Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live

DKT. MAHIGA AMWAKILISHA RAIS MAGUFULI KATIKA MKUTANO MAALUM WA WAKUU WA NCHI WA AU

0
0
Mhe. Augustine P. Mahiga (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alimwakilisha Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Mkutano Maalum wa 11 wa Wakuu Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika uliyofanyika tarehe 17-18 Novemba, 2018 mjini Addis Ababa, Ethiopia. Mkutano huo, uliitishwa kufuatia maamuzi ya Mkutano wa 31 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika uliofanyika mwezi Julai 2018 mjini Nouakchott, Mauritania ambapo Wakuu hao walielekeza uitishwe Mkutano Maalum kujadili kwa kina mabadiliko ya kitaasisi ndani ya Umoja huo. 

Mkutano huo ulijadili na kutolea maamuzi mapendekezo kuhusu Muundo wa Uongozi (Portfolios) za Kamisheni za Umoja wa Afrika; chaguzi za Uongozi wa Kamisheni; Kusitisha ajira za viongozi wa Kamisheni; na Mabadiliko ya kiutawala na fedha ikijumuisha utendaji.Mkutano ulikubaliana kupunguza idadi ya wajumbe wa Kamisheni klutoka 10 hadi 8 ambao ni Mwenyekiti wa Kamisheni, Makama Mwenyekiti na Makamishna 6. Maamuzi hayo yataanza kutekelezwa mwaka 2021 baada ya uongozi wa Kamisheni uliopo sasa kumaliza muda wake. Maamuzi yote yaliyotolewa yalilenga kuboresha utendaji wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika. 

Mhe. Waziri aliungana na viongozi wengine waliochangia katika mjadala wa kuboresha utendaji wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika kwa kuunga mkono mabadiliko ya kitaasisi katika Umoja huo. Mhe. Waziri alieleza kwamba maamuzi hayo yanalenga kuleta ufanisi kwenye kutekeleza majukumu ya Kamisheni na kuhakikisha Afrika inapata maendeleo inayostahili haswa kwa kuzingatia Agenda 2063 ya Umoja wa Afrika. 

Katika Mkutano huo Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Mhe. Paul Kagame alitoa salamu za rambirambi kwa Serikali za Tanzania, DRC na Malawi kufuatia vifo vya walinda amani wa nchi hizo nchini DRC.Mhe. Waziri alimshukuru Mhe. Kagame kwa salamu hizo za rambirambi na kuahidi kwamba Tanzania itaendelea kuwa mstari wa mbele kupigania amani ya kudumu barani Afrika.

Mkutano pia ulijadili Mamlaka ya Wakala wa Maendeleo ya Umoja wa Afrika (African Union Development Agency - AUDA). Mkutano ulifahamishwa kuwa mchakato wa kubadilisha Taasisi ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Uchumi (New Economic Partnership for Africa’s Development – NEPAD) kuwa AUDA utakamilika Februari 2019 kama inavyoelekezwa katika Maaumuzi ya Umoja wa Afrika Na. 691. Mkutano ulikubaliana na mapendekezo yote kuhusu Mamlaka ya AUDA na kwamba programu na miradi ya AUDA itafadhiliwa kupitia bajeti ya Umoja wa Afrika na misaada ya washirika wa maendeleo. 

Agenda nyingine iliyojadiliwa wakati wa mkutano huo ni mabadiliko katika Taasisi ya Mchakato wa Kujitathimini kiutawala Bora Africa (African Peer Review Mechanism - APRM), ambapo mapendekezo yalitolewa ya kuiunganisha APRM kuwa moja ya taasisi za Umoja wa Afrika na kugharamia shughuli zake kwa kutumia bajeti ya Umoja huo. Aidha, iliamuliwa kuwa Wanachama wote wa Umoja wa Afrika wawe Wanachama wa APRM na APRM iwe huru katika kutekeleza majukumu yake.

Agenda nyingine kuu iliyojadiliwa na kutolewa maamuzi ni mapendekezo ya makadirio mapya ya viwango vya kuchangia Umoja wa Afrika na mapendekezo ya adhabu kwa Nchi ambazo zitachelewa kulipa michango yake. Mkutano uliazimia kuitishwa kwa Mkutano kati ya Kamati ya Kudumu ya Mabalozi, Wataalam wa masuala ya Fedha kutoka nchi wanachama na Kamati ya Mawaziri wa Fedha kupitia makabrasha yote yanayohusu Viwango vya kuchangia na adhabu kwa nchi ambazo hazitoa michango yao kwa wakati. Mkutano huo, unatarajiwa kufanyika tarehe 28-29 Novemba, 2018, Addis Ababa, Ethiopia na mapendekezo ya wataalam yatawasilishwa kwenye Kikao kijacho cha Baraza la Mawaziri mwezi Februari 2019. 

Mkutano pia ulipokea mapendekeo ya mgawanyiko wa majukumu kati ya AU, Jumuiya za Kikanda na Nchi Wanachama. Mgawanyo wa majukumu unapendekezwa kuwezesha Jumuiya za Kikanda, Umoja wa Afrika na Nchi Wanachama kila moja kutekeleza majukumu yake na yale ambayo watachangia kwa pamoja. Pembezoni mwa Mkutano huho wa Dharura Wakuu wa Nchi na Serikali walizindua Mfuko wa Amani wa Umoja wa Afrika (AU Peace Fund) ambao utashughulikia masuala yote ya Amani na Usalama katika Nchi Wanachama ikiwemo viashiria vya uvunjifu wa Amani ili kuzuia kuibuka kwa migogoro. Mhe. Waziri alishiriki katika uzinduzi huo. 


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, 
Dodoma, 19 Novemba 2018 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika jijini Addis Ababa, Ethiopia. Nyuma yake ni Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Mhe. Bi. Naimi Aziz. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Rais Mpya wa Ethiopia, Mhe. Sahle Work Zewdu katika Ikulu ya nchi hiyo tarehe 18 Novemba 2018. Dkt. Mahiga alikwenda kumpongeza Mhe. Rais kwa kuteuliwa na wote wawili walisisitiza umuhimu wa kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Ethiopia. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga. (kushoto) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia, Mhe. Dkt Workneh Gebeyehu alipokwenda kumtembelea kwa ajili ya kufahamiana jijini Addis Ababa.

TUME YA TAIFA YA UMWAGILIAJI YATAKIWA KUHAKIKI ENEO LINALOFAA KWA KILIMO CHA UMWAGILIAJI NCHINI.

0
0
Naibu Waziri Wizara ya Kilimo Mhe. Omary Mgumba ameitaka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ishirikiane na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali na wataalam kutoka chuo kikuu cha ardhi kuhakiki eneo lenye ukubwa wa hekta 475,052 liloripotiwa na Tume hiyo kuwa linafaa kwa kilimo cha Umwagiaji nchini. 

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe. Mgumba ameyasema hayo alipofanya ziara katika ofisi za Tume Jijini Dar es Salaam ili kuongea na watumishi, ambapo aliwataka wao kama Tume washiriki kwanza kuhakiki eneo hilo na kuweza kutoa taarifa za uhakika. 

“Mnaweza kushirikiana na ofisi za kanda na halmashauri ili kuweza kurahisisha kufanyika kwa kazi hii , kwenye kilimo ni vyema tukaenda na mambo yote matatu, kilimo cha kutegemea maji ya mvua, kiimo cha kutegemea maji ya ardhini na kilimo cha kisasa cha umwagiliaji cha kutumia miundombinu, kilimo ambacho kitatuhakikishia uhakika wa chakula kwani ni kilimo ambacho mkulima analima zaidi ya mara moja kwa mwaka.” Alisema Naibu Waziri. 

Sambamba na hilo, Naibu Waziri ameitaka Tume pia kuwasilisha kwake taarifa ya utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi katika eneo la kilimo cha umwagiliaji kwa kipindi cha miaka mitatu ya serikali ya awamu ya tano na taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali. 

Awali akimkaribisha Naibu Waziri, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uenddelezaji wa Miundombinu ya Umwagiliaji Mhandisi Pascal Shayo alisema kumekuwa na ushiriki mdogo wa sekta binafsi kuwekeza katika miundombinu ya umwagiliaji ambapo mhandisi Shayo alieleza kuwa , kukabilina na changamoto hii Tume ina Mpango wa kuanzisha miradi ya ubia baina ya seka ya ya umma na sekta binafsi ili kuwavutia wawekezaji wengi zaidi katika kuendeleza miundombinu ya umwagailiaji na serikali itaendelea kuwajengea uwezo wataalam wake kwa kuwapatia mafunzo yanayohusu uwekezaji baina ya sekta ya umma na sekta binafsi na kuwe na uwekezaji kwa ajili ya kuongeza uelewa wa masuala ya ubia na manufaa yake kwa umma. 

Naibu Waziri Mgumba aliitembelea Tume ya Taifa ya Umwagailiaji akiwa na lengo la kufahamiana na watumishi kwani yeye ndiyo aliyepewa jukumu mahususi la kusimamia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe. Omary Mgumba akizungumza na watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, wakionekana baadhi katika picha jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Waziri Wizara ya Kilimo Mhe. Omary Mgumba akiongea na watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji wa Miundombimu ya Umwagiliaji Mhandishi Pascal Shayo, kulia ni katibu wa TUGHE tawi la Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Cretus Mbogo
Baadhi ya watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji katika kikao na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Omary Mgumba jijini kilichofanyika jijini Dar es Salaam leo.

