Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

WAZIRI HASUNGA AMUAGIZA KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO KUMSIMAMISHA KAZI MTUMISHI MMOJA KWENYE TIMU YA OPARESHINI KOROSHO

$
0
0
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kikao kazi na watendaji wa serikali sambamba na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Lindi katika ziara yake ya kikazi aliyoianza leo tarehe 4 Disemba 2018 mkoani humo. (Picha Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo).
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kikao kazi na watendaji wa serikali sambamba na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Lindi katika ziara yake ya kikazi aliyoianza leo tarehe 4 Disemba 2018 mkoani humo.
Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mhe Sarah Chiwamba, Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mhe Rukia Muwango na Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe Christopher Ngubiagai wakisikiliza kwa makini hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati akizungumza kwenye kikao kazi na watendaji wa serikali sambamba na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Lindi katika ziara yake ya kikazi aliyoianza leo tarehe 4 Disemba 2018 mkoani humo.


Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Mtwara

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe kumsimamisha kazi mtumishi George Mboje na kumuondoa kwenye timu ya Operesheni Korosho.

Pamoja na kumundoa kwenye timu hiyo pia Katibu Mkuu ametakiwa kumuondoa kwenye Bodi ya Nafaka na Mazao mchanganyiko."Katibu Mkuu, nataka umuondoe huyu George kwenye hii timu na pia sitaki kumuona kwenye Bodi na Taasisi yoyote katika Wizara ya Kilimo" Alisisitiza Mhe Hasunga .

Mhe Hasunga ametoa agizo hilo leo tarehe 4 Disemba 2018 wakati akizungumza kwenye kikao kazi cha Watendaji wa timu ya Oparesheni korosho kilichofanyika katika ukumbi wa CBT Mkoani Lindi na wakati wa kikao kazi na watendaji wa serikali sambamba na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Lindi katika ziara yake ya kikazi aliyoianza leo tarehe 4 Disemba 2018.

George Mboja ambaye yupo kwenye timu ya Oparesheni Korosho akiwakilisha Bodi ya Nafaka na Mazao mchanganyiko anatuhumiwa kwa Utovu wa nidhamu sambamba na kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo wakati wa Oparesheni Korosho inayoendelea nchini.Aidha, Waziri Hasunga amewahakikishia watendaji hao kuwa serikali ina fedha za kutosha kuwalipa wakulima wa Korosho lakini lazima wakulima wote wahakikiwe ili kujiridhisha kwamba anayelipwa ni mkulima wa mwisho na sio wafanyabiashara maarufu kama Kangomba.

Akizungumzia hatua iliyofikiwa na serikali kuhusu malipo ya wakulima wa korosho, alisema hadi kufikia Jana tarehe 3 Disemba 2018 uhakiki ulikwishafanyika kwenye vyama 220 kati ya vyama 504 vilivyopo katika Mkoa wa Mtwara, Lindi na Ruvuma na kati ya vyama 617 vinavyojihusisha na Korosho nchini.

Alisema kati ya vyama hivyo vilivyokwisha hakikiwa ni vyama 181 ndivyo ambavyo tayari vimelipwa fedha zao huku Bilioni 41.8 zikiwa zimelipwa.Aliongeza kuwa wakati zoezi hilo linaanza serikali ilikuwa inalipa Bilioni Moja kwa siku lakini kwa sasa utaratibu uliowekwa ni kulipa kati ya Bilioni 5 mpaka 10 kwa siku.

Katika taarifa yake Waziri Hasunga amesema kuwa jumla ya wakulima 40,208 wamekwishalipwa fedha zao.Mhe Hasunga aliongeza kuwa serikali imeamua kuwalipa wabebaji na wapakiaji wa mizigo kwenye maghala sambamba na kuanza kuwalipa malipo ya awali wasafirishaji kutoka kwenye vyama vya msingi kwenda kwenye vyama vikuu.

Kuhusu swala la magunia Waziri Hasunga alisema kuwa serikali imeamua kuyalipa magunia yote ili kurahisisha uhifadhi wa Korosho.

WAFANYAKAZI WA TBL GROUP WAPATIWA ELIMU KUHUSU UKATILI WA KIJINSIA

$
0
0
Kampuni ya Tanzania Breweries Limited inaungana na mashirika yanayopinga vitendo vya ukatili wa kijinsia na kutetea haki za binadamu katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi- Kitengo cha Dawati la Jinsia. 

Maadhimisho haya yalioanza wiki iliyopita huandaliwa kila mwaka na Shirika lisilo la kiserikali la WiLDAF kwa kushirikiana na mtandao wa mashirika yanayopinga ukatili wa kijinsia nchini (MKUKI), wadau wa maendeleo na taasisi mbalimbali za kiserikali na za binafsi. 

Afisa mawasiliano wa TBL Abigail Mutaboyerwa,amesema mwaka huu TBL itatumia njia mbalimbali kutoa elimu ya uelewa kwa jamii ikiwemo kuendesha semina kwa wafanyakazi wake na jamii katika maeneo mbalimbali kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kitengo cha Dawati. Vile vile wafanyakazi wa kampuni ya TBL wataungana na Polisi pamoja na wadau mbalimbali kushiriki katika kilele cha maadhimisho ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia yatakayoandaliwa na Polisi Ilala katika kata ya Kivule ,Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam Jumamosi tarehe 8 Desemba 2018.
ASP, Fatuma Mtalimbo kutoka Dawati la Jinsia Jeshi la Polisi akitoa mada kuhusiana na ukatili wa kijinsia kwa wafanyakazi wa kampuni ya TDL maarufu kama Konyagi.
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL wakifuatilia mada wakati wa semina kuhusiana na ukatili wa kijinsia.
ASP, Fatuma Mtalimbo kutoka Dawati la Jinsia Jeshi la Polisi akitoa mada kuhusiana na ukatili wa kijinsia kwa wafanyakazi wa TBL kituo cha mauzo na usambazaji kilichopo Ubungo jijini Dar es Salaam
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL wakifuatilia mada wakati wa semina kuhusiana na ukatili wa kijinsia.
Wafanyakazi wa TDL wakiwa katika picha ya pamoja na afande Fatuma Mtalimbo baada ya semina ya masuala ya jinsia.

Wateja wa Tigo Kanda ya Ziwa kufanya malipo kwa kutumia Mfumo wa Kielekroniki wa Malipo Serikalini (GePG)

$
0
0
Wateja wa Kampuni ya Tigo wa mikoa ya Kanda Ziwa sasa wanaweza kufanya malipo kutumia mfumo wa Kielektroniki wa Malipo Serikalini (GePG) baada ya kampuni hiyo kuongeza malipo ya Serikalini kwenye App yake ya Tigo Pesa. 

