Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1775 | 1776 | (Page 1777) | 1778 | 1779 | .... | 1897 | newer

  0 0


  NA. WAMJW, Dar es Salaam.

  Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umejivunia kuongeza wigo wa wanufaika kwa kuwafikia Wananchi mbalimbali ikiwemo Wakulima kupitia vyama vyao vya ushirika kwenye huduma ya Ushirika Afya na watoto kupitia huduma ya Toto Afya Kadi. Mfuko pia umewezesha upatikanaji wa huduma za Madaktari Bingwa katika mikoa ya pembezoni pamoja na kuwezesha upatikanaji wa vifaa tiba vya kisasa katika Hospitali hapa nchini.

  Hayo yameelezwa na Meneja Uhusiano wa Mfuko huo Bi. Anjela Mziray wakati wa ziara maalum ya Maafisa Habari wa Wizara ya Afya na taasisi zake katika kampeni maalum ya ‘Tumeboresha Sekta ya Afya’ inayolenga kueleza mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli.

  Wakiwa Makao Makuu ya NHIF, Maafisa hao waliweza kutembelea maeneo mbalimbali ya Mfuko huo kujionea namna huduma zinazotolewa na Mfuko huo sambamba na mafaniko waliyofikia katika sekta ya Afya.

  Awali akizungumza mambo mbalimbali Bi. Anjela Mziray aliwaeleza Maafisa hao kuwa Serikali inakusudia kuwafikia wananchi wote na huduma bora za afya. Katika kutekeleza hili Mfuko umewezesha Madaktari Bingwa wa magonjwa ya mbalimbali kama ya Wanawake, watoto, moyo, macho, kinywa na pua na mabingwa wa upasuaji kutoa huduma katika mikoa ya pembezoni kwa kipindi maalum.

  "Kwa ujumla watu zaidi ya 20,289 wamefikiwa na huduma hii na kati ya hao watu 938 wamefanyiwa upasuaji wa kitalaam na hii ni katika mikoa ya Kigoma, Katavi, Rukwa, Lindi, Mara, Manyara, Geita, Njombe na Ruvuma huku baadhi ya mikoa tukienda mara mbili” alieleza Bi. Anjela Mziray.

  Aidha, katika mafaniko mengine ya kuboresha upatikanaji wa huduma, Mfuko unashiriki juhudi za Serikali za uwekezaji katika viwanda. Mfuko kwa kushirikiana na baadhi ya taasisi zingine unawekeza katika kiwanda cha uzalishaji wa bidhaa za hospitali zitokanazo na malighafi ya pamba na kiwanda hiko kitajengwa Bariadi Mkoani Simiyu huku kikitarajiwa kuzalisha aina 24 za bidhaa hizo. Wadau wengine wanaoshiriki katika uwekezaji huu ni pamoja na Serikali ya mkoa wa Simiyu, WCF, TFDA, TBS, MSD, TIB, TIRDO na taasisi zingine.

  Katika jitihada za kuhakikisha wananchi wanapata huduma, alieleza kuwa Mfuko kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Ujerumani umenawezesha wamama wajawazito kupata bima ya afya ili waweze kupata huduma katika hospitali. Mpaka sasa wajawazito wapatao 1,044,000 wameshafikiwa na mpango huu katika mikoa ya Tanga, Mbeya, Njombe, Lindi na Mtwara.

  Mfuko huo pia umeweza kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa kutumia mifumo ya Tehama inayowezesha kutambua wanachama katika vituo, kurahisisha ulipaji wa madai ya watoa huduma kwa wakati, kurahisisha usajili wa wanachama na kuharakisha utoaji wa vitambulisho.

  Akizungumzia hili Meneja wa Mifumo ya Tehama Bw. Bakari Yahaya alisema kwa sasa mifumo inamwezesha mwanachama kupata ujumbe mfupi kwenye simu yake mara tu kadi yake au ya mtegemezi wake inapotumika kwa matibabu. 

  Mfuko huu sasa umefanikiwa kuwa na ofisi zake katika mikoa yote ikiwemo Tanzania Bara na Zanzibar huku wakiboresha mfumo wa mawasiliano kwa kuwa na kituo cha huduma kwa wateja kwa ajili ya kupokea simu za wadau siku zote za juma bila malipo kwa wapigaji. Simu hiyo ni 0800 110063.

  Akimalizia maelezo yake alisema, Mfuko umefanikiwa kupata cheti cha ubora wa huduma kwa viwango vya kimataifa ( ISO 9001:2015). "Katika hili tunajivunia kuimarika kwa huduma na ufanisi katika utekelezaji majukumu ya Mfuko kwa manufaa ya wadau wote wa Mfuko" alisema Bi. Mziray.
   Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bi. Angela Mziray akizungumza wakati wa ziara maalum ya Maafisa habari wa Wizara ya Afya na taasisi zake katika kampeni maalum ya ‘Tunaboresha Sekta ya Afya’ inayolenga kueleza mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli.  leo 11.1.2019, Makao makuu ya Mfuko huo Jijini Dar es Salaam
   Afisa wa kitengo cha Tehama Charles Charles akionesha namna ya mfuko wa kisasa unavyofanya kazi katika kitengo cha tehama
   Msimamizi wa nyaraka wa NHIF, Erasto Msigwa akieleza namna mfumo huo unavyofanya kazi  wa kutunza kumbukumbu kwa njia ya kisasa
  Sabrina Mponda wa kitengo cha CALL CENTER akitoa maelezo namna huduma wanayotoa ikiwemo kupokea simu zaidi ya 200 kwa siku katika kituo hicho ambapo wamefanikiwa kuwafikia watanzania mbalimbali   0 0

  Kwa mara ya kwanza katika historia ya soka la Wanawake hapa nchini Klabu za Simba na Yanga zinatarajia kukutana kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite utakaochezwa Jumapili, Januari 13,2019. Mchezo huo utachezwa saa 10 Jioni katika Uwanja wa Karume, Ilala makao makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). 

  Ligi kuu ya wanawake inadhaminiwa na kinywaji cha Serengeti Premium Lite kwa msimu wa pili mfululizo. Katika mchezo huo unaotarajiwa kuwa na msisimko mkubwa, kiingilio kitakuwa shilingi 2,000. Mashabiki wanahakikishiwa usalama huku vyombo husika vikihakikisha mchezo salama bila bughudha ya aina yoyote. 

  Mwenyekiti wa Kamati ya Mpira wa Wanawake, Amina Karuma, akizungumza kuelekea mchezo huo amesema msimu huu umeanza kwa msisimko mkubwa na ushindani wa aina yake hivyo ni matarajio yake kuwa mchezo huo wa watani wa jadi utaakisi ubora wa Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite. 

  “Mchezo huo unaingia kwenye rekodi za Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite kwa kuwa ndio mchezo wa kwanza kuzikutanisha timu hizo tokea kuanza kwa soka la Wanawake hapa nchini,” alisema Amina. Aidha amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kushuhudia mchezo huo na kujiona vipaji pamoja na ushindani wa hali ya juu kutoka pande zote za mchezo. 

  Naye Afisa masoko wa Serengeti Breweries Bw. George Mango amewahakikishia wadau wa soka la wanawake, mashabiki wa mpira wa miguu kuwa kinywaji cha Serengeti Lite kimejidhatiti kuhakikisha wanapata burudani ya hali ya juu kupitia mchezo huo kama ilivyokuwa kwa michezo mingine iliyotangulia. 

  “Mashabiki wakae tayari kuona namna kinyaji cha Serengeti Lite kilivyo tayari kuwaletea burudani ya hali ya juu kwenye mechi hii ya kusisimua,” amesema Mango. 

  Serengeti Premium Lite ni bidhaa ya kwanza Tanzania kujitokeza kudhamini ligi ya wanawake, na imejidhatiti kusaidia kupandisha viwango vya ligi hii kupitia kupitia udhamani, matangazo kwenye magazeti pamoja na viwanjani. Bia ya Serengeti Premium Lite inadhamini Ligi Kuu ya Wanawake kwa kitita cha Shilingi 450 milioni kwa kipindi cha miaka mitatu. MWISHO. 
  Mwenyekiti wa Kamati ya Mpira wa Wanawake, Amina Karuma akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani ) wakati wa kutangaza mchuano wa ligi kuu ya soka la wanawake ya SERENGETI LITE kati ya Klabu za Simba Queens na Yanga Princess ambazo zinatarajia kukutana kwenye mchezo utakaochezwa Jumapili, Januari 13,2019.Kushoto kwake ni Afisa masoko wa kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Bw. George Mango na kulia kwake ni Kocha wa Yanga Princess Hamis Kinonda . 

