Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

MKUTANO WA WADAU WA MAENDELEO ,MAAFISA WA SERIKALI NA MFUKO WA MAENDELEO YA JAMII-TASAF WAANZA JIJINI DAR ES SALAAM.

0
0
Na. Estom Sanga-DSM 

Mkutano wa siku tano utakaojadili utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF umeanza jijini Dar es salaam baada ya kukamilika kwa ziara katika maeneo ya utekelezaji wa Mpango huo katika mkoa wa Mwanza na kisiwa cha Unguja. 

Mkutano huo unaowashirikisha Wadau wa Maendeleo wanaochangia utekelezaji wa Mpango huo,Maafisa wa Serikali kuu na baadhi ya halmashauri na Wafanyakazi wa TASAF hufanyika kila baada ya miezi sita kwa kutembelea maeneo ya utekelezaji wa Mpango na kuona mfanikio na changamoto za utekelezaji kwa lengo la kuleta ufanisi zaidi. 

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bwana Ladislaus Mwamanga amesema kazi kubwa iliyoko mbele ya Mfuko huo,Wataalamu, Wadau wa Maendeleo ni kuhakikisha kuwa maelekezo ya Serikali ya kuweka utaratibu mzuri wa kuwashirikisha walengwa katika kufanyakazi kupitia Mpango wa Ajira ya Muda unazingatiwa kwa ukamilifu. 

Bwana Mwamanga amesema licha ya mafanikio makubwa ya utekelezaji wa Mpango huo unaojumuisha takribani Kaya za Walengwa zipatazo Milioni Moja na Laki Moja , bado kuwa idadi kubwa ya Wananchi walioko nje ya Mpango ambao wamekuwa wakiomba kujumuishwa ili nao pia waweze kunufaika na sera hiyo ya serikali ya kupambana na umaskini.

Amesema katika awamu ya pili ya utekelezaji wa Mpango huo inayotarajiwa kuanza mapema mwakani, suala la kushirikisha Walengwa hasa wenye uwezo wa kufanya kazi za maendeleo litapewa uzito mkubwa . 

Taarifa ya Utekelezaji kutoka TASAF makao makuu na baadhi ya Maeneo ya Utekelezaji wa Shughuli za Mpango inayonyesha kuweko kwa mafanikio makubwa kwa Walengwa kuanza kuboresha maisha yao kwa kutumia huduma za Mpango hususani katika nyanja za Elimu, Afya,Makazi na shughuli za uzalishaji mali kama ufugaji wa kuku, mbuzi na ng’ombe ambazo zimewaongezea kipato ikilinganishwa na hali ilivyokuwa kabla ya kujumuishwa kwenye Mpango huo wa Kunusuru Kaya Maskini.

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Bw. Ladislaus Mwamanga (aliyesimama) akimkaribisha Kiongozi wa Shughuli za TASAF katika Benki ya Dunia Bw. Mohamed Muderis (aliyeketi) kuzungumza kwenye mkutano wa Wadau wa Maendeleo,Maafisa wa Serikali na TASAF jijini Dar es salaam.

Kiongozi wa Shughuli za TASAF katika Benki ya Dunia, Bw. Mohamed Muderis (aliyesimama) akizungumza na Wadau wa Maendeleo, Maafisa wa Serikali na TASAF (hawapo pichani) mwanzoni mwa mkutano unaojadili utekelezaji wa Shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini jijini DSM.


Picha ya chini na juu ni baadhi ya Wadau wa Maendeleo , Maafisa wa Serikali na TASAF wakiwa kwenye mkutano unaojadili utekelezaji wa Shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ulioanza leo jijini DSM.



Mtaalamu wa Habari na Mawasiliano wa TASAF,Bi. Zuhura Mdungi (mbele) akiwa katika mkutano wa Wadau wa Maendeleo na Maafisa wa Serikali na TASAF ambapo aliwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ulioanza leo jijini Dar es salaam.

NDUNGULILE AWAPA NENO TFDA

0
0

NSSF TPB KUENDELEZA MAHUSIANO MAZURI YA KIBIASHARA KWA TAASISI HIZO

0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii


Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Ndugu Willam Erio na Mtendaji Mkuu wa TPB Ndugu Sabasaba Moshingi wamekutana leo jijini Dar es Salaam na kufanya mazungumzo ili kuendeleza mahusiano mazuri ya kibiashara kwa Taasisi zao.

Wakuu wa Taasisi hizo walikutana katika ofisi ya NSSF Makao Makuu na walizungumza mambo mbalimbali ikiwemo namna ya kuboresha mahusiano ya biashara baina ya Taasisi hizo mbili ambazo zimekuwa zikifanya huduma kwa muda mrefu.

Katika mazungumzo hayo Mkurugenzi mkuu wa NSSF Ndugu William Erio alimuahidi Mkurugenzi mtendji wa TPB aendelee kutarajia biashara yenye tija

Nae Mkurugenzi mkuu wa TPB Sebastia Moshingi amesema atawashawishi wastaafu wote wa NSSF waliokuwa wakilipwa pensheni zao kupitia Shirika la Posta wafungue Akaunti TPB ili waweze kufaidika na huduma mpya ya kulipa wastaafu wa NSSF ambapo mstaafu atalipwa pensheni yake moja kwa moja kwenye akaunti yake ya Benki hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Ndugu Willam Erio na Mtendaji Mkuu wa TPB Ndugu Sabasaba Moshingi wakiwa katika picha ya pamoja na kupeana mikono mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo ya ushirikiano wa huduma baina ya Taasisi wanazoziongoza
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Ndugu Willam Erio na Mtendaji Mkuu wa TPB Ndugu Sabasaba Moshingi pamoja na watendaji wamashirika yote mawili wakiwa katika kikao cha kujadili huduma watakazoshirikiana.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Ndugu Willam Erio na Mtendaji Mkuu wa TPB Ndugu Sabasaba Moshingi wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa mashirika wanayo yaongoza.

KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA ZANZIBAR ATILIANA SAINI NA MAKAMU WA RAIS HOSPITALI YA NANJING DRUM TOWER ZANZIBAR

0
0
 Katibu mkuu Wizara ya Afya Asha Ali Abdalla kushoto akitiliana saini na Makamu wa Rais wa Hospitali ya Nanjing Drum Tower ya China Yu Cheng Gong kuhusiana na Mradi wa kuchunguza Kansa ya Shingo ya kizazi,hafla iliofanyika Wizara ya Afya Zanzibar.
 Katibu mkuu Wizara ya Afya Asha Ali Abdalla kushoto akibadilishana hati ya  saini na Makamu wa Rais wa Hospitali ya Nanjing Drum Tower ya China Yu Cheng Gong kuhusiana na Mradi wa kuchunguza Kansa ya Shingo ya kizazi,hafla iliofanyika Wizara ya Afya Zanzibar. 
Mkurugenzi Tiba Hospitali ya Mnazi Mmjoa Dkt,Juma Salum, Mbwana kulia akikabidhiwa mashuka na Katibu wa Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar ZSTC Ali Hilal Vuai yaliotolewa msaada na shirika hilo kwa Hospitali mbalimbali za Wilaya Zanzibar.

PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

UPANUZI WA BANDARI GATI NAMBA MOJA WAFIKIA ASILIMIA 100

0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Upanuzi wa bandari ya Dar es Salaam umefikia hatua nzuri baada ya kukamilka kwa upanuzi wa gati namba moja kwa asilimia 100 huku meli ya kwanza ikitarajiwa kutia nanga wiki moja ijayo ikishuhudiwa na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano.

Hayo yameelezwa jana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Mhandisi Deusdediti Kakoko, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi wa Sh. bilioni 336.7 wa upanuzi wa bandari hiyo.

Amesema upanuzi huo umeiongezea uwezo gati hiyo yenye urefu wa mita 192 wa kubeba meli kubwa mbili za tani 45,000 hadi tani 60,000 kwa wakati mmoja kutokana na kuongezewa kitako cha upana wa mita 11.5 kinachobebwa na nguzo imara za zege zilizochimbiwa mita 70 chini ya bahari.

Amesema baada ya mkandarasi kukabidhi gati hiyo siku chache zijazo atakabidhiwa na kuanza kazi ya upanuzi wa gati namba mbili inayotarajiwa kukamilika Machi mwakani na upanuzi utaendelea hadi kufikia gati namba saba.

Akizungumzia ujenzi wa gati ya magari (RoRo Berth) pamoja na yadi ya kuegesha magari amesema mradi huo ulitakiwa uwe umekamilika lakini mkandarasi alikutana na changamoto ya kuwepo kwa udogo mbaya na hivyo kulazimika kutafuta udogo mzuri na kuujaza na kwamba ujenzi unatarajiwa kukamilika na kukabidhiwa Juni mwakani.

Kakoko amesema kukamilika kwa gati hiyo kutaiwezesha bandari hiyo kupokea magari 10,000 kwa siku kutoka uwezo wa kupokea magari 2500 na kwa mwaka itakuwa magari 200,000 kutoka magari 90,000.

"Kukamilika kwa gati hii kutaleta mapinduzi makubwa kwani tunàweza kupokea meli ya magari 3000 hadi 5000 na ikapakuliwa kwa siku moja tu," amesema na kusisitiza;"Ndugu wananchi na wadau hasa mawakala wa meli wakae mkao wa kula waachane na siasa za kuambiwa meli zina subiri sana hapa tuna meli 12 tu na zilishawahi kufika 18 tu naomba wananchi wawe na amani serikali yao inafanya kazi."

Ameongeza kuwa upanuzu wa gati utaenda sambamba na upanuzi wa lango la bandari kwa kuongeza kina kutoka mita 10 hadi 16 ambapo kwa sasa unafanyika usanifu na ifikapo Juni mwakani uchimbaji utaanza rasmi.

"Nia yetu ni hadi kufikia Disemba mwakani tuwe na gati kuanzia sifuri hadi namba tatu na upanuzi wa lango uwe umekamilika ili tuweze kupokea meli za kimataifa zenye kina cha mita 15 na uwezo wa kubeba hadi makasha 6000 kutoka meli za sasa zinazoweza kubeba makasha 2500 tu," alisema Kakoko.

Aliongeza, "Watu wa meli wajiandae hapa meli zitakuwa zinapishana kama daladala zinavyopishana, bandari hii ipo kwenye eneo ambalo Mungu amelibariki kijografia katika ukanda huu kuanzia Misri hadi Afrika Kusini na kwa sasa biashara ya dunia imehamia upande wa Mashariki kutoka Magharibi.

"Hivyo miaka mitatu ijayo tuna uhakika wa kurudisha ule utukufu wa bandari ya Dar es Salaam," alisisitiza.

Akifafanua zaidi kuhusu mradi huo Mkurugenzi wa Huduma za Uhandisi TPA, Charles Ogale, alisema mradi huo unahusisha uongezaji wa kina cha kutoka mita sita hadi mita 12.9 kutoka usawa wa bahari baada ya maji kupwa, upana wa mita 34 na itakuwa na urefu wa mita 320 pamoja na ujenzi wa yadi yenye ukubwa wa mita za mraba 69,000.

Alisema mradi mzima wa upanuzi wa gati ya magari ambayo ni 'zero berth' hadi gati namba saba ulioanza Juni 2017 unatarajiwa kukamilika Juni 29 2020."Upanuzi huu umeiongezea gati uwezo wa kubeba meli kubwa zaidi pasipo kupata misukosuko yeyote ," amesema.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Mhandisi Deusdediti Kakoko, akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya mradi wa upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam. 
Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Fredy Lihundi, akifafanua jambo
Wakandarasi wanaofanya upanuzi katika Bandari ya Dar es Salaam, wakijadili jambo katika mradi huo na viongozi wa TPA.
Mtambo wa kuchimba kina cha Bahari ukimwaga mchanga nje ya bahari katika Bandari ya Dar es Salaam.

TUSIMAMIE WAKANDARASI WANAOJENGA MJI WA SERIKALI DODOMA

0
0
Manaibu Mawaziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wamefanya ziara ya kutembelea na kukagua kiwanja kilichotolewa kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya Wizara hiyo ambapo Serikali imetoa shilingi bilioni moja kwa kila Wizara na kuelekeza kuwa ifikapo mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka huu Wizara zote ziwe zina majengo yake ya ofisi kwenye mji wa Serikali uliopo Ihumwa mkoani Dodoma.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa akiambatana na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akiwa na Katibu Mkuu wa Mawasiliano Mhandisi Dkt. Maria Sasabo na wataalamu wa Wizara hiyo wametembelea na kukagua eneo lenye ukubwa wa ekari 6.3 ambalo limetengwa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano lililopo Ihumwa mkoani Dodoma ambalo litagharimu jumla ya shilingi bilioni 1.120 na litajengwa na Vikosi vya Ujenzi, tawi la Dar es Salaam.

