Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46200 articles
Browse latest View live

Halotel kuwazawadia wateja na Chrismas BANG BANG.

0
0
Katika kuelekea msimu huu wa sikukuu kampuni ya simu ya Halotel imetoa punguzo la zaidi ya asilimia sitini (60%) katika kifurushi chake cha siku ambapo sasa wateja watapata GB 2 kwa shilingi 2000 ikiwa ni gharama nafuu zaidi ya vifurushi vya intaneti na kutoa punguzo kubwa la smartphone aina ya OXE 101.

Akizungumzia punguzo hilo kubwa, Mkuu wa Mawasiliano wa Halotel, Mhina Semwenda amesema ofa hiyo imezingatia mahitaji makubwa ya wateja wa mtandao huo katika msimu huu wa sikukuu na kutoa nafasi kwa wateja kupeana taarifa na fursa ya kutembelea mitandao mbali mbali ya kijamii.

“Msimu wa sikuu kuu unatoa fursa kwa wateja wetu, kutembelea maeneo mbalimbali ya nchi, wengi wanahitaji taarifa za maeneo wanayoenda, au wanaweza kupenda kushare matukio au hata kupata muda mwingi wa kutumia simu zao, hivyo tumeonelea ni vyema sasa, tuwape sababu ya kufurahia msimu huu wa sikukuu kwa kuwapatia ongezeko kubwa kabisa la GB za intaneti, Alisema Mhina na kuongeza.

Jambo kubwa kabisa la kuwahakikishia wateja wetu ni kuwa maeneo yote watakayo kwenda iwe vijijini au sehemu nyinginezo, watakuwa pamoja nasi na watakuwa na uhakika wa kutumia huduma zetu kutoka katika mtandao wetu uliosambaa Zaidi hapa nchini kwa kufikia Zaidi ya asilimia 95% ya Watanzania.

“Huduma hii ni zawadi kwa wateja wote wa Halotel nchini msimu huu wa sikukuu kwa kuendelea kutumia intanet yenye kasi zaidi nchini kipindi hiki cha mapumziko wakati wowote, ambapo kwa kujiunga na huduma ya CHRISTMAS BANG BANG mteja atapata kifurushi cha intenet cha GB 2 cha siku kwa sh 2000 tu tofauti na kirushi cha kawaida ambacho mteja angepata GB 1.3 kwa siku kwa sh 2000.

Zaidi tunapenda kuwakumbusha watanzania na wateja wetu wote wataweza kujipatia zawadi mbali mbali pindi watakapo fika kwenye maduka yetu ya Halotel nchi nzima katika kipindi msimu huu wa sikukuu. Tunatakia watanzania na wateja wa Halotel waipokee zawadi ya CHRISTMAS BANG BANG kutoka Halotel,. alisema Kanyamala na kuongeza.

Tunawahakikishioa wateja wetu kuwa tutafanya msimu huu wa sikukuu kuwa Bang Bang kwa kuendelea kuboresha huduma zetu.


Mkuu wa mawasiliano wa Halotel, Mhina Semwenda akizungumza na waandishi wa Habari katika Makao Makuu ya kampuni hiyo kuhusu Ofa mpya ya Krismasi na mwaka Mpya iliyozinduliwa leo inayokwenda kwa jina la “Christmas Bang Bang” namna itakayowawezesha wateja wote wa Halotel kupata GB2 za intaneti kwa sh. 2000 tu.na pia wateja wote watapata zawadi wataaakapofika maduka yetu yote nchi nzima. Pamoja nae katika picha kushoto ni Hindu Kanyamala Meneja Mawasiliano Halotel, (kulia) na Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Stella Pius.

Mkuu wa mawasiliano wa Halotel, Mhina Semwenda akizungumza na waandishi wa Habari katika Makao Makuu ya kampuni hiyo kuhusu Ofa mpya ya Krismasi na mwaka Mpya iliyozinduliwa leo inayokwenda kwa jina la “Christmas Bang Bang” namna itakayowawezesha wateja wote wa Halotel kupata GB2 za intaneti kwa sh. 2000 tu.na pia wateja wote watapata zawadi wataaakapofika maduka yetu yote nchi nzima. Pamoja nae katika picha, (kulia) na Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Stella Pius.

WAZIRI WA KILIMO AAGIZA VYUO VIKUU KUTANGAZA MATOKEO YA TAFITI ZAO

0
0
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza kwenye sherehe ya nne ya kukabidhi zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri kitaaluma katika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi tarehe 6 Disemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo).
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akimkabidhi zawadi ya mwanafunzi bora kitaaluma ngazi ya Stashahada ya Uhasibu na Uongozi Ndg Methusela Piniel kwenye sherehe ya nne ya kukabidhi zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri kitaaluma katika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi tarehe 6 Disemba 2018.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akimkabidhi zawadi ya mwanafunzi bora kitaaluma ngazi ya Shahada ya Biashara na Uchumi Bi Diana Kibodya kwenye sherehe ya nne ya kukabidhi zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri kitaaluma katika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi tarehe 6 Disemba 2018.
Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi Prof Faustine K. Bee akitoa taarifa ya chuo hicho kwenye sherehe ya nne ya kukabidhi zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri kitaaluma katika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi tarehe 6 Disemba 2018.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi sambamba na baadhi ya wahitimu kwenye sherehe ya nne ya kukabidhi zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri kitaaluma chuoni hapo tarehe 6 Disemba 2018.


Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Kilimanjaro

Imebainika kuwa tafiti na machapisho mengi yanayofanywa na wanataaluma na wanafunzi katika Vyuo mbalimbali si tu zinasaidia kujenga taswira za vyuo bali zinapaswa kuwa sehemu ya kufanya elimu iwe nzuri na bora zaidi.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 6 Disemba 2018 wakati akizungumza kwenye sherehe ya nne ya kukabidhi zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri kitaaluma katika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi.

Mhe Hasunga amewaagiza watendaji wa Chuo hicho sambamba na vyuo vingine nchini kufanya tafiti za kutosha katika tasnia ya ushirika na kuhakikisha kuwa Matokeo ya tafiti hizo yanawafikia walengwa. "Serikali nayo kwa upande wake imeweka na itaendelea kuweka mazingira rafiki zaidi yatakayosaidia kuimarisha dhana ya ushirika miongoni mwa jamii ya watanzania" Alisema

Alisisitiza kuwa moja ya kadhia inayovikumba vyuo mbalimbali nchini ni kutowekwa wazi kwa haraka machapisho na Tafiti mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutangaza ili zijulikane katika sehemu mbalimbali Duniani.

"Ndugu zangu hakuna nchi inaweza kuendelea bila kuwekeza kwenye utafiti hivyo ni lazima kuongeza jitihada na juhudi katika utafiti" Alisisitiza.Alisema kuwa Vyuo vikuu vinatambuliwa kama taasisi zilizobobea katika kufundisha, kujifunzia, kufanya tafiti na kutoa huduma za ushauri hivyo vinapaswa kutangaza matokeo ya Tafiti wanazozifanya.

Alisema, kupitia elimu hiyo itolewayo na vyuo vikuu, maarifa, ujuzi na mtazamo chanya kwa maendeleo vinaweza kujengwa, kuboreshwa, kuendelezwa na kusambazwa kwa walengwa mbalimbali. Kwa msingi huo, utoaji elimu bora inayokidhi viwango na inayoendana na mahitaji ya soko lazima izingatiwe. 

Akizungumzia Ushirika, Mhe Hasunga amesema kuwa Ushirika ni dhana ya kujisaidia wenyewe katika maendeleo. "Hatuna budi sisi kama wadau wa ushirika kuhakikisha kuwa tunajenga misingi imara ya elimu ya ushirika kwa wadau wetu ili waweze kujikwamua katika wimbi la umaskini kwa kuanzisha shughuli zenye tija (kwa mfano ushirika wa viwanda) zitakazowapatia kipato cha uhakika" Alisisisitiza 

Aidha, Waziri Hasunga ameupongeza uongozi Wa chuo kikuu cha Ushirika Mosho kwa kuendelea kutoa mchango mkubwa katika kuendeleza sekta ya Ushirika nchini kwa kuandaa na kutoa wataalamu katika sekta ya Ushirika kuanzia ngazi ya Astashahada, Stashahada hadi shahada za awali, Umahiri na Uzamivu.