DUCE YAENDESHA SEMINA MASUALA YA KIJINSIA NA RUSHWA YA NGONO KWA WANAFUNZI MWAKA WA KWANZA

0
0
Dk. Neema Gedion Mogha Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Elimu DUCE Chang'ombe jijinin Dar es salaam na Mkuu wa Idara ya Sayansi ya Viumbe Hai (Baiolojia) akifumgua semina ya Klabu za Jinsia (DUCE Gender Club) za wanafunzi wanaosoma katika chuo hicho iliyofanyika chuoni hapo mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo mada mbalimbali zilitolewa katika kuwajengea uwezo wanafunzi hao katika masuala ya kijinsia ili kujiepusha kufanya mambo mbalimbali yanayoweza kupelekea rushwa ya ngono.

Ikiwa ni pamoja na wanafunzi wanawake kujitoa bila woga katika masuala ya uongozi, katika picha kulia ni Bi. Upendo Mlungusye Msaidizi Mshauri wa Wanafunzi DUCE na kutoka kushoto ni Dorothea Fumpuni Mhadhiri na Mlezi wa klabu za Jinsia DUCE na Dk. Ikupa Moses Mratibu wa Kitengo cha Jinsia DUCE.
Dk. Neema Gedion Mogha Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Elimu DUCE Chang'ombe jijinin Dar es salaam na Mkuu wa Idara ya Sayansi ya Viumbe Hai (Baiolojia) akifafanua jambo wakati akifumgua semina ya Klabu za Jinsia (DUCE Gender Club) za wanafunziwa chuo hicho mwishoni mwa wiki iliyopita kulia ni Bi. Upendo Mlungusye Msaidizi Mshauri wa Wanafunzi DUCE na kushoto ni Dk. Ikupa Moses Mratibu wa Kitengo cha Jinsia DUCE.
Dk. Ikupa Moses Mratibu wa Kitengo cha Jinsia DUCE akimkaribisha Dk. Neema Gedion Mogha Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Elimu DUCE Chang'ombe jijinin Dar es salaam na Mkuu wa Idara ya Sayansi ya Viumbe Hai (Baiolojia) ili kufungua semina hiyo kutoka kulia ni Mhadhiri wa Chuo hicho Dk. Perpetua John Urio na Bi. Upendo Mlungusye Msaidizi Mshauri wa Mshauri wa Wanafunzi DUCE


Dk. Ikupa Moses Mratibu wa Kitengo cha Jinsia DUCE akizungumza katika semina hiyo.
Baadhi ya wanafunzi na wanachama wa klabu za jinsia Chuo Kikuu cha Elimu DUCE wakiwa katika semina hiyo
Baadhi ya viongozi wa klabu za jinsia chuoni hapo wakijitambulisha.
Dk. Neema Gedion Mogha Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Elimu DUCE Chang'ombe jijinin Dar es salaam na Mkuu wa Idara ya Sayansi ya Viumbe Hai (Baiolojia), kushoto Dk. Ikupa Moses Mratibu wa Kitengo cha Jinsia DUCE na Bi. Upendo Mlungusye Msaidizi wa Mshauri wa Wanafunzi DUCE wakifuatilia matukio katika semina hiyo.
Mmoja wa wanafunzi akionyesha kipaji chake katika kuimba wakati semina hiyo ikiendelea.
Msanii Finest akifanya vitu vyake katika semina hiyo.
Mhadhiri wa Chuo hicho Dk. Perpetua John Urio akitoa mada katika masuala ya kijinsia wakati semina hiyo ikiendelea.
Mwezeshaji Janeth Mawiza Mwenyekiti wa Taasisi ya WAJIKI akitoa mada kuhusu rushwa ya ngono kwa klabu za jinsia katika semina hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika chuo Kikuu cha DUCE jijini Dar es salaam
Mmoja wa wanafunzi na wanachama wa klabu za jinsia chuoni hapo akiuliza maswali katika semina hiyo.
Picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa semina hiyo.

WAZIRI JAFO AKABIDHI RASMI MASHINE MAALUMU ZA KUTIBU MAGONJWA MBALI MBALI HOSPITALI YA KISARAWE

0
0

Waziri wa chi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) kulia Selemani Jafo akikata utepe wakati wa sherehe ya kukabidhi mashine kwa ajili ya kutibu magonjwa mbali mbali katika hospitali ya Kisarawe, kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo
Mganga mkuu wa Wilaya ya Kisarawe kulia Jonathan Budenu akifafanua jambo kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Seleman Jafo mara baada ya kukabidhi mashine hizo katika hospitali ya Wilaya.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo akizungumza na wananchi hawapo pichana pamoja na wauguzi na madaktari katika halfa ya kukabidhiwa rasmi mashine maalumu kwa ajili ya kutibu magonjwa mbali mbali katika hospitali ya Wilaya ya Kisarawe.
Waziri wan chi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo kulia wakiwa na baadhi ya viongozi wengine wa serikali wa kati kati ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo na kushoto kwake ni Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Kisarawe Musa Gama katika halfa hiyo ya makabishiano ya mashine za kutibu magonjwa mbali mbali.

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo kushoto akimpatia maelezo mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Mussa Gama katika halfa hiyo ya makabidhiano ya mashine kwa ajili ya kutia magonjwa mbali mbali.(PICHA NA VICTOR MASANGU)



VICTOR MASANGU, KISARAWE

WAZIRI wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo amekemea vitendo vya upokeaji wa rushwa vinavyofanywa na baadhi ya wauguzi,wataalamu wa afya na madaktari kuwataka kuachana na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wahakikishe wanatoa huduma ya matibabu kwa wagonjwa kwa kuzingatia misingi ya weledi ya kazi yao bila kuwa na ubaguzi wowote.

Jafo alitoa kaul hiyo wakati akizungumza na wataalamu wa afya, pamoja na wananchi wakati wa sherehe za kukabidhi mashine maalumu kwa ajili ya uchunguzi wa magonjwa ya aina mbali mbali katika hospitali ya Wilaya ya Kisarawe ambapo viongozi wa serikali madiwani pamoja na viongozi wa dini waliweza kushiriki katika zoezi hilo.

Aidha Waziri Jafo alibainisha kwamba lengo kubwa la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inaboresha sekta ya afya kuanzia ngazi za maeneo ya vijijini kwa kuongeza ujenzi mpya wa zahanati, vituo vya afya pamoja na hospitali lengo ikiwa ni kuwaondolea adha wananchi katika suala zima la upatikanaji wa huduma ya matibabu kwa urahisi zaidi.

“Napenda kuchukua fura hii kuwambia ndugu zangu wananchi wa Kisarawe kwa kweli Rais wetu anafanya kazi kubwa sana ya kuhakikisha analeta maendeleo katika sekta mbali mbali hapa nchini na kwa sisi watu wa kisarawe tumepata bahati kubwa sana, kwa hiyo nipende kuwaambia tutaendelea kuboresha huduma ya afya katika zahanati zetu, vituo vya afya pamoja na ujenzi wa Hospitali nyingine mpya,”alisema Jafo.

Pia Jafo aliupongeza uongozi wa hospitali ya Wilaya hiyo pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe kwa kusirikiana kwa hali na mali mpaka kufanikisha kununua mashine hizo za kisasa ambazo zitaweza kutatua changamoto za wananchi ambao hapo awali walikuwa wanapata usumbufu mkubwa kuwenda kupata vipimo katika maeneo mengine.

Naye Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jonathan Budenu alisema hospitali ya Wilaya awali ilikuwa inakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo ukosefu wa vifaa tiba pamoja na upungufu wa watumishi kwa asilimia 36 huku akibainisha wamefanikiwa kununua mashine maalumu za uchunguzi wa magonjwa ambazo zimegharimu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 119 fedha ambazo zimetokana na makusanyo ya ndani ya hospitali hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate..amesema ataendelea kushirikiana bega kwa bega na viongozi wengine kwa lengo la kuweza kuwaletea mabadiliko chanya ya kimaendeleo wananchi wake hususana katika kuwaboresha huduma zaidi ya afya katika zahanati,vituo vya afya na kuongeza kuwa mipango waliyonayo ni kuifanya hospitali hiyo kuwa sehemu ya mfano katika nchi nzima.

“Jambo hili kwetu lina umuhimu mkubwa sana katika kuwaboreshea wananchi wetu huduma ya afya na kikubwa ni hapa tunamuunga Rais wetu Dr.John Pombe Magufuli katika kuhakikisha sekta ya afya inaboreshwa kwa kiwango cha hali ya juu ikiweo kununua vifaa tiba mbali mbali kama tulivyofanya katika hospitali yetu ya Wilaya kwa hiyo ni hatua kubwa”alisema Jokate.

Katika hatua nyingine Jokate amewataka wananchi wa Wilaya hiyo kuhakikisha wanajiunga katika bima ya afya ambayo itaweza kuwasaidia kupata matibabu kwa urahisi na kuondokana na kero ya kusumbuka kutibiwa pindi wanapokwenda hospitalini.

