Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1739 | 1740 | (Page 1741) | 1742 | 1743 | .... | 1898 | newer

  0 0

  WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewataka majambazi popote walipo nchini kujisalimisha pamoja na silaha zao wakati Polisi wakiendelea na msako mkali mpaka jambazi wa mwisho anatiwa mbaroni. Lugola amesema Jeshi la Polisi lipo imara na litawasaka majambazi hao usiku na mchana popote walipo na litahakikisha nchi inaendelea kuwa salama na wananchi wema wakiendelea kufanya shughuli zao za maendeleo kwa kulijenga Taifa.

  Akizungumza na mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Kasahunga, Kata ya Neluma, Jimbo la Mwibara, Wilaya ya Bunda, mkoani Mara, leo, Lugola amesema usalama wa nchi hauchezewi na mtu yeyote na watu wasijaribu kutikisa kiberiti kwa kulichezea Jeshi la Polisi. Lugola amesititiza kuwa, Serikali ya Awamu ya Tano ambayo inaongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, ujambazi hauna nafasi na pia amewataka majambazi hao wafanye kazi nyingine ya kuwaingizia kipato kwa njia halali.

  “Msijaribu kukitikisa kiberiti, Serikali ipo macho muda wote, Jeshi lenu lipo imara, majambazi wanaofanya uvamizi, tutahakikisha tunawasaka popote walipo jambazi mmoja baada ya mwingine, hatutalala wala kupumzika hadi jeshi letu litakapomtia mbaroni jambazi wa mwisho,” alisema Lugola. Kutokana na msako huo, Lugola alisema majambazi hao wajisalimishe wenyewe pamoja na dhana zao kwenye kituo cha polisi wanachoona kipo jirani na wao, vinginevyo hawatasalimika na hawatabaki salama.

  “Kama kuna ndugu zetu, watoto wetu, majirani zetu tuwaambie serikali hii ya magufuli nafasi hiyo ya kufanya ujambazi haipo, nimepata taarifa za uhalifu, wizi wa mifugo na uvamizi wa aina mbalimbali, tuone taarifa polisi ili tuweze kuwatia mbaroni majambazi hao kwa wale wote ambao mnahisi wanajihusisha na uhalifu, toeni ushirikiano bila woga ili meneo yetu yazidi kuwa na amani,” alisema Lugola.

  Hata hivyo, Lugola alisema ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo ndani ya Wizara yake ambavyo anavisimamia wapo baadhi ya askari wachache ambao wanajihusiha na vitendo vya rushwa na alishatoa onyo mara nyingi, hivyo atakao wakamata hatawaonea huruma. 
   
  “Kuna baadhi ya mazingira ambayo yanachangia rushwa zaidi ndani ya Jeshi la Polisi ikiwemo kutokutolewa kwa dhamana katika siku za mapumziko Jumamosi na Jumapili, baada ya kuona kunamianya ya rushwa nikatangaza nchi nzima vituo vyote vya polisi vitoe dhamana saa 24 na siku 365 na robo, pia kutowekwa mahabusu watuhumiwa ambao wanamakosa madogo madogo,” alisema Lugola.

  Lugola anaendelea na ziara jimboni kwake ya kuhamasisha wananchi kuanza maandalizi ya kilimo pamoja na kuendeleza miradi ya maendeleo huku wakiendelea kuheshimu sheria za nchi. 
    Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola, akizungumza na mamia ya wananchi wa Kijiji cha Kasahunga, Kata ya Neluma, Jimbo la Mwibara, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara, leo. Lugola aliwataka wananchi wa Mwibara washirikiane na polisi kuwafichua majambazi, na pia aliwataka majambazi wajisalimishe pamoja na silaha zao katika kituo chochote cha polisi nchini, kwa kuwa polisi usiku na mchana wanawasaka na watahakikisha wanamtia mbaroni jambazi wa mwisho. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (kushoto), akiwapelekea zawadi kikundi cha kwaya ya Kijiji cha Kasahunga, Kata ya Neluma, Jimbo la Mwibara, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara, wakati waimbaji hjao walipokua wanampokea kwa kijijini hapo. Lugola katika hotuba yake kwa wananchi zaidi ya 100 waliohudhuria mkutano huo, aliwataka wananchi wa Mwibara washirikiane na polisi kuwafichua majambazi, na pia aliwataka majambazi wajisalimishe pamoja na silaha zao katika kituo chochote cha polisi nchini, kwa kuwa polisi usiku na mchana wanawasaka na watahakikisha wanamtia mbaroni jambazi wa mwisho.

  0 0

  WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali imeweka mikakati mizuri kuhakikisha wananchi hususani wachimbaji wadogo wadogo wananufaika na uwepo wa rasilimali hiyo.

  Hivyo, Waziri Mkuu amewashauri wachimbaji wadogo wadogo wajiunge katika vikundi ili Serikali iweze kuwapatia misaada mbalimbali ikiwemo mkopo ili waongeze mitaji.

  Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Alhamisi, Novemba 29, 2018) alipozungumza na wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi jengo la halmashauri ya Mbogwe.Amewahamasisha wachimbaji hao watumie taasisi mbalimbali za kifedha na kukopa fedha na kununua mitambo ya uchimbaji na uchenjuaji kwa lengo la kujiongozea tija.

  Waziri Mkuu ambaye yuko mkoani Geita kwa ziara ya kikazi, amesema wachimbaji wadogo wadogo waendelee kuwa na imani na Serikali yao, kwa kuwa imewapangia mambo mazuri.Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewahakikishia wananchi wa wilaya hiyo kwamba Serikali imedhamilia kumaliza tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama.

  Amesema katika kumaliza tatizo la maji Serikali imetoa zaidi ya sh. bilioni moja kwa ajili ya uchimbaji visima virefu 11 na visima vifupi 43 katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.Amesema Serikali ya Awamu ya Tano ina mikakati ya kumaliza tatizo la maji nchini kupitia Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo kichwani.

  Waziri Mkuu amesema kampeni hiyo inalenga kuhakikisha wananchi katika maeneo yote wanapata huduma ya maji safi na salama karibu na maeneo yao ya makazi.“Serikali imedhamiria kuhakikisha wananchi wote nchini wakiwemo na wa wilaya ya Mbogwe wanapata huduma ya maji safi na salama karibu na makazi yao.”

  Kuhusua suala la wanafunzi kukatishwa masomo kwa kupata ujauzito wilayani Mbogwe, Waziri Mkuu ameitaka jamii kukemea vitendo hivyo. Wanafunzi 54 wamepata ujauzito.Amesema katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Septemba mwaka huu wanafunzi 20 wa shule za msingi na 34 wa sekondari wameacha shule baada ya kupata ujauzito.

  “Hali ni mbaya, Mbogwe inatia aibu kwa kuwa na idadi kubwa ya watoto waliopewa ujauzito. Naagiza msiwaguse wanafunzi wa kike ni moto utawaunguza. Tukikukamata jela miaka 30.”Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Madini, Dotto Biteko amesema wilaya ya Mbogwe inafanya vizuri katika sekta ya madini, ambapo ina viwanda 27 vya kuchenjulia dhahabu.

  Amesema katika kuhakikisha wachimbaji wadogo wadogo wanawezeshwa kufanya shughuli zao vizuri, Serikali imetenga eneo la hekta 547.64 kwa ajili ya kuwagawia wachimbaji hao.Akizungumzia kuhusu leseni za uchimbaji mkoani Geita amesema kuna jumla ya leseni 971 za uchimbaji mdogo wa madini na kati yake zinazofanyakazi ni leseni 184 tu.

  Waziri huyo amewataka wachimbaji wadogo wadogo waendelee na shughuli zao za uchimbaji kwenye maeneo yao waliyopangiwa na kwamba hakuna atakayewaondoa.

  Awali, Waziri Mkuu alikagua na kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa ofisi ya halmashauri ya wilaya ya Mbogwe katika kijiji cha Kasosobe. Ujenzi huo utagharimu sh. bilioni 4.3. Pia alikagua mradi wa uboreshaji miundombinu na kuzindua maabara ya Kituo cha Afya Masumbwe.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  ALHAMISI, NOVEMBA 29, 2018.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia Mkutano wa Hadhara kwenye Kiwanja cha Shule ya Msingi ya Masumbwe wilayani Mbogwe, Novemba 29, 2018. 
  Wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia Mkutano wa Hadhara kwenye Kiwanja cha Shule ya Msingi ya Masumbwe wilayani Mbogwe, Novemba 29, 2018. 
  Wananchi wakimshangilia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipoingia kwenye Kiwanja cha Shule ya Misngi ya Masumbwe wilayani Mbogwe kuhutubia Mkutano wa Hadhara, Novemba 29, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0


  0 0


  Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na waandishi wa habari tarehe 29 Novemba 2018 katika Ukumbi wa Bodi ya Korosho Mjini Mtwara ili kutoa tathmini ya hatua zilizofikiwa na serikali za ununuzi wa korosho za wakulima. (Picha Zote Na Mathias Canl, Wizara ya Kilimo)
  Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na waandishi wa habari tarehe 29 Novemba 2018 katika Ukumbi wa Bodi ya Korosho Mjini Mtwara ili kutoa tathmini ya hatua zilizofikiwa na serikali za ununuzi wa korosho za wakulima.  Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Mtwara

  Serikali imetangaza kuongeza kasi ya malipo ya wakulima wa Korosho ili kufikia kiasi cha shilingi Bilioni nne (4) kila siku kwani kufanya hivyo zoezi la malipo kukamilika haraka.

  Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 29 Novemba 2018 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Bodi ya Korosho Mjini Mtwara ili kutoa tathmini ya hatua zilizofikiwa na serikali za ununuzi wa korosho za wakulima.

  Amesema kuwa zoezi hilo litaenda sambamba na kuongezwa kwa wataalamu kwa ajili ya kuongeza nguvu ya malipo huku akisisitiza kuwa wataalamu wengine tayari wamekuwa na uzoefu wa namna ya kuhakiki na namna ya kulipa tangu kuanza kwa zoezi hilo.

  Mhe Hasunga alisema kuwa mikoa inayolima korosho ni mingi nchini hivyo wakati tathmini sambamba na malipo zikiendelea timu ya wataalamu wengine itaundwa kwa ajili ya kuanza kufanya tathmini katika mkoa wa Pwani na mikoa mingine inayolima korosho nchini.

  Katika hatua nyingine amesema kuwa serikali imejipanga kuwatambua wakulima wote wa korosho nchini ili kurahisisha kuwahudumia na kuainisha tathimini mahususi ya wakulima hao nchini.Kuwafahamu wakulima hao itaisaidia serikali namna ya kushirikiana nao na kuwasaidia ili wakulima hao waweze kuongeza uzalishaji na tija katika kilimo.

  Miongoni mwa changamoto ilizokutana nazo serikali katika zoezi la uhakiki ni pamoja na kutotolewa takwimu sahihi na Vyama vya msingi vya ushirika za wakulima wa korosho kwani takwimu hizo zinatofautiana na vyama vikuu vya ushirika.“Jambo hili la takwimu kwenda kinyume linatupa uhakika kwamba kuna taarifa zilikuwa zinapikwa ili kumnyonya mkulima lakini changamoto zingine ambazo zimetukumba ni pamoja na uchache wa maghala kwani yaliyopo hayatoshi” Alikaririwa Mhe Hasunga

  “Kuna changamoto za mgomo wa wapakuaji na wapakiaji wa mizigo, nasi kama serikali tutakuwa na kikao hivi karibuni na wasafirishaji ili kuhakikisha kuwa wanalipwa fedha zao haraka iwezekanavyo baada ya kupitia mikataba yao kujiridhisha jinsi walivyokubaliana” Alisema

  Tayari vyama 163 vya wakulima wa korosho vimekwisha hakikiwa mpaka kufikia jana jioni tarehe 28 Novemba 2018 kati ya vyama 617 vinavyojihusisha na zao la korosho nchini.Katika vyama hivyo vilivyohakikiwa tayari malipo yamevifikia vyama 97 ambapo wakulima 22,269 wameshalipwa huku kiasi cha korosho ambazo zimekwishalipiwa ni kilo 6,712,681 huku jumla ya Bilioni 22,151,00,000.8 zikiwa zimekwishalipwa.

  Aidha, mpaka kufikia jana jioni tarehe 29 Novemba 2018 serikali imekwisha hamisha kiasi cha Tani 9,347.2 kutoka kwenye maghala makuu.Pia Waziri Hasunga ameyataja matarajio ya serikali katika uzalishaji wa Korosho kuwa ni takribani Tani 245,495.8

  0 0
  Timu Shinda Zaidi na SportPesa imebahatika kumpata mshindi mwigine mwanamama akiwa ni mwanamke watatu kujishindia Bajaji kutoka jiji la Dar es Salaam, Goba.Katika droo ya 64 Petronila Sirinya ambaye alibashiri na moja kwa moja kuingia kwenye droo ya Shinda Zaidi na SportPesa na kujishindia Bajaji Re kutoka SportPesa.Mshindi Huyo wa Droo ya 64 alisema alianza kushawishika kucheza na SportPesa baada ya kuona vile watu wengine wanashinda kwenye promosheni ya Shinda zaidi ndipo na yeye kuchukua uamuzi wa kuanza kucheza na timu ya kushinda kuutafuta ushindi wake.

  "Nimeufurahia ushindi huu sijawahi kushinda kabisa tena mimi ni mama wa nyumbani sikufikiri kama ningeshinda lakini Mungu kanisaidia sasa ntaweza kumudu mahitaji yangu kutoka kukaaa nyumbani mpaka kumiliki bajaji yangu hizi ni baraka kubwa sana kutoka kwenu SportPesa" alisema Petronila.Aidha, Petronila alisema kipato atakachopata kupitia bajaj hiyo kitamsaidia kujiendeleza kielimu zaidi huku pesa nyingine ataziwekea mipango mizuri kumuwezesha mtoto kusoma shule nzuri.
  "Najua hata mume wangu atakuwa ameshawishika sasa maana wakati nacheza alikuwa ananiambia shauri yako unapoteza pesa zako lakini baada ya kushinda yeye ndio ananisisitiza niendelee kucheza kweli ushindi una raha yake " alisema Bi. Sirinya.Upande mwingine aliipongeza SportPesa kwa kutoa huduma bora kwa wateja wake sambamba na kuwajali kwa kuwatumia pesa za ushindi mara baada tu ya mechi kumalizia, huku akiweka wazi mikakati yake ya kuanza kusaka mtonyo wa Jackpot.
   
  Kutoka SportPesa, Meneja Uhusiano Bi. Sabrina H. Msuya alisema kampuni yetu inahuduma mbalimbali ambazo mteja akicheza anaweza kujishindia pesa ambazo anapata mara baada ya kuweka ubashiri wake na kupatia kiusahihi, Bajaji , Simu janja pamoja na Jezi orijino za Simba na Yanga


  “Wikii hii Jackpot yetu imepanda mpaka shilingi 403,525,820/= ambapo mteja akibashiri kwa usahihi mechi kumi na tatu, na kuzawadiwa bonasi kwa watakao bashiri kwa usahihi kwa usahihi kuanzia mechi kumi hadi kumi na mbili.

  0 0


  KAMPUNI ya Mojabet inayojishughulisha na mchezo wa kubahatisha kupitia mmoja ya michezo yake ya Boompesa leo imetangaza kudhamini fainali za Bongo Star Search (BSS) ambazo zinatarajiwa kufanyika tarehe 22 Disemba mwaka huu.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wakutangaza kudhamini Bongo Star Search msimu wa 9, Mkurugenzi wa Masoko kutoka kampuni ya Mojabet Diana Chacha alisema kuwa wameona ni muhimu kushirikiana na Bongo Star Search ili kuendelea kuimbua vipaji vipya vya muziki hapa nchini na pia kufanya vijana zaidi waweze kujiajiri kupitia muziki.

  Sisi lengo ni kuwafanya Watanzania wengi waweze kujiajiri kupitia zawadi za fedha taslimu ambazo huwa tunawapa washindi wetu. Kwa maana hiyo tumeona ni muhimu kutanua wingu wetu na kuelekeza kwenye muziki kwani huko pia kuna vipaji vyingi lakini kutokana na kutopata nafasi ya kuonekana, tunaamini kuwa ushirikiano wetu na BSS utaweza kutanua wingu na kufikia Watanzania wengi na hasa kupitia vijana kupitia Boompesa, alisema Chacha.

  Chacha aliongeza kuwa Boompesa ni mchezo ambao unachezwa kwenye mitandao yote ya simu za mkononi kwa kununua tiketi , na mara mshindi anaposhinda anapewa fedha zake papo hapo kwenye simu yake , na mchezaji anaweza kununua tiketi kuanzia shilingi 100 na kuendelea.

  Mojabet ni kampuni ya michezo ya Bahati na sibu na Boompesa ni mmoja ya michezo yetu.Mojabet kupitia Boompesa ni wadhamini wakuu katika Bss season 9.na nusu fainali na fainali Boompesa imeandaa zawadi nono na sio kwa washiriki wa bss tu Bali hata kwa wachezaji wa mchezo huo kwa kupitia code ya Bss.kwani kuna TZS 50 milioni imeandaliwa kwa wachezaji.hivyo ni fursa kwa kila MTU kucheza zaidi ili kujiongezea nafasi take ya kushinda.