Akitoa maelezo ya awali Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi Prof Faustine K. Bee wakati akimkaribisha mgeni rasmi alisema kuwa sekta ya Kilimo imekumbwa na changamoto mbalimbali ambazo ni pamoja na Ushirika kama dhana kuwa na mtazamo hasi kwa baadhi ya watu inayosababishwa na uendeshwaji Wa Ushirika usiokuwa na tija kwa wanachana, jamii na Taifa kwa ujumla.

"Vilevile migogoro ya Mara kwa mara katika vyama vya Ushirika kutokana na kuwepo kwa watu wachache wasiowaaminifu na kukosa maadili" Alikaririwa Prof Bee

Alisema Chuo hicho kinatambua kuwa vyama vya Ushirika ni vyombo muhimu sana katika utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa miaka mitano (2016/2017) - (2020/20121), Malengo yavMaendeleo endelevu 2030 pamoja na ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020.

TUCTA YAKIRI KUSHIRIKISHWA KWENYE MCHAKATO WA UTUNGWAJI WA KANUNI ZA MALIPO YA WASTAAFU

0
0
Rais wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Nyamhokya amekiri shirikisho hilo kuwa na majadiliano mbalimbali katika ngazi ya Utatu na Upili yaani Serikali, Wafanyakazi na Waajiri kuhusu hoja ya kuunganishwa kwa mifuko ya hifadhi za jamii nchini. 

Akizungumza na waandishi wa Habari mjini Morogoro leo sanjari na vikao vyao vya kikatiba takribani kwa siku mbili, Nyamhokya amesema wajumbe wamekuwa na fursa ya kujadili mambo mbalimbali yanayohusu Ustawi wa Wafanyakazi nchini pamoja na kutoa tamko baada ya kuhudhuria kikao hicho rasmi cha utendaji wa maswala yanayotakiwa kufanyiwa utekelezaji.

Moja ya agenda zilizojadiliwa kwa undani ni swala la uunganiswaji wa wa mifuko ya hifadhi ya jamii na mkanganyiko uliojitokeza baada ya serikali kutangaza kuanza kutumika kwa vikokotoo vya mafao ya pensheni kwa wastaafu wa mifuko ya PSSSF na NSSF kuanzia Agosti 8 2018.

Aliongeza kuwa Serikali na Wadau wengine wakiwemo Waajiri walipokea hoja ya wafanyakazi na kuanza mchakato wa uunganishwaji wa mifuko ambapo TUCTA kwa niaba ya wafanyakazi walishirikishwa kwa majadiliano ya Utatu kupitia Vikao vya Kisheria ambavyo pia vilitoa fursa ya wawakilishi wa wafanyakazi kukutana na kujadiliana na wadau wote wakiwemo Waajiri, Serikali, Kamati za Bunge, NGO's, Watumishi wa Mifuko iliyokuwepo kabla ya kuunganishwa na Wafanyakazi wenyewe. 

Amefafanua kwamba TUCTA kama mwakilishi wa Wafanyakazi nchini walishiriki katika mchakato mzima wa kutungwa kwa sheria ya PSSSF namba 2 ya mwaka 2018 kwa kutoa maoni na msimamo wao kwenye vikao mbalimbali vya wadau, ambapo mapendekezo yao kwenye sheria hiyo yalizingatiwa kwa kiwango kikubwa sana. 

Alisema pia baada ya wasilisho la TUCTA la hoja za wafanyakazi kwenye vikao hivyo vya wadau, Serikali na TUCTA walishindwa kufikia muafaka hivyo serikali iliamua hoja za pande zote ziwasilishwe kwenye Baraza la Utatu la Ushauri (LESCO), ambalo lina wawakilishi wa TUCTA (4), Waajiri (4), Serikali (4) na Wataalam wawili chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu.

Kwa mujibu wa Sheria, Kikao cha LESCO ndicho kiako cha mwisho cha Utatu katika kumshauri Waziri mwenye dhamana juu ya masuala mbalimbali yayanayohusiana na kazi ikiwa ni pamoja na utungwaji wa sheria na kanuni mbalimbali zinazogusa wafanyakazi nchini. Mvutano uliojitokeza ndani ya kikao hicho kuhusu vikokotoo vya 1/580, 25% na 12.5 ambavyo vilipendekezwa na serikali na Wafanyakazi kuvipinga ilisabibisha muafaka ufikiwe kwa kura. 

Uchache wa kura za Wawakilishi na Wafanyakazi ndani ya LESCO, upande wa Serikali na wadau wengine walishinda hivyo serikali kupitia Waziri mwenye dhamana ikandelea na hatua ya kutangaza kuanza kutumika kwa kanuni hizo.      
Rais wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Nyamhokya akizungumza na wanahabari mjini Morogoro leo, wakati wa kutoa tamko la Kamati ya TUCTA Taifa kuhusu mkanganyiko wa kikotoo cha mafao ya pensheni yatolewayo na mifuko ya Hifadhi ya Jamii Tannzania. Kushoto ni Makamu Rais wa TUCTA, Qambos Sulle, Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo, Dk Yahya Msigwa (wa pili kulia) na Naibu Katibu Mkuu Jones Majura. 
Sehemu ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), wakimsikiliza Rais wa shirikisho hilo, Tumaini Nyamhokya alipozungumza na wanahabari mjini Morogoro leo, wakati wa kutoa tamko la Kamati ya TUCTA Taifa kuhusu mkanganyiko wa kikotoo cha mafao ya pensheni yatolewayo na mifuko ya Hifadhi ya Jamii Tanzania. 
Sehemu ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), wakiimba wimbo wa 'Solidarity Forever' wakati wa mkutano huo. 
Sehemu ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), wakimsikiliza Rais wa shirikisho hilo, Tumaini Nyamhokya alipozungumza na wanahabari mjini Morogoro leo, wakati wa kutoa tamko la Kamati ya TUCTA Taifa kuhusu mkanganyiko wa kikotoo cha mafao ya pensheni yatolewayo na mifuko ya Hifadhi ya Jamii Tanzania. 

UPELELEZI KESI YA UHUJUMU UCHUMI YA AKRAM AZIZ BADO HAUJAKAMILIKA

0
0
Mshtakiwa wa  kesi ya uhujumu uchumi mfanyabiashara maarufu, Rostam Aziz, Akram Aziz akiwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Jijini Dar es Salaam.

Na Karama Kenyunko blogu ya jamii.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeiahirisha kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili, mdogo wa mfanyabiashara maarufu, Rostam Aziz, Akram Aziz, kwa sababu upelelezi bado haujakamilika.

Akram ambaye alifikishwa mahakamani hapo Oktoba 31, 2018 na kufunguliwa keai namba 82/2018 anakabiliwa na mashitaka 75 yaikiwemo ya kukutwa na nyara za serikali, silaha, risasi na utakatishaji fedha wa dola za Marekani 9,018.

Wakili wa Serikali, Mkunde Mshanga  amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustino Rwizile, kuwa kesi hiyo leo Desemba 6.2018 imekuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi bado haujakamilika.

Kufuatia taarifafa hiyo, Hakimu Rwizile ameahirisha kesi hiyo hadi Desemba 13, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Akram  anakabiliwa na mashitaka mawili ya kukutwa na nyara za serikali, mashitaka 70 ya kukutwa na silaha, mashitaka mawili ya kukutwa na risasi zaidi ya 6,496 na moja la utakatishaji fedha.

Inadaiwa  kuwa Oktoba 30, mwaka huu mshitakiwa akiwa maeneo ya Oysterbay wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, alikutwa na nyara za serikali ambayo ni meno sita ya tembo yenye thamani ya dola za Marekani 45,000 sawa na Sh 103, 095,000, mali ya serikali.

Pia inadaiwa Oktoba 30, mwaka huu maeneo ya Oysterbay wilayani Kinondoni, mkoani humo Akram alikutwa na nyara za serikali ambazo ni nyama ya nyati yenye uzito wa kilogramu 65, yenye thamani ya dola za Marekani 1,900 sawa na Sh 4,352,900 mali ya serikali bila kuwa na kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapoli nchini.

Katika mashitaka ya tatu hadi la 72, kwamba siku hiyo na eneo hilo hilo, mshitakiwa huyo alikutwa na silaha aina ya Pistol bila ya kibali cha mrajisi wa silaha.