Akiongea katika hafla fupi ya uzinduzi iliyofanyika jijini Mwanza, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) Mecky Manyama alisema mfumo wa GePG umerahisisha upatikanaji wa ankara na kufanya malipo kwa wananchi na kuongeza kuwa umeleta faida nyingi ikiwa ni pamoja na kuboresha uwekaji wa kumbukumbu, utoaji wa taarifa, kupunguza ubadhirifu na kuongeza mapato kwa idara mbali mbali na taasisi za Serikali 

“Mfumo wa GePG, pia imeongeza wigo wa upatikanaji wa huduma kwa wananchi na kuongeza fursa za biashara kwa kampuni zinazotoa huduma za malipo kama Tigo. Wananchi wanaweza kupokea ankara zao moja kwa moja kutoka ofisi na mashirika ya Serikali ikiwa ni pamoja na za kutoka MWAUWASA. Malipo pia yanaweza kufanyika kwa njia mbali mbali za kimtandao, na kufurahisi na mahali popote kwa njia ya simu za kiganjani, benki au kwa njia ya mtandao.,” alisema Manyama 

“Kufanya kazi kwa karibu na Serikali ili kufikisha huduma za kifedha kwa wananchi wengi ni moja kati ya malengo mkakati yetu,” alisema Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Uthuman Madatti 

Aliongeza “Zaidi ya wateja milioni 7 wanaotumia huduma yetu ya Tigo Pesa sasa wana uwezo zaidi wa kufanya malipo kwa haraka kwenda kwa taasisi, Wizara na wakala wa Serikali zaidi ya 300 kupitia Tigo Pesa USSD, Tigo Pesa App na QR Code,” 

Baadhi ya taasisi za Serikali ambazo malipo yanaweza kufanywa kwa Tigo Pesa ni pamoja na Wizara ya Ardhi, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mamlaka za Miji, Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Shirika la Hifadhi ya Taifa (TANAPA), Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Mamlaka ya Misitu (TFS), Wizara ya Utalii, Bodi ya Utalii, Idara ya Uhamiaji, Mamlaka za Maji katika miji ya Mwanza (MWAUWASA), Tanga (Tanga UWASA), Dar es Salaam (DAWASA), Dodoma (DUWASA), Hospitali mbali mbali kama vile Muhimbili, Mwananyamala na idara nyingine zaidi ya 300. 

Ili kufanya malipo kwa kutumia Tigo Pesa App na QR Code, wateja wa Tigo wanahitaji kupakua App ya Tigo Pesa na kuscan QR code kisha kuingiza namba ya siri ili kufanikisha muamala. 
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) Meck Manyama (kulia), akionyesha namna ya kutumia simu ya kiganjani kufanya malipo, wakati wa uzinduzi wa  Mfumo wa Kielektronic wa malipo ya serikali (GePG), ambao utatumika kufanya malipo kwa taasisi zaidi ya 300 za Serikali kwa kutumia mtandao wa Tigo. Kulia ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa Uthumaan Madatti.

Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa Uthumaan Madatti (kushoto), akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa Kielektronic wa malipo ya serikali (GePG)uliofanyika jijini Mwanza leo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) Meck Manyama
Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa Uthumaan Madatti (kulia), akionyesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) namna ambavyo simu ya kiganjani kupitia mtandao wa Tigo inaweza kutumika kulipa malipo mbali mbali kwa taasisi zaidi ya 300 za serikali wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa Kielektronic wa malipo ya serikali (GePG)uliofanyika jijini Mwanza leo. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Serikali wa Tigo Ally Maswanya
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) Meck Manyama (kulia), akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) , wakati wa uzinduzi wa  Mfumo wa Kielektronic wa malipo ya serikali (GePG), ambao utatumika kufanya malipo kwa taasisi zaidi ya 300 za Serikali kwa kutumia mtandao wa Tigo.Anayefuatia ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa Uthumaan Madatti na Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Serikali wa Tigo Ally Maswanya. 

Experts meet in Dar to discus food safety concerns in Africa

$
0
0
By Correspondent

African food experts, researchers and stakeholders will meet in Dar es Salaam today to discuss challenges and concerns related to food safety, food borne diseases and chart out strategies on the best ways to improve food safety, nutrition and security for millions of Africans.

The international meeting is part of the commemoration of the Africa Day for Food and Nutrition Security 2018, is organized under the main theme “Sustained Food Safety Action for Improved Nutrition and Health of Africans,” bringing together participants from various African countries and key international and national agencies, World Food Programme, UNICEF, World Health Organization, Food and Agriculture Organization of the United Nations, African Union Commission, NEPAD and Tanzania Food and Drugs Authority (TFDA).

The main agenda of the meeting, expected to be graced officially by the Permanent Secretary in the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Women, is food safety concerns and their associated main outcome, food-borne diseases, according to an official statement issued by the organizing agency, TFDA.

“Food-borne disease imposes large direct and economic burdens worldwide…Africans are not exception to this…” noted TFDA statement.

Experts says food borne disease are a constraint to the development and flourishing of domestic and exports food sectors in African economies, noting that “will be difficult to attain sustainable development goals or to meet the Malabo Declaration unless food borne disease in Africa is brought under control.”

TFDA said participants to the meeting will broadly and critically issues around food safety concerns, saying that “as developments advance towards a free trade zone for the continent, food safety concerns will become of even greater concern.”

There will be presentations of strategic and technical papers on food safety status in Africa, covering the health and economic burden, the riskier foods and people most at risk, current and previous food safety initiatives in the continent.

“Strategic papers will also include issues related to considerations on the nexus between food safety, nutrition and health and proposals on strategic directions towards improved food safety and regulatory frameworks,” noted part of TFDA statement.


Dr. Kandida Shirima, Director of Food Safety at TFDA, presenting a paper on food safety status in Africa at the Africa Day for Food and Nutrition Security—2018 conference being held in Dar es Salaam which discusses food safety concerns in Africa.
Participants to the Africa Day for Food and Nutrition Security—2018 conference following proceedings of the meeting being held in Dar es Salaam which will discuss food safety concerns in Africa.


Rais Magufuli ateua Mwenyekiti na Makamishna 5 wa Tume ya Utumishi wa Umma

CEO DAWASA AHIDI KUPELEKA HUDUMA YA MAJI BONYOKWA

$
0
0
Afisa mtendaji mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja ametoa ahadi ya kupeleka maji Bonyokwa wakati wa ziara ya Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa.

Prof Mbarawa amefanya ziara ya kusikiliza kero za wananchi kuhusiana na huduma ya Maji katika eneo hilo. 

Mhandisi Luhemeja ameeleza kuwa eneo hilo limekosa huduma ya Maji kwa muda mrefu kutokana na kukosa chanzo cha Maji cha Karibu na hivyo DAWASA imeamua kulaza bomba kubwa litakalo chukua Maji kutoka mtambo wa uzalishaji Maji wa Ruvu juu ili kuhudumia wakazi wa eneo hilo.