Kwandikwa amesema kuwa Serikali imetupa dhamana kubwa ya kuwa wakandarasi na kusimamia majengo ya Wizara zote, sisi kama Wizara tujenge vizuri kweli kweli ili tuwe mfano wa kuigwa na Wizara nyingine na tusimamie wakandarasi wengine wa JKT, NHC ambao wamepewa jukumu la kujenga ofisi za Wizara nyingine kwa kuwa sisi ndio wenye dhamana ya kusimamia wakandarasi wote nchini kama lilivyo agizo la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa kassimu Majaliwa. Ameongeza kuwa tuko tayari kukesha na kukesha ili kuhakikisha kuwa tunafanya kazi usiku na mchana.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) na Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa (wa pili kulia) wakisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Katibu Mkuu Mawasiliano Mhandisi Dkt. Maria Sasabo (hayupo pichani) kuhusu eneo linalojengwa ofisi ya Wizara kwenye mji wa Serikali, Ihumwa, Dodoma.
Katibu Mkuu Mawasiliano, Mhandisi Dkt. Maria Sasabo (wa kwanza kulia) akifafanua  jambo kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kushoto) wakati wa ziara ya kukagua eneo linalojengwa ofisi ya Wizara hiyo kwenye mji wa Serikali Ihumwa, Dodoma.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kulia) na Naibu Waziri wa Ujenzi Elias Kwandikwa (wa tatu kushoto)  wakisikiliza taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Barabara Wizarani Mhandisi Hapiness Mgalula kuhusu mipango ya ujenzi wa ofisi ya Wizara hiyo kwenye mji wa Serikali Ihumwa, Dodoma.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa (wa kwanza kulia) na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kulia) wakitembea kukagua eneo kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya Wizara hiyo kwenye mji wa Serikali Ihumwa, Dodoma.

TFDA YAFUNGUA MAFUNZO YA WACHUNGUZI WA MAABARA ZA DAWA KWA BARA LA AFRIKA

0
0

   NaEmmanuel Masaka,Globu ya jamii

MAMLAKA ya Chakula na Dawa nchini Tanzania(TFDA) imefungua mafunzo ya wachunguzi wa maabara za dawa kwa nchi za Afrika jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam katika Mkutano wa Kanda kwa nchi za Afrika, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Dk.Faustine Ndugulile ameeleza kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wachunguzi wa Maabara .

Dk.Ndugulile ameeleza kwa sasa duniani kumekuepo na usugu mkubwa  kwenye baadhi ya vyakula ambavo haviivi vizuri au  walaji wa nyama na mayai kutochunguza kwa makini kama kuna asilimia yoyote ambayo italeta madhara Kwenye miili yao pindi watakapokula vyakula ambavo si salama kwa afya zao.

Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya dawa na chakula ( TFDA)Adam Fimbo amefafanua zaidi kuwa lengo la mafunzo hayo si tu  kuwajengea uwezo wachunguzi wa maabara bali pia kutoa elimu kwa jamii jinsi gani wanatakiwa kuepuka vyakula ambavo vitaleta madhara baadae katika miili yao.

Fimbo amesema washiriki wa mafunzo hayo wapo 30 na nchi ambazo zinazoshiriki ni 22.Baadhi ya nchi hizo ni Algeria, Angola, Benin, Botswana, Burkina Faso, Burundi, Chad, DRC, Egypt, Kenya,Madagascar, Malawi, Mali, Mauritania, Morocco, Nigeria, SieraLeone, South Africa, Sudan, Uganda,  Tanzania na Zimbabwe.


Pia amewasisitiza  washiriki kuzingatia mafunzo hayo kwa ajili ya kunusuru na kupunguza kabisa uwezekano wa baadhi ya magonjwa ambayo si ya lazima endapo tutaweza kuyapatia ufumbuzi mapema .
Naibu waziri wa Afya maendeleo Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Dk.Faustine Ndugulile akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wachunguzi wa maabara za dawa kwa nchi za Africa, leo jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi wa TFDA,Adam fimbo akizungumza na waandishi wa habari (hawapi pichani) leo jijini Dar es Salaam katika mafunzo ya kuwajengea uwezo wachunguzi wa maabara za dawa kwa nchi za africa.

Makamu Mkurugenzi wa Maabara kutoka Nigeria Dkt.Flosade Oluwabamieo akifafanua jambo mbele washiliki wa mafunzo ya wachunguzi wa maabara za dawa leo jijini Dar es Salaam.


Sehemu ya washiriki wakimzikiliza Naibu Waziri wa Afya Maendeo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dr. Faustine Ndungulile (hayupo pichani) alipokua akifungua mafunzo ya wachunguzi wa maabara za dawa kwa nchi za Africa, leo jijini Dar es Salaam.(picha na Emmanuel Massaka wa MMG)

WAZIRI MKUU AFUNGUA MAFUNZO KWA WAKUU WA MIKOA NA MA’RAS

0
0

UJUMBE WA RAIS MAGUFULI KWA MAMLAKA YA MAPATO NCHINI

0
0

HUU NDIO UWEKEZEJI WA CHINA NCHINI TANZANIA

0
0

WAZIRI KAKUNDA AZUNGUMZIA UWEKEZAJI WA CHINA, MKURUGENZI MTENDAJI TIC APONGEZA TAMKO LA RAIS

0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Joseph Kakunda amesema China ndio nchi pekee ambayo imeweka fedha nyingi zaidi kwa ajili ya uwekezaji ambapo fedha waliyoweka kwenye kuwekeza ni Dola za Marekani bilioni 5.8 ambazo ni sawa na zaidi ya Sh.trilioni 12 huku akisisitiza umuhimu wa kujengwa kwa viwanda nchini ambako kutsaidia kuzalisha bidhaa nyingi ambazo zitauzwa nje ya nchi yetu.

Kakunda amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati mkutano uliowakutanisha wawekezaji kutoka nchini China, maofisa wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) pamoja na wadau mbalimbali wa sekta zinazojihusisha na uwekezaji nchini ambapo wametumia nafasi hiyo kujadili fursa za uwekezaji ambazo zipo nchini.

Akifafanua zaidi wakati anazungumzia ujio wa wawekezaji kutoka nchini China ambao wapo nchini kuangalia fursa za uwekezaji, amesema kuwa kwa sasa China ndio nchi ambayo imeweke fedha zake nyingi kwa ajili ya masuala ya uwekezaji ambao wamewekeza nchini.

"Nchi ya China au wawekezaji kutoka China ndio ambao wameka fedha nyingi sana katika maeneo ya uwekezaji.Wamewekeza kwenye viwanda vya aina mbalimbali, vimo viwanda vya saruji, viwanda vya kubangua kurosho na pia wapo pia kwenye uwekezaji katika eneo la ujenzi ambako nako huko wameweka fedha nyingi,"amesema Kakunda.

Amesisitiza pamoja na uwekezaji huo wa China ,Kakunda amefafanua mikakati ya Serikali ni kuhakikisha wawekezaji hao wa China wanajenga viwanda vingi nchini Tanzania na hiyo itasaidia katika kuongeza uzalishaji wa bidhaa ambazo zitauzwa nje ya nchi na kujipatia fedha nyingi.

Ameongeza kupitia ujenzi wa viwanda nchini Tanzania, kutakuwa na faida nyingi zikiwemo za nchi nyingine nazo kununua bidhaa zinazozalishwa nchini."Bado tunahitaji wawekeze zaidi kwenye uzalishaji bidhaa.Tukifanya hivyo tutakuwa tumepunguza urari wa kibiashara."

