Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1771 | 1772 | (Page 1773) | 1774 | 1775 | .... | 1897 | newer

  0 0

   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiondoa kipazia kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Jengo Jipya la Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, pamoja na Uzinduzi wa Maabara ya Vinasaba.(DNA),hafla hiyo imefanyika maruhubi Zanzibar.(Picha na Ikulu)
   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akikata utepe kuashiria kulifungua Jengo Jipya la Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Maruhubi Zanzibar, kushoto Kaimu Waziri wa Afya Zanzibar, Waziri wa Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Mhe. Rashid Ali Juma.
   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Slim Rashid Juma, akitowa maelezo ya picha ya jengo hilo jipya la Mkemia Mkuu baada ya kulifungua leo rasmin, ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar,
   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mchunguzi wa Maabara ya Vinasaba (DNA) (Genitic Analyzer) Bi. Saide Abdalla Mbarak,akitowa maelezo ya matumizi ya mashine hiyo wakati wa ufunguzi wa Maabara ya Vinasaba (DNA) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Jengo la Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Maruhubi Zanzibar, ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiongozana na Kaimu Waziri wa Afya na Waziri wa Kilimo,Maliasili Mifugo na Uvuvi Mhe. Rashid Ali Juma,wakiongea wakati wakielekea katika eneo maalum kwa ajili ya kuzungumza na Wananchi na Wafanyakazi wa Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali baada ya Uzinduzi wa Jengo Jipya na Maabara ya Vinasaba (DNA) ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  WAFANYAKAZI wa Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali  wakishangilia wakati wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia katika hafla ya Uzinduzi wa Jengo Jipya la Mkemia Mkuu wa Serikali Maruhubi.(Picha na Ikulu) 
   

  0 0

  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  MKOA wa Dar es Salaam umeweka wazi mipango yake ya kuhakikisha ujenzi na ukarabati wa madarasa 622 unakamilika kwa wakati lengo la kufanikisha wanafunzi 31,092 ambao ni sawa na asilimia 47 ya watoto 64,861 waliofaulu katika mkoa huo wanaendelea na masomo yao ya kidato cha kwanza.

  Lengo kuu ni kuhakikisha hakuna mwanafunzi yoyote ambaye ataachwa kwasababu ya kigezo cha uhaba wa madarasa huku Mkoa huo ukisisitiza umejipanga vema katika hilo kwa kuweka mikapango sahihi yatakayofanikisha lengo hilo.

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewaambiwa waandishi wa habari leo kwamba wanafunzi hao wote watakwenda shuleni na kwamba ongezeko la wanafunzi na ufaulu ni matokeo ya mafanikio ya Rais Dk.John Magufuli kutokana na kutengwa kwa fedha zaidi ya Sh.bilioni 29 kila mwezi kwa ajili ya kufanikisha elimu bure na kati ya fedha hizo Sh.bilioni 17.46 zinaenda kwenye elimu ya sekondari.

  "Tayari Serikali imejipanga na tayari tangu Januari 7 mwaka huu shule zote za sekondari 147 zimefunguliwa, hivyo kila mzazi ahakikishe anamuandikisha mtoto ili kuendelea na kidato cha Kwanza,"amesema na kusisitiza wanafunzi, wazazi na walezi wasiwe na wasiwasi kwenye hilo kwani wanaotakiwa kwenda shule wote watakwenda.

  Wakati huo huo Makonda amesisitiza katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba kwa Mkoa wa Dar es Salaam umekuwa kinara kutokana na kufaulisha wanafunzi 64,861 sawa na asilimia 92 ambapo kati ya hao wanafunzi 31,092 walikosa vyumba vya madarasa jambo lililoilazimu Serikali kupambana kuhakikisha kila aliefaulu anaendelea na masomo.

  Ameongeza lengo la ujenzi wa madarasa hayo ni kuhakikisha kila mwanafunzi anatumia fursa ya elimu bure inayotolewa na Rais Magufuli ya kuhakikisha mtoto wa maskini anasoma ili kujikwamua kiuchumi na mwisho wa siku Taifa liwe na wataalamu wa kutosha.Makonda ametumia nafasi hiyo kutoa onyo kwa wanafunzi ambao watabainika kukwepa masomo kwani watachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa kisheria na hivyo wote ambao wamefaulu na wanatakiwa kuingia kidato cha kwanza waendelee na masomo.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh.Paul Makonda akisikiliza kwa makini baadhi ya maswali yaliyokuwa yakiulizwa na baadhi ya Waandishi wa Habari aliyokuwa akizungumza nao leo Ofisini kwake kuhusu mipango yake ya kuhakikisha ujenzi na ukarabati wa madarasa 622 unakamilika kwa wakati, lengo la kufanikisha wanafunzi 31,092 ambao ni sawa na asilimia 47 ya watoto 64,861 waliofaulu katika mkoa huo wanaendelea na masomo yao ya kidato cha kwanza.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh.Paul Makonda akisizungumza mbele ya Waandishi wa Habari leo Ofisini kwake  kuhusu mipango yake ya kuhakikisha ujenzi na ukarabati wa madarasa 622 unakamilika kwa wakati, lengo la kufanikisha wanafunzi 31,092 ambao ni sawa na asilimia 47 ya watoto 64,861 waliofaulu katika mkoa huo wanaendelea na masomo yao ya kidato cha kwanza.

  0 0

  Waziri wa Kilimo, Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza mpango wa serikali kusaini mikataba ya ubanguaji wa korosho wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Bodi ya Korosho (CBT) Mkoani Mtwara, leo tarehe 8 Januari 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
  Waziri wa Kilimo, Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Bodi ya Korosho (CBT) Mkoani Mtwara, leo tarehe 8 Januari 2019.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Prof Siza Tumbo akifatilia mkutano wa Waziri wa Kilimo, Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Bodi ya Korosho (CBT) Mkoani Mtwara, leo tarehe 8 Januari 2019.

  0 0

  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  BENKI Kuu ya Tanzania(BoT) imetoa tangazo kwa umma kupitia tovuti yake (www.bot.go.tz) likiwataka watu na taasisi zote zinazofanya biashara ya huduma ndogo za fedha zilizoko Tanzania Bara (isipokuwa vyama vya ushirika vya
  akiba na mikopo – SACCOS) kutoa taarifa zitakazotumika katika utayarishaji wa Kanuni za Usimamizi wa Huduma Ndogo za Fedha.

  Hayo yamesemwa leo na Meneja Usimamizi wa Maduka ya Fedha na Huduma Ndogondogo za Fedha Victor Tarimu kutoka Kurugenzi ya Usimamizi wa Sekta ya Fedha Benki Kuu ya Tanzania(BoT).Tarimu amesema taarifa hizo zinatakiwa kutumwa Benki Kuu ya Tanzania hadi 31 Januari 2019 na kwamba inatoa ufafanuzi ufuatao kuhusu tangazo hilo kuwa lengo la siyo kuvifunga au kuvibana vikundi vya kijamii kama VICOBA, watu binafsi na taasisi zinazotoa huduma ndogo za fedha kama ambavyo inapotoshwa na baadhi ya watu na mitandao mbalimbali ya kijamii.

