Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46379 articles
Browse latest View live

TFDA yaongoza Afrika kwa kuwa na mfumo bora wa udhibiti wa dawa

$
0
0
Na. Immaculate Makilika- MAELEZO

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imetambulika kufikia ngazi ya tatu (Maturity Level 3) ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ya ubora wa mfumo wa udhibiti wa dawa, hatua ambayo imeifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kupata mafanikio hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, kuhusu mafanikio ya taasisi hiyo katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Adam Fimbo, alisema kuwa TFDA imepata mafanikio hayo makubwa kutokana na kuwa na mifumo thabiti ya udhibiti wa ubora, usalama na ufanisi wa dawa, ambapo Desemba mwaka huu, imetambulika kufikia ngazi ya tatu (Maturity Level 3) ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ya ubora wa mfumo wa udhibiti wa dawa, hatua ambayo imesaidia Tanzania kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kufikia hatua hiyo muhimu.

“Hii ni hatua kubwa kwa kuwa taasisi ya mfano barani Afrika katika udhibiti wa bidhaa za chakula, dawa, vipodozi, vifaa tiba na vitendanishi na hivyo kuvutia nchi mbalimbali kuja TFDA kujifunza mifumo iliyopo na kwenda kuitekeleza nchini mwao na sasa mifumo yetu imetambulika na kujulikana na nchi nyingi kwa mfano Zimbabwe, Rwanda, Kenya, Uganda, Ethiopia, Sudan Kusini, Botswana, Mauritius, Lesotho na Bangladesh” alisema Kaimu Mkurugenzi huyo wa TFDA

Sambamba na hilo, Kaimu Mkurugenzi huyo wa TFDA, aliongeza kuwa katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Tano mfumo wa usajili wa bidhaa umeendelea kuimarika mwaka hadi mwaka ambapo idadi ya bidhaa za chakula, dawa, vipodozi, vifaa tiba na vitendanishi vilizosajiliwa imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka,

Akitolea mfano katika kipindi cha 2015/16 hadi 2017/18, TFDA imesajili jumla ya bidhaa 14,345 kutoka bidhaa 8,866 zilizokuwa zimesajiliwa mwaka 2015/16 ambapo ni sawa na ongezeko la 62%. Ikiwa ni kuongezeka kwa uelewa wa matakwa ya sheria miongoni mwa wafanyabiashara na kukua kwa biashara.

Kaimu Mkurugenzi huyo wa TFDA, alifafanua kuwa tathmini na usajili wa bidhaa hufanyika kwa lengo la kuhakiki endapo bidhaa zinakidhi vigezo vya usalama, ubora na ufanisi kabla ya kuruhusiwa katika soko. Kuwepo kwa bidhaa nyingi zilizosajiliwa katika soko ni uthibitisho kuwa walaji wanapata bidhaa zilizo salama, zenye ubora na ufanisi.

Kuhusu udhibiti wa uingizaji na usafirishaji wa bidhaa ndani na nje ya nchi, alisema kuwa katika kutekeleza hilo ambalo ni agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, la mwezi Mei, 2017, TFDA imeweka wakaguzi wake ambao hufanya kazi masaa 24 kwa siku zote za juma, pamoja na mfumo wa kieletroniki wa utoaji vibali vya kuingiza na kutoa nchini bidhaa unaomwezesha mteja kutuma maombi, kufanya malipo popote alipo na hatimaye kupata kibali ndani ya masaa 24.

Aidha, kwa kutumia mifumo hiyo, mwenendo wa utoaji wa vibali vya uingizaji na utoaji wa bidhaa nje ya nchi umeongezeka ambapo katika mwaka 2017/18, jumla ya vibali 11,866 sawa na ongezeko la 91% ukilinganisha na 13,018 mwaka 2016/17 vilitolewa.

Vilevile, katika jitihada za kujenga Tanzania ya viwanda ifikapo 2025, TFDA imeendelea kutoa msaada wa kiufundi na kuwajengea uwezo wenye viwanda vya dawa nchini na kushawishi wawekezaji kujenga viwanda vya dawa, chakula, vipodozi na vifaa tiba. Ambapo hadi sasa jumla ya wawekezaji 70 wameonesha nia ya kuanzisha viwanda vya dawa huku viwanda vinne vikiwa vimeanza kujengwa katika maeneo ya Morogoro na Kibaha. 

Sambamba na hilo, Kaimu Mkurugenzi huyo alisema kuwa, mafanikio mengine ya TFDA yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitatau ya Serikali ya Awamu ya Tano ni pamoja na kuweka mifumo madhubuti ya ufuatiliaji wa madhara yatokanayo na matumizi ya chakula, dawa na vifaa tiba ili kuweza kutambua, kutathmini na kuzuia madhara yasiyovumilika yasitokee kwa wananchi.

Pia, kwa kipindi cha mwaka 2015/16 hadi 2017/18, matokeo ya uchunguzi wa sampuli yanaonesha kuwa bidhaa zilizochunguzwa zimekidhi viwango vya ubora na usalama kwa wastani wa 88%.

Alifafanua kuwa maabara ya uchunguzi wa dawa imekidhi vigezo vya kimataifa na kutambuliwa rasmi na Shirika la Afya Duniani (prequalification), maabara ya uchunguzi wa chakula na ile ya maikrobiolojia zimepata ithibati kwa kiwango cha kimataifa cha ISO/IEC 17025:2005. Hii inafanya majibu ya uchunguzi yanayotolewa na maabara kuaminika na hivyo kutambulika kitaifa na kimataifa, hali ambayo inamuhakikishia mwananchi uhakika wa maamuzi ya mamlaka kuhusiana na ubora wa bidhaa.

TFDA imefanikiwa kufikia na kuvuka malengo iliyojiwekea katika utekelezaji wa mipango kazi yake, ambapo katika kipindi cha mwaka 2017/18 itaendelea kutoa kipaumbele katika utekelezaji kwa ufanisi wa malengo mahususi nane (8) yaliyomo katika Mpango Mkakati mpya wa miaka mitano (5) yaani 2017/18 – 2021/22, ili kulinda afya ya jamii.

WAZIRI MKUU AZINDUA TAWI LA BENKI YA CRDB RUANGWA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Tawi la Benki ya CRDB la Ruangwa, Desemba 31, 2018. Kushoto ni Mkewe Mary, wapili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Hussein Laay, wapili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Ruangwa, Hashim Ngandirwa. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Tawi la Benki ya CRDB la Ruangwa, Desemba 31, 2018. Wengine pichani kutoka kulia ni Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Hussein Laay na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Tawi la Benki ya CRDB la Ruangwa, Desemba 31, 2018. Kushoto ni mkewe Mary, wapili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya CRDB, Ally Hussein Laay na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela. 
Jengo la Benki ya CRDB tawi la Ruangwa ambalo lilizinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Desemba 31, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi kompyuta mpakato Kiongozi wa Chama cha Msingi cha Umoja 2017, Omari Hassani Magoma baada ya kuzindua tawi la Benki hiyo la Ruangwa, Desemba 31, 2018. Kompyuta Mpakato 28 zilitolewa na Benki ya CRDB kwa Vyama vya Ushirika vya Msingi wilayani Ruangwa. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya CRDB, Ally Hussein Laay na watatu kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela. 
Kiongozi wa Chama cha Msingi cha Umoja 2017 wilayani Ruangwa, Omari Hassan Magoma akionyesha Kompyuta Mpakato aliyokabidhiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati Waziri Mkuu alipozindua tawi la Benki ya CRDB la Ruangwa, Desemba 31, 2018. Kompyuta mpakato 28 zilitolewa na Benki ya CRDB kwa vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) wilayani Ruangwa. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Hussein Laay na watatu kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela. 
Waalikwa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya kuzindua Tawi la Benki ya CRDB la Ruangwa, Desemba 31, 2018. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu 


*Asema litahamasisha ukuaji wa uchumi na wananchi watahifadhi fedha zao 

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amezindua tawi la benki ya CRDB wilayani Ruangwa na kuushukuru uongozi wa benki hiyo kwa kuwa tawi hilo litahamasisha ukuaji wa uchumi pamoja na kuwawezesha wananchi kujua umuhimu wa kuhifadhi fedha zao benki. 

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema ni vema kwa benki ya CRDB ikasogeza huduma hususan kwa wananchi waishio katika miji mikubwa iliyo mbali na makao makuu ya wilaya kwa kufungua ofisi za uwakala na kuwaondolea adha ya kutembea umbali mrefu. 

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatatu, Desemba 31, 2018) wakati akizungumza na wananchi wa wilaya ya Ruangwa mara baada ya kuzindua tawi la benki ya CRDB, ambapo ametumia fursa hiyo kuwahamisha wananchi kutumia benki kwa kuhifadhi fedha zao. 

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema kwa sasa benki hiyo inatakiwa itoe mikopo midogo, ya kati na mikubwa kulingana na uhitaji wa wajasiriamali ndani ya wilaya hiyo kwa sababu mikopo itawawezesha wananchi waweze kukuza mitaji na kujikwamua kiuchumi. Pia Waziri Mkuu ameipongeza benki ya CRDB kwa kumuunga mkono Rais Dkt. John Magufuli katika kuboresha maendeleo ya sekta mbalimbali zikiwemo za afya pamoja na elimu kupitia misaada mbalimbali inayotolewa na benki hiyo nchini. 

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema benki ya CRDB imekua na kupanua wigo wake wa kufikisha huduma kwa wateja na kuunga mkono sera ya Serikali ya kuhakikisha Watanzania wengi zaidi wanapata huduma za fedha. Alisema tawi hilo ni la sita katika ukanda wa Kusini mwa Tanzania, kwani tayari wanamatawi mengine manne ambayo ni Lindi mjini, Mtwara, Masasi, Tandahimba na tawi linayotembea katika Wilaya ya Newala. Pia wapo katika hatua za mwisho za ujenzi wa tawi Nachingwea. 

