Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1744 | 1745 | (Page 1746) | 1747 | 1748 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania PLC, Jacquiline Materu (wa pili kushoto) akimkabidhi zawadi ya simu mpya ya Tecno Camon 11Pro, kwa mhamasishaji wa Tecno Abdallah Sultan 'Dullivan' wakati wa uzinduzi wa simu hiyo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Simu hiyo itauzwa katika maduka ya Vodacom kwa kiasi cha TSh. 400,000. Kushoto ni Meneja wa Maduka ya rejareja ya Vodacom, Happiness Macha na  Meneja Uhusiano wa Tecno Erick Mkomoya kulia.
  Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania PLC, Jacquiline Materu (katikati) akiwaonesha waandishi wa habari ( hawapo pichani) simu mpya ya Tecno Camon 11pro wakati wa uzinduzi wa simu hizo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Simu hiyo itauzwa katika maduka ya Vodacom kwa kiasi cha TSh. 400,000. Kushoto ni Meneja wa Maduka ya rejareja ya Vodacom, Happiness Macha na Meneja Uhusiano wa Tecno Erick Mkomoya.
  Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania PLC, Jacquiline Materu (wa pili kushoto) akimkabidhi mpiga picha wa ITV Goodluck Maruti (kulia) zawadi ya simu mpya ya Tecno Camon 11pro, mara baada ya kuibuka mshindi wakati wa uzinduzi wa simu hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam. Simu hizo zitakazouzwa katika maduka ya Vodacom kwa kiasi cha TSh. 400,000 tu. Kushoto ni Meneja wa Maduka ya rejareja ya Vodacom, Happiness Macha na Meneja Uhusiano wa Tecno Erick Mkomoya.  Vodacom, kampuni nambari moja ya mawasiliano ya simu nchini imeungana na kampuni ya Tecno kuwaletea wateja wao toleo jipya la simu aina ya Tecno Camon 11, leo jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huu ni harakati ya Vodacom kuhakikisha jitihada zake za kuwezesha maisha ya kidijitali kwa wateja wao, kwa kupitia simu janja zinafanikiwa. 

  Akizungumza na waandishi wakati wa uzinduzi wa simu hiyo, Meneja Uhusiano wa kampuni ya TECNO Bw. Eric Mkomoya alisema, “Tumedhamiria kuhakikisha kila Mtanzania anamiliki simu janja na kwa pamoja tunalifanya taifa la Tanzania kuwa la kidigitali”. Uzinduzi huu uliohudhuriwa na wateja lukuki utawawezesha watumiaji wa matoleo ya awali wa simu za TECNO Camon kuweza kubadili simu zao ili kujipatia toleo hili jipya kwa kuongeza kiasi kidogo cha pesa. 

  Simu hii inapatikana kwa bei ya shilingi laki nne tu (Sh. 400,000) na inakuja na Intaneti ya GB 15 ambapo mteja anapata GB tano kwa miezi mitatu mfululizo. TECNO Camon 11 ina kamera ya mbele yenye uwezo wa mega pixel 16 na kamera mbili za nyuma yenye uwezo wa mega pixel 13 na 2 kwa picha bora zaidi. Simu hii pia ina uwezo wa 4G LTE pamoja na uwezo wa kuhifadhi laini mbili za simu.

  Pamoja na hayo, simu hii ina flashi iliyotengenezwa kwa rangi maalumu kuweza kusaidia mwanga kutoka vizuri huku ikiwa na kioo chenye ukubwa wa inchi 6.2 chenye uwezo wa FHD. Maduka yote ya TECNO yatatoa si huduma za TECNO tu bali pia kusajili laini za Vodacom. 

  “Tunafuraha kushirikiana na TECNO kuendelea kuimarisha zaidi azimio letu la kuzidi kuwawezesha wateja wetu kuwa katika ulimwengu wa kidijitali. Uzinduzi huu umekuja katika kipindi muafaka, hasa kwakuwa Watanzania wengi zaidi wanatumia huduma za simu janja” alisema Jacquiline Materu, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania. 

  Katika zama hizi za kidigitali, kupata taarifa, kununua na kulipia vitu, na kupata burudani za muziki na sinema, vinawezekana kwa kutumia simu janja, na toleo hili jipya kutoka TECNO litawezesha hayo yote na zaidi. “Uzinduzi huu umekuja sambamba na msimu wa sikukuu ili kuhakikisha wateja wetu, ambao ndiyo kipaumbele chetu wanasherehekea msimu huu kidigitali zaidi” aliongeza Materu. 

   Kwa sasa, wateja wote wenye matoleo ya zamani ya TECNO Camon wanaweza kutembelea maduka ya Vodacom na TECNO jijini Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na mikoa mingine saba nchini ili kubadilisha simu hizo na kupata simu mpya ya TECNO Camon 11. “Nimefurahi sana kupata simu hii, nimebadilisha simu yangu ya TECNO Camon CX na sasa nitasheherekea mwezi wa Disemba na marafiki zangu tukifurahia picha na kumbukumbu bila wasiwasi wa ubora wake. Ninawashukuru sana TECNO na mtandao wangu wa Vodacom.” Alisema Hawa

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa China Nchini, Mhe. Wang Ke wakati alipowasili kwenye Hoteli ya Hayyat Regency jijini Dar es salaam, Kutoa Tuzo za Mashindano ya TEHAMA ya HUAWEI, Desemba 5, 2018.  Wapili kushoto ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa  Joyce Ndalichako   na kulia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitia saini katika bango wakati alipowasili kwenye hoteli ya Hayyat Regency jijini Dar es salaam kutoa Tuzo za Mashindano ya TEHAMA ya HUAWEI, Desemba 5, 2018.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi walioshiriki katika sherehe za Utoaji Tuzo za Mashindano ya TEHAMA ya HUAWEI kwenye hoteli ya Hayyat Regency jijini Dar es salaam, Desemba 5, 2018. Kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi, Atashasta Nditiye, Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako, Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya HUAWEI nchini, Frank Zhou na  Balozi wa China nchini, Mhe. Wang Ke.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Tuzo Mshindi wa Kwanza wa Mashindano ya TEHAMA ya HUAWEI, Emmanuel  Chaula wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam katika sherehe za kukabidhi Tuzo hizo kwenye hoteli ya Hayyat Regency jijini Dar es salaam, Desemba 5, 2018.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipokabidhi Tuzo za Mashindano ya TEHAMA ya HUAWEI kwenye hoteli ya Hayyat Regency jijini Dar es salaam, Desemba 5, 2018.
     Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Viongozi wa Kitaifa na Kimataifa wakiwa katika picha ya pamoja na washindi wa Mashindano ya TEHAMA ya HUAWEI baada ya kuwakabidhi tuzo za ushindi washindi hao kwenye hoteli ya Hayyat Regency jijini Dar es salaam, Desemba 5, 2018.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Balozi wa China nchini, Mhe. Wang Ke (wapili kulia) na Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako wakati alipotoka kwenye ukumbi wa hoteli ya Hayyat Regency jijini Dar es salaam baada ya kutoa Tuzo kwa washindi wa Mashindano ya TEHAMA ya HUAWEI, Desemba 5, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

   Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Theobald Sabi, wakati alipomtembelea ofisini kwake Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es salaam leo 05/12/2018, kwa lengo la kuendelea kujenga ushirikiano baina ya benki hiyo na Jeshi la Polisi. Picha na Jeshi la Polisi.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Theobald Sabi, pamoja na watendaji wengine wa benki hiyo wakati walipomtembelea ofisini kwake Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es salaam leo 05/12/2018, kwa lengo la kuendelea kujenga ushirikiano baina ya benki hiyo na Jeshi la Polisi. Picha na Jeshi la Polisi.
  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mhe.Ali Hassan Mwinyi alipomtembelea kumjulia hali  Jijini Dar es Salaam.Disemba 5, 2018.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakiomba Dua Maalumu na Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mhe.Ali Hassan Mwinyi, Bi. Sitti Mwinyi (Mke wa Mzee Mwinyi) pamoja na Abdallah Mwinyi (Mtoto wa Mzee Mwinyi) alipomtembelea kumjulia hali Jijini Dar es Salaam.Disemba 5, 2018.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mhe.Ali Hassan Mwinyi alipomtembelea kumjulia hali  Jijini Dar es Salaam.Disemba 5, 2018.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Bi Sitti Mwinyi Mke wa Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mhe.Ali Hassan Mwinyi alipomtembelea kumjulia hali  Rais Mstaafu Jijini Dar es Salaam.Disemba 5, 2018.PICHA NA IKULU.

