Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1765 | 1766 | (Page 1767) | 1768 | 1769 | .... | 1898 | newer

  0 0


  NA LUSUNGU HELELA-GEITA


  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu amewaonya wananchi wanaofanya shughuli za kibinadamu ndani ya Hifadhi za Misitu nchini kuacha tabia ya kuwashambulia Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao.

  Onyo hili linakuja ikiwa zaidi ya watumishi watano wa TFS katika mikoa ya Pwani, Tabora ,Kigoma pamoja Kilimanjaro wakiwa wamepoteza maisha yao kwa kushambuliwa na wananchi wakati wakiwa wanatekeleza majukumu yao.

  Aidha, Mhe.Kanyasu amepiga marufuku kwa watumishi wa TFS kujichukulia sheria mkononi kwa kuwapiga wananchi wanapobainika kutenda makosa."Watumishi wa TFS hamruhusiwi kumpiga Mwananchi mnapomkamata ndani ya Hifadhi au akiwa anasafirisha mazao ya Misitu kinyume na sheria, atakayebainika sheria itachukua mkondo wake.

  Ametoa onyo hilo wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Mgusu wilayani Geita mkoani Geita ikiwa ni ziara yake ya kutatua migogoro ya mipaka kwenye msitu wa Hifadhi Geita iliyopo baina ya Vijiji ambapo jumla ya hekta 4,462.95 zimefutwa kwa tangazo la Serikali.

  Amesema shughuli za uhifadhi ni lazima zifanyike kwa ushirikishwaji kati ya wananchi na watumishi wa TFS." Uhasama unaozidi kujengeka kati yenu hauna tifa katika uhifadhi shirikianeni" amesisitiza Mhe.Kanyasu.Amewataka wananchi kuheshimu na kuzifuata sheria za uhifadhi ya Misitu nchini huku akiwataka watumishi kujiepusha na migongano kati yao na wananchi.

  Katika hatua nyingine, Mhe.Kanyasu amewataka wananchi wafuate sheria kwa kulipia vibali kwa TFS pale wanapokuwa na mahitaji ya mazao ya Misitu badala ya kusubilia mpaka wakamatwe na TFS.Mkuu wa Wilaya ya Geita, Mhe.Josephat Maganga amemueleza Naibu Waziri huyo kuwa hali ya Misitu katika wilaya hiyo ni mbaya kufuatia shughuli za kibinadamu zinazoendelea kufanyika Misitu hiyo.

  Hata hivyo, Mkuu huyo wa Wilaya hiyoMhe.Maganga alisema kufuatia hali hiyo tayari Kamati ya Ulinzi na Usalama kwa kushirikiana TFS wameshaanza kufanya doria ya kuwaondoa wafugaji na wakulima waliovamia Hifadhi.Katika hatua nyingine, Diwani ya Kata ya Mgusu, Pastory Lugusa amemuomba Naibu Waziri huyo kumegewa eneo la Hifadhi kwa vile idadi ya wakazi wa kata hiyo imeongezeka hali inayopelea kukosa maeneo kwa ajili ya malisho na Kilimo.

  Kwa upande wake Meneja wa Misitu wa wilaya wa TFS, Fedy Ndandika amemuhakikishia Naibu Waziri kuwa watashirikiana na wananchi hata hivyo tayari wameanza kutoa elimu ya umuhimu wa uhifadhi kwa jamii zinazozunguka Hifadhi.
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Geita mkoani Geita akipewa maelezo na Meneja wa Misitu wa wilaya wa Wakala wa Huduma ya Misitu Tanzania (TFS) Fedy Ndandika wakati alipotembelea eneo la Manga lililokuwa limevamiwa na wakulima ambayo ni moja ya eneo la Msitu wa Hifadhi Geita
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika kata ya Mgusu, Halmashauri ya wilaya ya Geita mkoani Geita akiwasisitiza wananchi umuhimu wakufuata sheria na kuacha tabia ya kuvamia Hifadhi za Misitu.
  Mkazi wa kata ya Mgusu, Anaeli Mbokile akizungumza mbele ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwasilisha ombi la kumegewa eneo la Hifadhi ya Msitu Geita ili liweze kutumika kwa ajili ya malisho na makazi baada ya wakazi wa kata ya Mgusu idadi ya kuongezeka.
  1. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiteta jambo na baadhi ya wanachama wa CCM wakati alipomaliza mkutano wa hadhara katika kata ya Mgusu mkoani Geita. (PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA).

   

  0 0


  Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) limetuma orodha ya Waamuzi wa Tanzania watakaochezesha mechi za kimataifa wakiwa na beji ya FIFA. 

  Katika orodha hiyo wapo waamuzi wa katikati na Waamuzi wasaidizi wa Kiume na wa Kike.

  Aidha wapo pia waamuzi watakaochezesha soka la Ufukweni.

  Waamuzi wa katikati Wanaume 
  1NASSORO Mfaume Ali
  2SASII Hery Ally
  3MWANDEMBWA Emmanuel Alphonce
  4SAANYA Martin Elifhas

  Waamuzi Wasaidizi

  1CHACHAFerdinand
  2KINDULI Mgaza Ally
  3LILASoud Iddi
  4KOMBA Frank John
  5MKONO Mohamed Salim
  6HAULE Mbaraka Haule

  Waamuzi wa Soka la Ufukweni 

  1MSILOMBO Jackson Steven
  2MWAMBONEKO Geofrey Tumaini

  Waamuzi wa katikati Wanawake 

  1KABAKAMA Jonesia Rukyaa
  2CHIEF Florentina Zabron

  Waamuzi wasaidizi Wanawake

  1MDUMA Hellen Joseph 
  2WAMALAGrace
  3BALAMAJanet Charles
  4MTWANA Dalila Jafari

  0 0

  Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano maarufu kama Kilimo IV Jijini Dodoma tarehe 2 Januari 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo)

  Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma


  Kwa mliganisho wa mahitaji na uzalishaji nchi ina ziada ya tani 3,013,515 na imejitosheleza kwa asilimia 123 na 120 mtawalia ambapo uzalishaji katika msimu wa 2016/2017 na 2015/2016 ulikuwa tani 15,900,864 na 16,172,841 mtawalia ambapo mahitaji ya chakula yanayoendana na uzalishaji huo ni tani 13,159,326, na 13,300,034 kwa mwaka wa ulaji 2017/2018 na 2016/2017 mtawalia.

  Uzalishaji wa mazao ya chakula katika msimu wa uzalishaji wa 2017/2018 ulifikia tani 16,981,974 zikiwemo tani tani 9,537,857 za mazao ya nafaka na tani 7,354,117 mazao yasiyo nafaka, kiwango ambacho kimeiwezesha nchi kutosheleza mahitaji yake ya chakula ya tani 13,569,285 katika mwaka 2018/2019 kwa kiwango cha utoshelevu (Self Sufficiency Ratio-SSR) cha asilimia 124.

  Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo tarehe 2 Januari 2019 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano maarufu kama Kilimo IV Jijini Dodoma.

