Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

Mbunge Nyamagana akagua miradi mbalimbali ya maendeleo 'vyoo vinatisha'.

$
0
0
Mbunge Jimbo la Nyamaganamkoani Mwanza, Stanslaus Mabula (CCM) ameendelea na ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Jimbo hilo ikiwemo elimu, afya, maji na barabara kusaidia ukamilishaji wa miradi hiyo kupitia fedha za mfuko wa jimbo.Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Ziara ya mbunge Stanslaus Mabula pia ilifika katika Shule ya Msingi Amani Kata ya Butimba na kujionea hali tete ya vyoo na kuchangia ukarabati wake.
Mbunge Stanslaus Mabula alifika katika Shule ya Msingi Amani iliyopo Kata ya Butimba na kutoa fedha kwa ajili ya kukamilisha jengo hili kwa ajili ya kupunguza uhaba wa vyumba vya madarasa.
Mbunge Stanslaus Mabula pia aliwasili katika Shule ya Msingi Igoma C na kusaidia ukarabati wa shule hiyo.
Ukarabati ukiendelea katika Shule ya Msingi Igoma C Jijini Mwanza.
Ukarabatai katika Shule ya Msingi Igoma C.
Mbunge Stanslaus Mabula pia alisaidia ujenzi wa Kituo cha Polisi Kata ya Kishiri.
Kituo cha Polisi Kata ya Kishiri Jijini Mwanza.
Mbunge Stanslaus Mabula pia alisaidia ujenzi wa Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Mahina Kati Kata ya Mahina inayojengwa kwa nguvu za wananchi.
Mbunge Stanslaus Mabula akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali katika Kata ya Mahina.Tazama BMG Online TV hapa chini

SERIKALI YAZIPA KANDARASI YA THAMANI YA 2.9BN KAMPUNI ZA VIJANA KUTEKELEZA MAFUNZO YA KILIMO CHA KITALU NYUMBA

$
0
0

Mafunzo kwa wakufunzi ya kilimo cha Kitalu Nyumba (Green House) na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia wenye ulemavu Mh Ikupa Stella Alex wakiangalia moja ya bidhaa wakati wa uzinduzi wa mafunzo kwa wakufunzi ya kilimo cha Kitalu Nyumba (Green House).
mafunzo kwa wakufunzi ya kilimo cha Kitalu Nyumba (Green House) akitembelea moja ya shamba darasa.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana **Mhe.Anthony Mavunde akizungumza katika uzinduzi wa mafunzo kwa wakufunzi ya kilimo cha Kitalu Nyumba (Green House).
Moja ya Green House


Serikali kupitia Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imezipa Kandarasi ya thamani ya shilingi 2.9 bilioni kampuni tatu za vijana wa Kitanzania ili kutekeleza mafunzo kwa wakufunzi ya kilimo cha Kitalu Nyumba (Green House).

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana Mhe.Anthony Mavunde wakati akizindua mafunzo hayo Januari 05, 2019 yanayoendelea katika Chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine mkoani Morogoro.

Programu hiyo ambayo itatumia jumla ya shilingi 2.9bilioni katika utekelezaji wake ambapo kampuni zilizoshinda kandarasi hiyo ni Kampuni za vijana wazalendo wa kitanzania ambao ni wabobezi katika masuala ya kilimo ikiwemo kampuni na Royal Agriculture Ltd, Holly Green Agriculture Group Ltd, na SUGECO.

Mafunzo haya yatafanyika katika Mikoa yote Tanzania Bara na kuhakikisha Halmashauri 84 zinafikiwa kwa awamu hii ya kwanza lengo likiwa ni kuwajengea vijana ujuzi kupitia kilimo cha kisasa ambapo tayari kwa mwaka huu wa fedha imeanza mafunzo hayo kwa kutumia teknolojia ya Kitalu Nyumba (Green House).


“Kwa kuanzia tutahakikisha kila Halmashauri tunatoa mafunzo kwa vijana 100 na kati yao vijana 20 watapatiwa mafunzo ya kujenga Vitalu Nyumba ili kwa wale watakaopenda kuendelea na kilimo hiki wasikose wataalamu wa kuwajengea Vitalu hivyo ”Alisisitiza Mavunde.

Aidha, Amewataka vijana kutumia fursa ya kilimo katika kujikwamua na changamoto za ajira na kuelezea umuhimu wa kilimo katika kuongeza pato la Taifa na kuchangia katika uchumi wa viwanda nchini.

“Wote tunatambua kwamba kilimo ni uti wa mgongo wa Taifa letu kwani kwasasa kimeajiri takribani asilimia 65.7 ya nguvu kazi nchini na kinachangia asilimia 29.1 ya pato la taifa, pia sekta ya kilimo ndiyo chanzo kikuu cha chakula, ajira, na malighafi ya viwanda”Alisisitiza Mavunde.


Naye Naibu Waziri anayeshughulikia masuala ya wenye ulemavu Mh Ikupa Stella Alex amebainisha kwamba program hii na jumuishi na hivyo kutoa rai kwa watekelezaji wa program hii katika ngazi za mikoa kuhakikisha wanawajumisha pia watu wenye ulemavu ili kunufaika na program hii.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa SUGECO Bw.Revocatus Kimario alieleza kuwa wataendelea kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha wanafikia kundi kubwa la vijana nchini na kushukuru mchango wa serikali katika programu za ukujazi ujuzi kwa vijana.

“Kipekee naishukuru Wizara hii kwa kuendelea kuunga mkono jitihada za kuhakikisha inatoa mchango mkubwa kwa vijana na kusaidia kuwakwamua kiuchumi.”Alisema Kimario

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Ajira Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Ally Msaki aliwataka vijana kutumia fursa hiyo kwa kujiimarisha kupitia mafunzo hayo watakayoyapata ili kujikwamua na tatizo la ajira nchini.

“Tunataka vijana wawe mstari wa mbele katika kilimo cha kisasa ili kuendana na mazingira ya sasa na kujikwamua katika kundi la wasio na ajira nchini”.Alisistiza Msaki.

LUGOLA AWATAKA NIDA WAPITIE UPYA USAJILI, UTOAJI WA VITAMBULISHO VYA TAIFA MIKOA YA KAGERA NA KIGOMA KWA LENGO LA KUWABAINI NA KUWAONDOA RAIA WA NCHI JIRANI

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na wananchi wa mjini Kyerwa Mkoani Kagera, katika Mkutano uliofanyika katika uwanja wa sokoni mjini humo, leo. Lugola amemuagiza Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa apitie upya usajili na utoaji wa vitambulisho vya taifa katika mikoa ya Kagera na Kigoma ili aweze kuwabaini na kuwaondoa raia wa nchi jirani zinazoizunguka mikoa hiyo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akiwasalimia viongozi wa Wilaya ya Kyerwa Mkoani Kagera, wakati alipokuwa anawasili katika uwanja wa sokoni mjini humo, leo, kwa ajili ya kuzungumza na wananchi. Katika hotuba yake, Lugola amemuagiza Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa apitie upya usajili na utoaji wa vitambulisho vya taifa katika mikoa ya Kagera na Kigoma ili aweze kuwabaini na kuwaondoa raia wa nchi jirani zinazoizunguka mikoa hiyo.


Na Felix Mwagara, MOHA-Kyerwa.


WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amemuagiza Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) apitie upya usajili na utoaji wa vitambulisho vya taifa katika mikoa ya Kagera na Kigoma ili aweze kuwabaini na kuwaondoa raia wa nchi jirani zinazoizunguka mikoa hiyo.

Akizungumza na mamia ya wananchi wa Mji wa Kyerwa katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa sokoni mjini humo, leo, Lugola alisema baadhi ya raia wa nchi jirani wamejipenyeza na kujipatia vitambulisho vya taifa ama kwa kuwatumkia wenyeji ama nguvu ya fedha.

“Hii haikubaliki na lazima tuwe makini katika hilo, nimepata taarifa kuhusu watu waliojipatia vitambulisho hivyo ambao hawastahili, kutokana na hilo natoa agizo kuwa, Mkurugenzi Mkuu wa NIDA ahakikishe anapitia upya zoezi la kusajili ili aweze kuwabaini ambao walijipatia kwa njia ambazo sio halali,” alisema Lugola.Lugola alisema kuwa, utoaji wa vitambulisho hivyo katika mikoa hiyo unasuasua kwasababu ya umakini unaofanyika katika kusajili waombaji wa vitambulisho.

