Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1740 | 1741 | (Page 1742) | 1743 | 1744 | .... | 1898 | newer

  0 0


  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua Mkakati wa Nne wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI 2018/19 - 2022/23 ambao unatarajia kupunguza maambukizi mapya ya VVU kwa asilimia 75 ifikapo mwaka 2020 na asilimia 85 ifikapo mwaka 2023. Matokeo mengine yanayotarajiwa kufikiwa kutokana na mkakati huo ni kupungua kwa maambukizi mapya ya VVU miongoni mwa watoto kwa chini ya asilimia 5 ifikapo mwaka 2023 na chini ya asilimia 2 ifikapo mwaka 2030.

  Waziri Mkuu amezindua mkakati huo leo (Jumamosi, Desemba 1, 2018) kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika Kitaifa jijini Dodoma na kusema kuwa matayarisho yake yamezingatia matokeo ya mapitio ya Mkakati wa Tatu wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI 2013/14 – 2017/18. Amesema mbali na matokeo hayo pia mkakati huo utawezesha kupungua kwa vifo vinavyohusiana na ukimwi  kwa asilimia  50 ifikapo mwaka 2020 na asilimia 70 ifikapo mwaka  2023 na kupunguza unyanyapaa na ubaguzi ifikapo 2023 na kuelekea kutokomeza kabisa ifikapo mwaka 2030. 

  Hata hivyo Waziri Mkuu amesema mkakati huo umewianisha na kupanga programu mbalimbali zinazosaidia mwitikio wa Taifa zikiwemo afua zinazotekelezwa kupitia mpango wa dharura wa Rais wa Marekani wa uKIMWI (PEPFAR). “Pia Mfuko wa Dunia wa kudhibiti UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria (Globa Fund) na jitihada nyingine za makubaliano ya ushirikiano baina ya nchi mbalimbali na ili kupata matokeo mazuri tunapaswa kuimarisha mawasiliano na uratibu miongoni mwa wadau wote sambamba na kufuata na kutekeleza vipaumbele vilivyoainishwa.”
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Mkakati wa Nne wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi Tanzania (2018/19 – 2022/23) katika Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani Kitaifa, kwenye Kiwanja cha Jamhuri jijini Dodoma, Desemba 1, 2018. Wapili kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na Kulia ni Naibu Waziri wa  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.  Faustine Ndugulile na Kushoto, Mkurugenzi Mtendaji  wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dkt. Leonard Maboko.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha Kitabu  cha  Mkakati wa Nne wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi Tanzania (2018/19 – 2022/23)  baada ya kuzindua  Mkakati huo katika Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani Kitaifa, kwenye Kiwanja cha Jamhuri jijini Dodoma, Desemba 1, 2018.  Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na Kulia ni Naibu Waziri wa  Afya, Maendeleo ya  Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.  Faustine Ndugulile.
   Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa  akimkabidhi Kitabu cha Mkakati wa Nne wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi Tanzania (2018/19 – 2022/23) Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa Nchini, Alvaro Rodriguez baada ya kuzindua Mkakati huo katika Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani Kitaifa, kwenye Kiwanja cha Jamhuri jijini Dodoma, Desemba 1, 2018. Watatu kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na Kulia ni Naibu Waziri wa  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile na Kushoto, Mkurugenzi Mtendaji  wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dkt. Leonard Maboko. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani kwenye Kiwanja cha Jamhuri jijini Dodoma, Desemba 1, 2018.
    Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakipita kwa maandamano mbele ya Mgeni Rasmi, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika Kilele  cha Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani Kitaifa, kwenye Kiwanja cha Jamhuri jijini Dodoma, Desemba 1, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


  0 0

  Na: Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma.

  Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli amesema kituo kipya cha ukaguzi Namanga kinatarajia kuingizia Tanzania Shilingi Bil. 58 mwaka huu wa fedha, 2018/2019. Rais Magufuli ameyasema hayo leo Namanga, Jijini  Arusha wakati wa ufunguzi wa kituo hicho uliofanyika mpakani mwa Tanzania na Kenya.

  Rais Magufuli amesema, kukamilika kwa kituo hicho kumeongeza mapato kutoka wastani wa shilingi Bil. 3 kwa mwezi hadi shilingi Bil. 4.5 kwa mwezi ambapo kwa mwaka huu wa fedha Serikali ya Tanzania inatarajia kukusanya jumla ya shilingi Bil. 58 kutoka katika kituo hicho.

  "Ujenzi wa vituo vya huduma za pamoja mipakani vimerahisha huduma za usafiri na kupunguza gharama za muda.Zamani watu walikuwa wakitumia siku nzima kuvuka mpaka, lakini sasa hivi mtu anatumia dakika 15 tu kuvuka mpaka huo," amesema Rais Magufuli.

  Amesema, kituo hicho kitawawezesha wafanyabiashara kuvusha bidhaa zao zaidi ya mara  Kumi kwa mwezi tofauti na ilivyokuwa mwanzo ambapo ilikuwa nadra kwa mfanyabiashara kuvuka mpaka huo hata mara Nne kwa mwezi.

  Aidha amesema, kituo hicho kitaimarisha shughuli za biashara na utalii kwa nchi zote mbili kutokana na kurahisishwa kwa huduma ya usafiri pamoja na miundombinu mingine katika kituo hicho.

  Kwa upande wake, Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta amesema ni jukumu lao viongozi kuhakikisha wananchi wanafanyabiashara bila kupingwa na waweze kuimarisha biashara kati ya nchi hizo mbili. Amesema dhumuni la ujenzi wa kituo hicho ni kuwarahisishia wafanyabiashara wadogo na wakubwa kufanya biashara zao kwa urahisi, ili kila mwana jumuiya wa Afrika Mashariki aweze kunufaika na umoja huo.

  Aidha amewataka wale wote waliopewa jukumu la kusimamia kituo hicho basi wajue kazi yao sio kumnyanyasa mwananchi bali kumsaidia mwananchi afanye biashara yake. Pia wananchi wajue kuwa wakisaidiwa kufanya biashara hawajaambiwa kufanya biashara ya madawa ya kulevya, kuua wanyama au biashara ya magendo bali wanatakiwa kufanya biashara ya haki ili mtu apate fedha yake ya haki.

  Nae, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe Balozi Dkt. Augustine Mahige amesema, kuwa na kituo kimoja cha forodha na uhamiaji kinaboresha soko la pamoja la Afrika Mashariki. Vile vile amesema, baada ya soko la pamoja, Jumuiya ya Afrika Mashariki inajiandaa kuwa na sarafu moja ifikapo 2020.

  Kituo cha pamoja Namanga kimejengwa kwa ufadhili wa nchi ya Japani kupitia Shirika la Maendeleo la JICA ambapo kwa upande wa Tazania jumla ya shilingi Bil. 18.6 zimegharamiwa . Aidha Benki ya Maendeleo ya Afrika imefadhili kiasi cha Dola za Marekani 117,000 kwa ajili ya kuweka vifaa vya ofisi kwa upande wa Tanzania na Kenya.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wanachi wa Kenya na Tanzania katika eneo la Mpakani Namanga mara baada ya hafla ya ufunguzi wa Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Tanzania na Kenya.  0 0

  Serikali imewahakikishia wafanyabiashara wa mafuta kutoka uganda kuwa imejipanga kutatua  changamoto zote zilizopo kwenye usafirishaji ili kupunguza gharama za uchukuzi  kati ya Tanzania na nchi hiyo. Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, amesema hayo wakati wa kikao maalum kilichowakutanisha wafanyabiashara wa Mafuta wa Uganda na taasisi za Uchukuzi za Tanzania na kusema kuwa Serikali inatekeleza hayo kwa kuboresha miundombinu ili kuvutia wafanyabiashara wengi zaidi

  “Niwahakikishie kuwa changamoto zote zilizoainishwa baada ya majumuisho ya ziara yenu ya siku 5 nchini tutazifanyia kazi", amesema Naibu Waziri  Nditiye. Aidha, Naibu Waziri Nditiye ameongeza kuwa Serikali inaendelea kuboresha miundombinu ikiwemo upanuzi wa bandari,ukarabati wa reli na ukarabati wa meli ili mizigo inayokwenda Uganda kupitia bandari ya Dar es Salaam ifike kwa wakati.

  Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Kampuni ya Meli, Eric Hamis amesema mpaka sasa tayari wamesafirisha zaidi ya tani elfu kumi na tano za Uganda kwa kutumia meli ya MV Umoja na kusema kuwa wamejipanga kusafirisha mzigo mkubwa zaidi kabla ya mwaka wa fedha kuisha. Sisi kama Kampuni ya meli tuliifanyia ukarabati meli ya MV Umoja na imekuwa ikisafirisha mzigo wa Uganda na niwahakikishie kuwa kupitia ziara hii na jitihada nyingine tunazozifanya tutapata wafanyabishara wengine ambao watasafirisha mizigo yao kwa kutumia meli hii” amesema Hamis.

  Kwa upande wake Mchumi Mwandamizi kutoka Wizara ya Ujenzi ya Uganda,  Gerald Akini,  amemwahidi Naibu Waziri Mhandisi Nditiye kuwa yale ya kisera yanayohusu Uganda atayafikisha katika ngazi husika ili yafanyiwe kazi ili kuimarisha ushirikiano uliopo kibiashara. Bw Gerald ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa utayari wake wa kuwapokea wafanyabiashara na kuweka mazingira mazuri ili watumie bandari ya Dar es Salaam.

  Aidha, ameipongeza Serikali kwa kuendelea kuboresha miundombinu ikiwemo kupunguza vituo vya mizani,ujenzi wa reli ya kisasa,uboreshaji wa bandari na kuahidi kuendeleza ushirikiano kwa kushawishi wafanyabiashara wengi zaidi kutumia bandari ya Dar es salaam. Wafanyabiashara wa mafuta kutoka nchini Uganda wamefanya ziara ya siku 5 nchini ambapo wametembelea bandari ya Dar es salaam, Tanga,Mwanza pamoja na kukagua miundombinu ya reli na meli za kampuni ya meli na kuridhishwa na hatua zinazochukuliwa na Tanzania kuimarisha biashara baina ya nchi hizo.
  Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, akiwa katika picha ya pamoja na wafanyabiashara wa mafuta wa Uganda mara baada ya kukutani nao jijini Mwanza.


  0 0

  Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila amefanya ziara ya kikazi tarehe 30.11.2018 kwa kukagua gwaride rasmi lililoandaliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwake.
  Katika ziara hiyo, Mhe.Chalamila alikabidhi magari mawili aina ya Probox kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya ili yatumike katika kuimarisha doria katika barabara kuu ili kupunguza ajali na kupambana na uhalifu.
  Aidha Mhe.Chalamila alikabidhi pikipiki nne aina ya FEKON zilizotolewa na mdau wa Jeshi la Polisi kwa askari Polisi walioonyesha uaminifu katika kazi kwa kukamata fedha zaidi ya Tshs.Milioni 17 zilizokuwa zimeibwa dukani kwa mfanyabiashara mmoja huko Wilayani Chunya.
  Sambamba hilo, Mhe.Mkuu wa Mkoa amekagua kambi ya Polisi Mbeya na kuahidi kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuhakikisha unafanyika ujenzi wa nyumba za kisasa za kuishi askari ili kuongeza morali ya kiutendaji kwa askari wa Jeshi la Polisi.
  Mhe.Mkuu wa Mkoa alikamilisha ziara yake ya kikazi kwa kuzungumza na askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya na kusisitiza uadilifu, nidhamu na uaminifu. Aidha amelitaka Jeshi la Polisi kuendelea kudhibiti ajali za barabarani hasa madereva wa Pikipiki @ bodaboda ambao hawataki kutii sheria za usalama barabarani.
  Pia Mhe.Mkuu wa Mkoa wa Mbeya alitumia ziara hii kutoa tamko kwa wakazi wa Mbeya kuwa siku ya tarehe 09.12.2018 [uhuru wa Tanganyika] watumishi wote wa umma watashiriki kazi mbalimbali ikiwemo ya ujenzi wa majengo ya umma, kufyetua tofali, kuchota maji kwa ajili ya ujenzi na kufanya usafi wa mazingira katika maeneo yote ya Mkoa wa Mbeya.

   Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila akiwasili kuanza  ziara ya kikazi
    Pikipiki nne aina ya FEKON zilizotolewa na mdau wa Jeshi la Polisi kwa askari Polisi walioonyesha uaminifu katika kazi kwa kukamata fedha zaidi ya Tshs.Milioni 17 zilizokuwa zimeibwa dukani kwa mfanyabiashara mmoja huko Wilayani Chunya.
    Magari mawili aina ya Probox kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya ili yatumike katika kuimarisha doria katika barabara kuu ili kupunguza ajali na kupambana na uhalifu.
   Mhe.Chalamila akikabidhi magari mawili aina ya Probox kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya
  Mhe.Mkuu wa Mkoa akikagua kambi ya Polisi Mbeya na kuahidi kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuhakikisha unafanyika ujenzi wa nyumba za kisasa za kuishi askari

  0 0

  Na Benny Mwaipaja. WFM, Dodoma

  CHUO Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, kimeanza ujenzi wa Kiwanda cha Kuchakata Ngozi na Kuzalisha Bidhaa za Ngozi katika Kata ya Idifu, Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma kitakacho gharimu zaidi ya shilingi milioni 500 kitakapo kamilika. Hayo yamesemwa na Kaimu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Hozen Mayaya wakati wa sherehe za mahafali ya 32 ya Chuo hicho Kampasi ya Dodoma, ambapo wahitimu 2,596 wametunukiwa vyeti na shahada mbalimbali.

  "Kupitia mradi wa Eco Act, unaofadhiliwa na Jumuiya ya Ulaya, Chuo kimetekeleza falsafa ya Mhe. Rais Dkt. John Magufuli, ya Ujenzi wa uchumi wa viwanda hiki ambacho kikikamilika kitakuwa na jumla ya wafanyakazi 70, kati ya hao 50 watakuwa wa kudumu na vibarua 20" alisisitiza Prof. Mayaya. Aidha, Prof Mayaya ameeleza kuwa Chuo hicho kinatekeleza mradi mwingine wa kuhimili mabadiliko ya Tabia nchi kwa kuzijengea uwezo Halmashauri za wilaya ya  Longido, Ngorongoro na Monduli mkoani Arusha ambao umepunguza changamoto za ufugaji katika jamii za wafugaji kwa kujenga mabwawa matatu ya kunyweshea mifugo.

  "Mradi huu ni wa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Taasisi za kimataifa za mazingira na Maendeleo (IIED), Mfuko wa Umoja wa Mataifa na Maendeleo (UNCDF LoCAL), mashirika yasiyo ya kiserikali ya Haki Kazi Catalyst (HKC) na Jumuiko la Maliasili Tanzania (TNRF), aliongeza Dkt. Mayaya. Kwa Upande wake, Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Bi. Mugabe Mtani, amesema utekelezaji wa miradi hiyo ya maendeleo ya wananchi umelenga kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano iliyojipambanua kuimarisha uchumi wa nchi na maendeleo ya wananchi kwa ujumla
   Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatib Kazungu akihutubia wahitimu na wageni mbalimbali waliohudhuria katika mahafali ya 32 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini  yaliyofanyika katika Kampasi ya Chuo hicho, Dodoma.
   Kaimu Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Prof. Hozen Mayaya, akitoa taarifa ya maendeleo ya Chuo kwa wahitimu na wageni mbalimbali waliohudhuria katika mahafali ya 32 ya Chuo hicho  yaliyofanyika katika Kampasi ya Chuo, Dodoma.
   Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu akimtunuku Shahada ya Uzamili, mmoja wa wahitimu katika mahafali ya 32 ya chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini yaliyofanyika katika Kampasi ya chuo hicho, Dodoma.
   Baadhi ya wahitimu wa kada mbalimbali katika chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini wakiwa katika sherehe za  mahafali ya 32 ya chuo hicho  yaliyofanyika chuoni hapo Jijini Dodoma.
  Baadhi ya wahitimu wa Shahada ya Uzamili katika Chuo cha Maendeleo Vijijini wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu,  wakati wa Mahafali ya 32  yaliyofanyika chuoni hapo Jijini Dodoma.   
  (Picha na Saidina Msangi-Wizara ya Fedha na Mipango)


  0 0

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi imewasihi wapiga kura wote waliojiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na wanaoishi kwenye kata Sita za Tanzania Bara, kujitokeza kwa wingi kupiga kura siku ya Jumapili  Desemba 2  mwaka huu ili kuwachagua viongozi wanaowataka wawaongoze kwa kipindi cha takribani miaka miwili ijayo.

  Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Semistocles Kaijage wakati akisoma risala ya uchaguzi mdogo wa Udiwani unaohusisha  kata za Miteja, Kivinje au Sigino , Somanga na Mitole  katika Halmashauri ya Kilwa, kata ya Muhinda katika Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe na Kata ya Nkoanekoli katika Halmashauri ya wilaya ya Meru.

  “Wapiga Kura wapatao 31,818 wanatarajiwa kupiga Kura kuwachagua Madiwani katika Kata 6 za Tanzania Bara na uchaguzi huo utafanyika katika Vituo 91 vya Kupigia Kura ambako ndipo Wapiga kura walijiandikishia kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2015. Aliwataka kwenda kupiga kura bila hofu, woga, wasiwasi au ushawishi kwani chini ya Kanuni ya 3.1 (b) ya Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015, Serikali imepewa wajibu wa kuhakikisha kuwa kuna hali ya usalama, amani na utulivu katika kipindi chote cha Uchaguzi.

  Mbali na wito huo, Jaji Kaijage aliwataka wananchi, vyama vya Siasa na wadau wote wa uchaguzi kushirikiana ili kuhakikisha kuwa viashiria vya kuvunjika kwa amani na utulivu vinaepukwa ili uchaguzi utakaofanyika uwe huru, wazi na wa haki. Jaji Kaijage alivisisitiza vyama vya siasa kufanya  mikutano ya kampeni inatakiwa kufikia mwisho leo Jumamosi  saa kumi na mbili kamili (12:00) jioni na baada ya muda huo, vyama, wagombea na mashabiki waache kufanya kampeni za aina yoyote, kama vile kutumia alama za vyama zinazoashiria kampeni, vipeperushi, bendera, mavazi na vitu vingine visivyokubalika katika siku ya Uchaguzi.

  “Aidha, wananchi waheshimu Sheria za Nchi wakati wote wa upigaji, kuhesabu, kujumlisha kura na kutangaza matokeo. Pale panapokuwa na malalamiko yoyote ya ukiukwaji wa Sheria na Taratibu za Uchaguzi, malalamiko hayo yafikishwe kwenye mamlaka inayohusika kwa utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa Sheria.”, alisema Jaji Kaijage na kuongeza kuwa:

  “Vivyo hivyo, Viongozi wa Vyama vya Siasa, Wagombea au wafuasi wao na wananchi kwa ujumla wajiepushe na vitendo vinavyoweza kusababisha fujo au vurugu katika vituo vya Kupigia, Kuhesabia na Kujumlishia Kura.” Jaji Kaijage aliwataka wapiga kura kuondoka kwenye maeneo ya kituo cha kupigia kura mara baada ya kupiga kura na kujiepusha na mikusanyiko au mikutano katika maeneo ya vituo vya kupigia kura kwani vyama vya siasa vimeweka mawakala vituoni ambao watalinda maslahi ya vyama husika na wagombea wao.  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe.Waziri Mhagama ameuagiza uongozi wa Shiriki la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kubadili mitazamo dhaifu ya kiutendaji na kuanza kufanya kazi kwa kuongozwa na uzalendo ili kuleta tija na kufikia malengo ya Shirika hilo.

  Ametoa kauli hiyo mapema mwishoni mwa wiki hii (Novemba 29, 2018) alipofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi inayoratibiwa na shirika hilo ikiwemo ya ujenzi wa nyumba za bei nafuu Dar es Salaam. Maeneo aliyotembelea ni pamoja na; miradi wa nyumba za bei nafuu za Dungu, Mtoni Kijichi, Tuangoma na Mzizima pamoja na nyumba za Dege Beach Jijini Dar es Salaam.

  Aidha, Kauli ya waziri imekuja mara baada ya kutoridhishwa na hali ya maendeleo ya ujenzi wa miradi hiyo na kuuagiza uongozi wa Shirika hilo kubadili mitazamo ili kuwa na malengo yanayotekelezeka na kwa wakati. “Kwa muda mrefu mmekuwa mkifanya kazi kwa kujitenga katika makundi, mnapaswa kubadili mitazamo hasi na kuwa na mitazamo chanya yenye utendajikazi katika hali ya umoja ili kuendelea kubadili NSSF ili iwe na uzalizaji wa tija”.alieleza Mhagama

  Waziri aliongezea kuwa Shiriki linapaswa kubadili hali za mazoea yaliyokuwa si mazuri ili kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano iliyojikita katika uwajibikaji wa kizalendo. “Lazima mbadili mitazamo ya uongozi  wa mazoea na kuanza kufanya kazi kwa umoja ili kuwa na matokeo chanya yanayokusudiwa ili kuwa na tija kwa jamii na Serikali kwa ujumla”.Alisisitiza Mhagama
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Waziri Mhagama akiuliza jambo kwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Bw.William Erio wakati wa ziara yake katika mradi wa ujenzi wa nyumba za Denge Beach Kigamboni Jijini Dar es Salaam Novemba 29, 2018.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Waziri Mhagama akiangalia ramani ya ujenzi wa mradi wa Dege Beach Kigamboni uliojengwa na Shirika la Mifuko wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF Dar es salaam, wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa mradi huo.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Waziri Mhagama akiuliza jambo kwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Bw.William Erio (mwe nye koti la kijivu) wakati wa ziara yake eneo la Dungu lenye nyumba 439 ambapo tayari nyumba 94 zimekamilika katika eneo hilo.
   Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya NSSF Bi Jayne Nyimbo akitoa maelezo ya ufafanuzi kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Waziri Mhagama wakati wa ziara yake katika mradi wa nyumba za Dege Kigamboni Dar es Salaam.