Inadaiwa katika mashitaka ya 73 kuwa, Oktoba 30, mwaka huu maeneo ya Oysterbay mshitakiwa alikutwa na risasi 4,092 na katika mashitaka mengine ilidaiwa mshitakiwa alikutwa na risasi 2,404 bila kuwa na kibali.

Katika mashitaka ya utakatishaji fedha, inadaiwa kuwa Oktoba 30, mwaka huu maeneo hayo ya Oysterbay, Akram alitakatisha USD 9,018 huku akijua kuwa fedha hizo ni zao la kujihusisha na makosa ya uhalifu

SERIKALI KUFIKISHA UMEME NANYAMBA MKOANI MTWARA KABLA YA SHEREHE ZA MWAKA MPYA 2019-DKT KALEMANI

0
0
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Kilimanjaro katika wilaya ya Nanyumbu
 Mbunge wa Jimbo la Nanyamba Abasi Chikota akizungumza na wananchi
 MKUU wa wilaya ya Nanyamba Evod Mmanda akizungumza
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani katika akitazama nguzo
 Sehemu ya wananchi wakimsikiliza Waziri wa Nishati Dkt Kalemani
Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani amesema dhamira yake ni kuhakikisha huduma ya umeme  inafika katika wilaya ya Nanyamba mkoani Mtwara kwenye maeneo mengi kabla ya Sherehe za mwaka mpya wa 2019 ili kuweza kutoa fursa ya wananchi kunufaika na huduma hiyo muhimu kwa maendeleo.

Dkt Kalemani aliyasema hayo kwenye  mtaa Kilimanjaro wilaya ya Nanyamba mkoani Mtwara wakati wa ziara yake ambapo alisema  haridhishwi na kasi ya mkandarasi aliyepewa kazi ya kuunganisha vijiji vya Nanyamba na kusema kuwa anatoa siku 20 kwa mkandarasi huyo kukamilisha kazi ya kuunganisha umeme mtaa wa kilimanjaro na maeneo ya jiran hasa kwenye taasisi zinazohudumia jamii kama hospitali na shule.

“Sijaridhishwa na kasi ya mkandarasi, Sasa leo wakati sisi tunaondoka mkandarasi yeye atabaki, ili kuhakikisha kabla ya sikukuu ya chrismas na mwaka mpya umeme Nanyamba unawaka, mkandarasi aweke magenge yake hapa nataka kazi ifanyike”

Aidha waziri Dkt.Kalemani amelitaka Shirika la Umeme Tanzania,TANESCO kufungua ofisi katika wilaya ya Nanyamba ili kusogeza huduma kwa wananchi, ambao wapo tayari kulipia huduma ya Umeme

“Wanamtwara wote ninaimani uwezo wa kulipa ela ya kuunganishiwa umeme mnayo, hasa kipindi hiki ambacho Serikali inanunua mazao ya korosho hapa mtwara, hivo naamini wote hapa kwa Sasa uwezo wa kulipia elfu 27ya umeme mnao"Alisema

Alieleza kutokana na hali hiyo Shirika hilo litafungua ofisi yao Nanyamba ili kusudi waweze kulipia na kuongeza kuwa vifaa maalum vya Umeme Tayari (UMETA) 250 vitatolewa kwa wananchi ambao hawana uwezo wa kutandaza nyaya katika nyumba zao ili waweze kuunganishwa na huduma ya Umeme.

Waziri wa Nishati Dkt.Medard kalemani yupo mkoani Mtwara, akifanya ziara ya kikazi ya kukagua maendeleo ya Miradi ya Umeme vijijini (REA)na kuwataka wananchi kuutumia umeme kama fursa ya kujiongeZea kipato kupitia biashara mbalimbali

WAZIRI MKUU AFUNGUA KIWANJA CHA TAIFA CHA MCHEZO WA BASEBALL

0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe wakati alipowasili kwenye Shule ya Sekondari ya Azania jijini Dar es salaam, Desemba 6, 2018 Kufungua Kiwanja Kipya cha Taifa cha Baseball na Kuzindua Mashindano  ya Taifa ya Baseball.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Balozi wa Japan Nchini,    Shinichi Goto wakati alipofungua Kiwanja Kipya cha Taifa cha Baseball na Kuzindua Mashindano ya  Taifa ya Baseball, kwenye Shule ya Sekondari ya Azania jijini Dar es salaam, Desemba 6, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza wakati alipofungua kiwanja Kipya cha Taifa cha Baseball na Kuzindu Mshindano ya Taifa ya Baseball   kwenye Shule ya Sekondari ya Azania jijini Dar es salaam, Desemba 6, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimtambulisha Mkwe wa Jackie Robinson, Muasisi wa Mchezo wa Baseball Duniani, Rutti David Robinson (katikati) na Mjukuu wa Muasisi huyo, Busaro David Robinson   (kulia) wakati alipofungua Kiwanja Kipya cha Taifa cha Baseball na Kuzindua Mashindano ya Taifa ya  Baseball   kwenye Shule ya Sekondari ya Azania jijini Dar es salaam, Desemba 6, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Kiwanja Kipya wa Taifa cha Baseball na Kuzindua Mashindano ya Taifa ya Baseball kwenye Shule ya Sekondari ya Azania jijini Dar es salaam, Desemba 6, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe wakati alipofungua Kiwanja Kipya cha Taifa cha Baseball na Kuzindua Mashindano ya Taifa ya Baseball  kwenye Shule ya Sekondari ya Azania jijini Dar es salaam, Desemba 6, 2018. Kulia kwake ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe na kushoto kwake ni Balozi wa Japan Nchini, Shinichi Goto.  Kushoto ni Mkwe wa Jackie Robinson ambaye ni Muasisi wa mchezo wa Baseball Duniani, Rutti David Robinson na wapili kushoto ni Mjukuu wa Muasisi huyo, Busaro Robinson. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akirusha mpira huku Balozi wa Japan Nchini, Shinichi Goto  (kushoto) akijiandaa kuuzuia wakati Waziri Mkuu alipofungua Kiwanja Kipya cha Taifa cha Baseball na Kuzindua Mashindano ya Taifa ya Baseball kwenye Shule ya Sekondari ya Azania jijini Dar es salaam, Desemba 6, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mmoja wa wadhamini wa Ujenzi wa Kiwanja Kipya cha Taifa cha Baseball, Dkt. Kazusue Konoike wakati alipofungua kiwanja hicho na  Kuzindua Mashindano ya Taifa ya Baseball kwenye Shule ya Sekondari ya Azania jijini Dar es slaam, Desemba 6, 2018. Katikati ni Balozi wa Japan Nchini, Shinichi Goto. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefungua kiwanja kipya cha Taifa cha mchezo wa Baseball na kuzindua mashindano ya Taifa ya Baseball nchini. Amewaagiza viongozi wa Wizara ya Habari, Sanaa, Michezo na Utamaduni na Ofisi ya Rais-TAMISEMI waone umuhimu wa kuuendeleza mchezo huo.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Alhamisi, Desemba 6, 2018) alipofungua kiwanja cha Baseball katika shule ya Sekondari ya Azania, jijini Dar es Salaam. Amesema iwapo mchezo huo utaratibiwa vizuri na kuingizwa katika michezo  UMISETA na UMITASHUMTA utaleta tija kwa wanafunzi wanaoucheza nchini.

Waziri Mkuu amesema thamani ya uwanja huo ni takribani Dola za Kimarekani 80.234 ambazo zimetolewa kwa msaada kutoka Serikali ya Japani.

Amesema anaishukuru Serikali ya Japan na amefarijika kwa dhamira yao ya kuunga mkono utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi CCM 2015-2020 hususan ibara ya 161.

Waziri Mkuu amesema ilani inaielekeza Serikali kujenga na kuimarisha miundombinu ya michezo nchini na kuifanya sekta ya michezo kutoa ajira hususan kwa vijana.

“Pia naishukuru Osaka Rotary Club ya nchini Japan kwa msaada wao wa dola za Kimarekani 12,856 kwa kufadhili mashindano hayo ya sita ya mchezo wa Baseball.”

Amesema jitihada hizo zitaufanya mchezo wa baseball kuwa ni mmoja wa mchezo huo kukua kwa kasi na unachezwa kuanzia ngazi za shule ya msingi na sekondari.

“Nina hakika baada ya hapo Tanzania itaweza kushiriki kwenye mashindano ya kitaifa na kimaifaifa na hasa yale ya Olimpiki ya Tokyo Japan 2020.