   
  Afisa masoko wa kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza mchuano wa ligi kuu ya soka la wanawake ya SERENGETI LITE kati ya Klabu za Simba Queens na Yanga Princess ambazo zinatarajia kukutana kwenye mchezo utakaochezwa Jumapili, Januari 13,2019.Kulia kwake Mwenyekiti wa Kamati ya Mpira wa Wanawake, Amina Karuma na kushoto kwake ni Kocha wa Simba Queens Omari Mbweze. 

  Nahodha wa Simba Queens Mwanahamis Omar akiongea na waandishi wa habari jinsi walivyojiandaa na Mchezo huo wa watani wa jadi hapa nchini Klabu za Simba na Yanga zinatarajia kukutana kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite utakaochezwa Jumapili, Januari 13,2019

  0 0


  Naibu Waziri wa Maji  Jumaa Aweso anaendelea na ziara yake ya kikazi Mkoani Kagera akiwa tayari amemaliza Ziara ya kutembelea, Kukagua na Kuzindua Miradi ya Maji ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba mnamo  Januari 11,Magufuli Mh. Aweso ametembelea na kukagua mradi wa Maji katika Kata ya Ibwera eneo la Rugaze ambapo mradi huo tayari unafanya kazi na unauwezo wa kuhudumia Wananchi 500 wa Vijiji jirani.

  Kisha Mh. Aweso ameendelea na Ziara hiyo katika kata ya Kibirizi ambapo ameweza kuzindua Mradi mpya wa Maji wenye zaidi ya Shilingi Milioni 500. Mradi huo uliopo katika Kijiji cha Kibirizi umeanza kuhudumia takribani vitongoji 10 kati ya 14 vinavyopatikana ndani ya Kijiji hicho na huku juhudi zikiendelea kufanyika kuwafikia wananchi wengine.

  Kwa upande mwingine mradi wa Maji Kijiji cha Kyamulalile na Mashule kwa sasa haufanyi kazi kutokana na athali ya tetemeko licha ya kuwa tayari Halmashauri imekwishatenga zaidi ya shilingi milioni 80, kwa ajili ya Ukarabati na tayari mkandarasi ameanza upembuzi yakinifu.

  Naibu Waziri Aweso ameendelea kuwaomba wananchi kutunza na kulinda miradi hiyo, huku pongezi nyingi zikimmiminikia Mh. Rais John Pombe Magufuli na Serikali yake jinsi anavyoendelea kupambana na adha hii ya Maji, na sasa akina asilimia kubwa ya akinamama hawatembei tena mwendo mrefu kufuata Maji na kampeni ya kuwatua Ndoo vichwani inaendelea.
   Pichani kati ni Naibu Waziri wa Maji  Mh.Jumaa Aweso akiwa na baadhi akibeba ndoo kichwani kuashiria uzinduzi wa Maji katika Kijiji cha Kibirizi, Halmashauri ya Bukoba,ambapo pia ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa kampeni ya kumtua Mama Ndoo ikiendelea kutekelezwa mkoani Kagera.Mh.Aweso anaendelea na ziara yake ya kikazi Mkoani Kagera akiwa tayari amemaliza Ziara ya kutembelea, Kukagua na Kuzindua Miradi ya Maji ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba  
   Pichani jiwe la msingi Kijiji Kibiri
  Naibu Waziri wa Maji  Jumaa Aweso akitoka kuzindua mradi wa maji kijiji cha Kibirizi,Bukoba mkoani Kagera,Mh Aweso anaendelea na ziara yake ya kikazi Mkoani Kagera akiwa tayari amemaliza Ziara ya kutembelea, Kukagua na Kuzindua Miradi ya Maji ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba ,ambapo pia ametembelea na kukagua mradi wa Maji katika Kata ya Ibwera eneo la Rugaze,ambao tayari unafanya kazi na unauwezo wa kuhudumia Wananchi 500 wa Vijiji jirani.

  0 0
 • 01/11/19--23:53: Waziri Biteko Aanza kazi

 • Waziri wa Madini Doto Biteko (katikati) akieleza jambo wakati wa kikao cha Menejimenti ya Wizara na Taasisi zake. Kulia ni Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo na kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara, Prof. Simon Msanjila.
  Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akizungumza jambo wakati wa kikao hicho.
  Baadhi ya Watendaji wa Wizara na Taasisi wakifuatilia kikao hicho
  Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Prof. Idris Kikula akizungumza jambo katika kikao hicho.  ……………………
  Waziri Biteko aanza kazi
  Awataka watumishi kufanyia kazi maagizo ya Rais Magufuli
  Amshukuru Waziri Kairuki kuwa, amemfundisha Mengi
  Aitaka STAMICO kuanza kutoa gawio kwa Serikali  Waziri wa Madini Doto Biteko amekutana na Menejimenti ya Wizara ya Madini, Taasisi zake pamoja na Wenyeviti wa Tume ya Madini na Bodi ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), jijini Dodoma, katika kikao ambacho pia kimejadili namna ya kutekeleza maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli aliyoyatoa wakati akimwapisha Waziri Biteko kushika wadhifa huo Januari 9, 2019.

  Biteko amewataka watumishi wa Wizara na Taasisi zake ambao hawayajayasikiliza maagizo yaliyotolewa na Rais Magufuli kuhakikisha kuwa wanayasikiliza ili kuweka uelewa wa pamoja na kushirikiana katika kutekeleza majukumu ya wizara kwa lengo la kuhakikisha kwamba sekta ya madini inaimarika.

  “ Tuliulizwa dhahabu inauzwa wapi? Basi tusisubiri tena Rais atuulize inauzwa wapi,” amesisitiza Biteko. Aidha, amesisitiza kuwepo kwa ushirikiano wa pamoja miongoni mwa watumishi wa wizara katika utekelezaji wa majukumu hayo na kusisitiza kuhusu mabadiliko yanayoonekana kupitia sekta ya madini ikiwemo kufanya kazi na kuongeza kuwa, “ Kinachotuunganisha mahali hapa ni kazi na wala si dini ama jambo lingine,”.

  Ameongeza kuwa, kiu kubwa ya Rais Magufuli ni kuona kuwa watanzania wote wananufaika na rasilimali madini huku akisisitiza kuwa, kiu yake binafsi ni kuona taswira nzuri inajengeka kuhusu sekta hiyo ikiwemo kufanya kazi kwa weledi na kuongeza kuwa, matokeo bado hayaonekani.

  “Vipaji mlivyonavyo mvitumie vizuri vitoe matokeo yanayoonekana. Fanyeni kazi ambazo zitaacha matokeo yatakayo dumu. Natamani ningezungumza na watumishi wote ili kila mmoja aelewe kile ninachosema,” amesisistiza Biteko.

  Vilevile, amewataka watendaji kuchukua hatua badala ya kutumia muda mrefu kutafuta miongozo wakati wanapotekeleza majukumu jambo ambalo linachelewesha utekelezaji wa majukumu. “ Unasubiri mwongozo gani ilhali unayo Sheria ya Madini?amehoji Waziri Biteko. Pia, amechukua fursa hiyo kumshukuru aliyekuwa Waziri wa Madini Angellah Kairuki na kueleza kuwa, ni kiongozi ambaye amemfundisha mambo mengi.

  “ Namshukuru sana dada yangu, rafiki yangu Angellah. Alinipokea vizuri sana. Hakuna ushirikiano nilioukosa kwake. Amenifundisha mengi ikiwemo kukaa kwenye kikao na kujadili mambo kwa kina,” amesema Biteko. Pamoja na hayo, Biteko ametumia fursa hiyo kumshukuru Naibu Waziri Nyongo kwa kuwa naye pamoja katika kipindi chote ambacho alikuwa Naibu Waziri katika wizara ya madini.

  Katika hatua nyingine, Waziri Biteko ameitaka STAMICO kuhakikisha kuwa, inaanza kutoa gawio kwa Serikali na ikiwezana, jambo hilo lifanyike kabla ya mwaka ujao wa fedha. Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, awali akizungumza katika kikao hicho, amewataka watumishi ambao hawakupata fursa ya kusikia maagizo ya Rais Magufuli kufanya hivyo ili kila mmoja asimame kwa lengo moja.

  “ Hatukusemwa vizuri. Nchi nzima imesikia na dunia imesikia. Tukiendelea hivi, hatutavumiliwa,” amesisitiza Nyongo. Pia, ameitaka Tume ya Madini kuhakikisha inazingatia na kutekeleza maagizo yaliyotolewa na Rais Magufuli ikiwemo kutekeleza wajibu wao.

  Awali, akizungumza katika kikao hicho, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Profesa Simon Msanjila amesema kwamba, kikao hicho ni cha kwanza na Waziri Mpya ikiwemo Mjumbe wa Bodi ya STAMICO na kuongeza kuwa, kinalenga kutoa utambulisho rasmi wa Waziri Mpya wa Madini na kusikia maelekezo ya Waziri Biteko kufuatia maagizo yaliyotolewa na Waziri.

  Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya STAMICO, Meja Jenerali Mstaafu Michael Isamuhyo amemweleza Waziri Biteko kuwa, anayapokea majukumu yote yaliyo mbele yake ya kuhakikisha kwamba shirika hilo linatekeleza majukumu yaliyo mbele yake.

  Kikao hicho kimefanyika tarehe 11 Januari, 2019

  0 0

  Na Ripota Wetu,Globu ya jamii


  MKUU wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Kizigo amezungumzia ziara ambayo imefanywa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Ufundi Dk. Leonard Akwilapo ambapo ameshukuru kwa kuchangia ujenzi wa madarasa manne kwa shule za sekondari Wilaya ya Namtumbo.

  Ambapo Kizigo amefafanua mchango huo umekuja wakati muhimu hasa kwa kuzingatia kwamba mwaka huu wanatarajia kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza wengi, hivyo kusababisha uhaba wa vyumba vya madarasa.

  Akizungumzia ziara ya Katibu Mkuu huyo, leo Januari 12,2018 Kizigo amesema alianza ziara kwa kutembelea semina ya mafunzo iliyohusisha Waalimu wakuu wa shule zote za Msingi 110 zilizopo wilaya ya Namtumbo. 

  "Semina hiyo ilihusu mafunzo ya jinsi ya kutumia mfumo mpya wa takwimu unaolenga kusaidia kuwa na takwimu sahihi za shule za msingi nchini," amefafanua.

  Aliwahimiza wazingatie mafunzo hayo ili iwe rahisi kwao kuutumia mfumo huo mpya.Pamoja na hayo aliwatia moyo na kuwataka wachape kazi kwani wao ndio wahandisi wanaotengeneza wataalam wa kila kada nchini.

  Kizigo amewema Katibu Mku pia alitembelea Shule ya sekondari Nasuli ambapo akiwa hapo alipokea taarifa ya shule na kukagua majengo (Hostel na madarasa) yaliyojengwa kwa fedha za mradi wa EP4R. 

  Pia alipata nafasi ya kusalimia wanafunzi wa kidato cha sita mchepuo wa CBG na kuwahusia wazingatie masomo na baada ya hapo wakaenda kutembelea chuo kipya cha Ufundi VETA Namtumbo ambacho kimekamilika kwa asilimia 100 kwa awamu ya kwanza.

  "Katibu Mkuu alionyesha kuridhishwa na ujenzi wa chuo hicho.Ammpongeza mkandarasi kwa kumaliza kujenga kwa," amesema Kizigo wakati anazungumzia ziara hiyo ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Ufundi Dk. Leonard Akwilapo sambamba na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo ,Sophia Kizigo (kushoto kwake) na viongozi wengine waandamizi wakitembelea maeneo mbambali ya chuo kipya cha VETA Namtumbo,ambapo chuo hicho kimekamilika kwa 100% kwa awamu ya kwanza. 
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Ufundi Dk. Leonard Akwilapo sambamba na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo ,Sophia Kizigo wakipata maelezo kutoka kwa mkandarasi wa ujenzi wa chuo hicho kipya cha VETA ndani ya Wilaya ya Namtumbo,ambacho kimekamilika kwa asilimia 100 
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Ufundi Dk. Leonard Akwilapo sambamba na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo ,Sophia Kizigo wakipata maelezo kutoka kwa mkandarasi wa ujenzi wa chuo hicho kipya cha VETA ndani ya Wilaya ya Namtumbo,ambacho kimekamilika kwa asilimia 100 .
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Ufundi Dk. Leonard Akwilapo akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo ,Sophia Kizigo alipokuwa akielezea jambo kuhusu chuo kipya cha VETA Namtumbo
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Ufundi Dk. Leonard Akwilapo alitembelea shule ya sekondari Nasuli kupokea taarifa ya shule na kukagua majengo (Hostel na madarasa) yaliyojengwa kwa fedha za mradi wa EP4R. 
  Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mh.Sophia Kizigo akisoma taarifa ya idara ya Elimu wilaya ya Namtumbo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Ufundi Dk. Leonard Akwilapo,ambapo pia alitumia nafasi hiyo kufafanua mambo mbalimbali yanayohusu elimu katika wilaya hiyo.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Ufundi Dk. Leonard Akwilapo akisalimiana na baadhi ya Wafanyakazi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo,Mh Sophia Kizigo pichani kushoto mara baada ya kuwasili kwenye ofisi hizo.

  0 0

  Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

  SHIRIKISHO la Vyama vya Wachimbaji wa Madini nchini (FEMATA) limefanya ziara ya kutembelea wachimbaji wa Mkoa Dar es salaam na Pwani ambapo wametumia nafasi hiyo kutoa elimu kwa wachimbaji pamoja na kusikiliza kero na kutatua.

  Ziara hiyo iliongozwa na Rais wa FEMATA John Bina akiwa ameambatana na uongozi wa chama cha wachimbaji Mkoa wa Dar es salaam na Pwani (DARCOREMA) ambapo pia ujumbe huo ulitembelea wadau wa sekta ya madini wakiwemo wazalishaji na wasambazaji wa vifaa vya wachimbaji vikiwemo Baruti na mitambo ya inayotumiwa na wachimbaji.

  Kwa mujibu wa Bina wachimbaji kupitia vyama vyao hawana budi kutatua changamoto zao kupitia meza ya mazungumzo baina hao na Serikali.

  Mojawapo ya kero zilizoonekana kukithiri Kwa wachimbaji ni pamoja na wengi wao kukosa mitaji na hivyo kulazimika kuingia ubia na wawekezaji wa Nje makubaliano ambayo Mara nyingi ukosa usawa kibiashara.

  Pia Bina amesema tayari shirikisho limeandaa mpango wa namna ya kuwasaidia wachimbaji kutatua changamoto hizo.
   Pichani kati aliyevaa suti nyeusi ni Rais wa FEMATA akiwa wizarani akizungumza na viongozi wa chama cha wachimbaji Mkoa wa  Dar es salaam na Pwani. 
   Baadhi ya viongozi wa Shirikisho la wachimba madini nchini wakipata maelezo baada ya kufanya ziara ya kuwatembelea wachimbaji wa madini Mkoa wa Dar es Salaam
    Baadhi ya viongozi wa Shirikisho la wachimba madini nchini wakiwa kwenye moja ya eno la uchimbaji madini wakipata maelezo kwenye ziara yao kuwatembelea wachimbaji wa madini Mkoa wa Dar es Salaam.

  0 0

  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi, Mhe. Rwegasira Mukasa Oscar (kushoto) akiwakaribisha wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi katika kikao na uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Bunge Dodoma tarehe 11 Januari 2019. 
  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro aliongoza ujumbe wa Wizara katika kikao na Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Bunge Dodoma tarehe 11 Januari 2019. Wengine katika picha, kuli ni Bw. Hamid Mbegu, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu na kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani, Bw. Japahary Kachenje. 
  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro aliwasilisha taarifa mbili katika kikao hicho. Taarifa ya kwanza ilihusu hatua zinazochukuliwa na Wizara katika mapambano dhidi ya Ukimwi na taarifa ya pili ilihusu namna Wizara inavyoshirikiana na mashirika ya kimataifa, kikanda na nchi mbalimbali katika kukabiliana na biashara haramu ya dawa za kulevya. 
  Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi na uongozi wa Wizara ukisikiliza kwa makini taarifa zilizokuwa zinawasilishwa na Mhe. Naibu Waziri. 
  Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi walioshiriki kikao hicho. 
  Mhe. Amina Mollel, Mbunge wa Viti Maalum akichangia jambo wakati wa kikoa kati ya Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi na Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 
  Mhe. Masoud Abdallah akichangia jambo katika kikao hicho. 
  Ujumbe wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ulioshiriki kikao kati ya Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi na uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje. 
  Sehemu nyingine ya Ujumbe wa Wizara ulioshiriki kikao hicho. 
  Waheshimiwa Wabjumbe wa Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi wakisalimiana na Mhe. Naibu Waziri kabla ya kikao kuanza. 
  Mhe. Allan Kiula, Mbunge wa Iramba Mashariki akisalimiana na Mhe. Naibu Waziri. 
  Mheshimiwa Mbunge akibadilishana mawazo na Mhe. Naibu Waziri kabla ya kuanza kikao. 
  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Joyce Kimey akiongea machache na Mhe. Naibu Waziri kabla hawajaingia katika kikao na Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi.

  0 0

  NA. MWANDISHI WETU
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama amewataka watendaji wa kiwanda cha Viatu na bidhaa za ngozi cha Karanga Wilaya ya Moshi Mkoa wa Kilimanjaro kuzalisha bidhaa zenye ubora na kuendana na Soko lililopo nchini.