SERIKALI YAJENGA SEKONDARI YA MFANO KWA WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUM MKOANI ARUSHA

0
0
picha 1
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na wadau wa Elimu pamoja na wanafunzi wenye mahitaji maalum ( Hawapo Pichani) katika ufunguzi wa Bonanza la Kilimanjaro Committee for Sports iliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro.
P2
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akimpongeza mwanafunzi mwenye mahitaji maalum baada ya kufanya vizuri katika maonyesho ya mavazi katika ufunguzi wa Bonanza la Kilimanjaro Committee for Sports iliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro ambapo amesema kwa Mkoa wa Kilimanjaro
P3
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akimkabidhi cheti za kutambua mchango wa CCBRT wa udhamini wa Bonanza la Kilimanjaro Committee for Sports lililoshirikisha wanafunzi wenye mahitaji maalum, ambapo alitoa wito kwa wadau wa Elimu kuendelea kushiriki katika kuboresha Elimu Maalum
P4
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akibadilishana mawazo na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Walemavu) katika ufunguzi wa Bonanza la Kilimanjaro Committee for Sports iliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro ambapo amesema kwa Mkoa wa Kilimanjaro
P5-min
Wanafunzi wenye mahitaji maalumu wakiwa katika maandamano wakipita mbele ya Mgeni Rasmi Prof. Joyce Ndalichako (Hayupo Pichani) wakati wa ufunguzi wa Bonanza la Kilimanjaro Committee for Sports iliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro ambapo amesema kwa Mkoa wa Kilimanjaro iliyoshirikisha wanafunzi kutoka shule mbalimbali mkoani Kilimanjaro zenye wanafunzi wenye mahitaji maalum

.......................

Serikali inajenga Shule ya Sekondari Maalum ya mfano kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika Chuo cha Ualimu Patandi kilichopo mkoani Arusha yenye uwezo wa kudahili wanafunzi 600 kwa mara moja ikiwa ni mkakati wake wa kuongeza fursa za udahili kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum.

Kauli hiyo ya Serikali imetolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako katika ufunguzi wa Bonanza la Kilimanjaro Committee for Sports iliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro ambapo amesema kwa Mkoa wa Kilimanjaro, ambapo amesema Serikali imekarabati miundombinu kwenye shule kongwe ya Moshi Ufundi inayopokea wanafunzi wenye mahitaji maalum.

“Serikali inaendelea kutekeleza mipango mbalimbali inayolenga kuongeza upatikanaji wa fursa na kuimarisha ubora wa elimu inayotolewa katika ngazi zote kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu ambapo tayari serikali imekarabati miundombinu ya shule kongwe ya Moshi Ufundi ambayo inapokea wanafunzi wenye mahitaji maalumu”. Alisisitiza Prof. Ndalichako.

Waziri Ndalichako amesema watu wenye mahitaji maalum wana fursa sawa ya kushiriki katika michezo na kufanya hivyo kunasaidia kuondoa kasoro za kimwili na kiakili na baadhi ya ulemavu unaweza kurekebishwa kwa kushiriki katika michezo na burudani.

Prof Ndalichako amesisitiza kuwa ushiriki katika michezo, hususan kwa watoto wenye mahitaji maalum ni muhimu sana kama ilivyowekwa bayana katika kifungu cha 52 cha Sheria ya Watu wenye Ulemavu Namba 9 ya mwaka 2010 kinachosisitiza umuhimu wa Watu wenye ulemavu kushiriki katika michezo, starehe na burudani.

Akizungumza katika Bonanza hilo Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Walemavu) Stella Ikupa amewataka wanafunzi wenye mahitaji maalum kuunga mkono juhudi za serikali ya Awamu ya Tano kwa kuendelea kujitambua, kujikubali na kujituma ili kujikwamua katika changamoto wanazokutana nazo katika masomo yao.

Waziri Ikupa amewataka wanafunzi hao pia kujiunga na vyuo vya ufundi ambavyo vitawawezesha kupata satadi ambazo watazitumia kwa ajili ya kujiari wenyewe badala ya kuwa tegemezi.

Naye Mratibu wa Bonaza hilo ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum (Vyuo Vikuu) Esther Mmasi amesema wakati wa maandalizi ya Bonanza hilo amebaini kuwepo kwa uhaba wa viwanja vya michezo katika shule zenye wanafunzi wenye mahitaji maalumu ambapo ameiomba serikali kuhakikisha inaboresha miundominu ili kuwajengea uwezo wanafunzi hao.

MWANAFUNZI CHUO KIKUU AJISHINDIA BAJAJI DROO YA SPORTPESA

0
0


Mgaya Hassan akiwa na fungo yake baada ya kukabidhiwa kufuatia kushinda droo ya 43

TANGU ameanza kucheza SportPesa haikuchukua muda mrefu mpaka pale alipotangazwa kuwa ni mshindi wa Shinda Zaidi na SportPesa na kufanikiwa kushinda bajaj mpya kabisa kutoka timu ya ushindi Huyu ni Mgaya Hassan mshindi wa Droo Ya 43 yeye ni mwanafunzi wa chuo kikuu na mkoani Morogoro lakini ushindi wa bajaj umemkuta akiwa hapa jijini Dar es Salaam wakati akimalizia likizo yake kwa kaka yake. 
 
Na Timu Ya Ushindi haikutaka Kumcheleweshea Ilimfuata mpaka Bunju Hapa Dar es Salaam Nyumbani kwa Kaka Yake Na Kumkabidhi Bajaj. Akikabidhiwa bajaji ya ushindi Hassan alisema alianza kucheza na SportPesa baada ya kusikia kwenye redio na tv kuwa kuna bajaj zinatolewa na yeye moja kwa moja akijasajili na kuanza kutupia bashiri kwenye mechi mbalimbali hatimaye kufanikiwa kushinda.


"Mimi ni mwanafunzi nasoma SUA Morogoro taarifa hizi za ushindi zimenikuta hapa Dar es salaam wakati nikiwa likizo, nimefurahi sana maana wakati nacheza wanafunzi wenzangu waliniambia mimi siwezi kushinda kwa sababu naweka pesa ndongondogo waliamini kuwa wanaoshinda ni wale ambao hubashiri kwa pesa nyingi kumbe sivyo kila mtu ana nafasi ya kushinda maana mimi nilikuwa nacheza kwa elfu moja moja pekee sasa nimeshinda najua wakiniona ndio wataamini yani nina furaha sana" alisema Hassan Aidha Hassan anasema bajaji hii itamkomboa kutoka kwenye maisha ya sintofahamu na kuingia kwenye maisha mazuri huku akitegemea kipato kitakachopatikana kutokana na bajaj kumsaidia kwenye mahitaji yake ya chuoni na nyingine kuwawezesha ndugu zake ambao hawako vizuri kiuchumi.

"Daaah maisha ya chuo ni magumu sana unatoka chuo umechoka wakati mwingine huna pesa ya kula familia zetu nazo zinatoka katika mazingira ya kimaskini unajikuta huna cha kufanya lakini kwa ushindi huu wa bajaj ntaweza jikimu mimi mwenyewe maana kila siku ntakuwa na uhakika wa kupata chochote kutokana na bajaji hii" aliongeza Hassan. 
 
Hassan aliwaomba wanafunzi wenzake wa vyuoni wale ambao wamefikisha umri wa miaka 18 na zaidi kucheza na SportPesa maana wanaweza jikuta wakiandika historia mpya kwenye maisha yao na kumudu gharama ndogondogo zinazopatikana chuoni.

MAKAMU WA RAIS AMALIZA ZIARA MKOANI MANYARA NA KUREJEA DODOMA

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amemaliza ziara yake ya siku 5 mkoani Manyara. Akizungumza kwenye kikao cha majumuisho ambacho kilihudhuriwa na Viongozi na Watendaji wa mkoa huo Makamu wa Rais aliwapongeza kwa kazi nzuri wanayofanya na kuainisha maeneo kadhaa ambayo yanatakiwa kutupiwa jicho.

Baadhi ya maeneo hayo ni Mazingira ambapo aliuambia Uongozi huo kupanda miti ya kutosha, kulinda maeneo yanayochimbwa madini kuwa kuwasimamia wachimbaji katika kutunza mazingira pamoja na kutunza vyanzo vya maji. Eneo jingine alilozungumzia Makamu wa Rais ni suala zima la Lishe bora kwa watoto na kuhamasisha wananchi kuwa na Bima ya Afya.

Makamu wa Rais ameutaka Uongozi wa mkoa huo kuliangalia suala la mimba za utotoni ambalo kwa kiasi kikubwa linaupa mkoa sura mbaya ambapo mpaka sasa kwa mujibu wa ripoti zaidi ya watoto 4200 wamepata mimba wakiwa na umri mdogo.

“Njia pekee ya kuwalinda watoto wa Kike ni kuwapeleka shule”alisema Makamu wa Rais. Aidha Makamu wa Rais amehimiza umuhimu wa elimu kwa kushirikisha Mabaraza ya Wazee wa Makabila ili kuzuia mila potufu za ukeketaji. “Si rahisi kumuachisha mila yake lakini tukiwaelewesha na kuwaelimisha vizuri taratibu watatuelewa na kuacha kabisa”

Makamu wa Rais ameuambia Uongozi wa mkoa huo wafuate miongozo ya kazi “Kazi za Serikali zina Miongozo, Sheria na Kanuni tulizojiwekea” Mwisho, Makamu wa Rais aliushukuru uongozi huo na kuahidi kurudi tena kwenye Wilaya ambazo hakufika. Kwa upande mwingine Mkuu wa Mkoa wa Manyara amemshukuru Makamu wa Rais kwa kufanya ziara mkoani humo ambapo alisema ziara hiyo imekuwa na Mafunzo, Ushauri na Maelekezo ambayo wataenda kutakeleza kama walivyoambiwa.

