Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live

Wananchi wahimizwa kuanza ujenzi wa Zahanati na Vituo vya Afya kabla ya Serikali kusaidia

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga kufuatilia na  kusimamia wananchi wa vijiji 12 vya bonde la ziwa Rukwa kuhakikisha kuwa wanaanza kujenga zahanati ili zahanati hizo ziweze kupunguza mzigo kwa vituo vya afya na hospitali ya wilaya.

Amesema kuwa ili hospitali ya Wilaya isiweze kuzidiwa na wagonjwa ni vyema vijiji vikawa na zahanati zao na kwa ngazi ya kata kuanza ujenzi wa vituo vya afya ili mgonjwa apitie katika ngazi hizo na hatimaye kufika katika ngazi ya hospitali ya wilaya tofauti na hapo hospitali hiyo inaweza kutumiwa na hata wagonjwa ambao wanaweza kutibiwa katika ngazi ya zahanati.

“Kwa upande wa vituo vya afya, jamani nisikitike hapa, katika kata 13 ambapo kila kata inapaswa iwe na kituo chake cha afya tunavyo vituo vya afya viwili peke yake, tuna kituo cha afya pale milepa na kituo cha afya hapa mtowisa, kwahiyo kata 11 hazina vituo vyake vya afya, kwahiyo hapa pia DC jipange tuanze,” Alisema.

Mh. Wangabo aliyasema hayo wikiendi hii katika songambele ya kuchimba msingi wa majengo saba kwaajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya katika kata ya Mtowisa na kuhusisha wananchi kutoka katika vijiji 10 na madiwani 13 wa kata zote za bonde la ziwa Rukwa ambapo hospitali hiyo inajengwa.

Akitoa taarifa ya ujenzi wa hospitali hiyo, mganga mkuu wa halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Fani Musa alisema kuwa hospitali hiyo itatumika kama kituo cha rufaa kutoka vituo vya afya na zahanati zote za halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga na kuongeza kuwa mradi utagharimu shilingi Bilioni 7.5 hadi kumamilika kwake ambapo itakuwa na majengo 22 na mpaka sasa halmashauri imepokea shilingi bilioni 1.5 kwaajili ya kuanza ujenzi huo.

“Fedha hizi za awamu ya kwanza zitatumika kujenga majengo saba, jengo la Utawala ambalo litatumia shilingi milioni 332, jengo la wagonjwa wa nje litatumia shilingi milioni 271, jengo la “Pharmacy” litatumia shilingi milioni 120, jengo la maabara litatumia shilingi milioni 171, jengo la vipimo vya mionzi (radiology, X-ray na Ultra Sound) litatumia shilingi milioni 121, jengo la kufulia litatumia shilingi milioni 110 na jengo la mwisho ni la wazazi litakalotumia shilingi milioni 379,” Alisema.

Katika hatua nyingine Mh. Wangabo amewataka wakala wa umeme vijijini kuhakikisha wanaongeza kasi ya kufikisha umeme kwenye bonde hilo ambalo lina wakulima wengi wa mahindi na mpunga pamoja na wavuvi ambapo mazao yao mengi huvushwa na kupelekwa mikoa ya jirani hivyo kuukosesha mkoa mapato na pia kwaajili ya kusaidia huduma za kiafya katika bonde hilo na kuongeza kuwa bila ya halmashauri kuongeza kasi ya kukusanya mapato malengo hayo ya kumalizia maboma hayatafikiwa.

Bonde la ziwa Rukwa lina vijiji 63, kati ya vijiji hivyo vijiji 24 vina zahanati, vijiji 17 vina maboma ya zahanati ambayo hayajaezekwa na vijiji 12 havina zahanati wala maboma, na kati ya kata 13 zilizopo katika bonde hilo ni kata 2 tu ndio zenye vituo vya afya na kufanya kata 11 kukosa vituo vya afya huku kata 3 zikiwa na maboma ya vituo hivyo.
Baadhi ya wananchi waliokuwa wamejitokeza kwenye songambele ya kuchimba misingi kwaajili ya majengo saba ya Hospitali ya Wilaya ya Sumbawanga itakayojengwa katika Bonde la Ziwa Rukwa, kata ya Mtowisa, Kijiji cha Mtowisa. 
 Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (wa pili toka kushoto ndani ya msingi) akisaidia kuchimba msingi wa itakayokuwa hospitali ya Wilaya ya Sumbawanga baada ya kushirikiki na wananchi wa bonde la ziwa Rukwa kwenye songambele ya uchimbaji wa misingi ambao ungegharimu shilingi milioni 8 kama wangetumika mafundi. 
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kushoto) akihamasisha wananchi waliojitokeza kwenye songambele ya uchimbaji wa misingi kwaajili ya ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Sumbawanga.
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (ndani ya msingi) akisaidia kuchimba msingi wa itakayokuwa hospitali ya Wilaya ya Sumbawanga baada ya kushirikiki na wananchi wa bonde la ziwa Rukwa kwenye songambele ya uchimbaji wa misingi ambao ungegharimu shilingi milioni 8 kama wangetumika mafundi. 
 Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule (kulia) akiendelea kuhamasisha wananchi walioshiriki kwenye songamebele ya kuchimba misingi kwaajili ya ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Sumbawanga.

Makabidhiano ya ofisi Wizara ya Ujenzi yafana

$
0
0
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Eng. Joseph Nyamhanga akimpongeza Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga mara baada ya kumkabidhi ofisi kufuatia kuhamishiwa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI wengine ni wajumbe wa Menejimenti ya sekta ya ujenzi.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Eng. Joseph Nyamhanga akisisitiza jambo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga katika hafla ya kumkabidhi ofisi wengine ni wajumbe wa Menejimenti ya sekta ya ujenzi.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga katikati akiwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Eng. Joseph Nyamhanga katika picha ya pamoja na wajumbe wa Menejimenti ya sekta ya ujenzi katika hafla ya makabidhiano ya ofisi mjini Dodoma.

Wahamiaji haramu 81 wakamatwa jijini Dar

$
0
0
WAHAMIAJI haramu 81 wamekamatwa wakiuza pipi, karanga na kahawa na kujifanya machinga. Akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake, Kaimu Afisa Uhamiaji mkoa wa Dar es Salaam, Mrakibu Novaita Mrosso alisema kati ya watu hao 35 ni raia wa Burundi ambao walikuwa wanafanya biashara hiyo kama machinga kwa kutembeza sehemu mbalimbali.

Wahamiaji hao, wamekamatwa mwishoni mwa wiki na Idara ya Uhamiaji wakifanya biashara hiyo jijini Dar es Salaam. Operesheni kali imekuwa inafanyika jijini zima ili kuhakikisha wahamiaji wote wanatiwa mbaroni ambapo wahamiaji hao baadhi wamejifanya machinga kukwepa kukamatwa. Hatua hiyo, imekuja baada ya mwishoni mwa mwaka jana, Rais Dkt. Magufuli kutoa vitambulisho maalum kwa ajili ya kuwatambua wafanyabiashara wadogo wadogo nchini ambapo kila Mkuu wa Mkoa alikabidhiwa.