  Ametoa kauli hiyo alipotembelea kiwanda hicho mwishoni mwa wiki ili kukagua shughuli za uendeshaji wa kiwanda hicho na kujiridhisha na ubora wa bidhaa zinazozalishwa. “Niwatake watendaji kuweka mikakati madhubuti ya kuendelea kutengeneza bidhaa zenye ubora kwa kuzingatia viwango vinavyotatiwa”, Mhagama

  Aidha Waziri aliwaasa watendaji wa kiwanda hicho kuendelea kutatua changamoto zinazowazunguka za kimfumo kwa kuzingatia sheria na taratibu za uendeshaji wa kiwanda hicho ili kuendana na ukuaji wa teknolojia na ushindani ulipo. “Nisingependa kuona kiwanda kinakwama kuzalisha bidhaa zenye ubora, hivyo ni vyema kuzingatia sheria na kanuni za uendeshaji wa kiwanda katika ufanisi wa hali ya juu”,alisisitiza mhagama.

  Waziri alieleza kuwa, ili kuwa na wateja wa uhakika ni vyema kutumia mbinu za kujitangaza juu ya shughuli na bidhaa zinazozalishwa kwa kutumia vyombo vya habari ili kuendana na soko lililopo nchini. Aidha waziri alieleza Mpango mkakati wa ujenzi wa kiwanda kikubwa cha Taifa katika eneo hilo la Gereza la Karanga na tayari eneo limetengwa kwa ajili ya ujenzi na kuboresha kiwanda kilichopo ili kuongeza uzalishaji kwa wakati na ubora unaotakiwa.

  “Uwekezaji unalenga kuboresha kiwanda cha zamani kutoka kuzalisha pair 150 kwa siku na kuzalisha pair 400 kwa siku ingawa mpango mkakati uliopo ni kuwa na kiwanda kikubwa kitakachozalisha pair 4000 kwa siku”,alisisita Waziri Mhagama.

  Naye Kaimu Mkuu wa Kiwanda hicho, Shalua Magandi alibainisha faida zinazotarajiwa kutokana na mradi wa kiwanda hichi ni pamoja na  uzalishaji wa ajira 5000 za moja kwa moja na zaidi ya ajira 4000 kutokana na shughuli za uzalishaji nchini, kuongeza Kodi kwa Manispaa, kuongeza uzalishaji wa bidhaa za ngozi, kuongeza manufaa kwa mkoa pamoja na mikoa inayozunguka kwa kuboresha mfumo wa maisha na kuongeza kipato kwa wananchi.

  Kwa upande wake Afisa masoko wa kiwanda hicho Bw. Fredrick Njoka aliwataka Watanzania kuendelea kununua viatu vinavyotengenezwa kwa bidhaa za ngozi kwa kuzingatia ubora na bei nafuu kwa kuwa kiwanda hicho kinatumia mashine za kisasa kutoa nchini Italia ambao ndiyo wenye ujuzi wa hali ya juu na teknoloji ya kisasa ya utengenezaji wa mashine hizo.

  “Wananchi msiogope kututembelea na kununua bidhaa zetu kwa kuzingatia zina ubora wa na bei nafuu, na tunapokea mahitaji ya kila aina kulingana na uhitaji wa wateja wetu”,alisema Njoka. Naye Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba alieleza namna watakavyotekeleza maagizo ya waziri pamoja na kuhakikisha usimamizi mzuri wa shughuli za serikali.

  “Nikushukuru kwa ziara yako inatukumbusha kuendelea kusimamia utendaji wenye tija kwa watumishi wa Serikali pamoja kuhakikisha kiwanda hiki kinazalisha bidhaa bora na kulingana na mahitaji ya wateja”, alisema Warioba. Kiwanda cha viatu cha Gereza Kuu Karanga, Moshi kilizinduliwa rasmi Juni 3, 1977 na Rais wa awamu ya kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Baba wa Taifa Mwalimu, Julius Kambarage Nyerere.Awali kilikuwa na ubia na Mfuko wa hifadhi ya jamii wa PPF ambapo baada ya mabadiliko ya kuunganishwa kwa mifuko hiyo , kwa sasa kina ubia na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PSSSF.
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akisalimiana na baadhi ya watendaji wa Kiwanda cha Viatu cha Gereza la Karanga lenye ubia na Mfuko wa hifadhi ya Jamii wa PSSSF alipofanya ziara kiwandani hapo Januari 09, 2019 Wilaya ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro.
   Kaimu Mkuu wa Kiwanda cha Viatu cha Karanga, Shalua Magandi akisoma taarifa ya kiwanda hicho kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama alipotembelea kiwandani hapo.
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akipokea maelekezo ya namna viatu vinavyopachikwa soli kutoka kwa Fundi Mkuu Msaidizi Kiwanda cha viatu Gereza la Karanga, George Komba wakati wa ziara yake katika kiwanda hicho kilichopo Moshi mkoani Kilimanjaro.
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akipokea maelekezo kuhusu moja ya kiatu kilichotengenezwa kwa ngozi kutoka kwa Afisa Masoko wa kiwanda cha Viatu cha Karanga Bw. Fredrick Njoka wakati wa ziara yake kiwandani hapo.
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akipokea maelezo kutoka kwa Fundi idara ya ushonaji Charles Botto kuhusu malighafi zinazotumika kutengeneza viatu vya ngozi katika kiwanda cha Viatu cha Gereza la Karanga.
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiangalia viatu vilivyotengenezwa kiwandani hapo.
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa katika ziara kiwanda cha Viatu na bidhaa za ngozi cha Gereza la Karanga Wilayani Moshi Mkoa wa Kilimanjaro.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa kiwanda cha viatu cha Karanga na watendaji wa Mfuko wa Hifadhi wa PSSSF na Ofisi ya Mkoa wa Kilimanjaro mara baada ya kumaliza ziara yake katika kiwanda hicho.Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)


  0 0

   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti  wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwapungua Mkono Wananchi akiwa katika gari Maalum ya Jeshi la Wananchi Tanzania JWTZ, wakati akiingia katika Uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba kuhudhuria Maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar, akiwa Mkuu wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar, Brigedia Jenerali Fadhil Omar Nondo.
   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akipokea shatu ya Gwaride rasmin la maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar, yaliofadhimishwa kisiwani Pemba katika Uwanja wa Gombani.

   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mkuu wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar, Brigedia Jenerali Fadhil Omar Nondo, alipowasili katika viwanja vya Gombani Kisiwani Pemba, kuhudhguria Maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Ali Mohamed Shein, akikagua Gwaride rasmin la Sherehe za Mapinduzi kuadhimisha Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika Uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba. leo (Picha na Ikulu)
   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Ndg.Phillip Mangula, alipowasili Jukwaa kuu baada ya kukagua gwaride rasmin la sherehe za Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar, zilizofanyika Uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba leo.
   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Rais Mstaaf wa Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume, alipowasili jukwaa kuu la Viongozi baada ya kumaliza kukagua gwaride rasmin la sherehe za Mapinduzi katika Uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba leo.
   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akiwa katika Jukwaa Kuu akizungumza na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.na Viongozi wa Serikal na Vyombo vya Ulinzi na Usalama.
   VIJANA wa CCM wakipita mbele ya Jukwaa Kuu la Mgeni Rasmin Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi wakiwa katika maandamano wamebeba picha za Viongozi.
   VIJANA wa Payunia wakipita mbele ya Mgeni rasmin Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, wakitowa heshima, wakati wa hafla ya Maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar, yalioadhimishwa katika uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba.
   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwapungia Wananchi wakipita katika jukwaa kuu kwa maandamano maalum yalioandaliwa kwa ajilin ya kuadhimisha Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  WANANCHI wakipita katika jukwaa kuu wakiwa na ngoma ya beni wakati wa maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(Picha na Ikulu)

  0 0

  WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewaonya madaktari nchini kuacha tabia za kuwa madalali wa maduka ya dawa kwa kuwaandikia wagonjwa dawa mara mbili mbili huku akiwaambia kwamba watakaobainika watachukuliwa hatua kali. 

  Huku akiagiza hospitali za Rufaa kote nchini kuhakikisha zinakuwa na maduka ya dawa litakalokuwa na uhakika wa dawa zote muhimu ili kuondosha kero hiyo na kuondoa mianya ya madaktari kudalalia dawa kwenye maduka binafsi. 

  Ummy ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani wa Tanga aliyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo na kauli hiyo inatokana na kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wananchi ambao walimsimamisha nje ya hospitali hiyo kabla ya kukutana nao. 

  Wananchi hao ambao walikuwa wakisubiri kuingia hospitalini hapa walimueleza kero hiyo ambapo alisema mbali na kero hiyo aliwaagiza madaktari nchi nzima kuhakikisha wanazingatia mwongozo wa kutoa dawa au matibabu ili kuepusha lawama kwa wagonjwa wa kubadilishiwa dawa na kila daktari. 

