Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

WIZARA YAZINDUA USHIRIKIANO MAMLAKA KUU SEKTA YA SHERIA

$
0
0
Na Sheiba Bulu.

Wizara ya katiba na Sheria imezindua ushirikiano wa Mamlaka Kuu za Sheria nchini zitakazokaa pamoja kubainisha uwezo na changamoto zinazoikabili sekta ya sheria nchini na kuzifanyia kazi ili kuongeza ufanisi wa sekta hiyo na hivyo kutoa mchango stahiki kwa taifa.
Ushirikiano huo umezinduliwa jijini Dar es Salaam na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (MB) na kuhudhuriwa na Jaji Mkuu Mhe. Prof Ibrahim Juma na Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome.

Akizindua ushirikiano huo Prof Kabudi amewataka wajumbe wa ushirikiano huo kufahamu kuwa wajumbe wote kwa ujumla wao wanajenga nyumba moja na wautumie ushirikiano huo kama chachu na hivyo kuleta tija na ufanisi kwa sekta ya sheria nchini ili iweze kutoa mchango wa kweli kwa Taifa.

“Sekta hii ni moja, wote hapa mnajenga eneo moja, tumieni ushirikiano huu kama chachu ya kuleta tija na ufanisi kwa sekta hii na muwe huru kushauri na kuzungumza ili kuifanya sekta ya sheria ambayo ni sekta mtambuka kutoa mchango wa kweli kwa taifa hili,” alisema Prof. Kabudi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Jaji Mkuu Mhe. Prof. Ibrahim Juma ameipongeza Wizara kwa  kuanzisha ushirikiano huo hasa ikizingatiwa kuwa sekta ya sheria ndio mama wa sekta zote nchini kwani sekta zote zinatumia sheria kujiendesha.

Amesema Ushirikiano ulioanzishwa utawezesha kuwepo kwa mashauriano baina ya mamlaka za sheria ili pamoja na mambo mengine utawezesha kuwa na msimamo mmoja juu ya masuala mbalimbali na pia utawezesha kutumika kama njia ya haraka ya kutatua changamoto mbalimbali katika sekta na kwa nchi kwa ujumla.

“ nipongeze kwa kuzindua ushirikiano huu, ni kitu kizuri kitawezesha kufanyika kwa mashauriano kwa pamoja na kutoka na msimamo mmoja kama timu, ushirikiaano huu unaweza kutumika kama njia ya haraka ya kutatua jambo na hivyo kutoa ushauri wa haraka kwa sekta husika kwa taifa na hata kwa uongozi wa nchi,” alisema Prof. Juma.

Ushirikiano huo unaongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kama Mwenyekiti na wajumbe wake ni Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Kisheria kwa Umma Wizara ya Katiba na Sheria, Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Sheria- Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mwandishi Mkuu wa Sheria, Mkurugenzi wa Mashtaka, Wakili Mkuu wa Serikali na Kabidhi Wasii Mkuu. 
 Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Shria Prof. Sifuni Mchome aliesimama akizungumza wakati wa uzinduzi wa ushirikiano wa mamlaka kuu za sheria nchini uliozinduliwa na Waziri wa Katiba na Sheria mhe. Prof. Palamagamba Kabudi jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi akizungumza wakati akizundua ushirikiano wa mamlaka za sheria nchini uliofanyika jijini Dar es Salaam leo, kushoto ni  Jaji Mkuu wa Tanzania Prof Ibrahim Juma.
 Jaji Mkuu wa Tanzania Prof Ibrahim Juma akizungumza wakati wa uzinduzi wa ushirikiano wa mamlaka za sheria nchini uliofanyika jijini Dar es Salaam  leo kulia ni Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi.
Wajumbe wa ushirikiano wa mamlaka kuu za sheria nchini katika picha ya pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi na Jaji Mkuu Mhe. Prof. Ibrahim Juma baada ya uzinduzi wa ushirikiano huo jijini Dar es salaam leo


WADAU WA MAENDELEO WACHANGIA MIFUKO 500 YA SARUJI ARUSHA

$
0
0
Na Vero Ignatus Arusha
Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG)  limetoa mifuko 500 ya saruji ili kusaidia ujenzi wa madarasa katika shule za sekondari zenye uhaba wa madarasa licha ya kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza mkoani Arusha.

Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Dr.Barnabas Mtokambali  amekabidhi mifuko hiyo kwa mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ikiwa ni kuunga mkono jitihada za serikali katika kuziba pengo la upungufu wa madarasa,ambapo amesema kuwa kanisa hilo limeaona lishiriki katika maendeleo ya jamii kwa kusaidia ujenzi wa madarasa.
Alisema kuwa kanisa linatambua juhudi zinazofanywa na serikali katika kutoa elimu kwa Watanzania hivyo wameamua kuungana na serikali kwa kutoa mifuko hiyo kama chachu ya maendeleo ya elimu katika mkoa wa Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema kuwa kanisa la TAG limekua la kwanza katika kutoa msaada kwa serikali na kuwezesha ujenzi wa madarasa kwani ufaulu umeongezeka kwa kiasi kikubwa huku madarasa yakiwa machache.
Gambo alisema kuwa serikali inatambua mchango wa taasisi za dini katika maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla hivyo wataendelea kushirikiana katika kuwahudumia Watanzania.
“Taasisi za dini ni wadau wakubwa wa maendeleo ambao licha ya miradi ya kuhudumia wananchi bado wanaliombea taifa amani ambayo ni nguzo muhimu kwa maendeleo ya taifa” Alisema Gambo
Muumini wa Kanisahilo Danford Massawe alisema kuwa makanisa yanapaswa kuiga mfano wa kanisa la TAG katika kushirikiana na serikali katika masuala ya maendeleo ili kuharakisha maendeleo.
1.Picha Wakwanza kushoto ni mkuu wa kanisa la Tanzania Assemblies of God nchini Tanzania Dkt. Barnabas Mtokambaki akimkabithi mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo mifuko 500 ya Saruji.

MAGAZETI YA LEO JUMANNEJANUARI 15,2019

SERIKALI YAFUTA MASHAMBA SITA YA MOHAMED ENTERPRISES

$
0
0
Na Munir Shemweta, KOROGWE 

Serikali imeyafuta mashamba sita yenye ukubwa wa hekari 12,915.126 ya kampuni ya Mohamed Enterprises yaliyopo korogwe mkoa wa Tanga. 

Uamuzi wa kufuta mashamba hayo unafuatia mapendekezo yaliyotolewa na halmashuri ya wilaya ya Korogwe kufutwa mashamba hayo kutokana na kutoendelezwa kwa muda mrefu na baadaye maombi hayo kuwasilishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wizara kwa nia ya kufutwa. 

Mashamba yaliyofutwa ni yale yaliopo eneo la Mombo, Mabogo pamoja na Kwalukonge wilayani Korogwe mkoani Tanga. 

Akizungumza mara baada ya kutembelea mashamba hayo Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk. Angeline Mabula alisema mashamba yaliyobatilishwa ni kati ya mashamba 14 yanayomilikiwa na kampuni ya Mohamed Enterprises Mazinde wilayani Korogwe na kubainisha kuwa uamuzi huo unalenga kujenga nidhamu kwa waliopewa rasilimali za serikali kuzingatia masharti ya uwekezaji. 

Alisema, mara baada ya halmashauri ya wilaya ya Korogwe kupeleka mapendekezo ya kufutwa mashamba ya Mohamed Enterprises, wizara ya ardhi ilifanya ufuatiliaji juu ya mambo ya halmashauri husika la kutoendelezwa mashamba na baada ya kujiridhisha ikawasilisha maombi hayo kwa rais na kuridhiwa. 

Alisema, uamuzi huo wa Rais kuridhia ubatilishaji mashamba sita kati ya 14 yanayomilikiwa na Mohamed Enterprises unalenga kuhakikisha wote waliopewa maeneo kwa ajili ya uwekezaji wanazingatia masharti na taratibu za uwekezaji. 