  "Bali ni kukusanya taarifa za awali kuhusu huduma hizo, kama amnavyo ilivyoainishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa kupitisha Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018, lengo la
  sheria hiyo ni kuwalinda wadau wote wanaohusika na huduma hizi (watoaji na watumiaji) kwa kuziwekea utaratibu mzuri zaidi wa uwekaji kumbukumbu, uendeshaji na uongozi kwa ujumla," amesema

  Pia kuwalinda wamiliki na watumiaji wa huduma hizo dhidi ya vitendo vinavyoweza kusababisha kupoteza fedha na mali zao, pamoja na
  kuzuia watu binafsi, taasisi na vikundi vya kijamii kutumika kufanya uhalifu ikiwemo utakasishaji fedha haramu.

  Ameongeza kuwa Benki Kuu inafahamu baadhi ya watu binafsi, taasisi na vikundi vinavyotoa huduma ndogo za fedha vikiwemo VICOBA, havina usajili rasmi na hivyo havitambuliki kisheria. "Kwa kutambua hilo, Sheria imeweka kipindi cha mpito cha mwaka mmoja (kuanzia sheria itakapoanza kutumika rasmi) kwa wote wanaojihusisha na utoaji huduma ndogo za fedha, kujipanga ili wawe tayari kusimamiwa pale kanuni zitakapokuwa zimetolewa rasmi.

  "Hivyo, katika kipindi hiki cha mpito, si kosa kwa watu binafsi, taasisi na
  vikundi vya kijamii kutokuwa na usajili rasmi. Aidha, Wadau wote watashirikishwa kikamilifu katikautayarishaji wa Kanuni hizo, na mara zitakapokuwa tayari na kutolewa na Benki Kuu ya Tanzania, maelezo
  zaidi kuhusu usajili yatatolewa," amesema.

  Amesisitiza Benki Kuu inawataka wananchi wote kutokuwa na taharuki na inasisitiza uamuzi wa kusimamia watoa huduma ndogo za fedha umechukuliwa kwa nia njema na kwa faida ya watumiaji na watoaji wa huduma hizi. Aidha, Benki Kuu inautahadharisha umma kujiepusha na taarifa na miongozo inayotolewa kiholela na watu, kampuni na mashirika ambayo yanajitangaza kufanya shughuli za uandikishaji wa watoa huduma ndogo za fedha kwa
  wananchi kwa niaba ya Serikali au Benki Kuu.

  "Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mtu, kampuni au shirika
  lolote litakalojihusisha na vitendo vya kuwakanganya wananchi kwa lengo la kupotosha au/na kujipatia mapato haramu.

  "Tunawahamasisha wananchi kufuatilia taarifa zaidi kuhusu tangazo hili zinazoendelea kutolewa na Benki Kuu katika vyombo mbalimbali vya habari kuhusu usimamizi wa watoa huduma ndogo za fedha Tanzania Bara," amesema Tarimu.

  0 0

  Na Munir Shemweta, WANMM Geita

  Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula amekerwa na makusanyo madogo ya mapato katika halmashauri mbalimbali nchini kupitia kodi ya ardhi.

  Akizungumza na watendaji wa sekta ya ardhi wa Halmashauri za Mji na Wilaya ya Geita jana mkoani Geita alipofanya ziara ya kushtukiza kufuatilia utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa katika halmashauri hizo, Dk Mabula alisema, mapato ya sekta ya ardhi katika halmashauri nyingi hayaridhishi na kueleza kuwa halmashauri nyingi mapato yake yako chini ya asilimia 30.

  Alisema pamoja na halmashauri hizo kuwa na mapato kidogo kupitia sekta ya ardhi lakini watendaji wake hawaoneshi jitihada zozote kuhakikisha wanakusanya mapato ya kutosha kupitia sekta hiyo na hivyo aliwataka watendaji hao kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato kwa kuwa msisitizo wa serikali ya awamu ya tano ni kukusanya kodi.

  ‘’Kwa staili hii tutafika kweli? Mna bahati mbaya sasa watendaji wa sekta ya ardhi katika halmshauri mtakuwa chini ya wizara moja kwa moja na rais amepiga kelele kuhuisiana na kodi ninyi mnarelax’’ alisema Dk mabula.

  Hata hivyo, Dk Mabula aliisifu halmashauri ya Mji wa Geita kwa kukusanya mapato kwa zaidi ya asilimia sitini. Kwa Mujibu wa taarifa ya Halmshauri ya Mji wa Geita, kuanzia mwezi Julai hadi Oktoba 2018, halmashauri hiyo imekusanya jumla ya shilingi 389,699,937.28 kati ya milioni 600,000,000 ilizopanga kukusanya.

  Kwa upande wake Halmashauri ya Wilaya ya Geita kupitia, Afisa Ardhi wake Faraja Kaluwa pamoja na halmashauri hiyo kupewa malengo ya kukusanya milioni 150 lakini kufikia desemba 2018 imefanikiwa kukusanya shilingi milioni 12,480,500 tu.

  Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliwataka wakuu wa idara za ardhi katika halmashauri za Mji na Wilaya ya Geita kutoa ahadi ya utekelezaji maagizo aliyoyatoa na hatua gani zichukuliwe kwao iwapo maagizo hayatatekelezwa kwa wakati.

  Maagizo aliyoyatoa Dk Mabula ni kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato ya kodi ya ardhi, uingizaji viwanja na mashamba katika mfumo wa kielektronik, utoaji hati za ardhi pamoja na utoaji hati za Madai (demand notes) kwa wadaiwa sugu wa kodi ya ardhi.

  Aidha, Dk Mabula ameziagiza halmashauri zote nchini kuhakikisha zinaingiza viwanja na mashamba kwenye mfumo wa malipo kwa njia ya kielektronik na kutaka kasi ya utoaji hati kuongezeka ili kuwawezesha wananchi kiuchumi na wakati huo kuiingizia serikali mapato kupitia kodi ya ardhi.

  Katika hatua nyingine, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula amezitaka halmashauri nchini kuhakikisha zinatoa leseni za makazi katika maeneo yenye nyumba zilizojengwa nje ya urasimishaji na mipango Miji na kueleza kuwa zoezi hizo linatakiwa kukamilika mwezi machi mwaka huu.

  Dk Mabula amezitaka Halmashauri kuanisha maeneo yote ya nyumba hizo na kupatiwa leseni za makazi kwa gharama ya shilingi 5000 sambamba na kuziingiza katika kumbukumbu za halmashauri na kubainisha kuwa leseni hizo ni hatua za kuelekea wamiliki wake kupatiwa hati.
  Naibu waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula akizungumza alipowasili ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita alipofanya ziara katika mkoa huo jana kufuatilia utekelezaji wa maagizo yake kuhusiana na sekta ya ardhi katika halmashauri za Mji na Wilaya ya Geita.

  0 0

  *Manara asema wametumwa na Rais, lazima wachukue ubingwa, wachezaji kutua kesho wakitokea Z'bar

  *Asifu uwezo wa Kocha wao,agusia umuhimu wa kununua jezi kuichangia Klabu yao

  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  KLABU ya Soka ya Simba imesema maandalizi ya mchezo wao dhidi ya JS Saoura ya Algeria Jumamosi ya Januari 12 katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam yanakwenda vizuri ,hivyo imewataka mashabiki ,wanachama wao na wapenzi wa soka kujitokeza kwa wingi na uwanja utakuwa wazi kuanzia saa nne asubuhi.

  Pia imesema kutokana na jukumu ambalo lipo mbele yao la kutumwa nchini kwenye mchezo huo la ligi hiyo ya mabingwa Afrika ,wameamua wachezaji wao waliopo kwenye Kombe la Mapinduzi Zanzibar watarudi kesho kwa ajili ya mechi iliyopo mbele yao.

  Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Msemaji wa Klabu ya Simba Hajji Manara amesema wakati wakijiandaa na mchezo huo wa Jumamosi ,mchezaji wao Eras to Nyoni amepata majeraha wakati wa mchezo dhidi ya KMKM ya Zanzibar.

  Amefafanua jopo la madaktari wa Simba pamoja na madaktari wataasisi nyingine wametoa ripoti kuwa Nyoni anahitaji tiba maalum na mapumziko ya kutosha,kimsingi ni kwamba atarudi uwanjani katikati ya Februari.Kuhusu mchezo wao dhidi ya JS Saoura amesema wanakwenda kucheza na timu kubwa na kwamba lengo lao la kwanza lilikuwa ni kuingia hatua ya makundi na baada ya hapo wanafikiria malengo makubwa zaidi.

  Amesema katika mipango yao ni kuhakikisha wanapata alama tisa nyumbani na uozefu unaonesha wakiwa nyumbani watanapata alama za ushindi huku akizungumzia weledi wa Kocha wao ambaye anajua mechi za Afrika.

  Pia amefafanua wanatambua Rais Dk.John Magufuli amewaagiza Simba kufanya vizuri kwenye michuano hiyo ya Ligi ya Mabibgwa Afrika na wanauhakika watachukua ubingwa mwaka huu.Manara amewahimiza mashabiki wa Simba kuwahi kufika uwanjani mapema badala ya kwenda uwanjani saa nane au saa tisa mchana na kwamba siku hiyo kutakuwa na burudani ya muziki kutoka bendi ya African Stars'Twanga Pepeta'.

  Amesema wamezindua kampeni maalum ya kuhamasisha Wana Simba kuujaza uwanja huo kwa kutumia kauli mbiu ya Yes We Can na wanaamini hakuna kitakachoshindikana kwani Simba ni nguvu moja.Wakati huo huo amewahimiza wana Simba wakaichangia Klabu yao kwa kununua jezi na kuingia uwanjani kwa wingi,wakifanya hivyo hakutakuwa na sababu ya kupitisha bakuli kuchangishana fedha.

  "Tunahamasisha Wana-Simba kununua jezi za timu yao kwa kufanya hivyo watakuwa wamechangia Klabu yao na hilo ni jambo la heshima.

  "Jezi zetu zinauzwa kwa utaratibu maalum na tumejipanga kuhakikisha hakuna wanaofanya hujuma katika uuzwaji wa jezi za Simba,akibainika tutawaambia Polisi wawakamate," amesema Manara.

  0 0

   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikata utepe kufungua jengo jipya la Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia, iliyopo Mbweni Wilayani Magharibi “B” - Unguja Januari 8, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiweka jiwe la msingi wa jengo jipya la Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia, iliyopo Mbweni Wilayani Magharibi “B” - Unguja Januari 8, 2019.
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia kitabu kwenye maktaba ya jengo jipya la Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia, iliyopo Mbweni Wilayani Magharibi “B” – Unguja baada ya kufungua jengo hilo Januari 8, 2019. 
    Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia mfumo wa umeme uliyebuniwa na mwanafunzi Abdulhamid Marijani, baada ya kufungua jengo jipya la Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia, iliyopo Mbweni Wilayani Magharibi “B” - Unguja Januari 8, 2019.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa kitengo cha kompyuta Safaa Haroub, baada ya kuweka jiwe la msingi wa jengo jipya la Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia, iliyopo Mbweni Wilayani Magharibi “B” - Unguja Januari 8, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)  *Asema kukamilika kwa taasisi hiyo kutakuwa na manufaa makubwa kwa jamii

  WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amefungua Jengo la Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia (KIST), wilaya ya Magharibi ‘B’ lililojengwa kwa ghararama ya sh. bilioni 4.2.

  Afungua jengo hilo leo (Jumanne, Januari 8, 2019) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya sherehe za miaka 55 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yaliyotokea Januari 12, 1964.Waziri Mkuu amesema kukamilika kwa Jengo la taasisi hiyo kuna manufaa makubwa kwa jamii ikiwemo kutoa elimu ya ufundi itakayowasaidia vijana kujiajiri na kuondokana na utegemezi.

  “Kusaidia azma ya Serikali ya kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025 na msukumo katika sekta ya viwanda kwa vijana kujiajiri na kuajiriwa katika sehemu mbalimbali pamoja na Serikalini.”Amesema manufaa mengine ya KIST ni kutoa mafunzo ya fani mbalimbali zinazokwenda sambamba na mabadiliko ya ulimwengu katika Nyanja za sayansi, teknolojia na ualimu.

  Kadhalika, Waziri Mkuu ameutaka uongozi wa KIST ubuni mbinu mbalimbali na utafute miradi mingine ya ujenzi itakayosaidia kuwa na miundombinu ya kisasa ya kutolea elimu.Amesema uongozi wa taasisi hiyo hauna budi kuweka mikakati ya kushirikiana na taasisi nyingine zinazotoa mafunzo ya ufundi ndani na nje ya nchi ili kubadilishana uzoefu.

  Waziri Mkuu amesema kulingana na maendeleo ya kiteknolojia na mahitaji ya soko uongozi wa KIST ujipange kutoa mafunzi ya biomedical Engineering na kuimarisha mafunzo ya matengenezo ya ndege na urubani katika ngazi ya stashahada.

  Awali, Waziri wa Elimu na Mafunzi ya Amali, Riziki Pembe Juma alisema Wizara yake itaendeleza taasisi hiyo ili kuwaendeleza vijana na baadae waweze kujiajiri na kuajiri.Alisema vijana wanaohitimu mafunzo ya fani mbalimbali katika taasisi hiyo wanapewa mikopo ya masharti nafuu na Serikali baada ya kujiunga kwenye vikundi.

  Waziri Huyo, alisema wahitimu hao kabla ya kupewa mikopo wanaandika andiko la miradi ambayo watakwenda kuitekeleza ambapo tayari vikundi zaidi ya 10 vya vijana vimeshawezeshwa.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMANNE, JANUARI 8, 2019.

  0 0

  Dkt. Francis Mollel ambae ni Mtaalamu wa Magonjwa ya wakina mama. Picha na Vero Ignatus.


  NA: VERO IGNATUS-ARUSHA.


  Kutokana na wingi wa wakinamama wenye tatizo la ugonjwa wa fistula kuendelea kujitokeza na kupata matibabu katika kituo maalumu cha Kivulini Maternity Center kilichopo wilayani Arumeru mkoani Arusha,imeelezwa kuwa kwasasa idadi ya wagonjwa wa tatizo hilo imepungua kwa kiasi kikubwa mkoani humo

  Akieleza ukubwa wa tatizo hilo daktari Francis Mollel ambae ni mtaalamu wa magonjwa wakina mama anasema kuwa kutokana na elimu ya masuala ya afya ya uzazi kumesaidia kupunguza idadi ya wagojwa wa fistula kwani husababishwa na uzazi pingamizi. Namba ya wagonjwa inaendelea kupungua kutokana na elimu ya afya imekuwa ikitolewa mara kwa mara, uelewa ni mkubwa kwa wagonjwa kwenda hospitali mapema kujifungua kwani tatizo hili la fistula linatokana na uzazi pingamizi. ''Alisema Dkt Mollel

  Dkt. Mollel amesema kuwa wagonjwa wa mwisho waliofanyiwa upasuaji walikuwa 23, na hivi karibuni wanatarajia upasuaji mwingine kufanyika machi 2019 idadi itaongezeka zaidi kwani wanatazamia kuingia kwenye kambi za wakimbizi pia .Katika hatua nyengine mtaalamu huyo amebainisha namna wanavyo wanawafikia na kuwahudumia wagonjwa wanaoishi na tatizo la fistula hususani katika maeneo ya vijijini ambapo amesema kambi ya fistula wanaifanya kila baada ya miezi mitatu.

