Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1761 | 1762 | (Page 1763) | 1764 | 1765 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Mlezi wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Time to help, Remziye Talu akifungua bomba la maji jana, ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa kisima cha maji katika shule ya sekondari Kibwegere ambacho kimejengwa na taasisi hiyo, Kibamba, Dar es Salaam.
  Mlezi wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Time to help, Remziye Talu akifungua bomba la maji jana, ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa kisima cha maji katika shule ya sekondari Kibwegere ambacho kimejengwa na taasisi hiyo, Kibamba, Dar es Salaam.
  Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Kibwegere (wa kwanza kushoto), Mkuu wa Shule ya Sekondari Kibweheri, Alexandra Ngonyani na Naibu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kibwegere, Halima Mgaya, wakimshukuru mlezi wa taasisi ya Time to help, Remziye Talu (kulia) mara baada ya uzinduzi wa kisima kilichojengwa na taasisi hiyo katika shule ya sekondari Kibwegere
  Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kibwegere wakipewa madaftari na zawadi zingine kutoka kwa wahisani wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Time to help mara baada ya uzinduzi wa kisima cha maji katika Shule ya Sekondari Kibwegere, jana. Taasisi hiyo imekabidhi visima vya maji vitatu katika shule za sekondari Kibweheri , Kibwegere shule ya msingi Kibwegere.

  Mkuu wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Time to help, Kubilag Talu (katikati), akivishwa skafu na kijana wa skauti mara baada ya kuwasili katika viwanja vya shule ya sekondari Kibwegere alipokwenda kukabidhi visima vitatu kwa shule tatu tofauti zilizopo katika eneo hilo, vilivyochimbwa na taasisi yake, Kibamba jijini Dar es Salaam. Picha na Joseph Zablon
  Naibu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kibwegere, Halima Mgaya (Kulia), akizungumza jana wakati wa hafla ya kukabidhiwa visima vitatu vilivyochimbwa na wahisani wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Time to help, jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni mkuu wa taasisi hiyo, Kubilag Talu. Picha na Joseph Zablon
  Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kibwegere wakitumbuiza wakati wa uzinduzi wa kisima cha maji katika Shule ya Sekondari Kibwegere, Kibamba jijini Dar es Salam ambacho kimejengwa na wahisani wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Time to help. Taasisi hiyo imechimba visima vya maji katika shule za sekondari Kibwegere, Kibweheri na shule ya msingi, Kibwegere. Picha na Joseph Zablon
  Skauti wakionyesha uwezo wao katika mchezo wa sarakasi wakati wakitumbuiza jana, wakati wa uzinduzi wa visima vitatu vilivyochimbwa na wahisani wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Time to help, jijini Dar es Salaam.

  Joseph Zablon

  Shirika lisilo la kiserikali la Time to Help limekabidhi visima vitatu kwa shule tofauti za wilaya mpya ya Kibamba, jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya mpango wa taasisi hiyo kusaidia shule za msingi na sekondari nchini katika kukabili changamoto tofauti.

  Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo kwa shule za sekondari Kibwegere, Kibweheri na shule za msingi Kibwegere, leo Mkuu wa tasisi hiyo Kubilaty Talu alisema wametoa msaada huo baada ya kuombwa kufanya hivyo.

  Alisema tasisi hiyo imelenga kuzisaidia shule mbalimbali nchini kukabili changamoto ya mahitaji ya maji na visima hivyo anaamini vitabadili mazingira na kuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi wa shule hizo tatu ambao pia walipewa zawadi za madaftari.

  awali Naibu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kibwegere, Halima Mgaya alisema visima hivyo vitasaidia mengi ikiwa ni pamoja na kulinda afya za watoto kutokana na uhaba wa maji hivyo pia kuwaepusha na magonjwa yanayotokana na uhaba wa maji safi na salama.

  Katika risala ya wanafunzi wa sule hiyo hizo ambayo iliwasilishwa kwa mtindo wa ngonjera, wanafunzi wa shule hizo waliomba msaada wa vyumba zaidi vya madarasa kutokana na uhaba uliopo na wameshukuru kupata huduma ya maji.

  Walisema ukosefu wa maji safi na salama ulisababisha baadhi ya wanafunzi kuugua magonjwa ya matumbo mara kwa mara kutokana na kutumia maji ya kunywa yasiyo safi wala salama.  0 0


  Askofu mkuu wa Tanzania Assemblies of God (TAG) Dkt. Barnabas Mtokambali amesema Mwenyezi Mungu anapenda maadhimisho kwa kuwa ni sehemu ya kujifunza, kumsifu, kujenga ushirika na kumtolea shukran. Dkt. Mtokambali amebainisha hayo Mjini Dodoma, kwenye sherehe za maadhimisho ya mchungaji Vangast Salum wa kanisa la TAG, kwa kutimiza miaka 40 ya wokovu na 36 ya huduma na kuweka wakfu kitabu.
  Amesema moja ya sababu za maadhimisho ni kujifunza, akitolea mfano mchungaji Vangast Salum, amepitia hatua mbalimbali za maisha na kiuchungaji na kwamba maadhimisho pia yanajenga ushirika zaidi na Mwenyezi Mungu kwa kuwaleta watu karibu.

  Kiongozi huyo wa juu wa kanisa la TAG Tanzania amesema kuwa sababu ya tatu ya maadhimisho ni kumsifu Mwenyezi Mungu kwa yote aliyoyafanya juu ya maisha ya mchungaji Vangast Salum kwa kipindi cha miaka 40 ya wokovu, na kumtaka kutoa shukran za kumsifu Mwenyezi Mungu.
  Wakati huo huo Askofu mkuu wa Tanzania Assemblies of God (TAG) Dkt. Barnabas Mtokambali amepata fursa ya kuzindua vitabu 500 vya mafundisho ya dini na uzinduzi wa jengo la darasa na Ofisi ya mchungaji wa kanisa hilo eneo la Area D Mjini Dodoma.

  0 0

  Na Ripota Wetu, Globu ya jamii

  MKUU wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Kizigo amezungumzia ziara ya kikazi ambayo imefanywa na Naibu Waziri wa Kilimo Innocent Bashungwa wilayani humo kwa lengo la kuangalia hali ya kilimo hasa kipindi hiki cha msimu wa kilimo kwa mwaka 2018 /2019.

  Akizungumza na Michuzi Blog , Mkuu wa Wilaya Sophia Kizigo amesema Bashungwa akiwa kwenye wilaya hiyo alipata nafasi ya kuzungumza na wakulima kuhusu hali ya kilimo kwa mwaka huu, pia alipata nafasi ya kuangalia iwapo mbolea imefika kwa wakati au laa.

  Kizigo amesema kwenye suala la mbolea, Naibu Waziri wa Kilimo alipata nafasi ya kwenda kwa wasambazaji wakubwa wa mbolea ambapo alikutambolea imefika kwa wakati na ipo ya kutosha na baada ya hapo akaenda kwawakulima ambako nako alikuta mbolea haina tatizo.

  "Hata hivyo kwa wakulima wa tumbaku wao wamenunua na kuanza kuitumia mbolea bila tatizo, ila kwa wakulima wa mahindi wengi wao licha ya mbolea kufika kwa wakati wameshindwa kuinunua kutokana na changamoto yakifedha.Sababu kubwa ya kutokuwa na fedha ya kununulia imetokana na beiya mahindi kwa msimu uliopita kuwa chini kwani kilo ya mahindi ilifikia Sh.200.