“Wilaya hii ya Ruangwa ni kiungo muhimu sana katika uchumi wa mkoa wa Lindi na Taifa kwa ujumla, hivyo uwepo wa mfumo rasmi wa kibenki, kupitia tawi hili la Benki ya CRDB, utasaidia sana kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi kwa kufungua fursa mpya.” 

Mkurugenzi huyo alisema CRDB wanajivunia utendaji mzuri wa tawi hilo, kwani katika kipindicha mwaka mmoja toka limeanza kazi, limeweza kupata matokeo makubwa ya kiutendaji ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa amana ambazo zimefikia kiasi cha shilingi bilioni 1.5. 

Pia jumla ya AMCOS 12 wanachama 4,600 zimejiunga na kufungua akaunti zao hivyo kuongeza usalama wa fedha zao. Pia jumla ya mikopo ya shilingi bilioni 1.2 imeshatolewa kwa wateja wa wilaya hiyo, ambapo shilingi milioni 409 zilitolewa katika kilimo cha korosho na ufuta, wakati shilingi milioni 790 zilitolewa kama mikopo kwa wafanyakazi na wafanyabiashara.

UHURU MEDIA GROUP YAWAPA MOTISHA WAFANYAKAZI WAKE WOTE

$
0
0
*Mkurugenzi Mtendaji Mkuu atangaza uhakiki wa wafanyakazi nchi nzima
*Azungumzia kuanza kufanya tafiti kubaini wasomaji,wasikilizaji wa vyombo vyao

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MKURUGENZI Mtendaji Mkuu wa Uhuru Media Group ambayo inasimamia vyombo vya habari vya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Faustine Sungura ameamua kuwapa motisha wafanyakazi wote wa kampuni hiyo kama sehemu ya kuthamini mchango wao.

Amesema motisha hiyo inakwenda sambamba na uhakiki wa wafanyakazi wote wa kampuni hiyo huku akielezea namna ambavyo amefurahishwa na utendaji kazi wa wafanyakazi wote na hasa katika kumuunga mkono Rais Dk.John Magufuli ambaye amefanya mambo makubwa kwa mwaka 2018.

Akizungumza leo ofisini kwake Sungura amesema Desemba 28 mwaka huu wa 2018 amekutana na wafanyakazi wote kwa kada mbalimbali na alitumia sehemu hiyo kuelezea mikakati ya kampuni hiyo ambayo imedhamiria kufanya mambo makubwa.

"Tulipokutana na wafanyakazi kuna mambo mengi ambayo tumeyazungumza.Pia nilitumia nafasi hiyo kuwashukuru kwa kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kazi nzuri anayofanya. Rais wetu amefanya mambo makubwa kwa mwaka huu yakiwamo ya kuboresha sekta ya anga, miundombinu kwa upanuzi wa barabara na ujenzi wa madaraja, umeme wa mto Rufiji ,ununuzi wa korosho, elimu bure na mambo mengine mengi ambayo yamefanyika.Hivyo wafanyakazi hawa wamekuwa wakiunga mkono kwa vitendo jitihada za Rais,"amefafanua.

Ameongeza wafanyakazi wa Uhuru Media Group kwa mwaka huu wa 2018 wamefanya kazi kwa bidii, hivyo ameamua kuwapongeza kwa kuwapa motisha kwani kesho ni Januari moja ni vema wakauanza mwaka vizuri."Kila mfanyakazi aliyeajiriwa na wasioajiriwa lakini wanafanya kazi kwenye vyombo vya habari vya chama tutawapa motisha hiyo.Tutafanya kwa walioko Dar es Salaam na wa mikoani," amesisitiza.

Aidha mbali ya kutoa motisha atatumia nafasi hiyo kufanya uhakiki wa wafanyakazi waliopo kwenye vyombo hivyo na iwapo kutakuwa na wafanyakazi hewa atawabaini."Nataka kumuona kila mfanyakazi uso kwa uso .Rais wetu aliamua kufanya uhakiki kwa watumishi wa Serikali ,nami namuunga mkono kwa kufanya uhakiki wa wafanyakazi wetu."amesema Sungura.

Amesema baada ya uhakiki wa majina ,hatua ya pili itakuwa ni uhakiki wa vyeti vyao vya kitaaluma na mwisho wa siku atatoa taarifa lakini ameeleza nia yake ni kuona wote ambao wanalipwa wawe ni wafanyakazi sahihi na wapo kwenye orodha yake.

Kuhusu mipango yao,amesema kuanzia mwakani wataanza kufanya utafiti utakaochukua muda wa miezi mitatu na lengo ni kufahamu wasomaji wao,wasikilizaji wao na watazamaji wao wanataka nini.Pia Februari mwaka 2019 watafanya 'uzinduzi laini' wa vyombo vyao na Aprili 2019 watafanya uzinduzi rasmi na hapo ndio watazungumza malengo na mikakati yao.

Amesema wanao mkakati wa kibiashara wa miaka minne na mkakati wa miaka 10 kwa ajili ya kulishika soko.Pia watajiimarisha kwenye mitandao ya kijamii ili kuhakikisha wanawafikia wasomaji wengi zaidi kwani utafiti unaonesha nusu ya watu wote duniani wanapata habari kutoka mtandaoni"Hivyo ili mambo yaende lazima mtandaoni nako tujiimarishe na mapema mwakani tutaweka nguvu kubwa katika eneo la mtandaoni kwa kuwa na timu maaluma," amesema.

Ametumia nafasi hiyo kuwatakia heri ya mwaka mpya wafanyakazi wote wa Uhuru Media Group huku akiwasisitiza waendelee kufanya kazi kwa bidii na kujituma kama ambavyo wamefanya mwaka 2018.
MKURUGENZI Mtendaji Mkuu wa Uhuru Media Group ambayo inasimamia vyombo vya habari vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Faustine Sungura akifafanua jambo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo kuwapa motisha wafanyakazi wote wa kampuni hiyo kama sehemu ya kuthamini mchango wao,aidha mbali ya kutoa motisha atatumia nafasi hiyo kufanya uhakiki wa wafanyakazi waliopo kwenye vyombo hivyo na iwapo kutakuwa na wafanyakazi hewa atawabaini.
MKURUGENZI Mtendaji Mkuu wa Uhuru Media Group Faustine Sungura akielezea mbele ya Waandishi wa habari leo Ofisini kwake jijini Dar,namna kampuni hiyo inavyojipanga ,amesema kuanzia mwakani wataanza kufanya utafiti utakaochukua muda wa miezi mitatu na lengo ni kufahamu wasomaji wao,wasikilizaji wao na watazamaji wao wanataka nini."Pia Februari mwaka 2019 tutafanya 'uzinduzi laini' wa vyombo vyetu na Aprili 2019 tutafanya uzinduzi rasmi,ambapo ndio tutazungumza malengo na mikakati yetu.",alifafanua Sungura.
MKURUGENZI Mtendaji Mkuu wa Uhuru Media Group Faustine Sungura akimkabidhi mmoja wa wafanyakazi kutoka Idara ya Utawala,Banga Lucas kiasi cha fedha ikiwa ni sehemu ya motisha iliyotolewa kwa wafanyakazi wote wa kampuni hiyo ikiwa kama sehemu ya kuthamini mchango wao.Picha na Michuzi Jr-MMG.

Shonza: Wasanii Jiungeni na Mfuko wa TAGOANE kujikwamua Kiuchumi

$
0
0
Na Anitha Jonas, WHUSM, Arusha

Naibu  Waziri  Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza ametoa wito kwa  wasanii kujitokeza na kujiunga na Mfuko wa Mkopo wa TAGOANE LOAN FUND.

Mheshimiwa Shonza ametoa wito huo leo Jijini Arusha  alipokuwa akizindua Mfuko Mkopo wa TAGOANE  LOAN  FUND katika Tamasha la Tukuza Festival  lililoandaliwa na Tanzania Gospel Artists Network (TAGOANE).

 “Tumekuwa tukishuhudia wasanii wengi wenye majina makubwa wakikosa fedha hata za matibabu  hili limekuwa ni suala lisilo pendeza hivyo ni vyema wasanii mkajiunga katika mfuko huu ambao utawasadia kupata mikopo yenye riba nafau na bima ya afya kupitia hili mnaweza kujikwamua kiuchumi  na kujifunza kuwekeza kwa maisha ya baadae ,“alisema Mhe.Shonza.

Kwa Upande wa Rais wa TAGOANE  Dkt.Godfrey Maimu alifafanua kwamba mfuko huo haubagui msanii kwani  msanii yeyote anayetaka kujiunga anaruhusiwa  kwani lengo la mfuko huo ni kuimarisha umoja wa wasanii na kuhakikisha maisha ya msanii yanaenda kubadilika badala ya msanii kuonekana ni mtu tegemezi  na wakuomba kusaidiwa hata kwenda studio kurekodi.
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza  akitoa wito kwa wasanii wote nchini kujiunga na Mfuko wa Mkopo wa TAGOANE (TAGOANE LOAN FUND) unaoratibiwa na Taasisi ya Tanzania Gospel Artists Network (TAGOANE) leo Jijini Arusha, alipokuwa akizindua mfuko huo ambapo amesisitiza kuwa  wasanii wa makundi yote wanaweza  kujiunga.
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza  aliyejifunika mgorori mwekundu wa kimasai akicheza na wanakwaya wa jamii ya Kimasai kutoka kanisa la KKKT Meserani  alipowasili kuzindua Mfuko wa Mkopo  unaoratibiwa na TAGOANE  (TAGOANE LOAN FUND) leo Jijini Arusha.
 Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza  (aliyeketi watatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa taasisi ya Tanzania Gospel Artists Network (TAGOANE) mara baada ya kuzindua Mfuko wa Mkopo wa TAGOANE (TAGOANE LOAN FUND) unaoratibiwa na taasisi ya Tanzania Gospel Artists Network (TAGOANE) leo Jijini Arusha,(aliyeketi wapili  kulia) ni Rais wa Tanzania Gospel Artists Network (TAGOANE) Dkt. Godfrey Maimu.
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo  Mhe. Juliana Shonza  (nyuma wapili kushoto) akicheza wimbo  Hapa Kazi Tu  uliyokuwa unaimbwa na Msanii Isack Chalo leo Jijini Arusha,mara baada ya uzinduzi wa  wa Mfuko wa Mkopo wa TAGOANE (TAGOANE LOAN FUND). 