  Mara nyingi tunawatuma wataalamu wetu kwenda kuwatafuta wagonjwa huko nje, ambapo wakishapimwa na kugundulika kuwa wana fistula yenyewe, tunawalaza, tunawafanyia upasuaji, mgonjwa anakaa hospitalini siku 14 na tunamuangalia kama hana tatizo tena tunamruhusu kurudi nyumbani akiwa ameshapona kabisa. '' Alisema Dkt.

  Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Arusha mrisho gambo ambae ametembelea kituo hicho kwa lengo la kufahamu maendeleo na changamoto za utioaji huduma kwa wagonjwa akatumia fursa hiyo kuahidi kufanyia changamoto zilizo katika kituo hicho ikiwa ni pamoja na changamoto ya hitaji la damu salama pamoja na barabara kufika eneo la kituo.

  ''Changamoto kubwa ya waliyonayo chanjo, damu salama na wametuomba kama mkoa kuwasaidia, pia wana changamoto ya barabara hivyo tumezungunza na Tarura kama wanaweza kutengeneza barabara ya kilometa 1.2''Alisema Gambo

  Mratibu wa TARURA Mhandisi Edward Amboka akiahidi kuanza kufanya tafiti kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo mara moja. Kituo hicho ni maalumu kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa mbalimbali wenye tatizo la Fistula na uzazi hususani wagojwa walio masikini bila gharama yoyote.

  0 0


  0 0

  Naibu Waziri wa Maji Juma Aweso ameliagiza jeshi la polisi mkoani Shinyanga kumkamata mhandisi wa maji Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Sylivester Mpemba kushindwa kusimamia kikamilifu utekelezaji wa mradi wa maji uliogharimu serikali kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni moja.

  Agizo hilo amelitoa  jana Januari 8,2019 wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Mwakitolyo kwenye mkutano wa hadhara ambapo wananchi waliopewa nafasi ya kuuliza maswali walijikita na changamoto ya upatikanaji wa maji kutokana na mradi uliopo kushindwa kutoa maji. Hata hivyo majibu ya mhandisi wa maji Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Sylivester Mpemba yalishindwa kujitosheleza licha ya serikali kutoa fedha kiasi cha shilingi bilioni moja,milioni mia nne na sitini na mbili. 

  Kufuatia kukosekana kwa majibu kuhusu namna pesa hizo zilivyotumika,Aweso alieleza kusikitishwa na ucheleweshwaji wa mradi huo akidai kuna uzembe wa Mhandisi huo hivyo kumwagiza Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko na jeshi la polisi kumkamata mhandisi huyo. 

  “Mradi wa maji Mwakitolyo gharama yake ni shilingi bilioni 1.482 mpaka sasa serikali ya imelipa kiasi cha bilioni 1.462, sisi tunaumia sana wakati mwingine huyu angekuwa daktari si angeshaua watu, mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ita polisi peleka ndani mtu huyu” ,alisema Aweso.

  Waziri Aweso pia alimuagiza kaimu mhandisi wa maji mkoa wa Shinyanga Julieth Payovela kuandika barua ya kujitathmini katika utendaji kazi wake,na kuwaagiza wahandisi wa maji nchini kutembelea na kukagua miradi ya maji iliyopo kwenye maeneo yao na kuhakikisha wananchi wanapata huduma hiyo ili kufikia azma ya kumtua mama ndoo kichwani.

  Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Solwa Ahmed Salum alisema wakazi wa jimbo hilo bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali za miundombinu ya barabara, elimu, umeme na huduma za afya na kuiomba serikali kuwatazama wakazi wa jimbo hilo kwani wanajihisi kutengwa licha ya baadhi ya wataalamu kukwamisha juhudi za serikali kuwapatia wananchi wake huduma bora za kijamii.

  “Jimbo la Solwa ni miongoni mwa majimbo nchini yanayokabiliwa na changamoto lukuki hasa katika sekta ya afya,elimu na miundombinu ya barabara, wananchi hawa hawana pa kukimbilia zaidi ya serikalini kutokana na mapato wanayoichangia serikali katika huduma za kimaendeleo” ,alisema Ahmed. 
  Naibu Waziri wa Maji Juma Aweso akizungumza na wakazi wa kata ya Mwakitolyo kwenye mkutano wa hadhara ili kusikiliza kero zinazowakabili - Picha zote na Malaki Philipo- Malunde1 blog
  Mhandisi wa maji halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Sylivester Mpemba(kushoto) akihojiwa na Naibu Waziri wa Maji Juma Aweso (kulia) kuhusu kushindwa kusimamia mradi wa maji kata ya Mwakitolyo.
  Naibu Waziri wa Maji Juma Aweso akizungumza na kuagiza Mhandisi wa maji halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Sylivester Mpemba akamatwe na polisi . 
  Polisi wakitekeleza agizo la kumshikilia na kumuweka chini ya ulinzi mhandisi wa maji halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Sylivester Mpemba.

   Mhandisi wa maji halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Sylivester Mpemba akiwa chini ya ulinzi.
  Wakazi wa kata ya Mwakitolyo wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea.
  Tenki la maji Mwakitolyo,mradi wa maji ambao umeigharimu serikali kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni moja na mradi haujawanufaisha wananchi.
  Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza na wakazi wa kata ya Mwakitolyo.
  Mbunge wa jimbo la Solwa Ahmed Salum akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wakati wa ziara ya Naibu waziri wa maji Mwakitolyo.
  Wakazi wa Mwakitolyo wakiwa kwenye mkutano.
  Awali Sada Khamis mkazi wa kijiji cha Mwakitolyo akieleza kero ya maji katika eneo hilo mbele ya Naibu waziri wa maji Juma Aweso.
  Mwenyekiti wa kijiji cha Mwakitolyo Nuhu Nshomi akieleza changamoto za elimu,maji na umeme wakati wa mkutano. Picha zote na Malaki Philipo- Malunde1 blog

  0 0

  Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Ephraim Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya Mfumuko wa Bei kwa mwezi Desemba 2018 leo jijini Dodoma.

  Na: Beatrice Lyimo-MAELEZO, Dodoma

  Wastani wa Mfumuko wa Bei wa Taifa kutoka Januari hadi Desemba Mwaka 2018 umepungua hadi asilimia 3.5 kutoka wastani wa asilimia 5.3 kama ilivyokuwa mwaka 2017.

  Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Ephraim Kwesigabo wakati akitoa taarifa kuhusu mfumuko wa bei wa mwezi Desemba 2018 pamoja na wastani wa mfumuko huo kwa mwaka mzima.

