Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1786 | 1787 | (Page 1788) | 1789 | 1790 | .... | 1896 | newer

  0 0


  Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo Pesa Hussein Sayed akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya inayojulikana kama #AppanaChezea Tigo Pesa App.
  Afisa Biashara Mkuu wa Kampuni ya Tigo Tarik Boudiaf, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya inayojulikana kama #AppanaChezea Tigo Pesa App.
  Meneja bidhaa, Tigo Pesa App Ian Ludovick akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya inayojulikana kama #AppanaChezea Tigo Pesa App.


  Pakua au huisha App yako ya Tigo Pesa bure

  Wateja wanaotumia #AppanaChezea Tigo Pesa App kufurahia faida nyingi ikiwamo kurudishiwa ada ya malipo, Mbs na muda wa maongezi

  Kampuni ya simu inayoongoza katika maisha ya kidigitali Tanzania, Tigo, imeanza mwaka 2019 kwa kutangaza uzinduzi wa App ya Tigo pesa katika kampeni inayojulikana kama #AppanaChezeaTigo PesaApp campaign.

  Kampeni ya #Appana ChezeaTigo Pesa App inaenda sambamba na filosofia ilinayojikita kwenye uvumbuzi na kumjali mteja kwa kutoa suluhisho za kidijitali zinazoendana na matakwa ya wateja tofauti tofauti hapa nchini.

  Kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu, Kampuni ya Tigo imewekeza kwa kiasi kikubwa kwenye mfumo wa malipo ya kidijitali ukilenga kuwapatia wateja huduma za kifedha zinazoendana na dunia ya kisasa. #AppanaChezea Tigo Pesa App campaign ni hatua mpya ya kuboresha uzoefu wa wateja wanaotumia na watakaotumia huduma ya Tigo Pesa. Pamoja na uzoefu huo mpya na wa kipekee, wateja watakaotumia Tigo Pesa App katika kipindi chote cha promosheni watafurahia faida lukuki kama kurudishiwa ada ya kufanya malipo, Mbs pamoja na muda wa maongezi.

  Akiongea wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo Hussein Sayed alisema mteja yeyote wa Tigo anayemiliki simu janja ana kila sababu ya kutumia Tigo Pesa App yenye kukidhi vigezo vya kimataifa vya App na hivyo kumhakikishia mteja urahisi na usalama wa hali ya juu anapofanya miamala yake. Tigo Pesa App pia haitumii data.

  “Leo tunayofuraha kuwaletea watumiaji wa simu janja habari njema. Mteja anapopakua au kuhuisha App yake ya Tigo Pesa, atapata dakika za muda wa maongezi na Mbs bure. Pamoja na ofa hii, mteja wa Tigo atakapotuma pesa kwa mteja mwingine wa Tigo atarudishiwa gharama alizotumia kutuma pesa,” alisema Hussein

  Kwa mujibu wa Hussein, Tigo Pesa App imetengenezwa kwa kuzingatia usalama wa hali ya juu kwa mteja anapokuwa anafanya miamala yake. Kupitia App hiyo, mteja wa Tigo pia ataweza kufanya malipo kwa zaidi ya taasisi 300 za Serikali ikiwamo Wizara, Mashirika, Mamlaka mbali mbali na watoa huduma za Serikali

  Afisa Biashara Mkuu wa Tigo Tarik Boudiaf alisema “Moja kati ya vipau mbele vya Tigo ni kurahisisha maisha ya wateja wake. Kuangalia salio kupitia Tigo Pesa App pia ni rahisi na ni bure. Kununua kifurushi au muda wa maongezi kumerahisishwa zaidi kwa kuwa unachohitajika kufanya ni kufuata hatua tatu rahisi na utakuwa umekamilisha zoezi hilo. Hii ndiyo sababu watu 9 kati ya 10 wanaotumia Tigo Pesa wameridhika na huduma hii na wanawashauri wasiotumia kuitumia,”

  Ikiwa rahisi,haraka na yenye ufanisi kwenye matumizi # AppanaChezea Tigo Pesa App campaign inawaletea wateja App bora na rahisi kutumia kuliko App nyingine zinazofanana nayo zilizopo sokoni. Tigo inamshauri kila mteja kuwa sehemu ya safari ya maisha ya kidijitali kwa kutumia huduma za kidijitali za kifedha zinazotolewa na Tigo. Uvumbuzi huu unaendelea kuwawezesha wateja na wafanyabiashara wa Kitanzania kupata huduma za kifedha pamoja kwa njia ya kidijitali na kuyafanya maisha yao yawe rahisi.

  0 0

   Kazi ya Kuhamisha kipande cha reli chenye urefu wa Kilometa 1.3 ikiendelea eneo la Kidete - Godegode umbali wa KM 337 - 338 ili kudhibiti mafuriko ya mto Mkondoa  yanayoathiri miundombinu ya reli na kupelekea kusitishwa kwa Huduma za Usafiri wa reli mara kadhaa wakati wa mvua kubwa. Kazi inajumuisha ujenzi wa tuta jipya la reli, ujenzi wa Makalavati pamoja na uwekaji wa reli katika tuta jipya hivi karibuni Januari 2019.

   Muendesha mtambo akiendelea na kazi ya kuweka kifusi na kupanga mawe kwenye kingo ya mto Mkondoa kwa ajili ya kudhibiti mafuriko ya mto Mkondoa  yanayoathiri miundombinu ya reli na kupelekea kusitishwa kwa Huduma za Usafiri wa reli mara kadhaa wakati wa mvua kubwa.
   Sehemu ya Mto Mkondoa ikiwa imewekewa kingo za mawe kwa ajili ya kudhibiti mafuriko ya mto Mkondoa  yanayoathiri miundombinu ya reli na kupelekea kusitishwa kwa Huduma za Usafiri wa reli mara kadhaa wakati wa mvua kubwa.
  Kazi ya Kuhamisha kipande cha reli chenye urefu wa Kilometa 1.3  ikiendelea eneo la Kidete - Godegode umbali wa KM 337 - 338 ilikudhibiti mafuriko ya mto Mkondoa  yanayoathiri miundombinu ya reli na kupelekea kusitishwa kwa Huduma za Usafiri wa reli mara kadhaa wakati wa mvua kubwa. Kazi inajumuisha ujenzi wa tuta jipya la reli, ujenzi wa Makalavati pamoja na uwekaji wa reli katika tuta jipya hivi karibuni Januari 2019.

  0 0

  Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii. 

  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Imemuachia huru Mkurugenzi wa zamani wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC). Tido Mhando, aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya matumizi mabaya ya madaraka inayomkabili baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yake.

  Hukumu hiyo imesomwa leo Januari 25.2019 na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi watatu wa upande wa mashtaka waliofika mahakamani hapo kutoa ushahidi wao dhidi ya mshtakiwa Tido. 

  Katika kesi hiyo Tido ameshtakiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka wakati akiongoza shirika hilo ambapo anakabiliwa na mashtaka manne ya matumizi mabaya ya madaraka na moja la kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh. Milioni 800

  Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Shaidi amesema, upande wa mashtaka kupitia mashahidi wake watano wameshindwa kuthibitisha mashtaka dhidi ya mshtakiwa kuwa kweli alitenda makosa hayo. 

  Akiuchambua ushahidi huo, Hakimu Shaidi amesema miongoni mwa mambo mengi yaliyozungumzwa yalikuwa ni suala la mikataba.Amesema katika ushahidi wao, wa mkataba ulionyesha kulikuwa na sahihi ya Tido na Channel 2 lakini hakuna sahihi ya Mwanasheria Mkuu, Bodi wala mamlaka nyingine.

  Ameongeza, Mshtakiwa Tido akiwa kama Mkurugenzi alikuwa ana wajibu wa kufata taratibu za zabuni na hivyo ili kitu kiwe mkataba lazima kipitie hatua lakini mkataba huo anaodaiwa kusaini Tido na Channel 2 hakuwa na sifa ya kuwa mikataba.

  Akiendelea kuuchambua ushahidi huo Hakimu Shaidi amesema, ushahidi uliotolewa mahakamani hapo hauelezi mahali ambapo malipo yamefanyikia, sababu malipo yamefanyika kwa mikataba ambayo haina vigezo.Upande wa mashitaka unadai mkataba huo haukufuata utaratibu wa kisheria.

