Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1741 | 1742 | (Page 1743) | 1744 | 1745 | .... | 1897 | newer

  0 0   Mmoja wa washindi wa zawadi ya kilaa siku ya shilingi milioni moja kwenye promosheni ya Jigiftishe inayoendeshwa na kampuni ya Tigo, Asha Shaban (wa pil kulia) akipokea mfano wa hundi kutoka kwa Meneja Bidhaa waa Tigo, Suleiman Bushangama (kushoto) pamoja na Jafary Othman – Mtaalam wa Huduma za Tigo (wa pili kushoto) katika hafla fupi ya kuwakabidhi washindi zawadi zao iliyofanyika eneo la Tabata jijini Dar es Salaam. Wa kwanza  kulia ni Balozi wa promosheni hiyo, mtangazaji Mina Ally.    
  6J9A0772-min
  Mmoja wa washindi wa zawadi kila siku ya shilingi milioni moja kwenye promosheni ya Jigiftishe inayoendeshwa na kampuni ya Tigo, Anna Eliudi Makala  (wa pili kulia) akipokea mfano wa hundi kutoka kwa Meneja Bidhaa wa Tigo, Suleiman Bushangama (kulia) pamoja na Jafary Othman – Mtaalam wa Huduma za Tigo (wa pili kulia) katika hafla fupi ya kuwakabidhi washindi zawadi iliyofanyika Tabata jijini Dar es Salaam. 
  6J9A0782-min
  Mshindi wa zawadi ya wiki ya shilingi milioni 10 katika promosheni ya Jigiftishe inayoendeshwa na kampuni ya Tigo, Iyaka Seifu Muinga (kulia) akipokea mfano wa hundi kutoka kwa Meneja Bidhaa wa Tigo, Suleiman Bushangama (kulia) pamoja na Jafary Othman – Mtaalam wa Huduma za Tigo (wa pili kulia) katika hafla fupi ya kumkabidhi washindi zawadi eneo la Tabata jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Balozi wa promosheni hiyo, mtangazaji Mina Ally.
  6J9A0805-min
  Mshindi wa zawadi ya wiki ya shilingi milioni 10 katika promosheni ya Jigiftishe na Tigo, Iyaka Seifu Muinga (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na washindi wengine wa kila siku wa
  6J9A0758-min
  Mmoja wa washindi wa zawadi ya kila siku ya shilingi milioni moja katika promosheni ya Jigiftishe inayoendeshwa na kampuni ya Tigo, Idrisa Selemani (kulia) akipokea mfano wa hundi kutoka kwa Meneja Bidhaa wa Tigo, Suleiman Bushangama (kushoto) pamoja na Jafary Othman – Mtaalam wa Huduma za Tigo (wa pili kushoto) katika hafla fupi ya kuwakabidhi washindi zawadi eneo la Tabata jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Balozi wa promosheni hiyo, mtangazaji Mina Ally. 
  …………………

  Kitita cha shilingi milioni 10 cha mshindi wa kila wiki katika promosheni inayoendelea ya Tigo Jigiftishe, kimenyakuliwa na Iyaka Seifu Muinga, anayefanya kazi ya kuosha magari Tabata jijini Dar es Salaam.
  Muinga anakuwa ni mshindi wa pili wa zawadi ya shilingi milioni 10 baada ya milioni kumi ya kwanza kuchukuliwa na David John Mmuni mkazi wa Changanyikeni jijini Dar es Salaam.

  Akipokea zawadi yake katika eneo analofanyia  kazi kutoka kwa Meneja wa Biashara wa Tigo, Suleiman Bushangama, mshindi huyo alielezea furaha yake na ksema kuwa Tigo imemkomboa kwa kuwa amepata mtaj wa kufungua biashara.
  ‘Nimefurahi sana kuibuka na mtaji huu kutoka promosheni ya Jigiftishe. Nitatumia pesa hizi kufungua biashara, ila kusema kweli sina mpango wa kuacha kazi yangu ya sasa,” Iyaka alisema huku akishangiliwa na wafanyakazi wenzake waliomsindikiza jukwaani kupokea zawadi.

  Akiongea  wakati akimkabidhi mshindi huyo zawadi yahe, Bushangama aliwataka wateja kuendelea kutumia huduma mbali mbali za Tigo ili kujishindia mamilioni ya shilingi yaliyotengwa kwa ajili ya kuwazawadia katika msimu huu wa sikukuu.

  Pamoja na kukabidhi zawadi  ya shilingi milioni kumi kwa mshindi wa wiki, washindi wengine kumi wa kila siku kutoka mkoa wa Dar es Salaam walizawadiwa shilingi milioni moja kila mmoja.Promosheni hiyo ya Jigiftishe inayoendeshwa na kampuni ya Tigo inalenga kuwazawadia wateja wanaotumia huduma za mtandao huo katika kipindi hiki cha sikukuu na mwaka mpya.

  Jigiftishe inalenga kuongeza idadi ya mamilionea katika mzimu huu wa sikukuu kwa kutoa zawadi kumi za shilingi milioni moja kila siku, zawadi  moja ya shilingi milioni kumi kila wiki na zawadi kwa washindi wa jumla za shilingi milioni 15, milioni 25 na milioni 50 itakayotolewa mwisho wa promosheni hiyo inayoendelea.

  0 0


  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (wapili kushoto), akimsikiliza Kamishna Jenerali wa Magereza, (CGP), Phaustine Kasike alipokua anamuonyesha moja ya mashine iliyoungua na moto mwezi uliopita katika Kiwanda cha Samani cha Magereza jijini Arusha, wakati Waziri huyo alipokitembelea kiwanda hicho leo, kuangalia moto ulivyokiteketeza kiwanda hicho. Lugola aliwataka viongozi wa Magereza kuanza maandalizi ya ujenzi wa viwanda vya samani vya kisasa katika Mikoa ya Arusha, Dar es Salaam na Tabora ikiwa ni hatua ya kwenda na kasi na uchumi wa viwanda nchini. Kulia ni Mkuu wa Kiwanda hicho, SP Victor Ngwale.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akimpa maelekezo Kamishna Jenerali wa Magereza, (CGP), Phaustine Kasike (kushoto), akiwa nje ya jengo la kiwanda cha Magereza cha samani ambacho kiliungua mwezi uliopita jijini Arusha. Lugola alikitembelea kiwanda hicho leo, kuangalia moto ulivyokiteketeza na kumtaka CGP kuanza maandalizi ya ujenzi wa viwanda vya samani vya kisasa katika Mikoa ya Arusha, Dar es Salaam na Tabora ikiwa ni hatua ya kwenda na kasi ya uchumi wa viwanda nchini.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati), akimsikiliza Mkuu wa Kiwanda cha Samani cha Magereza, jijini Arusha, SP Victor Ngwale (kulia), alipokua akimfafanulia jinsi kiwanda hicho kilipotekea kwa moto mwezi uliopita na kusababisha hasara ya mamilioni ya fedha. Lugola alikitembelea kiwanda hicho leo, kuangalia moto ulivyokiteketeza na kumtaka CGP kuanza maandalizi ya ujenzi wa viwanda vya samani vya kisasa katika Mikoa ya Arusha, Dar es Salaam na Tabora ikiwa ni hatua ya kwenda na kasi ya uchumi wa viwanda nchini. Kushoto ni Kamishna Jenerali wa Magereza, (CGP), Phaustine Kasike.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akimuaga Kamishna Jenerali wa Magereza, (CGP), Phaustine Kasike mara baada ya kumaliza ziara yake ya kukitembelea Kiwanda cha Magereza cha samani kilichoungua mwezi uliopita na kusababisha hasara ya mamilioni ya fedha. Lugola aliwataka viongozi wa Magereza kuanza maandalizi ya ujenzi wa viwanda vya samani vya kisasa katika Mikoa ya Arusha, Dar es Salaam na Tabora ikiwa ni hatua ya kwenda na kasi na uchumi wa viwanda nchini. Kulia ni Mkuu wa Kiwanda hicho. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


  Na Felix Mwagara (MOHA), Arusha

  WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amelitaka Jeshi la Magereza lianze maandalizi ya ujenzi wa viwanda vya samani vya kisasa kwa kuwa vilivyopo havina hadhi ya kwenda na kasi ya uchumi wa viwanda nchini.

  Alisema Viwanda vya Samani cha Ukonga, jijini Dar es Salaam, cha Arusha pamoja na cha Uyui Mkoani Tabora, havina hadhi ya kuitwa viwanda vya kisasa kutokana na uzalishaji wake kuwa mdogo na pia ukubwa wa viwanda hivyo ni mdogo.

  Akizungumza leo akiwa katika Kiwanda cha Samani cha Magereza kilichoungua moto mwezi uliopita eneo la Unga Limited, jijini humo, Lugola alisema kiwanda hicho kilichoungua hakuna haja ya kukijenga kingine katika eneo hilo kwa kuwa kiwanda hicho ni kidogo, hivyo maandalizi ya ujenzi wa kiwanda kipya cha kisasa uanze kuanzia sasa. Alielekeza kuwa, kwa kuwa eneo hilo ni dogo, linatakiwa liboreshwe kwa ajili ya kuhifadhiwa samani ambavyo zitakua zimetengenewa katika kiwanda cha kisasa kitakachojengwa jijini humo.

  “Kamishna Jenerali wa Magereza, aanzeni maandalizi ya ujenzi wa kiwanda kingine ambacho kitakua cha kisasa, hili eneo ni dogo mno, na pia hata cha kule Ukonga Dar es Salaam, eneo lake ni dogo, tafadhali anzeni kufikiria kwa upana zaidi kuanza maandalizi ya kutengeneza viwanda hivyo vya kisasa,” alisema Lugola. Lugola aliongeza kuwa, Jeshi la Magereza lina maeneo mengi nchini ya kuweza kujenga viwanda hivyo ambavyo vitaenda kuongeza kasi ya uchumi wa viwanda nchini ambao aliutangaza Rais Dk. John Magufuli katika mipango ya maendeleo ya nchi.

