Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1770 | 1771 | (Page 1772) | 1773 | 1774 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka wanaotoa huduma katika sekta ya afya kutoa Huduma bora.Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa jengo la kituo cha Mama na Mtoto katika hospitali ya KMKM Kibweni ikiwa sehemu ya maadhimisho ya shamrashamra za kutimiza miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

  Makamu wa Rais ametoa rai kwa Wataalamu wa Afya nchini kutambua kuwa wanatakiwa kutumia utaalamu wao katika kuokoa maisha ya mama na mtoto ili kuepuka vifo vitokanavyo na uzazi kwa ajili ya kujenga Taifa lenye kizazi imara. “Ni wajibu wenu kutumia utaalamu wenu na jukumu mlilopewa na Taifa katika kuleta mabadiliko ya kiutendaji na ufanisi katika sekta ya afya nchini” alisema Makamu wa Rais.

  Jengo la Kituo cha Mama na Mtoto ni la ghorofa mbili na limegharimu jumla ya shilingi 3, 648,400,000/- na kuzingatia watu wenye mahitaji maalumu.

  Huduma zitakazopatikana kwenye jengo hilo la ghorofa mbili ni Huduma ya Mama na Mtoto, Wodi ya Wazazi na Watoto,Huduma ya Upasuaji kwa Mama Wajawazito, Huduma ya Vipimo X Ray, Utra Sound na Maabara, Ofisi za huduma za madaktari, wauguzi na wahudumu wengineo.
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akipiga makofi ya pongezi mara baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo la Kituo cha Mama na Mtoto katika Hospitali ya KMKM Kibweni ikiwa sehemu ya shamra shamra za kuadhimisha sherehe za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar wengine pichani ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ  Haji Omar Kheir (kulia) na kushoto ni Mkuu wa KMKM Komodoo Hassan Mussa Mzee 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akihutubia katika hafla ya uzinduzi wa jengo la Kituo cha Mama na Mtoto katika Hospitali ya KMKM Kibweni ikiwa sehemu ya shamra shamra za kuadhimisha sherehe za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

   Sehemu ya waliohudhuria katika hafla ya uzinduzi wa jengo la Kituo cha Mama na Mtoto katika Hospitali ya KMKM Kibweni ikiwa sehemu ya shamra shamra za kuadhimisha sherehe za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar ambapo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alikuwa mgeni rasmi.
   Jengo la Kituo cha Mama na Mtoto katika Hospitali ya KMKM Kibweni, wilaya ya Magharibi mkoa wa mjini Magharibi, Unguja ambalo limefunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ikiwa sehemu ya shamra shamra za kuadhimisha sherehe za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)  0 0


  0 0

  *Amtaka kumthibitishia maneno yake kuwa Bunge nichombo dhaifu
  *Amtaka ajitafakari ...asema kauli zake nje ya nchi zimemsikitisha 


  Na Ripota Wetu, Globu ya jamii 

  HATIMAYE Spika wa Bunge Job Ndugai ametoa maagizo ya kumtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad kufika katika Kamati ya Maadili ya Bunge ifikapo Januari 21 mwaka huu na iwapo atashindwa kufika atapelekwa akiwa kwenye pingu.

  Spika Ndugai ametoa kauli hiyo leo Mjini Dodoma wakati anazungumza na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari nchini alipokuwa akielezea namna ambavyo Prof.Assad ametoa kauli ambayo haikustahili kuitoa kwa Bunge.

  Siku za karibuni Prof.Assad wakati anahojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa ambapo aliulizwa kuhusu jitihada ambazo ofisi ya CAG inafanya kila mwaka kwa kukagua na kutoa ripoti ambazo zinaoonesha kuna ubadhirifu wa fedha ambapo alijibu kazi yake ni kufanya ukaguzi na kukabidhi ripoti kwa Bunge, hivyo Bunge ndilo dhaifu kwa kushindwa kufanyia kazi ripoti hizo.

  Hivyo kauli hiyo ya Profesa Assad kudai Bunge ni dhaifu ndiyo iliyosababisha Spika wa Bunge leo kutangaza kumuita Kamati ya Maadili ili akahojiwe na kamati hiyo na iwapo atakaidi atapelekwa kwa pingu na hiyo itatosha kuthibitisha Bunge si dhaifu.

  "Bunge tumepokea kwa masikitiko makubwa kauli ya Profesa Assad.Anataka kuonesha kuwa ripoti ambazo anazitoa kwa Bunge hazifanyiwi kazi au zikifika Bungeni basi hakuna kinachoendelea kwa kuwekwa pembeni bila kufanyiwa kazi.Hii si kweli kabisa,"amesema Spika Ndugai na kuongeza "CAG na maofisa wake wamekuwa wakiingia kwenye Kamati ya Kudumu ua Hesabu za Serikali za Mitaa pamoja na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mashirika ya Umma.

  "Ripoti za CAG zikifika kwenye kamati hizo ambazo kimsingi zinaongozwa na upinzani , maofisa wa ofisi ya CAG wanakuwepo kueleza mapungufu waliyobaini wakati wa ukaguzi na hatua ambazo zinastahili kuchukuliwa.Tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani kuna jitihada kubwa zimefanyika na zinaendelea kufanyika katika kudhibiti matumizi ya fedha za umma, kuna mabadiliko makubwa yamefanyika kwa ushauri wa CAG,"amesema.

  Pamoja na hayo Spika Bunge amehoji ni hatua gani ambazo Profesa Assad anataka zichukuliwe huku akitumia nafasi hiyo kuwataka maofisa wa Serikali kuacha kutoa kauli za kulidhalilisha na kwamba Bunge linaweza kukosolewa lakini si kwa kauli za dharau.Pia amesema si uungwana kuisema nchi yako vibaya ukiwa nje ya nchi huku akitumia nafasi hiyo kumtaka Profesa Assad kujitathimini kwani Bunge haliko tayari kufanya kazi na mtu ambaye anaona chombo hicho ni dhaifu.

  "Kwa mujibu wa kifungu cha 4, kifungu kidogo cha kwanza A, cha nyongeza ya nane ya kanuni za Kudumu za Bunge toleo la Januari 2016 suala hili nalipeleka katika kamati ya haki , maadili na madaraka ya Bunge ili walifanyie kazi na kunishauri na kwa maana hiyo kulishauri Bunge.