  “Wastani huu wa mfumuko wa bei wa mwaka wa asilimia 3.5 ndiyo wastani mdogo kabisa kwa kipindi cha zaidi ya miaka 40 iliyopita ambapo tangu mwaka 1970 mfumuko huo ulikuwa 3.6,” ameongeza Kwesigabo. Aidha, akizungumzia kuhusu mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwezi Desemba ,2018, Kwesigabo amesema kuwa mfumuko huo umeongezeka hadi kufikia asilimia 3.3 kutoka asilimia 3.0 kwa mwezi Novemba 2018.

  “Kuongezeka kwa Mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Desemba, 2018 kumechangiwa hasa na kuongezeka kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi Desemba, 2018 zikilinganishwa na bei za mwezi Desemba, 2017, mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Desemba, 2018 umeongezeka hadi asilimia 1.0 kutoka asilimia 0.4 ilivyokuwa mwezi Novemba, 2018,” amefafanua Kwesigabo.

  Aidha amesema kuwa, baadhi ya bidhaa ya chakula zilizochangia kuongezeka kwa mfumuko wa bei ni pamoja na nyama kwa asilimia 4.6, samaki wabichi asilimia 8.2, dagaa asilimia 26.2, matunda kwa asilimia 4.3 na mbogamboga asilimia 8.5 baadhi ya bidhaa zisizo za chakula zilizochangia mfumuko wa bei ni pamoja na vitambaa vya kushonea nguo kwa asilimia 2.1, nguo za kiume na za kike kwa asilimia 6.1, nguo za watoto kwa asilimia 3.0, sare za shule kwa asilimia 3.1, dizeli kwa asilimia 27.6, petroli asilimia 10.8 na huduma za malazi kwa asilimia 6.8.

  Kwa upande wa nchi za Afrika Mashariki, mfumuko wa bei kwa mwaka unaoishia mwezi Desemba, 2018 nchini Kenya umeongezeka hadi kufika asilimia 5.71 kutoka asilimia 5.58 kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba, 2018 na mfumuko wa bei kwa mwaka unaoishia mwezi Desemba, 2018 nchini Uganda umepungua hadi kufika asilimia 2.2 kutoka asilimia 3.0 kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba, 2018.

  0 0


  United imepangwa kucheza mechi ya ufunguzi dhidi ya Kaimu bingwa wa Ligi Kuu ya Kenya, Bandari FC, katika michuano ya SportPesa Cup inayotarajiwa kutimua vumbi kwa msimu wa tatu mfululizo kuanzia Januari 22-27 katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam.


  Ratiba hiyo iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu, iliwekwa hadharani na waandaaji wa michuano hiyo, kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa ambapo mabingwa mara 27 wa Tanzania Bara, klabu ya Yanga wataumana na mabingwa wa Ngao ya Jamii ya SportPesa, timu ya Kariobangi Sharks kutoka nchini Kenya majira ya saa 10:15 jioni katika mechi ya pili ya siku ya ufunguzi

  Mabingwa watetezi Gor Mahia wataumana uso kwa uso na Mbao FC kutoka jijini Mwanza siku ya Januari 23 majira ya saa nane kamili mchana huku mtanange wa mwisho kwa hatua ya robo fainali ukipigwa kati ya Mabingwa wa Tanzania Bara, Simba SC watakaowavaa AFC Leopards majira ya saa 10:15 jioni.Mitanange ya nusu fainali itapigwa Januari 25 huku mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu ukipigwa January 27 majira ya saa 8:00 mchana ambayo ni siku ya mwisho ya mashindano.

  Nae Mkurugenzi wa Mashindano (TFF), Ndugu Salum Madadi amesema maandalizi yote ya shindano yamekamilika, huku akiwataka mashabiki wa soka nchini kujitokeza kwa wingi uwanjani kushuhudia mechi kali na za kusisimua.Mashindano ya mwaka huu sio ya kukosa kwa kila mpenzi wa soka nchini huku tukiwa na Imani kuwa timu zetu zitafanya vizuri na kubakisha Kombe nyumbani.

  Bingwa wa mashindano atakutana uso kwa uso na timu ya Everton kutoka Ligi kuu ya Uingereza katika mechi ya kirafiki itakayopigwa nchi atakayotoka mshindi. Hii itakuwa ni mara ya pili kwa klabu ya Everton kuzuru Afrika Mashariki baada ya kufanya hivyo mwaka 2017 ambapo walicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Gor Mahia aliyekuwa bingwa kwa mwaka huo.

  “Ratiba hii inatudhihirishia kuwa tutakuwa na wiki ya msisimko wa soka jijini Dar es Salaam. Nipende kutoa rai kwa mashabiki na wapenzi wa soka kuhudhuria uwanjani kwa wingi kuunga mkono maendeleo ya soka la ukanda huu,” alisisitiza Tarimba Abbas, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti SportPesa Tanzania.

  Mashindano ya SportPesa Cup yametajwa na wachambuzi wa soka kuwa jukwaa sahihi kwa wachezaji kupata fursa ya kuonekana kimataifa kama ilivyokuwa kwa mshambuliaji wa zamani wa Gor Mahia, Meddie Kagere and mlinzi Godfrey Walusimbi ambao wameweza kupata ofa kubwa za usajili baada ya kuonesha viwango maridhawa kwenye mashindano yaliyopita ya SportPesa Cup (zamani yakijulikana kama SportPesa Super Cup) yaliyofanyika Juni 2018 mjini Nakuru, Kenya

  0 0

  Na. Vero Ignatus,Arusha


  Vijana nchini Tanzania wametakiwa kuwa wabunifu kwa kubuni bidhaa zinazoweza kuhimili ushindani katika soko la pamoja la Afrika Mashariki ili waweze kunufaika na fursa za uwepo wa soko hilo pamoja na kuboresha maisha yao.


  Hayo yanesemwa na Wawakilishi wa vijana kutoka Majukwaa ya vijana Wilaya ya Arusha katika Mafunzo ya Ujasiriamali yanayolenga kukuza ubunifu na uwezo wa vijana kutumia fursa za kimasoko kujikwamua kiuchumi .

  Farida Charles na Denis George walisema kuwa ,vijana wengi wamekuwa wakijitahidi kubuni bidhaa zao lakini changamoto kubwa bado ipo katika ubora wa hizo bidhaa katika kushindana na soko la Afrika Mashariki.

  Kutokana na changamoto hiyo vijana hao kwa pamoja walijiwekea mikakati ya kuhakikisha kuwa bidhaa zote wanazozalisha ni lazima ziendane na soko la Eac ili kuweza kunufaika na fursa mbalimbali zilizopo na kupata masoko zaidi.

  Mratibu wa shirika la Vijana la Initiative for Youth ,Laurent Sabuni alisema kuwa, vijana wa kitanzania hawapaswi kuwa nyuma katika soko la pamoja la Afrika Mashariki kwani wanapaswa kuungana na kufanya biashara kwa kuvuka mipaka ya nchi na kuzalisha bidhaa bora zinazokidhi viwango vya kitaifa na kimataifa.

  Sabuni alisema kuwa, kumekuwepo na fursa nyingi Sana katika soko la jumuiya ya Afrika mashariki ambazo vijana wanatakiwa kuzichangamkia na kuondokana na dhana ya kulia ukosefu wa ajira, badala yake wajikite katika kuzalisha bidhaa zitakazoendana na soko hilo.

  Afisa Vijana Wilaya ya Arusha, Nimfa Ramadhani alisema kuwa ,Tanzania inaelekea kwenye uchumi wa viwanda, hivyo vijana wana fursa ya kutengeneza bidhaa za viwandani na kuanzisha viwanda vidogo vidogo ili waweze kuendana na kasi ya ujenzi wa viwanda iliyopo.