  0 0

  Na George Binagi-GB Pazzo, BMG.

  Chama cha Watoa Huduma za Afya Binafsi Tanzania (APHFTA), leo kimekabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya Tsh. Milioni 19 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Geita lengo likiwa ni kuboresha huduma ya upimaji Malaria kwa wananchi.

  Mkurugenzi wa Miradi APHFTA, Elizabeth Bonareri amesema vifaa hivyo ni pamoja na "Microscope" na kwamba chama hicho pia kimetenga Tsh. Milioni 30 kwa ajili ya kufanya ukarabati wa jengo la maabara ya Hospitali hiyo.

  Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Geita, Mhandisi Robert Gabriel, Katibu Tawala Msaidizi, Herman Matemu amesema vifaa hivyo vitasaidia utoaji wa huduma bora kwa wananchi na hivyo kuomba vitumike kwa malengo yaliyokusudiwa.

  Mganga Mkuu mkoani Geita, Dkt. Japhet Simeo amesema juhudi mbalimbali ikiwemo kunyunyizia dawa ya ukoko majumbani, elimu sahihi kuhusu matumizi ya vyandarua vyenye dawa, utunzaji mazingira/ kufyekya nyasi na kufukia madimbwi pamoja na kuwahimiza wananchi kuwahi katika vipimo zimekuwa zikifanyika katika kupambana na ugonjwa wa Malaria ambapo pia ameishukru taasisi ya APHFTA kwa namna inavyoshirikiana na Serikali kupambana na ugonjwa huo.

  Taasisi ya APHFTA kwa kushirikiana na kampuni ya Afya Micro-Finance kwa ufadhili wa wadau wa maendeleo "Comic Relief" inatekeleza mradi wa kupambana na Malaria mkoani Geita ambapo juhudi hizo zimesaidia kiwango cha maambukizi kupungua kutoka asilimia 38.1 mwaka 2015/16 hadi kufikia asilimia 17 mwaka 2017/18.
  Baadhi ya mashine (Microscopes) zilizotolewa na taasisi ya APHFA ili kusaidia huduma ya upimaji Malaria katika Hospitali ya Rufa ya Mkoa Geita.
  Mkurugenzi wa Miradi taasisi ya APHFTA, Elizabeth Bonareri (kushoto), akimkabidhi Katibu Tawala Msaidizi Mkoa Geita, Herman Matemu (kulia) printa kwa ajili ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo. Mashine hiyo ni miongoni mwa vifaa tiba vilivyotolewa na taasisi ya APHFTA kuboresha huduma hospitalini hapo.
   Katibu Tawala Msaidizi Mkoa Geita, Herman Matemu (katikati) akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Geita Mhandisi Robert Gabriel (hayuko pichani) baada ya kupokea vifaa tiba kutoka taasisi ya APHFA

  0 0

  Wagonjwa 54 wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo wamefanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua na bila kufungua kifua katika kambi maalum ya matibabu inayofanyika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).

  Matibabu hayo yanafanywa na madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete kwa kushirikiana na madaktari wa mradi wa Little Heart wa nchini Saud Arabia ambao ni moja ya mradi wa Afya ulioko ndani ya Taasisi ya Msaada ya Muntada yenye makao makuu yake mjini London nchini Uingereza.

  Upasuaji huo umefanyika kwa watoto 52 na watu wazima wawili wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo ambayo ni matundu na valvu .

  Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salam Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo kwa watoto kutoka JKCI Godwin Sharau alisema kwa upande wa upasuaji wa kufungua kifua wamefanya upasuaji kwa watoto 19 kwa kurekebisha valvu, kuziba matundu, kurekebisha mishipa ya moyo ambayo imekaa vibaya na kurekebisha mfumo wa uzungukaji wa damu katika moyo.

  Dkt. Sharau alisema watoto waliowafanyiwa upasuaji wanaendelea vizuri na wengine wameshatoka katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) na kupelekwa wodini kwa ajili ya kuendelea na matibabu ikiwa ni pamoja na kuanza mazoezi.

  Kwa upande wake Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto Godfrey Mbawala alisema wamefanya upasuaji wa bila kufungua kifua kupitia tundu dogo linalotobolewa katika mshiba mkubwa wa damu uliopo kwenye paja kwa wagonjwa 35 kati ya hawa watoto 33 na watu wazima wawili.

  Dkt. Mbawala alisema watu wazima waliowafanyia upasuaji wanaumri wa miaka 31 lakini matatizo ya moyo waliyokuwa nayo ni ya kuzaliwa nayo ambapo mmoja mshipa wake mkubwa wa moyo ulikuwa umebana na kushindwa kupitisha damu vizuri na mmoja alikuwa na tundu ambalo wameliziba.

  “Tunaendelea na matibabu kwa wagonjwa, hadi sasa kwa mgonjwa tuliyemfanyia upasuaji mwenye umri mdogo ni miezi sita na umri mkubwa ni miaka 31. Ninawasihi wazazi wenye watoto wenye matataizo ya moyo wasikate tama kwani magonjwa ya moyo yanatibika”, alisema Dkt. Mbawala.

  Naye Abubakari Matitu mwenye umri wa miaka 31 ambaye ni mkazi wa Kisarawe alisema alianza kuhisi kuwa na matatizo mwaka 2015 akiwa na umri wa miaka 28 akaamua kwenda kufanyiwa vipimo na mara baada ya kufanyiwa vipimo aligundulika kuwa na tatizo la tundu katika moyo na mshipa mkubwa wa damu unaotoa damu kwenye moyo na kupeleka mwilini haukuwa unapitisha damu vizuri.

  “Nilianza kliniki katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete mwaka 2015, mwezi huu siku ya Ijumaa nililazwa na kufanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua siku ya Jumatatu. Namshukuru Mungu baada ya kufanyiwa upasuaji najisikia hali ya tofauti ukilinganisha na nilivyokuwa mwanzo”.

  “Ninawashauri watanzania wenzangu wakipata matatatizo wafanye utaratibu wa kufikia katika hospitali kubwa kwa ajili ya kupatiwa huduma. Mimi nimetibiwa, kabla ya matibabu niliambiwa damu ilikuwa inashuka kwa tabu katika miguu baada ya matibabu ninasikia kabisa damu inashuka miguuni”, alisema Matitu ambaye kitaaluma ni Afisa Muuguzi.

  Jumla ya watoto 80 wanatarajiwa kutibiwa katika kambi hiyo ya siku nane iliyoanza tarehe moja na itamalizika tarehe nane mwezi huu .

  0 0


  Na. Paschal Dotto-MAELEZO

  Tanzania imeendela kuweka rekodi ya kuvutia wawekezaji kwa nchi zilizopo ukanda wa Afrika Mashariki kwa kuwa na mtaji wa uwekezaji wa Dola Bilioni 1.18, ikifuatiwa na Uganda wenye uwekezaji wa dola za kimarekani 700

  Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji (TIC) Godffrey Mwambe amesema nchi ya Kenya inashika nafasi ya Tatu wakiwa na uwekezaji wa dola za kimarekani 670 na hivyo kuiweka Tanzania kuwa juu ya nchini zingine Afrika Mashariki.

  Mwambe amesema kuwa Tanzania inaongoza kuvutia wawekezaji kutokana na mapinduzi makubwa yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano ambapo hadi sasa imewekeza jumla ya miradi mipya 905 katika sekta mbalimbali nchini miradi ambayo itatengeneza ajira 115,055 kwa watanzania na kuleta tija na manufaa kwa taifa

  Alisema kuwa katika kipindi hiki cha miaka mitatu TIC imeweza kuvutia wawekezaji na kuweza kuandikisha, mfano kuanzishwa kwa viwanda mbalimbali ambavyo vimeweza kuongeza pato la Taifa.