“Hakuna Mtanzania atakayekosa vitambyulisho vya taifa, kilka mtu anatapa ili mradi tu awe na sifa, na pia mpaka upate lazima upitie mchujo maalumu ili tuhakikishe wewe tunakupa kitambulisho ni Mtanzania halisi au sio.” Alisema Lugola.Aidha, Lugola pia juzi alimuagiza alimpa wiki mbili Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini (CGI) Dkt Anna Makakara, awe amefika katika mikoa hiyo kwa ajili ya kuanza maandalizi ya kufanya operesheni kubwa ya kuwaondoa Wahamiaji haramu katika Mikoa hiyo kabla ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kuanza mwezi Julai mwaka huu.

Lugola aliyazungumza hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Karagwe akisisitiza kuwa katika mikoa hiyo kuna idadi kubwa ya wahamiaji haramu .Lugola aliongeza kuwa, licha ya kutangaza operesheni hiyo, lakini viongozi wa uhamiaji katika mikoa hiyo wawe makini mara kwa mara kuhakikisha wanawafuatilia wahamiaji hao kwa kuwashirikisha wananchi waaminifu ili waweze kutoa taarfia sahihi za wahamiaji hao.

Waziri huyo pia aliwataka wananchi wa mikoa hiyo watoe ushirikiano na wasiwafiche wahamiaji hao kwasababu kumuhifadhi ni kosa kisheria, hivyo wanapaswa kuhakikisjha wanatoa taarifa za wahamiaji hao kwa maafisa uhamiaji ili waweze kukamatwa.

Lugola alisema alifanya ziara katika Mkoa wa Kigoma kwa kutembelea Wilaya zote kama anavyofanya Mkoa wa Kagera, anapewa kero hiyo katika ziara hiyo, hivyo anataka Uhamiaji wawaondoa wahamiaji wote ndani ya mikoa hiyo ili Watanzania waweze kuishi kwa amani wakiendelea kujionea maendeleo ya uongozi wa Rais Dkt. Magufuli.

Waziri Lugola amemaliza ziara yake Wilaya Kyerwa na Wilaya inafuata ni Ngara, Biharamulo na Muleba, ambapo akiwa katika ziara hiyo, pia uzungumza na wananchi katika mikutano ya hadhara pia ukutana na watumishi waliopo ndani ya Wizara yake ambao ni Jeshi la Polisi, Idara ya Uhamiaji, Jeshi la Magereza, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, pamoja na Idara ya Probesheni ambayo jukumu lake kuu ni kupunguza msongamano gerezani na kusimamia wafungwa waliopewa adhabu mbadala na Mahakama au wafungwa waliopata msamaha kupitia sheria ya huduma kwa jamii na kutumikia kifungo chao nje ya Gereza.

WAZIRI WA KILIMO AZITAKA NFRA NA BODI YA NAFAKA NA MAZAO MCHANGANYIKO KUWA NA MKAKATI WA KUNUNUA NAFAKA ZA WAKULIMA NCHINI

$
0
0
Mhe Japhet Hasunga (Mb) Waziri wa Kilimo, akikagua ujenzi vihenge vya kisasa (Silos) na maghala ya kuhifadhia nafaka kabla ya kuzungumza na wafanyakazi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) Kanda ya Songea Mkoani Ruvuma, Leo tarehe 5 Januari 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songea).
Mhe Japhet Hasunga (Mb) Waziri wa Kilimo, akikagua hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa Vihenge vya kisasa (Silos) na maghala ya kuhifadhia nafaka kabla ya kuzungumza na wafanyakazi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) Kanda ya Songea Mkoani Ruvuma, Leo tarehe 5 Januari 2019.
Muonekano wa hatua zilizofikiwa za mradi wa ujenzi wa Vihenge vya kisasa (Silos) na maghala ya kuhifadhia nafaka umaojengwa na Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) Kanda ya Songea Mkoani Ruvuma, Leo tarehe 5 Januari 2019.
Mhe Japhet Hasunga (Mb) Waziri wa Kilimo, akisalimiana na Mwenyeji wake ambaye ni Meneja wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) Kanda ya Songea Mkoani Ruvuma Ndg Nicodemus Massao wakati alipowasili kwa ajili ya kukagua ujenzi wa vihenge vya kisasa (Silos) na maghala ya kuhifadhia nafaka kabla ya kuzungumza na wafanyakazi wa NFRA Kanda ya Songea Mkoani Ruvuma, Leo tarehe 5 Januari 2019.
Mhe Japhet Hasunga (Mb) Waziri wa Kilimo, akikagua ujenzi vihenge vya kisasa (Silos) na maghala ya kuhifadhia nafaka kabla ya kuzungumza na wafanyakazi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) Kanda ya Songea Mkoani Ruvuma, Leo tarehe 5 Januari 2019.



Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songea

Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) pamoja na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko zimetakiwa kuandaa mikakati ya haraka kuanisha jinsi watakavyo nunua mazao ya wakulima nchini.

Wakati NFRA imetakiwa kuainisha namna ya kununua nafaka za wakulima kwa upande wa Bodi ya Nafaka na Mazao mchanganyiko yenyewe imetakiwa kujikita katika ununuzi wa mazao mbalimbali ya wakulima ikiwa ni pamoja na kutafuta masoko ya mazao ndani na nje ya nchi.

Kauli hiyo imetolewa jana tarehe 5 Januari 2019 na Mhe Japhet Hasunga (Mb) Waziri wa Kilimo, wakati akizungumza na wafanyakazi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) mara baada ya kutembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa maghala na vihenge vya kisasa.Alisema kuwa Wizara yake imekuwa ikihamasisha wakulima nchini kuzalisha kwa wingi mazao kwa ajili ya chakula na biashara lakini inapofika hatua ya kuuza bei zinakuwa ndogo jambo ambalo serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli haitalifumbia macho kamwe.

Pamoja na mambo mengine waziri Hasunga ameupongeza Uongozi wa wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula NFRA kwa ujenzi wa Maghala na Vihenge vya kisasa (Silos) katika maeneo nane ya kanda saba za wakala ambapo ujenzi huo utaongeza uwezo wa kuhifadhi mahindi kutoka Tani 251,000 za sasa hadi Tani 700,000 ifikapo mwaka 2025.

Mradi huo wa kuongeza uwezo wa kuhifadhi umeanza kujengwa katika Manispaa ya Songea (Ruvuma), Dodoma, Mpanda (Katavi), Makambako (Njombe), Mbozi (Songwe), Sumbawanga (Rukwa), Shinyanga Mjini (Shinyanga), na Babati (Manyara) ambapo Serikali ya Tanzania na Serikali ya Poland zilisaini mkataba wa mkopo wa masharti nafuu Septemba 2015 wa Dola milioni 55 sawa na sh. bilioni 124, kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo, ambao utaongeza uwezo wa hifadhi ya chakula.

Mhe Hasunga amesema kuwa pundi utakapokamilika ujenzi wa maghala na vihenge hivyo utapunguza gharama mbalimbali zilizokuwa zinatumika kwa ajili ya kununua madawa ya kufukiza mahindi sambamba na gharama za kununua magunia ya kuhifadhia mahindi.Katika hatua nyingine Waziri huyo amemtaka Kaimu Mtendaji Mkuu wa wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba kuweka msisitizo zaidi wa kununua nafaka ya mahindi kwani katika kipindi chake serikali haitotoa hela kwa ajili ya ununuzi wa mahindi badala yake NFRA ijipange kibiashara ili iweze kununua nafaka nyingi na kujiendesha.

Alisema kuwa huu sio muda wa NFRA kusubiri kupewa mtaji na serikali badala yake kufikiria tofauti na kuanza kufanya biashara ili kufikia walau ununuzi wa nafaka kwa Tani zaidi ya 300,000.Vilevile, ameutaka Wakala wa majengo Tanzania (TBA) kusimamia kwa weledi mradi wa ujenzi wa maghala na vihenge vya kisasa ili kuhakikisha kuwa mradi huo unakamilika kwa wakati ili kuwanufaisha wananchi.

