Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46313 articles
Browse latest View live

WAKALA WA MAJENGO TANZANIA YATAKIWA KUMALIZA KWA WAKATI UJENZI WA KITUO CHA KUMBUKUMBU NA NYARAKA ZA TAIFA CHA KANDA YA ZIWA KINACHOJENGWA JIJINI MWANZA

$
0
0

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Dorothy Mwaluko akitazama ramani ya mradi wa ujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza wakati wa ziara ya kikazi kuangalia maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Dorothy Mwaluko akitoa maelekezo ya kuboresha ujenzi wa Kituo cha kumbukumbu na Nyaraka za Taifa Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza kwa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wakati wa ziara ya kikazi kuangalia maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Dorothy Mwaluko akizungumza na Wataalam wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) mara baada ya kutembelea mradi wa ujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa Kanda ya Ziwa wakati wa ziara ya kikazi kuangalia maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho.



Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) imetakiwa kukamilisha kwa wakati mradi wa ujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa cha Kanda ya Ziwa uliopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza.

Wito huo, umetolewa na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Dorothy Mwaluko wakati wa ziara ya kikazi kuangalia maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho.

Bi. Mwaluko ameitaka Wakala hiyo kuhakikisha inakamilisha ujenzi kwa wakati ili kuiwezesha Serikali kukusanya, kuchambua, kutunza na kuhifadhi kumbukumbu mbalimbali kutoka katika Taasisi za Umma zilizopo kanda ya Ziwa kwa lengo la kulinda urithi andishi na historia ya Taifa letu.

Bi. Mwaluko ameielekeza Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa kuzungumza na Wakala wa Majengo Tanzania na kukubaliana tarehe rasmi ambayo jengo litakuwa limekamilika ili taarifa hiyo itolewe kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa iliyopanga kutembelea kituo hicho hivi karibuni kwa lengo la kujiridhisha na ujenzi uliofanyika.

Naye, Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Firimin M. Msiangi amesema, kituo hicho kitakapokamilika kitakuwa ni kitovu cha mafunzo ya namna bora ya utunzaji wa Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa katika kanda ya Ziwa kwa watumishi wa umma na wanafunzi wa vyuo wanaosoma masuala ya utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka.

Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) mkoani Mwanza, Bi. Doreen Swai amesema ili kukamilisha ujenzi kwa ubora unaotakiwa, TBA inategemea kukabidhi kituo hicho mwakani mwezi Februari, 2019.

Serikali katika bajeti ya fedha mwaka 2018/19, imeiidhinishia Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jumla ya shilingi 2, 000, 000,000/= za kitanzania ili kukamilisha ujenzi wa kituo kitakachokuwa na uwezo wa kuhifadhi makasha (archival boxes) 15,000 ya kumbukumbu tuli yenye uwezo wa kubeba jumla ya majalada 150, 000 kwa wakati mmoja. Aidha, kituo kitatumika kama kituo mbadala cha Mifumo ya TEHAMA ya kuhifadhi kumbukumbu iliyopo katika Kituo cha Taifa cha Kumbukumbu Dodoma.

WAZIRI LUGOLA ASHTUKIZA KITUO CHA POLISI CHANG’OMBE TEMEKE, AMTAKA RPC KUZIFANYIA KAZI KASORO ALIZOZIBAINI ZA KIUTENDAJI

$
0
0









Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akimsikiliza Askari wa zamu wa Kituo cha Polisi Chang’ombe Mkoa wa Polisi Temeke, Keneth Komba, alipokua anatoa taarifa za mahabusu waliopo ndani ya kituo hicho. Waziri Lugola alifanya ziara kushtukiza kituoni hapo saa sita mchana akifuatilia maagizo yake aliyoyatoa nchi nzima ya kutoa dhamana saa 24, kutobambikizia wananchi kesi pamoja na polisi kutoomba rushwa kwa wananchi.



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akimtaka Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Emmanuel Lukula (kushoto) kutoa ufafanuzi kuhusu msauala mbalimbali ya utendaji kazi katika kituo chake. Kulia ni Askari wa zamu wa Kituo hicho, Keneth Komba. Waziri Lugola alifanya ziara kushtukiza kituoni hapo saa sita mchana akifuatilia maagizo yake aliyoyatoa nchi nzima ya kutoa dhamana saa 24, kutobambikizia wananchi kesi pamoja na polisi kutoomba rushwa kwa wananchi.



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na waandishi wa habari nje ya kituo cha Polisi cha Chang’ombe Mkoa wa Kipolisi Temeke, jijini Dar es Salaam, leo. Waziri Lugola alifanya ziara kushtukiza kituoni hapo saa sita mchana akifuatilia maagizo yake aliyoyatoa nchi nzima ya kutoa dhamana saa 24, kutobambikizia wananchi kesi pamoja na polisi kutoomba rushwa kwa wananchi. Hata hivyo, Waziri huyo alimtaka Kamanda wa Polisi Mkoa huo kuhakikisha wanarekebisha kasoro mbalimbali alizozibaini kituoni hapo.



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati) akizungumza na MKamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke,Emmanuel Lukula (kulia), wakati Waziri huyo alipofanya ziara ya kushtukiza kituoni hapo. Kushoto ni Mkuu wa Upepelezi wa Wilaya ya Temeke, Kakwaya Jonas. Waziri Lugola alifanya ziara kushtukiza kituoni hapo saa sita mchana akifuatilia maagizo yake aliyoyatoa nchi nzima ya kutoa dhamana saa 24, kutobambikizia wananchi kesi pamoja na polisi kutoomba rushwa kwa wananchi. Hata hivyo, Waziri huyo alimtaka Kamanda wa Polisi Mkoa huo kuhakikisha wanarekebisha kasoro mbalimbali alizozibaini kituoni hapo.



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (wapili kulia) akiingia jengo la Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke. Waziri Lugola alifanya ziara kushtukiza Kituo cha Polisi Chang’ombe saa sita mchana akifuatilia maagizo yake aliyoyatoa nchi nzima ya kutoa dhamana saa 24, kutobambikizia wananchi kesi pamoja na polisi kutoomba rushwa kwa wananchi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Madaktari Bingwa MNH Waendelea kutoa Tiba Ligula

$
0
0

Daktari Bingwa wa uchunguzi wa magonjwa mbalimbali ya binadamu kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Innocent Mosha (kushoto) kwa kushirikiana na mtaalam wa Radiolojia Dkt. Maria Mtolera wakichukua sampuli ya uvimbe uliokua ndani ya ini kwa kutumia sindano wakiongozwa na mashine ya Utra sound.
Daktari Bingwa kutoka Muhimbili Judith Mwende akifanya upasuaji wa mtoto wa jicho leo katika Hospitali ya Ligula.
Wataalam wa afya wa MNH kwa kushirikiana na watalaam wa afya wa Hospitali ya Ligula wakimfanyia upasuaji mgonjwa mwenye matatizo ya magonjwa ya kike na uzazi.
Daktari Bingwa wa upasuaji wa pua, koo na masikio kutoka Muhimbili Willybroad Massawe (kulia) akimuhudumia mgonjwa mwenye tatizo la sikio.
Baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Mtwara ambao wamejitokeza leo kwa ajili ya kupata huduma za afya, ushauri na matibabu mbalimbali.

Mtwara ,Matibabu

Wataalam wa afya wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na wataalam wa afya wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Mtwara, Ligula wanaendelea kutoa huduma mbalimbali za afya kwa wananchi wa mkoa huo ikiwemo huduma za kibingwa ambazo awali hazikuwahi kufanyika hospitalini hapo.

Moja ya huduma za kibingwa zilizofanyika leo ni kuchukua sampuli ya uvimbe uliokua ndani ya ini kwa kutumia sindano wakiongozwa na mashine ya Utra sound.

