Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1727 | 1728 | (Page 1729) | 1730 | 1731 | .... | 1897 | newer

  0 0

  BENKI ya Biashara ya DCB ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu, Godfrey Ndalahwa,  wametembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma ikiwa ni muendelezo kampeni ya kuhamasisha uuzaji wa hisa zake kwa Wabunge na watanzania wote.

  Akizungumza wakati akimtambulisha Mkurugenzi mtendaji  huyo pamoja na ujumbe wake, Spika wa Bunge Job Ndugai aliwatangazia wabunge hao taarifa za uzinduzi huo na ya kwamba hisa zinaweza kununuliwa katika matawi ya benki hiyo, mawakala wa Solo la Hisa (DSE) kwa bei pungufu ya shs 265 na ya kwamba benki hiyo sasa ni benki ya biashara.

  DCB ilizindua zoezi la kuuza hisa zake Novemba 12 mwaka huu huku mwanahisa namba moja Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa akiwa mteja wa kwanza  kujitokeza kununua hisa.

  0 0

  0 0

  NA WAMJW-IRINGA 

  SERIKALI kupitia Wizara ya afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imerahisisha ukusanyaji wa takwimu za vifo vinavyotokea kwenye ngazi ya jamii nchini kwa kugawa vifaa maalumu vya kukusanyia takwimu hizo kwa Maafisa afya katika kata za mkoa wa Iringa. 
   
  Hayo yamezungumzwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendelo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Afya) Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati akikabidhi Kompyuta Kibao ( Tablets) zanye mfumo maalum wa kukusanyia takwimu hizo kwa Maafisa Afya leo Mkoani Iringa.
   
  “Takwimu zitakazokusanywa kuhusu vifo na Maafisa hawa wa afya kutokana na Mifumo hii zitawasaidia madaktari kujadili changamoto pamoja na sababu za vifo hivyo ili kupata ufumbuzi wa matatizo hayo na kuweza kupunguza idadi ya vifo nchini” alisema Dkt. Ulisubisya. 
  Aidha,Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema kuwa takwimu hizo zikikusanywa kikamilifu zitasaidia kutoa elimu kwa jamii na kupunguza imani za kishirikina kwa wananchi kwani zitaleta picha sahihi ya kugundua vyanzo vya vifo hivyo kwenye jamii husika. 

  Hata hivyo Dkt. Ulisubisya amewataka maafisa hao kutumia vifaa hivyo kwa matumizi ya kazi ya kukusanyia takwimu na sio matumizi binafsi na kama itatokea afisa afya yeyote atakayehama kituo cha kazi basi arudishe ofisini kwa ajili ya mtumishi mwingine atakayekuja. Kawa upande wake Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa iringa Bw. Fikira Kissimba amesema kuwa mfumo huo wa ukusanyaji taarifa zitasaidia pia uandikishwaji wa mirathi ya marehemu wakati ndugu husika anapokwenda kufungua mirathi yake mahakamani. 

  Naye Mratibu wa usajili wa Takwimu wa Masuala muhimu ya Binadamu nchini kutoka wizara ya afya Dkt. Gregory Kabadi amesema kuwa jumla ya Kompyuta kibao (Tablets) zilizogawiwa ni 106 kwa kila kata ya mkoani Iringa na thamani yake ni takribani shilingi Milioni 61.5. Aidha , Dkt Kabadi amesema kuwa zoezi hilo limeanza kwa majaribio katika halmashauri tano kwenye mikoa mitatu ikiwemo Pwani,Tanga na Morogoro na kufanya tathimini ya utekelezaji wa mifumo hiyo katika mkoa wa Iringa kabla ya kutumika nchi nzima. 