  "Hivyo wengi hawajanunua ingawa tayari wameshapanda mahindi,ila kinachoonekana watanunua mbolea kwa ajili ya kukuzia mahindi.Tunafahamu Wilaya ya Namtumbo inaongoza kwa kilimo na hasacha mahindi ambayo mengi yanatoka wilayani kwetu,"amesema Mkuu waWilaya Kizigo wakati anaelezea ziara hiyo ambayo imefanywa na Naibu Waziri wa Kilimo Bashungwa.

  Pia amesema akiwa humo amepata nafasi ya kutembelea wakulima kwabaadhi ya kata na kujionea hari ya wakulima hao katika kuandaa mashamba yao ambapo wengi wao wameshapanda kwani tayari msimu wa kilimoulishaanza ndani ya wilaya hiyo.

  Akizungumzia maandalizi ya kilimo wilayani humo ,Kizigo amesema amefurahishwa na juhudi ambazo zinafanywa na wakulima katika kuhakikisha wanautumia vema msimu huu kwa kuandaa mashamba mapemana kwamba wengi wao wameshapanda mbegu kwani msimu wa kilimo umeshaanza katika wilaya hiyo.
   MKUU wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Kizigo akiwa ameambatana na mgeni wake Naibu Waziri wa Kilimo Innocent Bashungwa pamoja na viongozi mbalimbali wa wilaya hiyo kwa pamoja wakitembelea mashamba ya mahindi katika vijiji mbalimbali kikiwemo kijiji cha Namanguli,kata ya Luchili wilayani Namtumbo
   Naibu Waziri wa Kilimo Innocent Bashungwa  akimsikiliza mmoja wa wakulima alipokuwa akizungumza nae kuhusu suala la upatikanaji wa mbolea,masoko na namna kilimo cha mahindi kinavyokwenda,kulia kwa Naibu Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mh Sophia Kizigo.
   Naibu Waziri wa Kilimo Innocent Bashungwa akimsikiliza Afisa Kilimo wa Wilaya alipokuwa akizungumza nae kuhusu namna ya wakulima wa Mahindi wananvyoandaa mashamba yao na kwa kiwango gani wanavuna mazao yao,na kwamba Mkulima anatakiwa alime heka ngapi ili asipate hasara,ambapo Afisa huyo alieleza kuwa Mkulima ili asipate hasara katika kilimo chake anapaswa kulima heka nne ili apate faida.
  Naibu Waziri wa Kilimo Innocent Bashungwa  pichani kulia akiwa sambamba na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mh Kizigo na wadau wengine wakikagua Shamba la mahindi katika kijiji cha Suluti kata ya Namtumbo.
   Ukaguzi wa shamba la tumbaku katika kijiji cha Suluti kata ya Namtumbo
   Wananchi walisimamisha msafara wa Naibu Waziri wa Kilimo Innocent Bashungwa katika kata ya Luchili kijiji cha Namanguli wakitaka wasikilizwe kero zao.
   Ukaguzi wa maduka ya pembejeo kuangalia mwenendo wa biashara na bei elekezi kama inazingatiwa ulifanyika pia.

  0 0  Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Meru Elizabeth Mohere akikabidhi Kadi ya Bima kwa Bi.Maria Solomon ,kadi hizo zimetolewa na Kituo cha Huduma ya Wazee Sakila  Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Meru Elizabeth Mohere akikabidhi Kadi ya Bima mmoja wa wazee kwenye kituo cha Huduma ya wazee Sakila
  Na. Vero Ignatus Arusha


  Jumla ya Wazee 264 katika Wilaya ya Meru mkoani Arusha wamepatiwa kadi za bima ya afya zitakazowawezesha kupata huduma za afya katika vituo mbali mbali vya afya hivyo kuboresha ustawi wa maisha ya wazee.

  Akikabidhi Bima hizo kwa wazee wanaohudumiwa na kituo cha Huduma ya Wazee Sakila kilichopo wilayani hapo ,Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Meru Elizabeth Mohere alisema kuwa kadi hizo zitawawezesha kupata matibabu kwa mwaka mzima kwa gharama nafuu.

  Elizabeth Alisema kuwa kuna uhitaji mkubwa wa kuwekeza kwenye afya za wazee kwani ni kundi muhimu katika jamii ambalo linapaswa kupawa kipaumbele kwenye huduma za kijamii.. "Ni muhimu kutunza kadi hizi muweze kufika nazo na kupewa matibabu ,tunawashukuru wadau kwa kujitoa kuhudumia wazee kwani serikali haiwezi kufanya kila kitu"

  Alisema Mratibu wa kituo cha huduma ya wazee sakila, Hamphrey Mafie alisema kuwa wazee hao wanapaswa kutunza kadi hizo zitazowawezesha kupata huduma za afya bure bila kulipia . Mafie anaeleza kuwa shirika la Dorcas International limewawezesha wazee kupata bima za matibabu pamoja na zawadi za sikukuu za krismas na Mwaka mpaya ambapo wazee walipatiwa chakula,mavazi pamoja na mahitaji mengine .

  Kwa Upande wake Mzee anayehudumiwa na kituo hicho Maria Solomon ameishukuru kituo hicho kwa kuwajali na kuwathamini kwani wazee hao walikua na changamoto ya matibabu kutokana na uwezo mdogo wa kifedha hivyo watapata fursa ya kutibiwa .

  0 0

  Afisa Muuguzi Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Happy Msemwa (kulia) akuzungumza jambo na Jane Mathias (30) mkazi wa Sinza aliyejifungua mtoto wa kiume usiku wa Desemba 25, 2018, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).  
  Jane Mathias (30), akimnyonyesha mtoto wake, Noel Alphonce mara baada ya kujifungua katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa njia ya kawaida akifurahi na kumshukuru Mungu. "alisema" 

  Nina kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kuniwezesha kumpata mtoto wa Kiume kwa njia ya kawaida na nipende  kuwashukuru Madaktari na wauguzi kwa huduma zao nzuri.  
   Mkunga katika mafunzo taraji Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Shukuru Siame akimpatia huduma, Asina Mkumba (29) mkazi wa Mbezi kwa Msuguri ambaye alijifungua mtoto wa kiume kwa njia ya upasuaji katika  Hospitalini hapo na kuzungumza na Muuguzi Mwandamizi Idara ya akina mama na watoto wachanga wa Hospitali hiyo, Mariam Mlawa "alisema" 

  Nashukuru Mungu watoto waliozaliwa katika usiku wa kuamkia mkesha wa Krismas Desemba 25, 2018, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ni watano.

  Kati ya hao wawili walizaliwa kwa njia ya upasuaji, Wakiume na wakike na kwanjia ya kawaida watatu, wawili wa kike na wakiume mmoja na halizao kwa ujumla zinaendelea vizuri. 

  Katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala, Muuguzi wa zam ambaye hakupenda kutaja jina lake "alisema" 

  Watoto waliozaliwa mkesha wa kuamkia Desemba 25, 2018,  ni Kumi na mbili, wakiume Tisa na Wakike 3 kati ya hao ni mapacha
  Afisa Muuguzi Msaidizi Hospitali ya Rufaa Temeke, Hadija Kamote (kulia) akimwelekeza jambo, Aisha Saiboko mkazi wa Maji Matitu Mbagala aliyejifungua kwa njia ya upasuaji usiku wa kuamkia mkesha wa Krismas katika Hospitali hiyo ambapo alijifungua mtoto wa kiume. 
  Afisa Muuguzi Msaidizi Hospitali ya Rufaa Temeke, Hadija Kamote (kulia) akimsaidia, Arafa Juma (27) kumuelekeza jinsi ya ubebaji mara atakapokuwa akiwanyonyesha watoto wake ambao walizaliwa katika mkesha wa kuamkia Desemba 25, 2018. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)

  0 0


  Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza jambo kuhusu upatikanaji wa umeme katika jimbo la Vwawa wakati akiwa katika ziara ya kikazi jimboni kwa ajili ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi. (Picha Zote Na Mathias Canal)
  Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza jambo kuhusu upatikanaji wa umeme katika jimbo la Vwawa wakati akiwa katika ziara ya kikazi jimboni kwa ajili ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi.

  Baadhi ya wananchi wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe wakifatilia mkutano wa Mbunge wa jimbo hilo ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga wakati akiwa katika ziara ya kikazi jimboni kwa ajili ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi.  Na Mathias Canal, Songwe

  Serikali imesema hakuna kijiji nchini kitakachoachwa bila ya kuunganishiwa umeme katika awamu ya tatu ya mradi unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (Rea).

  Aidha, Serikali imetenga Sh1 trilioni kwa ajili ya kusambaza umeme katika vijiji 8,000 ambavyo bado havijaunganishiwa na nishati hiyo huku ikiendela na uwekaji wa umeme katika vijiji zaidi ya 13400.

  Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe Mhe Japhet Hasunga amewahakikishia wananchi kuhusu upatikanaji wa umeme katika jimbo hilo hivyo wananchi wanapaswa kuondoa wasiwasi na serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli.

  Mhe Hasunga ameyasema hayo wakati wa mikutano yake katika kijiji cha Igale na Iyula A vilivyopo katika kata ya Iyula akiwa katika ziara ya kikazi jimboni humo iliyoanza juzi tarehe 22 Octoba 2018.

  Alisema kuwa upatikanaji wa umeme katika jimbo lake utasaidia kuongeza upatikanaji wa huduma mbalimbali za kijamii na kuwa chachu ya maendeleo kwa wananchi na Taifa kwa ujumla wake.

  Alisema kuwa utekelezaji wa Miradi hiyo ya umeme katika Jimbo la Vwawa unaenda sambamba na lengo la Serikali ya awamu ya Tano ya kuwa na uchumi wa kati kupitia viwanda ifikapo 2025.

  Mhe Hasunga amewataka wananchi hao kutumia fursa mbalimbali zitakazotokana na utekelezaji wa miradi katika sekta ya gesi na mafuta ili kujiongezea kipato na kuiwezesha nchi kutimiza malengo yake kuelekea kuwa nchi ya uchumi wa kati.

  Kuhusu malalamiko ya wananchi dhidi ya gharama kubwa za pembejeo za kilimo, Mhe Hasunga ambaye ni Waziri wa Kilimo amewahakikishia wananchi kuwa wizara yake imejipanga kuhakikisha kuwa mbolea zinapatikana kwa wakati ili wakulima wa mazao mbalimbali ya chakula na biashara waweze kunufaika na pembejeo hizo.

  Alisema kuwa kumekuwa na malalamiko mengi nay a muda mrefu kuhusu mbolea hivyo serikali itapitia upya utaratibu wa uuzaji wa mbolea ili kutafuta namna bora ya kurahisisha huduma hiyo kwa wakulima nchini.

  0 0

  Miongoni mwa vitu vilivyokuwa vikirudisha nyuma maendeleo ya kilimo ni wadudu wanaobangua nafaka, pamoja na wakulima wengi kujikita katika upuliziaji dawa ya kuzuia wadudu hao bado haikuzuia wadudu kushambulia nafaka kavu kwa asilimia 100.

  Kero hiyo ilisababisha wakulima kulazimika kuuza nafaka hizo kwa bei ya hasara ili mradi kukwepa usumbufu wa kupuliza dawa na wengine kuuza nafaka hizo kwa bei ya kupangiwa na wachuuzi wakihofia zitakapokaa muda mrefu zitapoteza ubora wake wa awali.

  Kero hiyo iliwasumbua wakulima wengi katika nchi za Kiafrika, kabla ya wasomi wa Chuo Kikuu cha Purdue cha Marekani ambacho kilifanya utafiti katika nchi za Afrika Magharibi na kisha kuanzisha teknolojia mpya ya kuhifadhi nafaka kwa kutumia mifuko maalumu ya tabaka tatu kwenye nchi ya Cameroon.

  Wasomi wa chuo hicho walitengeneza mifuko hiyo maalumu ya kuhifadhi nafaka iliyopewa jina la Purdue Improved Crops Storage (PICS) ambayo ni mahususi kwa kuhifadhi nafaka kavu bila kutumia kemikali.“Tanzania teknolojia ya PICS ilianza mwaka 2014 ambapo kiwanda cha PEE PEE Tanzania Limited (TTTL) cha Tanga kilipata kibali cha kutengeneza mifuko hiyo.

  “Wakati unaingia nchini, tayari mradi huo ulikuwa umeenea katika nchi za Afrika Magharibi na Mashariki ya mbali ukifanyika chini ya ufadhili wa Taasisi ya Melinda and Gates Foundation,” anasema meneja mradi wa PICS Tanzania, Ladislaus Ngingo.

  MATUMIZI YA MIFUKO YA PICS

  Ngingo anasema tofauti ya mifuko ya PICS na mingine ya salfeti ni kwamba ile ya PICS imetengenezwa maalumu kwa ajili ya kuhifadhia nafaka kavu bila kubanguliwa na wadudu kwa zaidi ya miezi sita na mkulima hatohitaji kupulizia dawa nafaka atakazohifadhi kwenye mifuko hiyo.

  “Katika kipindi chote hicho nafaka zitaendelea kubaki katika ubora ule ule kama kwamba ndiyo zimetolewa shambani muda huo, mifuko hii ina nailoni mbili ndani ambazo ni nzito kila moja ina ‘macron’ 80 ambazo zina upekee katika kuhifadhi nafaka kavu,” anasema Ngingo.


  Familiya kijijini Mnenia, Wilayani Kondoa ikitoa ushuhuda wa usalama wa mahindi yao. Yalihifadhiwa miaka miwili, na mifuko ya PICS.


  TEKNOLOJIA YA MAWASILIANO ILIVYORAHISISHA UPATIKANAJI PICS

  Mbali na wasomi wa Purdue kubuni teknolojia ya uhifadhi nafaka, watengenezaji wa mifuko hiyo nchini wamebuni njia rahisi ya kuwarahisishia wakulima kupatikana kirahisi mifuko hiyo kote nchini.

  Meneja Masoko wa PICS Tanzania, Thompson Mwakibinga anasema wamewarahisishia wakulima kwa kushirikiana na mitandao ya simu za mkononi ya Tigo na Airtel.“Unaweza kupata mifuko ya PICS au taarifa kuhusu mifuko hii kwa kubonyeza nyota 149 nyota 26 nyota 5 reli kisha unabonyeza kitufe cha kupiga simu ambapo itakuletea njia mbili za kuchagua, kwanza ni kutafuta wauzaji na nyingine ni kupata taarifa za PICS.

