Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

Rais Magufuli aungana na Waumini kusali Misa Takatifu ya Jumapili

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili kanisani kwa ajili ya kushiriki Misa ya Maadhimisho ya sherehe ya Familia Takatifu ya Yesu iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Jijini Dar es Salaam.Desemba 30,2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishiriki Misa ya Maadhimisho ya sherehe ya Familia Takatifu ya Yesu iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Jijini Dar es Salaam.Desemba 30,2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mkono wa Amani na Masista wa kanisa katoriki na waumini wengine wakati wa Ibada ya jumapili ya Maadhimisho ya sherehe ya Familia Takatifu ya Yesu iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Jijini Dar es Salaam.Desemba 30,2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na watoto wa kanisa katoriki wakati wa Ibada ya jumapili ya Maadhimisho ya sherehe ya Familia Takatifu ya Yesu iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Jijini Dar es Salaam.Desemba 30, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Paroko msaidizi Padre Asis Mendokta mara baada ya kuungana na waumini wengine katika Misa ya Maadhimisho ya sherehe ya Familia Takatifu ya Yesu iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Jijini Dar es Salaam.Desemba 30, 2018.
PICHA NA IKULU

Waziri Hasunga aziagiza Bodi za Mazao nchini kuwasajili Wakulima wote

$
0
0
Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na Wenyeviti wa Bodi za Mazao pamoja na Wakurugenzi wa Bodi hizo za Mazao, kwenye ukumbi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Jijini Dodoma jana tarehe 29 Disemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akifatilia mkutano wa Wenyeviti wa Bodi za Mazao pamoja na Wakurugenzi wa Bodi hizo za Mazao, uliongozwa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) kwenye ukumbi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Jijini Dodoma jana tarehe 29 Disemba 2018.
Wenyeviti wa Bodi za Mazao pamoja na Wakurugenzi wa Bodi hizo za Mazao,  wakifatilia mkutano wa kazi ulioongozwa na Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga (Mb) kwenye ukumbi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Jijini Dodoma jana tarehe 29 Disemba 2018.




Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga (Mb) amewaagiza Wakurugenzi wa Bodi za Mazao kuanza mara moja zoezi la kuwatambua na kuwasajili wakulima wa mazao yote nchini lengo likiwa kuwatambua ili kupanga mipango sahihi yenye kuongeza tija na uzalishaji katika mazao yote.

Ametoa agizo hilo jana tarehe 29 Disemba 2018 wakati akizungumza na Wenyeviti wa Bodi za Mazao pamoja na Wakurugenzi wa Bodi hizo za Mazao, kwenye ukumbi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Jijini Dodoma.

Mhe. Hasunga amesema ili kuongeza tija na uzalishaji katika Sekta ya kilimo na kuandaa mipango madhubuti ya kuendeleza mazao yote ni vyema kuwatambua Wakulima wote nchini na kuongeza kuwa Wakulima wa zao la korosho wametoa funzo kubwa kwa Wizara yake kufanya jambo kama hili katika mazao mengine hapa nchini.

Itakumbukwa kuwa wiki tatu zilizopita, Waziri Hasunga alitoa agizo kwa Bodi ya Korosho agizo kuandaa daftali maalumu la kuwatambua Wakulima wa korosho kote nchi ambapo moja ya taarifa ambazo zitajumuishwa katika daftali hilo ni pamoja na Jina Kamili la Mkulima, Mkoa, Wilaya, Kata na Tarafa anayotoka.Mambo mengine ni pamoja na Kitongoji, Mtaa au Jina la Kijijini anapotoka, mahali lilipo shamba pamoja na ukubwa wa shamba lake.

Waziri Hasunga ameongeza kuwa mipango sahihi ya kuwaendeleza Wakulima kuanzia kwenye kilimo chenyewe hadi kufikia katika hatua ya kuvuna, kuhifadhi na kulifikia soko ni vyema kuwa na mfumo maalumu wa kanzi data (Database) ya kuwafahamu ili kushughulikia mahitaji yao kisasa na kwa haraka zaidi.

Waziri Hasunga alienda mbali na kushauri matumizi ya TEHAMA na ya Mfumo wa GPS ili kuboresha daftari hilo kwa lengo la kuboresha uwekaji wa taarifa za Wakulima na maeneo wanayotoka Wakulima kwa usahihi zaidi.

“Tumepata changamoto kadhaa wakati wa kuwahakiki Wakulima wa korosho katika mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani na Ruvuma na kama Bodi ya Korosho ingekuwa makini kuandaa daftari la Wakulima zoezi la uhakiki lingekuwa rahisi, kwa ajili hiyo niliwaagiza Bodi ya Korosho kukamilisha zoezi hili mpaka Mwezi Machi, 2019 na Bodi za Mazao zilizobaki ukiacha Bodi ya Tumbaku ambao wao tayari walishafanya hivyo, kukamilisha Mwezi June, 2019”. Amekaririwa Mhe. Hasunga.

Waziri ameitisha kikao maalumu na Viongozi wa Bodi za Mazao, Wakala na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Kilimo kwa lengo la kuboresha mikakati na kuongeza ufanisi katika utendaji wa Wizara pamoja na kujitathmini kabla ya kufikia nusu mwaka wa utekelezaji wa vipaumbele vya bajeti ya Wizara ya mwaka 2018/2019 ili kujipanga kwa ajili ya utekelezaji wa bajeti ya Wizara ya kilimo ya mwaka ujao wa 2019/2020.

Bodi za Mazao zilizoshiriki mkutano huo ni pamoja na Bodi ya Korosho, Bodi ya Pamba, Bodi ya Mkonge, Bodi ya Pareto, Bodi ya Chai, Bodi ya Kahawa, Bodi ya Tumbaku, Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko na Bodi ya Sukari.Wakala zilizoshiriki ni pamoja na Wakala wa Taifa wa Mbolea (ASA) Wakala wa Wakulima Wadogo wa Chai (TSHTDA).

Taasisi nyengine za Wizara ya Kilimo zilizoshiriki ni pamoja na Taasisi ya Udhibiti wa Mbegu (TOSCI), Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO), Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya Ukanda wa Kitropiki (TPRI), Mfuko wa Pembejeo za Kilimo (AGITF), Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea (TFRA), Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI), Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Kampuni ya Taifa ya Mbolea (TFC) na Bodi ya Leseni za Maghala.