  Akifafanua zaidi anasema kuwa baadhi ya miradi mikubwa zaidi iliyowekezwa nchini ni pamoja na ikiwemo kiwanda cha Goodwill Ceremics Ltd kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani kinachojihusisha na utegenezaji vigae na kimewekeza jumla ya dola za kimarekani milioni 53, huku kikitoa ajira za moja kwa moja 1500 kwa watanzania na ajira zisizo za moja kwa moja 3,000.

  “Viwanda vingine ambavyo vimeiwezesha Tanzania kuwa kinara wa kuvutia wawekezaji ni KEDA (Twyford) Tanzania ceramic Ltd pia ni cha kutengeneza marumaru na hiki ni kikubwa zaidi kina mtaji wa Dola za kimarekani milioni 56, kimetoa ajira za moja kwa moja zipatazo 2,000 kwa watanzania na ajira zisizo za moja kwa moja 4,000” alisema.

  Anavitaja Viwanda vingine kuwa ni Sayona Friut Ltd yenye mtaji wa milioni 55, KEDS(T) Co.Limited mtaji wa dola milioni 11.8 pamoja na kiwanda cha nondo cha Kiluwa Steel Group ambacho ni kikubwa kwa ukanda wa afrika mashariki kina mtaji wa dola milioni 130 na kinazalisha jumla ya tani 200 za nondo.

  Aidha Mwambe alieeleza nchi zinazoongoza kwa kuwekeza nchini Tanzania ni pamoja na Jamhuri ya Watu wa China, Uingereza na Marekani.

  “Maendeleo ya China yaliyopatikana kwa miaka 40 kwa watanzania wote ni funzo kubwa la kuwa na uzalendo, China ndiyo inaongoza kuwa kuwekeza nchini tangu miaka ya 1990, na kwa sasa ina miradi ya uwekezaji 723”, Mwambe Mkurugenzi Mkuu, TIC.

  Alibainisha utaoji huduma, Mwambe anasema TIC imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika utoaji huduma kwa wateja ndani na nje ya nchi kwani kwa sasa huduma zote zinazomuhusu mwekezaji zinapatika TIC kupitia mfumo wa ‘Huduma za mahala pamoja’ ambapo huduma hii imeongeza wawekezaji kwa kuvutiwa zaidi na kuwezesha Tanzania kuwa kinara katika nchni za Afrika Mashariki.

  “Tumefanikiwa kuongeza Taasisi ambazo hazikuwepo katika huduma za mahala pamoja ndiyo maana tuliwatafuta kwenye maofisi yao na kuwaleta hapo katika Taasisi kama NIDA, OSHA,NEMC, TBS, TFDA pamoja na TANESCO , hawa wamekuja kuimarisha na kuondoa usumbufu kwa wawekezaji na sasa tunaongelea jambo la kuwa kinara wa kuvutia wawekezaji Afrika Mashariki” Mwambe.


   Mkurugenzi  Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji (TIC) Godffrey Mwambe akisisitiza  jambo kwa Waandishi wa Habari  (Hawapo  pichani), wakati wa mkutano wake na Waandishi wa Habari  kueleza mafanikio ya TIC ndani ya Miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Tano, Mkutano ulifanyika leo Disemba 5, 2018 katika ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO  Jijini Dar es Salaam. 
  : Waandishi wa Habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa TIC,Godffrey Mwambe (Kushoto) wakati wa Mkutano wake kueleza mafanikio ya TIC ndani miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Tano, Mkutano ulifanyika leo katika ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO Jijini Dar es Salaam.
  (Picha na MAELEZO).


  0 0

  Na Editha Shija, Tabora

  MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega mkoani Tabora Kiwele Michael Bundala ametoa onyoa kali kwa watendaji wa Vijiji na Kata watakaobainika kutafuna fedha za mapato wanayokusanya kutoka katika vyanzo mbalimbali katika halmashauri hiyo.

  Ametoa onyo hilo jana wilayani hapa baada ya kutoridhishwa na utendaji wa baadhi ya watumishi wa halmashauri hiyo kutowasilisha fedha za mapato kwa wakati ambapo amesema halmashauri inakusanya fedha nyingi kutoka katika vyanzo vyake mbalimbali lakini nyingi zinaingia mifukoni mwa baadhi ya watu.

  Pia amesisitiza kuwa watendaji wote wanapaswa kuhakikisha fedha zote zinakusanywa katika maeneo yao na kuletwa kama zilivyo na kwamba kuanzia sasa Mtendaji yeyote atakayebainika kutafuna fedha za mapato au kujihusisha na vitendo vya rushwa atachukuliwa hatua za kinidhamu pamoja na kutimuliwa mara moja.

  Amewasisitiza 'kuwa waadilifu na kutekeleza majukumu yao kwa kufuata kanuni,taratibu,na sheria huku akionya kuwa Serikali haina fedha za kuhamisha mtumishi mzembe anayeshindwa kutekeleza majukumu yake. Hata hivyo Mwenyekiti huyo amewataka madiwani wa kata zote kufuatilia kwa ukaribu watendaji wao na kuhakilisha fedha zote zinazokusanywa na kuwasilishwa ipasavyo.
   

  0 0


  0 0

   Mheshimiwa Aweso Naibu Waziri wa Maji akisalimiana na wakazi wa
  Likwaya Lindi Vijijini.
  BC207579-A0D8-471A-877B-DE869128926C-min
  Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akikagua ujenzi wa kilua cha
  kuchotea maji Nangumbu Ruangwa
  A1F6C4C2-1510-4288-AF36-D1F2C832CE03-min
  Naibu Waziri wa Maji Mheshimiwa Jumaa Aweso akiongea na wananchi wa
  Rutamba Lindi Vijijini.
  64ED4CD2-83B6-4BB0-82A6-8A9782517536-min
  Naibu Waziri wa Maji akifungua koki ya maji kujiridhisha kama mradi
  unafanya kazi Rutamba.
  ………………….
  Naibu Waziri wa Maji leo ameendelea na ziara yake ya kikazi Mkoani
  Lindi kwa kutembelea miradi ya maji ya Likwaya, Rutamba na Namangale
  iliopo Halmashauri ya Lindi vijijini.

  Pia aliongea na wananchi na kuwasikiliza kero zao zinazohusu sekta ya maji.
  Aidha, Mheshimiwa Aweso alitembelea miradi ya Nangumbu na Michenga
  iliopo Wilayani Ruangwa na kutoa maagizo.

  Katika ziara hizo Naibu Waziri alionesha kutoridhishwa na mwenendo wa
  jumuiya zinazosimamia miradi ya maji na kulazimika kuivunja jumuiya ya
  watumia maji ya Rutamba baada ya kutoridhishwa na utendaji kazi wao.

  0 0
  Wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya Kiserikali (NGOs) wametakiwa kutekeleza Kanuni Mpya za Sheria namba 24 ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya Mwaka 2002 ikiwa ni lengo la kuwa na uelewa wa pamoja katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika misingi ya uwazi na uwajibikaji.

  Hayo yamebainika jijini Dodoma wakati wa mahojiano kati ya waandishi wa habari na Mkurugenzi Msaidizi Usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Baraka Leornard wakati wa kikao baina ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini wanaotekeleza Sera zinazosimamiwa na Wizara.

  Bw. Baraka ameongeza wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wamepitishwa katika Kanuni mpya ili kuwa na uwelewa wa kutosha katika utekelezaji wa Kanuni za utendaji wa mashirika hayo kwa ajili ya kutambua nini kinatakiwa kufanya na nini hakitakiwi kufanyika ili kuepuka kukinzana na Sheria, Kanuni na taratibu husika.

  Amesisitiza kuwa mara baada ya kikao hicho Wadau watakuwa na uelewa mkubwa wa Kanuni hizo ambao utawasaidia kuweza kutekeleza wajibu wao bila kukiuka Kanuni zozote ambazo zinaenda na Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya Mwaka 2002.

  “Bado tunasisitiza uwazi na uwajibikaji kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika utoaji wa Taarifa za fedha na miradi wanayotekeleza ili kuona miradi inayoanzishwa inanufaisha wananchi zaidi ambao ndio walengwa wakuu” alisema Bw. Baraka

  Kwa upande wake Msajili na Mkurugenzi wa Idara ya Usajili na Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bi. Neema Mwanga amesema kuwa Kikao hicho baina ya Wizara na Serikali kitasaidia kuweka Mipango ya pamoja katika kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo ikianisha mchango wa Serikali na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika ngazi ya Taifa, Mkoa na jamii.