ASKARI ALIYENUSURIKA KUUAWA NA MAJAMBAZI APANDISHWA CHEO

$
0
0

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Jonathan Shanna akimvisha cheo Konstebo WP. 12415 Dominica Michael Nnko cheo kuwa Koplo kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro baada ya kujwatunukia vyeo hivyo.


NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA

MMOJA wa askari watano waliotunukiwa vyeo na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro, kutokana na utendaji wao amesema kuwa alinusurika kupigwa risasi na jambazi wakati wakijiandaa kuwakabili katika eneo la Nyegezi,jijini Mwanza.

Askari huyo WP 12415 Dominica Michael ambaye ametunukiwa cheo cha Koplo amesema wakati akizungumza na mtandao huu muda mfupi baada ya kuvishwa cheo hicho na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza Jonathan Shanna kwa niaba ya IGP Sirro.

Alisema kuwa Februari 2017, alinususurika kuuawa kwa kupigwa risasi baada ya kuwahiwa na jambazi lakini kwa ujasiri alitumia mbinu ya uaskari kuwahi kulala chini kabla jambazi huyo kufariki kwa kupigwa risasi na askari wenzake.

Koplo Michael alieleza kuwa usiku wa siku ya tukio hilo laambayo ilikuwa siku ya kuzaliwa kwake, walipangwa kuwakabili majambazi huko Nyegezi, kumbe eneo walikopangwa aliwahiwa na jambazi mmoja bila kumuona ambaye alimlenga kwa bunduki .

“Kwanza nashukuru kwa kupata cheo hiki ambacho sikukitarajia ambacho kinatokana na viongozi kutambua mchango wangu katika kulinda usalama wa raia na mali zao.Maishani mwangu sitasahau tukio la Februari 19, 2017 ambayo ilikuwa siku ya kuzaliwa kwangu nilinusurika kuuawa nikiwa kazini,” alisema Koplo Michael na kuongeza;

“Tukiwa katika mapambano na majambazi nilipagwa kwenye eneo tulikokuwa mmoja wa majambazi aliniwahi akitaka kunipa kwa risasi, kwa ujasiri, ukakamavu na mbinu za uaskari niliwahi kulala chini hivyo akanikosa kabla ya kuuawa na askari wenzangu.”

Alidai kuwa licha ya changamoto ya kufanya kazi ya kupambana na wahalifu katika miundombnu isiyo rafiki cheo hicho kimemuongezea, ujasiri, ukakamavu na kujituma kwa bidii kwenye utendaji wake na ushirikiano na wenzake.

Askari mwingine ambaye alishiriki kuokoa majeruhi wa ajali ya kuzama kwa kivuko cha MV. Nyerere Amon John alitunukiwa cheo cha Meja kutoka Sajenti Meja na kusema kuwa kwenye ajali hiyo alifanya kazi ya uokoaji kwa siku tatu bila kula usiku na mchana.

Aidha, Mrakibu Msaidizi wa Polisi Levina Jeremiah ambaye naye alipandishwa cheo na Rais John Magufuli kutoka Mkaguzi Msaidizi alisema atakitendea haki cheo hicho ili kumwonyesha Rais na viongozi wake kuwa hawakukosea.

Askari huyo ambaye alikuwa masomoni kwenye mafunzo ya uongozi jijini Dar es Salaam alikuwa miongoni mwa askari maofisa 10 bora kati ya 515 na kutunukiwa cheti cha heshima kutokana na kufanya vizuri kwenye masomo ya darasani,nje na nidhamu.

Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela amewakabidhi vyeti na kuwazawadia askari waliopata vyeo sh.200,000 kila mmoja na ofisa mmoja sh. 300,000 kutokana na utendaji wao wa weledi uliouletea sifa mkoa huo.

Akizungumza na maaskari baada ya kuwakabidhi vyeti Ofisa mmoja wa polisi na askari wengine watano Mongela alisema wananchi wanafanya shughuli za maendeleo kutokana na usalama wa uliopo mkoani humu kwa sababu askari polisi wanafanya kazi kwa weledi.

Alisema weledi huo umedhihirika baada ya askari waliokuwa mafunzoni kuwa miongoni mwa askari weledi lakini pia waliotimiza majukkumu yao kwa kupambana na kufanikiwa kuwauwa majambazi saba na kuokoa silaha sita kutoka mikononi mwa majambazi hao.

“Kama ilivyo kauli mbiu yenu ya Tenda kwa Weledi hakuna bla blaa Hapa Kazi Tu! Mwanza hakuna unyanyasaji na uonevu, kazi zinafanyika na najivunia sana utendaji wenye weledi unaofanywa na polisi na mkoa unabebwa na sifa hiyo,”alisema Mongela.

Alieleza kuwa wakati mwaka unaelekea mwishoni Mwanza ilikuwa salama licha ya matukio kadhaa yaliyotaka kuchafua taswira yake lakini kwa weledi wa hali ya juu yalidhibitiwa na hivyo anaamini wananchi watasherehekea salama mwaka mpya kwa amani na utulivu.

Hata hivyo alionya watu wenye tabia ya uhalifu wanaodhani kuwa muda wa kusherehekea mwaka mpya ndio muda wa kutimiza malengo yao wasithubutu kwani watadhibitiwa na watakaojaribu wasije kulaumu baadaye.

Pia aliwataka wananchi kuwa wazalendo na walinzi wa maeneo yao kwa kuwa ndio walinzi wa kwanza na kuahidi kuwapa zawadi ya fedha askari walipata vyeo mbali na zawadi y ash. 200,000 na 500, 000 walizopewa awali.

DC Uyui Aja na Mikakati ya Kuwakwamua Wananchi Kiuchumi

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora Mhe. Gift Isaya Msuya amesema kuwa Wilaya hiyo imejipanga kutekeleza miradi ya kimkakati itakayosaidia kuwakwamua wananchi kiuchumi katika kipindi cha mwaka 2019. 

Akizungumza katika mahojiano maalum amesema kuwa miradi hiyo itajikita katika sekta za Kilimo, Ufugaji, Elimu, Afya ambapo itawawezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika kukuza uchumi na kujiletea maendeleo . 

“ Tumelenga kujenga Mabwawa kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji kwa kuwa Wilaya yetu ina ardhi yenye rutuba na wananchi wanao uwezo mkubwa wa kushiriki katika uzalishaji kupitia sekta hii ndio maana tumeamua kuweka mikakati ya kukuza uzalishaji na kuchochea ujenzi wa uchumi wa viwanda”. Alisisitiza Mhe. Msuya 

Akifafanua amesema kuwa kilimo cha umwagiliaji kitasaidia kuongeza uzalishaji wa mpunga pamoja na mazao mengine ya biashara yatakayochochea ustawi wa wananchi na kukuza uchumi kwa ujumla. 

Akizungumzia huduma za afya amesema kuwa Wilaya hiyo imepokea shilingi Bilioni moja na nusu kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya hiyo na tayari maandalizi ya ujenzi yameanza ambapo mradi huo utakapokamilika utakuwa ukombozi mkubwa kwa wananchi wa Wilaya hiyo na maeneo ya jirani. 

Alitaja miradi mingine inayotekelezwa katika Wilaya hiyo kuwa ni pamoja na ujenzi wa kituo cha Afya katika jimbo la Igalula kilichogharimu milioni 400 ambapo ujenzi wake uko katika hatua za mwisho kukamilika ili wananchi waanze kupata huduma. 

Kwa upande wa kituo cha Afya Utege kilichopo jimbo la Tabora Kaskazini Mhe. Msuya amebainisha kuwa kimekamilika na kuanza kutoa huduma kwa wananchi wa eneo hilo hali inayoonesha dhamira safi ya Serikali kuleta ustawi kwa wananchi kwa kuboresha huduma za afya. 

“ Upatikanaji wa dawa katika Wilaya yetu kwa sasa umefikia asimilia 95 hivyo nachukua fursa hii kumpongeza Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwajali wananchi wanyonge kupitia huduma hizi muhimu zinazolenga kuleta ustawi kwa wananchi na Taifa kwa ujumla”. Alisisitiza Msuya. 

Akisisitiza kuhusu maendeleo katika Wilaya hiyo Msuya amesema kuwa Wilaya hiyo imejipanga kuhakikisha kuwa miradi yote iliyopangwa inakamilika kwa wakati ikiwemo ujenzi wa Hospitali ya Wilaya, miradi ya maji iliyokwama kwa muda mrefu ili kuongeza kasi ya maendeleo . 

Eneo jingine litakalopewa kipaumbe katika sekta ya elimu ni ujenzi wa mabweni katika Kata 15 Wilayani humo ili kuchochea maendeleo ya sekta ya elimu kwa kuwajengea wasichana mazingira rafiki katika shule wanazosoma  hali itakayochangia ukuaji wa kiwango cha elimu kupitia kampeni ya ” Nishike Mkono Kuboresha Elimu Uyui” iliyoanzishwa na mkuu wa Wilaya hiyo mara baada ya kuteuliwa. 

