Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46194 articles
Browse latest View live

Hafla ya kuwapongeza Waalimu Kata ya Mecco Manispaa ya Ilemela yafana

0
0
Diwani Kata ya Mecco Manispaa ya Ilemela, Godlisten Kisanga (CCM) akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha pamoja na waalimu wote wa Shule tatu za Msingi (Nundu, Nundu D na Nyamwilekelwa) katika Kata hiyo iliyolenga kuwapongeza waalimu hao kwa juhudi zao za kuimarisha ufaulu kwa wanafunzi wanaohitimu darasa la saba.
Afisa Elimu Kata ya Mecco Manispaa ya Ilemela, Mwl. Agnes Mugyabuso (kushoto), Shule zilizofanya vizuri kwa kila somo katika Kata hiyo kwenye mtihani wa darasa la Saba mwaka huu ambapo Shule hizo zilikabidhiwa cheti cha pongezi na Diwani wa Kata ya Mecco, Godlisten Kisanga.
Diwani Kata ya Mecco Manispaa ya Ilemela, Godlisten Kisanga (kulia), akimkabidhi Cheti cha pongezi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nyamwilekelwa, Mwl. Lyatura Mukama (kushoto) baada ya Shule yake kuibuka kidedea kwenye masomo ya Kiswahili na Kiingereza.
Alama za ufaulu/ ushindi zilizoshindanishwa ni A na B tu
Diwani Kata ya Mecco Manispaa ya Ilemela, Godlisten Kisanga (kulia), akimkabidhi Cheti cha pongezi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nundu D, Mwl. Lucas Robert (kushoto) baada ya Shule yake kuibuka kidedea kwenye masomo ya Hisabati na Maarifa ya Jamii.
Utaratibu huu wa kushindanisha Shule za Msingi Kata ya Mecco umelenga kuongeza kiwango cha ufaulu kwa alama A na B tu.
Diwani Kata ya Mecco Manispaa ya Ilemela, Godlisten Kisanga (kulia), akimkabidhi Cheti cha pongezi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nundu, Mwl. Charles Njuka (kushoto) baada ya Shule yake kuibuka kidedea kwenye somo la Sayansi.
Mtendaji Kata ya Mecco akitoa neno la pongezi kwa waalimu wa shule za Msingi katika Kata hiyo.
Diwani wa Kata jirani ya Buzuruga, Richard Machemba (Chadema), akiwasilisha salamu zake za pongezi kwenye hafla hiyo.
Mwakilishi wa mbunge Jimbo la Ilemela, akiwasilisha salamu zake.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Mecco, Charles Matiku akiwasilisha salamu zake kwenye hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Manispaa ya Ilemela, Mohamed Yusuph akizungumza kwenye hafla hiyo ambapo aliahidi kuanzia mwakani atasaidia kudhamini mitihani mbalimbali ya ushindani ili kuwajengea uwezo zaidi wanafunzi.
Baadhi ya waalimu wa Shule za Msingi Kata ya Mecco wakiwa kwenye hafla hiyo.
Baadhi ya waalimu wa Shule za Msingi Kata ya Mecco wakiwa kwenye hafla hiyo.
Diwani wa Kata ya Mecco Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, Godlisten Kisanga (CCM) amewapongeza waalimu wote wa Shule za Msingi katika Kata hiyo kwa juhudi zao za kuhakikisha kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa darasa la saba kinazidi kuongeza.


Kisanga alitoa pongezi hizo jana Disemba 06, 2018 kwenye hafla ya chakula cha pamoja na waalimu hao kutoka Shule za Msingi Nundu, Nundu D na Nyamwilekelwa iliyolenga kuwapongeza na kukabidhi vyeti vya pongezi kwa Shule zilizofanya vizuri kwa kila somo kwenye matokeo mtihani wa darasa la saba.
Tazama BMG Online TV hapa chini

Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo, BMG

MAGAZETI YA LEO IJUMAA DESEMBA 7,2018

0
0















NSSF YAJIPANGA KUPELEKA TAIFA KWENYE UCHUMI WA VIWANDA

0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

SHIRIKA la taifa la hifadhi ya jamii (NSSF) limeshiriki katika maonesho ya tatu ya bidhaa za viwanda vya Tanzania yaliyozinduliwa rasmi leo katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es salaam kwa kutoa huduma kwa wajasiriamali ikiwa ni mchakato kwa kukamilisha azma ya ujenzi wa Tanzania ya viwanda.

Akizungumza na blogu ya jamii Afisa mwandamizi kitengo cha sekta isiyo rasmi  (NSSF) Abas Cothema amesema kuwa, wameungana na shirika la kuhudumia viwanda vidogo vidogo nchini (SIDO)  katika maonesho hayo ya bidhaa za viwanda zinazozalishwa nchini ikiwa ni  kuunga mkono  jitihada za Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais Dkt. John Magufuli iliyodhamiria kujenga Tanzania ya viwanda.

Amesema kuwa NSSF imeshiriki maonesho hayo ili kuhakikisha wanawapatia hifadhi ya jamii wajasiriamali ili waweze kukingwa dhidi ya majanga yanayosababisha  upotevu wa kipato na kuwapa pensheni ya uzeeni, pensheni ya ulemavu, pensheni ya  urithi na bima ya afya ambazo vyote hivyo ni muhimu katika ujenzi wa Tanzania mpya ya viwanda.

Cothema amesema kuwa mwanachama akishiriki kwa kuchangia ada ya kima cha shilingi elfu ishirini kwa muda wa miezi mitatu atapata bima yeye na wategemezi wake wanne yaani watoto wanne walio na umri chini ya miaka 18 na watoto wanaosoma walio chini ya miaka 21 pamoja na mtegemezi wake na malengo ya kufanya hivyo ni kumkinga mwanachama na majanga ya maradhi na magonjwa ili aweze kuendelea na shughuli za ujenzi wa uchumi ambao Serikali umejizatiti kuufikia pia kufanya hivyo ni kusaidia serikali katika kutoa huduma kwa wananchi wake.

Ameeleza kuwa NSSF wana miradi mbalimbali ya kiuchumi ambayo imelenga kuwasaidia wananchi wa hali zote ikiwa ni pamoja na  viwanja vilivyo katika maeneo ya kiluvya na visiga ambavyo hupatikana kwa gharama ambayo kila mwananchi anaweza kumudu hata kwa mkopo au kwa malipo ya muda mrefu.

Pia amesema kuwa wanashirikiana bega kwa bega na serikali na wadau mbalimbali katika kuhakikisha azma ya ujenzi wa Tanzania ya  viwanda na kufikia uchumi wa kati mwaka 2025 inafikiwa.
Naibu wa Viwanda Biashara na Uwekezaji,Mhandisi Stella Manyanya aliyeambatana na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara,Edwin   Rutageruka, akisalimiana na mmoja wa afisa wakitego cha sekta isyo rasmi wa (NSSF) wakati alipotembelea Shirika la Taifa la hifadhi ya jamii (NSSF)  leo jijini Dar es Salaam katika  maonyesho Tatu ya Bidhaa za Viwanda.
Naibu Waziri wa Viwanda biashara na uwekezaji,Mhandisi Stella Manyanya (kushoto) akisisitiza jambo kwa,Abbas Cothema Ofisa Matekelezo kutoka Kitengo cha Hiari-NSSF alipotembelea banda la NSSF ndani ya maonyesho ya tatu ya bidhaa za wiwanda vya hapa nchini yaliyo funguliwa leo jijini Dar es Salaam.
Ofisa Matekelezo kutoka Kitengo cha Hiari-NSSF    Abbas Cothema akizungumza na Michuzi blog  katika maonyesho ya tatu ya bidhaa za wiwanda vya hapa nchini yaliyo funguliwa leo jijini Dar es Salaam.

Benki ya Azania Yazindua Rasmi Tawi lake Dodoma.

0
0
Benki ya Azania imezidi kujitanua baada ya hii leo kuzindua tawi lake jipya jijini Dodoma ikiwa ni muendelezo wa mkakati wa benki hiyo katika kukuza mtatandao wa matawi yake sambamba na kuunga mkono jitihada za Mh Rais John Magufuli kuifanya Tanzania kuwa nchi ya Viwanda, kupitia huduma bora za kibenki.

Akizungumza kwenye hafla fupi ya Uzinduzi wa tawi hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Charles Itembe alisema kwa sasa benki hiyo ina matawi kumi na tisa ikiwemo tawi hilo jipya lililopewa jina la Sokoine- Dodoma ikiwa ni ishara ya benki hiyo kutambua mchango wa Waziri Mkuu wa zamani, Hayati Edward Moringe Sokoine katika ustawi wa taifa kwa ujumla.

“Malengo yetu ya kimkakati kwa sasa ni kukuza mtatandao wa matawi ya benki yetu , angalau matawi matatu kwa mwaka, na pia kukuza nafasi yetu ya umiliki wa soko( Market share) angalau kwa 3% ndani ya miaka mitatu.’’ Alisema Bw Itembe. Alisema nia ya benki hiyo ni kuwa katika hadhi ya Mabenki Makubwa daraja la kwanza( Tier One ) ndani ya miaka hii mitano ya kimkakati wa kibiashara.

