Na. Vero Ignatus, Arusha
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini Fortunatus Musilimu amewaomba abiria kulisadia jeshi la polisi kwa kutoa taarifa pale wanapoona dereva amekaidi sheria ya usalama barabarani, wasisubirie hadi ajali itokee ndipo waanze kutoa malalamiko
Hayo ameyasema leo Jijini alipokuwa akifanya ukaguzi wa magari pamoja na askari wa usalama barabarani na wadau wengine wa usalama katika stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani ambapo aliwataka abiria kutokufumbia macho uzembe wowote atakaoufanya dereva wa kuhatarisha maisha ya abiria awapo safarini.
Aidha ameeaagiza abiria hao punde wanapomuona dereva anaotaka kulipita gari lingine kimakosa, mwendo kasi, lugha chafu kwa abiria, kuongea na simu sambamba na viashiria vyote vinavyoweza kupelekea kutokea ajali watoe taarifa kwa namba 0656111444
'' Piga simu muda wowote tunapambana sisi tunapambana na madereva wazembe hadi kuhakikisha tunakuwa salama barabarani "'' Tunapozungumzia maisha ya watu hatuna mchezo wacheni uzembe na mambo ya kitotokitoto muwapo barabarani dereva unakimbia kwenda wapi gari limejaa udereva ni taaluma, zingatia sheria uwapo barabarani"alisema Muslimu
Muslim ametahadharisha madereva ambao hawatazingatia na kutii sheria za usalama barabarani kuwa jeshi la polisi halitawafumbia macho sheria itafuata mkondo wake. Pia amesisitiza kuwa jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani lipo tayari kwaajili ya waananchi na kuhakikisha usalama wa maisha yao wawapo safarini.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa usalama barabarani mkoa wa Arusha Baraka Msangi amesema zoezi la Abiria paza sauti sambamba na ile ya Nyakua ya jeshi la polisi imesababisha ajali zimepungua katika Jiji la Arusha
Amewataka Madereva kuendelea kuwa makini na kuzingatia sheria za usalama barabarani kwasababu abiria wanawategemea wao wawapo safarini
'' Abiria fungeni mikanda yenu mnapokuwa kwenye vyombo vya moto, usikae kimya pale dereva anapokiuka sheria za usalama barabarani toa taarifa kwa askari yeyote atakapolisimamisha gari kwa ukaguzi '' alisema Bakari
Hamza Kasongo ni mjumbe kutoka Baraza la usalama barabarani Taifa katika kamati ya Elimu, mafunzo na uenezi amesema wao kazi yao kubwa ni kupanga mikakati na kushirikiana na jeshi la polisi ili kupunguza ajali na kila mwisho wa mwaka wanashirikiana nao kufanya ukaguzi nchi nzima
Amesema hadi sasa wameshatoa elimu hiyo na kufanya ukaguzi zaidi ya mikoa zaidi ya 11na lengo kuu ni kuepusha ajali za kizembe kwani mwisho wa mwaka ajali huwa zinaongezeka na wanafanya yote hayo kwa kishirikiana na Jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani
Msafiri Mussa Afisa Msafiri Mussa ni Afisa kutoka Sumatra yeye amesema kazi yao kubwa haswa katika sikukuu za mwisho wa mwaka nikuhakikisha kuwa abiria wanalipa nauli stahiki, tiketi, na wanasafiri salama
Aidha amesema kwa mwaka huu malalamiko haswa katika jiji la Arusha yamepungua kwani mwanzoni kulikuwa na mkanganyiko wa magari.
Awali ilikuwa mbili kwa tatu (three by two) lakini kwa sasa ni mbili kwa mbili(two by two) ambapo nauli kwa sasa zipo sawa, wamiliki wanatoza shilingi elfu 30,000-35,000 kwa msimu huu wa sikukuu ni shilingi 38,000 ambacho ni kiwango cha kawaida.
Wa Pili kutoka kulia ni Kamanda wa kikosi cha uslama. Barabarani SACP Fortunatus Musilim, akifuatiwa na Mrakibu msaidizi Joseph Bukombe mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Mkoani Arusha, Mjumbe wa Baraza la usalama barabarani Taifa Hamza Kasongo na wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa mabalozi wa usalama barabarani mkoa wa Arusha Bakari Msangi wakiwa stendi kuu leo asubuhi. Picha na Vero Ignatus.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani nchi SACP Fortunatus Musilimu akizungumza na abiria leo asubuhi katika stendi ya mabasi Jijini Arusha kabla hawajaanza safari. Picha na Vero Ignatus
Baadhi ya mabalozi wa usalama barabarani wakiwa tayari kwa kupaza sauti stendi kuu ya mabasi jijini Arusha.
Kutoka kulia ni Kamanda wa Kikosi cha usalama barabarani SACP Fortunatus Musilim ni mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Jijini Arusha Joseph Bukombe, Mwenyekiti wa mabalozi wa usalama barabarani Bakari Msangi. Picha na Vero Ignatus