  0 0

  Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Itete Sports Agency ,Antipas Mgungusi ambao ndio waandaaji wa Mbio za Morogoro Marathon akizungumza na  wanahabari kuhusu tukio hilo litakalo fanyika kesho katika uwanja wa Jamhuri ,kushoto kwake ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro Pascal Kihanga,Kaimu Afisa Michezo mkoa wa Morogoro ,Grace Njau na kulia ni Fuhad Hussein ,Meneja wa DSTV mkoa wa Morogoro ambao ndio wadhamini .
  Medali zilizoandaliwa kwa ajili ya washiriki wa mbio hizo ambazo zitatolewa Mbili kwa kila mshiriki .
  Meneja wa DSTV mkoa wa Morogoro ,Fuhad Hussein akizungumza juu ya zawadi za Ving'amuzi zitakazo tolewa kwa washindi wa mbio za Km 21 na Km 5.
  Mkurugenzi wa Mbio,Robert Kaliyahe akitoa ufafanuzi wa njia zitakazo tumiwa na wakimbiaji siku ya Kesho.
   Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii  .
  WAANDAAJI wa Mashindano ya Mbio za Morogoro Marathon 2018 wametangaza kutoa zawadi ya Medali mbili kwa kila mshiriki wa tukio hilo ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa tukio  kubwa la kimichezo katika mkoa wa Morogoro.
  Waandaaji hao ambao ni taasisi ya Itetet  Sports Agency imetangaza zawadi hiyo jana mbele ya waandishi wa habari wakati wa kuzungumzia maandalizi ya Mbio hizo zitakazofanyika kesho alfajiri katika uwanja wa Jamhuri mjini humo.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Itete Sports Agency ,Antipas Mgungusi alisema mbali na zawadi hizo kwa washiriki pia zipi zawadi kwa washindi wa mbio za Kilometa 21 kwa upande wa wanaume na wanawake ambapo mshindi wa kwanza atapata pesa taslimu kiasi cha sh 400,000 .
  “Tuna mbio za Kilometa 21 pamoja na kilometa tano,lakini uwanjani kutakuwa na mbio za kushirikisha watoto kwa maana ya mita 100 na mita 200 ,kwa kilometa 21 mbali na pesa taslimu mshindi pia atapata king’amuzi cha DSTV kutoka kwa wadhamini kampuni ya Multchoice “alisema Mgungusi.
  Alisema Mshindi wa pili atapata kiasi cha sh 250,000 pamoja na king’amuzi cha DSTV,mshindi wa tatu akiambulia kitita cha Sh 150,000 pamoja na king’amuzi cha DSTV huku wale watakaoshiriki mbio za Km tano mshindi wa kwanza atapata sh 100,000 pamoja na King’amuzi cha DSTV kwa jinsia zote mbili.
  “Mshindi wa pili kwa kilometa 5 tutatoa kiasi cha sh 50,000 pamoja na T shirt ,mshindi wa tatu atapata cheti pamoja na t shirt nah ii ni kwa wanawake na wanaume watakao shiriki lakini zawadi kubwa zaidi itakuwa ni udhamini kwa washindi watatu wa kilometa 21 na tani kwa wanaume watapata udhamini wa kushiriki mashindano yajayo hapo mwakani”alisema Mgungusi.
  Alisema katika eneo hilo washindi hao watagharamiwa ,fedha za safari,malazi na usajili kwa ajili ya kushiriki mashindano yajayo huku wengine washiriki wengine watakaoingia hatua ya 10 bora wao watashiriki mashindano yajao bila kulipia ada.
  Akizungumzia kuhusu maandalizi ,Mkurugenzi wa Mbio ,Robert Kaliyahe alisema maandalizi yamekamilika kwa kiasi kikubwa ikiwa ni pamoja na upimaji wa njia zitakazotumika kwa wakimbiaji wa mbio za kilometa 21 na zile za kilometa tano.
  “ tumefanya maandalizi ya kutosha katika mbio hizi,tayari tumewasiliana na wenzetu wa jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani kwa ajili ya kuhakikisha usalama kwa wakimbiaji wakati wa kuanza  mbio pale uwanja wa Jamhuri  na baada ya mbio kuhitimishwa.
  Mstahiki meya wa Manispaa ya Morogoro ,Pascal Kihanga amesema mkoa wa Morogoro unakwenda kuandika historia nyingine kwa kuuingiza mkoa huo katika medani ya mchezo wa riadha kwa kuanzisha mashindano ya Morogoro Marathoni.
  “Mrogoro inavivutio vingi ambavyo vimekuwa havitangazwi lakini kwa kupitia mashindano haya tutapata fursa mpya ya kutangaza vivutio vyetu ambavyo vitaendelea kuutangaza vyema mkoa wetu wa Morogoro.”alisema Kihanga .
  Mbio za Morogoro Marathon 2018 zinafanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Morogoro huku watu zaidi ya 3000 wakitazamiwa kuanza kukimbia kuanzia majira ya saa 12:30 na kwamba zoezi la usajili kwa wakimbiaji linaendelea katika vituo mbalimbali nchini na litafungwa saa 12:00 siku ya tukio.

  0 0
 • 12/01/18--10:54: Article 1

 • Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk. Leo Zekeng amesema kuwa kuwa shirika hilo litaendelea kushirikiana na Serikali katika mapambano dhidi ya Ugonjwa huo.

  Akizungumza jana Jijini Dodoma wakati wa kilele cha shughuli za vijana kuelekea maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani, Dk Zekeng alisema kwamba kuna haja kubwa ya kuhakikisha kwamba taifa linapambana na maambukizi mapya kwa kuhakikisha kwamba kunatolewa huduma rafiki miongoni mwa vijana ambao ndio kundi kubwa linalohitaji msaada kwa sasa ni jukumu la kila mwanajamii na kuomba ushirikiano wadau wote katika mapambano hayo.

  Alisema wakati taifa nusu yake ni vijana wenye umri kati ya miaka 15-24 na huku takwimu zikionesha kwamba kundi hilo linaathirika sana ipo kila sababu ya kutengeneza mkakati na kuweka mazingira rafiki ili kuokoa kizazi hicho. Alisema kwa sasa vijana wanahitaji kusaidiwa kwa kuwaweka katika mazingira rafiki ya kuhitaji huduma zinazotolewa katika kampeni ya kukabiliana na maambukzi ya VVU.
   Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mh. Antony Mavunde akihutubia wananchi wa Dodoma wakiwemo vijana wakati wa hafla ya kufunga wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.
   Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk. Leo Zekeng akitoa salamu za Umoja wa Mataifa wakati wa hafla ya kufunga wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.
   Balozi wa Vijana ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Mh. Jokate Mwegelo akizungumza na hadhira ya vijana (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kufunga wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko akitoa neno kwa mgeni rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mh. Antony Mavunde wakati wa hafla ya kufunga wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.
   Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mh. Antony Mavunde akikabidhi zawadi ya kombe ya mshindi wa kwanza kwa kapteni wa timu ya mpira ya vijana walio nje ya shule ya Panama, Bw. Dunia Salumu wakati wa hafla ya kufunga wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo  kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.
   Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mh. Antony Mavunde akikabidhi zawadi ya kombe ya mshindi wa kwanza kwa kapteni wa timu ya mpira wa pete ya Vijana Queens, Ngesa Selemani wakati wa hafla ya kufunga wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.
  Baadhi ya wakazi wa Dodoma walioshiriki hafla ya kufunga wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.


  0 0

   


  Makamu Mkuu wa chuo Kikuu Ardhi, Profesa Evaristo Liwa akimkaribisha Mkuu wa Chuo, Mhe Cleopa David Msuya kuhudhurisha mahafali ya 12 ya chuo Kikuu Ardhi yaliyfanyika jijini Dar es Salaam Disemba 1. 2018. Kulia ni Mwenyekiti Mpya wa Baraza la Cho, Balozi Costa Kahalu na viongozi waandamizi wa ARU. (Imeandaliwa na Robert Okanda)
  Bendi ya polisi ikitumbuiza wakati wa mahafali hayo jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti Mpya wa Baraza la Chuo, Balozi Costa Mahalu akitoa hotuba yake wakati wa kuhudhurisha mahafali ya 12 ya chuo Kikuu Ardhi yaliyofanyika jijini Dar es Salaam Disemba 1. 2018. Jumla ya wahitimu 974 wa shahada mbalimbali walitunukiwa stahili zao.  Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi, Mhe. Cleopa David Msuya akimtunuku Samweli Sanga Digrii ya uzamivu (Doctor of Philosophy) ya ARU wakati wa kuhudhurisha mahafali ya 12 ya chuo Kikuu Ardhi yaliyofanyika jijini Dar es Salaam Disemba 1. 2018. Kulia ni Mwenyekiti Mpya wa Baraza la Chuo, Balozi Costa Kahalu na Makamu Mkuu wa ARU, Profesa Evaristo Liwa. Jumla ya wahitimu 974 wa shahada mbalimbali walitunukiwa stahili zao.
  Sehemu ya wahadhiri waandamizi wa Chuo Kikuu Ardhi wakifuatilia mahafali hayo.
  Sehemu ya wahitimu wakifurahia baada ya kutunukiwa stahili zao.

  Sehemu ya wahitimu wakifurahia baada ya kutunukiwa stahili zao.

  Sehemu ya wageni na ndugu wa wahitimu wakifuatilia matukio katika mahafali hayo.

  Sehemu ya wahitimu wakifurahia baada ya kutunukiwa stahili zao. 