Akizungumzia uamuzi wa kufungua tawi hilo jijini humo, Bw Itembe alisema: “Dodoma ni katikati ya nchi, pili ni makao makuu ya shughuli za kiserikali na pia ni mkoa unaokuwa kwa kasi kibiashara.’’ Aidha, alibainisha kuwa kupandishwa hadhi kwa manispaa ya Dodoma na kuwa jiji kumeiweka benki hiyo katika nafasi nzuri kwa kuwa ukuaji wa jiji hilo unaendana sambamba na mahitaji ya kifedha.

“Katika kuunga mkono sera ya Mh Rais John Magufuli ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya Viwanda, ni lazima kuwa na mbinu ya kuweza kukuza kipato kupitia kufanya biashara na benki zenye msingi imara… Azania Benki tupo tayari kushirikiana na wananchi na serikali katika kufanikisha hilo,’’ alisema.

Akizungumza muda mfupi kabla hajazindua rasmi tawi hilo, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji mbali na kuipongeza menejimenti ya benki hiyo, alitoa changamoto kwa taasisi za fedha hapa nchini ikiwemo benki hiyo kuhakikisha zinajipanga kikamilifu kukabiliana na suala la mikopo chechefu sambamba na kupunguza gharama za uendeshaji ili ziweze kuwahudumia wateja wake kwa gharama za chini zaidi ikilinganishwa na hali ilivyo sasa.

“Chanzo cha mikopo chefu ni watumishi wasio waadirifu kwenye taasisi hizi na ndio maana naomba sana bodi na menejimenti ziwachukulie hatua sambamba na kupunguza gharama za uendeshaji kwasababu sisi kama serikali hatutavumilia uzembe wa aina yoyote katika utekelezaji wa hili.’’ Alisema. Dk Kijaju alitolea mfano uamuzi wa Benki Kuu kushusha riba kwa mabenki ya biashara kutoka asilimia 16 hadi asilimia 9, kuwa unalenga kuwapunguzia mzigo wa riba wateja wa benki hizo.

Aidha Dk Kijaji alionyesha kuridhishwa zaidi na namna benki hiyo inavyotoa kipaumbele katika kuboresha sekta ya ujasirimali mdogo na wa kati hatua aliyotaja kuwa itawasaidia makundi hayo kutoa mchango mkubwa katika sekta mbalimbali , ikiwemo ya viwanda vidogo ambayo ndiyo nia ya Serikali ya awamu ya tano.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo, Bw Eliud Sanga alisema benki hiyo inaenda vizuri kimikakati na kiutendaji na ndio maana mwaka wa kifedha ulioisha Desemba 2017, ilifunga na faida ya Tsh 1.8 bn/- toka kwenye hasara ya shs. 6 bn/- mwaka uliopita na kuweza kutoa gawiwo la faida kwa wanahisa wake.

Ili kufanikisha shughuli za kibenki hapa nchini hasa katika mkakati wa kujenga uchumi wa viwanda Bw Sanga alishauri masuala kadhaa ikiwemo kuwekeza nguvu ya elimu katika masuala ya fedha pamoja na vigezo vya kupata mikopo kwa kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati.

“Pia kuendelea na juhudi na kwa kasi nzuri ya kuboresha miundo mbinu kama vile barabara,umeme na huduma nyingine za msingi ili wafanyabiashara hawa waweze kufanya biashara zao kwa gharama ndogo zaidi na mabenki yaweze kuvutika kuwekeza maeneo hayo.’’ Alitaja.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi jipya la benki ya Azania linalofahamika kwa jina Sokoine-Dodoma wakati wa hafla fupi ya uzinduzi huoiliyofanyika jijini Dodoma leo. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Charles Itembe (kushoto) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo, Bw Eliud Sanga. 
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki ya Azania Bw Eliud Sanga (wa pili kushoto) akikabidhi zawadi maalum aliyoandaliwa iliyoandaliwa kwa ajili ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji (wa pili kulia) wakati wa hafla hiyo. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Charles Itembe (kulia). 
 Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Azania ,  Charles Itembe akizungumza kwenye hafla hiyo. 
 Muwakilishi wa familia ya Hayati Edward Moringe Sokoine akitoa salamu za familia kwenye hafla hiyo. Tawi hilo jipya limepewa jina la Sokoine- Dodoma  ikiwa ni ishara ya benki hiyo kutambua mchango wa Waziri Mkuu wa zamani,  Hayati Edward Moringe Sokoine katika ustawi wa taifa kwa ujumla.
 Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Gilles Muroto (kulia) akiwasili kwenye uzinduzi huo. Pamoja na mambo mengine Kamanda Muroto alizitoa hofu taasisi za kifedha jijini humo kuhusiana na suala zima la kiusalama kwa kuwa jeshi la Polisi jijini humo limejipanga kikamilifu kukabiliana na waalifu. 
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki ya Azania Bw Eliud Sanga akizungumza kwenye hafla hiyo.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji (kushoto) akisaini kitabu cha wageni wakati wa hafla hiyo. Anaeshuhudia ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Charles Itembe.
 Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Azania wakifuatilia matukio mbalimbali ikiwemo hotuba ya Naibu Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji wakati wa hafla hiyo.
 Baadhi ya wateja na wageni waalikwa wa benki ya Azania wakifuatilia matukio mbalimbali ikiwemo hotuba ya Naibu Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji wakati wa hafla hiyo.
 Muonekano wa ndani wa Tawi la benki ya Azania jijini Dodoma linalofahamika kwa jina la Sokoine-Dodoma.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji (katikati walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi na wafanyakazi wa benki ya Azania mara baada ya kuzindua rasmi tawi hilo jipya.
Burudani ya ngoma kutoka kwa kikundi cha Mwinamila ikiwaburudisha wageni waalikwa pamoja na wafanyakazi wa benki ya Azania wakati wa uzinduzi wa tawi hilo.


KATIBU MKUU KIONGOZI ATEMBELEA ENEO LA UJENZI WA MJI WA SERIKALI IHUMWA DODOMA.

0
0

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi akikagua michoro ya ramani ya Mji wa Serikali wa Ihumwa Jijini Dodoma alipotembelea kukagua hali ya ujenzi wa majengo ya Ofisi za Serikali, kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi.Maimuna Tarishi na wa kwanza kushoto ni Katibu wa Kikosi kazi cha Kitaifa cha kuratibu Mpango wa Serikali kuhamia Dodoma Bw.Meshach Bandawe.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi.Maimuna Tarishi akimuonesha Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi michoro ya ramani ya ujenzi wa Majengo ya Ofisi za Serikali Ihumwa wakati wa ziara yake eneo la Ihumwa Desemba 6, 2018.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof.Kitila Mkumbo wakati alipotembelea eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya Wizara yake katika Mji wa Serikali Ihumwa Dodoma, Desemba6, 2018.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi akiuliza jambo kuhusu ujenzi wa Ofisi za Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa Mhandisi kutoka SUMAJKT, Zabron Mahenge wakati wa ziara yake eneo lililotengwa kwa ujenzi wa Ofisi za Serikali la Ihumwa Dodoma.
Katibu wa Kikosi kazi cha Kitaifa cha kuratibu Mpango wa Serikali kuhamia Dodoma Bw.Meshach Bandawe akimuongoza Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi kuelekea eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ihumwa Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi akionesha jambo kwa Mhandisi kutoka TBA, Amon Nghamba wakati wa ziara yake katika eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ihumwa Dodoma .
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi akimsikiliza Msanifu Majengo Moses Wadelanga wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa ujenzi wa Majengo ya Ofisi za Serikali Ihumwa Dodoma.
Katibu wa Kikosi kazi cha Kitaifa cha kuratibu Mpango wa Serikali kuhamia Dodoma Bw.Meshach Bandawe akizungumza jambo kwa baadhi ya wajumbe wa kikosi kazi cha Miundombinu wanaoratibu ujenzi wa miundombinu katika Mji wa Serikali wa Ihumwa.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi akimsikiliza Msanifu Majengo Moses Wadelanga akifafanua jambo juu ya ujenzi wa Majengo ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika eneo la Ihumwa Jijin I Dodoma.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi (mwenye kofia ya kijivu) akikagua ujenzi wa Majengo ya Ofisi za Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora eneo la Ihumwa Jijini Dodoma wakati wa ziara yake eneo hilo.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi akifuatilia maelezo kuhusu michoro ya ujenzi wa Majengo ya Ofisi za Serikali Ihumwa Kutoka kwa Mkurugenzi Wakala wa Serikali Mtandao Bw.Michael Moshiro wakati wa ziara yake eneo hilo.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

MKUTANO KAZI BAINA YA WADAU WA MAENDELEO, MAAFISA WA SERIKALI NA WATENDAJI TASAF WAMALIZIKA KWA MAFANIKIO JIJINI DAR

0
0
Na Estom Sanga-DSM 

Mkutano wa Wadau wa Maendeleo ,Maafisa wa Serikali na Watendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF uliojadili kwa kina utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambao unatekelezwa na Serikali kupitia TASAF umemalizika jijini Dar es Salaam. 

Mkutano huo ambao hufanyika kila baada ya miezi sita , umefanyika kufuatia ziara ya washiriki hao katika wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza na Unguja ambako walikutana na Walengwa wa Mpango huo na kujionea namna Walengwa wanavyoendelea kunufaika na huduma zinazotolewa na Mpango huo kuboresha maisha yao. 