Vitambulisho hivyo jumla 25,000 na kila kitambulisho kitagharimu shilingi 20,000 kwa machinga. Uhamiaji imeingia kazini baada ya kugundua kuwa wapo baadhi ya wahamiaji haramu wamekuwa wanafanya biashara kama wamachinga na kazi hiyo ilifanyika Januari 17, mwaka huu hadi Januari 20 ambapo jumla ya watu 81 walikamatwa.

Mrakbu Mrosso alisema wahamiaji hao wamekuwa wanauza kahawa, karanga, pipi na vitu vidogo sehemu mbalimbali za jiji huku wakijifanya kama sehemu ya machinga kujificha.

"Tumewanasa na wanafikishwa mahakamani haraka kisha watarudishwa kwao,"alisema. Aliongeza kuwa bado wanaendelea kuwahoji wahamiaji wengine 46 kujua wanatoka nchi gani na kujua uhalali wao wa kuwepo hapa nchini. "Hapa tumebaini wapo wasomali,wanigeria, Mcameroon na wengine,"alisema. Mrakibu Mrosso alisema kazi ya kuwasaka wahamiaji haramu ni endelevu na wamekuwa wanashirikiana na viongozi wa serikali za mitaa ili kuwabaini wote.

"Nawaomba watu wenye taarifa watupe habari, sisi tutaendelea kuwaficha wale wote wanaopa ushirikiano ili kuwakamata wahamiaji,kamwe hawaponi tutawakamata wote na wale wanaowaleta,"alisema. Pia, amewaomba viongozi walioajiri wageni kutoa taarifa kwa vile hivi sasa wanaendelea na kazi ya kupitia kila sehemu ikiwemo viwanda,ofisi, baadhi ya makazi ili kuwanasa wageni wote wanaoishi kinyemela.

Alisema wamefanya kazi hiyo toka Novemba na Disemba,mwaka jana na kuhakiki jumla ya wageni 16,102 ambapo 7,000 walihakikiwa katika ofisi ya mkoa.Wengine 3,613 walihakikiwa katika ofisi ya Ilala, 3,668 Kinondoni,1,267 Temeke,356 Ubungo na 198 Kigamboni. Mrakibu Mrosso alisema kwenye zoezi hilo,wamefanya utambuzi na uandikishaji wa raia wa Malawi na wahamiaji walowezi ambapo jumla waliandikishwa ni 1,770.

Kwenye mabao Kinondoni(756),Ilala (548)Temeke(162),Ubungo (144) na Kigamboni ni 150. Ametoa onyo kali kwa wananchi wanaohifadhi wahamiaji haramu kuacha mara moja kwa vile mali zao na kifungo huenda kikawakumba. "Unajua sheria imebadilika hivi sasa kifungu cha 46 cha sheria uhamiaji sura ya 54 rejeo la 2016,mtu akikamatwa amehifadhianaweza kufungwa miaka 20,gari au nyumba inataifishwa pia na adhabu zote zinaweza kuwa za pamoja,"alionya.
 Wahamiaji haramu waliokamatwa mkoa wa Dar es Salaam wakiwa wamechuchumaa  baada ya kufikishwa makao makuu ya uhamiaji.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
Kaimu Afisa Uhamiaji  jijini Dar es Salaam, Novaita Edmund Mrosso akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wahamiaji haramu  waliokamatwa  maeneo mbalimbali ya jijini Dar es Salaam .
Kaimu kamishina wa Uhamiaji jijini Dar es Salaam,Novaita Edmund Mrosso akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.


MAGAZETI YA LEO JUMANNE JANUARI 22,2019

NMB YATOA MSAADA VIFAA VYA UJENZI VYENYE THAMANI YA SH MILIONI TANO WILAYANI KITETO.

$
0
0
Meneja wa NMB kanda ya kati Dodoma, Msolo Mlozi amewaomba wananchi wa Wilaya ya Kiteto, kujiunga na Benki ya NMB kwa kufungua akaunti kwa lengo la kunufaika na Benki hiyo kwa nyanja mbalimbali zikiwemo Elimu, Afya na misaada ya Majanga inapojitokeza.

Mlozi ameyasema hayo hivi karibuni akiwa katika Kijiji cha Chang'ombe alipofika kutoa msaada wa bati, mbao na misumari vya thamani ya milioni tano, kuondoa adha kwa wanafunzi wa shule ya msingi Matereka.
 Meneja wa NMB kanda ya kati Dodoma, Msolo Mlozi akikabidhi mbao kwa Uongozi wa shule ya msingi Matereka,katika kijiji cha Chang'ombewilayani Kiteto hivi karibuni.
Meneja wa NMB kanda ya kati Dodoma, Msolo Mlozi akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali katika Kijiji cha Chang'ombe alipofika kutoa msaada wa vifaa vya ujenzi kama vile Mabati, Mbao na Misumari vyenye  thamani ya shilingi milioni tano, kuondoa adha kwa wanafunzi wa shule ya msingi Matereka.
 Meneja wa NMB kanda ya kati Dodoma, Msolo Mlozi akikabidhi mabati kwa uongozi wa shule ya msingi Matereka,katika kijiji cha Chang'ombe wilayani Kiteto hivi karibuni.

WAZIRI WA KILIMO AKUTANA NA RAIS WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA USHIRIKA DUNIANI

$
0
0
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisalimiana na Rais wa Shirikisho la vyama vya Ushirika Duniani (ICA) Dkt Ariel Guarco wakati walipokutana na kufanya mazungumzo Jana tarehe 21 Januari 2019 Jijini Dar es salaam.
Rais wa Shirikisho la vyama vya Ushirika Duniani (ICA) Dkt Ariel Guarco akikagua Samani zinazotengenzwa na Chama cha Ushirika DACICO cha eneo la Kariakoo Jijini Dar es salaam, Jana tarehe 21 Januari 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na Rais wa Shirikisho la vyama vya Ushirika Duniani (ICA) Dkt Ariel Guarco wakati walipokutana na kufanya mazungumzo Jana tarehe 21 Januari 2019 Jijini Dar es salaam. Wengine ni viongozi wa Shirikisho hilo Barani Afrika na Tanzania.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Shirikisho la vyama vya Ushirika Duniani (ICA) Dkt Ariel Guarco wakati walipokutana na kufanya mazungumzo Jana tarehe 21 Januari 2019 Jijini Dar es salaam. Wengine pichani ni viongozi wa Shirikisho hilo Barani Afrika na Tanzania.



Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) Jana tarehe 21 Januari 2019 katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo maarufu (Kilimo I) Mtaa wa Tazara Jijini Dar es salaam amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Shirikisho la vyama vya Ushirika Duniani (ICA) Dkt Ariel Guarco.

Katika mkutano huo uliotanguliwa na ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ya vyama vya Ushirika Jijini Dar es salaam Rais huyo ameambatana Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho hilo Ndg Bruno Roelants pamoja na Rais wa Shirikisho la vyama vya Ushirika Afrika Ndg Japhet Magomere na Katibu Mkuu wa Shirikisho la hilo barani Afrika Bi Chiyoge Sifa

Pamoja na mambo mengine Mhe Hasunga amemuhakikishia kiongozi hugyo wa Shirikisho hilo kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli imedhamiria kuboresha mapungufu ya muda mrefu kwenye vyama vya Ushirika ikiwemo kushughulikia viongozi wabadhilifu.