Kadhalika, Waziri Mkuu ameagiza uwanja huo ulindwe na utunzwe ipasavyo ili utumike katika mashindano ya ndani na nje ili uwe sehemu ya kuitangaza nchi.

Awali, Balozi wa Japan nchini, Balozi Shinichi Goto alisema nchini Japan mchezo huo pia unasaidia katika kuwajenga vijana kukua kinidhamu na kujiamini.

Alisema anatarajia kwamba mashindano ya mchezo huo yatakuwa endelevu nchini na wachezaji watacheza vizuri kutokana na uwepo wa uwanja mzuri.

Balozi huyo alisema mchezo huo unafundishwa na walimu wa Kijapani katika mikoa mbalimbali Tanzania Bara na Zanzibar.

BENKI YA UBA YABORESHA HUDUMA ZA KIMTANDAO KWA KUZINDUA MAGIC BANKING

0
0
Ikiwa ni jitahada za kuendelea kuwa benki bora Barani Afrika kwa huduma za simu za mkononi na kuendelea kuendana na jinsi mtandao unapokuwa haraka na kuwa na bidhaa na huduma zilizo bora kabisa, benki ya UBA Tanzania leo imetangaza kuzindua huduma nyingine bora ya kutumia simu za mkononi ya UBA Magic ambayo inapatikana kwa kupiga *150*70# kwa hapa Tanzania.

Huduma hii ya Magic Banking itamfanya mteja kwa kutumia simu yake ya mkononi kuweza kufungua akaunti mpya, kuhamisha fedha, kununua muda wa maongezi, kulipia huduma mbali mbali kama vile Dawasco, kuangalia salio pamoja na huduma nyingine za kibenki kwa kupiga *150*70# bila malipo yoyote.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kuzindua huduma hii ya Magic Banking, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi na Huduma za Kimtandao UBA Bank Tanzania Asupya Nalingigwa alisema kuwa mbali na huduma ya Magic Banking kufanya kazi kwenye simu aina yeyote ile lakini huduma hii ni salama, ya haraka na nafuu na mteja haitaji kuwa na salio ili kufanya miamala. ‘Huduma ya Magic Banking inamfanya mteja kuweza kufanya miamala ya hadi TZS 1 milioni kwa siku kwa kutumia UBA Secure Pass ambayo inaongeza usalama kwa mtumiaji,’ alisema Nalingigwa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji UBA Tanzania Usman Isiaka alisema kuwa huduma ya Magic Banking itamfanya kila Mtanzania mwenye simu iliyosajiliwa kufungua akaunti papo hapo. ‘Mteja anayetumia simu ya mkononi bila kujali anatumia mtandao ngani wa simu anaweza kufungua akaunti na sisi kwa kupiga *150*70# bila gharama yeyote, alisema Isiaka huku akiongeza kuwa kuzinduliwa kwa huduma hii ya Magic Banking ni moja ya lengo ya benki ya UBA kuweza kuwafikia mamilioni ya wananchi ambao hawajafikiwa na huduma za kibenki kwa kuwaletea huduma ambazo ni rahisi, nafuu na za haraka zinazoendana na teknolojia. Vile vile tumelenga kufikisha huduma rahisi za kifedha kwa wananchi ili kuendana na matakwa ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), aliongeza Isiaka.

Isiaka aliongeza kuwa benki ya UBA Tanzania imedhamiria kuboresha huduma za kifedha za kuzindua bidhaa na huduma zenye ubunifu ili kuweza kuwafikia wananchi wengi kwa rahisi ya teknolojia. Ili kuweza kufanikisha yote haya tumewekeza rasimali nyingi na tuna uhakika tutaweza kuwafikia walengwa wetu, alisema AIsiaka.

Uzinduzi wa Magic Banking umeenda sambasamba na kuzindua UBA Mobile banking App ya benki hiyo ambayo mteja anaweza kupakua kwa kupitia App Store na Play Store kwa watumiaji wa simu aina ya iPhone na Android. App hiyo itamuwezesha mteja kuweza kulipia huduma mbali mbali, kuangalia salio, kuomba cheque pamoja na kufanya miamala nyingine ya kibenki kwa kutumia simu zao za mkononi.

Benki ya UBA Afrika imekuwa ikiongoza kwa huduma mbali mbali za kimtandao kwenye masoko yake ambayo yapo kwenye nchi 20 Barani Afrika. Kwa kutambua uwezo wake wa kutumia teknojia kwenye huduma za kifedha, benki ya UBA iliweza kushinda tuzo ya Best Digital Bank tuzo ambazo zilitolewa na Euromoney.


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya UBA Tanzania, Usman Isiaka akizungumza waandishi wa habari, Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya benki huduma ya kutumia simu za mkononi ya UBA Magic ambayo inapatikana kwa kupiga *150*70#. Kushoto ni Meneja wa Mifumo ya Malipo ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Thomas Mongella.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya UBA Tanzania, Usman Isiaka akimuelekeza Meneja wa Mifumo ya Malipo ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Thomas Mongella jinsi ya kufungua akaunti kwa kutumia simu ya mkononi wakati wa kuzindua huduma ya UBA Magic Banking ambayo mteja anaweza kufungua akaunti mpya, kuhamisha fedha, kununua muda wa maongezi, kulipia huduma mbali mbali kama vile Dawasco, kuangalia salio pamoja na huduma nyingine za kibenki kwa kupiga *150*70# bila malipo yoyote.

HARMONIZE ATOA PARANAWE YA KUFUNGIA MWAKA WA 2018

0
0
Na Baba Faisal

MWENAMUZIKI maarufu kwenye muziki wa kizazi kipya ambaye anafanya kazi zake chini ya Lebo ya WCB Rajab Abdul Kahali a.k.a

Harmonize ameamua kuachia wimbo wake mpya wa Paranawe ambao tayari umeanza kuwa gumzo kwenye vituo mbalimbali vya redio pamoja na mitandao ya kijamii.

Unajua kwanini wimbo huo umeanza kuwa gumzo ?Ukweli ni kwamba licha ya wimbo huo kuwa una siku mbili tangu kuachiwa rasmi na msanii huyo umekuwa gumzo kwasababu Harmonize kupitia wimbo huo amethibitisha yeye ni moja kati ya wasanii bora kutokana na aina ya staili yake anayotumia katika kuimba na nyimbo zake.

Kikubwa ambacho kimeongeza ladha ya wimbo wa Paranawe ni pale ambapo ameamua kumshirikisha Rayvany ambaye kwa hakika sauti yake imefanikiwa kupenya kwenye masikio ya mashabiki wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania.Hivyo Harmonize a.k.a Konde Boy ameamua kumpa nafasi Rayvany katika wimbo huo.

Ni jana tu ndio Harmonize ameachia wimbo huo ambao tayari umeshika kasi mtaani.Kama unavyojua tena kwenye bodaboda huko mtaani tayari wameshaweka kwenye flash zao na kilichobaki wanasikiliza mdundo huo wa Paranawe kama sehemu ya kuwa na watu wa kwanza kuusikiliza.

"Kwa mwaka huu ndio wimbo wangu wa kufunga mwaka, sitatoa nyimbo nyingine mpya hadi mwakani,"amesema Harmoze wakati anazungumzia wimbo huo kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijami huku akielezea namna ambavyo Rayvvan ameonesha umahiri wa hali ya juu. Msanii huyo hakusita kumwagia sifa Rayvvany a.k.a Vann Boy.

Hata hivyo Vann Boy naye hakusita kumuelezea Harmonize kutokana na wimbo wake huo ambapo ametumia akaunti yake ya mtandao wa kijamii kumsifu kwa namna ambavyo amefanya kazi kubwa kuhakikisha anatoa ngoma iliyo bora ya kufungia mwaka.Wakati wimbo huo ukiwa ndio kwanza umetoka, kitendo cha Harmonize kumshirikisha Rayvvany kunathibitisha wawili hao kuwa

wamoja na mambo yao ni motooo.Kwa kukumbusha tu za nyuma kulikuwa na mjadala kwenye vijiwe vya mashabiki wa muziki wa kizazi kipya kuwa wawili hao haziivi lakini wamethibitisha yaliyokuwa yanasemwa hayana ukweli.