MAJALIWA ATOA POLE KWA FAMILIA YA MAREHEMU NDEJEMBI JIJINI DODOMA

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitia saini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Mwanasiasa Mkongwe nchini, Pancras Ndejembi, nyumbani kwa marehemu eneo la Kilimani jijini Dodoma, Desemba 29, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole Bibi Leah Pancras Ndejembi, Mjane wa Mwanasiasa Mkongwe nchini, marehemu Pancras Ndejembi wakati alipokwenda nyumbani kwa marehemu eneo la Kilimani jijini Dodoma kutoa pole kwa familia, Desemba 29, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)PMO
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole, Edna Ndejembi ambaye ni binti Mwanasiasa Mkongwe nchini, marehemu Pancras Ndejembi wakati alipokwenda nyumbani kwa marehemu eneo la Kilimani jijini Dodoma kutoa pole kwa familia, Desemba 29, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi Job Lusinde wakati alipowasili nyumbani kwa Mwanasiasa Mkongwe nchini, marehemu Pancras Ndejembi eneo la Kilimani jijini Dodoma kutoa pole kwa familia Desemba 29, 2018. Kushoto ni Mbunge wa Dodoma Mjini na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde na watatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa na Waziri Mstaafu, William Kusila.. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na waombolezaji nyumbani kwa Mwanasiasa Mkongwe nchini, marehemu Pancras Ndejembi wakati alipokwenda nyumbani kwa maremu eneo la Kilimani jijini Dodoma kutoa pole kwa familia, Desemba 29, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

RAIS DKT.JOHN POMBE MAGUFULI AMJULIA HALI MAMA YAKE MZAZI BIBI. SUZANA MAGUFULI ANAYEPATIWA MATIBABU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Wasaidizi wake wakimuombea Mama yake Mzazi Bibi. Suzana Magufuli anayepatiwa Matibabu Jijini Dar es Salaam,Desemba 30, 2018. Bibi Suzana Magufuli anasumbuliwa na ugonjwa wa Kiharusi ambapo amekuwa akipatiwa matibabu kwa takribani miezi mitatu sasa.PICHA NA IKULU




MAJALIWA AWASILI MTWARA AKIWA NJIANI KWENDA RUANGWA

$
0
0


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mtwara akiwa njiani kwenda Ruangwa, Desemba 30, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara, Dkt. Jilly Elibariki Maleko wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mtwara akiwa njiani kwenda Ruangwa, Desemba 30, 2018. Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa, watatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi na kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi, Bibi Rehema Madenge.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akislimiana na viongozi wa mkoa wa Mtwara wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mtwara akiwa njiani kwenda Ruangwa, Desemba 30, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Naibu Waziri Shonza awapa TBC wiki moja kukamilisha ujenzi wa Kituo cha kurushia Matangazo Longido

$
0
0

Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Juliana Shonza (wa kwanza kulia) akitoa maelekezo ya kukamilika kwa ujenzi wa kituo cha kurushia matangazo Longido ndani ya wiki moja kwa Meneja wa Kanda ya Kaskazini Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Bw.Gerald Uisso (hayupo pichani) alipotembelea eneo hilo leo lilopo katika ofisi za Wilaya ya Longido,(katikati) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Longido Bw.Jumaa Mhina.
Meneja wa TBC Kanda ya Kaskazini Bw.Gerald Uisso (wa kwanza kulia) akimwonyesha Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Juliana Shonza (katikati) nyumba ambayo imejengwa kwa ajili ya kuweka busta za kurushia matangazo pamoja na mitambo leo alipotembelea eneo hilo Wilayani Longido linapojengwa mitambo hiyo kwa lengo ya kuthibiti changamoto ya usikivu wa matangazo ya TBC,wa (kwanza kushoto) ni Katibu Tawala Wilaya ya Longido Bw. Toba Nguvila.
Katibu Tawala Wilaya ya Longido Bw.Toba Nguvila (kushoto) akiwasisitiza TBC kukamilisha ujenzi wa kituo cha kurushia matangazo kwani wakazi wa Wilaya ya Longido wanakiu ya kusikia matangazo yao wakati Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Juliana Shonza (hayupo pichani ) alipofanya ziara katika Wilaya hiyo kukagua ujenzi wa kituo hicho kitakacho tatua kero ya usikivu.
Jengo litakalosimikwa mitambo na eneo la dishi la kurusha matangazo ya TBC kwa Wilaya ya Longido likiwa halijakamilika ambapo Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Juliana Shonza (hayupo pichani) ametoa maelekezo ujenzi wa kituo hicho ukamilike ndani ya wiki moja leo alipofanya ziara yake katika eneo hilo kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho.
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Juliana Shonza (wa kwanza kushoto) akimsikiliza Fundi Mitambo wa TBC Mhandisi Christopher Mkama akitoa maelezo kuhusu hali ya usikivu kwa eneo la Namaga alipotembelea kituo hicho cha kurusha matangazo ya TBC kilichopo Namanga leo ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kufuatiliaji wa usikivu kwa Kanda ya Kaskazini .



Na Anitha Jonas – WHUSM,Namanga

Arusha.

Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa naMichezo Mhe.Juliana Shonza ameuagiza uongozi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Kanda ya Kaskazini kukamilisha ujenzi wa kituo cha kurusha matangazo kinachojenga Makao Makuu ya Wilaya ya Longido ndani ya wiki moja.

Mheshimiwa Shonza ametoa agizo hilo leo Wilayani Longido alipotembelea kituo cha kurusha matangazo ya TBC kinachojengwa Wilayani hapo kwa lengo la kutatua kero ya kukosekana kwa usikivu wa matangazo ya TBC ambapo wananchi wa eneo hilo wamekuwa wakisikiliza radio za nchi jirani na hiyo imewafanya kukosa taarifa zenye ukweli na uhakika za ndani ya nchi.

“Chumba hichi cha kuhifadhi busta na mitambo mingine ni kidogo sana na ujenzi wake siyo wa kuchukua muda mrefu hakikisheni mpaka Januari 10,muwe mmekamilisha ujenzi wa Kituo hichi wananchi wa Longido wanakiu kubwa ya kutaka kusikia matangazo kutoka chombo hichi cha serikali chenye habari za ukweli na uhakika na hii ni haki yao,”alisema Mhe.Shonza.

Akiendelea kuzungumza katika ziara hiyo Naibu Waziri huyo aliwasisitiza viongozi hao wa TBC kuhakikisha ujenzi wa kituo hicho cha kurushia matangazo kinajengwa kwa kutumia vifaa imara kwani serikali ilitenga bajeti yenye fedha za kutosha kwa ajili ya kuhakikisha usikivu unaboreshwa katika maeneo ya mipakani na malengo ya serikali ni kabla ya mwa 2020 kero hii ya usikivu iwe imekwisha.

Kwa Upande wa Katibu Tawala Wilaya ya Longido Bw.Toba Nguvila asisitiza kuwa ukosekanaji wa usikivu wa Matangazo ya TBC Wilayani hapo umekuwa ni changamoto kubwa kwa utoaji na upokeaji wa taarifa muhimu kuhusu shughuli za kiserikali kwani wakazi wa eneo hilo wanashindwa kupata taarifa hizo kwa wakati ukizingatia jamii ya wakazi hao ni wafugaji na huishi kwa kuhama hama.

“Tungependa matangazo ya TBC yaanze kusikika hapa Longido haraka kwani yapo mambo mengi yanayohitajika kutolea elimu kwa wakazi wa eneo hili kupitia vipindi vya redio ,kwani TBC ni chombo kinacho rusha habari zenye ukweli na uhakika hivyo tungependa wananchi wa hapa nao waweze kusikia matangazo yenu, ”alisema Bw.Nguvila.