  Akiwa kwenye eneo hilo ambalo ni maalumu kwa ajili ya kupumzikia wananchi ambao wanakwenda kuwatazama wagonjwa wao kabla ya kuingia hospitalini hapo ndipo wananchi hao walipoamua kumueleza kilio hicho ambacho kimekuwa kikiwaumiza muda mrefu sana na kumuomba akishughulikie. 

  “Kwa kweli hii sio sawa kabla ya hapa nimepata wasaa wa kuzungumza na wananchi nje ya geti lakini kilio chao kikubwa ni kutokuridishwa na huduma tunazozitoa likiwemo suala la mgonjwa kuandikiwa dawa na kila daktari hii sio sawa naaagiza madaktari acheni kuwa madalali wa maduka ya dawa na sitaki kusikia hili siku nyengine “Alisema Waziri Ummy 

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti mbele ya waziri huyo Mmoja wa wananchi Mussa Jangwa alisema kwamba kwenye hospitali hiyo kumekuwa na changamoto kubwa ambazo wanakumbana nazo ni kila daktari anayeingia wodini anaandika dawa zake. 

  Alisema kwamba hatua hiyo imepelekea kuingi gharama kubwa huduma bado ni changamoto kutokana na kutumia fedha nyingi kutokana na kuwepo kuandikiwa dawa kila wakati na kulazimika kwenda kununua 

  “Mh Waziri tunashukuru kwa kuja na tungeomba viongozi wengine waige mfano wako hapa hospitali ya Bombo kuna tatizo kubwa sana unapo na mgonjwa wodini unapokuja daktari wa kwanza naandika dawa na mwengine akipita anaandika dawa kwenye zamu yake sasa mgonjwa hajui anunue zipo na ghamara zinakwenda “Alisema Mussa. 

  Alisema wakati wanapoandikiwa dawa hizo wanaelekezwa duka la kwenda kununulia huku wakitumia fedha nyingi ndani ya siku nne jambo ambalo limechangia kujikuta wakiwa hawana la kufanya zaidi ya kubaki kuingia gharama zisizokuwa za msingi huku mgonjwa akiwa bado hajatumia akizoandikiwa na hali yake ni mbaya. 

  “Unapozungumzia jambo la afya ni uhai wa binadahamu nichukue fursa hii kukupongeza kutembelea hospitali hii isiwe ni wewe tu viongozi wote wafanye ziara kama wewe huduma za afya bombo bado changamoto kubwa sana “Alisema 

  Naye kwa upande wake Pili Nzoya Alisema wakati mwengine daktari anaweza kupita wodini na kumuandikia mgonjwa dawa nyingi wakati ni za kununua na kila wakati wamekuwa wakifanya hivyo na kupelekea kuwepo kwa usumbufu mkubwa kwao. 

  Awali naye mkazi mwengine Amina Mrisho alimueleza Waziri Ummy kwamba wamekuwa wakiandikiwa dawa wakati bado nyengine walizokuwa nazo hawajazimaliza kitendo ambacho kinawapa wakati mgumu na kujikuta wakiingia hasara. 

  Alisema kwamba jambo ambalo limekuwa likiwashangaza ni kuandikiwa dawa na daktari halafu wanabadilishiwa dawa nyengine jambo ambalo ni hasara kwao huku wagonjwa wao wakiwa kwenye hali mbaya na baadae mgonjwa anafariki. 

  “Kwa mfano Mh Waziri umeandikiwa dawa leo za sh.40,000 kabla haujazimaliza unaandikiwa nyengine hili ni tatizo ambalo limekuwa likituumiza sisi wananchi tunaomba utusaidie “Alisema. 

  Hata hivyo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga (RMO) Dkt Asha Mahita alikiri kuwepo kwa changamoto hiyo lakini walikuwa wanafanya kwa nia njema lakini kama tukiwabaini ambao walikuwa wanafanya kwa nia binafsi tutawachukulia hatua. 
  WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoani Tanga (CCM) akizungumza na watumishi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo wakati wa ziara yake ya Jimbo la Tanga kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Asha Mahita kulia ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo Saidi Nondo.
  Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Asha Mahita akizungumza katika ziara hiyo kulia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu anayefuatia ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo Saidi Nondo.
  Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo Saidi Nondo akizungumza wakati wa ziara hiyo kushoto ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Asha Mahita.
  Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu katikati akiwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga (RMO) Dkt Asha Mahita mara baada ya kuwasili hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo.
  Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu akiwa na Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo Saidi Nondo wakitembelea maeneo mbalimbali kwenye hospitali hiyo 
  Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu akisalimiana na watumishi wa hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo wakati alipowasili kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga (RMO) Dkt Asha Mahita 
  Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu kulia akilakiwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Asha Mahita mara baada ya kuwasili kwenye hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo kushoto ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo Saidi Nondo 
  Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu kushoto akisikiliza malalamiko ya wananchi nje ya geti la Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo kabla ya kukutana na watumishi wa Hospitali hiyo 
  Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu kulia akimsikiliza kwa umakini Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Asha Mahita mara baada ya kuwasili kwenye hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo 
  mmoja wa watumishi akiuliza swali kwa Waziri Ummy 
  Sehemu ya watumishi wa Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo wakimsikiliza Waziri Ummy 

  Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa wa Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo kulia ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga (RMO) Dkt Asha Mahita

  0 0

  Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kigoma

  KAMATI ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Kigoma imeteketeza jumla ya nguo 1947 zinazofanana na sare za jeshi zilizokamatwa kwenye kambi za wakimbizi za Mtendeli na Nduta Wilayani Kibondo.

  Akiongea na wananchi baada ya kuteketeza nguo hizo Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Samson Anga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga alisema kuwa nguo hizo zinazofanana na sare za jeshi ziliingizwa kambini na Mkurugenzi wa shirika Danish refugees council kwaajili ya kugawa kwa wakimbizi katika kambi ya Nduta na Mtendeli Wilayani Kibondo.

  Alisema Viongozi wa serikali ya Wilaya walipata taarifa kutoka kwa mkuu wa makazi ya wakimbizi kuna nguo zimeingizwa kambini zinazofanana na sare za jeshi kwaajili ya kuwagawia wakimbizi kama msaada wa nguo.
  "Baada ya kupata taarifa wakazifanyia kazi kwa haraka na wakafanikiwa kuzidhibiti na hakuna mkimbizi hata mmoja aliyefanikiwa kupewa"alisema

  Anga amewataka wananchi kuacha tabia kutumia nguo zinazofanana na sare za kijeshi kwani ni kosa la kisheria,pia amewataka wale wenye nguo zinazofanana na sare hizo kuzisalimisha katika vyombo vya usalama kama kwenye vituo vya polisi.

  "Ni marufuku kuvaa,kusambaza na kuagiza nguo zinazofanana na sare za jeshi ni kosa la kisheria ukipatikana umevaa au kusambaza utachukuliwa hatua kali za kisheria"alisema.Alisema hatua za awali walizochukua mpaka sasa ni wamefungua jalada la uchunguzi,pia wamemkamata mkurugenzi wa shirika lililoungiza hizo,pia wametekeza nguo hizo.

  Jumla ya vipande 1947 vya nguo zinazofanana na sare ya jeshi zimeteketezwa na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa katika kiwanja cha mpira cha kawawa kilichopo eneo la Ujiji.
  Kamati ya ulinzi na usalama Mkoa wa Kigoma ikiteketeza jumla ya nguo 1947 zinazofanana na sare za jeshi zilizokamatwa kwenye kambi za wakimbizi za Mtendeli na Nduta Wilayani Kibondo. Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Samson Anga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga alisema kuwa nguo hizo zinazofanana na sare za jeshi ziliingizwa kambini na Mkurugenzi wa shirika Danish refugees council kwa ajili ya kugawa kwa wakimbizi katika kambi ya Nduta na Mtendeli Wilayani Kibondo.
  Kamati ya ulinzi na usalama Mkoa wa Kigoma ikishusha shehena ya nguo zipatazo 1947 zinazofanana na sare za jeshi zilizokamatwa kwenye kambi za wakimbizi za Mtendeli na Nduta Wilayani Kibondo,kwa ajili ya kuchomwa moto. 
  Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Samson Anga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari mara baada ya kuongoza zoezi la kuteketeza nguo zinazofanana na sare za jeshi zilizokamatwa katika makambi ya wakimbizi.
  Kamati ya ulinzi na usalama Mkoa wa Kigoma ikishusha shehena ya nguo zipatazo 1947 zinazofanana na sare za jeshi zilizokamatwa kwenye kambi za wakimbizi za Mtendeli na Nduta Wilayani Kibondo,kwa ajili ya kuchomwa moto. 
  Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Samson Anga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga akiongoza zoezi la kuteketeza nguo zinazofanana na sare za jeshi zilikamatwa katika makambi ya wakimbizi.
  Umati wa wananchi wakishuhudia nguo zinazofanana na sare za kijeshi zikiteketezwa na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa katika viwanja vya kawawa eneo la ujiji,mkoani Kigoma

  0 0

   
  Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi, Mhe. Irene Kasyanju (mwenye miwani) akiwa na washiriki wengine katika Maonesho ya Utalii ya Kimataifa yanayofanyika nchini Uholanzi kuanzia tarehe 9 hadi 13 Januari 2019. 
   