  " Kweli mkataba kuitwa mkataba ili ukamilike lazima kuwepo na watu ambao wanahusika na lazima kuwepo na mwanasheria hivyo mkataba huo sio halali bali ni makubaliano ya awali, " alisema.Baada ya uchambuzi huo, Hakimu Huruma alisema mshitakiwa huyo hakuna sehemu ilithibitisha kwamba ulikuwa ni mkataba hivyo anamwachia huru.

  Miongoni mwa mashahidi wa upande wa mashtaka waliotoa ushahidi katika kesi hiyo ni ofisa uchunguzi wa Takukuru, Victor Lesuya, mwanasheria wa TBC, Gwakisa Mlawa na mkurugenzi Mkuu mstaafu wa TBC, Clement Mshana.

  Katika kesi hiyo, inadaiwa Juni 16 mwaka Jana, huko Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), kwa makusudi alitumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mkataba wa kuendesha na utangazaji wa vipindi vya televisheni kati ya TBC na Channel 2 Group Corporation (BV1) bila ya kupitisha zabuni, kitu ambacho ni kinyume cha Sheria ya Manunuzi na kuinufaisha BVl.

  Katika shtaka la pili, Tido anadaiwa kusaini makubaliano ya utangazaji wa digitali duniani kati ya TBC na BVl.

  Katika shtaka la tatu, anadaiwa Agosti 11 na Septemba mwaka Jana, akiwa Dubai, Tido alitumia vibaya madaraka yake kwa kusaini mkataba wa makubaliano ya ununuzi, usambazaji na kufunga vifaa vya usambazaji na mnara wa utangazaji kati ya TBC na BVI na kuifaidisha BVI.

  Pia Tido anadaiwa, kutumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mkataba wa makubaliano kwa kuendesha miundombinu ya utangazaji (DTT Broadcast Infrastructure) kati ya TBC na BVI na kuinufaisha BVI.

  Katika shtaka la mwisho Tido anadaiwa kuwa kati ya Juni 16 na Novemba 16 mwaka huu akiwa UAE, aliisababishia TBC hasara ya Sh 887,122,219.19.

  0 0

  Na Mwandishi wetu-Hispania

  Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt. Hamisi Kigwangalla amewaita Wawekezaji kuja nchini Tanzania kwa ajili ya kuwekeza katika sekta ya Utalii wakati aliposhiriki kongamano la 10 la Uwekezaji na Biashara katika sekta ya Utalii Afrika.

  Kongamano hilo limefanyika jana katika jiji la Madrid nchini Hispania
  likiwa limeandaliwa na Shirika la Utalii la Umoja wa Mataifa (UNWTO)kwa
  kushirikiana na Taasisi za Casa Afrika pamoja na Taasisi yamaonesho ya
  Biashara ya Madrid (IFEMA) na kushirikisha nchi mbali mbali duniani.

  Katika Kongamano hilo, Waziri Kigwangalla alipata fursa ya kuwa mmoja wa wazungumzaji ambapo amewahakikishia Wawekezaji wenye nia ya kuja kuwekeza nchini Tanzania kwamba ni sehemu salama ukizingatia hali ya amani na utulivu iliyopo nchini lakini pia kuna vivutio vingi vya utalii na fursa za kuwekeza.

  "Nawakaribisheni nyote, Njooni Tanzania muwekeze kufuatia uwepo wa
  mazingira na miundombinu bora kwa ajili uwekezaji katika sekta ya utalii
  pamoja na viwanda" Alisema

  Waziri Kigwangalla pia alitumia nafasi hiyo kwa kuutangaza ukanda mpya wa kusini mwa Tanzania ambao umejaliwa kuwa na vivutio vya Utalii vya kipekee vinavyopatikana katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, Mikumi pamoja Pori la Akiba Selous.

  Katika hatua nyingine , Waziri Kigwangalla wakati akizungumza katika
  kongamano hilo aliwaeleza washiriki hao kuhusu juhudi mbalimbali
  zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Tanzania,John Pombe Magufuli kwa kutaja mifano michache kama vile kufufua kampuni yandege (ATCL) kwa kununua ndege mpya sita pamoja kujenga chanzo kikubwa cha kuzalisha umeme katika mto Rufiji.

  Alisema serikali ya Tanzania pia inaendelea na mradi wa kisasa wa ujenzi wa njia mpya ya kisasa ya reli (Standard Gauge) pamoja na kuboresha
  miundombinu ya barabara ili kurahisisha usafirishaji wa abiria na mizigo.

  Alibainisha kuwa kutokana na juhudi hizo zilizochukuliwa na Serikali hiyo,
  sekta ya utalii itaweza kusonga mbele ikiwa pamoja na kurahisisha usafiri
  kwa watalii pamoja na wawekezaji kwa ujumla.
  Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt. Hamisi Kigwangalla (wa tatu kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Washiriki wa kongamano la 10 la Uwekezaji navBiashara katika sekta ya Utalii Afrika (Investour) lililofanyika Janakatika jiji la Madrid nchini Hispania ambapo katika Kongamano hilo WazirivKigwangalla alitumia fursa hiyo kuwaita Wawekezaji kuja nchini kwa ajili yavkuwekeza katika sekta ya Utalii na viwanda.
   Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt. Hamisi Kigwangalla (mbele ) akiwa ni miongoni mwa washiriki akifuatilia kongamano la 10 la Uwekezaji na Biashara katika sekta ya Utalii Afrika (Investour)  lililofanyika Jana  katika jiji la Madrid nchini Hispania ambapo katika Kongamano hilo Waziri Kigwangalla alitumia fursa hiyo kuwaita Wawekezaji kuja nchini kwa ajili ya kuwekeza katika sekta ya Utalii na viwanda.
  Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt. Hamisi Kigwangalla (wa pili kulia) akiwa ni miongoni mwa Wazungumzaji  kwenye kongamano la 10 la Uwekezaji na Biashara katika sekta ya Utalii Afrika (Investour) lililofanyika jana katika jiji la Madrid nchini Hispania ambapo katika Kongamano hilo Waziri Kigwangalla alitumia fursa hiyo  kuwaita Wawekezaji kuja nchini kwa ajili ya kuwekeza katika sekta ya Utalii na viwanda.

  0 0

  PMO 9013 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Viongozi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Taifa, ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Januari 25, 2019. Kutoka kushoto ni Makamu wa Rais , Deus Seif, Mweka Hazina , Abubakar Allawi, Katibu Mkuu, Christopher Banda na Wapili kulia ni Rais wa CWT , Leah Ulaya.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Congo imeandika historia mpya kwa kukabidhiana madaraka kwa upendo na ana imani Viongozi wataendelea kufanya kazi kwa pamoja kwa ajili ya maendeleo na maslahi mapana ya nchi yao.

  Makamu wa Rais ambaye alimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameyasema hayo mara baada ya sherehe za kumuapisha Rais mpya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mhe. Felix Tshisekedi.

  “Linalofurahisha ni kwamba ni mara ya kwanza kwa nchi hii ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kufanya uchaguzi wa kidemokrasia na kukabidhiana madaraka kwa usalama kabisa” alisema Makamu wa Rais.

   Uchaguzi huo uliofanyika Desemba 30, 2018, Mhe. Felix Tshisekedi alipata takribani kura milioni 7 sawa na asilimia 38.57 ya kura zilizopigwa ambapo wagombea wenzake kama Martin Fayulu alipata ailimia 34 sawa na kura milioni 6.4, Bw. Emmanuel Ramazani Shadary alipata asilimia 23 sawa na takribani kura milioni 4.4.

