Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1762 | 1763 | (Page 1764) | 1765 | 1766 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Mtaalam Manunuzi,Bw. Jones Mapunda kutoka Kitengo cha Usimamizi wa Maboresho ya Mahakama, akitoa mafunzo ya Usimamizi wa Mikataba kwenye ukumbi wa kitengo hicho.
  Baadhi ya viongozi wa Mahakama ya Tanzania na Watumishi wakiwa katika mafunzo ya Usimamizi wa Mikataba yaliyofanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Kitengo cha Usimamizi wa Maboresho ya Mahakama.
  Mtaalam Manunuzi,Bw. Jones Mapunda kutoka Kitengo cha Usimamizi wa Maboresho ya Mahakama, akitoa mafunzo ya Usimamizi wa Mikataba kwenye ukumbi wa kitengo hicho kwa viongozi na Watumishi wa Mahakama. (Picha na Magreth Kinabo).
  Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Maboresho ya Mahakama, Mhe. Zahra Maruma akifafanua jambo wakati wa mafunzo ya Usimamizi wa Mikataba yaliyofanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Kitengo cha Usimamizi wa Maboresho ya Mahakama.
  Mtendaji wa Mahakama ya Rufaa, Bw. Solanus Nyimbi akifunga mafunzo ya Usimamizi wa Mikataba yaliyofanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Kitengo cha Usimamizi wa Maboresho ya Mahakama.

  0 0

  *Aagiza wakae na wakandarasi wao na kupima kama watamaliza kazi

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na Mawaziri na Makatibu Wakuu kwenye eneo la tenki la maji la kutolea huduma katika ujenzi wa mji wa Serikali Mtumba badala ya ukumbi wa Hazina kama alivyokuwa amepanga awali.

  Akiwa Ihumwa, Waziri Mkuu amewaagiza Mawaziri wafike kwenye maeneo ya ujenzi wa ofisi zao, watathmini uwezo wa wakandarasi wanaojenga majengo ya wizara na pale watakapojiridhisha kuwa uwezo wao ni mdogo, wawabadilishe mara moja.

  Ametoa agizo hilo leo mchana (Ijumaa, Desemba 28, 2018) akiwa kwenye kikao cha kazi (site meeting) na mawaziri 15 na manaibu mawaziri katika eneo la Ihumwa lililoko km. 17 kutoka jijini Dodoma.

  “Mawaziri mliopo na makatibu wakuu wote kaeni na wakandarasi wenu hapa site ili waeleze kazi hii itakamilishwa lini. Lengo letu ni kuhakikisha kuwa kazi hii inakamilishwa kwa wakati,” amesisitiza.

  Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwapa mrejesho Mawaziri juu ya changamoto alizokutana nazo jana alipofanya ukaguzi wa ujenzi kwa kila wizara. “Nataka Mawaziri ambao ofisi zao zinajengwa wa watu wa Mzinga, wakae nao na kutathmini uwezo wao na kama mtaona hawawezi, mkabidhi kwa mkandarasi mwingine,” amesema Waziri Mkuu.

  Amewataka wakandarasi wahakikishe wanaongeza idadi ya vibarua ili kazi hiyo iweze kwenda haraka. “Wizara iliyofanya vizuri kuliko zote ni ya Utumishi, wao wako hatua nzuri. Kwa maana ya uchapaji kazi, eneo nililokuta lina wafanyakazi wengi ni magereza,” amesema.

  Wakati huohuo, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. William Lukuvi alimweleza Waziri Mkuu kwamba kuna wagongaji wa kokoto ambao wamepokea fedha lakini wakaamua kufunga machimbo yao kwa sababu ya sikukuu.

  “Waziri wa Madini aongee nao hawa watu ili warejee na kufanya kazi kwa sababu baadhi yao wameshapokea fedha na mahitaji ya kokoto hapa ni makubwa na aliyebakia akifanya kazi ni Nyanza Road Works peke yake,” alisema.

  Naye Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani alimweleza Waziri Mkuu kwamba wizara yake imetoa transforma tisa za kusaidia kupoza umeme lakini ni wizara nne ambazo zimejitokeza na kulipia line za transforma hizo.

  “Wizara yetu tumetoa transforma tisa za kusaidia umeme upatikane eneo la ujenzi. Niwaombe mawaziri waliopo, walipie service linetu ambazo gharama yake ni sh. 921,000 ili wafungiwe transforma na kazi iweze kufanyika mchana na usiku. Hadi sasa, tumeshapokea maombi kutoka  wizara nne tu za Maji, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera), Elimu na Nishati ili kazi imalizike ndani ya muda mfupi,” alisema.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  S. L. P. 980,
  41193 – DODOMA,                      
  IJUMAA, DESEMBA 28, 2018.
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako wakati alipowasili kwenye eneo la Ihumwa jijini Dodoma, unapojengwa Mji wa Serikali kukutana na Mawaziri na Makatibu Wakuu, Desemba 28, 2018. Wengine pichani kutoka kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais  Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - TAMISEMI, Selemani Jafo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dkt. Augustine  Mahiga, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango na kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mawaziri na Makatibu Wakuu kwenye eneo la Ihumwa jijini  Dodoma unapojengwa mji wa Serikali, Desemba 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Dkt. Maulid Banyani baada ya kuzungumza na Mawaziri na Makatibu Wakuu kwenye eneo la Ihumwa jijini Dodoma unapojengwa Mji wa Serikali, Desemba 28, 2018.  Katikati ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi baada ya kuzungumza na Mawaziri na Makatibu Wakuu kwenye eneo la Ihumwa jijini Dodoma unapojengwa mji wa serikali, Desemba 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   

  0 0

  Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mwita Waitara amezitaka Halmashauri zote kutekeleza mpango wa anwani za makazi na postikodi nchi nzima kwenye Halmashauri zao bila ya kutumia kisingizio cha ukosefu wa bajeti za kufanya vikao vinavyohusu utoaji wa majina ya mitaa 

  “Suala la gharama halipo, tumieni vikao vyenu vya kawaida, vya kisheria kutaja majina ya mitaa, suala la anwani za makazi na postikodi iwe ajenda mahususi ya ulinzi na usalama”, amefafanua Waitara 

  “Wakurugenzi wote wa Halmashauri zote nchi nzima waliopo chini ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI wahakikishe kwamba wanatoa maelekezo mahususi kwa watendaji wote na kuhakikisha kuwa wanatoa majina ya mitaa,” amesema Waitara. Pia amewaelekeza Makatibu Tawala wote Tanzania Bara wahakikishe Halmashauri zote zinatekeleza mpango wa anwani za makazi na postikodi

  Waitara ameongeza kuwa mpango huu unatuwezesha kujitambua na kuwatambua watu wetu wanakoishi, na nini kilichowaleta eneo hilo kama ni biashara, uwekezaji na ni muhimu kwa ulinzi na usalama wa raia. Pia amesema kuwa suala la anwani za makazi na postikodi litawasaidia viongozi wao wenyewe kuwatambua wananchi, kuwezesha ukusanyaji wa kodi na kufikisha huduma za Serikali kwa wananchi

  “Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anataka watanzania walipe kodi, jambo hili likitekelezwa, watanzania watalipa kodi na mpango huu wa kuwatambua wananchi utasaidia kuongeza mapato ambayo yataleta maendeleo ya taifa letu na kujenga miundombinu ya barabara, huduma za afya na elimu,” amesema Waitara

  “Wenzetu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa upande wa Sekta ya Mawasiliano wametimiza majukumu yao, wanataka majina ya barabara na mitaa ili waweke namba za nyumba, naomba muwasaidie kutimiza wajibu wao, mtoe majina kwenye vikao vyenu ili Wilaya hii iwe kweli ya mfano,” amesema Waitara

  Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amesema kuwa Sengerema ni moja ya Wilaya chache zilizoteuliwa kuwa ya mfano kutekeleza mpango wa anwani za makazi na postikodi ambapo tunahitaji kila Wilaya Tanzania iwe na mitaa na majina ili tufahamu kila mtanzania anakaa wapi, hii itatusaidia katika masuala ya ulinzi, usalama na uchumi

  Naye Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole amekiri kuwa Sengerema imepata fursa ya kuwa Wilaya ya mfano na ya mwanzo katika utekelezaji wa mpango wa anwani za makazi na postikodi ambapo utekelezaji wa mpango huu kwa wilaya ya Sengerema ambayo iko mpakani itasaidia katika masuala ya ulinzi na usalama, ukusanyaji wa mapato na kodi za Serikali.