DKT BASHIRU ASHAURI WAKUU WA MIKOA KUJIFUNZA SIMIYU

$
0
0

Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally akizungumza na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali mkoani Simiyu, katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi Januari 05,2019 wakati wa ziara yake mkoani hapa.
Kutoka kushoto Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Mhe. Kheri James na Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally wakifurahia jambo katika kikao cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na viongozi na watendaji wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali mkoani Simiyu, kilichofanyika Mjini Bariadi Januari 05,2019 wakati wa ziara yake mkoani hapa.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally(wa pili kulia)akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe. Benson Kilangi mara baada ya kuwasili wilayani humo kuweka jiwe la msingi la Ofisi ya CCM ya Wilaya, wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM mkoani Simiyu Januari 05, 2019 .
Baadhi ya viongozi wa CCM wa Mkoa wa Simiyu wakicheza nyimbo za Chama wakati wakijiandaa kumpokea Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally(hayupo pichani) katika Mji mdogo wa Lamadi wilayani Busega, kwa ajili ya kuanza ziara ya siku mbili mkoani hapa Januari 05 na Januari 06 , 2019.
Kutoka kushoto Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Mhe. Kheri James na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo wakifurahia jambo katika kikao cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na viongozi na watendaji wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi Januari 05,2019 wakati wa ziara yake mkoani hapa.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akichangia hoja katika kikao cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na viongozi na watendaji wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi Januari 05,2019 wakati wa ziara yake mkoani hapa.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, mhe. Anthony Mtaka akiwasilisha taarifa ya Serikali katika kikao cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na viongozi na watendaji wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi Januari 05,2019 wakati wa ziara yake mkoani hapa
Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally(wa tano kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi na viongozi wa Serikali wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya k kikao chake na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi Januari 05, 2019

Na Stella Kalinga, Simiyu


Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally amewashauri Wakuu wa Mikoa hapa nchini kwenda(kuja) kujifunza namna ya kufanya kazi kwa umoja na mshikamano kati ya Chama na Serikali sambamba na ubunifu na uchapakazi wa viongozi wa mkoa huo.

Dkt. Bashiru ameyasema hayo Januari 05, 2019 wakati akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM pamoja na Viongozi na watendaji wa Serikali, Mjini Bariadi wakati akiwa katika ziara yake mkoani Simiyu.

Dkt. Bashiru amewapongeza Viongozi wa Serikali wakingozwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kwa namna wanavyoshirikiana na viongozi wa Chama kwa namna wanavyosimamia shughuli za maendeleo.

“Niwapongeze kwa namna mnavyosimamia shughuli za maendeleo, nilikuwa hapa mwaka 2005 kama msimamizi wa uchaguzi nilizunguka maeneo mengi mengine yalikuwa hayapitiki, leo nimekuja nikazungushwa maeneo machache tu, nimeona mambo mengi sana ya tofauti kwa hiyo uongozi wa mkoa huu kwa Chama na Serikali umefanya kazi kubwa na bado mna nafasi kubwa ya kufanya mambo makubwa zaidi” alisema

Aidha, amesema ili uchumi uwe imara, wa kisasa na wenye manufaa ni lazima uwe jumuishi na uwalenge watu walio wengi ambao ni wazalishaji wadogo hususani katika katika sekta ya kilimo na viwanda huku akisisitiza umakini zaidi ili uwepo wa viwanda na maendeleo ya kilimo viwanufaishe wengi.

Ameongeza kuwa wakati Mkoa wa Simiyu unapanga mipango mbalimbali ya maendeleo ya kiuchumi ni vema kukawa na mpango wa matumizi bora ya ardhi, ili kuondoa migogoro kwa watumiaji ambayo inakuwa chanzo cha chuki na watu kuishi kwa wasiwasi.Katika hatua nyingine Dkt. Bashiru amesema CCM imejipanga kuhakikisha kuwa itasimamia na kuimarisha ushirika ambao utasimamiwa na wataalam wenye taaluma na maadili ili uweze kuwanufaisha wanaushirika na kutatua changamoto zao.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema kuwa Viongozi na watendaji wa Serikali Mkoani humo watahakikisha wanasimamia utekelezaji wa Ilani ya CCM huku akisisitiza kuwa fedha zote zinazoletwa katika mkoa wa Simiyu zitasimamiwa vizuri na zitafanya kazi iliyokusudiwa.

Aidha, Mtaka amesema Mkoa wa Simiyu unafanya utafiti kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) ili kubaini fursa za kiuchumi zilizopo katika katika kila kijiji kwa Vijiji vyote 470, ambapo utekelezaji wa Falsafa ya Kijiji Kimoja Bidhaa Moja(OVOP) unatarajiwa kuzinduliwa rasmi mwezi Februari.

Ameongeza kuwa viwanda vikubwa vitatu vyenye uwezo wa kuajiri takribani wafanyakazi 2000 kikiwepo kiwanda cha chaki na kiwanda cha vifungashio (Maswa) kiwanda cha bidhaa 18 za afya zitokanazo na pamba(Bariadi) vitajengwa mwaka huu 2019 Simiyu.

“Ndugu Katibu Mkuu mwaka jana wakati Mhe. Rais anapokea ndege ya Air Bus alicheza muziki na ukiangalia ilikuwa ni kitu kinachotoka moyoni kuonesha furaha yake, ninaamini mwaka 2019 Mhe. Rais ataucheza muziki huo hapa Simiyu” alisema Mtaka.

Naye Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri James ambaye ni Mlezi wa CCM Mkoa wa Simiyu amesisitiza viongozi na wanachama kuimarisha uhusiano mzuri, kusaidiana na kupendana katika maisha ya siasa huku akiwasihi viongozi kulinda na kuheshimu dhamana walizopewa kwa kutimiza wajibu wao.

Akitoa salamu kwa niaba ya Wabunge wa Mkoa wa Simiyu, Mbunge wa Bariadi,Mhe. Andrew Chenge ametoa wito kwa viongozi na wanachama wa CCM mkoani Simiyu kudumisha upendo, umoja na mshikamano hususani katika kipindi cha kueleka uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally yuko Mkoani Simiyu kuanzia Januari 05,2019 kwa ziara ya kikazi ya siku mbili yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM mkoani humo.

MTENDAJI MKUU TEMESA AFANYA ZIARA MIKOA YA ARUSHA NA KILIMANJARO

$
0
0

 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle kulia akikagua mashine ya kuchongea vipuri vya injini za magari katika karakana ya TEMESA mkoa wa Kilimanjaro wakati wa ziara yake mkoani humo kukagua utendaji kazi na kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wafanyakazi wa wakala huo. Kushoto ni Meneja wa Temesa mkoani humo Mhandisi Ferdinand Mishamo.
????????????????????????????????????
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle kulia akielezea jinsi mashine ya kubadilishia tairi za magari inavyofanya kazi wakati akikagua mashine mbalimbali zilizopo katika karakana ya TEMESA mkoa wa Kilimanjaro. Kushoto ni Meneja wa TEMESA mkoani humo Mhandisi Ferdinand Mishamo.
????????????????????????????????????
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle kulia akitoa maelekezo wakati akikagua mashine ya kubadilishia tairi za magari katika karakana ya TEMESA mkoa wa Kilimanjaro alipotembelea kujionea utendaji kazi na kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wafanyakazi wa wakala huo. Kushoto ni Meneja wa TEMESA mkoani humo Mhandisi Ferdinand Mishamo.
????????????????????????????????????
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle kushoto akitoa maelekezo kwa mafundi na wafanyakazi wa karakana ya mkoa wa Arusha mara baada ya kukagua mtambo wa kuchenjua na kuchakata kokoto (Crusher) unaoonekana pichani.
????????????????????????????????????
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle katikati (aliyevaa koti) akikagua mitambo mbalimbali iliyopo katika karakana ya wakala huo mkoani Arusha.
????????????????????????????????????
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle kushoto akitoa maagizo kwa mafundi wakati akikagua kitengo cha matengenezo ya majokofu na viyoyozi katika karakana ya wakala huo mkoani Arusha.
????????????????????????????????????
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle kulia akiitazama gari iliyopakwa rangi katika kitengo cha upakaji rangi kilichopo katika karakana ya TEMESA mkoani Kilimanjaro, kushoto ni Meneja wa wakala huo mkoani Kilimanjaro Mhandisi Ferdinand Mishamo.



NA ALFRED MGWENO TEMESA


Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle amefanya ziara katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro na kuwataka wafanyakazi wa Wakala huo katika mikoa hiyo kuongeza juhudi katika kazi ili kuhakikisha wanazalisha kipato cha kutosha kuweza kufikia malengo au hata kuzidi mapato waliyojiwekea kwa mwaka huu wa fedha wa 2018/2019.