  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeandika historia kwa mara ya kwanza tangu ilipopata uhuru kwa kukabidhiana madaraka kwa njia ya Amani. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt Damas Ndumbaro pamoja na viongozi wengine wakati wa sherehe ya kumuapisha Rais mpya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika uwanja mkuu wa michezo mjini Kinshasa, wengine pichani ni Rais Felix Tshisekedi pamoja na Joseph Kabila.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt Damas Ndumbaro pamoja na viongozi wengine wakati wa sherehe ya kumuapisha Rais mpya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika uwanja mkuu wa michezo mjini Kinshasa

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi wa Uuguzi MOI, Fidelis Minja (Kulia) akiwakabidhi dawa na zawadi nyingine wazazi wa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi wanatibiwa katika Taasisi hiyo. Wengine ni viongozi kutoka kwenye kurugenzi hiyo. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
  Baadhi ya viongozi wakiandaa dawa pamoja na zawadi nyingine kabla ya kukabidhiwa
  Kaimu Mkurugenzi wa Uuguzi MOI akijadiliana na viongozi wa kurugenzi yake kabla ya kutoa msaada kwa watoto
  Viongozi wa kurugenzi ya Uuguzi wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa wazazi wenye watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi
  Viongozi wa kurugenzi ya Uuguzi wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa wazazi wenye watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi
  Kaimu Mkurugenzi wa Uuguzi Fidelis Minja akizungumza na waandishi wa habari (Pichani hawapo)

  NA KHAMISI MUSSA

  Viongozi wa kurugenzi ya Uuguzi wa Taasisi ya Mifupa MOI leo wametoa msaada wa kijamii pamoja na dawa kwa watoto wenye vichwa vikubwa na Mgongo wazi wanaopata huduma katika Taasisi ya MOI wodi 5A. Msaada huo umetolewa ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha jamii kujitolea kwa wale wenye mahitaji maalumu pamoja na kuhamsisha huduma bora kwa wateja

  Mkurugenzi wa huduma za Uuguzi wa MOI Bwana Fidelis Minja amesema imekuwa ni utamaduni wa kurugenzi hiyo kufanya shughuli za kijamii kwa lengo la kuonyesha mfano kwa jamii na pia kuwaunga mkono wanajamii ambao hujitolea kwa ajili ya watu wenye uhitaji hususani wagonjwa

  “Sisi kama viongozi wa Kurugenzi hii ya Uuguzi tumeamua tutoe msaada kwa Watoto hawa wenye vichwa vikubwa pamoja na kuwapatia dawa ambazo tumenunua kwa kuchangishana fedha zetu, pamoja na msaada huu tutawahudumia na kuwapa faraja wazazi wao. Tunaamini hili ni jambo jema kama ambavyo wengine wamekuwa wakifanya” Alisema bwana Minja

  Bwana Minja ameongeza kwamba hii ni sehemu ya utakelezaji wa mpango mkakati wa Taasisi ya MOI ambao pamoja na mambo mengine unaelekeza juu ya uboreshwaji wa huduma za uuguzi pamoja na kutoa huduma bora kwa wateja yaani ‘Customer care’

  “Tumefanya hivi ikiwa ni sehemu ya kuonyesha kwa vitendo kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali yetu pamoja na kazi kubwa inayofanywa na kiongozi wetu wa MOI Dkt Respicious Boniface ambaye amejitoa kwa dhati kuboresha hali ya utoaji huduma kwa wateja” Alsiema Bwana Minja

  Kwaupande wake muwakilishi wa wazazi wenye vichwa vikubwa na Mgongo wazi Bi Zuena Ally amesema anaishukuru Serikali kwa kuboresha huduma na pia anawashukuru wauguzi ambao watoa msaada pamoja na dawa kwaajili ya Watoto

  “Nawashukuru sana kwa kuteletea dawa, tulizoea kuona watu kutoka nje ndio wanatuletea msaada lakini leo mmekuja nyie, Mungu awabariki sana kwa moyo wa upendo.Mtoto wangu anaendelea vizuri nashukuru sana kwa huduma nzuri” Alisema Bi Zuena.

  Taasisi ya MOI ipo kwenye utekelezaji wa mpango mkakati wake wa miaka 5 ambao pamoja na mambo mengine umejikita katika kuboresha huduma kwa wagonjwa. 


  0 0

  Kikao cha Nne cha Mawaziri mbalimbali kutoka Uganda na Tanzania wanaohusika na utekelezaji wa mradi wa bomba la Mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Tanga Tanzania kinatarajiwa kufanyika leo jijini Kampala ambapo Mawaziri hao wanatarajiwa kupata taarifa za majadiliano yaliyokuwa yakifanyika kati ya Timu ya Kitaifa ya Majadiliano (GNT) ya Tanzania na Uganda ambayo yalianza Januari 21, 2019.

  Kutoka Tanzania Mawaziri watakaohudhuria kikao hicho ni Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba.

  Aidha Makatibu Wakuu kutoka Wizara ya Nishati, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi pia watahudhuria kikao hicho, hii ni baada ya kufanya kikao jana na Makatibu Wakuu kutoka Wizara mbalimbali nchini Uganda wanaohusika na utekelezaji wa mradi huo hivyo Makatibu Wakuu hao ndio wataokawasilisha taarifa  kwa Mawaziri kuhusu majadiliano ya wataalam wa pande zote.

  Kabla ya kufanya kikao na Mawaziri wa Uganda, Mawaziri hao kutoka Tanzania mapema leo walifanya kikao  na wataalam kutoka Taasisi mbalimbali nchini Tanzania walio katika  Timu ya Kitaifa ya Majadiliano ya Mradi huo ili kupata taarifa ya awali ya hatua ya majadiliano.

  Baada ya kupata taarifa ya hatua ya majadiliano yaliyofikiwa kati ya pande hizo mbili, Mawaziri hao watajadili taarifa hiyo na endapo wataiafiki, hatua nyingine za majadiliano zitaendelea  ambazo  sasa zitahusisha Serikali ya Uganda na Tanzania na wawekezaji wa mradi ambao ni kampuni ya Total E&P  ya Ufaransa, Tullow Oil ya Uingereza, CNOOC ya China na kampuni za Mafuta za Taifa za Tanzania na Uganda.

  Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Tanga Tanzania litakuwa na urefu wa kilometa 1445.
   Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (katikati), Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi ( wa pili kushoto), Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ( wa pili kulia) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba (wa kwanza kulia) wakiwa katika kikao na wataalam wa Tanzania (hawapo pichani) wanaohusika na majadiliano ya mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Uganda hadi Tanzania.
   Wataalam kutoka Taasisi mbalimbali nchini Tanzania walio katika Timu ya Kitaifa ya Majadiliano (GNT) ya Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Uganda hadi Tanzania wakiwa katika kikao na Mawaziri kutoka Tanzania (hawapo pichani) wanaohudhuria mkutano kuhusu mradi huo unaofanyika jijini Kampala-Uganda.
   Kikao kati ya Mawaziri  na Wataalam mbalimbali kutoka Tanzania  waliohudhuria Mkutano kuhusu mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi unaofanyika jijini Kampala-Uganda.
   Watendaji mbalimbali kutoka Tanzania wakiwa katika kikao na Mawaziri kutoka Tanzania wanaohudhuria Mkutano kuhusu mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi unaofanyika jijini Kampala Uganda.
  Watendaji mbalimbali kutoka Tanzania wakiwa katika kikao na Mawaziri kutoka Tanzania wanaohudhuria Mkutano  kuhusu mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi unaofanyika jijini Kampala Uganda.

  0 0

  Mwandishi wetu-MAELEZO 


  SERIKALI itaendelea kushirikiana na sekta binafsi katika kutoa fursa kwa watu wengi kwa kuwezesha utekelezaji wa miradi mingi kwa mapana, katika Taasisi za serikali na Taasisi binafsi. 

  Akizungumza katika mjadala wa Clouds Media katika kipindi cha The Big Breakfast chenye kauli mbiu ya The power of Man yaani Nguvu ya Pamoja kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Serena, Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt Hassan Abbasi alisema kuwa serikali inaendelea na jukumu la ujenzi wa nchi kwa kushirikiana na sekta binafsi. 

  “Tunatambua na kuheshimu nguvu ya wengi kama kauli mbiu hii inavyoeleza, katika dhana ya maendeleo kuna mengi Serikali inafanya ili kutekeleza azma yake kwa wananchi, mfano Ujenzi wa madaraja mbalimbali nchini, Miradi ya Maji, Miradi ya Umeme, Ujenzi wa vituo vya afya na Hospitali na kulete ndege, kwetu sisi haya ni maendeleo makubwa sana”, Dkt. Abbasi. 

  Katika dhana ya Nguvu ya pamoja, Dkt. Abbasi alisema kuwa kauli mbiu hii inaonesha namna gani sasa haya mambo ambayo Serikali inafanya yanawafikia wananchi na kuwanufaisha popote walipo. 

  Dkt.Abbasi alieleza kuwa katika mjadala wa nguvu ya pamoja dhana ya maendeleo ina nadharia mbili ambazo wasomi wanazijadili duniani kote ikiwa ni moja ya miongozo ya maenedeleo duniani, huku wakiamini katika nadharia ya maendeleo ni watu na wengine wakiamini katika nadharia ya maendelo ni vitu. 