  Kwa upande wake, Mratibu na Jaji Mkuu wa Bongo Star Search Rita Paulsen alisema kuwa fainali za mwaka huu zimekutakuwa tofauti na za miaka iliyopita kwani mshindi mbali na kujipatia fedha taslimu lakini pia ataweza kupata ajira kutoka kwa kampuni ya Mojabet

  Mojabet kupitia Boompesa wamefanya fainali za mwaka huu ziwe za kipekee, alisema Rita huku akiongeza kuwa mshindi wa BSS msimu wa tisa atapata fedha taslimu milioni tano, vile vile atakuwa Balozi wa Boompesa kwa muda wa mwaka mmoja ambapo atakuwa analipwa shilingi milioni mbili kwa mwezi.

  Tumeingia mkataba wa mwaka na kampuni kubwa ya muziki ambayo itakuwa ikizalishalisha na kusambaza kazi za mshindi wa mwaka huu kwa kipindi cha mwaka mmoja. Lengo ni kuhakikisha mshindi wetu anakuwa ni staa kweli, alisema Rita huku akitoa shukrani kwa kampuni ya Mojabet kupitia Boompesa kuweza kudhamini mashindano yam waka huu ambayo yamekuwa tofauti na ya miaka ya nyuma.

  Vile Vile, Rita aliongeza kuwa wakati wa kilele cha fainali hizo kutachezeshwa mchezo wa Boompesa ambapo mshindi atajinyakulia kitita cha shilingi milioni hamsini.
  Jaji Mkuu wa shindano ya Bongo Star Search (BSS) Rita Paulsen akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam wakati wa kutangaza zawadi na fainali za BSS msimu wa 9 ambapo mshindi atapata zawadi ya fedha taslimu TZS5M pamoja na mkataba wa mwaka mmoja kutoka kwa wadhamini wakuu ambao kampuni ya Mojabet inayojishughulisha na mchezo kupitia Boompesa. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko Mojabet Diacha Chacha.

  0 0
 • 11/30/18--00:33: TANZIA
 • UONGOZI wa Bodi na Menejimenti ya Baraza la Kilimo Tanzania unasikitika kutangaza kifo cha Mwakilishi wake katika Wilaya ya Wangi’ng’ombe Mkoani Njombe Bw. John Wihallah aliyefariki Dunia katika ajali iliyohusisha Basi alilokuwa amepanda la Rungwe Express lilokuwa likitokea Dar es saalm kuelekea Mkoani Mbeya kwa kugongana na Gari aina ya Coaster katika eneo la Iyovi Mkoani Morogoro.

  Bw. John alikuwa akitokea Jijini Dar es Salaam alikokuwa akishiriki Warsha ya Kitaifa ya Wadau wa Kilimo iliyofanyika Nov 26/27 na baadae kushiriki Mkutano Mkuu wa Baraza la Kilimo uliofanyika Nov 28. 

  Taarifa za kifo chake zimepokelewa kwa maskkitiko makubwa hasa ikizingatiwa Bw John alikuwa kiunganishi muhimu kati ya wakulima na Baraza la Kilimo Wilayani Wang’ing’ombe Mkoani Njombe,

  Uongozi wa Baraza la Kilimo Tanzania utamkumbuka kwa mchango wake mkubwa katika Sekta ya Kilimo lakini pia Baraza limeahidi kufanyia kazi mapendekezo na ushauri wote alioutoa wakati wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Kilimo Tanzania ambapo lipata fursa ya kuchangia masuala mbalimbali.

  Mwili wa Marehemu John Wihallah unatarajiwa kuzikwa nyumbani kwake Wilaya ya Wang;ing;ombe Mkaoni Njombe Jumapili Dec 02 Mwaka huu.

  Bwana alitoa Bwana ametwaa jina la Bwana lihimidiwe.

  Imetolewa na Baraza la Kilimo Tanzania,
  Dar es salaam.
  Nov 30, 201 

  Ndugu John Wihallah (enzi za uhai wake) akishiriki mkutano mkuu wa Baraza la Kilimo Tanzania Nov 28, Jijini Dar es Salaam, kabla ya kufikwa na mauti Nov 29 alipokuwa akirejea Mkoani Njombe.

  0 0


  Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Zanzibar.Balozi Seif Ali Idd (anayetazama kamera) akizungumza na Wadau wa Maendeleo na Maafisa wa TASAF ofisini kwake-mjini Unguja.
  Balozi Seif Ali Idd (aliyevaa Kaunda Suti nyeupe) akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bw. Ladislaus Mwamanga baada ya kikao na wadau wa maendeleo ofisini kwake.

  Makamu wa Pili wa Rais wa SMZ (walioketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wadau wa Maendeleo na Maafisa wa TASAF ofisini kwake kisiwani Unguja.


  Eneo la shamba darasa lililoandaliwa na Walengwa wa TASAF katika shehia ya Bungi kwa ajili ya kupanda mbogamboga kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato.
  Sehemu ya shamba darasa la Walengwa wa TASAF walilopanda mboga mboga katika shehia ya Bungi lililotembelewa na Wadau wa Maendeleo na Maafisa wa TASAF kuona utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.
  Kushoto (nyumba aliyokuwa akiishi mmoja wa Walengwa wa TASAF wilayani Misungwi mkoani Mwanza bi. Felista Sabini (kulia ) ni nyumba mpya ya mlengwa huyo aliyoijengwa baada ya kujumuishwa kwenye Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na TASAF .


  Na. Estom Sanga- Zanzibar.

  Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd amesema utekelezaji wa shughuli za Maendeleo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF kisiwani Zanzibar umekuwa wa mafanikio makubwa na wenye tija katika jitihada za serikali za kupunguza umaskini kwa wananchi.

  Balozi Seif Ali Idd ameyasema hayo alipokutana na Wadau wa Maendeleo na Maafisa wa TASAF Ofisini kwake mjini Unguja wakiwa katika ziara ya kutembelea Walengwa wa Mfuko huo ikiwa ni utaratibu wa kukutana na Walengwa kuona namna wanavyonufaika na huduma za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.

  Makamu huyo wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,amesema maeneo yote ambako TASAF kupitia Mpango wake wa Kunusuru Kaya Maskini unatekelezwa, Walengwa wameboresha maisha yao kwa kiwango kikubwa kwa kuanzisha miradi ya kiuchumi na kujiongezea kipato chao.

  Amesema ongezeko la kipato limezifanya Kaya za Walengwa kumudu gharama za kuhudumia Watoto na wengine kuboresha makazi yao ikilinganishwa na hali ilivyokuwa kabla ya kujumuishwa kwenye Mpango huo ulioanzishwa na serikali kwa lengo la kuboresha maisha ya Walengwa nchini kote.

  Balozi Seif Ali Idd amesema kutokana na mafanikio yaliyoanza kuonekana kutokana na huduma za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, Serikali itaendelea kusimamia kwa karibu mpango huo ili wananchi hususani wanaokabiliwa na kero ya umaskini waweze kuondokana na kero hiyo.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Ladislaus Mwamanga, amesema mafanikio ya utekelezaji wa Mpango huo wa kunusuru Kaya Maskini yamechangiwa kwa kiwango kikubwa na usimamizi wa karibu wa viongozi wa Serikali katika ngazi mbalimbali za uongozi kote nchini kote.

  Aidha bw.Mwamanga amesema mwelekeo wa utekelezaji wa shughuli za TASAF katika awamu ijayo utaweka mkazo zaidi katika kuhamasisha walengwa kote nchini kufanya kazi za uzalishaji mali kwa bidi huku akitoa rai maalumu kwa watalaamu wa sekta zikiwemo za kilimo, ufugaji,Maji ,hifadhi ya mazingira n.k kuwa karibu zaidi na Walengwa ili kuleta mabadiliko yenye tija zaidi.

  Naye kiongozi wa Shughuli za TASAF katika Benki ya Dunia hapa nchini , Bw. Mohamed Muderis amemweleza Balozi Seif Ali Idd kuwa Benki hiyo imevutiwa na namna Serikali ya Tanzania kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii- TASAF inavyosimamia na kutekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya maskini ambao amesema umeleta mageuzi makubwa miongoni mwa Walengwa na Jamii kwa ujumla.

  Ukiwa kisiwani Unguja, Ujumbe huo umetembelea na kukutana na Walengwa katika Shehia ya Bungi na kujionea Shamba darasa la mbogamboga lililoanzishwa na Walengwa wa TASAF ambalo licha ya mazao yake kuuzwa na kuwaongezea kipato lakini pia hutumiwa na Walengwa .

  Wadau hao wa Maendeleo na Maafisa wa TASAF pia wametembelea wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza ambako wamekutana na Walengwa na viongozi wa mkoa huo ambako wamepata taarifa ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini mkoani humo.