HALMASHAURI WILAYA YA KALIUA, WADAU WA MAENDELEO WAJIPANGA KUTATUA CHANGAMOTO YA UHABA WA MAJI

0
0
Na Editha Shija, Tabora

HALMASHAURI ya Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wilayani humo wamejipanga kumaliza kero ya maji kwa wananchi ambayo imekuwa ya muda mrefu katika maeneo karibu yote wilayani humo.

Akizungumza na Michuzi Blog ofisini kwake jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Dk.John Pima alibainisha kuwa ushirikiano mzuri wa watendaji na wataalamu wa halmashauri umechochea kasi nzuri ya ukusanyaji mapato, hivyo kumewezesha miradi mingi ya maji kutekelezwa kwa asilimia 100.

Amesema kuwa mfuko wa programu ya maji umekuwa chachu ya kufanikisha utekelezaji wa miradi hiyo na wana uhakika katika kipindi kifupi kijacho tatizo la maji litapungua kwa kiasi kikubwa kama si kumalizka kabisa.Pima ameongeza kutafuta ufumbuzi wa changamoto ya upatikanaji maji , ametaja miradi ya maji iliyotekelezwa kwa asilimia zote ni ujenzi wa mantenki mawili ya kuvunia maji mvua yenye ujazo wa lita 50,000 yaliyojengwa katika Shule ya Sekondari ya Uyowa na Mkindo na ujenzi wa tenki La chini ya ardhi lenye ujazo wa Lita 10,0000 lililojengwa katika Shule ya Sekondari ya Kaliua.

Miradi mingine iliyokamilishwa ni ukarabati wa visima virefu 4 katika vijiji vya uhindi viwili Songambele(1) Mwendakulima (1) pamoja na tenki moja la kuvunia maji ya mvua lenye ujazo wa Lita 50,000 katika zahanati ya kangemeAliongezea kwa kusema kuwa mradi mingine ni wa tenki la chini lenye ujazo wa Lita 10,0000 uliojengwa na kampuni ya FUM katika zahanati ya Nyasa huku kampuni ya wachina ya CHICCO iliyokuwa ikitengeneza barabara ya kaliuwa -Kazilambwa ikiwajengea miradi mitano ya maji.

Hata hivyo mkurugenzi huyo amewataka wananchi watunze miradi hiyo ili idumu kwa muda mrefu na kuwaondolea kero ya maji ya muda iliyokuwa inawakabiri.
 

BENKI YA NMB YATOA MSAADA WA STULI NA MEZA ZA MAABARA SHULE YA SEKONDARI MWANTINI

0
0
Benki ya NMB imetoa msaada wa Stuli 32 na meza 8 za maabara zenye thamani ya Shilingi milioni tano ili kusaidia wanafunzi kujifunza kwa vitendo masomo ya sayansi katika shule ya Sekondari Mwantini iliyopo katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga. 

Msaada huo umekabidhiwa leo Ijumaa Desemba 6,2018 na Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi James Katamba kwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga,Mheshimiwa Jasinta Mboneko. 

Katamba alisema msaada huo wa stuli na meza ni sehemu ya ushiriki wa benki hiyo katika maendeleo ya jamii akibainisha kuwa changamoto za sekta ya elimu nchini kwa NMB ni jambo la kipaumbele kutokana na kwamba elimu ni uti wa mgongo wa taifa lolote duniani. “NMB tulipokea maombi kuwa mnahitaji stuli na meza za maabara,tulifarijika na kuamua kuja mara moja kushirikiana nanyi ili kuwa chachu ya maendeleo ya elimu kwa watoto wetu katika shule hii”,alieleza. 

“Tunatambua kuwa kupitia jamii ndipo wateja wetu wengi wanapotoka,kwa hiyo kurudisha sehemu ya faida kwa jamii ni utamaduni,tutaendelea kuunga mkono juhudi za wadau wetu kuhakikisha changamoto za jamii zinapatiwa ufumbuzi”,aliongeza Katamba. Hata hivyo alisema kwa mwaka 2018,NMB imetenga zaidi ya shilingi bilioni 1 kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya wananchi ikiwemo kusaidia sekta ya afya na elimu hivyo kuifanya benki ya NMB kuwa benki ya kwanza kuchangia maendeleo kuliko benki yoyote nchini. 

Kwa Upande wake,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mheshimiwa Jasinta Mboneko aliishukuru benki ya NMB kwa mchango huo mkubwa katika shule ya Mwantini hali ambayo itawafanya watoto wajifunze kwa vitendo masomo ya sayansi. “Tunawashukuru sana NMB kwa jitihada mnazofanya katika sekta ya elimu,serikali pekee haiwezi kumaliza changamoto zote, ni lazima tushikirikiane tushirikiane na wadau”,alisema Mboneko. 

“Wanafunzi someni kwa bidii ,epukeni vishawishi na kataeni kuolewa katika umri mdogo,someni masomo ya sayansi kwani Tanzania ya Viwanda itajengwa kama kutakuwa na wataalamu wa Sayansi”,aliongeza. Naye Diwani wa kata ya Mwantini,Majenga Samson aliitaka halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kumalizia ujenzi wa jingo la maabara katika shule hiyo pamoja kujenga bweni kwa ajili ya wanafunzi wa kike. 

Hafla fupi ya makabidhiano hayo pia imehudhuriwa na Mwenyekiti wa ALAT taifa,mheshimiwa Gulam Hafeez Mukadam na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Gulam Hafeez Mukadam.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mheshimiwa Jasinta Mboneko na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Ngassa Mboje wakipokea moja kati ya stuli 32 kutoka benki ya NMB. Kulia ni Meneja wa Benki ya NMB Manonga,Baraka Ladislaus na Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi James Katamba. 
Kulia ni Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi James Katamba akishikana mkono na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mheshimiwa Jasinta Mboneko wakati wa zoezi la kukabidhi stuli 32 na meza 8 za maabara kwa ajili ya shule ya sekondari Mwantini.Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa ALAT taifa,mheshimiwa Gulam Hafeez Mukadam ambaye pia ni Mstahiki meya wa Manispaa ya Shinyanga.
 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mheshimiwa Jasinta Mboneko akisalimiana na wanafunzi wa shule ya sekondari Mwantini.
Picha ya pamoja wakati wa makabidhiano ya stuli na meza za maabara katika shule ya sekondari Mwantini. 

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mheshimiwa Jasinta Mboneko akiishukuru benki ya NMB kwa msaada wa stuli na meza za maabara katika shule ya sekondari Mwantini iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. Wa pili kulia ni Diwani wa kata ya Mwantini Majenga Samson,akifuatiwa na Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi James Katamba na Meneja wa Benki ya NMB Manonga,Baraka Ladislaus. 
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi James Katamba akizungumza wakati wa kukabidhi stuli 38 na meza 8 za maabara katika shule ya sekondari Mwantini.Alisema benki hiyo imekuwa ikisaidia miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi kwa kujikita zaidi kwenye elimu kwa kutoa madawati na viti na afya kutoa vitanda na magodoro pamoja na kusaidia pale majanga yanapotokea nchini.
Sehemu ya stuli na meza za maabara zilizotolewa na benki ya NMB kwa ajili ya wanafunzi katika shule ya sekondari Mwantini iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Meneja wa Benki ya NMB Manonga,Baraka Ladislaus akimkaribisha Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi James Katamba ili akabidhi stuli 32 na meza 8 za maabara kwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mheshimiwa Jasinta Mboneko kwa ajili ya shule ya sekondari Mwantini.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mheshimiwa Jasinta Mboneko akiwa katika picha ya pamoja na walimu,wanafunzi,viongozi wa benki ya NMB na viongozi mbalimbali. 
Picha nyingine ya pamoja. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