  0 0

  Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Bi. Mariam Mwaffisi akisoma hotuba yake wakati wa mahafali ya 12 ya chuo hicho yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu MUHAS, Profesa Andrea Pembe. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Profesa Andrea Pembe akisoma hotuba yake wakati wa mahafali ya 12 ya chuo hicho yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. Pembeni kulia ni Mkuu wa Chuo hicho Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Bi. Mariam Mwaffisi.
  Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Prof. Appolinary Kamuhabwa akiwakaribisha wakufunzi kusoma majina ya wahitimu.
  Mkuu wa  Chuo Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi akimtunuku Shahada ya Uzamili, mmoja wa wahitimu katika mahafali ya 12 ya Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
  Sehemu ya wahitimu waliotunukiwa astashahada, stashahada, shahada za awali na shahada za uzamili wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) jijini Dar es salaam.
  Bendi ya Jeshi ikisherehesha katika mahafali ya 12 ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS). 
  Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi akimtunuku astashahada, stashahada, shahada za awali na shahada za uzamili wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) wakati wa mahafali ya 12 yaliyofanyika jijini Dar es salaam. 
  Wahitimu wa astashahada, stashahada, shahada za awali na shahada za uzamili katika upande wa afya wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) wakila kiapo cha uaminifu wakati wa mahafali ya 12 yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.  Wahitimu wakifurahia.
  Meza kuu wakiimba wimbo wa Taifa wakati wa kuhitimisha sherehe.
  Meza kuu ikipata picha na baadhi ya wahitimu.

  0 0

  Wakati umefika kwa Watanzania wote kuitumia Ofisi ya Uratibu wa shughuli za SMZ Dar es salaam ili kupata maelekezo na Ushauri utakaowawezesha kupata huduma mbali mbali zinazotolewa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika ngazi na Sekta zote.

  Uamuzi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wa kuanzisha Ofisi hiyo muhimu Mwaka 2013 kuratibu wa Shughuli za Serikali umelenga kuwaondoshea usumbufu Wananchi wanaoishi upande wa Tanzania Bara pamoja na Taasisi za Kimataifa zinazohitaji huduma za Serikali.

  Mratibu Mkuu wa Ofisi ya Uratibu wa shughuli za SMZ Dar es salaam Ndugu Issa Mlingoti Ali alitoa kauli hiyo katika Kipindi Maalum cha matayarisho ya maandalizi ya sherehe za kutimia Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964 hapo Ofisini kwake Mjini Dar es salaam.

  Ndugu Mlingoti alisema huduma za Ofisi hiyo kwa kiasi kikubwa hivi sasa zinatumiwa zaidi na Viongozi Wakuu na wale Waandamizi jambo ambalo bado halijakidhi azma ya kuanzishwa kwake licha ya kwamba yapo mambo mengi na ya msingi yanayoweza kuratibiwa ambayo yanamuhusu pia Mwananchi wa kawaida.

  Alisema Ofisi hiyo kupitia Maafisa wake wa Sekta Tofauti ina mamlaka ya kusikiliza na kuyachukulia hatua matatizo yanayowakumba Wananchi sambamba na kuwa kiunganishi cha mawasiliano ya ushirikiano baina ya Taasisi za SMS na zile za Tanzania Bara pamoja na za Kimataifa katika Sekta tofauti.

  Mratibu Mkuu huyo wa Ofisi ya Uratibu wa Shughuli za SMZ Dar es salaam alifahamisha kwamba yapo mafanikio makubwa yaliyopatikana tokea kuasisiwa kwa Ofisi hiyo ndani ya Awamu ya Saba ya Uongozi wa SMZ ambayo yanafaa kuendelezwa.

  Nd. Mlingoti alitolea mfano uchelewaji wa malipo ya masomo kwa baadhi ya Wanafunzi wa Zanzibar wanasoma Vyuo tofauti vya Tanzania Bara pamoja na changamoto iliyowapata Wafanyabiashara wa Maboti ambapo Ofisi ilifanikiwa kukabiliana na changamoto hizo na kuzipatia ufumbuzi licha ya ukosefu wa Bajeti Maalum.

  Alisema katika kuimarisha ushirikiano na uhusiano wa Kimataifa Uongozi wa Ofisi hiyo tayari umeshazitembelea Ofisi za Kibalozi 18 na Jumuiya Tatu za Kimataifa ziara ambayo pamoja na mambo mengine yalifanyika mazungumzo na kuleta mafanikio kwa SMZ.

  “ Tumeshatembelea na kufanya mazungumzo ya ushirikiano na Uongozi wa Ofisi za Kibalozi za Ireland, Bahrain, Switzerland, Afrika Kusini, Namibia, Italily, Sweden, Norway, Brazil, Japan, na Taasisi za Kimataifa za Jica, Juice na Looks”. Alisema Mratibu Mkuu huyo wa Uratibu wa Shughuli za SMZ Dar es salaam.

  Ndugu Mlingoti alifahamisha kwamba hatua hiyo imepelekea Ofisi ya Uratibu kuingizwa katika Kamati Maalum ya ushirikiano kati ya Tanzania na Japan chini ya Jumuiya ya Maendeleo ya Japani {JICA}.

  Alisema Kamati hiyo tayari imeshaanzisha Mpango wa kuwaendeleza Watanzania kupata fursa za ajira pamoja na nafasi za masomo katika ngazi ya Shahada kwenye vyuo mbali mbali Nchini Japani ambapo Zanzibar tayari imeshafanikiwa kupata Wahitimu Wanane katika Awamu Nne tokea kuanzishwa Mpango huo.
  Mratibu Mkuu wa Uratibu wa Shughuli za SMZ Dar es salaam Nd. Issa Mlingoti Ali Kushoto akisalimiana na Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa huku Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifurahia wakati walipofika Nyumbani kwake Dar es salaam kutambulishwa Rasmi baada ya kuteuliwa kuwa Mratibu Mkuu.
  Mratibu Mkuu wa Uratibu wa Shughuli za SMZ Dar es salaam Nd. Issa Mlingoti Ali akisalimiana na baadhi ya Mabalozi wa Nchi za Nje waliopo Tanzania wakati akiwa katika ziara za kuimarisha ushirikiano kati ya Ofisi hizo za Kidiplomasia na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.Picha na – OMPR – ZNZ.

  0 0  Na Jeshi la Polisi.

  Jeshi la Polisi nchini limetangaza kuanza kwa Operesheni kali ya kuwabaini na kuwasaka watu wote wanaojihusisha na wizi wa mafuta katika mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR)unaoendelea kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro.

  Hayo yamesemwa na Mkuu wa Operesheni Maalum za Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi DCP Liberatus Sabas wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wafanyakazi wanaofanya kazi katika mradi wa reli hiyo katika kambi ya ujenzi ya Soga mkoani Pwani na Ngerengere wakati wa ziara yake katika mradi huo kufuatia kuwepo kwa vitendo vya wizi wa mafuta.

  Sabas amesema Operesheni hiyo haitamwacha salama yeyote atakayekutwa akishiriki na kufanikisha vitendo vya wizi katika mradi huo na kuwataka wafanyakazi hao kuwa wa kwanza kutoa taarifa pindi waonapo viashiria vya wizi katika maeneo yao ili mradi huo uwe salama.

  “Polisi tutatumia kila aina ya nguvu zetu kuhakikisha kuwa mradi huu unakuwa salama na tukikamata mwizi wa mafuta katika mradi huu hatasahau maisha yake yote kwa kuwa kuhujumu mradi huu muhimu kwa taifa ni kosa kubwa hasa ukizingatia gharama kubwa ambazo Serikali inatua kufanikisha jambo hili” Alisema Sabas.
  Katika hatua nyingine DCP Sabas amewaelekeza Makamanda wa Polisi wa mikoa ya Pwani na Morogoro kuweka mikakati kabambe kwa kushirikiana na Kikosi cha Polisi Reli ili kufanya doria za mara kwa mara katika vijiji vinavyozunguka mradi huo kwa kuwa ndipo kulikobainika kuuzwa mafuta ya wizi wa mradi huo.

  Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Kikosi cha Reli amesema wamekuwa wakifanya vikao vya mara kwa mara na wadereva wa mitambo na magari katika mradi huo kwa lengo la kuwataka kushiriki katika kutoa taarifa za wizi na kuacha kujihusisha na vitendo hivyo ambapo waliokamatwa tayari wamefikishwa Mahakamani.

  0 0

  SERIKALI ya Awamu ya Tano imeendelea kutumia ubunifu katika kuwahudumia wananchi ikiwemo kujibu na kufafanua kero zao papo kwa papo.

  Katika hatua isiyokuwa ya kawaida, Msemaji Mkuu wa Serikali leo akiwa ziarani mkoani Morogoro alilazimika kuwapigia simu baadhi ya watendaji wa Serikali akiwa moja kwa moja studio za Redio Abood FM na ATV ili wajibu kero za sekta zao.

  Afisa wa kwanza kukumbana na "kibano" hicho alikuwa Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), Bw. Paschal Shelutete ambaye alipigiwa kwa mstukizo na kuunganishwa moja kwa moja studio ili ajibu swali la mwananchi aliyelalamikia tembo kutoka hifadhi mbalimbali kuvamia mashamba ya wananchi na kuharibu mazao.

  Bw. Shelutete akionekana kulijua vyema eneo lake alifafanua kuwa kutokana na changamoto hiyo Tanapa na Mamlaka nyingine za Serikali kama Idara ya Wanyamapori zimekuwa na programu za kuwaelimisha wananchi wanaokaa karibu na hifadhi na mapori ya akiba.

  "Tunaendelea kuwaelimisha wananchi wahakikishe wanatoa taarifa hizi kila wanapowaona wanyama wa porini wanarandaranda katika maeneo yao ili mamlaka zichukue hatua stahiki," alifafanua akitoa maelekezo ya hatua za kufuatwa.

  Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Mawasiliano katika Shirika la Reli Tanzania (TRC), Jamila Mbarouk naye alipokurupushwa na kuunganishwa studio moja kwa moja kwa njia ya simu alifafanua vyema swali la mwananchi aliyetaka kujua utaratibu wa fidia kwa watakaoguswa na ujenzi wa reli ya kisasa (SGR).

  Bi. Jamila aliwahakikishia wananchi wote nchini ambao wataguswa na ujenzi unaoendelea sasa kuwa watalipwa kwa mujibu wa sheria na hakuna atakayeonewa na wale ambao hawajapokea malipo taratibu zinakamilishwa.Hata hivyo alifafanua kuwa wale waliojenga ndani ya hifadhi ya reli hawatahusika kulipwa ila wataombwa kupisha ujenzi huo ili uendelee kwa kasi kwa manufaa ya watanzania wote.

  Dkt. Abbasi alisisitiza kuwa watendaji wa umma kwa sasa wanapaswa kujua kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Haki ya Kupata Taarifa na Sheria ya Huduma za Habari wanapaswa wakati wowote kutoa habari na ufafanuzi muhimu kwa umma isipokuwa tu kwa masuala yaliyozuiwa kwa mujibu wa sheria.

  Aidha alisisitiza kuwa viongozi wa umma wakiwemo maafisa habari wanapaswa kutangaza utekelezaji wa ahadi za Serikali kwa kujua kinachoendelea wakati wote ili wananchi wasiwe na shida au kupata mkanganyiko usio wa lazima.

  Akizungumza wakati wa kuhitimisha kipindi hicho Dkt. Abbasi alisema Rais Dkt. Magufuli amedhamiria kuondoa kero za watanzania hivyo kila mtendaji wa Serikali lazima ashiriki katika safari hiyo na awe tayari kuzitatua kero zilizoko ktk eneo lake kwa haraka.

  "Kwa kuwa nimebaini wananchi yako maeneo mengi wameielewa ajenda ya Mhe Rais lakini yapo maeneo machache wanatakiwa kupata ufafanuzi zaidi kuanzia sasa viongozi wa ngazi zote wajiandae popote tulipo na wao popote walipo tutawapigia simu wafafanue na kujibu kero za wananchi.Utaratibu huu utaendelea kwa kustukiza hivi hivi," alisema Dkt. Abbasi.

  0 0


  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akifunua kitambaa, ishara ya kuweka jiwe la msingi la ukarabati wa kituo cha Afya Koromije, ikiwa in sehemu ya majukumu katika ziara yake ya kukagua hali ya ubora wa huduma za Afya Mkoani Mwanza.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiendelea na ukaguzi wa miundombinu katika kituo cha Afya Koromije, ikiwa in mwendelezo wa ziara yake ya kukagua hali ya ubora wa huduma za Afya Mkoani Mwanza.
  Mbunge wa Jimbo la Misungwi Mhe.Charles Kitwanga akisema jambo mbele ya wapiga kura wake (hawapo kwenye picha) katika kijiji cha Koromije Wilaya ya Misungwi Mkoa wa Mwanza wakati wa ziara ya Waziri wa Afya ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya kijijini hapo.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akihutubia wanakijiji wa Koromije (hawapo kwenye picha) pindi alipofanya ziara yake ya kukagua hali ya utoaji wa huduma za Afya Mkoani Mwanza.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiongea na watoto wa kike baada ya kutoa burudani ya ngonjera, wakati wa ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya Mkoani Mwanza.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiitazama chupa iliyo na Wine iliyotengenezwa na kikundi cha wanawake kijijini hapo kwa lengo la kujikwamua kiuchumi.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiangalia gharama za matibabu kwenye mbao ya matangazo katika Hospitali ya Wilaya ya Misungwi.


  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akimjulia hali mtoto aliyefika na mama yake katika Hospitali ya Wilaya ya Misungwi ili kupata huduma za Afya.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akikagua hali ya Dawa katika stoo yakuhifadhia Dawa katika Hospitali ya Wilaya ya Misungwi.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu (wakatikati) akikagua chumba cha kupima makohozi katika Hospitali ya Wilaya ya Misungwi.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akikagua jengo linaloendelea kujengwa la wagonjwa wa nje (OPD) katika Hospitali ya Wilaya ya Misungwi.

  ………………………….

  Na WAMJW – MISUNGWI, MWANZA

  SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeitaka Bohari Kuu ya Dawa nchini (MSD) kuhakikisha wanakamilisha kuleta vifaa vyote vinavyohitajika katika vituo vya Afya vinavyoboreshwa nchini kabla ya Januari 15, 2019 ili wananchi waweze kupata huduma.

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy wakati akiweka jiwe la msingi la ukarabati wa kituo cha Afya Koromije na kukagua hali ya utoaji Huduma za Afya katika Hospitali ya Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza.

  “Haina maana ya kuwa na majengo makubwa na mazuri ya Vituo vya Afya kama hakuna vifaa vinavyohitajika, huku Wananchi wanaendelea kupata tabu”, alisema Waziri Ummy.

  Aidha, Waziri Ummy amewahasa Wazazi na Wananchi wote kwa ujumla kutodharau huduma za Chanjo, hivyo kuwahimiza Wananchi wote kuwapeleka katika vituo vyakutolea chanjo watoto waliofika umri wa kupata chanjo

  “Kifafa, Kifaduro,Donda koo, Surua, hayapo siku hizi kwasababu ya Chanjo, kwahiyo tusije tukadharau chanjo, tuhakikishe kila mtoto mwenye umri wakupata chanjo , akapate chanjo” alisema Waziri Ummy Mwalimu.

  Aidha, Waziri Ummy amewataka Wananchi wa Misungwi kuhakikisha wanasafisha mazingira, na kutumia vyandarua vyenye dawa ili kuepuka kupata ugonjwa wa Malaria ambao umeendelea kuwa hatari nchini hasa kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5 na Wanawake Wajawazito.

  “Ugonjwa wa Malaria umepungua kutoka Asilimia 37 hadi Asilimia 27, kwahiyo niendelee kuwahimiza Wananchi wa Misungwi, kwanza kuhakikisha wanafukia vidimbwi vya maji, kusafisha mazingira na kulala kwenye vyandarua vyenye dawa” Alisema Waziri Ummy.