  Kwa upande wake Afisa afya wa kata ya Kitwilu Bw. Wilson Ntagondwa amesema kuwa kupitia mfumo huo waliokabidhiwa itawasaidia kukusanya takwimu kwa urahisi hivyo kupelekea kujua sababu zinazosababisha vifo na kusaidia kupanga maendeleo.
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendelo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Afya) Dkt. Mpoki Ulisubisya akiongea na baadhi ya Wakurugenzi wa halmashauri mbalimbali na Maafisa Afya mkoani Iringa wakati wa kukabidhi Kompyuta Kibao ( Tablets) zanye mfumo maalum wa kukusanyia takwimu za vifo ngazi ya jamii kwa Maafisa Afya mkoani humo. 
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendelo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Afya) Dkt. Mpoki Ulisubisya katikati akionesha Kompyuta Kibao ( Tablets) zanye mfumo maalum wa kukusanyia takwimu za vifo ngazi ya jamii pamoja na Maafisa afya wa kata mbalimbali Mkoani Iringa 
  Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa iringa Bw. Fikira Kissimba akiongea nna na baadhi ya Wakurugenzi wa halmashauri mbalimbali na Maafisa Afya mkoani Iringa wakati wa kukabidhi Kompyuta Kibao ( Tablets) zanye mfumo maalum wa kukusanyia takwimu za vifo ngazi ya jamii kwa Maafisa Afya mkoani humo. 
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendelo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Afya) Dkt. Mpoki Ulisubisyakushoto akimkabidhi Kibao ( Tablets) zanye mfumo maalum wa kukusanyia takwimu za vifo Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mafinga Mji bw. Fredrick Kayombo kulia wakati wa kukabidhi Kompyuta Kibao ( Tablets) zanye mfumo maalum wa kukusanyia takwimu za vifo ngazi ya jamii kwa Maafisa Afya mkoani humo. 
  Mkurugenzi Msaidizi wa Ufuatiliaji na Tathimini kutoa Wizara ya Afya Bw. Tumainieli Macha wa kwanza kulia akifuatilia kwa makini maelekezo ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendelo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Afya) Dkt. Mpoki Ulisubisya hayupo pichani wakati wa kukabidhi Kompyuta Kibao ( Tablets) zanye mfumo maalum wa kukusanyia takwimu za vifo ngazi ya jamii kwa Maafisa Afya mkoani Iringa.

  0 0

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

  Kampuni ya TanzaRice International Ltd imesema kuwa mchele una fursa ya ajira kubwa lakini watu bado hawana uelewe ya kufanya biashara hiyo.

  Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa kampuni hiyo Deo Mbasa amesema kuwa wamefanya utafiti na kuona biashara hiyo inaweza kuwakomboa wananchi kiuchumi kwa kuuza mchele huo kupitia kampuni.

  Amesema kuwa wajasiriaali wakijiunga na kampuni hiyo wanaweza kupata mchele na kuuza kwa jamii inayowazunguka.Mbasa amesema kuna faida ya kuuza mchele kwani kinachotakiwa ni uaminifu wa mtu kwa kuchukua mchele bila ya kuwa na hela mara baada ya kujiunga na kampuni hiyo.

  "Hatuwezi kila kitu tunafikiria mtaji wakati ukiwa na uaminifu unaweza kufanya biashara hata kama hauna mtaji na baadae ukawa umejikwamua kiuchumi"amesema Mbasa.
   Mkurugenzi wa TanzaRice Deo Mbasa akitoa maada wakati wa mafunzo ya wajasiriaali .
  Mjasiriamali wa bidhaa ya Mchele kupitia kampuni hiyo Even John akizungumza mafanikio ya biashara ya mchele.
   Bidhaa ya mchele ikioneshwa kwa wajasiriamali katika mafunzo yaliyoandaliwa na kampuni ya TanzaRice
   washiriki wa wajasiriaali wa Mchele wakiwa katika mafunzo yaliyoandaliwa na kampuni ya TanzaRice
  Mkurugenzi wa Kampuni ya TanzaRice Deo Mbasa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na fursa iliyopo katika bidhaa ya mchele.