  Wageni mbalimbali wanatembelea banda la Tanzania ili kupata maelezo kuhusu vivutio vya uwekezaji nchini 
   
  Banda la Tanzania linatia fora kwa kutembelewa na idadi kubwa ya watu wanaotaka kupata maelezo kuhusu fursa na vivutio vya utalii nchini. 
   
  Wageni katika banda la Tanzania. 
   
  Balozi Kasyanju na washiriki wenzake wakiwa katika badna la Tanzania tayari kuanza kazi ya kuuza vivutio vya utalii nchini Uholanzi. 


  Taasisi za Serikali na kampuni binafsi mbalimbali za utalii zipo nchini Uholanzi kushiriki maonesho ya utalii ya kimataifa kwa lengo la kutafuta fursa mpya za soko la utalii nchini humo.

  Maonesho hayo maarufu kama Holday Fair 2019 (Vakantiebeurs2019) yalianza tarehe 9 Januari na yatakamilika tarehe 13 Januari 2019, hufanyika kila mwaka katika mji wa Utrecht na kushirikisha taasisi mbalimbali kutoka duniani kote.

  Taasisi za Serikali zinazoshiriki ni Bodi ya Utalii Tanznaia (TTB), Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA). Kwa upande wa kampuni binafsi ni into Africa Eco Travel Ltd, Migada Adventures, Mbalaget Tented Camp Ltd, Kili Fair Promotions Ltd, East Africa Camps na Makasa Tanzania Safaris.

  Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi, Mhe. Irene Kasyanju amesema kuwa maonesho hayo ni fursa adhimu kwa nchi kutangaza vivutio vya utalii ambapo kwa mwaka 2019, waandaji kwa mara ya kwanza wametoa nafasi kwa Balozi za nje zilizopo nchini humo kutangaza pia fursa za biashara na uwekezaji.

  Balozi Kasyanju ambao Ubalozi wake unashiriki katika maonesho hayo alieleza kuwa maonesho hayo yataenda sanjari na Vakantiebeurs Travel Congress, Vakantiebeurs Consumer Day na Vakantiebeurs Trade Day ambapo washiriki watapata fursa ya kupeana taarifa muhimu kuhusu mwelekeo na maendeleo ya biashara ya utalii katika maeneo mbalimbali duniani, vivutio vipya pamoja na kufanya biashara.

  Ushiriki wa Tanzania katika maonesho hayo utasaidia washiriki kukutana na wadau na kuanzisha uhusiano wa kibiashara unaotarajiwa kufungua soko la utalii nchini baada ya wadau hao kupata maelezo ya kutosha kuhusu vivutio vilivyopo nchini na faida zake.


  Imetolewa na:
  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
  Dodoma, Tanzania
  11 Januari 2019 

  0 0


  Na Peter Haule, WFM, Kondoa

  WANAFUNZI wote 3,287 waliochaguliwa kujiunga Kidato cha Kwanza katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma, wanatarajia kuanza masomo baada ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango na Mbunge wa Jimbo la Kondoa, Dkt. Ashatu Kijaji, kutoa msaada wa mabati 1080 ya kuezekea vyumba 20 vya madarasa.

  Akikabidhi msaada huo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Bw. Mustapha Semwaiko, Dkt. Ashatu Kijaji, amesema kuwa kipaumbele chake kikubwa ni elimu na anataka kila mwanafunzi aliyefaulu na kuchaguliwa kuendelea na masomo anapata fursa hiyo ya kusoma.

  "Tumeamua kutumia mfuko wa Jimbo, zaidi ya sh. 20m zimetumika kununulia mabati haya na niombe Mkurugenzi wewe ndiye mwenye watendaji mpaka ngazi ya vijiji na vitongoji ambako shule zetu zipo, mabati haya yafikishwe kwenye kila shule ili inapofika mwisho wa mwezi Februari, 2019, watoto wote waanze kusoma" alisema Dkt. Kijaji

  Aidha, Dkt. Kijaji amewapongeza viongozi na wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa kwa jitihada zao za kukuza elimu na kufanikisha Wilaya hiyo kufanya vizuri katika matokeo ya darasa la saba mwaka 2018 ambapo shule nane kati ya kumi zilizofanya vizuri katika Mkoa wa Dodoma, zinatoka Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa.

  "Tunakwenda kwenye Tanzania ya Viwanda, hatuwezi kuwapeleka wanaKondoa wasio na elimu ndio maana tumefanya mapinduzi makubwa katika wilaya yetu kutoka kuwa ya mwisho kielimu katika Mkoa wa Dodoma miaka mitatu iliyopita hadi kuwa na shule 8 zilizofanya vizuri kati ya 10, kimkoa" aliongeza Dkt. Kijaji

  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Bw. Mustapha Semwaiko na Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya wilaya hiyo Bi. Hildegard Saganda, wamesema kuwa msaada huo umekuja wakati muafaka baada ya kuwa na wasiwasi wa namna ya kuwawezesha zaidi ya wanafunzi elfu 3 kupata nafasi ya kuingia kidato cha kwanza kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa uliokuwa ukiikabili Halmashauri ya Wilaya hiyo.

  "Mbati haya yatapelekwa kwenye shule ambazo wananchi wamejenga maboma na zimefikia hatua ya lenta ambazo ni Busi, Kikore, Changaa, Kalamba, Itaswi, Kwadelo, Hondomairo na Loo" alifafanua Bi. Hildegard Saganda

  Kwa Upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kondoa, ameelezea kuridhishwa kwake na namna Ilani ya CCM inavyotekelezwa katika wilaya yake katika nyanja mbalimbali na kumpongeza Dkt. Ashatu Kijaji kwa jitihada zake za kuiletea Maendeleo wilaya hiyo.
  Afisa Elimu Sekondari wa Hamashauri ya Wilaya ya Kondoa, Bi. Hildegard Saganda, akisoma taarifa ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, muda mfupi kabla Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mbunge wa Jimbo la Kondoa, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, kabla ya kukabidhi mabati 1080 yenye thamani ya Sh. milioni 20 yatakayotumika kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa 20 kwa ajili ya wanafunzi wa Kidato cha Kwanza.
  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kondoa Bw. Alhaji Othman Gora, akizungumza jambo wakati Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mbunge wa Jimbo la Kondoa, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji alipokabidhi mabati 1080 yenye thamani ya Sh. milioni 20 yatakayotumika kukamilisha vyumba vya madarasa 20 kwa ajili ya wanafunzi wa Kidato cha Kwanza katika Halmashauri ya Wilaya hiyo. Kulia ni Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb).
  Mabati 1080 yenye thamani ya Sh. milioni 20 yaliyokabidhiwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, yatakayotumika kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa 20 kwa ajili ya wanafunzi wa Kidato cha Kwanza takribani 3287 waliofaulu katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa ambapo kati ya Shule za Msingi kumi bora zilizoongoza kwa ufaulu Mkoani Dodoma kwenye mtihani wa darasa la saba, shule nane zinatoka katika Halmashauri hiyo.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mbunge wa Jimbo la Kondoa, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, akieleza umuhimu wa kuweka kipaumbele katika elimu kwa ujenzi wa taifa wakati akikabidhi mabati 1080 yenye thamani ya Sh. milioni 20 yatakayotumika kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa 20 kwa ajili ya wanafunzi wa Kidato cha Kwanza katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa.
  Naibu Waziri Wizara ya Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kulia), akimkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, Bw. Mustapha Semwaiko (wa pili kushoto), mabati 1080 yenye thamani ya Sh. milioni 20 yatakayotumika kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa 20 kwa ajili ya wanafunzi wa Kidato cha Kwanza katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa.
  Maafisa wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, wakishuhudia kukabidhwa mabati 1080 yenye thamani ya Sh. milioni 20 yatakayotumika kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa 20 kwa ajili ya wanafunzi wa Kidato cha Kwanza katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa.
  Mkurugenzi wa Wilaya ya Kondoa Bw. Mustapha Semwaiko, akimshukuru Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (hayupo pichani) baada ya kukabidhi mabati 1080 yenye thamani ya Sh. milioni 20 yatakayotumika kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa 20 kwa ajili ya wanafunzi wa Kidato cha Kwanza katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa tatu kulia) pamoja na viongozi na maafisa wa Halmashjauri ya Wilaya ya Kondoa wakizungumza jambo baada ya hafla ya kukabidhi mabati 1080 yenye thamani ya Sh. milioni 20 yatakayotumika kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa 20 kwa ajili ya wanafunzi wa Kidato cha Kwanza katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa.(Picha na Peter Haule- Wizara ya Fedha na Mipango).