  “Kama nilivyotangulia kueleza awali, teknolojia hii inawahusu watumiaji wa mitandao ya Tigo na Airtel na ukichagua kipengele cha kutafuta wauzaji, itakuletea majina na namba za simu za wauzaji wote wa mifuko ya PICS katika kila kanda nchini,” anasema Mwakibinga.

  Anasema kwenye kipengele cha taarifa za PICS nako inaonyesha bei halali ya mifuko hiyo kwa wanunuzi wa rejareja na pia inamuelekeza mkulima au mtumiaji wa PICS kutambua bidhaa bandia.“Tumeamua kutumia teknolojia hii ya mawasiliano ambayo ni rahisi na inatumika kila sehemu ambapo sasa itamuelekeza moja kwa moja mkulima mahali ambapo wakala halisi wa mifuko yetu anapatikana katika mkoa aliopo na itamuwezesha kuwasiliana naye moja kwa moja kwa kupata namba ya wakala ya mkononi akiwa hata shambani,” anasema.

  Anasema, kila mfuko mmoja wa PICS unaouzwa kwa Sh 5000 kwa bei ya rejareja una ujazo wa kilogramu 100 ambapo kwa kama Mkulima atakuwa na matumizi ya kawaida anaweza kuutumia kuhifadhia nafaka kavu kwa miaka mitatu.

  Ndg Ngingo(Meneja wa Mradi PPTL/ PICS) dukani Planet Commercial Agent & Vet Service, Wilayani Manyoni, Mkoani Singida.


  MAWAKALA, WAKULIMA WAELEZA FAIDA ZA PICS

  Magdalena Sendasenda ni wakala wa mifuko ya PICS katika kanda ya kati, yeye anasema mbali na kuuza ni miongoni mwa watu waliokwishaitumia katika kuhifadhi nafaka.“Aliyeiita mifuko ya PICS kuwa ni Kinga Njaa wala hakukosea, wakulima wa kanda ya kati (mikoa ya Dodoma na Singida) wanaichangamkia, wanaiona kama mkombozi wao katika kuhifadhi nafaka,” anasema Magdalena.

  Wakala Mkuu wa mkoa wa Shinyanga (Shinyanga farm), Adam James anasema mapokeo ya mifuko ya PICS kwa wakulima wa Shinyanga na mikoa jirani ya Tabora na Mwanza ni kubwa na kwa siku wana wastani wa kuuza hadi mifuko 50 mpaka 60 katika mkoa wa Shinyanga pekee.

  “Kipindi hiki kidogo upepo sio mzuri hivyo mahindi yaliyovunwa sio mengi sana ndiyo sababu tunauza idadi hiyo, lakini upepo wa kilimo ukichanganya tuna uwezo wa kuuza hadi mifuko 500 kwa siku,” anasema.Helena Magere ambaye ni kulima wa maharagwe na mahindi mkoani Tabora anasema amekuwa mdau mkubwa wa mifuko hiyo tangu 2015 alipoikuta kwenye maonyesho ya Nane nane mwaka huo.

  Anasema mwanzo hakuwa na Imani na mifuko, alichukua ili kufanya majaribio na sasa ndiye mkombozi wake mkubwa katika uhifadhi wa nafaka na hana presha ya mazao yake kuharibika hata baada ya msimu kupita.

  Mkulima mwingine, Bwire Shija wa Lamadi yeye anaifahamu mifuko ya PICS kwa jina la Kinga njaa, ambayo anasema ujio wake nchini umewasaidia sio tu kuhifadhi nafaka kavu bali pia kuuza mazao yao kwa bei ile ile tofauti na awali ambapo walilazimika kuuza kwa bei ya chini ili zisiwadodee na kuharibka.


  MAJARIBIO YALIFANYIKA KWENYE VIJIJI 4000


  Meneja mradi wa PICS Tanzania, Ladislaus Ngingo anasema kabla ya kusambaza mifuko hiyo walifanya ‘Demo’ ya matumizi kwenye Vijiji 4000 katika mikoa tisa nchini“Tulipata ushirikiano kwenye Serikali za vijiji, uliitishwa mkutano wa kijiji ambapo tulitoa kila kijiji mfuko mitano ambayo iliwekewa nafaka za kuonyeshea mfano, mmoja wa wanakijiji alielekezwa namna ya kuhifadhi ndani ya mifuko na wengine wakishuhudia.

  “Alipomaliza kuhifadhi kwa pamoja tuliandika tarehe ya siku ambayo nafaka kavu zimehifadhiwa juu ya mfuko na kuyahifadhi yale magunia yenye nafaka kwa wanakijiji, baada ya miezi sita tulikwenda tena kijijini na tulihitisha mkutano kwa ajili ya kufungua zile nafaka hakuna aliyeamini nafaka zilkuwa katika ubora ule ule kama kwamba zimetoka shambani siku hiyo” anasema.

  0 0


  0 0  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Jeneral Venance Mabeyo akipokea mkono wa Heri ya Krismasi kutoka kwa Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Muhashamu Liberatus Sangu, katika ibada ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayani Busega mkoani Simiyu, iliyofanyika Desemba 26, 2018.
  PICHA B
  Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Muhashamu Liberatus Sangu, akitabaruku altare kwa kupaka mafuta ya Krisma kuashiria uwepo wa Kristo katika Kanisa la Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayani Busega mkoani Simiyu katika ibada ya kubariki na kutabaruku kanisa hilo, iliyofanyika Desemba 26, 2018.
  PICHA C
  Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Muhashamu Liberatus Sangu akimshuhudia Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Jenerali Venance Mabeyo wakati akitia saini kama shahidi katika Hati ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya, katika ibada ya kubariki na kutabaruku  kanisa hilo, iliyofanyika Desemba 26, 2018.
  PICHA D
  Kutoka kushoto Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga, Naibu Gavana wa Benki Kuu, Dkt. Benard Kibese, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka,Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo wakiwa katika ibada ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayan Busega mkoani Simiyu, iliyofanyika Desemba 26, 2018.
  PICHA E
  Wanakwaya ya Mtakatifu Maxmillian kutoka Parokia ya Segerea jijini Dar es salaam wakiimba katika katika ibada ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayan Busega mkoani Simiyu, iliyofanyika Desemba 26, 2018.
  PICHA F
  Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Muhashamu Liberatus Sangu(kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(katikati), Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo(kulia) wakifurahia jambo mara baada ya kumalizika kwa ibada ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayan Busega mkoani Simiyu, iliyofanyika Desemba 26, 2018.
  PICHA G
  Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Muhashamu Liberatus Sangu, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo na viongozi wengine wakiwa na katika picha ya pamoja na watoto wenye ualbino wanaoishi katika kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum Lamadi, mara baada ya kumalizika kwa ibada ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayan Busega mkoani Simiyu, iliyofanyika Desemba 26, 2018.
  ……………………………………………………………………………………….
  Na Stella Kalinga, Simiyu
  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi hapa nchini Jenerali Venance Mabeyo ametoa wito kwa Viongozi wa Dini nchini kuendelea kuhubiri amani ili kujenga jamii iliyo bora yenye kudumisha upendo na mshikamano.
  Jenerali Mabeyo ametoa wito huo wakati wa ibada ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro, Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayani Busega ambayo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Kitaifa akiwepo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, Naibu Gavana wa Benki Kuu, Dkt. Benard Kibese na viongozi wengine wa Chama na Serikali, ambapo alisisitiza kuwa amani ni msingi wa maendeleo kwa Taifa lolote duniani.
  “Suala la amani na utulivu ni la msingi sana katika nchi yetu, kwa vile kila mwananchi ana dini yake tunaamini kuwa viongozi wa dini zote kwa kuwa wanasikilizwa sana  na waumini  wakiweka msisitizo katika suala la amani, amani itatawala na kutakuwa na utulivu”
  “Utulivu huu tunauhitaji sana ili tupate maendeleo,  kama  viongozi wetu wa kisiasa wanavyosisitiza kuwa tudumishe amani na utulivu  tupate maendeleo, bila utulivu watu wakiwa wanahaingaika hakuna maendeleo kwa sababu hakuna shughuli mtu anaweza kufanya kama hana amani na utulivu, hivyo hataweza pia kuleta maendeleo yake, familia, jamii na Taifa kwa ujumla” alisema Jenerali Mabeyo
  Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Simon Sirro amesema vitendo vingi vya uvunjifu wa amani na uhalifu ikiwemo ukataji wa mapanga na mauaji ya vikongwe na yanachangiwa na watu kukosa hofu ya Mungu; hivyo nyumba za ibada(makanisa na misikiti) zinapojengwa kwa wingi zitakuwa msaada mkubwa sana kwa watu kuwa na hofu ya Mungu.
  Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema jamii inayoamini uwepo wa Mungu haiwezi kuwa na vitendo vya kisasi, kukatana mapanga na mauaji ya vikongwe huku akiwaasa Watanzania kukaa kwa amani na upendo bila kufanya mambo yanayoweza kuhatarisha amani.
  Akibariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro, Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayani Busega, Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Muhashamu Liberatus Sangu amewataka Watanzania kupendana na kuacha roho ya ubinafsi na visasi.
  Aidha, Askofu Sangu ametoa wito kwa viongozi na waumini kufanya nyumba za ibada zibaki nyumba za sala kama yanenavyo maandiko matakatifu na kamwe zisitumike kama majukwaa la wanasiasa.
  ” Palipo na msamaha pana umoja, uelewano na usawa lakini palipo na  kisasi hapana maendeleo; nyumba ya ibada isitumike kama jukwaa la Wanasiasa alisisitiza Muhashamu Askofu Sangu.