  0 0

   Baadhi ya Wabunge na viongozi wa Serikali wakisakata muziki katika Tamasha la Tigo Fiesta mwaka 2018 lililofanyika katika uwanja wa Jamuhuri Mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki.
   Msanii wa muziki wa Hip Hop Fid Q akiwapagawisha mamia ya mashabiki walioshiriki katika tamasha la Tigo Fiesta mwaka 2018 lililofanyika uwanja wa Jamuhuri mkoani Dodoma.
   Msanii anayefanya vizuri kwenye muziki wa Hip Hop Rich Mavoko,  akiwaburudisha  mamia ya wakazi wa mkoa wa Dodoma na maeneo jirani walioshiriki katika Tamasha la Tigo Fiesta mwaka 2018 lililofanyika katika uwanja wa Jamuhuri Mkoani humo. 
   Msanii wa Bongo Flava ambaye ni zao la kundi la Tip Top Connection la jijini Dar es Salaam Dogo Janja au akitoa burudani kwa  mamia ya mashabiki walioshiriki katika tamasha la Tigo Fiesta mwaka 2018 lililofanyika katika uwanja wa Jamuhuri Mkoani Dodoma.
   Msanii wa muziki wa Bongo fleva Whozu pamoja na madensa wake wakilimiliki vilivyo jukwaa wakati wa alipokuwa  akitoa murudani ya kufunga mwaka kwenye Tigo Fiesta mwaka 2018 lililofanyika katika uwanja wa David Zimbihile Wilayani  Muleba Mkoani Kagera.Msanii Rosalee akifanya yake katika tamasha la Tigo Fiesta mwaka 2018 lililofanyika uwanja wa Jamuhuri mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki. 


  -Baadhi ya Wabunge wapanda jukwaani kusakata Kwaito, Bolingo
  -Bill Nas, Weusi , Whozu, Rosaree waacha historia


  Wabunge na viongozi wa Serikali, jana walikuwa ni sehemu ya burudani ya aina yake katika Tamasha kubwa la muziki la Tigo Fiesta 2018, lililofanyika katika uwanja wa Jamuhuri mjini Dodoma.

  Tamasha hilo lililofanikiwa kuwavuta mashabiki wa muziki wa bongo fleva kutoka mkoa huo na viunga vyake, lilianza kwa msanii Jay Melody kupanda jukwaani na kutoa burudani safi ‘iliyobamba’na kutengeneza mazingira safi kwa waliomfuatia .

  Baada ya wasanii kadhaa kupanda jukwaani i, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Patrobas Katambi alipanda jukwaani kuongea mawili matatu kabla ya kuomba kuwekewa muziki wa bolingo ambalo alisakata kwa ustadi kmubwa jambo lililozua shangwe za ktosha.

  Wakati Katambi akiendelea kusakata bolingo, baadhi ya wabunge wakiongozwa na mbunge wa Sengerema William Ngeleja waliomba kuwekewa muziki wa Kwaito ambao waliusakata kwa ufundi mkubwa na kusababisha shangwe kubwa kutoka kwa mashabiki.

  Wasanii wanaounda kundi la Weusi, Bill Nas, Barnaba, Rosaree ni baadhi ambao wataendelea kukumbukwa na wakazi wa Dodoma kutokana na kutoa burudani safi kwa wakazi hao ambao walionekana kuwa na kiu ya buruidani

  Ili kunogesha msimu wa Tigo Fiesta 2018, kampuni ya simu za Simu za mkononi ya Tigo imewaletea promosheni bab-kubwa inayojulikana ya Data Kama Lote inayowapa wateja bonasi ya hadi mara mbili kwa vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*0#. ‘Hii itawawezesha wateja wa Tigo kufurahia msimu huu wa vibes kupitia mtandao wa kasi ya juu zaidi wa Tigo 4G+,’ Mkurugenzi wa Tigo, Kanda ya Ziwa, Uthman Madati alisema katika tamasha la Mwanza.

  Tigo pia inatoa punguzo kubwa la bei kwa tiketi za tamasha la Tigo Fiesta 2018 zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa Masterpass QR. Wateja wanapaswa kupiga *150*01# na kuchagua 5 (lipia huduma) kisha kuchagua namba 2 (lipa Masterpass QR) na kutuma kiasi husika cha bei ya tiketi kwenda namba ya Tigo Fiesta 78888888. 

  Wateja wa Tigo pia wanaweza kujaribu umahiri wao wa kujibu maswali yanayohusiana na msimu wote wa vibes kupitia shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo Trivia. Washindi wanajinyakulia zawadi za kila siku za TSH 100,000, zawadi za wiki za TSH 1 milioni, simu janja za mkononi zenye thamani ya TSH 500,000 kila moja, pamoja na donge nono la TSH milioni 10 kwa mshindi wa jumla. Kushiriki wateja wanapaswa kutuma neno MUZIKI kwenda 15571 au kutembelea tovuti ya http://tigofiesta.co.tz na kuchagua Trivia.