  "Hivyo Profesa Assad anatakiwa kujitokeza Januari 21,2018 aende kujieleza kwenye kamati hiyo ili akathibitishe maelezo yake ambayo ameyatoa mahakamani.Na mnafahamu pamoja hatuna polisi, hatuna nini ila tunaweza kumleta mtu kwa pingu kwani tunataka kumthibitishia sisi sio dhaifu,"amesema Spika Ndugai.
   Baadhi ya Wanahabari wakimsikiliza Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (Mb), aalipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma   leo kuhusu kauli za kudhalilisha Bunge zilizotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),  Profesa Mussa Assad na Mbunge wa Kawe, Mhe. Halima Mdee. 
   Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (Mb), akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma kuhusu kauli za kudhalilisha Bunge zilizotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),  Profesa Mussa Assad na Mbunge wa Kawe, Mhe. Halima Mdee.


  0 0

   MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza na wajasiriamali kwenye soko la Muheza mjini wilayani humo ambako alikwenda kuwahimiza umuhimu wa kuwa na vitambulisho vya ujasiriamali ili waweze kutambulika rasmi na kufanya shughuli zao
    MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza na wajasiriamali kwenye soko la Muheza mjini wilayani humo ambako alikwenda kuwahimiza umuhimu wa kuwa na vitambulisho vya ujasiriamali ili waweze kutambulika rasmi na kufanya shughuli zao kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo
   MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kushoto akigawa vitambulisho kwa wajasiriamali wilayani Muheza wakati alipokwenda kuhamasisha wajasiriamali wasiokuwa kwenye sekta rasmi  ambapo kwa wilaya ya Muheza wamepewa vitambulisho 3000 ambavyo vitagawiwa kwa wajasiriamali wilayani humo
  Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kushoto akiwaga vitambulisho kwa mmoja wa wajasiriamali wilayani Muheza Bibi Monica Cheche kwenye soko la Muheza mjini  humo jana wakati alipokwenda kuhamasisha wajasiriamali hao kuwa na  vitambulisho ili waweze kutambulika rasmi
   Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akikagua bidhaa za mjasiriamali wilayani Muheza wakati alipokwenda kuhamasisha umuhimu wa wao kuwa na vitambulisho ili waweze kutambulika
   MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia akiwa na Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo wakitembelea maeneo mbalimbali Muheza mjini kuhamasisha wajasiriamali kuwa na vitambulisho vilivyotolewa na Rais Dkt John Magufuli ili waweze kutambulika rasmi
   MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kushoto akiwagawa vitambulisho kwa wajasiriamali wilayani Muheza wakati alipokwenda kuwahamasisha
   MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kushoto akisisitiza jambo kwa wajasiriamali wilayani Muheza kabla ya kuwakabidhi vitambulisho

  MJASIRIAMALI wa wilaya ya Muheza kulia akiandikishwa na maafisa wa TRA wilayani humo kabla ya kukabidhiwa kitambulisho na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella leo
  MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kushoto akimsikiliza kwa umakini mmoja wa wajasiriamali wilayani Muheza ambaye aliuliza swali wakati wa uhamasishaji huo uliofanywa na mkuu huyo wa mkoa
   Sehemu ya maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA wilayani Muheza wakiendelea na zoezi la kuandikisha wajasiriamali kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho wakati wa uhamasishaji huo uliofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella leo
   MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia akimsikiliza kwa umakini Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo mara baada ya kumaliza uhamasishaji wa wajasiriamali kuchangamkia fursa ya  vitambulisho vilivyotolewa na Rais Dkt John Magufuli
  Sehemu ya wajasiriamali wakifuatilia maelezo ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella ambaye hayupo pichani


  MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella amewahamisha wajasiriamali wilayani Muheza kuchangamkia fursa ya vitambulisho vilivyotolewa na Rais Dkt John Magufuli ili waweze kutambulika rasmi na kufanya shughuli zao.

  Huku akisisitiza dhamira ya kuendesha misako kuanzia siku ya Jumatano na ambao watakutwa hawana kitambulisho hicho watakuwa wanahusika ufanyaji wa biashara haramu za magendo ambazo hazitambuliki.

  Akizungumza mara baada ya kuwakabidhi vitambulisho kwa wajasiriamali wilayani Muheza,RC Shigella alisema wanapaswa kuchangamkia fursa hiyo muhimu kwa ajili ya kutambulika ili waweze kufanya kazi zao vema ambapo kwa wilaya ya Muheza vitagawiwa kwa wajasiriamali 3000.

  “Lakini niwaambie kwamba kitambulisho cha Uraia,Leseni ya gari na kile cha kupigia kura isiwe kigezo cha kukufanya ushindwe kupata kitambulisho cha mjasiriamali…unachotakiwa kufanya kama hauna unaandika jina lao mahali unapoishi namba yako ya simu unasaidiwa utakapokamilisha hivyo vyengine utawaletea”Alisema RC Shigella.

  Aidha pia aliwataka wajasiriamali wasiokuwa kwenye sekta rasmi kujitokeza kwa wingi ili waweze kupatiwa vitambulisho hivyo ili waweze kutambulika na hatimaye kuweza kuondaka na usumbufu wakati wakiendesha biashara zao

  “Ndugu zangu Rais wetu aliona wajasiramali na wafanyabiashara wanapata shida na usumbufu hivyo akaona ili kuweza kuondoa hilo akaona kuwepo na utaratibu wa vitambulisho”

  Alisema kwamba vitambulisho hivyo vinatolewa kwa yoyote asiyekuwa na TIN namba na ambaye alipi kodi hivyo kuwataka kuona umuhimu wa vitambulisho hivyo ili waweze kuendesha biashara zao.

  Naye kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo alisema wataendelea kuhamasisha ili wajasiriamali wengine waweze kuchangamkia fursa ya kuwa na vitambulisho hiyo.

  0 0

  WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kampuni zote zinazosambaza nguzo za umeme zinatakiwa zilipe ushuru wa halmashauri wanakotoa nguzo hizo amboa ni asilimia tano ya gharama ya kila nguzo kama ilivyoelekezwa na Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa.

  Ametoa agizo hilo leo (Jumatatu, Januari 7, 2019) baada ya kupata taarifa kuhusu kampuni ya New Forest ambayo inamkataba na TANESCO wa kusambaza nguzo za umeme, kwa muda mrefu kampuni hiyo imekuwa ikikaidi kulipa ushuru wa asilimia tano ya gharama ya kila nguzo. Ushuru huo umefikia sh. bilioni 2.9 hali iliyopelekea uongozi wa mkoa kuzuia nguzo hizo zisitoke.

  Wiki iliyopita akiwa katika ziara ya mkoa Ruvuma, Waziri Mkuu alipokea malalamiko kuhusu mkoa wa Iringa kuzuia kusambazwa kwa nguzo za umeme ndipo alipoamua kuwaita Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happi pamoja na wakuu wa wilaya, wakurugenzi pamoja na wenyeviti wa halmashauri wanaotoka katika wilaya zinazozalisha nguzo.

  Viongozi wengine waliohudhuria kikao hicho ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemevu, Jenista Mhagama, Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Josephat Kandege, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, Naibu Waziri Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya pamoja na maafisa wengine wa Serikali.