Akiwa njia kuelekea Dodoma, Makamu wa Rais alisimama barabarani na kuwasalimia wananchi wa Kondoa waliojitokeza ambapo aliwaeleza azma ya Serikali ya kuendelea kutekeleza ahadi zake kwa wananchi na kuwapongeza kwa kupata barabara nzuri inayotoka Dodoma mpaka Babati.
 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi na Watendaji wa mkoa wa Manyara wakati wa kikao cha Majumuisho ya ziara yake kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa uliopo Babati mkoani Manyara. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Sehemu ya Viongozi na Watendaji wa mkoa wa Manyara wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara yako mkoani humo. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Alexander Mnyeti mara baada ya kumaliza kikao cha Majumuisho ya ziara yake na Viongozi pamoja na Watendaji wa mkoa huo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini Mhe. Flatei Massay mara baada ya kumaliza kikao cha Majumuisho ya ziara yake na Viongozi pamoja na Watendaji wa mkoa huo

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimu wakazi wa wilaya ya Kondoa wakati akiwa njiani kurudi Dodoma akitokea mkoani Manyara ambapo alikuwa kwenye ziara ya siku tano ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE AKUTANA NA MWAKILISHI WA HESHIMA WA TANZANIA, PERTH PAMOJA NA BALOZI WA KENYA NCHINI

0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza na Konseli wa Heshima wa Tanzania kwenye Jimbo la Perth nchini Australia, Bw. Didier Murcia alipofika kwenye Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam tarehe 19 Novemba, 2018 kwa lengo la kujitambulisha kwa Mhe. Naibu Waziri pamoja na kumweleza utekelezaji wa majukumu yake katika kuiwakilisha Tanzania, Perth. 
Ujumbe uliofuatana na Bw. Murcia. Kutoka kushoto ni Bw. James Chialo na Bw. Thierry Murcia kutoka Kampuni ya Ndovu Resources ya jijini Dar es Salaam 
Bw. Murcia akimweleza jambo Mhe. Dkt. Ndumbaro wakati wa mazungumzo yao 
Mazungumzo yakiendelea. Kulia ni Katibu wa Mhe. Naibu Waziri, Bw. Charles Faini.
Wakati huohuo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro alikutana kwa mazungumzo na Balozi wa Kenya nchini, Mhe. Dan Kazungu. Mazungumzo hayo yalifanyika kwenye Ofisi ndogo za Wizara zilizopo jijini Dar es Salaam tarehe 19 Novemba 2018. Pamoja na mambo mengine walizungumzia namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizi mbili hususan kupitia Jumuiya ya Afrika Mashariki. Pia Balozi Kazungu alitumia fursa hiyo kumweleza Mhe. Naibu Waziri kuhusu Mkutano wa Kimataifa kuhusu Rasilimali Endelevu za Majini utakalofanyika nchini Kenya kuanzia tarehe 26 hadi 28 Novemba 2018 
Katibu wa Naibu Waziri, Bw. Charles Faini (kushoto) akiwa na Bw. Medard Ngaiza, Afisa Mambo ya Nje wakifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Dkt. Ndumbaro na Mhe. Balozi Kazungu ambao hawapo pichani 
Mhe. Balozi Kazungu akimweleza jambo Mhe. Dkt. Ndumbaro wakati wa mazungumzo yao 
Mhe. Balozi Kazungu akimkabidhi Mhe. Dkt. Ndumbaro moja ya nyaraka kuhusu Mkutano wa Kimataifa wa Rasilimali Endelevu za Majini utakaofanyika nchini Kenya. 
Mhe. Dkt. Ndumbaro akiagana na Balozi Kazungu mara baada ya mazungumzo kati yao

MAGAZETI YA LEO JUMANNE NOVEMBA 20.2018

0
0
















MAHAFALI YA PILI YA CHUO CHA MANJANO BEAUTY ACADEMY YAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
Wahitimu wa Chuo cha Urembo cha Manjano wametunikiwa vyeti katika nyanja ya urembo na vipodozi (Cosmetology). Baadhi ya wahitimu waliofika kwenye mahafali hayo walivikwa taji kama ishara ya mafanikio ya kitaaluma, na kuweka alama kwenye hatua muhimu katika maendeleo yao ya kitaaluma kwenye tasnia ya urembo na vipodozi. Zaidi ya wanafunzi 87 wamehitimu kwa mwaka huu wa 2018 na wataendelea na mafunzo ya utarajali (internship program) kwa kipindi cha miezi 12 katika masalon, kampuni na taasisi mbalimbali zenye kujihusisha na urembo na vipodozi ili kuweza kujijengea ujuzi (skills) na uzoefu (experience) katika kazi zao. Sherehe ilizinduliwa na Mkufunzi kutoka VETA, Mwl. Salehe Omari, akimwakilisha Kaimu Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Dar es Salaam, mama Florence Kapinga. 
Mkuu wa Chuo cha Urembo mama Shekha Nasser akizungumza machache wakati wa mahafali ya pili ya Chuo cha Manjano Beauty Academy. Amewataka wanawake kujiongezea elimu ya matumizi sahihi ya Vipodozi na Urembo ili kuweza kutoa huduma sahihi na yenye ueledi kwa wananchi. Mama Shekha alisema Tanzania kuna upungufu mkubwa wa Wataalamu, hasa walimu wenye sifa za kufundisha elimu ya Urembo na Vipodozi, hivyo aliwashauri wanawake wengi kujiunga na Chuo cha Manjano Beauty Academy ili waendeleze tasnia hii na kuboresha huduma zao kwa wateja. Aidha alitaja changamoto kubwa alizokabiliana nazo wakati anaanzishi Chuo hicho ikiwemo ukosefu wa wataalamu wazawa wa maswala ya Urembo na Vipodozi. Akieleza zaidi alisema sekta ya urembo ina fursa kubwa kwa ajira na inaweza kusaidia kujiongezea kipato na kuondokana na ukosefu wa ajira na umasikini.Mgeni rasmi, uongozi wa Chuo cha Manjano Bauty Academy na Wahitimu wakiwa katika picha ya pamoja.
Mgeni rasmi, Mwl. Salehe Omari, naye pia aliwashukuru wanawake wa Kitanzania waliojiunga kwenye chuo hicho kwa lengo la kupata ujuzi wa maswala ya urembo na vipodozi. Alisema Urembo, Vipodozi na mitindo ni moja kati ya sekta zinazoajiri mamilioni ya wanawake kwa sasa, na kuchangia kwa kiasi kwenye pato la Taifa. Akiendelea zaidi alisema, elimu na mafunzo kwa vitendo (Vocational training) ni elimu na mafunzo ambayo yanayotoa ujuzi na elimu muhimu kwa ajili ya ajira. Elimu ya aina hii ni ambayo humuandaa mtu kufanya kazi katika fani mbalimbali, kama biashara, utengenezaji wa vitu, au kama fundi. 

Hivyo aliwausia wahitimu kuitumia vizuri elimu na ujuzi walioupata kwenye Chuo cha Manjano. Alielezea pia kwa kusema elimu ya ufundi na ujuzi ni muhimu katika kuleta usawa kwenye jamii kwani ni moja ya kitovu cha kuleta maendeleo na kuendana na kasi ya Awamu ya Tano ya Uchumi wa Viwanda. Elimu ya ufundi, stadi za kazi au wa kazi za mikono ni mojawapo ya vipaumbele vya UNESCO. Kwani elimu hii inasaidia kuendeleza elimu ya ubora na usawa na fursa za kujifunza kwa wakati wote ule haijalishi umri wako, “wewe ni mwanafunzi wa kudumu alisema.”
Tunawatakia wasomi wetu wote kila la kheri katika kazi zao. Mkuu wa Chuo cha Urembo Mama Shekha Nasser akizungumza.
Shekha ni mmiliki wa kampuni ya Shear Illusions na mnamo mwaka 2015, kupitia bidhaa za LuvTouch Manjano alianzisha chuo cha Manjano Beauty Academy kwa lengo la kutoa elimu na ujuzi wa kuwawezesha wasichana na wanawake kujiajiri na kujiongezea kipato kupitia tasnia ya Urembo na Vipodozi.

Taarifa za Utafiti wa Madini Zitolewe kwa Wananchi- Biteko

0
0

Meneja Mkuu wa kampuni inayojishughulisha na uchimbaji wa madini ya jasi ya General Business and Equipment Supply Limited iliyopo katika eneo la Bumbua wilayani Itigi mkoani Singida, Yusuph Kibira (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (katikati) mara alipofanya ziara katika eneo la mgodi huo.
Sehemu ya wachimbaji wadogo wa madini wakiwasilisha kero mbalimbali mbele ya Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (hayupo pichani) kwenye mkutano wa hadhara wa wachimbaji wadogo wa madini uliofanyika katika tarafa ya Mang’onyi iliyopo wilayani Ikungi mkoani Singida.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Mgodi wa Dhahabu wa Shanta uliopo wilayani Ikungi mkoani Singida
Kutoka kulia, Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Mtaturu walisikiliza kero mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa na wachimbaji wadogo kutoka katika tarafa ya Mang’onyi iliyopo wilayani Ikungi mkoani Singida kwenye mkutano wa hadhara. (hawapo pichani).
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Mtaturu akifafanua jambo kwenye mkutano wa hadhara wa wachimbaji wadogo wa madini uliofanyika katika tarafa ya Mang’onyi iliyopo wilayani Ikungi mkoani Singida.