  0 0


  Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kimataifa Timu ya Simba imefanikiwa kuondoka na ushindi wa kwanza katika Kundi D baada ya kuifunga JS Saoura goli 3-0.

  Simba wakiwa wako katika uwanja wa nyumbani wa Taifa walianza kwa kasi kulisakama lango la JS Saoura na ilichukua dakika 45 kwa Mshambuliaji Emanuel Okwi kuandika bao la kuongoza kwa shuti kali baada ya ‘kuwapinduapindua’ mabeki wa JS Saoura kufuatia pasi ya kiungo Mzambia, Clatous Chama.

  Okwi aliyekuwa katika kiwango cha juu leo, alifunga bao hilo akitoka kukosa bao la wazi baada ya kugongesha nguzo ya juu akiwa tayari amemtoka beki anatazamana na kipa.    

  Simba Walifanya mabadiliko dakika ya 34 wakimtoa Nahodha wake, John Raphael Bocco ‘Adebayor’ baada ya kuumia nafasi yake kuchukuliwa na mshambuliaji mwenzake, Meddie Ksgere kutoka Rwanda. 

  Kipindi cha pili kilianza kwa Simba kurudi na nguvu mpya na kufanikiwa kupata mabao mawili zaidi yote yakifungwa na Kagere Goli la pili akifunga dakika ya 51 akimalizia pasi ya Okwi ambaye mabeki wa JS Saoura na lingine akifunga tena dakika ya 67 kwa mara nyingine akimalizia pasi nzuri ya Okwi.

  Nahodha wa Simba John Bocco amesema mwitikio wa mashabiki Uwanjani umewapa morali kubwa hali iliyowafanya wapate nguvu na kushinda  mabao 3-0 dhidi ya JS Saoura.

  Bocco amesema mashabiki wanaumuhimu na nguvu kubwa wakiwa Uwanjani anafurahi kuwaona namna wanavyokuwa begakwabega na timu yao."Tunachoangalia sisi ni pointi tatu bila kujali nani anafunga na nani anakosa, makosa yapo na kwenye mpira mengi yanatokea ila sapoti ya mashabiki inatupa nguvu ya kupambana," alisema Bocco.

  Mechi nyingine ya Kundi D inachezwa  Saa 4:00 usiku wa leo Uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria kati ya wenyeji, Al Ahly dhidi ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

  Baada ya mchezo wa leo, Simba SC itasafiri kuwafuata AS Vita mjini Kinshasa Januari 19, wakati JS Saoura watakuwa wenyeji wa Ahly Januari 18 nchini Algeria.

  Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Aishi Manula, Nicholas Gyan, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Juuko Murshid, Pascal Wawa, James Kotei, Hassan Dilunga/Muzamil Yassin dk65, Jonas Mkude, John Bocco/Meddie Kagere dk37, Emmanuel Okwi/Shiza Kichuya dk86 na Clatous Chama.
   Moja ya heka heka iliyotokea kwenye lango la JS Saoura wakati Kipa wa timu hiyo, Khaled Boukacem akichuana  na Mshambuliaji wa Simba SC, Emmanuel Okwi wakati akijaribu kutafuta namna kukwamisha mpira wavuni. 
   Mshambuliaji wa Simba SC, Meddie Kagere akishangilia moja ya bao alililofunga kwenye mchezo wa Kundi D la Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya JS Saoura ya Algeria katika mchezo uliopigwa katika dimba la Uwanja wa Taifa jiji Dar es Salaam, Simba iliondoka na ushindi wa bao 3-0
   Mshambuliaji wa Simba SC, Meddie Kagere akishangilia moja ya bao alililofunga kwenye mchezo wa Kundi D la Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya JS Saoura ya Algeria katika mchezo uliopigwa katika dimba la Uwanja wa Taifa jiji Dar es Salaam, Simba iliondoka na ushindi wa bao 3-0
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa akishuhudia mtanange huo baina ya Simba SC dhidi ya JS Saoura ya Algeria, mchezo uliomalizika jioni hii katika Uwanja wa Taifa.
   
   


  0 0

  Timu ya Hospitali ya Taifa Muhimbili tawi la Mloganzila (Mloganzila Sports Club) imeichapa mabao 6-0 timu ya Albino United ya Kibamba, mchezo uliyofanyika leo katika kituo cha michezo cha Jakaya Kikwete Youth Park Kidongo chekundu jijini Dar es salaam.

  Katika mchezo huo bao la kwanza lilifungwa dakika ya 18 kipindi cha kwanza na mchezaji machachari Jamal Msuya kutoka timu ya Mloganzila.
  Wafungaji wa mabao mengine kutoka timu hiyo ya Mloganzila Sports Club ni Ashirafu Katenda, Edger Mtitu na Adam Kingwande wakati magoli mawili yalifungwa na Goodluck Manji.

  Katika mechi hiyo wachezaji wa Mloganzila walionekana kumiliki mchezo na kuhakikisha timu yao inaibuka na ushindi mnono.Hadi dakika tisini timu ya Albino United haikuweza kutikisa nyavu za wapinzani wao ambao ni Mloganzila Sports Club.

  Awali kabla ya kuanza kwa mechi hiyo Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Tawi la Mloganzila Dkt. Mohamed Juma Mohamed amewapongeza wachezaji wote kwa kushiriki mchezo huo wa kirafiki ambao unadumisha umoja na kulinda afya.

  Dkt. Mohamed amewaeleza wachezaji hao kwamba uongozi wa hospitali utaendelea kushirikiana nao bega kwa bega ili kuhakikisha michezo inaendelea kudumishwa.

  Vilevile Hospitali ya Mloganzila imewapatia timu ya Albino United msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo mafuta maalum ya kupaka kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) pamoja na vifaa vya huduma ya kwanza.

  Naye Mwenyekiti wa timu ya Albino United Mohamed Kidunyo ameushukuru uongozi wa hospitali kwa kukubali kushiriki mchezo wa kirafiki sambamba na kuwapatia msaada wa vifaa hivyo ambavyo ni muhimu katika kulinda ngozi zao hasa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino).


  Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili tawi la Mloganzila, Dkt. Mohamed Juma Mohamed akiwasalimia wachezaji kabla ya kuanza kwa mchezo wa kirafiki kati ya timu ya Muhimbili-Mloganzila na timu ya Albino United ya Kibamba jijini Dar es Salaam
  Mchezaji wa timu ya Hospitali ya Taifa Muhimbili tawi la Mloganzila, Jamal Msuya akiifungia timu yake bao la kwanza katika mchezo uliochezwa katika Kituo cha Michezo cha Jakaya Kikwete Youth Park , Kidondo chekundu jijini Dar es Salaam.
  Mchezaji wa Muhimbili tawi la Mloganzila akipiga kichwa katika mchezo muda mfupi baada ya timu yake kufunga bao la kuongoza katika kipindi cha kwanza
  Mmoja wa wachezaji wa timu ya Albino United akikokota mpira baada ya kuwatoka wachezaji wa timu ya Muhimbili tawi la Mloganzila.
  Kapteni wa Timu ya Albino United, Suleiman Mussa akiwapatia maelekezo wachezaji wa timu yake wakati wa kipindi mapumziko.
  Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili tawi la Mloganzila, Dkt. Mohamed Juma Mohamed akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji hao
  Dkt. Mohamed Juma Mohamed akiwapatia wachezaji wa timu ya Albino United msaada wa mafuta maalum ya kupaka kwa watu wenye ulemavu wa ngozi pamoja vifaa vya huduma ya kwanza. Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)

  0 0


  Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi 'Sugu' leo amemvisha pete ya uchumba Happyness Msonga, shughuli iliyofanyika jijini Dar es Salaam ikiambatana na mbunge huyo kutoa mahari.

  0 0


  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  YES We Can!Ndivyo unavyoweza kuuzungumzia ushindi wa timu ya Simba wa mabao 3- 0 dhidi ya timu ya JS Saoura katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Slaam.

  Kabla ya mchezo huo uliofanyika jana jioni ya Januari 12,2019 ,Simba kupitia Msemaji wake Hajji Manara walizundua kampeni ya Yes we can ambayo kwa tafsiri ya Kiswahili inasema Ndio Tunaweza kwa lengo la kuhakikisha wanashinda mchezo huo na ndicho kilichotokea.

  Umahiri,umaridadi wa pasi, akili ya soka na kila aina ya udambwidambwi kwa wachezaji wa Simba ulitosha kuwafanya wachezaji wa timu ya JS Saoura kushindwa kumiliki vema mpira na hivyo wachezaji wa Simba kuonekana kuumiliki kila idara.