Hasunga alisema kuwa serikali kupitia Wizara ya Kilimo ipo katika mapitio ya sifa za viongozi wa Vyama vya Ushirika nchini ili kupata viongozi watakao ongoza kwa weledi sekta ya Ushirika.Alimueleza Rais huyo kuwa Dhana ya kuchagua viongozi wa ushirika wenye sifa ya kujua kusoma na kuandika imepitwa na wakati hivyo kuna kila sababu ya kuchagua viongozi wenye weledi na utashi katika utendaji.

Aliongeza kuwa mfumo wa ushirika ni nyenzo muhimu ambayo ukitumika vizuri itasaidia kuondoa umaskini wa wakulima hapa nchini na Dunia kote utaimarisha uanzishwaji wa viwanda kuleta tija katika kilimo hivyo ni lazima kuwa na juhudi za makusudi kuwa na viongozi wenye weledi.

Alisema kuwa Wizara yake pia imeanza kupitia upya sheria ya vyama vya Ushirika ili kuwa na Ushirika imara na wenye nguvu na tija kwa wakulima kwani kufanya hivyo kutaongeza Imani ya wananchi waliokata tamaa na Ushirika.

Alisema pia miongoni mwa changamoto zinazoikabili sekta ya Ushirika nchini ni kukosekana kwa taarifa sahihi za wanachama (Data Base) kuanzia vyama vya msingi (Union) hadi vyama Vikuu vya Ushirika (AMCOS) jambo ambalo kwa muda mrefu limepelekea kuwa na Ushirika usiokuwa na tija na manufaa kwa wakulima wanaotumia nguvu na rasilimali zao nyingi katika kilimo.Naye, Rais wa Shirikisho la vyama vya Ushirika Duniani (ICA) Dkt Ariel Guarco amesema kuwa msingi wa ziara yake hiyo katika Afrika Mashariki pamoja na nchi zingine ni sehemu ya utekelezaji wa wajibu wake ambapo alianzia Kenya, Rwanda na sasa Tanzania.

Alisema kuwa Tanzania ni miongoni kwa nchi zilizopo chini ya Jangwa la Sahara ambayo imepokea vyema dhana ya Ushirika ambapo serikali inaunga mkono kwa kiasi kikubwa hivyo ana Imani miaka michache ijayo kupitia mfumo huo wakulima watakuwa na mafanikio yasiyopimika.

Alisema kuwa amezuru nchini Tanzania kwa ajili ya kuonana na kufanya mazungumzo na wana Ushirika ikiwa ni sehemu ya kubaini na kuzitafutia ufumbuzi wa haraka changamoto mbalimbali kwenye sekta ya Ushirika. Vilevile ameeleza kuwa ziara hiyo ni sehemu ya kuendeleza na kuimarisha uhusiano uliyopo baina ya Tanzania na Shirikisho hilo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Shirikisho la vyama vya Ushirika Tanzania (TFC) Bi Aberhad Mbepera alisema kuwa ziara ya Rais huyo ni sehemu ya ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na ICA.Alitoa wito kwa wakulima kujiunga na vyama vya Ushirika kwani katika Ushirika kutaimarisha umoja na mshikamano kwa kufanya kazi kwa bidii na kuwa na kauli moja katika kupanga bei ya bidhaa zao pasina kugalalizwa.

Akitoa neno la shukrani Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini Dkt Titus Kamani alisema kuwa maisha ya watanzania yataimarika kupitia Ushirika hivyo Tume hiyo imejipanga kutoa elimu kwa wakulima nchini kuelewa umuhimu wa kujiunga na mfumo wa Ushirika.Alisema Ushirika ni nyenzo pana katika maisha halisi ya wananchi kwani hatua mbalimbali za wananchi zinategemea Ushirika kuanzia maisha ya kawaida, biashara na kilimo.

Aliongeza kuwa Tume ya Maendeleo ya Ushirika imedhamiria kuwanufaisha watu masikini kuwa na kipato cha kati kitakachomudu ukali wa maisha na kuwa na utajiri.

KAMATI YA BUNGE YAIPONGEZA WIZARA UKUSANYAJI MADUHULI

$
0
0

Na Asteria Muhozya, DODOMA

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeipongeza Wizara ya Madini kwa ukusanyaji maduhuli ambapo katika kipindi cha nusu Mwaka wa Fedha 2018/19, cha kuanzia mwezi Julai hadi 31 Disemba, 2018, ilikusanya shilingi 167,742,947,332 kati ya shilingi 310,598,007,000 iliyopangiwa.

Akiwasilisha taarifa kwa Kamati hiyo kwa niaba ya Katibu Mkuu, Kamishna wa Madini Mhandisi David Mulabwa, alisema kuwa, shilingi 310,320,0004,000 zilipangwa kukusanywa kupitia Tume ya Madini, na shilingi 278,003, 000 katika Makao Makuu ya Wizara na Chuo cha Madini Dodoma.

“ Mhe. Mwenyekiti, hivyo lengo la makusanyo kwa kipindi cha nusu mwaka Julai hadi Disemba 2018 ni shilingi 155,299,003,500. Hadi kufikia tarehe 31 Disemba, 2018, wizara ilifanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi 167,742,947,332 sawa na asilimia 108.01 ya lengo,” amesema Kamishna Mulabwa.

Akizungumzia juhudi za wizara katika kuvutia uwekezaji katika sekta ya madini, amesema wizara iliandaa kongamano la kutangaza fursa za uwekezaji katika sekta ya madini nchini lililojulikana kama China Tanzania mining Forum lililenga kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo katika sekta ya madini nchini, ikiwemo kutafuta soko la madini hayo nchini China na kuangalia fursa za ushirikiano kati ya Wizara ya madini Tanzania na Wizara ya maliasili ya China.

“ Mhe. Mwenyekiti kongamano hilo pia lilitumika kuwakutanisha wachimbaji wa Tanzania na watengenezaji wa mitambo mbalimbali ambayo hutumika kwenye shughuli za uchimbaji na uchenjuaji wa madini,”alisema Kamishna Mulabwa.

Kamishna Mulabwa ameongeza kuwa, katika kongamano hilo jumla ya wachimbaji wadogo 40 na wakubwa 4 kutoka Tanzania walishiriki kongamano hilo. Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akijibu hoja za Kamati kuhusu suala la ukusanyaji wa maduhuli alisema bado Wizara haijaridhika na kiwango kilichokusanywa na kuongeza kuwa, kama wizara katika mipango yake yenyewe ya ndani, imepanga kukusanya zaidi ya kiwango cha bilioni 310 iliyopangiwa.

“ Mhe. Mwenyekiti sisi wenyewe ndani tumejiwekea malengo yetu ya kukusanya zaidi ya kiasi tulichopangiwa. Tunajiongeza tuongeze kiwango hicho sisi wenyewe. Tunafanya hivyo ili mwakani hata kama tutaongezewa kiwango basi tuwe tayari tumekwisha jipanga,” amesisitiza Naibu Waziri Nyongo.