  0 0
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akiongea na wagonjwa kwenye dirisha la dawa lililopo hospitalini hapo ambapo wagonjwa walisema wanapata dawa hizo bila malipo


  Dkt.Mpoki akimjulia hali mmoja wa wagonjwa kwenye wodi ya wanaume hospitalini hapo na kuahidi wizara yake ipo mbioni kusogeza huduma za saratani kwenye baadhi za hospitali za rufaa za kanda na mkoa ili kuondoa adha ya kusafiri kwenda ocean road.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akisisitiza wananchi (hawapo pichani) kuandika maoni na kuweka kwenye Kisanduku kuhusiana na huduma zinatolewa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road ili uongozi uweze kusoma na kuyafanyia kazi maoni hayo.
  Katibu Mkuu akisikiliza wagonjwa waliofika kupata huduma kwenye hospitali hiyo.Dkt. Mpoki aliutaka Uongozi wa hospitali hiyo kufanyia kazi malalamiko ya ndugu wa wagonjwa kama mrejesho wa utoaji huduma
  ……………………………………………………………………

  Na.WAMJW, Dar es Salaam 

  Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya amewataka Madaktari wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road kutimiza wajibu wao katika kuwahudumia wagonjwa wanaofika hospitalini hapo kila siku na kumuagiza Mkurugenzi wa Huduma za Uhakiki na Ubora kutoka Wizarani kwake kufuatilia. 

  Dkt.Mpoki ametoa agizo hilo alipotembelea taasisi hiyo ili kujionea hali ya utoaji huduma pamoja na kusikiliza wagonjwa wanaofika kupata huduma kwenye taasisi hiyo kutokana na kulalamikiwa kwa baadhi madaktari na wauguzi “Taasisi hii ni ya faraja lazima mtengeneza mazingira mazuri yakuwahudumia wagonjwa,kwani ndugu wanafuatilia hali za wagonjwa wao hivyo jamii inapolalamika tusiseme moja kwa moja ni waongo bali tushughulikie malalamiko yao ,kama huna jibu muelekeze kwa mtu ambaye anaweza kumpa jibu ili aweze kupata faraja”.Alisisitiza Dkt.Mpoki. 

  Aidha, aliwataka watumishi wa taasisi hiyo kuvaa vitambulisho ambavyo vinaweka wazi utambulisho wao ili ndugu na wagonjwa waweze kuwatambua na kutaja ni nani ambaye hajatimiza wajibu wake ipasavyo.
  “watakaoshindwa kwenda nasi tutawapeleka kwingine,hatutaki maumivu yawe sehemu ya uzoefu wa wagonjwa wanaolazwa Ocean Road,nyinyi kazi yenu ni kuwahudumia wagonjwa”. 

  Hata hivyo aliwataka madaktari wabobezi (Mabingwa) kutimiza wajibu wao na sio kuwaachia jukumu la kuwahudumia wagonjwa madaktari waliopo mafunzo kwa vitendo”kuanzia sasa tukigundua mgonjwa ameachiwa daktari wa mafunzo kwa vitendo tutawaondoa wasifanye mazoezi hapa lazima tuishi kwa kutii na kufuata miiko ya taaluma zetu”alisema dkt.Mpoki 

  Aliagiza kufanyika mikutano ya ndani mara kwa mara ya kufuatilia utendaji kazi wa taasisi na kujibu malalamiko yanayotolewa kwenye mitandao ya kijamii pamoja na masanduku ya maoni ili kupata mrejesho kutoka kwa wananchi ili kuboresha huduma zinazotolewa kwenye taasisi. 

  Kuhusu adha ya umbali wa kufuata huduma kwenye taasisi hiyo Dkt. Mpoki aliwathibitishia wagonjwa na ndugu waliopo hospitalini hapo kuwa Serikali kupitia wizara ya afya iko mbioni kupeleka huduma za saratani kanda ya kusini mara tu itakapokamilika hospitali ya Rufaa ya kanda,pia huduma kama hizo zipo mbioni kupelekwa kwenye hospitali ya rufaa ya Tabora pamoja na hospitali maalum ya Benjamin Mkapa iliyopo jijini Dodoma kwani ni wajibu wao kuhakikisha huduma hizo karibu na wananchi.

  0 0

  Na. VERO IGNATUS, ARUSHA

  RAIS  Dkt John Magufuli na Rais Uhuru Kenyata (kesho) wanatarajia kuzinduwa kituo cha Forodha cha pamoja Namanga One Stop Bonder Point.

  Aidha Disemba mbili mwaka huu Rais John Magufuli ataweka jiwe la Msingi la mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya sh bilioni 520 unatoa katika Jiji la Arusha na baadhi ya maeneo katika wilaya ya Arumeru.

  Taarifa hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ambapo alisema kituo hicho cha Forodha kimejengwa kwa ushirikiano wa nchi ya Kenya na Tanzania.Kwa mujibu wa Gambo kituo hicho cha forodha kitakuwa mwarobaini wa kubithibiti vichochoro vya kupitisha magendo zikiwemo nyara za serikali.

  Alisema katika kuimarisha ulinzi wa kituo hicho mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Saimon Sirro ametoa mbwa wawili ambao watagundua aina yeyote ya magendo ikiwemo meno ya tembo,madawa ya kulevya na mlipuko."Niwasihi wananchi wote kuheshimu sheria za nchi kwa kuepuka kufanya vitendo vya kupitisha magendo kwenye mpaka wa Namanga kwa kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vimeimarisha ulinzi na watakaobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria.

  Kuhusu uwekaji msingi mradi huo wa maji Gambo alisema rais Magufuli ataweka jiwe la Msingi eneo la chanzo cha maji hayo kilichopo wilayani Arumeru.Alisema baada ya kuweka jiwe hilo la Msingi atatembelea ujenzi mradi huo kwenye maeneo mbalimbali ya Jiji la Arusha sambamba na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta walipokutana leo kabla ya kuanza kwa mkutano mkuu wa 20 wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Jijini Arusha(AICC) .Novemba 30,2018

  0 0

  Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii

  MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali mapingamizi yaliyowasilishwa na upande wa Serikali na kukubali kusikiliza rufaa ya Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini,  Esther Matiko ya kupinga kufutiwa dhamana na Mahakama ya Kisutu.

   Hatua hiyo imekuja baada ya Mahakama kutupilia mbali hoja za pingamizi la Serikali ambazo ziliiomba Mahakama iitupilie mbali rufaa hiyo bila hata kusikilizwa sababu zina mapungufu kisheria.

  Mbowe na Matiko wamekata rufaa Mahakama Kuu kupinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Novemba 23, 2018  kuwafutia dhamana katika kesi ya jinai inayowakabili mahakamani hapo inayosilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri, Kutokana na  maombi ya upande wa mashtaka, kwa madai ya kuwa wamekiuka masharti ya dhamana kwa kutokufika mahakamani tarehe ambazo kesi yao ilipangwa kwa ajili ya usikiljzwaji wa awali (PH).

  Rufaa hiyo ilitarajiwa kusikilizwa jana lakini upande wa Serikali uliwasilisha pingamizi la awali ikitoa sababu tatu za kutaka rufaa hiyo itupwe ikiwemo kuwa rufaa hiyo iko mahamakani isivyo  halali kwani inakiuka vifungu vya sheria.

  Akitoa uamuzi leo Novemba 30,2018 Jaji Sam Rumanyika
  amekataa sababu ya pingamizi la Serikali kuwa rufaa hiyo iko mahakamani isivyo halali.

  Jaji Rumanyika amesema kuwa rufaa hiyo iko mahakamani kihali kwani si lazima  kutaja kifungu cha kisheria kinachoipa mahakama mamlaka ya kusikiliza rufaa hiyo.

  Hata hivyo amekubaliana na hoja za Serikali za kupewa mwenendo wa kesi ya msingi wa shauri hilo uliochapishwa  ambao unasomeka vizuri. Pia Jaji Rumanyika amekubaliana na hoja  kuwa sababu mbili za rufaa za kupinga masharti ya dhamana zinakiuka matakwa ya sheria kwa kuwa zimekatiwa rufaa bila kutoa kwanza taarifa ya kusudio la kukata rufaa kupinga masharti hayo ya dhamana yaliyotolewa kati ya mwezi Machi na April.


  Hata hivyo imeelezwa kuwa rufaa hiyo itasikilizwa saa nane mchana.  


  0 0

   Picha mbalimbali zikionesha waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa Mji Mdogo wa Katoro mkoani Geita, Novemba 30, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
  PMO_0865PMO_0913

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Wajumbe kutoka Tanzania Girl Guides Association ambapo pamoja na mambo mengine alitambulishwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Bi. Anna Maembe na Wajumbe wengine wa Bodi hiyo kwenye ofisi ya Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  akifanya mazungumzo na Wajumbe kutoka Tanzania Girl Guides Association kwenye ofisi ya Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  akiwa kwenye picha ya pamoja na Wajumbe kutoka Tanzania Girl Guides Association kwenye ofisi ya Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

  0 0

  Na WAMJW - MARA.