  0 0


  0 0  Dunia ya sasa ni kijiji, na Ulimwengu wa sasa Unaendeshwa na mitandao ya kijamii.

  Jambo ambalo halikwepeki, bali inabidi tulielewe na kulitumia vizuri, ili liwe na faida kwetu Kwani ni Fursa kwa dunia ya sasa.

  Mitandao ya kijamii inaendesha Kuanzia maisha yetu binafsi , Serikali, Elimu, Uchumi na Mawasiliano mengi ambayo yanaendesha maisha yetu ya kila siku.

  KUKAJAH COMPANY kwa kutambua ilo, imeanzisha mchakato wa kuwashirikisha makundi mbalimbali ya wanachi wa Tanzania hususan Vijana, Weledi wa kutumia vizuri mitandao ya kijamii kwa manufaa yao binafsi pamoja na Taifa kwa ujumla.

  Jumamosi ya Tarehe 12/1/2019 Tutazindua mchakato wetu wa kwanza Mkoani Mbeya pale TUGHIMBE HALL kuanzia saa 5 asubuhi , Mpaka saa 9mchana ( 11am to 3pm).

  WANACHI WOTE MNAKARIBISHWA. HAKUNA KIINGILIO, NI BURE.

  Watoa mada ni Mamlaka ya mawasiliano Tanzania ( TCRA ). Pamoja tujenge Taifa letu. ASANTE cc@kukajahcompany

  0 0

   Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Cornel Muro na Rais wa Kilimanjaro Technology kutoka Marekani Bi Laurel Werner kwa pamoja wakizindua msaada wa matundu 10 ya vyoo vya kisasa katika shule ya msingi Seliani katika kata ya Kimnyaki Wilayani Arumeru
  Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Cornel Muro  akikabidhiwa na Rais wa Kilimanjaro Technology kutoka Marekani Bi Laurel Werner  msaada wa matundu 10 ya vyoo vya kisasa katika shule ya msingi Seliani katika kata ya Kimnyaki Wilayani Arumeru
   Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Cornel Muro,Rais wa Kilimanjaro Technology kutoka Marekani Bi Laurel Werner  na wadau wengine wakikagua msaada wa matundu 10 ya vyoo vya kisasa katika shule ya msingi Seliani katika kata ya Kimnyaki Wilayani Arumeru
   Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Cornel Muro akikagua baadhi ya mabomba ya maji ndani ya vyoo hivyo.
   
   
  Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Cornel Muro ameendelea kuungwa mkono na wadau mbalimbali wa Elimu ambapo Safari hii amepata msaada wa kujengewa Matundu kumi ya choo cha kisasa aina ya Swashi na wadau wa Kilimanjaro Technology kutoka Marekani, msaada wenye thamani ya Shilingi milioni 28.

  Dc Muro ambae Kwa kipindi Cha Miezi mitano tangu kuteuliwa amejipambanua katika kipaumbele Cha ujenzi wa mifumo imara ya Elimu kuanzia ngazi ya Shule Za Msingi na Sekondari amesema Wadau wameendelea kujitokeza kutokana na Kuwa na vipaumbele vinavyogusa kero na changamoto za kijamii ikiwemo Elimu ambapo amesema Wilaya ya Arumeru imeamua kujikita katika Elimu kama mpango endelevu wa Wilaya ambao umeanza kuonyesha mafanikio Kwa kuongoza kimkoa Kwa kushika nafasi ya kwanza katika matokeo ya kidato Cha Pili Mwaka 2018 na nafasi ya Nne kitaifa.

  Akikabidhi msaada huo wa matundu 10 ya vyoo vya kisasa katika shule ya msingi Seliani katika kata ya Kimnyaki Wilayani Arumeru Rais wa Kilimanjaro Technology kutoka Marekani Bi Laurel Werner amesema wameamua kuunga mkono kwa vitendo jitihada za Dc Muro katika kuboresha Sekta ya Elimu ambayo imeanza kuonyesha mafanikio Kutokana na Sera nzuri za Mhe, Rais Dkt. John Pombe Magufuli Kwa kutoa Elimu bure kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari hatua ambayo imewavutia na kuona Kuna haha ya kuunga mkono jitihada za Mhe Magufuli.

  Akizungumza na wazazi Mara baada ya uzinduzi huo Dc Muro amesema ndani ya Wiki mbili zijazo watazindua choo kingine cha kisasa chenye matundu 20 ambacho kimejengwa Kwa ushirikiano wa wananchi, serikali pamoja na wadau wengine wa Maendeleo ikiwa ni jitihada za kukabiliana na changamoto ya kutitia Kwa choo cha shule ya msingi Seliani kata ya Kimnyaki Halmashauri ya Arusha kilichotitia Tarehe 26/08/2018 na kujeruhi mwanafunzi mmoja wa darasa la kwanza


  0 0

  Na Veronica Kazimoto,Dar es Salaam

  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imefanikiwa kukusanya jumla ya shilingi trilioni 7.9 kwa kipindi cha miezi sita ya Mwaka wa Fedha 2018/19 ikiwa ni kuanzia Julai hadi Desemba, 2018 ikilinganishwa na shilingi trilioni 7.8 ambazo zilikusanywa kipindi kama hicho katika Mwaka wa Fedha wa 2017/18.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA Richard Kayombo amesema makusanyo ya mwezi Desemba, 2018 yaliongezeka kuzidi makusanyo ya miezi yote iliyopita kwa mwaka huu ambapo TRA ilikusanya jumla ya shilingi trillioni 1.63.

  “Mbali na makusanyo hayo ya mwezi Desemba, katika mwezi Novemba, 2018 TRA ilikusanya jumla ya shilingi trillioni 1.21 na mwezi Oktoba, 2018, zilikusanywa jumla ya shillingi trillioni 1.29. Nachukua fursa hii kuwashukuru walipakodi wote kwa kuendelea kulipa kodi kwa hiari na wakati”, alisema Kayombo.

  Kayombo aliongeza kuwa, katika kutatua kero na malalamiko mbalimbali ya walipakodi, uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania umeamua kwamba, kila siku ya Alhamisi itakuwa ni siku maalum kwa ajili ya Mameneja wa Mikoa na Wilaya wa TRA kote nchini kuwasikiliza na kutatua changamoto za walipakodi.

  “Pamoja na kutenga siku hiyo maalum, tumeanzisha Kituo cha Ushauri kwa Walipakodi kwa Mkoa wa Dar es Salaam ambacho kipo katika Jengo la NHC kwenye makutano ya Mtaa wa Samora na Bridge kwa lengo la kuongeza ufanisi na kuwa karibu na walipakodi. Tumeanza kwa Dar es Salaam lakini vituo hivi vitaendelea kufunguliwa katika mikoa mingine nchini”, alieleza Mkurugenzi Kayombo.

  Aidha, Kayombo amewakumbusha wamiliki wa majengo kote nchini kulipia Kodi ya Majengo ambayo viwango vyake ni shilingi 10,000 kwa nyumba za kawaida, shilingi 50,000/= kwa kila sakafu ya ghorofa na shilingi 20,000 kwa ghorofa za wilayani na vijijini.