‘’Mgonjwa huyu tumemfanyia kipimo cha sindano (FNAC) kwa kuongozwa na mashine ya Utra sound lengo ni kufanya uchunguzi zaidi ili mgonjwa aweze kupata tiba sahihi’’. Amesema Dkt. Mosha.

Maeneo mengine ambayo watalam wametoa huduma ni pamoja na magonjwa ya mfumo wa mkojo, magonjwa ya kike na uzazi, meno, macho, watoto, magonjwa ya koo, pua na masikio, maabara pamoja na magonjwa ya ndani.

Utoaji wa huduma hizo unaenda sambamba na kuwajengea uwezo watalaam wa Hospitali ya Ligula ili kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda kutibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

LOWASSA MGENI RASMI UZINDUZI WA ALBAMU YA MARIAM KILYENYI

$
0
0
 Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa albamu ya mwimbaji wa muziki wa Injili Mariam Kilyenyi, utakaofanyika Disemba 2, 2018 katika Kanisa la Kiinjili la Kirutheli Tanzania (KKKT)-Sinza Mapambano, jijini Dar es Salaam.
Mwimbaji wa muziki wa Injili Mariam Kilyenyi ambaye atazindua albamu yake skiku ya tarehe 2 mwezi wa 12 mwaka huu
Na mwandishi wetu, Dar es Salaam. 

Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa albamu ya mwimbaji wa muziki wa Injili Mariam Kilyenyi, utakaofanyika Disemba 2, 2018 katika Kanisa la Kiinjili la Kirutheli Tanzania (KKKT)-Sinza Mapambano, jijini Dar es Salaam.

Mbali na Lowassa, waimbaji watakaosindikiza uzinduzi wa albamu hiyo inayoitwa ‘Hakimu wa Haki’ ni Bahati Bukuku, Dk Tumaini Msowoya, Tumaini Njole, Tumaini Mbembela,  Madamu Ruth ,Iren Mwamfupe, Bony Mwaitege, Margie Muliri, Juvenalista Mabuma  Edson Mwasabwite.

Akizungumza na Mwananchi, Mariam alisema amemualika Lowassa kwa sababu ndiyo aliyeanza kuibu kipaji chake, alipompa nafasi ya kuimba siku ya sherehe yake ya kuzaliwa.“Lowassa ni baba yangu, aliibua kipaji change ndio maana nikatamani awe mgeni rasmi na amekubali, namshukuru sana Mungu kwa sababu hii,” alisema.

Alitaja nyimbo zilizo kwenye albamu yake kuwa ni Hakimu wa Haki, Pam Pam tukuza, Natafuta Mshauri, Chereko leo, Nasikia Kuitwa, Agano Langu, Ushindi Lazima na Mapambazuko.

“Nasikia kuitwa ndio wimbo ambao niliimba wakati nikianza mbele ya baba Lowassa, kwa hiyo ilipofika hatua ya kuandaa albamu yangu niliuweka na huo kwa sababu ndio ulionifungulia njia,” alisema.

Akizungumzia changamoto alizokutana nazo kwenye muziki huo, Mariam alisema ni gharama kubwa ya uandaaji wa muziki pamoja na kusambaza kazi hiyo.

“Naimba muziki kwa sababu nasikia kuitwa kwa ajili ya kazi hiyo, kusema kweli gharama za uandaaji wa kazi nzuri ni kubwa hata hivyo namshukuru Mungu kwa sababu nimeshakamilisha hatua ya kwanza,” alisisitiza.

Hata hivyo alisema, imekuwa rahisi kwake kufikia ndoto ya mafanikio kwa sababu ya sapoti kubwa kutoka kwa waimbaji waliotangulia.

Mariam amesema tayari tiem ya wacheza show ‘dancers’ imeingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya siku hiyo.

“Mara nyingi waimbaji wa muziki wa injili huwa tunapuuzia wacheza shoe lakini ni watu muhimu na hawa ndio huwa wanafanya watu wafurahie matamasha, kwa hiyo tayari nimeshawaingiza kambini,” alisema.

Akizungumzia uzinduzi huo, mwimbaji Jesca Gazuko anayetamba na wimbo wa ‘Bwana Amefanya’ alisema ujio wa Lowassa unaonyesha namba ambavyo viongozi wamekuwa wakisapoti kazi za waimbaji wanaochipukia.

WAZIRI MKUU AWAPONGEZA WANANCHI KWA UJENZI WA SHULE

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Ruangwa, Novemba 20, 2018. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Hashim Ngandirwa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Ruangwa, Novemba 20, 2018.

Baadhi ya wanawake waliojitokeza kushiriki katika ujenzi wa Shule ya Msingi katika kijiji cha Kilimahewa wilayani Ruangwa wakimshangilia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowasili kwenye eneo la ujenzi wa shule hiyo kukagua ujenzi na kushiriki katika ujenzi huo, Novemba 20, 2010

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Shule ya Msingi ya kwenye kijiji cha Kilimahewa unaofanywa na wananchi wa Kata ya Nachingwea wilayani Ruangwa, Novemba 20, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kukagua ujenzi wa Kituo cha Afya cha Mbekenyera wilayani Ruangwa, Novemba 20, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Viongozi wa Msikiti wa Mbekenyera wilayani Ruangwa na viongozi wa Mfuko wa Human Relief Foundation wakati alipowasili kwenye Msikiti huo kuuzindua, Novemba 20, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Msikiti wa Mbekenyera wilayani Ruangwa uliojengwa na Mfuko wa Human Relief Foundation, Novemba 20, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Msikiti wa Mbekenyera wilayani Ruangwa baada ya kuzindua Msikiti huo, Novemba 20, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Kibaha Vijijini, Hamoud Jumaa baada ya kuzindua Msikiti wa Mbekenyera wilayani Ruangwa, Novemba 20, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwaaga wananchi baada ya kuzindua Msikiti wa Mbekenyera wilayani Raungwa, Novemba 20, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 
………………………
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwaamewapongeza wakazi wa kata ya Nachingwea wilayani Ruangwa kwa kujenga shule ya msingi kwenye kijiji cha Kilimahewa. “Uamuzi wa kujenga shule ya msingi ni sahihi kwa kuwa huwapunguzia watoto kutembea umbali mrefu na pia utarahisisha mazingira ya kusomea kwa watoto wetu.” 

Waziri Mkuu ametoa pongezi hizo leo (Jumanne, Novemba 20, 2018) alipotembelea eneo la ujenzi wa shule ya msingi Lugalo na kuwataka waendelee na moyo huo. Amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli inataka kila mtoto aliyefikia umri wa kwenda shule aanzishwe shule na asome. Kadhalika, Waziri Mkuu ametaka wananchi hao waweke pembeni itikadi zao za kisiasa na badala yake washirikiane kujenga miradi ya maendeleo kwenye eneo lao. 

Nae, Mtendaji wa Kijiji cha Kilimahewa, Majuto Ungulu amesema ujenzi wa shule hiyo uliibuliwa na wakazi wa kijiji hicho, ambacho hakina shule ya msingi. Majuto amesema watoto wa kijiji hicho wanalazimika kutembea umbali wa kilomita mbili hadi shule la msingi Ruangwa, hivyo ujenzi huo utawawezesha kusoma karibu. Amesema kwa sasa wameanzia na ujenzi wa vyumba vinane vya madarasa, matundu 18 ya vyoo na ofisi mbili za walimu ambapo jumla yake ni sh. milioni 399.8. 

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ametembelea kituo cha afya cha Mbekenyera na kusema ameridhishwa na hatua iliyofikiwa na kuwataka wananchi wakitunze. Amesema kwa sasa wananchi hao hawana sababu ya kulipa nauli kwenda Ruangwa kufuata huduma za vipimo na matibabu katika hospitali ya wilaya. 

Ametaja baadhi ya huduma zinazopatikana kwa sasa kwenye kituo cha Afya Mbekenyera ambazo awali hazikuwepo ni upasuaji, maabara, mama na mtoto. Mapema, Waziri Mkuu alikagua eneo la ujenzi wa kituo cha Polisi Ruangwa, alitembelea mradi wa ujenzi wa Mahakama ya wilaya na kukagua ujenzi wa ofisi ya mkuu wa Wilaya.

