Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live

TAARIF YA WITO KWA WADAU KUTOA MAONI KUHUSU MISWADA MITANO YA SHERIA

0
0


TPSC YATAKIWA KUTOA MAFUNZO YATAKAYOWAWEZESHA WATUMISHI WA UMMA KUBORESHA HUDUMA KWA WANANCHI

0
0









Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) (hawapo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi alipowatembelea ofisini kwao makao makuu ya TPSC jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.



Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC), Dkt. Henry Mambo, akieleza majukumu ya TPSC kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi wa TPSC cha kuhimiza uwajibikaji kilichofanyika Makao Makuu ya chuo hicho jijini Dar es Salaam.Mkuu wa Chuo na Mtendaji




Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akikagua daftari la mmoja wa wanachuo wa Chuo cha Utumishi alipowatembelea wanafunzi hao katika moja ya madarasa ya Kampasi ya Dar es Salaam. Dkt. Mwanjelwa ametumia fursa hiyo kuwaasa wanachuo hao kusoma kwa bidii ili wawe watumishi wa umma bora hapo baadae.



Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akijaribu kutumia mashine ya kupiga chapa (typewriter) inayotumiwa kutolea mafunzo kwa wanafunzi wa TPSC alipotembelea moja ya darasa katika Kampasi ya Dar es Salaam ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania jijini Dar es Salaam.



Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiwahimiza wanachuo wa TPSC waliopo maktaba kutumia vema maktaba hiyo ya chuo kujisomea ili kuongeza uelewa wa masomo wanayosoma, alipoitembelea maktaba hiyo iliyopo Chuo cha Utumishi Utumishi wa Umma Kampasi ya Dar es Salaam.

……………………………………………………………………………….

Watumishi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kila mmoja kwa nafasi yake wametakiwa kutoa mafunzo bora yenye kuzingatia weledi, yatakayowajengea uwezo wa kiutendaji watumishi wa umma wanaopata fursa ya kujiendeleza katika chuo hicho ili waweze kutoa huduma bora na kwa wakati kwa wananchi.

Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati akizungumza na watumishi wa TPSC makao makuu na Kampasi ya Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji, kufahamu majukumu ya TPSC na kujiridhisha na utendaji kazi wa chuo hicho.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amewahimiza watumishi wa TPSC kuwa wabunifu kwa kuboresha mitaala itakayowaandaa vema watumishi wa umma, sekta binafsi na wananchi wanaohitimu katika chuo hicho ili waweze kuwa na mchango katika maendeleo ya taifa.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa ameongeza kuwa, katika ulimwengu wa sasa jamii inabadilika, uchumi unabadilika na siasa zinabadilika pia, hivyo amewataka watumishi wa TPSC wabadilike ili utendaji wao uwe wenye kujali matokeo na wenye tija.

Aidha, Dkt. Mwanjelwa alipata fursa ya kutembelea madarasa ya Kampasi ya Dar es Salaam ili kujionea vitendea kazi na kuzungumza na wanachuo ambao walimueleza kuwa, wanaridhika na elimu inayotolewa hivyo watatumia elimu na ujuzi wanaoupata katika kulitumikia taifa.

Naye, Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC), Dkt. Henry Mambo amesema, TPSC ilianzishwa ili kusaidia zoezi la kujenga uwezo wa watumishi wa umma uwe wenye kujali matokeo katika kutoa huduma bora kwa umma na kuongeza kuwa, kwa sasa chuo kina matawi sita yaliyopo Dar es Salaam, Mtwara, Singida Tabora,Tanga na Mbeya.

Dkt. Mambo amefafanua kuwa, madhumuni makubwa ya kuanzisha chuo ilikuwa ni kuziba pengo lililokuwepo la kukosekana kwa chuo rasmi kinachoshughulikia mafunzo ya watumishi wa umma ili waendane na mabadiliko yaliyoletwa na maboresho katika utumishi wa umma na kuongeza kuwa lengo lingine lilikuwa ni kusaidia, kukuza na kuboresha stadi za wafanyakazi, kubadili mtazamo juu ya utendaji wa watumishi wa umma katika suala zima la utoaji huduma bora kwa umma unaolenga kukuza uchumi na kuondoa umaskini kupitia mafunzo ya muda mfupi na mrefu.

Dkt. Mambo ameainisha kuwa, tangu chuo kianzishwe mwaka 2000 kimeweza kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa watumishi 61,221 katika nyanja ya uongozi, menejimenti na utawala .Aidha, Dkt. Mambo amesema kuwa, chuo kimeruhusiwa kutoa mafunzo ya muda mfupi na mrefu kwa sekta nyingine ikiwemo sekta binafsi iwapo wana mahitaji ya kupata mafunzo ya kuwawezesha kuboresha utendaji kazi wao wa kila siku.

Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania ni Wakala wa Serikali iliyoanzishwa mwaka 2000 chini ya Sheria ya Wakala wa Serikali ya mwaka 1997. Kuanzishwa kwa Chuo cha Utumishi kunafuatia muungano wa Chuo cha Watumishi wa Serikali, Dar es Salaam (Civil Service Training Centre) na kilichokuwa Chuo cha Uhazili Tabora (Tabora Secretarial College). Chuo cha Utumishi wa Umma kipo chini ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala.

RAIS WA ZANZIBAR MHE.DK. SHEIN AHUDHURIA TAARAB YA KUADHIMISHA MIAKA 55 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KISWANI PEMBA

0
0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Waziri wa Vijana Michezo Utamaduni na Sanaa Mhe.Balozi Ali Karume, wakifuatilia moja ya nyimbo ya kikundi hicho “Wakezi na Wakulima ” iliokuwa ikiimbwa na Msanii. Makame Faki, wakati wa hafla hiyo iliofanyika Uwanja wa Kufurahishia Watoto Tibirinzi Pemba.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mwanachama wa CUF Mbunge Mstaaf Mussa Haji Kombo, baada ya kumaliza hafla ya Taraab rasmi ya kusherehekea Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar, iliofanyika katika Uwanja wa Kufurahishia Watoto Tiborinzi Chakechake Pemba.kushoto Mwenyekiti wa CUF Taifa Mhe. Profesa Ibrahim Lipumba, wakiagana baada ya kumalizika kwa Taarab, jana usiku.12-1-2019.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na Waziri wa Vijana Michezo Utamaduni na Sanaa Mhe. Balozi Ali Abeid Karume, baada ya kumalizika kwa hafla ya Taraab rasmin ya kuadhimisha Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar iliofanyika katika Uwanja wa Kufurahishia Watoto Tibirinzi Chakechake Pemba,kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa amesimama baada ya kuwasili katika Uwanja wa Kufurahishia Watoto Tibirinzi Chakechake Pemba, wakati ukipigwa Wimbo wa Taifa na Kikundi cha Taraab cha Taifa, kulia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi na kushoto Waziri wa Vijana Michezo,Utamaduni na Sanaa.Mhe. Balozi Ali Karum, wa mwisho Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee.
BAADHI ya Mawaziri Viongozi wa Vyama vya Siasa na Wananchi wakiwa wamesimama wakati wa kupigwa Wimbo wa Taifa kabla ya kuaza kwa hafla hiyo ya Taraab Rasmin ya kuadhimisha Miaka 55 ya Mapinduzi Zanzibar iliopigwa na Kikundi cha Taraab cha Taifa Zanzibar.
BAADHI ya Wananchi waliokuwa wakihudhuria hafla ya Taraab rasmin ya kusherehekea Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar, wakiwa katika Uwanja wa Kufurahishia Watoto Tibirinzi Pemba wakifuatilia hafla hiyo.(Picha Ikulu)
MSANII wa Kikundi cha Taifa cha Tarab Zanzibar Bi. Amina Abdallah, akiwa jukwaani akiimbo “Wimbo Umewashuka) wakati wa hafla hiyo ya musherehekea Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar, iliofanyika katika Uwanja wa Tibirinzi Pemba jana usiku.(Picha na Ikulu)

WAZIRI LUGOLA, MWAKILISHI UNHCR WAJADILIANA MASUALA YA WAKIMBIZI WALIOPO NCHINI, JIJINI DAR ES SALAAM LEO

0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akimfafanulia jambo Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Chansa Kapaya (kulia) wakati Mwakilishi huyo alipomtembelea Waziri huyo ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam leo, kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya kuwahudumia Wakimbizi nchini. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya wakimbizi wa Wizara hiyo, Harrison Mseke. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akimsikiliza Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Chansa Kapaya (kushoto) alipokua anamfafanulia wakati walipokuwa wanaagana mara baada ya kumaliza kikao chao cha kujadili masuala mbalimbali ya kuwahudumia Wakimbizi nchini. Kikao hicho kilifanyika katika ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam leo. Wapili kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi wa Wizara hiyo, Harrison Mseke, wapili kushoto ni Mwakilishi Msaidizi wa UNHCR, Zephania Amuiri. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akimuaga Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Chansa Kapaya, mara baada ya kumaliza kikao chao cha kujadili masuala mbalimbali ya kuwahudumia Wakimbizi nchini. Kikao hicho kilifanyika katika ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam leo. Wapili kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi wa Wizara hiyo, Harrison Mseke, na wapili kushoto ni Mwakilishi Msaidizi wa UNHCR, Zephania Amuiri. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Na Felix Mwagara, MOHA

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amekutana na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Chansa Kapaya, ofisi ndogo ya Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo, na kujadiliana masuala mbalimbali ya wakimbizi nchini.