Pamoja na hayo nae Meneja wa TBC Kanda ya Kaskazini Bw.Gerald Uisso alieleza kuwa ameyapokea maelekezo hayo na atahakikisha ujenzi huo unakamilika ndani ya muda na vifaa vyake kuwa veye ubora.

Hata hivyo meneja huyo aliwahakikishia viongozi hao mara baada ya kukamilika ufungwaji wa mitambo hiyo usikivu wa matangazo katika eneo hilo utakuwa uko imara.

STEMPU ZA KIELEKTRONIKI ZA USHURU WA BIDHAA KUANZA KUTUMIKA JANUARI, 2019

$
0
0
Na Veronica Kazimoto,Dar es Salaam

Bidhaa zinazostahili kutozwa ushuru wa bidhaa kama vile sigara, mvinyo, pombe kali pamoja na bia zitaanza kutumia rasmi stempu za kielektroniki Januari, 2019 katika Mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro, Mwanza, Shinyanga na Mbeya ambapo mfumo wa stempu hizo umeshafungwa kwenye mitambo ya uzalishaji.

Akizungumza mara baada ya kumaliza kukagua ufungaji wa mfumo huo katika Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC) na Kiwanda cha kutengeneza vinywaji vikali cha Nyati Spirit Tanzania jijini Dar es Salaam, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere alisema kuwa mfumo huo mpya unaondoa mfumo wa zamani wa stempu za karatasi.

“Nimekuja kufanya ziara katika viwanda hivi ili kujiridhisha kama kweli mfumo huu wa stepu za kielektroniki umefungwa na nimejionea mwenyewe mfumo tayari umefungwa katika viwanda vyote nilivyotembelea. Hivyo, tunaachana na mfumo wa zamani wa stempu za karatasi na kwa sasa tunaendelea kufunga mfumo huu mpya wa stempu za kielektroniki kwenye mikoa mingine ambayo haitaanza katika awamu hii”, alisema Kichere.

Kichere alisema kuwa lengo la kuweka stempu za kielektroniki kwenye bidhaa hizo ni kupata idadi halisi ya uzalishaji wa bidhaa ili kutoza kodi stahiki na kuondoa dhana ya kusema kwamba TRA inawaonea wafanyabiashara wanaozalisha bidhaa hizo kwa kutoza kodi isiyoendana na uzalishaji.

“Lengo la kuweka stempu hizi za kielektroniki ni kupata kiasi halisi cha uzalishaji wa bidhaa hizi ili kila upande uridhike yaani mzalishaji alipe kodi sahihi na sisi TRA tutoze kodi stahiki bila kupingana wala kugombana na wateja wetu”, alisema Kichere.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa kiwanda cha kutengeneza vinywaji vikali cha Nyati Spirit Tanzania Rupa Suchak amesema kuwa amefurahishwa na kitendo cha serikali kufunga mfumo huo wa stempu za kielektroniki kwa sababu serikali itaongeza mapato na wafanyabiashara wataongeza uhiari wa kulipa kodi.“Ninaishukuru sana serikali yetu kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kuleta mfumo huu mpya ambao utaongeza mapato na kupanua wigo wa kodi lakini pia kwetu sisi wafanyabiashara tutaongeza uhiari wa kulipa kodi”, alisema Rupa.

Uwekwaji wa stempu za kielektroniki katika bidhaa nyingine kama vile juisi, maji ya chupa, bidhaa za muziki na filamu (CD\DVD\Tape) zitafuata kwa tarehe ambayo itatangazwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania hapo badae.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere akikagua bidhaa katika kiwanda cha kutengeneza vinywaji vikali cha Nyati Spirit Tanzania cha jijini Dar es Salaam ambapo Januari, 2019 Stempu za Kielektroniki za Ushuru wa Bidhaa zitaanza kutumika rasmi katika bidhaa hizo. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa kiwanda hicho Bi. Rupa Suchak.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere (kulia) akisaini kitabu cha wageni katika kiwanda cha kutengeneza vinywaji vikali cha Nyati Spirit Tanzania cha jijini Dar es Salaam wakati alipotembelea kiwanda hicho kukagua ufungaji wa mfumo wa stempu za kielektroniki ambapo Januari, 2019 bidhaa zote zinazozalishwa kiwandani hapo zinatakiwa kutumia Stempu za Kielektroniki za Ushuru wa Bidhaa.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere (katikati) akizungumza na watendaji wakuu wa kiwanda cha kutengeneza vinywaji vikali cha Nyati Spirit Tanzania cha jijini Dar es Salaam wakati alipotembelea kiwanda hicho kukagua ufungaji wa mfumo wa stempu za kielektroniki ambapo Januari, 2019 bidhaa zote zinazozalishwa kiwandani hapo zinatakiwa kutumia Stempu za Kielektroniki za Ushuru wa Bidhaa.

KIBITI ILIVYOJIPANGA NA ULINZI KATIKA SIKUKUU YA KUUKARIBISHA MWAKA MPYA 2019

$
0
0
Na Linda shebby , KIBITI

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji Onesmo Lyanga amesema kuwa hali ya ulinzi na usalama katika Mkoa wa Kipolisi Rufiji ni tulivu na salama hadi sasa hii  ni kutokana na jitihada za jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vyote vya ulinzi na usalama pamoja na mshikamano wa wananchi.

Kamanda Lyanga amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo amesema"Nachukua nafasi hii kuwapongeza wote kwa kusherehekea vyema sikukuu ya Krismas mnamo Desemba 25 mwaka huu ambapo wananchi wa Rufiji walisherehekwa kwa utulivu na amani".

Aidha alisema kuwa anapenda kuwajulisha kuwa jeshi la polisi litaendelea kuimarisha ulinzi na usalama kwa kushirikiana na wadau wote ili katika sherehe za kumaliza mwaka 2018 tuendelee kuwa na usalama kwa raia wote pamoja na mali zao.

"Niwatahadharishe kuwa katika kusherehekea kila mmoja azingatie sheria za nchi kwani kuvunja sheria kwa kigezo cha furaha ya kumaliza mwaka ama kwa sababu yoyote ile ikiwemo kufanya vitendo vya kihalifu mathalani kuchoma moto matairi barabarani au mitaani , ulipuaji wa fataki, baruti, kuendesha vyombo vya moto , shughuli za disko toto na ulevi wa kupindukia havitavumilika kwani vinaweza kuwa chanzo cha madhara mbalimbali kwa binaadamu pia natoa rai kwa kila kaya kuimarisha ulinzi katika makazi yao"alisema Lyanga.

Amesema kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na kuimarisha ulinzi na kufanya doria na misako katika kipindi hiki cha sikukuu kwa kutumia askari waendao kwa miguu, pikipiki na magari katika miji na barabara zote kuu.

"Tunaomba wananchi mtuunge mkono kwa maslahi mapana ya taifa letu"alisema Kamanda Lyanga.

PANITA WAZUNGUMZIA MAZURI YALIYOFANYIKA MWAKA 2018 KATIKA LISHE, WATOA USHAURI

$
0
0

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii


JUKWAA la Lishe Tanzania (PANITA) limesema kuna mambo kadhaa mazuri ambayo yamefanywa kwa mwaka huu 2018 katika eneo linalohusu lishe nchini Tanzania huku likitoa ushauri kwa Serikali kuhakikisha eneo la lishe linapewa kipaumbele zaidi kwa mwaka ujao wa 2019.