  Amesema lengo la kikao hicho lilikuwa kupata ufafanuzuzi kuhusu malalamiko yaliyotolewa dhidi ya uongozi wa mkoa wa Iringa kuhusu kuzuia usafirishaji wa nguzo za umeme zinazotomika kwenye miradi ya Kusambaza Nishati ya Umeme Vijiji (REA).

  Baada ya kupata maelezo hayo, Waziri Mkuu amemuagiza mkuu wa mkoa wa Iringa kuiandikia bili kampuni ya New Forest ili ilipe ushuru huo kuanzia Julai 2018 walipoanza kusambaza nguzo. Asilimia 90 ya nguzo za umeme nchini zinatoka Iringa. Tanzania ina viwanda tisa vya kutengeneza nguzo na kati ya viwanda hivyo vinane vipo Iringa na kimoja kipo Tanga.

  Kampuni ilizuiwa kutoa nguzo ndani ya mkoa wa Iringa tangu Novemba 2018 hadi Januari 2019 huku ikitakiwa kulipa ushuru wa asilimia tano ya gharama ya kila nguzo ambapo ilikaa ikitaka iendelee kulipa sh. 5,000 kwa kila nguzo kama walivyokubaliana na TANESCO jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

  Hata hivyo, nguzo za umeme ambazo zilikuwa zimezuiwa kwa muda mrefu katika maeneo ya uzalishaji hususani mkoani Iringa na kusababisha kukwama kwa baadhi ya miradi ya usambazaji umeme kwenye baadhi ya mikoa nchini juzi zimeanza kusambazwa huku taratibu nyingine za malipo zikiendelea.

  0 0


  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo amewapongeza Viongozi, watendaji, na wananchi wa wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma kwa utekelezaji mzuri wa miradi ya maendeleo. Waziri Jafo amefurahishwa Sana na ujenzi wa vituo vya afya vya Kagezi Mabamba kwani ujenzi wake umekuwa mzuri Sana unaoendana na thamani ya fedha iliyo tolewa na serikali.

  Katika ziara hiyo waziri Jafo alimpongeza Sana mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Eng. Nditiye kwani amekuwa akiwahangaikia Sana wananchi wake katika upatikanaji wa miradi hiyo ya maendeleo.

  Aidha, Waziri Jafo alimalizia ziara yake kwa kukagua miradi ya barabara ya Kibondo mjini pamoja na kutembelea shule ya sekondari Malagarasi ambapo ukarabati na ujezi wa miundombinu umefanyika shuleni hapo kwa gharama ya shilingi milioni 400.
  Waziri Jafo akikagua barabara za changarawe zilizojengwa na TARURA Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma
  Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Malagarasi wakimskiliza Waziri Jafo(hayupo pichani) alipowatembelea shuleni hapo.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo(katikati) akisomewa taarifa wakati alipotembelea Kituo cha Afya Kibamba kilichopo Kibondo Mkoani Kigoma.

  0 0

  Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu akitoa salamu za mkoa huo jana wakati wa kongamano la siku mbili linalojadili mikakati mbalimbali ya kuongeza uzalishaji wa asali na uanzishaji wa viwanda vya kuchakata na kusindika asali nchini.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasaili na Utalii Profesa Adolf Mkenda akifungua jana kongamano la siku mbili linalojadili mikakati mbalimbali ya kuongeza uzalishaji wa asali na uanzishaji wa viwanda vya kuchakata na kusindika asali nchini.  Baadhi ya wadau wa ufugaji nyuki wakiwa katika kongamano la siku mbili linalojadili mikakati mbalimbali ya kuongeza uzalishaji wa asali na uanzishaji wa viwanda vya kuchakata na kusindika asali nchini.

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasaili na Utalii Profesa Adolf Mkenda(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa ufugaji nyuki jana mara baada ya kufungua kongamano la siku mbili linalojadili mikakati mbalimbali ya kuongeza uzalishaji wa asali na uanzishaji wa viwanda vya kuchakata na kusindika asali nchini.

  …………………

  WADAU wa sekta ya ufugaji nyuki na uzalishaji wa asali na mazao yake wametakiwa kutumia uwepo wa utajiri wa mistu hapa nchini kuhakikisha wanazalisha asali kwa ubora na wingi kwa ajili ya masoko ya ndani na nje ya nchi.

  Hatua hiyo itasaidia kuongeza nafasi za ajira kwa wananchi na kuingizia nchi fedha za kigeni zinazotokana na mauzo ya asali nje ya Nchi.

  Kauli hiyo imetolewa jana mjini Tabora na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Profesa Adolf Mkenda wakati wa kufungua kongamano la siku mbili la wadau wa ufugaji nyuki na uzalishaji wa asali lililolenga uanzishaji wa viwanda vya kusindika na kuchakata asali na mazao yake. Alisema licha kuwa na mistu mikubwa hapa nchini bado uzalishaji wa asali uko chini ukilinganisha na baadhi ya Nchi ambazo zina mistu michache barani Afrika.

  Profesa Mkenda alisema wakati umefika kwa wadau kuhakikisha wanakuja na mikakati itakayoongeza uzalishaji wa asali hapa nchini na kuwawezesha wakazi wa kando kando ya mistu nchini kunufaika na uwepo wake kwa kuongeza kipato chao kupitia ufugaji nyuki na uzalishaji asali. Alisema lengo ni kutaka asali iwe sawa na dhahabu nyingine inayoliingizia Taifa fedha za kigeni zinazotokana na mauzo nje ya nchi kwa kuwa soko la asali ya Tanzania ni kubwa ndani na nje ya bara la Afrika.

  Aidha Katibu Mkuu huyo alisema ili kuhakikisha makazi ya nyuki hayaharibiwi Serikali kwa kushirikiana na wadau wa mistu wameanza kuedesha zoezi la kuwaondoa watu wote wanaondesha shughuli za kiuchumi katika maeneo ya mistu. Katika hatua nyingine Profesa Mkenda aliwaka wadau hao kuacha kulalamika kuwa uhaba wa asali unasababishwa na wanunuzi toka nje ya nchi wanaokwenda moja kwa moja kwa wafugaji wa nyuki na kununua bidhaa hizo kwa bei ya shilingi elfu 40,000/- kwa lita 20 wakati wao wananua kwa shilingi 120,000/- na kuwataka nao waende kwa wafugaji.

  Awali Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu aliwataka wadau hao kuhakikisha wanakabiliana na tatizo la uharibifu wa mistu na uchomaji ovyo wa moto hapa nchini. Alisema vitendo hivyo vinachangia kwa kiasi kikubwa upungufu wa asali nchini kwa kuwa visababisha uharibifu wa makazi wa nyuki na kuwafanya kukosa mimea kwa ajili ya kutengeza asali.

  Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki Semu Daudi alisema uzalishaji hafifu na mdogo unatokana na wafugaji kufuga bila kutumia watalaamu waliopo na hivyo kufanya bidhaa zao kukosa masoko nje na ndani ya nchi. Alisema njia pekee ya kumsaidia mfugaji wa nyuki ni kuongeza elimu na kumfanya afuge nyuki kisasa na kitaalamu ili aweze kuongeza uzalishaji na ubora wa bidhaa zake.

  Naye Mdau wa Nyuki kutoka Wilayani Kasulu Tanu Jumanne alisema uanzishaji wa Vyama vya ushirika wa wafugaji nyuki vitasaidia kuondoa unyonyaji wa unaofanywa na wanunuzi toka nje na pia utawezesha viwanda vinavyotakiwa kuanzishwa kuwa na malighafi za kutosha mwaka mzima.

  Alisema Vyama vya Ushirika vitamfanya mfugaji kuuza asali yake kwa bei nzuri na hata wakati wa shida atakwenda kukopa na kutofanya kuchukua pesa mapema na inapofikia kuuza na uuza kwa bei ya chini ili alipe deni kwa mnunuzi wa nje.

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amefafanua fursa mbalimbali za uwekezaji zinazopatikana katika Mkoa hasa sekta ya kilimo kwa wahitimu wa mafunzo kwa vitendo kutoka katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi waliotembelea mkoani hapa ili kujionea maendeleo ya mkoa. 

  Wahitimu hao kutoka katika nchi kadhaa barani Afrika wamelenga kutembelea katika viwanda vikubwa vinavypoaptikana katika mkoa, maeneo ya uwekezaji wa kilimo, kufika kwenye vivutio vya utalii, machimbo ya makaa ya mawe pamoja na hifadhi za misitu. 

  Mh.Wangabo alisema kuwa uwekezaji wa kwenye viwanda unahitajika kwasababu ya uwepo wa mazao ya kulisha viwanda hivyo ikiwemo viwanda vya kuchakata mahindi, maharage na mpunga na kuwaondoa shaka juu ya upatikanaji wa umeme kwani hadi kufikia mwaka 2020 vijiji vyote vya mkoa wa Rukwa vitakuwa na umeme. 

  “Maeneo mazuri ya uwekezaji upo kwenye viwanda hasa viwanda vya kuchakata mazao ndani ya mkoa wetu, pia mwaka huu tuna zao la alizeti kama zao la Kimkakati ambapo hadi sasa kuna tani za mbegu zaidi ya 11,000 ambazo zimeshanunuliwa na wakulima na kupandwa na hivyo tunategemea uzalishaji mkubwa wa alizeti kwa mwaka huu na hivyo tunawaalika wawekezaji kuweka viwanda vya uchakataji wa alizeti ikiwa ni zao la kimkakati kwenye mkoa wetu.” Alisema. 

  Aidha, alibainisha kuwa katika kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano, mkoa umejipanga kulima zao la kahawa ambalo ni moja ya mazao matano ya kimkakati kwa serikali, na kusisitiza kuwa upatikanaji wa samaki katika ziwa Tanganyika na ziwa Rukwa bado unahitaji uwekezaji ili kukuza sekta hiyo na hatimae kukuza vipato vya wavuvi wa maeneo ya maziwa hayo, huku akielezea uboreshwaji wa miundombinu ya barabara na kiwanja cha ndege cha mkoa. 

  Ameyasema hayo wakati akijibu swali la Brigedia Generali Mohamed Montaser muhitimu kutoka nchini Misri aliyetaka kujua maeneo ya vipaumbele katika uwekezaji kwa mkoa wa Rukwa. Halikadhalika, Kiongozi wa wahitimu hao Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Magereza SACP Justine Kaziulaya aliushukuru uongozi wa Mkoa wa Rukwa kwa mapokezi mazuri waliyoyapata na kuomba kupokewa tena endapo watarudi Mkoa wa Rukwa katika miaka inayofuata.

  Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Benard Makali (kulia) akipokea moja ya zawadi alizopewa na Uongozi wa chuo cha Ulinzi nchini ikiwasilishwa na Kiongozi wa Msafara huo Commodore M. Mumanga
  Picha ya apmoja kati ya Wahitimu wa Chuo cha Ulinzi nchini pamoja na Wataalamu wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa wakiongozwa na Mkuu wa mkoa Mh. Joachim Wangabo (wa tatu toka Kulia).
  Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kulia)akipokea moja ya zawadi alizopewa na uongozi wa chuo cha Ulinzi nchini kama shukrani ya kuwapokea vizuri katika Mkoa, zawadi iliyowasilishwa na Kiongozi wa Msafara huo Commodore M. Mumanga.

  0 0

  Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko (wa pili) akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Madini Prof. Simon Msanjila wakitoka katika jengo la ofisi za mwekezaji wa hifadhi za wanyamapori ya Makao, Mwiba Limited kuelekea eneo linalosadikiwa kuendesha shughuli za Uchimbaji hifadhini humo.
  Baadhi ya wanyama wanaoonekana katika hifadhi ya wanyama ya Makao katika Wilaya ya Meatu Mkoani Singida
  Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (wakwanza kulia) akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Madini, Prof. Simon Msanjila na wajumbe aliambatana nao wakiwa katika eneo linaloonesha dalili za uchimbaji wa madini katikati ya hifadhi ya wanyama ya Makao wilayani Meatu
  Pori kwa pori mbugani, Prof. Simon Msanjila akiongoza wajumbe walioambatana kujiridhisha, kukagua pamoja na kutoa kauli ya serikali kwa wafanya biashara wa madini wanaojihusisha na biashara hiyo kinyume na taratibu na sheria ya nchi, Nyuma yake mwenye suti ni Mkuu wa Wilaya ya Meatu Dkt. Joseph Eliaza Chilongani
  Wajumbe walioambatana na Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Simon Msanjila, Mkuu wa Wilaya ya Meatu Dkt. Joseph Eliaza Chilongani katika hifadhi ya wanyama ya Makao wilayani Meatu mkoani Simiyu.
  Mkuu wa Wilaya ya Meatu Dkt. Joseph Eliaza Chilongani akiongea jambo mara baada ya kupokea ugeni kutoka Wizara ya Madini katika wilaya yake ya Meatu
  Afisa Madini wa Mkoa wa Simiyu, Mhandisi Fredy Mahobe akizungumza jambo wakati wa kikao baina ya ujumbe kutoka Wizara ya Madini, Mkuu wa Wilaya ya Meatu Joseph Eliaza Chilongani na kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya Meatu.