  Dakika ya 45 mshambuliaji nyota wa Simba Emmanuel Okwi alipeleka shangwe,nderemo na vifijo kwa Simba na mashabiki wa soka nchini baada ya kupachika bao la kwanza.Uwanja mzima ulizizima kwa shangwe kutoka kwa mashabiki na wapenzi wa Simba .Hivyo wakati wanakwenda mapumziko Simba walikuwa mbele kwa bao moja.

  Katika mchezo huo wachezaji wa JS Saoura walionekana kutohimili stamina za wachezaji wa Simba kwani mara kwa mara walionekana wakianguka.
  Kipindi cha pili cha mchezo huo kilianza kwa kasi huku kwa Simba wakiwa na hamu ya kutaka kuongeza mabao wakati JS Saoura nao wakionekana kutaka kusawazisha.

  Hata hivyo kwa Simba ambao walioonekana kuendelea kulisakama lango la wapinzani wao. Kutokana na kusakata kabumbu vema Simba walifanikiwa kupata mabao mengine mawili kupitia kwa mchezaji wake Medie Kagere.
  Hakika ushindi wa Simba uliwafanya mashabiki wa soka kuwa na furaha ambapo kila aliyeuzungumzia mchezo huo wameonesha kuwa na matumaini na timu hiyo kufanya vema kwenye michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

  Michuzi Blog ilipata nafasi ya kuzungumza na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dk.Harrison Mwakyembe ambapo ameuzungumzia mchezo huo na kwamba ameridhishwa na kiwango cha Simba ambacho wamekionesha uwanjani hapo.

  "Kwa leo mimi ni mshibaki wa Simba,na ikitokea kesho timu yetu nyingine ikacheza na timu ya nje ya Tanzania nitakuwa kwa timu ya nyumbani.Simba wamecheza vizuri sana leo," amesema Waziri Mwakyembe.

  Alipoulizwa anatoa ujumbe gani kwa mashabiki wa soka nchini,Waziri Mwakyembe amejibu kuwa ni vema kuwa na uzalendo na timu za nyumbani zinapocheza na timu za nje."Tuwe wamoja timu zetu zinapocheza na timu kutoka nje.Ndio maana leo nilikuwa naishangilia Simba."

  0 0

  Katibu tawala wa Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Lutambi akifungua kikao kazi cha kuandaa jumbe za kuelimisha jamii kuhusu ukatili dhidi ya wanawake na watoto kulia kwake ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya watoto kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Sebastian Kitiku na wa kwanza kushoto ni Bw. Christopher Mushi Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii.
  Mkurugenzi Msaidizi Idara ya watoto kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Sebastian Kitiku akiongea wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha watendaji wa Mkoa pamoja na Wizara ya Afya kujadili jumbe za kuelimisha jumii kuhusu ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
  Baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha watendaji wa Mkoa pamoja na Wizara ya Afya wanao kaa mjini singida kujadili jumbe za kuelimisha jumii kuhusu ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

  Bw. Christopher Mushi Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii akitoa mada kuhusu Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto.  Na Anthony Ishengoma -Singida

  Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Lutambi amewataka watendaji wa serikali Mkoani Singida kuanzisha vituo vya Mkono kwa Mkono (One Stop Centres) ili waanga vitendo vya ukatili waweze kupata huduma kwa haraka tofauti na sasa wanapokumbana na mlolongo wa taratibu unaochangia kupotea kwa ushaidi.

  Dkt. Lutambi amesama hayo leo mjini Singida wakati wa kikao chake na baadhi ya watendaji wa mkoa wake wanaotengeneza jumbe za kupambana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa kushirikiana na Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii.

  Aidha Dkt. Lutambi amewataka watendaji hao kutengeneza jumbe ambazo zitatoa elimu pamoja na mambo mengine itawawezesha waanga wa ukatili kupata mahali pa kukimbilia ndio maana amewaagiza kuanzisha vituo vya mkono kwa mkono kwa lengo la kuwapatia huduma ya haraka waanga hao.

  Aidha alitaja urasimu na taratibu ngumu zinazojitokeza baada ya muanga wa ukatili kufika katika vituo vya polisi ambapo waanga wanalazimika kufuata PF3 pamoja na kufuata milolongo ya kumuona daktari jumbo ambalo lianasababisha baadhi ya waanga kukata tamaa na wengine kurubuniwa na kubadili mawazo hivyo kuacha vitendo hivyo viendelee kutokea.

  ‘’Muhanga wa ukatili anapofika polisi anadaiwa PF3 akifika hospitali anakuta Daktari wa zamu hayupo na wakati mwingine akifika polisi anaambiwa polisi wako doria jambo linalotoa mwanya wa kushawishiwa na watendaji wasio kuwa waadilifu na hatimaye kubadili mawazo’’. Aliendelea kusema Dkt. Lutambi.

  Aidha Dkt. Lutambi pia amewataka ndugu pamoja na raia wema kushirikiana na madawati ya jeshi la polisi kutokomeza kabisa vitendo vya ukatili kwa kutoa ushaidi mahakamani kwani kesi nyingi mahakamani zinakwama kutokana na kukosa ushahidi.

  Kwa mantiki hiyo basi mewataka watendaji hao kuweka mifumo imara itakayowezesha watendaji na waanga wa ukatili kufanikisha kukomesha vitendo vya ukatili sio tu kwa Mkoa wa Singida bali pia Tanzania nzima.

  Wakati huo huo Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Watoto kutoka Wizara ya Afya, Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Sebastian Kitiku wakati akiongea na vyombo vya habari ameutaja Mkoa wa Singida kuwa ni miongoni mwa mikoa mitano Nchini Tanzania inayoongoza kwa ukeketaji.

  Ameitaja mila ya ukeketaji kama mojawaopo ya mila inayopaswa kuachwa kwa kuwa inaacha makovu ya kisaikoloijia kwa mtu anayepata kufanyiwa tohara lakini pia ina madhara katika suala zima la Afya ya uzazi kwani mlengwa anaweza kupoteza maisha wakati wa kujifungua.

  Aidha Mkurugenzi huyo amewataka wananchi mkoa wa Singida kubadilika kifikra na kuacha vitendo vya ukatili ambavyo kwa mazingira ya ulimwengu wa kisasa hayana na nafasi tena.

  Kazi ya kutengeneza ujumbe kwa ajili ya kutokomeza mimba na ndoa za utotoni inaendelea itaendelea katika mikoa yenye takwimu za juu katika ukatili dhidi ya wanawake na watoto ambayo ni mikoa ya Shinyanga, Tabora, Singida na Rukwa.

  0 0

  KAMPUNI Ya usafirishaji abiria ya Moovn Driver kwa kushirikiana na umoja wa madereva wa mtandao (TODA), leo wametoa msaada wa vyakula na mavazi kwa kituo cha watoto yatima cha Maunga kilichopo Hananasifu, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza katika hafla hiyo, Katibu wa Umoja wa Madereva wa Mtandao (TODA), Fredy Peter, amesema kuwa msaada huo umelenga kuwapatia nafuu katika mazingira waliyomo na akatoa wito kwa makampuni na taasisi zingine ziige mfano huo kuwasaidia watu wenye mahitaji, hasa watoto wanaoishi kwenye vituo vya mayatima.

  Baadhi ya wawakilishi kutoka kampuni ya usafirishai abiria ya Moovn Driver wakishirikiana na umoja wa madereva wa mtandao (TODA), wenye T-shirt nyeusi, wakimkabidhi msaada mwanamama Zainab Bakari ambaye ni mlezi wa kituo cha watoto yatime cha Maunga cha Hananasifu, Kinondoni, Dar.
   
  Wakipeana mkono ikiwa ishara ya kufurahia kukutana na watoto yatima.

  0 0


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wapenzi wa mpira wa miguu alipofika kushuhudia Mechi kati ya Simba SC na JS Saoura ya Algeria, kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Januari 12, 2019. Katika mechi hiyo Timu ya Simba ilishinda goli 3-0 dhidi ya JS Saoura.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishangilia goli la pili la Simba, wakati akiangalia Mechi kati ya Simba SC na JS Saoura ya Algeria kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Januari 12, 2019. Timu ya Simba iliibuka mshindi wa goli 3-0 dhidi ya JS Saoura.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, wakati alipowasili kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kushuhudia Mechi kati ya Simba SC na JS Saoura ya Algeria, Januari 12, 2019. Timu ya Simba iliibuka mshindi wa goli 3-0 dhidi ya JS Saoura. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiangalia Mechi kati ya Simba SC na JS Saoura ya Algeria kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Januari 12, 2019. Timu ya Simba iliibuka mshindi wa goli 3-0 dhidi ya JS Saoura.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge Tulia Ackson, wakati alipowasili kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kushuhudia Mechi kati ya Simba SC na JS Saoura ya Algeria, Januari 12, 2019. Timu ya Simba iliibuka mshindi wa goli 3-0 dhidi ya JS Saoura. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

older | 1 | .... | 1775 | 1776 | (Page 1777) | 1778 | 1779 | .... | 1897 | newer