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TIC Geoffrey Mwambe ametumia nafasi hiyo kuzungumzia mazingira ya uwekezaji nchini ambayo ni tulivu na salama kwa wawekezaji kuwekeza.Pia amesema anapongeza na kuunga mkono tamko ambalo limetolewa na Rais Dk.John Magufuli jana akiwa mkoani Arusha kuhusu suala la kodi kuwa rafiki kwa wananchi wakiwamo wafanyabishara.

Mwambe amesema kuwa "Tunaunga mkono juhudi za Rais wetu ambaye jana tu ametoa tamko zito kuhusu suala la kodi, Rais amesisitiza mazingira ya uwekezaji nchini yawe salama na yenye kuvutia.Tamko kuhusu kodi naamini wawekezaji wengi na wafanyabiashara watakuwa wamelisikia na inaonesha namna ambavyo Rais hataki kuona kodi ambayo si rafiki.Tusilazimishe kukusanya kodi kwa siku moja na matokeo 
yake biashara zinafungwa."

Amesema kiongozi wa nchi amesisitiza kwenye ukusanyaji wa kodi kufanyika katika mfumo ambao utafanikisha zaidi ukusanyaji kodi ambao ni rafiki ili kuhakikisha kila mfanyabiashara au mwekezaji anamudu kodi ambayo anakadiriwa.

Wakati huo huo Godfrey Sembeye kutoka TPSF amesema sekta binafsi nchini 
imempongeza Rais Dk.Magufuli kwa kukemea tabia ya ukusanyaji kodi ambao si rafiki katika mazingira ya biashara na uwekezaji na kwamba kitendo cha Rais kuikemea TRA wananchi watakuwa na imani naye kwani wataamini anafahamu manyanyaso ambayo wanayapata kutokana na TRA.

"Tanashukuru Rais kwa tamko lake la jana kwani tumekuwa tukilalamikia 
manyanyasayo ambayo wafanyabiashara wamekuwa wakiyapata na hatimaye amesikia kilio chetu,"amesema Sembeye.

Kuhusu China amesema ni kama chai ambayo haipukiki na kwa kutambua umuhimu wao TPSF wameanzisha dawati maalumu kwa ajili ya kushughulikia raia Wachina waliko nchini kwenye masuala la biashara na uwekezaji kuhakikisha mambo yanakwenda sawa.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi(TPSF) Godfrey Sembeye akizungumza kwenye kongamano la uwekezaji baina ya wawekezaji waChina na Tanzania ambalo limefanyika leo jiiini Dar es Salaam.
 Baadhi ya  wawekezaji kutoka nchini China ambao wapo nchini wakiangalia fursa za uwekezaji wakimsikiliza Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Joseoh Kakunda wakati wa kongamano la uwekezaji kati ya China na Tanzania.wakimsiki
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini Tanzania(TIC)Geoffrey Mwambe (kulia) akiteta jambo na Balozi wa China nchini Tanzania Dk.Wang Ke wakati wa kongamano la uwekezaji ambalo limejumuisha wawekezaji wa nchi hizo mbili
 Mwenyekiti wa Baraza la Kukuza Uhusiano kati ya nchi zinazoendelea kutokana China Lyu Xinhua akizungumza kwenye kongamano la uwekezaji kati ya wawekezaji wa China na Tanzania leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Joseph Kakunda (kushoto)akiandika kabla ya kuzungumza kwenye kongamano la uwekezaji ambalo liliwahusisha wawekezaji kutokana nchini China ambao wamefika nchini kuangalia fursa za uwekezaji

ZIARA YA MBUNGE, NEEMA YAWASHUKIA WANA KOROGWE VIJIJINI

0
0


MBUNGE wa Korogwe vijijini Mh. Timotheo Mnzava amewataka wananchi wa jimboni kwake kuwa na uthubutu wa kuchangia miradi mbalimbali ya maendeleo ili kuipa nguvu serikali ili wapate kipaumbele katika kukamilisha miradi yao.
Ameyazungumza hayo akiwa katika ziara yake ya kata 29 ndani ya jimbo hilo ambapo ilianza tarehe 1 Disemba na kutarajiwa kumalizika tarehe 15 Disemba 2018.
IMG_8014
Aidha kufuatia kero na changamoto za jimbo hilo kuwa nyingi, Mnzava amewaomba wananchi kuainisha vipaumbele  ili kurahisha utatuzi wa kero hizo kuwa katika mtiririko unaofaa na kuepusha kugusa kila kero na hatimae kushindwa kuzimaliza kwa wakati.
IMG_7723
Aidha katika kata nne za Kalalani,Mashewa,Kizara na Foroforo ambazo tayari amezipitia, Mnzava ameahidi jumla ya Mifuko ya Simenti 270, ambapo katika mifuko hiyo 250 itatumika katika sekta ya afya na mifuko 20 katika sekta ya elimu pamoja na nondo 45 zitakazotumika kwenye ujenzi wa zahanati katika kata ya Foroforo.
IMG_7618
Aidha Mnzava amewataka wananchi kuondoa ukanda na ukabira ambao unapelekea kukwamisha shughuli za maendeleo ya korogwe vijijini na kuwaasa waishi katika misingi aliyoiachia baba wa taifa Mwalimu Nyerere juu kutanguliza utanzania na kuachanana tabia ya kubaguana kwa makabira.
IMG_7390
Aidha kufuatia ujenzi wa Hospitali ya wilaya inayotarajiwa kujengwa hivi karibuni, Mnzava amewataka wanachi kuunga juhudi za rais wa awamu ya tano dkt. John Magufuli anzozifanya katika kuboresha sekta ya afya, elimu pamoja na miundombinu akiwa na lengo thabiti la kuifikisha Tanzania katika uchumi wa kati ifikapo 2025.

BANC ABC YAWEKEZA KWENYE MAENDELEO YA WANANCHI.

0
0


Na Mwandishi wetu, Arusha.

Banc ABC nchini imeendelea na juhudi za kuwekeza kwenye maendeleo ya jamii kwa kutoa mikopo kwa wajasiriamali, kusaidia jamii kupata bima za afya ili kuharakisha maendeleo ya jamii nchini Tanzania.

Akizungumza jijini Arusha leo Meneja wa Banc ABC tawi la Arusha, Magabe Nyambuche amesema kwa mwaka huu 2019 wamejipanga kutoa mikopo kwa vikundi maalum vikiwemo vikoba na Saccos.

Vikundi mbalimbali vimekuwa vikipewa mafunzo na maafisa ustawi wa jamii ili waweze kunufaika na mikopo kwa kufanya shughuli za uzalishaji mali na kujinyanyua kiuchumi na taifa kwa ujumla.

Nyambuche amesema Banc ABC imekuwa karibu na jamii hata kuwafikia wananchi waliopo maeneo ya mbali kupitia ubunifu wa kutoa huduma za kifedha kwa njia ya mtandao na kuiwezesha benki hiyo kutwaa tuzo ya Ubunifu.“Tunamawakala 250 ambao wanahakikisha kuwa wateja wetu wanafikiwa na huduma za kifedha popote pale walipo,” alisema Nyambuche.