  Msajili huyo ameongeza kuwa Mada mbalimbali zimetolewa katika kikao hicho ikiwemo kutoka Idara ya Uhamiaji ambao wameelimisha kuhusu utoaji wa vibali vya wafanyakazi wa kigeni ambapo wafanyakazi wengi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wanatoka nje ya nchi hivyo kutakiwa kupata vibali vya kufanya kazi ndani ya nchi.

  Amezitaja mada nyingine zilizotolewa kuwa ni Haki na Ustawi wa Watoto, Jinsia na Maada kutoka Shirika la Wil-Daf waliobainisha yaliyojiri katika Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga Ukatili wa kijinsia kwa mwak 2018, na mada nyingine mbalimbali zilizotolewa na wadau kwa lengo la kuwa na uelewa wa pamoja katikapata uzoefu na uelewa wa afua mbalimbali zinazoweza kutekelezwa kwa pamoja.

  Naye Mratibu Msaidizi wa kutoka Idara ya Uhamiaji mkoa wa Dodoma Azia Mlawa ameyasisitiza Mashirika Yasiyo ya Kiseriklai ambayo yanachukua wafanyakazi kutoka nje ya Tanzania kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu za kuomba vibali vya kufanya kazi kwa wafanyakazi wao ili kuondokana na usumbufu utakaojitokeza kwa wafanyakazi na Shirika husika bila kufuata utaratibu.

  Aidha Katibu Mkuu wa Shirika la Dawa Asilia na ulinzi wa Mazingira Bw. Boventure Mwalongo amesema kuwa wadau wanaendelea kushirkiana na Serikali katika kutekeleza miradi mbalimbali na wamepokea maelekezo ya Wizara na watayatekeleza ili kuleta uwazi na uwajibikaji ambao ni nguzo pekee kati ya pande zote mbili yaani Serikali na Mahrika Yasiyo ya Kiserikali katika kutimiza majukumu yao.

  Msajili na Mkurugenzi wa Idara ya Usajili na Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bi. Neema Mwanga (katikati) akizungumza na wadau kutoka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakati wa kikao baina ya Wizara na wadau hao wanaotekeleza Sera zilizo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kilichofanyika jijini Dodoma kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Baraka Leornard na Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali BI. Tausi Mwilima. 
  Wadau kutoka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa wakati wa kikao baina ya Wizara na wadau hao wanaotekeleza Sera zilizo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kilichofanyika jijini Dodoma. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW 

  0 0

  NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA .

  WAKULIMA wa zao la korosho wilayani Kibaha mkoani Pwani ,wamesema maamuzi ya serikali chini ya Rais Dk John Magufuli kununua korosho ni mkombozi kwao. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mwenyekiti wa umoja wa vyama vya ushirika wa zao la korosho wilaya ya Kibaha (UVUKI) Adhu Mkomambo alisema ,hatua hiyo itasaidia kuondoa ubabaishaji wa malipo uliokuwepo kipindi cha nyuma. 

  Alifafanua, maamuzi hayo ni faida kubwa kwa wakulima kwani bei elekezi ni nzuri ya shilingi 3,300 kwa daraja la kwanza ambapo wafanyabiashara walisema watanunua kwa shilingi 2,700 hali ambayo ilikuwa ni mbaya. “Manufaa ya maamuzi haya ni kunufaisha wakulima ambao wamekuwa wakitaabika kwa muda mrefu ambapo wafanyabiashara walikuwa wanaangalia maslahi yao binafsi,” 

  “Hatuna cha kumlipa mh Rais, ila tunamuombea azidi kutetea wanyonge “alisema Mkomambo. Nae mwenyekiti wa chama cha ushirika Kongowe Amcos Deo Joseph alisema, maamuzi hayo yataondoa usumbufu mkubwa waliokuwa wanapata wakulima katika malipo Mara wanapopeleka korosho kwenye minada. 

  Mzee Mwinshehe ambaye ni mwenyekiti wa chama cha ushirika Misugusugu Amcos alieleza, wakulima tegemeo lao ni korosho hivyo kuwalipa fedha ndogo ni kuwakwamisha kimaisha kwani wanategemea zao hilo kusomesha na shughuli nyingine za maendeleo na bei elekezi itapunguza gharama za pembejeo.
   

  0 0


  Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel akiwasilisha mada kwa Maafisa Ununuzi na Ugavi (hawapo pichani) katika kongamano la Tisa la mwaka la maafisa hao.
  Baadhi ya Maafisa Ununuzi na Ugavi wakisikiliza mada iliyokuwa ikiwasilishwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel (hayupo pichani)
  Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel akisikiliza kwa makini michango mbalimbali iliyokuwa ikitolewa na Maafisa Ununuzi na Ugavi (hawapo pichani), mara baada ya kuwasilisha mada kwa maafisa hao juu ya uvumbuzi na ufanisi bora katika masuala ya ugavi.


  Na. Edward Kondela

  Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel amewataka Maafisa Ununuzi na Ugavi nchini kutambua na kuthamini miradi mbalimbali inayofanywa na serikali, kwa kuthaminisha miradi hiyo na thamani halisi ya fedha inayotumika katika miradi.

  Prof. Gabriel aliyasema hayo leo (05.12.2018) Jijini Dodoma, wakati akiwasilisha mada kuhusu uvumbuzi na ufanisi bora kwa Maafisa Ununuzi na Ugavi kutoka maeneo mbalimbali nchini, wakati wa siku ya ufunguzi wa kongamano la Tisa la mwaka la maafisa hao.

  “Katika ujenzi wa miradi mikubwa tunayoishuhudia kwa sasa nchini, fedha zinatumika, lakini jinsi gani sasa vifaa vinanunuliwa, malighafi zinanunuliwa ni jambo kubwa sana, kuna haja ya wahusika katika tasnia hii wawe wabunifu kadri iwezekanavyo na wawe ni watu wa kuleta mabadiliko”. Alisema Prof. Gabriel.

  Katibu mkuu huyo aliwataka maafisa hao kuwa wavumbuzi na kufanya kazi kwa ufanisi katika masuala ya ugavi na usambazaji bidhaa ili kuisaidia serikali, kupata thamani halisi ya fedha zinazotumika kujenga miradi mbalimbali ili iwe na tija kwa taifa.

  Aidha, Prof. Gabriel aliwataka Maafisa Ununuzi na Ugavi, kubadili mienendo yao ambayo haiwaletei tija katika ufanisi wa kazi, pamoja na kujiongezea thamani katika jamii kwa kufanya kazi kwa ufanisi ili waweze kuleta matokeo chanya kwa jamii na taifa kwa ujumla.

  0 0

  NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA 

  MKUU wa wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama amesema ataandika ombi la kufuta hati ya shamba la mmiliki Siemens, lililopo kata ya Pangani, kutokana na kuwa pori na kugeuzwa jalala la kutupwa miili ya marehemu pamoja na kutumika kwa uhalifu. 

  Hatua hiyo inakwenda pamoja na kuwakabidhi wananchi kulitumia kwa masharti ya kulima mazao ya muda mfupi wakati serikali ikiendelea na taratibu za kupima viwanja na kuuza kwa gharama nafuu. 

  Akitoa maamuzi hayo wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa kata hiyo, Assumpter alisema ifikie mwisho kujaza viwanja na mashamba pori wilayani hapo. Assumpter alitoa rai kwa wamiliki wenye mashamba na viwanja pori kuanza kuyaendeleza na kama watakaidi wananchi wakiyavamia ataruhusu wagawiane maeneo. 

  "Hii ni salamu tuu, mwenzio akinyolewa wewe anza kutia maji, wananchi wamechoshwa kulinda maeneo ya watu, kama mmeyashindwa yaacheni"alifafanua Assumpter. Awali diwani wa kata ya Pangani, Agustino Mdachi aliomba serikali ,kuangalia namna ya kufuta umiliki wa mashamba ambayo hayaendelezwi na kusababisha kutumika vificho vya wahalifu .