Kata zitakazonufaika na ujenzi wa mabweni ni ; Magiri, Igalula, Gaweko, Tura, Usagari, Ilolangulu, Mabama, Kizengi, Lutende, Shitage, Loya, Upuge, Ikongolo na Makazi. 

Pia aliwaomba wadau mbalimbali kujitokeza kuchangia katika kampeni ya ”Nishike Mkono Kuboresha Elimu Uyui” ili kuchangia katika kuinua kiwango cha elimu katika Wilaya hiyo kwa kujenga mazingira rafiki kwa watoto wa kike kupitia ujenzi wa mabweni hayo. 

“Miradi mingine inayotarajiwa kutekelezwa mwaka 2019 ni pamoja na ujenzi wa stendi mpya na eneo la maegesho ya magari makubwa”. Alisisitiza Mhe Msuya. Alitaja baadhi ya faida za miradi hiyo kuwa ni pamoja na kuchangia katika kukuza uchumi wa Wilaya hiyo kwa kuzalisha ajira. 

Aidha; Mhe Msuya alipongeza utaratibu wa kuwapatia Wajasiriamali wadogo maarufu kama wamachinga vitambulisho maalum vinavyowawezesha kutekeleza majukumu yao bila kubugudhiwa na pia kuchangia katika ujenzi wa uchumi. 

Wilaya ya Uyui ni moja ya Wilaya za mkoa wa Tabora ambayo ina ardhi yenye rutuba, misitu na inatarajia kuwainua wananchi wake kiuchumi kupitia mikakati mbalimbali iliyowekwa na Mkuu wa Wilaya hiyo kwa kushirikiana na Watendaji wengine ikilenga kuchochea maendeleo.

BODI YA MAABARA BINAFSI YACHARUKA

$
0
0



Mkurugenzi wa Tiba, Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima akisisitiza jambo katika mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa sheria ya umiliki wa maabara binafsi za Afya.
GW2
Kaimu Msajili wa Bodi ya Maabara Binafsi za Afya akijibu maswali ya Waandishi wa habari wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari uliohusu utekelezaji wa sheria ya umiliki wa maabara binafsi za Afya.
GW3
Wajumbe wa Sekretariet ya Maabara binafsi pamoja na kamati ya Afya ya msingi za manispaa za jiji la Dar es salaam wakifuatilia maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Tiba, Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima kuhusu utekelezaji wa sheria ya umiliki wa maabara binafsi za Afya katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam.
…………………………………………………………………………

 Dkt. Dorothy Gwajima, Mkurugenzi wa Tiba wa WAMJW ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Maabara Binafsi za Afya (Private Health Laboratory Board) (PHLB). amewatakia heri ya mwaka mpya 2019 na hongera wamiliki wa maabara binafsi za afya kwa kazi kubwa waliyofanya mwaka 2018 ya kushirikiana bega kwa bega na sekta ya afya katika kuhakikisha taarifa sahihi zinawafikia wananchi na wadau wote kokote waliko.
Katika kufikisha salaam zangu kwa wamiliki wa maabara binafsi, amewashukuru wamiliki hawa kwa kuchagua kuwekeza katika sekta ya afya nchini Tanzania, na kuwapongeza wale wote waliowekeza huku wakihakikisha wanafuata taratibu zote za kisheria za uwekezaji huo.

Aidha, amewakumbusha wamiliki wa maabara binafsi kuwa, umiliki huu unasimamiwa na sheria namba 10 ya mwaka 1997 inayowataka wamiliki wote kusajiliwa na kutambuliwa na PHLB kisheria. Hii ni hata kama maabara husika inajitegemea au iko ndani ya kituo cha kutolea huduma za tiba cha aina yoyote cha ngazi yoyote ile, maabara husika inatakiwa itimize matakwa ya kisheria.
Amesema  kufikia Septemba, 2018 PHLB ilikuwa inazitambua jumla maabara 641 zinazojitegemea na 719 zilizoshikizwa kwenye vituo vya tiba vya watu binafsi vya ngazi mbalimbali.
 Katika utekelezaji wa majukumu yake, Bodi imeendelea kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa shughuli za maabara binafsi kama sheria inavyotaka, na kupitia utekelezaji huo imebaini wako baadhi ya wamiliki ambao, hawatimizi matakwa ya kisheria.

Kutotekeleza matakwa ya kisheria siyo tu kunaifanya maabara husika kuwa mbali na macho ya Bodi katika kuhakikisha usimamizi wa ubora wa huduma, bali kunamfanya mmiliki husika kukwepa wajibu wake wa msingi kwa serikali ikiwemo kulipa tozo na ada stahiki zitokanazo na biashara anayofanya na hii ni kukwamisha juhudi za Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo kulingana na mipango yake. Hili halikubaliki hata kidogo.
 Kanuni za kumiliki maabara binafsi zinataka mmiliki kutekeleza mambo makubwa yafuatayo;-
 1. Kufuata utaratibu wa kusajiliwa (kwa maabara zinazojitegemea) na kufuata utaratibu wa kujiandikisha na kutambuliwa na Bodi husika kwa maabara ambazo zimesajiliwa pamoja na vituo vya tiba (zilizoshikizwa).2. Kulipa ada stahiki kila mwaka ambazo ni ada ya uhakiki wa ubora wa huduma na ingine ni ada ya ukaguzi.

Kutokana na baadhi ya wamiliki wa maabara binafsi hususan zilizoshikizwa kutofuata maadili ya uwajibikaji kisheria, bodi imebaini kuwa, kufikia Septemba 2018, kati ya vituo vya tiba 1731 vya watu binafsi vyenye maabara ndani ni maabara 1012 (58%) tu ndiyo zilikuwa zimetimiza wajibu wake wa kujiandikisha kwenye Bodi ya Usimamizi wa Maabara Binafsi na kutekeleza matakwa yote ya kisheria kama nilivyoeleza hapo awali.

Ni kweli kwamba, vituo hivi vya maabara binafsi viko ndani ya vituo vya tiba ambavyo, vinasimamiwa na Sheria ya Usajili wa Vituo Binafsi (PHAB) lakini, hili haliondoi utekelezaji wa sheria ya PHLB yenye dhamana ya kusimamia maabara binafsi. Wizara inakubalina na hoja kuwa, vema sheria hizi zikajumuishwa, na tayari imeanza kufanyia kazi na wadau wote wanafahamu na wameshiriki hivyo, hii haiwezi ikawa ndiyo sababu ya kutowajibika kutekeleza sheria halali ambazo bado ziko hai.

Wizara kupitia Bodi husika imeendelea kuelimisha na kufafanua juu ya mamlaka tofauti za sheria hizi mbili, lakini bado baadhi ya wamiliki wa maabara binafsi wamekuwa wakikwepa tu kuwajibika kwa makusudi.

Aidha, leo hii, watendaji wa sekretarieti ya bodi ya PHLB kwa kushirikiana na sekretarieti ya PHAB na viongozi wa sekta ya afya ngazi zote wakiwemo OR TAMISEMI, Ofisi za Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya mbalimbali, tumehitimisha ziara ya kufuatilia utekelezaji wa shughuli za maabara binafsi za afya katika mikoa mbalimbali ukiwemo mkoa wa Dar es Salaam.

Kupitia ziara hii, tumechambua na kubaini kuwa, wamiliki wengi wasiotekeleza sheria ya umiliki wa maabara binafsi wanatokea miongoni mwa wanaomiliki maabara zilizoshikizwa yaani, zilizomo ndani ya vituo vya tiba ngazi mbalimbali. Aidha, katika kundi hili, wapo watu ambao, kimsingi huwezi kuwatarajia kutokana na elimu zao, kazi zao na Imani zao kwa jamii inayowazunguka (wao wanajijua). Hii haivumiliki kabisa.

Kwa kuwa nilikuwa mstari wa mbele kuwafikia wale wamiliki wa maabara binafsi walioripotiwa kuwa eti wameshindikana, nimewafikia baadhi yao na kusikiliza hoja zao na kubaini kuwa, hazina mashiko kabisa. Eti, hoja yao ya msingi ni kuwa, wanapolipa kusajili kituo cha tiba huwa wanadhani kuwa, tayari na maabara imejumuishwa humo. Utetezi huu siyo wa kweli kwa kuwa, sheria ya kusimamia umiliki wa vituo binafsi vya tiba iko wazi na ina bodi yake na hii ya kusimamia umiliki wa maabara binafsi nayo iko wazi na ina bodi yake na siku zote wamekuwa wakielimishwa na mimi nimeshiriki mara nyingi kutoa elimu hiyo.

Nimeona leo nirudie tena kufafanua kuwa, bodi ya usajili wa vituo vya Tiba inajukumu lake na haiingiliani kabisa na sheria ya bodi ya usimamizi wa kumiliki maabara binafsi.
 Kwa kuwa wako wamiliki wa maabara binafsi ambao, wameamua kuamini kwenye kufuatiliwa kila siku, sasa ufuatiliaji na uelimishaji uliokwisha fanyika awali unatosha, wakati wa kuelewa somo umepita sasa ni saa ya KAZI TU !. Imefika zamu ya wamiliki wa maabara binafsi waliokuwa hawajatekeleza wajibu wao wa kumiliki maabara hizo kisheria kuchukua hatua mara moja za kwenda kutimiza wajibu wao bila shurti tena pasipo kuendelea kuisababishia Serikali gharama za ziada za kuwafuatilia. 

Hivyo, ifikapo tarehe 15/1/2019 ambaye hajatimiza wajibu wake ni kwamba, atafungiwa bila taarifa ya ziada na kushtakiwa. Iwapo kuna ambaye anayejiandaa kutotimiza matakwa hayo, bora atumie muda huu kufunga ofisi yake kabisa ili kuepuka usumbufu usio wa lazima. Hata hivyo, kufunga ofisi hakutamuepusha mvunja sheria yeyote yule kuwajibika kwa uvunjifu wa sheria alioufanya awali.