  Alisema Uzalishaji wa mahindi katika msimu wa 2017/2018, 2016/2017 na 2015/2016 ulikuwa ni tani 6,273,150; 6,680,758 na 6,148,699 mtawalia, wakati mahitaji yanayoendana na uzalishaji huo ni tani 5,462,390; 5,407,499 na 5,202,405 katika miaka ya ulaji ya 2018/2019, 2017/2018 na 2016/2017, Ambapo ziada ya tani 810,760(2018/2019); 1,273,259(2017/2018)  na 946,284(2016/2017) zilipatikana.

  Uzalishaji wa mchele katika msimu wa 2017/2018, 2016/2017 na 2015/2016 ulikuwa ni tani 2,219,628; 1,593,609; na 2,229,071 mtawalia, mahitaji yanayoendana na uzalishaji huo ni tani 990,044; 924,435; na 976,925 katika miaka ya ulaji ya 2018/2019, 2017/2018 na 2016/2017, Ziada ya tani 1,229,583(2018/2019); 669,175(2017/2018) na 1,252,146(2016/2017) zilipatikana.

  Mhe Hasunga alisema kuwa kutokana na ziada hizo za uzalishaji nchi imeendelea kuwa ghala la chakula kwa nchi jirani. Kwa mfano, kulingana na takwimu za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), katika kipindi cha mwezi Juni 2017 hadi Juni 2018 jumla ya tani 64,477.95 za Mahindi zenye thamani ya shillingi billioni 90.6 na Maharage tani 99,434.45 zenye thamani ya shillingi bilioni 222.0 ziliuzwa katika nchi za DRC, Rwanda, Burundi, Kenya, Uganda, Sudan ya Kusini na Uarabuni.

  Hasunga aliongeza kuwa Kati ya mwaka 2015/2016 na 2017/2018 uzalishaji wa mazao ya Asili ya Biashara umeongezeka kwa viwango tofauti tofauti, ambapo zao la korosho kwa sasa linalimwa katika mikoa 17 na Halmashauri 90 hapa nchini baada ya kuanza kwa mpango wa kuongeza uzalishaji wa zao la korosho mnamo mwaka 2013/2014 kupitia uhamasishaji wa kilimo hicho katika mikoa mipya. 

  Amesema kuwa Mikoa ya asili inayoongoza kwa kilimo cha zao la korosho ni Mtwara, Lindi, Ruvuma, Pwani na Tanga. Katika miaka ya hivi karibuni mikoa mingine mitano nayo imeanza kuzalisha korosho kwa kiasi kidogo ambayo ni Singida, Dodoma, Morogoro, Mbeya na Njombe.

  Alisema kuwa taarifa ya uhakiki na malipo kwa wakulima mpaka kufikia tarehe 29 Desemba 2018 tayari Vyama vilivyohakikiwa na kulipwa ni 450.

  Malipo yaliyohakikiwa na kuwasilishwa benki ni tsh 231,937,341,674, Malipo yaliyolipwa katika akaunti za Wakulima ni tsh 210,485,753,571, Korosho iliyolipiwa ni Kilo 70,284,043, Kiasi cha Korosho iliyokusanywa katika maghala makuu ni Tani 195,175.844, na Kiasi cha Korosho iliyosombwa na kupelekwa katika maghala ya Hifadhi ni Tani 35,175.844

  Katika taarifa yake na waandishi wa habari Mhe Hasunga ameeleza kuwa matumizi ya mbegu bora za pamba yameongezeka kutoka tani 14,500 mwaka 2015/2016 hadi tani 18,500 mwaka 2017/2018 na matarajio ni kufikia tani 25,000 msimu wa 2018/2019. Mpaka sasa kiasi cha mbegu tani 27,769 zimesambazwa na ni asilimia 37 zaidi ya kiasi kilichoombwa na Wilayaambacho kilikuwa tani 20,284.

  Aidha, Uzalishaji wa chai kavu umeongezeka kutoka tani 32,628 mwaka 2015/2016 hadi kufikia tani 34,010 mwaka 2017/2018. Matumizi ya mfumo wa ushirika umeongeza bei ya kilo moja ya majani mabichi kutoka wastani wa Shilingi 251 mwaka 2015/16 hadi  shilingi 314 mwaka 2017/18. Thamani ya mauzo ya chai nje ya nchi imeongezeka kutoka Dola za kimarekani 51,794,854.00 mwaka 2015/2016 hadi kufikia Dola za kimarekani 62,167,167.00 mwaka 2017/2018.

  Kuhusu zao la Mkonge uzalishaji umeongezeka kutoka tani 39,393 mwaka 2015/16 hadi tani 43,279 mwaka 2017/18. Bei ya tani moja ya Katani daraja la UG mwaka 2015/2016 ilikuwa Shilingi 2,200,000 na mwaka 2017/2018 imefikia Shilingi 3,330,000 sawa na asilimia 50. Thamani ya mauzo ya singa nje ya nchi ni kutoka dola za Kimarekani 35,991,161 mwaka 2015/16 hadi dola za Kimarekani 45,835,845 mwaka 2017/18.

  Akieleza kuhusu zao la Sukari Waziri Hasunga amesema kuwa Serikali imeimarisha udhibiti wa uingizaji holela wa sukari kutoka nje hali iliyoimarisha soko la sukari nchini.

  Udhibiti huo umechochea ongezeko la uzalishaji wa sukari kutoka tani 293,075 mwaka 2015/2016 hadi takriban tani 307,431.14 mwaka 2017/2018. Aidha, uzalishaji wa sukari unatarajiwa kuongezeka na kufikia tani 352,600 mwaka 2018/2019. 

  Vilevile, Serikali imeratibu uanzishwaji wa mashamba mapya ya miwa ya Mkulazi I (Ngerengere), Mkulazi II (Mbigiri) na Shamba la Bakhresa - Bagamoyo Sugar (Makurunge).  Sekta ya Sukari kwa ujumla inatoa ajira isiyo ya moja kwa moja kwa watu 57,000 pamoja na kutoa fursa ya ajira kwa watu wengine takriban 75,000 ambao wanahusika na shughuli zinazotoa huduma kwenye mnyororo wa thamani wa uzalishaji wa sukari nchini.


  0 0


  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inalaani na kukemea vikali vitendo vya ukatili dhidi ya watoto vinavyoendelea kujitokeza nchini. Vitendo hivi vinafanywa na kuhusisha ndugu na walezi wa karibu wa wataoto hivyo kuzua hofu kubwa kwa watoto na jamii kwani vinaathiri malezi na makuzi ya awali ya watoto kwa kutozingatia haki zao za msingi.

  Mapema wiki hii, imeripotiwa mwalimu wa shule ya msingi jijini Dodoma (jina limehifadhiwa) ambaye anatuhumiwa kumfungia mtoto mdogo ndani ya kabati kwa kipindi kirefu na kusababisha afya ya mtoto huyo kudhohofika. Mwalimu huyo anatuhumiwa pia kumfanyia vitendo vya ukatili mama mzazi wa mtoto huyo kwa kumpiga na kumsababishia maumivu mwilini yaliyopelekea binti huyo na mtoto wake kulazwa.