Waziri Lugola pamoja na Mwakilishi huyo, pia walijadiliana masuala ya ushirikiano kati ya Serikali na Shirika hilo la Kimataifa kwa mujibu wa sheria zinazowaongoza.

Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika leo Jumapili, Lugola alisema Wizara yake haiwezi ikafanikiwa kikamilifu katika masuala ya kuwahudumia wakimbizi nchini kama haitashirikiana ipasavyo na UNHCR.

“Licha ya kuwa baadhi ya wakimbizi wanaendelea kurudishwa kwa hiari nchini kwao Burundi, lakini katika kufanikisha zoezi hili, lazima tushirikiane ipasavyo kati ya Serikali pamoja na nyie UNHCR, naamini Wizara yangu itafanya vikao nanyi mara kwa mara ili kufanikisha zoezi hilo pamoja na mengineo yanafanikiwa,” alisema Lugola.

Kwa upande wake Mwakilishi wa UNHCR, Kapaya, alisema Serikali ya Tanzania inashirikiana na Shirika lake vizuri, na jambo lolote la majadiliano linapotokea ujadiliana ili kuweka sawa ushirikiano huo. “Mheshimiwa Waziri mimi nakushukuru sana kwa kuniruhusu kuja kufanya mazungumza nawe, nimefarijika na haya madiliano na pia tutaendelea kushirikiana zaidi,” alisema Kapaya.

Katika kikao hicho Mwakilishi wa UNHCR aliambatana na Msaidizi wake Zephania Amuiri, na Waziri Lugola aliambatana na Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi wa Wizara yake, Harrison Mseke

WANANCHI WA WAZO KUUSAHAU MGAO WA MAJI- CEO LUHEMEJA

0
0
Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA) imewahakikishia wananchi wa Kata ya Wazo kupata maji kuanzia leo usiku.

Akizungumza mbele ya wananchi hao na Mkuu wa Wilaya Kinondoni Daniel Chongolo, Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kuwa kulikuwa na changamoto kidogo ila kwa sasa wananchi wote waliokuwa kwenye mtandao wa maji wa zamani wataanza kupata maji kuanzia saa 2 usiku.

Luhemeja amesema, mradi huu wa sasa una uwezo wa kuzalisha maji lita milioni sita kwa sasa tofauti na ule wa zamani uliokuwa na uwezo wa kuzalisha maji lita elfu sitini na kupelekea mgao wa maji kwenye maeneo mengi.

“Kuanzia sasa hivi hakutakuwa na mgao wa maji kwenye maeneo yote yaliyo na mtandao wa maji, mradi huu una uwezo wa kuzalisha maji lita milioni sita na hivyo tatizo la maji kwa Kata ya Wazo, Madale na maeneo mengine limekwisha,”amesema Luhemeja.

Akielezea maeneo ambayo hayajafika mradi kutokana na kutokuwepo kwa mtandao wa maji, Mhandisi Luhemeja amesema kuna fedha takribani Bilioni 115 zimeshapatikana kwa ajili ya kusambaza mabomba yenye urefu wa Kilometa zaidi ya 1000 katika maeneo yote ya Mkoa wa Dar es Salaam.

“Kuna fedha bilioni 115 zimeshatengwa tayari zipo kwenye mchakato wa manunuzi pia tunakaribia kusaini mkataba na mkandarasi ambaye tumeshampata na nitawakaribisha wenyeviti wote kuja kushuhudia ikiwemo na Wakuu wa Wilaya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,”amesema Luhemeja.

Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya Mh.Daniel Chongolo amesema katika serikali ya awamu ya tano chini ya Dkt John Pombe Magufuli miradi mingi imekuwa ikitekelezwa na wananchi wawe na subira na wameshaahidiwa maji kutoka kuanzia usiku wa leo.

Chongolo amesema, yeye binafsi anaamini kuwa Mtendaji Mkuu wa DAWASA sio mwanasiasa hawezi kudanganya kazi imefanyika na inaonekana ya kutoka uzalishaji wa maji lita elfu sita hadi milioni sita kwa lisaa.

Ameongezea na kusema, atakuja kufuatilia maji kama yanatoka siku ya kesho kutwa (Jumanne) na kujionea kwa machi yake.DAWASA wamedhamiria kufika asilimia 95 Ya upatikanaji wa maji kwa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani kufikia Desemba mwaka huu.


Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza mbele ya wananchi wa Tegeta Wazo na kuwahakikishia maji safi na salama kufikia leo usiku.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo akizungumza na wananchi wakati alipotembelea Tenki la maji la Wazo na kuwahakikishia Watapata maji kama walivyoahidiwa na Afisa Mtendaji wa DAWASA
Busta Pampu zilizofungwa kwenye tenki la maji la Wazo
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja wakati alipotembelea tenki la maji la Wazo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo (kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja wakati alipotembelea mradi wa tenki la maji la Tegeta Wazo lenye uwezo wa kuhifadhi maji Lita Milioni sita.

MAKAMU WA RAIS AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA OFISI YA MAKAMU WA RAIS IHUMWA DODOMA

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Ofisi ya Makamu wa Rais itakuwa ya mfano katika kutunza mazingira.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Makamu wa Rais Ihumwa, Dodoma.

“katika kupamba maofisi yetu kwa miti sisi ni watu wa mazingira kwetu kuwe mfano wengine wakipita waseme kaangalieni ofisi ya Makamu wa Rais kulivyo kwa hiyo miti yetu tuitunze na bustani zimwagiliwe” alisema Makamu wa Rais.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba amesema ofisi yake imejitahidi kwa kadri ya uwezo wake kutekeleza maelekezo waliyopewa pamoja na kupanda miti katika eneo hilo.

Wakati huo huo Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo alimueleza Makamu wa Rais kuwa Wizara zote zimepewa kiasi sawa cha pesa hivyo Makatibu wa Kuu walikaa na kukubaliana mchoro utakaotumika kama ofisi. Akitoa maelezo kwa Makamu wa Rais, Katibu Kamati ya Taifa ya Kuratibu Mpango wa Serikali Kuhamia Dodoma Bw. Meshach Bandawe alisema kuwa tangia uamuzi ulivyopitishwa na Serikali ujenzi ulianza mara moja kwa ofisi 21 pamoja na ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na taasisi zingine na Ofisi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na eneo linalojengwa ofisi hizo limeshalipiwa fidia, na umeme umeshasambazwa, kwa sasa majengo yanayojengwa ofisi za chini lakini kila kiwanja kina eneo la kujenga ghorofa.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo (kulia) mara baada ya kuwasili katika eneo linalojengwa Ofisi ya Makamu wa Rais Ihumwa Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Katibu Kamati ya Taifa ya Kuratibu Mpango wa Serikali kuhamia Dodoma Bw. Meshach Bandawe (kulia) mara baada ya kuwasili katika eneo linalojengwa Ofisi ya Makamu wa Rais Ihumwa Dodoma 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya kina juu ya maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Makamu wa Rais Ihumwa Dodoma kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (kushoto). (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
 Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira ukiendelea kwa kasi nzuri Ihumwa Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhandisi Joseph Malongo akielezea namna jengo la ofisi ya Makamu wa Rais litakavyokuwa mara baada ya ujenzi kukamilika katika eneo la Ihumwa, Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya kina juu ya maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Makamu wa Rais Ihumwa Dodoma kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (kushoto). (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua  maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Makamu wa Rais Ihumwa Dodoma akiwa pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (kushoto) na Katibu Mkuu wa ofisi hiyo Mhandisi Joseph Malongo
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua  maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Makamu wa Rais Ihumwa Dodoma akiwa pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (kushoto) na Katibu Mkuu wa ofisi hiyo Mhandisi Joseph Malongo 
 Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira ukiendelea kwa kasi nzuri Ihumwa Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipanda mti wa kumbukumbu  mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Makamu wa Rais Ihumwa Dodoma  (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
 akamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimwagilia maji mti wa kumbukumbu  mara baada ya kuupanda katika eneo ambalo  Ofisi ya Makamu wa Rais inajengwa Ihumwa Dodoma  (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira ukiendelea kwa kasi nzuri Ihumwa Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

Kampuni ya Halotel yatoa SHUKRANI kwa wateja wake mkoani Mwanza

0
0



Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Katika kusherehekea miaka mitatu tangu kuanza kutoa huduma zake hapa nchini, kampuni ya mawasiliano ya simu Halotel imefanya tamasha kubwa na la wazi liitwalo “Shukrani Music Concert” katika uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza.

Tamasha hilo limefanyika Januari 12, 2019 ambapo watumiaji wa mtandao wa Halotel walijipatia zawadi mbalimbali ikiwemo simu za mkononi. Aidha kampuni hiyo pia ilitoa mashuka 50 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwanza Sekou Toure na mengine 50 katika Kituo cha Afya Bwisya wilayani Ukerewe.

Makamu Mkurugenzi wa Halotel tawi la Mwanza linalojumuisha mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara, Francis Mafuru alisema kampuni hiyo iliyoanza kutoa huduma zake hapa nchini Oktoba 15, 2015 pia imetumia zaidi ya shilingi Milioni Sita kununua madawa na vifaa tiba kwa ajili ya Kituo cha Afya Bwisya pamoja na Hospitali ya Sekou Toure.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia) ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye tamasha hilo akimkabidhi mwakilishi wa Mgangwa Mfawidhi wa Kituo cha Afya Bwisya, Cosmas Wanzara (kushoto), mashuka yaliyotolewa na kampuni ya Halotel.
Tamasha hilo lilipambwa na burudani kali kutoka kwa msanii Mr. Blue a.k.a BlueByser.