Naomba ifahamike kuwa, kutimiza wajibu wa matakwa ya kisheria kwa wamiliki husika wa mabaara binafsi ni pamoja na;-1. Kila mmiliki kuhakikisha amekidhi vigezo vyote vya kumiliki maabara binafsi kama ambavyo amekuwa akielekezwa na wataalamu walioko kila halmashauri na mikoa husika, pamoja na2. Kuhakikisha amelipa ada na tozo stahiki zikiwemo malimbikizo ya nyuma na faini zote stahiki.
 3. Amepata risiti halali za malipo hayo4. Anaendelea kulipa tozo stahiki kila mwaka ili, kuwezesha bodi husika kutimiza wajibu wake wa kufanya uhakiki wa ubora wa huduma kwa kila kituo kila mwaka na kufanya ukaguzi maalumu wa vituo husika kama vinaendelea kuwa katika viwango stahiki kama siku vilipopewa kibali cha kutoa huduma husika.
Kwa kuwa tumebaini kuwa, wasiofuata sheria wanatoa huduma bubu mita chache tu toka serikali za mitaa, Bodi imeendelea kuimarisha ushirikiano wake na vyombo vyote vya Serikali ngazi zote kuanzia OR TAMISEMI na ngazi zake zote za Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na sasa, Bodi inaandaa orodha ya maabara binafsi nchi nzima na itaweka katika gazeti la Serikali na vyombo vya habari na itasambaza kwa wadau wote.

Hivyo, yeyote ambaye hayumo katika orodha hiyo asithubutu kutoa huduma hizo maana, mamlaka za Serikali za mitaa zitambaini na taarifa zitafika mahali sahihi mara moja na hatua kali zitachukuliwa.Aidha, natoa wito kwa mamlaka zote za Serikali ngazi zote tuendelee kupeana taarifa kwa haraka zaidi na kujipanga vema zaidi katika kuhakikisha hakuna mvunja sheria anathubutu kutoa huduma za kijamii bila kibali.

Ni matumaini yangu kuwa mtatumia umahiri wenu katika kuhakikisha ujumbe huu unawafikia wadau wote kwa usahihi. Aidha, nina Imani kuwa, wadau husika sasa wataacha utetezi dhaifu na watatimiza wajibu wao mara moja.Mwisho, naomba kuwakumbusha wadau wote sekta ya afya kuwa, katika kujenga taifa letu, ni budi kila mmoja atimize wajibu wake ili, tuongeze kasi, kwa kuwa hakuna mtazamaji bali wote tuna majukumu na wajibu kamili.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE JANUARI 1,2019


DC Chongolo, Msuya Waaga Mwaka 2018 kwa Kueleza Mafanikio ya Serikali

$
0
0
Na. Frank Mvungi

Wakuu wa Wilaya za Kinondoni, Daniel Chongolo na Wilaya ya Uyui, Gift Msuya kwa pamoja wamepongeza Juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano katika kipindi cha mwaka 2018 ambazo zilizolenga kuboresha huduma za jamii na kuinua maisha ya wananchi.

Akizungumza leo katika mahojiano maalum na Idara ya Habari-MAELEZO, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo, amesema kuwa katika kipindi cha mwaka 2018, wananchi wameshuhudia uboreshaji wa miundombinu ya barabara, madaraja, vituo vya afya, Elimu, ujenzi Reli ya kisasa, Zahanati na ujenzi wa Hospitali mpya za Wilaya zipatazo 67.

"Ujenzi wa reli ya kisasa kwa Kiwango cha Kimataifa (SGR) hapa nchini utawezesha kufungua sekta mbalimbali ikiwemo uchukuzi, kukuza biashara kati ya Tanzania na mataifa ya jirani, kufungua uwekezaji ambao utachochea kwa kiwango kikubwa kukuza uchumi na ustawi wa wananchi", ameeleza Chongolo.
Akifafanua kuwa katika Wilaya ya Kinondoni, barabara zenye urefu wa kilomita 58.2 zinaendelea kujengwa kwa kiwango cha lami na baadhi zimeshakamilika.

Ametaja miradi mingine kuwa ni ujenzi wa Hospitali ya Wilaya inayojengwa katika eneo la Mabwepande pamoja na ujenzi wa kituo cha afya Kigogo vitaimarisha na kusogeza karibu huduma za afya kwa wananchi wa maeneo hayo.Kwa upande wa maji katika Wilaya ya Kinondoni amebainisha kuwa upatikanaji wa maji unatarajiwa kufikia zaidi ya asilimia 90 kutokana na maboresho na uwekezaji ulifanyika katika miundombinu ya maji.

Akizungumzia Wilaya ya Longido ambayo amewahi kuwa Mkuu wa Wilaya, Chongolo amesema kuwa kabla ya Serikali ya Awamu ya Tano kuingia madarakani Wilaya hiyo ilikuwa na Kituo cha Afya kimoja lakini hivi sasa vimejengwa vituo vya afya vinne vilivyojengwa katika Kata za Kitumbeine, Namanga, Engarenaibor na Olmoti.

Alibainisha kuwa upatikanaji wa huduma ya maji Wilayani humo unatarajiwa kufikia asilimia 130 kutokana na uwekezaji uliofanywa na Serikali katika sekta ya maji.Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mhe. Gift Isaya Msuya, ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kutoa Shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya Wilaya ambapo tayari maandalizi ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa na wa kihistoria yameanza.

Akizungumzia mikakati yakuwawezesha wananchi katika Wilaya hiyo, Msuya amesema tayari Serikali imeendelea kuwajengea mazingira wezeshi wananchi wa Uyui na mkoa wa Tabora kwa kuimarisha usafiri wa anga ambapo ndege za ATCL zimekuwa zikifanya safari za mara kwa mara mkoani Tabora jambo linalochochea maendeleo na ustawi wa wananchi kwa kufungua fursa za kukuza uchumi.

Ametaja miradi mikubwa inayoendelea kutekelezwa nchini wa kufua umeme kutoka Mto Rufiji, Barabara, madaraja, vivuko, na ujenzi na upanuzi wa viwanja vya ndege katika mikoa mbalimbali hapa nchini kuwa ni mafanikio makubwa kwa ujenzi wa uchumi na utoaji huduma bora kwa wananchi.

Aidha, amepongeza hatua ya Mhe. Rais kuwatambua wajasiriamali wadogo maarufu kama wamachinga kwa kuwapatia vitambulisho maalum vinavyowawezeshakufanya biashara bila kubugudhiwa hali itakayowainua kiuchumi na kuongeza wigo wa ukusanyaji wa mapato.

Wakuu hao wa Wilaya wameeleza kuwa kuwa katika mwaka 2019 wanatarajia kuendelea kutekeleza ahadi za Serikali ili kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi ikiwemo kuweka mazingira bora ya uwezeshaji kuichumi na utoaji wa huduma za jamii.

Ujenzi wa Kituo cha Afya Hamai wamchefua Jafo

$
0
0
Waziri wa Ncho Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo(katikati) akiwasili katika kituo cha Afya Hamai kukagua miundombinu ya afya inayoendelea kujengwa katika kituo hicho kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe. Simon Odunga na kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe. Mweshimiwa Rajabu.
Waziri wa Ncho Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akitoa maelekezo baada ya kukagua miundombinu ya afya katika kituo cha Afya Hamai, Chemba
Waziri wa Ncho Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akitoa maelekezo wakati wa kukagua miundombinu ya afya katika kituo cha Afya Hamai, Chemba
Mbunge wa Chemba Mhe. Juma Nkamia akizungumza wakati wa ziara ya kukagua miundombinu ya afya iliyofanywa na Waziri wa TAMISEMI Wilayani humo.


Nteghenjwa Hosseah, Chemba

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Selemani Jafo amechukizwa na kusuasua kwa ujenzi wa kituo cha Afya Hamai kilichopo katika Wilaya ya Chemba ambacho hakijakamilika ujenzi wa miundombinu ya Afya ilihali fedha za ujenzi zikiwa zimefikishwa kituoni hapo miezi kumi iliyopita.

Mhe. Jafo ameonyesha kuchukizwa kwake wakati wa ziara ya kukagua miradi ya Afya inayoendelea kujengwa katika Halmashauri hiyo mapema leo hii. Akizungumza katika ziara hiyo Mhe. Jafo amesema Kituo cha Hamai kimepokea fedha tangu Januari 2018 lakin mpaka sasa ujenzi haujakamilika wakati vituo vingine vyenye mazingira magumu zaidi vimekwishakamilisha ujenzi tena kwa ubora wa hali ya juu.

Mhe Jafo aliongeza kuwa fedha zilizoletwa hapa ni sh milioni 400 nimeambiwa kuwa zimekwishatumika zote na inahitajika tsh mil 29 zaidi ili kukamilisha majengo haya; Nashindwa kuelewa ni kitu gani cha gharama kilichowekwa katika kituo hiki ambacho kimepelekea fedha hizo kwisha kabla ya ujenzi kukamilika. “Inakuwaje halmashauri zingine wametumia kiasi hicho cha fedha kukamilisha miundombinu yao lakini kwa chemba fedha hizo zisitoshe kukamilisha kituo kuna tatizo gani hapa” alihoji Jafo

Hakuna fedha itakayoongezwa katika kituo hiki cha Hamai nataka majengo yote yaliyojengwa hapa yakamilike haraka iwezekenavyo na kwa ubora unaotakiwa bila kuwa na sababu zingine zozote mkatafute fedha popote mkamilishe kituo hiki aliongeza Jafo. Akizungumza na wananchi wa Hamai Mhe. Jafo aliwajulisha kuwa Halmashauri ya Chemba ni miongoni mwa Halmashauri zilizopata fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya Afya vitatu na Hospital ya Wilaya kwa hiyo hatavumilia kuona fedha hizo zikitumika vibaya atasimamia sharia na atakayekwenda kinyume na maelekezo atachkuliwa hatua kali.