  Asilimia 85 ya Wanawake Mkoani Mara wanajifungua kwenye vituo vya Afya, hali iliyosaidia kupunguza idadi kubwa ya vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua.

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu wakati alipotembelea Hospitali ya Mkoa wa Mara kukagua hali ya utoaji Huduma.

  "Mko Asilimia 85, kitaifa tupo Asilimia 51, kwahiyo niwapongeze kwa hilo, lengo letu ilikuwa ifikapo 2020 tunataka angalau Asilimia 80 ya wanawake wajawazito wajifungulie kwenye vituo vya Afya" Alisema Waziri Ummy.

  Pia Waziri Ummy ameitaka Mikoa mingine nchini kuiga jitihada zinazofanywa na mkoa wa Mara za kupunguza vifo vya mama na mtoto kwa kuhakikisha wanawake wajawazito wanajifungulia katika vituo vya kutolea huduma za Afya.

  "Sitaielewa mikoa mingine kwa kushindwa kuhamasisha na kuweka Mazingira mazuri kwa wanawake kwenda kujifungulia katika vituo vya kutoa huduma za Afya" alisema Waziri Ummy

  Hata hivyo Waziri Ummy Mwalimu amemwagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara kuhamasisha jamii hususan wanawake katika maeneo mbali mbali kuhudhuria kliniki angalau Mara 4 katika kipindi cha ujauzito.

  "Wanawake ambao wanahudhuria Kliniki angalau mara 4 ni Asilimia 45 hivyo hamjafanya vizuri kwasababu kitaifa ni Asilimia 51, mjenge tabia ya kuwahamasisha wanawake kuhudhuria kliniki angalau Mara 4, kama watoa huduma za Afya wanavyotushauri" alisema Waziri Ummy.

  Aidha, Waziri Ummy amemwagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara Dkt. Francis Mwanisi Kuhakikisha ifikapo Disemba 30 mwaka huu angalau kaya zote mkoani Mara ziwe na vyoo bora, na kumtaka kutoa elimu na kuhamasisha wananchi juu ya umuhimu wa matumizi ya vyoo bora kiafya na kiuchumi kwa mwanadamu.

  "Kaya zilizo na vyoo bora kwa Mkoa wa Mara naona ni Asilimia 40, Kwahiyo tunahitaji kuongeza elimu na kutoa mwamko kwa jamii kuhusu kujenga vyoo bora na kuvitumia" alisema Waziri Ummy

  Mbali na hayo Waziri Ummy amesema kuwa Serikali inaendelea kuboresha huduma za Afya Mkoani Mara kupitia kuboresha Vituo vya Afya 14, na kujenga Hospitali 3 za Wilaya ambazo ni Lorya, Musoma DC na Bunda, jambo ambalo litalopunguza mzigo kwa Hospitali ya Mkoa ili iweze kujikita katika kutoa huduma za rufaa.

  Sambamba na hilo Waziri Ummy amesema kuwa Serikali itaendelea kuboresha huduma Bora kwa wananchi kwa kupeleka jumla ya Watumishi 25 katika Hospitali ya Mkoa wa Mara huku akiwahasa Viongozi mkoani hapo kujenga Mazingira mazuri yakuwavutia Watumishi ili wafanye kazi kwa bidii na wabaki katika vituo vya kazi.

  Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Mara Dkt. Hosea Bisanda alisema kuwa Hospitali ya Mkoa imeweza kupunguza vifo vya akina mama vitokanavyo na uzazi kutoka vifo 23 mwaka 2015, vifo 14 mwaka 2016, vifo 10 mwaka 2017, na vifo 6 hadi kufikia Oktoba mwaka huu.

  Dkt. Bisanda amesema kuwa licha ya Serikali kuwaletea Watumishi 25 Hospitali ya Mkoa wa Mara inatakiwa kuwa na Watumishi 684, lakini Watumishi waliopo sasa ni 305, hivyo kupelekea kuwa na upungufu wa Watumishi 379 sawa na Asilimia 55.

  "Hospitali ya Mkoa wa Mara ina uhaba wa Watumishi hasa Madaktari Bingwa, Madaktari wasaidizi, Wauguzi, wateknolojia, Maabara pamoja na wateknolojia madawa" alisema Dkt. Hosea Bisanda

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akisikiliza maoni ya mmoja kati ya wagonjwa waliofika kupata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akihoji juu ya gharama za huduma za Afya zinazotolewa katika Hospitali ya Mkoa wa Mara, pindi alipofanya ziara ya kukagua ubora wa huduma na miundombinu katika Hospitali hiyo.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akisikiliza maoni ya mmoja kati ya wagonjwa waliofika kupata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akitoa maoni juu ya namba za mawasiliano zilizopo kwenye ubao mdogo wa matangazo katika Hospitali Rufaa ya Mkoa wa Mara, pindi alipofanya ziara ya kukagua ubora wa huduma.
  Picha ya pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu na Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Adam Malima wakati alipofanya ziara katika Hospitali ya Mkoa wa Mara.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akisisitiza jambo mbele ya Watumishi wa sekta ya Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara(hawapo kwenye picha) pindi alipofanya ziara ya kukagua ubora wa huduma katika. 
  Watumishi wa Kada mbali mbali za Afya wakimsikiliza mgani rasmi Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu (hayupo kwenye picha) wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya na uboreshaji wa miundombinu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara.

  0 0

  Na Khadija Seif, Globu ya jami
              
  TAASISI  ya Ustawi wa Jamii imewatunuku vyeti wahitimu 1,387 katika mahafali ya 42 ya chuo hicho katika ngazi ya astashahada,stashahada, katika fani ya Kazi za jamii kwa Watoto na vijana,Mahusiano kazini na Menejimenti ya sekta ya Umma( Industrial Relations and Public Management).

  Akizungumzana leo jijini Dar es Salaam katika mahafali hayo, Katibu Mkuu - Idara Kuu ya Maendeleo ya jamii -Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dk.John Jingu amesema wahitimu wote wamekula kiapo kwa ajili ya kulitumikia Taifa na ujuzi waliopatiwa ni rasilimali kwa ajili ya Taifa kwa ujumla.

  Dk.Jingu ameeleza fani ya ustawi wa jamii ni nyeti na muhimu katika jamii na wanapaswa kuwa katika sekta mbalimbali kwani wamefundishwa kujiajiri na kuajiri watu kwenye kazi. Aidha katika nchi zilizoendelea kuna hitajika kuwa na Ofisa Ustawi na chuo kwa sasa kinatakiwa kuweka wigo mpana kwa ajili ya kuendelea kuzalisha wataalam kwa lengo la kusaidia jamii na manufaa ya nchi kwa ujumla.

  Akizungumza na wanahabari Kaimu Mkuu wa  Taasisi, Mipango,fedha na utawala wa tasisi ya ustawi wa jamii Dk.Saliel Kanza ameeleza kuwa taasisi hiyo  ina changamoto kadhaa katika kutekeleza majukumu yake makuu matatu ambayo ni mafunzo,utafiti na kutoa ushauri wa weledi na changamoto hizo ni upungufu wa vifaa vya  Tehama katika kufundishia na kujifunza, uchakavu na upungufu wa Miundombinu ya kujifunza na kufundishia ikiwemo ofisi za walimu,vyumba vya semina,vyumba vya mihadhara(lecture theatre) na zahanati.

  Dk.Kanza pia amesema pamoja na ufinyu wa mapato,Taasisi imeendelea kuweka mikakati ya kuboresha mazingira bora ya kusomea kwa kubadilisha matumizi kwa baadhi ya Majengo na kuwa vyumba vya mihadhara.Pia ununuzi wa samani za ofisini na kompyuta ili kusaidia wanafunzi na wahadhiri kujifunza na kufundishia,Kufanya ukarabati wa miundombinu ya taasisi kama vile vyumba vya mihadhara kulingana na uwezo wa kifedha uliopo.

  Hata hivyo,mbali na kufanya hayo bado Taasisi Haina uwezo wa kutosha kifedha ili kutatua changamoto tajwa.Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi ya Magavana Sophia Simba amewapongeza wahitimu hao na kuwataka watumie elimu yao na ujuzi ili kusaidia jamii katika usuluhishi wa Migogoro mbalimbali katika jamii zetu.

  Simba amewahusia wahitimu katika fani zote kuwa ni kila nyanja katika jamii inauhitaji wa Ofisa ustawi kwani ni watu wenye ufanisi mkubwa sana katika kutatua,kusuluhisha,kusaidia maeneo yote kwa walemavu,makazini hata Mashuleni.
   Wahitimu wa chuo cha Ustawi wa jamii waliotunukiwa tuzo ya uzamili na Dkt John Jingu wakati wa mahafali hayo leo Jijini Dar es Salaam

  0 0

  Na. Vero Ignatus, Arusha

  Mkutano wa 20 wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika ya mashariki uliokuwa ufanyike leo Mkoani Arusha umeaihirishwa.

