Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46193 articles
Browse latest View live

MICHUZI TV: Irene Uwoya afichua siri ya mafanikio yake,ahidi kusomesha albino

0
0

VIJANA WA KITANZANIA WAPATA JUKWAA LAKUUNGANISHWA NA WAWEKEZAJI

0
0

Chaz Baba: Alikiba amenishangaza sana siku ya ndoa yangu...

0
0

MHANDISI KAMWELWE ALALAMA NA UTOAJI HUDUMA WA ATCL, VIWANJA VYA NDEGE NCHINI

0
0
*Ameagiza ifikapo January 2019 hataki kuona matatizo hayo, ataka wajirekebishe.

Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi, Isack Kamwelwe amelalamikia huduma zinazotolewa kwa Wateja na Kampuni ya Ndege (ATCL) na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini.

Akizungumza na Menejimenti ya Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi Mkoani Mbeya, Mhandisi Kamwelwe amesema huduma zinazotolewa na Mamlaka hiyo zimekuwa zikilalamikiwa na Abiria ambapo ametolea mfano uwepo wa Joto kali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Terminal 2).

Ameagiza kuwaondolea usumbufu Abiria wanaosafiri ambapo amesema abiria hao lazima wasikilizwe uhitaji wao.Pia ametaka kuendeleza ukarabati wa kiwanja cha Ndege cha Songwe kutokana na kutoridhishwa na ujenzi wa Kiwanja hicho kinachotegemewa kutua Ndege mpya.

Pia kuhusu sakata la Fastjet, Mhandishi Kamwele amesema kuwa Kampuni hiyo tayari ilipewa agizo la kujirekebisha hivyo walipewa siku 28 ambapo zikiisha imeelezwa hatowezo kufanya biashara hapa nchini, na hatoweza kufanya biashara sehemu nyingine mpaka alipe madeni ya Serikali.

Ameagiza Rubani wote na Watendaji wa SUMATRA kutokwenda likizo kipindi hiki cha mwisho wa mwaka kuhakikisha uhitaji bora wa usafiri kwa abiria. Amesema hakuna atakayeongeza bei ya nauli katika usafiri.

Amesema Ndege za AirBus za ATCL kuwasili Desemba 23, 2018 kama ratiba haijabadilika ambapo amesema tayari imetuma Crew wakiwemo Rubani nchini Canada kwa mafunzo. Uwanja wa Ndege Terminal 3 kukamilika mwezi May mwakani.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini, Richard Mayongela amemuahidi Waziri Kamwele kushughulikia changamoto zote ambazo zimelalamikiwa kwa Mamlaka hiyo katika utoaji huduma ifikapo January Mosi, 2019 ka ilivyoagizwa.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandishi Isack Kamwelwe akizungumza na Mejimenti ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini baada yakurejea kutoka kwenye ziara ya kikazi Mkoani Mbeya.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Richard Mayongela akitoa ufafuzi kwenye kikao cha pamoja baina ya Menejimenti ya Mamlaka hiyo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ambapo ameahidi kutatua changamoto ambazo zimetajwa katika Mamlaka hiyo.

Sehemu ya Menejimenti ikimsikiliza Waziri alipokuwa anazungumza.

Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu UDOM Prof Mubofu

0
0

MAGAZETI YA LEO JUMATANO DESEMBA 19,2018

0
0




















Mwasiti Featuring Roma - Fall in love (Official video)

0
0

MKAZI WA SENGEREMA AMPONGEZA RAIS DKT MAGUFULI

0
0

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Mama Madina Mbunda ambaye ni mkazi wa Katunguru wilayani Sengerema ametoa pongezi kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa namna anavyoendelea kuboresha sekta ya afya ikiwemo ukarabati wa Vituo vya Kituo Afya kama vile Katunguru na kutaka aendelee kuwa Rais hata baada ya muda wake kumalizika.

Mama Mbunda alitoa kauli hiyo jana baada ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella kufanya ziara katika Kituo cha Afya Karume kilichopewa shilingi Milioni 400 na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa majengo matano mapya ambayo ni nyumba ya mtumishi, maabara, wadi ya wazazi, jengo la upasuaji pamoja na jengo la kuhifahia maiti kupitia mfumo wa “Force Account”.

DC NAMTUMBO AONYA WANAOJIHUSISHA NA MAFUNZO YA KIGAIDI

0
0
*Asema baadhi yao wapo wanafunzi waliomaliza elimu ya msingi, adai anao ushahidi

Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

MKUU wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Mfaume Kizigo amewahatahadharisha vijana wanaomaliza darasa la saba na kidato cha nne ambao hawakubahatika kuendelea na masomo kuacha kujiunga na mafunzo ya kigaidi.