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wapenzi wa mpira wa miguu baada ya kukagua timu za Yanga na Namungo zilizocheza mechi ya kirafiki kwenye uwanja wa Majaliwa katika Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa Novemba 18, 2018. Kulia kwake ni mkewe Mary , wapili kushoto ni Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi. Timu hizo zilitoka sare 1-1. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

   Deus Kaseke wa Yanga akimili mpira katika mechi ya kirafiki kati ya timu yake na Namungo iliyochezwa kwenye uwanja wa Majaliwa katika Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, Novemba 18, 2018. Timu hizo zilitoka sare  1 – 1. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Andrew Vincent wa Yanga akizuia mpira kwa kichwa huku akizongwa na  Reliant Lusajo wa Namungo katika mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye uwanja wa Majaliwa katika Halmashauri ya wilaya ya Rungwa Novemba 18, 2018. Timu hizo zilitoka sare 1 – 1
   Mshambuliaji wa Yanga, Maka Edward   (kulia) akipiga  mpira huku akizuiwa na  beki wa Namungo, Hashim Manyanya katika mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye uwanja wa Majaliwa katika Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, Novemba 18, 2018. Timu hizo zilitoka sare 1-1
    Kiungo na mshambuliaji wa Yanga, Thaban Kamusoko akijaribu kufunga kwa tikitaka bila mafanikio mbele ya beki wa Namungo FC, Juma Jamal akimkabili katika mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye uwanja wa Majaliwa katika Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa Novemba 18, 2018. Kushoto ni Kipa wa Namungo FC,  Adam Oseja
   Reliant Lusajo wa Namungo FC  (kushoto) akimiliki mpira huku akizongwa na Juma Abdul wa Yanga katika mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye Uwanja wa Majaliwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Novemba 18, 2018. Katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare  1-1. 
  Mashabiki wakishangilia

  0 0


  NA TIGANYA VINCENT,TABORA

  BARAZA la Madiwani na Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua limeshauriwa kuanza zoezi la kuhamasiha wananchi katika ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa ajili ya wanafunzi wa Sekondari wanaotarajiwa kuanza masomo yao Januari mwakani.

  Kauli hiyo imetolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Dkt. John Pima wakati akijibu hoja za Madiwani katika kikao cha robo ya kwanza cha Baraza la Madiwani kilichokuwa kikipitia taarifa za utekelezaji.Alisema Wilaya ya Kaliua ina watoto 4,367 ambao wamepata sifa ya kuendelea na Kidato cha kwanza mwakani na hivyo kusababisha uwepo wa upungufu wa vyumba vya madarasa 76.

  Dkt. Pima alisema lengo la Halmashauri hiyo ni kwamba watoto wote waliofanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi na kupata sifa za kuingia kidato cha kwanza ni lazima waanze masomo yao Januari.Aliwaomba Madiwani kuweka kando mambo mengine ambayo yanaweza kusubiri na kuhakikisha kuwa jamii katika Shule zaSekondari zilizopo wanaongeza vyumba vya madarasa ili shule zitakapofunguliwa mwezi Januari wawe n sehemu nzuri ya kusomea bila kuwa na msongamano mkubwa darasani.

  “Nawaomba waheshimiwa Madiwani tuanze kwa kuhakikisha kuwa watoto wetu waliofaulu darasa la saba wanaingia kidato cha kwanza mwakani…mahitaji mengine yasisiyo ya lazima kuanza hivi sasa ni vema yakasubiri kwa sababu kipaumbe chetu ni watoto waingie madarsani…tusaidiane kuwahamaisha wananchi wetu wachangiea katika ujenzi wa madarasa ili Halmashauri itakapopeleka msaada wawe wapiga hatua” alisisitiza.