  ………………………………..
  Aeleza itafika kokote madini yanakochimbwa pasipo vibali halali

  Na Nuru Mwasampeta

  Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko amewaeleza watanzania wasiofuata Sheria katika utafutaji, uchimbaji na biashara ya madini nchini kuwa Serikali inaona na itafika popote madini yanapochibwa pasipo vibali halali vya kufanya shughuli hiyo.

  Biteko ameyasema hayo mwishoni mwa wiki, Tarehe 5 mwezi Januari, 2019 alipofanya ziara ya kukagua eneo ambako shughuli za uchimbaji wa madini ya shaba ulifanywa pasipo kibali na kubaini viashiria vya uchimbaji katika hifadhi ya Wanyama pori ya Makao iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu.

  Akizungumzia lengo la ziara hiyo, Biteko alisema kumekuwa na viashiria vya kuwepo kwa watu wasiokuwa waaminifu na kujiingiza katika shughuli ya uchimbaji pasipokuwa na vibali jambo ambalo halikubaliki na halitavumilika. “Sisi madini yanatuuma, tukisikia kuna watu wanachimba tutafika mahali popote kujua madini hayo yanachimbwa na kupelekwa wapi” Biteko alikazia.

  Aliendelea kwa kusema, huu mchezo ulifanyika sana na sasa nimekuja kuwaambia hautajirudia tena. Endapo mtu yeyote anataka kuchimba madini ya yoyote ikiwa ni pamoja na madini ya ujenzi kama vile mchanga wa kutengenezea barabara sharti afike katika ofisi zetu za madini aeleze nia na eneo analotakiwa kutengeneza barabara na wahusika watamuonesha eneo la kuchimba mchanga kwa utaratibu wa kisheria kwa matumizi hayo si kujiamlia tu.

  Biteko alisisitiza kuwa lengo la ziara hiyo si kutoa kibali kwa watu kuchimba katika hifadhi hiyo. “Sisi hatujaja kupromote watu wachimbe bali tumekuja kwa sababu watu wanachimba pasipo taratibu.

  Alibainisha kuwa ili mtu yeyote apate kibali cha kuchimba katika hifadhi hiyo sharti apate kibali kutoka mamlaka kuu nne ambazo ni Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Maji kwa sababu katika hifadhi hiyo kuna vyanzo vya maji, Mamlaka ya Mazingira (NEMC)pamoja na Wizara ya Madini.

  Katika ziara hiyo ya kushtukiza Biteko aliambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila aliyeelezea sheria na taratibu zinazopaswa kufuatwa ili mtu yeyote kuweza kujihusisha na shughuli za Madini.

  Aidha, Profesa Msanjila aliwataka watanzania kujua kuwa rasilimali madini zinazopatikana nchini ni kwa manufaa ya watanzania wote hivyo ni lazima wafuate utaratibu ili mapato yatokanayo na tozo mbalimbali kutokana na utafiti, uchimbaji na biashara ya madini ziwanufaishe watanzania wote. “Lazima niwaambie haya madini ni ya watanzania wote” alikazia.

  Akizungumzia chanzo cha taarifa ya kuwepo kwa uchimbaji katika hifadhi hiyo Leons Welenseile (Mjiolojia) alisema mnamo mwaka 2016 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu alifanya ziara iliyolenga kutatua mgogoro baina ya kampuni ya inayomiliki leseni ya uwindaji wanyamapori katika hifadhi hiyo Mwiba Holdings Limited na wananchi wanaozunguka hifadhi hiyo baada ya wananchi kutoridhishwa na kile walichokuwa wakikipata kutoka kwa mwekezaji huyo.

  Walipokuwa njiani kutoka katika kusuluhisha mgogoro huo ndipo wataalamu wa madini katika mkoa huo walikutana na loli lililobeba mchanga pasipokuwa na vibali halali vya kufanya uchimbaji huo nakubaini kuwa shughuli hiyo ilikuwa ikifanywa na kampuni hiyo ya mwiba kwa lengo la kukarabati barabara katika hifadhi hiyo pasipo kujua kuwa walipaswa kuwa na leseni ya kuchimba mchanga huo na kupigiwa hesabu iliyopelekea kulipa mrabaha wa milioni 50 baada ya kukiri kufanya shughuli hiyo kwa muda mrefu.

  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Meatu Dkt. Joseph Eliaza Chilongani alikiri kutokuwa na taarifa za uchimbaji huo na kuwataka wataalamu na maafisa madini katika eneo lake kutoa taarifa pindi masuala ya ukiukwaji wa taratibu na sheria za nchi yanapotokea katika eneo lake ili kuweza kushirikiana katika kutatua changamoto hizo.

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (katikati) akipata maelezo toka kwa Meneja wa TARURA Wilaya ya Kasulu kuhusu ujenzi wa barabara ya lamo ya katikati ya mji wa Kasulu
  Barabara ya Kasulu inayojengwa kwa kiwango cha Lami
  Kituo cha Afya Rusesa kinachoendelea kujengwa katika Wilaya ya Kasulu


  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI ametoa la Moyoni kwa kuwaeleza Mkuu wa Wilaya ya Kasulu pamoja na viongozi wenzake kwamba wamejipanga vyema katika kuwatumikia wananchi wa Kasulu. 

  Waziri Jafo ametoa kauli hiyo ya kufurahishwa baada ya kutembelea miradi minne ya sekta ya afya pamoja na barabara wilayani humo na kuridhishwa Sana na usimamizi mzuri wa miradi Hiyo. Miradi aliyo ikagua ni pamoja na ujenzi wa barabara ya Lami katika Halmashauri ya mji wa Kasulu, ukarabati wa Hospitali ya Mji Kasulu na Kituo cha Afya Kiganamo. 

  Pia katika halmashauri ya wilaya Kasulu Waziri Jafo alifanikiwa kukagua kituo kimoja cha Afya cha Rusesa ambacho ni moja ya kituo cha afya kati ya vituo vya afya vitatu vilivyojengwa na Serikali katika halmashauri hiyo. 

  Katika Zara hiyo waziri Jafo alimshukuru sana Mhe. Daniel Nsanzugwako Mbunge wa Jimbo la Kasulu Mjini na Mhe. Vuma Mbunge wa Jimbo la Kasulu vijijini kwa kufikisha kilio cha wananchi wao serikalini hadi serikali imefanikisha kutekeleza miradi hiyo muhimu yenye maslahi mapana kwa wananchi. 

  Wakati huo huo waziri Jafo amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Kigoma kuwezesha upatikanaji wa malighafi za ujenzi wa barabara ya Lami Kasulu Mjini kwani mkandarasi anayejenga barabara hiyo iliyo chini ya TARURA amekwama kupata malighafi za CRS ambayo inapatikana kwa eneo la wakandarasi wa Ki-China anayejenga barabara za TANROADS.