Banc ABC imedhamini mkutano mkuu wa wadau wamaendeleo yajamii jijini Arusha ikiwa ni juhudi mojawapo ya kusaidia jamii ambayo hunufaika na utaalamu wa Maafisa wa Maendeleo katika maeneo ya vijiji na mijini.

Pia, Banc ABC imejizatiti katika kuendelea kushirikiana na serikali kuharakisha maendeleo ya jamii kwa kutumia dhana ya uwezeshaji wamikopo yenye masharti nafuu.
Meneja wa Banc ABC tawi la Arusha, Magabe Nyambuche akizungumza jijini Arusha leo.


DKT. ASHATU KIJAJI AAGIZA MFANYAKAZI WA TRA DODOMA ASIMAMISHWE KAZI KWA KUKIUKA MAADILI YA KAZI

0
0

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akipewa maelezo na Meneja Msaidizi upande wa Ukaguzi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Mustapha Mkiramweri alipofanya ziara ya kushitukiza katika mmoja wa mitaa Jijini Dodoma, kusikiliza kero za wafanyabiashara zinazoelekezwa kwenye Mamlaka ya Mapato TRA mkoa wa Dodoma.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akipewa maelezo na Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Thomas Masese (kulia) alipokuwa akifanya ziara ya kuwatembelea wafanyabiashara na kujua changamoto wanazokumbana nazo kutoka kwa TRA mkoani Dodoma.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akiwa na Watumishi wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA), wakisikiliza malalamiko ya mteja kwa njia ya simu walipomtembelea ofisini kwake kujua changamoto wanazokumbana nazo kutoka kwa TRA mkoani Dodoma, baada ya mfanyabiashara huyo kuilalamikia TRA kumlazimisha kununua mashine za kutolea stakabadhi ya kielektroniki (EFD Machine)
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akiagana na mmoja wa viongozi waandamizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bi. Kabula Mwemezi, baada ya kufanya ziara ya kushitukiza katika mitaa ya Jiji la Dodoma kusikiliza changamoto wanazokumbana nazo kutoka TRA mkoani Dodoma.
Picha na Josephine Majura-Wizara ya Fedha na Mipango-Dodoma


Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma

NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, ameuagiza uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, kumsimamisha kazi maramoja mfanyakazi wake mmoja katika Ofisi ya TRA mkoa wa Dodoma, DANIEL KINGU, kupisha uchunguzi wa kuhusika kwake na tuhuma zinazomkabili za kumbughudhi mfanyabiashara mmoja Jijini humo.

Dkt. Kijaji, ametoa maagizo hayo baada ya kufanya ziara ya kushitukiza kwenye mitaa ya Jiji la Dodoma baada ya kupata malalamiko kutoka kwa mfanyabiashara mmoja kwamba amekuwa akipokea simu za vitisho kutoka kwa mfanyakazi huyo akishirikiana na watu wengine na kumtaka ampelekee shilingi laki 7 za kulipia mashine ya kutolea stakabadhi za kielektroniki (EFD Machine) la sivyo angefungiwa biashara yake.

“Mteja wetu awe salama!! na nitaendelea kufuatilia, lakini kuanzia muda huu Kingu aondoke ofisini, hatuwezi kuwavumilia watu wa jinsi hii hata kidogo kwa sababu kazi ya kuuza EFD machine si yake na anamwambia mteja aende ofisini kwake chumba namba fulani, anafanya haya mambo ndani ya ofisi ya Serikali, akitoka nje inakuwaje?” alihoji Dkt. Kijaji

Alisema hatasita kuchukua hatua hizo kwa wafanyakazi wengine wa Mamlaka ya Mapato popote walipo nchini wanaojihusisha na vitendo vya ukiukwaji wa maadili.

Naibu Waziri huyo wa Fedha na Mipango, amewataka watendaji wa TRA nchini kote kufanyakazi zao kwa kuzingatia maadili yao ya kazi, kukadiria kodi kwa haki, watumie lugha nzuri kwa wateja wao na kutoa elimu kwa umma kuhusu haki na wajibu wa wafanyabiashara katika masuala ya kodi badala ya kuwakadiria kodi kubwa isiyolipika.

“Ni lazima tuwalee wafanyabiashara hawa wadogo na ndio watakaotulipa kodi kubwa huko mbeleni badala ya kuwaumiza tangu wanapoanza biashara zao na ni lazima tuangalie viwango vyetu vya kodi tunavyotoza” Alisisitiza Dkt. Kijaji

Meneja wa TRA mkoa wa Dodoma, Bw. Thomas Masese, ameahidi kutekeleza maagizo hayo na kufanya uchunguzi wa kina kuhusu suala hilo huku naye akirejea wito kwa watumishi wa Mamlaka hiyo mkoani humo, kufanyakazi zao bila kuwanyanyasa wafanyabiashara pamoja na kutohusisha na vitendo visivyofaa ikiwemo kuomba rushwa

PROF. MBARAWA AAGIZA UJENZI WA TENKI LA MAJISAFI SARANGA

0
0
Waziri wa Maji Mhe. Prof Makame Mbarawa ameiagiza Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASA) kuanza ujenzi wa tenki la Maji safi lenye uwezo wa kuhifadhi Maji kiasi cha lita za ujazo milioni tano katika eneo la Saranga jijini Dar es salaam.

Alitoa maagizo hayo wakati alipotembelea katika maeneo ya Kimara Temboni na Saranga na kushuhudia changamoto ya upatikanaji wa huduma ya Maji safi katika maeneo hayo iliyosababishwa na jografia ya milima na kupelekea kuwepo kwa msukumo mdogo wa Maji katika maeneo hayo. Hali hiyo ilikuwa ikisababisha baadhi ya wakazi hao kukosa huduma ya Maji.

“Niwahakikishie kuwa mtapata huduma ya Maji safi kwa masaa 24 na siku saba kwa wiki kama maeneo mengine kwa kuwa nimewaagiza DAWASA wajenge tenki la Maji safi lenye ujazo wa lita milioni tano ambalo lita sambaza Maji katika eneo lote la Saranga. Tayari wameshaanza kazi ya kutafuta mkandarasi na baada ya muda mfupi ujenzi utaanza” alisema Prof. Mbarawa

Aidha kwa upande wa Afisa mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja amehaidi kutekeleza agizo la Waziri wa Maji kwa wakati ilikuendana na kasi na adhima ya serikali ya awamu ya tano ya kumtua mama ndoo ya Maji kichwani kwa kuwafikishia huduma hiyo karibu zaidi  ilikuondokana na kero ya kufuata huduma hiyo kwa umbali mrefu. 