Miongoni mwa mambo yaliyofanywa katika mkutano huo ni pamoja na kuweka mkakati wa utekelezaji wa awamu ya pili ya Mpangowa Kunusuru Kaya Maskini inayotarajiwa kuanza Mwezi Aprili hapo mwakani ambayo italenga zaidi katika kuwashirikisha Walengwa kufanyakazi za maendeleo kwenye maeneo yao na kisha kulipwa ujira. 

Akizungumza na Washiriki wa Mkutano huo Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF,Bw. Ladislaus Mwamanga ametoa wito maalumu kwa wadau na maafisa wa Mfuko huo kufanya kazi kwa bidii na kuweka mbele maslahi ya taifa ili lengo la serikali la kuwapunguzia kero ya umaskini wananchi liweze kufikiwa kwa ufanisi. 

Bwana Mwamanga amesema utekelezaji na mafanikio ya Mpango huo unategemea kwa kiwango kikubwa jitihada za pamoja hasa ikizingatiwa kuwa wananchi wanaolengwa ni wale ambao kwa kiwango kikubwa wamekuwa wakiishi katika hali ya umaskinina wengine kukata tamaa jambo ambalo amesema linapaswa kukabiliwa kwa nguvu za pamoja. 

Kwa upande wake Kiongozi wa shughuli za TASAF katika Benki ya Dunia hapa nchini Bwana Mohamed Muderis amepongezea jitihada za dhati zinazofanywa na Watumishi wa TASAF na wadau wengine katika kuwahudumia Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini na hivyo kuleta hamasa ya dhati ya Walengwa kuuchukia umaskini. 

Aidha Bwana Muderis ametoa rai kwa watumishi hao kuendelea na kukamilisha kwa wakati maandalizi ya sehemu ya pili ya Mpango wa kunusuru kaya maskini inayotarajiwa kuanza mapema mwakani na kuzingatia kwa dhati maelekezo ya serikali . 

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF upo kwenye maandalizi ya sehemu ya pili ya Mpango wa kunusuru Kaya Maskini baada ya kukamilika kwa sehemu ya kwanza huku mkazo ukiwekwa kuwawezesha walengwa kushiriki katika kazi za Ajira ya Muda, kuunda vikundi vya kuweka akiba na kukopeshana,ujenzi wa miundombinu hasa katika sekta za elimu, afya ,maji na kuanzisha shughuli za uzalishaji mali ili kujiongezea kipato.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Bw. Ladslaus Mwamanga (katikati) akiongoza mkutano wa Wadau wa Maendeleo, Maafisa wa Serikali na TASAF kwenye ukumbi wa Mfuko huo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Washiriki wa Mkutano wa Wadau ,Serikali na TASAF wakiwa kwenye ukumbi wa Mikutano wa TASAF jijini DSM katika mkutano uliojadili utekelezaji wa Shughuli za Mfuko huo na maandalizi ya awamu ya pili ya Mpango huo inayotarajiwa kuanza hapo mwakani.
Mmoja wa Watumishi wa TASAF,Shadrack Mziray akiwasilisha taarifa kwenye Mkutano wa Wadau ,serikali na TASAF jijini Dar es salaam.
Picha ya juu na chini menejimenti ya TASAF na ile ya Benki ya Dunia hapa nchini wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa TASAF, Serikali Na Wadau wa Maendeleo baada kuhudhuria mkutano wao wa pamoja jijini Dar es salaam.

MFANYABIASHARA JIJINI ARUSHA HANSPAUL AHUKUMIWA KULIPA FAINI YA MILIONI 60 AU KWENDA JELA MIAKA 2

0
0
NA Vero Ignatus -ARUSHA

MFANYABIASHARA maarufu Jijini Arusha,Kamaljit Hanspaul (58), anayejishughulisha na shughuli mbalimbali na wenzake watatu wamehukumiwa kulipa faini ya Sh Milioni 60 au kwenda jela miaka miwili kila mmoja baada ya kukutwa na hatia ikiwemo kuajiri wafanyakazi watatu raia wa kigeni kufanya kazi nchini bila vibali.

Mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha,washitakiwa wengine ambao uraia uko kwenye mabano Vemula Shivakumar, (27), (India) Sathasivam Krishanth, (29) (India) na Ralph Leonard, (54), (Ujerumani),ambapo watuhumiwa wote wanne walikiri kutenda makosa hayo mwanzoni mwa wiki.

Akisoma hukumu hiyo jana,Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo,Niku Mwakatobe,alisema Mahakama hiyo imemtia hatiani Hanspaul katika mashitaka matatu ambayo ni kuajiri raia watatu wa kigeni ambao hawakuwa na vibali vya kufanya kazi nchini.

Alisema baada ya mshitakiwa huyo kukiri mashitaka hayo Mahakama inamtoza faini ya Sh Milioni 10 kila kosa au kifungo cha miaka miwili,huku washitakiwa wengine wakitozwa faini ya Sh Milioni 10 kila mmoja au kifungo cha miaka miwili baada ya kukutwa na hatia ya kufanya kazi nchini bila vibali.

Washitakiwa wote wanne waliachiwa huru baada ya kulipa faini hiyo Sh Milioni 60,ambapo katika uamuzi wake,Hakimu Niku aliwataka raia hao iwapo wanataka kuendelea kufanya kazi hapa nchini,wafuate taratibu na sheria zilizowekwa.

Katika shauri hilo jamhuri ilikuwa ikiwakilishwa na Wakili Khalili Nuda huku utetezi ukiwakilishwa na Wakili Salumi Mushi,ambaye aliiomba Mahakama ipunguze adhabu ikizingatiwa ni mara ya kwanza kwa washitakiwa hao kukutwa na hatia na kuwa washitakiwa watatu ambao ni raia wa kigeni walishaaanza taratibu za kufuatilia vibali vya kufanya kazi nchini.

Naye Wakili Nuda aliiomba Mahakama licha ya watuhumiwa wote kutokuwa na rekodi ya kukutwa na hatia,wanaomba Mahakama iwaadhibu kwa mujibu wa sheria na kuomba iwaagize iwapo wanataka kuendelea kufanya kazi hapa nchini wafuate sheria na taratibu.

Awali katika shauri hilo namba 389 la mwaka huu kabla ya kusomewa hukumu hiyo washitakiwa hao walisomewa maelezo ya awali,ambapo Wakili Nuda alidai mshitakiwa wa kwanza,aliwaajiri Shivakumar, Krishanth na Ralph kufanya kazi kama washauri kwenye kampuni yake ya HansPaul Automechs iliyopo maeneo ya Njiro jijini hapa wakati akijua hawana vibali vya kufanya kazi nchini.

WAZIRI UMMY ATOA ONYO KWA WAUGUZI WANAOVUNJA MAADILI YA KAZI

0
0

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akipitia ubao wa matangazo ya gharama za matibabu katika Hospitali ya Rufaa Nanyumbu, akiwa katika ziara yake ya kukagua hali ya utoaji wa huduma za Afya na uhamasishaji kwa wananchi kujiunga na Bima ya Afya Mkoa wa Mtwara.
Waziri wa Afy, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akisoma cheti cha mtoto aliyefikishwa na baba yake Hospitali ya Wilaya Nanyumbu ili kupata huduma za Afya.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akisisitiza jambo mbele ya wananchi wa Nanyumbu (hawapo kwenye picha), wakati wa ziara yake ya kukagua hali ya utoaji wa huduma za Afya na uhamasishaji kwa wananchi kujiunga na Bima ya Afya Mkoa wa Mtwara.

Wananchi wa Nanyumbu wakiongozwa na Wazee waliojitokeza kumsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu pindi alipokuwa katika ziara yake ya kukagua hali ya utoaji wa huduma za Afya na uhamasishaji kwa wananchi kujiunga na Bima ya Afya Mkoa wa Mtwara.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiwasalimia wanafunzi wa shule ya awali pindi tu alipowasili kwaajili ya mkutano wa hadhara na wananchi wa Nanyumbu ili kusikiliza kero zao na kuwaeleza Maendeleo ya Sekta ya Afya kwaujumla.

Na WAMJW - Nanyumbu, Mtwara

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu ametoa onyo Kali kwa Wauguzi wote kwenye vituo vya  kutolea huduma za afya nchini wanaovunja maadili na miiko ya kazi za uuguzi ikiwemo matumizi ya lugha chafu kwa wagonjwa na wanaowapiga akina mama wajawazito wakati wakijifungua.

Ameyasema hayo  wakati alipotembelea Hospitali ya Wilaya Nanyumbu, akiwa katika ziara yake Mkoani Mtwara ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya na uhamasishaji kwa wananchi juu ya umuhimu wa kujiunga na Bima ya Afya hasa katika msimu huu wa Biashara ya Korosho.

Waziri Ummy alisema kuwa Serikali kupitia Baraza la Uuguzi litawafutia usajili Muuguzi yeyote atakayegundulika ametenda kosa la kumpiga mama mjamzito au kumtolea lugha chafu wakati wa kujifungua.

"Tunataka kumjua huyo, ambae ni hodari sana wakupiga wanawake wajawazito, makofi wakati wakujifungua, kwa kweli huyo ni wa kumfukuza kazi, Mimi mkiniletea namfutia Leseni yake kabisa, hafanyi kazi Serikalini, hafanyi kazi Sekta Binafsi" alisema Waziri Ummy.

Pia, Waziri Ummy alitoa Maagizo kwa Mganga Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Wilaya ya Nanyumbu Mhe.Hamis Dambaya kuhakikisha  Wauguzi na Watumishi wote wanavaa vitambulisho vya kazi wakati wote wakiwa eneo la kazi ili wananchi wanaokwenda kupata huduma za Afya waweze kuwatambua majina yao.