  0 0

  Na Abdullatif Yunus - Bukoba.

  Katika kutekeleza Agizo la Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Wamezindua zoezi tekeleza agizo la Mh. Rais Magufuli la kugawa Vitambulisho kwa wajasiliamali wadogo wadogo katika Halmasahauri yao, Zoezi ambalo limefanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Bukoba (chemba) mnamo Januari 7, 2019. 

  Akizungumza mara baada ya kugawa Vitambulisho hivyo Mh. Deogratius Muganyizi Kashasha (Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bukoba) Amewataka wajasiliamali hao kuwa mabalozi wa wengine ambao hawajapata Vitambulisho hivyo ili wafanye Hima kujipatia Vitambulisho, sambamba na kuwakumbukusha jukumu la kulipa kodi kwa maendeleo ya Taifa.

  Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Ndg, Solomon Kimilike Amenukuliwa akisema kuwa Zoezi hilo la Ugawaji wa Vitambulisho linaendelea kwa wajasiliamali wengine ambao wameshindwa kufika katika Uzinduzi, kutokana na sababu mbalimbali na kuongeza kuwa Kuanzia Januari 09, 2019 Watakuwa na ziara ya kuzungukia Vijiji na Kata ndani ya Halmashauri ili kugawa Vitambulisho hivyo kwa Wajasiliamali wenye sifa na vigezo.

  Aidha kwa upande mwingine Mkurugenzi huyo amewataka wananchi hasa wafanyabiashara wakubwa kutofanya Udanganyifu kwa kuwatumia wajasiliamali wadogo kujipatia vitambulisho, na kuwa kwa yeyote atakayebainika kufanya hivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

  Tayari Vitambulisho 37 kati ya 1,317 vimegawiwa kwa Wajasiliamali baadhi ambao wamejitokeza kuchukua Vitambulisho hivyo huku wakionekana kuwa na Imani na Serikali ya awamu ya Tano, chini ya Dkt. John Pombe Magufuli, kwa kuwasaidia watanzania wenye hali ya chini.

  Pichani ni Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Bukoba Mh. Kashasha akimkabidhi Kitambulisho chake Mjasiliamali Kutoka Kata ya Rubale Bwn.Edisoni Nicholaus, Katikati ni Mkurugenzi Ndg. Solomon.

  Pichani: Wanaonekana wajasiliamali Bi. Praxeda Rauliani, Bi. Liliani Richard na Bi Alistidia Petro wakiwa na furaha mara baada ya kukabidhiwa Vitambulisho vyao katika ukumbi wa Halmashauri ya Bukoba.
  Makamu Mwenyekiti Mh. Kashasha akisitiza jambo mara Baada ya Kukabidhi Vitambulisho 37 kwa wajasiliamali wadogo kati ya Vitambulisho 1,317, pembeni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bukoba Ndg. Solomon Kilimike.
  Bwn Edisoni Nicholausi mkazi wa Rubale, akiwa ameshikilia Kitambulisho cha ke mara baada ya kukabidhiwa

  0 0  0 0
  Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mhe. Gift Msuya akizungumza na Mama Wadogo (Young Mothers) wakati wa ufunguzi wa mafunzo yaliyofanyika Wilaya ya Uyui, Mkoa wa Tabora.
  Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Bw. Julius Tweneshe akifafanua jambo kwa Mama wadogo walioshiriki mafunzo hayo kuhusu malengo ya mafunzo hayo yanayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu).
  Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Godfrey Massawe akieleza jambo kwa Mama wadogo walioshiriki kwenye mafunzo hayo.

  Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bi. Atupokile Mhalila akitoa mada kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kwa Mama wadogo walioshiriki kwenye maunzo hayo yalifanyika Wilaya ya Uyui.


  Baadhi ya Mama wadogo wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mhe. Gift Msuya (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Uyui.
  Baadhi ya Mama wadogo wakifuatilia mada zilizokuwa zinawasilishwa na Afisa Maendeleo ya Vijana Bi. Atupokile Mhalila (hayupo pichani) kuhusu uundwaji wa vikundi vya uzalishaji mali .
  Afisa Lishe wa Wilaya ya Uyui Bi. Pereciah Bynmanyilwohi akiwasilisha mada kuhusu Lishe bora kwa Mama wadogo walioshiriki kwenye mafunzo hayo.
  Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mhe. Gift Msuya (katikati) akielezea jambo kwa baadhi ya Mama wadogo walioshiriki mafunzo hayo yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Uyui.
  Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bi. Dorah Meena (kulia) akijadili jambo kuhusu uundwaji vikundi vya uzalishaji mali kwa Mama wadogo walioshiriki kwenye maunzo hayo yalifanyika Wilaya ya Uyui. (Kushoto) ni Afisa Maendeleo ya Vijana wa Uyui Bi. Johari Gunda
  Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mhe. Gift Msuya akiwa kwenye picha ya pamoja na Mama wadogo walioshiriki mafunzo mara baada ya ufunguzi. (Kushoto) ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Bw. Julius Tweneshe .PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)


  Na OWM (KVAU) – Tabora

  Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu inaratibu mafunzo maalum kwa mama wadogo yanayolenga kuwawezesha kujitambua na kujithamini.

  Mafunzo hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Uyui iliyopo Mkoani Tabora ambapo mama wadogo takribani 45 wamefundishwa mada mbalimbali ikiwemo Ujasiriamali, kilimo biashara, taratibu za kuunda vikundi vya uzalishaji mali, fursa za uwezeshaji wa vijana kiuchumi, malezi bora na familia, afya na lishe.

  Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mhe. Gift Msuya amesema kuwa Serikali inatambua tatizo la mimba za utotoni na imeonesha dhairi ufuatiliaji wa suala hilo kwa kuwachukulia hatua za kisheria wanaohusika na vitendo hivyo.

  “Takribani asilimia 45 ya mabinti wanaoandikishwa kujiunga na kidato cha kwanza wanashindwa kumaliza kidato cha nne kutokana na changamoto za mimba za utotoni, ndoa za utotoni na umbali wa kupata huduma ya elimu.” alisema Msuya

  Aidha, Msuya alieleza kuwa Halmashauri yake imeanzisha kampeni ya “Nishike Mkono, Boresha Elimu Uyui” inayolenga kuwainua watoto wa kike kwa kuwaboreshea mazingira ya elimu yatakayo wawezesha kupata elimu bora.

  Aliongeza kuwa Mkoa wa Tabora umekuwa ukitekeleza kwa vitendo Mpango wa Kitaifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto wa mwaka 2017/18 – 2021/22 ambapo miongoni mwa mikakati ya mpango huo ni kupunguza kiwango cha mimba kwa vijana wa kike.

