Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1730 | 1731 | (Page 1732) | 1733 | 1734 | .... | 1898 | newer

  0 0


  Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Bunge la Vijana mwaka 2018 linalofanyika katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma kulia kwake ni Spika wa Bunge la Vijana Mhe. Zephania Sane na kushoto kwake ni Naibu Spika wa Bunge la Vijana, Mhe. Ashiruna Mhunzi
  Mapambe wa Bunge akiongoza msafara wa Spika wa Bunge la Vijana kuingia Ukumbini kwa ajili ya kuanza Kikao cha Kwanza cha Bunge hilo kwa mwaka 2018 kilichofanyika katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma.
  Spika wa Bunge la Vijana, Mhe. Zephania Sane akiapa kushika nafasi hiyo mbele ya Katibu wa Bunge hilo, Ndugu Alphonsina Ambrosi. Mkutano wa Bunge la Vijana mwaka 2018 unaendelea katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma.

  Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Vijana mwaka 2018 wa wakila kiapo cha utii mbele ya Spika wa Bunge hilo la vijana, Mhe. Zaphania Sane.wengine ni Makatibu Kamati wa Bunge hilo.

  Spika wa Bunge wa Bunge , Mhe. Job Ndugai akisalimiana na Spika wa Bunge la Vijana mwaka 2018 Mhe. Zephania Sane kabla ya kuanza kwa kikao cha Bunge hilo katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma. Mhe. Ndugai alikuwa mgeni ramsi na alifungua Bunge hilo la Vijana.


  ………………….
  Na.Alex Sonna wa Fullshangweblog,Dodoma

  Spika wa Bunge Job Ndugai amewataka wabunge Bunge la Vijana, kutumia mafunzo ya Bunge hilo kwa weledi wa kutosha juu ya uendeshaji wa Bunge na kuwa mabalozi wazuri watakaporejea vyuoni.

  Spika ameyasema leo jijini Dodoma alipokuwa akifungua mkutano wa Bunge la Tano la Vijana ukiwa na lengo la kuwaandaa Vijana kuwa viongozi bora wa baadaye lakini pia kuwa na mijadala inayofika mwisho bila kugombana.Mkutano Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na UNDP kupitia mradi wa kuwajengea uwezo wabunge awamu ya pili (LSP II) na kufanyika katika ukumbini wa Pius Msekwa.

  Spika amesema kuwa mkutano wa Bunge hili ambao umejumuisha vijana kutoka Vyuo vya Elimu ya juu , lina lengo la kuwawezesha Vijana hao kutumia mijadala zaidi na viongozi wao wawapo vyuoni badala ya kukimbilia migomo katika kutafuta suluhisho la changamoto zinazowakabili.

  Aidha Spika amebainisha kuwa, shabaha ya Bunge hilo ni kuwawezesha vijana kuelewa taratibu za uendeshaji wa Bunge,kuwafundisha Vijana Utamaduni wa kuvumiliana kwa kubishana kwa hoja na kuheshimu wengine kuwaelimisha Vijana juu ya changamoto mbalimbali zinazoikabili Jamii na Taifa kwa ujumla na kuwafundisha vijana umuhimu wa kufikia maamuzi baada ya mjadala wa pamoja.

  Spika amewaomba wabunge kutumia mafunzo ya Bunge hilo kuwa na weledi wa kutosha juu ya uendeshaji wa Bunge na kuwataka kuwa mabalozi wazuri watakaporejea vyuoni. Akimkaribisha Ndugai, Spika wa Bunge hilo Zephania Sane amesema kuwa matarajio yao ni kujifunza jinsi Bunge linavyofanya kazi hususan ya kupitisha miswada na kutungwa Sheria za Nchi.Mhe.Sane amesema kuwa Vijana wapo pamoja na Rais John Magufuli na wanamuunga katika kila anachokifanya kwa mustakabali wa wananchi na Taifa kwa ujumla.

  Bunge hilo ambalo linafanyika kwa muda wa siku tano, limejumuisha Vijana 60 kutoka Vyuo vya Mipango na Maendeleo Vijijini (IRDP),Chuo Kikuu cha Dodoma,Chuo cha Biashara Tawi la Dodoma (CBE) Chuo Kikuu cha Mzumbe,Chuo Kikuu cha Kiislam cha Morogoro na Chuo Kikuu cha Uhasibu Moshi Mkoani Kilimanjaro.

  0 0

  Madaktari Bingwa wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na wataalam wa afya wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Mtwara-Ligula- leo wanawafanyia upasuaji wagonjwa 10 wenye matatizo ya mafindofindo. 

  Matibabu hayo ya kibingwa hayafanyiki katika Hospitali ya Ligula kutokana na ukosefu wa wataalam waliobobea katika maeneo ya pua, koo na masikio. 
  Daktari Bingwa wa upasuaji pua, koo na masiko kutoka Muhimbili Willybroad Massawe amesema wanawafanyia upasuaji watu wazima pamoja na watoto na kwamba upasuaji huo umeanza kufanyika leo. 

  ‘’Tumeanza kufanya upasuaji huu leo asubuhi na lengo letu ni kumaliza wagonjwa wote kumi leo hii’’ amesema Dkt. Massawe. 

  Kwa mujibu wa mtaalam huyo ugonjwa wa mafindofindo unasababishwa na maambukizi ya mara kwa mara katika njia ya hewa na kwa wengine unatokana na mzio (allergies) zilizokithiri. 

  Hospitali ya Taifa Muhimbili imeanzisha programu ya kutoa huduma kwa njia ya mkoba ili kujenga uwezo wa Hospitali za Rufaa za Mikoa nchini hasa katika maeneo yenye wataalam lakini wanahitaji kuongezewa ujuzi zaidi katika fani mbalimbali ili kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda kutibiwa Muhimbili. 

  Daktari Bingwa wa upasuaji pua, koo na masikio Willybroad Massawe akimtoa mgonjwa matezi ya koo na matezi ya nyama ya pua (mafindofindo), upasuaji huo umefanyika leo katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Mtwara-Ligula.
  Mtaalam wa usingizi (nusu kaputi) Dkt. Amon Kingu (kushoto) pamoja na watalaam wengine wa Hospitali ya Ligula wakiwamuandaa mgonjwa kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji.

  0 0

   Leandra Gabriel na Karama Kenyunko Blogu ya jamii.

  SERIKALI imesema ipo katika mpango wa kutengeneza muongozo ambao utasaidia katika utoaji huduma kwenye hospitali binafsi ikiwemo suala la ongezeko la gharama ambazo zinawafanya wananchi wa kawaida kushindwa kupata huduma.

   Mkurugenzi  wa tiba kutoka Wizara ya Afya, maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto Dkt. Dorothy Gwajima amesema hayo leo Novemba 20.2018 wakati wa uzinduzi wa mkutano wa 19 wa wadau wa afya na hospitali binafsi. Amesema kuwa muongozo huo utasaidia hospitali binafsi ambazo hutoa huduma  kwa gharama kubwa kuacha kuwabagua wagonjwa wa dharula kwani ni lazima afya ya mtu ije kwanza.

  "Tunashughulikana  hospitali zenye  tozo kubwa kwa wagonjwa, kwani ni sawa kwao kuweka gharama zao kutokana na mfumo wa kutibu magonjwa maalumu, ni sawa kwa hospitali hizo kuwa na gharama zao ila kwa magonjwa ya dharura lazima huduma zitolewe bila kuangalia hadhi ya hospitali hizo" ameeleza Dkt. Gwajima.

  Aidha amesema kuwa malengo ya kufanya mkutano huo ni kujadili juu ya kuimarisha utoaji wa huduma katika vituo vyao vya kutolea huduma. Dkt. Gwajima amesema kuwa sekta binafsi zinamiliki asilimia 40 za  utoaji wa huduma za afya nchini  na pia wanashiriki sana katika utoaji ajira na wao kama serikali wanatambua mchango wao na changamoto zao lazima wazifanyie kazi.
   Mwenyekiti wa chama cha wamiliki binafsi wa vituo vya afya nchini (APHFTA) Dkt. Kaushik Ramaiya (kushoto) wakifuatilia mjadala uliozinduliwa na Mkurugenzi wa tiba leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Afisa mtendaji wa APHFTA Dkt. Samwel Ogillo. (Picha na Erick Picson, Blogu ya jamii)
  Mkurugenzi wa tiba kutoka Wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza wakati akifungua mkutano wa 19 wa wanachama na wamiliki binafsi wa vituo vya afya leo jijini Dar es Salaam.
   Afisa mtendaji  wa wanachama wa wamiliki binafsi wa vituo vya afya Dkt. Samwel Ogillo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi wa mkutano huo ambao umejikita zaidi katika kujadili namna ya kuimarisha zaidi sekta ya afya nchini .
  Afisa mtendaji  wa wanachama wa wamiliki binafsi wa vituo vya afya Dkt. Samwel Ogillo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi wa mkutano huo ambao umejikita zaidi katika kujadili namna ya kuimarisha zaidi sekta ya afya nchini .  0 0