Akizungumzia udhibiti wa madini, alisema kuwa, Wizara inaendelea za jitihada na kudhibiti utoroshaji madini ambapo kwa upande wa madini ya tanzanite udhibiti unaendelea na kusema kuwa, kwa sasa madini hayo yanapita katika mfumo unaoeleweka.

“Januari 22, tutakuwa na mkutano wa Kisekta, watakuja wachimbaji na wafanyabiashara naamini watamweleza Mhe. Rais kero zao na tutasikia. “Lakini pia tumewaalika wakuu wa Mikoa ambayo shughuli za madini zinafanyika, tunataka kuweka mazingira mazuri kwa sekta.

Kuhusu changamoto za masoko ya madini, alisema wizara inataka kuhakikisha kwamba biashara ya madini inakuwa wazi na halali huku ikijipanga kukusanya zaidi kodi za serikali na kuongeza kuwa, wizara inajipanga kuweka mfumo mzuri wa soko la madini jambo ambalo litazinufaisha pande zote.

“ Mhe. Rais anataka tununue tuweke reserve. Lakini pia Serikali ikinunua kwa bei ya soko, hata wachimbaji watafurahi,” amesema Nyongo.

Akizungumzia suala la uhifadhi wa mazingira alisema kuwa wizara imeweka utaratibu wa pindi wawekezaji wanapoanzisha mgodi ni lazima waweke mpango wa namna watakavyofunga migodi huku suala la uhifadhi wa mazingira likipewa umuhimu wake.

Aliongeza kuwa, wizara inaweka mkazo kwa migodi kueleza mpango wa ufungaji migodi ambao utaacha mazingira yakiwa salama. Wakizungumza katika kikao hicho kwa nyakati tofauti, wajumbe wa Kamati hiyo, licha ya kuipongeza wizara kwa ukusanyaji wa maduhuli, waliitaka wizara kuweka mikakati madhubuti katika suala uongezaji thamani madini kutokana na zuio la usafirishaji madini ghafi nje ya nchi.

Aidha, wajumbe hao waliiitaka Wizara kuendelea kukiimarisha Kituo chake cha Jimolojia Tanzania (TGC) ili kuweza kutoa wataalam wa kutosha katika tasnia hiyo ya uongezaji thamani madini.

Wizara ilianza kukutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Januari 21 hadi 23, 2019.

MADEREVA MAGARI YA ABIRIA NZEGA WAILALAMIKIA HALMASHAURI YA MJI KUWAKAMATA,KUWATOZA FAINI

$
0
0
Na Amisa Mussa

MADEREVA  wa magari  madogo ya abiria ya Noah na Hiace wilayani Nzega mkoani Tabora wamelalamikia  hatua  zinazochukuliwa  na  Halmashauri  ya  Mji  wa Nzega  kuwakamata  na kuwatoza faini kwa madai  ya kutopakia  na  kushusha  abiria  katika  kituo  mpya  ya mabasi  badala  yake  wanatumia  kituo cha zamani  ambayo  hairuhusiwi  kwa mujibu  wa  namna  walivyosajiri  safari  za  magari  yao.

Wakizungumza na Michuzi Blog ,baadhi ya madereva hao wamelelemikia oparesheni za kamatakamata  zinazodaiwa kufanywa na halmashauri ya mji kwa kile kinachoelezwa kuwa wanakiuka  utaratibu  wa halmashauri  wa kubeba  abiria  nje  ya kituo kipya.

Kutokana na kukamatwa na kutozwa faini madereva hao wameiomba Serikali wilayani humo kuwatazama kwa jicho la tatu kwa kuwaruhusu kutumia stendi ya zamani kupakia na kushusha abiria kwa kuwa katika stendi mpya hawapati wateja wengi.

Dereva Hassan Amiri na Fredrick Ruangisa  wamesema endapo gari la dereva litabainika kuwa na makosa ni vyema watendaji wa halmashauri ya mji wa Nzega wakatoa taarifa kituo cha Polisi kwa kuwa askari ndio wenye mamlaka ya kukamata magari na si vinginevyo.

"Tunaomba kwa yeyote mwenye dhamana watusaidie turudishwe stendi ya zamani huko ndio rafiki kwetu tunapata wateja wengi," amesema Hassan

Kwa upande wake Zungu Joseph na Lucas Lusumo ambao ni wamiliki wa magari madogo wameisisitiza Serikali kuwatazama kwa jicho la huruma ili warudishwe stendi ya zamani kupakia na kushusha abiria.

Kutokana na malalamiko hayo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Nzega Philemon Magesa amesema msimamo  wa halmashauri hiyo ni kusimamia  kanuni  na taratibu  iliyojiwekea.

Amefafanua kuwa kwa sasa Mamlaka ya Usimamizi wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini(SUMATRA) Mkoa wa Tabora wapo wilayani humo kwa ajili ya kuzipaka rangi gari ndogo zinazofanya safari za mizunguko ya ndani.

Aidha imeelezwa kuwa Halmashauri  ya  mji  wa  Nzega  ilifanya  uamuzi  wa  kujenga  stend mpya  ya  mabasi  ili  kupanua  wigo  wa  ukusanyaji mapato  ya  Serikali  kwa mwezi na ikajiwekea  utaratibu  kwa  magari  yote  yanayobeba  abiria  kuhamishiwa  katika  stend  hiyo  mpya  ya mabasi  hatua  ambayo  imekuja  kusababisha  mzozo  baina  yake  na madereva  wa magari madogo,  wakidai  kuwa  stend  hiyo  mpya  wanakosa  abiria  wa  kutosha  kama ilivyo  kwa  stend  ya  zamani  waliyoizoea  ambayo  ipo  mjini.i.
Magari  madogo ya abiria ya Noah na Hiace
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Nzega,Philemon Magesa

CCM PANGANI YAMTUNUKU TUZO YA SHUKRANI RAIS DKT MAGUFULI KWA KURIDHIA KUTIA SAINI UJENZI WA BARABARA YA TANGA-PANGANI HADI BAGAMOYO

$
0
0
CHAMA Cha Mapinduzi wilaya ya Pangani kimemtunuku tunzo ya shukrani Rais John Magufuli kutokana na uwamuzi wake wa kuridhia na kutia saini kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Tanga Pangani hadi Bagamayo hivi karibuni .

Akikabidhi tunzo hiyo hapo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya wa Umoja wa wanawake wa chama hicho UWT Taifa Jesca Mbogo wakati akiwa katika ziara ya kukagua shughuli za maendeleo wilayani humo

Mwenyekiti CCM wilayani humo Hamis Mnegero alisema kuwa wameamua kutoa tunzo hiyo kama sehemu ya kurudisha shukrani kwa Rais Magufuli kutoka na kufanikiwa kutekeleza ndoto ya siku nyingi ya kuwa na barabara ya kiwango cha lami wilayani humo.

“Tunajua kuna juhudi kubwa ambazo zilikuwa zimechukuliwa na marais waliotangulia lakini ndoto hizo hazikuweza kutimia lakini kwa juhudi kubwa za Rais wa awamu ya tani tumeona ujenzi huo sasa unakwenda kufanyika”alisema Mnegero. Alisema kuwa barabara hiyo ilikuwa ni kilio cha muda mrefu kwa wananchi wa wilaya hivyo anaamini kwa kuanza kwa ujenzi huo kutaweza kufufua matumaini mapya kwa wilaya hiyo.