  Kipekee, Wizara inawapongeza wanajamii wote walioibua tukio hili na kuwezesha Jeshi la Polisi kumkamata mtuhumiwa kwa ajili ya uchunguzi ili Sheria iweze kuchukua mkondo wake. TunaaminiJeshi la Polisi watafanya upelelezi wa tukio hili kwa weledi mkubwa ili hatua stahiki za kisheria ziweze kuchukuliwa.Matukio ya ukatili wa watoto yanapotokea majumbani yanarudisha nyuma jitihada za Serikali za kulinda na kuendeleza haki na ustawi wa watoto katika ngazi ya familia ambayo ndio kitovu cha jamii wakiwemo na watoto.

  Kufuatia kitendo hicho kilichofanywa na mwalimu wa shule ya msingi ambaye ni mlezi wa watoto, Wizara inawataka wazazi, walezi na jamii kuzingatia wajibu wa ulinzi wa watoto ili kuwahakikishia usalama wao katika maeneo ya majumbani, shuleni, mtaani, njiani na katika jamii kwa ajili ya kutekeleza lengo la kupunguza matukio ya ukatili kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2021/2022.

  Aidha, Wizara inatoa rai kwa jamii na wananchi wema kuwa makini na matumizi ya mitandao ya kijamii ili kuepuka makosa ya kisheria yanayoweza kutokea kwa kusambaza, kuchapisha na kupiga picha za watoto ambao ni wahanga wa ukatili na kuziweka wazi kinyume na Sheria ya Mtoto Na. 21 ya Mwaka 2009.

  Wizara inatoa pole kwa wazazi, ndugu, marafiki na familia ya mtoto aliyefanyiwa ukatili huo. Tunawaomba wanajamii kuendelea kutoa ushirikiano katika kufichua vitendo vyote vya ukatili dhidi ya watoto vinavyojitokeza katika maeneo yao. Aidha, katika kipindi hiki ambapo uchunguzi unaendelea kufanyika tunaomba pawe na utulivu na uvumilivu ili kutoa nafasi kwa vyombo vya dola kufanya uchunguzi kwa makini na Sheria iweze kuchukua mkondo wake.

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto
  (Idara Kuu Maendeleo ya Jamii)
  02/01/2019

  0 0


  Meneja Uchumi Benki kuu ya Tanzania tawi la Zanzibar Moto Ng'winganele Lugobi akijibu maswali yalioulizwa katika hafla ya Utoaji wa Takwimu za Bei ambapo imeonesha kushuka kutoka asilimia 4.4 kwa Mwezi wa Novemba hadi asilimia 3.5 kwa mwezi wa Disemba hafla iliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Mazizini Mjini Zanzibar.


  Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika hafla ya Utoaji wa Takwimu za Bei ambapo imeonesha kushuka kutoka asilimia 4.4 kwa Mwezi wa Novemba hadi asilimia 3.5 kwa mwezi wa Disemba hafla iliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Mazizini Mjini Zanzibar.
  Mkuu wa Takwimu za Bei kutoka Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Khamis Abdul-rahman Msham katikati akitoa maelezo kuhusiana na Takwimu za Bei ambapo imeonesha kushuka kutoka asilimia 4.4 kwa Mwezi wa Novemba hadi asilimia 3.5 kwa mwezi wa Disemba hafla iliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Mazizini Mjini Zanzibar.kulia ni Afisa Mwandamizi Mkuu Benki kuu Tawi la Zanzibar Malik Ali Suleiman na kushoto ni Afisa Uchumi na Biashara (Zura)Omar Ali Yussuf
  Mhadhiri na Mkuu wa Idara ya Uchumi Chuo Kikuu cha Taifa (SUZA)Dkt.Suleiman Simai Msaraka akitolea ufafanuzi maswala mbalimbali yalioulizwa katika hafla ya Utoaji wa Takwimu za Bei ambapo imeonesha kushuka kutoka asilimia 4.4 kwa Mwezi wa Novemba hadi asilimia 3.5 kwa mwezi wa Disemba hafla iliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Mazizini Mjini Zanzibar.

  0 0


  Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO

   
  Vituo vya mafuta nchini vimekumbushwa kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana ili kuepusha usumbufu unaojitokeza kwa wateja na kuwasaidia wadau kufanya maamuzi stahiki kuhusu manunuzi ya bidhaa za mafuta.

  Hayo yamesemwa hivi karibuni na Kaimu M
  kurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Nzinyangwa Mchany wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu bei kikomo za mafuta aina ya petroli zilizoanza kutumika leo januari 2, 2019.

  “Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja, adhabu kali itatolewa kwa kituo husika kwa kutotekeleza matakwa ya kisheria kwa mujibu wa kanuni husika”, alisema Mchany.

  Mchany ameongeza kuwa mabango hayo yanatakiwa kuonesha bei ya mafuta, punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika ili wateja waweze kuwa na uwanja mpana wa kuchagua wapi pa kununua.Aidha, Mchany ametoa rai kwa wateja kununua bidhaa za mafuta katika vituo vinavyouza mafuta kwa bei nafuu zaidi ili kushamirisha ushindani.

  Kwa upande mwingine wauzaji wa mafuta ya petroli wamekumbushwa kutoa risiti za mauzo kutoka kwenye mashine za EFPP (Electronic Fiscal Pump Printers) na wanunuzi wametakiwa kuhakikisha wanapokea stakabadhi hizo za malipo zinazoonyesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita.

  Amefafanua kuwa Stakabadhi hizo za malipo zitatumika kudhibiti watoa huduma wasio waaminifu pale ambapo wanunuzi wa mafuta watakuwa na malalamiko ya kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko bei kikomo au kuuziwa mafuta yasiyo na kiwango cha ubora kinachofaa, pia stakabadhi hizo zitasaidia kurahishisha ukusanyaji wa kodi za Serikali zitokanazo na nishati mafuta.

  Bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya aina zote zimepungua ambapo kwa mwezi Januari 2019, bei za rejareja za Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa zimepungua kwa Shilingi 141/lita (sawa na asilimia 5.80), Shilingi 212/lita (sawa na asilimia 8.69) na Shilingi 167/lita (sawa na asilimia 7.03).

  Vilevile, bei za jumla za Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa zimepungua kwa Shilingi 140.81/lita (sawa na asilimia 6.09), Shilingi 212.12/lita (sawa na asilimia 9.14) na Shilingi 166.02/lita (sawa na asilimia 7.40).