“Sisi DAWASA tutaleta huduma ya Maji hapa Bonyokwa kwa kuwa ni muda mrefu mmeteseka na tatizo kubwa la eneo hili ni kukosa chanzo cha Maji cha kuhudumia hapa kutokana na jiografia yake ila sasa tumeamua kutoa Maji kutoka mtambo wa Ruvu juu na kuyaleta hapa, tayari pia baadhi ya vifaa vimefika hapa na kuanzia Siku ya Jumatatu tutaanza kazi rasmi ya kulaza mabomba hivyo wananchi mjitokeze kwa ajira uchimbaji mitaro” alisema mhandisi Luhemeja.

Aidha Prof. Makame Mbarawa katika mkutano huo amewatoa wasiwasi wakazi wa eneo hilo kwa kuwaeleza kuwa atahakikisha DAWASA inafikisha huduma ya Maji kwa wakati na kumuagiza meneja wa DAWASA Mkoa wa Tabata kusimamia hilo. Pia amebainisha kuwa lengo la serikali ni kufikisha huduma ya Maji safi kwa asilimia tisini na tano kwa maeneo yaliyopo mijini kufika 2020.

Kwa niaba ya wakazi wa eneo hilo Meya wa Ilala na Diwani wa eneo hilo Charles Kwiyeko ameshukuru jitihada za serikali pamoja na DAWASA zakutaka kufikisha huduma ya Maji kwa kuwa ni kero kubwa na ya muda mrefu kwa wananchi wake.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa akizungumza na wananchi wa Bonyokwa na kuwaondoa hofu na kuwahakikishia watapata maji kwenye maeneo yote yaliyokuwa hayana maji.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akiwa anatembelea maeneo ya Bonyokwa akiwa ameambatana na Meneja wa DAWASA Tabata na Diwani wa kata hiyo. 
Wananchi mbalimbali waliofika katika mkutano huo.

WAZIRI MKUU ATEMBELEA TIC AITAKA IMALIZE URASIMU

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Watendaji, kwenye Ofisi za Kituo hicho jijini Dar es salaam, Desemba 4, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwenye viwanja vya Ofisi za Kituo hicho jijini Dar es salaam, Desemba 4, 2018. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Profesa, Faustine Kamuzora na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Ilala, Sophia Mjema.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza, Afisa wa NEMC katika Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Linda Mutafungwa wakati alipotembelea Kituo hicho, Desemba 4, 2018. Wapili kulia ni Mkurugenzi wa TIC, Geofrey Mwambe.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Maofisa wa Kodi na Forodha wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Leonard Mapunda (wapili kulia) na Helen Haule (kulia) wakati alipotembelea Kituo hicho, Desemba 4, 2018. Kushoto ni Mkurugenzi wa TIC, Geofrey Mwambe.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Maofisa wa Kodi na Forodha wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Leonard Mapunda (kulia) na Helen Haule ( wapili kulia) wakati alipotembelea Kituo hicho, Desemba 4, 2018. Kushoto ni Mkurugenzi wa TIC, Geofrey Mwambe.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Wajumbe wa Bodi ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) wakati alipotembelea Kituo hicho jijini Dar es salaam, Desemba 4, 2018. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekitaka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimalize urasimu ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake. Kadhalika, ameuagiza uongozi wa TIC uweke kipaumbele cha kwanza katika kulinda rasilimali za nchi na maliasili zake ikiwemo ardhi, mazao ya uvuvi, misitu, madini.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo jioni (Jumanne, Desemba 4, 2018) alipozungumza na Bodi ya Wakurugenzi wa TIC na Menejimenti, jijini Dar es Salaam. “Katika kuvutia wawekezaji hasa wa nje ni lazima tuweke kipaumbe katika kulinda rasilimali zetu kama ardhi, madini fukwe ili zisiporwe kwa kisingizio cha uwekezaji.” Amesema eneo hilo linahitaji umakini na uadilifu mkubwa, hivyo ni muhimu kwa kituo hicho kuhakikisha kinatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia maslahi ya Taifa. Amesema ili kupata matokeo mazuri ni lazima waimarishe mawasiliano na uratibu miongoni mwa wadau wote sambamba na kutekeleza vipaumbele vilivyoainishwa.

“Serikali imedhamiria kuwa nchi ya uchumi wa kati kupitia sekta ya viwanda ifikapo 2025, TIC inatakiwa iongoze kwa kuvutia wawekezaji wengi wa ndani na nje ya nchi.” Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema kuwa wawekezaji ambao TIC inatakiwa ivutie ni walio mahiri wenye nia thabiti ya kutufikisha huko na siyo wachuuzi au madalali. Kadhalika,Waziri Mkuu amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli inataka TIC iwe kioo cha nchi ambacho kitavutia wawekezaji. Amesema Serikali inataka TIC mpya ambayo itakuwa kimbilio la wawekezaji wengi wa ndani na nje, badala ya kuwa kikwazo na kusababisha wawekezaji wakija kukimbilia.

Hivyo, Waziri Mkuu ameuagiza uongozi wa kituo hicho ubadilishe muundo wa kuwapokea wawekezaji, wawapokee vizuri na wawaeleze fursa za uwekezaji zilizopo. “ Pia, TIC iweke mazingira rafiki ya kuwawezesha Watanzania wengi kumiliki uchumi kwa kuanzisha miradi mipya wao wenyewe au miradi ya ubia kati ya wawekezaji.” Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema kila mtumishi wa umma ni lazima afanye kazi kwa bidii, maarifa na ubunifu, uadilifu, weledi, uaminifu na kuzingatia sheria, kanuni na taratibu.

Waziri Mkuu amesema ni lazima wahakikishe vitendo vya rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma vinaepukwa na kila mtumishi.” Serikali haivumii watumishi wa aina hiyo.” Kwa upande wake,Mkurugenzi wa TIC, Geofrey Mwambe amemuomba Waziri Mkuu awasaidie kwa kuwapatia ofisi kwa kuwa eneo wanalofanyia kazi kwa sasa halitoshi. Pia amesema kituo hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya upungufu wa rasilimali watu, sasa wanahitaji watumishi 31 wakiwemo mameneja 11.

Awali, Waziri Mkuu alitembelea eneo la kutolea huduma za pamoja zilizopo ndani ya Kituo hicho cha Uwekezaji Tanzania na kusema kwamba ameridhishwa na utendaji.

MKAZI WA IRINGA AJISHINDIA GARI KUPITIA PROMOSHENI YA TBL KUMENOGA, TUKUTANE BAA'

$
0
0

Gari alilojishindia Bw.Frank Nathan hilo.
Meneja wa Udhamini na Mawasiliano ya Wateja wa TBL, David Tarimo ( wapili kushoto) akiongea kwa sim una mshindi wakati wa droo ya pili ya promosheni ya TBL Kumenoga iliyofanyika jijini Dar Salaam. Kushoto ni Meneja masuala endelevu wa TBL, Irene Mutiganzi, , Asam Keta na Afisa Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni hiyo Abigail Mutayoberwa
Meneja wa Udhamini na Mawasiliano ya Wateja wa TBL,David Tarimo ( katikati) akiongea kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakati wa droo hiyo.Kushoto ni Meneja Masuala Endelevu wa TBL ,Irene Mutiganzi na Afisa Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni hiyo Abigail Mutayoberwa. --- Mkazi wa Iringa Bw, Frank Nathan (38), amejishindia gari mpya aina ya Renault KWID, kupitia droo ya pili ya promosheni ya wateja ya TBL Kumenoga, Tukutane Baa’iliyofanyika jijini Dar es Salaam chini ya usimamizi wa Bodi ya Taifa ya Michezo ya kubahatisha. 
 