Hata hivyo Waziri Mbarawa ameigiza pia DAWASA kuweka mitandao wa Maji safi kwa Maeneo yote yasiyokuwa na mitandao kabisa ili tenki hilo la Maji safi likikamilika liweze kunufaisha wakazi wote wa eneo la Saranga.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji  Prof Makame Mbarawa akionesha jambo kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji safi na Maji taka Dar es Salaam ( DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja ( wapili Kulia)  wakati alipotembelea maeneo la Saranga na Kimara Temboni na kuagiza kujengwa kwa Tenki la Maji litakalohudumia eneo hilo.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa akizungumza na wananchi wakati alipotembelea  maeneo ya Saranga na Kimara Temboni.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa  Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akielezea jambo kwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa wakati alipotembelea maeneo la Saranga na Kimara Temboni na kuagiza kujengwa kwa Tenki la Maji litakalohudumia eneo hilo.


WAZIRI MKUU MSTAAFU DKT SALIM ATOA SALAMU ZA RAMBI RAMBI KUFUATIA MSIBA WA RAIS WA ZAMANI WA MAREKANI

0
0
Waziri Mkuu Mstaafu na Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) Dr Salim Ahmed Salim leo asubuhi ametembelea ubalozi wa taifa la Marekani kutoa salamu za rambirambi kwa serikali na watu wa Marekani kutokana na msiba wa Rais wa 41 wa taifa hilo Bwana George W. H Bush. 
 
Mheshimiwa Salim ni mmoja wa watanzania wachache waliopata nafasi ya kufanya kazi na kumjua Marehemu Bush Snr wakati Mheshimiwa Salim alipokuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa na Rais Bush Snr akiwa Mwakilishi wa Kudumu wa Taifa la Marekani .

Moja ya mambo yaliyowakutanisha ni pamoja na harakati na hatimaye tukio la Taifa la China kurejeshewa haki na hadhi yake ya Uanachama wa Umoja wa Mataifa mnamo mwaka 1971.

Pichani Mheshimiwa Salim akipokewa na Kaimu Balozi wa Marekani Bwana Andy Karas na Naibu Kaimu Balozi Bwana Brian Rettmann.

Halotel, Biko kunogesha michezo msimu wa sikukuu.

0
0

      Na.Khadija seif,globu ya jamii

KAMPUNI ya Mawasiliano ya simu za mkononi ya Halotel nchini  imeingia katika makubaliano rasmi na kampuni ya michezo ya kubahatisha na kubashiri ya Biko ili kuongeza msisimko na ushiriki kwa wadau wa michezo hiyo nchini katika msimu wa huu sikukuu.

Akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya Ofisi za Halotel Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Halotel Mhina Semwenda amesema ushirikiano huu baina ya Kampuni ya Halotel na Biko utawezesha wateja wetu kuweza kushiriki na kupata fursa ya kujishindia fedha zitazowawezesha kujiongezea kipato na hivyo kuboresha maisha yao.

Pia ameeleza kuwa hii ni fursa kwa wateja  wote wa Halotel mijini na vijiini kuweza kushiriki katika michezo ya kubahatisha na kubashiri kama vile mpira wa miguu , mpira wa kikao,rugby,cricket,Tennis na mingineyo ambapo hapo kabla hawakuweza kupata fursa kushiriki katika michezo hiyo.

Kwa upande wake Meneja Masoko Biko Goodhope Heaven  amefafanua kuwa Biko ni kampuni kubwa na madhubuti inayojihusisha na michezo ya kubahatisha kwa kufanya miamala Kwenye simu za Mkononi.

Aidha heaven ameeleza ushirikiano huo utawezesha wateja wanaotumia mtandao wa Halotel kupitia huduma ya kifedha ya Halopesa kupata fursa ya kuvuna mamilioni kutoka Biko kwa kubahatisha na pia kubashiri matokeo ya michezo mbalimbali na Bikosports.

Biko inaendelea kusisitiza wabashiri kuanzia umri wa miaka 18 na kuendelea na mpaka sasa watu waliobashiri na kubahatika kushinda wameneemeka kwa kutokana na kushinda zawadi za fedha,pikipiki na nyuma aliongezea  heaven.
 Mkuu wa mawasiliano wa Halotel, Mhina Semwenda  akizungumza na waandishi wa Habari jinsi mteja wa Halopesa anavyoweza kujiunga na kushiriki katika michezo ya kubashiri inayoendeshwa na kampuni ya Biko. Pamoja nae kulia ni Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven (kulia) na Mkuu wa Biashara wa Halopesa Magesa Wandwi.
Meneja Masoko wa Biko Goodhope Heaven, akizunguzumza na  waandishi wa Habari  jinsi mteja wa Halotel  anavyoweza kushiriki mchezo wa bahati nasibu ya biko na kupata nafasi ya kushinda Nyumba na Mamilioni ya Biko katika msimu huu wa sikukuu (kulia) ni Mkuu wa mawasiliano Halotel, Mhina Semwenda (kushoto).

SPORTPESA YAENDELEA KUBORESHA MAISHA YA WATANZANIA

0
0


Promosheni ya Shinda Zaidi na SportPesa tayari imekabidhi bajaj 74 kwa Watanzania ambao hivi sasa maisha yao yamebadilika na kuwa ya juu kutokana na kujiongezea kipato kupitia bajaj wanazoshinda.Unataka na wewe uwe mmoja wa Watanzania walioboresha maisha yao? Ni rahisi sana unachotakiwa kubashiri matokeo ya michezo kupitia SportPesa pekee.

Kwani bado bajaj 26 zimebakia kwa washindi wa michezo ya kubashiri ya SportPesa, hivyo kama unataka ni kuanza kuweka ubashiri wako hivi sasa kupitia SportPesa.Katika mahojiano maalum na Meneja Uhusiano wa SportPesa, Sabrina Msuya ameizungumzia promosheni hiyo inayoendelea hapa nchini.

Unaizungumziaje mwitikio wa promosheni

“Ipo kubwa tofauti na mwaka jana ambayo ilianza kutokana na mwitikio mkubwa wa Watanzania wengi kubashiri michezo mbalimbali kupitia SportPesa.Hivyo, kutokana na mwitikio huo mkubwa tumeona tuongeze zawadi nyingine tofauti na bajaj hizo tunazozitoa na lengo ni kuwanufaisha Watanzania.

Washindi sita kwenda Hispania, UingerezaNi kati ya zawadi tutakazozitoa kupitia promosheni hii ya Shinda Zaidi na SportPesa, tofauti na bajaj tumepanga kutoa tiketi kwa washindi wetu kwenda kuangalia baadhi ya mechi za Ligi ya Uingereza na Hispania.

“Tiketi sita ndiyo tulizopanga kuzitoa kwa washindi wetu, wakiwa huko SportPesa itawagharamia kila kitu ikiwemo chakula, malazi na usafiri wa ndani kwa kipindi chote watakachokaa huko.“Na sisi ndiyo tutakaochagua mechi za kwenda kuzitazama huko Uingereza na Hispania, hivyo ubashiri ndiyo utakaowawezesha wao kupata nafasi ya kwenda huko kutazama ligi kubwa.