  Kuhusu majengo ya Shule za Msingi Shikizi yaliyokamilika , alisema watajitahidi kutafuta kibali ili ifikapo Jamuari , ziwe zimesajiliwa na wanafunzi wa Shule hizo waweze kuyatumia.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kaliua Dkt. John Pima (kulia) na Mbunge wa Jimbo wa Kaliua Magdalena Sakaya(kushoto) wakijadiliana jana wakati kikao cha Baraza la Madiwani cha kupitia taarifa za utekelezaji za robo mwaka.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kaliua Dkt. John Pima akitoa ufafanuzi jana wakati kikao cha Baraza la Madiwani cha kupitia taarifa za utekelezaji za robo mwaka .
  Mbunge wa Jimbo wa Kaliua Magdalena Sakaya akichangia taarifa ya utekelezaji wa robo mwaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani jana.
  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Haruna Kasele akifungua kikao cha kujadili taarifa za utekelezaji wa robo mwaka wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani jana.
   

  Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kikao kilichokuwa kikijadili taarifa za utekelezaji wa robo mwaka kilichofanyika jana.
  Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua wakiwa katika kikao kilichokuwa kikijadili taarifa za utekelezaji wa robo mwaka kilichofanyika janaBaadhi ya wananchi wakifuatilia jana mjadala wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani kilichokuwa kikipitia taarifa za utekezaji wa robo mwaka.

  0 0

  Tangu ameanza kucheza SportPesa haikuchukua muda mrefu mpaka pale alipotangazwa kuwa ni mshindi wa Shinda Zaidi na SportPesa na kufanikiwa kushinda bajaj mpya kabisa kutoka timu ya ushindi.

  Huyu ni Mgaya Hassan mshindi wa Droo Ya 43 yeye ni mwanafunzi wa chuo kikuu na mkoani Morogoro lakini ushindi wa bajaj umemkuta akiwa hapa jijini Dar es Salaam wakati akimalizia likizo yake kwa kaka yake.

  Na Timu Ya Ushindi haikutaka Kumcheleweshea Ilimfuata mpaka Bunju Hapa Dar es salaam Nyumbani kwa Kaka Yake Na Kumkabidhi Bajaj. Akikabidhiwa bajaji ya ushindi Hassan alisema alianza kucheza na SportPesa baada ya kusikia kwenye redio na tv kuwa kuna bajaj zinatolewa na yeye moja kwa moja akijasajili na kuanza kutupia bashiri kwenye mechi mbalimbali hatimaye kufanikiwa kushinda.

  "Mimi ni mwanafunzi nasoma SUA Morogoro taarifa hizi za ushindi zimenikuta hapa Dar es salaam wakati nikiwa likizo, nimefurahi sana maana wakati nacheza wanafunzi wenzangu waliniambia mimi siwezi kushinda kwa sababu naweka pesa ndongondogo waliamini kuwa wanaoshinda ni wale ambao hubashiri kwa pesa nyingi kumbe sivyo kila mtu ana nafasi ya kushinda maana mimi nilikuwa nacheza kwa elfu moja moja pekee sasa nimeshinda najua wakiniona ndio wataamini yani nina furaha sana" alisema Hassan

  Aidha Hassan anasema bajaji hii itamkomboa kutoka kwenye maisha ya sintofahamu na kuingia kwenye maisha mazuri huku akitegemea kipato kitakachopatikana kutokana na bajaj kumsaidia kwenye mahitaji yake ya chuoni na nyingine kuwawezesha ndugu zake ambao hawako vizuri kiuchumi. 

  "Daaah maisha ya chuo ni magumu sana unatoka chuo umechoka wakati mwingine huna pesa ya kula familia zetu nazo zinatoka katika mazingira ya kimaskini unajikuta huna cha kufanya lakini kwa ushindi huu wa bajaj ntaweza jikimu mimi mwenyewe maana kila siku ntakuwa na uhakika wa kupata chochote kutokana na bajaji hii" aliongeza Hassan.

  Hassan aliwaomba wanafunzi wenzake wa vyuoni wale ambao wamefikisha umri wa miaka 18 na zaidi kucheza na SportPesa maana wanaweza jikuta wakiandika historia mpya kwenye maisha yao na kumudu gharama ndogondogo zinazopatikana chuoni.
    Mgaya Hassan mshindi wa Droo Ya 43 yeye ni mwanafunzi wa chuo kikuu na mkoani Morogoro lakini ushindi wa bajaj umemkuta akiwa hapa jijini Dar es Salaam wakati akimalizia likizo yake kwa kaka yake.