  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Buchosa, Joseph Henry Kanyumi akizungumza kwa niaba ya viongozi na watumishi waliohudhuria mafunzo ya mpango huo alisema kuwa wametambua umuhimu wa mpango huo. “Nasi tumenufaika na mafunzo hayo na ifikapo tarehe 15 Januari, 2019 tutakuwa tumekamilisha utoaji wa majina ya mitaa,” alisema Kanyumi

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Mawasiliano, Dkt. Jim Yonazi alisema kuwa ni muhimu kuweka sheria ndogo ndogo katika Halmashauri ili mpango huu uweze kutekelezwa na kudhibiti ujenzi holela pamoja na kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ili mfumo huu uweze kufanya kazi

  Mpango wa Anwani za Makazi na Postikodi ulianza kutekelezwa kwa majaribio mwaka 2009 kwenye mikoa minne ya Dar es Salaam, Arusha, Dodoma na Zanzibar ambapo sasa utekelezaji huo unaendelea kwenye Halmashauri 12 na utafanyika kwenye Halamshauri zote nchi nzima. Aidha, hadi sasa kata zote nchi nzima zina postikodi ambazo zimeridhiwa na Umoja wa Posta Duniani (UPU) ambapo tangazo la Serikali Na. 220 lilitolewa kwa mara ya kwanza tarehe 22 Juni mwaka 2012 na kuboreshwa na kutolewa tena tangazo la Serikali Na. 140 tarehe 22 Aprili mwaka 2016. Vile vile, Serikali imeandaa mwongozo wa postikodi na anwani za makazi ili watendaji wa Halmashauri waweze kuzingatia na kutumia kufanikisha utekelezaji wa mpango huu

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,

  Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

   Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kushoto) akijadiliana jambo na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mwita Waitara wakiwa wanatoka kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Sengerema (hayupo pichani) wakati wa ziara yao wilayani humo ya utekelezaji wa mpango wa anwani za makazi na postikodi
   Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mwita Waitara akizungumza na viongozi na watumishi wa Halmashauri ya Sengerema na Buchosa (hawapo pichani) kuhusu utekelezaji wa mpango wa anwani za makazi na postikodi wakiwa Nyehunge, Mwanza. Wa tatu kushoto ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye, wa tatu kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Mawasiliano, Dkt. Jim Yonazi na wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole
   Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akifafanua jambo kwa viongozi na watumishi wa Halmashauri ya Sengerema na Buchosa (hawapo pichani) wakati wa mafunzo ya kujenga uelewa kuhusu utekelezaji wa mpango wa anwani za makazi na postikodi yaliyofanyika Nyehunge, Mwanza. Wa nne kushoto ni Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mwita Waitara na pili kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Mawasiliano, Dkt. Jim Yonazi
   Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa nne kushoto) akiwa na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mwita Waitara (wa tatu kushoto) kuhusu kituo cha telesenta wakati wa ziara yao Wilayani humo
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Mhandisi James Kilaba akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kushoto) na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mwita Waitara (wa pili kushoto) kuhusu kituo cha telesenta wakati wa ziara yao wilayani Sengerema.  Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Emmanuel Kipole.

  0 0


  0 0

  Mwenyekiti wa Tahsisi ya Maendeleo ya Vunjo (VDF) Askofu Mstaafu wa KKKT dayosisi ya Kaskazini ,Dkt Martin sham akizungumza wakati wa Sherehe ya siku ya Wanavunjo (Vunjo Day) iliyofanyika chuo cha Ualimu Marangu na kukutanisha wananchi na viongozi mbalimbali.
  Mbunge wa jimbo la Munjo na Katibu wa Taasisi ya Maendeleo ya Vunjo (VDF) Mh James Mbatia akizungumza katika sherehe hizo ambas zinafanyika kwa mara ya kwanza Latina jimbo hilo na kukutanisha wenyeji wa Vunjo waishio nje na ndani ya jimbo hilo.
  Mchungaji Kiongozi wa Usharika wa Kijitonyama ,Dayosisi ya Mashariki na Pwani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Eliona Kimaro ambaye pia ni mwenyeji wa Jimbo la Vunjo akizungumza latina sherehe hizo.
  Viongozi mbalimbali walioshiriki katika sherehe hizo wakipiga makofi .


  VUNJO-KILIMANJARO 

  MBUNGE wa Vunjo, James Mbatia amesema kuanzia wiki ya pili ya mwezi Januari mwaka ujao, mitambo yote ya ujenzi wa barabara iliyokuwa imezuiwa na serikali ya Wilaya ya Moshi kuendelea na kazi za upanuzi wa barabara, itarejea kazini.

  Alitangaza uamuzi huo mbele ya mamia ya wananchi, viongozi wa dini mbalimbali, madiwani na watendaji wa vjijiji waliohudhuria hafla ya siku ya wana Vunjo iliyofanyika Chuo cha Ualimu Marangu, Wilaya ya Moshi.

  “Tumeingiliwa lakini tujipe moyo kwa sababu jambo lolote likipata msukosuko sana, ni jambo lenye heri. Mwezi wa 11 mwaka huu Rais (Magufuli) aliagiza kazi hii iendelee mara moja, kwa hiyo naomba nitangaze kwa niaba ya bodi ya VDF (Taasisi ya Maendeleo ya Vunjo), wiki ya pili ya mwezi Januari 2019, vyombo vyote vinarudi kazi na kazi inaendelea,”alisema Mbatia

  Wakati Mbatia anatangaza uamuzi huo, tayari upanuzi na ujenzi wa barabara hizo za vijijini katika Jimbo la Vunjo kwa kiwango cha changarawe, umezuiwa na serikali Wilaya ya Moshi.Mradi huo unahusisha barabara zenye urefu wa kilometa 389.3 ambazo zitagharimu sh. bilioni 12.077 kutokana na utafiti wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (Tarura).

  Awali akizungumza katika hafla hiyo, Mchungaji Kiongozi wa Usharika wa Kijitonyama wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Eliona Kimaro alisema maendeleo ya mtu na utu wake na nguvu ya jamii ndivyo pekee vinavyoweza kuchochea kuleta maendeleo katika nchi yeyote ile.

  “Nguvu ya jamii katika kuleta maendeleo na kutatua matatizo yao binafsi na ya serikali ni kinyume kabisa katika maendeleo kwa kanuni za kiuchumi.Zaidi Much, Kimaro alieleza: "Kufikiri kwamba nchi tu ndiyo inaweza ikaleta maendeleo ni makosa, ndio maana wanasiasa wengi wa Marekani wamekuwa wakisema ili uwe Rais wa nchi au kiongozi wa serikali lazima uwe na mawazo haya, kwamba unakwenda kuifanyia nini nchi na sio nchi imfanyie yeye,”alisisitiza 

  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa VDF ambaye ni Askofu Mstaafu wa Dayosisi ya Kaskazini, Dk. Martin Shao alisema dhamira ya kuanzishwa kwa taasisi hiyo ni si kuboresha tu miundo mbinu ya barabara, bali pia kuna sekta za afya, elimu, maji na sekta ya mazingira.Alisema taasisi hiyo ndio mwanga wa alfajiri uliopewa jina la ‘ngatuni yetu’ ambayo inataka kuifanya Tanzania kuwa sehemu bora, salama na pazuri pa kuishi, kwa vile itatekeleza jukumu hilo nchi nzima.

  0 0

  Wilaya ya Kigamboni imeongoza katika utoaji wa vitambulisho kwa wajasiriamali katika mpango wa kuwatambua wafanyabiashara wadogo wadogo baada ya kuwa ya kwanza katika Mkoa wa Dar es salaam kuwafikia wafanybiashara wengi zaidi.

  Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mh. Sara Msafiri alipokutana na wandishi wa habari ofisini kwake  jana. Mkuu wa Wilaya amesema ofisi yake ilipokea vitambulisho elfu tano toka ofisi ya Rais-Tamisemi na vikiwa na lengo la kukusanya jumla ya shilingi Milioni mia moja lakini mpaka jana Desemba 28,2018 jumla ya shilingi milioni 94 sawa na asilimia 97 ya lengo.