  “nilichokisema ni kwamba duniani kuna mjadala mkubwa sana katika suala la maendeleo, wapo wanaoamini kwamba maendeleo ni watu kwa mambo yanafanyika moja kwa moja na yanagusa watu, wapo wanaoamini kwamba maendeleo ni vitu kwamba huwezi kuwaendeleza watu bila kuwajengea miundombinu kama vile barabara, reli, umeme na maji”, Dkt Abbasi. 

  Katika kuunga mkono kauli mbiu ya nguvu ya pamoja, Dkt Abbasi alieleza kuwa katika nadharia mbili za maendeleo Serikali inaamini katika nadharia zote yaani maendeleo ni vitu kwani inatekeleza miradi mbalimbali kama barabara, Umeme, Maji, Afya na elimu, huku ikiwawezesha wananchi kupata elimu bure, dawa katika vituo vya afya na umeme, ambao kwa sasa unafika mpaka vijijini kwa maana ya maendeleo ni watu. 

  Aidha Dkt Abbasi alieleza kuwa kauli mbiu ya Nguvu ya pamoja kutoka Clouds Media ni moja ya njia kubwa katika kutimiza malengo la wananchi kwa kutekeleza na kusimamia miradi mbalimbali ambayo ndiyo inawawezesha wananchi kufanya shughuli zao za maendeleo. 

  Kwa upande wa sekta ya habari Dkt.Abbasi alieleza kuwa Serikali inafanya kazi kubwa kwa kushirikiana na sekta binafsi katika sekta hiyo muhimu pamoja na sekta zingine ambazo zinawezesha wananchi kujikwamua kimaendeleo. 

  “Serikali ndiyo mwezeshaji mkuu wa sekta mbalimbali, Sekta haiwezi kufanya kazi nchini bila Serikali kuiwezesha kwa hiyo katika dhana hiyo hiyo ya Nguvu ya pamoja Serikali inashiriki kwa nguvu zote”, Dkt Abbasi. 

  Dkt. Abbasi aliongeza kuwa Serikali itaendelea kuheshimu uwepo wa sekta binafsi katika sekta ya habari kwani mpaka sasa imewezesha upatikanaji wa leseni kwenye majarida na mageti 202, Vituo vya Televisheni 35 na Redio 160. 

  Alieleza pia kuwa nguvu ya pamoja ni pamoja na watendaji wa Serikali kushirikiana na sekta binafsi ili kuwawezesha kupata huduma mara moja pale inapohitajika kwa sababu watakuwa wanatenda jambo la kuwafanya wengi kupata ajira katika sekta hizo. 

  “Ukiangalia uanzishwaji wa viwanda ni lazima kuna mtendaji alijituma kutoa leseni, maendeleo ya biashara mbalimbali, kilimo na sekta zingine ni lazima upate leseni ni hata kwenye sekta ya habari hii inamaana kuwa mtendaji wa Serikali unapoharakisha kwa kufuata sheria na taratibu kuhakikisha mtu anapata leseni ya kuanzisha kiwanda, Biashara kubwa au gazeti utakuwa umeajiri watu wengi bila kujua na hii ndiyo the power of man (Nguvu ya pamoja)”, Alisisitiza Dkt. Abbasi. 

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu na Mumiliki wa Clouds media Group Joseph Kusaga aliahidi kushirikiana na Serikali katika kutangaza maendeleo ya nchi hasa kwenye sekta ya usafiri wa anga (shirika la ndege la Tanzania AirTanzania) pamoja na sekta ya utalii katika kampeni mbalimbali zitakazokuwa zinatangazwa Clouds Media.

  0 0

  Na: Sekela Mwasubila,Halmashauri yamKondoa Mji

  Halmashauri ya wa Mji Kondoa imepongezwa kwa kufanya uzinduzi wa baraza la wafanyakazi ikiwa ni halmashauri ya pili katika mkoa wa Dodoma kufanya hivyo.

  Pongezi hizo zilitolewa na Katibu Tawala wa Wilaya Andrea Mwani wakati akizindua baraza hilo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya uzinduzi uliofanyika katika ukumbi wa Kondoa Irangi Kondoa Mjini.

  Alisema kuwa uwepo wa baraza hilo ikawe chombo cha kusema katika kufikisha matakwa ya watumishi na kuimarisha ushirikiano na mwajili na kuwa anauhakika katika baraza hilo wajumbe watawasilisha wanayoona yatafaa katika kushirikiana na mwajiri kutatua changamoto za kazini.

  ”Mnaweza mkaona katika uongozi huu wa awamu ya tano jinsi Mheshimiwa Rais anavyofanya mabadiliko ya kuiendeleza nchi na wakuyafanya haya ni sisi wafanyakazi hivyo kila mmoja awajibike katika eneo lake na kujitathmini ili tuendane na upepo uliopo.”Alisema Mwani

  Aidha alisisitiza wafanyakazi kufanyakazi na kutimiza majukumu yao walioajiliwa nayo kwa asilimia zote pamoja na melekezo wanayopewa kwani kwa kufanya hivyo wanamsaidia Mheshimiwa Rais, Mkuu wa Wilaya, Halmashauri na wananchi wanaowahudumia.

  Aidha kwa upande wake Mkurugenzi wa Mji Kondoa Msoleni Dakawa alisema kuwa baraza limeanzishwa baada ya kuona umuhimu wa wafanyakazi kwa kuwa katika serikali mfanyakazi ndio mzalishaji na mtekelezaji wa maagizo na ahadi zinazotolewa na serikali.

  “Niombe kwa wakati mwingine kwa umoja huu tuliouonyesha na vyama vya wafanyakazi tuendelee nao iwe wakati wa shida na raha kwani lengo ni kuhakikisha mambo yanaenda nai tuna wajibu wa kupambana kama anavyofanya Mheshimiwa Rais lengo likiwa kuwahudumia wananchi na kuwapatia haki zao watumishi.” Alisisitiza Dakawa

  Naye mwakilishi wa vyama vya wafanyakazi ambaye ni Katibu wa TUGHE mkoa wa Dodoma Bwana Mchenya John alisema kuwa baraza la wafanyakazi ni chombo muhimu cha maamuzi kwa halmashauri na kuwataka wajumbe wa baraza kuacha uoga na kujadili mambo yatakayowasaidia kuendesha halmashauri na maslahi ya watumishi.

  “Namshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kulitolea maamuzi suala la kikokotoo kwani liliwakatisha taama sana wafanyakazi na nilishakuja hapa mwaka jana nikapata fursa ya kuongea na wafanyakazi na nashukuru walinielewa na kuwa watulivu wakati wote wa mpito hadi Mheshimiwa Rais alipolitolea maamuzi.”Alimaliza Bwana Mchenya.
  Katibu Tawala wa Wilaya ya Kondoa Andrea Mwani akiongea wakati wa uzinduzi wa baraza la wafanyakazi la Halmashauri ya Mji wa Kondoa. 
  Wajumbe wa baraza la wafanyakazi Kondoa wakiwa katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa baraza hilo.

  0 0

  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndungulile akizungumza katika hafla ua uzinduzi wa bidhaa ya kikombe hedhi na teknolojia ya simu ya mkononi ya mzunguko wa hedhi iliyozalishwa na Kampuni ya AnuFlo Industries Ltd. Jijini Dar es Salaam
  Na Karama Kenyunko Globu ya Jamii 

  NAIBU Waziri  wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndungulile amesema elimu ya hedhi bado ni changamoto hapa nchini, kwa sababu hakuna mfumo rasmi wa elimu hiyo na wengi hawaelewi kuhusu mzunguko.

  Dk. Ndungulile ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa bidhaa ya kikombe hedhi na teknolojia ya simu ya mkononi ya mzunguko wa hedhi iliyoanzishwa na Kampuni ya AnuFlo Industries Ltd. Jijini Dar es Salaam

  Akizungumza wakati wa uzinduzi huo amesema, elimu inatakiwa kutolewa ili kusaidia jamii kujua kuhusiana na mzunguko wa hedhi kwa sababu kuna baadhi ya wanafunzi wanakosa masomo wakiwa katika hali hiyo kwa kuhofia kuwa wapo tofauti na wengine.

  Amesema,  elimu hiyo inatakiwa kutolewa kwa wanaume pia kwani nao wanapaswa  kuujua juu ya mzunguko huu, tusiishie kwenye mzunguko wa mpira tu," amesema Dk.Ndungulile
  Amebainisha kuwa asilimia 50 ya watanzania wanaguswa na watoto hili hasa wasichana wenye umri  wa kati ya 15 hadi 18 asilimia 27 kwani  wengi wao ni wajawazito au ameshakuwa na mtoto.