  0 0

    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Songea kuanza ziara ya kikazi mkoani  humo, Januari 2, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (wapili kulia) wakisalimiana  na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Ruvuma, Oddo Mwisho  wakati walipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Songea kuanza ziara ya kikazi mkoani humo, Januari 2, 2018. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, ambaye pia ni Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama na watatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina, Mndeme. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Viongozi wa Mkoa wa Ruvuma wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Songea kuanza ziara ya kikazi mkoani humo, Januari 2, 2018. Kulia ni mkewe Mary na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  BOTI ya Kisasa ya Uokozi na Uzamiaji ya Kikosi cha KMKM Zanzibar imezinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk Ali Mohamed Shein,.leo katika bandari ya Mkoani Kisiwani Pemba, wakati wa Uzinduzi wa Mradi wa Vituo Vya Uokozi vya KMKM.(Picha na Ikulu)
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizindua Boti ya Mradi wa Vituo vya Uokozi na Uzamiaji vya Kikiso cha KMKM Zanzibar,uzinduzi huo umefanyika katika, bandari ya Mkoani Pemba leo,2-1-2019.kushoto Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Vikosi Maalum. Mhe Haji Omar Kheri na kulia Mkuu wa KMKM Commodere Hassan Mussa Mzee.(Picha na Ikulu)
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza CDR.Hussein Ali Makame, akitowa maelezo kwa Rais wakati akitembelea Boti hiyo baada ya kuizindua leo katika Bandari ya Mkoani Kisiwani Pemba ikiwa ni shamrashamra za Sherehe za Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika Boti ya KMKM ya Uokozi baada ya kuizindua akiwa na Mkuu wa KMKM Commodore Hassan Mussa Mzee, (Picha na Ikulu) NO 5665///RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe Hemed Suleiman wakiondoka katika eneo la Bandari ya Mkoa baada ya Uzinduzi wa Boto ya KMKM ya Uokozi na Uzamiaji.
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizindua Kituo cha Mradi wa Uokozi na Uzamiaji cha KMKM Zanzibar, wakati wa shamrashamra za Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Ali Mohamed Shein, akimsikiliza CDR. Hussein Ali Makame. akitowa maelezo ya kimoja ya vifaa vya Uokozi baada yya kukifungua Kituo cha KMKM Cha Mradi wa Uokozi na Uzamiaji katika Bandari ya Mkoani Pemba.(Picha na Ikulu).
  JENGO Jipya la Kituo cha KMKM la Mradi wa Vituo vya Uokozi na Uzamiaji lilioko katika Bandari ya Mkoani Zanzibar.(Picha na Ikulu)
   

  0 0

  *Ni kuhusu vijana waliofaulu darasa la saba

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameutaka uongozi wa mkoa wa Ruvuma uhakikishe kuwa vijana wote wanaomaliza darasa la saba kwenye kila Halmashuri za mkoa huo wanakwenda kuanza kidato cha kwanza.

  Aametoa agizo hilo leo (Jumatano, Januari 2, 2018) wakati akizungumza na viongozi wa mkoa wa Ruvuma baada ya kuwasili kwenye uwanja ndege wa Songea kuanza ziara ya kikazi ya siku nne mkoani Ruvuma.Waziri Mkuu amesema Halmashuri zote za mkoa huo zijikite katika kujenga madarasa ili wanafunzi wote waliofaulu ambao wanatakiwa kwenda sekondari waende.

  Amesema Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kwa dhati kuahakikisha kwamba watoto wote wenye sifa za kupata elimu ya seondari wanapata elimu hiyo kote nchini hivyo juhudi za makusudi lazima zifanywe na kila Halmashauri ili kutimiza azma.Akizungumzia suala la utoro shuleni, Waziri Mkuu amesema hilo ni moja kati ya maeneo yanayozorotesha juhudi kubwa za Serikali za kuwapatia watoto wa Tanzania elimu katika maeneo mengi nchini na lazima viongozi wa wilaya na mikoa wasimame imara ili kukomesha hali hiyo.

  Amesema viongozi wa ngazi zote katika mikoa na wilaya ndiyo hasa wanaoweza kumaliza tatizo la utoro wakishirikiana kwa karibu na wanavijiji ambao wanaishi na watoto hao na wanajua ni watoto wangapi hawaendi shule.Hivyo, Waziri Mkuu amewataka viongozi hao kutoa maelekezo na miongozo itakayowabana watoto watoro pamoja na wazazi au walezi wao kwani wanayo mamlaka na uwezo wa kuchukuwa hatua kwa mujibu wa sheria za nchi.

  Akizungumzia zao la korosho , Waziri Mkuu amewataka viongozi wa mkoa wa Ruvuma kuwaondolea hofu wananchi wanaolima zao hilo katika mkoa huo kwa kuwahakikishia kwamba Serikali inazo fedha za kutosha kununua korosho zote ziliyovunwa na wakulima.

  Kuhusu ukusanyaji wa mapato ya Serikali, Waziri Mkuu amewataka viongozi wa mikoa na wilaya kubeba dhamana waliyopewa na Taifa ambayo ni pamoja na kusimamia ukusanyaji mapato ya Serikali kwa kishirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). "Halmashauri zote na wakuu wa wilaya wasimamie kwa dhati ukusanyuaji wa kodi."

  Akiwa mkoani Ruvuma, Waziri Mkuu kesho anatarajiwa kufungua soko la mazao la Lilambo katika wilaya ya Songea, kufungua ghala la mazao la Mgazini na kuweka jiwe la msini la ujenzi wa zahanati ya Luganga na kisha kuhutubia mkutano wa hadhara.

  Keshokutwa Waziri Mkuu ataongoza kikao cha wadau wa zao la kahawa kitakachowashirikisha pia Waziri wa Kilimo na Mrajisi wa Ushirika. Wengine watakaoshiriki katika kikao hicho ni viongozi wa AMCOS, UNION na viongozi wa Bodi ya kahawa.

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Viongozi wa Mkoa wa Ruvuma wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Songea kuanza ziara ya kikazi mkoani humo, Januari 2, 2018. Kulia ni mkewe Mary na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0


   Kifusi cha mchanga kilicholetwa muda mfupi kabla  ya Waziri Suleiman Jafo kuwasili
  image2
  Waziri Suleiman Jafo akitembelea eneo la ujenzi kituo cha afya mikumi
  image3
  Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe.  Adam Mgoyi pamoja na Mbunge wa Mikumi Mh. Joseph Haule wakinuahidi waziri Jafo usimamizi wa makini wa ujenzi wa Kituo cha Afya Mikumi
  …………………………………………………………..
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Sulemani Jafo ameonyesha kukerwa sana na uzembe uliofanywa na watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilosa kwa kusasua ujenzi wa kituo cha Afya Mikumi licha ya kupokea fedha tangu mwishoni mwa mwezi June 2018.
  Katika ziara hiyo ya kushtukiza watendaji wa Halmashauri ya wilaya Kilosa inaonekana walidamka asubuhi ya leo na kupeleka mchanga zaidi ya Maroli sita pamoja na fundi aliyekuwa akichanganya mchanga huo ili ionekane kazi inaendelea lakini waziri Jafo aligundua janja hiyo na kutoa maagizo mazito kwa Uongozi wa Halmashauri hiyo.
  ‘ Niwatake Mkurugenzi wa Kilosa,  Mweka Hazina, Mkanga Mkuu wa Wilaya,  Afisa Mipango pamoja na Mhandisi kuwasilisha barua zenu haraka sana Ofisi ya Rais Tamisemi za kujieleza kwanini msichukuliwe hatua kutokana na uzembe mlioufanya katika kituo hiki’ aliagiza Jafo.
  Aliongeza kuwa Mpaka sasa  kituo hikinwapo katika hatua ya msingi wakati wenzao wa maeneo mengine waliopewa fedha wakati mmoja wakiwa katika hatua za umaliziaji.
  Ziara hiyo ya waziri Jafo Mkoani Morogoro amefanikiwa kutembelea ujenzi wa kituo cha afya Mikumi,  ujenzi wa kituo cha afya Kidodi, pamoja na kutembelea eneo la Luhembe ambapo patajengwa daraja kubwa litakalo gharimu zaidi ya shilingi milioni mia nane.