PANITA limetoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam baada ya Michuzi Blog kutaka kufahamu ni mambo gani mazuri ambayo yamefanyika katika eneo la lishe kwa mwaka huu 2018 ambao umebakisha siku moja ya kesho kumalizika.

Uongozi wa PANITA pamoja na mambo mengine mazuri ambayo yamefanywa na wadau wa masuala ya lishe nchini, umesema kwa mwaka huu 2018 wamefurahishwa na ongezeko la bajeti iliyotengwa kwa ajili ya lishe toka Sh.bilioni 11 kwa mwaka 2017/18 mpaka Sh.bilioni 14 mwaka 2018/19.Pia wamezungumzia kufurahishwa na kusainiwa kwa mikataba ya kutekeleza afua za lishe kati ya wakuu wa mikoa na Makamu wa Rais kupitia Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) imeongeza uwajibikaji wa Lishe katika ngazi zote.

"Tukiri kwa mwaka huu kuna mambo mengi mazuri ambayo yamefanyika na kuonesha jitihada za dhati katika kuhakikisha eneo la lishe kwa Watanzania lipata nafasi ya kuwepewa kipaumbele.Kumewepo na mikutano ya mipango na bajeti za lishe iliyoshirikisha pia asasi imeongeza umiliki wa mipango.Pia Ofisi ya Waziri Mkuu kuahidi kutunga sheria ya kubana,"amesema.

Uongozi wa PANITA umefafanua Waziri mkuu aliahidi kushawishi Bunge kuwe na sheria ya kubana fedha za lishe zisitumike vinginevyo.PANITA imetoa mwito umefika wakati kuwa na vyanzo vya fedha vya ndani katika 
kushughulikia suala la lishe ili kupunguza utegemezi wa wafadhili

.Pia wameshauri Serikali kujenga nyumba za kunyonyeshea ili kuwapa nafasi ya kunyonyesha watoto vizuri hususani miji yenye foleni.

VIDEO' INAYOSAMBAA MITANDAONI YAWAIBUA TFS

$
0
0
*Yaomba radhi wasafiri, yafafanua utaratibu kusafirisha mazao ya misitu
*Pia yamzungumzia Ofisa wake wa Misutu, kumchukulia hatua za kinidhamu 


Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WAKALA Wakala wa  Huduma za Misitu Tanzania (TFS)  umepokea taarifa kupitia mitandao ya kijamii na wadau  mbalimbali  zinazohusisha  namna  Ofisa  Misitu  wa Wilaya  ya  Korogwe mkoani Tanga ambavyo alikuwa akitekeleza majukumu ya kusimamia Sheria ya Misitu Na. 14 ya Mwaka 2002 pamoja na Kanuni
zake za  mwaka 2004.

Ofisa huyo  alikuwa akitekeleza  majukumu hayo kwa mujibu wa  kifungu cha 93 (Powers of officers with respect to offences) inayompa mamlaka Ofisa Misitu au Ofisa wa Jeshi  la  Polisi  kukagua,  kukamata  na  kuzuia  mazao  yanayodhaniwa  kupatikana  kinyume  na sheria.

Kwa kukumbusha tu leo kwenye mitandao ya kijamii kulikuwa na video inayosambaa kwa kasi kubwa ikionesha namna ambavyo wananchi wanalalamikia kitendo cha Ofisa Misutu akilumbana na abiria baada ya kulisamamisha gari na kubaini kuna vitanda vimebebwa.Hivyo kukaibuka malumbano ambayo yamechangia TFS kuamua kutoa ufafanuzi kwa vyombo vya habari.

Taarifa ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) iliyotolewa leo Desemba 30,2018 imesema uongozi wa  TFS  umefanya uchunguzi wa haraka na kubaini  kuwa abiria mmoja  alikuwa akisafirisha  vitanda  viwili vipya  kwa  basi. Vitanda hivyo vililipiwa  ushuru wa Serikali kupitia mfumo wa Kielektroniki wa Malipo Serikalini (GePG) na kupewa stakabadhi halali ya Desemba 26, 2018 katika kituo cha Mkata, Handeni Mkoani Tanga.

Imefafanua katika kutekeleza  majukumu  yake,  Ofisa  wao alimtaka  abiria  huyo  kuonesha  hati  ya Kusafirishia  bidhaa  hizo  kwa  mujibu  wa  Kanuni  za  Misitu  Kifungu  cha  13, sehemu ndogo ya 4 ambayo inakataza mwenye chombo chochote  cha usafiri kusafirisha mazao ya  misitu  ambayo  hayana  hati  ya  usafirishaji  ambapo  abiria  huyo  hakuwa  nayo. 

"Hata  hivyo, Ofisa  wetu  alishindwa  kutafsiri  masharti  ya  kifungu  hiki  na  mahitaji  ya  utoaji  wa  hati  ya usafirishaji  kwani  kama  msafirishaji  binafsi  kwa  matumizi  ya  nyumbani  asingeweza  kukidhi vigezo vya kuwa na hati hiyo. Hati ya usafirishaji huhitaji msafirishaji kuonesha  usajili, leseni ya  biashara, 
utambulisho  wa  mlipa  kodi  na  namba  ya  usajili  wa  chombo  kinachotumika kusafirisha mazao hayo pamoja na kuonesha vituo atakavyopaswa kukaguliwa,"imeeleza taarifa ya TFS ambayo imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano.

Imeeleza kutokana na tukio hilo Wakala wa  Huduma za Misitu Tanzania  unamwomba  radhi  abiria huyo  na umma wa watanzania kwa    tukio hilo  na usumbufu uliojitokeza na kwamba wakala unaendelea kufuatilia suala  hilo,  na  utahakikisha  kuwa  tukio  kama  hilo halijirudii  tena. Aidha hatua  za  kinidhamu zitachukuliwa kwa mujibu wa Kanuni za utumishi wa umma dhidi ya mtumishi aliyehusika na utoaji  wa  lugha  isiyo  na  staha  wakati  akitekeleza  sheria  ya  misitu  ambapo  alitegemewa  kutoa elimu stahiki kwa umma. Hata hivyo TFS imefafanua ikiwa mwananchi yeyote amenunua samani mpya kutoka kwa watengenezaji au wauzaji mahali popote kuhakikisha anapatiwa risiti halali kwa malipo aliyofanya. 

"Hivyo, mmiliki wa samani mpya kwa matumizi binafsi halazimiki kuwa na  Hati ya Usafirishaji anaposafirisha toka eneo moja kwenda jingine isipokuwa awe tayari kuonesha uthibitisho wa nyaraka za malipo halali ya samani hizo kwa ukaguzi pale itakapohitajika. Mwananchi  yeyote  anayesafirisha  samani  zilizotumika  kutoka  eneo  moja  hadi  jingine halazimiki kuwa hati za malipo wala kuwa na hati ya kusafirishia samani hizo. 