  0 0

  Katika kuhakikisha tatizo la mimba za utotoni Mashuleni linatoweka Mkoani Ruvuma, Mbunge wa Viti maalum Mkoani humo Kupitia chama cha Mapinduzi(CCM) Jackline Ngonyani Msongozi ametoa mifuko 50 ya Saruji katika shule ya sekondari Makita iliyopo Wilaya Ya MBinga kwa Ajili ya ukarabati wa Mabweni ili kuwapunguzia changamoto wanazokutana wanafunzi wakike pindi wanapokuwa wanarudi kutoka shule.
  Attachments area

  0 0


  0 0  WAZIRI MKUU AKAGUA UJENZI WA MJI WA SERIKALI
  *Akuta baadhi ya wakandarasi wanasuasua, wengine wako vizuri
  *Aitisha kikao cha Mawaziri, Makatibu Wakuu wote kesho saa 5 asubuhi
  *Ataka leo jioni apewe taarifa ya kila taasisi inayohusika Ihumwa

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua ujenzi wa eneo la Mji wa Serikali lililoko Ihumwa na kubaini kuwa baadhi ya wakandarasi hawaendi na kasi inayotarajiwa na Serikali.

  Waziri Mkuu ameamua kuitisha kikao cha Mawaziri wote na makatibu wakuu wote kesho (Ijumaa) saa 5 asubuhi ili waeleze kazi hiyo itakamilishwa lini.

  Ametoa agizo kauli hiyo leo mchana (Alhamisi, Desemba 27, 2018) mara baada ya kukagua ujenzi wa ofisi za wizara zote pamoja na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika eneo la Mtumba lililoko km. 17 kutoka jijini Dodoma.

  “Nimekagua maeneo yote na kukuta baadhi ya wakandarasi wanatakiwa kujenga majengo ya wizara nne hadi tano. Sijaridhika na baadhi ya kazi, nimeitisha kikao cha Mawaziri wote kesho ili tuangalie ni mkandarasi yupi anaweza kumudu hii kazi.”

  “Nimebaini kuna tatizo kubwa la upatikanaji wa vifaa vya ujenzi kama kokoto, nondo, matofali na kikao cha kesho kitahusisha Mawaziri, Makatibu Wakuu, viongozi wa Mkoa na Jiji la Dodoma, wakandarasi wote ili tukubaliane kazi hii inaisha lini,” amesema.

  Akitoa mfano, Waziri Mkuu amesema wajasiriamali wanaotengeza matofali Dodoma wako wengi lakini matofali tyao yako chini ya kiwango, kwa hiyo wanatakiwa watu wa kutengeneza matofali mengi yenye uimara. “Tuna ujenzi wa wizara 24, tunataka matofali imara siyo yale ambayo ukilishika tu, mchanga unamomonyoka,” amesisitiza.

  Akisisitiza uharaka wa kazi hiyo, Waziri Mkuu amesema kazi hiyo ina malengo maalum na inatakiwa ikamilike haraka sana. “Tarehe ya mwisho ya kukamilisha ujenzi iliyotolewa na Mheshimiwa Rais ilikuwa Desemba 31, mwaka huu lakini kuna sababu zimetajwa kukwamisha ujenzi huo zikiwemo mvua na uhaba wa kokoto,” amesema.

  Hata hivyo, Waziri Mkuu amesifia kazi nzuri iliyofanywa kwenye Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, Utumishi, Ujenzi, Katiba na Sheria, Maji na Elimu. Kazi hizo zimefanywa na wakandarasi ambao ni Magereza, SUMA JKT, Wakala wa Majengo (TBA) na Vikosi vya Ujenzi vya Mwanza na Dar es Salaam vilivyoko chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

  Wakandarasi walioboronga ni JWTZ – Mzinga, National Housing na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST).

  Waziri Mkuu amemwagiza Katibu wa Kamati ya Kitaifa ya kuratibu zoezi la Serikali kuhamia Dodoma, Bw. Meshack Bandawe ahakakishe anapokea taarifa kutoka kila taasisi inayohusika na ujenzi huko Ihumwa na akishaijumuisha, aiwasilishe kwake ifikapo leo jioni.

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemuagiza Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Bw. Godwin Kunambi ashirikiane na Mkurugenzi wenzake wa Chamwiono kuhakikisha vijana wengi wanapata fursa za ajira kwenye mradi huo.

  “Mkurugenzi wa Jiji wasiliana na Mkurugenzi mwenzako wa Chamwino mhakikishe vijana na akina mama wanakuja kufanya kazi hapa. Pia itisha kikao cha waandishi wa habari uwaeleze wananchi wako fursa zilizopo, kuanzia ufyatuaji wa matofali, uuzaji wa nondo, kokoto na utengenezaji wa pavement blocks, hizi zote ni fursa, tuna wizara 24 na mahitaji ni makubwa,” alisisitiza.

  Mapema, akitoa taarifa mbele ya Waziri Mkuu, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Bw. Anthony Mavunde alisema zoezi la kusafisha eneo la ujenzi wa mji wa Serikali lilianza Novemba 28, mwaka huu.