WAZIRI LUGOLA AWASIMAMISHA KAZI VIGOGO WATANO SAKATA LA KUNASWA SARE ZA JESHI KAMBI ZA WAKIMBIZI MKOANI KIGOMA

0
0
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Kangi Lugola
 
 
*Aagiza wachunguzwe, atoa maagizo mazito kwa Katibu Mkuu Mambo ya Ndani

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii


WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Kangi Lugola amewasimamisha kazi vigogo watano wanaohusika na wakimbizi katika kambi ya Mtendele na Nduta mkoani Kigoma, baada ya kubainika uwepo wa sare za Jeshi zikiwa kwenye marobota ya nguo za misaada.

Akizungumza leo Januari 13,2019 , Waziri Lugola amesema kumebainika uwepo wa sare hizo kwenye marobota hayo ya nguo za misaada ambazo yalikuwa yanapelekwa katika kambi ya Wakimbizi Mtendeli na Kambi ya wakimbizi ya Nduta mkoani Kigoma.

Amefafanua katika kambi ya Mtendeli kumebainika kuwepo kwa sare za jeshi 1325 na katika kambi ya Nduta kumebainika uwepo wa sare 622 na hivyo kufanya jumla ya idadi ya sare zote kuwa 1947.

"Kwa Serikali hii inayoongozwa na Rais Dk.John Magufuli haiko tayari kuona tukio hilo linaachwa bila kuchukua hatua.Kama nguo hizo zimeweza kubainika maana yake kesho au kesho kutwa zinaweza kuingizwa silaha.Tulitarajia wahusika walitakiwa kubaini nguo hizo mapema kabla ya kuingia kwenye makambi hayo.

" Lazima tuhakikishe nchi yetu iko salama kwa kuhakikisha hakuna ambacho kinaingia nchini kwetu.Hivyo nimeamua kuchukua hatua za kuwasimamisha kazi baadhi ya watumishi wa kambi hizo za wakimbizi,"amesema Waziri Lugola wakati anazungumzia sare hizo.

Amewataja aliosimamishwa kazi ni Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa Wakimbizi Harson Mseke, Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma kwa Wakimbizi upande wa Menejimenti ya Makambi na Makazi, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Huduma kwa Wakimbizi anayeshughulikia Usalama na Operesheni.

Wengine ni Mkuu wa Kambi ya Wakimbizi Mtendeli John Mwita pamoja na Mkuu wa Kambi ya Wakimbizi Nduta Peter Bulugu .Pia amesema Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani anatakiwa kumchukulia hatua Mratibu wa Wakimbizi Mkoa wa Kigoma Tony Laiza.

Akizungumzia zaidi tukio hilo la kubainika kwa sare hizo ,Lugola amesema tayari amemuagiza Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ndani ya siku mbili kuanzia kesho kuunda tume kuchunguza sare hizo na kisha baada ya siku 10 awe amempa taarifa ya uchunguzi na uwe umekamilika.

"Nimemuagiza Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani kuunda timu maalum kuchunguza suala hili na ndani ya siku 10 awe amekamilisha ripoti na kunikabidhi,"amesema Lugola huku akifafanua uwepo wa sare hizo nchi ya Burundi inaweza kuwa na mawazo hasi kwa kudhani huenda Tanzania inawasaidia Wakimbizi kuunda jeshi jambo ambalo si kweli.

Waziri Lugola amefafanua kuwa siku za karibuni kulikuwa na mchakato wa kuwarudisha wakimbizi waliokubali kwa hiyari yao kurudi nchini Burundi na hivyo kubainika kwa sare hizo huweza kutafsiriwa kwamba walikuwa wanataka kuwapa sare hizo kwenda kufanya uasi.

" Lazima tuchukue hatua katika hili,nasubiri ripoti ya uchunguzi itakavyoeleza,"amesisitiza Waziri Lugola huku akiwataka WaTanzania kutoa taarifa zozote ambazo zitasaidia kuifanya nchi yetu kuwa salama .

Na kwamba hata kama kuna misaada inayotolewa na mashirika ya kimataifa kwa ajili ya Wakimbizi walioko nchini isiwe sababu ya kutumika kuingiza sare za jeshi au silaha.

Kamati ya ulinzi na usalama Mkoa wa Kigoma ikiteketeza jumla ya nguo 1947 zinazofanana na sare za jeshi zilizokamatwa kwenye kambi za wakimbizi za Mtendeli na Nduta Wilayani Kibondo hivi karibuni. Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Samson Anga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga alisema kuwa nguo hizo zinazofanana na sare za jeshi ziliingizwa kambini na Mkurugenzi wa shirika Danish refugees council kwa ajili ya kugawa kwa wakimbizi katika kambi ya Nduta na Mtendeli Wilayani Kibondo.

Kamati ya ulinzi na usalama Mkoa wa Kigoma ikishusha shehena ya nguo zipatazo 1947 zinazofanana na sare za jeshi zilizokamatwa kwenye kambi za wakimbizi za Mtendeli na Nduta Wilayani Kibondo,kwa ajili ya kuchomwa moto.

MTANZANIA, MOHAMED MANSOUR AENDELEA TENA KULIWAKILISHA NA KULITANGAZA VYEMA TAIFA ANGA ZA KIMATAIFA

0
0
 Mtanzania, Mohamed Mansour Nassor anaetokea Zanzibar ambae anafanya masomo kiwango cha juu ya PhD katika fani ya Uchumi ambae pia ndio Raisi wa Umoja wa Vijana na Wanafunzi wa Nchi zote za Afrika(ASSAFSTU) katika Chuo Kikuu kwa Jina maarufu la Patrice Lumumba(RUDN University) ametunukiwa tunzo kubwa ya Kimataifa kwa Kuhamasisha vijana wa nchi za Afrika nchini Urusi.


Na ujumbe wake ulisema kama ifuatavyo:


Leo tarehe 12/01/2019 kwa uwezo wa Mungu nimefikia tena kutambuliwa Kimataifa na najivuna tumeendelea tena kulitangaza vyema Taifa letu la Tanzania katika anga za Kimataifa. 
Kwa heshima kubwa kwangu na kwa nchi yetu, nimetunukiwa Tunzo ya kufanya vyema sana katika kuhamasisha vijana wa Afrika nchini Urusi katika masuala ya Taaluma(Elimu) na Maendeleo ya Jamii(Community Development) kupitia Shirika la vijana wa Kiafrika lisilo la Kiserikali(NGO) la Youth of Large Exploit(YOLE) katika hafla yao iliofanyika mjini Moscow.
Kwa uwezo wa Mungu, pamoja na tunzo huu ya leo tayari inakua ni kwa mara pili kutambuliwa Kimataifa kwa mwaka huu wa 2019 tangu uanze ambapo pia mwezi huu wa Januari nilichapishwa na kutambuliwa Kimataifa kama Mtanzania maarufu zaidi katika Watanzania waliowahi kusoma vyuo vya Sovieti ya Urusi na Urusi katika jarida la Kimataifa(Encyclopedia) la Wahitimu wote wa kigeni waliosoma nchini Urusi yani SOYUZ Alumni. 

Lakini si hivyo tu Tarehe 11 Mwezi Novemba 2018 nilifikia hatua kubwa katika masuala ya uongozi Kimataifa ambapo nilichaguliwa kuwa Raisi wa Vijana wote wa Nchi za Afrika katika Chuo Kikuu Cha Urafiki Cha Watu Wa Urusi au maarufu kama Chuo Kikuu Cha Patrice Lumumba ambapo nafasi hii ndio kwa mara ya Kwanza inshikwa na Mtanzania tangu kuanzishwa kwa Chuo hiki miaka ya 1960. 
Aidha licha ya hivyo bado, nimekua nikifanya kazi za uongozi kama Makamu Mwenyekiti wa Diaspora ya Watanzania nchini Urusi na nchi za CIS yani TADIRU na kama Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Kiswahili Cha Moscow(CHAKIMO) chini ya Ulezi wa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kwa Urusi,Mheshmiwa Simon Marco Mumwi. Namshukuru sana mheshimiwa Balozi wetu na Ubalozi kwa ujumla kwa mwongozo, nasaha, usahuri na kunipa dira na kunipa msaada mkubwa katika majukumu yangu na harakati zangu.
Nawashukuru sana viongozi wa shirika la YOLE na pia Chama chetu Cha SOYUZ Alumni Association of Tanzania walioniamini ili kuwawakilisha Kimataifa kama Balozi wao. 

Napenda pia kuwashukuru Watanzania wote wanaounga mkono juhudi zangu na harakati zangu na kwa dua zao njema kwangu hasa kwa maslahi mapana ya Taifa letu la Tanzania linaloongozwa na Raisi Makini kabisa, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli.
Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania!
Ahsante sana!  