Kwa upande wake Naibu Katibu mbogo alisema kuwa serikali ya awamu ya tano inajitahidi kuboresha mazingira bora katika sekta mbalimbali ili kuhakikisha kila mtanzania anapata fursa ya kupata maendeleo na unafuu wa maisha.

“Kama mnavyoona utekelezaji wa sera ya elimu bure pamoja na uboreshwaji wa huduma za afya hii yote ni kuhakikisha mtoto wa kitanzania anakuwa na afya bora lakini anapata fursa ya elimu bora”alisema Naibu Katibu huyo. Naibu Katibu Mkuu Mbogo yupo mkoani Tanga kwa ziara ya siku tatu kwa ajili ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali pamoja na kuzungumza na wanachama wa UWT mkoani hapa.

Mwenyekiti Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Pangani Hamis Mnegero akizungumza na waandishi wa habari hatua yao ya kumtunuku tunzo ya shukrani Rais John Magufuli kutokana na uamuzi wake wa kuridhia na kutia saini kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Tanga Pangani hadi Bagamayo hivi karibuni kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa UWT Taifa Jesca Mbogo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa
Mwenyekiti Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Pangani Hamis Mnegero akizungumza na waandishi wa habari hatua yao ya kumtunuku tunzo ya shukrani Rais John Magufuli kutokana na uamuzi wake wa kuridhia na kutia saini kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Tanga Pangani hadi Bagamayo hivi karibuni kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa UWT Taifa Jesca Mbogo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa
Mwenyekiti Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Pangani Hamis Mnegero katikati akimkabidhi tuzo ya shukrani ya Rais John Magufuli ,Naibu Katibu Mkuu wa UWT Taifa Jesca Mbogo kutokana na uwamuzi wake wa kuridhia na kutia saini kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Tanga Pangani hadi Bagamayo hivi karibuni kulia ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah
Mwenyekiti Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Pangani Hamis Mnegero katikati akimkabidhi tuzo ya shukrani ya Rais John Magufuli ,Naibu Katibu Mkuu wa UWT Taifa Jesca Mbogo kutokana na uwamuzi wake wa kuridhia na kutia saini kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Tanga Pangani hadi Bagamayo hivi karibuni kulia ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah
Naibu Katibu Mkuu wa UWT Taifa Jesca Mbogo kushoto akitazama tuzo aliyotunukiwa Rais Dkt John Magufuli ya Shukrani na Chama cha Mapinduzi wilaya ya Pangani kutokana na uwamuzi wake wa kuridhia na kutia saini kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Tanga Pangani hadi Bagamayo hivi karibun katikati ni Mwenyekiit wa CCM wilaya ya Pangani Hamisi Mnegero kulia ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah
Naibu Katibu Mkuu wa UWT Taifa Jesca Mbogo kushoto akitazama tuzo aliyotunukiwa Rais Dkt John Magufuli ya Shukrani na Chama cha Mapinduzi wilaya ya Pangani kutokana na uwamuzi wake wa kuridhia na kutia saini kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Tanga Pangani hadi Bagamayo hivi karibun katikati ni Mwenyekiit wa CCM wilaya ya Pangani Hamisi Mnegero kulia ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah
 

RAIS DKT MAGUFULI AKIONGOZA MKUTANO MKUU WA KISEKTA WA WACHIMBAJI,WAFANYABBIASHARA NA WADAU WA SEKTA YA MADINI LEO JIJINI DAR

$
0
0
  Mhe. Rais John Pombe Magufuli anawasikiliza baadhi ya wachimbaji wadogo wa madini wakitoa kero zao katika mkutano Mkuu wa kisekta  wa wachimbaji, wafanyabiashara na wadau wa sekta ya Madini katika ukumbi wa Mwalimu J.K Nyerere jijini Dar es salaam 22, 2019.
 Mhe. Rais John Pombe Magufuli anawasikiliza baadhi ya wachimbaji wadogo wa madini wakitoa kero zao katika mkutano Mkuu wa kisekta  wa wachimbaji, wafanyabiashara na wadau wa sekta ya Madini katika ukumbi wa Mwalimu J.K Nyerere jijini Dar es salaam 22, 2019.
 Baadhi ya wadau wa sekta ya madini na wafanyabiashara waliohudhuria Mkutano Mkuu wa kisekta katika ukumbi wa Mwakimu J.K. Nyerere jijini Dar es salaam 22, 2019.
 Baadhi ya wadau wa sekta ya madini na wafanyabiashara waliohudhuria Mkutano Mkuu wa kisekta katika ukumbi wa Mwakimu J.K. Nyerere jijini Dar es salaam 22, 2019.

 Rais wa shirikisho la vyama vya Wachimbaji wadogo wadogo wa madini (FEMATA) John Bina alipokuwa akisoma hotuba kuwakilisha wachimbaji wenzake katika Mkutano Mkuu wa kisekta jijini Dar es salam, Mkutano huo unafanyika katika ukumbi wa Mwalimu J.K Nyerere leo Januari 22, 2019.
Mmoja wa Baadhi ya wadau wa sekta ya madini  akizungumza changamoto wanazokumbana nazo,mbele ya Rais Dkt John Pombe Magufuli kwenye Mkutano Mkuu wa kisekta katika ukumbi wa Mwakimu J.K. Nyerere jijini Dar es salaam leo Januari 22, 2019.
 Baadhi ya wadau wa sekta ya madini na wafanyabiashara waliohudhuria Mkutano Mkuu wa kisekta katika ukumbi wa Mwakimu J.K. Nyerere jijini Dar es salaam 22, 2019.

  Baadhi ya wadau wa sekta ya madini na wafanyabiashara waliohudhuria Mkutano Mkuu wa kisekta katika ukumbi wa Mwakimu J.K. Nyerere jijini Dar es salaam 22, 2019 wakifurahia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa ukumbini humo.

IGP Simon Sirro Afanya Mabadiliko Ya Makamanda Wa Polisi Wa Mikoa Mitatu

MBUNGE HALIMA MDEE AFIKA MBELE YA KAMATI YA BUNGE YA HAKI, MAADILI NA MADARAKA YA BUNGE

$
0
0
 Mbunge wa Kawe, Halima Mdee akiwa mbele ya kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge akiitikia wito wa hutuma zinazomkabili za kulilidhalilisha Bunge, tukio lililofanyika leo tarehe 22 Januari, 2019 katika ofisi za Bunge Jijini Dodoma. (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA YAWASILISHA TAARIFA YAKE YA UTEKELEZAJI KAMATI YA BUNGE YA HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII

$
0
0

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia leo imewasilisha taarifa yake ya utekelezaji wa bajeti kwa nusu mwaka ( Julai- Desemba, 2018) kwenye kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Mendeleo ya Jamii.