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko akielezea mikakati ya Wizara ya Madini katika kuboresha shughuli za uchimbaji mdogo wa madini kwenye mkutano wa hadhara wa wachimbaji wadogo wa madini uliofanyika katika tarafa ya Mang’onyi iliyopo wilayani Ikungi mkoani Singida.




Na Greyson Mwase, Singida

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ameuagiza Mgodi wa Dhahabu wa Shanta uliopo katika wilaya ya Ikungi mkoani Singida kuhakikisha unatoa taarifa za tafiti zake zilizofanyika katika maeneo mbalimbali ili wachimbaji wadogo waweze kuzitumia katika kubaini madini yaliyopo na kuanza kuchimba kwa kufuata sheria na kanuni za madini.

Naibu Waziri Biteko alitoa agizo hilo leo tarehe 19 Novemba 2018 kwenye mkutano wa hadhara na wachimbaji wadogo wa madini uliofanyika katika tarafa ya Mang’onyi wilayani Ikungi mkoani Singida kama sehemu ya ziara yake katika mkoa huo yenye lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wachimbaji wa madini

Aliongeza kuwa Serikali kupitia Wizara ya Madini imeweka mazingira bora ya uchimbaji wa madini kwa wachimbaji wadogo ikiwa ni pamoja na kuwapatia taarifa mbalimbali za utafiti zilizofanywa na Wakala wa Utafiti na Jiolojia Tanzania (GST) na kampuni za utafiti wa madini lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa uchimbaji wao unakuwa wa uhakika na sio wa kubahatisha.

Akielezea maboresho mengine yaliyofanywa katika sekta ya madini, Biteko alisema Serikali imeboresha Sheria ya Madini inayotambua madini kama mali ya watanzania yanayosimamiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.Aliendelea kusema kuwa, Serikali imeweka mkakati wa kurasimisha wachimbaji wadogo wa madini wasio rasmi na kuwapatia leseni za madini ili uchimbaji wao ulete tija kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Biteko aliwataka wachimbaji wadogo wa madini kuunda vikundi na kupewa leseni ili waanze kuchimba na kulipa kodi serikalini.“Sisi kama Serikali kupitia Wizara ya Madini lengo letu ni kuhakikisha kuwa tunaweka mazingira bora kwa wachimbaji wadogo wa madini ili uchimbaji uongeze kasi ya ukuaji wa uchumi kupitia kodi na tozo mbalimbali,” alisema Biteko.

Wakati huohuo Biteko aliwataka wananchi wanaoishi karibu na Mgodi wa Dhahabu wa Shanta kutokuharibu miundombinu ya maji iliyowekwa ili iweze kunufaisha wananchi wote.Awali wakiwasilisha kero mbalimbali wakazi hao waliiomba Wizara ya Madini kuwapatia maeneo kwa ajili ya uchimbaji wa madini ili waweze kujiingizia kipato na kulipa kodi serikalini.Akizungumza kwa niaba ya wachimbaji wadogo wa madini katika tarafa ya Mang’onyi iliyopo wilayani Ikungi mkoani Singida, Consolata Joseph alisema kuwa uchimbaji wao umekuwa ni wa kubahatisha na hata kuvamia maeneo yenye leseni kubwa ya madini inayomilikiwa na Kampuni ya Dhahabu ya Shanta.

Aliongeza kuwa, kama wachimbaji wadogo wapo tayari kulipa kodi stahiki serikalini mara baada ya kupatiwa maeneo na kuanza kuendesha shughuli za uchimbaji wa madini.Awali akizungumza katika ziara hiyo, Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Shanta uliopo wilayani Ikungi mkoani Singida, Philbert Rweyemamu alisema mgodi umeshaanza kutoa fidia na kuongeza kuwa mpaka sasa umeshatoa shilingi bilioni 2.6 pamoja na ujenzi wa makazi mbadala ambapo mpaka sasa wameshajenga nyumba sita.

Aliongeza kuwa mpaka ifikapo mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka huu, mgodi unatarajia kukamilisha ujenzi wa nyumba nyingine sita na kufanya idadi ya nyumba kuwa 12 kama sehemu ya kuhakikisha wananchi wanaolipwa fidia wanaishi katika mazingira mazuri.Akizungumzia changamoto za mgodi wake, Rweyemamu alieleza kuwa ni pamoja na wachimbaji wadogo haramu kuvamia eneo la mgodi na kuchimba madini, miundombinu kuhujumiwa na baadhi ya wananchi kugomea fidia inayotolewa na kampuni hiyo.

WAZIRI MKUU AZINDUA MSIKITI NA KUSISITIZA UTUMIKE VIZURI

0
0

*Awataka waumini wautumie kwa kufanya ibada na kuhamasisha amani

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua msikiti wa Nandagala na amewataka waumini wa dini ya Kiislamu katika Kata ya Nandagala wilayani Ruangwa wautumie vizuri msikiti huo kwa kufanya ibada na kuhamasisha amani na si vinginevyo.

“Msikiti huu ninauzindua leo (jana) naomba tuutunze vizuri na tuutumie kwa kufanya ibada na si ibada za kiuanaharakati. Watakaokuja msikitini na kufanya mambo ya hovyo Mwenyezi Mungu atawalaani.”Waziri Mkuu alizindua msikiti huo jana jioni (Jumatatu, Novemba 19, 2018), ambapo alitumia fursa hiyo kuwasisitiza waumini wa dini ya Kiislamu kuhakikisha muda wa kufanya swala unapofika waende msikitini hapo kufanya ibada.

Kadhalika, Waziri Mkuu aliwataka waumini hao waanzishe madrasa na kuwafundisha watoto quran lengo likiwa ni kuwafundisha misingi ya dini na kuwaandaa vizuri na kuwawezesha kukua kiimani ili waje kuwa waja wema.

Hata hivyo, Waziri Mkuu alimshukuru Mzee Suleiman na familia yake kwa uamuzi wao wa kujitolea kujenga msikiti huo ambao utawawezesha waumini katika kijiji cha Nandagala kufanya ibada zao. “Namshukuru na Mzee Mamboleo na mkewe kwa kutoa eneo lao bure ili litumike kujengea msikiti.”

Kwa upande wake Sheikh Hilal Kipozeo ambaye alihudhuria uzinduzi wa msikiti huo aliwasisitiza waumini wa dini ya Kiislam watumie muda mwingi kwa ajili ya kufanya ibada na wajiepushe na vitendo vyenye kumuasi Mwenyezi Mungu na wadumishe amani.“Mtume Muhammad (S.A.W) baada ya kutoka katika mji wa Makka na kuhamia Madina kitu cha kwanza alijenga msikiti ili watu waweze kumwabudu Mwenyezi Mungu, alijenga soko ili watu washiriki shughuli za kiuchumi na alifanya upatanishi kwa makabila mawili kwa lengo la kuonesha kuwa kuishi kwa amani ni kitu bora.”

Wananchi na waumini wa dini ya Kiislamu katika kijiji cha Nandagala walimshukuru mfadhili aliyejenga msikiti huo kwa sababu utawawezesha kuwa na eneo la kufanyia ibada baada ya lile la awali kubomolewa kwa kuwa walijenga katika hifadhi ya barabara.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,JUMANNE, NOVEMBA 20, 2018.



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Msikiti wa Nandagala wilayani Ruangwa, Novemba 19, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishiriki katika dua iliyoongozwa na Sheikh Hilal Shaweji, maarufu Sheikh Kipozeo (watatu kulia) wakati alipozindua Msikiti wa Nandagala wilayani Ruangwa Novemba 19, 2018. Wapili kulia ni Mfadhili ambaye kwa pamoja na familia yake alijenga Msikiti huo, Mzee Suleyum Mohammed Ahmed. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi baada ya kuzindua Msikiti wa Nandagala wilayani Ruangwa, Novemba 19, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

PONGEZI ZA WAKULIMA WA KOROSHO WA KIJIJI CHA MTONYA B, WILAYANI TUNDURU KWA RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI

0
0

BENKI KUU YAFANYA OPARESHENI MAALUM YA UKAGUZI, UDHIBITI WA BIASHARA HARAMU YA FEDHA ZA KIGENI NA UKIUKAJI WA SHERIA KATIKA KUENDESHA BIASHARA YA UBADILISHAJI FEDHA

0
0

*Wenye maduka ya kubadilisha fedha waliokiuka sheria kukiona,leseni zao zatakiwa BoT
*Pia kuzuia kuendelea kwa ukiukaji wa sheria na kudhibiti uendeshaji wa biashara ya ubadilishaji fedha

Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

BENKI Kuu ya Tanzania(BoT) imesema imefanya oparesheni ya kushtukiza ya kukagua maduka ya ubadilishaji fedha na baadhi ya maduka bubu ambayo hayana leseni lakini yalikuwa yakiendesha biashara hiyo kinyume na sheria.