   Amesema  takwimu Hizo ambazo hizo sio nzuri kwa nchi yetu, zimechangiwa zaidi na ukosefu wa elimu ya hedhi, na kuwashaurii kwa wadau mbalimbali waendelee kutoa elimu hiyo.

  Aidha Dk. Ndungulile ametaja changamoto ya upatikanaji wa vifaa vya hedhi salama kuwa bado ni kubwa kiasi ambacho mtu anaweza kupata maambukizi ya maradhi kama hajatumia vifaa salama.

  "Mimi kama daktari nalielewa sana jambo hili kwa upana, linaashilia kuwa kijana amepevuka na linaumuhimu katika ukomo wa hedhi, ambapo ndiyo mwisho wa kupata mtoto, kwa hiyo elimu hii ni muhimu kwa kila mmoja," alisema Dk.Ndungulile

  Ameongeza kuwa,  wakitokea wajasiliamali kama hawa tunahakikisha tunawashika mkono  kuhakikisha wanatimiza malengo yao.
  Naye,  Mkurugenzi wa Kampuni ya Anuflo, Flora Njelekela amesema tafiti za hedhi salama nchini zinaonesha, kuwa asilimia 65 ya wanawake nchini kupata hedhi kila mwezi huku asilimia 82 ya Wasichana na wanawake akiwa hawana uelewa juu ya afya na hedhi salama.

  Amesema, ukosefu bidhaa hedhi salama hulazimisha msichana mmoja kati ya 10 kukosa masomo kwa siku tatu hadi tano kila mwezi ambazo ni sawa na asilimia 20 ya siku za masomo kwa mwaka.

  Njelekela amesema  kutokana na uhaba wa bidhaa hizo,  garama takwimu, na tafiti zilizofanywa kuhusiana na hedhi salama ndiyo maana Kampuni yake ikajikita katika kuzalisha kikombe cha hedhi, kwa sababu ni salama ni hakina madhara, kinadumu kwa muda mrefu na Pia kitawafanya wanafunzi wasome kwa raha.

  Alisema kikombe hedhi hicho,  kimekuja kukabiliana na tatizo la uchafuzi wa mazingira, kwa sababu kitatumika kwa kipindi cha miaka mitano na  pia kinawekwa kwa masaa 12 asubuhi hadi jioni ndiyo mtu anakitoa.
  Mkurugenzi huyo amesema hiyo imetengenezwa kwa kuzingatia ubunifu makini na teknolojia za kisasa kwani kimetengenezwa kwa asilimia 100 ya LFGB medical silicone ambayo haileti Madhara 

  Kwa upande wake, Muwakilishi wa Ofisa  Elimu Mkoa, Maimuna Mtanda amesema kikombe hicho kitaondoa suala la utorosho shuleni , sio kwamba wanafunzi hawapendi kwenda shule ni kutokana na kutokuwepo na mazingira rafiki ya wao wakiwa kwenye hedhi.


  Naye, Dada Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana, Jangwani, Jackline Shio alisema walikuwa wanapata changamoto katika kipindi cha hedhi , kutokana na gharama za taulo za kike kuwa kubwa ila Flora ameweza kulitatua tatizo hilo kwa kuwaletea kikombe cha hedhi.

  Mwanafunzi huyo alitoa pendekezo kuwa elimu hiyo iendelee kutolewa ili kuokoa wanafunzi wanaokosa masomo, kipindi ambacho wanakuwa na hali hiyo.
  0 0

  Na Karama Kenyunko globu ya Jamii. 
  JAJI Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahimu Juma amewataka wasajili wa mahakama zote nchini kuhakiksha kesi zenye dosari haziingii kwenye Mfumo wa mahakama yoyote hapa nchini.

  Profess Juma, ameyasema hayo leo Aprili 25.2019 Jijini Dar e Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhudu maadhimisho ya wiki na siku ya sheria nchini, Ambayo hufanyika kila mwanzoni mwa mwaka yanayoashiria kuanza rasmi kwa mwaka wa Mahakama. 

  Amesema kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu Mahakama ya Rufaa pamoja na mahakama Kuu kutupilia mbali mashauri mbalimbali yanayopelekwa ambapo amebainisha kuwa hali hiyo inatokanana  na dosari zinazojitokeza kwe kesi hizo.

  Amesema, watu wengi wanalalamikia Mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu kutupilia mbali Mashauri kwa sababu ya dosari zinazojitokeza na kujiuliza kama Mahakama haiko makini ama la.

  Muhimbili wa mahakama upo wazi sana, kila kitu tunachokifanya kinapimika, unapofungua kesi unapewa muda wa kujibu, unaleta mashahidi, kesi inarekodiwa, hukumu inatolewa,"Hatupendezwi na malalamiko ya jumla jumla kwani kuna mfumo wa kupokea malalamiko, sisi tupo wazi na 

  Huwezi kuwazuia Wanasiasa wasizungumze ndio kazi yao, sisi tunafanya kazi kimya kimya na ukitaka majibu utayakuta katika nyaraka" amesema Jaji Profesa Juma.Aidha amemsifu Msajili aliyesimama kidete kukataa kusajili kesi yenye dosari, nampongeza kwa ujasiri, tuna Majaji wachache hatutaki kuwapangia kesi nyingi kisha wazifute" amesema Jaji Mkuu. 

  Kwa upande mwingine, aJi profesa Juma amewata wananchi ambao wamezoea kubeba mabango ya malalamiko, siku kilele cha wiki ya sheria waache kufanya hivyo na badala yake watumie wiki ya sheria kutafuta suluhu ya malalamiko hayo,ambayo mwaka huu Kitaifa itafanyikia jijini Dodoma katika viwanja vya Nyerere Square kuanzia Januari 31 na kuitimishwa Februari 6.2019 jijini Dar es Salaam. 

  Rais wa Jamuhuri ya  Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika siku ya kilele hicho ambacho kauli mbiu yake itakuwa ni, Utoaji wa Haki kwa wakati: wajibu wa Mahakama na wadau.

  Pamoja na mambo mengine Jaji Profesa Juma amesema mashauri mengi ya kesi yanachelewa kumalizika kutokana na uelewa mdogo wa wannchi ikiwa ni pamoja na kutokufahamu miongozo ya mashauri mbalimbali paomja na haki zao.

  Achilia mbali hayo pia amebainsha mafanikio ambayo wameweza kuyapata tofuati na miaka mingine ikiwa ni pamoja na kuanzisha matumizi ya usajili wa mashauri kwa njia ya elektroniki huku akisema kuwa licha ya njia hizo bado kasi ya mawakili kisajili mashauri bado ni ndogo
  Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani).
  Msajili wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania, Mhe. John Kahyoza (kushoto) na Mtendaji wa Makhakama Kuu ya Tanzania, Bw. Leonard Magacha (Kulia) wakimsikiliza Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu Maadhimisho ya Wiki na Siku ya Sheria nchini.
  Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi akizungumza wakati wa Mkutano wa Jaji Mkuu na Waandishi wa Habari kuhusu Maadhimisho ya Wiki na Siku ya Sheria nchini.
  Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari wakati wa mkutano kati yao na Jaji Mkuu wa Tanzania.
  Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati akizungumza wakati wa Mkutano huo. Kulia ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi.

  0 0


  Picha ya pamoja ya washiriki baada ya kupokea Tuzo ya ushindi wa kwanza kwa upande wa Banda bora la maonesho lilipambwa kwa unadhifu na kuvutia watu wengi [The Winner of Best Decoration Award] katika Maonesho ya Kimataifa ya Utalii ya Mwaka 2019 Jijini Mumbai, India tarehe 25 Januari, 2019. 
  Waziri wa Nchi anayeshughulikia masuala ya Utalii wa India, Mhe. K. J. Alphons akiwa katika banda la Tanzania. Kulia kwake ni Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda akiwa na washiriki wengine katika Maonesho ya Kimataifa ya Utalii ya Mwaka 2019 Jijini Mumbai, India tarehe 23 Januari, 2019
  Wageni mbalimbali wanatembelea banda la Tanzania ili kupata maelezo kuhusu vivutio vya utalii nchini. 
  Wageni katika banda la Tanzania wakipata maelezo kuhusu fursa na vivutio vya utalii nchini. 