Taarifa hiyo ya Wizara imewasilishwa na Kaimu Katibu Mkuu Prof. James Mdoe na imeainisha kazi zilizotekelezwa na Wizara ikiwa ni pamoja na kusajili jumla ya shule 163 kati ya 175 zilizoomba, Wizara imekagua jumla ya Asasi 11,327 zikiwemo shule za Msingi 8,785, Sekondari 2,480 na vyuo vya Ualimu 62.

Wizara pia imeandaa mkakati wa Taifa wa Elimu Jumuishi wa mwaka 2018-  2021, kudahili sana huo 5842 waliojiunga na mafunzo ya Elimu ya Ualimu kwa mwaka wa fedha 2018/2019 kati ya 8,152 waliotarajiwa kujiunga na vyuo vya ualimu.

Prof. Mdoe pia ameieleza Kamati hiyo ya Bunge kuwa Wizara imeratibu skolashipu za wanafunzi wa vyuo Vikuu zinatolewa na nchi rafiki za Jumuiya ya Madola pamoja na nchi nyingine, kufuatilia Maendeleo ya udahili na uandikishaji wa wnafunzi katika Taasisi za Elimu ya Juu, kufuatilia utendaji wa vituo umahiri vya Afrika katika kanda ya Afrika Mashariki na Kusini.

Wizara pia imewezesha vyuo 20 vya Maendeelo ya Wananchi Kutoa Mafunzo ya Ufundi, kuzijengea uwezo taasisi za VETA, NACTE, na TCU ili kusimamia ubora wa Elimu ya Ufundi na stadi za Kazi.
 Viongozi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wakiongozwa na Waziri Joyce Ndalichako wakimsikiliza mwenyekiti wa kamati. 
 Baadhi ya maofisa kutoka katika taasisi mbalimbali zilizo chini ya Wizara ya Elimu wakiwa katika kikao cha kamati. 
 Wabunge wakiwa katika kikao hicho cha Kamati ya Bunge ya Huduma na Mendeleo ya Jamii.
 Baadhi ya maofisa kutoka katika taasisi mbalimbali zilizo chini ya Wizara ya Elimu wakiwa katika kikao cha kamati. 
wabunge wakifuatilia mijadala.

TAMASHA SAUTI ZA BUSARA MSIMU WA 16 KURINDIMA FEBRUARI 7-10 ZANZIBAR

$
0
0

NA ANDREW CHALE

BUSARA Promotions ambao ni waandaaji wa Tamasha kubwa la muziki la Sauti za Busara ambalo ni la msimu wa 16 linatarajiwa kurindima kwenye viunga vya Ngome Kongwe Zanzibar kwa kushuhudia shoo 44 kutoka kwa wanamuziki wa hapa nchini na Ukanda wa Afrika.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Tamasha hilo, Yusuf Mahmoud ‘Dj Yusuf’ amebainisha kuwa mambo kwa sasa yamepamba moto na maandalizi yamekamilika kwa asilimia kubwa hivyo watu mbalimbali wajiandae kufika kulishuhudia.

“Wadau na wapenzi wa muziki kutoka sehemu mbalimbali Afrika tutakutanika tena palepale Zanzibar katika kufurahia muziki bora kabisa Muziki wa Afrika ambao umekutanisha vipaji kutoka nchi za Afrika zikiwemo Moroco, Naigeria, Zimbabwe, Algeria. Pia zipo nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Uganda, Kenya na zingine nyingi za Ukanda huu bila kusahau Fi Q, Damian Soul, Mkubwa na Wanawake Crew, Tausi Women Taarab na Wengine wengi” alisema Yusuf.

Aidha, Yusuf amesema kwa mwaka huu wameamua kutumia kauli mbiu ya ‘Potezea rushwa sio dili’ wakiamini kuwa wasanii wanaweza kutumia sauti zao kukabiliana na tatizo hilo wakati wanasheherekea utajiri na mkusanyiko wa tamaduni mbalimbali za muziki wa Afrika.

“Katika kuunga mkono wasanii wanaotumia muziki kusimamia amani, umoja, haki za binadamu na uhuru wa kujieleza, ujumbe wenye nguvu ambao unaonekana katika tamasha la mwaka huu ni “Potezea Rushwa, Sio Dili!” alisema Yusuf.Aliongeza kuwa, “Rushwa ni janga linalotafuna na linalomomonyoa maadili ya jamii zetu barani Afrika na nje ya Afrika. Kibaya zaidi imefikia hatua kuwa hata baadhi ya watu wamekuwa wakichukulia ni jambo la kawaida.

“Tamasha moja pekee haliwezi kubadili jamii yote kikamilifu, hivyo, tunashirikiana pamoja na washirika wa ndani na wa kimataifa kuendeleza majadiliano kubadili mitazamo na kuchochea hatua mbalimbali kwa ajili ya uongozi bora,” alimalizia Yusuf.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Busara Promotions, Bi. Julia Bishop amesema kuwa tamasha hilo limekuwa likikuwa kila mwaka huku wastani wa watu wanaofika kushuhudia zaidi 20,000 ambapo ametumia wasaha huo kuendelea kuwaomba wadau wajitokeze kusaidia katika udhamini kwani mbali na kutoa burudani pia limesaidia kukuza mila, desturi na tamaduni za Mwafrika.

Nae Meneja wa Tamasha hilo Journey Ramadhan amesema kwa mwaka huu steji zinatarajiwa kuwa tatu huku ikiwemo ya Ngome Kongwe, Amphieter na ile ya wazi ya viunga vya Forodhan ambapo hapo kila mtu atashuhudia tamasha bure.Aidha, Journey ametaja baadhi ya Wasanii hao ni watakaopamba mwaka huu ni pamoja na a Faith Mussa (Malawi), Fadhilee Itulya (Kenya), Fid Q (Tanzania), BCUC (Afrika Kusini) na wengineo wengi.

Pia ameongeza kuwa, tamasha hilo linaendelea kuzitangaza Tanzania na Zanzibar ulimwenguni kote, kwa kuwa tamasha huvuta waandaaji wengi wa matamasha wa kimataifa, hivyo linatoa fursa kwa wasanii wa muziki wa Afrika Mashariki kusambaza muziki wao na kuifikia hadhira ya kimataifa.

“Orodha yetu ambayo inaonekana kuwa ni ya kawaida sana lakini yenye utajiri mkubwa wa vipaji, inahusisha upekee wa sauti kutoka Zanzibar na Tanzania, pamoja na makundi yale yanayojiandaa kwa ajili ya kuudhihirishia ulimwengu mkusanyiko wa aina mbalimbali ya miziki ya wazawa hasa,” alisema Ramadhan.

Kwa upande wake Balozi wa Norway, Nchini ambao ni wadhamini wakuu wa tamasha hilo, Bi. Elizabeth Jacobsen amesema wataendelea kudhamini tamasha hilo kwa kuthamini mchango wa sanaa kwa jamii hasa bara la Afrika.“Natoa wito kwa wadau wengine kujitokeza kutoa mchango wa kudhamini tamasha ili kulipa nguvu zaidi na liweze kuendelea kwa miaka yote” alisema Balozi Bi. Elisabbeth Jacobsen.