Akizungumza na wafanyakazi hao kwa nyakati tofauti, Mhandisi Maselle alisema anatambua kwamba TEMESA inakumbwa na changamoto nyingi za kiutendaji ikiwemo ukosefu wa vifaa vya kutendea kazi hasa vya karakana pamoja na upungufu wa wafanyakazi lakini aliwataka mameneja wa mikoa hiyo pamoja na watumishi wake kujitahidi kufanya kazi zao kwa ufansi na kwa ushirikiano huku akiangalia namna ya kuwaongezea vitendea kazi na kujaza nafasi za watumishi zilizoachwa wazi baada ya kustaafu.


Katika mazungumzo yake Mhandisi Maselle alisisitiza kwamba, Kiongozi mzuri ni yule ambaye anafanya kazi bega kwa bega na wafanyakazi wenzake pale anapoona mapungufu na kuwatia moyo hivyo meneja ajitahidi kuwa karibu na watumishi wake.

Awali, Meneja wa TEMESA Mkoa wa Kilimanjaro Mhandisi Ferdinand Mishamo, alimpitisha Mtendaji Mkuu katika karakana ya mkoa ambapo alipata nafasi ya kukagua mashine na mitambo mbalimbali iliyopo katika karakana hiyo na baadae alimkaribisha katika kikao na watumishi na kumkumbushia kuhusu changamoto zinazoukumba wakala kubwa likiwa ni upungufu wa wafanyakazi ambapo karibu kila kitengo kina mtumishi mmoja mmoja ikiwemo kitengo cha uhasibu na kitengo cha manunuzi na kumuomba kuzifanyia kazi kwa wakati ili kuhakikisha watendaji wa mkoa huo wanapata wasaidizi ili waweze kutenda kazi zao kwa ufanisi. Mhandisi Maselle alimuahidi kumuongezea watumishi hasa katika upande wa karakana ambapo ndipo kuna upungufu mkubwa.

Katika hatua nyingine, akiwa mkoani Arusha, Mhandisi Maselle alipata pia wasaa wa kukagua mashine mbalimbali za kuchonga vipuri vya injini za magari, mashine za kuchomelea pamoja na mitambo mikubwa iliyopo katika karakana hiyo. Mtendaji Mkuu alimaliza ziara yake kwa kuzungumza na wafanyakazi wa mkoa huo na kuahidi kuzitafutia ufumbuzi kero zao kwa wakati ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi. Mhandisi Masellle alibanini kuwa matatizo ya karakana katika mikoa yote hiyo yanafanana na hivyo hayana budi kuchukuliwa hatua stahiki ili kuboresha utendaji wa karakana hizo.

VIONGOZI NA WANANCHI WILAYANI NEWALA WAJUMUIKA NA WAZIRI MKUCHIKA KUOMBOLEZA KIFO CHA MAMA TECLA MKUCHIKA

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akiwaongoza wanafamilia kuwasha mishumaa juu ya kaburi la Bibi Tecla B. Mkuchika, aliyefariki tarehe 2 Januari, 2019 katika Hospitali ya Misheni Ndanda alikopelekwa kupatiwa matibabu. 
Askofu wa Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Masasi, Dkt. James Almasi Askofu Mstaafu Dkt. Mwachiko Boma, Askofu Oscar Mnung’a wa Dayosisi ya Newala na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakiwa katika ibada ya mazishi ya mama mzazi wa Mhe. Mkuchika kabla ya kumpumzisha mama Tecla B. Mkuchika katika nyumba yake ya milele kijiji cha Nambunga Wilayani Newala.
Baadhi ya waombolezaji waliojitokeza kushiriki ibada ya mazishi ya Bibi Tecla B. Mkuchika ambaye ni mama mzazi wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb), aliyefariki tarehe 2 Januari, 2019 katika Hospitali ya Misheni Ndanda alikopelekwa kupatiwa matibabu.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akiwa na ndugu zake wakiweka shada la maua kwenye kaburi la mama yao mpendwa, Bibi Tecla B. Mkuchika aliyefariki tarehe 2 Januari, 2019 katika Hospitali ya Misheni Ndanda alikopelekwa kupatiwa matibabu.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiweka shada la maua kwenye kaburi la mama mzazi wa Mhe. Mkuchika, Bibi Tecla B. Mkuchika aliyefariki tarehe 2 Januari, 2019 katika Hospitali ya Misheni Ndanda alikopelekwa kupatiwa matibabu.



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akipewa pole ya kufiwa na mama mzazi na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) alipoenda kumfariji nyumbani kwake katika kijiji cha Nambunga wilayani Newala.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akipewa pole ya kufiwa na mama mzazi na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Dorothy Mwaluko alipoenda kumfariji nyumbani kwake katika kijiji cha Nambunga wilayani Newala.

………………………….

Viongozi mbalimbali wa serikali, dini, vyama vya siasa, watumishi wa umma na wananchi wilayani Newala wamejitokeza kwa wingi kuungana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt. (Mst) George Mkuchika (Mb) kuomboleza kifo cha mama yake mzazi, Bibi Tecla Bernadetha Mkuchika aliyefariki tarehe 2, 2019 akiwa na umri wa miaka 93 na kuenzi mchango alioutoa katika taifa enzi za uhai wake akiwa mtumishi wa umma na mtumishi katika hospitali zinazoendeshwa na taasisi za kidini.

Akisoma wasifu wa marehemu wakati wa ibada takatifu ya mazishi iliyofanyika katika Kanisa la Anglikana la Msalaba Mtakatifu lililopo kijiji cha Nambunga wilayani Newala, Msemaji wa familia Bw. Noel Boma alisema marehemu alijiunga na Mafunzo ya Ukunga katika Chuo cha kanisa Anglikana (UMCA) mwaka 1943 na mara baada ya kuhitimu alianza kazi St. Mary’s Hospital Newala.

Bw. Boma aliongeza kuwa, marehemu Bibi Mkuchika alihamishiwa Serikalini kutokana na uchapakazi wake, weledi na uadilifu aliokuwa nao wakati akifanya kazi kwenye zahanati ya kanisa la Nambunga na Mnyambe.

Bw. Boma aliainisha kuwa, marehemu akiwa serikalini alifanya kazi katika zahanati za Mihambwe, Mchichira, kitangari, Kilidu na Nambunga mpaka anastaafu.

Aidha, Bw. Boma alisisitiza kuwa, marehemu Bibi. Mkuchika ataendelea kukumbukwa na jamii kwa mchango wake mkubwa alioutoa wakati akihudumu Zahanati ya Kilidu ambayo hivi sasa inatambulika kama Samora kwa kitendo cha kushiriki kikamilifu kutoa huduma usiku na mchana kwa majeruhi wa vita vya ukombozi wa Msumbiji ambavyo vilipamba moto wakati huo.

Sanjari na hayo, Bw. Boma alisema marehemu atakumbukwa kwa sifa ya ucheshi, ukarimu na huruma kwa wagonjwa hususani wa uzazi, sifa ambazo ziliishawishi Serikali kuendelea kumuomba mara kwa mara kuwahudumia wazazi katika kijiji cha Nambuga licha ya kustaafu.

Naye, Baba Askofu wa Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Masasi, Dkt. James Almasi aliwataka waombolezaji kuwalea vizuri wazee katika maeneo wanayoishi kama alivyolelewa Bibi Mkuchika ikiwa ni namna bora ya kutambua na kuenzi mchango walioutoa katika taifa.

Askofu Dkt. Almasi amewahimiza waumini na waombolezaji, kuhakikisha wanawatunza wazazi kwani kwa kufanya hivyo wataishi miaka mingi na yenye heri duniani kama maandiko matakatifu yanavyosema, na kuongeza kuwa asiyetunza wazee wake ni mbaya kama shetani na kamwe hawezi kupata baraka za mwenyezi Mungu ambaye ni mwingi wa rehema.

Naye, Bi. Tecla Mkuchika ambaye ni mtoto wa kwanza wa Mhe. Mkuchika kwa niaba ya wajukuu wote, amewasilisha mchango wa shilingi 1, 000,000/= kwa ajili ya kuendeleza shule ya awali ya watoto ya kanisa la Anglikana la Nambunga ikiwa ni sehemu ya kuenzi upendo aliokuwa nao marehemu kwa watoto wadogo wakiwemo wao wenyewe wajukuu.