  Akitaja sababu za kuahirishwa kwa mkutano huo Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika ya mashariki kutoka Uganda Kirunda Kivejinja amesema nchi ya Burundi imekwamisha mkutano huo kwa kitokutuma muwakilishi

  Waziri wa mambo ya nje ya nchi ya Tanzania Mhe. Augustino Mahiga amesema marais wawili wa Sudan ya Kusini na Rwanda wametuma wawakilishi lakini Rais wa Burudi hakutuma muwakilishi yeyote kwenye vikao vyote

  '' Kwenye mikutano kama hii kuna kuwa na maandalizi ya ngazi tatu kwanza ni maafisa wataalam,makatibu wakuu na mwisho ya mawaziri na hatimaye inakuwa mkutano wawakuu lakini Burundi haikuleta wawakilishi kabisa na hawakutoa maelezo hivyo hatujui ninini kiewapata''alisema Mahiga

  Hivyo kutokana na sheria za mkataba wa Afrika ya Mashariki kikao cha mawaziri kilishindwa kuchukua maamuzi, kwani hata kikao cha maamuzi lazima kiwe na wawakilishi kutoka nchi zote sita ."Hivyo kikao cha mawaziri hakikutoa maamuzi yeyote, tulijadiliana tu hayo ni kutokana na kilichopo katika mkataba wetu"

  Amesema kuwa Marais na mawaziri walipokuja walikuwa na matumaini kuwa pengine Burundi wangetuma taarifa ama wawakilishi lakini toka walipoanza mkutano asubuhi kulikuwa hakuna taarifa yeyote hivyo wakuu wa nchi walipokutana wakaona haitawezekana kuendelea na mkutano huo

  "Na hata kama wangekuwa wanazungumza mazungumzo yao yasimgelikuwa na mashiko kisheria na maamuzi ya kisheria kwahiyo wakaamua huu mkutano uhairishwe ndiyo maana huo mkutano ukaahirishwa" alisema Mahiga. Hata hivyo Mahiga amesema itawalazimu kufanya mkutano mkuu wa Wakuu wa nchi zote sita na ni lazima iwe ndani ya mwaka huu, na ndani ya mwezi disemba 2018 kikatiba

  Jumuiya ya Afrika Mashariki inaundwa na nchi sita ikiwemo Tanzani, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudani Kusini.Mkutano huo wa 20 wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki uliokuwa umebeba kauli mbiu isemayo kuhuisha utengamano wa kijamii, kisiasa na kiuchumi wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki


  Mkutano wa 20 wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika ya mashariki uliokuwa ufanyike leo Mkoani Arusha umeairishwa.

  Akitaja sababu za kuahirishwa kwa mkutano huo Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika ya mashariki kutoka Uganda Kirunda Kivejinja amesema nchi ya Burundi imekwamisha mkutano huo kwa kitokutuma muwakilishi

  Waziri wa mambo ya nje ya nchi ya Tanzania Mhe. Augustino Mahiga amesema marais wawili wa Sudan ya Kusini na Rwanda wametuma wawakilishi lakini Rais wa Burudi hakutuma muwakilishi yeyote kwenye vikao vyote

  '' Kwenye mikutano kama hii kuna kuwa na maandalizi ya ngazi tatu kwanza ni maafisa wataalam,makatibu wakuu na mwisho ya mawaziri na hatimaye inakuwa mkutano wawakuu lakini Burundi haikuleta wawakilishi kabisa na hawakutoa maelezo hivyo hatujui ninini kiewapata''alisema Mahiga

  Hivyo kutokana na sheria za mkataba wa Afrika ya Mashariki kikao cha mawaziri kilishindwa kuchukua maamuzi, kwani hata kikao cha maamuzi lazima kiwe na wawakilishi kutoka nchi zote sita . "Hivyo kikao cha mawaziri hakikutoa maamuzi yeyote, tulijadiliana tu hayo ni kutokana na kilichopo katika mkataba wetu"

  Amesema kuwa Marais na mawaziri walipokuja walikuwa na matumaini kuwa pengine Burundi wangetuma taarifa ama wawakilishi lakini toka walipoanza mkutano asubuhi kulikuwa hakuna taarifa yeyote hivyo wakuu wa nchi walipokutana wakaona haitawezekana kuendelea na mkutano huo

  "Na hata kama wangekuwa wanazungumza mazungumzo yao yasimgelikuwa na mashiko kisheria na maamuzi ya kisheria kwahiyo wakaamua huu mkutano uhairishwe ndiyo maana huo mkutano ukaahirishwa" alisema Mahiga

  Hata hivyo Mahiga amesema itawalazimu kufanya mkutano mkuu wa Wakuu wa nchi zote sita na ni lazima iwe ndani ya mwaka huu, na ndani ya mwezi disemba 2018 kikatiba.Jumuiya ya Afrika Mashariki inaundwa na nchi sita ikiwemo Tanzani, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudani Kusini

  Mkutano huo wa 20 wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki uliokuwa umebeba kauli mbiu isemayo kuhuisha utengamano wa kijamii, kisiasa na kiuchumi wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki


  0 0


  Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Ndani wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Profesa William Matuja akiwasilisha utafiti wake juu ya Ugojwa wa Kifafa katika muhadhara wa Kiprofesa uliofanyika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS). Profesa Matuja alifanya utafiti wa Ugonjwa wa Kifafa kwa muda wa miaka minne katika Wilaya ya Mahenge, Morogoro. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
  Mwenyekiti wa Muhadhara huo, Prof. Gadi Kilonzo akifungua majadiliano ya kuulizana maswali juu somo la ugonjwa wa kifafa alilolitoa Profesa William Matuja (kushoto).
  Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Ndani wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Profesa William Matuja akiwasilisha utafiti wake juu ya Ugojwa wa Kifafa katika muhadhara uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS). Profesa Matuja alifanya utafiti wa Ugonjwa wa Kifafa kwa miaka minne katika Wilaya ya Mahenge, Morogoro.

  Wageni waalikwa wakifuatilia muhadhara huo.
  Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Ndani wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Profesa William Matuja (kushoto) akikabidhiwa zawadi ya cheti shukrani na Mhadhiri mwandamizi idara. Dkt. Tumaini Nagu mara baada ya kumaliza kuwasilisha utafiti wake juu ya ugonjwa wa kifafa. Katikati ni Kaimu Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Ndani Dkt. Patricia Munseri.
  Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Ndani wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Profesa William Matuja (kulia) akikabidhiwa zawadi na Mhadhiri mwandamizi idara ya Magonjwa ya Ndani Dkt. Tumaini Nagu mara baada ya kumaliza kuwasilisha utafiti wake juu ya ugonjwa wa kifafa.
  Dkt Pilly Chillo akikabidhi zawadi ya ua.
  Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Ndani wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Profesa William Matuja (kulia) akikabidhiwa zawadi na Kaimu Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Ndani Dr. Patricia Munseri mara baada ya kumaliza kuwasilisha utafiti wake juu ya ugonjwa wa kifafa.
  Afisa Uhusiano wa MUHAS, Hellen Mtui akitoa shukrani kwa wageni waliofika katika muhadhara huo.
  Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Ndani wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Profesa William Matuja akiwa na uongozi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili pamoja na wanafamilia.
  Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Ndani wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Profesa William Matuja akiwa na uongozi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili pamoja na wafanyakazi wa kitengo chake.


  Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

  Imani potofu ndiyo inayopelekea kuongezeka wa Ugonjwa wa Kifafa katika maeneo mbali mbali ya nchi ya Tanzania hasa Wilaya ya Mahenge, Morogoro.
   
  Hayo ameyasema Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Ndani wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Profesa William Matuja wakati akiwasilisha ufatifi wake katika muhadhara uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) ili kuweza kutoa mapendekezo yake njia za kuweza kusaidia jamii.

  Profesa Matuja amesema Jamii inahitaji kuondokana na imani potofu maana watu wengi wamekuwa wakijua kuwa ugonjwa unasambabishwa na ushirikina.Ameongeza kuwa jamii ni bora kujitokeza kupima mara kwa mara ili kuweza kupatiwa tiba mahususi ili kuweza kuondokana na tatizo hilo.

  "Nimefanya utafiti katika wilaya ya Mahenge, Morogoro ila tulichogundua mwanzo ni jamii haikuwa na ueleza zaidi kuhusiana na ugonjwa wa kifafa na hivyo kupelekea watu wengi sana kuugua ugonjwa huo, lakini wengi wao wanafikiria imani potofu hasa haya mambo ya ushirikina," ameongeza Prof Matuja.

  Aidha ameongeza kuwa ni vyema serikali na wadau wote wa afya kujitokeza kuipa elimu ya kutosha jamii ili kuweza kutambua jinsi ugonjwa wa kifafa unavyopatikana na tiba yake.