  Ubalozi wa Tanzania, New Delhi, Taasisi za Serikali na kampuni binafsi mbalimbali za utalii nchini zimeshiriki Maonesho ya Kimataifa ya Utalii ya Mwaka 2019 nchini India yajulikanayo kama OTM 2019 [Outbound Travel Mart-2019] kwa lengo la kutangaza na kutafuta fursa mpya za soko la utalii nchini humo.

  Maonesho hayo maarufu na makubwa kabisa katika ukanda wa Asia-Pasifiki yalianza tarehe 23 Januari, 2019 na yamemalizika leo tarehe 25 Januari, 2019, Maonesho haya hufanyika kila mwaka katika Jiji la Mumbai na kushirikisha taasisi mbalimbali za utalii duniani.

  Taasisi za Serikali zinazoshiriki ni Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na Kituo cha Kutangaza Utalii wa Zanzibar India [Zanzibar Tourism Promotion Centre]. Kwa upande wa kampuni binafsi ni Leopard Tours, Zara Tours, Ngarawa Hotel and Resort, DOTCOM Safaris Ltd na Jackal Adventures.

  Katika Maonesho hayo, Banda la Tanzania limeibuka Mshindi wa Kwanza kwa upande wa Banda bora lilopambwa kwa unadhifu na kuvutia watu wengi [The winner of Best Decoration Award].

  Balozi wa Tanzania nchini India Mhe. Baraka Luvanda amesema kuwa maonesho hayo ni fursa adhimu kwa nchi kutangaza vivutio vya utalii ambapo wafanyabiashara wapatao 15,000 wanaojishughulisha na masuala ya utalii walishiriki kutoka katika mataifa zaidi ya 50 duniani. Washiriki wamepata fursa ya kupeana taarifa muhimu kuhusu mwelekeo na maendeleo ya biashara ya utalii katika maeneo mbalimbali duniani, vivutio vipya pamoja na kufanya biashara.

  Akiwa katika maonesho hayo, Balozi Luvanda alieleza kuwa maonesho yalisaidia washiriki kukutana na wadau na kuanzisha uhusiano wa kibiashara unaotarajiwa kufungua soko la utalii nchini baada ya wadau hao kupata maelezo ya kutosha kuhusu vivutio vilivyopo nchini na faida zake. Kwa ujumla, India ina soko kubwa la utalii. Tunategemea idadi ya watalii kutoka India wanaokwenda Tanzania itaongezeka mara dufu baada ya kuanza kwa safari za ndege za Shirika la Ndege la Tanzania [Air Tanzania] moja kwa moja kutoka Tanzania kuja India ambapo zinategemewa kuanza kabla ya mwezi wa Juni 2019.

  ‘Nachukua fursa hii kwa dhati kuwapongeza sana Maafisa wote walioshiriki katika Banda letu la Tanzania la Maonesho kwa kazi nzuri iliyowezesha ushindi huo wa kwanza kwa upande wa Banda bora lilopambwa kwa unadhifu na kuvutia watu wengi [The winner of Best Decoration Award]”, alisema Balozi Luvanda.


  Imetolewa na:

  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
  Dodoma.
  25 Januari 2019

  0 0


  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

  MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imewaagiza wasanii walioingia mikataba na kampuni za simu au mawakala kwa ajili ya kutumia kazi zao kama miito ya simu lakini hawajalipwa stahiki zao, wawasilishe katika ofisi hizo kwa ajili ya kupatiwa haki zao kuanzia 2016 hadi 2018

  Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James Kilaba, ameyasema hayo kumaliza kikao na wasanii na mawakala waliokuwa wakijadili kuhusu kutokuwapo na mgawanyo sawa wa malipo ya miito ya simu baina ya wasanii wa muziki, kampuni za simu na mawakala wanaouza kazi za wasanii na kufanya wasanii hao kupoteza haki zao.

  Katika kikao hicho, walikubaliana malipo kuwa kwa kipindi cha miezi sita ya kutafuta suluhu ya kudumu, malipo ya kazi za wasanii, mawakala, kampuni za simu na mtoa huduma yawe 50 kwa 50 kabla ya kuja na mfumo rasmi.

  “TCRA tumekutana na wadau wote ili kupata muafaka na hatimaye pasiwepo na malalamiko tena kutoka upande wowote na tukakubaliana kuwa kampuni za simu ziwasiliane na wasanii moja kwa moja badala ya kuishia kwa mawakala,” amesema.

  Amesema wamekubaliana kuwa upo uwezekano wa msanii kusaini makubaliano ya kutumiwa kwa kazi zake kama miito ya simu kwenye kampuni husika ya simu moja kwa moja na endapo atataka kutumia wakala afanye hivyo.

  Pia walikubaliana kuwa kampuni za simu ziwasilishe TCRA mgawanyo halisi wa gharama za utayarishaji wa kazi hizo za wasanii ambazo hutumika kama miito ya simu.

  Mhandisi Kilaba, amesema azimio lingine ni TCRA kuangalia uhalisia wa mikataba inayoingiwa baina ya kampuni za simu na mawakala au wasanii kuona kama ni rafiki katika mazingira ya biashara ya miito ya simu kuangalia unufaika kwa wasanii.

  Kilaba amesema June mwaka huu, tutakuwa tumeshaangalia namna ya gharama watakazokuwa wanalipana kati ya kampuni za simu, mawakala na wasanii.

  Aidha amesema mwaka jana walikuwa na kikao kwa ajili ya kujadili wanafanya nini na walikutana na mitandao yote ya simu. Lengo kufahamu nini kinaendelea katika kazi za wasanii wanazozitumia.
   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini TCRA Mhandisi James Kilaba akizungumza na waandishi mwafaka waliyofikia katika mapato yatokanayo na miito ya simu kwa miziki ya wasanii.
   Wadau wa muziki wa wakijadili mwafaka wa mgawanyo wa mapato yatokanayo na miito ya simu.
   Msanii Abdul Nasibu (Diamond Platinum) akichangia Mada ya mapato yatokanayo na miito ya simu katika mkutano ulioitishwa na TCRA.
   Mkutano kati ya Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA)   na Wadau wa muziki wakiwa katika mkutano wa kujadili kufikia mwafaka wa mgawanyo wa mapato yatokanayo na miito ya simu.
  Wadau wa muziki wakijadili mwafaka wa mgawanyo wa mapato yatokanayo na miito ya simu.

  0 0

   Askari Polisi akiwa amewashikilia ,Mhandisi wa Maji wa wilaya ya Monduli,Charles Saidea (kulia) na Mkandarasi ,Ayo Jeremia wa kampuni ya Meru Constructions mara baada ya Naibu Waziri kuamuru wakamatwe kutokana na kubainika kufanya udanganyifu katika mradi huo. 
   Mhadisi wa Maji wa wilaya ya Monduli,Charles Saidea akiingia kwenye gari la Polisi mara baada ya kushikiliwa kwa amri ya Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Juma Aweso baada ya kubaini kuwepo kwa udanganyifu katika mradi wa Maji unaendelea katika kijiji cha Lendenyika wilayani Monduli. 

   Mkandarasi ,Ayo Jeremia wa kampuni ya Meru Constructions akiingia kwenye gari la Polisi mara baada ya kushikiliwa kwa amri ya Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Juma Aweso baada ya kubaini kuwepo kwa udanganyifu katika mradi wa Maji unaendelea katika kijiji cha Lendenyika wilayani Monduli. 

   Mkandarasi ,Ayo Jeremia wa kampuni ya Meru Constructions pamoja na Mhandis wa Maji wa wilaya ya Monduli ,Charles Saidea wakiwa kwenye gari la Polisi mara baada ya kushikiliwa kwa amri ya Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Juma Aweso baada ya kubaini kuwepo kwa udanganyifu katika mradi wa Maji unaendelea katika kijiji cha Lendenyika wilayani Monduli. 
   Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliji,Juma Aweso akitizama namna mafundi wakiunganisha Bomba za Maji katika mradi unaopeleka maji katika Kata ya Sopeko kikiwemo kijiji cha Lendikinya wilayani Monduli katika mkoa wa Arusha.
   Mafundi wakiendelea na uunganishaji wa Bomba za kupeleka Maji katika kijiji cha Lendikinya wilayani Monduli mkoa wa Arusha. 
   Mhadisi wa Maji wa wilaya ya Monduli Charles Seidea akimueleza Naibu Waziri wa Maji ,Juma Aweso kuhusu namna mradi huo ulivyotekelezwa katika kijiji cha Lendenyika wilayani Monduli. 