Kwa mwaka huu kiingilio kwa Mtanzania kwa siku ni Tsh. 10,000 huku kwa atakayenunua kwa siku zote nne atapata tiketi kwa Tsh. 20,000. Pia gharama za tiketi kwa wageni wa nje ya Afrika bei zinapatikana katika mtandao wa tamasha hilo hilo pamoja na getini wakati wote wa tamasha.

Uzinduzi wa tamasha hilo hiyo Februari 7 mwaka huu linatarajiwa kuwa na shughuli mbalimbali ikiwemo maandamano ya Parade mtaani ambayo yataambatana na shamrashamra za vikundi vya ngoma na wanamuziki pamoja na wananchi kupita mitaani kujivunia utamaduni wa mwafrika.

Mkurugenzi wa Tamasha la Busara Promotions, Yusuf Mahmoud ‘Dj Yusuf’ akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa utambulisho wa tamasha hilo kwa vyombo vya habari Jijini Dar es Salaam leo Januari 22,2019.
BUSARA Promotions ambao ni waandaaji wa Tamasha kubwa la muziki la Sauti za Busara ambalo ni la msimu wa 16 linatarajiwa kurindima kwenye viunga vya Ngome Kongwe Zanzibar kwa kushuhudia shoo 44 kutoka kwa wanamuziki wa hapa nchini na Ukanda wa Afrika.
 Meneja wa Tamasha la Sauti za Busara, Journey Ramadhan akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa utambulisho wa tamasha hilo kwa vyombo vya habari Jijini Dar es Salaam leo Januari 22,2019
 Meneja wa Tamasha la Sauti za Busara, Journey Ramadhan akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa utambulisho wa tamasha hilo kwa vyombo vya habari Jijini Dar es Salaam leo Januari 22,2019

 Mkurugenzi wa Tamasha la Busara Promotions, Yusuf Mahmoud ‘Dj Yusuf’ akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa utambulisho wa tamasha hilo kwa vyombo vya habari Jijini Dar es Salaam leo Januari 22,2019.

TPDC YAFUNGUA MILANGO YA USHIRIKIANO NA ZPDC

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Mhandisi Kapuulya Musomba (kushoto) akipokea zawadi ya mlango kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Zanzibar (ZPDC) ikiwa ni ishara ya kufungua milango ya ushirikiano baina ya TPDC na ZPDC. Viongozi mbalimbali wa TPDC na ZPDC wakifuatilia kwa makini maelezo yanayotolewa na Juvent Ndege (pipeline shift supervisor) katika kituo cha Kinyerezi jijini Dar es Salaam. 


Hivi karibuni Shirika la Maendeleo ya Petroli Zanzibar (ZPDC) lilifanya ziara yake ya kwanza kutembelea Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na kufanya mazungumzo yenye lengo la kufungua milango ya ushirikiano baina ya mashirika haya ya mafuta na gesi hapa nchini. Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa ZPDC Bi. Mwanamkaa Abdulrahman Mohamed. 

Katika historia fupi ya ZPDC iliyosomwa na Bi Mwanamkaa Mohamed, alisema na kusisitiza kuwa ZPDC bado ni changa na hivyo basi kupitia ushirikiano huo wanahitaji kujifunza mengi na kufanya kazi kwa bidii ili kufikia viwango ikiwa bado wapo kwenye maboresho ya mfumo wa shirika. “Tumesema tuje na kitu cha kuonyesha alama ya kufungua milango ya ushirikiano” alisema Bi Mwanamkaa huku akikabidhi alama ya mlango ikiwa ni ishara ya kufungua milango ya ushirikiano.

Naye Meneja mipango wa TPDC Lwaga Kibona aliungana na viongozi hao wa Zanzibar pamoja na wataalamu wa miradi ya gesi katika kutembelea miradi mbalimbali ya TPDC ikiwemo inayosambaza gesi asilia kwa matumizi ya viwandani, majumbani pamoja na kituo cha kujaza gesi kwenye magari (CNG) cha Ubungo na kituo cha kupokea gesi asilia Kinyerezi. 

Katika kituo cha kupokelea gesi cha Kinyerezi, Mhandisi Baltazari Thomas ambaye ni Kaimu Meneja Mkuu wa kampuni tanzu ya TPDC ijulikanayo kama GASCO alifafanua mambo mbalimbali yanayohusiana na gesi asilia ikiwemo upatikanaji wake na jinsi inavyopokelewa na kusambazwa kwa wateja mbalimbali ikiwemo Tanesco kwa ajili ya kuzalisha umeme. 

Baada ya kupokea maelezo hayo waliungana na wataalamu wengine kutembelea eneo hili kujionea namna kazi zinavyofanyika. Ujumbe kutoka Zanzibar ulionekana kuwa na maswali mengi yote yakiwa na lengo la kuwaongezea uelewa katika sekta hii ya mafuta na gesi pamoja na usimamizi wake. Kupitia wataalam wabobezi wa TPDC wageni hawa walipata fursa ya kujifunza na kujiongezea uelewa ambapo mwishoni kabisa walilishukuru shirika kwa maelezo ambayo wameyatoa na kuweka ahadi ya kwenda kuwajibika katika njia hizo hizo na zaidi ili kuleta manufaa kwa nchi.

TBA WAPEWA WIKI MBILI KUPELEKA FEDHA ZA UJENZI WA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA SIMIYU

$
0
0




Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitoa maelekezo kwa Injini mkuu wa TBA Simiyu Bw. Likimaitare Naunga wakati akipotembelea ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Simiyu. Kulia ni Mkuu wa mkoa huo Bw. Anthony Mtaka.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimsalimia ndugu wa mgonjwa aliyelazwa (jina halijafahamika) katika hospitali teule ya Somanda alipotembelea hospitali kuona hali ya utaoaji huduma za afya. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya Bi. Juliana Mahongo na Daktari zamu.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisisitiza jambo wakati alipotembelea wodi za Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Simiyu. Kushoto ni Mganga Mkuu wa mkoa Dkt. Mageda Kihulya, Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki Bi. Happines Lugiko na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Bw. Anthony Mtaka.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitembelea ujenzi wa jengo la uchunguzi na mama na mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Simiyu. Waliongozana nae ni viongozi waandamizi wa mkoa wakiongozwa na Mkuu wa mkoa huo Anthony Mtaka.



Na WAMJW-SIMIYU


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ameiagiza wakala wa ujenzi (TBA) kupeleka fedha za ujenzi zilizotolewa na Serikali katika ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu kuhakikisha zinafika ndani ya wiki mbili.

Agizo hilo limetolewa leo wakati alipotembelea ujenzi wa jengo la Uchunguzi na jengo la Mama na Mtoto na kutoridhishwa na kasi ya ujenzi huo huku sababu kubwa inayopelekea kusuasua ikitajwa ni fedha kidogo zilizopokelewa na wakala wa ujenzi wa mkoa wa Simiyu kiasi cha Shilingi Milioni 430 wakati serikali imetoa Bilioni 1.064 kwa ajili ya ujenzi huo.

“Ninawashngaa TBA kwanini wanakaa na fedha wakati wanajua mradi wa ujenzi unaendelea huku, serikali imetoa Bilioni 1.064 ili zitumike katika ujenzi wa Hospitali hii lakini TBA wameleta milioni 430 tu, hizo fedha zingine ziko wapi?”. Alihoji waziri Ummy.