  Waziri Ummy aliendelea kusisitiza kuwa sio kila homa ni Malaria, hivyo kuwataka Wananchi kutotumia dawa bila kwenda kupata vipimo katika Kituo cha kutolea Huduma za Afya na kuthibitishwa kuwa una Malaria.

  Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt. Rutha Thomas alisema kuwa Mkoa wa Mwanza unaishukuru Serikali kwa kuwapatia jumla ya shilingi Bilioni 2 zitakazotumika katika ujenzi wa Hospitali 2 za Hamashauri za Ilemela na Bushosa.

  0 0

  Na. VERO IGNATUS, ARUMERU

  Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mhe John pombe magufuli anatazamia kuweka jiwe la msingi katika mradi wa uboreshaji wa huduma ya maji safi na usafi wa mazingira jijini Arusha na baadhi ya maneo ya wilaya ya Arumeru

  Mradi huo uliotiliwa saini hivi karibuni utazinduliwa katika kijiji cha kimyaki majira ya saa nne asubuhi na baadae kuzungumza na wananchi katika kijiji cha mringarimga

  Wakizungumzia hali ya maji mkazi wa eneo mringaringa Josephat Joshua amesema wakinamama wanalazimika kwenda kutafuatamaji ya kunywa kutoka mringaringa kilometa mbili katika sehemu inayoitwa njoro au kwa wavii.Wakati mwingine sisi wakina baba tunabakia na watoto nyumbani.

  '' Wakinamama wanafuata maji, hadi arudi nyumbani anakuwa tayari amechoka sana kutokana na kufuta maji umbali wote huo bado majukumu mengine yanamsubiria"alisema Joshua.Kwa akizungumza kwa bi Miriam Zakayo amesema inawalazimu kutembea umbali mrefu na kushindwa kutimiza majukumu yao kwa wakati 

  '' Maji tunayoayatumia ni ya mto nayo yanachukua muda mrefu hadi kufunguliwa kwa sababu wengine tunayatumia katika mifugo, mashamba, hivyo tukitaka maji ya kunywa tunayafuata mbali"alisema Miriam.Mkazi mwingine wa kijiji hicho Saning'o Lebang'ute Laizer amesema kwa ujio wa Rais Magufuli kwao ni neema kwani itawatatulia tatizo hilo sugu la maji safi, barabara na umeme

  ''Tunashukuru sana kwa kuja kutufikia kwetu ni neema, barabara, hii inawahudumia watu wa kimmyaki, Ilikiding' a na Sambasha, mradi wa umeme, ni fursa kwetu pia"alisema Laizer.
   Mkazi wa kijiji cha mringarimga Miriam Zakayo akienda kufuata maji safi umbali wa km 2 kutoka kijiji cha Kimnyaki.Aidha katika kuhakikisha tatizo la upatikanaji safi na salama wilayani Arumeru linapungua ,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Dkt John pombe magufuli leo anatarajia kuweka jiwe la msingi katika mradi wa uboreshaji wa huduma ya maji safi na usafi wa mazingira jijini Arusha na baadhi ya maneo ya wilaya ya Arumeru.
  Mkazi wa kijiji cha mringarimga Miriam Zakayo akienda kufuata maji safi umbali wa km 2 kutoka kijiji cha Kimnyaki,katika kuhakikisha tatizo la upatikanaji safi na salama wilayani Arumeru,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Dkt John pombe magufuli anatarajia kuweka jiwe la msingi katika mradi wa uboreshaji wa huduma ya maji safi na usafi wa mazingira jijini Arusha na baadhi ya maneo ya wilaya ya Arumeru.
  Pichani kulia ni 
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo na Wananchi  wa Arumeru akiwa sambamba na 
  Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Jerry Muro kwa pamoja wakimkaribisa Rais Dkt. John Pombe Magufuli  katika ziara rasmi ya kikazi katika wilaya ya Arumeru leo Jumapili  katika kata ya Kimnyak  na kuweka jiwe la Msingi la ujenzi wa visima vikubwa vya maji zaidi ya 20 ambavyo ni Sehemu ya Mradi mkubwa wa Maji Kwa Jiji la Arusha ambao utasaidia pia kutoa huduma ya Maji katika kata Saba za Wilaya ya Arumeru , Mradi utakuwa na thamani ya zaidi ya Bilioni 500.

  0 0


  Mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera (Julia) akipokea taarifa ya mkoa kuhusu hali ya maambukizi ya UKIMWI toka kwa Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt Magdalena Zenda (kushoto).Tukio hili limefanyika Leo mjini Tunduru wakati wa maadhimisho ya siku ya UKIMWI kimkoa
  Sehemu ya wananchi wa Tunduru waliojitokeza kwenye maadhimisho ya siku ya UKIMWI kimkoa wakiwa na mabango yenye ujumbe maalum.
  Vikundi vya burudani vilivyotumbuiza kilele cha siku ya UKIMWI mkoa wa Ruvuma iliyofanyika wilaya ya Tunduru leo

  …………………….
  Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amezitaka taasisi na wadau wa mapambano dhidi ya UKIMWI kuongeza jitahada za kuzuia maambukizi mapya kuongezeka.

  Ametoa agizo hilo Leo (Jumamosi tarehe 01.Desemba,2018) katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika kimkoa katika uwanja wa Baraza la Idd wilaya ya Tunduru.

  Akitoa hotuba kwa niaba ya Mkuu huyo wa Mkoa,Mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera amesema takwimu zinaonyesha Ruvuma ina kiwango cha maambukizi ya VVU/UKIMWI cha asilimia 5.6 zaidi ya kile cha Taifa cha asilimia 4.7 kwa mwaka 2016/2017.
  Takwimu hizi ingawa zinaonekana kushuka kwa kiwango cha maambukizi kutoka asilimia 7 mwaka 2011/2012 bado kunahitajika nguvu na mikakati mipya ya kushusha zaidi kiwango cha maambukizi ya VVU.

  Ili kuhakikisha maambukizi mapya yanapungua Mndeme amesisitiza mkakati wa upimaji wa hiari wa VVU uimarishwe kwenye wilaya zote tano.

  Ameongeza kusema ni wakati sasa kuhakikisha watu wote wanaokutwa na VVU wanaanzishiwa tiba mara moja.

  Mkuu wa wilaya Homera ameishukuru serikali ya awamu ya Tano kwa kuongeza bajeti ya dawa hadi kufikia Shilingi Bilioni1.3 kwa mkoa wa Ruvuma kufikia mwezi Juni 2018 ikilinganishwa na shilingi milioni 297.5 zilizotolewa mwaka 2016/2017 kwenda Bohari Kuu ya Dawa (MSD). Mafanikio haya amesema yamesaidia wananchi wengi wa mkoa wa Ruvuma kuwa na uhakika wa matibabu hivyo kuongeza jitihada za kupunguza kasi ya maambukizi ya VVU.

  Kwa upande wake Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt.Magdalena Zenda amesema katika kipindi cha Januari hadi Octoba 2018 jumla ya wananchi 456,777 walipimwa hali zao za maambukizi.

  Kati yao waliogundulika na maambukizi ni 8,494 ambapo wanaume walikuwa (3,764) na wanawake (4,730). Dkt .Zenda ameongeza kusema hadi kufikia mwezi Octoba 2018 Mkoa umefanikiwa kusajili na kuanzisha dawa za kufubaza Virusi (ARV) kwa WAVIU 63,671 tangu huduma hizi zianze mwaka 2004.

  “Kati yao wanaotumia dawa hadi sasa ni 42,056 ,wanaume ni (14,336) na wanawake (27,720) wanaendelea kupata huduma katika kliniki za tiba na matunzo (CTC) kote mkoani ” alisema Dkt.Zenda.

  Ametaja changamoto kubwa ni idadi ya wanaotumia ARV wapatao 14,899 kuhamia vituo vingine nje ya mkoa na 11,368 ni waVVU waliopoteza ufuasi.