  “Tuongeze kasi kwa kuanza kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya kisasa, nyie mmeshakua wazoefu, eneo hili litatufanya tuwe na ufinyu wa mawazo kwasababu hata nusu eka halifiki, hili eneo ni dogo mno, na pia mkijenga kiwanda kikubwa mtaweza kutenganisha pia fenicha za chuma na fenicha za mbao katika kiwanda hicho, mnauwezo sana Magereza wa kutengeneza fenicha za kisasa zaidi na kwa wingi,” alisema Lugola.

  Kwa upande wake Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP), Phaustine Kasike, alisema amepokea maelekezo hayo na atakaa na viongozi wenzake kuyafanyia kazi kwa kuwa Jeshi lake lina maeneo ya kujenga viwanda nchini. “Tumepokea maelekezo yako mheshimiwa Waziri, tunaahidi tutayafanyia kazi ipasavyo na pia tunakushukuru kwa kuja kututembelea na umefanikiwa kukiona kiwanda hiki kilichoungua na kutusababishia hasara ya mamilioni ya fedha” alisema CGP Kasike.

  Kiwanda hicho kiliteketea moto usiku wa kuamkia Novemba 17, 2018 na kusababisha hasara ya zaidi ya milioni nane kutokana na mashine mbalimbali, mbao pamoja na nyaraka zilizopo katika kiwanda hicho ziliteketea moto.

  0 0


  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akitoa maelezo ya tathmini ya kitaifa ya operesheni sangara awamu ya III, mwaka 2018 kanda ya Ziwa Victoria kwa washiriki wa operesheni hiyo (hawapo pichani).
  Afisa Mfawidhi kanda ya Ziwa Victoria Bw. Didas Mtambalike akisoma tathmini ya kitaifa ya operesheni sangara awamu ya III, mwaka 2018 katika kanda hiyo, kwa washiriki wa kikao kilichoongozwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega.

  Baadhi ya washiriki wa operesheni sangara awamu ya III, mwaka 2018 wakifuatilia maelezo ya tathmini ya operesheni hiyo ilivyokuwa ikitolewa katika kikao hicho.


  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi washiriki wa operesheni sangara awamu ya III, Mwaka 2018 katika Kanda ya Ziwa Victoria.


  ……………………


  “Operesheni uvuvi haramu yapaisha mapato ya serikali kuu”

  Operesheni za kudhibiti uvuvi haramu hapa nchini, zimeiwezesha serikali kuu kupata mrabaha wa Shilingi Bilioni 2.2 kuanzia Mwezi Desemba mwaka 2017 hadi Mwezi Novemba mwaka 2018, kutoka Shilingi Milioni 457.

  Hayo yalibainishwa (01.12.2018) Jumamosi jijini Mwanza na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega wakati akiongoza kikao cha kufanya tathmini ya operesheni sangara kitaifa awamu ya tatu kwa mwaka 2018, kanda ya Ziwa Victoria, kikao kilichohudhuriwa na maafisa waliohusika katika operesheni hiyo, ambapo amesema kiasi hicho cha pesa kimeongezeka kutokana na mafanikio ya udhibiti wa mianya ya utoroshaji fedha.

  “Mwaka 2017 mpaka tunafunga mwaka mwezi Desemba mrabaha wa serikali kuu kabla ya kufanya operesheni ulikuwa Shilingi Milioni 457, mwaka 2018 hadi Mwezi Novemba mrabaha wa serikali kuu ni Shilingi Bilioni 2.290, kutoka Shilingi Milioni 457 mpaka Shilingi Bilioni 2.290 unaweza kuona kwamba ni ongezeko la zaidi ya asilimia 200, hii maana yake kulikuwa na utoroshaji mkubwa wa fedha ambazo zingeingia katika mfumo mkuu wa serikali.” Alisema Mhe. Ulega.

  Aidha, katika kikao hicho ambacho kilihudhuriwa na baadhi ya wafanyabiashara wa samaki, Mhe. Ulega alisema kabla ya kuanza kwa operesheni za kudhibiti uvuvi haramu, takwimu zilionesha uwepo wa samaki wachanga zaidi ya Asilimia Tisini, lakini baada ya operesheni hizo samaki walianza kuongezeka kauli iliyoungwa mkono na wafanyabiashara waliohudhuria kikao hicho ambao walisema samaki wakubwa wameanza kupatikana kwa wingi katika ukanda wa Ziwa Victoria.

  Awali katika kikao hicho, akiwasilisha taarifa ya operesheni sangara kitaifa awamu ya tatu mwaka 2018 katika ukanda wa Ziwa Victoria, Afisa Mfawidhi wa kanda hiyo Bw. Didas Mtambalike alisema tangu kuanza kwa operesheni hiyo tarehe 18 Mwezi Oktoba Mwaka 2018 hadi tarehe Moja Mwezi Desemba Mwaka 2018 Shilingi Bilioni 1.172 zilipatikana kutokana na malipo ya faini walizotozwa waliojihusisha na mtukio ya uvuvi haramu.

  Bw. Mtambalike pia alisema zoezi hilo limewezesha vyombo vingi vya uvuvi na biashara za bidhaa za uvuvi kusajiliwa na kupatiwa leseni kutokana na elimu ambayo wavuvi walikuwa wakipatiwa ili kufanya shughuli zao kwa kufuata sheria na taratibu za nchi.

  “Kitu ambacho tumekibaini ni kwamba vyombo vingi sasa hivi vimesajiliwa vile vya uvuvi, vile ambavyo viko chini ya halmashauri vimesajiliwa lakini pia vile ambavyo viko chini ya serikali kuu vimesajiliwa ambavyo ni zaidi ya urefu wa mita 11.” Alisema Bw. Mtambalike

  Baadhi ya wadau wa uvuvi ambao walipata nafasi ya kutoa maoni yao katika kikao hicho, walimuomba Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega, uwepo wa bei elekezi kwa mazao ya samaki ili wavuvi waweze kuuza samaki kwa bei ya uhakika, pamoja na kulifanyia kazi ombi lao la kuendelea kuvua dagaa kwa kutumia taa zinazotumia mwanga wa jua kutokana na kusitishwa kwa ya taa hizo kwa shughuliza uvuvi hususana wa dagaa kutokana na uwepo wa madai ya samaki hao kuathiriwa na taa hizo, jambo ambalo Mhe. Ulega alisema serikali inalifanyia kazi.

  Kikao cha tathmini ya operesheni sangara kitaifa awamu ya tatu mwaka 2018 katika kanda ya Ziwa Victoria kiliongozwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega, ambapo kimefanya tathmini ya kutokomeza uvuvi haramu katika maeneo ya Singida, Sengerema, Ukerewe, Simiyu, Mwanza, Kagera, Geita na Mara ambayo yote yapo chini ya kanda ya Ziwa Victoria, ambapo kikao hivcho kimeridhishwa na mafanikio makubwa ambayo yamepatikana katika kudhibiti uvuvi haramu.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa Maji safi na usafi wa Mazingira katika jiji la Arusha. Wengine katika picha ni Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Isaack Kamwelwe pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Alex Mubiru.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa mradi mkubwa wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira utakaosaidia jiji la Arusha katika sherehe zilizofanyika katika kijiji cha Kimyaki Arumeru mkoani Arusha.  
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia maji yanayotoka katika moja ya visima virefu vilivyopo katika mradi huo mkubwa wa maji safi na usafi wa mazingira katika jiji la Arusha. Mradi huo utakapokamilika utaweza kuzalisha lita za ujazo milioni 200  kwa siku tofauti na sasa ambapo lita za ujazo ni 45 milioni wakati mahitaji ya jiji la Arusha ni lita za ujazo milioni 90.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Alex Mubiru wakati wa mkutano na wananchi wa Arumeru jijini Arusha mara baada ya kuzindua mradi huo wa maji. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Arumeru mara baada ya kuweka  jiwe la msingi mradi wa Maji safi na usafi wa Mazingira katika jiji la Arusha
   Wananchi wa Arumeru wakishangilia wakati wa hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika kijiji cha Kimnyaki Arumeru. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi wakati akiondoka katika eneo la mkutano. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Meya wa jiji la Arusha Kalist Lazaro mara baada ya kuwahutubia wananchi wa Arumeru. PICHA NA IKULU

  0 0

  Kampuni ya TBL Group, imeadhimisha Siku ya Ukimwi Duniani kwa wafanyakazi wake kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya, Moshi na Arusha, kushiriki zoezi la upimaji wa afya zao,kufanya mazoezi na kutoa misaada kwa vituo vinavyolea watoto yatima. 

  Afisa Mahusiano ya wafanyakazi wa TBL Group,Salma Nyangasa,alisema maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yamekuwa yakiadhimishwa na kampuni kila mwaka kwa kuwashirikisha wafanyakazi wake kupima afya zao “Suala la afya za wafanyakazi ni jambo ambalo kampuni inalipa umuhimu mkubwa ndio maana tumetumia siku hii kupima afya sambamba na kushiriki kufanya mazoezi ya kujenga mwili na kupatiwa semina za kukabiliana na magonjwa mbalimbali”alisisitiza.
  Baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha TBL Ilala wakishiriki zoezi la kupima afya katika kuadhimisha siku ya Ukimwi Duniani
  Baadhi ya wafanyakazi wa TBL wakiwasha mshumaa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani mwishoni mwa wiki.
   Baadhi ya wafanyakazi wa TBL wakishiriki mazoezi wakati wa siku ya kuadhimisha Siku ya Ukimwi Duniani.
  Baadhi ya wafanyakazi wa kitengo cha TEHAMA (IT) wa TBL, wakikabidhi msaada kwa Mkuu wa kituo cha kulea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Msimbazi Centre,Sister Stela, ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani.