Hata hivyo, Dk Mabula alisema mashamba ambayo hayajabatilishwa yamewekewa utaratibu kwa nia ya kuyaboresha kwa kuwa baadhi yake yanahitaji maboresho kwa nia ya kufanya vizuri. 

Ameitaka halmashauri ya Korogwe kupanga mpango wa matumizi bora ya ardhi katika eneo la mashamba yaliyofutwa na kipaumbele kwa watakaopewa maeneo katika mashamba hayo ni wananchi waliokuwa wakiishi katika mashamba hayo na sehemu itakayobaki atafutwe mwekezaji mwingine kwa kuwa lengo la serikali ni kuwa na uwekezaji wa viwanda.

Aidha, Dk Mabula alimpongeza Mkuu wa mkoa wa Tanga Martin Shigela kwa kufanya kazi nzuri ya kufutilia na kusimamia maagizo mbalimbali tangu Rais John Pombe Magufuli alipoanza kubatilisha mashamba ambayo hayajaendelezwa katika mkoa wa Tanga. 

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Tanga Martin Shigela aliwataka wananchi wa Korogwe kutovamia maeneo ya mashamba yaliyobatilishwa hadi hapo Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe itakapopanga matumizi bora ya ardhi katika mashamba hayo. 

Alisema, ndani ya wiki hii ataitisha mkutano na wataalamu wa sekta ya ardhi katika mkoa huo pamoja na wale wa bodi ya Mkonge kuangalia matumizi ya ardhi iliyobatilishwa kwa wananchi na uwekezaji. 
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula akimsikiliza Meneja wa Mashamba ya Mkonge ya Mohamed Enterprises ya Mazinde Korogwe mkoa wa Tanga Alhaji Imam Sheketo wakati alipofanya ziara katika mashamba ya mkonge mkoani Tanga leo tarehe 14 Januari 2019, kulia kwa waziri ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela.
Mkazi wa Mabogo Korogwe mkoani Tanga Said Mbazi Idawa akiwasilisha malalamiko yake wakati wa ziara ya Naibu waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula katika Mashamba ya Mkonge Korogwe mkoa wa Tanga.
aibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula akiwasikiliza wananchi wa Mabogo Korogwe mkoa wa Tanga wakati alipotembelea mashamba ya mkonge mkoani Tanga leo tarehe 14 Januari 2019.
Meneja wa Shamba la Mkonge la Mohamed Enterprises lilipo Korogwe mkoani Tanga Alhaj Imam Sheketo akimuonesha Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela sehemu ya mashine za kutengeneza katani katika shamba lilipo eneo la Mabogo Korogwe Tanga.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela na Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Kisa Gwakisa wakimuongoza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula kuangalia eneo la mashine za kutengeneza katani katika shamba la Mohamed Enterprises lililopo Mabogo Korogwe mkoani Tanga. (PICHA ZOTE NA MUNIR SHEMWETA-WIZARA YA ARDHI)

WATEJA 6 WAJINYAKULIA SIMU SAMSUNG S9+ SHINDANO LA MASTABATA YA NMB

$
0
0
SHINDANO la Benki ya NMB kuhimiza matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' linalojulikana kama 'MastaBata', leo limeendelea kuchezeshwa huku wateja sita wakijishindia simu janja za kisasa 'Samsung S9+' zenye thamani ya shilingi milioni 2,300,000/- kila moja.

Katika droo hiyo ya nne pia wateja 20 wengine wa benki hiyo wamejishindia fedha taslimu shilingi 100,000/- ambazo zitaingizwa kwenye akaunti zao moja kwa moja ndani ya saa 24 tangu kuchezeshwa kwa droo hiyo. Droo hiyo ya nne iliyochezeshwa leo jijini Dar es Salaam imefikisha wateja 80 hadi sasa ambao wameshindia kiasi cha shilingi 100,000/- kila mmoja.

Akizungumza na wanahabari mara baada ya kuchezeshwa droo ya leo, Meneja Mwandamizi kutoka kitengo cha kadi cha Benki ya NMB, Manfredy Kayala alisema mbali na droo hiyo kupata washindi 20 wa shilingi 100,000/- kila mmoja, wateja 6 wengine wamejishindia simu aina ya Samsung S9+' kila mmoja yenye thamani ya shilingi milioni 2,300,000/-.

Alisema wateja hao wamepatikana baada ya kuchezeshwa droo iliyojumuisha wateja wote wa NMB waliolipa au kufanya manunuzi kwa kutumia mfumo wa 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' na wao kujishindia zawadi hizo.

Hata hivyo, aliwaomba wateja wa NMB kuendelea kutumia huduma hiyo, kwani kampeni hiyo inayotarajia kuwazawadia zaidi ya shilingi milioni 100 wateja wa NMB inaendelea na takribani wateja 200 watanufaika na shindano hilo.

Meneja wa NMB Tawi la Mlimani City, akizungumza katika droo hiyo iliyofanyika kwenye tawi lake.

Meneja kutoka kitengo cha Kadi cha Benki ya NMB, Sophia Mwamwitwa (kulia) akizungumza kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa Droo ya nne ya kampeni ya matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' inayojulikana kama 'MastaBata' Bodi. Katikati ni Ofisa Mwandamizi Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humudi Semvua akisimamia droo hiyo na Domitila Silayo wa NMB (kushoto).

Mtaalam kutoka kitengo cha Kadi cha NMB, Domitila Silayo (kulia) akiwasiliana na mmoja wa wateja wa NMB waliojishindia simu janja za kisasa 'Samsung S9+' yenye thamani ya shilingi milioni 2,300,000/- kwenye droo ya nne ya Shindano la MastaBata. Katikati ni Ofisa Mwandamizi Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humudi Semvua akisimamia droo hiyo pamoja na Sophia Mwamwitwa wa NMB akishuhudia (kushoto).
Meneja Mwandamizi kutoka kitengo cha kadi cha Benki ya NMB, Manfredy Kayala akizungumza na waandishi wa habari kufafanua wateja walivyojishindia zawadi anuai kwenye Masta Bata ya NMB.

Nkasi waitikia wito wa serikali katika kukikuza kilimo cha kahawa Mkoani wa Rukwa.

$
0
0
Wakulima katika halmashauri ya wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa wameitikia wito wa kuunga mkono juhudi za serikali katika kukuza zao la kahawa mkoani Rukwa na kuhakikisha wanalima zao hilo kwa wingi ili kubadili kipato chao na hatimae kushawishi wawekezaji wa kuchakata zao hilo kuwekeza Mkoani humo ili kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Zao la kahawa ni miongozi mwa mazao matano ya kimkakati yanayohimizwa na serikali ya awamu ya tano katika kuinua kipato cha wananchi pamoja na pato la nchi kwa ujumla.

Wakulima hao wakiongozwa na mkulima mzoefu wa zao hilo Elias Mwazembe alisema kuwa zao la kahawa linastawi katika mkoa mzima wa Rukwa hivyo aliushukuru uongozi wa Wilaya pamoja na Mkoa kwa kuendelea kuwasaidia pale wanapokwama mbali na changamoto aliyoipata mara ya kwanza alipolima katika hifadhi yam situ wa mfili na kuondolewa na serikali.

“Nilipoona kwenye Mkoa inakubali na kwenye wilaya ikabidi nije huku (Kijiji cha) Kalundi nikaanzisha kulima mwezi wa tatu nikaona ile kahawa inastawi vizuri kwahiyo nikaona hapa sio pa kuachilia niendelee na zao la kilimo lakini sikutulia niliendeleza hamasa kwa watu wengine kuwaambia kuwa zao la kahawa mkoani Kwetu linakubali ingawa changamoto ikawa mtu alikuwa anahitaji avune kwa mwaka huo huo nikasema mbegu iliyopo ni miaka miwili unaweza kuvuna kahawa na kwa umri nilionao nitavuna mpaka vitukuu,” alisema.