  Pia alitoa rai kwa vijana walioshiriki mafunzo hayo, wakawe mabalozi wazuri kwa kufikisha elimu kwa vijana wenzao ili wafahamu njia za kuepuka mimba zisizo tarajiwa na waweze kuchangamkia fursa mbalimbali zitakazowawezesha kujikwamua kiuchumi.

  Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Bw. Julius Tweneshe alieleza kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu inaratibu programu ya mama wadogo kitaifa inayokusudia kuwawezesha kupata mbinu na stadi za kujitambua, kuthubutu, kufanya maamuzi sahihi na kujiwekea malengo katika maisha yao.

  “Tutatumia mafunzo haya kuhakikisha vijana wanachangamkia fursa za kiuchumi kupitia vikundi vya uzalishaji mali ambavyo vitawasaidia kujipatia kipato na kuweza kutunza watoto wao.” alisema Tweneshe

  Naye Afisa Ustawi wa Jamii wa Mkoa wa Tabora Bw. Baraka Mackona aliweza kuishukuru Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu kwa kuandaa mpango wa mafunzo hayo ya mama wadogo kwa kuanza na Halmashauri ya Uyui na Kaliua.

  “Tumeanza na halmashauri hizi mbili kutokana na ukubwa wa tatizo, hivyo kuwajengea uwezo vijana wa kike kutachangia kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo hili la mimba za utotoni.” alisema Mackona

  0 0

  World Bank Group President Jim Yong Kim today announced that he will be stepping down from his position after more than six years in which the institution’s shareholders provided strong support to multiple initiatives to ensure that the Bank Group retains strong leadership in the world of global development.

  “It has been a great honor to serve as President of this remarkable institution, full of passionate individuals dedicated to the mission of ending extreme poverty in our lifetime,” said Kim. “The work of the World Bank Group is more important now than ever as the aspirations of the poor rise all over the world, and problems like climate change, pandemics, famine and refugees continue to grow in both their scale and complexity. Serving as President and helping position the institution squarely in the middle of all these challenges has been a great privilege.”

  Under Kim’s leadership, and with the backing of the Bank Group’s 189 member countries, the institution in 2012 established two goals: to end extreme poverty by 2030; and to boost shared prosperity, focusing on the bottom 40 percent of the population in developing countries. These goals now guide and inform the institution in its daily work around the globe.

  In addition, shareholders strongly supported measures to ensure that the Bank Group be even better positioned to respond to the development needs of clients:
  · The Bank Group’s Fund for the Poorest, IDA, achieved two successive, record replenishments, which enabled the institution to increase its work in areas suffering from fragility, conflict, and violence.

  · In April 2018, the Bank Group’s Governors overwhelmingly approved a historic USD$13 billion capital increase for IBRD and IFC that will allow the Bank Group to support countries in reaching their development goals while responding to crises such as climate change, pandemics, fragility, and underinvestment in human capital around the world.

  Over the past 6+ years, the institutions of the World Bank Group have provided financing at levels never seen outside of a financial crisis.

  Recognizing the power of capital markets to transform development finance, the Bank Group during Kim’s tenure also launched several new innovative financial instruments, including facilities to address infrastructure needs, prevent pandemics, and help the millions of people forcibly displaced from their homes by climate shocks, conflict, and violence. The Bank is also working with the United Nations and leading technology companies to implement the Famine Action Mechanism, to detect warning signs earlier and prevent famines before they begin.

  During his term, President Kim emphasized that one of the greatest needs in the developing world is infrastructure finance, and he pushed the Bank Group to maximize finance for development by working with a new cadre of private sector partners committed to building sustainable, climate-smart infrastructure in developing countries.

  To that end, Kim has announced that, immediately after his departure, he will join a firm and focus on increasing infrastructure investments in developing countries. The details of this new position will be announced shortly.In addition to working on infrastructure investments, Kim announced that he will also be re-joining the board of Partners In Health (PIH), an organization he co-founded more than 30 years ago.

  “I look forward to working once again with my longtime friends and colleagues at PIH on a range of issues in global health and education. I will also continue my engagement with Brown University as a trustee of the Corporation and look forward to serving as a Senior Fellow at Brown’s Watson Institute for International and Public Affairs.”

  Kristalina Georgieva, World Bank CEO, will assume the role of interim President effective February 1.

  0 0

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “B” Silima Haji Haji, wakati akiwasili Zanzibar kwa ziara ya kikazi ya siku moja Januari 8, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  WAGONJWA 45 KUFANYIWA UPASUAJI WA MOYO WA KUFUNGUA NA BILA KUFUNGUA KIFUA KATIKA KAMBI MAALUM YA MATIBABU YA MOYO INAYOFANYIKA KATIKA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE KUANZIA TAREHE 7/01/2019  HADI 18/01/2019


  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kupitia madaktari wake bingwa wa magonjwa ya moyo kwa kushirikiana na Madaktari Afrika na Shirika la Cardio Start wote kutoka nchini Marekani  wameanza  kambi maalum ya matibabu ya moyo  ya siku 12  kwa watu wazima .

  Matibabu yanayofanyika  katika kambi hiyo ni upasuaji wa kufungua kifua na bila kufungua kifua. Upasuaji wa bila kufungua kifua unafanyika kupitia tundu dogo linalotobolewa kwenye paja kwa wagonjwa kuzibuliwa mishipa ya moyo iliyoziba (Percutaneous Coronary Intervention - PCI) na kuwekewa vifaa  vinavyosaidia kurekebisha mapigo ya moyo ambavyo ni (Permanent Pacemaker na High powered devices CRT-P, CRT –D) .

  Wagonjwa watakaofanyiwa upasuaji ni wale wenye matatizo ya moyo ambayo ni  valve, mishipa ya moyo iliyoziba, moyo kushindwa kufanya kazi vizuri, matibabu kwa watu wazima waliozaliwa na matatizo ya moyo na wale wenye matatizo ya moyo yaliyotokana  na ugonjwa wa Kisukari

  Kambi hii inaenda  sambamba na utoaji wa elimu kwa madaktari na wauguzi pamoja na kubadilishana ujuzi wa kazi kwa wageni na wataalamu wetu. Katika kambi hii tunatarajia kufanya upasuaji wa kufungua kifua kwa wagonjwa  20 na bila kufungua kifua kwa wagonjwa 25. Hadi leo tarehe 8/1/2019 jumla ya wagonjwa nane wamefanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua na wagonjwa wanne wamefanyiwa upasuaji wa kufungua kifua.

  Hii ni kambi ya kwanza ya matibabu ya moyo tangu kuanza kwa mwaka huu wa 2019 na ni mara ya kwanza kwa shirika Cardio Start  kuja  hapa nchini kufanya kazi na sisi.
  Imetolewa na:

  Kitengo cha Uhusiano
  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
  08/01/2019

  0 0

  Na Khadija Seif,Globu ya jamii

  BENKI ya I&M imentangaza washindi watano katika  droo ya tatu na ya mwisho ya  promosheni ya JIDABO na I&M benki.
   