  0 0  Na Khadija Seif,Globu ya jamii

  ALIYEKUWA Mbunge wa Jimbo la Temeke jijini Dar es Salaam Abdallah Mtolea amewaambia wajumbe wa Baraza la Hamashauri ya Manispaa ya Temeke kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) kuwa amefanya uamuzi sahihi kujiunga na Chama hicho.

  Mtolea ambaye alikuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia Chama cha Wananchi(CUF)alitangaza kujiuzulu ubunge na nafasi zote ndani ya CUF siku za hivi karibuni akiwa Bungeni Mjini Dodoma.

  Hivyo kwa sasa amejiunga na CCM na leo wakati anazungunza kwenye baraza hilo la halmashauri ya manispaa ya Temeke ameeleza kwa kina sababu za kuondoka CUF.Akifafanua zaidi wakati akifungua kikao cha baraza hilo Mtolea amesema uamuzi sahihi kurudi CCM katika kuendeleza na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora katika kila sekta nchini.

  Amebainisha kuwa wapinzani wapo kwa ajili ya kupinga juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano na kazi kubwa ni kubeza na kushawishi vijana kufanya ushabiki ambao hauna manufaa kwa maslahi ya nchi na Taifa kwa ujumla.Pia Mtolea amezungumzia wasanii ambapo amesema hawajakatazwa kufanya kampeni bali wasanii wa Mkoa husika wapatiwe vipaumbele katika kuonesha vipaji vyao.

  Kwa upande wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana Kata ya Temeke kupitia CCM Fadhili Faungo amesema kuwa Rais Dk.John Magufuli amekuwa anashirikiana bega kwa bega na vijana kwani anaamini vijana ndio nguvu kazi ya Taifa .Pia amesema lengo la kukutana kwa wajumbe wa Baraza hilo ni kuangalia miradi ya maendeleo ambayo itatekelezwa kupitia fedha ambazo zimetolewa na Serikali.

  Wakati huo huo imeelezwa kuwa baadhi ya wajumbe wameshawasilisha mawazo yao katika matumizi ya kufungua biashara ambazo zitaleta chachu ya kuongeza pato la Taifa.
  ALIYEKUWA Mbunge wa Jimbo la Temeke jijini Dar es Salaam Abdallah Mtolea akizungumza mbele ya Wajumbe wa Baraza la Hamashauri ya Manispaa ya Temeke kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) kuwa amefanya uamuzi sahihi kujiunga na Chama hicho.

  0 0

  Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle kulia akitoa maagizo wakati akikagua gari ya kubeba mitambo mbalimbali (low bed truck) katika karakana ya TEMESA mkoa wa Tanga wakati wa ziara yake mkoani humo kukagua utendaji kazi na kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wafanyakazi wa wakala huo. Kushoto ni Kaimu Meneja Mhandisi Mhangaiko Ngoroma.
  Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle akikagua Propela ya kivuko cha MV. PANGANI II ambacho kinafanyiwa ukarabati mkubwa katika yadi ya Songoro, kivuko hicho kinatarajiwa kuungana na kivuko cha MV. TANGA kutoa huduma katika eneo la Pangani na Bweni katika eneo la mto Pangani mara baada ya kukamilika kwa matengenezo yake. Nyuma yake ni Mkuu wa Kivuko cha Pangani Bweni Mhandisi Abdulrahman Ameir.
  vuko cha MV. TANGA kinachotoa huduma katika mto Pangani, kati ya Pangani na Bweni wilayani Pangani mkoani Tanga kikielea majini wakati kikiendelea kutoa huduma ya kuvusha abiria na magari.
  Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle wa pili kushoto akisisita umuhimu wa kuzingatia usalama wa vivuko kwa wafanyakazi wa kivuko hicho wakati wote wanapotoa huduma hiyo katika kivuko cha MV TANGA kinachotoa huduma katika mto Pangani, kati ya Pangani na Bweni wilayani Pangani mkoani Tanga wakati wa ziara yake ya kukagua usalama wa vivuko.
  Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle katikati (aliyevaa koti) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi na mabaharia wa kivuko cha MV TANGA kinachotoa huduma katika mto Pangani, kati ya Pangani na Bweni wilayani Pangani mkoani Tanga mara baada ya kumaliza kikao na wafanyakazi hao. PICHA ZOTE NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO (TEMESA)  ………………………………

  ALFRED MGWENO (TEMESA TANGA)

  Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Mhandisi Japhet Y. Maselle, amehitimisha ziara yake mkoani Tanga kwa kuwataka watendaji na viongozi wa Wakala mkoani humo kuendelea kufanya kazi kwa bidii na weledi mkubwa ili kuinua mapato ya kituo hicho.

  Akizungumza na wafanyakazi wa TEMESA Tanga pamoja na mafundi wa karakana mara baada ya kuwasili mkoani humo, mhandisi Maselle aliwasisitizia suala la ubunifu hasa katika upande wa karakana ambapo aliwataka kuiga mfano kutoka mkoa wa Singida ambao uzalishaji wake umeongezeka kwa kipindi cha hivi karibuni kutokana na kubuni njia mbalimbali ili kuongeza pato lake ikiwemo kuepuka kupeleka kazi ndogo ndogo za ufundi katika karakana teule. Vilevile alipata pia fursa ya kusikiliza changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika utendaji kazi wao pamoja na kukagua baadhi ya mitambo iliyopo katika karakana hiyo. Changamoto kubwa iliyoonekana ilikuwa ni uchakavu wa mitambo ambapo Mhandisi Maselle alisema kuwa ni vyema sasa Wakala ukaanza utaratibu wa kununua mitambo mipya ili kuongeza ufanisi zaidi upande wa Ukodishaji mitambo.

  Mhandisi Maselle pia alitembelea kivuko cha MV. TANGA ambacho kinatoa huduma ya kuvusha abiria kati ya Pangani na Bweni katika mto Pangani mkoani Tanga ambapo alikagua hali ya usalama wa kivuko hicho na kuendelea kusisitiza suala hilo kupewa kipaumbele kikubwa wakati wote wa uvushaji, ‘’hakikisheni mnatoa mafunzo ya usalama walau mara mbili kwa wiki maana wanaovuka hapa kila siku asilimia kubwa ni wakazi wa hapa hapa’’, alisema Mhandisi Maselle.

  Aidha Kaimu Mtendaji Mkuu, aliwapongeza kwa kuzingatia suala la nidhamu kwa viongozi wao lakini pia kusifia muonekano wa mabaharia wa kivuko hicho ambao walikua wamevalia sare zao zinazoweza kuwatambulisha kiurahisi kwa abiria na kuweza kupatiwa msaada pindi wanapohitaji.

  Pamoja na kusikiliza kero, changamoto na maoni yao, Kaimu Mtendaji Mkuu alipata pia wasaa wa kukagua kivuko cha MV. PANGANI II (kilichokuwa awali kinaitwa MV. UTETE kilichohamishwa kutoka Utete wilaya ya Rufiji mkoani Pwani) ambacho kinafanyiwa ukarabati mkubwa na Kampuni ya Kizalendo ya Songoro Marine Boatyard ya jijini Mwanza, kivuko hicho kinatarajiwa kuungana na kivuko cha MV. TANGA kutoa huduma eneo hilo mara tu ukarabati wake utakapokamilika.

  0 0
 • 12/02/18--10:49: Article 0
 • Mkuu wa wilaya ya Temeke Mhe. Felix Lyaniva akikimbia KM 10 mbio Kimataifa za Kigamboni mapema leo zilizoanzia eneo la Fun City jijini Dar es Salaam. Pembeni yake ni Ofisa Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigamboni Rahel Mhando (kushoto) nyuma ni Meya wa Kigamboni Mhe. Maabadi Suleiman Hoja (CCM). Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
  Mkuu wa wilaya ya Temeke Mhe. Felix Lyaniva akikimbia za mbio KM 10 za Kigamboni mapema leo eneo la Fun City jijini Dar es Salaam. Pembeni yake ni Ofisa Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigamboni Rahel Mhando (kushoto).
  Wakimbiaji wa KM 41 wakifukuza upepo katika mchuano mkali.
  Kila mmoja akionyesha umahili wake wa kufukuza upepo katika mbio za Kigamboni International Marathon 2018 zilizofanyika Kigamboni jijini Dar es Salaam.
  ...Wakiwa na nyuso za uchovu.... kila mmoja kamnunia mwenzake
  Mkuu wa wilaya ya Temeke Mhe. Felix Lyaniva aakifutahia mara baada ya kumaliza mbio za mbio KM 10 za Kigamboni mapema leo eneo la Fun City jijini Dar es Salaam. Katikati ni Ofisa Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigamboni Rahel Mhando na Kushoto ni Meya wa Kigamboni Mhe. Maabadi Suleiman Hoja (CCM).
   Kila mmoja alikuwa na furaha baada ya kupokea medali yake...
   Muandaaji Dimo Dibwe akiwa na Imani Kajula mara baada ya kumaliza shindano.

  0 0

  Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa hamsini na mbili wa Tanzania Bara wanatarajiwa kushiriki katika programu ya mafunzo ya uongozi kwa kipindi cha wiki moja kuanzia Jumatatu ya tarehe 3 Disemba, 2018 hadi Ijumaa ya tarehe 7 Disemba, 2018, mkoani Dodoma. 

  Warsha hiyo ya mafunzo ambayo imeandaliwa na Taasisi ya UONGOZI kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) itafunguliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) leo. 

  Kwa mujibu wa Taasisi ya UONGOZI, programu hii ya mafunzo ya uongozi, ni ya kwanza ya aina yake iliyoandaliwa mahususi kwa ajili ya Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa. 