  Alisema, kwa kipindi cha miezi sita miili zaidi ya kumi zimeokotwa kwenye mtaa huo ambapo kati yao wengine walinusurika kifo na kuokolewa na wengine wakiwa wamefariki dunia. Nae mwenyekiti wa mtaa wa Pangani Jitihada Ndiali alisema maeneo hayo yamegeuzwa dampo au sehemu ya kutupia maiti pia madereva bodaboda kuporwa pikipiki zao kisha kutupwa .

  Kwa upande wa wananchi akiwemo Lillian Godfrey alimpongeza mkuu wa wilaya kwa maamuzi yake. Alisema, wamekubali kulima mazao ya muda kama mihogo, mbaazi, maharage na mbogamboga hadi hapo serikali itakapofanya maamuzi ya moja kwa moja.

  0 0


  Kesi ikiendeshwa kwa njia ya Mtandao- ‘Video Conferencing’ kwa mara ya kwanza katika kituo cha Mafunzo cha Mahakama ya Tanzania kilichopo Kisutu jijini Dar es salaam. Kulia pichani ni Shahidi namba tatu , Stela Janot akitoa ushahidi wake akiwa nchini Ufaransa.
  Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Biashara Mhe.Lugano Mwandambo akiendesha kesi kwa njia ya Mtandao ‘Video Conferencing’ aliyekaa mezani (katikati amevaa tai )katika Kituo cha Mafunzo cha Kisutu. Kushoto ni Makarani wa Mahakama Martha Cosmas na Fortunata Barnabas.  Na Magreth Kinabo-Mahakama ya Tanzania

  Mahakama ya Tanzania kwa mara ya kwanza imeanza kuendesha kesi kwa kutumia mfumo wa Mawasiliano kwa njia ya picha za video yaani ‘Video Conferencing’ kwa kutumia vitendea kazi vyake yenyewe kwa kumsikiliza shahidi akiwa nchini Ufaransa.

  Kesi hiyo imesikilizwa leo katika kituo cha Mafunzo cha Mahakama ya Tanzania kilichopo Kisutu jijini Dar es Salam na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Biashara Mhe. Lugano Mwandambo. Hatua ya kuanza kusikilizwa kwa kesi kupitia mfumo huu ni hatua ya mafanikio katika Maboresho ya Utoaji wa Huduma za Mahakama kwa wakati na kwa viwango kumfikia mteja.

  Kesi hiyo ya madai namba 6 ya mwaka 2017 iliyosikilizwa kwa njia picha za video inayohusu mdai ambaye ni kampuni ya Sogea Saton anayeidai zaidi ya shilingi bilioni 3.8 Bank of Africa. Aidha kupitia mfumo huo wa Video Conferencing, shahidi huyo aliweza kutoa ushahidi wake mbele ya Jaji na Mawakili wa upande wa mdai ambao walikuwa ni Dilip Kesaria na Veronika Mwanajengwa, wakati mawakili wa upande wa utetezi walikuwa ni Peter Swai na Rosan Mwambo. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 2, mwakani.

  Mahakama ya Tanzania imeamua kutumia Tehama ili kurahisisha utoaji wa haki kwa wakati na pia kuokoa muda na kupunguza gharama kwa wananchi wanaofika Mahakamani kutafuta haki zao. Aidha, mfumo wa Mawasiliano kwa njia ya picha za video (Video Conferencing) ulioanza kutumiwa na Mahakama ya Tanzania katika kusikiliza mashauri Mahakamani tayari umefungwa katika Kituo cha Mafunzo cha Mahakama kilichopo Kisutu jijini Dar es Salaam na Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Mbeya.

  Mpango uliopo ni kufunga Mfumo huu kwenye Mahakama Kuu zote nchini pamoja na chuo cha Uongozi wa Mahakama kilichopo Lushoto mkoani Tanga.

  0 0


  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akizungumza na baadhi ya Wakurugenzi wa Wizara hiyo mara baada ya kutembelea eneo ambalo jengo la ofisi ya Wizara ya Maliasili na Utalii litakapojengwa ndani ya siku 30 katika mji wa kiserikali wa Ihumwa jijini Dodoma kwa kandarasi ya SUMA JKT litakalogharimu bilioni moja.

  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akipewa maelezo na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu wa Wizara hiyo, Bw. Lusius Mwenda mara baada ya kutembelea eneo ambalo jengo la ofisi ya Wizara ya Maliasili na Utalii litakapojengwa ndani ya siku 30 katika mji wa kiserikali wa Ihumwa jijini Dodoma kwa kandarasi ya SUMA JKT litakalogharimu bilioni moja.

  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akioneshwa eneo na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu wa Wizara hiyo, Bw. Lusius Mwenda mara baada ya kutembelea eneo ambalo jengo la ofisi ya Wizara ya Maliasili na Utalii litakapojengwa ndani ya siku 30 katika mji wa kiserikali wa Ihumwa jijini Dodoma kwa kandarasi ya SUMA JKT litakalogharimu bilioni moja.
  (Picha zote na Lusungu Helel

  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe .Constantine Kanyasu ametoa siku 30 kwa mkandarasi wa SUMA JKT, aliyepewa kazi ya kujenga jengo la ofisi ya wizara hiyo katika mji wa serikali eneo la Ihumwa, Jijini Dodoma, kuhakikisha jengo hilo linakamilika ndani ya siku hizo alizopewa
  Amemshauri Mkandarasi huyo kufanya kazi usiku na mchana ili aweze kukamilisha ujenzi wa jengo hilo ndani ya siku hizo 30. 

  Ametoa rai hiyo mara baada ya kutembelea eneo hilo la ujenzi wa jengo la ofisi za Wizara hiyo linalotarajiwa kugharimu shilingi bilioni moja za kitanzania katika eneo la Ihumwa jijini Dodoma. 

  Aidha, Mhe.Kanyasu ameitaka kandarasi ya SUMA JKT ihakikishe inajenga jengo hilo kwa umakini, umahiri na viwango vya ubora wa hali ya juu vinavyokwenda sambamba na hadhi ya Wizara yenye mchango mkubwa kwenye pato la Taifa.
  Pia, Mhe.Kanyasu ameielekeza SUMA JKT wakati ikiendelea na maandalizi ya ujenzi wa jengo iwe inatoa taarifa kila siku kwa kila hatua inayofikia katika Ujenzi wa jengo hilo kwa Uongozi wa Wizara. 

  Awali, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw.Lusius Mwenda amemueleza Naibu Waziri huyo kuwa eneo hilo patakapojengwa Ofisi za Wizara hiyo lina ukubwa wa Hekta 2.27 .Ameongeza kuwa hata hivyo kuna eneo ambalo Wizara ilipewa mwanzo ambapo hatua kubwa zimeshafanyika ikiwa pamoja na kulifanyia usafi eneo hilo lakini baadaye wamepewa eneo jipya ambalo tayari hatua za maandalizi tayari zinaendelea. 

  Eneo la Ihumwa katika Mji wa Dodoma ni eneo rasmi ambalo limetengwa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya serikali yakiwemo ya wizara ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ofisi za serikali kuhamia rasmi Mjini Dodoma, kutokana na agizo lililotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli wakati akiingia madarakani mwezi Novemba 2015.

  0 0


  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola, akizungumza na Wananchi wa Kata ya Nansimo, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara, leo. Lugola aliwataka Watanzania ambao hawajajiandikisha waende kujiandikisha ili waweze kupata kitambulisho cha taifa kwakuwa sio jambo la hiari bali ni lazima kwa kila Tanzania aliyeko ndani ya mipaka ya nchi kutambuliwa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (aliyemshika mtoto), akitoka mkutanoni baada ya kuzungumza na Wananchi wa Kata ya Nansimo, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara, leo. Lugola aliwataka Watanzania ambao hawajajiandikisha waende kujiandikisha ili waweze kupata kitambulisho cha taifa kwakuwa sio jambo la hiari bali ni lazima kwa kila Tanzania aliyeko ndani ya mipaka ya nchi kutambuliwa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (kushoto), akimpongeza mwanachama mpya wa CCM, Andrea Mutesigwa (kulia) ambaye amerudisha kadi ya Chadema katika Mkutano wa Wananchi wa Kata ya Nansimo, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara, leo. Katika mkutano wake na wananchi hao, Lugola aliwataka Watanzania ambao hawajajiandikisha waende kujiandikisha ili waweze kupata kitambulisho cha taifa kwakuwa sio jambo la hiari bali ni lazima kwa kila Tanzania aliyeko ndani ya mipaka ya nchi kutambuliwa. 