  Alisema wizara zote zimepata viwanja na zimeanza ujenzi isipokuwa Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana) ambao bado wanasubiri kupatiwa fedha.

  Alisema kazi ya ujenzi wa Mji wa Serikali inasimamiwa na Kamati ya Kitaifa ya kuratibu zoezi la Serikali kuhamia Dodoma, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
    S. L. P. 980,
   41193 – DODOMA,                      
  ALHAMISI, DESEMBA 27, 2018.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisoma ramani ya Mji wa Serikali wakati alipokagua Ujenzi wa mji huo, eneo la Ihumwa jijini Dodoma, Desemba 27, 2018. Wengine pichani kutoka kushoto ni Afisa Mipango Miji katika jiji la Dodoma, William Alfayo, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde, Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Godwin Kunambi na Kulia ni Katibu  wa Kikosi Kazi cha  Kuhamishia Shughuli za Serikali jijini Dodoma, Meshack Bandawe. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Katibu  wa Kikosi Kazi cha  Kuhamishia Shughuli za Serikali jijini Dodoma, Meshack Bandawe kuhusu Ujenzi wa Mji wa Serikali wakati alipokagua Ujenzi huo, eneo la Ihumwa jijini Dodoma, Desemba 27, 2018.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua Ujenzi wa jengo Ofisi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakati alipokagua Ujenzi wa Mji wa Serikali katika eneo la Ihumwa jijini Dodoma, Desemba 27, 2018. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama kazi ya kusuka nondo  kwa ajili ya nguzo za jengo la Ofisi za Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakati alipokagua Ujenzi wa Mji wa Serikali, eneo la Ihumwa jijini Dodoma, Desemba 27, 2018.  Kulia kwake ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu,  Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua Ujenzi wa Msingi  wa jengo la Ofisi za Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wakati alipokagua Ujenzi wa Mji wa Serikali, eneo la Ihumwa jijini Dodoma, Desemba 27, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)  0 0

  Na OWM, Kigoma.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), ameitaja mikoa 11 ambayo ilianzisha mabaraza ya Biashara na hadi sasa yako hai na kubainisha kuwa mikoa mingine ilitekeleza agizo la kuanzisha mabaraza hayo tu lakini utendaji wa Mabaraza hayo umekuwa siyo endelevu.

  Waziri Mhagama ameitaja Mikoa hiyo 11 ambayo Mabaraza yake yako hai hadi sasa kuwa ni Dodoma, Kigoma, Tanga, Geita, Morogoro, shinyanga, Dar es Salaam, Pwani, Iringa, Songwe na Mbeya. Aidha, Mhagama amebainisha kuwa Mikoa mingine ambayo mabaraza yake hayafanyi vikao inakiuka Waraka wa Rais Na. 1 wa mwaka 2001 unaosisitiza kuanzishwa kwa mabaraza hayo na utendaji wake kuwa endelevu.

  Akiongea wakati wa kufuatilia utekelezaji wa shughuli za Baraza la Taifa la Biashara mkoani Kigoma, Waziri Mhagama alifafanua kuwa Dhumuni kuu la kuanzisha mabaraza ya biashara hususani katika ngazi ya wilaya na mikoa ni kuweka mfumo rasmi wa kuwakutanisha viongozi wakuu wa Serikali na Sekta Binafsi katika kila ngazi ya utawala, kujadiliana jinsi ya kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini kwa ajili ya kukuza sekta binafsi ambayo ndio muhimili muhimu wa kukuza uchumi wa nchi.

  “Hatuwezi kuwa tunamshuhudia Mhe. Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Magufuli anaitisha vikao vya Baraza la Taifa la Biashara katika ngazi ya Taifa lakini katika ngazi ya mkoa na wilaya hamtekelezi maagizo hayo, lazima mabaraza yakutane ili kutatua kero za wafanyabiashara na wawekezaji katika ngazi ya mkoa na wilaya, lakini pia itasaidia kuibua fursa za uwekezaji na kuzinadi fursa hizo, na sisi tumeamua kukagua mkoa mmoja baada ya mwingine ili kupunguza kero za wafanya biashara na wawekezaji” Amesema Mhagama

  Wakiongea kwa nyakati tofauti wakati Waziri Mhagama alipokutana na Wajumbe wa Baraza la Mkoa la Biashara, Mkuu wa mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga , Mkuu wa wilaya ya Kigoma, Samson Anga na Katibu Tawala wa Mkoa huo, Rashid Mchata, walieleza kuwa kupitia Mradi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji (LIC), wameweza kuimarisha mfumo wa majadiliano kati ya serikali na sekta binafsi kupitia Mabaraza ya Biashara ya Mikoa na Wilaya.

  Naye Mratibu wa Mradi huo, Andrew Mhina alibainisha kuwa Mradi huo unalenga kuhakikisha kuwa unaboresha mazingira ya Biashara na uwekezaji nchini tayari kwa kushirikiana Baraza la Taifa la Biashara wameandaa mwongozo wa Majadiliano Kati ya Serikali na Sekta Binafsi ngazi ya Mkoa na Wilaya ili kuyajengea uwezo Mabaraza ya Mikoa yaweze kuwa endelevu na yenye ufanisi.

  Baraza la Taifa la Biashara lilianzishwa kwa Waraka wa Rais Na. 1 wa mwaka 2001 na kuchapishwa kwenye Gazeti la Serikali Na. 39 la tarehe 28 Septemba 2001. Baraza hilo ni jukwaa la majadiliano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, na lengo kuu la Baraza ni kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji kwa njia ya majadiliano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi.Aidha Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, akisisitiza jambo wakati alipokutana na wajumbe wa Baraza la Biashara Mkoa wa Kigoma, wakati alipofika mkoani humo kufuatilia utekelezaji wa shughuli za Baraza la Biashara la Taifa, kulia kwake ni Mkuu wa mkoa huo, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga, Katibu Tawala wa mkoa huo, Rashid Mchata na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Samson Anga.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, akimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa Kigoma, Rashid Mchata, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Baraza la Biashara la mkoa huo, wakati Waziri alipofika mkoani humo kufuatilia utekelezaji wa shughuli za Baraza la Biashara la Taifa
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, akimsikiliza Mratibu wa Mradi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji (LIC), Andrew Mhina akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mradi huo mkoani Kigoma, wakati Waziri alipofika mkoani humo kufuatilia utekelezaji wa shughuli za Baraza la Biashara la Taifa
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, akiongea na Mjasiriamali aliyekuwa akihudumiwa katika kituo cha Biashara (One Stop Business Center) wilayani Kigoma, wakati alipofika mkoani Kigoma kufuatilia utekelezaji wa shughuli za Baraza la Biashara la Taifa.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Biashara la Mkoa wa Kigoma, wakati Waziri alipofika mkoani humo kufuatilia utekelezaji wa shughuli za Baraza la Biashara la Taifa


  0 0


  0 0

  * Asema kustaafu sio dhambi bali ni heshima kwa Taifa
  * Asisitiza hakuna sababu ya kuwasumbua wastaafu

  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  RAIS Dk.John Magufuli amerejesha matumaini mapya kwa wafanyakazi na kuagiza wastaafu wote nchini walipwe kwa kutumia kikotoo cha zamani cha asilimia 50.