  Profesa Matuja amesema kwa sasa kuna aina mpya ya kifafa ambayo ni Kifafa cha Kichwa kuanguka kifuani (Nodding Syndrome) ambao ulionekana kwa mara ya kwanza 1960 katika wilaya ya Mahenge na kwa nchi nyingine Kifafa hichi kimeonekana miaka ya 1980 Liberia, Cameroon, Sudan Kusini na Uganda Magharibi miaka ya 2000.

  Amesema njia kuu za kujikinga na kifafa Tanzania ni:-


  1. Kujikinga na visababishi vinavyozuilika kama kumjali mama mjamzito kipindi cha ujauzito kwa kumshauri kuhudhuria kliniki pamoja na kumpatia vipimo mara kwa mara, ugunduzi na matibabu ya haraka kwa watoto wanaopata homa, matumizi ya choo, kunawa mikono na kula nyama ya nguruwe iliyoiva vizuri.

  2. Kuwepo na muendelezo wa kutoa elimu vjijini ili kutonyanyapaa na kuwabagua kwa makundi kutokana na matatizo yao; mfano mashuleni kwa ngazi zote ikiwemo walimu.

  3. Kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa afya juu ya chanzo, jinsi ya kujikinga na matibabu sahihi kwa watu wenye kifafa.

  4. Kutoa elimu maalum inayohitajika kwa watoto wenye kifafa na uwezo wa kusoma.

  5. Serikali ihakikishe kuwepo na utoaji wdawa za kutosha.

  0 0

  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  CHAMA cha Wanasheria Wanawake(TAWLA) kimewakutanisha wadau mbalimbali kwa lengo la kujadili , kuchambua na kuweka mikakati ya namna ya kuwasaidia watoto  ambao wapo kwenye ukinzani wa kisheria hasa kipindi hiki ambacho mmomonyo wa maadili kwenye jamii umekuwa mkubwa na kusababisha watoto wengi kujikuta wakiingia kwenye ukinzani huo wa kisheria.

  Baadhi ya wadau ambao wamekutanishwa na TAWLA ni polisi, maofisa ustawi wa jami, wanasheria wenyewe, mahakimu, masheikh na wachungaji pamoja na wadau wengine wanaojihusisha na masuala ya watoto nchini  Tanzania.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania(TAWLA)Tike Mwambipile amesema wameamua kukaa pamoja na kisha kutazama nini wafanye katika kuwasaidia watoto walioko kwenye ushindani wa kisheria na kwamba wakati wa najadiliana kwenye hilo watatumia nafasi hiyo kuulizana maswali ya msingi ya kisheria likiwamo la wapi wamekosea.

  Amefafanua sheria inasema kesi ya mtoto isikilizwe ndani ya siku mmoja na hiyo ni changamoto kwani ni ngumu kutumia siku moja kusikiliza kesi ambapo utahitaji pia mashahidi na mambo mengine ya kisheria na hivyo wadau hao wataangalia nini kifanyike angalau kutoa nafasi ya kutosha ya kusikiliza kesi za watoto kwenye makosa ya haki jinai.

  " Tumekutana wadau mbalimbali leo hii kwa lengo la kukaa pamoja na kutazama kitu gani hasa tufanye hasa kwa kuzingatia kwenye jamii yetu kunachangamoto ya maadili ambayo inachangia watoto wengi kuingia kwenye sheria kinzani.Hivyo tutaka na majibu ambayo angalau yatatuongoza ili tuweze kumsaidia mtoto ambaye atakuwa na kosa jinai,"amesema.

  Amefafanua kuna milolongo mingi kwenye sheria zinazohusu mtoto na hivyo ni wakati sahihi wa kuangalia nini kifanyike kuwaisaida watoto wenye makosa mbalimbali na wamefikishwa mbele ya sheria."TAWLA tunaamini kupitia kikao hicho wadau watajadiliana na kutoka na majibu ya wapi tunatakiwa kwenda na wapi tulikosea katika sheria zinazohusu watoto,"amesema Mwambipile.

  Kwa upande wake Wakili Barnabas Kaniki amefafanua kwa kina kuhusu masuala ya kisheria hasa zinazohusu watoto na kwamba sheria inazungumzia kuanzishwa kwa mahakama za watoto wilayani lakini kinachotokea haziko nchi nzima.

  Amesema japo sheria inataka ianzishwe mahakama maalumu ya watoto na sheria imeeleza namna ambavyo kesi za watoto zinavyotakiwa kuendeshwa na kwamba kuna hatua nzuri ambayo imefikia kwenye eneo hilo.

  Wakili Kaniki amesema pamoja na kwamba kuna taratibu maalum za kuendesha kesi za watoto changamoto iliyopo ni kwamba bado watoto wanapelekwa kwenye mahakama za wakubwa. "Ukweli ni kwamba wakati wadau tumekutana kujadili kwa kina kuhusu haki jina kwa mtoto , wenzetu wa mahakama wamekwenda mbele zaidi kwa kuzipa mamlaka mahakama za wilaya kusikiliza kesi za watoto."

  Amesisitiza sheria ya mtoto ya mwaka 2009 imeleta mapinduzi makubwa kwenye suala zima la ulinzi wa mtoto nchini Tanzania na kufafanua sheria imetaka kuanzishwa kwa mahakama hizo za watoto.

  Alipoulizwa ni makosa gani ambayo watoto wengi wanashitakiwa nayo na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria, amejibu kuwa watoto wengi wanafikishwa mahakamani kwa makosa ya wizi ambao aidha wa kusingiziwa au wa kweli , makosa ya ubakaji na makosa mengine mbalimbali ambayo yanakuja kwa mtindo tofauti.

  Amesema sheria ya Tanzania inamtambua mtu mwenye umri wa miaka chini ya 18 ni mtoto na hivyo anapofanya kosa na akafikishwa mahakamani hata akiwa na miaka 17 au 18 maana yake kwa mujibu wa sheria lazima suala lake  lishughulikiwe kwa kuangalia sheria ya mtoto inavyotaka.

  Wadau wengine ambao wamekutana kujadili sheria za mtoto nchini wameimbia Michuzi Blog kuwa wanaipongeza TAWLA kutokana na kutambua na kuona umuhimu wa kuwanisha wadau hao ili kuangalia namna gani bora katika kuwasaidia watoto wenye matatizo ya kisheria.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA), Tike Mwambipile akizungumza na Michuzi TV pamoja na Michuzi Blog leo jijini Dar es Salaam wakati wa semina maalum iliyoandaliwa na chama hicho kujadili haki za Watoto wenye matatizo ambao wanahitaji msaada wa kisheria.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA), Tike Mwambipile akisoma moja ya Kitabu kinachohusu masuala ya kisheria wakati wa semina ya kujadili namna ya kumsaidia mtoto ambaye ameingia kwenye ukinzani wa kisheria.Semina hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Wakili Barnabas Kaniki akizungumzia mjadala ulioandaliwa na Chama hicho, uliokuwa unajadili haki za watoto wenye matatizo ambao wanahitaji masaada wakisheria.
  Baadhi ya washiriki wa mjadala huo wakiwa kwenye semina maalum iliyoandaliwa na Chama cha Wanasheria Wanawake(TAWLA) walipokutaa leo jijini Dar es Salaam.