BUNGE LA CHINA LAIPONGEZA SERIKALI YA TANZANIA KWA KASI YA UJENZI WA MIRADI

$
0
0
Na Grace Semfuko-MAELEZO
Bunge la Jamhuri ya Watu wa China limepongeza kasi ya ujenzi wa Miradi inayofanywa na Serikali  ya Tanzania na kwamba ushirikiano uliopo baina ya China na Tanzania utaendelea kuimarishwa ili kuzifanya nchi hizo kuzidi kuwa na maendeleo ya kuichumi.

Hayo yamebainishwa na Makamu wa Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya watu wa China Bw. Cai Defang alipotembelea Daraja la Nyerere Kigamboni Jijini Dar Es Salaam lililojengwa na Kampuni ya China Railway Jiangchang Engineering CRJE na China Major Bridge Engineering Company  ujenzi ulioanza mwaka 2012 na kukamilika April 2016.

Daraja hilo linalovuka mkondo wa maji wa Kurasini hadi Kigamboni  Jijini Dar Es Salaam lina urefu wa mita 680 na njia sita za kupitishia magari ni daraja kubwa katika nchi za Afrika Mashariki na lilizinduliwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli April 19 mwaka 2016 na kupewa jina la Julius Nyerere kwa heshima ya Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania Hayati  Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Ujenzi wa Daraja la Nyerere ulibuniwa na Serikali lengo likiwa ni kupunguza msongamano wa magari uliokuwepo katika kivuko cha Magogoni Jijini Dar Es Salaam na kurahisisha usafiri lengo ni kuwaondolea watanzania changamoto kwenye sekta ya usafirishaji.
Akizungumza katika ziara hiyo Makamu Mwenyekiti huyo wa Bunge la Jamhuri ya Watu wa China Cai Defang amesema ni muda muafaka sasa kwa daraja hilo kutumika kama njia za kiuchumi kwa watu wa Tanzania.

“Nimefurahishwa na ujenzi wa Daraja hili uliojengwa na Kampuni ya CRJE ya wachina,wamefanya kazi nzuri, kwa Tanzania daraja hili ni fursa za kiuchumi kwani litarahisisha usafirishaji na kuepukana na vikwazo vilivyokuwepo awali kabla ya dara hili” alisema Cai Defang Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya watu wa China.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la hifadhi ya jamii la NSSF Bw. William Erio amesema kukamilika kwa daraja hilo kumekuwa na manufaa makubwa kwa Serikali kwani limekuwa likiingizia Serikali mapato yatokanayo na kuvusha magari fedha ambazo zimekuwa zikienda kufanya shughuli zinazoinufaisha jamii ya kitanzania.

“Tunashukuru Serikali kuendelea kubuni miradi mbalimbali ya kimaendeleo ambayo inasaidia jamii kwa asilimia mia moja,mfano daraja hili ni moja ya vyanzo vya kiuchumi kwani fedha za makusanyo hapa zinasaidia kuongeza kasi ya kuhudumia jamii kupitia ujenzi wa miradi mingine” alisema William Erio wakati akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya watu wa China alipotembelea kwenye mradi huo wa daraja.
 Makamu wa Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya watu wa China Bw. Cai Defang na watendaji wa (NSSF) wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na uongozi unaosimamia huduma za daraja la Nyerere baada ya kukagua daraja hilo leo jijini Dar Es Salaam.
 Makamu wa Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya watu wa China Bw. Cai Defang (wa katika)  akiwa ameambatana na  viongozi mbalimbali wa wakitembelea daraja la Nyerere, Kigamboni jijini Dar es Salaam leo.(Picha na Emmanuel Massaka MMG)
 Makamu wa Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya watu wa China Bw. Cai Defang (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la hifadhi ya jamii la (NSSF) Bw. William Erio leo alipotembelea Daraja la Nyerere Kigamboni jijini Dar es Salaam.
 Muonekano wa Daraja kwa sasa
Picha ya pamoja

HOSPITALI YA APOLLO YA INDIA YATOA OFA YA MATIBABU KWA WANAMUZIKI WA TANZANIA

$
0
0
Daktari Bingwa wa kutibu bila ya kufanya upasuaji kutoka Hospitali ya Apollo, Dr Sandip Jhala akielezea namna wanavyofanya upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye kizazi, tezi dume na magonjwa mengine katika mkutano uliowakutanisha Wanaumoja wa Wanamuziki Tanzani (TAMUFO) pamoja na wawakilishi wa Hospitali ya Apollo hapa nchini mkutano uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Rais wa TAMUFO, Dkt. Donald Kisanga akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwanamuziki Kasim Salehe Mafanya, akiwa na mwanamuziki wa nyimbo za injili katika mkutano huo.
Viongozi wa TAMUFO na wadau wa muziki wakiwa meza kuu. 
Lina Munisi aliyetolewa uvimbe na Dr.Jhala bila ya kupasuliwa katika Hospilati ya Apollo nchini India akitoa ushuhuda wake kwa wanamuziki.
Mlezi wa TAMUFO, Dk.Juliana Pallangyo, akizungumza kwenye mkutano huo.
Wadau mbalimbali pamoja na wanamuziki wakiwa kwenye mkutano.
Mwanamuziki mkongwe Mzee Makassy akiwa kwenye mkutano huo.
Katibu Mkuu wa TAMUFO, Stellah Joel, akizungumza kwenye mkutano huo. 




Na Kulwa Mwaibale

Hospitali ya Kimataifa ya Apollo yenye makao makuu yake nchini India, imetoa ofa ya matibabu kwa wanamuziki wa Tanzania.

Akizungumza mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, kwenye mkutano baina ya wawakilishili wa Hospitali ya Apollo nchini Tanzania pamoja na wanachama wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), Parwez Audax alisema lengo la kutoa ofa hiyo ni kuhakikisha wanamuziki nchini wanakuwa na afya njema.

Audax alisema, baada ya kubaini watu wengi nchini wanasumbuliwa na maradhi hususan ya uvimbe kwenye kizazi kwa wanawake, tezi dume, saratani ya ini pamoja na magonjwa ya mgongo na uti wa mgongo wameamua kutoa ofa ya matibabu kwa gharama nafuu kwa wanamuziki.

"Kwa kuanzia tumeamua kutoa ofa ya gharama nafuu kwenu wanamuziki kwa watakaojiunga na bima ya afya ya Apollo," alisema mwakilishi huyo.

Naye Dr Sandip Jhala ambaye ni miongoni mwa madaktari bingwa wanaotibu bila kufanya upasuaji wa Hospitali ya Apollo, alisema baada ya kuona watu wengi kutoka nchi za Afrika wanasumbuliwa na uvimbe kwenye kizazi, tezi dume na magonjwa mengine aliamua kuja Afrika kutoa tiba.

"Nilipoona watu wengi kutoka Afrika hususan Tanzania wanakuja kwenye hospitali yetu ya Apollo India kutibiwa niliamua kuja kufanya utafiti kujua ukubwa wa tatizo na kutoa tiba," alisema Jhala.Dr. Jhala alisema matibabu ya kuondoa uvimbe katika kizazi kwa wanawake bila ya kufanya upasuaji hayahitaji nusu kaputi na mgonjwa hutumia siku mbili tu kukaa hospitali na anakuwa na asilimia 33 mpaka 53 ya kupata mtoto.

Daktari huyo alisema ugonjwa wa tezi dume ambao chanzo chake ni njia ndogo ya kupitisha haja ndogo kubana na kufanya ugumu wa haja ndogo kupita unatibika kwa muda mfupi.Dr. Jhala aliwashauri wanamuziki wa Tanzania kujiunga na bima ya afya ya Hospitali ya Apollo ili waweze kupata ofa ya matibabu kwa gharama nafuu watakapokwenda kutibiwa India au hapa nchini.