   Baadhi ya Wananchi katika kijiji cha Lendenyika wilayani Monduli wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Juma Aweso (hayupo pichani) alipotembelea mradi huo kujionea maendeleo yake. 

   Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Juma Aweso akiwa ameongozana na Mbunge wa jimbo la Monduli ,Julius Kalanga pamoja na wananchi wakienda kujionea namna mkandarasi alivyopitisha Bomba za Plastiki kwenye Korongo badala ya Bomba za Chuma. 


   Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Juma Aweso akitizama Bomba za Plastiki zilizopitishwa katika Makorongo badala ya Bomba za Chuma katika mradi wa maji wa kusaidia vijiji 10 vya kata ya Sopeko wilayani Monduli. 

   Baadhi ya Bomba za Plastiki zikiwa zimepita kwenye Korongo badala ya Bmba za Chuma . 
   Baadhi ya wananchi katika kijiji cha Lendenyika wakishuhudia wakati watalaamu hao wakichukuliwa katika gari la Polisi.
  Anaandika Dixon Busagaga,Monduli.

  NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Juma Aweso ameamuru kukamatwa na kuwekwa mahabusu kwa Mhandisi wa Maji wa wilaya ya Monduli ,Charles Saidea na Mkandarasi kutoka kampuni ya Meru Constructions ,Ayo Jeremia kwa tuhuma za kufanya udanganyifu katika miradi wa maji inayoendelea katika vijiji 10 vya Halmashauri ya wilaya ya Monduli .

  Waziri Aweso ametoa agizo hilo katika kijiji cha Lendinyika wakati wa ziara yake ya siku moja katika wilaya ya Monduli kukagua utekelezaji wa Miradi ya Maji katika vijiji 10 vya Halmashauri hiyo,ziara ambayo hata hivyo alilazimika kuikatisha mara baada ya kubaini kuwepo kwa taarifa zinazo kinzana na taarifa ya utekelezaji wa mradi wa maji wenye thamani ya Sh Bil 1 na Mil 79 .

  Mbali na uwepo wa dosari nyingi za kiufundi ,mradi huo unaotajwa kukamilika kwa asilimia 85 bado haujaanza kutoa maji huku Mkandarasi akieleza kuidai Serikali sehemu ya fedha za mradi hu jambo ambalo Mhandisi alionekana kupinga uwepo wa madai hayo.

  Hoja ya kuwepo kwa Mabomba ya plastiki yaliyopita katika Makorongo iliibuliwa na mmoja wa wakazi wa kijiji cha Lendikinya Lemta Naisikie baada ya kutaka kujua kama ni sahihi kwa mkandarasi kupitisha Bomba hizo katika sehemu za wazi badala ya bomba za chuma.

  “Swali langu ni moja ,Bomba zilizotandazwa kuleta maji katika kisima kuu ,kuna sehem za Makorongo zote zimewekwa hii bomba la mpira ,hii naona ni changamoto afadhali ingewekwa bomba la chuma na maeneo mengine kuna mawe tungeomba mkandarasi atandaze bomba la chuma ili zisilete athari baadae”alisema Naisikie.

  Baada ya kutolewa kwa hoja hiyo Naibu Waziri ,Aweso aliamua kutembelea baadhi ya Makorongo na kujionea Bomba la Plastiki likiwa limepita juu badala ya Bomba la Chuma ndipo akaamua kutoa maelekezo .

  “Viongozi wenu wote wanazungumzia swala la maji ,Lendikinya ni moja ya vijiji vyenye changamoto kubwa sana ya maji ,Mbunge wenu amepiga sana kelele kuhusu maji kwa wananchi wa Monduli,sasa sisi leo tumekuja hapa tumeona kuna mradi wa zaidi ya sh Bil 1 na Mil 79 lakini mradi uko zaidi ya asilimia 80 lakini maji kwa wananchi hakuna .”alisema Aweso 

  “Unawauliza wataalamu wetu wakupe taarifa zile sahihi ,hawakupi ,leo mwananchi huyu wa kawaida kabisa anakupa taarifa sahihi mahala ambapo yalitakiwa kuwekwa mabomba ya chuma yameweka mabomba ya plastiki na hakuna usimamizi wa iana yoyote .”aliongeza Aweso.

  0 0


  0 0


   
  Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti John Wanyancha(kushoto) akimshukuru Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Mwanza Mkadam Mkadam alipozindua mafunzo kwa wadau wa usafiri jijini Mwanza, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Usinywe na Kuendesha.

  Mkurugenzi wa mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti John Wanyancha, akizungumza na wadau wa usafiri jijini Mwanza, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Usinywe na Kuendesha.
  Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Mwanza Mkadam Mkadam, akizungumza na wadau wa usafiri jijini Mwanza, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Usinywe na Kuendesha.  


  Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Mwanza Mkadam Mkadam, akizungumza na wadau wa usafiri jijini Mwanza, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Usinywe na Kuendesha,kushoto ni Mkurugenzi wa mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti John Wanyancha na kulia ni Mrakibu wa Polisi Mwandamizi Audax Majaliwa. 


  Mkurugenzi wa mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti John Wanyancha, akiwasilisha mada ya kuepuka kunywa na kuendesha kwa wadau wa usafiri jijini Mwanza, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Usinywe na Kuendesha.
  Wadau wa usafiri jijini Mwanza wakifuatilia mada wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Usinywe na Kuendesha inayofanywa na kampuni ya Bia ya Serengeti.


  Mwanza, Januari 25, 2019-Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imezindua kampeni inayolenga kutoa elimu kwa umma juu ya unywaji wa kistaarabu, ikiwa ni moja ya hatua muhimu inayochukuliwa na kampuni hiyo kuzuia ajali nyingi zinazosababishwa na madereva wanaoendesha wakiwa wametumia vilevi

  Kampeni hiyo inayobeba ujumbe wa, “Usitumie Kilevi na Kuendesha Chombo cha Moto’ imezinduliwa jijini Mwanza leo na ilianza na kongamano lililojadili unywaji wa kistaarabu ambalo liliwaleta pamoja wadau kama vile Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani, Mamlakka ya Usafirishaji wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA), madereva, abiria, na wadau wengine katika sekta ya usafirishaji

  Akiongea wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika katika hoteli ya Gold Crest, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani (RTO) mkoani Mwanza Mkaddam Hamis Mkaddam, alisema kwa kulishirikisha jeshi la Polisi kampuni ya SBL imeiunga mkono serikali katika kuelimisha umma juu ya unywaji wa kistaarabu na kusisitiza umuhimu wa kutatua tatizo hilo.

  Mkaddam alisema baadhi ya watu na haswa madereva hunywa kiasi kikubwa cha pombe pasipo kujali madhara yanayoweza kusababishwa na kitendo hicho na kuonya kuwa vitendo vya aina hiyo vinaweza kusababisha ajali mbaya.

  “Sote tunafahamu kuwa matumizi ya vileo yana uhusiano mkubwa na uendeshaji mmbovu ambao unaweza husababisha ajali mbaya za barabarani zenye athari kubwa kwa jamii zetu. Athari zake siyo tu zinawagusa watumiaji wa vilevi bali hata maisha ya wengine na kusababisha upotevu wa maisha na ulemavu kwa watu ambao wangeweza kuchangia uchumi wa nchi,” alisema Mkaddam.

  Alisema pamoja na kusababisha vifo visivyotarajiwa na majeraha, unywaji usiokuwa wa kistaarabu una maadhara makubwa kwenye sekta ya afya kwa kuwa kiasi kikubwa cha fedha kinatumika kwa ajili ya huduma, madawa na vifaa tiba kwa waathirika wa ajali za barabarani na hivyo kuwa ni mzigo kwa Serikali.

  “Ajali hizi pia ni mzigo kwa vyombo vyetu vya utekelezaji wa sheria kwa kuwa maofisa wanalazimika kuzishughulikia wakati zinaweza kuzuilika ambazo zinasabishwa na madereva wanaondesha wakiwa wametumia vilevi,” Mkaddam aliongeza.

  Akizungumzia namna kampeni hiyo itaisadia jamii, mkuu huyo wa usalama barabarani alisema, “sote kwa pamoja ikiwamo sisi polisi, madereva, jamii na wadau wengine tuna jumuku la kutafuta suluhisho la kumaliza tatizo la kutumia vilevi na kuendesha vyombo vya moto. Ninayo furaha kuona SBL pamoja na kwamba biashara yao ni kuuza vilevi, wameona wanawajibu wa kuhimiza unywaji wa kistarabu”.