Kizigo aliyasema hayo kwenye kikao cha ushauri cha Wilaya ya Namtumbo kilichofanyika jana ukumbi wa Halmashauri ya wilaya hiyo ambapo amedai 

kuwepo kwa ushahidi wa wazi wa jeshi la polisi ambao unadai wanafunzi wanaomaliza darasa la saba na wale wanaomaliza kidato cha nne na kutobahatika kuendelea na masomo ndio wanaojiunga na mafunzo hayo ya ugaidi wilayani humo.Hata hivyo kupitia kikao hicho Mkuu wa wilaya huyo aliagiza wanafunzi wote wanaomaliza darasa la saba na kidato cha nne ambao hawatapata nafasi ya kuendelea na masomo na wanapohitajika na taasisi za kidini kwa kisingizio cha kwenda kufanya kazi lazima wapate kibali kutoka katika ofisi yake.

Kwa upande wa Katibu wa Chama cha Wananchi (CUF) wilayani Namtumbo Rashidi Mfaume pamoja na kumpongeza mkuu wa wilaya kwa hatua hiyo lakini alimwomba kuwashirikisha wenyeviti wa serikali za mitaa na vitongoji katika utoaji wa vibali hivyo.Pamoja na hayo kikao hicho cha ushauri cha wilaya kilipitia muhtasari wa maadhimio ya mwaka 2016 ambapo adhimio la kuanzisha Wilaya ya Sasawala wajumbe walidai liindelee kufuatiliwa kulingana na umuhimu wake pamoja na adhimio la kuongezewa jimbo la Sasawala nalo lilibaki kama lilivyopitishwa katika kikao cha mwaka 2016.

Kuhusu azimio la kuyarudisha mashamba yanayomilikiwa na (NAFCO)Shirika la chakula la taifa ambayo kwa sasa hayaendelezwi yarudishwe kwa wananchi pamoja na shamba la Likenangena ambalo nalo awali lilionekana kumilikiwa na wizara ya fedha nalo haliendelezwi .

Mafunzo ya kigaidi wilayani humo yalibainika kufanywa katika misitu ya kijiji cha Mchomoro na Masuguru wilayani humo ambapo Jeshi la polisi Kwa umahiri wake walifanikiwa kuwakamata wahusika na kusambaratisha mafunzo hayo.

DC ARUMERU AZINDUA KAMPENI YA KUHAMASISHA UTALII WA NDANI,AWAOMBA WANANCHI KUTENGA MUDA WA KUTEMBELEA VIVUTIO VYA UTALII NCHINI

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Jerry Muro amezindua kampeni ya kuhamasisha utalii wa Ndani Kwa kuwataka wananchi kutenga muda wa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini .

Mhe Muro amewataka Watanzania wanaotoka katika mikoa ya kanda ya Kaskazini Tanga,Kilimanjaro, Arusha na Manyara ambao Wana tabia ya kwenda nyumbani nyakati za sikukuu ya Xmass na Mwaka mpya kuweka utamaduni wa kutembelea pia Hifadhi za taifa za Wanyama zilizojirani na maeneo yao ikiwemo Hifadhi pekee ya taifa ya Arusha ambayo iko mjini Kabisa .

Mhe Muro amewapongeza Wafanyakazi na Mhifadhi Mkuu wa Arusha National Parks Kwa uamuzi wao wa kuhamasisha utalii wa ndani Kwa kupunguza Ada ya viingilio pamoja na kufanya maandalizi ya kutoa Usafiri maalum utakaobeba wananchi na kuwapeleka kwenye hifadhi ili kutoa nafasi Kwa wananchi wengi zaidi kutembelea hifadhi ya Wanyama Arusha  
 Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Jerry Muro akizindua  kampeni ya kuhamasisha utalii wa Ndani kwa kuwataka wananchi kutenga muda wa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini 
  Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Jerry Muro akizungumza na baadhi ya Wananchi wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha utalii wa Ndani kwa kuwataka wananchi kutenga muda wa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini
  Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Jerry Muro akiwa na furaha tele baada ya kuzindua kampeni ya kuhamasisha utalii wa Ndani kwa kuwataka wananchi kutenga muda wa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini.

BENKI YA EXIM YATAMBA TUZO YA MWAJIRI BORA

0
0


Kaimu Ofisa Mkuu wa Teknolojia wa Benki hiyo Bw David Lusala (kushoto) akipokea kwa niaba ya benki hiyo tuzo ya mwajiri bora wa ndani wa mwaka 2018 (Best Local Employer of the year 2018) kutoka kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (kulia) kwenye hafla ya tuzo za Mwajiri Bora (EYA) za mwaka 2018 zilizoandaliwa na Chama cha Waajili Tanzania (ATE) na kufanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Mkuu wa Matawi ya Benki ya Exim Bi Elizabeth Mayengoh (wa tatu kulia) akifurahia pamoja na wafanyakazi wengine wa benki hiyo mara baada ya kukabidhiwa tuzo ya kuwa miongoni mwa waajiri wa ndani bora wa mwaka 2018 (Best Local Employer of the year 2018) kwenye hafla ya tuzo za Mwajiri Bora (EYA) za mwaka 2018 zilizoandaliwa na Chama cha Waajili Tanzania (ATE) na kufanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Wengine ni pamoja na Kaimu Ofisa Mkuu wa Teknolojia wa Benki hiyo Bw David Lusala (katikati) pamoja Meneja Msaidizi wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo Bw Abdulrahman Nkondo.
Wafanyakazi wa benki ya Exim wakifurahia kwa pamoja tuzo hiyo.