  “Sambamba na kuwakumbusha wamiliki wa majengo kulipia kodi ya majengo, napenda kuchukua fursa hii kuwasisitiza wafanyabiashara wadogo wadogo kuchangamkia vitambulisho vya wamachinga ambavyo vinapatikana nchi nzima katika Ofisi za Wakuu wa Mikoa na Wilaya kwa shilingi 20,000/=. Vitambulisho hivyo ni maalum kwa wale tu ambao mauzo yao ghafi hayazidi shilingi 4,000,000/= kwa mwaka”, alisisitiza Kayombo.

  Mkurugenzi huyo wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Richard Kayombo ametoa wito kwa walipakodi na wananchi wote kwa ujumla kuendelea kulipa kodi kwa hiari na wakati na kusema kuwa, TRA imeanza kampeni rasmi ya usajili wa walipakodi wapya kote nchini kwa kuwapatia Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) bure katika maeneo wanayofanyia biashara.
  Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Richard Kayombo akiongea na Waandishi wa Habari kuhusu Makusanyo ya kodi kwa kipindi cha miezi sita kwa Mwaka wa Fedha 2018/19, katika Ofisi za TRA Makao Makuu Jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Richard Kayombo akiongea na Waandishi wa Habari kuhusu Makusanyo ya kodi kwa kipindi cha miezi sita kwa Mwaka wa Fedha 2018/19, katika Ofisi za TRA Makao Makuu Jijini Dar es Salaam. (PICHA NA BENEDICT LIWENGA).

  0 0  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza jambo na baadhi ya Wanachama wa NSSF waliofika kwenye ofisi za NSSF Ilala/Temeke leo kufuatilia madai yao mbalimbali kufuatia maagizo ya Rais Dk.John Magufuli aliyoyatoa katika mkutano kati ya viongozi wa vyama vya wafanyakazi, Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa sekta ya Hifadhi ya jamii(SSRA), watendaji wakuu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na Chama cha waajiri uliofanyika Desemba 28, 2018 Ikulu jijini Dar es salaam. Waziri Mhagama akiwa ameambatana na Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),William Erio amefanya ziara leo katika ofisi za Ilala,Temeke na Kinondoni kufuatilia utekelezaji wa Maagizo ya Rais na kusikiliza changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo Wanachama hao wakati wa kufuatilia madai yao kwenye ofisi hizo.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),William Erio,wakati alipofanya ziara leo ya kutembelea ofisi za Ilala,Temeke na Kinondoni kufuatilia utekelezaji wa Maagizo ya Rais na kusikiliza changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wanachama katika ofisi hizo.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama pamoja na Uongozi wa NSSF wakimsikiliza mmoja wa Wanachama akieleza changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wakati wa kufuatilia madai yao ya mafao. 
  Mwalimu wa Shule ya Sekondari Tusiime,Nobert Kamugisha ambaye amekwenda  kufuatiia madai yake kwenye Ofisi za NSSF Ilala Boma leo,akieleza changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo mbele ya  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani).
  Baadhi ya Wanachama wa NSSF wakiwa kwenye Ofisi za Ilala Boma wakifuatilia madai yao mbalimbali,walipokuwa wakimsikiliza  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani).
  Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),William Erio akitoa ufafanuzi kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo madai ya Wanachama wa shirika hilo,mbele ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama .

  Baadhi ya Wanachama wa NSSF wakiwa kwenye Ofisi za Ilala Boma wakifuatilia madai yao mbalimbali,walipokuwa wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani).
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama pamoja na Uongozi wa NSSF wakiwasikiliza baadhi ya Wanachama wa shirika hilo waliofika kufuatilia madai yao mbalimbali katika ofisi za shirika hilo zilizopo Ubungo Plaza,jijini Dar.

  ======  ======  ========

  WAZIRI JENISTA MHAGAMA ATOA MAAGIZO KWA NSSF, AKERWA NA TABIA YA NENDA RUDI KUFUATILIA MAFAO 

  Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

  WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu(Sera, Bunge, Kazi ,Vijana na Ajira) Jenista Mhagama ameutaka Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii(NSSF) kuhakikisha wanalipa mafao ya wastaafu kwa wakati huku akiwataka watumishi wa mfuko huo kufanya kazi kwa kujituma ya kuhudumia wastaafu nchini.

  Mhagama ametoa kauli hiyo leo wakati alipofanya ziara ya kutembelea ofisi za NSSF za Ilala na Temeke jijini Dar es Salaam kwa lengo la kufuatilia iwapo maagizo ya Rais Dk.John Magufuli ya kuwalipa wastaafu ambao wanadai mafao yao kama yameanza kutekelezwa ama la. Akiwa kwenye ofisi hizo Waziri Mhagama amesema, ameshuhudia maagizo ya Rais Magufuli yameanza kutekelezwa na NSSF lakini bado kuna baadhi ya changamoto ambazo lazima zipatiwe ufumbuzi. 


  Amesema,moja ya changamoto ni tabia ya nenda rudi kwa wastaafu na wanapowaambia waondoke wanaondoka na fomu zao badala ya kuacha zishughulikiwe."Tabia hii ya nenda rudi sasa iwe basi na nimeshatoa maagizo ya kuwepo kwa mabango yenye namba za simu zote kwa kuwekwa wazi,"amesema.

  "Waziri Magufuli amesisitiza umuhimu wa mafao ya wastaafu kushughulikiwa kwa wakati na kama watumishi hawatoshi kwenye ofisi hizo za Ilala na Temeke basi walioko makao makuu wahamishiwe kwenye ofisi hizo ili kutoa huduma kwa wanachama wao"."Ni vema NSSF wakahakikisha wanatoa huduma bora kwa wanachama, Kipaumbele lazima kiwe kuwahudumia wanachama wetu ambao ni wastaafu kwani wamefanya kazi kwa heshima, wao ni mashujaa na lazima washughulikiwe kishujaa badala ya kuwasumbua,"amesema Waziri Mhagama.

  Amesema kuna baadhi ya watumishi wa NSSF wamekuwa na kauli za hovyo kwa wanachama wao na hivyo kutoa maagizo kwa kuwataka wenye tabia hiyo kuacha mara moja huku akiwasisitiza kufanya kazi kwa bidii na kujituma kama sehemu ya kuenzi kazi nzuri inayofanywa na Rais Magufuli ya kuwapigania wastaafu nchini.

  Pia amesema kuna mameneja ambao wanataka kuonwa kwa apointiment na hivyo ametaka tabia hiyo iachwe mara moja na kwamba hata yeye ofisini kwake wanaohitaji kumuona wanakwenda bila apointment.Waziri Mhagama amewataka NSSF kufanya mabadiliko ya kimfumo ya kiutendaji kwa lengo la kuleta ufanisi wa kuwahudumia wanachama wao na kwamba anachotaka kuona ni kwamba kuna kuwa na urahisi wa kulipwa kwa mafao."Kuwe na malipo jana, yaani kwa maana ya kwamba wakati mwanachama anakuja NSSF tayari akute utaratibu wa kushughulikia malipo yake ulishafanyika kabla na anapokuja ni kuchukua fedha zake na kuondoka,"amefafanua Waziri Mhagama.

  Wakati huo huo, Waziri Mhagama amesema kuna baadhi ya watu wasiowaaminifu wanatumia kipindi hiki kutaka kufanya udanganyifu ili walipwe mafao kwa kupeleka nyaraka za uongo na hivyo amewataka wenye
  tabia hiyo watambue watachukuliwa hatua."Kuna baadhi ya watu wanakwenda na vielelezo feki ili wapewe mafao na NSSF, tutaanza kuja na askari kanzu kwa ajili ya kuwakamata watu wa aina hiyo ambao kimsingi wanataka kufanya utapeli.Pia kwa NSSF lazima mboreshe mfumo wenu ambao utabaini wale wanaotaka kufanya utapeli wa fedha hizi za wanachama,"amesema.