Nae Afisa kilimo wa Kijiji cha Kalundi Jiasi Muyunga alikiri kuwa kitendo cha mkulima huyo Elias Mwazembe kufika katika Kijiji hicho kumepelekea wakulima wengi kutaka kujihusisha na kilimo hicho cha kahawa baada ya kuona kuwa kinastawi vizuri katika Kijiji hicho na hivyo kutoka wito kwa maafisa ugani wenzie juu ya kuwasaidia wakulima na kuwakikishia kuwa zao hilo ndilo litakalokuwa mkombozi.

Kwa upande wake Afisa kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi alisema kuwa baada ya kubaini kwamba kata 18 zilizopo ufipa ya juu zenye eneo la hekta 48,000 kuwa zinafaa kulima zao hilo hal,mashauri ilianisha maeneo ya kuanza nayo huku wakishirikiana na kituo cha utafiti cha Tacri kilichopo Mbimba Wilaya ya Mbozi, ili kujua mbegu inayofaa katika maeneo hayo na hatimae kuwapeleka wataalamu na wakulima kwenda kujifunza.

“Mkulima ambaye tumemtembelea leo ndugu Mwazembe ni mmoja wa wakulima hao ambao nae alikwenda kujifunza Mbimba na baada ya kutoka huko aliendeleza juhudi za kufanya kilimo hiki cha kahawa na tunae mkulima mwingine yupo Kijiji cha Kakoma kata ya Namanyere nae pia mepanda kahawa karibu miche 500 na kitaluni ana miche karibu 12,000 na kuna taasisi zaidi ya sita ambazo tumepa miche iliyotokana na kilo 100 za mbegu ambapo kila kilo moja inatoa miche 4000, hivyo tunaamini baada ya miaka mitatu halmashauri itaanza kuona faida yake,” Alisisitiza.

Aidha Afisa kilimo wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa Ocran Chengula aliwashauri wakulima wote wanaotarajia kuanza kilimo hicho cha kahawa kuhakikisha kuwa wanaandaa mashimo mapema na kuweka mbolea ili iweze kuchangayikana na udongo

“Tunatakiwa kuandaa mashimo mapema, kama unategemea kupanda mwaka huu maana yake unaze kuandaa mashimo mwezi wa nane ama wa tisa kwa kuchimba mashimo na kuweka mbolea ili mbolea iweze kuchanganyikana na udongo ikishaanza mvua mwezi wa kumi na moja ile miche inatakiwa ihamishwe kwenye mashamba ili mvua itakavyonyesha iweze kushika na kuwa na nguvu zaidi ya kuweza kukua,” Alifafanua.

Mkoa wa Rukwa unategemea kuwa na miche 1,040,000 ifikapo mwakani inayotokana na kilo 260 za mbegu za kahawa inayopandwa kwenye vitalu mwaka huu ili kuweza kuisambaza kwa wakulima na taasisi mbalimbali ikiwa ni kuhamasisha kilimo cha zao hilo pamoja na kuinua kipato cha wananchi, mkoa na taifa kwa ujumla.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo alipotembelea kitalu cha mkulima wa kahawa Elias Mwazembe katika Ziara yake ya siku nne katika Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi.

Mamlaka ya mkemia mkuu wa serikali kuanzisha maabara ya vinasaba vya wanyama

$
0
0

NA WAMJW, ARUSHA

Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Kanda ya Kaskazini - Arusha, ipo mbioni kuanzisha Maabara maalum Vinasaba vya wanyama ambayo itasaidia kutambua asili ya mnyama ikiwemo wanyama waliopo ama waliokufa.

Akizungumza wakati wa ziara maalum ya Maafisa Uhusiano waliotembelea Kanda hiyo leo, Meneja Kanda ya Kaskazini Christopher Anyango abainisha kuwa kwa sasa wapo katika ukarabati wa jengo ambalo Maabara hiyo itakuwepo. Awali ujenzi wa jengo hilo ulisimama baada ya ufadhili wake kukoma na hivyo kuilazimu Mamlaka kufanya ukarabati ili kujipatia sehemu ya kufanyia kazi.

"Maabara ya vinasaba vya wanyama ni muhimu sana. ukanda huu kutokana na kuwa na wanyama wengi na pia eneo la Kanda ya Kaskazini kuwa na watalii wengi ambao wanakuja kuona wanyama . Kwa sasa utaratibu unaendelea wa Kumalizia jengo hili na baadaye vitendea kazi kuwekwa "ameeleza Anyango.

Anyango ameongeza kuwa suala la kuwatunza wanyama ili waendelee kuwepo, Ni suala la msingi na Maabara itakapokamilika hakuna sampuli zitakazosafirishwa nje ya Kanda ya Kaskazini kwa uchunguzi.

"Pale hitaji litakapokuwapo kwa ajili ya uchunguzi wa wanyama hawa, baasi Kazi hii itafanyika hapa hapa Arusha." Alisema Anyango.Aidha, ametaja faida ambazo zitapatikana kwa Nchi ni pamoja na uwepo wa data zao kwa wanyama hao ikiwemo wanyama wanaolindwa Kimataifa kama Kifaru, tembo na wanyama wengine wengi ambao wapo hatarini kutoweka.

Maabara hii inatarajiwa kuwa ya kwanza Nchini na itakuwa ndio maabara Bora kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki.Maabara hiyo itaweza kufanya uchunguzi kwa wanyama wote wakiwemo walio hai na waliokufa.

Aidha, wamemshukuru Serikali ya awamu ya tano ya Mhe. Rais Dk Joseph Pombe Magufuli kwa kutenga na kuridhia kiasi cha bajeti ya Shilingi Milioni 950 ya kwa ajili ya kumalizia jengo hilo.
Jengo la mamlaka ya maabara ya mkemia mkuu wa serikali kanda ya kaskazini-Arusha
Meneja Kanda ya Kaskazini Christopher Anyango akiwatembeza maofisa  habari wa wizara na taasisi wa wizaravya afya wakati walipotembelea Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wakati wa kampeni ya "Tumeboresha Sekta ya Afya"ambayo imeanza kwa mikoa ya Dar es Salaam,Arusha na Kilimanjaro.

RC Kilimanjaro atoa pole Msiba wa Mama Mzazi Kaimu Rais wa Chemba ya Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA)

$
0
0
Na Nicolas Glliard, Moshi

Kaimu Rais wa TCCIA ambaye pia ni Mkurugenzi wa Makampuni ya OpenSanit amefiwa naMama  yake Mzazi Mwalimu Luciana Leon kilichotokea juzi Ijumaa tarehe 11.01.2019 katika hospitali ya KCMC na mazishi yatafanyika kesho Jumatano Shambani kwake Longuo , Moshi tarehe 16.01.219.

Mwalimu Luciana (66) alifundisha shule mbali mbali Mkoani Kilimanjaro kabla ya kuwa Afisa Elimu na Mhifadhi kwenye Makumbusho ya ya Taifa, Azimio la Arusha ARUSH, kijiji cha makumbusho na na Makao makuu kabla ya kustaafu na kuwa Mhifadhi kujitegemea na Mkulima .

Mungu aiweke Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi Amina.

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro akitoa akitoa pole kwenye msiba wa Mwalimu Luciana Leon Mama wa Mzazi wa Kaimu Rais wa Chemba ya Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) Octavian Mshiu Nyumbani kwa Marehemu Leo Longuo , Moshi.
 

NHIF ni nguzo muhimu kwetu- KCMC

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Moshi

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), umetajwa kuwa nguzo muhimu katika uimarishaji wa huduma za matibabu katika hospitali mbalimbali nchini.