"Tumewaambia wavae vitambulisho, ili mtusaidie kutaja jina la Wauguzi wanaovunja maadili ya kazi zao, hapa naomba nisiwahukumu wote, Mganga Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi mpo hapa, nikirudi tena nisisikie kuna Muuguzi anapiga makofi wajawazito wanaokuja kujifungua" alisema Waziri Ummy.

Kwa upande mwingine Waziri Ummy amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya italeta mashine mpya ya kisasa ya digitali ya X-Ray ndani ya miezi mitatu itayosaidia wananchi wa Nanyumbu hasa kutokana na Wilaya hiyo kuwa katika Bara bara kuu ya kutoka Masasi hadi Songea.

Aidha, Waziri Ummy ametoa Rai kwa wananchi wa Nanyumbu kuhakikisha kabla ya kufika Disemba 31 mwaka huu, kaya zote katika eneo hilo lazima liwe limejenga na kutumia choo bora ili kupunguza magonjwa ya Bakteria yanayoigharimu Serikali pesa nyingi katika matibabu na Dawa.

"Ndugu zangu nendeni pale Hospitali, katika kila Wagonjwa 100, Wagonjwa 60 wana magonjwa ya kuhara,magonjwa ya tumbo, magonjwa yanayohusiana na kiwango duni cha usafi, nimekuwa nikiimba wimbo huu tangu nikiwa Waziri wa Afya, na hapa tulipofikia ni agizo la Waziri Mkuu pindi alipokutana na maafisa Afya wa Halmashauri na Mkoa jijini Dodoma" alisema Waziri Ummy

Waziri Ummy aliendelea kusema kuwa akiwa kama Waziri wa Afya kazi kubwa aliyonayo ni kuhakikisha anawakinga watu wasiumwe na pale wanapoumwa waweze kupata Huduma Bora za Afya, lazima niwe mkali kwenye kinga, mimi ni Waziri wa Afya sio Waziri wa Wagonjwa" alisema Waziri Ummy.

NEC YATANGAZA KUFANYIKA KWA UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA TEMEKE NA KATA 46 ZA TANZANIA BARA.

0
0
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza kufanyika kwa uchaguzi mdogo katika Jimbo la Temeke, Mkoani Dar es Salaam na kwenye Kata 46 za Tanzania Bara.

Akitangaza kufanyika kwa uchaguzi huo Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji (Rufaa), Semistocles Kaijage amesema kuwa uchaguzi huo utafanyika Januari 19 mwaka 2019 na fomu za uteuzi wa wagombea zitatolewa kuanzia tarehe 14 hadi tarehe 20 Desemba 2018.

"Uteuzi wa Wagombea utafanyika tarehe 20 Desemba, mwaka huu. Kampeni za Uchaguzi zitafanyika kati ya tarehe 21 Desemba, hadi tarehe 18 Januari, mwaka 2019 na siku ya uchaguzi itakuwa ni tarehe 19 Januari mwaka 2019,” amesema Jaji Kaijage.Jaji Kaijage amebainisha kuwa Tume imetangaza uwepo wa nafasi wazi ya Ubunge kwenye Jimbo la Temeke baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai juu ya uwepo wa nafasi wazi ya Ubunge katika jimbo hilo.

Amesema kuwa Tume ilipokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye kwa kuzingatia kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, aliitarifu Tume uwepo wa nafasi wazi ya Mbunge wa Jimbo la Temeke katika Halmashauri ya Wilaya ya Temeke Mkoani Dar es Salaam kufuatia Kujiuzulu uanachama wa Chama Wananchi CUF kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Maulid Said Abdllha Mtolea.

Kwa upande wa nafasi wazi za Udiwani Jaji Kaijage amesema kuwa Tume ilipokea taarifa kutoka kwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali ya Mtaa akiitaarifu Tume juu ya uwepo wa nafasi wazi za Udiwani katika Kata 46.“Tume imepokea Taarifa kutoka kwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaaa mbaye kwa kutumia mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, aliitarifu Tume uwepo wa nafasi wazi za Madiwani katika Kata 46 za Tanzania Bara,” amesisitiza Jaji Kaijage.

Ametoa wito kwa vyama vya siasa na wadau wote wa uchaguzi kuzingatia Sheria, Kanuni, Maadili ya Uchaguzi, Taratibu, Miongozo na maelekezo yote yatakayotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakati wa kipindi cha Uchaguzi mdogo.Jaji Kaijage amefafanua kuwa kuwa uchaguzi huo mdogo utafanyika ndani ya Halmashauri 28 zilizopo kwenye Mikoa 14 ya Tanzania Bara.

Halamashauri na Kata zitakazokuwa na Uchaguzi ni pamoja na Ngorongoro (Sale,Misigyo,Malambo, Orgosorok na lorien/Magaiduru),Arusha(Kimnyak), Kilwa (Kiranje ranje, Kikole, Pande Mikoana), Liwale (Kata Kichonda na Mlembwe), Babati(Dareda na Magara,Kiteto(Makame), Simanjiro(Loiborsiret, Ruvu Remit, Naberera), Kwimba(Walla), Sengerema(Nyampulukano), Ulanga(Msogezi),Mvomero(Mtibwa, Tchenzema, Mangae), Kilosa(Magomeni), Temeke(Keko), Kinondoni(Magomeni).

Halmashauri nyingine ni pamoja na Kasulu (kata ya Kitanga), Kasulu Mji( Kata za Kigondo na Msambara), Buhigwe(Mnyegera),Bukoba(Buhendagabo, Nyakato, Kikomelo), Misenyi(Kanyigo), Ngara(Nyamiaga), Mbinga(Utiri), Songea(Mpitimbi), Mbozi(Ilolo, Hasanga, Ihanda), Tandahimba(Nahyanga, Namikupa), Dodoma(Dodoma Makulu), Serengeti(Geitasamo), Bariadi(Nkundwabiye) naBariadi Mji(Nyangokolwa).

RAIS DKT.JOHN MAGUFULI ATOA SALAMU ZA KUMBUKUMBU MIAKA 57 YA UHURU WA TANZANIA BARA

0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa Salamu za miaka 57 ya Uhuru wa Tanzania Bara Ikulu jijini Dar es Salaa. PICHA NA IKULU

WAZIRI LUGOLA AMBANA AFISA ELIMU KWA KUKATAA KUANDIKISHA WANAFUNZI DARASA LA KWANZA

0
0
 Mwandishi Wetu, MARA.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amepiga marufuku wanafunzi wanaoanza darasa la kwanza kutokuandikishwa mpaka wazazi wao walipe michango wanaodaiwa katika shule mbalimbali jimboni kwake Mwibara, Wilayani Bunda, Mkoa wa Mara.  Lugola ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, amemtaka Afisa Elimu wa Kata ya Chitengule, Jimboni humo, Thadeo Lukinisha kuruhusu shule za msingi zilizopo katika Kata yake kuandikisha wanafunzi hao bila kikwazo chochote kwakuwa elimu ya shule ya msingi ni bure nchi nzima.

Akizungumza na mamia ya wananchi wa Kijiji cha Nakatuba katika Kata hiyo, Lugola alipiga marufuku utaratibu huo ambao amesema hauna msingi wowote kwasababu unawaonea watoto ambao hawana kosa lolote hata kama kuna madeni ambayo wazazi wa wanafunzi hao wanadaiwa kutokana na watoto wao wanaoendelea na masomo katika shule zilizopo jimboni humo.  “Huu utaratibu sio sawa, haukubaliki, kipindi hiki wanafunzi wanaandikishwa kuanza darasa la kwanza waandikishwe bila kikwazo chochote ili waweze kupata elimu yao kama inavyostahili, michango yenu haihusiani na wanafunzi kuanza shule,” alisema Lugola. 

Hata hivyo, Afisa Elimu huyo tukio hilo lipo lakini walifanya hivyo kutokana na baadhi ya wazazi kutolipa kiasi cha shilingi mia nne ambayo inachangwa kwa ajili ya kila mwanafunzi anachangia kwa ajili ya kumlipa mpishi pamoja na mafuta ambayo fedha hiyo inalipwa kwa mwaka. Lugola alipata taarifa hiyo ya wazazi kukataliwa kuandikishwa watoto wao kuanza darasa la kwanza, baada ya mzazi mmoja kuulalamikia utaratibu huo na kuwafanya wazazi kutokuanidisha watoto hao kutokana na kudaiwa michango hiyo.

“Sitaki kusikia hili, Afisa Elimu huu sio utaratibu sahihi, lazima watoto waandikishwe kuanza masomo, na niwataka wazazi wote wahakikishe watoto wao wanaandikishwa haraka iwezekanavyo,” alisema Lugola huku akishangiliwa na wananchi waliohudhuria mkutano huo. Kwa upande wake Afisa Elimu huyo baada ya kauli ya Waziri Lugola aliwaelekeza walimu wa shule zilizopo katika Kata hiyo waweze kaundikisha watoto wao bila kikwazo chochote. 