  Pamoja na hilo amesema kuwa kustaafu si dhambi bali ni heshima kwa Taifa.
  Ametoa uamuzi huo leo hii Desemba 28, mwaka 2018 katika kikao chake kilichohudhuriwa na wadau wote wa mifuko ya hifadhi ya jamii ,wafanyakazi na viongozi wa ngazi mbalimbali wa mifuko hiyo.

  Baada ya Rais kutangaza kutumika kwa kikotoo cha zamani ukumbi wa Ikulu uligeuka kuwa sehemu ya shangwe ambapo nyimbo za mshikamano kwa wafanyakazi zilianza kuimbwa huku Rais akiwaambia "Wafanyakazi Hoyee...wafanyakazi ni muhimu katika kipindi hiki na lazima wapewe stahiki zao na fomuka nzuri ni ile ya kuboresha maslahi ya watu na sio kuwa na fomula inayotesa wafanyakazi."

  Akifafanua wakati anatoa uamuzi huo Rais Mafuli amesema kwamba "kustaafu si dhambi bali ni jambo la heshima. Anayestaafu anastahili kuheshimiwa na Taifa hili na hivyo hatakiwi kupata shida , kikokotoo kilichokuwa kinatumika huko nyuma kitumike katika kipindi hiki cha mpito hadi mwaka 2023," amesema Rais huku akishangiliwa.

  Amefafanua kuwa kwa takwimu alizonazo ni kwamba kwa kipindi cha mpito ambacho ni kuanzia sasa hadi mwaka 2023 watakaostaafu ni wanachama 58, 000 na hao walipwe kwa kikotoo cha asilimia 50 huku akisisitiza mifuko yote ilipe kama ilivyokuwa inalipa awali.

  Ameongeza kuwa Serikali iliyopo madarakani imeweka mfumo imara wa ukusanyaji kodi na miongoni mwa walipa kodi wazuri ni wafanyakazi na hivyo lazima waendelee kulipwa kama zamani ndani ya kipindi hicho cha mpito .

  Awali kabla ya uamuzi huo Rais Magufuli alieleza kuwa maelezo yanayotolewa kuhusu mafao yamekuwa ya kitaalamu zaidi.Hivyo amesema kustaafu ni jambo la heshima kwa anayestaafu kwani mfanyakazi anakuwa amejitolea kwa miaka yote halafu mwishoni anakuja kusumbuliwa baada ya kustaafu.

  Amesema kuwa yeye amefanya kazi kuanzia mwaka 1981 na anajua changamoto na hayupo tayari kuwachanganya wafanyakazi.Hata hivyo ameelezea historian ya kuunganishwa kwa mifuko ambapo amefafanua Oktoba 20 mwaka 217 kwenye baraza la mawaziri walipitisha uamuzi wa kuunganisha mifuko ya hifadhi ya jamii na kisha ibaki mifuko miwili ambayo ni NSSF na PSSSF kwa lengo la kuhakikisha mifuko hiyo inatimiza wajibu wake.

  Amesema hatua hiyo ilitokana na ombi la muda mrefu la wafanyakazi baada ya kuona mifuko hiyo inaelekea kufa.Hivyo baadae Bunge lilipitisha sheria.
  Amesema jumla ya wanachama wa mifuko yote ni milioni 1.267 na kwamba mwanachama anachangia asilimia 10 na mwajiri anachangia asilimia 10 na mfuko ili ufanye kazi lazima mwajiri achangie na muajiriwa achangie.

  Amefafanua kuwa mifuko baadhi ya ilikuwa inaendeshwa kiajabu ajabu na mingine ilikuwa imejikita kwenye ujenzi wa majengo kwasababu kulikuwa na asilimia 10.Amesema waliokabidhiwa kutunza mifuko ndio waliokuwa wanaamua aina ya miradi bila kushirikisha wadau na kwamba wakati Serikali ya awamu ya Tano inaingia madarakani walikuta deni la zaidi ya Sh.trilioni 1.2 na wamefanikiwa kulipa madeni yote.

  "Sh.Trilioni 1.23 ambazo Serikali imelipa kwa mifuko ya hifadhi ya jamii.Kuna deni la Sh.bilioni 740 nazo zitalipwa kabla ya Januari mwakani na kati ya hizo Sh.bilioni 500 zimelipwa tayari kwa wanachama 8000 waliokuwa wanadai mafao yao.

  Baada ya ufafanuzi huo Rais Magufuli amesema pamoja na changamoto hizo bado lazima ufumbuzi upatikane ili kuondoa malalamiko yaliyopo.Amesema wafanyakazi wamefanya kazi zao kwa uadilifu na hivyo anatarajia kupata mafao yake.Na kwamba anatambua kuna wafanyakazi wanataka mafao halafu anaambia asubiri.

  Mkuu hiyo wa nchi alihoji iwapo mbunge akimaliza muda wake anapewa stahiki sake zote lakini kwa wastaafu wengine wanaambiwa watalipwa kidogokidogo.Pia amefafanua Serikali inatoa Sh.bilioni 126 kwa mwezi kwa ajili ya michango ya wafanyakazi na hapo hapo lazima mishahara yao ilipwe ambayo ni Sh.bilioni 560.Amesema ili kukabiliana na mambo yote hayo lazima kunahatua zichukuliwe kuhakikisha mambo yanakwenda sawasawa.

  "Makatibu wakuu wa wakati ule walishiriki kutengeneza fomula ya ukokotoaji kwani nao waliokuwa wananufaika,"amesema Rais.

  Rais Magufuli ametoa ombi kwa mifuko ya hifadhi waboreshe daftari la wastaafu kwa mifuko ili kuondoa wastaafu hewa kwani kama kulikuwa na wafanyakazi hewa,mbolea hewa, wanafunzi hewa lazima kutakuwa na wastaafu hewa au ambao wanalipwa mara mbili.

  Hivyo amewataka wadau wa mifuko kuhakikisha wanapitia upya orodha ya wanachama wa mifuko hiyo na hilo ndilo agizo lake la kwanza.Agizo la pili mifuko ya hifadhi watumie vizuri fedha za wanachama amesema wanaweza wakawa wanaona tatizo ni kikokotoo kumbe changamoto ni matumizi mabaya ya fedha.

  Amesema kuna hifadhi inatumia Sh. bilioni 1.3 kwa ajili ya kutengeneza kalenda ,pia imeajiri walinzi ambao wanalipa zaidi ya Sh.bilioni 3 kwa mwaka.Hivyo lazima matumizi ya fedha yawe ya uangalifu.

  Amesisitiza ni marufuku kufanya uwekezaji ambao hauna tija na kwamba kibaya zaidi wanachama hawahusiki kwenye kuamua katika kupanga aina ya miradi.