Sambamba na kumuagiza Mkurugenzi kutaftua fedha za kukamilisha ujenzi huo Waziri Jafo ametoa muda wa wiki mbili kukamilisha ujenzi huo na ameahidi kurejea tena Hamai mnapo Januri 15,2019 kuja kukagua maendeleo ya ujenzi huo. Naye Mbunge wa Chemba Mhe. Juma Nkamia amesema kuwa kumekua na kusuasua kwa ujenzi wa kituo cha Afya Hamai umetokana na ujanja ujanja wa baadhi ya watumishi kutaka kufanya vitu wenyewe bila kushirikisha kamati za ujenzi na mara nyingi wanaposhauriwa hawakutaka kusikiliza ushauri huo ndio baadhi ya sababu zilizochangia kutokamilika kwa ujenzi huo kwa wakati.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chemba Dkt. Semistatus Mashimba amesema changamoto zilizojitokeza katika ujenzi wa kituo cha Afya Hamai zimetokana na uhaba wa watumishi hususan katika idara ya ujenzi na manunuzi ndio ndio muhimu katika kusimamia shughuli zote za ujenzi wa vituo vya Afya.

Vituo vya Afya vilivyopokea fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya Afya katika Wilaya ya Chemba ni vitatu ambavyo ni Hamai, Mrijo na Kwamkoro ambapo kila kimoja kimepata sh mil 400 huku hospital ya Wilaya ikipatiwa kiasi cha sh Bil 1.5.

WAZIRI LUGOLA KUANZA ZIARA NDEFU MKOANI KAGERA KESHO, AWATAKA WANANCHI KUMLETEA KERO KATIKA MIKUTANO YAKE YA HADHARA

$
0
0
Na Felix Mwagara, MOHA-Bukoba. 

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewasili mjini Bukoba Mkoani Kagera leo, kwa ajili ya kuanza ziara yake ya kikazi ya siku nane kwa kutembelea Wilaya zote za Mkoa huo akisikiliza kero za wananchi pamoja na kufuatilia maagizo yake aliyoyatoa kwa vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo ndani ya Wizara yake. 

Waziri Lugola anatarajia kuanza ziara hiyo rasmi kesho Januari 2, 2019 mjini Bukoba kwa kukutana na Mkuu wa Mkoa pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na kupokea taarifa ya Kamati hiyo, kabla ya kuanza kuzungumza na Wakuu wa vyombo vyake na baadaye kuzungumza na Baraza la Askari na Watumishi wote wa Wizara hiyo waliopo mjini humo. 

Akizungumza na Mwandishi wa habari hii, leo, Lugola amesema baada ya kuzungumza na Askari na Watumishi wa Wizara yake pamoja na kupokea changamoto zao, atafanya mkutano mkubwa wa hadhara wa wananchi utakaofanyika uwanja wa uhuru mjini humo ili aweze kusikiliza na kuzitatua kero mbalimbali zinazowakabili. 

“Nitafanya mkutano mkubwa wa hadhara utakaofanyika Uwanja wa Uhuru eneo la Mayunga hapa mjini Bukoba, ambapo utaanza saa 10:00 hadi 12:00 jioni, hivyo nawaomba wananchi wa mji huu wajitokeze kwa wingi kunisikiliza kile ambacho nimepanga kuwaambia na pia nitawapa nafasi wananchi waulize maswali bila woga, waniambie kero zao nami nitazitatua katika mkutano huo,” alisema Lugola. 

Pia Lugola alisema lengo la ziara hiyo ni kufuatilia maagizo yake mbalimbali ambayo aliyatoa mwaka jana 2018 katika mikutano yake kama yalifanyiwa kazi na viongozi wa Taasisi anazoziongoza au yalipuuzwa, yakiwemo ya dhamana zitolewe saa 24 katika vituo vyote vya polisi nchini, na pia kupiga marufuku tabia ya baadhi ya Polisi kubambikizia kesi wananchi, na pamoja na agizo la pikipiki zote zilizopo vituoni ziondolewe. 

Lugola alisema katika ziara yake aliyoifanya mwaka jana Mkoani Kigoma aligundua wananchi wanakabiliwa na changamoto mbalimbali hivyo hawezi kulala akiwa ofisini, lazima afanye ziara nchi nzima kuwasaidia wananchi kutatua kero zao ambapo wengi wao wakiwalalamikia Polisi wakiwaonea. 

Waziri Lugola ameongeza kuwa, kupitia mikutano yake ya wananchi mkoani Kigoma ndipo ameamua kufanya ziara ya pili kwa kuutembelea Mkoa wa Kagera ambao changamoto zake zinafanana kwa sehemu kubwa kwa kuwa mikoa hiyo ni ya mipakani na changamoto kubwa ni uwepo wa wahamiaji haramu pamoja na matukio kadhaa ya ujambazi ambayo kwa kiasi kikubwa Serikali inaendelea kuyadhibiti. 

“Wananchi wanapojitokeza kwa wingi inasaidia kusikiliza matatizo yao yanayowakabili, ndio mana nimepanga kufanya ziara kama hizi nchi nzima, hii inasaidia sana kujua matatizo mbalimbali ya wananchi pamoja na kuangalia utendaji kazi wa Taasisi zangu zilizopo ndani ya Wizara hii, na hakika Serikali ya Dokta Magufuli inawajali wananchi wake ndio mana inawafuata mahali walipo, ili wazungumze na Serikali yao uso kwa uso,” Alisema Lugola. 

Waziri Lugola baada ya kumaliza ziara yake mjini Bukoba, ataenda Wilaya za Misenyi, Karagwe, Kyerwa, Ngara, Biharamulo na Januari 8, 2019 atamalizia ziara yake Wilaya ya Muleba ambapo katika Wilaya hizo pia atazungumza na wananchi pamoja na watumishi waliopo ndani ya Wizara yake ambao ni Jeshi la Polisi, Idara ya Uhamiaji, Jeshi la Magereza, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, pamoja na Idara ya Probesheni ambayo jukumu lake kuu ni kupunguza msongamano gerezani na kusimamia wafungwa waliopewa adhabu mbadala na Mahakama au wafungwa waliopata msamaha kupitia sheria ya huduma kwa jamii na kutumikia kifungo chao nje ya Gereza.

NHIF YAKUTANA NA VIONGOZI WA VYAMA VYA USHIRIKA TUNDURU

$
0
0
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF)mkoa wa Ruvuma,umekutana na wanachama na viongozi wa vyama viwili vya msingi vya ushirika vinavyojihusisha na kilimo cha zao la korosho katika wilaya ya Tunduru.

Lengo ni kuhamasisha wanachama na viongozi wa vyama hivyo kujiunga na mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa ajili ya kupata huduma za matibabu pindi wanapoumwa kwa kuwa shughuli za kilimo zinahitaji mtu mwenye afya njema ambayo itamruhusu kuendelea na majukumu yake katika kipindi cha msimu wa kilimo.

Wanachama hao ni kutoka vyama vya Naluwale na Mumsasichema kata ya Muhwesi ambayo ni maarufu kwa uzalishaji mkubwa wa korosho wilayani hapa.Akizungumza na Wanachama hao kaimu Meneja wa mfuko huo Antony Mgima alisema, mpango huo unalenga kutoa huduma kwa mwanachi mmoja kwa gharama ya shilingi 78,600 ambapo mwanachama atapata fursa ya kuhudumiwa kuanzia ngazi ya zahanati,kituo cha Afya na Hospitali zote Nchini.

Alisema, mpango huu wa sasa utasaidia sana kila mmoja kunufaika nao tofauti na hapo awali ambapo ni watumishi wa umma pekee yao ambayo walikuwa na sifa ya kuwepo katika mpango wa huduma za matibabu.

Kwa mujibu wake, mwanachama wa NHIF ana hiari ya kumlipia fedha kama michango kwa mtu yoyote ambaye anaona anastahili kuwemo katika mpango hasa ikizingatia kuwa, kwa sasa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umeboresha sana huduma zake .

Mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera,ameitaka NHIF kuhakikisha wanawashirikisha viongozi wa vijiji na kata katika kuhamasisha wananchi wengi zaidi ili nao waweze kujiunga na mfuko huo badala ya kulenga wanachama na viongozi wa vyama vya ushirika.

Alisema, hatua hiyo itasaidia sana kupata wananachi wengi kwani tabia ya wananchi wanataka kusikia kauli za viongozi wao wa serikali na sio vyama vya msingi kwa sababu baadhi ya viongozi wa vyama hivyo wanalalamikiwa sana kutokana na kuwaibia wakulima ambao ni wanachama wao.

“ni vema sasa mkaenda mbalki zaidi kufanya mikutano na wananchi wengine katika vijiji vyetu hasa kipindi hiki ambacho minada ya korosho inatarajia kuanza,ni lazima sisi sote tuwe na mkakati wa pamoja kutangaza huduma zinazotolewa na NHIF badala ya kuelekeza nguvu kubwa kwa wanachama wa vyama vya msingi vya ushirika”alisema Homera.

Hata hivyo, amewataka wakulima ambao ni wanachama wa vyama vya msingi vya ushirika kuchangamkia fursa ya kujiunga na NHIF kwa ajili ya kupata huduma ya matibabu hasa kwa kutambua kuwa,watu wenye Afya njema watakuwa na uwezo wa kushiriki kikamilifu katika shgughuli za uzalishaji mali.