Rais wa TAMUFO, Dk. Donald Kisanga aliwashukuru wawakilishi hao wa Hospitali ya Apollo nchini kwa ofa hiyo ya matibabu waliyoitoa kwa wanamuziki."Tunawashukuru sana kwa ofa mliyotupatia, tutaichangamkia kwa kujiunga na bima yenu mara tutakapokaa nanyi ili mtupe muongozo wa kujisajili," alisema.

Katibu Mkuu wa TAMUFO, Stellah Joel aliwashukuru Apollo kwa kuwajali wanamuziki wa Tanzania na kusema kwa kuwa wanazo hela watajiunga na mfuko wao wa bima ili waanze kunufaika na ofa waliyowapatia.

Mlezi wa TAMUFO, Dk. Juliana Pallangyo aliwashukuru Apollo kwa ofa waliyowapa na kusema wameo

MAGAZETI YA LEO JUMATANO NOVEMBA 21,2018

$
0
0




 
 









Vikosi kazi vya TNBC vyazinduliwa rasmi

$
0
0
Katibu Mkuu Kiongozi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Baraza la Taifa la Biashara(TNBC) Balozi John Kijazi(kushoto) akisalimia na Kaimu Katibu Mkuu wa TNBC Bi.Oliver Vengula(kulia) mara baada ya kuwasili katika kikao cha uzinduzi wa vikundi kazi vinne vya Baraza hilo jijini Dar es salaam. Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania(TPSF) Salum Shamte na wapili kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu, Prof.Faustine Kamuzora
Katibu Mkuu Kiongozi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Baraza la Taifa la Biashara(TNBC) Balozi John Kijazi akizungumza jambo na wajumbe wakamati tendaji wakati wa uzinduzi wa vikundi kazi vinne vya Baraza hilo jijini Dar es salaam zitakavyoleta mapendekezo ya kuboresha sera ,sheria na miongozi ili kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara nchini.


KATIBU Mkuu Kiongozi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Baraza la Taifa la Biashara(TNBC), Balozi John Kijazi amezindua vikundi kazi vya baraza hilo kwa lengo la kujenga na kuimarisha mahusiano kati ya sekta za umma na binafsi katika kuibua changamoto na
kuzijadili kwa mustakabali wa maendeleo ya Tanzania.

Akizungumza mara baada ya uzinduzi wa vikundi kazi hivyo jijini Dar es salaam juzi, Balozi Kijazi alisema madhumuni ya kuunda vikundi kazi hivyo vilivyowajumuisha wataalum katika sekta mbalimbali vitawezesha majadiliano juu ya changamoto zajadiliwe kwa kina zaidi kabla ya
kupelekwa katika ngazi ya Baraza.

“jumla ya vikundi kazi vinne nimevizindua leo (juzi) ikiwa ni pamoja na kikundi kazi cha Mazingira ya Biashara, Viwanda, Misitu na Kilimo vitavyokwenda kuibua changamoto na kuleta mapendekezo yatakayosaidia kuboresha sera na miongozo iliyopo,” alisema Balozi Kijazi. Alisema ushirikiano kati ya sekta binafsi na Sekta ya umma unahitajika sana ili kuweza kuibaini changamoto na kuzijadili na kuja na mapendekezo yatakayo leta tija katika mustakabali wa kujenga uchumi wa
Taifa.

“Serikali itapokea mapendekezo yote yatakayowakilishwa na timu za wataalum kutoka katika vikundi kazi hizi na tutayafanyia kazi mapendekezo yote, zaidi kwa mengine yanayoweza kuchukuliwa na maamuzi kwa ngazi yenu endeleeni lengo ni kupunga majadiliano katika ngazi ya
taifa,” alisema Balozi Kijazi Alisisitiza kuwa mijadala ya vikundi kazi hivi ifanyike kwa uhuru na
usawa kwa kutoa hofia cheo cha mtu au mali wote wawekitu kimoja ili majadiliano yaweze kuleta tija na mapendekezo yatakayofanya mazingira ya biashara kuboresheka zaidi.

“Vikundi kazi hizi vikapitiwe Sera,Miongozo na Sheria zilizopo ili waje na mapendekezo yatayoboresha mazingiria ya biashara kuwa rafiki kwa wawekezaji na wafanyabiashara nchini,” alisema Alisema kuwa kumekuwa na malalamiko mengi juu ya tozo , mamlaka za uthibiti na kero mbalimbali katika uanzishaji wa biashara nchini hivyo ni muhimu vikundi kazi hizi zikajana na mapendekezo katika maeneo hayo ili tuyafanyie kazi.

“Uongozi wa awamu ya tano umefanikiwa kupunguza baadhi ya changamoto ikiwemo utitiri wa kodi kwa wafanyabiashara, hivyo ni matumaini yangu tutakwenda kumaliza kabisa changamoto zilizopo na kupelekea nchi yetu kupiga hatua kiuchumi,” alisema Balozi Kijazi. Pia Balozi Kijazi alisema kikosi kazi cha kilimo kisimamie utekelezaji wa nguzo kumi za kilimo kwanza na pia kufanya mapitio ya Mpango wa Awamu ya Pili wa Maendeleo ya Kilimo(ASDP- II) na kuleta mapendekezo
ya utekelezaji wake.

“Lengo letu ni kutizima azma ya Serikali ya kufikia uchumi wa kati na viwanda ifikapo 2025, vikundi kazi hizi ndiyo vitatupa mwanga wa kufikia malengo kwa kuja na mapendekezo yenye tija na utekelezaji ufanywe maendeleo yapate kuonekana,” alisema Balozi Kijazi kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania(TPSF)Bw.Salum Shamte ambaye pia mwenyekiti mwenza wa kamati tendaji ya baraza alisema kuundwa kwa vikundi kazi hizi kumeonyesha
nia ya dhati ya Sererikali ya kuboresha mazingira ya biashara nchini.

“Sisi sekta binafsi tumefurahiswa na hatua zinazofanywa na Serikali, ushirikiano wetu katika kivundi kazi hizi utakuwa mkubwa na mapendekezo yanayotakiwa katika kuboresha sera ,Sheria tutawasilinao Serikai ili yafanyiwe kazi,” alisema Bw.Shamte alisema lengo kubwa ni kuboresha mazingira ya kufanya biashara nchini na hii ni kutoakana na kero mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara na wawekezaji katika hatua za kuwekeza nchini.

Mwenyekiti wa Kikundi kazi cha Mazingira ya Baishara ambaye pia ni Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof.Faustin Kamuzora alisema atakwenda kushirikiana na wajumbe wenzake wa kamati hiyo kuibua mapendekezo yatayosaidia kuboresha mazingira ya biashara
nchini.

Fanyeni kazi Kwa Bidii Huku Mkimtanguliza Mungu Mbele kwani Huduma Wanayoitoa Inagusa Uhai wa Watu – Prof. Mohamed Janabi

$
0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni moja mfanyakazi bora wa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2018/2019 Ramadhani Mpili wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wastaafu na kumpongeza mfanyakazi bora iliyofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo uliopo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi cheti cha kutambua utendaji wake wa kazi kwa kipindi chote cha utumishi wa Umma Afisa Muuguzi Mkuu Msaidizi Mstaafu Agnes Mtaki wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wastaafu na kumpongeza mfanyakazi bora iliyofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo uliopo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Huduma ya Uuguzi wa Taasisi hiyo hiyo Robert Mallya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi ngao ya kutambua utendaji wake wa kazi mhudumu wa Afya Mwandamizi Mstaafu Magdalena Masanno wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wastaafu na kumpongeza mfanyakazi bora iliyofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo uliopo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Huduma ya Uuguzi wa Taasisi hiyo hiyo Robert Mallya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwa katika picha ya pamoja na wastaafu Magdalena Masanno na Agnes Mtaki na baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi hiyo mara baada ya kumalizika kwa hafla fupi ya kuwaaga wastaafu hao na kumpongeza mfanyakazi bora iliyofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo uliopo jijini Dar es Salaam.