  Katika kipindi cha mwaka 2004 hadi sasa mkoa umekuwa na vifo vitokanavyo na UKIMWI 7,168 .

  Mkoa wa Ruvuma wenye watu takribani 1,449,830 kwa sensa ya mwaka 2012 una vituo vya kutolea huduma za afya 314.

  Kati yake hospitali zipo (11),vituo vya afya (32) na zahanati (271) hii inafanya huduma za upimaji na matibabu ya VVU kupatikana karibu maeneo yote.

  Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya UKIMWI mwaka huu 2018 inasema ” Know your status” -Pima,Jitambue,Ishi.

  0 0


  0 0  Mkuu wa Wilaya ya Kiteto mhandisi Tumaini Magessa ambaye ametangazwa na Mkuu wa mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti kuwa ndiyo anaongoza kwa uchapakazi.
  Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, mhandisi Zephania Chaula akisalimiana na wananchi wa eneo lake, mkuu wa mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti amesema anashika nafasi ya pili kwa kuchapa kazi.
  ………………………..

  MKUU wa Mkoa wa Manyara Alexander Pastory Mnyeti amewafagilia wakuu wa Wilaya za Kiteto mhandisi Tumaini Magessa na Simanjiro mhandisi Zephania Chaula kuwa ndiyo wakuu wa wilaya bora kwa sasa kwenye mkoa wake, wenye kuchapa kazi na kuhudumia wananchi. Mnyeti akizungumza mjini Babati alisema mkuu wa wilaya ya Kiteto mhandisi Tumaini Magessa na mkuu wa wilaya ya Simanjiro mhandisi Zephania Chaula, ndiyo wakuu wa wilaya bora kwa sasa mkoani Manyara.

  Alisema anataja majina hayo mawili ya wakuu hao wa wilaya ili iwe changamoto kwa wakuu wengine wa wilaya za mkoa huo wenye wilaya tano, kutekeleza wajibu wao ipasavyo. Alisema wakuu wengine wa wilaya ambao hawajatajwa wasife moyo ila waongeze bidii na juhudi katika kuwatumikia wananchi na kutekeleza wajibu wao ipasavyo. Alisema anatangaza majina ya wakuu hao wa wilaya wanaongoza mkoani humo baada ya yeye kushauriana na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa huo Simon Lulu na Katibu Tawala wa mkoa huo Missaile Mussa, ndipo wakapatikana hao.

  Alisema mkuu wa wilaya anapaswa kutoa maamuzi kwenye eneo lake la utawala na siyo kupiga simu kwa mkuu wa mkoa kila wakati kuomba msaada ili hali uwezo wa kutoa maamuzi anayo. Alisema wameangalia namna wanavyotoa maamuzi yao, utulivu wa wilaya, wanavyowasimamia watumishi wao wa ngazi ya chini na kudhibiti ufujaji wa fedha za miradi ya maendeleo.

  “Changamoto zenu pambaneni nazo kwani hata mimi napambana na nafasi yangu siyo kila wakati napiga simu kwa mheshimiwa Waziri Mkuu Kasim Majaliwa kuomba msaada ila mkizidiwa itajulikana hapo kweli ni haki,” alisema Mnyeti. Alisema hata Rais John Magufuli alipotangaza kuwa mkuu wa mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka anaongoza kwa wakuu wa mikoa yeye hakulalamika hivyo na wakuu wa wilaya wengine wasihofie hilo. 

  “Najua mkuu wa wilaya ya Hanang Joseph Mkirikiti atasema ohoo yeye hana mwaka tangu afike Hanang’ lakini hata mimi, alipotangazwa wa Simiyu sikusema sina mwaka tangu nije Manyara,” alisema Mnyeti. Mkuu wa wilaya ya Kiteto, mhandisi Tumaini Magessa alisema baada ya kuwepo utulivu eneo la Emboley Murtangos sasa wanageukia hifadhi ya msitu wa mlima wa simu ili kulinda uhifadhi. 

  Mkuu wa wilaya ya Simanjiro mhandisi Zephania Chaula alisema ataendelea kusimamia maendeleo kwenye eneo lake na kuhakikisha wanazidi kupiga hatua nyingine zaidi ya hapo walipo

  0 0


  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia na kutowa nasaha zake kwa Uongozi wa ZSTC na wananchi waliohudhuria hafla ya kuadhimisha Miaka 50 ya Shirika hilo zilizofanyika jana usiku katika viwanja vya hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar.2-12-2018.(Picha na Ikulu).

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Afisa Masoko wa Shirika la Biashara la Taifa (ZSTC) Nassor Salum Nassor, wakati akitembelea maonesho ya Bidhaa za ZSTC wakati wa maadhimisho ya 50 zilizofanyika katika viwanja vya Hotel Verde Mtoni Zanzibar,kushoto Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein,Mke waMakamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman, Makamu Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif na Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Mhe. Balozi Amina Salumu Ali, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya hotel Verde jana usiku.

  MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akisalimiana na Mama Fatma Karume, wakati akiwasili katika ukumbi wa hafla ya sherehe za kuadhimisha Miaka 50 ya ZSTC zilizofanyika katika viwanja vya Hoteli Verde Mtoni Zanzibar, jana usiku.
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Balozi Seif Ali Iddi na Mama Mwanamwema Shein, na Viongozi wengi wakiwa wamesimama wakati ukiimbwa wimbo wa Taifa na Kikundi cha Taifa cha Taraab Zanzibar, jana usiku katika hoteli ya Verde Mtoni
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguji Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud na kulia Waziri wa BiashaRA NA Viwanda Zanzibar,Mhe Balozi Amina Salum Ali na Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman, wakifuatilia onesho la “ Documentary “ ya Miaka 50 ya ZSTC,hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya hotel Verde Mtoni Zanzibar, jana usiku.
  WADAU wa ZSTC wakifuatilia hafla hiyo ya Maadhimisho ya sherehe za Miaka 50 ya Shirika hilo tangu kuazishwa kwake Zanzibar 1968, zilizoadhimishwa katika viwanja vya Hoteli Verde Mtoni Zanzibar, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar Mhe. Dk. Shein, akihutubia hafla hiyo, jana usiku.
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akikata Keki Maalum ya miaka 50 ya Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) kulia Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Mhe. Balozi Amina Salum Ali na Mwenyekiti wa Bodi ya ZSTC Ndg.Kassim Ali na kushoto Mkurugenzi Muendeshaji wa (ZSTC)Dkt. Said Seif Mzee, Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda Mhe. Hassan Hafidh na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Viwanda Ndg. Ali Juma, wakisherehekea wakati wa hafla hiyo ya ukataji wa Keki Maalum ya Miaka 50 ya ZSTC, katika viwanja vya hoteli Verde Mtoni Zanzibar, hafla hiyo imefanyika jana usiku.2-12-2018.
  MWENYEKITI wa Bodi ya Shirika la Bishata la Taifa Zanzibar (ZSTC) Ndg. Kassim Ali, akisoma taarifa ya mafanikio ya Shirika hilo wakati wa hafla ya kuadhimisha Miaka 50 ya ZSTC zilizofanyika jana usiku katika viwanja vya hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar.
  WAZIRI wa Biashara na Viwanda Zanzibar Mhe. Balozi Amina Salum Ali, akimkabidhi zawadi Maalum Mdau wa Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar, (ZSTC) Ndg.Tarun. Pandey, kutoka Kampuni ya Afcom Trading dmcc, kutoka Nchini Dubai.wakati wahafla hiyo ya kuadhimisha Miaka 50 ya ZSTC zilizofanyika jana usiku katika viwanja vya Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar


  WASANII wa Kikundi wa Kikundi cha Kachara kutoka kisiwani Pemba wakitowa burudani wakati wa sherehe za kuadhimisha Miaka 50 ya ZSTC zilizofanyika jana usiku katika viwanja vya Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar.2-12-2018

older | 1 | .... | 1740 | 1741 | (Page 1742) | 1743 | 1744 | .... | 1898 | newer