Nathan, akiongea baada ya kupigiwa simu na Meneja wa Udhamini na Mawasiliano ya wateja wa TBL, David Tarimo, kumfahamisha kuwa ameibuka mshindi, alisema kwa furaha kuwa anayo furaha kuona ndoto yake ya muda mrefu ya kumiliki gari inatimia kupitia promosheni hii. “Habari hizi naziona kama ndoto kwangu, nashukuru TBL kwa kufanikisha ndoto yangu ya kumiliki gari “alisema kwa furaha. 
 
Meneja wa Udhamini na Mawasiliano ya wateja wa TBL, David Tarimo, kwa niaba ya kampuni ya TBL alimpongeza mshindi huyo na kutoa wito kwa wateja wote wa vinywaji vya TBL nchini, kuendelea kuichangamkia promosheni hii ili kuweza kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo zawadi kubwa ya gari mpya aina ya Renault KWID. 
 
“Tunayo furaha kubwa kumpata mshindi wa pili wa zawadi kubwa ya mwezi ambayo ni gari mpya, kwa sasa imebaki gari moja na zawadi nyinginezo nyingi kwa ajili ya wateja wetu watakaoshiriki promosheni hii hususani katika kipindi hiki tunachoelekea kwenye msimu za sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya” alisema Tarimo. Tarimo, aliongeza kuwa, promosheni hii inafanyika kwenye mabaa katika siku za mwisho wa wiki yaani Ijumaa, Jumamosi na Jumapili kupitia bia za Safari Lager, Kilimanjaro Lager, Castle Lite na Balimi Extra Lager. 
 
Kwa upande wake, Meneja wa Ukuzaji wa Masoko wa TBL, Edith Bebwa, alisema promosheni inafanyika kwenye mabaa zaidi ya 5,000 nchini kote. “Wateja wetu wazidi kuitafuta bendera ya TBL Kumenoga, kwani ilipo bendera hii ndipo wateja na TBL wanapokutana katika promosheni.
 
’ Alifafanua zaidi kuwa ili kuingia kwenye droo ya kujishindia gari jipya kupitia promosheni hii ya ‘TBL Kumenoga, Tukutane Baa’ mteja atatakiwa kununua bia tatu kati ya Safari Lager, Kilimanjaro Lager, Castle Lite au Balimi Extra Lager kwenye promosheni, ambapo atapatiwa kuponi yenye namba, kisha anatakiwa kutuma namba hiyo kwa meseji kwenda 15451, hii ni kwa wateja wenye mitandao ya VODACOM, TIGO na AIRTEL. Kwa wateja wa mitandao mingine watatuma namba iliyo kwenye kuponi kupitia tovuti ya www.tblkumenoga.co.tz.

MAGAZETI YA LEO JUMATANO,DESEMBA 5,2018

DC NAMTUMBO AIAGIZA TAKUKURU KUICHUNGUZA HALMASHAURI .

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Mfaume Kizigo ameiagiza taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU wilayani Namtumbo kuchunguza shilingi milioni 950 zilizobadilishiwa matumizi na Halmashuri ya Namtumbo.

Kizigo aliyasema hayo hivi karibuni katika mkutano wa baraza la madiwani wilayani humo baada ya kubaini baraza la madiwani kutoridhika na taarifa ya mkaguzi wa ndani wa Halmashauri hiyo juu ya kubadilisha matumizi ya fedha shilingi milioni 950.

Taarifa ya mkaguzi wa ndani wa Halmashuri hiyo bwana John Mwingira ilidai Halmashuri hiyo imebadilisha matumizi ya fedha kiasi cha shilingi milioni 950 na kutumika kwa matumizi mengineyo tofauti na ilivyokusudiwa .

Aidha bwana Mwingira katika taarifa yake hiyo alidai kuwa fedha hiyo imetumika kwa nia njema lakini zinatakiwa kurudishwa katika shughuli iliyokusudiwa na serikali kwa kutumia mapato ya ndani ambayo kwa sasa yanasuasua.

Taarifa hiyo ilisema katika shilingi milioni 950 milioni 500 zilikuwa Ruzuku ya serikali zikiwa na lengo la kujenga Hospitali ya wilaya ambapo katika fedha hiyo milioni 200 zilibadilishwa matumizi na kumalizia zahanati saba viporo vya Halmashuri hiyo na kuanza kutumika na milioni 20 nazo zilibaki kujenga jengo moja katika Hospitali ya wilaya na milioni 156 zilipelekwa kukamilisha chumba cha upasuaji katika kituo cha afya lusewa katika mamlaka ya mji mdogo wa Lusewa.

Milioni 450 kati ya hizo milioni 950 zilipokelewa na Halmashuri hiyo kutoka bodi ya mikopo ya serikali za mitaa LGLB ambazo nazo zililenga kujenga soko zilibadilishwa matumizi na kulipia deni la vifaa vya viwandani milioni 214 zilizokopa Halmashuri hiyo na milioni 26 zilitumika kununulia mashine ya kukusanyia ushuru (POS)ishirini.

Diwani wa kata ya Hanga bwana Kassimu Ntara alidai anasikitishwa na taarifa hiyo ya kubadilishwa matumizi ya fedha kiasi cha shilingi milioni 397 zaidi ya kile kilichokubaliwa katika kamati ya fedha ,uongozi na mipango lakini pia idhini iliyotolewa na baraza la madiwani ya kutumia shilingi milioni 214 pekee.

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa wilayani Namtumbo wameanza kuitekeleza agizo la mkuu wa wilaya huyo kuchunguza matumizi ya fedha hizo kwa kuhoji wahusika waliohusika kutoa fedha hizo na kuruhusu zitumike kinyume na malengo ya serikali.

Mwisho. picha ya kwanza DC Namtumbo na picha ya pili Diwani wa kata ya Hanga akichangia kwenye baraza hilo

Tony Elumelu kufungua dirisha Programu ya Wajasiriamali Afrika, Januari 1, 2019

$
0
0
Na Bakari Kimwanga -DAR ES SALAAM 

TAASISI ya Tony Elumelu (TEF), imetangaza kufungua mzunguko wa tano wa programu ya Wajasiriamali Afrika kuanzia Januari 1, 2019 

Maombi hayo yatatumwa na kushughulikiwa kwenye kwenye jukwaa kubwa la mitandao kwa wajasiriamali wa Afrika, TEFConnect - www.tefconnect.com

Taarifa iliyotolewa na Taasisi ya Tony Elumelu yenye makao makuu yake Lagos, nchini Nigeria ilieleza kwamba kuanzia Januari 1, 2019, saa 12 asubuhi, Tony Elumelu itaanza kupokea maombi ya mzunguko wa tano wa Programu ya Wajasiriamali. Ambapo waombaji 1,000 waliochaguliwa wataunganishwa msimamizi wa sasa wapatao 4,470 katika program hiyo. 