Operesheni hiyo iliratibiwa na Kitengo cha Ukaguzi cha Benki Kuu katika kutekeleza majukumu yake kisheria na kwamba hiyo ni oparesheni ya tatu kufanyika. 

Akizungumza leo Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania amesema uchunguzi wa kina katika miezi sita iliyopita ulibaini kuongezeka kwa biashara za kubadilisha fedha kinyume cha sheria, na kukua kwa biashara haramu ya fedha za kigeni na utakatishaji fedha, hususan kupitia maduka ya kubadilisha fedha.

Amesema BoT kupitia juhudi za Kitengo cha Ukaguzi kuwapata wahusika hazikuzaa matunda katika oparesheni mbili zilizopita. Hiyo ni kwa sababu iligundulika kuwa kuna mtandao mpana na madhubuti wa shughuli hizo na ambao ulilenga kuhakikisha kuwa shughuli za udhibiti hazifanikiwi. Baada ya mashauriano na wataalam na kushirikisha vyombo vya upelelezi na usimamizi ilionekana kuwa ili kufanikisha operesheni hiyo lililokusudiwa ni muhimu wahusika wote wadhibitiwe kwa wakati mmoja na kufanyiwa ukaguzi.

" Hii ilihitaji ushiriki wa maofisa wengi sana kutoka vyombo mbalimbali na kuhakikisha kila mahali ambapo ukaguzi uliendeshwa kuna usalama wa kutosha na Wananchi wanaarifiwa kutoingia sehemu husika kwa wakati huo. Baadhi ya washiriki katika zoezi hilo ni askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania wakiwa katika sare zao bila silaha.

"Hii ni kwa sababu siku oparesheni ilipofanyika askari wengi wa Jeshi la Polisi wapo kwenye kusimamia usalama katika vituo vya mitihani ya kidato cha pili inayoendelea," imeeleza taarifa hiyo ya BoT.Napenda kuwaarifu wananchi kuwa oparesheni hii imeisha salama na bila kuathiri mtu yeyote na tunawashukuru wananchi wa Jiji la Arusha kwa ushirikiano, hasa kwa kuwa watulivu,"amesema.

Amefafanua taratibu zinazoendelea ni za kisheria na kwamba mahojiano na wahusika yanakamilishwa na wale watakaokutwa na tuhuma za ukiukaji sheria watashughulikiwa kufuatana na taratibu za kisheria. Aidha amesema Benki Kuu inachukua hatua zifuatazo kuzuia kuendelea kwa ukiukaji wa sheria na kudhibiti uendeshaji wa biashara ya ubadilishaji fedha. Kwa takribani miezi mitatu sasa benki hiyo imesitisha utoaji wa leseni za biashara ya ubadilishaji fedha. 

Gavana amesema maombi yote yamesitishwa na maombi mapya hayatapokelewa mpaka taratibu mpya za uendeshaji wa biashara hiyo zitakapokuwa tayari na kusisitiza Wale wote watakaopatikana na makosa ya uvunjaji wa sheria leseni zao zitafutwa na hawataruhusiwa kufanya biashara hiyo tena. 

"Katika kipindi hiki wakati kesi zao zinashughulikiwa kisheria na ili kuzuia kuendelea kwa biashara haramu, leseni zao zinasitishwa na wanatakiwa kuzirudisha Benki Kuu mpaka kesi zao zitakapokamilika.

" Baada ya hapo taratibu mpya zitatumika;

Wale wote ambao walipatikana na tuhuma za ukiukaji sheria katika oparesheni mbili zilizopita na kufikishwa Polisi, wanatakiwa kurejesha leseni zao Benki Kuu mara moja. Leseni hizo pia zinasitishwa mpaka kesi zao zitakapokamilika;

Uchunguzi uliofanyika umebaini waendeshaji wengi wa maduka ya kubadilisha fedha hawakukidhi vigezo vyote japokuwa leseni zilitolewa kwao baada ya taarifa kupotoshwa,"amefafanua.Amsisitiza hao wote watapewa notisi ya kusitisha leseni na maduka yao kufungwa. Yeyote ambaye anajua kuwa upatikanaji wa leseni yake una dosari anashauriwa kurejesha leseni hiyo kwa hiari; na

Wale ambao wanaendesha maduka ya kubadilisha fedha bila leseni au kwa kutumia leseni zisizo zao wanatakiwa kufunga maduka hayo mara moja kabla hawajafikiwa na mkono wa sheria. "Ili kuzuia watu wasiostahili kupenyeza na kujipatia leseni za biashara ya ubadilishaji fedha Benki Kuu imefanya mabadiliko ya ndani na inakamilisha taratibu mpya kuhusu uendeshaji wa biashara hiyo. Taarifa itatolewa hapo baadaye.

"Kwa vile oparesheni hii sasa inaingia katika hatua za kisheria zinazoweza kupelekea baadhi ya wahusika kupelekwa mahakamani, Benki Kuu haitaendelea kutoa taarifa zinazowahusu wahusika kwa sababu kwa kufanya hivyo kunaweza kupelekea kuingilia uhuru wa Mahakama," amesema Gavana wa Benki Kuu.

KANYASU AWATOA HOFU WATUMISHI JUU YA MASLAHI YAO BAADA YA UJIO WA JESHI USU

0
0

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu (wa pili kushoto) akimsikiliza Mhifadhi ,kuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya enoe la n Ngorongoro, Dkt.Freddy Manongi wakati alipowatembelea jana katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa ajili ya kuzungumza na kuwasikiliza watumishi wa Mamlaka hiyo juu ya changamoto mbalimbali zinazowakabili ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu ( kushoto) akipewa maelezo na Dkt. Maurus Msuha (katikati) wakiwa kwenye sehemu ya kuonea wanyamapori (View point) ya Ngorongoro Kreta wakati alipotembelea jana kwa ajili ya kuzungumza na kuwasikiliza watumishi juu ya changamoto mbalimbali zinazowakabili ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu ( wa kwanza kushoto) akiwa ameongozana na Menejimenti ya Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro akipewa maelezo wakati alipotembelea jana kabla ya kuzungumza na kuwasikiliza watumishi wa Mamlaka hiyo juu ya changamoto mbalimbali zinazowakabili ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi
Watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu wakati alipowatembelea jana.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akiwa na baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro wakiamungalia Faru mwenye umri wa miaka 65 ambaye ni faru mzee duniani

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akisalimiana na Kanali Martin Kilugha mara baada ya kuwasili kati geti kuu la kuingia Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro .
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akipewa maelezo na Juma Hamadi jinsi mfumo wa malipo unavyofanya kazi kwa watalii wanaoingia katika Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (PICHA NA LUSUNGU HELELA-WMU)

NA LUSUNGU HELELA .

Naibu Waziri Wizara ya Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amewatoa hofu watumishi wa Taasisi zenye jukumu la kulinda na kuhifadhi Wanyamapori na Misitu nchini kuwa hakuna maslahi yao yatakayobadilika baada ya ujio wa Jeshi Usu
 
Naibu Waziri Kanyasu ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro ikiwa ni mara yake ya kwanza kukutana na watumishi hao tangu alipoteuliwa kushika wadhifa wa Naibu Waziri katika Wizara hiyo nyeti kwa uchumi wa nchi. Amesema ziara yake imelenga kuzifahamu Taasisi anazoziongoza ili kujua namna zinavyotenda kazi na changamoto zinazowakabili ili kuzipatia ufumbuzi. 

Akizungumza kuhusu utendaji wa Jeshi USU, Naibu Waziri Kanyasu amesema kufuatia mabadiliko ya mfumo wa utendaji kutoka katika mfumo wa kiraia na kuwa Jeshi USU kutakuwa na mabadiliko kiutendaji yatakayoendana na taratibu za Jeshi USU lakini utakaoheshimu na kulinda maslahi ya watumishi. 

Naibu Waziri huyo ameeleza kuwa, uanzishwaji wa Jeshi hilo haukusudii kubadili maslahi ya watumishi hao na endapo maslahi hayo yatabadilika basi yatakuwa na mabadiliko chanya kwao. Naibu Waziri Kanyasu ameongeza kuwa Jeshi USU litaongeza nidhamu uwajibikaji na maadili kwa watumishi wa sekta ya Maliasili na Utalii ili waweze kusimamia ipasavyo uhifadhi endelevu wa maliasili na si vinginevyo. 

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Kanyasu ameiagiza Menejimenti ya Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro ibuni vivutio vipya vya Utalii vitakavyosaidia kuongeza mapato kwa Serikali kwa kuzingatia majukumu makuu ya Taasisi. 
 
Kwa upande wake, Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro, Freddy Manongi amewahakikishia watumishi hao kuwa maslahi yao hayatabadilika na ikiwezekana yataongezwa kwa sababu uwajibikaji utaongezeka baada ya ujio wa Jeshi Usu Ameongeza kuwa mfumo wa Jeshi Usu haumaanishi kuwa Watumishi hawapaswi kupewa maslahi yao na badala yake yanahitaji kuboreshwa zaidi ili waweze kuwa na ari ya kufanya kazi katika kulinda Wanyamapori na Misitu nchini. 

” Kati ya masuala ambayo nayapigania yasiweze kubadilika baada ya ujio wa Jeshi Usu ni maslahi yenu” amesema Dkt. Manongi. Jeshi USU lilizinduziwa rasmi tarehe 17 Novemba mwaka huu na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan katika Uwanja wa Fort Ikoma wilayani Serengeti mkoa wa Mara.