LIVE RAIS MAGUFULI AKIWEKA JIWE LA MSINGI UPANUZI WA BARABARA YA KIMARA-KIBAHA

0
0

BancABC yadhamini mkutano wa chama cha Wanawake wafanyabiashara Tanzania (Tanzania Women Chamber of Commerce – TWCC)

0
0

Mkuu wa Kitengo cha Digitali BancABC Tanzania Silas Matoi akiwazilisha mada wakati wa mkutano wa chama cha Wanawake wafanyabiashara Tanzania (Tanzania Women Chamber of Commerce) ambao uliwaleta pamoja wanachama zaidi ya 250 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar kuzungumzia jinsi ya kufanya biashara na changamoto wanazokutana nazo. Mkutano huo ulifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na kudhaminiwa na benki ya BancABC Tanzania.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa benki ya BancABC Tanzania Upendo Nkini akizungumza na wanachama wa chama hicho wakati wa mkutano wa chama hicho ambao uliwaleta pamoja wanachama zaidi ya 250 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar kuzungumzia jinsi ya kufanya biashara na changamoto wanazokutana nazo. Mkutano huo ulifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na kudhaminiwa na benki ya BancABC Tanzania. 

Wafanyakazi wa benki ya BancABC wakimsikiliza kwa makini mmoja wa mwanachama wa chama cha Wanawake wafanyabiashara Tanzania (Tanzania Women Chamber of Commerce) Anna Simbeye wakati wa mkutano wa chama hicho ambao uliwaleta pamoja wanachama zaidi ya 250 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar kuzungumzia jinsi ya kufanya biashara na changamoto wanazokutana nazo. Mkutano huo ulifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na kudhaminiwa na benki ya BancABC Tanzania.

Mkuu wa Kitengo cha Digitali BancABC Tanzania Silas Matoi akiwazilisha mada wakati wa mkutano wa chama cha Wanawake wafanyabiashara Tanzania (Tanzania Women Chamber of Commerce) ambao uliwaleta pamoja wanachama zaidi ya 250 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar kuzungumzia jinsi ya kufanya biashara na changamoto wanazokutana nazo. Mkutano huo ulifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na kudhaminiwa na benki ya BancABC Tanzania.
Mkuu wa Kitengo cha Digitali BancABC Tanzania Silas Matoi akiongea kwa umakini wakati akiwazilisha mada wakati wa mkutano wa chama cha Wanawake wafanyabiashara Tanzania (Tanzania Women Chamber of Commerce) ambao uliwaleta pamoja wanachama zaidi ya 250 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar kuzungumzia jinsi ya kufanya biashara na changamoto wanazokutana nazo. Mkutano huo ulifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na kudhaminiwa na benki ya BancABC Tanzania.

BancABC Tanzania ambayo ni kampuni tanzu ya Atlas Mara na ambao imeorodhesha kwenye soko la hisa la London, mwishoni mwa wiki ilidhamini mkutano wa kila mwezi wa chama cha wanawake wafanyabiashara Tanzania (Tanzania Women Chamber of Commerce TWCC) mkutano ambao uliwaleta pamoja wanachama zaidi ya 250 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar kuzungumzia maendeleo yao na changamoto ambazo wanakubana nazo.

Akiongea wakati wa mkutano huo, Mkurugenzi wa Kitengo cha Digitali BancABC Tanzania Silas Matoi alisema kuwa benki ya BancABC inatambua ni umuhimu wa wanawake kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi na ndio sababu benki yake imeweka mikakati ya kuendelea kuwawezesha na kufikia hatua ya leo ya kuungana na Chama cha Wanawake wafanyabiashara Tanzania (TWCC) kwenye mkutano wake huu wa kila mwezi.

Matoi alisema kuwa kwenye mkutano huo BancABC imeweza kutambua kuwa wanachama wa TWCC huwa wanashiriki maonyesho mengi nchini China akitolea mfano kuwa kwa mwezi wa Oktoba na Aprili mwaka huu, wanachama 150 walishiriki baadhi ya maonyesho ya biashara nchini China. Hata hivyo, Malai alisema kuwa wakati wa safari zao nchi China wananchama hao wamekuwa wakikubana na changamoto kadhaa na hasa linapokuja suala ya kubadilisha fedha na hasa inapotokea dharura.

Ninayo furaha kuwafahamisha ya kuwa BancABC Tanzania inayo suluhiso ya jinsi ya kupata fedha za kigeni mnapokuwa safarani China. Tunayo kadi ya malipo ya kabla – YUAN pre-paid Visa card, ambayo itawawezesha kufanya malipo kwa kwa fedha za China. Kadi ya YUAN ni kadi maalum ambayo inawafanya watumiaji waweze kupata fedha za Uchina kwa thamani ile ile ambayo imewekwa kwenye kadi yake na hivyo itapunguza sana changamoto za kubadilisha fedha ambazo nyinyi wafanyabiashara huwa mnazipata pale wanapohitaji fedha za Uchina mkiwa China au popote pale duniani, alisema Matoi.