Tangu mwaka 2015, Mpango wa Biashara wa TEF – imekuwa ni kichocheo kiliasisiwa kwa misingi ya Afrika ambapo aina hiyo, imewawezesha wajasiriamali 4,470 wa Afrika, ambao kila mmoja amenufaika kwa kupatiwa Dola 5,000 kila mmoja. 

Hatua hiyo huenda sambamba na mjasiriamali kuhudhuria mafunzo ya biashara yanayoendeshwa kwa wiki 12, ambao hupata ushauri na uzoefu na kujifunza zaidi mazingira ta Biashara ya Afrika. 

Wanufaika wa Programu wamefanikiwa kuhojiwa kwenye vyombo vya habari vya kimataifa, ikiwa ni pamoja na Forbes (Afrika) 30 chini ya orodha 30. Ambapo wamevutia wawekezaji, na pia wamepewa tuzo za Impact Google na Tuzo ya "Venture" kwa wajasiriamali. 

Programu ya ujasiriamali imewezesha kubadilishana uzoefu kati ya wajasiriamali wa Afrika na viongozi wa sekta ya umma na wa kimataifa, wawekezaji na washirika wa maendeleo ya namna bora ya kuongeza biashara zao. 

Sambamba na hilo pia wameweza kuongeza fursa na kuonyesha ubunifu wao na kutambua njia za kuimarisha mazingira ya biashara katika Bara la Afrika. Mnamo Juni 2017, Foundation iliandaa Jukwaa na Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa na wajasiriamali wadogo wa Kiafrika walihudhuria. 

Na pia mnamo Oktoba mwaka huu (2018), TEF ilifurahi kuwa na Rais wa Jamhuri ya Ghana Nana Akufo-Addo wa Ghana na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ambao kwa pamoja waliweza kuzungumza na mkusanyiko wa wajasiriamali wadogo wa Afrika katika jukwaa hilo lililofanyika Lagos, Nigeria. 

Uwekezaji wa Foundation, umekuwa na mafanikio kutokana na kujitolea kuendeleza ujasiriamali na inaangaziwa kwamba ni ufunguo kwa Bara la Afrika kuweesha mabadiliko Afrika. 

Lengo la Tony Elumelu Foundation ambayo ilizindua Programu ya Uwekezaji, mpango wake kuwekeza Dola milioni 100 kwa kipindi cha miaka 10, ambapo wajasiriamali 10,000 wa Afrika watanufaika kutokana na kuwasilisha mawazo ambayo yana uwezo wa kubadilisha bara la Afrika. 

Hatua hiyo inakwenda sambamba na lengi kuu la kuwekeza katika biashara ambazo zinaweza kuzalisha angalau ajira 1,000,000 na kuchangia angalau dola bilioni 10 katika mapato ya kila mwaka ya Afrika. 

Programu ya Wajasiriamali ya TEF ni wazi kwa wananchi na wakazi wananchi wote wa nchi zote za Bara la Afrika, ambapo huendesha biashara zilizo chini ya miaka mitatu. Pia mpango huu unasistiza kwamba hata mawazo ya biashara ambayo bado hayajaanza yanapokewa na kufanyiwa kazi. 

Maombi ya mwaka 2019 yatashughulikiwa kwenye jukwaa kubwa la mitandao ya digital kwa Afrika TEFConnect on www.tefconnect.com.
Mwasisi wa jukwaa hilo, Tony Elumelu (kushoto), akiwa na Rais wa Ghana, Nana Akufo-Addo, wakiwa na kijana mshiriki wa kongamano kutoka nchini Ghana baada ya kijana huyu kutaka ufafanuzi kwa Rais wake wa namna vijana wanavyopewa kipaumbele katika ujenzi wa uchumi wa nchi hiyo. Mkutano huo ulifanyika Lagos, Nigeria Oktoba mwaka huu.
Sehemu ya vijana walioshiriki jukwaa kubwa la wajasiriamali Afrika, lilofanyika Oktoba mwaka huu, Lagos, Nigeria

Sheria Mpya ya Zana za Kilimo kuchochea Mapinduzi ya Viwanda – Mhandisi Mtigumwe

$
0
0

Sheria Mpya ya Zana za Kilimo kuchochea Mapinduzi ya Viwanda – Mhandisi Mtigumwe Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew Mtigumwe Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew Mtigumwe aliyevaa koti la kahawia katikati akiwa pamoja na Mhandisi Peter Chisawilo kulia kwake ambaye alikuwa Mwenyekiti wa mkutano huo sambamba na Wadau wa Zana za Kilimo mara baada ya kuufungua mkutano huo jana katika ukumbi wa Mvuvi House, Jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Zana za Kilimo Wizara ya Kilimo, Mhandisi Joseph Lubilo akitoa maelezo ya utangulizi kwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew Mtigumwe aliyevaa koti la kahawia katikaki akiwa pamoja na Mhandisi Peter Chiswalo kulia kwake ambaye alikuwa Mwenyekiti wa mkutano huo, jana katika ukumbi wa Mvuvi House, Jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew Mtigumwe ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa Wadau wa Zana za Kilimo wenye lengo la kupitia rasimu ya maboresho ya Sheria ya Zana za Kilimo nchini na kusisitiza kuwa Sheria mpya itatosaidia kuongeza tija na uzalishaji wa mazao ya kilimo ambayo ndiyo malighafi za viwanda vingi nchini. 

Akifungua mkutano huo, Mhandisi Mtigumwe amesema kilimo cha Tanzania kimepitia mageuzi mengi ya kisera na kimkakati na kwamba maboresho ya sheria ambayo Wadau wamekutana ili kuiboresha Sekta ya Zana za Kilimo, yana nafasi kubwa ya kuongeza tija na uzalishaji mkubwa katika kilimo na kuongeza kuwa ni vyema Wataalam wakijikita katika kutoa maoni na michango mizuri itakayochangia katika kuboresha. 

Mhandisi Mtigumwe amekaririwa akisema “Lengo la mkutano huu ni kuwaleta pamoja Wadau wa zana za kilimo ili kushiriki katika kuchangiaAndiko la Sheria ya Zana za Kilimo nchini kwa kutoa maoni na ushauri kuhusu Sheria inayotaka kupendekezwa”. “Aidha, Sheria hii inatarajiwa kuleta uwiano mzuri wa maamuzi kati ya Watengenezaji, Waagizaji, Wasambazaji na Watumiaji wa zana na mashine mbalimbali za kilimo ili kuimarisha na kutambua wajibu wa kila Mdau”. Amekaririwa Katibu Mkuu. 