  “Lengo la programu hii ni kuimarisha uwezo wa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala katika kufanya maamuzi ya kimkakati, kuongoza watu na kusimamia rasilimali nyingine, pamoja na kujijengea sifa binafsi za uongozi,” alisema Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo, Prof. Joseph Semboja. 

  Prof. Semboja pia alisema, “Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa wana nafasi muhimu katika kuwezesha ukuaji na maendeleo ya nchi. Hivyo, tunatarajia kwamba kupitia programu hii, uwezo wao wa kuongoza utaimarika na kuwawezesha kuchangia katika jitihada za kuleta maendeleo endelevu nchini na hatimaye, barani mwetu.” 

  Prof. Semboja aliongezea kwamba huu ni mwendelezo wa jitihada za Taasisi ya UONGOZI na Ofisi ya Rais, TAMISEMI zinazolenga kuwafikia viongozi wengi iwezekanavyo wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ili kupanua uelewa wa masuala ya uongozi na kuongeza tija ya shughuli wanazozifanya za kuwatumikia wananchi. Kati ya Mei 2017 na Oktoba 2018, mafunzo ya uongozi yalitolewa kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa na Wilaya, kwa awamu tano tofauti. 

  Warsha hiyo ya mafunzo ya siku tano itajumuisha mada kuu zifuatazo; Uongozi Binafsi na Akili Hisia, Mwingiliano na Mahusiano baina ya Viongozi wa Kisiasa na Viongozi Watendaji, Mawasiliano ya Kimkakati, Itifaki, Masuala yanayohusu Ulinzi na Usalama, Usimamizi wa Fedha za Umma na Rasilimali Nyingine, Manunuzi katika Sekta ya Umma na Udhibiti wa Madawa ya Kulevya.

  0 0

  NA MWAMVUA MWINYI, BAGAMOYO

  MKUU wa wilaya ya Bagamoyo ,Mkoani Pwani ,Zainabu Kawawa ameagiza 
  watumishi wa idara ya fedha wanaoshughulika na ukusanyaji mapato katika halmashauri ya Chalinze, wakamatwe ili kupisha uchunguzi na watakapobainika kusababisha upotevu wa mapato hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

  Amefikia hatua hiyo, kufuatia hali ya ukusanyaji mapato katika halmashauri hiyo kuwa chini ya kiwango ,kutoka wastani wa sh. milioni 950 kwa mwezi na kushuka hadi milioni 550-659 .#

  Zainabu alitoa agizo hilo ,wakati alipokuwa akizungumza na watumishi wa halmashauri hiyo.Aliwataja wahusika hao kuwa ni pamoja na mweka hazina David Rubibira na wahasibu watatu ambao ni Waziri Ally,Jumanne Sanga na Maneno Kwambwa,ili kupisha uchunguzi .

  Zainab alisikitishwa na ukusanyaji mapato kwa kudai kuna mianya ya ubadhirifu wa mapato kwani mapato yakikusanywa kwa umakini yanafikia sh. milioni 920 kwa mwezi kwa chanzo cha madini ya kokoto nje ya vyanzo vingine kwa maana ya sh. milioni 33 kwa siku.

  Hata hivyo ,kutokana na makisio hayo Zainab aliondoa imani na mapato yanayokusanywa katika halmashauri hiyo ambayo ni wastani wa milioni 550 hadi 659 kwa mwezi.Katika kikao hicho alimtaka mkuu wa polisi Chalinze kuwaweka chini ya ulinzi na kuwachukua kwa ajili ya uchunguzi .

  "Nimekuwa nikifuatilia ukusanyaji mapato kuna mianya mingi ya utoroshaji mapato, tusitafutane wala kujaribiana kwa kuvujisha mapato tumepoteza mapato sana kwenye makrasha kwa siku tuna uwezo wa kukusanya milioni 33 ,kwa mwezi tuna uwezo wa kukusanya zaidi ya milioni 900"

  "Badala ya kufuatilia na kukagua mnakaa ofisini ,katika hili hatuwezi kuvumiliana hata kidogo,,"mkurugenzi nakuagiza watumishi wanaohusika na mapato wakae pembeni kwa hatua zaidi kuanzia leo .Zainab alisisitiza , vyombo vya usalama vifanye kazi katika kuchunguza suala hilo.

  0 0

  Na Mwashungi Tahir - Maelezo Zanzibar

  MWAKILISHI wa Jimbo la Magomeni Rashid Makame Shamsi amewaomba wananchi wa magomeni wandaras kuwa na mashirikiano na viongozi wao ili wanapopeleka huduma muhimu za maendeleo kwa jamii zipate ufumbuzi.

  Hayo ameyasema huko Magomeni Wandaras wakati alipokuwa akikabidhi wananchi mipira ya maji katika shehia hiyo ikiwa anatimiza ahadi yake ili wananchi wa shehia hiyo waweze kupata huduma ya maji safi na salama kwa ukaribu na kupunguza masafa marefu yaliyokuwa yakiwakabili.

  Amesema iwapo viongozi wa jimbo wanajitokeza kwa kuleta huduma za maendeleo inapaswa kuthamini na kuyafanyia kazi kwa moyo mmoja ili na wao waweze kufarijika zaidi na kuongeza kutatua changamoto nyengine zitazojitokeza .

  Amesema wakati mliponichagua niliahidi kutatua changamoto na kuleta mambo ya maendeleo katika jimbo kati ya ahadi hizo ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma zote muhimu miongoni mwa hayo ni maji safi na salama hii ikiwa ilani ya Chama chetu cha Mapinduzi kuwajali wananchi wake katika pande zote.

  Aidha alisema kiongozi mzuri ni yule anaeahidi kwa wananchi wake na kutimiza ahadi zile alizoziahidi na asipotimiza huwa ni mnafiki na hata mwenyezi Mungu anahimiza ahadi zitimizwe kwani ahadi ni deni

  “Kiongozi anaeahidi asitimize huwa ni mnafiki ni wajibu wetu kutimiza ahadi zetu kwa wananchi wetu ili na wao wajenge Imani na viongozi wao”.Alisema mwakilishi huyo.

  Pia alisema Serikali yetu ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na Rais wetu wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein hivi sasa ina miradi ya maji ambapo wafadhili wake ni India, Japan ifikapo 2020 maeneo mengi ya mijim yetu kwa asilimia kubwa itapata maji safi na salama.

  Vi le vile viongozi ndani ya majimbo ni wajibu kutimiza ahadi zetu iwapo hatutotimiza maendeleo yeyote baada ya miaka mitano tukitaka kurudi wananchi hawatotuelewa na pia chama chetu tutakirudisha nyuma lakini tukikamilisha ahadi zetu tutazidi kusonga mbele kwa kuaminiwa na chama chetu tutakirahisishia ushindi wa kishindo ifikapo 2020.

  Nae Mwenyekiti wa Wadi ya Magomeni Hussein Ali Mdungi amesema kukabidhiwa mipira hii kumewafurahisha sana na wanatoa shukurani zao za dhati kwani kutawapunguzia usumbufu wa maji waliokuwa wanaupata kwa kipindi kirefu na kuwaomba kuthamini jitihada za viongozi wetu wanazozifanya .

  Pamoja na hayo Mzee wa mtaa Azizi Mbarouk Omar na wananchi wa shehia hiyo wametoa pongezi zao kwa kiongozi huyo na kusema wamepokea mikono miwili msaada wa mipira hiyo na kumuhakikishia wataitunza ili waweze kufaidika na huduma hiyo katika maeneo hayo ili huduma hiyo iendelee kwa muda mrefu.

  Jumla ya laki sita na arubaini elfu imetumika katika kupatiwa mipira hiyo ikiwa ametimiza ahadi aliyoitowa katika shehia hiyo.
  Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Rashid Makame Shamsi akikabidhi Mipira ya maji kwa Mzee wa mtaa Azizi Mbarouk Omar ( Kushoto) huko Shehia ya Magomeni Wandaras Mjini Unguja.Picha na Mwashungi Tahir – Habari Maelezo.

  0 0

   Watumishi wa serikali kutoka idara mbalimbali wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga vijijini ambao ni makada wa Chama Cha Mapinduzi -CCM, wameandamana kumpongeza Rais John Magufuli kwa kazi nzuri anayofanya ya kizalendo na kutetea wakulima kwa kupambana na wanyonyaji ambao wamekuwa wakitajirikia jasho lao na wao kubaki maskini.

  Maandamano hayo yamefanyika leo Jumapili Desemba 2,2018 kutoka katika Soko Kuu la mjini Shinyanga hadi kwenye ofisi za Makao Makuu ya CCM Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kufikisha ujumbe wao kwa Rais Magufuli za kuunga juhudi za utendaji wake kazi. 

  Akizungumza mara baada ya kumaliza maandamano hayo. Msemaji wa umoja huo wa watumishi wa Serikali ambao ni makada wa CCM Christopher Malengo,sambamba na kutoa tamko lao mbele ya katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Haula Kachwambwa, amesema wameguswa na kazi ya kizalendo ambayo anaifanya Rais Magufuli ya kupigania maslahi ya wanyonge wakiwamo wakulima.

   Amesema Rais Magufuli amekuwa akijikita katika misingi ya ujamaa,utu,uzalendo na haki kama alivyokuwa akifanya hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwenye utawala wake, katika kuhakikisha anapigania maslahi ya wanyonge na kukomesha wanyonyaji ili wananchi wote waweze kupata haki sawa, vitendo ambavyo zinapaswa kupongezwa.

   “Sisi kama watumishi wa serikali kutoka halmshauri ya wilaya ya Shinyanga vijijini ambao ni makada wa CCM, tumeamua kuungana kwa pamoja ili kumpongeza Rais Magufuli kwa kazi nzuri anayofanya ya kizalendo ya kupigania maslahi ya watanzania wote wakiwamo wakulima,” amesema Malengo. 