Matoi aliongeza kuwa BancABC Tanzania kwa kushirikiana na TWCC itaweza kufaidika kwa kuwa moja ya taasisi duniani ambayo imejidhatiti kutatua changamoto za wanawake na hasa kwenye masuala ya kiuchumi, kuongeza upatikanaji wa huduma na bidhaa zake, kuongeza ushirikiano pamoja na kukuza na kuongeza idadai ya wateja wake.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TWCC Mwanjuma Hamza alisema kuwa TWCC ni chama kinachounganisha wanawake kwenye sekta zote na mikoa yote, Tanzania Bara na Zanzibar.

Lengo letu ni kufanya wanawake wakue kiuchumi ikiwa ni pamoja na kukuza na kuendeleza biashara zao kwa kushiriki maonyesho kadhaa ya kibiashara ndani nan je ya nchi, alisema Hamza akiongeza kuwa kutoka Januari mpaka Disemba mwaka huu, wanawake wanachama wa TWCC walishiriki kwenye maonyesho kuanzia ngazi ya mkoa, taifa na kimataifa na hivyo kuwajengea uwezo wa kukuza biashara zao kutoka na ujuzi wanaoupata.

Akifafanua zaidi, Hamza alisema wanawake wananchama wa TWCC 150 walishiriki maonyesho nchini China, 100 Ujerumani na kwa sasa kuna wanawake wapatao 30 ambao wanaendelea na maonyesho Eldoret, Kenya.

NMB YAITOA MABATI 229 KUPIGA TAFU UJENZI WA WODI YA WAKINA MAMA HOSPITALI YA WILAYA YA MUHEZA

0
0
  Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Cosmas Gabriel kushoto akimkabidhi mabati 229 Katibu wa UWT Mkoani Tanga Sophia Nkupe kwa ajili ya ujenzi wa wodi wakina mama hospitali ya wilaya ya Muheza kulia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo
 Katibu wa UWT Mkoani Tanga Sophia Nkupe kulia akimkabidhi 229 Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo mabati 229 kwa ajili ya ujenzi wa wodi wakina mama hospitali ya wilaya ya Muheza kushoto ni Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Cosmas Gabriel
 Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo kushoto akimkabidhi mabati 229 Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza kwa ajili ya ujenzi wa wodi wakina mama hospitali ya wilaya ya Muheza kushoto ni Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Cosmas Gabriel
  Katibu wa UWT Mkoani Tanga Sophia Nkupe akizungumza katika halfa hiyo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo
  Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Cosmas Gabriel akizungumza katika halfa hiyo
Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza katika halfa hiyo kushoto ni Katibu wa UWT Mkoa wa Tanga Sophia Nkupe na kulia ni Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Cosmas Gabriel
 Meneja wa NMB Tawi la Muheza akizungumza katika halfa hiyo.
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muheza akizungumza katika Halfa hiyo kushoto ni Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Cosmas Gabriel
 Sehemu ya watumishi wa benki ya NMB wilaya Muheza wakiwa kwenye halfa hiyo
 Sehemu ya wananchi wilaya Muheza wakishuhudia makabidhiano hayo



NA MWANDISHI WETU, MUHEZA.

BENKI ya NMB nchini imetoa mabati 229 kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya wakima mama katika hospitali ya wilaya ya Muheza ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt John Magufuli kuhakikisha wananchi wanaondokana na changamoto za afya kwenye maeneo yao.

Halfa ya makabidhiano hayo yalifanyika mjini Muheza na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa maendeleo akiwemo Katibu wa UWT Mkoani Tanga Sophia Nkupe na Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo.

Akizungumza baada ya kupokea mabati hayo Katibu wa UWT huyo aliishukuru na kuwapongeza benki ya NMB kwa kuwakubalia ombi lao la kuwasaidia mabati kwa sababu wamekuiwa mstari wa mbele kusaidia lakini wanafanya hivyo kuunga mkono juhudui za Rais katika dhamirta yake ya kuhakikisha huduma za afya zinakuwa bora,.

Nkupe alisema pia wana mpongeza Rais Dkt John Magufuli kwa juhudi kubwa anazofanya kuhakikisha wananchi wanaondokana na changamoto mbalimbali ikiwemo za huduma ya afya na nyenginevyo

“Lakini pia nikushukuru Mh DC Mhandisi Mwanasha Tumbo kwa juhudi zako unazozifanya kuhakikisha wilaya ya Muheza inapata maendeleo makubwa pia niwaombe NMB mtusaidie wakina mama kwa sababu tunateseka sana wanachombezwa na taasisi mbalimbali za mikopo yenye riba kubwa”Alisema Katibu huyo wa UWT.

Awali akizungumza wakati akikabidhi msaada huo wa mabati Kaimu Meneja ya NMB Kanda ya Kaskazini Cosmas Gabriel Sadat alisema wameona watoe msaada huo kutokana na ushirikiano mkubwa ambao wamekuwa wakiupata hauna kifani huku wakiupongeza uongozi wa wilaya na Mganga Mkuu wa wilaya hiyo.