  0 0  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Ndg. Salum Kassim Ali, hafla hiyo imefanyika leo 1-12-2018 Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
  IMG_0814
  VIONGOZI walioteuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, hivi karibuni wa  kwanza Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi  Zanzibar Ndg. Thabit Idarous  Faina, Katibu wa Tume ya Maadili ya Viongozi  wa Umma  Zanzibar Bi. Asma Hamid Jidawi na Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ndg. Salum Kassim Ali, wakipitia Hati zao za kiapo kabla ya kuaza kwa hafla hiyo iliofanyika leo 1-12-2018 Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
  IMG_0819
  MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi  Seif Ali Iddi, akisalimiana na Mkurugenzi Mpya wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar kabla ya kuapisha  Ndg. Thabit Idarous Faina, alipowasili katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar kuhudhuria hafla hiyo ya kuapishwa leo Ikulu 1-12-2018.(Picha na Ikulu)
  IMG_0829
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisaini hati ya kiapo ya Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Ndg. Salum Kassim Ali, baada ya kumuapisha hafla hiyo imefanyika leo 1-12-2018 Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
  IMG_0839_1
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Katibu  Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma  Zanzibar Bi.Asma Hamid Jidawi, hafla hiyo imefanyika leo  1-12-2018 Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
  IMG_0841
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisaini hati ya Kiapo ya Katibu wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma Zanzibar.Bi. Asma Hamid Jidawi, baada ya kumuapisha leo 1-12-2018, hafla hiyo imefanyika Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
  IMG_0849
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC)Ndg. Thabit Idarous Faina, hafla hiyo imefanyika leo 1-12-2018, Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
  IMG_0854
  AIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisaini hati ya Kiapo ya Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Ndg. Thabit Idarous Faina, baada ya kumuapisha , hafla hiyo imefanyika leo 1-12-2018 Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
  IMG_0861
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimkabidhi hati ya kiapo Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Ndg. Thabit Idarous Faina,hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
  IMG_0865
  BAADHI ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakifuatilia hafla ya kuapishwa kwa Viongozi walioteuliwa hivi karibu kuchukua nyadhifa hizo, hafla hiyo imefanyika Ikulu Zanzibar,1-12-2018. (Picha na Ikulu)
  IMG_0868
  MWANASHERIA Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Said Hassan Said, wa kwanza kulia akiwa na baadhi ya Mawaziri waSerikali ya Mapinduzi Zanzibar, wakihudhuria hafla ya kuapishwa kwa Viongozi walioteuliwa hivi karibu kushika nyadhifa hizo, hafla hiyo imefanyika Ikulu Zanzibar.1-12-2018.(Picha na Ikulu)
  IMG_0873
  BAADHI ya Wanafamilia wa Viongozi walioteuliwa hivi karibuni wakihudhuria hafla hiyo ya kuapishwa iliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
  ????????????????????????????????????
  BAADHI ya Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakihudhuria hafla ya kuapishwa kwa Naibu Katibu  Mkuu Wizara ya Nchi  Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi , Mkurugenzi  wa  Tume ya Uchaguzi  Zanzibar na Katibu wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma Zanzibar  Bi.Asma Hamid Jidawi, hafla hiyo imefanyika leo 1-12-2018  Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
  ????????????????????????????????????
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiingia katika ukumbi wa  mkutano Ikulu Zanzibar, kwa ajili ya hafla ya kuwaapisha Viongozi aliowateua hivi karibu kushika nyadhifa hizo, hafla hiyo imefanyika Ikulu leo,1-12-2018 .(Picha na Ikulu)

  IMG_0927
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti  wa  Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein,kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Ndg.Salum Kassim Ali, Katibu wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma Zanzibar.Bi. Asma Hamid Jidawi  na kulia Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid, Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar(ZEC)Ndg Thabit Idarous Faina na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Saleh Omar Kabi,  wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika hafla hiyo, iliofanyika Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)

  0 0

  Jamii imetakiwa kupiga vita mila potofu, mimba na ndoa za utotoni kwani zinachangia uwepo wa maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa vijana na watoto mkoani Shinyanga.

  Rai hiyo imetolewa leo Jumamosi Desemba 1,2018 na Afisa Mradi wa Afya ya Uzazi na Ujinsia kwa Vijana wa Shirika la Agape AIDS Control Program la Mjini Shinyanga Lucy Maganga wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani ambapo katika wilaya ya Shinyanga yamefanyika katika kijiji cha Shilabela kata ya Pandagichiza.

  Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga,Boniface Chambi kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko.Maganga alisema ili kutokomeza Maambukizi ya VVU ni lazima jamii ipewe elimu ya afya uzazi na madhara ya mila potofu, mimba na ndoa za utotoni kwani vinachangia maambukizi ya VVU na Ukimwi hasa kwa vijana na watoto.

  Alisema katika kuhakikisha maambukizi ya VVU kwa watoto yanatokomezwa mkoani Shinyanga,shirika la Agape limekuwa likitoa elimu ya afya uzazi kupitia mradi wake wa wa Afya ya Uzazi na Ujinsia kwa Vijana katika wilaya ya Shinyanga.

  Maganga alisema lengo la mradi huo unaotekelezwa na Agape kwa ufadhili wa Shirika la Kimataifa la Sida la nchini Sweden, ni kuwajengea uwezo watoto na vijana kujitambua,kujithamini na kujitunza dhidi ya tabia hatarishi zinazoweza kuwasababishia mimba za utotoni na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi pamoja na magonjwa ya zinaaa.

  “Tupo hapa kuungana na wadau wengine kuadhimisha siku ya Ukimwi Duniani kwani, kwetu Ukimwi ni suala mtambuka,Ukimwi upo, siku ya leo inatukumbusha kuwa ni jukumu letu sote kujilinda na kuwalinda wengine dhidi ya maambukizi ya VVU”,alieleza Maganga.

  “Katika kuadhimisha siku ya Ukimwi duniani mwaka huu,Agape tumetoa elimu kuhusu VVU na Ukimwi kwa njia ya sinema katika vijiji vya kata ya Shilabela,Sayu na Pandagichiza tukilenga makundi yote katika jamii wakiwemo watoto na vijana”,alisema.Kwa upande wake,Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga,Boniface Chambi aliwataka wananchi kutoogopa kupima na kutumia ARVs hivyo wajitokeze kupima afya zao ili kuhakikisha malengo ya 90 tatu yanafikiwa.

  “Tunataka ifikapo 2020, asilimia 90% ya watu wenye maambukizi ya VVU wawe wamefikiwa na kupimwa,kati yao asilimia 90% ya walioathirika watapewa dawa za kufubaza virusi (antiretroviral treatment) na asilimia 90% ya watakaotumia dawa hizo hawataweza kuwaambukiza wenza watakaojamiiana nao kwasababu virusi vitakuwa vimefubazwa na tiba hiy”,alisema Chambi.

  Naye Mganga Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Dkt.Amos Mwenda alisema wanaendelea kushirikiana na wadau waliopo katika halmashauri hiyo ili kuongeza nguvu kwenye huduma za upimaji VVU,uanzishaji wa dawa za kufubaza VVU na kutoa huduma stahiki kwa watu waishio na VVU.

  Hata hivyo alizitaja changamoto wanazokabiliana nazo kuwa ni ushiriki duni wa jamii hasa wanaume katika suala la upimaji VVU na huduma ya afya ya baba,mama na mtoto pamoja na upungufu wa wataalamu wa afya kwa ajili ya utoaji huduma shirikishi za UKIMWI.

  Shirika la Agape limetumia fursa ya maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani kutoa msaada wa sare za shule kwa wanafunzi yatima 10 wanaosoma katika shule ya msingi Pandagichiza kwa ajili ya kuwapa hamasa wapende shule na kufanya vizuri kwenye masomo yao.


  Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga,Boniface Chambi akikabidhi sare za shule zilizotolewa na shirika la Agape kwa ajili ya watoto yatima/wanaoishi katika mazingira wanaosoma katika shule ya msingi Pandagichiza wakati wa maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. 

  Mgeni rasmi Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga,Boniface Chambi kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani wilaya ya Shinyanga ambayo yamefanyika katika kijiji cha Shilabela kata ya Pandagichiza.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
  Afisa Mradi wa Afya ya Uzazi na Ujinsia kwa Vijana wa Shirika la Agape AIDS Control Program la Mjini Shinyanga Lucy Maganga akizungumzawakati wa Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani ambapo katika wilaya ya Shinyanga ambayo yamefanyika katika kijiji cha Shilabela kata ya Pandagichiza. 
  Wanafunzi na wananchi wa Pandagichiza wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani Desemba 1,2018.
  Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Ngasa Mboje akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani katika wilaya ya Shinyanga.
  Mganga Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Dkt.Amos Mwenda akisoma taarifa kuhusu maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani Desemba 1,2018.
  Mgeni rasmi Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga,Boniface Chambi kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko akikabidhi sare za shule kwa mmoja wa wanafunzi/watoto yatima 10 wanaosoma katika shule ya msingi Pandagichiza iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.Sare hizo zimetolewa na Shirika la Agape ambalo linatekeleza Mradi wa Afya ya Uzazi na Ujinsia kwa Vijana katika halmashauri hiyo. 
  Mwanafunzi wa shule ya msingi Pandagichiza akipokea sare ya shule.
  Wanafunzi wa shule mbalimbali katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakisubiri kupewa zawadi mbalimbali ikiwemo ya sare za shule,madaftari na kalamu.
  Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga,Boniface Chambi akikabidhi zawadi ya madaftari na kalamu kwa mwanafunzi.
  Wadau mbalimbali wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani Desemba 1,2018.
  Wanafunzi na wananchi wa Pandagichiza wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani Desemba 1,2018.  Wanafunzi wa shule ya msingi Pandagichiza wakifurahia zawadi ya sare za shule walizopewa na shirika la Agape.Kulia ni Mwalimu wa shule hiyo,Lucia Maungo.
  Wanafunzi wanaosoma katika shule ya msingi Pandagichiza halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakiwa wameshikilia zawadi ya sare za shule zilizotolewa na shirika la Agape.
  Wanafunzi wanaosoma katika shule ya msingi Pandagichiza halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,walimu wa shule ya msingi Pandagichiza na wafanyakazi wa shirika la Agape wakiwa katika picha ya pamoja.


  Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

older | 1 | .... | 1739 | 1740 | (Page 1741) | 1742 | 1743 | .... | 1898 | newer