    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo  kutoka kwa Saidi Kanimba  kuhusu viatu vya ngozi vinavyotengenezwa   katika Halmashuri ya wilaya Uyui mkoani Tabora katika Maonyesho ya  Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji Mkoani Tabora yailyofanyika kwenye Viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Novemba 21, 2018. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama sabuni za Kampuni ya Matabula Soap Investment ya Kaliua mkoani Tabora, Imani Matabula  (kulia)  katika  maonyesho   ya Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji Mkoani Tabora yaliyofanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Novemba 21, 2018. Katikati ni Mkuu wa Mkoa huo, Aggrey Mwanri. Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Imani Matabula. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Imani Matabula  (kulia)  kuhusu sabuni zinazotengenezwa na Kampuni yake ya Matabula Soap Investment ya Kaliua mkoani Tabora katika maonyesho   ya Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji Mkoani Tabora yaliyofanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Novemba 21, 2018. Katikati ni Mkuu wa Mkoa huo, Aggrey Mwanri.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama chupa yenye ujazo wa nusu lita yA mkojo wa sungura wakati alipotembelea banda la wanawake wajasiriamali wasindikaji wa Tabora katika maonyesho ya Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji katika Mkoa wa Tabora yaliyofanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Novemba 21, 2018. Kwa mujibu wa Mratibu wa Wajasiriamali hao, Bibi Ashura Mwazembe, mkojo wa Sungura unatumiwa kama mbolea ya mazao ya kilimo na pia ni dawa nzuri sana ya kuua wadudu waharibifu wa mazao. Lita moja ya mkojo huo inauzwa sh. 10, 000/=. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

   Waziri Mkuu, Kasssim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji mkoani Tabora kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo, Novemba 21, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  CHAMA cha Riadhaa nchini (RT), kimetoa baraka kwa wandaaji was mbio za kujifurahisha Mbezi Fun Run zilizopangwa kufanyika Desemba Mosi jijini Dar es Salaam.

  Katibu Mkuu wa RT, Willihelmi Gudagudai alisema RT imetoa kibali kwa wandaaji hao baada ya kufuata taratibu zote."Tumewataka baada ya tamasha lao, wawasiliane na RT ili mbio zao ziingizwe kwenye kalenda ya mwaka ya matukio ya RT."alisema.

  Kwa upande wa waandaji hao kupitia kwa katibu Mbezi Fun Run Omary Kimbau alisema mandalizi ya mbio hizo yamekamilika kwa asilimia 90 mpaka Sasa, na kwamba kuanzia leo wataweka wazi vituo mbali mbali vya kujiandikisha kwa yeyote anayependa kushiriki.

  "Kushiriki ni bure, hakuna kingilio chochote na mlango upo wazi kwa yeyote, ila kuna tisheti na beji kwa wakimbiaji, beji shilingi 10,000 na atakayependa kutumia fulani zetu bei ni shilingi 25,000."alisema.Kimbau alisema mbio hizo zimeandaliwa na umoja wa wakazi wa Mbezi Beach zikiwa na lengo la kufahamiana na kubadilishana mawazo na kusaidia kwenye changamoto mbali mbali huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Ummy Mwalimu.

  “Kama mnavyojua siku hiyo ya Desemba Mosi itakuwa ni siku ya ukimwi duniani hivyo pia tumemualika Waziri Ummy Mwalimu awe mgeni rasmi na tutafanya nae mazoezi ya pamoja, na pia kutakuwa na zoezi la uchangiaji damu.“Damu salama inahitajika kwenye banki ya damu, kama haijanisaidia mimi itamsaidia ndugu yangu, jamaa au mtanzania yoyote yule, hivyo tumeona siku hiyo pia tuitumie kuchangia damu salama na pia kupima afya yetu kwa kupima maambukizi ya virusi ya ukimwi.”alisema.

  Naye mwakilishi kutoka kitengo cha afya Angaseege Getruda Kafuko, akizungumza kwa niaba ya mganga Mkuu wilaya ya Kinondoni alisema wamefurahishwa na uamuzi wa waandaaji wa Mbezi Fun Run kuona umuhimu wa kuchangia damu."Kupima afya pia ni jambo zuri hasa kwa wanaume, kupitia Kampeni ya Afya yangu, wajitokeze kwa wingi ili wajue afya zao na kuelimishana kuishi katika mtindo bora wa maisha." alisema.

  Naye mkurugenzi wa ufundi wa mbio hizo Isihaka Mlawa akizungumzia njia watakazopita wakimbiaji hao alisema mbio zitakua za kilomita 15, 10 na kilomita tano.Alisema kwa upande wa Kilomita 15 wakimbiaji wataanzia Ramada hotel, hadi clouds fm, kushukia barabara ya tank bovu, na kurejea Ramada.Wakati wa Kilomita 10 wataanzia Ramada hadi njia panda ya kwa Kusaga na mkurejea Ramada wakati wale wa Kilomita tano wataanzia Ramada mpaka Rainbow na kurejea Ramada.

  Kwa upande wa mwenyekiti wa bonaza hilo la Mbezi Run Fun Loraa George ‘Robelo’ alisema ni wakati sasa watanzania kufanya mazoezi na ili kuepuka magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo sukari na shinikizo la damu.“Bonaza hili linajumuisha wana Dar es Salaam yoyote atakayependa kushiriki, lengo ni kujumuika pamoja na kufahamiana, mbali na kukimbia pia kutakuwa na burudani nyingine nyingi ikiwemo mashindano ya kucheza mziki na michezo mbali mbali ya watoto.”alisema Loraa.

  Alisema burudani katika bonaza hilo itatolewa na K- Mondo Sound na Up town intertaiment.


  Pichani kati ni mwenyekiti wa bonaza hilo la Mbezi Run Fun Loraa George ‘Robelo’ alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya mbio hizo ambazo anaeleza kuwa kwa asilimia 90 yamekamilika,kulia ni Katibu wa Mbezi Fun Run Omary Kimbau na kushoto ni mwakilishi kutoka kitengo cha afya Wilaya ya kinondoni Getruda Kafuko.
  Katibu wa Mbezi Fun Run Omary Kimbau akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari jana kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya mbio hizo  kwa asilimia 90 mpaka Sasa,na kuongeza kuwa vitakuwepo vituo mbali mbali vya kujiandikisha kwa yeyote anayependa kushiriki.

  "Kushiriki ni bure, hakuna kingilio chochote na mlango upo wazi kwa yeyote, ila kuna tisheti na beji kwa wakimbiaji, beji shilingi 10,000 na atakayependa kutumia fulani zetu bei ni shilingi 25,000."alisema.Kimbau alisema mbio hizo zimeandaliwa na umoja wa wakazi wa Mbezi Beach zikiwa na lengo la kufahamiana na kubadilishana mawazo na kusaidia kwenye changamoto mbali mbali huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Ummy Mwalimu.
  Mkurugenzi wa ufundi wa mbio za Mbezi Fun Run Isihaka Mlawa akionesha kibali walichopewa mara baada ya kufuata na kukamilisha taratibu zote kutoka chama cha Riadhaa nchini (RT).

  0 0


  0 0


  Kumekucha Kwenye Promosheni ya Shinda Zaidi na SportPesa maana watanzania wanazidi kushinda bajaj kutokana na ubashiri wanaofanya kupitia timu ya ushindi.

  Safari hii kambi ya timu ya ushindi imehamia hapa jijini Dar es salaam katika viunga vya Mbezi Juu ambapo kuna mshindi wa droo ya 57 Emmanuel Nzuki anayekabidhiwa bajaj baada ya ushindi.

  Akizungumza baada ya kukabidhiwa bajaj hiyo Nzuki alisema hakuamini kama anaweza kushinda maana mara kadhaa alikuwa anacheza mara nyingi lakini hakubahatika kumbe wakati wake ulikuwa haujafika kubahatika sasa ndio ameamini baada ya kuupokea ushindi huo

  "Ama kweli nimeamini bahati ya mtu haipotei unajua vile nilikuwa nikiona wengine wakishinda nilijua labda wanaoshinda ni wale wenye kipato cha chini kabisa kumbe hata sisi wenye kipato cha kati inawezekana, siku ya leo yote naitumia kusherekea ushindi wangu" alisema Nzuki.

  Aidha mshindi huyo aliongeza kuwa bajaj hiyo itaweza msaidia kuinua kipato chake na kuacha maisha ya kutegemea mshahara pekee. "Sikia nikwambie aisee ni kweli nina mshahara mzuri lakini bado bajaj hii itakuwa msaada mkubwa kwangu maisha ya kutegemea mshahara pekee ni magumu sana lakini kupitia bajaj hii naweza sasa boresha maeneo mengine mfano kulipia watoto wangu ada ya shule kuwasaidia ndugu na pesa nyingine naweza malizia malipo ya kiwanja changu na kuanza kujenga.

  Mshindi huyo wa droo ya 57 aliwasisitiza watanzania kuacha woga na kujaribu bahati na SportPesa maana hata yeye wakati anaambiwa acheze hakuamini kama angeshinda lakini sasa tayari amefanikiwa kushinda na anamiliki bajaj yake aliyoshinda na SportPesa.