  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Dkt.Salim Ahmed Salim hospitalini Jijini Dar es Salaam, alipomtembelea pamoja na Mkewe Janeth Magufuli ili kumjulia hali.Januari 2 ,2019
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu Dkt.Salim Ahmed Salim hospitalini Jijini Dar es Salaam, alipomtembelea pamoja na Mkewe Janeth Magufuli ili kumjulia hali.Januari 2 ,2019

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakiomba Dua Maalumu na Mama Janeth Magufuli pamoja na Mama Amne Salim (Mke wa Dkt.Salim) ya kumuombea Waziri Mkuu Mstaafu Dkt.Salim Ahmed Salim, walipomtembelea ili kumjulia hali Jijini Dar es Salaam. Januari 2 ,2019
  PICHA NA IKULU

  0 0

  Na Abullatif Yunus - Kagera. 

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Kangi Lugola, ameanza Rasmi ziara yake Mkoani Kagera kwa kukutana na Idara pamoja na Taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo, na kisha kufanya Mkutano wa hadhara licha ya Mkutano huo kuchelewa kutokana na Majukumu yaliyokuwepo.

  Mh. Kangi Lugola katika hotuba yake iliyojaa ufafanuzi wa Utekelezaji unaofanywa na Mh. Rais John Pombe Magufuli, katika Kusimamia Amani ya Nchi na Watanzania kwa Ujumla, na kuwa Mh. Rais hapendi kusikia Mwananchi yeyote akionewa, na kunyimwa haki kwa namna yoyote ile.

  Sambamba na hilo Mh. Waziri Lugola, katika kuwakumbusha Watendaji na watumishi ndani ya Vyombo vya Ulinzi vya Usalama kuendelea kutenda haki na kulinda Amani bila kuchoka, isipokuwa wale wachache ambao wamekuwa wakichafua Vyombo vya Ulinzi kutafuta Kazi nyingine ya kufanya, akitolea mfano baadhi ya Askari wa Jeshi la Polisi wanaofukuza Bodaboda, na kukamata Bodaboda Gulioni.

  Kuhusu Wananchi wanaowakaribisha Raia wasio Watanzania na Wahamiaji haramu amewatahadhalisha wenye kufanya hivyo waache Mara moja kwani kwa kufanya hivyo ni kuhatarisha Usalama wa Nchi yetu, ikiwa ni sambamba na wale wanaofanya shughuli za magendo.

  Katika Mkutano huo wa hadhara Mh. Waziri Lugola amepata nafasi ya kusikiliza kero mbalimbali kutoka kwa Wananchi nakuahidi kuzishughulikia ndani ya muda mfupi kabla hajaondoka Mkoani Kagera.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Kangi Lugola akizungumza na Wananchi waliohudhuria kumsikiliza katika Uwanja wa Mayunga Mjini Bukoba. 
   Bi Sauda Amiri (34) Mkazi wa Bukoba Manispaa, Akitoa kero yake kwa Mh. Lugola juu ya Uonevu aliofanyiwa kwa kuchomewa Nyumba yake pamoja na  kufyekewa shamba lake la miche ya nyanya 1500.
   Sehemu ya Umati uliojitokeza katika Viwanja vya Mayunga Bukoba kumsikiliza Mh. Kangi Lugola Januari 2, 2019.


  0 0

   Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro amezindua zoezi la utoaji wa vitambulisho Kwa ajili ya wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama wamachinga ambao mauzo ghafi Hayazidi Shilingi milioni 4.,kama aonekanavyo pichani DC Muro akikambidhi mmoja wa machinga kitambulisho hicho,aidha zoezi hilo  limefanyika katika Halmashauri ya Arusha Dc, eneo la Ngaramtoni na Halmashauri ya Meru katika eneo la Uwanja wa Ngaresero ambapo limehudhuriwa na mamia ya wafanyabiashara Ndogondogo
   Baadhi ya Wafanyabiashara ndogo ndogo wakiwa wamejitokeza kwa wingi wakisubiri kupewa vitambulisho hivyo,ambavyo vimeonekana kuwa umuhimu mkubwa kwao.
    Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro pichani katikati akitoa maelekezo kwa baadhi ya Wafanyabiashra ndogo ndogo,mara baada ya kuzindua zoezi hilo la utoaji wa vitambulisho Kwa ajili ya wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama wamachinga ambao mauzo ghafi Hayazidi Shilingi milioni 4.


   
  Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro amezindua zoezi la utoaji wa vitambulisho Kwa ajili ya wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama wamachinga ambao mauzo ghafi Hayazidi Shilingi milioni 4.

  Akizindua zoezi hilo la utoaji wa Vitambulisho ambalo limefanyika katika Halmashauri ya Arusha Dc eneo la Ngaramtoni na Halmashauri ya Meru katika eneo la Uwanja wa Ngaresero ambapo limehudhuriwa na mamia ya wafanyabiashara Ndogondogo ambao watanufaika na zoezi hilo ambapo Kwa kuanzia Wilaya itatoa zaidi ya vitambulisho elfu sita Kwa wafanyabiashara ndogondogo Wilayani Arumeru.

  Awali Ndugu Muro akitoa taarifa ya utekelezaji wa zoezi la ugawaji wa vitambulisho hivyo , Meneja wa mamlaka ya mapato nchini TRA Wilayani Arumeru Bwana Musa Sudi amesema wataendelea kutoa Elimu kwa wafanyabiashara ili waweze kutambua fursa zilizopo katika kufanya Biashara kupitia vitambulisho vya Magufuli hatua ambayo itawarahisishia ulipaji wa kodi pamoja na kuwasaidia kukua kibiashara.

  Wakizungumza Kwa nyakati tofauti wakati wa zoezi la utoaji wa vitambulisho hivyo , wakurugenzi wa Halmashauri za Arusha na Meru Ndugu Emanuel Mkongo pamoja na Dkt . Charles Mahela wamesema Halmashauri zimeweka utaratibu mzuri wa Kuwatambua wafanyabiashara pamoja na kuwaratibu ili waweze kutambuliwa na kuingizwa kwenye Mfumo rasmi ambao utatoa fursa ya wao kuweza kukua na kuepuka migongano ya mara Kwa mara katika kufanya biashara.

  0 0

  Ziara ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Taifa, Dkt. Bashiru Ally Kakurwa Mkoani Kagera, imehitimishwa Januari 02, 2019 kwa kukutana na Viongozi, Wanachama na wajumbe wa Halmashauri ya Wilaya Bukoba Vijijini, katika Kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Bukoba Coop Mjini Bukoba.

  Katika Mkutano huo pamoja na mambo mengine, Dkt. Bashiru amehitimisha kwa kuwataka wajumbe wa Kikao hicho kusitisha mchakato na mgogoro uliokuwa ukifukuta ndani ya CCM, baina ya Mbunge wa Jimbo la Bukoba Vijijini Mh. Jasson Rweikiza pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bukoba, Ndg. Murshidi Ngeze kuacha Mara moja kwani hauna tija wala faida ndani ya Chama, zaidi ni kuzorotesha Maendeleo.

  Akirejea mgogoro huo kabla ya kusuluhisha, amenukuliwa akisema kuwa kumekuwepo na hali isiyokuwa ya kawaida kati ya Madiwani wanoumuunga mkono Mbunge na wale wanaomuunga mkono Mwenyekiti kuhusu wapi ijengwe Hospitali ya Wilaya ya Bukoba. 