Afisa Muuguzi Mkuu Msaidizi Mstaafu Agnes Mtaki na mhudumu wa Afya Mwandamizi Mstaafu Magdalena Masanno wakikata keki wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wastaafu hao na kumpongeza mfanyakazi bora iliyofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) . Kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Fedha Agnes Kuhenga na kulia ni Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Huduma ya Uuguzi Robert Mallya.



Picha na Genofeva Matemu – JKCI

………………………

Na Mwandishi Maalum

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi amewataka wafanyakazi wa Taasisi hiyo kufanya kazi kwa bidii huku wakimtanguliza Mungu mbele kwani huduma wanayoitoa inagusa uhai wa watu.

Prof. Janabi ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo ameyasema hayo leo wakati wa hafla fupi ya kuwaaga maafisa uuguzi wawili ambao wamestaafu kwa mujibu wa sheria ya utumishi wa umma na kumpongeza mfanyakazi bora wa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa Julai-Septemba 2018.

Alisema kazi ya kuwahudumia wagonjwa siyo kazi rahisi sana kuna wakati wagonjwa wanakuwa wakali wao na ndugu zao jambo la muhimu ni kuwa wavumilivu na kuwahudumia kwa moyo wa upendo.

“Leo hii tunawaaga wafanyakazi wenzetu ambao wanastaafu kwa mujibu wa sheria ya utumishi wa umma, kazi waliyoifanya ni ngumu wanastahili pongezi. Mmoja amefanya kazi miaka 40 na mwingine miaka 35 katika kipindi chao chote walichokuwa kazini hawakuwahi kushtakiwa kwa utovu wa nidhamu”.

“Jambo la muhimu kwetu sisi tunaobaki tuwaige mfano tujitahidi kuwahi kazini , tuwepo eneo la kazi na kufanya kazi muda wote wa kazi, tushirikiane na tuheshimiane kwa kufanya hivi tutaweza kutoa huduma bora kwa wagonjwa wetu wa moyo”, alisema Prof. Janabi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kurugezi ya Huduma ya Uuguzi Robert Mallya aliwasisitiza wauguzi hao wanaostaafu kwenda kuwahudumia wananchi pale itakapohitajika kufanya hivyo kwani taaluma yao iko palepale na jamii inahitaji kupata huduma yao .

Akizungumza kwa niaba ya mstaafu mwenzake Afisa Muuguzi Mkuu Msaidizi Mama Agnes Mtaki aliwashukuru wafanyakazi hao kwa moyo wa upendo waliouonyesha katika kipindi chote walichofanya kazi pamoja katika Taasisi hiyo.

Mama Mtaki alisema, “Jambo la muhimu ninalowahusia ni mfanye kazi kwa bidii huku wakimtanguliza Mungu mbele kwani huduma mnayoitoa ni ya kiroho. Kazi ya kuwahudumia wagonjwa inahitaji uvumilivu, unyenyekevu na ushirikiano”,.

Alimalizia kwa kuwataka wafayakazi hao kuheshimu kazi wanayoifanya hii ikiwa ni pamoja na kuwahi kazini, kwani kuwa na kazi kumewafanya waheshimike, wasomeshe watoto na ndugu zao na kuweza kujikwamua kiuchumi.

Wafanyakazi hao wastaafu walipewa zawadi ya mabati 100, mifuko 100 ya smenti, ngao, cheti cha kutambua kazi waliyoifanya kwa kipindi chote walichokuwa kazini pia walikabidhiwa fedha za nauli za kurudi nyumbani kwao waliko zaliwa ambako ndiko watakapokwenda kuishi.

Mfanyakazi bora alipewa zawadi ya shilingi milioni moja, cheti cha kutambua kazi aliyoifanya na ngao kwa ajili ya kutoa hamasa kwa wafanyakazi wengine ili waendelee kufanya kazi kwa bidii na maarifa.

WAJASIRIAMALI 250 KUSHIRIKI MAONESHO YA SIDO KANDA YA KASKAZINI JIJINI TANGA

$
0
0
ZAIDI ya wajasiriamali 250 wamekwisha wasili Jijini Tanga kwa ajili ya  maonyesho ya Shirika la kuhudumia viwanda vidogovidogo (SIDO)Kanda ya  Kaskazini yanayotarajiwa kuanza kesho Nov 22 hadi 26 ambapo mgeni anatarajiwa  kuwa Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Joseph Kakunda

Hayo yamezungumzwa na Afisa Uendelezaji Biashara (SIDO) Mkoa Tanga  Gladness Foya alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na  maonyesho hayo ambayo yatafanyika katika viwanja vya tangamano Jijini hapa  na kushirikisha Nchi toka Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Foya alisema maandalizi yapo vizuri na tayari baadhi ya wafanyabaishara  toka Nchini Uganga na Burundi wamekwisha wasili kwa ajili ya maonyesho hayo  ambayo yanajumuisha mikoa ya Tanga,Kilimanjaro.Arusha na Manyara.“Tumekwisha anza pokea wageni na wapo zaidi ya wajasiriamali 250 wamekwisha  wasili na watatu toka Uganda na watano toka Burundi na tunatarajia kupokea  wageni zaidi katika maonyesho haya”Alisema Foya.

Awali akizungumzia maonyesho hayo Mkuu wa Mkoa Tanga Martin Shigella  alisema ni fursa kwa Watanzania na wananchi wa ndani ya jiji na nje  kujifunza namna Serikali ya awamu ya tano inavyotekeleza kwa vitendo uchumi  wa viwanda.Aidha alisema tayari taasisi za kifedha,wamili wa viwanda na wasindikaji  wamekwisha wasili Jijini hapa kwa ajili ya maonyeshoi hayo ambayo  yatawajenga katika nyanja hiyo ya uchumi wa viwanda na ujasiriamali.

“Tunaowageni wengi tumekwisha anza wapokea na zaidi ni fursa kwetu na  wajasiriamali maana watapata muda wa kuuza bishara zao na kuona bidhaa  zinazozalishwa na sido na wanaweza kuomba kutengenezewa labda niseme tu ni  fursa kubwa”Alisema Shigella.

Hata hivyo aliwaomba wafanya biashara kuyatumia maonyesho hayo ili kuweza  kujinufaisha kibiashara na namna ya kuweza kupata bidhaa bora toka shirika  hilo la Sido.
 MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia akizungumza kuhusiana na maonyesho hayo kushoto ni Mhasibu wa SIDO mkoani Tanga Janeth Kiwale
 Afisa Uendelezaji Biashara (SIDO) Mkoa Tanga  Gladness Foya akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na  maonyesho hayo ambayo yatafanyika katika viwanja vya Tangamano Jijini Tanga kesho na kushirikisha Nchi toka Jumuiya ya Afrika Mashariki kulia ni Mhasibu wa SIDO Mkoani Tanga Janeth Kiwale
Sehemu ya waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali Jijini Tanga wakifuatilia mkutano huo

Dkt Abbasi Awataka Waandishi kufuata Sheria ya Habari

$
0
0
Na Grace Semfuko-MAELEZO

Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt Hassan Abbasi amewataka waandishi wa habari kutumia haki na wajibu wao katika kulinda maadili yao ya uandishi na kutotumia taaluma yao kukejeli na kuchafua watu wengine

Amesema Sheria mpya namba 12 ya mwaka 2016 ya huduma za vyombo vya habari kifungu cha 7 ingawa inawapa Waandishi wa Habari kukusanya,kuhariri na kusambaza habari lakini haiwapi fursa waandishi hao kuandika habari ambazo zinachafua wengine.