  Kwa upande wa SportPesa Meneja Uhusiano Bi Sabrina Msuya alisema prom0sheni yetu ni kwa mitandao yote ya simu na mteja anaweza kushiriki kupitia simu yake ya mkononi kwa kupiga * 150*87# na kuweka pesa kwenye akaunti yake ya SportPesa kupitia AirtelMoney, MPESA, TigoPesa na Halopesa kisha kuweka ubashiri wake.

  “Mbali na kushinda fedha za ubashiri wake ambazo huingizwa papo hapo kwenye akaunti ya mteja mara baada ya kubashiri kwa usahihi michezo aliyoweka, mteja anaweza kujishindia zawadi mbalimbali kama Bajaji, Simu janja(Smartphone), Jersey za Simba na Yanga pamoja na safari ya kwenda Hispania na Uingereza kushuhudia mitanange ya ligi zinazoendelea nchini humo”

  “Michezo anayoweza kushiriki ni pamoja na Jackpot (yenye mechi 13 ambayo kwa sasa ni zaidi ya shilingi milioni 394 yaani karibia milioni 400, hii ni Jackpotyenye kiasi kikubwa kuliko Jackpot zingine zozote nchini, pia mteja akibashiri kwa usahihi mechi kuanzia 10 hadi 12 anajipatia bonus kama zawadi”

  “Napenda kuwahamasisha watanzania wote kwamba washiriki na waendelee kubashiri na SportPesa kwani kuna mambo mbalimbali yanaendelea na wategemee mazuri zaidi kutoka kwetu”
   mshindi wa droo ya 57 Emmanuel Nzuki aliyekabidhiwa bajaj baada ya ushindi.

  0 0


  Baadhi ya Wachungaji na viongozi wa Makanisa ya Ameki nchini waliohudhuria ibada hiyo ya shukrani wakiwa na Baba askofu pamoja na makamu wa askofu katika ibada ya pamoja
  Makamu wa Askofu wa kanisa la Ameki William Msafiri Ayo akizungumza katika Ibada hiyo ya Shukrani akiwashukuru kwa uvumilivu wao wa msukosuko wa kanisa ndani ya miaka 13
  Makamu Askofu wa Kanisa la AMEKI William Msafiri Ayo Tanzania Baltazari Kaaya akishikana mkono Baba Askofu Baltazari Kaaya mbeke ya waumini wao kama ishara ya Amani ya kumaluza tofauti zao zilizodumu kwa takribani miaka 13
  Askofu wa Kanisa la AMEKI Tanzania Baltazari Kaaya akishikana mkono na makamu wa askofu William Msafiri Ayo mbele ya waumini wao kama ishara ya Amani ya kumaluza tofauti zao zilizodumu kwa takribani miaka 13
  Katibu mkuu mstaafu wa kanisa hilo Mchungaji Mshana akimshika mkono Baba Askofu Baltazari Kaaya kama ishara ya kutangaza Amani mara baada ya kumaliza tofauti zilizokuwepo ndani ya miaka 13
  Baadhi ya mchungaji kutoka kanisa la Ameki akidhikana mkkono na Baba Askofu Baltazari Kaaya akimpongeza kwa hatua hiyo ya maridhiano.
  Msaiduzi wa Askofu katika kanisa hilo la AMEKI akizungumza na waumini katika ibada hiyo ya kumshukuru Mungu kumalizika kwa mgogoro uliodumu kwa takribani miaka 13
  Baadhi ya waumini katika kanisa la Ameki waliohuduria katika Ibada ya shukrani baada ya mgogoto huo uliodumu zaidi ya miaka 13 kumalizika
  Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro akizungumza katika la AMEKI mara baada ya pande mbili hizo kuondoa tofauti zao na kuamua kuwa wamoja na uongozi mmoja
  Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro Akizungumza katika ibada hiyo ya shukrani katika kanisa la AMEKI ambapo yeye alikuwa chachu ya kusuluhisha pande zote mbili zikizokuwa na mgogoro ndani ya miaka 13
  Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akiteta jambambo na msaidizi wa Askofu katika kanisa la AMEKI katika ibada ya shukrani.
  Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akimpongeza Baba Askofu wa kanisa la Ameki lililopo Wilayani hapo kata ya Usariva mara baada ya kuondoa tofauri zao na kutangaza Amani
  Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akimpongeza Makamu wa Askofu wa kanisa la Ameki lililopo Wilayani hapo kata ya Usariva mara baada ya kuondoa tofauri zao na kutangaza Amani
  Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akimpongeza Katibu mkuu mstaafu wa kanisa la Ameki lililopo Wilayani hapo kata ya Usariva mara baada ya kuondoa tofauri zao na kutangaza Amani


  Na. Vero Ignatus, Arusha


  Mgogoro uliodumu kwa takribani miaka 13 wa kanisa la AMEKI wilayani Arumeru kata ya Usariva umemalizika kwa pande mbili kukubaliana kwa kuondoa tofauti zao na kuamua kuwa na kanisa moja na uongozi mmoja

  Akizungumzia mgogoro huo uliodumu kwa miaka 13 mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro amewapongeza viongozi kwa hatua kubwa waliyoifikia kwani kwa miaka yote hali ilikuwa nzito na mgogoro ulidumaza maendeleo ya kanisa ,ustawi wa wananchi,maendeleo ya shughuli za serikali katika wilaya hiyo.

  "Mhe. Baba Askofu, Mhe. Msaidizi wa , Askofu nimesimama hapa kwa niaba ya serikali kuwapongeza kwa hatua kubwa mliyofikia, tumekuwa na changamoto za mgogoro uliodumu kwa miaka 13''alisema Jerry.Jerry amesema kuwa serikali itaendelea kusimama na kanisa la AMEKI kuwaunga mkono katika juhudi za kuwaletea wananchi maendeleo sambamba na ukuaji wa kiroho na maendeleo ya waumini wao

  '' Ndani ya miezi mitatu kama mkuu wa wilaya namshukuru sana Mungu kunifanya kuwa chachu ya kuwapatanisha viongozi hawa wa kanisa na leo wamekuwa wamoja na kanisa moja naamini sasa baraka zaungu zitaonekana''alisema Jerry .Sambamba na hayo amesema kwakuwa mgogoro umeisha,serikali inaanza kazi mara moja ndani ya wiki moja serikali itahakikisha kuwa inatatua changamoto zote ya maeneo yote ambayo yalikuwa ya kanisa

  Nitangazia Arumeru,Arusha,Tanzania Afrika dunia ,Tanzania na Arusha kuwa mogoro uliodumu kwa takribani mika 13 sasa tumeumaliza umemalizika tukiwa wamoja na tukiendelea mbele kwa umoja wetu"alisema Jerry

  Akizungumza juu ya mgogoro huo ulioligawa kanisa hilo Askofu Baltazari Kaaya amesema kuwa wameamua kuwa na maridhiano kwani ulisababisha kukosekana kwa amani na maendeleo yalidorora.Amesema kuwa waliamua kuwaita wawakilishi wawakristo na wachungaji wa pandezote mbili ili kuwajulisha kuwa wameshaungana ndipo baadae wakaamua kwenda kwa mkuu wa wilaya

  Askofu amesema kuwa baada ya maridhiano hayo wamekubaliana wote kwa pamoja ndani ya miaka 4 kuunda katiba ya kanisa hilo."Tumeondoa tofauti zetu na tukaanza kupita sharikani nuongozi wote kwa pamoja tarehe 27.9.2018 tulikwenda usharika wa Ambureni na kuongeza ibada ya pamoja na washirika walifurahi sana kwani mgogoro wetu ulikuwa umewaathiri na wao pia" alisema askofu Baltazari

  Kanisa la Ameki lilianzishwa mwaka 1995 ambapo lilimeguka kutoka Dayosisi ya Kaskazini kanisa la KKKT, mara baada ya kumeguka waliwezakufanya mkutano mkuu wa kwanza wa kumchagua mchungaji Abel Pallangyo(marehemu kwa sasa) kuwa kuwa askofu wa kwanza wa kanisa hilo. Mchungaji Mshana alichahaguliwa kuwa katibu mkuu wa kwanza, ikumbukwe kuwa kanisa hilo halikuwa moja ya vuguvuvu ya vurugu ya Dayosisi ya mlima meru bali ilichangia kuanzishwa kwa kanisa hilo.

  Wakati makanisa mengine yakiwa na historia ya wamishionari kutoka nje ya nchi kanisa hilo linabakia kuwa na historia ya kuazishwa hapa nchini pasipokuwa na ufadhili kutoka wamishionari wa nje.Aidha kanisa hilo lilifanikiwa kufungua makanisa katika mikoa mbalimbali apa nchini ikiwemo Arusha ambapo ndipo makao makuu yalipo Kilimanjaro, Manyara, Kagera, Dar es salaam Tabora, na Manyara

  Viongozi na waumini wa kanisa la Ameki, Wamemshukuru Rais Magufuli kwa kumpeleka mkuu wa wilaya Arumeru Jerry Muro kwani kwa ujio wake wilayani hapo wameshuhudia suluhu imepatikana kwa Amani.Wakati makanisa mengine yakiwa na historia ya wamishionari kutoka nje ya nchi kanisa hilo linabakia kuwa na historia ya kuazishwa hapa nchini pasipokuwa na ufadhili kutoka wamishionari wa nje

  0 0

  Na Chalila Kibuda .

  Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) Kanda ya Mashariki imesema kuwa mawasiliano lazima yafuate sheria kwa wadau wote ili kulinda ustawi wa Taifa.

  Hayo ameyasema Meneja wa Kanda ya Mashariki Mhandisi Lawi Odiero wakati walipotembelea Shule ya Sekondari Morogoro kwa ajili ya utoaji wa elimu ya mawasiliano ,amemesema watumiaji wa mawasiliano wanatakiwa kufuata sheria ili kutumia mawasiliano hayo kwa malengo yaliyowekwa.

  Amesema kutokana na sheria iliyopo kwa mawasiliano yanaweza kumgharimu mtu yeyote kwa kukipa faini au kifungo cha hadi miaka mitatu.
  Odiero amesema ni makosa kutumia laini ya simu ambayo haijasajiliwa pamoja na simu moja kumiliki zaidi ya mtu mmoja.Amesema kuwa simu ya biashara ya fedha inatakiwa kutumika kwa biashara hiyo tu katika kuondoa usumbufu wa mawasiliano mengine.
   
  Mkuu wa Sule ya Sekondari Morogoro Boniface Gonjo amesema elimu iliyotolewa na TCRA wameielewa na kuahidi kuwa mabalozi katika mawasiliano.
  Amesema TCRA iendelee kuwafikia watu wote kwani watu wengi wanatumia mawasiliano lakini hawajui madhara ya matumizi mabaya ya mawasiliano  Mkuu wa Shule wa Sekondari ya Morogoro Boniface Gonjo akizungumza kuhusiana na Ujio wa TCRA katika Shule hiyo
  Afisa Elimu Mkoa Rhoda Mursuli akizungumza umuhimu wa matumizi bora ya mawasiliano kwa ustawi wa taifa
  Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Morogoro wakisikiliza mada kwa wataalam wa TCRA namna bora ya matumizi ya mawasiliano.

  0 0  Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

  MEYA  wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Shirika la kutetea haki na ustawi wa watu wenye ualbino la Under The Same Sun, tawi la Tanzania.

  Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika jana shirika hilo lililowakilishwa na Ofisa Uraghibishaji Kondo Seif, limeomba fursa ya kukutana na  madiwani wa Mkoa wa Dar es salaam wanapokuwa kwenye vikao vya kazi, ili kuwaeleza masuala mbalimbali yanayohusu dhana nzima ya ualbino na changamoto zake.

  Taarifa ya Ofisa Habari wa Ofisi ya Meya Christina wa Jiji la Dar es Salaam Christina amesema Mwagala Meya wa jiji
  Meya Mwita aliridhia ombi la shirika la Under The Same Sun na kuahidi ofisi yake kusaidia kwenye jitihada za kumaliza madhila wanayoyapata watu wenye ualbino.

  Itakumbukwa katika miaka ya 2006, Tanzania iligubikwa na habari za matukio ya mauaji na ukataji wa viungo vya watu wenye ualbino, na kutumia viungo vya miili ya watu hao  kwa imani za kishirikina, kwa kuamini kuwa watafanikiwa kwenye shughuli zao za kiuchumi.


  Tangu wakati huo, shirika la Under The Same Sun limekuwa likizunguka maeneo mbalimbali nchini kutoa elimu kuhusu ualbino, jinsi unavyopatikana sambamba na kutoa ufadhili wa kielimu kwa watu wenye ualbino, ambapo zaidi ya wanafunzi 400 nchi nzima wanafaika kwa kulipiwa gharama za elimu kuanzia ngazi ya elimu ya msingi hadi vyuo vikuu.
   Afisa uraghibishaji wa shirika la Under the Same Sun, Kondo Seifu akimuonesha  Mstahiki Meya Isaya Mwita picha mbalimbali zilizomo kwenye kitabu hicho  jumbe mbalimbali zinazo elezea walemavu hao
   Afisa uraghibishaji wa shirika la Under the Same Sun, Kondo Seifu akizungumza jambo na Mstahiki Meya Isaya Mwita jumbe mbalimbali zinazo elezea walemavu hao
   Afisa uraghibishaji wa shirika la Under the Same Sun, Kondo Seifu akimkabidhi Mstahiki Meya Isaya Mwita jumbe mbalimbali zinazo elezea walemavu hao

  0 0


  Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Kinywa, Mataya na Uso wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Doraha Kiwale (kulia), Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Kinywa, Mataya na Uso, Dkt. Daud Shaban wa Muhimbili (katikati) na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Kinywa, Mataya na Uso, Dkt. Baraka Kileo wa Muhimbili wakifanya upasuaji wa kuondoa uvimbe chini ya shingo ya mgonjwa ambao umeziba mshipa mkubwa wa kupeleka damu kwenye ubongo. Wa pili kutoka kulia ni Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Kinywa, mataya, na Uso, Prof. Thaer Raifallah kutoka Hospitali ya Kansas City na Chuo Kikuu cha Missouri huko Marekani akishiriki kwenye upasuaji huo.
  Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Kinywa, Mataya na Uso wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Daud Shaban akizungumza na mwandishi wa habari kuhusu upasuaji wa kinywa, mataya na uso ambao unafanywa na wataalam wa Muhimbili kwa kushirikiana na wataalam kutoka Hospitali ya Kansas City na Chuo Kikuu cha Missouri nchini Marekani.
  Wataalam wa wakiendelea na upasuaji katika hospitali hiyo.

  Wataalam wabobezi wa upasuaji wa kinywa mataya na uso (Oral & maxillofacial surgeons) wa Hospitali ya Taifa 

  Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na wenzao wa Marekani kwa mara ya kwanza kupitia Hospitali ya umma nchini, wamefanya upasuaji wa ubingwa wa kuunganisha mifupa ya fuvu kwa mgonjwa aliyepata ajali na sura yake kuharibika.

  Upasuaji huo ambao ulifanywa na wataalam wa Muhimbili kwa kushirikiana na wenzao kutoka Hospitali ya Kansas City na Chuo Kikuu cha Missouri nchini Marekani, ulifanikiwa kurejesha sura ya mgonjwa huyo katika hali yake ya kawaida.

  Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Kinywa, Mataya na Uso, Dkt. Daud Shaban amesema upasuaji mwingine uliofanyika unahusisha wagonjwa waliokuwa na uvimbe mkubwa sehemu ya taya na uso. Amesema pia wataalam wenzake walifanya upasuaji wa kutengeneza taya jipya kwa mgonjwa aliyepata ajali na taya lake kuharibika ambapo wamechukua kipande cha mfupa kutoka kwenye sehemu ya kiuno chake na kukiunganisha na taya ili kulikamilisha upasuaji huo.

  Katika hatua nyingine, watalaam hao wamefanikiwa kuondoa uvimbe chini ya shingo ambao ulikuwa umeziba mshipa mkubwa wa damu wa kupeleka damu kwenye ubongo. “Uvimbe huo ulisababisha mgonjwa kuumwa kichwa kwa muda mrefu na kumsababishia dalili za kiharusi, kuzimia mara kwa mara na kupoteza kumbukumbu. Hakuna shaka kwani baada ya uvimbe kuondolewa, sasa mgonjwa ataendelea na maisha yake ya kawaida vizuri,” amesema Dkt Shaban.

  Amesema ujio wa watalaam hao umeowaongezea ujuzi wa kuendelea kufanya upasuaji mkubwa kwa wagonjwa wenye matatizo mbalimbali kutoka kila pembe ya Tanzania. “Pia, wameleta msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya Tshs. 250 milioni ambavyo vitaendelea kutumiwa na watalaam wa MNH kutoa huduma kwa wagonjwa wenye matatizo hayo,” amesema daktari huyo.

  Vifaa hivyo ni pamoja na mashine za kuchimbia mifupa kwenye mashimo ya taya na vyuma vya kufungia taya na mifupa iliyovunjika, nyuzi za kushonea wagonjwa baada ya upasuaji pamoja na dawa mbalimbali. Upasuaji wa wagonjwa hawa ungegharimu kiasi cha Tshs. 420 milioni kama wangeenda kutibiwa nje ya nchi.

  0 0


  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akizungumza na Watumishi wakati alipowatembelea leo katika Chuo cha Misitu cha Olmotonyi jijini Arusha ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu aliposhika nyadhifa hiyo.( Picha na Lusungu Helela-MNRT)
  Makamu Mkuu wa Chuo cha Misitu cha Olmotonnyi Bw.Steve Kigwere akisoma taarifa mbele ya Naibu Waziri, Mhe. Kanyasu wakati alipotembelea leo Chuo hicho kilichopo jijini Arusha kwa ajili ya kuzungumza na kuwasikiliza watumishi juu ya changamoto mbalimbali zinazowakabili ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi.( Picha na Lusungu Helela-MNRT)
  Mkufunzi wa Chuo cha Misitu Olmotony,Charles Giliba akizungumza mbele ya Naibu Waziri Mhe, Kanyasu, wakati alipotembelea jana Chuo hicho kilichopo jijini Arusha kwa ajili ya kuzungumza na kuwasikiliza watumishi juu ya changamoto mbalimbali zinazowakabili ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi .( Picha na Lusungu Helela-MNRT)

  …………………………………………………………………. 