  Katibu Bashiru amethibitishia Kikao juu ya Kuomba radhi na Kukiri mbele ya Kamati ya Siasa kwa Mwenyekiti kuwa aliyumba kimaamuzi licha ya suluhisho kupatikana kuwa Hospitali ijengwe eneo la Kanazi kulingana na hoja za kitaalamu na Ukubwa wa eneo husika.

  Kufuatia maelezo hayo Viongozi hao wawili Mbunge na Mwenyekiti wakapata nafasi ya kujieleza na kisha kumaliza tofauti zao za kisiasa huku Katibu Mkuu akimuomba Ndg. Rweikiza (MB) kurudisha malalamiko yake ndani ya Chama na sio Mhakamani kwa kile anacholalamika kuwa Ndg. Ngeze (Diwani Kata Rukoma) alimdhalilisha kwa kumtuhumu kuwa Mbunge Rweikiza alitoa Rushwa katika mchakato wa Uchaguzi. 

  Tayari Mh. Rweikiza amekubali kurejea kwenye Vikao vya suluhisho na maadili ya Chama kulalamika upya, ingawa Dkt. Bashiru kaelekeza Viongozi hao kwenda kutoa ufafanuzi mzuri eneo la Ikimba ambalo baadhi ya watu walipotosha kuwa wametengwa kufuatia Hospitali kutojengwa eneo lao.

  Aidha Dkt. Bashiru amepata nafasi ya kuwakaribisha rasmi madiwani waliorudi kutoka Vyama pinzani, huku kivutio kikubwa akiwa ni Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bukoba Kapteni Mstaafu wa Jeshi la Wananchi Ndg. Kateme ambae baada ya kushindwa katika kinyanganyiro cha Uchaguzi katika Kara ya Kaibanja, alitimkia CUF na sasa ameamua kurejea kutokana na kuridhishwa na muundo wa Serikali iliyopo madarakani, na Utendaji kazi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuli.
  Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Taifa, Dkt. Bashiru Ally Kakurwa akizungumza  wakati akihitimisha ziara yale leo Bukoba mkoani Kagera kwa kukutana na Viongozi, Wanachama na wajumbe wa Halmashauri ya Wilaya Bukoba Vijijini, katika Kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Bukoba Coop Mjini Bukoba.
  Baadhi ya Wanachama na wajumbe wa Halmashauri ya Wilaya Bukoba Vijijini wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Taifa, Dkt. Bashiru Ally Kakurwa  katika Kikao chao kilichofanyika katika Ukumbi wa Bukoba Coop Mjini Bukoba.

  0 0

  Mkazi mmoja wa jijini Dar es Salaam ametoa msaada wa vifaa tiba aina ya (suction machines) kwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ili kusaidia wagonjwa wenye matatizo katika mfumo wa hewa baada ya kuvutiwa na huduma nzuri za matibabu alizopatiwa mtoto wake.

  Mashine aina ya suction inatumiwa na wataalam wa afya kwa ajili ya kunyonya makohozi mdomoni, puani na katika koo la mgonjwa kwa lengo la kumpatia mgonjwa tiba iliyokusudiwa. Msaada huo una thamani ya shilingi 800,000 na umetolewa leo na mkazi wa Kigamboni jijini Dar es Salaam, Bi. Elizabeth Amandus kutokana na huduma nzuri ambayo alipatiwa mtoto wake Februari 28, 2018 baada ya kumfikisha Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi.

  Bi. Elizabeth alisema alijifungua mtoto wake katika hospitali nyingine, huku akiwa hajatimiza umri unaotakiwa (njiti) na kupewa rufaa ya kumpeleka Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi.

  “Wataalam wa Muhimbili walinipokea vizuri, nikahudumiwa mimi na mtoto wangu hivyo nimeamua kutoa msaada wa mashine hizi mbili ili ziwasaidie watoto wachanga wanaoletwa hapa,” amesema Bi. Elizabeth.

  Akipokea msaada huo, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi wa hospitali hiyo, Sista Zuhura Mawona amesema msaada huo umewatia moyo na kwamba wataendelea kufanya kazi kwa juhudi kubwa. “Kwa niaba ya uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, natoa shukrani kwa Bi. Elizabeth kutokana na kutambua juhudi zetu za kutoa huduma bora kwa wagonjwa, ametutia moyo kuchapa kazi kwa bidii zaidi,” amesema Sista Mawona. 
  Mkurugezi wa Huduma za Uuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Sista Zuhura Mawona akipokea msaada wa mshine ya kusaidia wagonjwa wenye matatizo kwenye mfumo wa hewa kutoka kwa Bi. Elizabeth Amandus baada ya mtoto wake kupatiwa huduma nzuri za matibabu na wataalam wa hospitali hiyo.
  Mkurugezi wa Huduma za Uuguzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Sista Zuhura Mawona akizungumza baada ya kupokea msaada huo leo kutoka kwa Bi. Elizabeth Amandus.
  Sista Mawona akiwa katika picha na baadhi ya wataalam wa Muhimbili pamoja na ndugu wa Bi. Elizabeth. 


  0 0


  Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Dk,Sira Ubwa Mamboya akibonyeza kitufe kuashiria Uzinduzi wa Mfumo Mpya wa kutolea huduma za Kibenki uliofanyika katika Makao makuu ya PBZ Mpirani Wilaya ya Mjini Unguja Ikiwa Shamra shamra za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Dk,Sira Ubwa Mamboya akisisitiza jambo alipotoa hotuba ya Ufunguzi wa Mfumo Mpya wa kutolea huduma za Kibenki uliofanyika katika Makao makuu ya PBZ Mpirani Wilaya ya Mjini Unguja Ikiwa Shamra shamra za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  Baadhi ya Wafanyakazi wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ)waliohudhuria katika Uzinduzi wa Mfumo Mpya wa kutolea huduma za Kibenki uliofanyika katika Makao makuu ya PBZ Mpirani Wilaya ya Mjini Unguja Ikiwa Shamra shamra za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

  Katibu Mkuu Fedha na Mipango Khamis Mussa Omar akitoa hotuba na kumkaribisha mgeni rasmi katika hafla ya Uzinduzi wa Mfumo Mpya wa kutolea huduma za Kibenki uliofanyika katika Makao makuu ya PBZ Mpirani Wilaya ya Mjini Unguja Ikiwa Shamra shamra za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  Mkurugenzi mtendaji wa PBZ Juma Ameir Hafidh akitoa hotuba katika hafla ya Uzinduzi wa Mfumo Mpya wa kutolea huduma za Kibenki uliofanyika katika Makao makuu ya PBZ Mpirani Wilaya ya Mjini Unguja Ikiwa Shamra shamra za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

  0 0

  NA MWAMVUA MWINYI, PWANI 

  MAKOSA ya ubakaji yametajwa kuongezeka kutoka 206 kwa mwaka 2017 na kufikia 271 mwaka 2018,mkoani Pwani .

  Aidha kupatikana na silaha mwaka 2017 yalikuwa makosa tisa ambapo mwaka uliopita yameongezeka na kufikia 26 .