Ibada ya mazishi ya Bibi Tecla Bernadetha Mkuchika ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Katibu Mkuu Ikulu, Dkt. Mosses Kasiluka aliyehudhuria kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Wakuu wa Wilaya, Waheshimiwa Wabunge, Wakuu wa taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na watumishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Newala, Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri, Makatibu Tawala Wilaya, Viongozi wa Dini na Vyama vya Siasa na Wananchi wilayani Newala.

aliyewahi kuwa mkuu wa wilaya mbalimbali AFARIKI DUNIA

$
0
0
ALIYEWAHI kuwa mkuu wa wilaya tofauti hapa nchini wakati wa serikali ya awamu ya kwanza na baadaye kushika nyadhifa mbalimbali serikalini ,Waziri Juma Waziri amefariki dunia akitibiwa hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar es salaam Juzi na anatarajiwa kuzikwa leo nyumbani kwao Sungwi baada ya swala adhuhuri.

Kwa mujibu wa watu wa karibu na mzee Waziri, msiba upo nyumbani kwake Tandika Berege Nyumba namba tatu.Mzee Waziri ambaye mwaka huu anatimiza miaka 89 alikufa siku chache tu baada ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa.Akiwa amehudumu katika wilaya mbalimbali zikiwamo Ngara, Pangani , Morogoro, Dodoma, Singida ni mmoja wa watumishi wa serikali waliofanyakazi kubwa ya kupambana na Nyarubanja, mfumo wa umiliki uliokuwa ukiendeshwa Mkoa wa Ziwa Magharibi.

Akiwa amesoma shule ya Msingi Pugu na kisha kusoma sekondari ya Minaki ni mmoja wa watanzania wa mwanzo waliokuwa na kazi kubwa ya kuonesha njia katika siasa za ujamaa na kujitegemea wakifuata maelekezo ya mwalimu.Katika mahojiano yake ya Mwisho na wandishi wa habari waliokuwa wanatengeneza dokumentari, alisema kwamba wakati wa utawala wa mwalimu Nyerere, rushwa na matumizi amabaya ya ofisi yalikuwa ni mambo yasiyovumilika.

Aidha alisema kwamba viongozi walikuwa na kazi kubwa ya kuelimisha watu kuelewa utawala maana yake nini na kushiriki katika kazi za kujenga taifa kwa uhuru na kujituma zaidi.Mzee Waziri ameacha watoto kadhaa, wajukuu na vitukuu.Miongoni mwa watoto wake ni Maida Waziri ambaye ni mjasiriamali na mhamasishaji maarufu wa ujasiriamali nchini na barani Afrika.

Aidha Maida Waziri ni mmoja wa wanawake wanaojulikana sana katika sekta ya ujenzi nchini Tanzania akimiliki kampuni ya ujenzi ya Ibra Contractors.

WAZIRI UMMY ASHIRIKI UJENZI WA BWENI LA WASICHANA SHULE YA SEKONDARI KIRARE JIJINI TANGA.

$
0
0

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu mkoani Tanga (CCM) Ummy Mwalimu katika akishiriki ujenzi wa vyumba vya bweni la Wasichana shule ya Sekondari Kirare Jijini Tanga jana mara baada ya kuwakabidhi mabati 100 kwa ajili ya zahanati ya Mapojoni na bweni hilo ikiwa ni kuunga mkono juhudi za wananchi kushoto ni Diwani wa Kata hiyo (CCM) Mwagilo
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu mkoani Tanga (CCM) Ummy Mwalimu katika akishiriki ujenzi wa vyumba vya bweni la Wasichana shule ya Sekondari Kirare Jijini Tanga mara baada ya kuwakabidhi mabati 100 kwa ajili ya zahanati ya Mapojoni na bweni hilo ikiwa ni kuunga mkono juhudi za wananchi kushoto ni Diwani wa Kata ya Kirare (CCM) Mwagilo
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu mkoani Tanga (CCM) Ummy Mwalimu katika akishiriki ujenzi wa vyumba vya bweni la Wasichana shule ya Sekondari Kirare Jijini Tanga mara baada ya kuwakabidhi mabati 100 kwa ajili ya zahanati ya Mapojoni na bweni hilo ikiwa ni kuunga mkono juhudi za wananchi kushoto ni Diwani wa Kata hiyo (CCM) Mwagilo anayefurahia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa

MBUNGE wa Viti Maalumu mkoani Tanga (CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameshiriki ujenzi wa bweni la Wasichana kwenye shule ya Sekondari Kirare Jijini Tanga ambalo litakapokamilika litawasaidia kuwaepusha na vishawishi wanavyoweza kukutana nazo wanapokwenda shuleni na kukwamisha ndoto zao.

Ummy ambaye alikuwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa wilaya ya Tanga akiwemo Mkuu wa wilaya hiyo Thobias Mwilapwa ambapo alikwenda Kata ya Kirare kuwakabidhi mabati 100 kwa ajili ya bweni hilo na zahanati ya mapojoni alipofika kwenye eneo hilo la ujenzi huo alichanganya mchanga na sarauji na baadae kuchapia ukutani.

Ujenzi huo wa Bweni la Wasichana kwenye shule hiyo litasaidia kuondosha changamoto ya watoto kutembea umbali wa kilomita kumi na tano kufuata huduma ya elimu jambo ambalo linaweza kupelekea kukumbana na vishawishi ambavyo vinaweza kukwamisha ndoto zao.

Akizungumza mara baada ya kushiriki ujenzi huo Waziri huyo ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) mkoa wa Tanga alisema atashirikiana na wananchi kuhakikisha changamoto mbalimbali zinazowakabili zinapatia ufumbuzi. Alisema kwamba Serikali ya awamu ya tano itaendelea kuchapa kazi kwa ufanisi mkubwa ili kuweza kutatua changamoto wa wananchi ili ziweze kupata ufumbuzi haraka na kuweza kuchochea kasi ya ukuaji wa maendeleo kwao na jamii zinazowazunguka.

Sambamba na Waziri huyo kuchangia mabati hayo wakati huo huo Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto imeguswa na changamoto hiyo na kuchangia mabati 50 na saruji 70 katika ujenzi wa bweni la wasichana la shule ya Sekondari Kirare na kushiriki kwenye shughuli za ujenzi.

Alisema atahakikisha anashirikiana na wananchi kwenye maeneo mbalimbali kuona namna ya kuzipatia ufumbuzi changamoto za Afya ambazo zinaweza kuwa kikwazo kwenye kujiletea maendeleo.

“Labda niwaambie tu kwamba Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wetu Dkt John Magufuli imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha changamoto mbalimbali zinapatiwa ufumbuzi hivyo endeleeni kushirikiana nayo kuweza kupata mafanikio “Alisema Waziri Ummy.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU JANUARI 7,2019

NSSF YAANZA KUTEKELEZA MAAGIZO YA RAIS DK.MAGUFULI

$
0
0
SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) imeanza utekelezaji wa maagizo ya Rais Dk.John Magufuli aliyoyatoa katika mkutano kati ya viongozi wa vyama vya wafanyakazi, Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa sekta ya Hifadhi ya jamii(SSRA), watendaji wakuu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na Chama cha waajiri uliofanyika Desemba 28, 2018 Ikulu jijini Dar es salaam.

Taarifa ya NSSF kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana Januari 6,2019 imesema Mfuko unaendelea kupokea na kuhakiki madai mbali mbali kutoka kwa wanachama ambao ajira zao zimekoma na walikuwa kwenye ajira za muda maalumu kwenye sekta mbali mbali kama vile madini, viwanda, ujenzi na kilimo.

Imesema madai yote yanayothibitishwa kuwa ni halali baada ya kuhakikiwa, mwanachama atalipwa mafao yake. Meneja Kiongozi wa Matekelezo (Chief Manager Compliance and Data Management ) Cosmas Sasi amesema NSSF inaendelea kulipa mafao mbali mbali kwa wanachama wake kwa wakati.

Kwa upande wa mafao ya uzeeni takribani Sh. bilioni 5 zimekuwa zinalipwa kila mwezi kwa wastaafu wetu kuanzia julai 2018.Wakati kwa pensheni ya Desemba,2018 Sh. Bilioni 4.83 kimeshalipwa kwa wastaafu 18,631 walikuwepo kwenye daftari la wastaafu.

Kwa upande wa malimbikizo ya mafao hadi kufikia julai 2018 jumla ya Sh. bilioni 108 zilikuwa zinadaiwa kwenye Shirika, ambapo kiasi cha Sh. bilioni 85 kimelipwa kwa wanachama waliokuwa na madai mbali mbali baada ya uhakiki kukamilika, kiasi kilichobaki cha sh. bilioni 23 kitalipwa baada ya uhakiki unaondelea kukamilika.