    Mkuu wa Wilaya amesema  kuwa kiwango hicho kimefikiwa baada ya kuwa na mpango wa ushirikishwaji wa watendaji wa mitaa na wenyeviti ambapo waliweza kuwafikia wajasiriamali wengi katika mitaa yao.

  Kwa upande wake meneja wa mamlaka ya mapato (TRA) Mkoa wa Temeke Bw.Gamaliel Mafie amesema wao kama mamlaka wamefurahia huo mpango kwa kuwa umewajumuisha watu ambao hawakuwa kwenye mfumo rasmi wa walipa kodi. Ameongeza kuwa hata wao wamepokea mpango huo kwa furaha kwa kuwa umepanua wigo wa walipa kodi kwa mpango wa kuchangia.

  Akihitimisha kikao hicho, Mkuu wa Wilaya  ametuma ombi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ili aweze kupatiwa vitambulisho elfu tatu (3000), kukidhi idadi kubwa ya wafanyabishara ambao bado hawajafikiwa mpaka sasa.
   Mkuu wa wilaya ya Kigamboni,Sara Msafiri akizungumza na waaandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa wilaya ya Kigamboni,Sara Msafiri akimkabidhi kitambulisho cha mjasiriamali,Amina Rashidi jana  jijini Dar es Slaam.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
  Meneja wa Mamlaka ya mapato (TRA) mkoa wa Temeke,Gamaliel Mafie akifafanua jambo katika mkutano huo uliofanyika jana  jijini Dar es Salaam.

  0 0


  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (wa kwanza kushoto)akionyeshwa maendeleo ya ujenzi wa madarasa unaoendelea ili kuhakikisha shule inapofunguliwa mwezi wa kwanza wanafunzi wanapata fursa ya kuendelea na masomo.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akishiriki msingi wa ujenzi wa madarasa ya shule ya msingi Msia alipokwenda kuangalia ujenzi unaoendelea.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo
  Kipeta Sekondari – Jengo la Utawala la shule ya Sekondari Kipeta likiwa limeezuliwa paa.

  ……………………………………………………………………………….

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amechangia shilingi milioni tatu ili kuharakisha ukarabati wa ujenzi wa shule ya msingi Msia pamoja na shule ya sekondari Kipeta zote za bonde la ziwa rukwa, Wilayani Sumbawanga ikiwa ni kuunga mkono juhudi za wananchi katika kurudisha miundombinu ya shule hizo zilizoharibika baada ya upepo na mvua kali iliyonyehs amwanzoni mwa mwezi huu.

  Kati ya fedha hizo shilingi milioni mbili zitatumika katika shule ya msingi Msia na shilingi milioni moja zitatumika kuikarabati shule ya sekondari kipeta ambapo zimebaki wiki mbili shule hizo kufunguliwa na wanafunzi kutakiwa kuendelea na masomo.

  Mh. Wangabo aliwashukuru wananchi waliojitokeza kuchangisha fedha kwaajili ya ukarabati wa shule ya msingi Msia zilizofikia kiasi cha shilingi 5,595,000/= ambapo wananchi wa kawaida walichangia shilingi 5000/=, wafanyabiashara wadogo shilingi 20000/=, mfangabiashara wa kati shilingi 50000/= na wafugaji shilingi 100000/= ambapo fedha hizo zinatarajiwa kufanya ukarabati na ujenzi wa madarasa manane.

  Awali akisoma taarifa ya harambee ya ukarabati wa shule Mtendaji wa kijiji cha Msia Andrew Sanga alieleza mikakati ya kijiji kuwa ni kuongeza vyumba vya madarasa vitatu, na ofisi moja ya walimu na msingi umeshaaza kujengwa, kukusanya michango kwa wananchi ambao bado kuchangia na hivyo kutimiza lengo la kujenga madarasa nane, ofisi mbili ndani kabla ya shule kufunguliwa mwanzoni mwa mwezi wa kwanza.

  “Mheshimiwa mkuu wa mkoa mapungufu yaliyopo ni kama ifuatavyo, bati, madirisha, nondo, misumari, madirisha, milango na rangi, ili kukamilisha majengo tunayoendelea kuyajenga kwani shule hiyo yenye wanafunzi 866 ina uhitaji wa madarasa 22,” Alibainisha.

  Katika kuunga Mkono juhudi hizo Mh. Wangabo alisema,”Pamoja na pongezi ambazo nilizitoa kwa wadau wote ambao wamechangia, na mimi nipende kushirikiana nanyi, nitachangia vifaa ambavyo inaweza ikawa mabati, au inaweza ikawa saruji, kulingana na hesabu zitakazokuwa zinapigwa na Mkurugenzi pale, nitachangia hivyo vifaa kwa shilingi milioni mbili.”

  Pia aliwasihi mafundi wa madarasa hayo kujiahidi kuzingatia ubora katika ujenzi kuliko ilivyokuwa imejengwa hapo awali na kuwaomba wachukulie kazi hiyo ni kama ya kujitolea mchango wao katika kuunga juhudi za wananchi kumaliza shule hiyo.

  Pia kwa upande wa shule ya sekondari ya Kipeta alichangia shilingi milioni moja kama mwanzo wa harambee itakayofanyika mwanzoni mwa mwezi wa kwanza mwaka 2019 ili kuhamasisha wananchi wa kijiji cha kipeta kuweza kuiboresha shule hiyo ambayo iliezuliwa mapaa yote pamoja na baadhi ya nyumba 4 za walimu ikiwemo ya mwalimu Mkuu.

  Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Sebastina Mwilima alisema kuwa tayari halmashauri imeshaagiza vifaa vyenya thamani ya shilingi milioni 23 kwaajili ya kufanikisha zoezi la kukarabati shule hizo ambapo shule ya msingi Msia madarasa manne yalianguka na shule ya sekondari Kipeta, madarasa, mabweni pamoja na nyumba za waalimu kuezuliwa mapaa.

  0 0


  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi ametembelea eneo linapojengwa jengo la Wizara yake na kuagiza timu maalum kupiga kambi eneo hilo ili kuhakikisha ujenzi unafanyika usiku na mchana huku wakizingatia viwango vya ubora katika ujenzi wa jengo hilo.

  “Nataka ujenzi uharakishwe kama ambavyo Waziri Mkuu alivyogiza lakini viwango vya ubora katika ujenzi vizingatiwe” alisema Prof. Kabudi.
  Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome amemtaka mkandarasi anayejenga jengo la Wizara hiyo kuhakikisha anakusanya mahitaji yote yanayotakiwa eneo la ujenzi ili kufanikisha kasi ya ujenzi inaenda kama inavyotakiwa.

  Ujenzi wa Jengo la Wizara ya Katiba na Sheria unatarajiwa kukamilika mapema ifikapo tarehe 15 Januari 2019.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na wananchi pamoja na wafanyakazi wa machinjio ya Vingunguti wakati akitoa zawadi ya mwaka mpya ya ng’ombe 20 kwa wagonjwa na wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Hospitali ya Ocean Road, na hospitali za rufaa za Mkoa wa Dar es Salaam ikiwamo Hospitali ya Temeke, Amana na Mwananyamala.
  Baadhi ya wananchi na maofisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakimsikiliza mkuu wa mkoa kabla ya kutoa zawadi ya mwaka mpya.
  Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Yacoub Hassan Mohamed akimshukuru Mh. Makonda kwa kulipatia jeshi hilo zawadi ya mwaka mpya ya ng’ombe 20. Kushoto ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, Mhe. Makonda na Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu na Utawala wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Bwana Makwaia Makani
  Mhe. Makonda akikagua ng’ombe ambao ametoa zawadi ya mwaka mpya kwa hospitali za Mkoa wa Dar es Salaam, Jeshi la polisi na Jeshi la Ulinzi la Wananchi la Tanzania (JWTZ).
  Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa akizungumza katika mkutano huo baada ya kukabidhiwa zawadi ya ng’ombe 20 kwa ajili ya mwaka mpya 2019. Katikati ni Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Yacoub Hassan Mohamed na Mhe. Makonda.
  Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Makonda kabla ya kutoa zawadi ya mwaka mpya kwa hospitali hizo, JWTZ na jeshi la polisi.
  Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Grace Maghembe akimshukuru Makonda kwa kutoa zawadi ya mwaka mpya kwa hospitali za mkoa huo.
  Baadhi ya ng’ombe wakiwa katika machinjio ya Vingunguti leo baada ya Mhe. Makonda kukabidhi kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Grace Maghembe. Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)


  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa zawadi ya ng’ombe 20 kwa ajili ya mwaka mpya 2019 kwa wagonjwa na wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) pamoja na hospitali za rufaa za Temeke, Ilala na Kinondoni ikiwamo Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI).