  Akielezea tathmini ya hali ya uhalifu katika kipindi cha mwaka 2018 ikilinganisha na mwaka 2017 ,kamanda wa polisi mkoani Pwani (ACP) Wankyo Nyigesa alisema tathmini ya kijumla inaonyesha wamepunguza matukio 151 makubwa .

  Alisema, makosa ya ubakaji yameonekana kupanda kutokana na uelewa kwa jamii na mwamko wa kuripoti matukio hayo polisi. Wankyo alieleza, matukio ya mauaji yalikuwa 61 ikilinganisha na matukio 70 yaliyoripotiwa mwaka 2017 ."Makosa ya kufanya biashara ya kusafirisha binadamu mwaka 2018, yalikuwa 03 ikilinganishwa na makosa 05 yaliyorekodiwa mwaka 2017"alifafanua Wankyo. 

  Kamanda huyo alisema kuwa, makosa ya unyang 'anyi wa kutumia silaha mwaka 2017 yalikuwa 21 na mwaka 2018 makosa hayo ni 13.Unyang'anyi wa kutumia nguvu mwaka 2017 yaliriporiwa makosa 126 ,wakati mwaka 2018 makosa ya namna hiyo yameripotiwa makosa 52 .

  Alisema, jeshi hilo pia limefanikiwa kudhibiti uingizaji bidhaa kupitia bandari bubu wilayani Bagamoyo kwa kukamata makosa 27,watuhumiwa 31 pamoja na madumu 5,435 ya mafuta ya kula aina mbalimbali .

  "Sukari kutoka nchi za nje mifuko 78, mabello 20 ya nguo za mitumba aina mbalimbali ikiwemo manne ya khanga na vyombo vya moto vilikamatwa ikiwa ni pamoja na pikipiki sita na magari matatu. "alieleza Wankyo.
  kamanda wa polisi mkoani Pwani (ACP) Wankyo Nyigesa  akitoa ufafanuzi .

  0 0

  Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii.

  Wakili wa upande wa mashtaka Katika kesi ya uchochezi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe  na viongozi wenzake nane,  Process Abdallah Safari ameuhoji upande wa mashtaka iwapo rufaa waliyokata Mahakama ya rufaa ilikuwa chini ya hati ya dharura na kama Hawakufanya  hivyo ni kwa nini.

  Hatua hiyo imekuja baada ya wakili wa Serikali Mkuu, Paul Kadushi kuieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa kesi  hiyo leo January 3.2019 imekuwa kwa ajili ya kutajwa. Akijibu Awali hilo, wakili Kadushi amedai, hakuna uhalali wa kisheria kuhusu swali hilo mahakamani hapo, labda lingeulizwa Mahakama Kuu au Mahakama ya Rufaa

  Katika kesi hiyo  inayounguruma mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,  Wilbard Mashauri,  Mbowe, na Mbunge wa Tarime mjini, wanasota eyande baada ya kukiuka masharti ya dhamana na kufutiwa dhamana yao hiyo. 

  Mbowe na Matiko watandelea kusota rumande hadi tarehe tajwa kufuatia Mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam kusimamisha usikilizwaji wa rufaa iliyokatwa na upande wa mashtaka wakipinga maamuzi ya Mahakama ya Mahakama Kuu ya kusikiliza rufaa iliyowasilishwa ya na washtakiwa kudinga kufutiwa kwao dhamana. 

   Novemba 26, 2018 Washtakiwa hao walifutiwa dhamana zao baada ya kukiuka masharti ya dhamana. Baada ya mabishano kidogo, Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi January 17,2019 huku akisema swali hilo la rufaa wakalihoji Mahakama Kuu.
   
  Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Katibu wa Chadema, Dk. Vincent Mashinji, Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya  na Katibu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu  

  Wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 13, ikiwemo kula njama,  kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai kati ya February Mosi na 16,  mwaka huu maeneo ya  Dar es Salaam.

  Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe akitoka mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kurejea rumande mara baada ya kesi yake kuahirishwa na kutajwa tena january 17 /2019.
  Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe akiwa na washtakiwa wenzie akizungumza na Wakili wake Prof Award Safari.
  Mbunge wa Kibamba kupitia Chadema, John Mnyika, akizungumza na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Vicent Mashinji mara baada ya kutoka katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu
  Mbunge wa Kawe, Halima Mdee akitoka nje ya jengo la Mhakama mara baada ya kuahirishwa kwa kesi inayowakabili katika mahakama hiyo.
  Baadhi ya Viongozi Waandamizi Wachadema wakitoka katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu mara baada ya kuahirishwa kwa kesi ya Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe.

  0 0


  • Thamani ya HaloPesa hadi 356%
  . Malengo kuwafikia wateja wa Halopesa 1.5 million 2019

  2018 ulikuwa mwaka mzuri kwa Kampuni ya Halotel Tanzania ikiwa moja ya Kampuni ya Mawasiliano iliyosajiliwa nchini ikifanikiwa kuongeza idadi ya wateja na mawasiliano katika maeno mbalimbali nchini.

  Takwimu zilizopo zinaonyesha watumiaji wa mtandao wa Halotel hadi Septemba imeweza kufikia wateja Milioni 4 ikikua kutoka wateja 3.7 Milioni Septemba Mwaka 2017 .Halkadhalika idadi ya watumiaji wa Halopesa ikionekana kuongezeka kwa kasi kutoka watumiaji 358,217 Septemba Mwaka 2017 hadi watumiaji 800,000 Septemba Mwaka 2018.

  Akizungumza Jijini Dar es Salaam leo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Nguyen Van Son, kuongezeka kwa mafanikio hayo ya Kampuni hiyo hususani katika huduma za watumiaji wa Halopesa kumetokana na mpango wa utoaji huduma kwa wateja uliozinduliwa na Kampuni mapema Mwaka 2018.

  “Kwa kifupi kampuni imeweza kukua katika utoaji wa huduma zake mbalimbali kwa kipindi chote cha mwaka uliopita, katika kipindi hicho Halotel imezindua huduma mbalimbali ikiwemo huduma shirikishi inayomwezesha mteja kutuma au kupokea Fedha kutoka Halopesa kwenda katika akaunti yake au mtandao mwingine wowote wa simu; pia tulizindua huduma ya utoaji mkopo ijulikanayo kama ‘HaloYako’.

  “Aidha katika kipindi hicho pia tulikuja na mpango wa ulipaji malipo mbalimbali Serikalini kumwezesha mteja kuondokana na usumbufu mbali na hiyo pia tumeweza kumrahisishia mteja kuweza kutuma fedha katika benki zaidi ya 20 zilizopo nchini” alisema Son.HaloPesa ilikuwa na mawakala hai wapatoa 10,367 Mwaka 2017 lakini hadi tunapozungumza hivi sasa idadi hiyo imeongezeka na kufikia Mawakala 155,000 nchini kote

  Aidha alisema mapato yaliyotokana na thamani ya manunuzi ya HaloPesa pia yaliongezeka hadi kuifikia 183%, "Tuliona kiwango cha 356% katika thamani ya manunuzi ya HaloPesa na ongezeko kwa 167% alisema.