Dkt Abbasi aliyasema hayo katika mahojiano na kipindi cha Hallow Tanzania kinachorushwa na Radio Uhuru ya Jijini Dar Es Salaam alipokuwa akijibu maswali ya wananchi kutoka katika maeneo mbalimbali Nchini.

“Sheria Mpya ya Habari inawapa fursa Waandishi kufanya kazi zao za kukusanya,kuhariri na kusambaza habari,sheria hii haijamnyima Mwandishi wa Habari kupata habari, lakini pia haijatoa fursa za kusambaza habari za kukejeli na kuchafua wengine, sheria itachukua nafasi yake kwa atakaebainika kufanya hivyo” alisema Dkt Hassan Abbasi Msemaji Mkuu wa Serikali.

Alisema katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Magufuli kuna baadhi ya vyombo vya habari ambavyo vilichukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni sehemu ya kulinda maadili ya uandishi wa habari na kuvitaka vyombo vingine kuendelea kuheshimu,kulinda na kutetea maslahi ya Taifa.

Akihojiwa na Mtangazaji wa kipindi hicho Aggrey Manzi kuhusiana na baadhi ya watu wanaotumia mitandao ya kijamii katika kuchafua wengine, Dkt Abbasi alisema sio sahihi kutumia mitandao hiyo katika kuona wengine hawafai, bali mitandao itumike kutangaza habari za Maendeleo.

Kuhusu wanaobeza Maendeleo ya nchi yanayofanywa na Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais Dkt John Pombe Magufuli swali lililoulizwa na Mkuu wa Vipindi wa Radio hiyo Bw. Abdallah Hussein ,Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt Hassan Abbasi alisema Serikali itaendelea kufanya Maendeleo na kwamba wanaobeza hawazuii utekelezaji huo

“Walisema hakuna ndege, ziliponunuliwa pia walisema kuwa nani atapanda, wakasema hakuna miundombinu ya barabara inajengwa bado wanasema, pia daraja la Mfugale limejengwa, Mradi Mkubwa wa umeme wa Stiglers Gorge unajengwa, Reli ya Kisasa ya standard Gauge inajengwa lakini bado wanasema, waache waseme tu, hawatuzuii kufanya miradi ya Maendeleo kwa ajili ya wananchi”

Akizungumzia kuhusu ukuaji wa uchumi kwa wananchi mmoja mmoja swali lililoulizwa kwa njia ya simu na Abdallah Athumani Mkazi wa Chalinze Dkt Abbasi alisema ukuaji wa uchumi unatokana na kuimarisha miradi ya Maendeleo na kwamba wakazi wanaponufaika na miradi hiyo uchumi unakua kwa mtu mmpja mmoja.

“Unapoenda kutibiwa kwa gharama nafuu katika Hospitali ambazo zimejengwa na Serikali unakuwa umehifadhi fedha zako ambazo zitatumiwa kwa matumizi mengine hii ina maana umeepukana na matumizi makubwa ya gharama za hospitali, tunaposema elimu bure ina maana Mzazi halipii gharama za elimu na fedha hizo zinafanya kazi nyingine, kwa ujumla uchumi umekua kwa nchi na kwa mtu mmoja mmoja” alisema Dkt Hassan Abbasi Msemaji Mkuu wa Serikali.

DKT SINARE AONGOZA KIKAO CHA SIKU MBILI CHA BODI YA WAKURUGENZI BARAZA LA KILIMO TANZANIA.

$
0
0

Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Baraza la Kilimo Tanzania Dkt Sinare Yusuph Sinare akisisitiza jambo wakati wa kikao cha siku mbili cha Bodi ya wakurugenzi wa Baraza la Kilimo kilichoanza leo Jijini Dar es Salaam na kuhudhuliwa na wajumbe wa Bodi pamoja na Menejimenti ya Baraza la kilimo Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Kilimo Tanzania Bi Janeth Bitegeko akiwasilisha taarifa ya fedha kwa wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya Baraza la Kilimo Tanzania, kikao hicho cha Bodi kitafanyika Dar es Salaam kwa siku mbili ikiwa ni kikao cha kawaida .
Mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya Baraza la Kilimo Tanzania Bw. Eneck Ndondole (kati kati) akichangia jambo kuhusu utekelezaji wa Mradi wa Ubia wa Kilimo Tanzania, Baada ya Mratibu wa Mradi huo kuwasilisha ripoti ya utekelezaji wa mradi huo kwenye kikao cha Bodi ya wakurugenzi.
Mratibu wa mradi wa ubia wa kilimo Tanzania Bw Mark Magila akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kwenye kikao cha bodi ya wakurugenzi kilichoanza leo jijini dare s salaam, kushoro ni Mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa Baraza la Kilimo Bw Omary Mwaimu.
Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Baraza la Kilimo Tanzania Dkt Sinare Yusuph Sinare akiongoza kikao cha Bodi ya wakurugenzi ya Baraza la Kilimo, kikao hicho cha siku mbili kilichoanza leo jijini Dra es salaam pia kilihudhuliwa na wajumbe wa Bodi na Menejiment ya Baraza la Kilimo ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Kilimo Bi Janeth Bitegeko.
Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Baraza la Kilimo Tanzania Dkt Sinare Yusuph Sinare akiongoza kikao cha Bodi ya wakurugenzi ya Baraza la Kilimo, kikao hicho cha siku mbili kilichoanza leo jijini Dra es salaam pia kilihudhuliwa na wajumbe wa Bodi na Menejiment ya Baraza la Kilimo ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Kilimo Bi Janeth Bitegeko.

WAZIRI LUGOLA AWAAMBIA MABALOZI NCHI IPO SALAMA, AAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NAO

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akiagana na Balozi wa Afrika Kusini nchini, Thami Mseleku, nje ya jengo la ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam, mara baada ya kumaliza mazungumzo yao kuhusu masuala mbalimbali ya usalama wa nchi pamoja na ushirikiano kati ya Afrika Kusini na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika jijini humo leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akimfafanulia jambo Balozi wa Italia, Roberto Mengeni, kuhusiana na masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya nchi yake na Tanzania. Lugola alimuhakikishia Balozi huyo kuwa, Tanzania itaendelea kuwa salama na kuimarisha ushirikiano na Italia. Mazungumzo hayo yalifanyika ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akimfafanulia jambo Balozi wa Afrika Kusini, Thami Mseleku, kuhusiana na masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya nchi yake na Tanzania. Lugola alimuhakikishia Balozi huyo kuwa, Tanzania itaendelea kuwa salama na kuimarisha ushirikiano na Afrika Kusini. Mazungumzo hayo yalifanyika ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam leo
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akimfafanulia jambo Balozi wa Italia, nje ya jengo la ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam, kabla ya kuagana na Balozi huyo baada ya kumaliza mazungumzo yao kuhusu masuala mbalimbali ya usalama wa nchi pamoja na ushirikiano kati ya Italia na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika jijini humo leo
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akimfafanulia jambo Balozi wa Kenya, Dan Kazungu kuhusiana na masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya nchi yake na Tanzania. Lugola alimuhakikishia Balozi huyo kuwa, Tanzania itaendelea kuwa salama na kuimarisha ushirikiano na Kenya. Mazungumzo hayo yalifanyika ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

………………………….

Na Felix Mwagara, MOHA.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amefanya mazungumzo na Balozi wa Italia, Kenya na Afrika Kusini katika ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam, na kuwaambia ulinzi na usalama wa wananchi na mali zao nchini upo vizuri.

Akizungumza katika kikao cha mabalozi hao waliofika ofisini kwake kwa nyakati tofauti leo, Lugola pia aliwaomba wawakilishi hao wa nchi zao hapa nchini waendelee kushirikiana na Wizara yake na nchi kwa ujumla.