  Watumishi wa Chuo cha Misitu cha Olomotonyi wamemuomba Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ashughulikie changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo kufanya kazi kwa muda mrefu bila kupandishwa vyeo.

  Pia, watumishi hao wamesema wamekuwa hawapandishwi vyeo kwa muda mrefu jambo ambalo limekuwa likishusha ari ya kufanya kazi kwa bidii.
  Wameyasema hayo leo mbele ya Naibu Waziri Mhe. Kanyasu wakati alipokuwa akisikiliza changamoto za watumishi wa Chuo hicho jijini Arusha ikiwa ni mara yake ya kwanza kukutana na watumishi hao tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo .

  Akizungumza kwa niaba ya Watumishi wenzake, Mkufunzi wa Chuo hicho, Philipina Shao amesema kwa muda wa miaka 12 hajapandishwa cheo na kwa sasa anakaribia kustaafu. Mbali na malalamiko hayo, Watumishi hao wamemueleza Naibu Waziri huyo kuwa Chuo hicho kimekuwa kama gereza kwa vile baadhi ya watumishi ambao wameonekana kufanya vibaya maeneo mengine huhamishiwa katika Chuo hicho kama adhabu. 

  Wakizungumzia kuhusu watumishi hao ambao wamekuwa wakihamishiwa katika Chuo hicho kuwa wengi wao huwa wamebakiza miaka michache kustaafu, hivyo wanakuwa hawana mchango wowote kwa Chuo. 

  Aidha, Mkufunzi wa Cho hicho,Dkt.Lupala Zacharia amesema kumekuwa na ushirikishwaji hafifu kati ya Chuo na Idara ya Misitu na Nyuki hali inayopelekea kujiona kuwa wao sio sehemu ya Wizara ya Maliasili na Utalii. Ameongeza kuwa kumekuwa na mambo mengi ambayo yamekuwa yakifanywa na Idara pasipo kushirikishwa Naye Mkufunzi Charles Giliba amesema Chuo hicho kimetengwa kwa muda mrefu hata pale inapotea vikosi kazi vinapoundwa Wizarani vya kufanya kazi fulani wamekuwa hawapati nafasi ya kushirikishwa. 

  “Hatutaki tubebwe, tuna sifa stahiki na tunajisikia tunadhulumiwa haki yetu kwa vile hatutumiwi ipasavyo” amesema Giliba Katika hatua nyingine, Wamemueleza Naibu Waziri huyo kuwa hata teuzi zinapotokea za kushika nafasi za juu katika masuala ya misitu, Chuo hicho kimekuwa hakipati nafasi ilhali kina wataalamu wabobezi na wenye uwezo hali ya juu. 

  Aidha, Watumishi hao wamesema licha ya kuwa Chuo hicho kipo kwenye mfumo wa NACTE lakini hata hivyo Wakufunzi wamekuwa wakilipwa mshahara kama mafisa misitu kufuatia kukosekana kwa muundo wa utumishi. Hivyo wamemuomba Naibu Wazi huyo ashughulikie muundo huo ili waanze kulipwa stahili zao kama vyuo vingine ambavyo vipo katika mfumo huo
  Kwa upande wake,Naibu Waziri Mhe.Kanyasu wakati alipokuwa akijibu kero hizo amewahakikishia Watumishi hao kuwa atazishughulikia baadhi ya changamoto hizo haraka iwezekanavyo. 

  Pia, Amesema Chuo hicho hakijatengwa ila kumekuwa na mazoea ya viongozi walio wengi kuteua majina ya watalaamu kutoka vyuo vikubwa wakiamini huko ndiko kuna wataalamu. Katika hatua nyingine, Naibu Waziri huyo ameishauri Menejimenti ya Chuo hicho isikae kimya badala yake isikume mambo hasa pale inapodhani yakifanyika yataweza kuisaidia Wizara pamoja na taifa kwa ujumla.

  0 0

  Ni kupitia zoezi la ‘Treasure Hunt’
  Luninga hiyo inauzwa shilingi 570,000 mtandaoni lakini mteja auziwa kwa shilingi 5,700!
  Ijumaa hii bodaboda yenye thamani ya shilingi 1,850,000/- itauzwa kwa shilingi 18,500 tu kwa mteja atakayeipata. 

   Jumia imetangaza kutoa pikipiki aina ya Skymark yenye thamani ya shilingi 1,850,000 kupitia zoezi la ‘Treasure Hunt’ siku ya Ijumaa ya kesho. Zoezi hilo litafanyika kupitia App ya Jumia kwenye simu za mkononi pekee ili kutoa fursa kwa kila mtu kushiriki muda na mahali popote walipo. Mshindi mwenye bahati atakayefanikiwa kuipata pikipiki hiyo atauziwa kwa bei ya punguzo la asilimia 99 ambayo ni sawa ni shilingi 18,500 tu!

  Jumia inaendesha kampeni yake kubwa kabisa ya mauzo ya mwaka inayokwenda kwa jina la Black Friday. Kampeni hii ilizinduliwa Novemba 16 na itafikia ukomo mnamo Desemba 7. Tofauti na miaka mingine ambayo Jumia hufanya Black Friday kwa siku moja tu ya Ijumaa ya Novemba 23, mwaka huu wateja watafaidi ofa za Black Friday kwa Ijumaa nne mfululizo. Lengo kubwa la kampeni hii ni kuwarahisishia wateja na watanzania kwa ujumla kufanya manunuzi yao hususani kipindi cha msimu wa sikukuu za Krisimasi na mwaka mpya ambazo zipo njiani wiki chache zijazo.

  Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja Uhusiano wa Umma wa Jumia Tanzania, Bw. Kijanga Geofrey amefafanua kuwa, “zoezi la kuficha bidhaa mtandaoni ili wateja kuzisaka na kujishindia au ‘Treasure Hunt’, ni mojawapo ya vitu vichache vinavyoendelea katika kampeni hii ya Black Friday. Miongoni mwa ofa zinazopatikana ni pamoja na punguzo la bei mpaka asilimia 70 na mauzo ya bidhaa maalum kwa bei nafuu zaidi ndani ya muda mfupi ndani ya siku au ‘Flash Sales.”

  “Hii ni fursa kwa watanzania kuanza na kujizoesha kutumia mfumo wa manunuzi kwa njia ya mtandaoni. Kuna faida nyingi kufanya manunuzi mtandaoni kwa sababu unaokoa muda na gharama za kwenda dukani, unaweza kuperuzi bidhaa mbalimbali kutoka kwa wauzaji tofauti kwa wakati mmoja, muda wowote na mahali popote ulipo. Lakini kikubwa zaidi ni kwamba baada ya kufanya manunuzi utaletewa bidhaa zako mpaka hapo ulipo,” aliongezea Meneja Uhusiano wa Umma kutoka Jumia Tanzania.

  “Leo tumekabidhi luninga ya kisasa kabisa ambapo mteja ameinunua kwa shilingi 5,700 badala ya bei ya shilingi 570,000 inayopatikana kwenye mtandao wetu. Tunatoa fursa nyingine kwa wale ambao hawakufanikiwa kushinda au kushiriki, kujishindia pikipiki aina ya Skymark ambayo itafichwa siku ya kesho ya Ijumaa ya Novemba 23 kuanzia saa 9 mchana,” alisema na kumalizia Bw. Geofrey, “Pikipiki hii ambayo inauzwa shilingi 1,850,000 kwenye mtandao wa Jumia itakabidhiwa kwa mteja atakayetakiwa kulipa shilingi 18,500 tu! Ili kuhakikisha kila mtanzania anashiriki zoezi hili, ‘Treasure Hunt’ itafanyika kupitia App yetu Jumia inayopatikana kwenye simu zote za mkononi, iwe ni Google Play au App Store. Ningependa kuwatakia kila la kheri katika zoezi la kesho, huwezi kujua namna zawadi hii itakavyobaidilisha maisha yako. Hakikisha unashiriki.”
  Meneja Uhusiano wa Umma wa Jumia Tanzania, Bw. Kijanga Geofrey akizungumza na Wanahabari leo jijini Dar kuhusu ufafanusi  wa  “zoezi la kuficha bidhaa mtandaoni ili wateja kuzisaka na kujishindia au ‘Treasure Hunt’,alisema na kuongeza kuwa ni mojawapo ya vitu vichache vinavyoendelea katika kampeni hii ya Black Friday. Kijanga amebainisha kuwa Miongoni mwa ofa zinazopatikana ni pamoja na punguzo la bei mpaka asilimia 70 na mauzo ya bidhaa maalum kwa bei nafuu zaidi ndani ya muda mfupi ndani ya siku au ‘Flash Sales.”


  0 0

  Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu yamezinduliwa rasmi tarehe 14 Novemba 2018 huku Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) ikipewa jukumu la kuratibu mchakato wa mashindano katika makundi mawili ambayo ni Wabunifu wa Ufundi Stadi na Wabunifu wa kutoka Sekta Isiyo Rasmi, hivyo kupata majina matano ya kila kundi kuingia kwenye fainali.