MAGAZETI YA LEO JUMATATU JANUARI 14,2019

0
0



















MAWAZIRI WATANO WATEMBELEA MRADI WA KUFUA UMEME STIEGLER'S GORGE

0
0
Waziri wa Nishati, Medard Kalemani akizungumza na baadhi ya Mawaziri pamoja na Makatibu wakuu waliofanya ziara jana ya kutembelea mradi wa kufua umeme wa Mto Rufiji kwa ajili ya kukagua Miundombinu Wezeshi ikiwemo maji, barabara, umeme pamoja na nyumba za watumishi kabla ya kumkabidhi Mkandarasi huyo kwa ajili ya kuanza ujenzi wa bwawa la kuzalisha Umeme.
Waziri wa Nyumba, Ardhi na Maendeleo ya Mkazi, Mhe. William Lukuvi akiwa ameshika moya nguzo za umeme zilizotengenezwa kwa zege yenye urefu wa mita 17 ambazo zimewekwa katika Pori la Akiba la Selous ili wanyama kama vile tembo na twiga waziweze kuziangusha wakati Mawaziri watano walipofanya ziara katika mradi huo wa kufua umeme wa mto Rufiji mkoani Morogoro. Wengine wanaoangalia ni mawaziri na makatibu wakuu.
Mratibu wa Mradi wa Kufua Umeme wa Mto Rufiji, Mhandisi Justus Mtolela akizungumza na Mawaziri pamoja na viongozi mbalimbali walioambatana na katika Pori la Akiba la Selous kabla ya kuanza kufanya ziara ya kukagua Miundombinu Wezeshi katika mradi wa kufua umeme wa mto Rufiji.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe, Constantine Kanyasu akizungumza na Waziri wa Nyumba, Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi baada ya kukagua Nyumba za kuishi watumishi wanaokuja kufanya kazi katika mradi wa kufua umeme wa mto Rufiji wakati Mawaziri hao walipofanya ziara jana Mkoani Morogoro ya kukagua Miundombinu Wezeshi kwa ajili ya Mkandarasi kuanza kazi.
Mratibu wa Mradi wa Kufua Umeme wa Mto Rufiji, Mhandisi Justus Mtolela akitoa maelezo kwa Mawaziri pamoja na viongozi mbalimbali walioambatana nao katika Pori la Akiba la Selous wakati wakiangalia daraja amabalo linatakiwa kujengwa upya kutokana na daraja hilo kuwa na uwezo mdogo wa kuhimili mzigo mizito itakayoanza kusafirishwa na Mkandarasi kwa ajili ya ujenzi wa bwawa la kufua umeme wa mto Rufiji mkoani Morogoro.
Baadhi ya Mawaziri pamoja na viongozi wengine wakikagua Nyumba za kuishi watumishi watakaokuja kufanya kazi katika mradi wa kufua umeme wa mto Rufiji wakati wa ziara iliyofanyika katika Pori la Akiba la Selous mkoani Morogoro
Baadhi ya Mawaziri pamoja na viongozi wengine wakiangalia sehemu ya kujengwa Bwawa la kufua umeme katika mto Rufiji wakati Mawaziri hao walipofanya ziara jana katika Pori la Akiba la Selous Kanda ya Matambwe mkoani Morogoro
Eneo la Fuga ni sehemu ambayo mizigo itakuwa ikitelemshwa kwa njia ya reli itakayotumika kwa ajili ya ujenzi wa mradi kufua umeme katika mto Rufiji katika Pori la Akiba la Selous katika Kanda ya Matambwe mkoani Morogoro.(PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA)





NA.LUSUNGU HELELA-MOROGORO

Serikali imesema maandalizi ya miundombinu wezeshi kabla ya kumkabidhi Mkandarasi aliyepewa kazi katika Mradi wa kufua umeme wa Mto Rufiji tayari imekamilika kwa asilimia themanini.

Miundombinu hiyo ni pamoja na maji, umeme, barabara pamoja na nyumba za kukaa wafanyakazi.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mawaziri wa Wizara tano kutoka Nishati, Maliasili na Utalii, Nyumba, Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Fedha na Mipango baada ya kutembelea na kujionea miundombinu hiyo ambayo kwa kiasi kikubwa imeshakamilika.


Ziara hiyo katika Pori la Akiba la Selous kanda ya Matambwe mkoani Morogoro iliongozwa na Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani ikilenga kukagua hatua zilizofikiwa katika ujenzi wa miundombinu wezeshi ili kumuwezesha Mkandarasi kuanza kusafirisha mizigo kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo.

Alisema kukamilika kwa miundombinu hiyo kutamuwezesha Mkandarasi huyo kuanza maandalizi ya awali ikiwemo kuanza kusafirisha mizigo kuileta katika maeneo ya ujenzi wa bwawa.Aliongeza kuwa kutokana na Mkataba uliopo Mkandarasi huyo ataanza kazi rasmi Juni 15 mwaka huu na ataukamilisha mradi huo ifikapo mwezi April 2022. 

Katika upande wake Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu alitoa tahadhari kwa wafanyakazi wanaokuja kufanya kazi katika mradi huo wasiende kupumzika vichakani kuna wanyama wakali kama vile Simba, Nyati pamoja na tembo.

" Wale wenye tabia ya kujipumzisha vichakani baada ya kufanya kazi chonde chonde jiepusheni na haya mazoea la sivyo mtaliwa na Simba.Aidha, Mhe.Kanyasu alitumia fursa hiyo kuiomba Wizara ya Utumishi kutoa kibali cha kuajiri Askari Wanyamapori zaidi ya 200 ambao watatoa ulinzi kwa Wafanyakazi wa mradi huo,

Ombi hilo linakuja kufuatia Askari wanyamapori 115 kutoka mapori mengine kuhamishiwa kwa muda katika Pori hilo katika kanda ya Matambwe kwa lengo la kuongeza nguvu baada ya askari 115 waliokuwepo kuonekana hawatoshi.

Hata hivyo , Mhe.Kanyasu alisema hatua za haraka zimeanza kuchukuliwa ikiwa ni pamoja kutengeneza vyoo, malazi pamoja na maji kwa vile miundombinu iliyokuwepo katika Kanda hiyo ilikuwa na uwezo wa kuhudumia Askari Wanyamapori 85 tu lakini hadi hivi sasa kuna jumla ya askari 230.

Kukamilika kwa mradi huo wa kufua umeme, Bwawa hilo la Rufijin litakuwa la nne kwa ukubwa kwa Afrika na la kwanza kwa Afrika Mashariki, Duniani ni la 60 katika ya mabwawa sabini makubwa.

TFDA yaimarisha udhibiti wa bidhaa katika vituo vya forodha

0
0

NA WAMJW-ARUSHA

MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Kaskazini imeeleza kuwa, itaendelea kulinda soko la ndani la bidhaa  za vyakula ,dawa, vipodozi, vifaa tiba na vitendanishi kwa kuimarisha huduma kwenye mipaka yote nchini ikiwemo mpaka wa Namanga, Mkoani Arusha.

Udhibiti katika mipaka hiyo ni unalenga kuhakikisha kuwa bidhaa bora, salama na zenye ufanisi pekee ndiyo zinaingia nchini ili kulinda afya ya wananchi.

Hayo yamebainishwa  katika kituo cha TFDA kilichopo Mpaka wa Namanga mkoani hapa wakati wa Maafisa Uhusiano wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto pamoja na Taasisi zilizo chini ya wizara hiyo walipotembelea Kituo hicho cha ukaguzi ikiwa ni mwendelezo wa Kampeni ya ‘ Tumeboresha Sekta ya Afya’ inayolenga kueleza mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli.

Maafisa ukaguzi  wa Mpaka wa Namanga ambao unatenganisha nchi za Tanzania na Kenya  walieleza mikakati ya utoaji wa huduma za ukaguzi kutokana na Serikali kuwekeza rasimali watu pamoja vitendea kazi katika kurahisisha utoaji wa huduma katika Mpaka huo.

Kaimu Meneja  TFDA Kanda ya Kaskazini, Benny John amesema ofisi ya Kanda imeendelea kutekeleza majukumu yake mbalimbali ikiwemo udhibiti wa bidhaa za chakula, dawa vipodozi, vifaa Tiba na vitendanishi kwa kuhakikisha wafanyabiashara wanafuata kanuni  na sheria zilizowekwa katika kuhakikisha wanalinda maslahi mapana ya kulinda afya ya wananchi.

"Udhibiti wa bidhaa zinazoingia nchini umeongezeka kwa wafanyabiashara kulipa ada na tozo za Serikali na hivyo  kuongeza pato la Taifa" alisema Kaimu Meneja huyo.

Nae Mkaguzi wa Dawa wa TFDA Mpaka wa Namanga, Bw. Elia Nyeura amesema takwimu za uingizaji wa mizigo katika kituo cha Namanga  zimeongezeka kutoka  shehena  724 mwaka 2015/16 hadi kufikia 1,223 kwa mwaka  2016/2018.

"Kwa sera ya awamu ya tano ya kuwa  na Tanzania ya viwanda, bidhaa zinazodhibitiwa na TFDA na kuruhusiwa kwenda nje ya nchi  hususani zilizosindikwa kwa kipindi cha miaka mitatu zimeongezeka kutoka shehena 429 hadi kufikia 640 kwa 2017/18 " amesema Nyeura na kuongeza kuwa, mamlaka imepunguza upotevu wa mapato kutokana na bidhaa zisizofaa kwa kuimarisha ukaguzi". Alisema.

Hata hivyo  amebainisha kuwa thamani ya bidhaa zilizokamatwa kwa kuingizwa nchini bila kufuata utaratibu zimepungua kutoka  Milioni 630.3 hadi kufikia Milioni 24.7 kwa kipindi cha mwaka 2015 hadi 2018.

Aidha, maafisa Uhusiano hao wameweza kutembelea maeneo mbalimbali ya kituo hicho ikiwemo chumba maalum cha Maabara na kujionea namna bidhaa za dawa zinavyochunguzwa katika kuangalia ubora wake kabla hazijaingizwa  Nchini.