  Zawadi hiyo imetolewa kwa wagonjwa waliolazwa katika hospitali hizo pamoja na wafanyakazi ikiwa ni sehemu ya kuwapongeza kutokana na huduma bora ambazo wanazozitoa na hivyo kupunguza malalamiko kutoka kwa wananchi.

  Akizungumza katika machinjio ya Vingunguti, Mkuu wa Mkoa Makonda amewataka watumishi wa hospitali hizo kuongeza juhudi katika sehemu zao za kazi ili Mkoa wa Dar es Salaam uwe namba moja katika kutoa huduma mbalimbali za afya. “Idadi ya malalamiko imepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na huduma za matibabu kuimarika,” amesema Makonda.

  Pia, mkuu huyo wa mkoa ametoa zawadi ya ng’ombe 20 kwa Jeshi la Polisi na ng’ombe 20 kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa ajili ya sikukuu ya mwaka mpya 2019. Katika hatua nyingine, Makonda amesema kwamba Serikali itajenga machinjio ya kisasa na kwamba ujenzi wake utagharimu shilingi bilioni 8.5.

  Amesema lengo la kujengwa kwa machinjio ya kisasa ni kupanua soko la nyama na kwamba jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi huo litawekwa Januari mwakani. Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Grace Maghembe amemshukuru mkuu wa mkoa kwa kutoa zawadi ya mwaka mpya 2019 kwa kuwa itaongeza uwajibikaji katika hospitali hizo.

  Dkt. Maghembe amesema katika juhudi za kuboresha huduma za afya kwa wananchi, mkoa huo kwa kushirikiana na wataalam wa Muhimbili, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na hospitali za wilaya wamefanikiwa kupima afya zaidi ya wananchi 100,000 mkoani Dar es Salaam.

  Pia, amemshukuru kiongozi huyo kwa kuwezesha upatikanaji wa vifaa vya kujifungua kwa kinamama wajawazito.

  0 0

  Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amemtaka mkandarasi anayetekeleza kazi ya ujenzi wa Jengo la Wizara ya Nishati linalojengwa katika Mji wa Serikali, Ihumwa jijini Dodoma kuhakikisha kuwa anakamilisha kazi hiyo kwa wakati uliopangwa.

  Akizungumza katika eneo la Ihumwa Waziri Kalemani amesema kuwa, ili kufanikisha utekelezaji wa kazi hiyo kwa wakati ni vyema mkandarasi huyo ambaye ni Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) akahakikisha kuwa vifaa vyote vinavyotakiwa katika kutekeleza kazi hiyo vinakuwepo katika eneo la kazi.

  “Ni Lazima mkandarasi uhakikishe kuwa matofali, mchanga, simenti, mabati, kokoto, rangi, madirisha, nondo na vifaa vyote vinavyotakiwa hapa kwa ajili ya ujenzi vinapatikana kwa wakati wote katika eneo hili la ujenzi ili kuharakisha utekelezaji wa kazi hii kama ulivyopangwa na si vinginevyo”;

  Akifafanua, Dkt. Kalemani amesema kuwa atakuwa akitembelea eneo hilo mara kwa mara kuona hatua za utekelezaji wa kazi hiyo na kuwaasa watendaji wa Wizara yake kuhakikisha kuwa wanafuatilia kwa karibu kazi husika ili itekelezwe kwa viwango vinavyotakiwa na kwa wakati.

  Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hamisi Mwinyimvua amemtaka mkandarasi huyo kuhakikisha kuwa anaongeza mitambo inayotakiwa katika kutekeleza ujenzi huo ili kuongeza kasi ya utekelezaji.

  Ujenzi wa jengo la Wizara ya Nishati ni utekelezaji wa Agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa Wizara zote kujenga majengo katika eneo hilo la Ihumwa unakojengwa mji wa Serikali unaojumuisha majengo ya Wizara zote.

  0 0

  Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI.

  OFISI ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za mitaa (Tamisemi) imebaini matumizi mabaya ya fedha za serikali Sh. bilioni 2.98 katika halmashauri ya Ulanga mkoani Morogoro na kuagiza wakuu wa idara wote waliohusika wavuliwe nyadhifa zao huku watumishi wengine waondolewe majukumu ili vyombo vya dola viendelee na hatua kwa mujibu wa sheria dhidi yao.

  Hayo yamebainishwa na Waziri wa nchi ofisi ya Rais Twala za mikoa na Serikali za mitaa Mhe. Selemani Jafo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya uchunguzi maalum uliofanywa kwa halmashauri ya wilaya hiyo.

  Jafo alisema kuwa Ofisi ya Rais Tamisemi imefanya uchunguzi maalum katika halmashari 12 nchini ambazo ni Ulanga, Same, Mbulu, Meru, Itigi, Misungwi, Nyang’hwale, Serengeti, Bahi, mpwapwa, Morogoro Dc na Kibaha Tc ambapo katika halamasahuri ya Ulanga uchuguzi ulianza Novemba 13 hadi 23 mwaka huu.

  Alisema uchunguzi huo ulifanyika kufuatia malalamiko ya wanachi mbalimbali pamoja na mbunge wa jimbo la Ulanga Mhe. Goodluck Mlinga kutokana na ubadhirifu uliokuwepo. Aidha alisema kiasi hicho kimebainika kupotea kutokana na matumizi mabaya ya fedha za serikali ambapo watumishi wasio waadilifu katika halmashauri hiyo walikiuka taratibu na kufanya manunuzi hewa na kutumia vibaya fedha kinyume na malengo yaliyopangwa.

  “Halmashauri hii imekuwa ikifanya udanganyifu katika taarifa za miradi ya maendeleo taarifa za mfuko wa wanawake na vijana, kwa ujumla inausimamizi mbovu wa mapato na kuwa na udhibiti hafifu wa makusanyo na matumizi ya fedha za Umma”alisema Jafo. Jafo alisema kuwa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Ulanga, Yusufu Daud Semguruka kwa nafasi yake ya afisa masuhuli alishindwa kusiomamia sheria ya fedha za serikali za mitaa katika kudhibiti na kuweka mifumo dhabiti ya kuhakikisha fedha ziko salama kuanzia makusanyo hadi matumizi yake.

  “Hii ni pamoja na kushindwa kumsimamia mweka hazina wa halmashauri katika kutekeleza majukumu yake na kwa kushindwa kutekeleza majuku hayo amesababisha hasara halmashauri ya shilingi 2,980,172,763.60″alisema Jafo. Alifafanua kuwa Rajabu Siriwa,ambaye alikuwa ni mweka hazina wa halmasahuri hiyo alichangia kuhujumu mapato ya serikali kwa kuweka utaratibu ambao umeisababishia hasara serikali.

  Alisema kuwa mweka hazina huyo aliidhinisha malipo ya sh. 225,586,400 nje ya bajeti bila idhini ya ofisi ya Rais Tamisemi ambapo malipo hayo yalihusisha posho ya safari ya mkurugenzi mtendaji Sh. 192,000,000. “Pia kukusanya mapato na kutoyapeleka benki, katika mfumo wa LGRCIS umeonyesha halmashauri ilikusanya fedha ambazo hazikupelekwa benki kabisa shilingi 760,686,732.43 fedha hizi hazijulikani matumizi yake halisi ni nini”alihoji Jafo.

  Aidha alisema kuwa mweka hazina huyo aliandaa taarifa zenye udanganyifu kwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotumia fedha za makusanyo ya ndani. “Halmashauri imeripoti kupeleka shilingi 301,442,686 uhalisia wamepeleka 113,406,106.34 na udanganyifu katika mfuko wa vijana na akina mama halmashauri inaripoti kupeleka shilingi 120,000,000 uhalisia wamepeleka sh. 31,500,000 kwa mwaka 2017/18 na 2018/19 hadi novemba 2018 wakati uchunguzi unakamilika”alisema

  Aidha Jafo alisema kuwa Mhandisi David Kaijage akiwa anakaimu ofisi ya mkurugenzi februari mosi mwaka huu hadi Februari nane alihusika kwenye kuihujumu halmashauri kwa mapato ya Sh. 470,000,000 yaliyopolelewa kutoka kiwanda cha kilombero Valley Teak Company kwa kuzirejesha kwa mlipaji siku hiyohiyo waliyopokea. “Pia alisaini hati ya malipo kumlipa bahari Phamarcy kwa siku ambayo hakuwa kaimu mkurugenzi na mkurugenzi alikuwepo”alisema.Wakati huo huo Bw. Stanley Godwil Nyange na Bw. Isaack Mwasankope Salumu ambao wote ni wahasibu wameihujumu Halmashauri kwa kutumia akaunti zao binafsi kupokea fedha za makusanyo ya Halmashauri kiasi cha sh 203.398,700 aliongeza.