  0 0

   Mtoa huduma wa Vodacom Tanzania, Bi. Devotha Majura akitoa elimu kwa wakazi wa Mbagala Charambe kuhusu pointi za Tuzo katika kampeni ya Tuzo Points 'Baki Mule Mule Utunzwe na Tuzo Points' iliyofanyika eneo la Mbagala Charambe na Chamazi jijini Dar es Salaam. Tuzo Points ni programu ambayo inawazawadia wateja wa Vodacom pointi pale wanaponunua salio au kufanya miamala kupitia M-Pesa. Pointi hizo zinaweza kubadilishwa kuwa fedha, salio au bando, katika msimu huu wa sikukuu Vodacom Tanzania inawazawadia wateja wao Point za Tuzo zenye thamani ya shilling Bilioni moja.
   Mtoa huduma wa Vodacom Tanzania, Bi. Stella Richard akizungumza na kumuelimisha mfanyabiashara jinsi ya kuzipata na kuzitumia pointi za Tuzo, hapo jana katika kampeni ya Tuzo points 'Baki Mule Mule Utunzwe na Tuzo Points' iliyofanyika eneo la Mbagala Charambe na Chamazi jijini Dar es Salaam. Katika msimu huu wa sikukuu Vodacom Tanzania inawazawadia wateja wao Point za Tuzo zenye thamani ya shilling Bilioni moja.
   Kiongozi wa Timu ya watoa huduma wa Vodacom Tanzania, Nashon Leonard akizungumza na watoa huduma wa Vodacom Tanzania mara baada ya kumaliza kutoa elimu ya kampeni ya Tuzo Points 'Baki Mule Mule utunzwe na Tuzo Points' iliyofanyika eneo la Mbagala Charambe na Chamazi jijini Dar es Salaam.
  Kikundi cha burudani kinachofahamika kwa jina la Respect Crew wakitoa burudani kwa wakazi wa Mbagala wakati wa utoaji elimu wa kampeni ya Tuzo Points 'Baki Mule Mule utunzwe na Tuzo Points' jijini Dar es Salaam.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa meza kuu na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama na viongozi wa wafanyakazi na wa mifujo ya hifadhi ya jamii wakiwa wameshikana mikono kwa furaha huku wakiimba wimbo wa hamasa wa mshikamao wa wafanyakazi wa "Solidarity Forever" baada ya kuwasikiliza hoja zao, kuwahutubia na hatimaye kulipatia jawabu swala la vikokotoo vya wafanyakazi alipokutana nao Ikulu jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Desemba 28, 2018.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa meza kuu na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipoongea na viongoz wa wafanyakazi na wa mifujo ya hifadhi ya jamii  baada ya kuwasikiliza hoja zao, kuwahutubia na hatimaye kulipatia jawabu swala la vikokotoo vya wafanyakazi alipokutana nao Ikulu jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Desemba 28, 2018
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa  na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama  (hawapo pichani) na viongozi wa wafanyakazi na wa mifujo ya hifadhi ya jamii wakiwa wameshikana mikono kwa furaha huku wakiimba wimbo wa hamasa wa mshikamao wa wafanyakazi wa "Solidarity Forever" baada ya kuwasikiliza hoja zao, kuwahutubia na hatimaye kulipatia jawabu swala la vikokotoo vya wafanyakazi alipokutana nao Ikulu jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Desemba 28, 2018.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa meza kuu na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama na viongozi wengine waandamizi   katika picha ya pamoja na viongoz wa wafanyakazi na wa mifujo ya hifadhi ya jamii wakiwa wameshikana mikono kwa furaha huku wakiimba wimbo wa hamasa wa mshikamao wa wafanyakazi wa "Solidarity Forever" baada ya kuwasikiliza hoja zao, kuwahutubia na hatimaye kulipatia jawabu swala la vikokotoo vya wafanyakazi alipokutana nao Ikulu jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Desemba 28, 2018.

  PICHA NA IKULU


  0 0  0 0


  Na Mwandishi ,Mkuranga. 

  Shirika lisilo la Kiserikali linalojihusisha na msuala ya Kisaikolojia nchini (REPPS) limeanza kufanya kampeni ya kupambana na tatizo la mimba na ndoa za utotoni baada ya tafiti nyingi kuonyesha bado tatizo hilo ni kubwa.

  Takwimu za Democratic and Health Survey , zinaonyesha kuwa tatizo la mimba za utotoni nchini limeongezeka kutoka asilimia 23 mwaka 2010 hadi kufikia 27 mwaka 2016/17, kutokana na ukosefu wa huduma pamoja na elimu ya afya ya uzazi kwa vijana wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 19.

  Mkurugenzi Mkazi wa Repps, Tanzania Edwick Mapalala amesema kampeni hiyo wanaiendesha kwa kuzungumza na jamii kwenye vijiwe, shambani, maeneo ya masomo na mikusanyiko yote ili kufikisha elimu ya namna ya kuwalea na kuwatunza watoto kimaadili.“Tatizo la mimba na ndoa za utotoni lipo kwenye jamii yenyewe, wazazi na walezi wakijua umuhimu wa malezi bora tatizo hili halitakuwepo kabisa,” amesema.

  Amesema kama watoto wa kike wataendelea kukatisha masomo yao kwa mimba na ndoa itakuwa vigumu kufikia ndoto ya Tanzania yenye viwanda kwa sababu nguvu kazi inayoachwa njiani ni kubwa.“Mtoto wa kike akipata elimu na kusoma kwa bidii atatimiza ndoto yake na kuja kuchangia maendeleo kwenye taifa lake,” amesisitiza.

  Amesema kupitia kampeni hiyo wanayoiendesha kwa ushirikiano na Shirika lililo chini ya Kanisa la Roman Katoliki jimbo kuu la Dar es Salaam (PASADA), vijana wameweza kupewa elimu ya afya ya uzazi na kujitambua itakayowasaidia kufikia ndoto zao.Kaimu Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Parang’andam Felisian Magulu amesema kupitia kampeni hizo jamii inapata ufahamu wa madhara ya mimba kwa watoto na kujua namna ya kupambana na tatizo hilo.

  Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Mkuranga, Dunia Mabufu alikiri kuwepo kwa kampeni za aina hiyo kunasaidia katika kubadilisha fikra za wengi zinazoendeshwa na mila na desturi kandamizi dhidi ya wasichana na wanawake.
  Mkurugenzi mkazi wa taasisi inayojishughulisha na maswala ya kisaikolojia (RESPSSI) Tanzania,Edwick Mapalala akizungumza wakati wa kampeni ya kutomeza tatizo la ndoa na mimba za utotoni.
  Mkurugenzi mkazi wa taasisi inayojishughulisha na maswala ya kisaikolojia (RESPSSI) Tanzania,Edwick Mapalala akizungumza wakati wa kampeni ya kutomeza tatizo la ndoa na mimba za utotoni
  Baadhi ya vijana wa boda boda waliochangia mjadala wa kupinga ndoa na mimba ya utotoni.
   

  0 0

  Baadhi ya Wamiliki wa Vyombo vya Habari waliohudhuria katika Mkutano kuhusiana na Mabadiliko ya Teknolojia Ulioandaliwa na Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA)wakishirikiana na Tume ya Utangazaji Zanzibar.katika ukumbi wa Sheikh Idris Abdulwakil Kikwajuni mjini Unguja.
  Mhandisi Mkuu wa Utoaji Leseni za Mawasiliano TCRA Andrew Kisaka (aliesimama)akitoa maelezo kuhusu Mabadiliko ya Teknolojia katika mkutano uliowashirikisha Wamiliki wa Vyombo vya Habari uliofanyika Ukumbi wa Sheikh Idris Abdulwakil Kikwajuni mjini Unguja.
  Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Khadija Bakari Juma akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Mkutano kuhusiana na Mabadiliko ya Teknolojia Ulioandaliwa na Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA)wakishirikiana na Tume ya Utangazaji Zanzibar.katika ukumbi wa Sheikh Idris Abdulwakil Kikwajuni mjini Unguja.PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

older | 1 | .... | 1761 | 1762 | (Page 1763) | 1764 | 1765 | .... | 1897 | newer