  0 0


  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhe. Kangi Alphaxard Lugola, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha kwa Rais wa Zanzibar Mhe. Dk. Shein, akiwa na Viongozi wa Wizara hiyo Katibu Mkuu Meja Jenerali.Jocob G.Kingu na Naibu Katibu Mkuu Ndg. Kailima Ramadhan, leo Ikulu Zanzibar Novemba 19/11/2018.

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Kangi Alphaxard Lugola, alipofika Ikulu Zanzibar na Viongozi wa Wizara hiyo kujitambulisha rasmin kwa Rais wa Zanzibar Dk. Shein leo Ikulu Zanzibar.Novemba 19/11/2018(Picha na Ikulu)
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Kangi Lugola, walipofika Ikulu Zanzibar kuona na Rais wa Zanzibar Dk. Shein, kwa kujitamulisha na kufanya mazungunzo leo Ikulu Zanzibar, novemba 19/11/2018.(Picha na Ikulu)
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizuingumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Kangi Lugola alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na Rais wa Zanzibar Mhe. Dk. Shein, novemba 19/11/2018.(Picha na Ikulu)
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Mhe. Kangi Lugola, baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu Zanzibar leo 19/11/2018.(Picha na Ikulu )
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Mhe. Kangi Lugola, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika Ikulu Zanzibar leo 19/11/2018.(Picha na Ikulu )

  0 0

  Wajasiriamali Nchini kuendelea kunufaika na Mpango wa Kurasimisha Biashara katika mwaka wa fedha 2018/2019 ikiwa ni moja ya hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuwaniunua wajasiriamali hao. 

  Akizungumza wakati wa mafunzo kwa Wajasiriamali wa Halmashuri ya Mji wa Njombe yanayolenga kuwajengea uwezo wajasiriamali ili waweze kurasimisha biashara zao na hivyo kuongeza tija na kuchangia katika ujenzi wa Taifa, Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania ( MKURABITA) Bi. Seraphia Mgembe amesema kuwa lengo ni kuwajengea uwezo ili waweze kurasimisha Biashara zao. 

  “Tunashukuru Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe Rais, Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Bunge kwa kuiwezesha MKURABITA kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi hasa katika eneo la kuwasaidia wajasiriamali wadogo ili warasimishe Biashara zao;’’ Alisisitiza Mgembe 

  Akifafanua amesema kuwa mafunzo yakuwajengea uwezo Wajasiriamali hao yameendeshwa kwa siku 10 ambapo kila kundi lilikuwa na siku mbili za kujifunza mada mbalimbali zilizotolewa na wataalamu kutoka Taasisi mbalimbali zikiwemo benki kama; CRDB Bank na NMB . 

  Taasisi nyingine zilizoshiriki katika kutoa mada katika mafunzo hayo ni pamoja na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo SIDO, Mamalaka ya Mapato nchini (TRA), Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) pamoja na wataalamu wengine wa ujasiriamali. 

  Pia, alipongeza ushirikiano ulipo kati ya MKURABITA na Mkoa wa Njombe hali iliyosaidia katika kufanisha mafunzo kwa wajasiriamali na pia urasimishaji ardhi kwa wananchi ambapo baadhi yao wameweza kupata mikopo katika Taasisi za fedha na hivyo kuinua uchumi wao kutokana na kukua kwa shughuli za ujasiriamali walizokuwa wanafanya na hasa kutokana na mikopo waliyopata kutoka katika Taasisi za fedha zikiwemo Benki. 

  Taasisi nyingine zilizowawezesha wajasiriamali kupata mikopo baada ya kurasimisha biashara zao ni pamoja na SIDO ambayo imekuwa ikiwajengea uwezo wajasiriamali waliojikita katika usindikaji wa bidhaa za mbogamboga na matunda ili kuongeza thamani na hivyo kuchochea ujenzi wa uchumi wa Viwanda katika Mkoa wa Njombe ambao unazalisha matunda ya aiana mbalimbali yakiwemo maparachi. 

  Mafunzo yakuwajengea uwezo wajasiriamali hao wa Halmashuri ya Mji wa Njombe ili waweze kwenda na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano inasisistiza ujenzi wa uchumi wa Viwanda. 