  Waziri Jafo pia alisema kuwa uchunguzi huo pia umebainisha kuwa Isaack Mwasankope, Salehe Mbogoso pamoja na Johson Mwanyombole ambao wote ni wahasibu wa halmashauri hiyo walihusika kuchukua fedha taslim za makusanyo katika kituo cha kivukoni na kisha kuzitumia bila kuzipeleka Benki sh 168,000,000.

  Yassin Galahenga na Mohamed Majaliwa Saidi wataalam wa mifumo (TEHAMA) walishirikiana na wahasibu kurekebisha Ankara na kufuta madeni bila idhini ya Mkurugenzi alibainisha Waziri Jafo.Waziri Jafo aliongeza kuwa Bw. Willy Ndabila ambaye alikua afisa manunuzi alihusika na manunuzi hewa ya madawa yenye thamani y ash. 73,212,909.40 pamoja na kulipa fedha zaidi yaani sh 146,425,818 huku Goodluck Mbata ambaye ni muhasibu wa hospital aliandaa malipo na kusainisha mara mbili kwa watu tofauti huku akijua kufanya hivyo ni kuandaa malipo mara mbili kwa hitaji moja (double paymet).

  Waziri Jafo aliagiza ofisi ya mkuu wa mkoa wa Morogoro kuhakikisha kuwa wakuu wa idara na vitengo waliohusika akiwemo Willy Ndabila ambaye amehamishiwa itilima,na Rajabu Siriwa ambaye amehamishiwa Gairo wavuliwe nyadhifa zao na mamlaka za nidhamu na vyombo vya dola viendelee na hatua kwa mujibu wa sheria.

  Aliongeza kuwa watumishi wote waliohamishiwa Halmashauri ya ulanga wakiwa na makosa yaani DPMU Willy Ndabila na DT Rajabu Siriwa warejee halamashauri ya Ulanga ili kuiwezesha halmashauri na vyombo vya Dola kufanya kazi yake.“Maelezo juu ya mkurugenzi huyu wa Ulanga yenyewe yatatolewa baadaye na serikali”alifafanua Jafo.

  Hatahivyo Jafo alisema kuwa mkuu wa mkoa wa Morogoro ahakikishe kuwa Ofisi ya Rais Tamisemi imepata maelezo kwanini wataalamu hao hawakuchukuliwa hatua stahiki zenye tija dhidi ya taarifa za mkaguzi wa ndani ya robo ya tatu ya mwaka wa fedha2017/18 kabla ya januari 15 mwakani.


  0 0

  MTOTO Manahil Mundhir Rashid mwenye umri wa miaka mitano (pichani), amepotea kwenye mazingira ya kutatanisha eneo la Mkunazini mjini Unguja Visiwani Zanzibar.

  Baba wa mtoto Mundhir Rashid, amesema kuwa mtoto wake alipotea Oktoba 14, mwaka huu baada ya kushuka kwenye basi wakati akitoka shule.

  “Nipo kwenye mashaka ni zaidi ya miezi miwili sasa sijamuona mtoto wangu sijui yuko wapi na kwenye mazingira gani Mungu wangu.“Binafsi nina mashaka makubwa na usalama wa mtoto wangu na hata mimi na mke wangu. Tumejawa na hofu ni wapi alipo mtoto wetu,” amesema Rashid

  Kutokana na hali hiyo amesema walitoa taarifa Kituo cha Polisi Madema mjini Unguja ambapo lilifunguliwa jalada ya uchunguzi namba MAD/R.B 8011/18.Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa ya polisi ilieleza kuwa tayari mtu mmoja ameshakamatwa Oktoba 17, mwaka huu katika Bandari ya Malindi, Zanzibar kwa kosa hilo la kudaiwa kutorosha mtoto.

  Baba huyo wa mtoto huyo aliwaomba wananchi kwa yeyote atakayemuona atoe kituo kituo chochote cha polisi kilicho karibu yake au awasiliane na baba mzazi wa mtoto huyo kwa namba ya simu 0773044899
  0 0


  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  SHIRIKA la Bima la Taifa Tanzania(NIC) limeshauri kwamba ufike wakati sasa kuwepo na sera ambayo itahimiza mashirika, taasisi na wadau mbalimbali kushiriki kwa vitendo katika mapambano dhidi ya vita ya dawa za kulevya nchini.

  Ushauri huo umetolewa leo Desemba 28,2018 na Ofisa Masoko wa Shirika la Bima la Taifa Tanzania(NIC) Israel Severe wakati wa tamasha la Kataa Mihadarati liloandaliwa na Taasisi ya Binti Filamu chini ya Mwenyekiti wake muigzaji maarufu wa filamu Ndumbagwe Misayo a.k.a Thea .Mgeni rasmi kwenye tamasha hilo alikuwa Naibu Waziri Stella Ikupa.

  "Shirika la Bima la Taifa Tanzania tumeamua kushiriki kwenye tamasha hilo kutokana na kutambua umuhimu wake kwa jamii.Tunajua moja ya jukumu letu ni kushughulika na mambo ya bima lakini kwetu ni muhimu zaidi kuona jamii tunayoihudumia inakuwa salama kiafya.Sote tunatambua athari za matumizi ya
  dawa za kulevya, hivyo tumeamua kushiriki kikamilifu kwenye vita hii ili kukomesha dawa hizo nchini.

  "Tunashauri ifike wakati kuwe na sera ambayo itazungumzia umuhimu wa mashirika na taasisi mbalimbali nazo kushiriki kwenye vita hii ya dawa za kulevya.Hivyo ni wakati muafaka kwa Serikali kuweka sera itakayokwa chachu kwa mashirika na taasisi zote kushiriki kwa vitendo na iwe ni wajibu wetu,"amesema
  Severe.

  Kuhusu tamasha hilo , Severe amesema anaupongeza uongozi wa Binti Filamu kwa uamuzi wake wa kuandaa tamasha hilo lenye lengo la kutoa elimu kuhusu madhara ya matumizi ya dawa za kulevya kwa kushirikisha wadau mbalimbali wakiwamo wao ambao wamedhamiria kwa dhati kukomesha dawa hizo nchini kwetu.

  "Tunawapongeza Binti Filamu kwa kuandaa tamasha hilo ambalo kwetu sisi tunaona ni mwanzo mpya kwa wasanii kuamua kushirikiana na wadau wengine kukomesha dawa za kulevya.Wanastahili kuendelea kuungwa mkono na sisi NIC tutaendelea kuwaunga mkono kadri watakavyokuwa wanaandaa matamasha haya ya kukataa mihadarati,"amesema Severe.

  Kwa upande wa Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi ,Vijana,Ajira na Wenyeulemavu Stella Ikupa ametumia nafasi hiyo kuelezea jitihada zinazofanywa na Serikali kupambana na dawa za kulevya nchini na kwamba tatizo la dawa za kulevya, hivyo unapoona kuna jitihada za wadau lazima utoe pongezi.

  "Tunawapongeza Binti Filamu kwa kuandaa tamasha hilo linalofahamika kwa jina la Kataa mihadarati.Athari za dawa za kulevya kwa namna moja au nyingine zinamgusa kila mtu kwenye jamii yetu.Serikali katika kuhakikisha inakomesha dawa za kulevya iliamua kuunda mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ambayo hakika imefanya kazi kubwa,"amefafanua Ikupa.

  Ametoa ushauri kwa Binti Filamu kuhakikisha katika matamasha yanayokuja waende kwenye mikoa ambayo athari za matumizi ya dawa za kulevya ni kubwa na kwa kufanya hivyo watasaidia kuikoa jamii kupitia elimu ambayo wanaitoa kuhusu madhara yatokanayo na utumiaji wa dawa hizo.Kuhusu mapendekezo ambayo yametolewa na wadau mbalimbali kwenye tamasha hilo yakiwemo ya Serikali kutoa elimu kwa Watanzania kuhusu dawa za kulevya amesema ameyachukua na watayafanyia kazi kwani ni mambo yanayowezekana.