Alisema, kutokana na changamoto kubwa ya matibabu kwa baadhi ya maeneo hapa Nchini,mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umeamua kuisaidia serikali katika kukabiliana na tatizo hilo na kuhaidi kuwa,serikali ya wilaya na NHIF kwa pamoja itahakikisha inapita viijini ili kuhamasisha watu wengi kujiunga na mfuko huo.

Baadhi ya wanachama wa vyama hivyo Hussen Namkuhule na Ali Mbemba wameuomba mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kuongeza idadi ya wategemezi ambao wataingizwa katika utaratibu wa uanachama na kupata matibabu badala ya kuwa na ukomo.

RAIS WA ZANZIBAR AFUNGUA SKULI YA MSINGI CHIMBA

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Dk. Ali Mohamed Shein, akiondoa kipazia kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Skuli ya Msingi ya Chimba, Shehia ya Chimba ikiwa katika shamrashamra za Sherehe za Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar,ufunguzi huo umefanyika leo 1-1-2019.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akikata utepe kuashiria kuizungua Skuli ya Msingi Chimba Shehia ya Chimba Wilaya ya Micheweni Pemba, uzinduzi huo umefanyika leo, 1-1-2019.(Picha na Ikulu)



RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akikagua moja ya Madarasa ya Mskuli ya Msingi Chimba Wilaya ya Micheweni Pemba Shehia ya Chimba, akiwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, baada ya uzinduzi wa Skuli hiyo uliofanyika leo.1-1-2019, ikiwa ni shamrashamra za sherehe za Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(Picha na Ikulu) 







RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwasili katika viwanja vya Skuli ya Msingi Chimba Wilaya ya Micheweni Pemba akiongozana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma, akielekea katika majengo ya Madarasa kwa ajili ya Uzinduzi wake ikiwa ni shamrashamra za Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(Picha na Ikulu)


BAADHI ya Wanafunzi wa Wilaya ya Micheweni Shehia ya Chimba, wakifuatilia hafla ya ufunguzi wa Skuli ya Msingi Chimba leo, ikiwa ni shamrashamra za Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(Picha na Ikulu)
WANAFUNZI Hairat Ali Omar na Rehema Haji Bakari wakisoma Utenzi wakati wa hafla ya ufunguzi wa Skuli ya Mshini ya Chimba Wilaya ya Micheweni Pemba, wakati wa sherehe za shamrashamra za Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(Picha na Ikulu)
WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma, akizungumza kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, kuzungumza na Wananchi wa Shehia ya Chimba Wilaya ya Michewni Kisiwani Pemba, .(Picha na Ikulu)
BAADHI ya Wananchi wa Shehia ya Chimba wakifuatilia Hutuba ya Ufunguzi wa Skuli ya Msingi Chimba, wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia hafla hiyo, ikiwa ni maadhimisho ya sherehe za shamrashamra za Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Wananchi wa Wilaya ya Micheweni Shehia ya Chimba, wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Skuli ya Msingi ya Chimba, ikiwa ni shamrashamra za Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Skuli hiyo leo.1-1-2019.(Picha na Ikulu)
WAZEE wa Shehia ya Chimba Wilaya Micheweni Kisiwani Pemba wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, wakati akiwahutubia Wananchi katika sherehe za shamrashamra za Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(Picha na Ikulu

MAJALIWA ASHIRIKI KATIKA DUA YA KUMSHUKURU MUNGU MKESHA WA MWAKA MPYA

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na ndugu, jamaa na marafiki waliofika nyumbani kwake katika kijiji cha Namahema wilayani Ruangwa , mkesha wa mwaka mpya kushiriki katika Dua ya kumshukuru Mungu kwa kuwajalia watanzania na viongozi wao kuumaliza salama mwaka 2018 na kumuomba Mungu aendelee kulilinda taifa letu na viongozi wake kwa mwaka 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki waliofika nyumbani kwake katika kijiji cha Namahema wilayani Ruangwa mkesha wa mwaka mpya, kushiriki katika Dua ya kumshukuru Mungu kwa kuwajalia watanzania na viongozi wao kuumaliza salama mwaka 2018 na kumuomba aendelee kulilinda taifa letu na viongozi wake kwa mwaka 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama saa wakati alipojumuika na ndugu, jamaa na marafiki waliofika nyumbani kwake katika kijiji cha Namahema wilayani Ruangwa mkesha wa mwaka mpya kushiriki katika Dua ya kumshukuru Mungu kwa kuwajalia watanzania na viongozi wao kuumaliza salama mwaka 2018 na kumuomba Mungu aendelee kulilinda taifa letu na viongozi wake kwa mwaka 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na ndugu, jamaa na marafiki waliofika nyumbani kwake katika kijiji cha Namahema wilayani Ruangwa , mkesha wa mwaka mpya kushiriki katika Dua ya kumshukuru Mungu kwa kuwajalia watanzania na viongozi wao kuumaliza salama mwaka 2018 na kumuomba Mungu aendelee kulilinda taifa letu na viongozi wake kwa mwaka 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAKAZI DISUNYARA WATUMIA SH. 4,000 KUFUATA VIPIMO IKIWEMO CHA MALARIA UMBALI WA KM. 10 KWENDA NA KURUDI

$
0
0

Mbunge viti maalum mkoani Pwani, Subira Mgalu akizungumza wakati alipokwenda kutembelea zahanati ya Disunyara, huko Kibaha Vijijini. (picha na Mwamvua Mwinyi) .
.
NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA VIJIJINI 

ZAHANATI ya Disunyara, kata ya Kilangalanga Kibaha Vijijini, inakabiliwa na ukosefu wa maabara hali inayosababisha kufuata vipimo ikiwemo cha malaria na damu kituo cha afya Mlandizi ambako kuna umbali wa km kumi kwenda na kurudi na nauli ya pikipiki sh. 4,000.

Kutokana na hali hiyo wakazi wa eneo hilo wamejitolea kuanza ujenzi wa maabara ambapo mbunge wa viti maalum mkoani Pwani, Subira Mgalu amechangia mifuko 30 ya saruji . 
 
Akichangia mifuko hiyo,alisema vipimo ni suala muhimu ambalo inahitajika nguvu ya pamoja kumaliza ujenzi huo. “Baada ya kusikia wananchi wameanza juhudi hizo ndipo nilipoguswa kuwaunga mkono ili kuendelea na ujenzi,alielezea Subira. 

Nae diwani wa kata hiyo, Mwajuma Denge alisema wananchi wanapata shida kufuata huduma ya vipimo umbali mrefu. Aliwaomba wadau kuendelea kujitokeza kuchangia ili kumaliza ujenzi huo waweze kupata japo vipimo vya awali karibu. Kwa upande wake mganga mfawidhi wa zahanati ya Disunyara ,Maimuna Yusuph alitaja tatizo la ukosefu wa chumba cha maabara kunasababisha akinamama wajawazito kwenda Mlandizi kufuata vipimo na wakati mwingine hushindwa kutokana na ukosefu wa nauli. 

Tatizo jingine ni vitanda vya kuzalia kwani kilichopo ni kimoja, kingine kibovu hivyo mahitaji ni vitanda vingine viwili ili kukidhi mahitaji. Mkazi wa Disunyara Mwajuma Juma alimshukuru Subira kwa kuwashika mkono ili kumkomboa mwanamke. Alisema endapo maabara hiyo ikikamilika itasaidia wakazi wenye mahitaji ya vipimo hasa akinamama na watoto.

DKT. BASHIRU - WAWEKEZAJI WA KIUCHUMI WEKEZENI UCHUMI WA KIMATAIFA, NA WAKISASA.

$
0
0
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi –Taifa ameendelea na Ziara yake ya Kikazi Mkoani Kagera Januari Mosi, 2019 kwa kutembelea Kiwanda cha Kusindika Kahawa cha TANICA kilichopo Bukoba Manispaa, Mkoani kagera na kuagiza Uongozi wa Kiwanda hicho kutafuta Masoko ya Kimataifa ikiwemo Nchi za nje kama vile China.

Akiwa katika Kiwanda cha TANICA Katibu Mkuu Dkt. Bashiru amekutana na kuzungumza na Bodi ya Usimamizi wa Kiwanda hicho na kuwataka Wasimamizi hao kuendesha kiwanda hicho katika mfumo wa Kitaasisi ya kibiashara inayojulikana Kimataifa, na kisasa zaidi, ili kuleta tija katika kile alichotaja kuwa ni Vita ya Kiuchumi, huku akishangazwa na Kahawa ya Kagera kushindwa kuuzika katika soko la Kimataifa kama China, wakati Uganda tayari wameweza kupenyeza hadi katika Soko hilo.

Aidha Dkt. Bashiru amefafanua kuwa Vita ya kiuchumi i wa Kitaifa na Uchumi wa kisasa ni ile hasa inayolenga kukidhi mahitaji ya Taifa kwanza, walengwa wakiwa ni Watanzania wenyewe kujikwamua Kiuchumi kutokana na fursa zinazowazunguka, huku akiagiza Uongozi wa Kiwanda hicho kuboresha miundo mbinu ya Kitekenelojia na kubuni miradi mingine zaidi kama Uvuvi, Mvinyo, Kusindika Ndizi n.k

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa TANICA Bwn. Linus R . Leopord Licha ya kubainisha baadhi ya mafanikio waliyoyapata kwa kipindi cha kuanzia Mwezi Mei mpaka Oktoba Mwaka jana, ambayo ni pamoja Kuendelea kulipa madeni sugu ya Kiwanda hicho, wamefanikiwa pia kukusanya zaidi ya shilingi Bilioni Nne,na huku wakiwa wameshachangia pato la Taifa zaidi ya shilingi Milioni Mia Nane, hakusita pia kuzitaja changamoto za Kiwanda hicho, ambazo ni pamoja na Uongozi uliopo madarakani kutishiwa Vifo na waliokuwa wafanyakazi na Viongozi walioachishwa Kazi, Kugushiwa kwa Nembo ya Kampuni na kusababisha Kuchafuliwa kwa Soko la Kahawa yao, Hali ya Mishahara na Ajira kwa wafanyakazi wenye Taaluma.