  Akizindua mashindano hayo sambamba na Mwongozo wa Kuendeleza Ugunduzi, Ubunifu na Maarifa Asilia, kwenye Ukumbi wa Kambarage, Nyerere square jijini Dodoma, Waziri wa sayansi na teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako alisema mashindano hayo yataongozwa na kaulimbiu ya “Kukuza Ujuzi na Ubunifu kwa Uchumi wa Viwanda,” na yatahusisha makundi mbalimbali ya wabunifu wa kisayansi, teknolojia katika maeneo na nyanja mbalimbali nchini kote, ambapo kilele chake kitakuwa Januari 2019.

  Alisema ili nchi yetu iweze kunufaika na matokeo ya ubunifu, uvumbuzi na maarifa asilia, kuna umuhimu wa kuwahamasisha wagunduzi, wabunifu na wamiliki wa maarifa asilia.

  “Kwa hiyo, mashindano haya yatasaidia kuibua vipaji na kuhamasisha uendelezaji wa teknolojia na ubunifu utakaoweza kuchangia kwa kiasi kikubwa katika maendeleo endelevu ya viwanda, kuongeza tija ya uzalishaji wa malighafi, kuongeza thamani ya bidhaa zinazozalishwa nchini pamoja na kuboresha shughuli nyingine za kiuchumi. Kutokana na kutambua umuhimu wa sayansi, teknolojia na ubunifu, Wizara yangu ina mpango wa kufanya mashindano haya yafanyike kila mwaka ili uibuaji wa vipaji vya namna hii uwe endelevu,  ” alisema.

  Aliongeza kuwa Mwongozo wa Kuendeleza Ugunduzi, Ubunifu na Maarifa Asilia utakuwa ni nyenzo ya kuongeza ufanisi wa taasisi zinazoshughulikia masuala ya ugunduzi, ubunifu na umiliki wa maarifa asilia.

  Akifafanua juu ya umuhimu wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kwa maendeleo na ustawi wa taifa Profesa Ndalichako alisema Sayansi, Teknolojia na Ubunifu zimeleta mapinduzi makubwa katika sekta mbalimbali kama vile habari, biashara, viwanda na huduma mbalimbali za kijamii huku akitoa mfano wa mabadiliko katika huduma za kifedha yaliyosababishwa na ubunifu wa matumizi ya teknolojia ya simu za kiganjani.

  Alisema mchakato wa mashindano hayo utaratibiwa kwa ushirikiano wa Kurugenzi ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia; Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH); Taasisi ya Teknolojia (DIT); Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) na Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

  Mashindano hayo yatahusisha jumla ya makundi sita ambayo ni Wabunifu kutoka Shule za sekondari wakiratibiwa na TAMISEMI; Wabunifu wa Ufundi Stadi na Wabunifu wa Sekta Isiyo Rasmi wakiratibiwa na VETA; Wabunifu wa Ufundi wa Kati wakiratibiwa na DIT; na Wabunifu wa Vyuo Vikuu na Wabunifu wa Taasisi za Utafiti wakiratibiwa na COSTECH.

  Awali kabla ya kumkaribisha Waziri, Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Daktari Leonard Akwilapo, alitaja malengo mahususi ya mashindano hayo kuwa ni pamoja na Kuibua na kutambua ubunifu mahiri nchini katika eneo la sayansi na teknolojia; Kukuza hamasa ya ubunifu katika nyanja ya sayansi na teknolojia; Kuhamasisha matumizi ya sayansi, teknolojia, ubunifu na hisabati katika shughuli za kiuchumi na kijamii; Kuchochea ugunduzi na ubunifu wa kisayansi na teknolojia utakaotegemeza maendeleo ya uchumi wa viwanda; na Kushirikisha wadau ili kupata mawazo ya jinsi sayansi, teknolojia na ubunifu yanavyoweza kuchangia katika kujenga uchumi wa viwanda.

  Alisema wabunifu bora watano kutoka katika kila kundi watachaguliwa katika mchujo wa awali ili kuingia katika mashindano ya fainali yatakayofanyika jijini Dodoma ili kupata washindi watatu wa fainali.

  0 0  0 0  Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Baraza la Kilimo Tanzania Dkt Sinare Yusuph Sinare akisisitiza jambo wakati wa kikao cha siku mbili cha Bodi ya wakurugenzi wa Baraza la Kilimo, kulia kwake ni Makamo Mwenyekiti Bi Jacqueline Mkindi .
  Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Kilimo Tanzania Bi Janeth Bitegeko akiwa katika moja ya vikao vya Bodi ya wakurugenzi ya Baraza la Kilimo Tanzania. 


  Waziri wa kilimo Nchini Mh Japhet Hasunga anatarajia kufungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Kisera wa Baraza la Kilimo Tanzania unaotarajiwa kufanyika Nov 26 na 27 mwaka huu jijini Dra es salaam wenye lengo kukusanya maoni ya yahusuyo Sera za Kilimo ili kuona namna zinavyoweza kufanyiwa marekebisho.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Kilimo Tanzania Bi Janeth Bitegeko imesema mkutano huo wenye kauli mbiu ya Kilimo na Maendeleo ya Viwanda Tanzania unatarajiwa kuhudhuliwa na wadau wa sekta ya kilimo zaidi ya 100 kutoka ndani na nje ya nchi.

  Bi Janeth alitaja mada zitakazowalishwa katika mkutano huo kuwa ni apmoja na mada kuu ya Kilimo na Maendeleo ya Viwanda Tanzania, Fursa ya Sekta Binafsi Katika Utekelezaji wa ASDP II, Nafasi ya Vijana na Utekelezaji wa ASDP II ikiwa ni pamoja na Kuimarisha Ushirika kwa Faida ya Wazalishaji.

  “ Kwetu Baraza la Kilimo Mkutano huu ni muhimu kwa sababu ndiko tunapopata changamoto za kisera zinazowakabili wadau wa kilimo nchini na kwenda kukaa meza moja na serikali na kuzifanyia kazi, ndio maana utaona tumewaalika wadau wote wa kilimo nchini,

  “ Na tumegusa wadau wote wanaojihusisha na mboga mboga, maziwa, mifugo kwa ujumla, kilimo , Uvuvi na yeyote anayeguswa na sekta nzima ya kilimo tunaamini kwa kuwaweka pamoja wote hawa tutatoka na maazimio mazuri yatakayolenga kuendelea kuiboresha sekta ya kilimo nchini” alisema Bi Janeth Bitegeko Mkurugenzi Mtendaji Baraza la Kilimo Tanzania.

  Katika mkutano huo na vyombo vya habari ofisini kwake aliongeza kuwa “ Mambo yote yatakayojadiliwa katika mkutano huu ndio kipaumbele chetu kwa mwaka ujao 2019, kwasababu tumekuwa tukiyafanyia kazi na kumekuwa na matokeo chanya kwasababu sisi tumekuwa tukifanya kazi na serikali kwa karibu zaidi ndio maana unaona masuala mengi yaliyokuwa changamoto kwa wakulima kama vile tozo serikali imekwisha kuyafanyia kazi”.

  “Katika Mkutano huu pia tutatoa mrejesho wa yote yaliyoibuliwa katika Mkutano wa Mwaka jana 2017, lakini pia tutatoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Baraza la Kilimo kwa mwaka mzima, hii pia itakuwa ni fursa pekee kwa wanachama wa baraza kujua nini kilifanyika kwa mwaka mzima”.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Baraza la Kilimo Tanzania Bw Timothy Mmbaga aliwaeleza wanahabari kuwa maandalizi yote ya Mkutano huo yamekwisha kukamilika na tayari Waziri wa Kilimo Mh Japhet Hasunga amethibitisha kushiriki katika mkutano huo wa Nov 26 nq 27.

  “Baraza la Kilimo limekuwa likifanya kazi na taasisi pia za kimataifa kama .SACAU na EAFF nao pia wamekwisha kuthibitisha kushiriki mkutano huu, kwahiyo ni rai yangu kwa wadau wengine wa kilimo kushiriki mkutano huu muhimu kwa sababu ndio nafasi pekee ya wao kusema sera zipi kwao ni kikwazo na wangependa serikali izifanyie kazi ili kuzidi kuiimarisha sekta ya kilimo nchini ” alisema Bw Mmbaga.

  Aidha ilielezwa kuwa mafanikio makubwa yaliyokwisha kufikiwa na Baarza la Kilimo Tanzania yametokana na mikutano ya kisera ambapo kupitia mikutano hiyo mambo kadha wa kadha yalifikiwa na wadau wa kilimo na baadae serikali kuyafanyia kazi.