"Serikali  itaendelea  kufanya  mapitio  ya  Sheria  ya  Misitu  na  Kanuni  zake  ili  kuepuka mkanganyiko  wowote  wa  tafsiri  ya  sheria  unaoweza  kujitokeza  na  kuondoa  usumbufu kwa wananchi. Wakala  wa  Huduma  za  Misitu  Tanzania  unapenda  kutoa  rai  kwa  wananchi wote  kuendelea kuzingatia  Sheria  za  uhifadhi  wa  misitu.  Aidha,  Wakala  hauna  nia  ya  kuzuia  utengenezaji, usafirishaji  na  matumizi  ya  samani  za  mbao  mahali  popote  nchini  ilimradi  tu  upatikanaji  wa malighafi  zake  uwe  umefuata  utaratibu.  Lengo  ni  kuhakikisha  kuwa  rasilimali  za  misitu zinatunzwa  na  kutumika  kwa  njia  endelevu  kwa  maendeleo  ya  Taifa. 

"Wakala  wa  Huduma  za Misitu Tanzania utaendelea kutoa elimu kwa umma pamoja na watumishi wake kuhusu taratibu za  uvunaji,  usafirishaji  na  biashara  ya  mazao  ya  misitu  nchini  kupitia  njia  mbalimbali  na kuhakikisha huduma bora kwa wananchi,"imesema sehemu ya taarifa hiyo ya TFS

WAZIRI MPANGO ATOA TAARIFA HALI YA UCHUMI NA UTEKELEZAJI WA BAJETI KUU YA SERIKALI 2018/2019

$
0
0


Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akielezea kuhusu Hali ya Uchumi wa Taifa na utekelezaji wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2018/2019 katika kipindi cha Julai-Novemba, 2018), ambapo alisema Tanzania inaendelea kuwa miongoni mwa nchi tano zinazokua kwa kasi kiuchumi Barani Afrika, wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.

WAZIRI MPANGO ATOA TAARIFA HALI YA UCHUMI NA UTEKELEZAJI WA BAJETI KUU YA SERIKALI 2018/2019

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akielezea kuhusu Hali ya Uchumi wa Taifa na utekelezaji wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2018/2019 katika kipindi cha Julai-Novemba, 2018), ambapo alisema Tanzania inaendelea kuwa miongoni mwa nchi tano zinazokua kwa kasi kiuchumi Barani Afrika, wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.
Baadhi ya Viongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango na Wadau wengine wakifuatilia kwa makini Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa na utekelezaji wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2018/2019, kwa kipindi cha Julai - Novemba, 2018, wakati wa Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango na Waandishi wa Habar,i katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma. 
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (katikati), akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari Jijini Dodoma, kuhusu ufadhili wa wahisani ambapo alisema Wahisani wengi wanamasharti magumu hivyo akasisitiza umuhimu wa wananchi kulipa kodi ili nchi iweze kujitegemea. 
Meza Kuu ikiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango(Mb), (katikati), wakifuatilia kwa makini baadhi ya maswali ya Waandishi wa Habari kuhusu taarifa iliyotolewa ya Hali ya Uchumi wa nchi na Utekelezaji wa Bajeti Kuu ya Serikali, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.


MKAZI WA TARIME AJISHINDIA MILIONI 10 ZA TIGO JIGIFTISHE

$
0
0

Mkazi wa Tarime Mkoani Mara Ahia Stephen (kushoto), akipokea mfano wa hundi ya Sh 10m/- kutoka kwa Meneja wa Tigo kanda ya Ziwa Daniel Mainoya baada ya kuibuka mshindi wa wiki katika promosheni ya Tigo Jigiftishe katika hafla fupi ya kumkabidhi zawadi yake iliyofanyika Tarime mwishoni mwa wiki.
Meneja wa Tigo kanda ya Ziwa Daniel Mainoya (kulia) akisisitiza jambo kwa mshindi wa zawadi ya Sh 10m- katika promosheni ya Tigo Jigiftishe Ahia Stephen (kati kati) muda mfupi kabla ya kumkabidhi zawadi yake katika hafla fupi iliyofanyika Tarime mkoani Mara. Kushoto Meneja wa Tigo Mkoa wa Mara Abdillahi Luhorera
Mshindi wa zawadi ya wiki ya sh 10m/-katika promosheni ya Tigo Jigiftishe kutoka Tarime Mkoani Mara Ahia Stephen (katikati)akifurahia mfano wa hundi muda mfupi baaba ya kukabidhiwa zawadi yake wilayani Tarime mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja wa Tigo Mkoa wa MaraAbdillahi Luhorera na kulia ni Meneja wa Tigo kanda ya Ziwa Daniel Mainoya
Mshindi wa zawadi ya wiki ya sh 10m/-katika promosheni ya Tigo Jigiftishe kutoka Tarime Mkoani Mara Ahia Stephen (kushoto) akiwapungua wakazi wa mji mdogo wa Tarime waliofika katika viwanja vya stendi ya Tarime kushuhudia akikabidhiwa zawadi yake. Kushoto ni Meneja wa Tigo Mkoa wa MaraAbdillahi Luhorera.




Mkazi wa Wilaya ya Tarime Mkoani Mara Ahia Stephen, ameibuka mshindi wa wiki katika promosheni ya Tigo Jigiftishe na kujinyakulia kitita cha shilingi milioni 10.

Stephen anakuwa mshindi wa sita wa zawadi ya shilingi milioni kumi baada ya David Mmuni, Iyaka Muinga, Jane Jisandu wote wa Dar es Salaam pamoja na Mbwana Mbela mkazi wa Mpwapwa mkoani Dodoma na Flora Somba wa Morogoro.

Akizungumza muda mfupi baada ya kukabidhiwa zawadi yake wilayani Tarime mwishoni mwa wiki, mshindi huyo aliishukuru kampuni ya Tigo kwa zawadi hiyo na kusena itamsaidia kutimiza baadhi ya malengo yake kwa urahisi. “Naishukuru promosheni hii kwa kunipatia Sh 10m/-. Fedha hii imekuja muda muafaka kwa kuwa itanisaidi kulipa ada za shule kwa watoto wangu na pia itanisaidia kupanua mradi wangu wa ufugaji wa kuku. Natarajia pia kuanza ujenzi na fedha hii itakuwa nia ya msaada mkubwa kufanikisha lengo hili,” alisema

Stephen alisema alifanikiwa kushinda zawadi hiyo kutokana na kutumia huduma za Tigo Pesanikiwa bni pamoja na kutumua pesa, kukunua vifurushi mbali mbali nakuongeza kuwa ilikuwa vigumu kuamini kuwa amejishindia kiasi hicho pesa kwa urahisi alipopigiwa simu kuambiwa kuwa ni mshindi .Kwa upande wake Meneja wa Tigo kanda ya Ziwa Daniel Mainoya, alimpongeza Styephen kwa kuibuka mshindi na kuwataka watu kuendelea kutumia huduma za tigo ili waweze kuingia katika droo ambazo wanayo nafasi ya kujishindia shilingi milioni 50,25 na 15

Kuweza kujishinda mamililioni katika promosheni ya Tigo Jigiftishe ni rahisi sana, haina makato ya pesa wala kujiunga, ukitumia huduma zetu za tigo unaibuka mshindi” alisema Mainoya.