“Napenda kutangaza kuwa, kuanza sasa wanafunzi waandikishwe bila kikwazo chochote katika shule ya Nakatuba na zinginezo ndani ya Kata hii ya Chitengule,” alisema Lukinisha.  Shule zilizopo katika Kata hiyo wanapewa chakula cha msaada na Shirika lisilokua la Serikali la PCI ambapo wazazi uchangia fedha kidogo ya mafuta na ya mlinzi hivyo uliwekwa utaratibu wa kila mwanfunzi katika shule hizo wachange shilingi 400 ili ziweze kuchangia huduma hizo.

Lugola anaendelea na ziara yake kwa kutembelea vijiji vyote jimboni kwake Mwibara akisikiliza kero za wananchi pamoja na kuhamasisha kilimo cha mazao ya pamba, mahindi, mpunga, viazi na mengineyo ambayo wakazi wa jimbo lake wanalima mazao hayo kwa wingi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akimsalimia Mkazi wa Kijiji cha Namalebe, Kata ya Chitengule, Jimbo la Mwibara, wilayani Bunda, Kaswanila Molore kabla ya kuanza mkutano wa hadhara na Wananchi wa Kijiji hicho. Akizingumza na wananchi wa Kata hiyo, Lugola amepiga marufuku wanafunzi wanaoanza darasa la kwanza kutokuandikishwa mpaka wazazi wao walipe michango wanaodaiwa katika shule mbalimbali jimboni humo. Na Mpiga Picha Wetu.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

RAIS DKT. SHEIN AZUNGUMZA NA MWENYEKITI WA JUMUIYA YA WAFANYABIASHARA WENYE VIWANDA YA SHARJAH IKULU LEO

0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara   Wenye Viwanda ambae pia ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Al Rawabi ya Sharja Bw.Abdallah Sultan Owais, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na Rais wa Zanzibar Ikulu leo,akiwa na Ujumbe wake kulia Sheikh.Majid Faisal Khalid Al.Qasemi Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza mgeni wake Mwenyekiti w a Jumuiya ya Wafanyabiashara Wenye Viwanda ya Sharjah,ambae pia ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Al Rawabi, Bw.Abdallah Sultan Owais, wakiwa nje ya ukumbi baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika leo Ikulu Zanzibar,7-12-2018.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na mgeni wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Wenye Viwanja Sharjah  ambae pia ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Al Rawabi Bw.Abdallah Sultan Owais, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika Ikulu Zanzibar, leo 7-12-2018.(Picha na Ikulu)

TAHA IKISHIRIKIANA NA STANBIC BANK WAANDAA MAONESHO YA TAASISI ZA KIFEDHA JIJINI ARUSHA

0
0

Mwenyekiti wa Muungano wa vyama vya wakulima nchi za SADEC Dkt Sinare Yusuph Sinare
Mwenyekiti wa (TAHA) Erick Ngimario akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya AICC jijini Arusha leo
Meneja wa Fredrick Max Meneja wa Bank ya Arusha Stanbic Bank akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya Taasisi za Kifedha Jijini Arusha Leo


Na. Vero Ignatus, Arusha


Wito umetolewa Taasisi za kifedha kuna kuwekeza kwenye sekta ya kilimo kwani kuna fursa kubwa haswa kilimo cha mbogambogaHayo yamesemwa na Dkt Sanare Yusuph Sanare katika maonyesho za Taasisi ya Kifedha kuhusu fursa za mitaji kwenye kilimo yameliyozinduliwa leo Jijini Arusha

Kauli mbiu uhakika wa mitaji ili kukuza kilimo. Biashara kuelekea kuelekea uchumi wa viwanda Mgeni rasmi katika maonyesho Dkt Sanare amesema lengo kuu la maonyesho hayo ni kuwaunganisha watoa huduma za kifedha na wakulima haswa wa mbogamboga(hot culture)

Dkt Sanare amesema tatizo kubwa la mkulima ni mtaji ambapo benki za biashara nyingi zilikuwa hazitoi mkopo kwenye sekta ya kilimo lakini hivi sasa kumeanza kuwa na mabadiliko makubwa wameanza kuona umuhimu wa kutoaKwa upande wake Mwenyekiti wa TAHA Erick Ngimario amesema kuwa Tanzaniabya Viwanda ambayo watu wote wanaiwania msingi wake mkubwa ni kilimo ambapo tasnia ya kilimo cha mbogamboga ni sehemu kubwa sana

Amesema Tanzania inakwenda vizuri na kilimo cha mbogamboga kwani kuna ardhi nzuri yenye rutuba, maji kwa kiasi kikubwa, maziwa na mito na sehemu zote ambazo zinauwezekano wa kulima mboga, viungo na matunda ambapo ni sehemu kubwa ya kilimo hapa nchini

'' TAHA inaamini kuwa kilimo hichi cha hotculture ni kilimo cha biashara ni kilimo ambacho kina faida na hasara na kila anayeingia humo anaangalia faida" alisema''Amesema kutokana na hayo lazima mkulima apate fursa ya kukopa ili aweze ili aweze kuendesha kilimo na apate faida kwani taasisi ambazo zimeweka maonyesho zinamuwezesha mkulima kukopa, kufanya kazi na kulipa

'' Hakuna tasnia ambayo ni rahisi sana kulipa kama tasnia ya kilimo cha mbogamboga kwani haitegemei sana mvua, na mambi ambayo hayana usimamizi maana kinategemea umwagiliaji''Amesema kilimo hicho hutegemea sana mpangilio ulime wakati upi na vilevile kuvuna uvune wakati upi kwani masoko nayo ni mihimu.Aidha amesisitiza kuwa maonyesho hayo siyo ya mara ya kwanza kwani kumeshakuwa na maonyesho Kama hayo mara nyingi na wengi wawanachama wao wameitumia fursa hiyo na wamefanikiwa

Amesema TAHA siku zote imekuwa ni kuingo kati ya wakulima na masoko, kati ya wakulima na serikali na Taasisi za serikali na katika ugani ambapo wakulima wanapata ushauri wa kilimo, ushauri wa masoko, na wanatumia mitandao kufanya hivyo '' Kwa jumla wanachama wetu ambao mtandao wetu ambao umeenea karibia nchi nzima wanategemea mambo mengi kutoka TAHA''alisema Ngimario.

Kilimo kinahitaji uwekezaji mkubwa wa mitaji na wakulima mwenyewe kwa wenyewe inakuwa vigumu kufanya hivyo Amesema STANBIC BANK Fredrick Max mwaka huu 2018 wameanzisha dawati la Kilimo litakuwa linaangalia mazingira yote ya kilimo nchini Tanzaniab

Amesema kuwa Banki hiyo inakijitahidi kufanya kazi na washirika kama TAHA, PASS, wakulima na wafanyabiashara wa kilimo kwa ujumla Maonyesho hayo yameshirikisha mabenki mbalimbali sambamba na watoa huduma nyingine ikiwemo TRA na RITA

WAZIRI WA KILIMO ASISITIZA MAWAZIRI JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUONGEZA MSHIKAMANO SEKTA YA KILIMO

0
0
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Katikati), Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Luhaga Mpina (Kushoto) na Waziri wa Kilimo, Mifugo, Maliasili na Utalii-Zanzibar Mhe Rashid Ally Juma wakiwa katika picha ya pamoja katika ukumbi wa mikutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Jijini Arusha, Leo tarehe 7 Disemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo).
Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhe Christophe Bazivamo, Waziri anayeshughulikia EAC nchini Burundi Mhe Isabelle Ndahayo, Waziri wa Kilimo nchini Kenya Mhe Mwangi Kiunjuri, Katibu Mkuu wa Kilimo nchini Rwanda Ndg Musabyimana Jean Claude, Waziri wa Kilimo Sudani Kusini Mhe Onyoti Adigo Nyikwec, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Tanzania Mhe Luhaga Mpina (Mb), Waziri wa Kilimo Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb), na Waziri wa Kilimo, Mifugo, Maliasili na Utalii-Zanzibar Mhe Rashid Ally Juma wakiwa katika picha ya pamoja katika ukumbi wa mikutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Jijini Arusha, Leo tarehe 7 Disemba 2018.


Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo-Arusha

Waziri wa Kilimo nchini Tanzania Mhe Japhet Hasunga amewataka mawaziri wenzake wa sekta ya Kilimo kutoka nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki kuongeza umoja na mshikamano ili kuakisi matakwa ya jumuiya katika Uzalishaji wa bidhaa bora za Kilimo.

Waziri Hasunga ameyasema hayo Leo tarehe 7 Disemba 2018 wakati akizungumza mara baada ya kumalizika mkutano wa 12 wa Baraza la kisekta la mawaziri wa Kilimo na usalama wa chakula wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwemo wenyeji Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudani Kusini.

Mhe Hasunga alisema kuwa kadri ushirikiano mwema utakavyoendelezwa ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa bidii itaimarisha tija na mafanikio ya soko la bidhaa katika jumuiya hiyo na dunia kwa ujumla.Aidha, amewataka watendaji wote katika nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki kutekeleza taarifa mbalimbali zinazoandikwa kwa ustadi mkubwa kwani kwa kiasi kikubwa kumekuwa na utekelezaji duni wa mipango hiyo.

Mkutano huo wa mawaziri wa sekta za Kilimo umetanguliwa na vikao vya ngazi ya wataalamu na ngazi ya makatibu wakuu vilivyoanza tarehe 3 Disemba 2018.Katika mkutano huo maeneo yaliyojadiliwa ni pamoja na kuhusu mchakato wa CAADP katika Jumuiya hususani ripoti ya taaarifa ya utekelezaji wa Azimio la Malabo na kupitisha Mkakati wa kuendeleza Sekta ya Kilimo na Chakula (REGIONAL AGRICULTURE INVESTMENT PLAN - RAIP) sambamba na Programu ya kudhibiti sumukuvu (aflatoxin prevention and control).