Kufuatia hali hiyo Waziri Ummy ameahidi kushughulikia suala hilo na kuahidi fedha hizo zitafika katika mradi huo ndani ya wiki mbili ili ziweze kusaidia kuongeza kasi ya ujenzi wa majengo hayo ambapo yanatarajiwa kukabidhiwa na kuanza kutoa huduma kuanzia mwezi Juni mwaka huu.

Kwa upande wake Injinia mkuu wa TBA anayesimamia ujenzi huo Bw. Likimaitare Naunga amesema fedha zilizoletwa katika mradi huo hazitoshi na ndiyo sababu kubwa inayochangia kusuasua kwa mradi huo huku akitaka wakala wa ujenzi (TBA) kuhakikisha fedha hizo zinafika mapema ili zisaidie kuongeza kasi ya mradi na kufikia lengo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Bw. Anthony Mtaka amemuahidi Waziri Ummy kuwa atasimamia kwa karibu upatikanaji wa fedha hizo zilizopo TBA zinafika katika mradi na kuhakikisha mradi unakamilika ndani ya muda uliopangwa ili huduma muhimu za kibingwa zianze kutolewa Hopitalini hapo.

Wakati huo huo waziri Ummy ametembelea Hospitali teule ya Somanda iliyopo wilayani Bariadi na kuonekana kutoridhishwa na huduma zinazotolewa katika jengo la Mama na Mtoto ambapo alishuhudia huduma mbaya zinazotolewa kwa akinamama wajawazito na watoto wachanga.

Pia Waziri Ummy ameshangazwa baada ya kuona hakuna chumba cha kuhifadhia watoto wenye uhitaji wa huduma maalum kama huduma za joto kwa watoto waliozaliwa kabla ya muda (Njiti) na kuitaka Hospitali hiyo kuwa na chumba hicho muhimu.

Aidha, Waziri Ummy ameshangazwa na kutokuwepo kwa huduma za upasuaji katika jengo hilo huku sababu ikitajwa kutokuwepo kwa Sinki, hali inayosababisha usumbufu mkubwa kwa akinamama wajawazito wanaofika kupata huduma hospitalini hapo.

Kufuatia hali hiyo waziri huyo ametoa siku tatu kwa uongozi wa Hospitali hiyo chini ya Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Mageda Kihulya kuhakikisha wananunua sinki hilo na huduma za upasuaji zianze kutolewa mara moja katika jengo hilo.

Waziri Ummy yupo Mkoani hapa katika ziara ya kikazi ya kutembelea mikoa ya Simiyu, Geita na Shinyanga ili kuweza kuona hali ya miundombinu na utoaji huduma katika hospitali za rufaa za mikoa.

TANROADS NA JICA WASAINI MKATABA UJENZI WA DARAJA LA GEREZANI

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isack Kamwelwe akishuhudia utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa daraja la Gerezani kati ya Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (Tanroads), Eng. Patrick Mfugale (kushoto) na Meneja Mkuu wa Ujenzi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), Ichiro Aoki (kulia).
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (Tanroads), Eng. Patrick Mfugale (kushoto) na Meneja Mkuu wa Ujenzi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), Ichiro Aoki (kulia) wakibadilishana hati za mkataba wa ujenzi wa daraja la Gerezani mara baada ya kutia saini jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Waziri ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga (katikati) akifuatilia kwa makini hotuba ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isack Kamwelwe (hayupo pichani) kwenye hafla ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa daraja la Gerezani jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (Tanroads), Eng. Patrick Mfugale pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Barabara Nchini (Tanroads), Dakta Damas Lucas Nyahoro. 
Sehemu ya wawakilishi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) wakiongozwa na Mwakilishi Mkazi wa JICA Tanzania Bw. Toshio Nagase (kulia), wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isack Kamwelwe (hayupo pichani) kwenye hafla ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa daraja la Gerezani jijini Dar es Salaam.Imeandaliwa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isack Kamwelwe akitoa maelekezo kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (Tanroads), Eng. Patrick Mfugale (kulia) kabla ya kusaini makubaliano ya ujenzi wa daraja la Gerezani jijini Dar es Salaam leo, kati ya Tanroads na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA).
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (Tanroads), Eng. Patrick Mfugale (kushoto) akisisitiza jambo kwa Katibu Mkuu wa Waziri ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga kabla ya kusaini makubaliano ya ujenzi wa daraja la Gerezani jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isack Kamwelwe akisisitiza jambo wakati wa hafla ya utiaji saini wa makubaliano ya ujenzi wa daraja la juu eneo la Gerezani jijini Dar es Salaam leo kati ya Wakala wa Barabara Nchini (Tanroads) na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA).

TAZAMA TANZANIA SAFARI CHANNEL

TAARIFA MAALUM KWA WADAU WOTE WA ZAO LA MUHOGO NCHINI

DTB TANZANIA YATWAA UBINGWA WA MASHINDANO YA KIKAPU KWA TAASISI ZA FEDHA

$
0
0

Wachezaji wa kikapu kutoka DTB Tanzania wakisherehekea baada ya kuiadhibu NMB kwa pointi 90-73 katika pambano la fainali ya michuano ya Kikapu kwa Taasisi za fedha (Bankers Basketball League) kwa mwaka 2018/2019. Fainali ya pambano hilo ilifanyika Januari 19 kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es salaam. DTB-Tanzania walitwaa ubingwa huo bila kupoteza mchezo hata mmoja. Benki zilizoshiriki kwenye michuano hiyo ni pamoja na Azania CRDB, TADB na NMB.
Mlinzi mahiri wa timu ya kikapu ya DTB Tanzania, Frank Mwemezi akipokea kikombe kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa NMB, Juma Kimori baada ya kuibuka Mlinzi bora wa michuano ya kikapu kwa taasisi za fedha (Bankers Basketball League) kwa mwaka 2018/2019. Pambano la fainali ya michuano hiyo lilifanyika Januari 19 katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam ambapo DTB iliinyuka NMB kwa pointi 90-73. Benki nyingine zilizoshiriki kwenye michuano hiyo ni pamoja na Azania CRDB, TADB na NBC.
Wachezaji wa timu ya kikapu ya DTB Tanzania wakipiga picha aina ya ‘Selfie’ baada ya kuibuka washindi wa jumla wa michuano ya mpira wa kikapu kwa taasisi za fedha (Bankers Basketball League) kwa mwaka 2018/2019. Pambano la fainali ya michuano hiyo lilifanyika Januari 19 katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam ambapo DTB iliinyuka NMB kwa pointi 90-73. Benki nyingine zilizoshiriki kwenye michuano hiyo ni pamoja na Azania CRDB, TADB na NBC.
Wachezaji wa timu ya kikapu ya DTB Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kuibuka washindi wa jumla wa michuano ya kikapu kwa taasisi za fedha (Bankers Basketball League) kwa mwaka 2018/2019. Pambano la fainali ya michuano hiyo lilifanyika Januari 19 katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam ambapo DTB iliinyuka NMB kwa pointi 90-73. Benki nyingine zilizoshiriki kwenye michuano hiyo ni pamoja na Azania CRDB, TADB na NBC.
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live




Latest Images