Mhandisi Mtigumwe ameongeza kuwa azma ya Serikali ni kuendeleleza mapinduzi ya kweli ya kilimo yatakayosaidia katika kuongeza uzalishaji, ufanisi na tija katika sekta ya kilimo. Lengo likiwa ni kukiwezesha kilimo chetu kiwe cha kisasa na cha kibiashara kupitia Sera ya Kilimo (2013) pamoja na Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo (ASDP II) ambazo zinaweka mkazo katika kuongeza tija katika uzalishaji, kuongeza thamani ya mazao na kuweka mazingira wezeshi ya kiuzalishaji na kiuwekezaji. Katibu Mkuu amesema lengo hilo, mkazo umewekwa katika kuhakikisha kunakuwa na uwekezaji zaidi katika Sekta ya Kilimo ili kuongeza bidhaa za viwandani kwa kutumia zana bora za kilimo, pembejeo za kilimo hususan mbegu bora, mbolea na madawa ya kudhibiti visumbufu vya mimea. 

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Zana za Kilimo, Mhandisi Joseph Lubilo amesema katika kipindi kirefu nchini kumekuwepo na changamoto mbalimbali zinazohusiana na matumizi ya zana za kilimo. Miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na ubora hafifu wa mashine na zana za kilimo zinazoingizwa na kutengenezwa nchini; Ugumu wa upatikanaji na bei kubwa ya vipuri; kukosekana kwa Vituo vya kutoa huduma baada ya mauzo karibu na watumiaji wa zana za kilimo na kukosekana kwa ujuzi wa kutosha kwa Waendesha mitambo na masharti magumu ya upatikanaji wa mikopo ya zana za kilimo.

 Mhandisi Lubilo amesema sheria inayokuja ina lengo la kuboresha changamoto hizo na kwamba Mkulima atakuwa salama na atalindwa Kisheria tofauti na ilivyokuwa hapo kabla. Mhandisi Lubilo amekaririwa akisema “Baadhi ya faida tunazotarajia kuziona mara sheria hii ikipita ni pamoja na Wakulima watapata zana bora za kilimo zinazokidhi viwango kwa wakati; Kutaongezeka matumizi bora ya zana za kilimo na kuwawezesha wakulima kuzalisha kwa tija na kibiashara;Kutaimarishwa huduma za zana za kilimo kabla na baada ya mauzo ikiwa ni pamoja na mafunzo, matengenezo na usambazaji wa zana na vipuri na pia itasaidia kuangalia mahitaji muhimu ya zana kwa Wakulima wadogo wa Kati na Wakubwa. Mkutano huo muhimu wa Wadau wa Zana za Kilimo nchini ulianza jana katika Ukumbi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dar es Salaam na umefungwa leo. 
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew Mtigumwe
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew Mtigumwe aliyevaa koti la kahawia katikati akiwa pamoja na Mhandisi Peter Chisawilo kulia kwake ambaye alikuwa Mwenyekiti wa mkutano huo sambamba na Wadau wa Zana za Kilimo mara baada ya kuufungua mkutano huo jana katika ukumbi wa Mvuvi House, Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Zana za Kilimo Wizara ya Kilimo, Mhandisi Joseph Lubilo akitoa maelezo ya utangulizi kwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew Mtigumwe aliyevaa koti la kahawia katikaki akiwa pamoja na Mhandisi Peter Chiswalo kulia kwake ambaye alikuwa Mwenyekiti wa mkutano huo, jana katika ukumbi wa Mvuvi House, Jijini Dar es Salaam

MRADI WA LTA WAMALIZA MIGOGORO YA ARDHI KATIKA KIJIJI CHA MAGUBIKE KWA KUTOA HATI MILIKI ZA KIMILA

$
0
0
Mwenyekiti wa halmashauri ya iringa Stephen Mhapa akiwa na mkurugenzi wa mradi wa feed the future Malaki Msingwa wakati wa kukabidhi hati miliki za kimila kwa wananchi wa kijiji cha Magubike kilichopo kata ya Nzii mkoani Iringa 
Mwenyekiti wa halmashauri ya iringa Stephen Mhapa akiwa na mkurugenzi wa mradi wa feed the future Malaki Msingwa wakimkabidhi hati mmoja wa wananchi wa kijiji cha Magubike
Mwenyekiti wa halmashauri ya iringa Stephen Mhapa akiwa na mkurugenzi wa mradi wa feed the future Malaki Msingwa wakicheza nyimbo za asili pamoja na wananchi wa kijiji cha Magubike wakati wa ugawaji wa hati za kimila



NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Migogoro ya ardhi katika kijiji cha magubike kata ya nzii wilaya ya iringa imebakia kkama historia baada ya mradi wa feed the future (LTA) kufanikiwa kupima ardhi na kuwakabidhi hatimiliki ya kimila kwa wananchi wa kijiji hicho.

Akizungumza wakatika wa kukabidhi hati hizo za kimila mwenyekiti wa halmashauri ya iringa Stephen Mhapa alisema kuwa kutolewa kwa hatimikili za kimila kunamaliza migogoro ya ardhi kwa wananchi wote waliopata hati hizo.

“Sasa tunaelekea kipindi cha kilimo ambapo ndio kuna kesi nyingi za mipaka ya ardhi, hivyo uwepo wa mradi huu wa LTA umetusaidia kumaliza kabisa migogoro ya ardhi naomba kuchukua nafasi hii kwa niaba ya serikali kuwashukuru kwa kazi mliyoifanya” alisema Mhapa 

Mhapa aliwaomba viongozi wa mradi wa LTA kuhakikisha wanapima vijiji vyote vya halmashauri ya wilaya ya Iringa ili kuondoa migogoro yote ambayo imekuwa ikirudisha nyuma maendeleo ya wananchi.

“Kama serikali ikisema ipime ardhi yote ni kazi nzito,kazi hii ilitakiwa kufanywa na serkali kutokana na ukosefu wa rasilimali fedha na rasilimali watu imekuwa tatizo kubwa kwa serikali hivyo lazima mpongezwe kwa kazi yenu mnayoifanya” alisema Mhapa

Aidha Mhapa alisema kuwa kutolewa ka hati miliki za kimila zinaondoa kabisa mfumo dume kwa kuwa kwa sasa wanawake nao wamepewa hati kutoka kwa waume zao.

“Akina mama walikuwa hawatambuliwi kutokana na mila zetu zilivyo lakini hii leo kupitia mradi wa feed the future (LTA) wanawake hii leo wanamiliki ardhi na kuondoa kabisa mfumo dume kwenye sekta ya ardhi na kuwa na maamuzi ya matumizi ya ardhi yao” alisema Mhapa

Mhapa aliwataka wananchi wa kijiji cha Magubike wazingatie kuzitunza hati miliki za kimila kwa kuwa sasa ni dhamana ya maisha yetu hivyo mnatakiwa kuwa makini kwa kuzitunza vilivyo hati hizo.Naye naibu mkurugenzi wa mradi wa feed the future Malaki Msingwa amesema kuwa kupatikana kwa hati hizo kunawakuwa na uhakika wa kumili ardhi ambayo huwezi kusumbuliwa na mtu yeyote Yule.