Alisema kwa sababu wakati DMO alipoona uwepo wa changamoto hiyo ya jengo la wakima mama hawakuwaza mbali nao na walijua kwamba mkombozi wao ni NMB na hivyo kupeleka maombi yao ambayo yalifanyiwa kazi kwa uhakika hatua iliyowawezesha kunufaika na msaada huo ambao utakuwa chachu kwao .

“Asanteni sana kwa kutupa dhamana hii,mliona mnawadau wa uhakika wa kupeleka kilio chenu,tunatambua juhudi kubwa za serikali hasa ya awamu ya tano zimekuwa na nguvu kuhakikisha watanzania wa kawaida wanaishi maisha ya neema”Alisema Kaimu Meneja huyo

Aidha alisema kwamba benki hiyo haiwezi kuiacha serikali bila kuisaidia wao wapo nao bega kwa bega na jamii popote pale nchini kuhakikisha inapata afya iliyo bora na elimu iliyobora ili neema ya watanzania wote tuweze kuionja.

Naye kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo alisifu juhudi kubwa zinazofanywa na benki hiyo kwa kuwapatia msaada huo na kuwaomba wasiwachoke waendelee kushirikiana nao ili kuhakikisha huduma za afya wilaya humo zinaweza kupatikana kwa urahisi ili kila mmoja anapotaka kupata aweze kufika kwa urahisi na kuweza kuendelea shghuli zao kwa wakati na kuchochea kasi ya maendeleo.

JESHI LA MAGEREZA LAZINDUA MPANGO MKAKATI WA MIAKA MITANO (2019-2023) DHIDI YA HIV/AIDS NA TB

0
0
Kamishna wa Huduma za Urekebishaji wa Jeshi la Magereza Augustine Mboje,ambaye alimuwakilisha Kamishna Jenerali wa Magereza (wa tatu toka kulia) akikata utepe kuzindua Mpango Mkakati wa miaka mitano dhidi ya HIV,AIDS na TB.
Kamishna wa Huduma za Urekebishaji wa Jeshi la Magereza Augustine Mboje,ambaye alimuwakilisha Kamishna Jenerali wa Magereza, akifungua kikao cha Mpango Mkakati wa miaka mitano dhidi ya HIV,AIDS na TB kwenye ukumbi wa kivukoni katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam tarehe 18 December 2018. Aliyekaa ni Kamishna wa Mafunzo Zanzibar, Ally Abdala.
Kamishna wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar, Ally Abdala akichangia mada kwenye mjadala wa Mpango Mkakati wa miaka mitano dhidi ya HIV, AIDS na TB.
Daktari Fulgency Binagwa akitoa semina ya Mpango Mkakati wa miaka mitano dhidi ya HIV,AIDS na TB kwenye ukumbi wa kivukoni katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Afisa Mradi Kitaifa wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayopambana dhidi ya madawa ya kulevya na uhalifu Bi. Immaculate Nyoni akimshukuru  Kamishna wa Huduma za Urekebishaji wa Jeshi la Magereza Augustine Mboje kwa kuzindua Mpango Mkakati dhidi ya HIV,AIDS na TB.
 Kamishna wa Huduma za Urekebishaji wa Jeshi la Magereza Augustine Mboje (wa tatu toka kushoto,walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau waliowezesha kukamilika kwa Mpango Mkakati wa miaka mitano dhidi ya HIV,AIDS na TB katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Picha zote na Jeshi la Magereza


KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI PWANI CHAKUSANYA MIL. 228.4 ZA MADENI

0
0

NA MWAMVUA MWINYI, PWANI 

JESHI la polisi mkoani Pwani, kupitia kikosi cha usalama barabarani limekusanya kiasi cha sh. milioni 228.440 za madeni ya makosa ya usalama barabarani .

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, kamanda wa polisi mkoani Pwani, Wankyo Nyigesa alisema ,fedha hiyo imepatikana kutokana na madereva waliofanya makosa kipindi cha nyuma kutakiwa kufanya hivyo . 

Alieleza, kwa muda mrefu kumekuwepo na tabia kwa madereva wanaofanya makosa na kuandikiwa kulipa tozo la serikali kwa njia ya POSS mashine kushindwa kufanya hivyo kwa dhana ya kuwa hawataweza kubainika kwa kuwa mfumo mpya wa ulipaji wa tozo humtaka dereva husika kwenda kulipia yeye ndani ya siku saba. 

Wankyo aliwataka, madereva ambao wanatambua kuwa wanadaiwa kulipa mara moja kwani hatutakuwa na muhali nao pindi watakapowakamata.Kamanda huyo alifafanua ,wanaendelea kupambama na mabasi yanayosafiri kupitia barabara za mkoa wa Pwani kwa kuyakagua na kuona kama yana ubora wa kufanya usafirishaji wa abiria. "Kudhibiti ujazaji ndani ya mabasi kwa kuweka abiria kwenye vigodoro, uzidishaji wa nauli kwa abiria kwa kushirikiana na SUMATRA, malori na kuyafanyia ukaguzi wa kina katika maeneo yao ya maegesho na yanapopita kwenye barabara zetu "alisisitiza. 

