati wa hafla hiyo Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Dkt. Rita Lyamuya amemshukuru Makamu wa Rais kwa kuwakumbuka watoto waliozaliwa hospitalini hapo ambapo alisema kuwa watoto 36 wamezaliwa katika siku ya leo na kwa kipindi cha robo mwaka watoto  1779 walizaliwa  kati ya hao waliozaliwa kwa upasuaji ni 586.

  Aidha, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Mashariki Aikansia Muro amesema Benki ya NMB inaunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya tano katika kuboresha huduma zote za kijamii hususani sula zima la  afya na elimu na wataendelea kushirikiana na Serikali katika kuboresha huduma za kijamii ambapo leo wamemuunga mkono Mhe. Makamu wa Rais kwa kutoa Vitanda vinne vya kujifungulia, Vifaa vya kumsaidia mama kujifungulia (delivery kit) 8, pamoja na vifaa vingine ambavyo kwa ujumla vinagharimu shilingi milioni 5.

  Kwa Upande mwingine Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro Bw. Clifford Tandari ameishukuru Serikali kwa kutenga shilingi bilioni 8.5 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali 3 na vituo vya afya 11 katika mkoa wa Morogoro.

older | 1 | .... | 1787 | 1788 | (Page 1789) | 1790 | 1791 | .... | 1897 | newer