  Akizungumzia tamasha hilo msanii wa muziki wa Bongo Fleva Haruna Kahena Inspekta Haroun amesema kitendo cha Binti Filamu kuandaa tamasha hilo ni wazi wameonesha dhamira njema ya kupambana na dawa za kulevya ambapo kwa sehemu kubwa wapo baadhi ya wasanii wamekuwa wakiyatumia.Wakati huo huo Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania Simon Mwakifamba ambaye pia ni Katibu wa Uenezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam amesema umefika wakati wa kuunga mkono juhudi za Rais Dk.John Magufuli katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya.

  Amesema kuna wasanii wengi wamekuwa wakijihusisha aidha kutumia dawa za kulevya au kugeuzwa makontena wa kubeba dawa hizo kwa maslahi ya wafanyabiashara lakini madhara yake ni makubwa, hivyo umefika wakati wa kukataa kuwa sehemu ya makontena na watumiaji wa dawa hizo.
   Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Stella Ikupa akimkabidhi cheti Bw. Israel Severe ambaye ni Ofisa Masoko wa Shirika la Bima la Taifa Tanzania(NIC) kutokana na mchango wa shirika hilo katika mapambano dhidi ya madawa ya kulevya wakati wa tamasha la (Kataa Mihadarati Festival) lililoandaliwa na tasisi ya Binti Filamu inayoundwa na wasanii wa filamu, tamashahilo limefanyika aktika viwanja vya Barafu Mburahati Foundation jijini Dar es salaam.
  Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Stella Ikupa akimkabidhi cheti Kamishna wa Kitengo cha Tiba na Kinga kutoka Mamalaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Dk.Peter Mfisi kutokana na mchango Mamlaka hiyo katika mapambano dhidi ya madawa ya kulevya wakati wa tamasha la (Kataa Mihadarati Festival) lililoandaliwa na tasisi ya Binti Filamu Foundation inayoundwa na wasanii wa filamu, tamashahilo limefanyika aktika viwanja vya Barafu Mburahati jijini Dar es salaam.
  Bw. Israel Severe ambaye ni Ofisa Masoko wa Shirika la Bima la Taifa Tanzania(NIC) akizungumza katika tamasha hilo lililofanyika kwenye viwanja vya Mburahati Barafu jijini Dar es salaam.
  Kamishna wa Kitengo cha Tiba na Kinga kutoka Mamalaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Dk.Peter Mfisi akizungumza na wananchi waliohudhuria katika tamasha hilo.
  Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fisoo akizungumza na wananchi waliohudhuria katika tamasha hilo.
  Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Stella Ikupa akihutubia wananchi waliofika katika tamasha hilo kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bi. Joyce Fisoo.
  Baadhi ya wasanii wa filamu wakifurahia baadhi ya burudani zilizokuwa zikitolewa katika tamasha hilo.
  Baadhi ya waalikwa wakiwa katika tamasha hilo.
  Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Stella Ikup kushoto, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bi. Joyce Fisoo na Kamishna wa Kitengo cha Tiba na Kinga kutoka Mamalaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Dk.Peter Mfisi wakipunga mikono yao juu wakati msanii Inspector Haroun hayupo pichani alipokuwa akitumbuiza katika tamasha hilo.
  Baadhi ya wasanii wa filamu wakiwa katika tamasha hilo.


  0 0


  Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Julianna Shonza akitoa maelekezo ya mambo ya kuzingatia kabla ya kusimika mitambo ya usikivu kwa Meneja wa Shirika la Utangazaji Taifa (TBC) Kanda ya Kaskazini Bw.Gerald Uisso (hayupo pichani) leo katika Kijiji cha Kwemashai alipotembelea eneo hilo walilosimika mitambo yao wakati wa ziara yake ya kukagua maeneo iliyoko mitambo ya TBC kwa Kanda ya Kaskazini.
  Mtambo wa kurushia matangazo ya Shirika la Utangazaji Taifa (TBC) uliyopo katika Kijiji cha Kwemashai Wilayani Lushoto ambapo Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Julianna Shonza alitembelea eneo hilo leo ikiwa ni ziara yake ya kukagua maeneo iliyopo mitambo ya TBC kufuatia changamoto ya usikivu katika maeneo hayo ya Kanda ya Kaskazini.
  Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (wapili kulia) akitizama mitambo iliyopo Lushoto, (watatu kulia)Meneja wa Shirika la Utangazaji Taifa Kanda ya Kaskazini Bw.Gerald Uisso akimwonyesha mitambo ya kurushia matangazo ya TBC iliyoko katika eneo la Kijiji cha Kwemashai alipofanya ziara yake aliyoifanya leo ya kukagua maeneo yaliyisimikwa mitambo ya TBC kutokana na kuendelea kuwepo kwa kero ya usikivu katika eneo hilo.
  Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akikagua Uwanja wa Michezo wa Sabasaba unaomilikiwa na CCM Wilaya ya Lushoto ambao uongozi wa CCM unautafutia mwekezaji wa kuuendeleza leo alipofanya ziara yake ya kikazi leo Wilayani Lushoto.
  Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akiwashauri viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Lushoto kuuendeleza uwanja wa michezo wa Sabasaba kwa kuomba wataalamu Wizarani wa kuwapa ushauri wa kiutalamu wa namna ya kuboresha uwanja huo alipotembea uwanja huo leo,wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa CCM Wilayani Lushoto Bw.Amiri Shekelata .

  ………………………..

  Na Anitha Jonas – WHUSM,Lushoto -Tanga

  Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo amewataka viongozi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC )kusikiliza ushauri wa wazawa wa maeneo wanayoenda kusimika mitambo yao pale wanapofanya utafiti wa maeneo yatakayofaa kulingana na Jiografia ya eneo husika.

  Mheshimiwa Shonza ametoa kauli hiyo leo Wilayani Lushoto alipotembelea eneo lililowekwa mitambo ya TBC iliyoko katika eneo la Kwemashai kwa lengo la kutaka kubaini changamoto zinazosababisha kutokuwepo kwa usikivu kwa baadhi ya maeneo Wilayani hapo.

  “Changamoto kubwa katika Wilaya hiyo ya Lushoto ni Jiografia ya eneo hilo kwani inamilima mingi sana kati maeneo yake yote hivyo ni vyema mkashirikiana na Halmashauri katika kuelekezana eneo abalo itakuwa na mlima mrefu zaidi kushinda yote ambao utawafaa kwakuweza kusimika mtambo wenu utakao rusha matangazo katika maeneo yote ya Wilaya hii,”alisema Mhe.Shonza.

  Akiendelea kuzungumza katika ziara hiyo Naibu Waziri huyo aliusisistiza uongozi wa TBC kanda ya Kaskazini kuhakikisha wanafanya utafiti huo haraka na kusimika mitambo hiyo mapema kwani lengo la Serikali ni kuhakikisha inakamilisha usikivu kwa mikoa iliyoko karibu na maeneo ya mipakani kabla ya mwaka 2020 na ndiyo maana fedha za bajeti ya kuboresha usikivu zinatolewa kila mwaka.

  Naye Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Bw.January Lugangika alimwomba Naibu Waziri huyo kuzungumza na uongozi wa TBC kuweza kuwapatia mwandishi kwa Wilaya hiyo ya Lushoto kwani kuhusu suala la ofisi tayari wamekwisha muandalia ipo.

  “Tumekuwa tunapata changamoto kubwa ya mwandishi wa TBC kwani inatulazimu kumtumia mwandishi aliyeko Tanga ambaye inamlazimu kusafiri kwa basi kwa mwendo wa masaa matatu hii changamoto kwetu na Wilaya hii inafursa nyingi ya kuzitangaza na tunaamini kuwa TBC wanawza kushirikiana nasi katika kufanikisha hili,”alisema Mhe.Lugangika.

  Kwa upande wa Meneja wa Shirika la Utangazaji Taifa (TBC) Bw.Gerald Uisso alieleza kuwa amapokea maelekezo yote na ofisi yake itahakikisha inazingatia ushauri na kufanikisha zoezi hilo la kuboresha usikivu mapema .