“mradi huo umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa kutoa Hati kwa usawa Wanawake na Wanaume” alisema Msigwa.Msigwa aliwapongeza wataalamu wa mradi huo kwa kuhakikisha wanawasaidia wananchi wa kijiji cha Magubike kupima maeneo yao na kupata hati miliki za kimila ambazo zitakuwa msaada mkubwa kwenye maendeleo ya kiuchumi.

“Baadhi ya miradi imeibuliwa wakati wa upimaji wa ardhi hivyo ni fursa sasa kwa wananchi wenyewe kuitumia vizuri ardhi waliyopimiwa na kupewa hati miliki za kimila na kwa kuwa asilimia fulani kijiji hiki kimepimwa hivyo wanaweza kuwa kijiji cha mfano kwa kuwapa maendeleo hata wawekezaji wazuri kwa faida yao” alisema Msigwa

Msigwa alisema kati ya vijiji hivyo 41 vitakavyotayarishiwa mipango ya matumizi bora ya ardhi na kila mwenye ardhi kupimiwa na kupewa hati miliki za kimila, vijiji 36 vipo wilayani Iringa na vitano vipo wilayani Mbeya.

“Baada ya kukamilisha zoezi la upimaji mashamba na urasimishaji wa kijiji chote cha Lupembelwasenga, hivi sasa mradi unaendelea na upimaji mashamba katika vijiji vya mradi ambavyo vipo wilayani Iringa” alisema Msigwa

WIZARA, IOM WAJADILI CHANGAMOTO ZA KUWARUDISHA WAKIMBIZI WANAOTAKA KUREJEA MAKWAO

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa (IOM), Dkt. Qassim Sufi (kulia), alipofika Ofisi Ndogo ya Wizara kujadili changamoto mbalimbali za kusafirisha wakimbizi wanaoendelea kurejea makwao baada ya kuimarika kwa amani katika nchi zao. Mazungumzo hayo yamefanyika leo jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa (IOM), Dkt. Qassim Sufi (kulia), akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, alipofika Ofisi Ndogo ya Wizara kujadili changamoto mbalimbali za kusafirisha wakimbizi wanaoendelea kurejea makwao baada ya kuimarika kwa amani katika nchi zao. Mazungumzo hayo yamefanyika leo jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

BENKI YA NMB YATOA MSAADA WA KOMPYUTA MIKOCHENI SEKONDARI DAR

$
0
0
 Mwanafunzi wa shule hiyo, Suleiman Khamu, akielezea teknolojia ya Tehama kupitia  kompyuta walizo kabidhiwa na benki hiyo.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd, akimkabidhi, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mikocheni, Salama Ndyetabura, moja kati ya kompyuta tano zilizotolewa na benki hiyo leo hii kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wa shule hiyo. Wa pili  kutoka kushoto ni Meneja wa benki hiyo, Tawi la Msasani, Halima Mcharazo. Wengine ni wanafunzi wa shule hiyo.

 Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd, akizungumza kwenye hafla hiyo..
 Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mikocheni, Salama Ndyetabura, akitoa taarifa ya shule hiyo kabla ya kupokea msaada huo.
 Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mikocheni, Salama Ndyetabura, akimkabidhi taarifa ya shule hiyo, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd.

 Mwanafunzi wa shule hiyo, Anwar Mohamed, akielezea teknolojia ya Tehama kupitia  kompyuta walizo kabidhiwa na benki hiyo.
Mwanafunzi wa shule hiyo, Thomson Athanas, akielezea teknolojia ya Tehama kupitia  kompyuta wazizo kabidhiwa na benki hiyo.Na 

 Meneja wa benki hiyo, Tawi la Msasani, Halima Mcharazo, akizungumza kwenye hafla hiyo.

 Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mikocheni, Salama Ndyetabura, akizunguza wakati akipokea msaada huo.
 Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd, akizungumza kwenye hafla hiyo.



BENKI ya NMB imetoa msaada wa kompyuta tano kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi kompyuta hizo, Dar es Salaam leo, Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd alisema kompyuta hizo zitachangia kuongeza ufanisi katika ufundishaji na ujifunzaji hasa kipindi hiki ambacho dunia inaongea zaidi juu ya sayansi na teknolojia.

"Kompyuta tunazozitoa leo hii ni sehemu ya mchango wetu kwa jamii tunaimani zitaweza kuleta matokeo chanya kwa wanafunzi hususani kwenye masomo ya Tehama" alisema Idd.Aliongeza kuwa kompyuta hizo tano zitasaidia kuimarisha mafunzo ya Tehama shuleni hapo na kuongeza uelewa mzuri wa masomo ya Tehama kwa wanafunzi wawapo shuleni na hata baada ya kumaliza masomo yao.

Idd alisema kuwa kompyuta hizo ni sehemu ya kompyuta 150 zinazopelekwa mashuleni kwa mwaka huu ambapo pia katika Wilaya ya Same wamebahatika kupata mgao wa kompyuta tano.

Akizungumzia kuhusu benki hiyo alisema ndiyo inayoongoza nchini kwa kuwa na matawi mengi kwani ina matawi zaidi 228, ATM zaidi ya 800 nchi nzima, NMB wakala zaidi ya 6000 pamoja na idadi ya wateja zaidi ya milioni 3 idadi ambayo ni hazina kuwa ukilinganisha na benki zingine na kuwa imezifikia wilaya zote kwa asimilimia 100 pamoja na kuboresha huduma za kibenki kwa njia ya mtandao ili kufikisha huduma za kibenki kwa wananchi wengi.

Mkuu wa shule hiyo, Salama Ndyetabura akipokea msaada huo alisema kwa nyakati tofauti shule hiyo imepokea misaada mbalimbali kutoka kwa wadau wa elimu yenye thamani ya sh.milioni 108,516,780 katika kipindi cha Januari 2015 hadi Oktoba 2018.

Alisema kwa msaada huo walioupokea kutoka Benki ya NMB, umeonesha dhamira ya dhati katika kuunga mkono nia ya dhati ya Rais Dkt.John Magufuli ya kutoa elimu ya msingi bila malipo yoyote kwa watanzania.

Katika hatua nyingine Ndyetabura alisema kwamba katika kuhakikisha wanafanikiwa kitaaluma shule hiyo ilipata wafadhili ambao waliwapatia kompyupa tano na kuwaunganisha kwenye mkongo wa Taifa huduma ambayo inawawezesha kupata makala na mambo mbalimbali na kufundisha kwa njia ya mtandao ambapo ameiomba benki hiyo kuwasaidia kwa mara nyingine kupata Projekta ambayo itasaidia kufundisha wanafunzi kwa njia ya teknolojia kwa urahisi zaidi kufundisha masomo yote ambapo wataweza kutekeleza sera ya elimu ya mwaka 2007.