“Na washindi hao watasafiri kwenda kushuhudia ligi hizo Januari, mwakani baada ya promosheni hiyo kufikia kilele mwishoni mwa mwaka huu. “Zawadi nyingine tuliyoiongeza ya jezi za Simba na Yanga na simu za smartphone ambazo zinaendelea kutolewa kila siku kwa washindi wetu wanaoweka ubashiri wao kupitia SportPesa.

Utofauti upoje mwaka huu na mwaka jana

“Upo mkubwa na hilo limedhihirisha kutokana na washindi kupatikana kutoka mikoa mipya na hiyo imeonyesha ni jinsi gani watu wengi wanabashiri kupitia SportPesa.“Mwaka huu washindi wengi wametoka mikoa Mara, Dar es Salaam, Morogoro, Mwanza, Kigoma na Tanga lakini mwaka wa jana washindi wa bajaj wanatoka Makambako, Newela, Arusha ambao ulitoa bajaj zaidi ya 20.




Washindi waliopita wamefaidika vipi na promosheni hiyo?


“Kiukweli kabisa tunajivunia kama SportPesa, kwa kupitia promosheni hii tumefanikiwa kubadili maisha kwa Watanzania kupitia ushindi wao wa ubashiri wa matokeo.

“Mabadiliko yapo mengi kati ya hayo ni wamenunua viwanja na wengine wamejenga nyumba kwa kupitia bajaj wanazoshinda kupitia promosheni hii inayoendelea.

“Wengine wanawalipia ada watoto zao ambalo ndiyo jambo la msingi kuona watu wakiendelesha familia zao kupitia ubashiri wao.Promosheni hii inatoa ajira kwa Watanzania, kwani wapo baadhi ya washindi ni waajiriwa wanaposhinda bajaj wanapa watu wawafanyie biashara, hivyo utaona ni jinsi gani hapo tumehusika katika kuajiri.

“Pia, tumewasaidia Watanzania kujifunza mbinu za kufanya biashara kwani kabla ya kushinda bajaj hizo walikuwa hawafanyi biashara zozote, lakini wanaposhinda wanaanza kujifunza kufanya biashara kwa kupitia hizo bajaj.

Malengo yenu ni yapi?

“Ni kuona Watanzania wengi wakibadili maisha yao kupitia promosheni hii inayoendelea hapa nchini na kikubwa ni kuona wakifanya ujenzi wa nyumba, kununua viwanja na kuendeleza familia zao kupitia ushindi wa ubashiri wa matokeo kutoka SportPesa.

“Na hilo linawezekana kabisa, kikubwa wanachotakiwa kuanza kubashiri kuanzia leo na baada ya muda mchache wataona mabadiliko baada ya kushinda kupitia SportPesa.

“Kwani tayari tumewashuhudia Watanzania wakibadili maisha yao kupitia ubashiri huu unaoendelea ambao hivi sasa wanamiliki viwanja na nyumba kutokana na kipato wanachokipata kutokana na bajaj zao wanazoshinda.

Jinsi ya kujiunga na SportPesa

“Ili kujiunga na SportPesa, piga *150*87# au bofya www.sportpesa.co.tz kubashiri mechi kali kila siku kuanzia Sh. 1000 TU ukiwa na simu yoyote ya mkononi.

Jackpot yapanda

“Wiki hii Jackpot yetu imepanda mpaka shilingi 412,871,420/= ambapo mteja akibashiri kwa usahihi mechi 13, anazawadiwa bonasi kwa watakaobashiri kwa usahihi kuanzia mechi 10 hadi 12.

Huduma kwa wateja


0764115588
0685115588

0692115588

WAKILI MWAE AHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 5 AU KULIPA FAINI YA SHILINGI MILIONI 200

0
0
NaVero Ignatus ,Arusha

Hukumu ya kesi ya utakatishaji fedha haramu iliyokuwa inamkabili wakili maafuru Jijini Arusha Mediam Mwale imetolewa desema 3 na Jaji Isa Maige wa Mahakama kuu kanda ya Arusha ambapo amemuhukumu kwenda jela miaka mitano au kulipa faini ya shilingi milioni 200

Mshtakiwa analazimika kulipa faini na kama akishindwa atatumikia kifungo cha miaka mitano na kwa kipindi ambapo atakuwa hajakidhi matakwa ya adhabu hiyo atabaki kizuizini 

Jaji Isa ameiambia mahakama kuwa mshitakiwa Mediam Mwale amekiri makosa kwa hiari yake mwenyewe na kwamba hiyo ni dalili tosha ya kuwa ameungama na anajutia makosa na kukiri kwake kuna faida mbili katika mfumo mzima wa haki jinai mshtakiwa ameokoa muda na rasilimali za mahakama

Ameiambia mahakama kuwa kukiri kwa mshtakiwa wakwanza kumeondoa uwezekano kukwepa kwa njia za kiufundi hayo ameyazingatia kwani mshtakiwa ni kosa lake la kwanza siyo mkosaji sugu asiyeweza kurekebishika, kuungama kwake kunaonyesha kuwa yupo tayari kujirekebisha 

''kwa minajili hiyo muelekeo wa wa kujirekebisha ni hatua stahiki katika kutoa adhabu hiyo''''Mshtakiwa amekuwa kizuizini kwa zaidi ya miaka saba tangia alipokamatwa kama mambo yote yangeenda katika hali ya kawaida si ajabu kwamba mshtakiwa wa kwanza angelikuwa ameshahukumiwa na kutuikia kifungo cha zaidi ya miaka saba'' alisema Jaji Maiga

Akisoma hukumu hiyo Jaji Issa Maige Mahakama kuu kanda ya Arusha adhabu makosa 30 yanaomkabili mshatakiwa wa kwanza ambayo ni makosa ya kughushi kinyume na kifungu namba 337 kwa ambapo adhabu yake kifungo cha miaka 5 kwa kila kosa ,kughushi kinyume na kifungu namba 338 adhabu yake miaka 7 

Makosa mengine ni kuandaa nyaraka za kughushi adhabu miaka 2 kwa kila kosa,kukutwa na vitu vilivyopatikana kwa njia isiyosahihi miaka 2 kosa la 2,na 29 la utakatishaji fedha faini yake ni shilingi milioni 100 kwa kila kosa ,kosa la kula njama miaka 5 kwa kuzingatia ya kwamba takwa la kisheria 

Jaji Maige ameiambia mahakama kabla ya kutoa hukumu amezingatia hoja za upande zote mbili na maombi ya mawakili upande wa utetezi kuwa mshtakiwa ni mgonjwa, anawategemezi, mzazi wa miaka 78 na mtoto wa miaka 8, kukaa kizuizini zaidi ya miaka saba 