Wakati huo huo Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa UmaLulu Mengele amesema Mfuko ulianza mchakato wa kuhakiki wastaafu wake kuanzia Desemba 1, 2018 na bado unaendelea kwenye ofisi mbali mbali za NSSF zilizoko mikoa yote ya Tanzania Bara ."Wastaafu ambao hawajajitokeza kuhakiki, wanaombwa wafike kwenye ofisi zetu 65 zilizoko katika maeneo mbali mbali katika mikoa yote Tanzania bara kwa upande wa wastaafu wanaoishi Zanzibar watahakikiwa kwenye ofisi za ZSSF.

" Wastaafu wanatakiwa kuwa na nyaraka zifuatazo picha, kitambulisho cha Taifa au cha mpiga kura pamoja na kadi ya benki,"amesema na kuongeza kwamba "malipo ya pensheni kwa wastaafu ambao hawatahakikiwa yatasitishwa mwishoni mwa mwezi wa Januari 2019."Pia malipo ya wastaafu yatafanyika moja kwa moja kwenye akaunti za wastaafu ili kumrahisishia mstaafu kupata malipo yake ya pensheni kwa haraka na bila usumbufu.Mchakato wa uhakiki utakuwa endelevu ili kuboresha taarifa zilizokuwepo kwenye daftari la wastaafu

Mengele amesema Shirika linasisitiza kwa wafanyakazi na maofisa utumishi
kuhakikisha madai yanayoletwa kwenye Mfuko ni sahihi na mtu atakayebainika kuleta madai ya kugushi atachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kupelekwa mahakamani kwani hilo ni kosa la jinai.
Meneja Kiongozi wa Matekelezo ,Cosmas Sasi Kutoka Shirika NSSF,akizungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichani) jana jijini Dar kuhusu namna ambavyo NSSF imeanza utekelezaji wa maagizo ya Rais Dk.John Magufuli aliyoyatoa katika mkutano kati ya viongozi wa vyama vya wafanyakazi, Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa sekta ya Hifadhi ya jamii (SSRA), watendaji wakuu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na Chama cha waajiri uliofanyika Desemba 28, 2018 Ikulu jijini Dar es salaam.


Sasi alisema kuwa NSSF ilianza mchakato wa kuhakiki wastaafu wake kuanzia Desemba 1, 2018 na bado unaendelea kwenye ofisi mbali mbali za NSSF zilizoko mikoa yote ya Tanzania Bara ."Wastaafu ambao hawajajitokeza kuhakiki, wanaombwa wafike kwenye ofisi zetu 65 zilizoko katika maeneo mbali mbali katika mikoa yote Tanzania bara kwa upande wa wastaafu wanaoishi Zanzibar watahakikiwa kwenye ofisi za ZSSF",alisema.Pichani kulia ni Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Uma,Lulu Mengele
Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Uma,Lulu Mengele akizunguma na Waandishi wa habari (hawapo pichani) jana jijini Dar akifafanua kuhusu uhakiki wa Wananchama wao,Lulu alisema kuwa Mfuko wa NSSF unaendelea kupokea na kuhakiki madai mbali mbali kutoka kwa wanachama ambao ajira zao zimekoma na walikuwa kwenye ajira za muda maalumu kwenye sekta mbali mbali kama vile madini, viwanda, ujenzi na kilimo.

"Madai yote yanayothibitishwa kuwa ni halali baada ya kuhakikiwa, mwanachama atalipwa mafao yake. kwa hiyo NSSF kwa sasa inaendelea kulipa mafao mbali mbali kwa wanachama wake kwa wakati,",alisema Lulu.Pichani kushoto ni 
Meneja Kiongozi wa Matekelezo ,Cosmas Sasi Kutoka Shirika NSSF.

SERIKALI KUTUMIA SH.TRILIONI 1.3 KWA AJILI YA MIRADI YA MAJI MIJI 28 NCHI NZIMA-PROF. MKUMBO

$
0
0

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo kulia akizungumza na waandishi wa habari ambao hawapo pichani wakati wa ziara yake kushoto ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga-Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly

SERIKALI inatarajia kutumia Shilingi Tirioni 1.3 kupitia mkopo toka Exim benki ya nchini India kwa ajili ya miradi mikakati ya maji katika Miji 28 nchi nzima ili kukabiliana na tatizo la maji.

Hayo yamebaimnishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo alipofanya ziara katika mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga(Tanga-Uwasa) na kuzungumza na watumishi wa mamlaka hiyo.

Profesa Mkumbo alifanya ziara katika mamlaka hiyo kwa ajili ya kujionea utendaji wa kazi zao na zaidi kuona changamoto zinazowakabili watumishi hao na mamlaka husika na namna ya kuzitafutia ufumbuzi. Profesa Mkumbo alisema katika fedha hizo zaidi ya Shilingi Bilioni 140 zitainufaisha Miji ya Pangani,Muheza na Korogwe ambapo matarajio ya Serikali kuhakikisha kufikia malengo ya asilimia 85 Vijijini na 95 Mijini hadi kufikia 2025.

Alisema katika Miji hiyo Pangani imepangiwa kiasi cha Shilingi Bilioni 22.5,Muheza Bilioni 5.6 na Korogwe kupitia mradi Mkuu wa maji Korogwe na Handeni BILIONI 112.5(HTM). “Matarajio ya Serikali ni kuhakikisha inapunguza kwa kiasi kikubwa kero ya maji vijijini na mijini na kufikia malengo yaliyojiwekea hadi kufikia mwaka huo wa 2025”Alisema Profesa Mkumbo.

Aidha lisema mchakato wa miradi hiyo mikakati umekwisha anza kwa hatua za awali ya usanifu na kupata Mtaalamu mshauri kwa ajili ya miradi hiyo katika Miji ambayo imebainishwa kunufaika na fedha hizo kwa nchi nzima. Alisema hadi kufikia juni mwaka huu miradi hiyo itakuwa imekwisha dizainiwa na mwezi Sept wakandarasi watatkiwa kuwa katika maeneo ya kazi katika miji hiyo 28 kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo.

Hata hivyo alitumia fursa hiyo kuwataka makandarasi kuhakikisha wanafanyakazi kwa uwadilifu na watambue Serikali haitomzulumu mkandarasi yoyote na fedha zao zitalipwa bila ya mashaka yoyote. “Tunajua madai ya makandarasi wengi nchi nzima lakini tutawalipa waondoe shaka koila mwezi tulipa shilingi Bilioni 8-12 hivyo tutwalipa tu”Alisema.

Awali akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga-Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly alisema changamoto kubwa kwa sasa mkoani hapa ni namna ya kuongeza huduma ya taka ndani ya Jiji.

“Mbali na fedha zilizoainishwa na Katibu Mkuu lakini tunatarajia kupokea zaidi ya shilingi bilioni 400 kwa ajili ya miradi ya maji taka,kubadilisha miundombinu ya mabomba,ujenzi wa matank”Alisema Mhandisi Hilly.

TAASISI YA IMETOSHA YAJITOLEA KUSOMESHA WATOTO WENYE ULEMAVU WA NGOZI (ALBINO)

Mkazi wa Zanzibar aondoka na 15m/ -za Tigo Jigiftishe

$
0
0
Mshindi wa Promosheni iliyomalizika ya Tigo Jigiftishe Abdulrazak Abdallah  (wa tatu kushoto) akipokea mfano wa hundi ya Sh 15m/- kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Pwani Deogratias David (wa pili kulia) huku akishangiliwa na baadhi ya wafanyakazi wa Tigo na mtangazaji wa Clouds FM Meena Ally (kushoto) katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya Jang’ombe kisiwani Zanzibar mwishoni mwa wiki.
Mshindi wa zawadi ya Sh 15m/- katika Promosheni iliyomalizika ya Tigo Jigiftishe kutoka Zanzibar Abdulrazak Abdallah, akimuonyesha mtangazaji wa Radio Clouds FM Meena Ally hali ya nyumba anayoishi. Mshindi huyo alisema atatumia sehemu ya fedha alizoshinda kukarabati nyumba hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Tigo waliofika kisiwani Zanzibar mwishoni mwa kumkabidhi Abdulrazak Abdallah ambaye aliibuka mshindi wa zawadi ya shilingi milioni 15 katika Promosheni iliyomalizika ya Tigo Jigiftishe , wakifurahi pamoja na mshindi huyo wakati wa makabidhiano wa mfano wa hundi. W kwanza kulia ni mtangazaji wa Radio Clouds FM Meena Ally.