Bunge la China lasifu Juhudi za Serikali za Ujenzi wa Miradi

0
0

 Makamu wa Rais wa Bunge la Jamhuri ya Watu wa China Mhe. CAI Dafenga akipunga mkono wakati alipotambulishwa  Bungeni mapema leo Jijini Dodoma. Wa pili toka kulia ni Naibu Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Balozi wa China nchini Bi. WANG wa kwanza kulia. Makamu huyo wa Rais ametembelea Bunge la Tanzania akiambatana na Wabunge kumi na tano kwa lengo la kudumisha ushirikiano baina ya pande zote mbili.
…………………..

Na Grace Semfuko-MAELEZO
Bunge la Jamhuri ya Watu wa China limepongeza kasi ya ujenzi wa Miradi inayofanywa na Serikali  ya Tanzania na kwamba ushirikiano uliopo baina ya China na Tanzania utaendelea kuimarishwa ili kuzifanya nchi hizo kuzidi kuwa na maendeleo ya kuichumi

Hayo yamebainishwa na Makamu wa Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya watu wa China Bw. Cai Defang alipotembelea Darala la Nyerere Kigamboni Jijini Dar Es Salaam lililojengwa na Kampuni ya China Railway Jiangchang Engineering CRJE na China Major Bridge Engineering Company  ujenzi ulioanza mwaka 2012 na kukamilika April 2016.

Daraja hilo linalovuka mkondo wa maji wa Kurasini hadi Kigamboni  Jijini Dar Es Salaam lina urefu wa mita 680 na njia sita za kupitishia magari ni daraja kubwa katika nchi za Afrika Mashariki na lilizinduliwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli April 19 mwaka 2016 na kupewa jina la Julius Nyerere kwa heshima ya Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Ujenzi wa Daraja la Nyerere ulibuniwa na Serikali lengo likiwa ni kupunguza msongamano wa magari uliokuwepo katika kivuko cha Magogoni Jijini Dar Es Salaam na kurahisisha usafiri lengo ni kuwaondolea watanzania changamoto kwenye sekta ya usafirishaji.Akizungumza katika ziara hiyo Makamu Mwenyekiti huyo wa Bunge la Jamhuri ya Watu wa China Cai Defang amesema ni muda muafaka sasa kwa daraja hilo kutumika kama njia za kiuchumi kwa watu wa Tanzania.

“Nimefurahishwa na ujenzi wa Daraja hili uliojengwa na Kampuni ya CRJE ya wachina,wamefanya kazi nzuri, kwa Tanzania daraja hili ni fursa za kiuchumi kwani litarahisisha usafirishaji na kuepukana na vikwazo vilivyokuwepo awali kabla ya dara hili” alisema Cai Defang Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya watu wa China.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la hifadhi ya jamii la NSSF Bw. William Erio amesema kukamilika kwa daraja hilo kumekuwa na manufaa makubwa kwa Serikali kwani limekuwa likiingizia Serikali mapato yatokanayo na kuvusha magari fedha ambazo zimekuwa zikienda kufanya shughuli zinazoinufaisha jamii ya kitanzania.

“Tunashukuru Serikali kuendelea kubuni miradi mbalimbali ya kimaendeleo ambayo inasaidia jamii kwa asilimia mia moja,mfano daraja hili ni moja ya vyanzo vya kiuchumi kwani fedha za makusanyo hapa zinasaidia kuongeza kasi ya kuhudumia jamii kupitia ujenzi wa miradi mingine” alisema William Erio wakati akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya watu wa China alipotembelea kwenye mradi huo wa daraja.

RAIS DK.SHEIN AJUMUIKA NA WAUMINI WA DINI YA KIISLA KATIKA SHEREHE ZA MAULIDI YA KUZALIWA MTUME (S.A.W) VIWANJA VYA MAISARA SULEIMAN ZANZIBAR

0
0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Rais Mstaaf wa Tanzania Mhe. Ali Hassan Mwinyi, alipowasili katika viwanja vya Maisara Suleiman, katika hafla ya Maulid ya Kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W ), Maisara Zanzibar.jana usiku 19-11-2018.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Viongozi wa jukwaa kuu wakiwa wamesimama wakati ikisomwa Qaswida ya Kumtakia Rehema Mtume (S.AW) kabla ya kuaza kwa hafla hiyo ya Maulid yaliofanyika katika viwanja vya Maisara Suleiman Zanzibar jana usiku.19-11-2018.

NAIBU Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Hassan Othman Ngwali, akizungumza na kutowa maelezo ya hafla hiyo ya Maulid ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW) yaliofanyika katika viwanja vya Maisara Suleiman Zanzibar jana usiku,19-11-2018.

MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwa na Wake wa Viongozi na Wananchi akihudhuria Maulid Matukufu ya kuazaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika katika viwanja vya Maisara Suleiman Zanzibar jana usiku.19-11-2018.

WAUMINI wa Dini ya Kiislam Zanzibar wakihudhuria hafla ya Maulid Matukufu ya Kuzaliwa Mtume Muhammad(S.A.W) yaliofanyika katika viwanja vya mpira vya Maisara Suleiman Zanzibar usiku tarehe 19-11-2018.

MUFTI Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Saleh Omar Kabi akiongoza dua ya ufunguzi wa Maulid ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika viwanja vya mpira Maisara Suleiman Zanzibar, kulia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk Alhajj Ali Mohamed Shein na kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi.

/WANAFUNZI wa Madrassa Nouru’l Iman kutoka Karakana Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, wakisoma Qaswida wakati wa hafla ya Maulidi ya Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika Kitaifakatika viwanja vya Maisara Suleiman Zanzibar jana usiku 19-11-2018

RAIS DKT. MAGUFULI AAHIRISHA MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA UHURU

0
0







Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza kuhusu uamuzi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli wa kuahirisha Maadhimisho ya sherehe za Uhuru yaliyotarajiwa kufanyika 9 Desemba, 2018, Kwenye ukumbi wa Mkuu wMkoa wa Lindi, Novemba 20, 2018. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi

………………..

*Aagiza fedha zilizotengwa zikatumike katika kujengea hospitali Dodoma

Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameahirisha maadhimisho ya siku ya Uhuru, Disemba 9, 2018 na fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya kufanikisha shamrashamra hizo ameelekeza zitumike kujenga hospitali mkoani Dodoma ambayo itaitwa Uhuru Hospitali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo (Jumanne, Novemba 20, 2018) na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Rais Dkt. Magufuli ameagiza kiasi cha shilingi milioni 995.182 zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya kufanikisha sherehe hizo zitumike kwa ajili ya ujenzi wa hospitali mkoani Dodoma.

Waziri Mkuu ametoa taarifa hiyo wakati alipokutana na viongozi waandamizi wa mkoa wa Lindi pamoja na wilaya zake katika kikao cha maandalizi ya shughuli za kuzima Mwenge kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano kwenye ofisi wa Mkuu wa Mkoa wa Lindi. Amesema hospitali hiyo itakayojengwa katika eneo la kati ya barabara ya kwenda Hombolo na Chamwino kwenye barabara ya kwenda Dar es Salaam itakuwa inawahudumia wakazi wa mkoa wa Dodoma pamoja na wananchi wengine watakaokuwa mkoani humo.

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema Rais Dkt. Magufuli amewaagiza wakuu wa mikoa na wilaya waandae matukio watakayoyatekeleza katika maeneo yao yatakayoashiria maadhimisho ya siku ya Uhuru. “Wanaweza kutumia siku hiyo kwa kufanya usafi maeneo ya wazi au kwenye hospitali.”

Kufuatia maagizo hayo, Waziri Mkuu amewataka wananchi katika maeneo yote nchini wajiandae kufanya shughuli mbalimbali za kijamii zitakazopangwa na wakuu wao wa mikoa na wilaya kufanyika katika maeneo yao.

MAKAMU WA RAIS AZINDUA MASHINDANO YA SHIMMUTA JIJINI DODOMA

0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akipungia mkono maandamano ya washiriki wa mashindano ya SHIMMUTA wakati yakiingia katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Timu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania wakipita mbele ya mgeni rasmi wakati wa sherehe za uzinduzi wa mashindano ya SHIMMUTA jijini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa mashindano ya michezo ya SHIMMUTA jijini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwasalimia wachezaji wa timu ya mpira wa pete (Netball) ya Geita Gold Mine wakati wa uzinduzi wa mashindano ya SHIMMUTA kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwasalimia wachezaji wa timu ya mpira wa pete (Netball) ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wakati wa uzinduzi wa mashindano ya SHIMMUTA kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

……………………….

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Wakuu wa Mashirika na Taasisi kutenga fedha kwa ajili ya michezo.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo kwenye uzinduzi wa Mashindano ya SHIMMUTA uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. “Kwa Wakuu wa Taasisi, kwa kuwa kalenda za michezo hii inajulikana ni vyema mkahakikisha bajeti zinapangwa mapema” alisema Makamu wa Rais.

Akiwa Mlezi wa SHIMMUTA Makamu wa Rais amesema angependelea kuiona SHIMMUTA ya 2019 ikiwa sawa na ya miaka ya 60 ambapo timu zaidi ya 60 zilishiriki. Makamu wa Rais ametoa rai kwa Taasisi, Mashirika na Makampuni kuwajibika kikamilifu kuhakikisha mashindano haya yanakuwa endelevu ikiwa pamoja na kupata mbinu mbadala za kupata washirika zaidi wa kugharamia michezo hii.