Wankyo alisema ,watadhibiti usafiri wa magari madogo aina ya Noah yanayobeba abiria kwa kushirikiana na SUMATRA yasizidishe abiria na yasiende umbali wa kilometa zaidi ya 50#.Pamoja na hayo wana mikakati waliyojiwekea kuendelea pia kutoa elimu kwa madereva wa pikipiki katika wilaya zote wapatao 444.

Alielezea, lengo kuu likiwa ni kuhakikisha wanapunguza ajali kwa waendesha pikipiki ambao wengi wao wamekuwa hawakidhi vigezo vya kuendesha vyombo vya moto, kutojua sheria na kanuni za usalama barabarani na udereva wa kujihami.

WIZARA YA ARDHI YASHIRIKI KUPAMBANA NA VVU/UKIMWI

0
0
kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mathias Kabundunguru, akifuatiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Utawala; Gideon Malabeja na Afisa Utumishi Mwandamizi; Joyce Mlowe katika ufunguzi wa Mafunzo Maalum ya Afya mahali pa kazi yaliyotolewa na Timu ya Wataalam wa Afya kutoka Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) na Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika ofisi za Wizara ya Ardhi – Dodoma. 
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mathias Kabundunguru akiwa kwenye zoezi la upimaji wa VVU/UKIMWI baada tu ya Mafunzo maalum ya Afya mahali pa kazi yaliyotolewa na Timu ya Wataalam wa Afya kutoka Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) na Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika ofisi za Wizara ya Ardhi – Dodoma. 
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mathias Kabundunguru akiwa kwenye zoezi la upimaji wa Uwiano wa Urefu na Uzito (Body Mass Index /BMI) baada tu ya Mafunzo maalum ya Afya mahali pa kazi yaliyotolewa na Timu ya Wataalam wa Afya kutoka Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) na Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika ofisi za Wizara ya Ardhi – Dodoma.


Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mathias Kabundunguru amewaongoza watumishi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika Upimaji hiari wa Virusi Vya UKIMWI (VVU) na UKIMWI na magonjwa mengine wakati wa Mafunzo maalum ya Afya katika mahali pa kazi, yaliyofanywa na Timu ya Wataalam wa Afya kutoka Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) na Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika ofisi za Wizara ya Ardhi – Dodoma.


Magonjwa mengine yaliyofanyiwa upimaji ni pamoja na Kisukari, Shinikizo la damu (Pressure) na Uwiano wa Urefu na Uzito (Body Mass Index /BMI).

Akiongea na Watumishi wa Wizara katika Mafunzo hayo. Bwn. Kabundunguru alisema; “ Mafunzo ya Afya kwa Watumishi ni muhimu na yanalenga kuwapa uelewa zaidi na kuwawezesha Watumishi kupima Afya, kutambua hali za Afya zenu mapema na kuwawezesha kuishi kulingana na hali ya afya zenu huku mkiendelea kutoa huduma katika Utumishi wa Umma”.

Naye Afisa mwitikio wa Taasisi za umma (Public institutions response officer, Dkt. Hafidh Ameir kutoka Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS); Pamoja na mambo mengine, alieleza kuwa dhumuni Kuu pia la Mafunzo ni kuwaarifu watumishi wa umma kuhusu umuhimu wa kuchukua tahadhari ya magonjwa husika, hususani VVU na UKIMWI. Alisema; “ Watumishi wa umma wanasisitizwa kutambua kwamba mbali ya kuwa suala la afya dhaifu huathiri uwezo wao wa kufanya kazi kwa ufanisi, pia linawaathiri wao binafsi, hivyo watumishi wenyewe wanawajibika pia kujali afya zao.

Akiongea katika Mafunzo hayo, mmoja wa watumishi wa Wizara ya Ardhi, mjumbe wa Mafunzo ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema; “ Kwakweli katika Mafunzo haya, mimi nimehamasika sana kupima VVU/UKIMWI japo sikuwa na mpango wa kufanya hivyo, ila Mtaalamu aliposisitiza kuwa hata kama unajua unavyoishi kuwa hakuhatarishi kupata magonjwa kama ya Ukimwi ila kuna njia nyingine ambazo mtu unaweza kupata UKIMWI bila kutarajia kabisa; kama zile njia za kupata michubuko katika utumiaji wa ncha kali katika mazingira ya kila siku mbalimbali tuliyopo, mfano; Majumbani na katika Saloon. Hivyo nimeona ni vyema nipime kuweza kutambua hali yangu kwa uhakika “.

Serikali katika jitihada za kudhibiti maambukizi ya VVU na UKIMWI, ilitoa Waraka wa Watumishi wa Umma Na. 2 wa mwaka 2006, ulioelekeza kutolewa huduma kwa Watumishi wa Umma wanaoishi na VVU na wenye UKIMWI. 
 
Madhumuni ya Waraka huo ilikuwa ni kuweka utaratibu wa namna ya kutoa huduma kwa watumishi wanaoishi na VVU na kuhamasisha watumishi kupima na kujua hali ya afya zao. 
 