  “Tumeona mfano mzuri alioufanya kwenye zao la Korosho huko Mtwara amewapigania wakulima dhidi ya wanyonyaji pamoja na kuagiza zao hilo iuzwe kwa bei ya Shilingi 3,300 jambo ambalo ana stahili pongezi sana, na tunamuomba ageukie na mazao mengine likiwamo Kahawa na Pamba,”ameongeza.

  Aidha amesema Sekta ya kilimo ndiyo injini ya mapinduzi ya viwanda, ambapo malighafi nyingi za uzalishaji bidhaa hutegemea mazao, hivyo jambo ambalo anafanya Rais ana paswa kuungwa mkono ili Tanzania tuweze kufikia uchumi wa kati mwaka 2025. 

  Kwa upande wake katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Haula Kachwambwa amewapongeza watumishi hao wa Serikali kwa kutambua kazi anayofanya Rais Magufuli na kuwataka wasimwangushe bali waige mfano wake na kuchapa kazi kwa kutatua matatizo mbalimbali ya wananchi. T Watumshi wa Serikali katika idara mbalimbali wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga vijijini ambao ni Makada wa Chama Cha Mapinduzi CCM wakiwa kwenye maandamano ya kumpongeza Rais John Magufuli kwa utendaji wake mzuri wa kizalendo hasa kupigania maslahi ya wakulima,huku wakiwa wamebeba mabango ya pongezi hizo.  Maandamano yakiendelea kutoka eneo la Soko Kuu na kuelekea kwenye ofisi za Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga ili kufikisha ujumbe wao wa pongezi kwa Rais Magufuli.  Maandamano yakiendelea sambamba na ubebaji wa mabango yenye Ujumbe wa pongezi kwa Rais John Magufuli.  Maandamano yakiendelea.  Maandamano baada ya kufika katika ofisi za CCM Mkoa wa Shinyanga.  Watumishi wa Serikali ambao ni Makada wa CCM wakifurahi mara baada ya maandamano hayo kupokelewa na katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Haula Kachwambwa.  Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Haula Kachwambwa akipokea mabango yenye ujumbe mbalimbali wa kumpongeza Rais John Magufuli kwa utendaji wake kazi hasa kupigania wanyonge ili kuwainua kiuchumi.  Upokeaji wa mabango ukiendelea.  Watumishi wa Serikali ambao ni Makada wa CCM wakiingia ukumbini kwa ajili ya kutoa tamko lao juu ya kupongeza Rais John Magufuli kwa utendaji wake kazi wa kizalendo na kufuata misingi ya ujamaa, utu na uzalendo kama alivyokuwa akifanya hayati Baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwenye utawala wake.  Msemaji wa umoja huo wa watumishi wa Serikali kutoka halmshauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini ambao ni Makada wa CCM, Christopher Malengo akisoma Tamko la Pongezi kwa Rais Magufuli juu ya uchapakazi wake kazi wa dhamira ya kuinua uchumi wa nchi na kujenga miundombinu mbalimbali ikiwamo barabara,Reli ,kununua Ndege, pamoja na kupigania maslahi ya wakulima.  Wajumbe wakiwa ukumbini wakisikiliza uwasilishwaji wa Tamko lao kwa Rais John Magufuli..  Wajumbe wakiendelea kusikiliza kwa makini..  Wajumbe wakiwa ukumbini kwenye ofisi za CCM Mkoa wa Shinyanga.  Wajumbe wakiwa ukumbini.  Msemaji wa umoja huo wa watumishi wa Serikali ambao ni Makada wa CCM Christopher Malengo akimkabidhi Tamko lao la Pongezi kwa Rais John Magufuli, katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Haula Kachwabwa, ili kuliwasilisha kwa Rais.  Muonekano wa nje wa Tamko hilo la Kumpongeza Rais John Magufuli kwa utendaji wake kazi mzuri.  Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Haula Kachwambwa, akiwapongeza watumishi hao wa Serikali ambao ni Makada wa CCM kwa kutambua kazi anayofanya Rais Magufuli, na kuwataka wasimwangushe bali waige mfano wake na kuchapa kazi kwa kutatua matatizo mbalimbali ya wananchi pamoja na kuwaahidi Tamko hilo litamfikia Rais John Magufuli. Na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog.

  0 0


  Washiriki wa Mashindano ya Mbio za Morogoro Marathoni akiwemo Mgeni rasmi Mkuu wa mkoa wa Morogoro wakiwa wamejiapnga tayari kuanza mbio za Kilometa 21 zilizoanzia jirani na ofisi ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro.
  Kikundi cha Mazoezi cha Mzimuni Jogging Club wakiwa katika maandalizi ya kushiriki mbio hizo ambazo zimefanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Morogoro.
  Kundi la Arusha Runners pia walikuwa ni washiriki wa tukio hilo .
   Washiriki wa Mbio za Km 21 ,Morogoro Marathon wakipita katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Morogoro. 
   Wanariadha nguli ,Marko Joseph,Dickson Marwa,Faraja Lazaro ,Anthony Moya na Chacha Boy wakichuana vikali katika Mashindano mapya ya Morogoro Marathon yaliyofanyika mkoani Morogoro kwa upande wa km 21
   Wanariadha Amina Mohamed na Rozalia Fabian kutoka klabu ya Jkt Arusha wakikimbia mbio za Kilometa 21 katika Mashindano mapya ya Morogoro Marathon yaliyofanyika mkoani Morogoro. 
  Mshindi wa kwanza katika Mashindano Mapya ya Morogoro Marathon ,Amina Mohamed akimaliza mbio za Kilometa 21 kwa kutumia saa 1:21:47 akimshinda mpinzani wake ,Rozalia Fabian
  Mwanariadha Mkongwe Dickson Marwa akimaliza Mbio za Km 21 katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.

  Baadhi ya Washiriki mbalimbali wakimaliza Mbio hizo katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.
  Mgeni rasmi katika Mashindano hayo,Mkuu wa Mkoa wa Morogoro ,Kebwe Stephen Kebwe akizungumza kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa Mbio za Morogoro Marathoni.
  Baadhi ya Washiriki wa Mbio hizo wakimsikiliza Mgeni Rasmi katika Mashindano ya Mbio za Morogoro Marathoni .
  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro Kihanga akizungumza katika Mashindano hayo.
  Mgeni rasmi katika Mashindano ya mchezo wa Riadha ya Morogoro Marathon ,Mkuu wa mkoa wa Morogoro ,Kebwe Stephen Kebwe akimkabidhi mshindi wa kwanza wa mbio za km 21 kwa wanawake Amina Mohamed zawadi ya king'amuzi cha DSTV.
  Mgeni rasmi katika Mashindano ya mchezo wa Riadha ya Morogoro Marathon ,Mkuu wa mkoa wa Morogoro ,Kebwe Stephen Kebwe akimkabidhi mshindi wa pili wa mbio za km 21 kwa wanawake Rozalia Fabian zawadi ya king'amuzi cha DSTV.
  Mgeni rasmi katika Mashindano ya mchezo wa Riadha ya Morogoro Marathon ,Mkuu wa mkoa wa Morogoro ,Kebwe Stephen Kebwe akimkabidhi mshindi wa tatu wa mbio za km 21 kwa wanawake Monica Nicolaus zawadi ya king'amuzi cha DSTV.
  Mgeni rasmi katika Mashindano ya mchezo wa Riadha ya Morogoro Marathon ,Mkuu wa mkoa wa Morogoro ,Kebwe Stephen Kebwe akimkabidhi mshindi wa kwanza wa mbio za km 21 kwa wanaume ,Marko Joseph zawadi ya king'amuzi cha DSTV.
  Mgeni rasmi katika Mashindano ya mchezo wa Riadha ya Morogoro Marathon ,Mkuu wa mkoa wa Morogoro ,Kebwe Stephen Kebwe akimkabidhi mshindi wa tatu wa mbio za km 21 kwa wanaume Faraja Lazaro zawadi ya king'amuzi cha DSTV.
   Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Itete Sports Agency ambao ndio waandaaji wa Mbio za Morogoro Marathon ,Antipas Mgungusi akizungumza mara baada ya zawadi kukabidhiwa kwa washindi. 
  Na Dixon Busagaga,Morogoro.

  WANARIADHA Marko Joseph wa Singida na Amina Mohamed wa JKT –Arusha jana wamewek rekodi mpya baada ya kufanikiwa kushika nafasi ya kwanza kwa mbio za kilometa 21 kwa wananume na wanawake katika mashindano ya Mbio mpya za Morogoro Marathon 2018.

  Joseph alifanikiwa kushika nafasi hiyo baada ya kutumia saa 1:05:50 akifuatiwa na mwanariadha Faraja Lazaro w JKT –A rusha aliyemaliza mbio hizo zilizoanzia na kumalizikia katika uwanja wa Jamhuri akituia saa 1:0:04.

  Nafasi ya tatu imechukuliwa na mwanariadha mkongwe Dickson Marwa aliyemaliza mbio hizo kwa kutumia saa 1:07:42 huku nafasi ya nne ikichukuliwa na mwanariadha Anthony Moya aliyemaliza mbio kwa kutumia saa 1:07:42.

  Kwa upande wa wanawake Amina Mohamed amefanikiwa kushika nafasi ya kwanza baada ya kutumia saa 1:21:47 akifuatiwa n Rozalia Fabiani liyemaliza mbio kwa kutumia saa 1:23:59 huku Monica Nicolaus akishika nafasi ya tatu kwa kutumia saa 2:00:08.

  Washindi wa Mbio za Kilometa tano wametangazwa Hashim Athuman (18:50:07) kwa upande wa wanaume huku kwa wanawake akishika nafasi ya kwanza Rosemary Mustapha kutoka mjini Magharibi Zanzibar (23:41:66).