Maeneo mengine ni kuhusu Programu ya masuala ya afya ya mimea na wanyama (SPS programme) hususani kuhusiana na biashara za kimataifa, ushirikiano kati ya EAC na Marekani katika masula ya biashara ya mazao ya kilimo, masuala ya pembejeo hususani mbegu na viuatilifu, Chakula na Lishe Mawaziri wameridhia Mkakati na Mpango kazi wa kutekeleza masuala ya Chakula na Lishe wa Jumuiya. 

Mkakati na mpango huo utatekelezwa katika mipango na mikakati ya nchi wanachama, Kwa Tanzania kupitia mpango wa kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP II) na miradi mingine inayoendelea, Mradi wa kuhamasisha vijana kujiajiri katika Kilimo ambapo Vijana watatu watatu kutoka nchi zote wanachama watapokea tuzo za ushindi katika kujihusisha na kilimo.

Mjadala huo pia umehusu ripoti ya mifugo na samaki katika Jumuiya ambapo Maeneo muhimu yaligusa udhibiti wa magonjwa ya wanyama yanayovuka mipaka, Mkakati wa pamoja wa usimamizi wa magonjwa yanayoambukiza wanyama na binadamu, Masuala ya uvuvi yamezingatia changamoto za uvuvi haramu na jinsi zinavyoshughulikiwa, Sera ya uvuvi na ukuzaji wa viumbe kwenye maji.

Pia mkutano huo wa 12 wa Baraza la kisekta la mawaziri wa Kilimo na usalama wa chakula wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki umejadili kuhusu Utafutaji wa rasili za kutekeleza mipango na mikakati ya Jumuiya, lakini Maeneo mengine ya muhimu yaliyojadiliwa ni pamoja na kirusi kinachoathiri mahindi, viwavi jeshi, homa ya bonde la ufa kwa upande wa mifugo, mabadiliko ya tabia nchi na namna ya kukabiliana nayo na masuala ya umwagiliaji.

Vilevile Waziri Hasunga amesema kuwa mkutano huo umemalizika kwa mafanikio makubwa ambapo mjadala kuhusu chakula na usalama wa chakula umekuwa na tina kwani umegusa maslahi ya wananchi.

MANAIBU MEYA WAWILI KUPEANA ZAMU YA KUONGOZA JIJI LA DAR

0
0
HATIMAYE Baraza la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam limeamua kutumia busara kwa kufanya maridhiano ya kupata manaibu meya wawili kwa ajili ya kuongoza Jiji hilo ambapo wamekubaliana kila Naibu Meya ataongoza kwa miezi mitatu.

Hatua hiyo imefikiwa leo na Baraza hilo ambalo lilikutana kwa ajili ya kufanya uchaguzi wa Naibu Meya lakini yaliibuka malumbano makali kati ya wajumbe wa baraza hilo upande wapinzani dhidi ya CCM.Pia malumbano kati ya Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salam Spora Liana na upinzani.

Wakati wa malumbano hayo ikafikia hatua baadhi ya wajumbe wakaamua kuweka wazi hawapo tayari kuendelea kulumbana wao kwa wao na kusababisha vinyongo katika kupata Naibu Meya kwani malumbano yanakwamisha maendeleo ya Dar es Salaam.Baadhi ya wajumbe wa baraza hilo wakiwamo wabunge na madiwani waliweka wazi idadi ya wapiga kura kwa CCM ni 12 na upinzani ni 12, hivyo watavutana bila sababu ya msingi na kila wanapokutana fedha za umma zinatumika na hakuna muafaka.Hivyo walimua leo iwe iwavyo ni lazima wafanye uchaguzi na Naibu Meya apatikane.

Kutokana na maridhiano hayo wagombea Mariam Rulida ambaye ni Diwani wa Kata ya Mchafukoga kupitia CCM na Alli Mohammed ambaye ni Diwani wa Kata ya Makumbusho kupitia CUF ndio wamepitishwa na baraza hilo kushika nafasi hiyo ya Naibu Meya.Akitangaza uamuzi huo Meya wa Jiji la Dar es Salaam Issaya Mwita amesema wajumbe wa baraza hilo ambalo ndio wapiga kura wamekubaliana Naibu Meya aMariam Rulida aanze kushika nafasi na kwamba ataanza kuitumia kuanzia Desemba 30, 2018 hadi Machi 30 mwaka 2019 na baada ya hapo Naibu Meya mwingine Alli Mohammed atashika nafasi hiyo kuanzia Machi 30 hadi Juni 30 mwaka 2019.

"Tumekubaliana na kuridhia wote kwa pamoja tuwe na manaibu meya wawili na wataongoza kwa zamu nafasi hiyo.Tuanza na Naibu Meya wa CCM na kisha atafuata Naibu Meya kutoka CUF.Tumefanya hivi kwa nia njema na yenye maslahi mapana kwa Jiji la Dar es Salaam.Hatutaki kuendelea kulumbana kila linapofika suala la kuchagua Naibu Meya,"amesema Meya Mwita.
Wajumbe wa Baraza la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wakiwa kwenye kikao cha kujadili uchaguzi wa kumpata Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam. Baraza hilo limekutana leo jijini.

Mtawa awataka wauguzi nchini kuzingatia miongozo ya kazi

0
0
Wauguzi nchini wametakiwa kutimiza wajibu wao ili kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi kwa kufuata miongozo iliyopo ikiwamo taratibu, kanuni na sheria.

Hayo yamesemwa na Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Bi. Agnes Mtawa katika mkutano wa kikao kazi uliowashirikisha wauguzi wakuu wa mikoa ya Tanzania, wauguzi wakuu wa hospitali za rufaa za kitaifa na hospitali maalum, baadhi ya wakuu wa vyuo vinavyotoa mafunzo ya uuguzi na ukunga pamoja na baadhi ya wauguzi wakuu wa wilaya nchini.

Bi. Mtawa amesema kwamba taaluma ya uuguzi inaongozwa na sheria na kanuni ambazo zimeainisha miongozo jinsi ya kumuwajibisha muuguzi anayekwenda kinyume na taratibu na maadili.“Kutokana na muongozo huu, viongozi wa baraza ngazi ya mikoa, wilaya na vyuo wanapaswa kutimiza wajibu wao katika kusimamia miongozo,” amesisitiza Bi. Mtawa.

Mkurugenzi huyo amewataka wauguzi kuzingatia pia matumizi ya miongozo mipya kama muongozo wa kusimamia utoaji wa huduma ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) uliyoboreshwa yaani NIMART, muongozo wa mafunzo ya kujiendeleza yaani CPD, muongozo wa ufuatiliaji wa huduma za uuguzi na ukunga pamoja na mfumo mpya wa TEHAMA ambao utasaidia kuweka kumbukumbu za huduma zinazotolewa na wauguzi na wakunga kwa kielectroniki.

Pia, Bi. Mtawa amewataka wauuguzi kuwa na vyeti vya taalama yao vinavyotambulika na mamlaka husika kwani wenye vyeti vya kughushi watakamatwa na kushtakiwa katika vyombo vya sheria.Amesema baraza hilo lina mfumo imara ambao una uwezo wa kutambua waauguzi wenye vyeti vya kughushi vya kitaalama, hivyo amewataka kuwa makini.

“Mfumo huu utasaidia sana kutatua changamoto ya wimbi la kughushi vyeti vya kitaaluma ambalo limeibuka katika kipindi hiki. Mpaka sasa jumla ya kesi 15 ziko mahakamani kwa sababu ya watumishi walioghushi vyeti vya uuguzi na ukunga pamoja na leseni,” amefafanua Bi. Mtawa.

Lengo la kikao kazi hicho lilikuwa kuwakumbusha na kuwajengea uwezo wauguzi na viongozi juu ya wajibu wao wa kusimamia utoaji wa huduma za uuguzi na ukunga Tanzania, kusimamia maadili ambayo bado yanalalamikiwa na wananchi.

Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania ni mamlaka iliyoundwa kisheria ambayo moja ya majukumu yake ni kusimamia taaluma ya uuguzi na ukunga Tanzania.
Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Bi. Agnes Mtawa akiwaonyesha washiriki sheria na kanuni inayosimamia taaluma ya uuguzi na ukunga nchini.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia kikao hicho ambacho kimefanyika kwenye ukumbi wa ofisi za baraza hilo, Wilaya ya Kibaha, mkoani Pwani.
Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Bi. Agnes Mtawa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa baraza hilo.

Wananchi zaidi ya Milioni 4 Dar kupatiwa Kingatiba dhidi Matende na Mabusha

0
0

NA WAMJW, DAR ES SALAAM

WAKAZI wa Dar es Salaam wapatao Milioni 4.3 wanatarajiwa kumeza Kingatiba dhidi ya magonjwa ya matende na mabusha (Ngirimaji) pamoja na minyoo ya tumbo, kuanzia Disemba 15 hadi 20, mwaka huu.

Hayo yamebainishwa na Mratibu wa Taifa wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele (NTD), Dkt. Upendo Mwingira wakati wa Warsha ya Wanahabari kuhusu magonjwa hayo hapa nchini.