Mpaka wa Namanga ni moja ya mipaka ambayo tayari imeanza kufanya kazi kwa kufanya ukaguzi wa bidhaa kwa upande mmoja tu wa Nchi (One Stop Boder Post-OSBP) ambapo bidhaa inaingia na kukaguliwa kwa pamoja na wakaguzi wa nchi mbili (Tanzania na Kenya) ili kupunguza muda wa wadau kukaa mpakani kwa muda mrefu kwa ukaguzi.

Kaimu Meneja  TFDA Kanda ya Kaskazini, Benny John akizungumza na  Maafisa Uhusiano wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto pamoja na Taasisi zilizo chini ya wizara hiyo (hawapo pichani) walipotembelea Makao makuu ya TFDA Kanda ya Kaskazini, Mkoani Arushai ikiwa ni Kampeni ya ‘ Tumeboresha Sekta ya Afya’ inayolenga kueleza mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli.
 Meneja wa Mawasiliano na Elimu kwa Umma wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Gaudensia Simwanza akizungumza katika kituo cha Namanga  wakati Maafisa Uhusiano wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo katika Kampeni ya Tumeboresha Sekta ya Afya kwa kuangalia uwekezaji uliofanywa na serikali ya Awamu ya Tano ya Rais Dkt John Pombe Magufuli katika miaka mitatu.

Mkaguzi wa Dawa wa TFDA mpaka wa Namanga Elia Nyeura akielezea taarifa fupi kwa   Maafisa Uhusiano wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto pamoja na Taasisi zilizo chini ya wizara hiyo (hawapo pichani) walipotembelea Mpaka wa Namanga panapokaguliwa na  TFDA Kanda ya Kaskazini, Mkoani Arushai ikiwa ni Kampeni ya ‘ Tumeboresha Sekta ya Afya’ inayolenga kueleza mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli. Anayefuatia ni Kaimu Meneja TFDA Kanda ya Kaskazini, Benny John
 Afisa Ukaguzi katika Kituo cha Namanga wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali GCLA, Michael Benarnd  akizungumza namna wanavyodhibiti uingiaji wa kemikali nchini katika kituo hicho, wakati Maafisa Uhusiano wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo walipotembelea kituo cha Namanga.

mkaguzi wa dawa wa TFDA kituo cha Namanga akiendelea na majukumu yake katika tukio hilo
 Afisa Ukaguzi wa TFDA akionesha Maabara hamishika wanavyotumia katika ukaguzi wa dawa,vifaa tiba pamoja vitendanishi katika kituo cha Ukaguzi wa pamoja cha Namanga.

Kaimu Meneja  TFDA Kanda ya Kaskazini, Benny John akionesha kielelezo cha ulinganifu wa bidhaa zilizoingia nchini (Istogram) kwa  Maafisa Uhusiano wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto pamoja na Taasisi zilizo chini ya wizara hiyo (hawapo pichani) walipotembelea Mpaka wa Namanga panapokaguliwa na  TFDA Kanda ya Kaskazini, Mkoani Arushai ikiwa ni Kampeni ya ‘ Tumeboresha Sekta ya Afya’ inayolenga kueleza mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli.
 Maafisa Uhusiano wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa Kanda ya Kaskazini ya TFDA iliyopo mkoani Arusha.
Picha ya pamoja ya maofisa habari wa wizara,taasisi pamoja na maofisa wa kituo cha Namanga wakiwa nje ya kituo hicho mara baada ya kuona kazi zinazofanya kwenye kituo hicho

WAZIRI WA AFYA UMMY MWALIMU AKABIDHI MAGARI 10,PIKIPIKI 35 KWA LENGO LA KUBORESHA SEKTA YA AFYA

0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amekabidhi magari 10 na pikipiki 35 kwa mikoa mbalimbali nchini huku akisisitiza Serikali ya Awamu ya Tano imejikita kuboresha sekta ya huduma ya afya kwa Watanzania.

Magari na pikipiki amekabidhi leo Januari 14, 2019, Mwalimu amesema tukio hilo la kukabidhi rasmi Magari 10 na Pikipiki 35 kwa uongozi wa mikoa kwa ajili ya kwenda kusimamia na kuhakikisha kwamba wananchi wanapatiwa huduma za Kifua Kikuu na Ukoma ipasavyo ni muhimu . 

"Kama mnavyofahamu bado nchi yetu inakabiliwa na janga la ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) na Ukoma. TB ni hatari kwani inasababisha vifo, na Ukoma husababisha vifo na ulemavu wa kudumu. TB pia inaongoza kusababisha vifo vingi miongoni mwa wananchi wenye VVU," amefafanua Waziri Mwalimu.

Ameongeza kila mwaka Tanzania inakadiriwa kuwa na wagonjwa wapya wa TB wapatao 154,000 ambao kati yao ni 44% (69,818) tu ndio waliogunduliwa. Changamoto kubwa ni jinsi ya kufikishia wananchi wote huduma za kufanya uchunguzi na upimaji pamoja na kuwapatia elimu ya kutosha kuhusu magonjwa hayo.

Ameongeza Serikali ya Awamu ya Tano imekuwa inafanya jitihada kubwa kuhakikisha wananchi wanapata huduma hizo ili kuongeza kasi ya ugunduzi wa ugonjwa wa TB na kwamba mojawapo ya juhudi hizo ni pamoja na ununuzi wa mashine za kupima vinasaba vya Kifua Kikuu kitaalamu Gene-Xpert.

Ambapo zimeongezeka kutoka 64 mwaka 2015 hadi 210  Disemba 2018 na kufanya 85% (158/186)  ya Halmashauri zote nchini kuwa na  mashine hizi zinazoweza kupima TB kwa haraka na kwa ufanisi zaidi. 

"Mashine hizo hutoa majibu ndani ya saa 2 tofauti na kipimo cha Hadubini ambazho huto majibu baada ya saa 48. Lengo ni hadi kufikia mwisho wa mwaka huu wilaya zote ziwe na mashine hizi. Kipimo hiki cha Gene-Xpert hutolewa bure," amesema.

Waziri Mwalimu amesema Serikali hiyo imepeleka huduma ya kifua kikuu sugu karibu kwa wananchi, huduma ambayo wakati Serikali ya awamu ya tano inaingia madarakani ilikuwa inapatikana katika hospitali moja tu ya Kibong’oto lakini kwa sasa inapatikana katika vituo 81 katika mikoa 23. 

"Ni katika kuongeza juhudi hizi, Serikali kupitia Wizara imenunua magari 10 na pikipiki 35 tunazozikabidhi leo kwa lengo la kuhakikisha Waratibu hawa wanawatumikia wananchi kwa kwenda kuhakikisha kama huduma zinawafikia kwa wakati.

" Magari haya 10 yamegharimu kiasi cha Sh.Milioni 611,869,741 na Pikipiki 35, zilizogharimu Sh.milioni 167,042,538. Jumla ni  milioni 778. Mikoa inayopatiwa Magari ni Pwani, Songwe, Ilala II, Kilimanjaro, Lindi, Kagera, Tabora, Mtwara, Ruvuma na Rukwa. 

"Pikipiki 35 zinatolewa kwa Halmashauri 35 ambazo ni Nzega Mjini, Urambo, Kasulu, Ujiji Manispaa, Ngara, Kyerwa, Mkalama, Itigi, Msalala, Kishapu, Bariadi, Same, Mbarali, Kyela, Mbulu, Hanang, Chato, Mbozi, Ileje, Kilolo, Chamwino, Amana, Madaba, Wanging’ombe, Ilemela, Mpanda, Kalambo, Nanyumbu, Mtwara, Mbagala, Mburahati, Tanga Jiji, Muheza, Kilombero na Gairo ," amefafanua.

Pia amesema magari hayo na Pikipiki zinazokabidhiwa kwa uongozi wa mikoa vitasaidia katika usimamizi wa shughuli za Mpango, kuhakiksha wagonjwa wa TB na Ukoma wanapatiwa elimu, wanagunduliwa na kupatiwa matibabu.

 Amesema vyombo hivyo vitatumika kwa shughuli zinginezo za mikoa na wilaya zinazolenga kumfikishia huduma bora za afya mwananchi. Ametoa rai yake kwa uongozi wa Mikoa inayopatiwa vyombo hivyo vya usafirishaji vitumike kwa shughuli iliyokusudiwa kuimarisha huduma za Kifua Kikuu na Ukoma.

Amesisitiza vyombo vitumike kwa malengo yaliyokusudiwa na si vinginevyo na wanaamini kwamba Mikoa hiyo itaongeza kwa kasi ugunduzi wa wagonjwa wa Kifua Kikuu na kutokomeza ugonjwa wa Ukoma katika mikoa yenu. 

Ameongeza lengo la Serikali ni kuhakikisha ifikapo 2020 tunawaibua na kuwapatia matibabu asilimia 70 ya watu wanaougua TB kutoka asilimia 48 ya hivi sasa.

Waziri Mwalimu amesema kwa upande wa ugonjwa wa Ukoma ni malengo ya Serikali kutokomeza ugonjwa huo katika Wilaya 20 zilizobakia ambazo ni Liwale, Mkinga, Nkasi, Lindi DC, Ruangwa, Nanyumbu, Shinyanga Manispaa, Kilombero, Mafya, Pangani, Mvomero, Masasi, Chato, Mpanda TC, Nachingwea, Rufiji, Korogwe, Ulanga, Morogoro DC na Kilwa DC.