Lugola aliwahakikishia Mabalozi hao kuwa Tanzania itaendelea kuwa salama kwa kuwa Wizara yake imejipanga vizuri kuendelea kuwalinda raia na mali zao pamoja na wageni wote waishio nchini. “Mheshimiwa Balozi nashukuru sana kwa kunitembelea, najisikia furaha kwa ujio wako na karibu sana wakati wowote, Wizara yangu pamoja na nchi yangu kwa ujumla tutaendelea kushirikiana nanyi katika masuala mbalimbali,” alisema Lugola.

Hata hivyo, Balozi wa Afrika Kusini, Thami Mseleku alisema akiwa nchini anajiona kuwa yupo nyumbani kwasababu nchi yake ina historia kubwa ya ushirikiano na Tanzania. Hata hivyo, Balozi wa Italia, Roberto Mengoni alimpongeza Waziri Lugola kwa kuteuliwa na Rais John Magufuli kuiongoza Wizara hiyo na pia alimuakikishia ushirikiano zaidi kati ya nchi yake na Tanzania.

“Hongera sana mheshimiwa Waziri kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani na pia nimefurahi kuja katika ofisini yako kufanya mazungumzo nawe,” alisema Balozi Mengoni. Naye Balozi wa Kenya Nchini, Dan Kazungu alisema Tanzania ni nchi yake na anajisikia furaha kuwepo nchini kwasababu alishawahi kufanyakazi miaka kadhaa iliyopita hapa nchini, hivyo nchi yake itaendelea kutoa ushirikiano katika masuala mbalimbali Tanzania.

BALOZI WA NORWAY NCHINI TANZANIA AMTEMBELEA SPIKA WA BUNGE

$
0
0

Balozi mpya wa Norway nchini Tanzania Mheshimiwa Elisabeth Jacobsen amemtembelea Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai ofisini kwake bungeni leo. Balozi huyo amempa Spika salamu mbalimbali kutoka serikali ya nchini kwake.
5Y2A93935Y2A9403

WANAFUNZI WA VYUO MBALIMBALI WAWASILI BUNGENI TAYARI KWA MAANDALIZI YA BUNGE LA VIJANA

$
0
0



Mkurugenzi idara ya Uhusiano wa Kimataifa na Itifaki Ndugu Eliufoo Daniel akiwakaribisha wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali ambao wamefika bungeni tayari kwa ajili ya kuanza bunge la vijana.

Afisa wa Bunge Idara ya Kamati Ndugu Michael Chikokoto akiwapa elimu jinsi Idara ya kamati inavyofanya kazi bungeni.
Wanafunzi mbalimbali waliokuja bungeni kwa ajili ya bunge la vijana wakipata picha ya pamoja mbele ya mlango wa kuingia ukumbi wa bunge.

MKUTANO MKUU APHFTA WAWAKUTANISHA WADAU, SUALA LA ADA NA USAJILI LATOLEWA MAJIBU

$
0
0
Leandra Gabriel, na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii

SERIKALI imesema ipo katika mpango wa kutengeneza muongozo ambao utasaidia katika utoaji huduma kwenye hospitali binafsi ikiwemo suala la ongezeko la gharama ambazo zinawafanya wananchi wa kawaida kushindwa kupata huduma.

Mkurugenzi wa tiba, Wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto Dkt. Dorothy Gwajima amesema hayo leo Novemba 20.2018 wakati wa uzinduzi wa mkutano wa 19 wa wadau wa afya na hospitali binafsi.

Amesema kuwa muongozo huo utasaidia hospitali binafsi ambazo hutoa huduma kwa gharama kubwa kuacha kuwabagua wagonjwa wa dharula kwani ni lazima afya ya mtu ije kwanza."Tunashughulikana hospitali zenye tozo kubwa kwa wagonjwa, kwani ni sawa kwao kuweka gharama zao kutokana na mfumo wa kutibu magonjwa maalumu, ni sawa kwa hospitali hizo kuwa na gharama zao ila kwa magonjwa ya dharura lazima huduma zitolewe bila kuangalia hadhi ya hospitali hizo" ameeleza Dkt. Gwajima.

Aidha amesema kuwa malengo ya kufanya mkutano huo ni kujadili juu ya kuimarisha utoaji wa huduma katika vituo vyao vya kutolea huduma.Dkt. Gwajima amesema kuwa sekta binafsi zinamiliki asilimia 40 za utoaji wa huduma za afya nchini na pia wanashiriki sana katika utoaji ajira na wao kama serikali wanatambua mchango wao na changamoto zao lazima wazifanyie kazi.

Aidha amesema kuwa kuwa sekta binafsi ni muhimu na pasipo sekta binafsi utoaji wa huduma za afya hazitaweza kutekelezeka kwa ubora hivyo lazima kuwepo na mabadiliko katika mtazamo chanya wa kusimamia sera za afya.Amesema kuwa bado serikali inaendeleza mikakati ya kuongeza wataalam wa afya katika vyuo mbalimbali ili kuongeza huduma bora katika vituo vya afya nchini.

Na amewataka kuwa na umoja ili kuweza kusaidia agenda ya Tanzania katika kuboresha sera ya afya nchini ambayo ni moja kati ya vipaumbele kwa serikali ya awamu ya tano.Aidha amesema kuwa wamepokea maelekezo kutoka Wizara ya afya katika kuhakikisha bodi zinazosajili maabara na vituo afya na zahanati kuwa kitu kimoja katika utendaji na kuhakikisha ada zinazolipwa ni tatu pekee na watoa huduma wataokikiuka hilo APHFTA litoe taarifa ili wachukuliwe hatua.

Pia amewataka sekta binafsi kutimiza majukumu yao na vituo vyote viwe vilivyojiandikisha na kusimamiwa vizuri na serikali bado ina imani nazo kwa kuwa zina mchango mkubwa katika sekta ya afya.Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa APHFTA Dkt. Samwel Ogillo amesema kuwa hicho ni kikao chao cha mwaka ambapo kimewakutanisha wadau wa sekta binafsi na umma na kujadili namna ya kuimarisha sekta ya afya.

Dkt. Ogillo amesema kuwa changamoto kubwa ilikuwa ni katika usajili wa vituo na maabara na wamefurahi kusikia kuwa ni ada tatu pekee ndizo wanazotakiwa kulipa na kuwa na taasisi moja ya kusimamia usajili wa vituo hivyo.

Pia amesema kuwa suala la tozo katika kununua bidhaa nchini litawarahisishia katika mchakato wa kutoa huduma kama urasimu ukikoma kwa kuwa kuaagiza vifaa nje ya nchi kunachangia katika upandishwaji wa gharama za matibabu katika hospitali binafsi.

Afisa mtendaji wa wanachama wa wamiliki binafsi wa vituo vya afya Dkt. Samwel Ogillo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi wa mkutano huo ambao umejikita zaidi katika kujadili namna ya kuimarisha zaidi sekta ya afya nchini .
Mwenyekiti wa chama cha wamiliki binafsi wa vituo vya afya nchini (APHFTA) Dkt. Kaushik Ramaiya (kushoto) wakifuatilia mjadala uliozinduliwa na Mkurugenzi wa tiba leo jijini Dar es salaam, kulia ni Afisa mtendaji wa APHFTA Dkt. Samwel Ogillo. (Picha na Erick Picson, Blogu ya jamii)
Mkurugenzi wa tiba kutoka Wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza wakati akifungua mkutano wa 19 wa wanachama na wamiliki binafsi wa vituo vya afya leo jijini Dar es salaam.

Baadhi wa wadau wa sekta binafsi na umma walioshiriki mkutano huo, wakifuatilia mjadala wa ufunguzi wa mkutano wa 19 wa wanachama na wamiliki binafsi wa vituo vya afya, zahanati na maabara.

TCRA YAWATAKA WAUZA RUNINGA NA MAFUNDI SIMU KUJISAJILI KWENYE MAMLAKA HIYO

$
0
0
Na Ahmed Mahmoud Arusha

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania(TCRA)imewataka wale wote wenye kuuza bidhaa za mawasiliano ikiwemo simu za mkononi,Radio na Runinga kuhakikisha wanajisajili kwao ili wananchi wapate huduma zilizo sahihi.