Akizungumza na Maofisa Uhusiano wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mkurugenzi wa Hospitali ya Kanda KCMC, Gileard Masenga alisema kuwa mchango wa NHIF umekuwa ni mkubwa katika upande wa mapato pamoja na uimarishaji wa miundombinu na vifaa tiba.

"Kwa kweli niseme ukweli kabisa NHIF kwetu ni uti wa mgongo katika uendeshaji wa shughuli zetu na ndio maana kila siku nikikutana na Mkurugenzi Mkuu Konga huwa namwambia watulindie sana huu Mfuko maana umekuwa mkombozi mkubwa sana katika sekta ya afya," alisema Dkt. Masenga.

Alieleza kuwa maboresho makubwa yaliyofanywa katika eneo la wagonjwa wa dharula hospitalini hapo yanatokana na NHIF. " Kwa sasa wagonjwa wanapata huduma katika eneo zuri na lenye nafasi ikilinganishwa na awali," alisema.

Kwa upande wa Meneja wa wa NHIF Mkoa wa Arusha, Isaya Shekifu amesema kuwa Mfuko umekuwa na mpango wa uimarishaji wa miundombinu na upatikanaji wa vifaa tiba kupitia fursa ya mkopo nafuu kwa lengo la kuboresha huduma za matibabu.Shekifu amesema kuwa katika kipindi cha uongozi wa Awamu ya Tano, NHIF imekuwa na Mafanikio makubwa katika utoaji wa huduma kwa wanachama wake ikiwemo kuwafikia wananchi katika maeneo yao.

Alisema kuwa usogezaji wa huduma kwa kuwa na ofisi kila Mkoa umesaidia kutoa huduma bora kwa wananchi na kupanua wigo wa wanachama lengo likiwa ni kuwafikia asilimia 50 ya wananchi ifikapo mwaka 2020."Tumejipanga vizuri kutokana na serikali awamu ya tano ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli kuwekeza kwa nguvu katika sekta ya afya hatutarudi nyuma na kumwachia Rais Mwenyewe...lazima tuwafikie wananchi ili waweze kupata huduma kirahisi kupitia NHIF," amesema Shekifu.

Naye Afisa Uhusiano wa NHIF, Grace Michael alitoa wito kwa wananchi kujiunga na huduma za Mfuko ili wawe na uhakika wa kupata huduma za matibabu wakati wowote."Mfuko umejipanga vizuri kuhakikisha unafika kijiji kwa kijiji ili kila Mtanzania apate elimu ya Bima ya Afya na hatimaye ajiunge na kwa kufanya hivyo atakuwa na uhakika wa kupata matibabu na uhakika wa kutunza Afya yake," alisema Grace.
Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa NHIF akiwa katika picha ya pamoja na maafisa Uhusiano wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo walipotembelea ofisi ya Kanda mkoani Arusha.
Afisa Uhusiano wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya (NHIF) Grace Michael akizungumza katika ofisi ya Kanda ya NHIF mkoani Arusha wakati Maafisa Uhusiano wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo walipotembelea ofisi hiyo ikiwa ni Kampeni ya Tumeboresha Sekta ya Afya inayofanywa Maafisa hao.
Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya (NHIF) Isaya Shekifu akizungumza na maafisa Uhusiano wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo wakati walipotembelea Ofisi ya Kanda hiyo mkoani Arusha ikiwa ni kuangalia uwekezaji uliofanywa na serikali ya Awamu ya Tano Rais Dkt John Pombe Magufuli ikiwa ni Kampeni ya Tumeboresha Sekta ya Afya ya Maafisa hao.

BODI YA MISHAHARA YATAKIWA KUTOFANYA KAZI KIMAZOEA KUTEKELEZA JUKUMU LAKE

$
0
0
Watumishi na wajumbe wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma wametakiwa kutofanya kazi kimazoea katika kutekeleza jukumu lake la msingi la kuishauri Serikali namna bora ya kuoanisha na kuwianisha mishahara na masilahi ya watumishi wa umma nchini kwa lengo la kuwavutia na kuwabakiza watumishi katika Utumishi wa Umma ili waweze kuwahudumia vizuri wananchi katika Taasisi za Umma.

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati akizungumza na watumishi na Wajumbe wa Bodi ya Mishara na Masilahi katika Utumishi wa Umma  makao makuu ya bodi hiyo, wakati wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji, kufahamu majukumu ya bodi na kujiridhisha namna bodi hiyo inavyotekeleza majukumu yake.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema kuwa, yeye ni muumini wa ufuatiliaji hivyo atakuwa akifanya ziara za kushtukiza katika ofisi za Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma kwa lengo la kujiridhisha na utendaji kazi wa bodi hiyo, hivyo amewataka watumishi hao kubadilika na kuachana na utendaji kazi wa kimazoea ili bodi hiyo iwe na tija na manufaa kwa watumishi wa umma nchini.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesisitiza kuwa, pamoja na kuwataka watumishi na wajumbe wa bodi hiyo kufanya kazi kwa uzalendo, uaminifu na uadilifu lakini pia amewataka kuwa wabunifu katika kutekeleza majukumu yao ili kuisadia Serikali ya Awamu ya Tano kutimiza azma yake ya utoaji motisha kwa watumishi wa umma ili waweze kuwa na ari ya utendaji kazi. 

Aidha, Dkt. Mwanjelwa amewataka wajumbe wa bodi ambao ni wastaafu na wazoefu katika utumishi wa umma, kila mmoja kwa nafasi yake kutoa mchango utakaowezesha bodi kutekeleza majukumu yake kikamilifu na kwa wakati, na kuongeza kuwa, yeye binafsi anaamini kwa uzoefu wa wajumbe wanaounda bodi hiyo, Serikali itapata ushauri bora wa kuoanisha na kuwianisha mishahara na masilahi ya watumishi wa umma nchini.

Kwa upande wake, Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma, Bibi Mariam G. Mwanilwa amesema kuwa, lengo la kuanzishwa kwa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma ni kuwa na chombo kimoja cha kuoanisha na kuwianisha mishahara na masilahi ya watumishi wa umma ili kuwa na mfumo endelevu unaoondoa malalamiko kuhusu masilahi miongoni mwa watumishi wa umma kwa lengo la kuwavutia na kuwabakiza watumishi katika Utumishi wa Umma.

Bibi Mwanilwa ameeleza kuwa, hivi sasa bodi inafanya utafiti wa hali ya masilahi na uhusiano wake na mifumo ya upimaji wa utendaji kazi katika Utumishi wa Umma na kuongeza kuwa, utafiti huo unafanywa ili kubaini uhusiano uliopo kati ya utoaji wa motisha mbalimbali na utendaji wa kazi kwa lengo la kuwavutia na kuwabakisha watumishi wa Umma. 

Bibi Mwanilwa amefafanua kuwa, kwasasa hatua inayoendelea katika utafiti huo ni uchambuzi wa taarifa za utafiti huo, hivyo bodi inatarajia kuwasilisha taarifa hiyo serikalini ifikapo mwezi Februari, 2019.

Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma, Bw. Donald S.B. Ndagula amesema bodi yake inamtambua Dkt. Mwanjelwa kama mlezi, hivyo amemhakikishia kuwa, imepokea nasaha, ushauri na melekezo aliyoyatoa na ameahidi kusimamia utekelezaji wa maelekezo yote.

Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma imeanzishwa kwa mujibu wa Ibara ya 36 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na kuundwa kwa Hati ya Rais iliyotolewa kwenye Tangazo la Serikali Na. 162 la tarehe 3 Juni, 2011.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na Watumishi na wajumbe wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma (hawapo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi alipowatembelea  ofisini kwao makao makuu ya bodi jijini Dar es Salaam  kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.
 Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma, Bibi Mariam G. Mwanilwa, akieleza  majukumu ya Bodi kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa kikao kazi na Naibu Waziri huyo na watumishi  na Wajumbe wa Bodi ya Mishahara na Masilahi  katika  Utumishi wa Umma cha kuhimiza uwajibikaji  kilichofanyika Makao Makuu ya bodi hiyo jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma, Bw. Donald S.B. Ndagula akifafanua majukumu ya bodi yake kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa kikao kazi na Naibu Waziri huyo na watumishi  na Wajumbe wa Bodi ya Mishahara na Masilahi  katika  Utumishi wa Umma cha kuhimiza uwajibikaji  kilichofanyika Makao Makuu ya bodi hiyo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya watumishi wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa kikao kazi na Naibu Waziri huyo na watumishi na Wajumbe wa Bodi ya Mishahara na Masilahi  katika  Utumishi wa Umma cha kuhimiza uwajibikaji  kilichofanyika Makao Makuu ya bodi hiyo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe na watumishi wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma mara baada ya kumalizika kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi na Wajumbe wa Bodi hiyo ya Mishahara na Masilahi  katika  Utumishi wa Umma cha kuhimiza uwajibikaji  kilichofanyika Makao Makuu ya bodi hiyo jijini Dar es Salaam.

RAIS DKT. MAGUFULI ASITISHA ZOEZI LA KUONDOA VIJIJI NA VITONGOJI VILIVYOPO NDANI YA MAENEO YA HIFADHI

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamis Kigwangala, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt.John Kijazi,Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega,Katibu Mkuu TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamuhanga pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Doroth Mwanyika  kuhusu kusitisha zoezi la kuwaondoa Wananchi wanaoishi katika Vijiji na Vitongoji vilivyopo katika maeneo ya Hifadhi. Ikulu Jijini Dar es salaam leo Januari 15, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahi jambo na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamis Kigwangala, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt.John Kijazi,Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega,Katibu Mkuu TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamuhanga pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Doroth Mwanyika  mara baada ya kumaliza mazungumzo na viongozi hao  kuhusu kusitisha zoezi la kuwaondoa Wananchi wanaoishi katika Vijiji na Vitongoji vilivyopo katika maeneo ya Hifadhi. Ikulu Jijini Dar es salaam leo Januari 15, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamis Kigwangala, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt.John Kijazi, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega, Katibu Mkuu TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamuhanga pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Doroth Mwanyika  mara baada ya kumaliza mazungumzo na viongozi hao  kuhusu kusitisha zoezi la kuwaondoa Wananchi wanaoishi katika Vijiji na Vitongoji vilivyopo katika Maeneo ya Hifadhi za Taifa. Ikulu Jijini Dar es salaam leo Januari 15, 2019. PICHA NA IKULU.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza kusitishwa mara moja kwa zoezi la kuviondoa vijiji na vitongoji vinavyodaiwa kuwepo katika maeneo ya hifadhi na amewataka viongozi wa wizara zote zinazohusika kukutana ili kubainisha na kuanza mchakato wa kurasimisha maeneo ya vijiji na vitongoji hivyo.

Mhe. Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo tarehe 15 Januari, 2019 Ikulu Jijini Dar es Salaam alipokutana na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamis Kigwangallah, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi John Kijazi, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhandisi Joseph Nyamhanga na Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Bi. Dorothy Mwanyika. 

Pamoja na agizo hilo Mhe. Rais Magufuli ametaka viongozi wa wizara husika kubainisha maeneo ya hifadhi za wanyamapori na misitu ambayo hayana wanyamapori ama misitu ili yagawiwe kwa wafugaji na wakulima ambao kwa sasa wanataabika kupata maeneo ya kufugia wanyama na kuzalisha mazao.

Mhe. Rais Magufuli pia ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kuangalia upya zoezi la uwekaji wa mipaka ya hifadhi na makazi, na kutumia busara katika uwekaji wa mawe ya mipaka hiyo ili kutowaondoa wananchi katika maeneo ambayo hayana ulazima wa kuwaondoa.

“Mimi sifurahii kuona wafugaji kila mahali wanafukuzwa, kama kuna eneo ambalo tunafikiri lilikuwa hifadhi ya wanyama lakini halitumiki, tutabadilisha sheria, tunalimega na tunaligawa kwa wafugaji, vivyo hivyo hata kwa wakulima kama kuna eneo tunaona ni hifadhi lakini halina msitu wala wanyamapori, na lina rutuba, na wakulima wanataka kulima nalo tunalimega tunawapa wakulima.

Baadaye tutajua kabisa eneo hili ni la hifadhi, hili ni la mifugo, hili ni la wakulima, hili ni la makazi. Kwa hiyo nyinyi Mawaziri na Makatibu Wakuu mkakae mkatangulize maslahi ya hawa tunaowaongoza ambao ni wakulima, wafugaji, wavuvi nakadhalika, lakini pia tunahitaji wanyamapori, sijasema sasa hifadhi zote za wanyama tunazimaliza, hapana, hifadhi za wanyama lazima tuzihifadhi” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.

Mhe. Rais Magufuli ameagiza vijiji vyote 366 vilivyoainishwa kuwepo ndani ya maeneo ya hifadhi hapa nchini visiondolewe katika maeneo hayo na badala yake ametoa mwezi mmoja kwa viongozi wa wizara zote zinazohusika kubainisha maeneo ya vijiji hivyo na kuanzisha mchakato wa mabadiliko ya sheria ili yawasilishwe katika kikao kijacho cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Amefafanua kuwa ni lazima Serikali ifanye maamuzi haya sasa kwa kuwa idadi ya Watanzania imeongezeka hadi kufikia Milioni 55, idadi ya mifugo imeongeza hadi kufikia Milioni 35 na hivyo kuna ongezeko kubwa la mahitaji ya maeneo ya ardhi ikilinganishwa na wakati nchi inapata uhuru ambapo Watanzania walikuwa Milioni 9 na mifugo ilikuwa Milioni 10.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli ameagiza sheria ya vyanzo vya maji pia iangaliwe upya ili kutowazuia Watanzania wanaozalisha mazao kandokando mwa mito na ameelezea kutofurahishwa kwake na vitendo vya kufyeka mazao ya wakulima kwa madai kuwa wamelima ndani ya mita 60.

Halikadhalika Mhe. Rais Magufuli ameipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kuwasilisha kwake mapendekezo ya kufutwa kwa mashamba ambayo hayajaendelezwa na ameagiza wizara hiyo iendelee kumpelekea mapendekezo ya mashamba yote yaliyotelekezwa ili ayafute na wananchi wagawiwe kwa ajili ya kuyatumia kwa uzalishaji wa mazao na mifugo.

Hata hivyo Mhe. Rais Magufuli amesema maagizo hayo hayana maana kuwa sasa wananchi waruhusiwe kuvamia maeneo ya hifadhi, na ametaka zoezi la uwekaji wa mipaka lifanyike haraka na kwa uwazi.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
15 Januari, 2019 

BOT YATANGAZA KUHAMISHA MALI NA MADENI YA BENKI M KWENDA BENKI YA AZANIA

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

BENKI Kuu ya Tanzania(BoT) imetangaza kukamilisha mchakato wa ufumbuzi wa madeni ya iliyokuwa Benki M ambayo ilikuwa inakabiliwa na ukwasi na hivyo kuihamishia katika Benki ya Azania Limited.

Akizungumza leo Januari 15,2019 jijini Dar e Salaam Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dk.Bernard Kibesse amesema kuwa BoT kwa mujibu wa  mamlaka iliyopewa chini ya kifungu cha 59(4)cha sheria ya mabenki na tasisi za fedha ya mwaka 2006 mchakato wa kupata ufumbuzi wa matatizo ya Bank M umekamilika na madeni kwa madeni yake kuchukuliwa na benki 
nyingine kama njia ya ufumbuzi wa matatizo.