Baadhi ya wananchi wa Zanzibar waliofika katika viwanja vya Jang’ombe kushuhudia mshindi wa zawadi ya Sh 15m/- katika Promosheni ya Tigo Jigiftishe Abdulrazak Abdallah kutoka visiwani humo akikabidhiwa zawadi yake katika hafla iliyofanyikaa mwishoni mwa wiki.




Mkazi wa Unguja kisiwani Zanzibar Abdulrazak Abdallah, ameibuka mshindi wa zawadi ya shilingi 15m/- katika Promosheni iliyomalizika ya Tigo Jigiftishe.

Abdulrazak ni mmoja kati ya washindi wakubwa watatu wa promosheni ya Tigo Jigiftishe. Wengine ni Emma Kauka mkazi wa Dar es Salaam aliyejishindia shilingi milioni 25 na Sadiki Kilipamwambu mkazi wa Songea alijishindia shilingili milioni 50.

Akipokea zawadi yake kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Pwani Deogratius David, mshindi huyo alisema zawadi hiyo ya fedha imekuja wakati muafaka kutokana na kuwa anakabiliwa na shida ambazo zinahitaji fedha ili kuweza kuzitatua.“Hii kwangu ni zawadi ya kipekee ambayo Mungu amenipatia kupitia Tigo. Nitatumia sehemu ya fedha kukarabati nyumba ninayoishi ambayo ni kama gofu ili iweze kuwa nyumba kama zilivyo nyumba nyingine. Namshukuru Mungu na Tigo kwa zawadi hii,” alisema

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Tigo kwa kanda ya Pwani Deogratias David alisema ni jambo la furaha kuona Promosheni ya Tigo Jigiftishe imekwisha huku ikiwa imeboresha na kubadilisha maisha ya wateja wake.

“Promosheni ya Tigo Jigiftishe imetoa jumla ya shilingi milioni 600 kwa wateja wake. Tunayo furaha kuonna kuwa fedsha hizi zimeweza kuboresha maisha ya wateja wetu,” alisema.Promosheni ya Tigo Jigiftishe ililenga kuwazawadia wateja wanaotumia huduma za mtandao huo katika kipindi hiki cha sikukuu na mwaka mpya.

Kupitia promosheni hiyo, wateja kumi wa Tigo waliweza kujishindia shilingi milioni moja kila siku, huku mshindi mmoja wa wiki akijishindia shilingi milioni 10 huku washindi wakubwa wakijishindia shilingi milioni 15, milioni 25 na milioni 50.

NAIBU WAZIRI, MHE.KANYASU ATEMBELEA IHUMWA MJI WA SERIKALI KUKAGUA UJENZI JENGO LA MALIASILI NA UTALII

$
0
0

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu (katikati) akiangalia hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii linalojengwa ndani ya mji wa Serikali wakati alipotembelea kwa ajili ya kukagua maendeleo ya jengo hilo katika eneo la Ihumwa Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu (katikati) akizungumza na Mkandarasi wa Suma JKT, Luteni Mturi wakati alipotembelea kwa ajili ya kukagua maendeleo ya jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii linalojenga katika mji wa serikali katika eneo la Ihumwa Jijini Dodoma., kushoto ni Fundi Sanifu Ujenzi, Agastoni Kayugwa ambaye ni Muwakilishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa pamoja wameeleza kuwa wanaridhishwa na spidi inayoendelea katika ujenzi wa jengo hilo.
Muonekano wa hatua iliyofikiwa ya jengo jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii linalojenga katika mji wa serikali katika eneo la Ihumwa Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akipewa maelezo kutoka kwa Mkandarasi wa Suma JKT, Luteni Mturi wakati alipotembelea kwa ajili ya kukagua maendeleo ya jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii linalojenga katika mji wa serikali katika eneo la Ihumwa Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea kwa ajili ya kukagua maendeleo ya jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii linalojenga katika mji wa serikali katika eneo la Ihumwa Jijini Dodoma. (PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA-MNRT)


NA.LUSUNGU HELELA

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu amesema ameridhishwa na hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii linalojengwa ndani ya mji wa Serikali katika eneo la Ihumwa Jijini Dodoma.

Ameyabainisha hayo wakati alipotembelea eneo hilo kwa ajili ya kukagua maendeleo yaliyofikiwa katika ujenzi wa jengo hilo. “Kazi hii inafanywa kwa uhodari mkubwa, nawapongeza kwa maendeleo yaliyofikiwa na ninaamini kwamba Jengo hili litakamilika ndani ya muda uliopangwa’’

Aidha, Mhe. Kanyasu wakati alipotembelea eneo hilo ameweza kukutana na timu ya Wakadiliaji Majengo kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ambao kwa pamoja na Fundi Sanifu Ujenzi, Agastoni Kayugwa ambaye ni Muwakilishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa pamoja wameeleza kuwa wanaridhishwa na spidi inayoendelea katika ujenzi wa jengo hilo.

Kwa upande wake, Mkandarasi wa SUMA JKT, Luteni Mturi amemueleza Naibu waziri huyo kuwa wanatarajia kumaliza ndani ya muda uliopangwa kwa vile kwa sasa kuna upatikanaji wa uhakika wa vifaa vya ujenzi ikiwematofali ya kutosha na yenye ubora wa hali ya juu pamoja na wafanyakazi wa kutosha

‘’Kesho tunategemea kuanza kumwaga zege katika kipande cha kwanza ambapo hadi kesho kutwa tutamalizia kipande cha pili’ ameeleza Mturi. Hata hivyo, Mkandarasi huyo ameeleza changamoto ya utayari wa wafanyakazi kufanya kazi usiku kuwa wengi wao wamekuwa hawapo tayari kufanya kazi muda huo licha ya kuwa awali SUMA JKT ilipanga kujenga jengo hilo mchana na usiku.

WASTARA afichua siri nzito,kutapeliwa mamilioni ya pesa...

SIMANJIRO WAZINDUA UGAWAJI VITAMBULISHO

$
0
0
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Tumaini Magessa amezindua utoaji wa vitambulisho vya wafanyabiashara wadogowadogo kwa kuwataka wafanyabiashara wakubwa na wakati kutojihusisha na zoezi hilo.  Magessa aliyasema hayo mji mdogo wa Mirerani, wakati wa kugawa vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo.

Magessa alisema wafanyabiashara waliosajiliwa kwenye mfumo wa mamlaka ya mapato nchini (TRA) hawapaswi kupatiwa vitambulisho hivyo. "Serikali ipo pamoja nanyi wafanyabiashara wadogo, ndiyo sababu Rais John Magufuli akawatambua na kuagiza vitambulisho vyenu vitengenezwe," alisema Magessa. 

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Yefred Myenzi alisema wafanyabiashara wanapaswa kuwa wazalendo kwa kulipa kodi ili kufanikisha maendeleo. "Kupitia kodi ndiyo serikali inafanikisha maendeleo mbalimbali ikiwemo kujenga vyumba vya madarasa yahoo shule za sekondari na msingi ambavyo watoto wetu watasoma," alisema  Myenzi.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Yefred Myenzi akizungumzia umuhimu wa ulipaji kodi kwa wafanyabiashara wakati wa uzinduzi wa utoaji wa vitambulisho vya wafanyabiashara wadogowadogo wilayani humo.
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Zuwena Omary akielezea namna ya upatikanaji wa vitambulisho hivyo wakati wa uzinduzi wa utoaji wa vitambulisho vya wafanyabiashara wadogowadogo wilayani humo.
 Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, mhandisi Tumaini Magessa akielezea sifa za wafanyabiashara wadogo wanaopaswa kupata vitambulisho hivyo vilivyotolewa na Rais John Magufuli. 
Wafanyabiashara wadogo wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara wakifuatilia kikao cha Kaimu Mkuu wa Wilaya hiyo mhandisi Tumaini Magessa wakati wa uzinduzi wa utoaji wa vitambulisho vya wafanyabiashara wadogowadogo wilayani humo.

WASTARA ALIA NA WANAOMUITA TAPELI,AKANA KUHUSU UKAHABA

CCM IRINGA WAPATA MWENYEKITI MPYA

$
0
0
NA DENIS MLOWE, IRINGA

CHAMA cha Mapinduzi mkoa wa Iringa, kimemchagua mwadhili wa chuo kikuu cha Ruaha mkoani hapa, Dk. Abel Nyamahanga kuwa mwenyekiti mpya wa chama hicho kuchukua nafasi ya mwenyekiti aliyejiuzulu ambaye kwa sasa ni mkuu wa mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila.