  “Unajua sisi kama Baraza la Kilimo tunajifunia kuwa vinara kwa sababu nini sisi tulioshawishi hadi kuanzishwa Banki ya Kilimo Tanzania na mnaona inavyofanya kazi, ni sisi pia tulioshawishi hadi serikali ikaja na Kilimo Kwanza lakini pia ni sisi Baraza la Kilimo tulihakikisha SAGCOTT inaanzishwa,

  “ Kwa hivyo unaweza kuona nguvu ya ushawishi tuliyonayo lakini yote haya yanawezakana kupitia mikutano kama hii ya kisera kwa sasa sisi kama Baraza tunaamini katika ushirikishwaji na ndio maana tumekuwa tukifanikiwa katika masuala mengi yanayohusu sekta yetu ya Kilimo” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Bazaar la Kilimo Bi Janeth Bitegeko.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Baraza la Kilimo Tanzania anayemaliza muda wake Dkt Sinare Yusuph Sinare alisema kwa muda wote ambao amehudumu katika nafasi ya uenyekiti wa Bodi, mikutano ya kisera imekuwa na manufaa makubwa na wamefanikiwa kuweza kufanyia kazi changamoto zote zilizokuwa zikiibuliwa na wadau wa kilimo

  “ Kimsingi naondoka kwenye nafasi ya uenyekiti nikiwa sina shaka kabisa na uwezo wa Baraza la Kilimo Tanzania katika kushughulikia changamoto hasa za kisera zinazoikabili sekta ya kilimo kwa hivyo naamini hata yatakayojili katika mkutano wetu wa Nov 26 na 27 pia yatafanyiwa kazi kwa umahili uleule” alisema Dkt Sinare anayetarajiwa kumaliza muda wake katika mkutano mkuu wa Baraza la kilimo utakaofanyika Nov 28 mwaka huu..

  Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Baraza la Kilimo Tanzania miongoni mwa wadau wa kilimo watakaoshiriki mkutano huo kutoka ndani na nje ya nchi ni pamoja na Shirikisho la Vyama vya Wakulima vya Afrika ya Mashariki, Muungano wa Vyama vya Wakulima Kusini mwa Afrika ikiwa ni pamoja na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania.

  0 0


  Mkuu wa Mkoa wa Arusha akiangalia moja ya Visima ambavyo ni chanzo cha Maji yanayotarajiwa kuhudumia Jiji la Arusha.
  Mkuu wa Mkoa Mrisho Gambo (wa kwanza kushoto) akipokea maelezo ya mapito ya mtandao wa maji taka.

  Mafundi wa kampuni ya Cheil Engeneering wakiwa katika uchimbaji wa kisima kilichopo wilayani Arumeru
  Miundo mbinu ya mfumo wa maji taka, mabwawa haya yanajengwa katika eneo la Terrat pembezoni mwa Jiji la Arusha. Mabwawa haya yanakadiriwa kuwa na uwezo wa kutibu takribaniita Milioni 22 kwa siku za Maji Taka.  Na. Vero Ignatus, Arusha


  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ameanza ziara yake ya siku tatu katika wilaya za Arusha, Arumeru na Longido kukagua maendeleo ya Miradi Mikubwa ya Maji inayotekelezwa katika wilaya hizo.

  Akiwa katika halmashauri ya Jiji la Arusha Gambo ametembelea mradi mkubwa wa Maji unaotekelezwa Jijini humo pamoja na baadhi ya kata za wilaya ya Arumeru.Gambo ameitaka Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafishaji Mazingira Jiji la Arusha AUWSA kuweka kipaumbele katika utunzaji wa vyanzo vya Maji vilivyopo katika mlima Meru ili kuhakikisha miradi hii inayotumia fedha nyingi inakua endelevu.

  “Nimewahi kusikia wataalam wa Maji wakisema Vita ya Tatu ya dunia itahusisha kugombea maji, ninaomba sisi tuanze kujihami kwa kutunza vyanzo vyetu vya maji''alisema Gambo

  Ameotaka bodi ya AUWSA kuandika andiko la mradi ambalo watalipigia debe katika Ofisi ya Makamu wa Rais inayoshughulikia Mazingira ili kuweza kupata ufadhili wa kampeni hiyo ya utunzaji wa Vyanzo vya Maji. "Itakua haina maana kutumia kiasi kikubwa hivi cha fedha ikiwa baada ya miaka michache ijayo vyanzo vyote vitakauka” alisema Gambo"

  Naye Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (AUWSA) Mhandisi Ruth Koya alisema mradi huo utakamilika Juni mwaka 2020 na wanatarajia Arusha itanufaika na mradi huo kwa kuwa ukosefu wa maji utakua historia.

  "Kwa kuanza tayari wakandarasi wameanza kusambaza mtandao wa maji safi na taka kwa kuweka mabomba ya kisasa yanayoendana na mahitaji ya sasa, lengo ni mazingira yawe safi na wananchi wapate huduma za maji safi na taka kufikia asilimia 100 tofauti na hali ilivyo sasa ambapo ni asilimia 44 tu ya wananchi wanapata huduma hiyo,"alisema

  Amesema uzalishaji wa maji utaongezeka toka wastani wa lita Milioni 40 hadi lita Milioni 200 kwa siku na kushusha upotevu wa maji toka asilimia 40 za sasa hadi kufikia wastani wa asilimia 25.Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya AUWSA, Dk.Richard Masika ameipongeza serikali ya awamu ya tano kwa kuweza kutoa fedha nyingi katika mradi huu mkubwa, pia ametoa rai kwa wananchi wa Arusha kuitunza miundo mbinu inayopita katika maeneo yao kwa ajili ya manufaa ya leo na baadae.

  Mradi huu unatekelezwa kwa fedha za mkopo wa riba nafuu kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) wa jumla ya shilingi zipatazo bilioni 520 (233.9 Mil. USD).Gambo anaendelea na ziara yake katika wilaya ya Longido ambapo anatarajiwa kutembelea mradi wa Maji wa Mto Simba unaotarajiwa kumaliza kero ya Maji wilayani humo

  0 0

  Na. Vero Ignatus Arusha

  Siku chache baada ya Benki kuu ya Tanzania kutoa ufafanuzi Juu ya Oparesheni ya Ukaguzi wa Maduka ya kubadilishia Fedha za Kigeni Jijini Arusha ,Wizara ya Mali asili na Utalii imejitokeza na kusema Zoezi hilo halijaathiri shughuli za Kitalii

  Naibu waziri wa maliasili na Utalii Constatine Kanyasu ameyasema hayo wakati lipotembelea taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo kwenye mkutano wake na wafanyakazi wa shirika la hifadhi za taifa(TANAPA) jijini Arusha na kusema watalii wanaendelea kupata huduma kwani zoezi hilo ni la kawaida na limelenga maslahi ya nchi.

  Mara baada ya Mazungumzo hayo Naibu Waziri akiwa nje ya Ukumbi wa Mamlaka hiyo , amezungumza na Wanahabari kisha kugusia suala la oparesheni iliyofanywa na Benki Kuu hivi karibu Jijini hapa.Ameeleza kuwa zoezi hilo lililovishirikisha vyombo vya dola na halijaathiri uchumi katika sekta ya fedha za kigeni hasa kwa upande wa utalii kwa kuwa ni zoezi hilo la mara moja kuwahusisha wanajeshi ambao wanawajibu wa kulinda rasilimali za nchi yao.

  '' Wanajeshi hawawezi kuathiri uchumi wa nchi hasa sekta ya utalii kwakuwa wanawajibu wa kulinda rasilimali zetu‘’alisema Kanyasu .Akiongelea suala la migogoro ya Ardhi na mipaka kwa baadhi ya mipaka amesema wizara yake imejipanga kukomesha changamoto hiyo ambayo imekuwa ikitumia fedha nyingi bila kupatiwa ufumbuzi.

  Aidha amesema migogoro baina ya Hifadhi na Wananchi,Naibu waziri anasema hakuna mtu ama taasisi inayonufaidika na Migogro hiyo na imekuwa ikichochewa na makundi machache na tayari serikali imekwisha anza kuchukua hatua.Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Tanapa Jumla ya Vijiji mia tatu tisini na mbili vitanufaika na zoezi la upimaji wa matumizi bora ya ardhi lenye lengo la Kupunguza

  Migogoro ambapo tumepanga billion 2.5 kwa miradi midogo midogo kuweza kuweka nguvu kwa wananchi kuondoa misuguano isiyo na lazima ambayo inaathiri kiasi kikubwa shughuli za uhifadhi.


  Naibu Waziri Wizara ya Mali asili na Utalii Constatine Kanyasu

  0 0

  Na Richard Mwaikenda-Dar 

  WANAFUNZI waliomaliza Kidato cha Nne, wametakiwa kuachana na tabia ya kupoteza muda kusubiri kurithi mali za wazazi wao, bali wajitambue kwa kufanya kazi kwa bidii kujiletea maendeleo.

  Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Hope For All , Edger Mwamfupe wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kujitambua wanafunzi waliomaliza Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari ya Makongo Juu, Dar es Salaam hivi karibuni.

  “Kila mmoja ajitambue kivyake,, simama wewe kama wewe, jitambue wewe ni nani, ukijiami kama unaweza na utaweza kweli. Mkome kutegemea kurithi mali za baba zenu,” aliwaaasa Mwamfupe.

  “Msiruhusu ndoto zenu zife, hata kama mtakumbana na mazingira magumu majumbani kwenu, mzishikile msiruhusu ndoto zenu zife, Kawaida wewe ndiyo unaamua kuwa tajiri au masikini , utajiri uko kichwani kwako,” alisisitiza Mwamfupe huku akipigiwa makofi na wanafunzi.

  Mwamfupe, hakusita kujitolea mfano yeye kuhusu maisha yake ya ujana, ambapo aliwaeleza kuwa licha ya utajiri wa babake, lakini yeye aliamua kujitegemea tangu akiwa anasoma na kwamba alipokuwa ana miaka 19 alinunua gari aina ya Toyota Corola (Mayai).Pia, kupitia kipaji chake cha kucheza mpira na ngoma za asili kilifanya kwa mara ya kwanza apande ndege kwenda Romania kuiiwakilisha Taifa katika Tamasha la Ngoma. 