UGANI WA KATA YA SASU WILAYANI KALIUA AINGIA MATATIZO KWA KUTOKUWEPO KITUONI KWAKE

$
0
0

NA TIGANYA VINCENT

MKUU wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amemwagizwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua kumchukua hatua Afisa Ugani wa Kata ya Sasu Amos Kafulila kwa kosa la kutokuwepo katika Kituo chake cha kazi bila ruhusa.

Alisema hatua hiyo inakwenda kinyume cha agizo la Mkoa la kuwataka watumishi wote wanaohusika na Kilimo kuwa karibu na wakulima kipindi hiki cha msimu wa kilimo ili kuwasaidia kulima kilimo cha kisasa. Mwanri alitoa agizo hilo juzi katika Kata ya Sasu wilayani Kaliua wakati wa ziara yake ya kikazi ya kuhamasisha kilimo bora ikiwemo kilimo cha pamba kwa kuzingatia Sheria na kununi 10 za zao hilo na kumkuta hayupo katika Kituo chake cha kazi.

Alisema Ofisi ya Mkoa ilishatoa maelekezo kuwa Maofisa Ugani wote katika kipindi hiki cha kilimo ,likizo zao zitaharishwa hadi hapo baadaye ili waende vijijini kuwasaidia wakulima kulima kilimo chenye tija , lakini wapo baadhi yao wamekaidi na kuondoka katika maeneo yao bila hata kutoa taarifa kwa viongozi jambo ambalo ni utovu wa nidhamu. Mwanri alisema mkulima ni lazima asaidiwe kuondokana na kilimo cha kizamani cha kupata chakula cha kujikimu na badala yake azalishe ziada kwa ajili ya maendeleo yake na ujenzi wa viwanda nchini.

Alisema kimsingi Ofisi ya Mkoa haijazuia likizo ilichofanya ni kusogeza mbele ili Maofisa Ugani na watumishi wanaohusika na kilimo watumie kipindi hicho cha kilimo kuwasaidia wakulima kukabiliana na matatizo yanayorudisha nyuma maendeleo yao. Mwanri alisema Afisa Kilimo hakuajiriwa kukaa Ofisini bali ni kwenda kwa wakulima na kuwafundisha na kuwaelekeza mbinu sahihi za kilimo.

Alisema Afisa Ugani ambaye atakuwa na matatizo ambayo yanahitaji ruhusu ni lazima aombe kwa Mkurugenzi Mtendaji wake na kisha Mkuu wa Wilaya husika na Mkoa ufahamishe na sio kuondoka bila mamlaka ya juu kupewa taarifa.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(kushoto) akitoa ushauri jana kwa Mwenyekiti wa Halmashauri wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Haruna Kasele(kulia) juu ya kuunga mkono juhudi za wakazi wa kijiji cha Miti mitano za ujenzi wa Shule ya Msingi .Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Dkt. John Pima.

PAMBA FIFI ILIYOKUWA IMEBAKI WILAYANI URAMBO YAPATA UFUMBUZI NA TIGANYA VINCENT

$
0
0
SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imeagiza Bodi ya Pamba Tanzania (TCB) kuhakikisha inanunua pamba iliyobaki Daraja B (fifi) ya wakulima wa Urambo ili kutowakatisha tamaa ya kuendelea na kilimo hicho.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri kufuatia malalamiko kutoka kwa wakulima wa zao hilo katika Kijiji cha Itengamatwi wilayani Urambo juu ya uwepo wa pamba ambao hadi hivi sasa iko katika maghala na wakulima hawajalipwa fedha.

Aliwataka wakulima kutokuwa na wasiwasi kwa kuwa jitihada zinaendelea ili kuhakikisha pamba yao fifi(daraja B) ambayo hadi hivi sasa bado iko katika maghali ya kuhifadhi mazao inanunuliwa na Bodi ya Pamba Tanzana baada ya wanunuzi wa awali kusimamisha ununuzi na kuzima mashine.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka wakulima kuzingatia kanuni 10 za kilimo cha zao hilo ili kuepuka kuzalisha pamba Daraja B ambalo ndio wakati mwingine linakuwa kigezo cha wanunuzi kuwapa bei mbaya na wakati mwingine kukataa kununua pamba yao.

Alisema azimo la Mkoa wa Tabora katika msimu wa kilimo cha zao ujao ni kila mkulima ni lazima azingatite kanuni kumi za zao hilo ikiwemo kuvuna kwa wakati na kuhifadhi katika hali ya usafi.Mwanri alisema hatua hiyo itasaidia kulinda ubora wa zao hilo na kumsaidia mkulima kupata Daraja A na kulipwa bei ya juu itakayompa fedha nyingi ambazo zitasaidia kuboresha maisha yake.

Kwa upande wa Afisa Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora Modest Kaijage aliwahakikishia wakulima wa pamba wilayani Urambo ambao wana pamba fifi(Daraja B) kuwa Bodi imeamua kuinunua na itawalipa malipo yao.Alisema Mkurugenzi Mkuu wa TCB amesema kuwa wanafanya utaratibu ili waweze kununua pamba iliyobaki ambapo wao ndio wataifanyia uchambuzi kwa ajili ya msimu ujao.

Awali baadhi ya wakulima walisema kuwa walipokuwa wakihamasishwa kulima pamba na wakati wa ununuzi waliambiwa kuwa pamba ina madaraja mawili lakini wakati wa mauzo pamba yao daraja B haikununuliwa na bado ipo katika maghali jambo linalowakatisha tamaa kuendelea na kilimo hicho.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akitoa somo kuhusu Sheria na kanuni 10 za kilimo cha pamba juzi katika kijiji cha Ugansa wilayani Kaliua jana .
Baadhi ya wakijiji wa Ugansa wilayani Kaliua wakisikiliza somo la Sheria na Kanuni 10 za zao la pamba kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora (hayupo katika picha) jana .picha na Tiganya Vincent


Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Abel Busalama akitoa salamu za Wilaya kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Tabora aggrey Mwanri ili atoe somo kuhusu Sheria na kanuni 10 za kilimo cha pamba juzi katika kijiji cha Miti mitano
Baadhi ya wakijiji wa Miti mitano wilayani Kaliua wakisikiliza somo la Sheria na Kanuni 10 za zao la pamba kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora (hayupo katika picha) jana .

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASILI KIJIJI CHA NANDAGALA WILAYANI RUANGWA,APOKELEWA KWA SHANGWE

$
0
0


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wananchi wakati alipowasili katika kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa, Desemba 30, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wananchi wakati alipowasili katika kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa, Desemba 30, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

SHILINGI BIL. 222 ZIMELIPWA KWA WAKULIMA WA KOROSHO-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema jumla ya shilingi bilioni 222 zimelipwa na Serikali kwa wakulima wa zao la korosho na kuwataka wakulima wawe na subira.