BENKI YA EXIM YATOA MILIONI 10/- KUSAIDIA KAMBI MAALUM YA TAFITI ZA MAGONJWA

$
0
0
 Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano Exim Bank Ndugu Stanley Kafu  (wan ne kulia) akikabidhi Mfano wa Hundi ya Shilingi Millioni 10 kwa kamati tendaji ya “Rotary Oyster Bay Corporate Cricket Gala 2018” ikiwa ni sehemu ya kuchangia kambi maalumu ya tafiti za magonjwa mikoani inayoendeshwa na taasisi hiyo ya Rotary.

Mrembo OFFICIAL LYYN aja kivingine na Mziki wa Bongo Fleva.

Washindi wa Tigo Jigiftishe Moshi na Arusha wakabidhiwa fedha zao

$
0
0

Mratibu wa Usambazaji na Tigo Pesa Mkoa wa Kilimanjaro Wolfgan Miraro akimkabidhi mfano wa Hundi ya Shilingi milioni moja mmoja wa washindi wa Promosheni ya Jigftishe Yussuph Miraro kutoka mkoani Arusha.
Mratibu wa Usambazaji na Tigo Pesa Mkoa wa Kilimanjaro Wolfgan Miraro akimkabidhi mfano wa Hundi ya Shilingi milioni moja mmoja wa washindi wa Promosheni ya Jigiftishe mkazi wa Moshi mkoani Kilimanjaro Hilda Lema.
Mratibu wa Usambazaji na Tigo Pesa Mkoa wa Kilimanjaro Wolfgan Miraro akimkabidhi Mkazi wa Moshi mjini, mkoani Kilimanjaro Albina Mmbaga mfano wa Hundi ya Shilingi milioni moja baadaya kufanikiwa kuibuka mshindi wa Promosheni ya Jigiftishe.
Mratibu wa Usambazaji na Tigo Pesa Mkoa wa Kilimanjaro Wolfgan Miraro (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa zawadi ya shilingi milioni moja wlizoshinda kupitia promosheni ya Tigo Jigiftishe kutoka mkoa wa Kilimanjaro na Arusha muda mfupi baada ya kuwakabidhi zawadi zao mjini Moshi jana.

Wafanyabiashara wajazwa mamilioni kwa kufanya miamala

$
0
0
Mmoja wa washindi wa promosheni ya ‘Shinda mtaji’, Godfrey Kitende akionesha hundi ya Sh milioni moja aliyoshinda baada ya kukabidhiwa jana na Kampuni ya Selcom inayoshirikiana Mastercard kutoa zawadi kwa wafanyabiashara wanaotumia huduma ya Masterpass QR.
Mmoja wa washindi wa promosheni ya ‘Shinda mtaji’, Godfrey Kitende akipokea hundi ya Sh milioni moja kutoka kwa Meneja Masoko wa Kampuni ya Selcom, Juma Mgori. Kampuni hiyo inashirikiana Mastercard kutoa zawadi kwa wafanyabiashara wanaotumia huduma ya Masterpass QR


Kampuni ya Selcom kwa kushirikiana na Mastercard imetoa zawadi ya Sh milioni tatu kwa wafanyabiashara wanaotumia huduma ya Masterpass QR katika kupokea malipo mbalimbali kwenye maeneo yao ya biashara. 

Zawadi hizo zimetolewa jana katika promosheni ya “Shinda Mtaji” iliyoanza rasmi Novemba mwaka huu kwa lengo la kuwarahisishia wafanyabiashara hao kutumia huduma ya Masterpass QR kufanya miamala mbalimbali. 

Akizungumza promosheni hiyo, Meneja Masoko wa Selcom, Juma Mgori alisema promosheni hii inamuwezesha mfanyabiashara kujishindia Sh milioni moja kila wiki kwa muda wa miezi mitatu kuanzia Novemba mwaka huu hadi Januari mwaka 2019. 

Aidha, aliwataja wateja walioshinda milioni moja kila mmoja kuwa ni Boaz Wales, Hamisi Kilenga wote wa mkoani Dar es Salaam na mfanyabiashara mmoja kutoka Arusha. 

Alisema kila mfanyabiashara atakayejiunga na Masterpass QR na kuanza kupokea miamala kutoka kwa wateja, ataingia moja kwa moja kwenye droo ya promosheni kwa wiki hiyo na kupata nafasi ya kujishindia hivyo kumuwezesha kujiongezea mtaji wa biashara yake. 

“Masterpass QR ni huduma inayomuwezesha mteja kufanya malipo ya bidhaa na huduma mbalimbali kutoka kwenye akaunti ya simu au akaunti ya benki kwa kuingiza Pay Number ya mfanyabiashara au ku-skani kodi ya QR iliyopo kwenye eneo la mfanyabiashara kwa kutumia Smartphone. 

“Kupitia huduma ya Masterpass QR, mteja ataweza kufanya malipo kupitia mitandao ya simu kutoka Tigo Pesa, M-Pesa, Airtel Money, Halopesa, Ezypesa na Selcom Card. 

Aidha, alisema kwa upande wa huduma ya mobile banking mteja ataweza kufanya malipo kutoka Access Bank, I&M Bank, NBC Bank, Akiba Commercial Bank, Amana Bank, BancABC, Canara Bank, Exim Bank, TPB Bank, NMB Bank, FINCA Microfinance Bank na Standard Chartered Bank. 

“Wateja wa benki hizo pia wataweza kupakua Masterpass Tanzania App kupitia Smartphone na kujisajili ili kufanya malipo kwa Masterpass QR moja kwa moja kutoka kwenye akaunti zao za benki,” alisema. 

Aliongeza kuwa ili mfanyabiashara aweze kusajiliwa na huduma ya Masterpass QR atatakiwa kujaza fomu ya kujiunga ambayo inapatikana kwenye ofisi za Selcom, atawasilisha leseni ya biashara, hati ya TIN na kitambulisho chake na itachukua siku 2 hadi 3 kuunganishwa na huduma ya Masterpass QR,” alisema. 

Mmoja wa washindi hao Boazi Walesi alisema huduma ya Masterpass QR imemwezesha kuwaondoa adha ya kubeba fedha taslimu au kuwa na kadi ya benki muda wowote wanapohitaji kufanya malipo. 

“Pia imeondoa usumbufu na gharama pamoja na kuleta usalama kwa wafanyabiashara ambao walikuwa wakikaa na fedha nyingi sehemu zao za biashara,” alisema. 

Naye Hamisi Kitenga alisema mfanyabiashara anapojiunga kutumia huduma hiyo fedha za mauzo ya siku zitatumwa kwenye akaunti yake ya benki au simu siku hiyo hiyo baada ya siku ya kazi kuisha.

WAZIRI MKUU ATEMBELEA TIC AITAKA IMALIZE URASIMU

Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images