JESHI LA MAGEREZA LAFANYA MAADALIZI YA UZINDUZI WA DAWATI LA JINSIA LEO JIJINI DAR

0
0
 Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike akitoa hotuba  katika ufunguzi wa mafunzo ya siku moja  kuhusu mambo ya Dawati la Jinsia kwa Waratibu na Watendaji  wa Dawati hilo kutoka  Magereza yote nchini leo Desemba 06, 2018  ikiwa ni maandalizi ya uzinduzi wa Dawati la Jinsia ndani ya Jeshi la Magereza utakaofanyika  Desemba  07, 2018 katika viwanja vya Karimjee jijini  Dar es Salaam.
 Mwenyekiti  wa Taifa wa Dawati la Jinsia katika Jeshi la Magereza Kamishna wa Magereza Tusekile Mwaisabila akichangia jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku moja  kuhusu mambo ya Dawati la Jinsia kwa Waratibu na Watendaji  wa Dawati hilo kutoka  Magereza yote nchini  ikiwa ni maandalizi ya uzinduzi wa Dawati la Jinsia ndani ya Jeshi la Magereza yatakayofanyika  Desemba  07, 2018.
 Meneja Huduma na Mikopo Binafsi kutoka Benki ya NMB Bw. Emmanuel Mahodaga akitoa mada kuhusu huduma za NMB hasa kwa watumishi wa Umma. NMB ni mmoja wa wadhamini wa shughuli za Uzinduzi wa Dawati la jinsia katika Jeshi la Magereza unaotarajiwa kufanyika kesho tarehe 07 Desemba, 2018 katika viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam.
 Mtendaji Mkuu wa Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA) Bi. Tike Mwambipile akichangia mada katika mafunzo  kuhusu mambo ya Dawati la Jinsia kwa Waratibu na Watendaji  wa Dawati hilo wa Magereza yote nchini  yaliyofanyika leo Desemba 06, 2018 katika Bwalo Kuu la Magereza ikiwa ni maandalizi ya uzinduzi wa Dawati la Jinsia ndani ya Jeshi la Magereza utakaofanyika Desemba  07, 2018 katika viwanja vya Karimjee jijini  Dar es Salaam.
 Baadhi ya washiriki wakifuatilia  mafunzo  kuhusu mambo ya Dawati la Jinsia kwa Waratibu na Watendaji  wa Dawati hilo kutoka  Magereza yote nchini yanayofanyika katika Bwalo Kuu la Magereza Ukonga, Dar es salaam  ikiwa ni maandalizi ya uzinduzi wa Dawati la Jinsia ndani ya Jeshi hilo. Uzinduzi huo utafanyika Desemba  07, 2018 katika viwanja vya Karimjee jijini  Dar es salaam.
 Mtoa Mada kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Mapunda  John ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii akifafanua jambo wakati wa mafunzo ya jinsia kwa Waratibu na Watendaji  wa Dawati la Jinsia kutoka  Magereza yote nchini yaliyofanyika leo Desemba 06, 2018 katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Magereza Ukonga, Dar es Salaam.
  Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maafisa na askari wa kike kutoka magereza mabalimbali hapa nchini ambao ni waratibu wa Dawati la Jinsia waliohudhuria mafunzo kuhusu Dawati la Jinsia yaliyofanyika leo Desemba 06, 2018 katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Magereza Ukonga, Dar es Salaam.
  Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wenye cheo cha Mkaguzi Msaidizi wa Magereza waliohudhuria mafunzo kuhusu Dawati la Jinsia yaliyofanyika leo Desemba 06, 2018 katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Magereza Ukonga, Dar es Salaam.
Baadhi ya watoa mada na wafadhili  wakiwa katika picha ya pamoja na  Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (katikati waliokaa) wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Dawati la Jinsia kwa Waratibu na Watendaji wa Dawati hilo kutoka magereza yote nchini yaliyofanyika leo Desemba 06, 2018. Kushoto ni Mkuu wa Magereza wa Mkoa wa Pwani ACP Rehema Songelaeli,  Mratibu wa Dawati la Jinsia Makao Makuu ya Magereza SACP Betha Minde na Mwenyekiti waTaifa wa Dawati la Jinsia ndani ya Magereza Kamishna wa Magereza Tusekile Mwaisabila. Kulia ni Afisa Mnadhimu wa Magereza Mkoa wa Morogoro ACP Elizaberth Mbezi, Mkuu wa Magereza wa Mkoa wa Lindi ACP Josephine Semwenda na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam SACP Julius Ntambala. (Picha zote na Jeshi la Magereza)

MKUU WA WILAYA NAMTUMBO SOPHIA KIZIGO AONGOZA OPERESHENI YA KUONDOA WAVAMIZI NDANI YA HIFADHI

0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

KAMATI ya Ulinzi na Usalama ikongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Kizigo imeamua kufanya operesheni maalumu ya kusaka na kuwaondoa watu waliovamia maeneo ya hifadhi ya Mbarang'andu ambapo kuna watu kadhaa wamekamatwa na sasa wanaohojiwa.

Akizungumzia operesheni hiyo Mkuu wa Wilaya Kizigo ameiambia leo, Michuzi Blog kuwa wameanza kuifanya juzi na jana (Desemba 4 na Desemba 5 mwaka 2018) ambapo mbali ya kamati ya ulinzi na usalama pia kulikuwepo na vikosi kazi na timu ya wataalam mbalimbali kutoka Halmashauri ya wilaya hiyo na kwamba uamuzi huo wa kufanya msako umekuja baada ya doria ya kwanza iliyofanyika kwa njia ya anga (ndege) ambapo walijionea uharibifu uliofanyika kwenye hifadhi ya Ushoroba wa Selous , Niassa, Mbarang'andu , Kisungule na Kimbanda.

"Kwa kutumia usafiri wa anga ambao tumefanya kwenye maeneo mbalimbali ya hifadhi tumejionea namna ambavyo kuna uharibu wa mazingira.Hivyo jana tumeamua kufanya msako maalumu wenye lengo la kuwaondoa wavamizi ambao wanaharibu hifadhi hiyo,"amesema Mkuu wa Wilaya Kizigo.

Amesema katika kuhakikisha wanafanikiwa kwenye operesheni hiyo juzi na jana waliamua kwenda kwa miguu maeneo ambayo yamefanyiwa uharibifu na tayari kuna baadhi ya watu ambao wamewakamata kwa kutuhuma za kuharibu hifadhi ambapo pia amesema wapo watu ambao wanaingia kwenye msitu huo kwa ajili ya kufanya ujangiri kwa kuua wanyama.

Amesema baadhi ya watu ambao wamewahoji wamedai wanaingia kwenye hifadhi hiyo kwa ajili ya kilimo lakini ukweli ni kwamba watu hao hao ndio wamekuwa wakihusika na ujangiri, uharibifu wa mazingira kwa kutaka miti bila mpangilio."Tunaendelea kuwahoji watu ambao tumewakamata ndani ya hifadhi na kisha sheria itachukua mkondo wake,"amesisitiza Mkuu wa Wilaya hiyo.

Wananchi mbalimbali ambao wamezungumza na Michuzi Blog kuhusu operesheni hiyo wamempongeza Mkuu wa Wilaya kwa hatua anazochukua kuhakikisha hifadhi zilizopo ndani ya wilaya yao zinakuwa salama kwa kutoharibiwa na watu ambao wamekuwa na tabia ya kuvamia na kufanya matukio ya ujangiri. Wamemuahidi Mkuu wa Wilaya pamoja na wasaidizi wake kuendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali ikiwa ni pamoja na kuwataja kwa majina watu ambao wanavamia misitu hiyo na kufanya uharibifu.





KAMATI ya Ulinzi na Usalama ikongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Kizigo wakiendelea kukamata vifaa mbambali vya watu waliovamia maeneo ya hifadhi ya Mbarang'andu ambapo kuna watu kadhaa wamekamatwa na sasa wanaohojiwa.
Sehemu ya Kamati i ya Ulinzi na Usalama ikongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Kizigo (wa pilia kulia) wakiwa kwenye operesheni maalumu ya kusaka na kuwaondoa watu waliovamia maeneo ya hifadhi ya Mbarang'andu ambapo kuna watu kadhaa wamekamatwa na sasa wanaohojiwa.
Baadhi ya Watuhumiwa waliokamatwa na kamati ya Ulinzi na Usalama ikongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Kizigo  (hayupo pichani) walipokuwa wakifanya operesheni maalumu ya kusaka na kuwaondoa watu waliovamia maeneo ya hifadhi ya Mbarang'andu ambapo watu kadhaa wamekamatwa na sasa wanaohojiwa.

SERIKALI YAZISHAURI BENKI NCHINI KUSHUSHA RIBA ZA MIKOPO KUCHOCHEA UCHUMI WA VIWANDA

0
0
Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, amezitaka Benki nchini kushusha viwango vya riba za mikopo ili kuwawezesha wananchi wengi zaidi wakiwemo wakulima kunufaika na huduma za kifedha zinazotolewa na taasisi hizo za fedha kwa ajili ya kujiletea maendeleo yao.