  Pamoja na hayo nae Mwenyekiti wa Chama cha CCM Wilaya ya Lushoto alimweleza Naibu Waziri huyo kuwa chama hicho kimeanzakutafuta mwekezaja wa kuendeleza uwanja wa michezo wa Sabasaba ilikuweza kuuweka katika hali nzuri itakayo faa kwa kutumika katika michezo mbalimbali.

  0 0

  Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma SACP Gemini Mushy amesema kuwa mnamo disemba 27 majira ya jioni Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) katika kambi ya Chandarua iliyopo Wilayani Songea Mkoani Ruvuma askari aitwaye Ssgt Juma Uwesu Mkele akiwa kazini pamoja na raia Veronika Kayombo waliuawa kwa kupigwa risasi na askari wa JWTZ aitwaye Sgt Batisin Philip Samda akitumia bunduki aina ya SMG.

  Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma SACP Gemini Mushy amesema kuwa askari Magereza aitwaye Adam Kunwa ambaye ni mganga katika Zahanati ya ya Gereza la Kitai lililopo Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma akiwa lindoni alijiua kwa kujipiga Risasi kichwani na kufariki na upelelezi wa polisi unaendelea ili kuweza kubaini nini chanzo


  0 0

  DROO ya pili ya kampeni ya matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' inayojulikana kama 'MastaBata', imefanyika tena kwa mara ya pili Ofisi Kuu za Benki ya NMB jijini Dar es Salaam ambapo wateja 20 wengine wamejishindia shilingi 100,000/- kila mmoja.

  Akizungumza katika droo hiyo ya pili leo, Meneja Mahusiano Kitengo cha Kadi, Yusuph Achayo alisema washindi hao 20 wamepatikana baada ya kuchezeshwa droo ya pili ya shindano hilo, na wamebahatika baada ya kufanya malipo mbalimbali kwa kutumia mfumo wa 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass'.

  Akifafanua zaidi Bw. Achayo alisema washindi hao wamepatikana baada ya kuchezeshwa droo iliyojumuisha wateja wote wa NMB waliolipa au kufanya manunuzi kwa kutumia 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' na wao kuibuka washindi.Droo hiyo ya pili iliyofanyika leo inakamilisha jumla ya idadi ya wateja 40 ambao hadi sasa wamejishindia shilingi 100,000/- kila mmoja huku ikiendeshwa kwa wazi na wateja wakipigiwa simu kuarifiwa ushindi wao na baadaye fedha hiyo kuingizwa moja kwa moja kwenye akaunti ya mshindi.

  Aidha aliwaomba wateja wa NMB kuendelea kutumia huduma hiyo, kwani kampeni hiyo inayotarajia kuwazawadia zaidi ya shilingi milioni 100 wateja wa NMB inaendelea.Alisema takribani wateja 200 wa NMB ambao watafanya malipo kwa mfumo wa 'NMB Mastercard au 'NMB Masterpass' watakuwa kwenye uwezekano wa kujishindia zawadi za fedha, simu janja za kisasa 'Samsung S9+' na mwisho washindi wengine 3 kati yao wawili kujishindia safari iliyolipiwa ya mapumziko kwenda Dubai.
  Meneja Mahusiano Kitengo cha Kadi, Yusuph Achayo akizungumza jana kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa droo ya pili ya kampeni ya matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' inayojulikana kama 'MastaBata' Bodi. Kushoto ni Meneja Mahusiano Selcom Sebastian Msuya akifuatilia zoezi hilo.
  Meneja Mahusiano Kitengo cha Kadi, Yusuph Achayo akizungumza jana kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa droo ya pili ya kampeni ya matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' inayojulikana kama 'MastaBata' Bodi. Kushoto ni Meneja Mahusiano Selcom Sebastian Msuya na Meneja NMB Kitengo cha Kadi, Stephene Jilala (kulia) wakifuatilia zoezi hilo.
   

  0 0


  Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza kuhusu ofisi yake kuunga mkono kwa vitendo kampeni ya kulifanya jiji la Dodoma kuwa la kijani iliyozinduliwa na Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan mara baada ya watumishi wa ofisi yake (hawapo pichani) kukamilisha zoezi la upandaji miti katika ofisi inayojengwa Ihumwa kwenye mji wa serikali jijini Dodoma.  Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Mathew Kirama akishiriki katika zoezi la upandaji miti Ihumwa katika mji wa serikali jijini Dodoma, eneo ambalo Ofisi ya Rais-Utumishi inajengwa ili kutoa huduma kwa umma.  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Musa Joseph akishiriki kuchimba mashimo kwa ajili kupanda miti Ihumwa katika mji wa serikali jijini Dodoma, eneo ambalo Ofisi ya Rais-Utumishi inajengwa ili kutoa huduma kwa umma.  Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakiwa tayari kupanda miti katika ofisi inayojengwa Ihumwa kwenye mji wa serikali jijini Dodoma ili kuunga mkono kwa vitendo kampeni ya kulifanya jiji la Dodoma kuwa la kijani, iliyozinduliwa na Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan Julai 21,2017.

  ………………………………………………………………………………………..

  Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imeunga mkono kwa vitendo kampeni iliyozinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kulifanya jiji la Dodoma kuwa kijani kwa kupanda miti katika ofisi yake inayojengwa Ihumwa jijini Dodoma kwenye mji wa serikali.

  Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro mara baada ya watumishi wa ofisi yake kukamilisha zoezi la upandaji wa miti katika mji wa serikali Ihumwa, eneo ambalo Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora inajengwa ili kutoa huduma kwa umma.

  Dkt. Ndumbaro amesema kuwa, zoezi la upandaji wa miti katika eneo hilo ni endelevu na kuongeza kuwa, Ofisi yake itahakikisha miti hiyo inatunzwa kwa kuimwagilia maji ili hatimaye kuwe na mandhari ya kijani pindi ofisi yake itakapokamilisha ujenzi wa jengo kubwa.

  Naye, mmoja wa watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Menyeaichi Koka ameongeza kuwa, watumishi wa Ofisi ya Rais – Utumishi wameitikia wito wa Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan wa kupanda miti ili kulifanya jiji la Dodoma kuwa kijani na kuishukuru menejimenti ya ofisi kwa kusimamia vema zoezi hilo ambalo kila mtumishi amelifanya kwa hiyari na kwa moyo mkunjufu.

  Bi. Koka ahaidi kuwa, atahakikisha mti alioupanda anauhudumia vizuri kwa kuumwagilia maji ya kutosha ili uweze kustawi vizuri na kuwa ni miongoni mwa miti iliyopandwa na kufanikiwa kukua vizuri na hatimaye kuchangia jiji la Dodoma kuwa kijani.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan alizindua kampeni za kulifanya jiji la Dodoma kuwa kijani Julai 21, 2017 kwa kuongoza zoezi la upandaji wa miti ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono kwa vitendo uamuzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli wa kuhamishia Makamo Makuu ya Nchi kutoka Dar es Salaam kuja jijini Dodoma.

  0 0


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua uboreshaji wa Mandhari ya eneo la kupumzikia la Chinangali jijini Dodoma, wakati alipokagua Mradi wa Uendelezaji wa Miji ya Kimkakati katika Jiji hilo, Desemba 29, 2018. Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge na kulia ni Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Gowin Kunambi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Maegesho ya Malori Makubwa katika eneo la Nala jijini Dodoma, wakati alipotembelea Mradi wa Uendelezaji wa Miji ya Kimkakati katika jiji la Dodoma, Desemba 29, 2018. Watatu kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde na wapili kushoto ni Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Godwin Kunambi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Maegesho ya Malori Makubwa katika eneo la Nala jijini Dodoma wakati alipotembelea Mradi wa Uendelezaji wa Miji ya Kimkakati katika jiji hilo, Desemba 29, 2018. Watatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge na kulia ni Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Godwin Kunambi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua utekelezaji wa agizo alilolitoa Oktoba 21, 2018 kwa uongozi wa jiji la Dodoma la kubomoa uzio wa mabati uliojengwa kwenye eneo la wazi lililotengwa kwa ajili ya kuchezea watoto na kuziba barabara ya tisa katika Mtaa wa Mji Mpya Kata ya Madukani jijijini Dodoma. Mheshimiwa Majaliwa alikuwa katika ziara ya kukagua Mradi wa Uendelezaji Miji ya Kimkakati katika jiji la Dodoma, Desemba 29, 2018. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Godwin Kunambi, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  ………………………………………………………………………………….