  Mafaniko hayo yalitokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Halotel kwa kuweka miundombinu katika maeneo mbambali nchini katika kipindi cha Mwaka 2018.Alisema hatua hiyo ilichangiwa na ushirikiano wa kampuni hiyo na Serikali hasa katika utekelezaji wa awamu ya pili ya uboreshaji wa mawasiliano kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) ulioiwezesha Halotel kufiksha mawasiliano katika Vijiji 240 katika kipindi cha Mwaka jana.

  Kampuni pia imeweza kuunganisha mawasiliano kupitia mkongo zenye urefu wa Kilomita 2000 katika maeneo yenye miundombinu yake kwa ajili ya kuwezesha upatikanaji wa data kwa maeneo mapya; kupitia hilo Halotel imeendelea kuwa chaguo la kwanza kwa wateja pale linapokuja suala la huduma za Intaneti.

  “Hii ndio sababu tumeweza kuongeza dakika zaidi za kupiga kwenda katika mitandao yote hasa kupitia kifurushi cha kila kikimpta mteja unafuu wa hadi asilimia 32% lengo ni kumpa mteja kitu anachostahili kupitia ofa hiii maalumu ni hii ilitokana na mahitaji hasa kwa wateja wa Dar es Salaam na Manyara” alisema Son.

  Akizingumzia malengo ya mwaka 2019, “Tunaamini kuwa Mwaka huu utakuwa ni wenye mafanikio makubwa kwa Halotel na Halopesa kwa ujumla tukilenga kuwafikia wateja zaidi 1.5 Milioni ifikapo mwisho wa mwaka 2019. Aliongeza Son.

  Alisema chini ya utekelezaji wa mpango wa awamu ya tatu ya UCSAF iliousaini Desemba Mwaka 2018, Halotel inatarajia kufikisha mawasiliano na kuviunganisha vijiji zaidi 328 nchi nzima.

  Kupitia hatua hiyo anaamini kampuni itazidi kuweka maboresho katika huduma za kifedha kupitia mtandao mara mbili zaidi.Alisema pia Halotel pia itazindua ufumbuzi zaidi wa malipo, na zaidi ikijipanga kuendelea h kuwa kiongozi katika ufumbuzi wa ICT nchini.  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel, Nguyen Van Son, akizungumza mbele ya Waandishi wa habari leo jijini Dar kuhusu mafaniklio iliyopata katika kipindi cha mwaka 2018, ikiwemo kuimarika kwa huduma ya Halopesa na kwa mkongo wa mawasiliano wa kampuni hiyo ambao umefikishwa katika vijiji zaidi ya Kumi na tatu elfu nchi nzima,kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel, Mhina Semwenda.
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel, Mhina Semwenda, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam, leo kuhusu mafanikio iliyopata katika kipindi cha mwaka 2018, ikiwemo kuimarika kwa huduma ya Halopesa na kwa mkongo wa mawasiliano wa kampuni hiyo ambao umefikishwa katika vijiji zaidi ya Kumi na tatu elfu nchi nzima. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji , Nguyen van Son.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na mamia ya wananchi mjini Bukoba Mkoani Kagera, katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Uhuru, Mayunga mjini humo, leo. Lugola licha ya kuwa amewataka waendesha bodaboda wafuate sheria za usalama barabarani, lakini ametoa onyo kwa Polisi mjini humo kuacha kuwakamata waendesha bodaboda wakiwa hawajavaa sare.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akimsikiliza Mkazi wa mjini Bukoba alipokuwa anaeleza kero yake mara baada ya Waziri huyo kuwaita wananchi hao mbele waweze kutoa kero zao, mara baada ya kumaliza kuzungumza na wananchi hao katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Uhuru, Mayunga mjini humo, leo. Lugola licha ya kuwa amewataka waendesha bodaboda wafuate sheria za usalama barabarani, lakini ametoa onyo kwa Polisi mjini humo kuacha kuwakamata waendesha bodaboda wakiwa hawajavaa sare.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akimsalimia Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Bashiru Ally, wakati alipoonana naye Uwanja wa Ndege wa Bukoba, leo. Lugola yupo Mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi akitembelea Wilaya zote, akisikiliza kero mbalimbali za watumishi wa Wizara yake pamoja na wananchi mkoani humo.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akitoka Kituo Kikuu cha Polisi cha mjini Bukoba mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Kituo hicho, leo, kwa kufuatilia utendaji kazi wao. Katikati ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Revocatus Malimi, na kulia ni Mkuu wa Jeshi la Magereza Mkoani humo, ACP Raymond Mwampashe. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.  Na Felix Mwagara, MOHA-Bukoba.

  WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amepiga marufuku tabia ya baadhi ya Askari Polisi nchini kukamata pikipiki wakiwa hawana sare za Jeshi.

  Akizungumza na mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa uhuru, Mayunga, mjini Bukoba Mkoani Kagera, leo, Lugola alisema polisi wanapaswa kufuata utaratibu wa kijeshi hasa wanapokamata vyombo vya moto na siyo kuvunja utaratibu.

  Lugola aliongeza kuwa, bodaboda zinazovunja sheria za usalama barabarani zinapaswa kukamatwa bila kuwaonea huruma, ila ni kosa Polisi kuwanyanyasa vijana hao ambao wanapata ridhiki kupitia biasahara hiyo. “Mnapaswa kukamata hizi bodaboda zinapofanya makosa, tabia ya kukurupuka huku mkitafuta fedha zisizo halali, huko ni kuwaonea waendesha bodaboda,” alisema Lugola.

  Pia Lugola aliwataka waendesha bodaboda mjini Bukoba na Tanzania kwa ujumla wafuate sharia za usalama barabarani zikiwemo kuvaa kofia ngumu, kutokubeba abiria zaidi ya mmoja na pia wakiendesha wanapaswa kuwasha taa. Lugola ameanza ziara yake ya siku nane mkoani humo akitembelea Wilaya zote za Mkoa huo akisikiliza kero za wananchi pamoja na kufuatilia maagizo yake aliyoyatoa kwa vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo ndani ya Wizara yake.

  Lugola mwaka jana alitoa maagizo kwa makamanda wa mikoa nchini ambayo ni dhamana zitolewe saa 24 katika vituo vyote vya polisi nchini, na pia kupiga marufuku tabia ya baadhi ya Polisi kubambikizia kesi wananchi, na pamoja na agizo la pikipiki zote zilizopo vituoni ziondolewe.

  Waziri Lugola tayari amemaliza ziara yake kwa Wilaya ya Bukoba na Kesho ataanza ziara Wilaya za Misenyi, baadaye Karagwe, Kyerwa, Ngara, Biharamulo na Januari 8, 2019 atamalizia ziara yake Wilaya ya Muleba ambapo katika Wilaya hizo pia atazungumza na wananchi pamoja na watumishi waliopo ndani ya Wizara yake ambao ni Jeshi la Polisi, Idara ya Uhamiaji, Jeshi la Magereza, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, pamoja na Idara ya Probesheni ambayo jukumu lake kuu ni kupunguza msongamano gerezani na kusimamia wafungwa waliopewa adhabu mbadala na Mahakama au wafungwa waliopata msamaha kupitia sheria ya huduma kwa jamii na kutumikia kifungo chao nje ya Gereza.

older | 1 | .... | 1765 | 1766 | (Page 1767) | 1768 | 1769 | .... | 1898 | newer