Amesema wakulima walioanza kulipwa ni wale wenye kilo zisizozidi kilo 1,500 na wale wenye kilo zaidi ya 1,500 na kuendelea Serikali inaendelea na uhakiki kisha watalipwa.”Fedha zipo, hakuna mkulima ambaye atapoteza haki yake wote watalipwa. Tunaendelea na uhakiki kwa wale wenye korosho nyingi ili kubaini kama hawajanunua kangomba.”

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumapili, Desemba 30, 2018) alipozungumza na wananchi wa kijiji cha Nandagala ‘A’ baada ya kufungua ofisi ya CCM kata ya Nandagala.Amesema baadhi ya watu wamekutwa na kilo zaidi ya 1,500 na wameshindwa kuonesha mashamba yao ya mikorosho, hali inayodhihirisha kwamba amenunua kupitia kangomba.

Waziri Mkuu amesema baadhi ya waliokutwa na korosho nyingi ni vijana wadogo ambao hawana hata uwezo kifedha hivyo Serikali itahakikisha inawakamata watu wanaowatuma.Amesema lengo la Serikali inayoongizwa na Rais Dkt. John Magufuli ni kuhakikisha wakulima wananufaika na kilimo chao, hivyo biashara ya kangomba lazima lidhibitiwe.Waziri Mkuu ambaye leo ameanza ziara yake kwa kikazi wilayani Ruangwa, Mkoani Lindi amesema zoezi la ulipaji kwa wakulima wa korosho linaendelea, wakulima wawe na subira.

Serikali iliamua kununua korosho zote za mwaka huu baada ya kubaini wafanyabiashara wamepanga kuwadhulumu wakulima kwa kupanga kununua kwa bei ndogo.Wakati huo huo, Waziri Mkuu ametembelea eneo la ujenzi wa shule ya sekondari ya kata ya Matambalale wilayani Ruangwa ambapo amewataka wahakikishe ujenzi unakamilika.

Amewataka wananchi wa kata hiyo kushirikiana na kuhakikisha wanachangia nguvu kazi katika ujenzi wa vyumba vya madarasa ili mwakani wanafunzi waanze kusoma.Tunataka tuondoe dhiki ya watoto wetu kutembea umbali mrefu hadi Namichiga kutafuta elimu, tunataka watoto wetu wote wasome katika maeneo yaliyo karibu na makazi yao.”

Amesema wanafunzi zaidi ya 200 wamefaulu na hawana pa kwenda hivyo ni lazima ujenzi wa shule zote za sekondari za Matambalale, Chibura na Ruchelegwa ukamilike.Waziri Mkuu amesema hadi Januari 10, 2019 shule hizo zote lazima ujenzi wake ukamilike ili wanafunzi waanze kusoma, hivyo viongozi washirikiane na wananchi kukamilisha ujenzi.


IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,JUMAPILI, DESEMBA30, 2018.

Doto Biteko Atoa Maagizo Mazito kwa Wachimbaji kokoto Dodoma

$
0
0

Fundi wa mashine katika mgodi wa WADI Gao Peng (wa pili kushoto), akieleza jambo kwa Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (Wa pili kutoka kulia) na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana Anthon Mavunde (wa Kwanza kushoto) walipofanya ziara katika machimbo hayo ili kujionea kinachoendelea, wa kwanza kulia ni Afisa Madini wa Mkoa wa Dodoma mhandisi Jonas Mwano.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko akisaini kitabu cha wageni alipotembelea katika machimbo ya kokoto ya kampuni ya Laroy Aggregate Co. Ltd, Kulia kwake ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana Anthon Mavunde na kushoto ni msaidizi wake Kungulu K. Masakala
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko, akitoa tamko la Serikali kwa wachimbaji wa kokoto alipofanya ziara kujionea kinachoendelea katika machimbo hayo baada ya kubainika uhaba wa kokoto katika eneo la ujenzi wa ofisi za Serikali Ihumwa jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (kushoto) pamoja na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana Anthon Mavunde (Kulia) wakiangalia moja ya kifaa kinachotumika katika kuchoronga mawe kwa ajili ya kokoto ambacho kwa sasa hakifanyi kazi kutokana na kuharibika. Katikati ni Fundi wa mashine katika mgodi wa WADI Gao Peng



Na Nuru Mwasampeta

Kufuatia ziara ya Mhe. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa aliyoifanya hivi karibuni katika eneo la Ihumwa ambako ujenzi wa Mji wa Serikali unaendelea na kubaini uhaba wa kokoto katika ujenzi huo, leo Disemba 30, Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko akifuatana na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Ajira na Vijana Anthony Mavunde wamefanya ziara ya kushtukiza kwenye maeneo yanayochimba kokoto hizo na kubaini madudu.

Naibu Mawaziri hao wamebaini machimbo ya kokoto yakiwa yamefungwa kwa madai kuwa wafanyakazi wako likizo, zikiwemo mashine za kusagia mawe hayo zikiwa zimeharibika kwa takribani miezi mitatu na hivyo kupelekea uzalishaji kusimama.

Akizungumza katika eneo hilo la machimbo, Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko amesema anashangazwa kuona kuwa watumishi katika mgodi wa kokoto wanakwenda likizo wakati mahitaji ya kokoto ni makubwa na soko la uhakika.

“Mmechukua zabuni kwa ajili ya kusambaza kokoto kutoka kwa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),na kampuni ya MZINGA wenye uhitaji mkubwa kwa ajili ya ujenzi wa mji wa Serikali unaoendelea halafu mnadai mko likizo,?” amehoji Biteko.

Akizungumza kwa njia ya simu na Mkurugenzi wa Kampuni ya Laroy Aggregate Co. Ltd , Biteko amemtaka mkurugenzi huyo aliyefahamika kwa jina la Joel Mchovu kuhakikisha kuwa, ifikapo Januari 2, 2019 kokoto ziwe zimezalishwa na kusambazwa kwa wahitaji kama walivyokubaliana ili ujenzi uendelee kwa kasi iliyokusudiwa.

Aidha, amewataka watendaji hao kufanya kazi kwa juhudi na weledi mkubwa ili kuzalisha kiasi kinachotosheleza mahitaji vinginevyo oda zitahamishwa na kupewa kampuni za zinazozalisha kokoto zilizopo Chalinze ambazo zinaonesha uwezo mkubwa katika uzalishaji wa kokoto.

“Mfahamu kwamba endapo tutatoa oda kwa watu wa Chalinze maana halisi ya ujenzi wa mji wa Serikali kwa watu wa Dodoma haitakuwepo kwani hamtanufaika na ujenzi huu,” amesisitiza Biteko.

Biteko amewataka wananchi wa Dodoma kutambua kuwa, ujenzi wa mji wa Dodoma ni fursa kwao ya kuweza kujikwamua kiuchumi na kuboresha maisha yao binafsi hivyo, wanapaswa kuwajibika ili kupata manufaa hayo. “Fursa kubwa imepatikana na soko la uhakika lipo nitawashangaa kuona kuwa mnapoteza fursa hii,” amesisitiza.