"Hivyo kwa mamlaka iliyopewa chini ya kifungu cha 58(20)(h) cha sheria ya Mabenki na Tasisi za fedha ya mwaka 2006 ,benki kuu imeamua kuhamisha kwa mujibu wa sheria (aquisition by Operation of the law) mali na madeni yote ya bank M kwenda Azania Bank Limited,"amesema Dk.Kibesse.
 
Ameongeza kuwa kwa sasa Benki kuu,Azania Bank Limited na wadau wengine 
wanaendelea kuandaa taratibu za kisheria za kukamilisha mchakato wa uhamishaji wa mali na madeni ya Bank M kwenda Azania Bank Limited.

Pia wateja wenye Amana na wadai wengine wa Bank M watataarifiwa tarehe ya kuanza kupata huduma za kibenki kupitia Azania Bank Limited.Kwa wateja wenye mikopo amesema wanatakiwa kuendelea kulipa mikopo yao kulingana na mikataba yao huku akisisitiza kuwa Benki Kuu inawaakikishia kuwa Azania Bank Limited itakuwa na Mtaji na Ukwasi wa kutosha katika kuwahudumia wateja wake na wateja wapya kutoka Bank M baada ya kuchukua mali na madeni ya benki hiyo, hivyo Azania Bank inatarajiwa kuwa na mtaji wa Sh.bilioni 164.

Alipoulizwa jitihada gani zimefanywa na Benki Kuu ili kuinusuru Benki M , Dk.Kibesse amesema kuna hatua mbalimbali ambazo zilifanyika ikiwa pamoja na kufanya vikao vya mara kwa mara kati yao na benki hiyo lakini kutokana na kutokuwa na mtaji wa fedha wameamua kuhamisha mali na 
madeni yake Benki ya AZania.

Hata hivyo amefafanua kuwa Benk M haikuwa imefikia pointi ya ukwasi huku akisisitiza kuwa kilichofanya Benki Kuu kuiweka Benk M chini ya usimamizi wake na kisha kuamua kuhamisha mali na madeni Benki ya Azania imetokana na tatizo kubwa la ukwasi.

Kuhusu deni lililokuwa Benki M, Dk.Kibesse amesema kulikuwa na deni ya Sh.bilioni 618 na kwa mazingira hayo ilikuwa vigumu kwa walioweka fedha kutaka kuchukua fedha na hivyo Benki Kuu moja ya jukumu lake ni kuhakikisha inaangalia hali hiyo kwa kuhakikisha wateja wanalindwa.

"Ndio maana tumesema Mkurugenzi Benki ya Azania atakapokuwa amekamilisha tararibu zote za kisheria, mteja ambaye alikuwa anataka huduma atakwenda na atahudumiwa na ile fedha ya ada ambayo mhusika alikuwa ameikosa ataipata,"amesema Dk.Kibesse  
 Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania ,Dk .Bernard Kibesse akizungumza na Waandishi wa Habari Juu ya hatua zilizochukuliwa na Benki Kuu kuhamisha amana zote za Benki M na Madeni yake kwenda Benki ya Azania.
 Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania ,Dk .Bernard Kibesse akizungumza na Waandishi wa Habari Juu ya hatua zilizochukuliwa na Benki Kuu kuhamisha amana zote za Benki M na Madeni yake kwenda Benki ya Azania.
 Mkurugenzi wa Benki ya Azania Katikati Mwenye Tai Nyekundu akiwa na wadau wengine wa Masuala ya Kibenki waliohudhuria Mkutano wa BOT na Waandishi wa Habari
 Mwandishi wa Habari Kutoka Gazeti la Nipashe, Beatrice Moses akiuliza Swali kwa Gavana juu ya Mchakato wa kuhamishwa kwa benki hiyo.
Sehemu ya Waandishi wa Habari walioshiriki Mkutano huo ulikuwa ukitangaza maamuzi ya kuhamisha Benki Mkwenda Azania Bank.

RAIS DKT. MAGUFULI ASHUHUDIA UTIWAJI SAINI MAKUBALIANO KATI YA SERIKALI NA AIRTEL

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabud na Mwenyekiti wa kampuni ya Bharti Airtel  Bw. Sunil Mittal  wakitia saini makubaliano mapya ya ubia kati ya serikali itayokuwa na asilimia 49 na Airtel  na asilimia 51 kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 15, 2019. Katikati ni Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mwenyekiti wa kampuni ya Bharti Airtel  Bw. Sunnil Mittal baada ya kutiwa saini kwa makubaliano mapya ya ubia kati ya serikali itayokuwa na asilimia 49 na Airteml asilimia 51 kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 15, 2019. Katikati ni Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi
 DONE DEAL: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabud akipeana mikono na Mwenyekiti wa kampuni ya Bharti Airtel  Bw. Sunnil Mittal baada ya kutiwa saini kwa makubaliano mapya ya ubia kati ya  serikali itayokuwa na asilimia 49 na Airtel asilimia 51 kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 15, 2019. Katikati ni Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mwenyekiti wa kampuni ya Bharti Airtel  Bw. Sunil Mittal baada ya kushuhudia zoezi la kutiwa saini kwa makubaliano mapya ya ubia kati ya serikali itayokuwa na asilimia 49 na Airtel na asilimia 51 kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 15, 2019. Katikati ni Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Bw. Sunil Colaso baada ya makubaliano mapya ya ubia kati ya serikali itayokuwa na asilimia 49 na Airtel yenye asilimia 51 kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 15, 2019. Katikati ni Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza  Mwenyekiti wa kampuni ya Bharti Airtel  Bw. Sunil Mittal baada ya kushuhudia zoezi la kutiwa saini kwa makubaliano mapya ya ubia kati ya serikali itayokuwa na asilimia 49 na Airtel na asilimia 51 kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 15, 2019. Katikati ni Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi aliyeongoza timu ya Serikali katika mazungumzo na kampuni ya Bharti Airtel katika kufikia makubaliano mapya ya ubia kati ya serikali itayokuwa na asilimia 49 na kampuni hiyo asilimia 51 kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 15, 2019. Wengine ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Katibu Mkuu wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James, Mwenyekiti wa Bharti Airtel Bw. Sunnil Mittal na ujumbe wake pamoja na ujumbe wa serikali.
  FURAHA YA MAKUBALIANO MUAFAKA: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na  Mwenyekiti wa kampuni ya Bharti Airtel  Bw. Sunnil Mittal na ujumbe wake pamoja na ujumbe wa serikali baada ya kupata picha ya pamoja ya kumbukumbu ya kutiwa saini kwa makubaliano mapya ya ubia kati ya serikali itayokuwa na asilimia 49 na Airteml asilimia 51 kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 15, 2019. Katikati ni Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi

PICHA NA IKULU

ABBAS TARIMBA AZIONYA SIMBA NA YANGA, AZITAKA KUACHA MZAHA KATIKA MICHUANO YA SPORTPESA

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MKURUGENZI wa Uendeshaji wa SportPesa nchini Tanzania Tarimba Abbas amezionya timu za Tanzania hasa timu za Simba na Yanga kwa kuzitaka kuacha mzaha kwa mwaka huu katika michuano ya Kombe la SportPesa.

Tarimba amesema hayo leo Januari 15,2019 wakati anazungumzia mashindano hayo ambayo yanatarajia kuanza Januari 22 hadi Januari 27 mwaka huu na kwamba vigogo wa timu nane kutoka Tanzania na Kenya
watashiriki.Katika kuhakikisha michuano hiyo inapewa nafasi ya kuangaliwa na mashabiki wengi wa soka SportPesa imeamua kushirikiana na SuperSport kuonesha michuano hiyo.

Akizungumzia michuano hiyo Tarimba amesema kutokana na timu za Tanzania kushindwa kufanya vema, waliamua kufanya kikao na viongozi wa timu za Tanzania na waliochowaambia ni kwamba mwaka huu SportPesa hawataki mzaha kabisa.