  Nafasi ya pili kwa wanaume ni Mathayo Jeremia (Dar es Salaam), kwa wanawake niNeema Masoud wa JKT-Arusha huku nafas ya tatu kwa wanaume ikichukuliwa na Elias Maayunga na kwa wanawake ni Vaireth Kidosi.

  Washindi katika mashindano hayo yanayoandaliwa na taasisi ya Itete Sports Agency walikabidhiwa zawadi zao na Mkuu wa mkoa wa Morogoro ,Kebwe Stephen Kebwe aliyekuwa mgeni rasmi ambaye pia alishiriki mbio za Kilometa tano.

  Washindi kwa nafasi ya kwanza kwa mbio za kilometa 21 kwa wanaume na wanawake wamejishindia fedha taslimu kiasi cha sh 400,000 na king’amuzi cha DSTVkutoka kampuni ya Mult choice ambayo ilikuwa moja wa wadhamini wa mbio hizo.

  Washindi wa pili kwa mbio za km 21 wamejinyakulia kiasi cha Sh 250,000 pamoja na king’amuzi cha DSTV huku washindi wa tatu wakijinyakulia kiasi cha Sh 100,000 pamoja na king’amuzi cha DSTV huku washiriki wengine wakiambulia zawadi za Medali .

  0 0


  Diwani wa Kata ya Tuangoma iliyopo Mbagala Dar es Salaam Mohamed Suleiman akifungua Hostel ya wanafunzi wa kike kwa shule za serikali iliyopo eneo la Mzinga kata ya Tuangoma Dar es Salaam, hosteli iliyojengwa kwa ufadhili wa taasisi ya kimataifa ya NAMA Foundation.Kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Pamoja Foundation Haji Mrisho.
  Diwani wa Kata ya Tuangoma iliyopo Mbagala Dar es Salaam Mohamed Suleiman akizungumza wakati wa uzinduzi wa Hostel ya wanafunzi wa kike kwa shule za serikali iliyopo eneo la Mzinga kata ya Tuangoma Dar es Salaam leo, hostel hiyo imejengwa kwa ufadhili wa taasisi ya kimataifa ya NAMA Foundation. Kushoto kwa Diwani ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Pamoja Foundation Haji Mrisho.
  Diwani wa Kata ya Tuangoma iliyopo Mbagala Dar es Salaam Mohamed Suleiman (kulia) akiangalia vitanda katika moja ya vyumba vya Hostel ya wanafunzi wa kike kwa shule za serikali iliyopo eneo la Mzinga kata ya Tuangoma Dar es Salaam, hosteli hiyo imejengwa kwa ufadhili wa taasisi ya kimataifa ya NAMA Foundation. Wa pili Kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Pamoja Foundation Haji Mrisho.
  Diwani wa Kata ya Tuangoma iliyopo Mbagala Dar es Salaam Mohamed Suleiman akikata utepe kuzindua Hostel ya wanafunzi wa kike kwa shule za serikali iliyopo eneo la Mzinga kata ya Tuangoma Dar es Salaam, hosteli hiyo imejengwa kwa ufadhili wa taasisi ya kimataifa ya NAMA Foundation.
  Mkurugenzi wa Taasisi ya Pamoja Foundation Haji Mrisho akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua Hostel ya wanafunzi wa kike kwa shule za serikali iliyopo eneo la Mzinga kata ya Tuangoma Dar es Salaam iliyojengwa kwa ufadhili wa taasisi ya kimataifa ya NAMA Foundation.
  Mwenyekiti wa Bodi ya taasisi ya Pamoja Foundation Khamis Awadh akizungumza katika hafla ya kuzindua Hostel ya wanafunzi wa kike kwa shule za serikali iliyopo eneo la Mzinga kata ya Tuangoma Dar es Salaam, hosteli hiyo imejengwa kwa ufadhili wa taasisi ya kimataifa ya NAMA Foundation.
  Baadhi ya akina mama waliojitokeza katika hafla ya kuzindua Hostel ya wanafunzi wa kike kwa shule za serikali iliyopo eneo la Mzinga kata ya Tuangoma Dar es Salaam hosteli hiyo imejengwa kwa ufadhili wa taasisi ya kimataifa ya NAMA Foundation.
  Sehemu ya wananchi waliojitokeza katika hafla ya kuzindua Hostel ya wanafunzi wa kike kwa shule za serikali iliyopo eneo la Mzinga kata ya Tuangoma Dar es Salaam hosteli hiyo imejengwa kwa ufadhili wa taasisi ya kimataifa ya NAMA Foundation.

  ………………………………………………………………………….

  Na Mwandishi wetu

  Katika kuwasaidia watoto wa kike kupata elimu kwa ufanisi zaidi taasisi ya Pamoja Foundation kwa ufadhili wa taasisi ya kimataifa ya NAMA Foundation imezindua hostel kwa ajili ya wanafunzi wa kike wa shule za serikali.

  Uzinduzi wa hostel hiyo uliogharimu jumla ya shilingi milioni 50 umefanywa leo na Diwani wa Kata ya Tuangoma Mohamed Suleiman kwa niaba ya Mbunge wa jimbo la Mbagala Ally Mangungu katika eneo la Mzinga wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi wa hostel hiyo, Diwani wa Kata ya Tuangoma Selemani amepongeza ubunifu uliofanywa na taasisi ya Pamoja foundation kwa kuanzisha mradi wa kusaidia wasichana hasa katika masuala ya elimu na kuzitaka taasisi nyingine kushirikiana katika kusaidia masuala ya elimu ili kuleta maendeleo katika sekta ya elimu.

  Aidha, aliwaasa wananchi wengine kuiga mfano wa mwananchi wa eneo la Mzinga kwa kutoa eneo la wakfu kwa ajili ya kujengwa hostel hiyo ambapo alisema uamuzi huo utawezesha kujenga hostel nyingi na kubainisha kuwa eneo la Tuangoma ulipo mradi wa viwanja 20000 yeye kwa kushirikiana na mbunge wa jimbo la Mbagala ataangalia namna ya kupata kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa hostel kwa kuwa katika mradi huo kuna maeneo yametengwa kwa ajili ya shule.

  Diwani huyo wa kata ya Tuangoma alizishauri taasisi nyingine kuangalia namna ya kuwasaidia wanafunzi wanaoshindwa kuendelea na masomo katika fani mbalimbali katika eneo la uchumi ili baadaye nao waweze kusaidia watu wengine.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Pamoja Foundation Haji Mrisho alisema hostel iliyozinduliwa yenye uwezo wa kuwatunza wanafunzi 40 itajulikana pia kama Kituo cha Kuendeleza Wanafunzi ni kwa ajili ya wanafunzi wa shule za serikali.

  Kwa mujibu wa Mrisho, uamuzi wa kuanzisha hostel hiyo unatokana na utafiti uliofanywa na taasisi yake katika wilaya za Ilala, Temeke na Kigamboni kuonesha wanafunzi wanaoishi shule za bweni wanafanya vizuri ukilinganisha na na wale wa shule za kutwa.

  Mkurugenzi huyo wa Pamoja Foundation alisema, kiwanja ilipojengwa hostel ni kiwanja kilichotolewa wakfu na kubainisha bila msaada huo ingekuwa vigumu kuamilisha mradi huo lengo kuunga mkono juhudi za ardhisetikali elimu bure na kuhamiasisha kuunga mkono Serikali kwa kuwa wadau wanaweza kusaidia aidha kwa maabara, hostel ama madarasa.

  Alisema Taasisi yake imeanzisha hosteli hiyo ikiwa ni jitihada za kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano kutoa elimu bure na mwakani taasisi hiyo inatarajia kuanzisha hostel ya wavulana sambamba kuwa na kituo cha mafunzo ya ujasiriamali ili kuwawezesha watakaoshindwa kuendelea na masomo katika viwango tofauti kupata taaluma zitakazowasiadia kimaisha.

  Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo wa Pamoja Foundation, mbali na makazi wanafunzi watakaoishi katika hostel hizo watapatiwa elimu,vifaa mbalimbali vya kujisomea pamoja na mpango wa afya ili wasihangaike katika masuala ya elimu.

  Mrisho alibainisha kuwa, awali taasisi ya Pamoja Foundation ilikuwa na mpango wa kupanga jengo kwa ajili ya hostel lakini kupatikana kwa jengo la kudumu kumewapa faraja kubwa kwa kuwa sasa wamepata mradi wa kudumu.

  Mrisho alisema, lengo Ia uanzishwaji hostel ya wasichana kwa wanafunzi wa shule za Serikali ni kuwawezesha kusoma vizuri hasa ikizingatiwa watoto wa kike wamekuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo majukumu mengi wanapokuwa majumbani ukilinganisha wavulana.

  Mlezi wa Kituo cha Malezi cha Ibnu Jazar kilichopo Vikundi Picha ya Ndege Dar es Salaam Mfaki Mohamed alishauri wasichana watakaopata fursa ya kukaa katika hosteli hiyo kutunzwa vyema ikiwa ni pamoja na wale watakaokuwa na jukumu la kuwalea kuzungumza nao katika njia iliyo bora na kuachana na ile dhana ya kuona kuwa viboko kama njia pekee ya kuwalea wasichana ama wanafunzi na kusisitiza ulelewaji mzuri kwa wasichana basi kutaepusha mzozo

  Kwa mujibu wa Mfaki kwa sasa kuna adui mazingira kwa wasichana ambapo kumekuwa na vishawishi vinavyorudisha nyuma wasichana hasa katika masuala ya maadili na kushauri njia bora ya kukabiliana na hali hiyo ni kuwandaa wasichana kimaadili ili kuepukana vishawishi mbalimbali kwa wale watakaopata fursa katika hosteli hiyo.

  0 0


  Na Hassan Silayo - MAELEZO

  Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas ameendelea na utaratibu wa kuwapigia simu Wakuu wa Taasisi ili kujibu hoja za wananchi moja kwa moja katika ziara yake kwa vyombo habari inayoendelea nchini.