Ametumia nafasi hiyo shukurani kwa  Mfuko wa Dunia (GF – ATM) kwani, fedha hizo ni sehemu ya mfuko huu wa mzunguko wa 2018 – 2020.
Baadhi ya piki piki kati ya 35 na Magari 10 yatakayosambazwa katika mikoa mbalimbali, zilizokabidhiwa leo jijini Dar na Waziri  wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kwa uongozi wa mikoa kwa ajili ya kwenda kusimamia na kuhakikisha kwamba wananchi wanapatiwa huduma za Kifua Kikuu na Ukoma ipasavyo. 

Mikoa 10 inayopatiwa Magari ni Pwani, Songwe, Ilala II, Kilimanjaro, Lindi, Kagera, Tabora, Mtwara, Ruvuma na Rukwa na Pikipiki 35 zinatolewa kwa Halmashauri 35 ambazo ni Nzega Mjini, Urambo, Kasulu, Ujiji Manispaa, Ngara, Kyerwa, Mkalama, Itigi, Msalala, Kishapu, Bariadi, Same, Mbarali, Kyela, Mbulu, Hanang, Chato, Mbozi, Ileje, Kilolo, Chamwino, Amana, Madaba, Wanging’ombe, Ilemela, Mpanda, Kalambo, Nanyumbu, Mtwara, Mbagala, Mburahati, Tanga Jiji, Muheza, Kilombero na Gairo.

Magari haya 10 yamegharimu kiasi cha Sh.Milioni 611,869,741 na Pikipiki 35, zilizogharimu Sh.milioni 167,042,538

 WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akimkabidhi Mganga Mkuu wa mkoa wa Rukwa Dkt Boniface Kasululu moja ya piki piki kati ya 35 zitakazosambazwa katika mikoa mbalimbali kwenye hafla fupi iliofanyika leo jijini Dar.Waziri Ummy amekabidhi magari 10 na pikipiki 35 kwa mikoa mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha Waratibu wanawatumikia wananchi kwa kwenda kuhakikisha kama huduma zinawafikia kwa wakati.
 WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akimkabidhi Mganga Mkuu wa mkoa wa Kagera Dkt Marco Mbata ufunguo wa moja ya gari kati ya 10,yatakayosambazwa katika mikoa 10 ,hafla  ya makabidhiano hayo imefanyika leo jijini Dar.Waziri Ummy amekabidhi magari 10 na pikipiki 35 kwa mikoa mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha Waratibu wanawatumikia wananchi kwa kwenda kuhakikisha kama huduma zinawafikia kwa wakati.
 WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akisoma maandishi yaliyoandikwa kwenye moja ya magari hayo kabla ya kukabidhiwa kwa viongozi waandamizi wa mikoa mbalimbali leo jijini Dar.
  WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwa katika picha pamoja na viongozi waandamizi wa mikoa mbalimbali waliokabidhiwa Piki piki 35 na Magari 10 leo jijini Dar.

KOZI MPYA YA UCHAMBUZI YAKINIFU KUPITIA VIASHIRIA HATARISHI KATIKA MFUMO WA UTOAJI MIKOPO YAZINDULIWA LEO JIJINI DAR

0
0
MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya Mabenki Tanzania (TIOB), Patrick Mususa(kulia), akizungumza wakati wa kumkaribisha Meneja wa Usimamizi wa Taasisi za Fedha wa Benki Kuu ya Tanzania(BOT), Nassor Omar,kuzindua Kozi mpya ya Uchambuzi yakinifu kupitia viashiria hatarishi katika Mfumo wa Utoaji Mikopo(The basics of Credit Risk Modelling) kwa Wakurugenzi Wakuu wa Mabaenki na Taasisi za Fedha,uliofanyika Dar es Salaam, jana.

CHUO KIKUU MZUMBE CHAANZISHA SAFARI YA MABADILIKO WEZESHI KATIKA SEKTA YA AJIRA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI

0
0

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof.Lughano Kusiluka,akizungumza na Wahadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe waliohudhuria warsha ya mabadiliko katika Sekta ya ajira kwa manufaa ya Jamii Afrika Mashariki (TESCEA) inayoendelea Morogoro.
Mwezeshaji wa warsha hiyo toka nchini Kenya Prof. Charles Kingsburry akifafanua kuhusu mradi huo kwa Waandishi wa Habari.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe (Taaluma) Prof. Ganka Nyamsogoro akiwasisitiza washiriki umuhimu wa warsha hiyo katika kubadili mbinu za ufundishaji.
Baadhi ya washiriki wakiwa katika majadiliano.
Mratibu wa mradi wa TESCEA Dkt. Albogast Musabila akifafanua kuhusu mradi huo kwa Waandishi wa Habari.
Mwezeshaji toka Chuo Kikuu, Afrika Nazarene cha nchini Kenya Dkt. Kendi Muchungi akieleza umuhimu wa mpango huo na jinsi unavyoweza kunufaisha wasomi na Jamii zao.
Mratibu Msaidizi wa mradi wa TESCEA wa Chuo Kikuu Mzumbe Dkt. Jennifer Sesabo akitambulisha mpango wa mradi huo kwa Washiriki.
Washiriki wakifuatilia maelekezo yanayotolewa katika warsha hiyo inayoendelea Hoteli ya Morogoro.
Washiriki wa warsha ya TESCEA katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi rasmi. Chuo Kikuu Mzumbe kupitia mradi wake mpya wa ‘TESCEA’ kimeendesha warsha ya kuwajengea uwezo wahadhiri katika mbinu bora za ufundishaji zinazosaidia wanafunzi kuweza kujiajirika pindi wanapohitimu masomo yao ya elimu ya juu .
 
 Akizungumza katika uzinduzi wa warsha hiyo inayoendelea katika hoteli ya Morogoro, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof.Lughano Kusiluka amesema Chuo Kikuu Mzumbe ni mahiri katika kufundisha masomo ya biashara na menejimenti na sasa kinakwenda hatua ya mbele zaidi kwakuwaandaa wahitimu wa ndani na hata nchi nyingine kutengeneza ajira kabla ya kuhitimu masomo yao. 
 
Prof.Kusiluka ameeleza kuwa kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa waajiri dhidi ya wahitimu wa vyuo vikuu nchini na kuonekana kutokuwa na ujuzi wa kutosha na umahiri katika fani walizosomea pindi wanapotaka kuajiriwa. Hivyo, Chuo Kikuu Mzumbe kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dodoma na vyuo vikuu viwili kutoka Uganda (Uganda Martys na Gulu), pamoja na asasi za AFELT, LIWA, ASHOKA kutoka Kenya na INASP kutoka Uingereza, wameanza kwa kuwajengea wahadhiri ili kubadili mbinu za ufundishaji zitakazowawezesha wahitimu kuwa na maarifa, ubunifu na ujuzi zaidi kutambua na kutumia fursa zilizopo ili kutengeneza ajira au kuajiriwa. 
 
Kwa upande wake mwezeshaji wa warsha wa asasi ya umoja wa Vyuo vikuu vinavyofundisha mbinu zinazohitajika katika kuboresha ufundishaji Afrika Mashariki (AFELT) na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Daystar cha Kenya Prof. Charles Kingsburry, amesema ni muhimu sasa kubadili mfumo wa ufundishaji unaowafanya wahitimu kujua vitu kulingana na elimu wanayofundishwa darasani pekee na kwa kutegemea mitandao ya intaneti na badala yake mbinu mpya za ufundishaji ziwajenge katika ubunifu ,maarifa,mbinu na stadi halisia zitakazowawezesha kujiajiri wao na kuweza kuajiri watu wengine. 
 
Hii ina lengo si tu la kuwafanya wahitimu kujua vitu tofauti bali kuwajenga kuwa watu tofauti wanaoleta mabadiliko chanya kwa jamii nzima na kujinufaisha wao na jamii zinawazunguka kupitia elimu waliyopata. Naye mwezeshaji mwingine toka Asasi ya AFELT na mhadhiri wa Chuo Kikuu, Afrika Nazarene cha nchini Kenya Dkt. Kendi Muchungi amesema wahitimu wa Vyuo Vikuu vyote vya Afrika Mashariki hawatofautiani na wamekuwa wakikosa uwezo wa kujiajiri na kuajiriwa na hivyo kushindwa kuisaidia jamii katika suala la ajira kupitia elimu waliyopata,badala yake wamekuwa wakitegemea kuajiriwa. 
 
Hivyo ni imani yake kuwa mpango huo utaleta mabadiliko kwa wahadhiri wa vyuo vikuu katika ufundishaji na kunufaisha jamii nzima ya Afrika Mashariki kupitia wasomi wachache. Wakati huo huo mratibu wa Mradi wa ‘TESCEA’ kutoka Chuo Kikuu Mzumbe,Dkt.Albogast Musabila amesema pamoja na lengo kuu la mpango wa mradi huo la kuwajengea wahitimu uwezo wa kujiajiri na kuajiri,Chuo Kikuu Mzumbe kwa ushirikiano na wadau wa Sekta ya ajira, wahadhiri na wanafunzi kimeanza mchakato wa kukusanya maoni ya wadau kwa ajili ya kuandaa mapendekezo yatakayozingatiwa wakati wa kuboresha mitaala na kuanzisha mitaala mipya.