"Safari hii tumeshirikiana na SuperSort kuonesha michuano ya SportPesa ambayo itashirikisha timu nane kutoka Tanzania na Kenya.Hii ni mara ya tatu kufanyika kwa michuano hii na mwaka jana timu ya Golmahia walienda kucheza Uingereza.

"Kutokana na hali hiyo tulilazimika kufanya kikao kizito na viongozi wa timu za Simba na Yanga, na kikubwa ambacho tunakisema kwamba mwaka huu hatutaki mzaha.Timu hizo hatutarajii kuona wanapeleke wachezaji wa daraja la pili.Na tunaomba wasifanye kama ambavyo wamefanya kwenye michuano ya Mapinduzi kwa kupeleka wachezaji ambao hawapewi nafasi ya kutosha kwenye mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara," amesema Tarimba.

Amefafanua lengo la mashindano ya SportPesa si kupata fedha nyingi bali kukuza viwango vya soka katika nchi mbalimbali na ndio maana wamekuwa wakidhamini timu kubwa katika ligi mbalimbali duniani ikiwemo Ligi Kuu nchini Uingereza na hivyo hawataki kuona vilabu vya Tanzania vinafanya mzaha.

Tarimba amesema kwake yeye mashindano hayo ni sehemu ya kuonesha vipaji vya wachezaji na hivyo wanaimani timu ya Simba na Yanga ambayo inaongoza Ligi Kuu Tanzania Bara kufanya vema.Amefafanua mashindano hayo yamo kwenye kalenda ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) pamoja na Shirikisho la Mpira la Mpira wa Miguu nchini Kenya.Pia amesema hata CAF inatambua na kwamba hata kusimama kwa Ligi Kuu inatokana na mashindano ya sportPesa.

Alipoulizwa kuhusu uhakika wa timu za Simba na Yanga kama kweli wataleta wachezaji hao wenye uwezo ,amejibu wameingia nao mkataba na makubaliano ,hivyo wanauhakika watashiriki vema."Kwa kutambua umuhimu wa michuano hii ndio maana tunasisitiza hatutaki mzaha,na hata uamuzi wa kushirikiana na SuperSport kuonesha michuano hii ni kutokana na kutambua umuhimu wake.Hivyo ni kuziambia timu zetu.ziache mzaha na tunaomba Yanga au Simba iwe bingwa ili acheze na timu ya Evarton ya nchini Uingereza," amefafanua Tarimba.

Ameongeza anatambua uwezo mkubwa wa timu za Simba na Yanga na viwango vya wachezaji wao, hivyo ni wakati muafaka wa kuhakikisha wanaonesha ubora wao kwenye michuano hiyo ambayo ni mikubwa ambayo ilianza mwaka 2017 katika michuano iliyofanyika nchini Tanzania ambapo mshindi Gor Mahia ilicheza na Everton hapa hapa nchini.

Asema msimu wa pili wa mashindano hayo yalifanyika huko Nakuru nchini Kenya mwaka jana na mshindi kwa mara ya pili Gor Mahia alikwenda kucheza na Everton huko Liverpool nchini Uingereza Novemba.Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoise Tanzania Jacqueline Woiso amesema kwa kuwa mshirika rasmi ,SuperSport imepata idhini ya kuonesha michuano hiyo mubashara kupitia DStv.

"Tunafurahi kuujulisha umma wa Watanzania kuwa hamu yao ya kushuhudia michuano hii mubashara kupitia DStv sasa imepata jibu,watashuhudia burudani hii ya aina yake tena kuanzia kifurushi cha chini kabisa cha Bombs,amesema Woiso na kwamba michezo yote itaonekana kupitia DStv
SuperSport 9 ambayo inapatikana katika vifurushi vyote."Tumeamua kufanya hivyo ili kuwapa Watanzania fursa ya kushuhudia mashindano haya ambayo yanazidi kujipatia umaarufu kila uchao,"amefafanua Woiso.

WAZIRI LUGOLA AWAONGOZA WATENDAJI WAKUU WA WIZARA YAKE KIKAO CHA KAMATI YA BUNGE YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA, JIJINI DODOMA LEO

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akiweka sawa taarifa zake kabla ya kuziwasilisha katika Kikao cha Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, katika Ukumbi wa Mikutano wa Bunge, jijini Dodoma leo. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati), akisoma Taarifa ya Wizara yake kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, katika Ukumbi wa Mikutano wa Bunge, jijini Dodoma leo. Wapili kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati), akisoma Taarifa ya Wizara yake kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, katika Ukumbi wa Mikutano wa Bunge, jijini Dodoma leo. Wapili kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati), akisoma Taarifa ya Wizara yake kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, katika Ukumbi wa Mikutano wa Bunge, jijini Dodoma leo. Wapili kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu (kulia), akimwelekeza jambo Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, (CGP) Phaustine Kasike, kabla ya Kikao cha Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, hakijaanza, katika Ukumbi wa Mikutano wa Bunge, jijini Dodoma leo

WAFANYAZI WAWILI KAMPUNI YA AIRTEL, WENGINE TISA WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA KUINGILIA MIFUMO YA MAWASILIANO

$
0
0

Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii

WAFANYAKAZI wawili wa Kampuni ya Simu ya Airtel na wengine tisa, leo January 15, 2019 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kujibu mashtaka saba yakiwemo kuingilia mifumo ya mawasiliano ya Airtel.

Akisoma hati ya mashtaka Wakili wa Serikali Ester Martin akisaidiana na Erick Shija amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Kelvin Mhina, amewataja washtakiwa hao kuwa ni Erick Fidelisi, Zephaniah Maduhu, Anthony Masaki, Lumuli Stanford, Ndeshiwonasiya Malle, Davis Waseda, Goodluck Nyakira, Michael Onyango, Sylvester Onyango, Rodgers Laizer na Nancy Mwenda.

Katika kosa la kwanza imedaiwa, kati ya Septemba 9 na Desemba 24 mwaka 2018 ndani ya Jiji na Mkoa wa Dar es Salaam washtakiwa kwa pamoja walikula njama ya kutenda kosa la wizi. Shtaka la pili imedaiwa siku na mahali hapo, washtakiwa hao huku wakijuwa kuwa ni kinyume cha sheria walijaribu kutenda kosa la wizi.

Pia imedaiwa mahakamani hapo kuwa katika shtaka la tatu, washtakiwa Laizer na Mwenda kwa makusudi na kinyume cha sheria walisababisha Kuingilia mfumo wa mawasiliano wa Kampuni ya simu ya Airtel bila ya kuwa na kibali. Aidha katika shtaka la nne imedaiwa washtakiwa wote, wanadaiwa kutoa taarifa za mfumo wa mawasiliano kinyume cha sheria.

Imedaiwa kuwa washtakiwa Laizer na Mwenda wanadaiwa kutoa taarifa ya mfumo wa mawasiliano ya kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel kwa watu ambao hawahusiki na kampuni hiyo kinyume cha sheria.Katika shtaka la sita imedaiwa pia, siku na mahali hapo washtakiwa hao waliingilia ufanyakazi wa
mfumo wa mawasiliano wa kampuni ya simu ya Airtel bila ya kuwa na idhini.

Wakati katika shtaka la saba, imedaiwa washtakiwa walipokea taarifa kupitia kompyuta bila idhini ya kampuni ya Airtel.Hata hivyo washtakiwa Wamekana kutenda makosa hayo na washtakiwa Masaki, Stanford, Waseda na Mwenda walifanikiwa kupata dhamana huku wengine wakirudishwa rumande kwa
kushindwa kutimiza masharti ya dhamana. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Januari 29 kwa ajili ya kutajwa upelelezi bado haujakamilika.
 WAFANYAKAZI wawili wa Kampuni ya Simu ya Airtel na wengine tisa, leo January 15, 2019 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kujibu mashtaka saba yakiwemo kuingilia mifumo ya mawasiliano ya Airtel.
 