Dkt. Kijaji ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati akifungua rasmi Tawi la Benki Azania, Sokoine, na kusisitiza kuwa Benki zina nafasi kubwa wa kuisaidia nchi kufikia azma yake ya kuwa ya viwanda ifikapo mwaka 2025 kwa kukuza mitaji na biashara za wananchi.

Alisema kuwa hivi karibuni Serikali imechukua hatua madhubuti za kiutawala na kisera ili kuhakikisha kuwa riba za mikopo katika soko zinapungua, ikiwemo Benki Kuu kutoa mikopo ya muda mfupi kwa benki za biashara, kushusha riba kutoka asilimia 16.0 hadi asilimia 9.0.

"Tumepunguza kiwango cha chini cha amana kinachotakiwa kuwekwa Benki Kuu na benki za biashara kutoka asilimia 10.0 hadi asilimia 8.0, hatua ambazo zimesaidia kupunguza riba katika soko kutoka wastani wa zaidi ya asilimia 20 hadi asilimia 17" aliongeza Dkt. Kijaji

"kama haya yote yamefanyika, iweje benki ziendelee kutoza riba ya asilimia 17 kwa kisingizio cha kuogopa mikopo chechefu wakati Serikali kupitia Benki Kuu, imeanzisha kanzi data ya kuhifadhi na kutoa taarifa ya wakopaji (Credit Reference Bureau System)" alihoji Dkt. Kijaji

 Aidha, Dkt. Kijaji ameelezea kusikitishwa kwake na hatua ya benki hiyo kuwa miongoni mwa benki 5 zilizofungiwa kwa kipindi maalum kushiriki katika kuuza na kununua fedha za kigeni baada ya kukiuka taratibu za biashara hiyo.

" Kisheria, benki zote za biashara zinatakiwa kutoa taarifa Benki Kuu kuhusu miamala ya Soko la Fedha za Kigeni kati ya Mabenki waliyofanya kwa siku lakini Benki yako ni miongoni mwa benki zilizovunja utaratibu huu, hii niaibu!" alisisitiza Dkt. Kijaji "

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania Bw. Charles Itembe, amesema Benki yake imeendelea kufanya vizuri katika soko kwa kupata faida na kwamba imejipanga kutoa mikopo na huduma za kifedha kwa wananchi mkoani Dodoma kwa viwango vya juu.

"Benki yetu, mwaka 2017, imetengeneza faida ya shilingi bilioni 1.81 ikilinganishwa na hasara ya Shilingi bilioni 6 iliyoripotiwa Desemba 2016, na imeongeza rasilimali zake kutoka sh. bilioni 338 hadi bilioni 390" alisema Bw. Charles Itembe.

Alisema kuwa Benki yake imeongeza kiasi cha mikopo iliyotoa kutoka sh. bilioni 129 mwaka 2016 hadi sh. bilioni 187.7  mwaka 2017, sawa na ongezeko la asilimia 10.23 huku akiba za wateja zikiongezeka kutoka shilingi bilioni 236 mwaka 2016 hadi sh. bilioni 271 mwaka jana.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Azania ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ya Watumishi wa Umma (PSSSF) Bw. Eliud Sanga, ameitaka Benki hiyo kutekeleza mkakati wake wa kuanza kutoa mikopo ili kuimarisha Sekta ya ujenzi wa viwanda nchini.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akiwa katika ufunguzi wa tawi jipya la Benki ya Azania, Sokoine, Jijini Dodoma. Kulia ni Mkurugenzi wa Benki hiyo Bw. Charles Itembe na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki hiyo Bw. Eliud Sanga.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akihutubia wakati wa ufunguzi wa tawi jipya la Benki ya Azania, Sokoine, Jijini Dodoma, ambapo aliipongeza benki hiyo kwa kuwa miongoni mwa benki chache zilizofanya maamuzi sahihi ya kuunga sera ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuhamia Dodoma kwa vitendo.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akihutubia wakati wa ufunguzi wa tawi jipya la benki ya Azania, Sokoine Jijini Dodoma, ambapo alitoa wito kwa benki hiyo kupunguza riba za mikopo ili wananchi wengi zaidi waweze kunufaika.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa bodi ya Benki ya Azania, Bw. Eliud Sanga, baada ya kuhutubia katika ufunguzi wa tawi la benki hiyo la Sokoine Jijini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa tawi jipya la Benki ya Azania, Sokoine, Jijini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa tawi jipya la Benki ya Azania, Sokoine Jijini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akiagana na Mkurugenzi wa Benki ya Azania, Bw. Charles Itembe, mara baada ya kukamilisha ufunguzi rasmi wa tawi jipya la benki hiyo, Sokoine na kutembelea ofisi za tawi hilo, Jijini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na menejimenti na wageni waliokuwa meza kuu mara baada ya kufungua rasmi Tawi la Benki ya Azania iliyopewa jina la Sokoine, Jijini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na menejimenti na watumishi wa Benki ya Azania baada ya ufunguzi rasmi wa tawi jipya la benki hiyo la Sokoine, Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa benki ya Azania ambao walihudhuria katika ufunguzi wa tawi jipya la benki hiyo Sokoine Jijini Dodoma.(Picha na Saidina Msangi-Wizara ya Fedha na Mipango)

BENKI YA NMB YATOA MSAADA WA VITANDA NA MASHUKA VYENYE THAMANI YA TSH. MILIONI 1O, KWA HOSPITALI YA MNAZI MMOJA

0
0

Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud (alievaa tai rangi ya bluu) akimkabidhi Kitanda na Mashuka Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Mnazimmoja Dkt. Ali Salum (kulia) Mbunge wa viti Maalum Wanawake CCM Asha Abdalla Juma, Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Zanzibar Abdalla Duchi na (kushoto) Meneja Uhusiano Faraja Kaziulaya kutoka Dar es Salam. 

Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Zanzibar Abdalla Duchi akimkabidhi Mashuka na Kitanda Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud (kulia) ni Mbunge wa viti Maalum Wanawake CCM Asha Abdalla Juma (Mshua) na Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Mnazimmoja Dkt. Ali Salum. 

Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud (alievaa tai rangi ya bluu) akimkabidhi Kitanda na Mashuka Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Mnazimmoja Dkt. Ali Salum (kulia) Mbunge wa viti Maalum Wanawake CCM Asha Abdalla Juma, Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Zanzibar Abdalla Duchi na (kushoto) Meneja Uhusiano Faraja Kaziulaya kutoka Dar es Salam.
Mbunge wa viti Maalum Wanawake CCM Asha Abdalla Juma (Mshua) na Mdau wa mambo ya afya akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada wa Vitanda na Mashuka kwaajili ya huduma za Kujifungulia katika Hospitali Kuu ya Mnazimmoja jengo la Dodoma.
Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Zanzibar Abdalla Duchi akizungumza na Mgeni Mwalikwa pamoja na Watendaji wa Hospitali ya Mnazi Mmoja kabla ya kukabidhi msaada wa Vitanda nane (8) na mashuka mia moja na ishirini (120) kwaajili ya Hospitali hiyo.
Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud ambae ni Mgeni Mwalikwa katika hafla ya kukabidhi Vitanda na Mashuka akizungumza machache kabla ya kukabidhiwa msaada huo( kulia) ni Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Zanzibar Abdalla Duchi, Meneja Miradi Benki ya NMB Lilian kisamba na Mbunge wa viti Maalum Wanawake CCM Asha Abdalla Juma (Mshua).
Watendaji wa Hospitali ya Mnazimmoja waliohudhuria katika hafla ya kukabidhiana msaada wa Vitanda na Mashuka.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MKUU MSTAAFU WA USALAMA WA TAIFA IKULU JIJIN DAR

0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Bw. Apson Mwang’onda Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa, alipomtembela Ikulu jijini Dar es Salaam.Disemba 6,2018.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Bw. Apson Mwang’onda Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa, wakati wanaagana mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.Disemba 6,2018.

AWESO AFANYA ZIARA RUANGWA NA NACHINGWEA -LINDI

0
0
Naibu Waziri wa Maji Mheshimiwa Jumaa Aweso (Mb) jana  amehitimisha ziara Ruangwa Mkoani Lindi kwa kukagua miradi ya Kitandi, Mihewe na Mbekenyera. Aidha Aweso amefanya ziara Wilayani Nachingwea kwa kukagua miradi ya Mtua na Chimbendenga.
 Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akipewa maelezo juu mitambo ya kusafisha maji ya mradi wa Mbekenyera – Ruangwa.
IMG_8213
 Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akiongea na Mkazi wa Mtua alipokuwa akikagua mradi wa maji katika kijiji hicho wakati wa ziara yake aliyoifanya jana IMG_8254
Naibu wa Maji Jumaa Aweso akiongea na wananchi wa Chimbenenga Nachingwea wakati wa wa ziara yake ya kukagua miradi ya maji.