WIZARA YAWAKUMBUSHA WADAU KUHUSU UMUHIMU WA KULINDA MFUMO WA FEDHA NCHINI, KUDHIBITI UTAKATISHAJI FEDHA

0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

WIZARA ya Fedha na Mipango kupitia Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) imeandaa warsha kuhusu udhibiti wa utakasishaji wa fedha haramu na ufadhili wa ugaidi kwa wadau wa sekta ya fedha nchini.

Lengo la warsha hiyo ni kuendelea kuwakumbusha wadau kuhusu umuhimu wa kulinda mfumo wa fedha wa nchi yetu ili usitumiwe vibaya na wahalifu na watu wasio waaminifu.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo kuhusu udhibiti wa utakatishaji wa fedha haramu na ufadhili wa ugaidi, Kamishna na Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) Onesmo Makombe alisema tatizo la utakasishaji wa fedha haramu ni tatizo kubwa ulimwenguni kote na katika jamii.

Amesema ni kwasababu ya kuwepo kwa vitendo mbalimbali vya uhalifu vinavyowapatia wahalifu pato haramu. Uhalifu huo ni pamoja na ukwepaji kodi, biashara haramu ya dawa za kulevya, biashara haramu ya watu, biashara haramu ya silaha, rushwa, kughushi, ujangili, uharamia, uvunaji haramu wa magogo, uuzaji wa bidhaa bandia, ujambazi na uporaji

Aidha amebainisha madhara ya utakasishaji wa fedha haramu kuwa ni ya kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiusalama. Madhara hayo pamoja na uhalifu kuendelea kushamiri kwa uhalifu na wahalifu kujiimarisha; wahalifu kuwa na nguvu kiuchumi.

Pia kuhatarisha utawala wa sheria na usalama kwani uhalifu unaposhamiri na makundi ya uhalifu yanapojiimarisha hupata nguvu na kujaribu kudhibiti vyombo vya au kushindana na vyombo vya dola; kuharibu ushindani wa kibiashara katika uchumi kutokana na wahalifu kuwa na mitaji inayotokana na fedha haramu.

Amefafanua madhara mengine ni wafanyabiashara halali hushindwa kuhimili ushindani; kushusha hadhi ya nchi kimataifa na kusababisha nchi kutonufaika na mfumo wa fedha wa kimataifa; kushusha imani ya wawekezaji na kusababisha uwekezaji kupungua.

"Na wawekezaji wapya kutotaka kuwekeza kutokana na kushamiri kwa uhalifu, wawekezaji huwa na hofu kuwa mitaji na mali zao havitakuwa salama; imani ya washirika wa maendeleo na jumuiya ya kimataifa hupungua na nchi huathirika kiuchumi; kushuka kwa hadhi ya taasisi za fedha na mfumo mzima wa fedha.

"Na nchi kushindwa kufikia malengo ya maendeleo kwani rasilimali huwa mikononi mwa wahalifu wachache badala ya kutumika kutekeleza ajenda pana ya maendeleo ya nchi," amesema Makombe.

Wakati huo huo Kamishna wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu amewakumbusha washiriki wa warsha hiyo kuendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali kutekeleza wajibu wao wa kisheria kwa uadilifu na uaminifu ili kusaidia katika kubaini wahalifu wanaoweza kutumia mfumo wa fedha wa nchi kutakasisha fedha haramu na kufadhili vitendo vya kigaidi na kuhatarisha usalama wa nchi. 

Warsha hiyo imejumuisha washiriki kutoka benki na taasisi zinazotoa huduma za kibenki na huduma ndogo ndogo za fedha.
Kamishna na Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) Ndugu Onesmo H. Makombe akizungumza na Watumishi wa Taasisi Mbalimbali za kifedha nchini
Kamishna Msaidizi ,Huduma za Kompyuta Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) Gilbert .R.Nyombi akizungumza na Watumishi wa Taasisi Mbalimbali za kifedha nchini alipokuwa akitoa mada juu ya kudhibiti fedha haramu.
Baaadhi ya Washiriki wa Warsha hiyo wakifatilia mada zilizokuwa zikitolewa na Mtaalamu kutoka FIU Kwa umakinimu.
Washiriki wakiwa katika Makundi kujadili mada zilizowashirishwa na wao kuchangia katika suala zima la utakatishaji fedha kutumia taasisi za kifedha. 
Washiriki wa Warsha hiyo wakiwa katika Picha ya Pamoja na AmuKamishna na Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) Ndugu Onesmo H. Makombe 
Washiriki wa Warsha hiyo wakiwa katika Picha ya Pamoja na AmuKamishna na Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) Ndugu Onesmo H. Makombe.

Wananchi kata ya Kala wamlilia RC baada ya kukosa mawasiliano ya simu na radio

0
0
Wananchi wa kata ya Kala yenye vijiji vitano iliyopo katika wilaya ya Nkasi wamefikisha kilio chao cha kukosa mawasiliano ya simu kwa mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo ili aweze kuwasaidia kutatua kero hiyo ambayo inakwamisha maendeleo ya kata

Kilio hicho kimetolewa wakati wa kusoma risala ya maendeleo ya kata na msoma risala Felix kapoze alipokuwa akielezea changamoto mbalimbali zinazoikabili kata hiyo kwa muda mrefu jambo linalokwamisha utendaji kazi pamoja na kufanya mawasiliano kuwa magumu.

“Changamoto nyingine kubwa ilipo hapa Kijijini kutokuwapo kwa mtandao wa simu, hii inapelekeana kukwama kwa taarifa nyingi hasa katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo hivyo tunaiomba ofisi ya Mkuu wa Mkoa itusaidie kupatikana kwa mtandao wa simu ili kurahisisha mawasiliano,” Alifafanua.

Halikadhalika jambo hilo liliungwa mkono na mbunge wa jimbo la Nkasi Kusini Desderius Mipata wakati akielezea changamoto hiyo na hatua alizochukua kuhakikisha kuwa mawasiliano hayo yanapatinaka na hatimae kurahisisha utendaji kazi wa shughuli za maendeleo katika kata hiyo.

“Hawa wananchi ni pekee ambao hawazungumzi na wenzao katika taifa na katika jimbo, juhudi nilizozifanya kama kiongozi wa jimbo ni kuitaka wizara ihakikishe kwamba tunapata mtandao, tunashukuru mungu wametusikiliza na sasa wanajenga minara miwili katika Kijiji cha kilambo cha mkolechi na Kijiji cha Kala, wanasema Kala itazungumza wantuambia katika kipindi kisichozidi miezi miwili,” Alibainisha.

Nae Wangabo aliwahakikishia wananchi wa kata hiyo kuwa mawasiliano yataimarishwa “Tutaimarisha hayo mawasiliano na juzi nilikuwa naongea na waziri wa ujenzi alikuja pale ofisini na tuliongea swala hili la minara ya mawasiliano, uzuri wameshaanza kufanyia kazi, kwahiyo tutaongeza nguvu kule ili mitandao ya mawasiliano ifanye kazi n ahata radio nkasi iweze kuwafikia huku,” Alisema.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo (kushoto) akiongea na wananchi wa Kijiji cha Mpasa, Kata ya Kala mwambao wa ziwa Tanganyika Wilayani Nkasi
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo (katikati) akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mpasa, Kata ya Kala mwambao wa ziwa Tanganyika Wilayani Nkasi.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo akiongea na mlemavu wa miguu aliyesimamisha msafara wa Mkuu huyo ili kumsalimia katika kijiji cha mlambo kilichopo katikati ya Kijiji cha Mpasa na Kingombe vilivyotengwa kwa kilometa 34 na hakuna mawasiliano ya simu wala radio katika Kata ya Kala  Wilaya ya Nkasi. 
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo akisalimiana na mlemavu wa miguu aliyesimamisha msafara wa Mkuu huyo ili kumsalimia katika kijiji cha mlambo kilichopo katikati ya Kijiji cha Mpasa na Kingombe  Kata ya Kala  Wilaya ya Nkasi.

Wananchi wa kata ya Kala yenye vijiji vitano iliyopo katika wilaya ya Nkasi wamefikisha kilio chao cha kukosa mawasiliano ya simu kwa mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo ili aweze kuwasaidia kutatua kero hiyo ambayo inakwamisha maendeleo ya kata

Wafanyakazi wa Taasisi ya JKCI waadhimisha sherehe ya miaka mitatu tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo

0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akikata keki ya kuadhimisha miaka mitatu tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo Septemba 5, 2015 katika sherehe iliyofanyika  hivi karibuni kwenye  hoteli ya Protea Court Yard Sea view iliyopo jijini Dar es Salaam.
 Mchekeshaji Bob Shaw kutoka Shirika la Cardiostart International la nchini Marekani akitoa burudani kwa wafanyakazi wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) pamoja na wageni waalikwa wakati wa sherehe ya maadhimisho ya miaka mitatu tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo Septemba 5, 2015 iliyofanyika  hivi karibuni kwenye  hoteli ya Protea Court Yard Sea view jijini Dar es Salaam.
 Wafanyakazi wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) pamoja na wageni waalikwa wakicheza mziki wa iyokote uliokuwa ukipigwa na bendi ya Cocodo African Music wakati wa sherehe ya maadhimisho ya miaka mitatu tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo Septemba 5, 2015 iliyofanyika  hivi karibuni kwenye  hoteli ya Protea Court Yard Sea view iliyopo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi cheti cha  shukrani mwandishi wa habari wa gazeti la Mtanzania Veronica Romwald kutokana na mchango wa gazeti hilo wa kutoa  elimu kwa umma kuhusu magonjwa ya moyo wakati wa  sherehe ya maadhimisho ya miaka mitatu tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo iliyofanyika hivi karibuni katika hoteli ya Protea Court Yard Sea view iliyopo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi cheti cha  shukrani mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania Daima  Asha Mwakyonde  kutokana na mchango wa gazeti hilo wa kutoa  elimu kwa umma kuhusu magonjwa ya moyo wakati wa  sherehe ya maadhimisho ya miaka mitatu tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo iliyofanyika hivi karibuni katika hoteli ya Protea Court Yard Sea view iliyopo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi cheti cha  shukrani mwandishi wa habari wa kituo cha Televisheni cha East Africa Oliver Nyeriga  kutokana na mchango wa kituo hicho  wa kutoa  elimu kwa umma kuhusu magonjwa ya moyo wakati wa  sherehe ya maadhimisho ya miaka mitatu tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo iliyofanyika hivi karibuni katika hoteli ya Protea Court Yard Sea view iliyopo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi cheti cha  shukrani mwandishi wa habari wa gazeti la Uhuru Baraka Loshiraa kutokana na mchango wa gazeti hilo wa kutoa  elimu kwa umma kuhusu magonjwa ya moyo wakati wa  sherehe ya maadhimisho ya miaka mitatu tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo iliyofanyika hivi karibuni katika hoteli ya Protea Court Yard Sea view  iliyopo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi cheti cha  shukrani mwandishi wa habari wa gazeti la Habarileo  Regina Kumba kutokana na mchango wa gazeti hilo wa kutoa  elimu kwa umma kuhusu magonjwa ya moyo wakati wa  sherehe ya maadhimisho ya miaka mitatu tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo iliyofanyika hivi karibuni katika hoteli ya Protea Court Yard Sea view  iliyopo jijini Dar es Salaam.
Wakurugenzi watano wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakifungua Champaign wakati wa  sherehe ya maadhimisho ya miaka mitatu tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo Septemba 5, 2015 iliyofanyika hivi karibuni katika hoteli ya Protea Court Yard Sea view  iliyopo jijini Dar es Salaam. Picha na JKCI

DKT. ZAINAB ATINGA OFISI KUU, WIZARA YA AFYA JIJINI DODOMA.

0
0
Na WAMJW - DODOMA

KATIBU Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto-Idara kuu Afya Dkt. Zainab Chaula leo amekutana na Wakurugenzi wa idara na Wakuu wa Vitengo wa wizara hiyo tangu alipoapishwa siku chache kushika nafasi hiyo, akitokea TAMISEMI.

Katika kikao hicho Dkt. Chaula amemshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuendelea kumuamini na kumpa nafasi hiyo, huku akihimiza kila mmoja kufanya kazi kwa ushirikiano na kwa weledi ili kulinda taaluma zao. "Tujiandae kufanya kazi kama timu moja katika kutekeleza sera na miongozo ya sekta ya afya na kuhakikisha dhamana tuliyopewa tunaitumikia kadri inavyowezekana".Alisisitiza Dkt.Chaula

Hata hivyo Dkt.Chaula alimshukuru Katibu Mkuu aliyeondoka Dkt.Mpoki Ulisubisya kwa mifumo mizuri aliyoiweka na kuahidi kuendeleza kwa kuanza na changamoto zilizopo.Aidha,aliwataka wakurugenzi hao kutimiza majukumu yao kwa kufanya kazi kwa kujituma, huku akiwatoa hofu kuwa ofisi yake iko wazi muda wote na yeyote mwenye wazo zuri la kujenga asisite kumuona, kwani lengo ni kuboresha Sekta ya Afya

"uwezo wa kufanya kazi tunao hivyo.mabadiliko ni vitendo, tufanye kazi kwa matokeo". Alisema Dkt. Chaula .Wakati huo huo, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula ametembelea ujenzi wa mji mpya wa Serikali Ihumwa na kujionea maendeleo ya ujenzi wa Wizara ya Afya.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula (Wakulia) akipokea nyaraka za makabidhiano kutoka kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Ulisubisya Mpoki leo katika Ofisi Kuu za Wizara ya Afya jijini Dodoma.

Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akiteta jambo na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Bakar Kambi baada ya Kikao cha kumkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula.
Kikao chaWakurugenzi, Wakuu wa Vitengo na Wakuu wa Idara Wizara ya Afya kikiongozwa na aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati wakimpokea Katibu Mkuu mpya Dkt. Zainab Chaula leo katika Ofisi Kuu za Wizara ya Afya jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula (Wakulia) akiteta jambo na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Mpoki Ulisubisya leo katika Ofisi Kuu za Wizara ya Afya jijini Dodoma, katika kikao na Wakurugenzi, Wakuu wa Vitengo na Wakuu wa Idara Wizara ya Afya.
Picha ya Pamoja ikiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula, Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya, Naibu Katibu Mkuu Afya TAMISEMI Dkt. Dorothy Gwajima na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Bakar Kambi, pamoja na Wakurugenzi, Wakuu wa Vitengo na Wakuu wa Idara Wizara ya Afya baada ya kikao kifupi cha ukaribisho wa Dkt. Chaula.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula, akiwaonesha namna ya ufuatiliaji ili kuboresha Ujenzi wa Mji mpya wa Serikali Ihumwa wakati alipotembelea ujenzi wa TAMISEMI ili kujifunza, Wakwanza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Afya TAMISEMI Dkt. Dorothy Gwajima, anaefuata ni Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Bakar Kambi na Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile akimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula pindi walipokutana kwenye ziara ya kutembelea ujenzi wa Wizara ya Afya katika Mji mpya wa Serikali Ihumwa, jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula (Wakwanza Kushoto) akibadilishana mawazo na aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya (Watatu kulia) pamoja na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Bakar Kambi
Ujenzi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ukiendelea kwa kasi katika Mji mpya wa Serikali Ihumwa, jijini Dodoma.

KILIMANJARO WAZINDUA KAMPENI YA KUOTESHA MITI YA MATUNDA JUU YA KABURI.

0
0
Anaandika Dixon Busagaga,Moshi 

Shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na utunzaji wa Mazingira lijulikanalo kama LEPAJE limezindua kampeni ya uoteshaji wa miti ya matunda juu Makaburi kwa lengo la kuendeleza mapambano dhidi ya uharibifu wa mazngira nchini kwa kubadili wafu kuwa mti wa matunda.

Katika kampeni hiyo iliyozinduliwa mapema mwezi huu katika kijiji cha Kifuni juu kata ya Kibosho Umbwe wilaya ya Moshi vijijini,mkoani Kilimanjaro,tayari miti ya matunda ya Parachichi imeoteshwa katika makaburi matano ya mfano huku makaburi zaidi ya 200 yakitaraji kuoteshwa kupitia kampeni hiyo.

Leonard Massawe ni mkurugenzi wa Shirika la Lepaje anasema katika kijiji hicho wamekubaliana kuotesha miti ya matunda ya muda mfupi na yanayopendwa na jamii ambayo yatakuwa tayari kuliwa katika kipindi cha mwaka mmoja.

“Kwenye maeneo yetu haya ya baridi tumeamua kuotesha ,miti ya matunda ambayo yanastawi vizuri na ambayo yanapendwa zaidi na jamii yetu ya huku,tumeotesha Parachichi za kikonyo ,hata hivyo kampeni hii inahitaji kuungwa mkono na Serikali ,Wanahabari,viongozi wa Dini,taasisi za elimu na jamii kwa ujumla”alisema Massawe.

Amesema Makaburi matano ya mfano yaliyooteshwa miti ya matunda ni ya familia yake akiwemo mama yake mzazi na kaka zake wawili akieleza kuwa kampeni hiyo ni rahisi huku akisisitiza jamii kuinga mkono ili kufikia lengo.

“Kuishawisi jamii kuotesha miti ya matunda juu ya kaburi inahitaji ujasiri mkubwa ,mimi nimeotesha mti wa tunda la Parachichi kwenye kaburi la Mama yangu mzazi ili iwe mbegu ya utunzaji wa mazingira Duniani”alisema Masawe.Alisema muda umefika kwa jamii ya Wachaga kubadili mtazamo wa kuotesha majani yajulikanayo kama “Isale” na badala yake waoteshe miti ya matunda muda mfupi tu baada ya kumzika ndugu yao.

Alisema mwaka 2019 ni mwaka wa kubadili wafu kuwa Matunda katika mkoa wa Kilimanjaro huku akiitaka jamiii katika makaburi ya ndugu zao hata kama walizikwa miaka mingi iliyopita na kwamba hali hiyo itachangia kuboresha hali ya hewa kwa mkoa wa Kilimanjaro.

Mmoja wa wananchi katika kijiji hicho Lucia John amesema uoteshaji wa miti a matunda katika kaburi pia utasaidia kuimarisha afya kwa jamii lakini pia utachangia uchumi wa mtu mmoja mmoja kwa kuuza matunda na mengine yanaweza kusafirishwa nje ya nchi.

Hii ni kampeni ya 32 kwa shirika lisilo la kiserikali la kuhifadhi mazingira ambapo awali limefanya kampeni za kuotesha miti katika wilaya za mkoa wa Kilimanjaro kupitia mchezo wa riadha iliyojulikana kama Lepaje Marathon.



Viewing all 46206 articles
Browse latest View live




Latest Images