HOTELI YA KIFAHARI YASHAMBULIWA KENYA, HOFU YATANDA KWA WANANCHI KILA KONA

$
0
0
Na Ripota Wetu

INASIKITISHA !Hivyo ndivyo unavyoweza kuelezea tukio la kushambuliwa kwa Hoteli ya kifahari ya DusitD2 nchini Kenya.

Tukio la kushambuliwa kwa hoteli hiyo iliyopo eneo la 14 Riverside Nairobi nchini Kenya limetokea leo Januari 15,2019.Shambulio hilo limeibua hofu na taharuki kwa wananchi walio wengi.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wamedai kuwa wakati wa shambulio ilisikika milipuko na milio ya risasi katika eneo la hoteli hiyo na kwamba kuna milio mikubwa miwili isikika kwa kishindo kikubwa.

Kutokana na shambulio hilo la mlipuko inaelezwa watu kadha wamejeruhiwa ambapo maofisa wa Shirika la Msalaba Mwekundu waliamua kutoa msaada kwa kushirikiana na watu wengine waliokuwa eneo hilo baada ya kutokea kwa tukio hilo.

Mwandishi wa BBC ambaye yupo eneo la tukio muda mfupi baada ya tukio hilo kutokea mchana wa saa saba, Fredinand Omondi anaripoti kupitia mtandao wake wa Twitter kuwa kikosi maalumu cha Recce squad kimewasili eneo la tukio ili kuongeza nguvu ya uokozi wa raia na kupambana na wavamizi.

Pia Omondi pia anaripoti kuwa moja ya maofisa usalama waliopo eneo la tukio amemwambia "hali sio nzuri".Hata hivyo Jeshi la Polisi nchini Kenya linaelezwa kuwa limeimarisha ulinzi eneo hilo huku wakiamua kuweka katazo la watu na magari kupita eneo ambalo limeshambuliwa.
 

Asiyetaka kuchukua kitambulisho cha ujasiliamali asubiri kubughudhiwa- RC Wangabo.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh.Joachim Wangabo amewataka wajasiliamali wote mkoani humo kujitokeza kupatiwa vitambulisho vya ijasiliamali vilivyotolewa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa mikoa na wilaya zote nchini ili kuwaepusha wajasiliamali hao na bughudha wanazozipata katika kuendesha biashara zao za kila siku.

Amesema kuwa kila halmashauri kati ya halmashauri nne za mkoa wa Rukwa ilipatiwa vitambulisho 6,250 katikati ya mwezi Disemba mwaka 2018 lakini hadi kufikia leo katikati ya mwezi wa kwanza vitambulisho vilivyogawiwa havizidi 150 kwa mkoa mzima hali iliyopelekea Mh. Wangabo kuahirisha ziara ya siku nne aliyopanga kuifanya katika halmashauri ya Wilaya ya Kalambo ili kujionea miradi mbalimbali ya maendeleo.

“Nawataka waende katika halmashauri zote haraka i

wezekanavyo vinginevyo watakosa hii nafasi ya kuapata vitambulisho na kitakachofuata kinaweza kisiwe kizuri kwa wajasiliamali, kwasababu hiki ni kitambulisho ndicho kinachomfanya mjasiliamali huyu mdogo atambulike na asibughudhiwe kama mheshimiwa rais alivyosema, sasa usipopata kitambulisho maana yake ni kinyume chake ndicho kitakachokuja, unapata kitambulisho ili usibughudhiwe, lakini wewe hujapata kitambulisho inamaana utabughudhiwa, mimi nisingependa wajasiliamali wapate bughudha,” Alibainisha.

Ameyasema hayo baada ya kupata taarifa ya Wilaya ya Kalambo juu ya miradi mbalimbali ya kimaendeleo, mapokezi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza, ukusanyaji wa mapato na matumizi ya halmashauri, ugawaji wa vitambulisho hivyo pamoja na hali ya kilimo ya Wilaya kabla ya kutaka kuanza ziara yake katika wilaya hiyo.

Aidha amesisitiza kuwa tathmini ya ugawaji wa vitambulisho hivyo itafanyika baada ya siku kumi tangu leo tarehe 15.1.2019 hadi tarehe 25.1.2019 ili kuona muitikio wa wajasiliamali hao kwa halmashauri zote na kuwaagiza wakurugenzi wa halmashauri hizo kuhakikisha wanaongeza kasi ya kuwasajili na kuwakabidhi wajasiliamali hao vitambulisho vyao bila ya bughudha yoyote.

Wakati akiwasilisha taarifa ya wilaya, katibu tawala wa wilaya ya Kalambo Frank Sichalwe alisema kuwa tangu kufanyika kwa uzinduzi wa ugawaji wa vitambulisho hivyo mwanzoni mwa mwaka huu ni wajasiliamali kumi tu ndio waliopatiwa vitambulisho hivyo pamoja na kuendelea na hamasa ya kuwatambua wajasiliamali wengine.

“Zoezi la hamasa na ugawaji wa vitambulisho linaendelea ili vitambulisho vingi zaidi viweze kutolewa na kuwanufaisha wajasiliamali katika sekta isiyorasmi kama mheshimiwa Rais alivyokusudia, mpaka sasa Ulumi tumepata wajasiliamali 80, Mwimbi 30, Kasanga 30, Mwazye 20 na Matai wamejitokeza wajasiliamali zaidi ya 100 mpaka sasa,” Alisema.

Vitambulisho vya ujasiliamali viligagiwa kwa wakuu wote wa mikoa 26 mwanzoni mwa mwezi Disema mwaka 2018 na kila mkoa kupata vitambulisho 25,000 ili kuweza kuvigawa kwa wakuu wa wilaya na hatimae kufika mikononi mwa wakurugenzi ili kuwapatia wahusika wa vitambulisho hivyo kwa lengo la kupunguza bughudha kwa wajasiliamali wataopata vitambulisho hivyo vyenye gharama ya shilingi 20,000 kwa kila kitambulisho.

RPC WANKYO AWAKOMALIA TRAFIK WAOMBA RUSHWA PWANI

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, PWANI 

ASKARI wa usalama barabarani mkoa wa Pwani, wametakiwa kufanya kazi zao kwa weledi na kuacha kuomba na kupokea rushwa.

Hayo yalisemwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Kamishina msaidizi Mwandamizi Wankyo Nyigesa ,wakati akizungumza na askari wa kikosi cha barabarani mkoa wa Pwani katika ukumbi wa Polisi Maisha plus Kibaha.

Alieleza yamekuwepo malalamiko kwa baadhi ya askari wa usalama barabarani kujihusisha na vitendo vya kuomba na kupokea rushwa jambo ambalo limekuwa likichafua taswira ya Jeshi la Polisi.

"Katika kipindi cha uongozi wangu nitakuwa mkali na sitosita kuchukua hatua kwa askari yoyote atakayebainika kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa madereva"alisisitiza.

Aidha Wankyo, aliwataka askari hao kuzingatia utoaji wa huduma bora kwa wateja wanaowahudumia kila siku na kuacha vitendo malumbano na majibu yasiyozingatia utu kwa wale wanaowahudumia katika barabara zetu.

Pia, aliwaasa ,madereva wanaoingia ndani ya mkoa wa Pwani kuzingatia sheria za usalama barabarani na wale watakaokaidi kutii sheria hizo watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Kamanda wa polisi Pwani,Wankyo Nyigesa akizungumza katika kikao cha kikazi na askari wa usalama barabarani .(picha na Mwamvua Mwinyi)

MAGAZETI YA LEO JUMATANO JANUARI 16,2019

Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images