Wajumbe 597 kati ya 631 waliohudhuria wa Mkutano mkuu maalumu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Iringa wametumia haki yao ya kidemokrasia kwa kufanya uchaguzi wa kumpata Mwenyekiti mpya wa chama hicho chini ya msimamizi wa uchaguzi aliyekuwa waziri mkuu awamu ya nne, Mizengo Pinda.

Mkutano huo maalum uliohudhuriwa na wadau mbalimbali mkoani hapa ulikuwa wa upinzani mkali ambapo kutokana na wajumbe waliozidi akidi ya matakwa ya mkutano wa CCM mkoa kwa mujibu wa maelekezo ya kanuni za uchaguzi wa CCM wajumbe wote ni 631.

Wajumbe hao walitakiwa kuwapigia kura wanachama watatu ambao ni Vitusi Mushi, Amani Mwamwindi na Dk. Abel Nyamahanga ambao majina yao yalirudishwa kutoka kamati kuu ya CCM taifa kwa lengo la kupigiwa kura. Katika uchaguzi huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kichangani, wajumbe walilazimika kurudia uchaguzi kwa awamu ya pili baada ya awamu ya kwanza mshindi kutovuka nusu ya kura zilizopigwa kutokana na upinzani mkali.

Baada ya matokeo kutoka ndipo wa majina mawili ya Amani Mwamwindi na Dk. Abel Nyamahanga yalipigiwa kura kutokana na wajumbe 548 waliobaki baada yaw engine kutoka ukumbini na kuweza kupata mwenyekiti mpya baada ya Vitus Mushi kupata kura chache zaidi ambazo hazikukidhi kanuni za uchaguzi wa CCM.
Hivyo baada ya awamu ya pili ya uchaguzi huo ndipo, Dk Abel Nyamahanga aliibuka kidedea kwa kupata kura 318 kati ya 548 ambapo kura 6 ziliharibika na Aman Mwamwindi kupata kura 224.

Wakizungumza mara baada ya kusaini na kukubali matokeo hayo, Amani Mwamwindi na Vitusi Mushi walilalamikia mchezo mchafu uliokuwepo katika uchaguzi huo hadi kufikia hatua ya msimamizi wa uchaguzi, Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda kumtaka Mushi kuandika malalamiko yake na kuwasilisha ngazi za juu za chama hicho.

Akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi, Mwenyekiti Mpya wa CCM mkoa wa Iringa, Abel Nyamahanga aliwashukuru wapiga kura kwa kumchagua na kuwataka wanaccm kuungana na kuondokana na makundi kwa lengo la kukijenga chama zaidi kuibuka na ushindi katika chaguzi za mitaa. Nyamahanga amewahakikishia wajumbe na wanachama wa CCM mkoa wa Iringa kuwa atzunguka kata kwa kata kubaini changamoto za wanaccm zinazosababisha kushindwa kuchukua jimbo la Iringa mjini na kuzifanyia kazi na kuanza kwa ushindi wa chaguzi za serikali za mitaa mwaka huu.

Alisema kuwa dhamira ya wanaccm ni moja kuhakikisha serikali na wananchi wanakuwa kitu kimoja na sio kuwagawa kwa misingi ya vyama badala yake ni kupigania chama kinacholeta maendeleo kwa wananchi bila ubaguzi wa vyama na kutaka ushirikiano zaidi kwa wagombea walishika nafasi ya pili na tatu.

Kwa upande wake mlezi wa CCM mkoa wa Iringa ambae pia ni waziri mkuu mstaafu Mizengo Pinda amewataka wanaccm kuhakikisha 2020 Jimbo la Iringa mjini linarudi Ccm pamoja na kata zake kuwataka kuwa kitu kimoja katika kukijenga chama. Alisema kuwa ataahakikisha anaanza ziara ya kata kwa kata katika mkoa wa Iringa ili kukirudisha chama kwa wanachama kuanzia ngazi za chini na kuahidi kushirikiana na wanachama wote katika kuhakikisha chama kinafata misingi yake.

Aidha alitoa ushauri kwa wagombea ambao hawajaridhika kuandika malalamiko yao kwa ngazi za juu na kuongeza kuwa ni muda muafaka wa wanachama na wajumbe wa ccm kujitathimini ni makosa gani huwa wanafanya wakati wa uchaguzi mpaka jimbo la Iringa kwenda upinzani.

Mwenyekiti mpya wa CCM mkoa wa Iringa Dk Abel Nyamahanga akiwa na wagombea wa nafasi hiyo. kushoto kwake ni Aman Mwamwindi na kulia kwake ni Vitus Mushi.
 Baadhi ya wajumbe wa mkutano maalum wa uchaguzi wa mwenyekiti wa ccm mkoa wa Iringa wakiwa ukumbini kabla ya zoezi la kupiga kura
 Msimamizi wa uchaguzi wa mwenyekit wa ccm mkoa wa Iringa Mizengo Pinda akizungumza kabla ya zoezi la kupiga kura kuanza katika uchaguzi wa Mwenyekiti mpya wa CCM mkoa wa Iringa uliofanyika katika ukumbi wa Kichangani.

BENKI YA NMB YATUNUKIWA TUZO YA KUWA MSHIRIKA BORA KATIKA MASUALA YA KIFEDHA AFRIKA KWA MWAKA 2018

$
0
0
NMB Bank PLC imeshinda tuzo na kutajwa kuwa Mshirika Bora katika Masuala ya Kifedha Afrika kwa benki zinazofanya kazi na Shirika la Kimataifa la Fedha (IFC) la Benki ya Dunia. Hafla ya kukabidhiwa Tuzo hiyo ilifanyika Jijini Dar es Salaam. 

Akipokea tuzo hiyo kutoka kwa Mwakilishi Mkazi wa IFC Afrika Mashariki (IFC Resident for East Africa) Bw. Dan Kasirye, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Bi. Ruth Zaipuna alisema "Tumefurahishwa kwa namna ya pekee kupokea tuzo hii ya Kimataifa kutokana na mafanikio yetu; ni ushuhuda wa uwekezaji wetu katika teknolojia huku tukipanua mtandao wa matawi yetu na kuimarisha uwezo wetu wa kutoa huduma nzuri na za kisasa kwa wateja wetu." 

Aidha, Bi. Zaipuna aliongeza kuwa “katika miaka minne iliyopita, tumetoa huduma na bidhaa za kisasa na kuendelea kukidhi mahitaji ya wateja wetu nchini kote na kuziba pengo lililoachwa na benki nyingine katika soko. Kwa sasa tuna mtandao mpana zaidi nchini wenye matawi 228, ATM zaidi ya 800 na NMB Wakala zaidi ya 6,000 na hivyo kufanya upatikanaji wa huduma zetu nchini kuwa kwa asilimia 100%”. 

Kwa upande wake, Mwakilishi Mkazi wa IFC kwa Afrika Mashariki Bw. Dan Kasirye alisema “NMB Bank imeshinda tuzo hii kutokana na uwezo wake wa kutoa huduma mseto za kifedha zinazomfikia mtumiaji wa chini kabisa. NMB Bank ni mshindi wa ushirikishwaji wa kifedha barani Afrika iking’ara zaidi kuliko benki nyingine zote ambazo zimeshafanya kazi na IFC. NMB imeonyesha uwezo wake katika kuwashirikisha wanawake, biashara ndogo, kubwa na za kati, pamoja na biashara ya kilimo Tanzania.” 

TUZO NYINGINE AMBAZO BENKI YA NMB IMESHINDA 
Katika kipindi cha miezi 12, Benki ya NMB imeshinda tuzo nyingine mbili za kimataifa ambazo ni; Benki Bora Tanzania kutoka Euromoney Awards for Excellence; Benki Bora ya Wateja Wadogo na Benki Bora ya Biashara Tanzania kutoka Banker East Africa Magazine. Pia benki ya NMB imeshinda tuzo mbalimbali za ndani kama vile; tuzo ya Afya na Usalama Kazini (OSHA) 2018 na tuzo ya utoaji wa taarifa bora za kifedha 2018 kutoka Bodi ya wahasibu na wakaguzi wa mahesabu (NBAA). 
Kaimu Mkurugenzi wa NMB Bank – Ruth Zaipuna akiwa na tuzo kutoka Shirika la Kimataifa la Fedha ambalo ni tawi la Benki ya Dunia ((IFC) iliyoitaja benki hiyo kuwa Mshirika Bora katika Masuala ya Kifedha kwa nchi za Afrika miongoni mwa benki zinazofanya kazi na shirika hilo.

Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images