Kaulimbiu ya mwaka huu inasema ‘ufanisi katika utendaji kazi hutegemea afya bora ya wafanyakazi, tuhumize michezo sehemu za kazi’ Timu 21 zinashiriki SHIMMUTA ya mwaka huu na michezo yote itachezwa kwenye viwanja vya michezo vya chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Kwa upande mwingine Naibu Waziri wa Michezo, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Julliana Shonza amesema Wizara yake inatambua uwepo wa mashindano hayo na kutoa pongezi kwa kamati iliyoanda michezo hiyo mwaka huu. Wakati huo huo Mwenyekiti wa SHIMMUTA Dkt. Hamis Mkanachi amesema michezo hiyo ilianzishwa mwaka 1967 ikiwa na lengo la kuhimiza michezo sehemu za kazi na kuwaweka Watendaji, Taasisi na Mashirika na kudumisha mahusiano na kutangaza shughuli za Taasisi zao.

Katika ufunguzi wa leo timu ya mpira wa miguu TPDC na Geita Goldmine walifungua dimba wakati kwa upande wa mpira wa pete (netball) timu ya Chuo Kikuu Dodoma na Geita Goldmine zilifungua dimba.

NDITIYE AMEITAKA MAMLAKA YA BANDARI TANZANIA KUSITISHA MPANGO WAKE WA KURASIMISHA BANDARI BUBU ZA DAR ES SALAAM

0
0

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kulia) akipata maelezo kuhusu bandari bubu kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Zainabu Kawawa (mwenye koti nyekundu) wakati wa ziara yake ya kukagua bandari bubu hizo wilayani humo. Anayesikiliza ni Msimamizi wa Bandari ya Bagamoyo, Witharo J. Witharo
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati) akitoa maelekezo kwa Msimamizi wa Bandari ya Bagamoyo, Witharo J. Witharo (wa kwanza kulia) kuhusu kudhibiti bandari bubu zilizopo wilayani Bagamoyo wakati wa ziara yake kwenye bandari hizo
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akitoa maelekezo kwa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Bagamoyo kuhusu kudhibiti bandari bubu zilizopo wilayani humo wakati wa ziara yake ya kukagua bandari hizo



Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye ameitaka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kusitisha mpango wake wa kurasimisha bandari bubu zilizopo mkoa wa Dar es Salaam

Hayo yameelezwa na Nditiye wakati wa ziara yake Wilayani Bagamoyo ya kukagua bandari bubu zilizopo ambapo amebaini uwepo wa bandari bubu zaidi ya kumi na tisa zinazosafirisha bidhaa kwenye eneo la mwambao wa bahari lililopo wilayani Bagamoyo. Amesema kuwa uwepo wa bandari bubu hizo ni kipenyo cha baadhi ya wafanyabiashara kukwepa kulipa kodi kwa kutumia bandari rasmi na hivyo kupunguza mapato ya Serikali na kuihujumu nchi kwa kufifisha jitihada za Serikali za kufikia uchumi wa kati na azma yake ya ujenzi wa viwanda, utoaji wa huduma za afya, elimu, maji, umeme na ujenzi wa miudombinu ya sehemu mbali mbali nchini

Nditiye ameielekeza TPA iache mara moja mpango huo wa kurasimisha bandari bubu zilizopo Mbweni na Temeke kwa kuwa Dar es Salaam ipo bandari na itumike hiyo kwa shughuli za usafirishaji wa bidhaa na abiria. “TPA wafute mara moja mpango wao wa kurasimisha bandari bubu za Mbweni, Temeke kuwa bandari rasmi wakati kuna bandari ya Dar es Salaam,” amesema Nditiye. Pia, ameongeza kuwa fedha zilizotengwa na TPA kwa ajili ya mpango huo lipewe jeshi la bandari ili waweze kununua vifaa kwa ajili ya kufanya doria ya kuimarisha ulinzi kwenye mwambao wa bandari

Amefafanua kuwa yapo majahazi yanayofanya shughuli za usafirishaji ufukweni mwa bahari ya Hindi kwenye mwambao upatao kilomita 300 kwenye eneo la Bagamoyo ambapo majahazi yanashusha mizigo kinyemela. “Nimeshuhudia taratibu za nchi zikikiukwa na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Bagamoyo inapata changamoto ila inawadhibiti kwa namna moja au nyingine japo yapo majahazi yanayoshusha bidhaa na kuficha kwenye misitu iliyopo ndani ya bahari,” amesema Nditiye.

Pia ameielekeza Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini (TASAC) kufanya utaratibu wa kusajili majahazi yasiyozidi ishirini kwenye eneo la Bagamoyo ili yaweze kuwahudumia wananchi wa Bagamoyo na wengine wote watumie bandari Dar es Salaam. “Yapo baadhi ya majahazi yamesajiliwa ila mengine yanafanya shughuli zake kinyemela na yanaenda sehemu mbali mbali na baadhi yao wasio waaminifu wanatumia vibaya vibali vyao na wanashusha mizigo baina ya saa tano na saa tisa usiku,” amesema Nditiye. Amefafanua kuwa majahazi haya yanakiuka taratibu za nchi kwa kuwawezesha wafanyabiashara kukwepa kodi na hivyo kupunguza mapato ya Serikali na jitihada za Serikali za kufikia uchumi wa wakati

Naye Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Zainabu Kawawa amekiri uwepo wa bandari bubu zaidi ya 19 na amemweleza Nditiye kuwa wilaya hiyo inakabiliwa na changamoto za uwepo wa bandari bubu ambazo zinatumia usafiri wa majahazi kuvusha bidhaa mbali ili kukwepa ushuru wa mamlaka mbali mbali kwa mujibu wa sheria za taasisi husika ambapo wanavusha sukari, mafuta ya kula, matairi ya magari, maziwa ya unga, vitenge, khanga, vipodozi na wahamiaji haramu ambapo hadi sasa kuna wafungwa wapatao 203 waliopo gerezani kutokana na uwepo wa wahamiaji haramu.

Kawawa amefafanua kuwa majahazi hayo yanashusha mizigo nyakati za usiku wakiwa ndani ya bahari mara nyingine bila kufika ufukweni kwa kufaulisha na kupakia kwenye mitumbwi ijulikanayo kwa jina maarufu la ngwanda ili iweze kufikishwa nchi kavu kwa ajili ya kusambazwa kwenye maeneo mbali mbali ili kukwepa kodi.
 
 Amesema kuwa kamati ya ulinzi na usalama imekuwa ikifanya doria kwenye maeneo hayo ili kudhibiti jambo hilo japo wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa vifaa vya kufanya doria baharini na uwepo wa baadhi ya watumishi wa umma wachache wasio waaminifu ambao wanashirikiana na wafanyabiashara kuihujumu Serikali kwa kutumia bandari bubu zinazotokana na uwepo wa bahari ya Hindi wilayani humo ambapo bandari bubu hizo ni pamoja na bandari bubu ya Mlingotini, Kasiki, Kaole, Magambani, Kilimani, Badeco, Msalabani, Nunge, Mtailindi, Jicho Kuu, Mto Ruvu, Razaba, Gama, Kayanjo – shamba la chumvi, Saadani, Kitongoji cha Gwaza, Changwahela na Duza

Naye mmoja wa wamiliki wa majahazi Khatib Ayubu Mwagala wa bandari bubu ya Mlingotini amekiri kuwa majahazi yanatumika kusafirisha mizigo na abiria ambapo amesema kuwa, “naweza kusafirisha wahamiaji waharamu 100 kwa mara moja na bidhaa kama vile mkaa, mbao na mafuta ya kula”. Aidha, mkazi wa Bagamoyo mzee Ali Nassir Issa amesema kuwa amekuwa akishuhudia mizigo mingi inashushwa kama vile viongozi wa mamlaka husika hawaoni na wanakosa mapato.

Naye Afisa Mfawidhi Msaidizi Bagamoyo, Noel Makere amesema kuwa katika Wilaya ya Bagamoyo kuna bandari bubu nyingi na ni changamoto katika ukosefu wa mapato. “Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ina kitengo cha kudhibiti magendo kinachofanya doria kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi hasa nyakati za usiku ili kudhibiti hali hii,” amesema Makere. Ameongeza kuwa tumefarijika kwa maelekezo aliyotoa Naibu Waziri Nditiye kwa kamati ya ulinzi na usalama na suala la usajili wa vyombo hivyo itatusaidia kusimamia, kufuatilia na kuvitambua vyombo halali na visivyo halali na itasaidia kukusanya mapato ya Serikali.

Naye Msimamizi wa Bandari ya Bagamoyo, Witharo J. Witharo amesema kuwa bandari bubu ya Mlingotini ina majahazi na mitumbwi midogo maarufu kwa jina la vingwanda ambapo inatumika kusafirisha bidhaa kinyume na taratibu. Witharo ameiomba Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) makao makuu iwapatie boti ya doria kwa kuwa fukwe hiyo iko wazi na kuna misitu ambapo bidhaa za magendo zinapitishwa humo. Pia, ametoa rai kwa wateja kufika bandarini na kutumia huduma za bandari zilizo rasmi na kulipa kodi kwa maendeleo ya taifa letu
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live




Latest Images