  Katika mahojiano na kituo cha Redio cha Jembe FM 93.7 mkoani Mwanza, 

  Dkt. Abbasi alimpigia simu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii (SSRA), Dkt. Irene Isaka , ambaye alifafanua kuhusu Sheria mpya ya Hifadhi ya jamii.

  Dkt. Irene alisema kuwa baada ya kuunganisha Mifuko mafao yamezidi kuboreshwa ili mstaafu awe anapokea fao kubwa la mwezi.

  Dkt. Isaka amesema kuwa mstaafu atalipwa fao la mkupuo la 25% na baada ya hapo fao la mwezi litakuwa kubwa zaidi tofauti na ilivyokua awali ambapo fao la mkupuo lilikuwa kubwa lakini fao la kila mwezi likawa dogo kumfanya mstaafu ashindwe kumudu maisha.

  Aidha, Mkurugenzi wa SSRA ametaja faida zingine za Sheria mpya kuwa ni familia ya mstaafu kuendelea kulipwa kwa miaka mitatu baada ya mstaafu kufariki, fao la kuachishwa kazi, kuweka usawa katika kulipa mafao na kuwa hivi sasa wanaweka utaratibu wafanyakazi wapate mikopo ya nyumba kupitia pensheni zao.

  Katika mahojiano hayo ya moja kwa moja na Kituo cha Jembe FM, Dkt. Abbasi pia alimpigia simu Mkurugenzi wa Wakala wa Hufuma za Meli (MSCL), Bw. Erick Hamisi kujibu hoja na masuala ya usafiri wa maji hasa ununuzi w meli mpya Ziwa Victoria ulipofikia.

  Bw. Hamisi alielezea vema hatua ambazo Serikali imechukua na inaendelea kuzichukua kuboresha usafiri wa majini.

  Ameeleza kuwa mpaka sasa Serikali imeishatekeleza ujenzi wa meli kubwa ya abiria na mizigo ambao umeanza, ukarabati wa Meli ya MV Victoria ambayo ilikuwa imesimama kutoa huduma Kwa miaka mitano, ukarabati wa MV Ukerewe ambayo ilikuwa haifanyi kazi tangu mwaka 2010 na MV Butiama ambayo baada ya kukamilika itafanya safari za visiwa vya Nansio.

  Amewahakikishia Watanzania kuwa Serikali itaendeleza mageuzi makubwa katika kuufanya usafiri wa majini uendelee kuwa bora na salama.

  Katika mahojiano hayo Dkt. Abbasi alisema kuwa Diplomasia ya Tanzania imeendelea kuimarika kwa kutumia mabalozi wetu bila hata Rais kusafiri nje ya nchi mara kwa mara na imeleta matokeo mazuri katika eneo la uwekezaji.

  Dkt. Abbasi aliongeza kuwa Diplomasia ya Uwakilishi imefanya Tanzania kuwa nchi inayoongoza kwa kuvutia wawekezaji ktk nchi za Afrika Mashariki.“Bila hata Rais kusafiri kwenda China, lakini Tanzania imepata soko kubwa la muhogo kupitia Balozi wetu aliyopo huko na kulifanya zao la muhogo kuwa la biashara,” alisema Dkt. Abbasi

  Akiongelea suala la Ulinzi na Usalama, Dkt. Abbasi alisema kuwa Tanzania imeendelea kuheshimika duniani kwa kushiriki kikamilifu katika ulinzi wa amani duniani na pia kuendelea kuhifadhi wakimbizi kutoka nchi jirani.
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali akifanya mahojiano maalum na kituo cha Radio cha Jembe Fm cha Jijini Mwanza kuhusu miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli
  Mtangazaji wa Kituo cha Redio cha Jembe FM 93.7 mkoani Mwanza, Jimmy Kagaruki akisoma maswali yaliyokuwa yakitumwa na waskilizaji yaliyohusumiaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

  0 0

  Na Zanab Nyamka, Globu ya Jamii.

  Mahafali ya kumi na moja (11) ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) yamefanyika jana kwa jumla ya wahitimu 1769 wametunukiwa katika ngazi mbalimbali.

  Kwenye mahafali hayo wahitimu 1736 wametunukiwa digrii za awali katkka fani mbalimbali, 26 wakitunukiwa stashada ya uzamili katika elimu na 7 wakitunukiwa shahada ya umahiri.

  Akitoa hotuba kwa Mkuu wa Chuo Kikuu Dar es salaam Dkt Jakaya Mrisho Kikwete , Rasi wa Chuo Kikuu Kishirikishi Professa Bernadeta Killian amesema kuwa kati ya wahitimu wote wa mwaka huu wanaume ni 1255 na wanawake ni 514.

  Amesema idadi ya wahitimu kwa upande wa digrii za awali ni kubwa ikilinganishwa na wahitimu wa miaka yote iliyopita, kwani wahitimu wa digrii za awali kwa mwaka 2017 ilikua ni 1443 ambalo ni ongezeko la wahitimu 239 na kufikia 1736 na wahitimu wa masomo ya sayansi kuongezeka mara mbili kutoka 231 kwa mwaka 2017 kufikia 472 kwa mwaka 2018.

  "Ongezeko hilo ni kielelezo cha mafanikio katika jitihada za serikali za kupambana na upungufu wa walimu wa masomo ya Sayansi katika shule za umma na binafsi na kufikia mahafali haya chuo kinakuwa kimetimiza wahitimu 11,436 waliobobea kwenye fani mbalimbali tangu kuanzishwa kwake.

  Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi wa DUCE, Profesa William Anangisye aliwaomba wahitimu wote watambue kuwa maisha ya mtaani sio mepesi yanahitaji kujituma na kufanya kazi kwa bidii hivyo mtalazimika kufanya kazi wakati mwingine katika mazingira magumu lakini kwa maarifa na ubunifu, kuhakikisha mnajikomboa na umaskini na kuisadia Tanzania kufikia maendeleo endelevu.

  Katika mahafali hayo Mkuu wa Chuo Dkt Kikwete alitoa zawadi kwa wahitimu waliofanya vizuri na kuwakabidhi vyetu vyao kabisa.
  Mkuu wa Chuo Kikuu Dar es Salaam, Dkt Jakaya Kikwete akitoa cheti kwa Mwanafunzi Bora wa kike kutoka kitivo cha Elimu Irene Loshiro wakati wa mahafali ya 11 ya Chuo Kikuu Shirikishi cha Elimu Dar es Salaam (DUCE).Mahafali ya kumi na moja (11) ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) yamefanyika jana ambapo jumla ya wahitimu 1769 wametunukiwa katika ngazi mbalimbali.
  Mkuu wa Chuo Kikuu Dar es Salaam Dkt Jakaya Kikwete akitoa cheti kwa Mwanafunzi Bora wa kiume kutoka kitivo cha Sayansi Mohamed Hassan wakati wa mahafali ya 11 ya Chuo Kikuu Shirikishi cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) .
  Mkuu wa Chuo Kikuu Dar es Salaam Dkt Jakaya Kikwete akiwa na  Mwanafunzi Bora wa kike kutoka kitivo cha ElimuIrene Loshiro  na Mwanafunzi bora wa Kiume Kitivo cha Sayansi Mohamed Hassan wakati wa mahafali ya 11 ya Chuo Kikuu Shirikishi cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) jana.
  Wahitimu wakiwa wanatunukiwa kwenye mahafali ya 11 ya Chuo Kikuu Kishirikishi cha Elimu Dar es Salaam (DUCE).
  Maandamano ya Kitaaluma yakiingia uwanjani wakati wa Mahafali ya 11 ya Chuo Ikuu Kishirikishi cha Elimu Dar es Salaam (DUCE).

  0 0


  BY STAFF REPORTER

  Mastercard and Selcom have expanded their collaboration by signing a strategic partnership agreement to introduce a variety of payment solutions in the country, thus supporting Tanzania’s goal of becoming a cashless economy.

  In collaboration with Selcom, Hub 255 has organized the first of its kind Hackathon that has brought together 44 hackers with different skill sets; designers, data scientists, technology and business developers that will showcase utilization of the Masterpass Quick Response (QR) payment Application Programming Interface (API).

  The API allows for consumers to gain access to a wide variety of payment solutions that are accessible on mobile money platforms or via their bank. According to the Marketing Manager of Selcom, Sabrina Munir said Masterpass QR enables millions of micro, small and medium enterprises (MSMEs) across Africa to accept fast and secure digital payments for the first time.

  She said the service addresses challenges previously faced by small business owners who were unable to afford point of sale infrastructure and were forced to transact in cash. As for consumers, this technology eliminates the need to carry cash or traditional bank cards. “Selcom is wholly Tanzanian-owned, with a vision to enhance financial inclusion across Africa through strategic partnerships and alliances to facilitate the seamless movement of funds electronically at all levels,” she said.

  However, One of the Co-founder of Hub255, Jones Mrusha said Hub255 is the first Tanzanian social innovation and entrepreneurship hub that is sector agnostic. “We work with start-ups that are past ideation with either a prototype or significant traction in terms of users or revenue. We provide business development support and product development skills.

  “At Hub255 our startups pass through the innovation framework that requires you to have incorporated at least two sustainable development goals,” he said. He added that Tanzanians have been enabled to transact more conveniently, quickly and securely at more than 20,000 payment acceptance locations. Already consumers, retailers and local businesses are benefiting from the introduction of Masterpass QR currently being implemented across various retailers and merchants.

  Masterpass QR, now available across Africa, provides a fast, convenient and secure payment solution for consumers and a reliable acceptance offering for merchants. Consumers are guaranteed the security of being able to pay for in-store purchases by scanning the QR (Quick Response) code displayed at the checkout on their Smartphone’s or on the printed acceptance materials, or by entering a merchant identifier into their feature phones and using USSD menu.