  Na Felix Mwagara, (MOHA), MARA. 

  WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewataka Watanzania ambao hawajajiandikisha waende kujiandikisha ili waweze kupata kitambulisho cha taifa kwakuwa sio jambo la hiari bali ni lazima kwa kila Tanzania aliyeko ndani ya mipaka ya nchi kutambuliwa. 

  Akizungumza na wananchi wa Kata ya Nansimo, Mwibara, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara, Lugola amesema katika Mkoa na mikoa mingineyo zoezi la kujiandikisha lilishakamilika ila wale ambao hawakuandikishwa kipindi kile ambacho Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wanaandikisha wananchi mitaani, wanapaswa kwenda katika ofisi Wilaya za Mamlaka hiyo ili waweze kujiandikisha. 

  “Wapo ambao kipindi kile NIDA wanaandikisha wananchi mitaani hawakuwepo hilo nalijua, na pia kuna wale ambao kipindi kile zoezi la kuandikishwa linafanyika walikua hawajafikisha miaka 18, hao wote ambao hawajaandikishwa wanapaswa sasa kwenda kujiandikisha haraka iwezekanavyo katika ofisi za NIDA katika Wilaya zao,” alisema Lugola. 

  Lugola ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara aliongeza kuwa, zoezi la vitambulisho vya utaifa ni lalazima kwa kila mtanzania aliye hapa nchini, ni kosa bwa kama wewe ni raia akaamua kukaidi ikiwa Rais Dk John Magufuli ameamua kutoa vitambulisho hivyo bure bila malipo yoyote nchini. 

  “Ndugu wananchi wa Mwibara na kote nchini, kupata kitambulisho ni jambo kubwa la nchi hivyo tusililinganishe na jambo lingine lolote na tusilichukulie kirahisirahisi tu, na ninawaambia baada ya mchakato huu kuisha tukamkuta mtu hana kitambulisho maelezo yake yatakuwa ni magumu kueleweka kama kweli yeye ni mtanzania halali,” alisema Lugola.
   
  Lugola alisema kwa Mkoa wa Mara tayari zoezi lilikamilika na kinachofanyika sasa ni Kuhakiki, kuyafanyia kazi mapingamizi pamoja na Uchakataji, likikamilika zoezi hilo kwa wale waliojiandikisha na ambao wana sifa watapewa vitambulisho vyao. 

  “Hakuna Mtanzania mwenye sifa atakayekosa kitambulisho cha taifa, lakini lazima muwe na subira wakati zoezi la utambuzi wa watu gani wanaweza kupata vitambulisho hivi, na pia katika utambuzi tunapaswa kuwa makini sana kwasababu tusije tukapenyeza wasio raia wasiostahili na wao wakaweza kupata vitambulisho na baadaye tukaja kupata shida,” alisema Lugola. 

  Aidha, Waziri Lugola aliwataka wananchi wa jimbo lake waanze maandalizi ya kilimo cha mazao ya chakula na biashara ili kuepuka janga la njaa lisije liwakumba endapo hawata lima. Hata hivyo, kijiji hicho alichokitembelea, kwa mujibu wa taarifa ya mipango yao ya kilimo walisema kuwa wana upungufu mkubwa wa mbegu za mazao mbalimbali hasa zao la pamba. 

  Lugola anaendelea na ziara yake kwa kutembelea vijiji vyote jimboni kwake Mwibara akisikiliza kero za wananchi pamoja na kuhamasisha kilimo cha mazao ya pamba, mahindi, mpunga, viazi na mengineyo ambayo wakazi wa jimbo lake wanalima mazao hayo kwa wingi.

  0 0

  Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii

  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeiahirisha kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mdogo wa mfanyabiashara maarufu nchini Rostam Aziz, Akram Aziz, kwa sababu upelelezi bado haujakamilika.

  Akram ambaye alifikishwa mahakamani hapo Oktoba 31, 2018 na kufunguliwa kesi namba 82/2018 anakabiliwa na mashitaka 75 yakiwemo ya kukutwa na nyara za Serikali, silaha, risasi na utakatishaji fedha wa dola za Marekani 9,018 ambapo Wakili wa Serikali, Mkunde Mshanga amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustino Rwizile kuwa kesi hiyo leo Desemba 6, 2018 imekuja kwa
  ajili ya kutajwa na upelelezi bado haujakamilika.

  Kutokana na taarifafa hiyo, Hakimu Rwizile ameahirisha kesi hiyo hadi Desemba 13, 2018 kwa ajili ya kutajwa.Akram anakabiliwa na mashitaka mawili ya kukutwa na nyara za Serikali, mashitaka 70 ya kukutwa na silaha, mashitaka mawili ya kukutwa na risasi zaidi ya 6,496 na moja la utakatishaji fedha.

  Inadaiwa kuwa Oktoba 30, mwaka huu mshitakiwa akiwa maeneo ya Oysterbay wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, alikutwa na nyara za Serikali ambayo ni meno sita ya tembo yenye thamani ya dola za Marekani 45,000 sawa na Sh 103, 095,000, mali ya Serikali.Pia inadaiwa Oktoba 30, mwaka huu maeneo ya Oysterbay wilayani Kinondoni mkoani humo Akram alikutwa na nyara za Serikali ambazo ni nyama ya nyati yenye uzito wa kilogramu 65, yenye thamani ya dola za Marekani 1,900 sawa na Sh 4,352,900 mali ya Serikali bila kuwa na kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapoli nchini.

  Katika mashitaka ya tatu hadi la 72, kwamba siku hiyo na eneo hilo hilo, mshitakiwa huyo alikutwa na silaha aina ya Pistol bila ya kibali cha mrajisi wa silaha.Inadaiwa katika mashitaka ya 73 kuwa, Oktoba 30, mwaka huu maeneo ya Oysterbay mshitakiwa alikutwa na risasi 4,092 na katika mashitaka mengine ilidaiwa mshitakiwa alikutwa na risasi 2,404 bila kuwa na kibali.

  Katika mashitaka ya utakatishaji fedha, inadaiwa kuwa Oktoba 30, mwaka huu maeneo hayo ya Oysterbay, Akram alitakatisha USD 9,018 huku akijua kuwa fedha hizo ni zao la kujihusisha na makosa ya uhalifu.
  Pichani kati ni Mfanyabiashara  Akram Aziz anaetuhumiwa na kesi ya uhujumu uchum

  0 0

  Na Karama Kenyunko blogu ya Jamii.
  Kesi ya uchochezi dhidi ya Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, Mbunge wa Tarime mjini, Ester Matiko  na wenzao saba inayounguruma katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepigwa kalenda hadi Desemba 21 mwaka huu.

  Aidha mahakama hiyo imetoa ruhusa kwa Mbunge wa Kawe, Halima Mdee kuendelea kuhudhuria michezo ya Afrika Mashariki nchini Burundi na pia imeruhusu Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, kumuuguza mkewe ambaye amejifungua kwa upasuaji hivi karibuni.

  Mbowe na Matiko wataendelea kukaa mahabusu kwa muda usiojulikana pengine hadi mwakani,  baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kusimamisha usikilizwaji wa rufaa iliyokatwa na washitakiwa hao kupinga maamuzi ya Mahakama ya Kisutu ya kuwafutia dhamana.

  Hatua hiyo imetokana na upande wa serikali kukata rufaa kupinga maamuzi ya Jaji Sam Rumanyika aliyesema kuwa rufaa ya kina Mbowe ipo mahakamani hapo kisheria na kwa maana hiyo, haina mamlaka ya kuendelea na usikilizwaji wa rufaa hiyo.

  Akitoa maamuzi hayo mwishoni mwa wiki iliyopita, Jaji Rumanyika alisema. DPP anapewa mamlaka ya kukata rufaa kwa uamuzi mdogo ambao haumalizi kesi chini ya kifungu cha 6 cha Sheria ya Mamlaka ya Rufaa na kwamba kunapokuwepo taarifa ya kusudio la kukata rufaa Mahakama ya Rufani, mahakama ya chini haiwezi kuendelea na shauri.