Aidha, mwaka 2007, Serikali ilitoa Mwongozo wa Kudhibiti UKIMWI katika Utumishi wa Umma wa mwaka 2007. Mwongozo huo ulilenga kupunguza maambukizi ya VVU miongoni mwa Watumishi wa Umma na kutoa utaratibu wa kuwahudumia Watumishi wanaoishi na VVU na wale wenye UKIMWI mahali pa kazi katika Utumishi wa Umma.

Katika Mafunzo hayo ilielezwa kuwa Tanzania inapambana kutokomeza UKIMWI kabisa ifikapo mwaka 2030. Ilielezwa kuwa nchi nyingi nyingine zinaendelea kuhudumia wagonjwa wanaoishi na VVU, lakini zimeshafanikiwa kutokomeza UKIMWI.

WATUMISHI WA UMMA WATAKIWA KUWA TAYARI KUFANYA KAZI MAHALI POPOTE NCHINI ILI KUWAHUDUMIA WANANCHI

0
0
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akisisitiza uwajibikaji kwa watumishi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (hawapo pichani) alipoitembelea idara hiyo kwa lengo la kufahamu majukumu ya idara na kuhimiza uwajibikaji.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora alipoitembelea idara hiyo kwa lengo la kufahamu majukumu ya idara na kuhimiza uwajibikaji.
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Mathew Kirama (wa pili kutoka kulia) akifafanua majukumu ya Idara yake kwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (kulia) alipoitembelea idara hiyo kwa lengo la kufahamu majukumu ya idara na kuhimiza uwajibikaji.

………………………………………………………………………………

Watumishi wa umma wametakiwa kuwa tayari kufanya kazi mahali popote na katika mazingira yoyote nchini ili waweze kuwahudumia wananchi ambao ndio walengwa wakuu wa huduma zinazotolewa na Taasisi za Umma.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) alipokutana na watumishi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa lengo la kufahamu majukumu ya Idara hiyo na kuhimiza uwajibikaji.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema, kitendo cha watumishi wa umma kuwa tayari kufanya kazi mahali popote na katika mazingira yoyote bila kujali maslahi binafsi kinaashiria uzalendo kwa Taifa na kinatoa haki kwa wananchi katika maeneo yote hususan ya pembezoni kupata huduma bora wanayostahili.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa ameitaka Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma kutorubuniwa na baadhi ya watumishi na waajiri wanaoomba vibali vya uhamisho kwa maslahi binafsi hivyo kuathiri utoaji huduma kwa umma.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa ameongeza kuwa, Idara hiyo inatakiwa kujiridhisha na hoja zinazowasilishwa kuombea vibali vya uhamisho kama hoja hizo zina tija na manufaa katika maendeleo ya Taifa.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesisitiza kuwa, watanzania wote wana haki sawa ya kupata huduma bora bila kujali mazingira waliyopo hivyo, ni wajibu wa Idara hiyo kuhakikisha kuwa uhamisho wa watumishi hauathiri mahitaji ya huduma kwa wananchi.

Awali, akielezea majukumu ya idara yake, Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Bw. Mathew Kirama amesema, Idara hiyo ina Sehemu ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Sehemu ya Watumishi Waandamizi na Sehemu ya Huduma na Ushauri wa Kisheria ambazo kwa pamoja zinalenga kufanikisha uendeshaji wa utumishi wa umma kwa kuwezesha Taasisi za Serikali kupata watumishi wenye sifa na weledi unaohitajika kulingana na malengo yanayotekelezwa na Taasisi hizo.

Bw. Kirama amefafanua kuwa, idara hiyo ina jukumu la kutoa ushauri wa kitaalamu kwa waajiri na watumishi kuhusu sera, sheria, kanuni na nyaraka mbalimbali za masuala ya ajira katika Utumishi wa Umma, kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu masuala ya sheria ikiwa ni pamoja na kusimamia taratibu mbalimbali zinazotawala utumishi wa umma.

Akizungumzia suala la uhamisho, Bw. Kirama amesema, katika kuleta tija na ufanisi kwenye utumishi wa umma, watumishi wa umma wanaruhusiwa kuhama ikiwa wamezingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo iliyopo likiwemo sharti la kukaa kwenye kituo kimoja cha kazi si chini ya miaka mitatu na uwepo wa nafasi iliyotengewa fedha kwenye kituo husika. Aidha alieza kuwa, Serikali inaweza kumhamisha mtumishi kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma katika maeneo yenye upungufu wa watumishi.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) ameitembelea Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake katika Idara na Vitengo vya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ili kuhimiza uwajibikaji.

KUAHIRISHWA KWA KIKAO CHA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA KILICHOPANGWA KUFANYIKA TAREHE 21 NA 22 DISEMBA, 2018 ZANZIBAR

0
0
Natumia fursa hii kuwafahamisha wajumbe wote wa Baraza la Vyama vya Siasa kuwa, nimepokea taarifa rasmi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa, tarehe 20 Disemba, 2018 kutakuwa na zoezi la uteuzi wa wagombea Katika Jimbo la Temeke Dar-es Salaam na Kata 48 zilizopo katika maeneo ya Wilaya mbalimbali za Tanzania Bara.