  Users are also able to use the solution at any location where Masterpass QR is accepted, locally and across the continent. Event was sponsored by Abel & Fernandes Communications and Raha. 
  Winners of Tsh 1,000,000 during the Selcom Masterpass QR- Hackathon at HUB255 from the left Product designer UX/UI, Mbwana Habibu, joined by one of the judges Mercy Kitomari, Andorid Developer, Jackson Twalipo, Head of Software Development at Selcom, Rosario Arun and Back end developer, Athjuman Mwinami. Event has been sponsored by Abel & Fernandes Communications and Raha
  1. First runner-up of Selcom Masterpass QR Hackathon at Hub255 (Sheria kiganjani) from left Advocate, Nabiry Jumanne, Developer- Peter Daniel, Judge- Mercy Kitomari, Head of Software Development at Selcom, Rosario Arun, Business Development Manager- Chris Bweno and Graphics Designer Justine Peterson. Event has been sponsored by Abel & Fernandes Communications and Raha. 
  Second runner-up of Selcom Masterpass QR Hackathon at Hub255 (team locate) from left Software programme- Erick Justin, Judge- Mercy Kitomari, Business personell- Bavius Muganga, Head of Software Development at Selcom, Rosario

  0 0

  Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Mtwara

  Timu ya wataalamu wa Uhakiki wa wakulima wa Korosho imeongezeka katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma kutoka 11 mpaka kufikia timu 20 ili kuongeza uharaka wa uhakiki kwa ajili ya malipo ya wakulima.

  Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga ameyasema hayo tarehe 3 Disemba 2018 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa CBT Mkoani Mtwara kutoa ufafanuzi juu hali ya ununuzi wa korosho.

  Katika mkutano huo pia Waziri Hasunga amesema kuwa timu ya wataalamu tayari imewasili mkoani Pwani kwa ajili ya kuanza uhakiki wa wakulima wa korosho kuanzia leo tarehe 3 Disemba 2018 ambapo mkoa wa Pwani utakuwa mkoa wanne kuhakikiwa ukiungana na mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma.

  Alisema kuwa hadi kufikia tarehe 1 Disemba 2018 jumla ya vyama vya ushirika 212 vilikwisha hakikiwa kati ya vyama 504 vilivyopo katika mikoa hiyo mitatu ya kusini.Aidha, Vyama 157 vimekwishalipwa fedha zao kati ya vyama 617 vinavyojihusisha na korosho nchini.

  Mhe Hasunga alisema kuwa tayari Bilioni 35,540,709,854 zimekwishalipwa kwa wakulima wa korosho ambapo kilo Milioni 10,769 za korosho zimekwishalipiwa.
  Mhe Hasunga ameviambia vyombo vya habari kuwa idadi ya wakulima ambao wameshalipwa mpaka tarehe mosi Disemba ni wakulima 34,938

  Amefafanua zaidi kwa kusema kuwa katika mkoa wa Lindi tayari Bilioni 12.7 zimelipwa ilihali katika Mkoa wa Ruvuma ni Bilioni 4.9 na Mkoa wa Mtwara ni Bilioni 17.9Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa CBT Mkoani Mtwara kutoa ufafanuzi juu hali ya ununuzi wa korosho Tarehe 3 Disemba 2018. (Picha Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo)

  0 0

  Na Said Mwishehe

  UONGOZI na walimu wa Shule ya Mikochen English Medium ya jijini Dar es Salaam wamepongezwa kwa kuendelea kufavya vizuri kielimu ambapo imekuwa ya pili kiwilaya, tano kimkoa na 54 kitaifa katika kundi la shule zenye watoto chini ya 40 katika mtihani wa Taifa wa darasa la saba.

  Pia wamepongezwa kwa kuwandaa wanafunzi katika misingi ya dini na malezi bora wakiwamo wa hitimu wa elimu ya msingi ambao wamefanya mahafali ya grade seven ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Uvuvi Abdalah Ulega.

  Pongezi hizo zimetolewa leo wakati wa mahafali ya shule hiyo ambapo pia viongozi na walimu wamepongezwa kwa namna wqnavyowaandaa wanafunzi katika kuhakikisha wanazingatia masomo.

  Akizungumza kwa niaba ya mgeni rasmi Ulega, Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi kutoka Wizara ya Kilimo na Mifugo Zacharia Kera amesema anaipongeza shule hiyo kwani imepiga hatua kimaendeleo na hasa katika kuwaandaa wanafunzo wake kitaaluma.

  Wakati wa mahafali hayo wazazi na walezi wamejitokeza kwa wingi kuhakikisha wanashuhudia mahafali hayo huku mgeni rasmi akitumia nafasi hiyo kutoa pongezi pia kwa walimu waliofanikisha kuwajenga kielimu wanafunzi ambao wamehitimu shuleni hapo.

  Kera amesema amefurahishwa na namna ambavyo wanafunzi wa shule hiyo wakiwamo wahitimu wa shule ya hiyo ambavyo wameandaliwa vema na kwamba wamejengwa kwenye misingi imara ya kielimu.

  Amewataka wahitimu hao kutambua elimu ndio msingi wa maisha na hivyo wahakikishe wanasoma kwa bidiii kwani mchango wao unahitajika katika kulitumikia taifa kwa siku zijazo huku akioneshwa kufurahishwa na mafunzo ya lugha mbalimbali za kimataifa ambayo yanatolewa shuleni hapo.Amefafanua ili kuendana na dunia ya ushindani ambayo inahitaji mawasiliano ni vema mtu akafahamu alau lugha mbili za kimataifa ambazo zitamuwezesha kuwasiliana na mataifa mengine.

  Pia Kera ameeleza kuwa mzazi au mlezi anatamani kuona mtoto anapata elimu bora,hivyo ameisifu shule hiyo kwa namna ambavyo inatambua kuwaandaa wanafunzi kwenye msingi wa masomo."Najua lengo la mzazi ni mtoto wake kupata elimu nzuri.Niwapongeze viongozi na walimu wa shule ya Mikochen English Medium kwa namna mnavyojitahidi kutoa elimu ambayo imeambatana na misingi ya malezi yaliyobora," amesema.

  Pia amehimiza watoto kulelewa katika misingi ya dini na kwamba shule hiyo ni mfano bora huku akiwataka wanafunzi kutokata tamaa huku akiwahimiza walimu kuendelea kuwalea wanafunzi wa shuleni hapo kwa kuwajenga kimaadili.Ametumia nafasi hiyo kuhimiza wazazi kulipa kodi kwa maendeleo ya nchi yetu na kwamba wawe wanadai risiti kwa miamala ambayo wanaifanya.Kuhusu ombi la kompyuta ambalo limetolewa na uongozi wa shule hiyo, Kera amesema ombi hilo atalifikisha kwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi na anaamini atakuwa sehemu ya watakaosaidia kutafuta ufumbuzi wa ombi hilo.

  Kwa upande wa uongozi wa shule hiyo umeeleza kufurahishwa na hatua mbalimbali za kimaendeleo huku wakizungumzia namna ambavyo wamefaminikiwa kwa wahitimu wao kufanya vema kwenye masomo kwa kupata alama za juu katika mitihani ya Taifa.Wakati huo huo walimu ambao wamewezesha wanafunzi kupata alama A kwenye masomo yao wamezawadiwa fedha ambapo kila alama ya A thamani yake ni Sh.25, 000.

  Hivyo mwalimu wa somo la hesabu katika darasa la saba shuleni hapo ambaye amefanikisha wanafunzi wake kupata alama A 26 na hivyo uongozi wa shule mmempa fedha zaidi ya Sh.600,000 kutokana na jitihada zake za kuwafundisha wanafunzi hao ambao wamefanya vema kwenye mtihani wa taifa wa kumaliza elimu ya msingi.
  Mkuu wa shule ya msingi   Mikocheni English Medium, Zuwena Khamis Omar akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika mahafali dalasa la saba yaliyo fanika mikocheni jijini Dar es Salaam. Shule hiyo imekuwa ya  pili kiwilaya, tano kimkoa na 54 kitaifa.
  Sehemu ya wazazi na walezi wakiwa katika mahafali ya darasa la saba katika Shule ya Mikochen English Medium iliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam. 
   Baadhi ya wazazi na walezi wakiwa katika mahafali ya darasa la saba yaliyofanyika katika Shule ya Mikochen English Medium ya jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Utawala wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Zacharia Kera akizungumza na waandishi wa habari katika mahafali ya darasa la saba ya shule Mikocheni English Medium ambapo amewataka wahitimu kuwa na nidhamu, bidii na kutanguliza uzalendo katika yale watakayokuwa wakifanya ili kufikia malengo yao. (Picha na Emmanuel Massaka wa MMG).
  Sehemu ya wanafunzi wanaomaliza elimu ya dalasa la saba katika shule ya Mikochen English Medium iliyopo jijini Dar es Salaam.


  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akifungua Mafunzo kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa kwenye ukumbi wa Hazina jijni Dodoma, Desemba 3, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
    Baadhi ya Makatibu  Tawala wa Mikoa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakati alipofungua Mafunzo kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa kwenye Ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Desemba 3, 2018. 
    Baadhi ya Wakuu wa Mikoa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua  Mafunzo kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa kwenye Ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Desemba 3, 2018.
   Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Mikoa baada ya kufungua Mafunzo kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa kwenye Ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Desemba 3, 2018. 
   Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Tawala wa Mikoa baada ya kufungua Mafunzo kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa kwenye Ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Desemba 3, 2018. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda baada ya kufungau Mafunzo kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala  wa Mikoa  kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Desemba  3, 2018. Wengine  pichani kutoka kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo,  Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Profesa Joseph Semboja, Waziri Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma  na Utawala Bora, Kapt. (Mst.), George Mkuchika na Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Josephat Kandege.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


older | 1 | .... | 1741 | 1742 | (Page 1743) | 1744 | 1745 | .... | 1897 | newer