  Mapema leo,Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi amedai mbele ya Hakimu Wilbard Mashauri kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba washitakiwa Mdee na Heche hawapo mahakamani.

  Wakili wa utetezi, Peter Kibatala amedai kuwa Heche alitolewa taarifa kuhusu kufanyiwa upasuaji mdogo kwa mke wake lakini afya ya mtoto sio nzuri sana na kwa upande wa Mdee yupo nchini Burundi kushiriki mashindano ya Mabunge ya Afrika Mashariki.

  Mdhamini wa Mdee, Fares Robinson aliieleza mahakama hiyo kuwa Mdee yupo safarini kwenda Burundi kwa safari za kibunge na kwamba Katibu wa Bunge aliandika barua kwa Hakimu Mfawidhi wa mahakama kumtaarifu kuwa mshitakiwa huyo atakuwa nje kwa shughuli za kibunge na kwamba atarudi Desemba 20, mwaka huu.

  Akijibu hoja hiyo, Wakili Nchimbi alidai walipokea hati ya wito ikiambatanishwa na maombi ya ruhusa ya kupitia Mdee kupitia kwa Katibu wa Bunge.

  Alidai kwa mantiki hiyo wanaona washitakiwa wanafuata taratibu na hawana pingamizi na hilo na kuhusu Heche anayemuuguza mkewe pia hawana pingamizi ikizingatiwa shauri lilikuja kwa ajili ya kutajwa.

  Baada ya kuelezwa hayo, Hakimu Mashauri alisema kuwa walipokea barua kutoka kwa Katibu wa Bunge kuomba ruhusa ya Mdee kwenda Burundi kuhudhuria michezo ya EAC na kwamba pande zote za utetezi na mashitaka walikuwa Mahakama Kuu kwa kesi nyingine.

  "Mahakama inamruhusu mshitakiwa kuhudhuria michezo na ruhusa ya Heche ya kumuuguza mkewe imekubaliwa lakini wazingatie kuwepo mahakamani siku ya kutajwa kesi hiyo Desemba 21, mwaka huu, " alisema Hakimu Mashauri.

  Muda wrote wakati kesi hiyo inaendelea  mahakamani hapo kulikuwa na ulinzi mkali wa polisi ambapo uliwazuia baadhi ya wafuasi wa chama hicho kuingia mahakamani na badala yake waliwaruhusu viongozi wa chama hicho  pekee.

  Washitakiwa wengine ni Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Katibu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji, Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya  na Katibu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu  

  Wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 13, ikiwemo kula njama,  kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai kati ya Februari 1 na 16, 2018, Dar es Salaam.

  Mwisho
  [02:54, 12/6/2018] Karama: Na Karama Kenyunko blogu ya jamii.

  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeiahirisha kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili, mdogo wa mfanyabiashara maarufu, Rostam Aziz, Akram Aziz, kwa sababu upelelezi bado haujakamilika.

  Akram ambaye alifikishwa mahakamani hapo Oktoba 31, 2018 na kufunguliwa keai namba 82/2018 anakabiliwa na mashitaka 75 yaikiwemo ya kukutwa na nyara za serikali, silaha, risasi na utakatishaji fedha wa dola za Marekani 9,018.

  Wakili wa Serikali, Mkunde Mshanga  amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustino Rwizile, kuwa kesi hiyo leo Desemba 6.2018 imekuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi bado haujakamilika.

  Kufuatia taarifafa hiyo, Hakimu Rwizile ameahirisha kesi hiyo hadi Desemba 13, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

  Akram  anakabiliwa na mashitaka mawili ya kukutwa na nyara za serikali, mashitaka 70 ya kukutwa na silaha, mashitaka mawili ya kukutwa na risasi zaidi ya 6,496 na moja la utakatishaji fedha.

  Inadaiwa  kuwa Oktoba 30, mwaka huu mshitakiwa akiwa maeneo ya Oysterbay wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, alikutwa na nyara za serikali ambayo ni meno sita ya tembo yenye thamani ya dola za Marekani 45,000 sawa na Sh 103, 095,000, mali ya serikali.

  Pia inadaiwa Oktoba 30, mwaka huu maeneo ya Oysterbay wilayani Kinondoni, mkoani humo Akram alikutwa na nyara za serikali ambazo ni nyama ya nyati yenye uzito wa kilogramu 65, yenye thamani ya dola za Marekani 1,900 sawa na Sh 4,352,900 mali ya serikali bila kuwa na kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapoli nchini.

  Katika mashitaka ya tatu hadi la 72, kwamba siku hiyo na eneo hilo hilo, mshitakiwa huyo alikutwa na silaha aina ya Pistol bila ya kibali cha mrajisi wa silaha.

  Inadaiwa katika mashitaka ya 73 kuwa, Oktoba 30, mwaka huu maeneo ya Oysterbay mshitakiwa alikutwa na risasi 4,092 na katika mashitaka mengine ilidaiwa mshitakiwa alikutwa na risasi 2,404 bila kuwa na kibali.

  Katika mashitaka ya utakatishaji fedha, inadaiwa kuwa Oktoba 30, mwaka huu maeneo hayo ya Oysterbay, Akram alitakatisha USD 9,018 huku akijua kuwa fedha hizo ni zao la kujihusisha na makosa ya uhalifu. 
  Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe akiwa na washtakiwa wenzake leo Mahakamani Kisutu.
  viongozi mbalimbali wa Chadema wakiwa mahakamani Kisutu.


  0 0

  *Wanaoishi maeneo hayo wamuangukia Waziri William Lukuvi, wamuomba aingilie kati *Diwani ajitosa kuzungumzia ukweli eneo hilo...adai wananchi wamevamia, waondoke

  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  WANANCHI wa Mtaa wa Mbweni Maputo jijini Dar es Salaam wapatao 270 wamemuomba Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi kuingilia kati mgogoro wa ardhi wa eneo ambalo linadaiwa kuwa ni mali ya aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT) Daud Balali(sasa marehemu) ambalo baada ya kuwa pori na kichaka cha uhalifu waliamua kusafisha eneo hilo na kisha kuweka makazi yao.

  Wakizungumza na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari leo katika eneo hilo la mtaa wa Mbweni Matupo jijini Dar es Salaam wananchi hao ambao wanadaiwa kuwa ni wavamizi wameeleza wazi kuwa ni kweli wao waliamua kusafisha eneo hilo baada ya kuwa kero kwa wananchi wa maeneo hayo ya Mbweni na walifanya hivyo baada ya kuona limekaa muda mrefu bila kuendelezwa huku wakidai wamefuatilia wizarani na kubaini halina mwenyewe kwani ni eneo ambalo halijapimwa ila wanachokiona kuna watu wameamua kutengeneza hati ili kujionesha kama wao ndio wamiliki.

  Wamewaambia waandishi wa habari kutambua kuwa katika eneo hilo hadi sasa kuna watu karibu watano wamekwenda na kila mmoja anasema la kwake.Hata hivyo wananchi hao wakiomba kuoneshwa hati hakuna mwenye hati miliki huku wakidai kuwa kwa kuwa wao wanyongwe watu wenye uwezo wa kifedha wanatumia kama fimbo ya kuwanyanyasa na kutishia kwamba waondoke na kinyume na hapo nyumba zao zitabomolewa.

  Akizungumza na kwa niaba ya wananchi wenzake ambao wapo eneo hilo Raphael Joseph amesema kuwa hawana tatizo iwapo sheria itawataka kuondoka eneo hilo lakini kwa haki ila kinachowasumbua ni namna ambavyo watu ambao hawana hati ya umiliki wa eneo hilo wanavyoamua kutumia utajiri wao wa fedha kuwanyanyasa na kuwatishia kuwa makazi yao yatabolewa.