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea Mradi wa Uendelezaji wa Miji ya Kimkakati katika jiji la Dodoma na kukagua ujenzi wa maegesho ya malori makubwa katika eneo la Nala na uboreshwaji wa mandhari ya eneo la kupumzikia la Chinangalijijini Dodoma.

  Pia amemuagiza Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Godwin Kunambi andelee kutenga maeneo ya mapumziko ili wananchi wapate sehemu za kukutana na kubadilishana mawazo baada ya kumaliza kufanya kazi. Waziri Mkuu amekagua maeneo hayo leo (Jumamosi, Desemba 29, 2018) ambapo ameupongeza uongozi wa jiji la Dodoma kwa kubuni wazo hilo na kusema kwamba ni muhimu kwa miji mikubwa kutenga maeneo ya kwa ajili ya mapumziko.

  Amesema lazima jiji la Dodoma lipangwe kisasa na amewataka wahandisi wahakikishe maeneo ya mapumziko yatengwa na yanatumika kama ilivyokusudiwa. Pia amemtaka Mkurugenzi wa Jiji, Kunambi aendelee kusimamia ujenzi wa kimkakati ndani ya jiji hilo. ”Hatuwezi kuwa tumejaza nyumba kila eneo, watu hawana mahali pa kupumzika na kukutana na marafiki zao plan ya Chinangali Park ni nzuri, Jiji la Dar es Salaam plan ya awali kulikuwa na maeneo ya mapumziko lakini watu wa Idara ya Ardhi waliyauza.”

  Katika hatua nyingine,Waziri Mkuu amekagua utekelezaji wa agizo alilolitoa Oktoba 21, 2018 kwa uongozi wa jiji la Dodoma la kubomoa uzio wa mabati uliojengwa kwenye eneo la wazi lililotengwa kwa ajili ya kuchezea watoto na kuziba barabara ya tisa katika Mtaa wa Mji Mpya Kata ya Madukani jijijini Dodoma. Waziri Mkuu amesema ameridhishwa na utekelezwaji wa agizo lake baada ya kutembelea eneo hilo na kukuta uzio umebomolewa na sasa kuna bustani iliyojengwa kwa ajili ya mapumziko na pia barabara imefunguliwa na wananchi wanaendelea kuitumia kama ilivyokuwa awali.

  Uzio huo ambao mbali na kujengwa katika eneo la wazi lililotengwa kwa ajili ya kuchezea watoto kwenye mtaa wa Mji Mpya kata ya Madukani pia uliziba barabara ya tisa, hivyo kusababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa barabara hiyo. Waziri Mkuu ameendelea kusisistiza uongozi wa jiji kutenga ardhi na kupima viwanja kwa ajili ya matumizi mbalimbali yakiwemo ya biashara, makazi, taasisi, huduma za jamii, viwanda pamoja na maeneo ya wazi kwa ajili ya mapumziko.

  Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma amesema jiji la Dodoma ni miongoni mwa majiji manane nchini yanayotekeleza mradi wa uboreshaji wa miji ya kimkakati unaofadhiliwa na Serikali kupitia mkopo wa Benki ya Dunia. Amesema katika jiji la Dodoma mradi huo unahusisha ujenzi wa miundombinu ya barabara katika maeneo ya Kikuyu, Chidachi, Kinyambwa, Itega, Njedengwa, Mapinduzi, Ilazo, Ipagala, Chamwino, Kilimani, Majengo, Mlezi pamoja na maingilio na stendi kuu ya mabasi na soko kuu zenye jumla ya urefu wa kilomita 26.6.

  Mkurugenzi huyo amesema barabara hizo zinajengwa kwa kiwango cha lami, pia zitawekwa taa za barabarani takriban 925 zinazotumia mfumo wa umeme wa jua. Hata hivyo mradi huo utahusisha ujenzi wa kituo cha maegezo ya malori makubwa takribani 300 katika eneo la Nala.

  Ameongeza kuwa mradi huo unahusisha ujenzi wa kituo kikuu cha mabasi na soko kuu katika eneo la Nzuguni, ujenzi wa vituo sita vya watembea kwa miguu, ujenzi wa vizimba saba vya kukusanyia taka ngumu, uboreshaji wa mandhali ya eneo la kupumzikia katika eneo la Chinangali na ujenzi wa mtaro wa maji ya mvua wenye urefu wakilomita 6.5 katika eneo la Ipagala.

  0 0

  Na Mwandishi Wetu,Calabar, Nigeria

  Mnenguaji nyota wa muziki wa dansi Mtanzania, Hassan Mussa 'Super Nyamwela' na bendi yake Ubuntu Traditional juzi alifanikiwa kuwachengua maelfu ya watu waliofurika katika shamra shamra za tamasha la kimataifa Calabar Carvinal Festival, linalofanyika mjini Calabar nje kidogo ya jiji la Abuja nchini Nigeria.

  Nyamwela na bendi yake walitumia fursa ya dakika tatu walizopewa na waandaji wa tamasha hilo Serikali ya Nigeria kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii ili wasalimie tu na kuangusha shoo ya nguvu iliyofanya washangiliwe kwa nguvu.

  Maelfu ya watu waliojipanga pembezoni mwa barabara za mji wa Calabar waliwashangilia wasanii hao kwa namna walivyoamsha dude na kusababisha gumzo.

  Ubuntu ilitumia nafasi hiyo kuonyesha watanzania wamekuja Calabar kwa ajili ya kutangaza utamaduni wa Tanzania na si kutalii hivyo kipande cha shoo hiyo ni sehemu ndogo ya makubwa waliyojiandaa kuyafanya siku ya kupanda jukwaani rasmi ambayo ni leo usiku wa Jumamosi Desemba 29.

  Hii ni mara ya pili kwa Nyamwela na bendi yake ya Ubuntu kushiriki tamasha hilo ambalo linashirikisha nchi zaidi ya 60 duniani.Kwa Tanzania ni Ubuntu pekee ndiyo imepata nafasi ya kutumbuiza katika tamasha hilo ambalo hufanyika kila mwaka kwa udhamini wa serikali ya Nigeria ambayo imekuwa ikilitumia kutangaza utalii wa nchi yake.

  Tamasha hilo lilianza rasmi Desemba 4 mwaka huu na linatarajia kufikia tamati Januari 4 mwaka 2019.
   Mnenguaji nyota wa muziki wa dansi Mtanzania, Hassan Mussa 'Super Nyamwela' na bendi yake Ubuntu Traditional juzi alifanikiwa kuwachengua maelfu ya watu waliofurika katika shamra shamra za tamasha la kimataifa Calabar Carvinal Festival, linalofanyika mjini Calabar nje kidogo ya jiji la Abuja nchini Nigeria.
   
  Baadhi ya Wananchi wakifuatilia onesho hilo

  0 0


  Tamasha kubwa la mkesha wa kufunga 2018 na kufungua mwaka 2019 linatarajiwa kufanyika Desema 31 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

  Mkesha huo utakaokuwa wa aina yake unatarajia kumdondosha Mwanamuziki wa nyimbo za injili kutoka nchini Nigeria anaejulikana kwa jina la Chris Shalom, anayetamba na wimbo wake maarufu uitwao 'my beautifier' na nyingine nyingi.

  Pamoja Na Chris Shalom pia waimbaji wengine mbalimbali mahiri kutoka hapa nchini akiwemo Jesica Honore, Goodluck Gosbert, Joel Lwaga Na John Lisu wanatarajiwa kutumbuiza katika mkesha huo.

  Mkesha wa mwaka 2019 umeandaliwa na Nabii (prophet) Clear Malisa wa Passion Java ministry, kutoka ubungo kibangu jijini Dar es Salaam.Waigizaji/wachekeshaji na watu maarufu mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania wanatarajiwa pia kuwepo akiwemo Pastor Kuria kutoka show ya churchchill nchini Kenya.

  Katika tamasha hilo hakuna kiingilio na usafiri utatolewa kwa watu wote katika vituo vyote vikubwa vya usafiri Dar es Salaam.Mkesha wa mwaka 2019, umedhaminiwa Na Clouds media group, Elishadai shopping center Na Fair Travel adventures.


older | 1 | .... | 1762 | 1763 | (Page 1764) | 1765 | 1766 | .... | 1898 | newer