Kimsingi, matukio yote mawili, uteuzi wa wagombea wa ubunge na udiwani uliopangwa kufanyika tarehe 20 Disemba, 2018 na kikao cha Baraza la Vyama vya Siasa kilichopangwa kufanyika tarehe 21 na 22 Disemba, 2018 ni muhimu na hayo yote yanahusisha wadau walewale. Tofauti ni kuwa, ni rahisi kuahirisha kikao cha Baraza la Vyama vya Siasa kuliko kuahirisha siku ya uteuzi wa wagombea.

Hivyo, Kwa mujibu wa Kanuni ya 16(4) ya Kanuni za Baraza la Vyama vya Siasa, nimeshauriana na wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa na tumeamua kuahirisha kikao cha Baraza la Vyama vya Siasa mpaka baada ya uchaguzi mdogo wa tarehe 19 Januari, 2018, ili kuwezesha Vyama vya Siasa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mdogo wa tarehe 19 Januari, 2018.

Tunaomba samahani kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

MASAUNI AONGOZA MAOMBI MAALUMU YA KUMUOMBEA RAIS DKT. MAGUFULI NA KUOMBEA UCHAGUZI MKUU WA SERIKALI ZA MITAA

0
0

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati wa Dua Maalumu ya Kumuombea Rais kwa kutimiza Miaka mitatu madarakani na Kuombea Uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa.Kulia ni Askofu Silvestre Gamanywa na Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano Tanzania iliyoandaa maombi hayo, Asha Kassim.Maombi hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Sabasaba, jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akionyesha Tuzo ya Heshima aliyopewa Rais Dkt. John Magufuli na Jumuiya ya Maridhiano wakati wa Dua Maalumu ya Kumuombea Rais kwa kutimiza Miaka mitatu madarakani na Kuombea Uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Jumuiyahiyo, Asha Kassim. Maombi hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Sabasaba, jijini Dar es Salaam.
Sheikh Nurdin Mangochi akizungumza wakati wa Dua Maalumu ya Kumuombea Rais kwa kutimiza Miaka mitatu madarakani na Kuombea Uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa..Maombi hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Sabasaba, jijini Dar es Salaam.
Askofu Silvestre Gamanywa akizungumza wakati wa Dua Maalumu ya Kumuombea Rais kwa kutimiza Miaka mitatu madarakani na Kuombea Uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa.Maombi hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Sabasaba, jijini Dar es Salaam
Viongozi wa dini wakiwa katika Dua Maalumu ya Kumuombea Rais kwa kutimiza Miaka mitatu madarakani na Kuombea Uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa. Maombi hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Sabasaba, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi




Watanzania wametakiwa kuwa wamoja na kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli kwa kumuombea dua katika kipindi hiki ambacho nchi inapitia kipindi cha mabadiliko makubwa ya kiuchumi huku Serikali ikikataa kupokea misaada yenye masharti ya kudhalilisha mila na desturi za Watanzania.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, wakati akimuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika Dua Maalumu ya Kumuombea Rais Magufuli na Kuombea Amani Uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa, iliyoandaliwa na Taasisi ya Kidini ya Maridhiano Tanzania, katika Ukumbi wa Mikutano wa Sabasaba,jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa maombi hayo Naibu Waziri Masauni alisema nchi sasa inapitia kipindi cha mabadiliko makubwa ya kiuchumi yanayosimamiwa na Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli lengo ikiwa ni kuifanya Tanzania isiwe tegemezi na kupewa masharti yanayodhalilisha mila, tamaduni na dini zetu.

“Watanzania tumuunge mkono Rais Magufuli, anayoyafanya ni kwa faida ya Watanzania wote bila kujali dini, rangi, kabila au itikadi na hatutakuwa tayari kupangiwa na wageni ambao wanatuletea mambo ya hovyo,demokrasia ya nchi yetu tunaijua wenyewe Watanzania na sio aje mtu kutoka nje atuambie demokrasia ya kufuata, hawezi kuja mtu atupangie tufuate mambo ya ushoga,” alisema Masauni

Akizungumza katika dua hiyo, Sheikh Nurdin Mangochi aliwataka Watanzania waitunze amani iliyopo na wala wasikubali kushawishiwa na mtu yoyote kuvuruga amani iliyopo.“Kuna nchi jirani amani imetoweka na tunaona madhara yake, muhimu hii amani tuliyonayo tuitunze na kuilinda kwani nchi yetu Tanzania imekua darasa la amani kwa nchi jirani wanaokuja kujifunza jinsi Watanzania tunavyoishi bila kuwepo machafuko,” alisema Sheikh Mangochi

Naye Askofu Silvestre Gamanywa aliwataka Watanzania kuwa na Uzalendo na nchi yao kwa kuiongelea mema nchi katika maisha yao yote hali itakayopelekea kuwapo na mapenzi ya nchi kwa kila mtanzania.

“Uzalendo sio lazima kufia nchi yako,uzalendo ni kuwa na mtazamo chanya wa kuisemea na kuitetea nchi yako pamoja na kuitalia mema na sio kuiongelea vibaya,” alisema Askofu Gamanywa
Viewing all 46193 articles
Browse latest View live




Latest Images