Awali Dkt. Bashiru amepata fursa ya kutembelea Bandari Ndogo ya Kemondo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba na kuzungumza na Wananchi wa maeneo yale pamoja na Viongozi wa Serikali na Kichama. Miongoni mwa maelekezo aliyoyatoa ni juu ya Uongozi wa Bandari hiyo kuangalia upya namna ya Tozo inayolipwa getini kwa sasa, pia Tozo inayolipwa kwa Kampuni inayojihusha na Ubebaji mizigo, sambamba na Uvuvi haramu na kuutaka Uongozi husika kubainisha wahusika wa vitendo hivyo ili watiwe Nguvuni na sheria ichukue mkondo wake.
Dkt. Bashiru Kakurwa Akipata maelezo ya Bidhaa ya Kahawa kutoka kwa Rewina Peter (Afsa masoko - TANICA) mara baada ya kuwasili Kiwandani hapo.
Meneja Mkuu wa TANICA Bwn. Linus R. Leopord akitoa ufafanuzi Kwa Dkt. Bashiru namna ya kupeleka Bidhaa yao katika Soko la Kimataifa.
Pichani dkt. Bashiru akizungumza na wannchi katika Bandari ya Kemondo, pembeni ni Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mh. Deodatus Kinawiro na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bukoba Bwn. Murshidi Ngeze.
Wajumbe wa Bodi ya TANICA pamoja na Uongozi wakiwa wameketi Kikao na Katibu Mkuu Dkt. Bashiru.

TANGAZO LA KIFO

$
0
0
Selina Mushi wa Mlandizi Njia Panda JKT anasikitika kutangaza kifo cha mume wake mpendwa Clement Thomas Ndeleokasi Shayo  kilichotokea Alhamsi tarehe 29, Novemba 2018 katika hospitali ya Muhimbili - Mloganzila. 

Mazishi yalifanyika nyumbani kwa marehemu, Uparo-Kirua Vunjo Moshi, Kilimanjaro siku ya Jumanne tarehe 4 Desemba, 2018. Watoto wa marehemu, Frederick Clement Shayo na Regina Clement Shayo, pamoja na mama yao Selina Mushi na dada wa marehemu Clementina Thomas Shayo  wakishirkiana na famlia ya Mtika na ukoo wote wa Shayo, pamoja na familia ya Lesiaki Mushi wanatoa shukrani za dhati kwa wauguzi wa hospitali ya Muhimbili-Mloganzila kwa juhudi zao za kujaribu kuokoa maisha ya mpendwa wao Clement. 

Shukrani zao za pekee zinatolewa kwa Sista Agatha wa kituo cha Afya cha Mtakatifu Joseph, Luguruni Dar es Salaam, ndugu, jamaa na marafiki wote waliomhudumia Clement wakati wa kuugua kwake.  Marehemu aliugua akalazwa hospitali kwa muda mfupi na kuruhusiwa; kisha akapata stroke.  

 Kifo cha Clement kimekuwa mshtuko mkubwa kwa ndugu, jamaa, marafiki, na wote waliomfahamu Tanzania, Marekani na Canada. Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa, Jina Lake Lihimidiwe. Mwenyezi Mungu aipokee roho ya marehemu Clement katika Furaha ya Milele, Amina

MAGAZETI YA LEO JUMATANO JANUARI 2,2019

FAMILIA YA DAUDI LIANA YATOA MSAADA WODI YA WAZAZI WILAYANI MWANGA

$
0
0

Familia ya Daudi Liana, Usangi-Mwanga Kilimanjaro wakitoa msaada wa mashuka kwa wodi ya wazazi ya hospitali ya Wilaya ya Mwanga, Usangi, Kilaweni.. Picha ya pamoja ya familia ya Daudi Liana wakiwa pamoja na uongozi wa hospitali ya wilaya ya Mwanga, Usangi KilaweniPicha ya pamoja ya familia ya Daudi Liana wakiwa pamoja na uongozi wa hospitali ya wilaya ya Mwanga, Usangi Kilaweni
Mmoja ya wanafamilia ya Daudi Liana wa Usangi-Mwanga Kilimanjaro akionesha moja ya misaada ya mashuka kwa wodi ya wazazi ya hospitali ya Wilaya ya Mwanga, Usangi, Kilaweni.

NAIBU WAZIRI SHONZA AWATAKA WASANII KUJIJENGEA TABIA YA KUJIWEKEA AKIBA

$
0
0

Naibu waziri wa Habari, sanaa utamaduni na michezo, Juliana Shonza akizungumza katika tamasha Tukuza Festival Genesis one katika hotem ya Corido Spring Jijini Arusha. Picha/habari na Vero Ignatus.
Rais wa Mtandao wa wasanii wa Injili na Maadili Tanzana Dkt. Godwin Maimu
Naibu Waziri wa Habari, sanaa, Utamaduni na michezo Juliana Shonza akipeana mikono na Rais wa Tagoane Dkt. Godwin Maimu mara baada ya kuzindua mfuko wa Tagoane Loan Fund Jijini Arusha.
Afisa michezo wa Jiji la Arusha Benson Maneno akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika katika Hotel ya Corido Spring Jijini Arusha
Naibu waziri wa habari sanaa, utamaduni na michezo Mhe. Juliana Shonza akizungumza katika uzinduzi wa Mfuko wa Tagoane Loan Fund jijini Arusha.
Rais wa Mtandao wa wasanii wa Injili na Maadili Tanzania Dkt. Godwin Maimu akizungumza na wasanii mbalimbali waliohudhuria katika tamasha la Tukuza festival Genesis one Jijini Arusha.
Naibu waziri wa Habari sanaa utamaduni na michezo Juliana Shonza akisalimiana na Mkurugenzi wa Newlife Band Fortunatus Mabondo(Hondo)
Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na michezo Juliana Shonza akivishwa skafu na mmoja wa Skauti Jijini Arusha
Mkurugenzi wa Newlife Band Fortunatus Mabondo(Hondo) Mabondo akipeana mkono wa pongezi na Rais wa Mtandao wa wasanii wa Injili na Maadili Tanzana Dkt. Godwin Maimu
Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, utamaduni na michezo akipokelewa na kikundi cha ngoma cha jamii ya wamasai cha Meserani Jijini Arusha
Picha ya pamoja Naibu Waziri wa habari, sanaa, utamaduni na michezo Juliana Shonza, Rais wa Tagoane Tanzania Dkt. Godwin Maimu, Katibu mkuu mtendaji wa Tagoane Taifa Silvanus Mumba, Afisa michezo Jiji la Arusha Maneno.
Picha Naibu Waziri wa Habari, sanaa, utamaduni na michezo Juliana Shonza akiwa na wasanii mbalimbali pamoja na viongozi wa Tagoane.


Na Vero Ignatus, Arusha

Naibu waziri wa Habarui, sanaa utamaduni na michezo Mhe. Juliana Shonza amewataka wasanii wa Injili kjijengea tabia ya kujiwekea akiba ili punde wapatapo matatizo waweze kuyatatua kwa urahisi.

Ameyasema hayo hivi karibuni alipokuwa akizindua mfuko wa Tagoane LoanFund Jijini Arusha ambapo amepongeza uongozi wa Tagoane kufikia hatua hiyo. Ameyataka mashirikisho yote ya muziki wa Injili nchini Tanzania kuiga mfano nzuri wa Tagoane ili waweze kuwa na mashirikisho ambayo ni hai na yanayoleta mshindo kwenye jamii.

Amesema yeye kama mlezi wa wasanii wote nchi amewaomba waamke wachangamkie fursa na wasiwe wavivu kujifunza kutoka kwa wenzao waliofanikiwa .Amewataka wasanii kukaa kwa pamoja Kuonyeshe Uzalendo kwa nchi yao wajadili changamoto mbalimbali wanazozipitia na kutafuta namna ya kutazua changamoto zinazowakabili.

Kwa upande wake Rais wa Tagoane Taifa Dkt. Godwin Maimu amesema kuwa wanedhamiria kuanzisha mfuko wao wa Tagoane Loan Fund ambapo mpaka sasa umekuwa na wanachama ambao wameshachangia akiba zao zipatazo shilingi milioni kumi.Amesema mfuko huo unatarajiwa kuanza kutoa mikopo kwa wanachama wavhqngiaji kuanzia 2 januari 2019

maendeleo kama vijana hayawezi kuendelea ukiwa na jitihada za mtu mmoja mmoja bali balintunapounganisha nguvu zetu kwa pamoja mwisho wa siku tunapata kitu cha kuweza kutusaidia. Alisema Dkt Maimu

Amesema lengo la mfuko huo ni kuwakwamua wasanii watakaokuwa na miradi ya uwekezaji, makampuni makubwa, na watakaoweza kutoa fursa na ajira kwa vijana hapa nchini na kulipa kodi kama wananchi wengine

Aidha tamasha hilo lililoshorikisha wasanii mbalimbali wakiwemo wajasiriamali, wachoraji, wachongaji, sanaa za ubunifu ni fursa ambayo Tagoane wameileta na kuwataka wasanii waitumie kwaajili ya kujikwamua kiuchumi na kuoata maendeleo katia jamii nzima

Tamasha hilo la Tukuza festival lilizinduliwa rasmi mwaka 2017 likiwa linafanyika kwa mara ya pili limebeba kauli mbiu isemayo toto yatima haihitaji chakula a mavazi peke yake ila awezeshwe nyenzo za kutimiza malengo yake.
Viewing all 46379 articles
Browse latest View live




Latest Images