  0 0

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Doto Biteko kuwa Waziri wa Madini. Kabla ya Uapisho huo Mhe. Biteko alikuwa Naibu Waziri wa Madini. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.Januari 9,2019
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini hati mara baada ya kumuapisha Mhe. Doto Biteko kuwa Waziri wa Madini. Kabla ya Uapisho huo Mhe. Biteko alikuwa Naibu Waziri wa Madini. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.Januari 9,2019
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi vitendea kazi Mhe. Doto Biteko alipoapishwa kuwa Waziri wa Madini. Kabla ya Uapisho huo Mhe. Biteko alikuwa Naibu Waziri wa Madini. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.Januari 9,2019
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Zainabu Chaula kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (anayeshughulikia afya). Kabla ya Uapishohuo Dkt. Chaula alikuwa Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI (afya). Hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.Januari 9,2019
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bi. Dorothy Mwaluko kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uwekezaji). Kabla ya Uapisho huo Bi. Mwaluko alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.Januari 9,2019
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi vitendea kazi Bi. Dorothy Mwaluko alipoapishwa kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uwekezaji). Kabla ya Uapisho huo Bi. Mwaluko alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.Januari 9,2019
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Arch. Elius Mwakalinga kuwa Katibu Mkuu Ujenzi. Kabla ya uapisho huo Arch. Mwakalinga alikuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) na anachukua nafasi ya Mhandisi Nyamuhanga ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu TAMISEMI. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.Januari 9,2019
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Prof. Faustin Kamuzora kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera.Kabla ya Uapisho huo Prof. Kamuzora alikuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Uratibu na anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Athumani Diwani Msuya ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU). Hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.Januari 9,2019
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Dorothy Gwajima kuwa Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI (Afya). Kabla ya Uapisho huo Dkt. Gwajima alikuwa Mkurugenzi wa Tiba wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.Januari 9,2019
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Francis K. Michael kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Kabla ya uapisho huo Dkt. Francis K. Michael alikuwa Mhandiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.Januari 9,2019
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Jaji Mstaafu Dkt. Steven James kuwa mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.Januari 9,2019
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha George Daniel Yambesi kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.Januari 9,2019
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Yahaya Fadhil Mbila kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.Januari 9,2019
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Daniel Ole Njoolay kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.Januari 9,2019
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi John Michael Haule kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.Januari 9,2019
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Khadija Ali Mohamed Mbarak kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.Januari 9,2019
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Immaculate Peter Ngwale kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.Januari 9,2019
   Viongozi mbalimbali walioapishwa wakila Kiapo cha Maadili ya Viongozi wa Umma mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.Januari 9,2019
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kuwaapisha Viongozi mbalimbali  Ikulu jijini Dar es Salaam.Januari 9, 2019.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali,Bunge, Mahakama pamoja na Waziri wa Madini Dotto Biteko,Makatibu wakuu wapya,Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera mpya,na Mwenyekiti na Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma.Mara baada ya kuwaapisha viongozi mbalimbali Ikulu Jijini Dar es salaam.Januari 9, 2019. PICHA NA IKULU


  0 0

   Rais wa mtandao wa wasanii wa Injili na Maadili Dkt. Godwin Maimu akizungumza katika Tamasha hilo lililofanyika Buza Jijini Dar es salaam Buza Kipera
   Picha ya Viongozi wa Mtandao wa wasanii wa Injili na maadili wa pili kutoka kulua ni Rais wa Tagoane Taifa Dkt. Godwin Maimu, aliyrpo kushoto kwake ni Katibu mkuu Mchungaji Lucy, wa kwanza kushoto ni Katibu mkuu mwenza Silvanus Mumba akifuatiwa na Makamu wa Rais Tagoane, Florah Sungura. 
   Mchungaji mwenyeji Tamasha lilipofanyika Apostal Israel Popapo kutoka  Jijini Dar es salaam, katika  kanisa la ETERNITY GOSPEL CHURCH, Buza Kipera
   Uimbaji ukiendelea kama inavyoonekana katika picha kafika kanisa la ETERNITY GOSPEL CHURCH Buza Kipera
   Picha ya pamoja ya wasanii mbalimbali wa Injili waluohudhuria katika tamadha hilo lililopewa jina la Madhabahu ya shukrani


  NA.VERO IGNATUS

  Mtandao wa wasanii wa Injili na maadili Nchini(Tagoane) wanafanya Tamasha leo la kutoa shukrani kwa Mungu kwa kuwapa ulinzi na Kibali tangia kuanzishiswa kwa mtandao huo

  Akizungumza  katibu mkuu mtendaji  Tagoane Taifa Silvanus Mumba amesema kuwa Tamasha hilo wamelipa jina la Tukuza Festival Madhabahu ya shukrani ambapo wananzia Jijini Dar es salaam ndipo wataelekea mikoa mingine

  Amesema lengo kuu ni kumshukuru Mungu kwa matendo makuu aliyowatendea tangia kuanzishwa kwa mtandao huo sambamba na mafanikio yaliyopatikana ya kuwaleta waimbaji wa pamoja.

  Silvanus amesema kuwa hadi sasa wamekuwa na  Mafanikio Makubwa tangia kuanzishwa kwa TAGOANE, wameweza kusaidia Watoto Yatima, wameutangaza Utalii wa ndani wameweza kusaidia Vifaa vya matibabu katika  Hospitali Mount Meru sambamba na kusaidia Vijana Elimu juu ya ujasiliamali,

  Akielezea matazamio waliyonayo ni  kuweza kuwasaidia wasanii Kuwa na UCHUMI imara kupitia Mfuko wa TAGOANE LOAN FUND, Kuwa na Wasanii walio Tayari kujito kwaajili ya Jamii na makundi Maalumu Kama Wazee, Yatima, wajane, vilema, na Wagonjwa

  Amesema kuwa  wanaendelea Kuwa na Utaratibu wa Kuibua vipaji Mashuleni kwa Kushirikiana na Taasisi ya waalimu wa shule BinafsiTanzania (TPTU) Lakini pia Kujiunganisha na wadau wa Maendeleo Kama SIHAONE TUNAPENDANA Ltd

  Tunapenda kuwaambia Wasanii wote, wakristo walio Kwenye sekta ya Sana, kujiunga na TAGOANE kwasababu ndio Pahala sahihi amvako wataweza kujiweka Akiba na kukopa inapohitajika, Kupata Fursa ya Mafunzo ya ujasiliamali na Sheria ya hatimiliki, Elimu juu ya Ubunifu Lakini pia Watajitolea kwa jamii pia ifaidike kupitia yeye

  Mikoa mingine ambayo wanatazamia kufanya Tamasha hilo ni pamoja na Dodoma, Morogoro, kwa sasa wameanza na Jiji la Dar es salaam mikoa mingine wataendelea kutoa taarifa ,  lengo kuu ni Kumpelekea Mungu Shukurani za pekee kwa Kuisimamisha Tagoane Kuwa ya Mfano. 


older | 1 | .... | 1771 | 1772 | (Page 1773) | 1774 | 1775 | .... | 1897 | newer