  "Hatuko juu ya sheria lakini tunaomba ifahamike ili eneo lilikuwa pori, hivyo likawa linatishia uhai wa wananchi wa eneo hili la Mbweni Maputo.Wananchi tukaamua kusafisha eneo hili na baadae tukaanzisha makazi kama ambavyo mnaona.Hatuko juu ya sheria lakini tunaomba haki ifuatwe.Tulienda kufungua kesi mahakamani ambayo ipo Mahakama Kuu , sasa kabla ya kesi kutolewa huku tunambiwa tuondoke.Tunakwenda wap? Hivyo tunamuomba Rais wetu mpendwa anayejali wanyonge atusaidie.Pia tunamuomba Waziri wa Aridhi atusaidie ili haki itendeke.Eneo hili lote halijapimwa lakini tunashangaa baadhi ya watu wanakuja na hati,"amesisitiza.

  Ameongeza kuwa wamefuatilia historia ya eneo hilo na kubaini kuwa Daud Balali enzi za uhai wake aliomba eneo hilo kwa moja ya wazee wa Mbweni ambapo alipewa kipande kidogo kwa ajili ya kujenga hoteli ya kitalii lakini hata hivyo hakuendeleza na kubaki pori kwa muda mrefu

  MJUMBE SERIKALI YA MTAA

  Kwa upande wake Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Mbweni Maputo Costantine Malifa amekiri kuutambua mgogoro wa ardhi ya eneo hilo huku akifafanua wananchi hao wapo eneo hilo kwa zaidi ya miaka sita sasa ila kinachoshangaza ni idadi ya watu wanaofika eneo hilo na kudai ni mali yao.

  Hata hivyo amesema kwa sasa amejitokeza mke wa Daud Balali aliyemtaja kwa jina la Anna Muganda ambaye anasema ni eneo lake na hivyo amewataka wananchi hao waondoke na tayari amepeleka kampuni ya udalali ya Suma JKT kwa ili wabomoe makazi ya watu."Eneo hilo lilikuwa pori la muda mrefu , hivyo wananchi zaidi ya 270 waliamua kwenda kuanzisha makazi yao kama ambavyo
  mmeona.Leo hii anakuja mtu anasema ni eneo lake.Bila kujali ya uamuzi wa Mahakama Kuu anataka watu waondoke,"amesema.

  Amefafanua wananchi hao wanachotaka ni kujua ukweli wa eneo hilo na kutaka isitambulike kuwa wamevamia bali waliamua kuweka makazi baada ya kuona eneo hilo haliendelezwi na kubaki pori ambalo lilikuwa linatishia usalama wa maisha ya watu huku akisisitiza Mahakama Kuu ikitoa hukumu ya kuwataka wananchi waondoke basi wataondoka na kama atatakiwa kupewa Muganda ambaye anatajwa kama mkewe marehemu Daud Balali basi atapewa.

  DIWANI AVUNJA UKIMYA...ATOA UFAFANUZI

  Wakati huo huo Diwani wa Kata ya Mbweni jijini Dar es salaam Hashim Mbonde amesema kuwa analifahamu vema eneo hilo na ukweli ni kwamba mmiliki halali ni Anna Muganda ambaye ni mkewe Daud Balali, hivyo wananchi hao wamevamia na ni vema wakaondoka.Amesema awali kuna wananchi walitoka eneo la Bunju na kuvamia eneo hilo ambao walikuwa 100 lakini yeye kama
  kiongozi wa wananchi aliamua kuwaondoa lakini baadae wamekuja wengine na kuvamia eneo hilo lenye heka 12 na lina umiliki halali wa Muganda.

  Amesema kutokana na Muganda kulimiliki kihalali alikwenda Manispaa ya Kinondoni kuomba kibali kwa ajili ya ujenzi na baada ya kutaka kuanza ujenzi wananchi hao waliamua kuwatimua, hivyo akalazimika kuomba ulinzi ambapo kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya."Nimekuwa diwani wa eneo hili kwa muda mrefu na mchakato wote wa ununuzi wa Balali eneo hilo nilikuwepo, hivyo naufahamu vema na unaponiuliza nani mmiliki halali jibu langu ni kwamba mkewe marehemu Daud Balali ndio mmiliki.Hivyo niwaombe wananchi waheshimu sheria na wapishe eneo hilo kwani si la kwao,"

  Ametumia nafasi hiyo kueleza namna ambavyo baadhi ya viongozi wa Serikali ya Mtaa wa Maputo ambavyo wanapotosha ukweli wa eneo hilo na kuwataka kuwa wa kweli kwani mwenye eneo hilo ni Anna Muganda ambalo amelirithi kutoka kwa mumewe.Amefafanua kuwa yeye anamtambua mjane wa Daud Balali ambaye ni Anna Muganda kuwa ndio mwenye eneo hilo kwa kuwa na hati zote na hati yake ya umiliki haina shaka hata kidogo lakini kinachoshangaza wananchi hao ambao wamewaita wavamizi wanamzuia asifike kwenye eneo lake kwa ajili ya kuliendelea huku akisistiza umuhimu wa wananchi kufuata sheria.

  Kuhusu haki za binadamu amesema wanatambua hilo na ndio maana wananchi walioko eneo hilo wamepewa notisi ya siku 14 ili waondoke kwa hiyari yao.

  BARUA YA NOTISI YABANDIKWA MTAANI

  Wakati hayo yakiendelea Kampuni ya Udalali ya Suma JKT nayo imefika eneo hilo na kisha kubandika barua ya notisi inayowataka wananchi walioko ndani ya eneo hilo waondoke.Hata hivyo Mjumbe wa Serikali ya Mtaa aligoma kuitambua barua hiyo ya notisi wala kwenda kuonesha eneo lenye mgogoro ambapo amesema hawezi kwenda kuonesha eneo bila ya kuona barua ya nakala ambayo
  imetoka Mahakama Kuu kwani kesi bado iko mahakamani ya kutafuta uhalali wa nani mmiliki sahihi wa eneo hilo.

  MJANE WA DAUD BALALI AOMBA ULINZI ....

  Pamoja na yote hayo aliyekuwa mkewe Daud Balali Anna Muganda Julai 26 mwaka huu wa 2018 aliamua kuomba ulinzi katika mchakato wa kuwatoa wananchi hao ambao amewaita wavamizi wa eneo lake.Kupitia barua yake ya tarehe hiyo kwenda kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni amesema yeye Anna Muganda Balali mwenye eneo Mbweni Ploti namba 1007 Block B lenye
  ukubwa wa wa 36,197 Sqm ambalo limepimwa na kupewa hati namba 155638.

  Hata hivyo anasikitishwa na kutendo cha wananchi kuamia eneo hilo na kwenye barua hiyo anaonesha kuwa aliwahi kuomba ulinzi ili

  aweze kuwaondoa wavamizi hao katika eneo hilo.
   Baadhi ya wananchi wa Mbweni Maputo jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye kikao cha kuangalia namna ya kuomba msaada wa Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi kuingilia kati kwani kwa sasa wanaishi maisha ya hofu
   Mkazi wa Mtaa wa Mbweni Maputo jijini Dar es Salaam Raphael Joseph akizungumzia mgogoro wa eneo ambalo wao wameamua kufanya makazi baada ya mrefu kudai lilikuwa pori ambapo wanamuomba Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuingilia kati ili haki itendeke kwani kuna watu wanawatishia kuwaondoa  kwa nguvu
   Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Mbweni Maputo Costantine Malifa akionesha barua ya kampuni ya udalali ya Sums JKT ambayo inawataka wananchi hao kuondoka ndani ya siku 14 kuanzia jana.Hata hivyo amekataa kuitambua hiyo kwa mdaia suala la eneo hilo liko mahakamani ,hivyo hawezi kutoa usharikiano kwenye jambo analoona linakwenda kinyume na sheria
   Diwani wa Kata ya Mbweni Hashimu Mbonde(kulia)akitoa ufafanuzi kuhusu eneo hilo ambalo amedai mmiliki halali ni Anna Muganda ambaye ni mke wa aliyekuwa Havana wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT) Daud Balali ambaye kwa sasa ni marehemu
   Mkazi wa Mtaa wa Mbweni Maputo John Julius akitoa ufafanuzi namna ambavyo wamefika eneo hilo na kuweka makazi yao huku akiiomba Serikali kuingilia  kati eneo hilo ili haki ipatikane

   

older | 1 | .... | 1744 | 1745 | (Page 1746) | 1747 | 1748 | .... | 1897 | newer