TRA YAWATAKA MAWAKALA FORODHA KUHAKIKISHA NAMBA ZAO ZA UTAMBULISHO WA MLIPAKODI (TIN)

0
0
Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) imewataka Mawakala wa Forodha wote kuhakakisha wanafanya uhakiki wa namba zao za Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza na kuisaidia mamlaka hiyo kukusanya mapato mengi.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Naibu Kamishna wa Kodi za Ndani wa mamlaka hiyo, Abdul Zuberi katika Semina iliyowakutanisha na makampuni ya mawakala wa forodha iliyojadili masuala mbalimbali ya kodi na ushuru wa forodha.

Amesema kuwa mawakala hao wanatakiwa kuhakiki TIN zao kutokana na kuwepo mkanganyiko kuwa na zaidi TIN hali inayowapa shida ya kutambua idadi ya mawakala wanaotakiwa kulipa kodi.“ Kuna watu wana TIN zaidi ya moja wanazitumia bila kufanyiwa uhakiki na wengine wanazifanyia udanganyifu inatupa tabu kuwatamabua hivyo ni vema mkazifanyia uhakiki,” amesema.

Amebainisha kuwa TRA mawakala watakaobainika kutumia TIN zaidi ya moja bila kuzifanyia uhakiki watachukuliwa hatua za kisheria.Amesisitiza kuwa mawakala wa forodha watakaofanya uhakiki wa TIN zao watapatiwa cheti cha utambulisho ili kuondokana usumbufu wakati wa kuwakagua.

Ameongeza kuwa mawakala wanatakiwa kuwasilisha taarifa sahihi za mapato yao kwa mwaka pamoja kulipa Kodi ya Ongezeko la Mapato (VAT).

Amefafanua kuwa mamlaka hiyo itatoa kwa mawakala jinsi ya kutambua Mashine za Kielektroniki feki (Efd) na kwamba kufanya kutawasaidia kuwaepusha kukumbwa na mkono wa sheria na faini.Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Mawakala wa Forodha (TAFA) ambaye pia Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam,Frank Kamugisha ameiomba mamalaka hiyo kujenga utaratibu wa kukutana nao kuzungumzia changamoto mbalimbali zinazowakabili ili ziweze kutafutiwa ufumbuzi. 

Kamugisha amesema anaamini mambo yaliyojadiliwa yatafanyiwa kazi ili kuondoa sintofahamu kati yao na TRA kwenye masuala ya kodi na forodha. 
Pia amesema chama hicho kitayapa umuhimu yale yote walioelekezwa ili kujenga uchumi wa nchi kwa kuisaidia mamlaka hiyo kukusanya kodi.

Dkt. Abbasi Awapiga Msasa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa

0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiwasalisha mada kuhusu umuhimu wa Mawasiliano ya Kimkakati katika kuisemea Serikali wakati wa kikao cha Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa Leo Jijini Dodoma

Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiwaonesha Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa jarida Maalum utekelezaji wa Miradi Mbalimbali ya Maendeleo katika kipindi cha Miaka Mitatu ya Rais Dkt. John Magufuli Leo Jijini Dodoma.



Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiwaonesha Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa jarida Maalum utekelezaji wa Miradi Mbalimbali ya Maendeleo katika kipindi cha Miaka Mitatu ya Rais Dkt. John Magufuli Leo Jijini Dodoma.



Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akichangia Mada baada ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi kuwasilisha mada kuhusu umuhimu wa Mawasiliano ya Kimkakati katika kuisemea Serikali wakati wa kikao cha Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa Leo Jijini Dodoma



Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Christina Mdeme akichangia Mada baada ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi kuwasilisha mada kuhusu umuhimu wa Mawasiliano ya Kimkakati katika kuisemea Serikali wakati wa kikao cha Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa Leo Jijini Dodoma


Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Ally Hapi akisoma jarida Maalum utekelezaji wa Miradi Mbalimbali ya Maendeleo katika kipindi cha Miaka Mitatu ya Rais Dkt. John Magufuli Leo Jijini Dodoma.

Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Bi. Theresia Mbando akisoma jarida Maalum utekelezaji wa Miradi Mbalimbali ya Maendeleo katika kipindi cha Miaka Mitatu ya Rais Dkt. John Magufuli Leo Jijini Dodoma.

SERIKALI YAIAGIZA BODI YA WATAALAM WA UNUNUZI NA UGAVI KUDHIBITI MAADILI YA WATAALAM WA UNUNUZI NA UGAVI

0
0
Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Mipango wa Wizara hiyo, Bw. Richard Mkumbo, akifunga Kongamano la Tisa la Bodi ya Wataalam wa ununuzi na ugavi (PSPTB), kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bi. Susana Benard Mkapa, ukumbi wa DCC, Dodoma.
Baadhi ya Washiriki wa Kongamano la Tisa la Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPSTB), wakiimba wimbo wa Taifa wakati wa hafla ya kufunga kongamano hilo la siku tatu lililofanyika Jijini Dodoma na kuwashirikisha wataalam 650 kutoka Tanzania Bara.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi Sr. Dkt. Hellen Bandiho, akisoma hotuba ya ukaribisho kwa mgeni rasmi Kaimu Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Richard Mkumbo (hayupo pichani), wakati wa hafla ya kufunga Kongamano la Tisa la Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), iliyofanyika katika ukumbi wa DCC, Jijini Dodoma
Kamishana wa Idara ya Sera ya Ununuzi wa Umma wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Frederick Mwakibinga (kushoto), na mjumbe wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) Dr. Laurent Shirima, wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi, Kaimu Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Richard Mkumbo, wakati akifunga kongamano la Tisa la Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), katika ukumbi wa DCC, Jijini Dodoma.
Baadhi ya Washiriki wa Kongamano la Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPSTB), wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi, Kaimu Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Richard Mkumbo, wakati akifunga Kongamano la Tisa la Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), katika ukumbi wa DCC, Jijini Dodoma.
Waandaji na waratibu wa Kongamano la Tisa la Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (waliosimama nyuma) wakiwa katika picha ya pamoja na meza kuu baada ya kufungwa kwa Kongamano hilo katika ukumbi wa mikutano wa DCC, Jijini Dodoma.


Na Josephine Majura, WFM, Dodoma


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Susana Mkapa, ameiagiza Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi nchini (PSPTB), kuhakikisha kuwa inadhibiti maadili ya wafanyakazi wa sekta ya ununuzi na ugavi ili fedha za serikali zinazotumika kwenye ununuzi ziwe na tija kwa wananchi.

Bi. Mkapa ametoa maagizo hayo Jijini Dodoma, katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Kaimu Naibu Katibu Mkuu ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mipango wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Richard Mkumbo, wakati akifunga kongamano la tisa la wataalam wa ununuzi na ugavi kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara.

Bw. Mkumbo amebainisha kuwa licha ya vitengo vya matumizi mabaya ya fedha za umma kupitia sekta ya ununuzi na ugavi, ikiwemo rushwa kuendelea kupungua, Bodi inatakiwa kuhakikisha kuwa vitendo vya rushwa vinadhibitiwa ipasavyo.

Amesema asilimia 75 ya fedha za umma zinatumika kupitia mchakato wa manunuzi ambao taarifa ya mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za serikali (CAG) na Mamlaka ya Ununuzi nchini PPRA, umebaini kuwepo kwa viashiria vya rushwa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya wananchi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi, Sister Dkt. Hellen Bandiho, amesema kuwa Bodi yake itahakikisha inasimamia kikamilifu maadili ya watumishi wa sekta ya ununuzi ili iweze kushiriki katika kukuza uchumi wa viwanda.

Kongamano hilo limewashirikisha wataalam wa ununuzi na ugavi wapatao 650 kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara

KWA MARA YA KWANZA TANZANIA YAPATA MADAKTARI BINGWA WA UPASUAJI UBONGO,MGONGO NA MISHIPA YA FAHAMU

0
0


Viewing all 46200 articles
Browse latest View live




Latest Images