  Kampeni hii inalenga kuwafikia vijana na watu wengine na kuwaeliisha juu ya madhara ya unywaji usiokuwa wa kistaarabu huku ikiwataka kubadili tabia kwa manufaa yao na jamii kwa ujumla

  Akiongea wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL John Wanyancha alisema kampeni ya unywaji wea kistaarabu inalenga kuielimisha jamii kuwa wanywaji wanapaswa kunywa kwa kiasi na kuhakikisha unywaji wao hauna madhara kwao na kwa watu wanaowazunguka.

  “SBL imedhamiria kuungana na serikali na wadau wengine kuhakikisha kuwa jamii na haswa madereva ambao wanakunywa na kuendesha vyombo vya moto wanaelimishwa juu ya madhara ya vitendo hivyo na kutakiwa kubadilisha tabia,” alisema Wanyancha.

  0 0

  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amekutana na Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika Dkt. Izeduwa Derex-Briggs kutoka shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Wanawake(UN Women) kwa lengo la kumpa taarifa ya Mkutano wa 63 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya wanawake duniani utakaofanyika Mjini New York Mwezi Machi Mwaka huu.

  Aidha Waziri Afya pamoja na Kiongozi huyo walifanya mazungumzo na kubadilishana mawazo kuhusu maeneo ambayo shirika la UN Women linayafanyia kazi kwa kushirikiana na serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

  Katika kikao cha muda mfupi ofisni kwa Waziri Ummy kiongozi huyo pia alimwalika Waziri Ummy kushiriki katika Mkutano wa Afrika wa kujenga msimamo wa pamoja ambao ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano Mkutano wa 63 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya wanawake duniani utakaofanyika Jijini Cairo mwezi Februari mwaka huu.

  Bi. Derex-Briggs pia ameitaka Tanzania kuhakikisha inaingiza masuala ya Jinsia katika taarifa yake itakayotoa katika Mkutano wa kimataifa wa Jukwaa la Juu la Kisiasa (High Level Political Forum) utakaofanyika Mwezi Julai ,9-18 Jijini New York Marekani mwaka huu.

  Wakati huohuo Waziri Ummy Mwalimu amemwambia Mkurugenzi huyo kuwa Wizara yake imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na Shirika la UN Women na kusema vipaumbele vyake kama Waziri mwenye dhamana imekuwa ni kuhakikisha wanawake wote wanapata huduma ya kujifungua salama katika vituo vya Afya.

  Aidha Waziri Mwalimu amesema maeneo mengine ya kipaumbele kwasasa ni uwezeshaji wanawake kiuchumi, juhudi za kuhakikisha kunakuwepo uwakilishi wanawake katika maamuzi ya kisiasa unaendelea kufikia 50/50 lakini pia kupunguza mimba na ndoa za utotoni ambazo ni kikwazo kwa wasichana wengi kufikia ndoto zao.

  Kuhusu suala la uwezeshaji wa wanawake kiuchumi Waziri Ummy amesema kuna asilimia 4 ya fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri zimekuwa zikitolewa kwa ajili kuwazesha wanawake kiuchumi lakini kuna idadi dogo ya wanawake wanaojitokeza kuomba mikopo hiyo.

  Katika sula la uwezeshaji wa wanawake kisiasa Waziri Ummy bado kuna changamoto ambazo zinahitaji kufanyia kazi ili wanawake waweze kujitokeza kwa wingi kushiriki katika masuala ya kisiasa kwani uwakilishi wanaume bungeni bado ni mkubwa ukilinganisha na wanawake.

  Naye mwakilishi wa shirika la UN Women Nchini Tanzania Bi. Hodan Addou amemwahakikishia Waziri Umy kuwa Shirika lake litaendelea kuchangia katika Maendeleo ya Wanawake Nchini kwani mpaka sasa limechangia katika Maeneo yote ya vipaumbelea kwa kushirikiana na Wizara.

  Aidha Bi. Derex-Briggs anaitembelea Tanzania kwa ziara ya kikazi tayari ametembelea Ofisi ya Taifa ya Takwimu na amekuwa Jijini Dodoma kutembelea Bunge la Tanzania ambapo amepata fursa ya kuongea na baadhi ya wabunge wanawake na kubadilishana nao mawazo kuhusiana na mstakabali wa masuala ya wanawake.
  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiongea na Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika Dkt. Izeduwa Derex-Briggs kutoka shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Wanawake(UN Women) ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam wa kwanza kulia ni Bi. Hodan Addou Mwakilishi wa Shirika hilo hapa Nchini.
  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiongea na Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika Dkt. Izeduwa Derex-Briggs kutoka shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Wanawake(UN Women) ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiongea na Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika Dkt. Izeduwa Derex-Briggs kutoka shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Wanawake(UN Women) ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam wa kwanza kulia ni Bi. Hodan Addou Mwakilishi wa Shirika hilo hapa Nchini. 
  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiagana na mgeni wake ambaye ni Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika Dkt. Izeduwa Derex-Briggs kutoka shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Wanawake(UN Women) ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika Dkt. Izeduwa Derex-Briggs kutoka shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Wanawake(UN Women) ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Mhe. Balozi Modest J. Mero (kulia) na Mwakilishi wa Kudumu wa Bosnia na Herzegovina katika Umoja wa Mataifa, Mhe. Ivica Dronjic wakiweka saini Makubaliano ya kuanzisha Mahusiano ya Kidiplomasia kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Bosnia na Herzegovina. Makubaliano hayo ambayo yatazingatia Mkataba wa Vienna wa masuala ya mahusiano ya kidiplomasia wa Mwaka 1961 uliwekwa saini New York, Marekani tarehe 25 Januari 2019. 
  Afisa wa Ubalozi, Bibi Lilian Mukasa akitoa maelekezo ya namna Waheshimiwa Mabalozi watakavyosaini Makubaliano ya kuanzisha mahusiano ya kidiplomasia baina ya nchi zao. 
  Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Mhe. Balozi Modest J. Mero (kulia) na Mwakilishi wa Kudumu wa Bosnia na Herzegovina katika Umoja wa Mataifa, Mhe. Ivica Dronjic wakibadilishana Nyaraka ya Makubaliano baada ya wawili hao kuweka saini.

  0 0

  Mhe. Kigwangalla kifuatilia maelezo kutoka kwa mdau wa utalii wa Tanzania Bw. Denis Lebouteux alipotembelea banda la Tanzania wakati wa maonesho ya FITUR 2019.
  Mhe. Dkt. Hamis Kigwangalla, Waziri wa Maliasili na Utalii akiongea na wadau wa utalii wakampuni ya Tanganyika Expedition Bw. Oscar Gabaldon (Kushoto) na Denis Lebouteux (katikati) punde alipowasili katika banda la Tanzania.
  Waziri Kigwangalla akiwa na wadau wa utalii wa Tanzania.
  Wadau wa Utalii akiongea na wadau wa utalii punde alipowasili katika banda la Tanzania.


  Na: Augustina Makoye

  Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamis Kigwangalla ametembelea banda la Tanzania katika maonesho ya kimataifa ya Feria 

  Internacionale de Turismo (FITUR) yanayofanyika Madrid nchini Spain na kuzungumza na wadau wa utalii kutoka Tanzania wanaoshitiki maonesho hayo.

  Waziri Kigwangalla amesema kuwa hii ni mara yake ya kwanza kuhudhuria maonesho ya Kimataifa ya utalii na amefurahi sana kukutana na kuongea na washiriki kutoka Tanzania na hivyo kupata uzoefu na kujifunza mambo mengi pamoja na changamoto zilizopo kwa Tanzania kushiriki maonesho ya Kimataifa.

  Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) ndiyo inayoratibu ushiriki wa Tanzania katika maonesho haya ambapo jumla ya makampuni binafsi manne (4) ya watoa huduma za utalii yanashiriki pamoja na Taasisi mbili (2) za serikali ambazo TTB Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA).

  Waziri Kigwangala yupo nchini Hispania kuhudhuria kongamano la kumi la uwekezaji katika sekta ya utalii na biashara linalofanyika katika eneo la Feria de Madrid yanapofanyika maonesho ya Fitur 2019.

older | 1 | .... | 1786 | 1787 | (Page 1788) | 1789 | 1790 | .... | 1896 | newer