Dkt. Upendo Mwingira amewataka wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kwenye zoezi hilo kwani kingatiba hiyo itatolewa bila malipo katika maeneo yote ya Jiji la Dar es Salaam.“Hii sio chanjo. Ni kijngatiba na zoezi hili linaenda kumkinga mtu dhidi ya magonjwa ya mabusha na matende pamoja na minyoo na itatolewa kuanzia umri wa miaka 5 na kuendelea” Amasema Dkt.Upendo Mwingira.

Ameongeza kuwa, “Wananchi watakaojitokeza watamezeshwa kingatiba hizo papohapo na zoezi hili utolewa kila mwaka mara moja” amebainisha.
Magonjwa ambayo hayapewi kipaumbele ni pamoja na Usubi,Vikope (Trakoma), Matende, Mabusha (Ngirimaji), na Minyoo ya tumbo.

Zoezi hilo la ugawaji wa dawa litatekelezwa katika vituo vyote vya Afya, Zahanati,Hospitali, sokoni,vituo vya usafiri,pamoja na Ofisi za Serikali, maeneo ya mikusanyiko ya watu wengi na Mashirika ya Umma na hivyo wananchi wanaombwa kujitokeza kwa wingi kupata huduma hiyo ambayo haina malipo yoyote.
Mratibu wa Haifa wa Mpan go wa Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele kutoka Wizara ya Afya Dkt.Upendo Mwingira akitoa ufafanuzi kuhusu zoezi la umezeshaji wa Kinga Tiba za matende na mabusha(ngirimaji ) kwenye warsha ya waandishi wa habari iliyofanyika ofisi ndogo za wizara zilizopo Jijini Dar es salaam
Afisa Mpango Oscar Kaitaba akiwaonesha Kinga tiba hizo waandishi wa habari(hawapo pichani).Zoezi la umezeshaji kwa Mkoa wa Dar es Salaam linalotarajiwa kuanza disemba 15 hadi 20 mwaka huu
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikali ,Wziara ya Afya Catherine Sungura akiongea na waandishi wa Habari wakati ya warsha hiyo kulia ni afisa Mawasiliano kutoka kitengo cha Elimu ya Afya kwa Umma Said Makora Waandishi wa Habari walioshiri warsha ya umezeshaji Kinga tiba kwa Mkoa wa Dar es Salam iliyofanyika kwenye ukumbi wa ofisi Mdogo za wizara zilizopo Jijini Dar es salaam
Baadhi ya wandishi wakifuatilia mada katika semina hiyo.
Waandishi wa Habari walioshiriki warsha ya umezeshaji Kinga tiba kwa Mkoa wa Dar es Salam iliyofanyika kwenye ukumbi wa ofisi Mdogo za wizara zilizopo Jijini Dar es salaam

WAZIRI MBARAWA ATAKA KERO YA MAJI MTONI ITATULIWE

0
0
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akijibu hoja za wananchi mara baada ya kusikiliza kero zao eneo la Mtoni, katika Wilaya ya Temeke.
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akimsikiliza mmoja wa wakazi wa Mtoni, Wilaya ya Temeke wakati akielezea kero yake kuhusu maji.







Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akimsikiliza Meneja wa Mtambo wa Maji Mtoni, Mhandisi Deusdedit Rwegasila alipokuwa ziarani katika eneo la Mtoni, wilayani Temeke.
Fundi Sanifu Mwandamizi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Robert Chenge akitoa maelezo kuhusu hali ya huduma ya maji kwa Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa alipokuwa eneo la Mtoni.

Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa ametaka kero ya maji kwa wakazi wa Mtoni itatuliwe haraka iwezekanavyo mara baada kujionea hali huduma ya maji kwa wananchi.

Amezungumza hayo katika muendelezo wa ziara yake ya kusiskiliza kero za wananchi jijini Dar es Salaam, na kuitaka DAWASA itafute suluhisho la kufikisha huduma ya maji kwa wananchi, ukizingatia uwepo wa chanzo cha maji na mtambo wa kusafishia maji katika eneo la Mtoni.

Profesa Mbarawa amesema haoni sababu ya wananchi hao kukosa maji kwa kuwa kuna chanzo cha maji cha uhakika, kinachohitajika ni kuweka mkakati mzuri wa ujenzi wa miundombinu itakayofikisha maji kwa wananchi kwa kuwa chanzo kipo.

Akiwa kwenye Mtaa wa Mashine ya Maji, Profesa Mbarawa amekutana na kero ya maji kutoka kwa wananchi ambao wamesema maji wanayotumia yanayotoka kwenye kisima usalama wake ni mdogo, kumuomba Waziri wa Maji awatatulie changamoto hiyo.

Aidha, wamemuomba Waziri wa Maji aipatie ufumbuzi changamoto ya kisima kilichochimbwa na Halmashauri ya Temeke kilichokuwa kikitumika awali kwa ajili ya kutoa huduma ya maji kwa wananchi kuhodhiwa na mtu binafsi wakati wao wakiwa na uhitaji mkubwa wa maji.

Akijibu hoja za wananchi hao Profesa Mbarawa amesema atatuma timu ya wataalamu wa DAWASA ifike eneo hilo Jumatatu ijayo, ili waweze kufuatilia jambo hilo kabla ya kuchukua hatua zinazostahili. Pia, waangalie namna jinsi watakavyoweza kufanikisha zoezi la kufikisha huduma ya maji kwa wakazi hao.

Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa amemaliza ziara yake ya siku tano katika Jiji la Dar es Salaam; ambapo ametembelea maeneo yenye changamoto kubwa ya upatikanaji wa maji ya Kimara, Bonyokwa, Salasala na Mtoni kusikiliza kero za wananchi ambazo amekuwa akizisikia kwa lengo la kuzipatia ufumbuzi. Pamoja na Kiwalani ambapo alikwenda kupata mrejesho kutoka wa wananchi kuhusu maendeleo ya Mradi wa Maji Kiwalani uliozinduliwa hivi karibuni.

MWANAMKE APAMBANA NA JAMBAZI MWENYE SILAHA AKIMUOKOA MUMEWE,

0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akimwangalia mgonjwa ambaye ni Mkazi wa Kijiji cha Mahyolo, Wilayani Bunda, Samson Malegesi aliyevamiwa na jambazi na kukatwakatwa mapanga mwili nzima, jana. Hata hivyo, Mke wa mgonjwa huyo, Busimba Malegesi (katikati), alifanikiwa kumuokoa mumewe kwa kumnyang’anya silaha jambazi hilo. Mgonjwa huyo amelazwa katika Hospitali ya Kibara, Wilayani humo akiendelea kupewa matibabu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akimwangalia mgonjwa ambaye ni Mkazi wa Kijiji cha Mahyolo, Wilayani Bunda, Samson Malegesi aliyevamiwa na jambazi na kukatwakatwa mapanga mwili nzima, jana. Hata hivyo, Mke wa mgonjwa huyo alifanikiwa kumuokoa mumewe kwa kumnyang’anya silaha jambazi hilo. Kulia ni Muuguzi wa hospitali ya Kibara, Godliver Josephat, ambapo mhonjwa huyo amelazwa akipatiwa matibabu. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati), akiingia Hospitali ya Kibara Wilayani Bunda kumwangalia mgonjwa aliyevamiwa na jambazi na kukatwakatwa mapanga mwili nzima, jana. Hata hivyo, Mke wa mgonjwa huyo alifanikiwa kumuokoa mumewe kwa kumnyang’anya silaha jambazi hilo. Kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Polisi Kibara, Wilayani humo, Mkaguzi Boniface Mwalupale. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akiondoka Hospitali ya Kibara Wilayani Bunda, Mkoa wa Mara, mara baada ya kumwangalia mgonjwa aliyevamiwa na jambazi na kukatwakatwa mapanga mwili nzima, jana. Hata hivyo, Mke wa mgonjwa huyo alifanikiwa kumuokoa mumewe kwa kumnyang’anya silaha jambazi hilo. Kulia ni Mkuu wa Kituo cha Polisi Kibara, Wilayani humo, Mkaguzi Boniface Mwalupale.




Na Felix Mwagara, (MOHA) MARA.

Mkazi wa Kijiji cha Mahyolo, Kata ya Nyamihyolo, Wilayani Bunda, Mkoa wa Mara, Busimba Malegesi amemuokoa mumewe asiuawe na jambazi mwenye silaha ambaye alivamia katika nyumba yao na kuanza kumshambulia mwanaume huyo kwa kumkatakata mapanga mwili mzima.

Busimba alimrukia jambazi huyo kiunoni na kumuangusha chini na kufanikiwa kumnyang’anya panga pamoja na tochi ambazo alikua nayo wakati anamshambulia mumewe aitwaye Samson Malegesi (62).

Tukio hilo la kusikitisha lilitokea saa 7:30 usiku wa kuamkia Ijumaa wakati familia hiyo ikiwa imelala ndipo jambazi huyo alivunja mlango na kuingia moja kwa moja chumbani kwa wanandoa hao na kuwasha tochi kumsaka Malegesi na baada ya kufanikiwa kumuona alianza kumshambulia kwa kumpiga mapanga kichwani, mikononi, kwenye mbavu na kusababisha damu nyingi kumwagika.