  Akizungumza Na waandishi wa habari katika droo hiyo ,Meneja Masoko na Mawasiliano Emmanuel Kiondo amesema Kampeni ya "JIDABO na I&M Benki ilizinduliwa mwanzoni mwa mwezi Oktoba na imedumu kwa miezi mitatu ambapo kila mwezi washindi watano wamekua wakipatikana na kutangazwa.

   Washindi watano waliopatikana leo wanafanya jumla ya idadi ya washindi wote waliopatikana katika kipindi cha miezi mitatu ya promosheni ya "JIDABO na I&M Benki" kufikia 15 ambapo kila mshindi hupata mara mbili ya akiba iliyopo kwenye akaunti yake hadi kufikia kiasi cha juu cha sh.milioni tano za " amesema Kiondo.

  Hata hivyo Kiondo amefafanua jinsi vigezo vilivyopaswa mshiriki azingatie ikiwemo kufungua Akaunti ya Akiba,Akaunti ya Biashara ,Akaunti ya Mshahara,Akaunti ya mtoto katika tawi lolote la benki ya I&M katika kipindi cha promosheni.

  Kwa upande wa muwakilishi kutoka  Bodi ya Taifa ya Michezo ya kubahatisha Humud Abdul Hussein amesema ni muamko mkubwa kuona watanzania wengi wameshabadilisha maisha ya kupitia Michezo ya kubahatisha kama ya JIDABO na I &M Benki ambapo washindi wengi wameweza kusomesha watoto,kuendesha familia zao pamoja na biashara.

  Hata hivyo ametoa pongezi kwa benki hiyo kwa kufanya promosheni hiyo na leo kufika tamati na kutangaza washindi watano waliopatikana katika droo hiyo ya mwisho wakiwemo Poulomi Joshi ,Jenipher Fredrick ,Thomas Obadia Malisa,Kefren Charles Buhongo  pamoja na Kampuni ya Unisoft Technologies.

   Aidha  mshindi wa droo ya promosheni hiyo iliyopita ya mwezi Novemba  Kennedy George amesema pesa alizoshinda ataweza kufanyia biashara zake pamoja na kumalizia ujenzi wa nyumba yake.Pia ametoa rai kwa watanzania kuwa Michezo ya kubahatisha ni michezo ambayo hakuna mtu ambae anapangwa na hakuna njia ya panya yoyote inayotumika katika kutafuta mshindi.
   Meneja Masoko na Mawasiliano Emmanuel Kiondo, Benki ya I & M akiwa na muwakilishi kutoka Bodi ya Taifa ya Michezo ya Kubahatisha Humudi Abdul pamoja na mshindi wa droo ya mwezi novemba Kennedy George wakichezesha droo ya pili iliyofanyika leo na kuwatangaza washindi  watano wa Promoshei ya JIDABO na I & M Bank chini ya usimamizi kutoka bodi ya Taifa ya Michezo ya Kubahatisha.
   Muwakilishi kutoka Bodi ya Taifa ya Michezo ya Kubahatisha Humudi Abdul akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam wakati wa kutangaza washindi watano walioshinda kwenye promosheni ya JIDABO na I&M benki jijini Dar es salaam
   Meneja Masoko na Mawasiliano Emmanuel Kiondo  akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam wakati wa kutangaza washindi wa  droo ya mwisho ya promosheni ya JIDABO na I&M benki

  0 0

  Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF) umepongezwa kwa utekelezaji mzuri wa Sera ya Uchumi wa Viwanda inayohimizwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoa mikopo kwa makundi maalumu ya watu wenye ulemavu, akina mama na vijana wanaojihusisha na shughuli za ujasiriamali jijini Dar es Salaam.

  Pongezi hizo zimetolewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa ziara ya kikazi ya kuwatembelea watumishi wa Mfuko wa Rais wa Kujitegemea  kwa lengo la kufahamu majukumu ya mfuko huo na kuhimiza uwajibikaji, ambapo alipata fursa ya kujionea wanufaika wa mikopo inayotolewa na mfuko huo.

  Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema kuwa, makundi yaliyopatiwa mikopo ambayo ni kundi maalumu la walemavu la Furaha ya Wanawake Wajasiriamali Viziwi Tanzania (FUWAVITA), kikundi cha UWAZI  SHALOOM cha akina mama wasindikaji, Kikundi cha MAKINI FOOD SUPPLIES cha akina mama wasindikaji na kikundi cha MAB cha vijana ni mfano mzuri wa kuigwa kwa kutekeleza sera ya Uchumi wa viwanda kwa vitendo kwani wanazalisha bidhaa zenye ubora ambazo ni mvinyo, viungo vya mchuzi, viungo vya chai, siagi ya karanga, mango pickle na mabeji ya wanafunzi wa shule za awali, za msingi na vyuo.
   Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF) wakati wa ziara ya kikazi alipowatembelea ofisini kwao jijini Dar es Salaam  kwa lengo la kufahamu majukumu ya mfuko na kuhimiza uwajibikaji, ambapo pia alipata fursa ya kujionea wanufaika wa mikopo inayotolewa na mfuko huo.
   Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akikabidhiwa nyaraka mbalimbali na Mkurugenzi wa Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF) Bi. Haigath Kitala mara baada ya mkurugenzi huyo kuwasilisha taarifa ya utekelezaji  wakati wa ziara ya kikazi ya Dkt. Mwanjelwa katika ofisi za PTF jijini Dar es Salaam,  ziara ilikuwa na lengo la kufahamu majukumu ya mfuko na kuhimiza uwajibikaji.
   Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akisikiliza maelezo ya Bi. Rose Kalulika kuhusu bidhaa zinazozalishwa  na kikundi cha akina mama cha UWAZI SHALOOM  wakati wa ziara ya  kikazi katika ofisi za PTF jijini Dar es Salaam,  ambapo alipata fursa ya kuzungumza na wanufaika hao wa mikopo inayotolewa na PTF.
   Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akishuhudia bidhaa zinazotengenezwa na  kikundi cha Furaha ya Wanawake Wajasiriamali Viziwi  Tanzania (FUWAVITA), kikundi cha UWAZI  SHALOOM cha akina mama wasindikaji, Kikundi cha MAKINI FOOD SUPPLIES cha akina mama wasindikaji na kikundi cha MAB cha vijana  wakati wa ziara yake ya  kikazi katika ofisi za PTF jijini Dar es Salaam,  ambapo alipata fursa ya kuzungumza na wanufaika hao wa mikopo inayotolewa na PTF.  0 0older | 1 | .... | 1770 | 1771 | (Page 1772) | 1773 | 1774 | .... | 1897 | newer