Akizungumza kwenye semina ya huduma za utangazaji kwa channeli zinazotazamwa bila malipo Meneja wa mamlaka hiyo Mhandisi Fransis Msungu amesema kuwa hapa Arusha mamlaka hiyo imebaini kuwa wafanyabiashara wengi wana leseni za biashara lakini za mamlaka hiyo wengi wao hawana.

Amesema kuwa maswali mengi yalioelekezwa kwa mamlaka hiyo imeonyesha mafundi wa simu na maduka mengi hayana leseni za mamlaka hiyo hivyo kutoa wito kwao kuangalia na kujisajili haraka kwao ili kuweza kumlinda mlaji.

“Nawasihi wote kuhakikisha wanajisajili haraka kwao ili kuwezakuondoa malalamiko yanayotolewa na walaji kwa mamlaka yetu utaona hapa Arusha kuna maduka 40 yenye leseni zetu mengi yaliopo bado hayajasajiliwa sanjari na mafundi wa simu”alitanabaisha Msungu.

Kwa Upande wake Katibu Tawala wa wilaya ya Arusha David Mwakiposa amesema kuwa mbali na malalamiko mbali mbali yaliotolewa na washiriki wa mkutano huo suala zima ni mashirikiano kati ya Tcra na wadau mbalimbali na semina hiyo imefungua milango kwa wananchi kwani elimu itawafikia walengwa ambao ni wananchi.

Amesema kuwa semina hiyo inatakiwa kuwa endelevu na watendaji wamejipanga kuhakikisha kuwafikishia wananchi kwenye maeneo yao na tutarajie kuondoa changamoto mbali mbali zinazo wakabili wananchi hususani ya wizi wa mtandao.

“Natoa rai kwa TCRA kuhakikisha changamoto mbali mbali zinazoelekezwa kwao kuzitafutia ufumbuzi ili kuondoa kero na adha wanayokutana nayo wananchi katika maeneo mbali mbali hapa nchini tunashukuru sana sisi tumepata uelewa wa masuala haya ya channel zisizolipiwa na tunaahidi kutoa elimu kwa wananchi”alisema Mwakiposa

Aidha Baadhi ya washiriki mbali mbali walioshiriki katika semina hiyo wamepata uelewa ila wakaitaka Tcra kuenda mbele zaidi katika suala zima la utoaji wa elimu kwa wananchi sanjari na kutatua changamoto mbali mbali wanazokutana nazo walaji wa mamalaka hiyo.

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AZUNGUMZA NA BARAZA LA TAIFA LA BIASHARA IKULU ZANZIBAR LEO

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara Zanzibar Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimfungua mkutano huo wa Baraza la Biasha la Taifa Zanzibar katika ukumbi wa Ikulu leo, 21/11/2018.(Picha na Ikulu)
 BAADHI ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakifuatilia Mkutano wa Baraza la Taifa la Biashara Zanzibar wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akifungua mkutano huo uliofanyika ukumbi wa Ikulu Zanzibar leo 21/11/2018.
BAADHI ya Makatibu Wakuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akifungua mkutano huo leo Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu ) 

DKT. MPOKI AKEMEA TABIA YA ABIRIA NA MADEREVA KUCHIMBA DAWA MAENEO YASIYOHUSIKA

$
0
0



NA WAJMW-DODOMA

Madereva wa mabasi yaendayo mikoani na abiria wametakiwa kuacha tabia ya kujisaidia “Kuchimba dawa” katika maeneo yasiyo rasmi ili kutunza na kuepuka uharibifu wa mazingira unaoweza kujitokeza ikiwa ni pamoja kusababisha magonjwa ya milipuko.

Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati akifungua mkutano unaojumuisha Maafisa Afya kutoka mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini pamoja na wadau wa mazingira, katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.

Dkt. Mpoki amekemea tabia hiyo hatarishi kwa ustawi wa mazingira huku akiwataka maafisa Afya na wadau wa mazingira nchini kusimamia afua zilizowekwa zinaendelea kutekelezwa ili kulinda mazingira ambayo yanatuzunguka.

“Kuna watu wengine nimeshawahi kuwaona kwenye basi wanatupa taka ovyo na mabasi mengine yanasimama porini ili abiria wajisaidie, hii tabia siyo nzuri na inatakiwa ikemewe kwa nguvu zote, Idara ya Kinga Pamoja na wadau wao wanakuja na mpango mkakati wa kuondoa kabisa dhana ya watu kusimama kujisaidia porini, "sisi tunatakiwa kuwa msitari wa mbele kupiga marufuku mabasi kusafiri bila kuchafua mazingira”.

Dkt. Mpoki amesema ni aibu kubwa kwa taifa kuona watu hawafuati kanuni za usafi huku akiwataka Maafisa Afya kuhakikisha wanafanya kazi kwa nguvu ili ionekane kuwa kero kwa watu wengine na watakaobainika kuchafua mazingira wachukuliwe hatua za kinidhamu na kisheria.

Aidha, Dkt. Mpoki ameongeza kuwa jamii inatakiwa kuzingatia matumizi ya vyoo bora na kunawa mikono mara baada ya kujisaidia ili kuepuka magonjwa ya milipuko yanayoweza kusababishwa na tabia ya uchafu ikiwa ni pamoja na kuacha tabia ya kujisaidia ovyo porini ili kaulimbiu ya “Nyumba ni Choo” iweze kutekelezwa ipasavyo kwa kujenga vyoo vya kisasa katika maeneo mbalimbali ili huduma ipatikane mahala pote.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi amesema takwimu zinaonesha kaya zilizokua na vyoo bora mwaka 2012 zilikua asilimia 19.5 lakini hivi sasa nchi nzima kaya zenye vyoo bora ni asilimia 51.4.

Dkt. Subi amesema kutokana na takwimu hiyo inaonesha kuna mafanikio katika uhamasishaji kwa jamii kutumia vyoo bora na kuacha kutumia vyoo ambavyo havina viwango na salama kwa matumizi, na badala yake serikali inaendelea kutoa elimu na kusisitiza jamii kutumia vyoo bora ili kuepuka magonjwa yanayoweza kuzuilika ikiwemo kipindupindu, magonjwa ya tumbo na kuhara.

Pamoja na hayo, maafisa Afya wametakiwa kuongeza nguvu katika kutoa elimu kwa umma, kuhamasisha usafi wa mazingira na kufikia maeneo ya mazalia ya vimelea vya ugonjwa wa Malaria ili kutokomeza ugonjwa huo ambao umekua hatari kwa jamii hasa kwa wanawake wajawazito na watoto.

Mkutano huo unaojumuisha Maafisa wa Afya nchi nzima una lengo la kutoa elimu na kubadilishana uzoefu wa kufanya kazi lakini msisitizo mkubwa ikiwa ni utunzaji wa mazingira na kuzingatia kanuni bora za afya pamoja na usafi wa mazingira na usafi na afya ya binadamu.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya akitoa neno mbele ya Maafisa Afya wa Mkoa, Halmashauri pamoja na Wadau wa Mazingira leo katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya akikagua maonesho ya vyoo baada ya kufungua kikao cha Maafisa Afya wa Mkoa, Halmashauri pamoja na Wadau wa Mazingira leo jijini Dodoma katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete.


 Maafisa Afya wa Mkoa na Halmashauri wakifuatilia kwa makini ufunguzi wa Mkutano wao uliofunguliwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya leo jijini Dodoma katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete wenye lengo la  kusisitiza umuhimu wa mazingira.
 Picha ya Pamoja ikiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya katika baada ya kikao cha  Maafisa Afya wa Mkoa, Halmashauri pamoja na Wadau wa Mazingira kilichofanyika leo jijini Dodoma.
Viewing all 46313 articles
Browse latest View live




Latest Images