''Kama alivyosema Omari wakili wautetezi mshtakiwa ameokoa muda wa mahakama kama kesi ingesikilizwa upande wa jamhuri walipanga kuleta mashahidi 59 na vielelezo 64 baadhi ya mashahidi walitakiwa kutoka nje ya nchi bila shaka hili lingepelekea shauri hili kuchukua muda mrefu na kutumia gharama kubwa sana "alisema Jaji Maiga

Aidha Jaji Maiga ametoa ufafanuzi kuhusiana na amri ya kukamatwa kwa mali ziizopatikana kinyume cha sheria ameiambia mahakama wakili wa serikali aliiomba mahakama ifanye hivyo lakini wakili msomi kwa upande wa utetezi aona swala hilo ni busara likasubiri hadi maombi maalumu yatakapo fanyika

Jaji amesema kwa msingi wa sheria namba 351 cha sheria husika kinaruhusu  mahakama kuweza kutoa kama hiyo lakini kifungu kidogo cha (3)kwamba mahakama inatakiwa izingatie taratibu nyingine maalum ambazo zimewekwa kuhusiana na adhabu husika 

Katika makosa haya haswa la utakatishaji fedha sheria husika inazungumza katika kifungu kidogo cha 28 zinatoa utaratibu katika kifungu cha( 9)kwamba mwanasheria mkuu wa serikali anaweza akafanya maombi kwaajili ya kuhakikisha mali hizo zinakamatwa matakwa ya kisheria yanaonyesha wanaweza wahakusika watu wengine zaidi

''Kwakuwa zile mali hazijaainishwa bayana naona ni busara kama maombi haya yakifanyika kwa utaratibu wa kisheria ili yaweze kusikilizwa kwa umakini na kujua ni mali gani zinzpaswa kukamatwa''alisema

Kuhusiana na kughushi chini ya kifungu cha sheria namba 338 ambapo sheria imeruhusu moja kwamoja kutoa amri ya kukamatwa au kuteketeza nyaraka ambazo zimeghushiwa hivyo ametoa amri ya kamba nyaraka zote ambazo zimeghushiwa chini ya kifungu cha sheria namba 338 zikamatwe zote na ziteketezwe baada ya kuisha muda wa kukata rufaa

Amefafanua adhabu stahiki inayomsatahili mshtakiwa wa kwanza kwa kosa la kwanza ni njama ya kufanya kosa kinyume na kifungu namba 384 cha kanuni ya adhabu,ambapo adhabu ya juu kabisa ya kosa hilo adahabu ya miaka 7 au adabu inayoendana sawa na adahabu ya juu ya kosa husika,adhabu ya chini ni miaka 5

'' Mbali ya makosa yote ni miaka saba kwasasa mshtakiwa anatakiwa alipe faini ya kutakatisha fedha ambapo kila kosa atatakiwa kulipa shilingi milioni 100 akishindwa kulipa atakwenda kutumikia jela miaka mitano makosa yote aliyohukumiwa mahakama imezingatia muda wa kukaa kwake mahakamani akishindwa ''alisema

Wakili Mwale na wenzake wanatete watatu wanatetewa na Mawakili Omary Omary, Innocent Mwanga, Bukheri Ngoseki na Mosses Mahuna ,

Kwa upande wa Jamhuri unaongozwa na wakili mkuu wa serikali serikali wapo Osward Tibabyemkomamya,wakili mwandamizi Hashimu Ngole.

MICHAEL WAMBURA ARIPOTI TFF NA BARUA YA MAHAKAMA

0
0
Baada ya Mahakama Kuu kumrejesha kwenye nafasi yake ya Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) Michael Wambura Novemba 30, leo amewasili ofisini hapo kuripoti kwa mujibu wa Mahakama Kuu.

Wambura amesema kuwa majukumu yake aliyopewa na Mahakama Kuu ameyatekeleza hivyo kwa sasa yeye ni Makamu wa Rais wa TFF kwa kuwa hakufutwa cheo chake bali alifungiwa kutojihusisha na masuala ya soka. 

"Ofisini wengi nimekuta hawapo zaidi ya mkurugeni wa fedha, na wahudumu wengine wa chini, ila kikubwa nimeweza kutimiza masharti ya Mahakama ambayo kwanza ni kuripoti ofisini, pili naleta taarifa ya mahakama ambayo imepokelewa na nimeweza kufika, kama utekelezaji hautafanyika basi nitarejea mahakamani. 

"30 Novemba nilianza kazi baada ya mahakama kuu ilipotoa maagizo, cha msingi ni kwamba nilikuja kutoa taarifa kwamba mimi nipo, walinisimamisha kujihusisha na soka ila hawakufuta cheo changu cha umakamu wa rais," alisema. 

Machi mwaka huu Kamati ya Maadili ya TFF chini ya mwenyekiti wake, Hamidu Mbwezeleni ilimfungia maisha Wambura kutojihusisha na masuala ya soka kwa kumtuhumu kwa makosa matatu. Katika taarifa yake, TFF ilisema kwamba ilichukuwa hatua hiyo kwa mujibu wa kifungu cha 73(1) (c) cha Kanuni za Maadili ya TFF Toleo la 2013. 

Hiyo ni baada ya kikao chake cha Machi 14, mwaka huu ambacho pamoja na mambo mengine, kilimjadili Wambura aliyefikishwa kwenye Kamati hiyo kwa tuhuma za makosa matatu ya kupokea fedha za TFF malipo yasiyo halali, kugushi barua na kushusha hadhi ya TFF. 

Wambura alifikishwa kwenye Kamati ya Maadili na Sekretarieti ya TFF iliyodai baada ya Kamati ya Ukaguzi kukutana na kupitia mambo mbalimbali ya ukaguzi na suala hilo la Wambura ilionekana linatakiwa kufika kwenye Kamati ya Maadili. ”Nimefika hapa na barua yangu ambayo ilitolewa na mahakama na kutumwa TFF kuwa nirudishwe kazini na imepokelewa TFF na ikasainiwa kwahiyo leo nimekuja na itambulike kuwa nimeshaanza kazi tangu Novemba 30 siku ambayo uamzi wa mahakama ulitolewa”, amesema Wambura. 

Hata hivyo Wambura amesema licha ya kutowakuta viongozi wa juu, lakini yeye atafanya kazi kama kawaida kwasababu hakufungiwa kuwa makamu wa Rais bali alifungiwa kujihusisha na soka na uamzi huo umetenguliwa kwahiyo yupo huru kuendelea na nafasi yake. Aidha amesisitiza kuwa endapo hawatampa ushirikiano atarudi mahakamani kwenda kutoa taarifa kuwa maamuzi ya mahakama hayajatekelezwa. 

Wambura alifungiwa maisha kutojihusisha na soka, Machi 15, 2018, siku 10 kabla ya Machi 25, Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ilipomteua Athumani Nyamlani kukaimu nafasi hiyo ya makamu wa rais
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live


Latest Images