  Pia aliwahi miliki bendi ya Muziki wa dansi.Mkuu wa Kitengo cha Vijana cha Taasisi hiyo, Harrison Edger aliwataka vijana wenzie wanapoingia mitaani ambako kuna mambo mengi mazuri na mabaya , inatakiwa wajiwekee mipango yao ya maendeleo ya muda mfupi na muda mrefu.

  “Mungu alituumba watu wote tukiwa na bongo moja, hakuna mwenye bongo mbili, hivyo hata wewe unaweza, ondoa hofu utashinda. Fanyeni mambo yenu mazuri mapema ili baadaye mkizeeka mje muishi vizuri.”

  Naye Mkuu wa Kitengo cha Wanawake na Watoto wa Taasisi hiyo, Juliana Mushi aliwaasa watoto wa kike kuacha tabia ya kujihusisha na umalaya ili waje kuwa wazazi wazuri wa baadaye. Aliwataka badala ya kujihusisha na mambo hayo mabaya bali wawe wanajishughulisha na mambo ya uzalishaji mali, ikiwemo ujasiriamali.

  Wakati wa mafunzo hayo wanafunzi walipata wasaa wa kila mmoja kuelezea kuwa ndoto yake ya maisha atakuwa nani. Baadhi wanataka kuwa wajasiriamali, madaktari, mawaziri, walimu, wakandarasi, wasanii maarufu, waandishi wa habari na mmoja aitwaye Davis Eugene yeye alitaka awe Rais wa Nchi.

  Taasisi hiyo ina mpango wa kuanzisha Klabu za mafunzo kama hayo katika shule mbalimbali nchini na kwa Dar es Salaam wameanza kuweka klabu katika shule hiyo ya Makongo Juu. Lengo ni kuwataka wanafunzi waliomaliza elimu hiyo kuwa na kazi ya kufanya wanaposubiri matokeo ya kujiunga kidato cha tano na wanaoshindwa kujiunga waendeleze ndoto zao.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Hope For All , Edger Mwamfupe (Kulia), akimsikiliza mmoja wa wanafunzi aliyekuwa akijieleza jinsi atakavyokabiliana na maisha baada ya kumaliza shule..
  Wanafunzi wakisikiliza kwa makini wakati wa mafunzo hayo
  Mkuu wa Kitengo cha Vijana cha Taasisi hiyo, Harrison Edger akiwa tia moyo wanafunzi hao
  aitwaye Davis Eugene ambaye ndoto yake ni kuwa Rais wa Nchi.
  Wanafunzi wakimsikiliza kwa makini Meneja Utawala wa Taasisi hiyo, Fides Uisso alipokuwa akiwaeleza jinsi ya kuwa na uthubutu wa kutimiza ndoto zao
  Wanafunzi wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Kitengo cha Vijana, Harrison  alipokuwa akifundisha jinsi ya kujiandaa kimaisha kwa kuanzisha miradi mbalmbali ya maendeleo.
  Fides Uisso akibadilishana mawazo na wanafunzi kwenye viwanja vya shule hiyo
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Hope For All , Edger Mwamfupe akipata chakula cha mchana wanafunzi wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kujitambua wanafunzi waliomaliza Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari ya Makongo Juu, Dar es Salaam hivi karibuni.

  0 0


  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (kushoto) akisoma nyaraka za matibabu za Bi. Mary Nyange (kulia) anayepatiwa huduma za matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini KCMC.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (kushoto) akihojiana na Bw. Longini Mtalo, Mteknolojia kutoka kituo cha utengenezaji wa viungo bandia katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini KCMC huku akiwa ameshika sampuli ya kiungo bandia kilichotengenezwa na kituo hicho.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akikagua benki ya damu zilizopo katika jokofu Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini ya KCMC.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akionyesha mafuta maalum kwa ajili ya kuwakinga wenye ulemavu wa ngozi dhidi ya miale ya jua yanayotengenezwa na kitengo cha Kilimanjaro Sunscreen Production kilichopo Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini ya KCMC.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (kushoto) akihojiana na Bw. Prosper Kaaya, Mteknolojia kutoka kituo cha utengenezaji wa viungo bandia katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini KCMC huku akiwa ameshika kiungo bandia kilichotengenezwa na kituo hicho.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (aliyesimama) akisema jambo wakati wa kikao na watumishi wa Hos.pitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini KCMC (hawapo pichani) aliye upande kulia ni Mganga Mkuu Mkoa wa Kilimanjaro Dkt. Best Magoma upande wa kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskasini KCMC Dkt. Gileard Masenga
  Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini KCMC wakisiliza jambo wakati wa kikao kazi na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (hayupo pichani) aliyetembelea hospitali hiyo Novemba 22, 2018.

  ……………………………..

  Sekta ya afya inakua kwa kasi huku huduma muhimu za afya kwa sasa zikiwa zinapatikana hapa hapa nchini”

  Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile alipokua akizungumza na watumishi wa Hospitali ya rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC) iliyopo katika Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro jana Novemba 22, 2018.

  Dkt. Ndugulile amesema kuwa Sekta ya Afya imepewa kipaumbele cha hali ya juu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli katika kipindi cha miaka mitatu mageuzi makubwa ndani ya sekta ya afya yameanza kuonekana huku huduma za matibabu ya kibingwa yakiwa zikipatikana hapa hapa nchini.

  “Tunasimama hapa kifua mbele tukiona mabadiliko katika hali ya upatikanaji wa dawa kuimarika zaidi, bajeti ya dawa imeongezeka toka Shilingi Bilioni 30 mpaka Shilingi Bilioni 270 yaani mara tisa zaidi ndani ya miaka mitatu” alisema Mhe.Naibu Waziri na kuendelea “Tumeboresha vituo vya afya takribani 300, huku Mkoa wa Kilimanjaro ukiwa na Vituo 8 vilivyoboreshwa vilivyogharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 3.5 na kwa mwaka huu 2018 Serikali imeanza kujenga Hospitali za Wilaya 67 nchini”

  Aidha, Dkt. Ndugulile alisema kuwa Serikali imetenga Shilingi Bilioni 30 kwa ajili ya Hospitali mpya za Rufaa za Mikoa ili ziweze kutoa huduma za kibingwa, kupunguza msongamano wa wagonjwa na ucheleweshwaji wa huduma katika Hospitali za rufaa za kanda.

  Naibu Waziri huyo Aliendelea kusema kuwa fedha hizo Shilingi Bilioni 30 zitaelekezwa katika maeneo makuu matano ambayo aliyataja kuwa ni kuhakikisha kila Hospitali ya Mkoa ina Kitengo cha dharura, chumba cha upasuaji, kitengo cha uangalizi wa wagonjwa mahututi pamoja na kitengo cha mama na mtoto.

  “Hospitali hii inatakiwa kuhudumia wagonjwa waliopata rufaa toka hospitali za mikoa ya jirani waje huku kupatiwa huduma za matibabu na sio wagonjwa wa malaria na mafua alisema Dkt. Ndugulile.

  Katika kuhakikisha huduma bora za afya zinatolewa kwenye hospitali za rufaa za mikoa, Dkt. Ndugulile amesema kuwa Serikali imeweka maeneo muhimu katika mafunzo kwa watumishi wa kada ya afya huku akitaja watumishi wenye kuhitajika zaidi kwa sasa kuwa ni madaktari wa magonjwa ya ndani, watoto, wakina mama, upasuaji, mifupa pamoja na madaktari wa usingizi.

  Kuhusu upatikanaji wa huduma za kibingwa, Dkt.Ndugulile alisema mafanikio kuona huduma hizo zikiwa zinapatikana hapa nchini tofauti na zamani “Tunafanya upandikizaji wa figo pamoja na upandikizaji wa vifaa vya usikivu kwa wa watoto huduma ambazo zilikuwa ni za kufikirika ndani ya miaka mitatu sasa zinapatikana hapa nchini” alisema Dkt. Ndugulile.

  Awali akitoa taarifa yake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya KCMC Dkt. Gileard Masenga aliishukuru Serikali kwa kuendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Hospitali hiyo “Licha ya kumilikiwa na Taasisi ya kidini lakini Serikali imeendelea kutupatia wataalam, misamaha ya kodi za malighali zinazoingizwa nchini ambazo hutumika kutengeneza mafuta ya kuwakinga wenye ulemavu wa ngozi dhidi ya jua.

  Aidha, Dkt.Masenga alisema hospitali yake imetengewa Shilingi Bilioni 1 kwa ajili ya dawa za Saratani huku fedha kiasi cha Shilingi Milioni 250 tayari zimeshapelekwa Bohari ya dawa kwa ajili ya ununuzi wa dawa hizo.

  Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto yupo Mkoani hapa kwa ziara ya kikazi inayolenga kukagua shughuli za huduma ya Afya,Maendeleo ya Jamii pamoja na kuongea na watumishi wa sekta hizo.

older | 1 | .... | 1730 | 1731 | (Page 1732) | 1733 | 1734 | .... | 1898 | newer