Wakati jambazi hilo akiendelea kumshambulia Malegesi, mkewe alikua naye anapambana kwa kumzuia asimshambulie mumewe, lakini jambazi hilo lilizidiwa baada ya mwanamke huyo kupata nguvu zaidi na kufanikiwa kumuangusha chini na kuhakikisha silaha aliyoishika mkononi akinyang’anywa kwa urahisi kutokana na kubanwa kwa juu na mwanamke huyo.

Mwanamke huyo wakati akipambana na jambazi huyo alikua akipiga kelele lakini sauti yake haikuweza kuwafikia majirani ili waweze kumpa msaada, hata hivyo jambazi huyo baada ya kuona anakosa nguvu baada ya kukandamizwa chini, akafanikiwa kupata upenyo ndipo akakimbia kutoka katika nyumba hiyo.

Hata hivyo, baada ya jambazi huyo kukimbia, mwanamke huyo alitoka nje kuomba msaada zaidi kwa majirani na walifanikiwa kufika na walimpeleka Hospitali ya Misheni ya Kibara Wilayani humo ambapo alifikishwa akiwa hajitambui na kuanza kupewa matibabu ya haraka ili kuokoa maisha yake.

Muuguzi wa Hospitali hiyo, Godliver Josephat alisema amempokea mgonjwa huyo akiwa na waaguzi wenzake, saa 9:00 usiku akiwa hajitambui na ndipo wakashirikiana na madaktari wakamuwekea dawa ya kuzindua uhai wa mgonjwa huyo na kufanikiwa kuzinduka na wakaendelea na tiba zingine ikiwemo kuzuia kutoka damu pamoja na kushonwa sehemu alizokatwa mapanga.

“Tumempokea mgonjwa huyo saa tisa usiku akiwa ana hali mbaya sana, jitihada zetu zilifanikiwa kumpa huduma ya kwanza kwa kumuwekea dawa ya kuzindua uhai wake na baadaye tukaendelea kumpa huduma zingine ikiwemo kuanza kumshona kwasababu alikatwa panga la kichwa, mikono yake yote miwili ilijeruhiwa, mbavu zake upande wa mgongoni alichimbwa kwa kukatwa na panga, hivyo hali yake ilikua tete, hata hivyo tumefanikiwa kumuhudumia kwa umakini mkubwa na sasa mnamuona anaweza kuzungumza,” alisema Godliver.



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola ambaye alikua katika ziara ndani ya jimbo lake ambapo tukio hilo limetokea, mara baada ya kupata taarifa ya tukio hilo alfajiri ya jana, alifika hospitalini hapo na kuelekea chumba cha upasuaji akakuta madaktari wakiendelea kumshona sehemu mbalimbali za mwili wake zilizojeruhiwa.

Lugola ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo hilo la Mwibara, aliwasili Hospitali hapo akiwa na Mkuu wa Kituo cha Polisi Kibara (OCS), Mkaguzi Boniface Mwalupale pamoja na madiwani na viongozi wa Halimashauri wa Wilaya ya Bunda ambao uambatana nao wakati akiwa katika ziara zake jimboni mwake.

“OCS hakikisheni hamlali mpaka mnalipata jambazi hili kwa kutumia njia zote za kiintelejinsia mulizosomea ili muweze kumsaka na kumtia mbaroni haraka iwezekanavyo, huu ni unyama na lazima akamatwe, mtafuteni usiku na mchana, msikae ofisini kunywa chai, hakikisheni huyu mtuhumiwa anakamatwa.” Alisema Lugola.

Lugola baada ya kutoa maelekezo hayo saa mbili asubuhi, alitoka hospitali hapo na kuendelea na mikutano ya hadhara jimboni humo na akasisitiza kuwa majambazi wasiibipu serikali kwa kuwa bado ipo macho kuhakikisha wananchi wake wapo salama, kutokana na tukio hilo Polisi watafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha mtuhumiwa anakamatwa.

“Nampongeza sana mwanamke aliyepambana na jambazi ili amuokoe mumewe, hakika kama sio ushujaa wa mwanamke huyo tungempoteza mumewe kwasababu jambazi huyo alidhamiria kumuua kwa kumkata mapanga zile sehemu ambazo ni hatari zaidi kwa uhai wa ubinadamu,” alisema Lugola alipokua anazungumza na wananchi wa Kijiji cha Busagara, Kata ya Chitengule, jimboni humo jana jioni.

Kwa upande wa Mkuu wa Kituo cha Polisi Kibara, Mwalupale alisema baada ya kupata taarifa ya tukio hilo, tayari askari wapo katika msako mkali wa kumsaka jambazi huyo na wamemhakikishia Waziri Lugola pamoja na wananchi kuwa watamkamata mtuhumiwa huyo.

“Jambazi huyo alifanya uvamizi huo lakini hakuiba chochote ndani ya nyumba hiyo, inaonyesha kuwa, lengo la jambazi hilo alitaka kumvamia mtuhumiwa pekee. Ila tunaendelea kufanya uchunguzi kujua lengo la mtuhumiwa huyo kufanya tukio hilo la kinyama, na tutahakikisha tunamkamata na kumfikisha mahakamani,” alisema Mwalupale.

Hata hivyo, Waziri Lugola baada ya kumaliza mikutano yake jioni alirudi tena hospitalini hapo na kumkuta mgonjwa huyo ametoka chumba cha upasuaji na amepelekwa wodini kwa ajili ya kuendelea na matibabu.

Lugola alitoa pole kwa ndugu na wananchi waliokuwepo hospitalini hapo kutokana na unyama aliofanyiwa mwananchi huyo na kuhahidi Serikali ipo pamoja nao na watahakikishia jambazi hilo pamoja na wengine watakamatwa.

MAJALIWA AZUNGUMZA BAADA YA KUTEMBELEA SHAMBA LA MIWA LA MKULAZI NA MBIGIRI MKOANI MOROGORO

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imeanzisha Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania kwa lengo la kuwasaidia wakulima wapate mitaji ili waongeze tija.

Pia amewataka wakuu wa wilaya za Kilosa na Mvomero mkoani Morogoro wahahakikishe wanawahamasisha wananchi katika maeneo yao kuchangamkia fursa ya kilimo cha miwa.Waziri Mkuu aliyasema hayo jana jioni (Ijumaa, Desemba 7, 2018) alipotembelea shama la miwa Mkulazi na MbIgiri mkoani Morogoro alipokuwa njiani kwenda jijini Dodoma.

Alisema lengo la kuanzishwa shamba la mwa la Mkulazi ni katika jitihada za Serikali za kuhakikisha mahitaji ya sukari nchini yanafikikia katika kiwango kinachohitajika.Waziri Mkuu alisema Serikali imepanga kuzalisha sukari itakayotosheleza mahitaji na njia pekee ni kuboresha kilimo cha miwa, kujenga viwanda vitakavyozalisha sukari ya kutosha.

Alisema shamba hilo linaendeshwa kwa ubia kati ya NSSF na Jeshi la Magereza, hivyo, aliiagiza Menejimenti mpya ya Mkulazi kuhakikisha shamba hilo linasimamiwa kikamilifu.Waziri Mkuu pia, alimuagiza Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike apeleke wataalamu wengi wa kilimo katika shamba hilo ili wasaidie kusimamia kitaalamu.

“Nataka shamba hili lisimamiwe kitaalamu, uzalishaji uwe wa kitaalamu na liwe mfano na mashamba mengine, tusishindwe na watu binafsi,” alisema.Kuhusu suala la maji hususan kipindi cha mvua ambayo huaribu shamba, Waziri Mkuu aliwataka watafute namna nzuri ya kuyahifadhi ili wayatumie kipindi cha kiangazi.

Kadhalika, Waziri Mkuu aliwataka watafute mashine nyingine zitakazotosha kumwagilia shamba hilo wakati wa kiangazi ili miwa isiharibike na iendelee kuwa ya kijani wakati wote.Nae, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenistar Mhagama, alisema shamba la Mkulazi II ni miongoni mwa mashamba mawili yanayomiilikiwa na wabia wawili yaani NSSF na Jeshi la Magereza.

Alisema walikubaliana wao na Magereza wafanye kazi kwa kuongozwa na uzalendo, maadili ya utendaji wa kazi, uaminifu ili mwisho wa siku mradi huo uwe na tija na uweze kuwafikisha katika malengo yaliyokusudiwa.Alisema wanaamini fedha zilizowekezwa kwenye mradi huo ambazo ni za wanachama zinatakiwa zirudishe faida kwa wanachama wenyewe na kujenga uchumi wa Taifa.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Kilimo, Omari Mgumba, alimshukuru Rais Dkt. John Magufuli kwa dhamira yake ya dhati ya kuhakikisha tatizo la upatikanaji wa sukari nchini linakuwa historia.

Alisema mbali ya shamba hilo la Mkulazi II pia kuna lingine la Mkulazi I ambalo ni kubwa zaidi, hivyo alishauri liendelezwe ili limalize tatizo la sukari nchini. Waziri Mkuu alimtaka ashughulikie shamba hilo kwa kuwa lipo Wizara ya Kilimo.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (kulia)  wakati alipowasili kwenye shamba la miwa la Mkulazi na Mbigiri mkoani Morogoro,
PMO_1450
          Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipotembalea shamba la miwa la Mkulazi na Mbigiri mkoani Morogoro, Desemba 7, 2018. Wapili kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na kushoto ni Naibu Waziri wa Kilimo, Omari Mgumba. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Stevene Kebwe.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Viewing all 46194 articles
Browse latest View live




Latest Images