Naye, Fundi wa Mitambo ya kuchoronga mawe katika mgodi wa WADI, Gao Peng, amesema kuwa, kampuni hiyo iko katika hatua za kutengeneza mashine iliyoharibika ili kuwawezesha kuendelea na uzalishaji wa kokoto hizo na kueleza kwamba mashine hiyo imeharibika kwa takribani kipindi cha miezi mitatu sasa na hivyo kufanya uzalishaji wa kokoto hizo kusimama.

Kwa upande wake, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana Anthony Mavunde, amesema anajisikia vibaya kuona kazi katika maeneo ya machimbo hazifanyiki na kuwataka wananchi wanaofanya shughuli hizo kuongeza nguvu, weledi na ufanisi ili waweze kunufaika.

“Dodoma tumejaliwa kuwa na mawe mengi ya kuzalisha kokoto na madini mengine ya ujenzi, mahitaji ni makubwa kutokana na kasi ya ujenzi iliyopo lakini bado wana Dodoma mmelala,” amesema Mavunde.

Kwa upande wake, Afisa Madini wa Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Jonas Mwano amekiri kuwepo kwa leseni hai za uchimbaji wa madini ya kokoto 75 katika mji wa Chigongwe na leseni 66 zimekwisha tolewa kwa waliowasilisha maombi ya leseni hizo na hivyo kuwataka wamiliki wa leseni hizo kuhakikisha wanazifanyia kazi leseni zao vinginevyo zitagawiwa kwa watu wengine.

Aidha, Mwano amekiri kuwa, awali wamiliki wengi wa leseni za madini ya kokoto walikuwa hawazalishi vya kutosha kwa madai kuwa soko lilikuwa adimu lakini sasa soko ni la uhakika na hivyo kuwataka wazalishe kokoto za kutosha ili kutoiangusha Serikali.

Pia, Mhandisi Mwano ameahidi kutembelea maeneo ya uchimbaji wa kokoto kila siku kufuatia maagizo ya Naibu Waziri Doto Biteko ili kuhakikisha kazi ya uzalishaji wa kokoto hizo unaridhisha na kutosheleza mahitaji ya ujenzi katika jiji la Dodoma.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU DESEMBA 31,2018

NAIBU WAZIRI MHE.KANYASU AWATAKA WANANCHI WANAOISHI NDANI YA HIFADHI YA MISITU KULIPA TOZO BILA SHURUTI

$
0
0

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Costantine Kanyasu akizungumza na  wananchi wanaoishi na kufanya shughuli za uzalishaji mali ndani ya Hifadhi ya msitu ya Kisiwa cha  Kome Mchangani ambayo ni Kambi ya Uvuvi iliyopo wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza wakinyoosha mikono ikiwa ni ishara ya kukubali kuwa watalipa tozo za serikali bila kulazimishwa alipofanya ziara ya kutatua kero zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo.
2
 Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Mhe. Dkt. Charles Tizeba akizungumza na wananchi wa Jimboni kwake  kwenye mkutano wa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu wa kutatua kero za  wananchi wanaoishi ndani ya  Hifadhi ya msitu ya Kisiwa cha  Kome Mchangani ambayo ni Kambi ya Uvuvi iliyopo wilayani Sengerama mkoani Mwanza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanya  katika kijiji cha Kisaba na Bugombe
3
 Mwenyekiti wa Kijiji cha Buhama kata ya Buhama, Thomas Sabuni, akizungumza  na wananchi kwenye mkutano wa hadhara kabala ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu kwa ajili ya kuzungumza na wananchi ikiwa lengo  kutatua kero za wananchi wa Kisiwa hicho wilaya ya Sengerama mkoani Mwanza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanya katika eneo la Kome mchangani.
4
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Costantine Kanyasu akiteta jambo na Meneja wa Shamba la Buhindi , Ayoub Kigongwira wakati wa  mkutano wa hadhara uliofanyika katika Hifadhi ya msitu ya Kisiwa cha Kome Mchangani ambayo ni Kambi ya wavuvi wakati alipofanya ziara ya kutatua kero zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo.
5
Baadhi  ya wananchi wakifuatilia mkutano wa hadhara wa  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Costantine Kanyasu ndani  ya Hifadhi ya msitu ya Kisiwa cha Kome Mchangani ambayo ni Kambi ya wavuvi wakati alipofanya ziara ya kutatua kero zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo.
6
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu (katikati) akiwa na baadhi ya viongozi wa kijiji cha Buhama  wakati alipowasili katika Hifadhi ya msitu ya Kisiwa cha Kome Mchangani ambayo ni Kambi ya wvuvi kwa ajili ya kutatua kero zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo.
7
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akiiangalia taarifa mara baada ya kukabidhiwa taarifa Mwenyekiti wa kijiji Buhama, Thomas Sabuni  wakati alipowasili katika Hifadhi ya msitu ya Kisiwa cha Kome Mchangani ambayo ni Kambi ya wvuvi kwa ajili ya kutatua kero zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo.                (PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA-MNRT)
 
………………………
NA LUSUNGU HELELA-MWANZA
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Costantine Kanyasu amewataka wananchi wanaoishi na kufanya shughuli za uzalishaji mali ndani  ya Hifadhi ya misitu ya Visiwa vya  Kome  na Maisome vilivyoko wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza kulipa tozo za serikali bila kulazimishwa.
Kauli hiyo ameitoa  wakati alipokuwa akizungumza na wakazi wanaoishi ndani ya Hifadhi ya  Msitu wa Shigala ulioko Kome Mchangani ambayo ni kambi ya wavuvi wakati alipofanya ziara ya kutatua kero zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo.
Mbunge wa Jimbo la Buchosa Dkt. Charles Tizeba amemueleza  Naibu Waziri hiyo kuwa kumekuwepo na changamoto ya ulipaji  tozo kubwa hata kama mtu ana eneo dogo na ndipo wananchi walilazimika kugoma kulipa tozo hiyo kwa lengo la kupata msaada zaidi.
Amefafanua kuwa mtu anayemiliki hekari moja  anatakiwa kulipa Tsh.425,000 kwa mwaka lakini hata mtu anayemikili eneo dogo la mita 20 naye anatakiwa kulipa kama wa hekari moja  kitendo kilichowafanya wananchi hao kushindwa kulipa na kusubili maelekezo ya wizara husika.
Mmoja wa wananchi wanaoishi ndani ya Hifadhi hiyo,Juma Ramadhani amemwomba Naibu Waziri kuangalia upya sheria hiyo ili wananchi wapate nafuu ya kulipa na serikali iweze kupata mapato yake.
Kaimu Meneja wa TFS Kanda ya Ziwa, Thomas Moshi amesema kuwa tozo hizo zipo kwa mujibu wa sheria kinachotakiwa ni wananchi kulipa na siyo kugomea kulipa tozo hizo na wanapofanya hivyo wanakwenda kinyume na matakwa ya sheria ya hifadhi ya misitu.
Kanyasu amewahakikishia wananchi hao kuwa suala hilo atalipatia majibu kwa haraka lakini amewataka watu wanaomiliki hekari moja  kulipa tozo hizo kwa wakati na wale wenye maeneo madogo madogo wajiunge katika vikundi ili waweze kuilipa pesa hiyo
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images