  Kwa upande wake Afisa kutoka mfuko wa NSSF Bw. Celestine Michael amesema kuwa kuna kila sababu ya kuendelea kuimarisha huduma zote zinazotolewa kwa wananchi. ni kuona kuwa matokea tarajiwa yanafikiwa kwa maslahi ya wananchi. Baada ya urasimishaji wananchi wote wmetakiwa kutumia fursa za jambo hilo katika kukuza uchumi na Ustawi wa wananchi. 

  Aidha, Aliwaaasa Wajasiriamali kutumia Kituo cha Huduma kwa Pamoja (One Stop Centre) kurasimisha Biashara zao ili kuchochea maendeleo na ustawi wajamii. Akizungumzia hatua ya kuanzishwa kwa kituo hicho Bw. Michael amesema kuwa ni hatua kubwa katika kuwawezesha wajasiriamali kwani wataweza kurasimisha Biashara zao hali itakayowaongezea wigo wa kufanya ujasiriamali na kukuza masoko. 

  “Tunapongeza juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano kupitia MKURABITA kwani uwezeshaji wananchi kurasimisha biashara zao ni hatua kubwa katika kuchochea uchumi wa Viwanda na ujasiriamali kwa ujumla”; Alisisitiza Michael 

  Kwa upande wake Afisa Mapato kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Njombe Bw. Stanley Sulle amesema kuwa mafunzo kwa wajasiriamali wa Halmashauri ya mji wa Njombe yatasaidia katika kutoa mwamko kwa wananchi katika kukuza Shughuli za ujasiriamali wanazofanya na kusaidia kupanua wigo wa ukusanyaji mapato. 

  Kituo kimoja cha huduma kitajumuisha taasisi kama , Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini, Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA). 

  Akizungumzia kuanzishwa kwa Kituo Kimoja cha Huduma amesema kuwa kitaongeza na kitasaidia kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi hali itakayopunguza muda waliokuwa wakiutumia katika kufuatilia huduma hizo katika Taasisi husika kwa kuwa zote zitakuwa katika eneo moja. 

  Aliongeza kuwa katika swala la muamko wa kulipa kodi wajasiriamali katika mkoa huo wamekuwa na mwamko mkubwa kutokana na elimu ambayo imekuwa ikitolewa na Mamlaka hiyo kwa kushirikiana na wadau. 

  “ Lengo la Serikali kumfikishia mjasiriamali pale alipo ili aweze kuchangia katika kukuza uchumi kwa kufanya biashara yake kwa kuzingatia sheria kanuni na taratibu ikiwemo kulipa kodi kwa wakati, kutunza kumbukumbu za mauzo na manunuzi ili kuendana na azma ya Serikali kuwaletea wananchi maendeleo”; Alisisitiza Sulle. 

  Mafunzo kwa wajasiriamali wa Halmashauri ya mji wa Njombe yamefanyika kwa siku kumi ambapo yaligawanyika katika makundi yaliyopewa mafunzo kwa siku mbili kila kundi na hivyo kuwafikia mamia ya wajasiriamali hao hali itakayoongeza chachu katika kujenga uchumi na ustawi wa Taifa. 
   Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Biashara na Rasilimali za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) Bi. Seraphia  Mgembe akizungumza na sehemu ya wajasiriamali wa Halmashauri ya Mji wa Njombe wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo ili waweze kurasimisha Biasharaza zao hali itakayowawezesha kuongeza tija na kupata mikopo katika Taasisi za fedha.hiyo ilikuwa Novemba 16,2018 Mkoani Njombe.
   Sehemu ya Wajasiriamali wa Halmashuri ya Mji wa Njombe wakimsikiliza Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Biashara na Rasilimali za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) Bi. Seraphia  Mghembe (Hayupo pichani)  leo mjini Njombe wakati wa mafunzo kwa wajasiriamali wa  Halmashauri hiyo yanayolenga kuwajengea uwezo wa kurasimisha Biashara zao.
   Afisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania  (TRA) Mkoa wa Njombe Bw. Stanley Sulle Akiwasilisha mada kwa wajasiriamali hao kuhusu taratibu za ulipaji kodi wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo ili waweze kurasimishaji biashara zao na hivyo kushiriki katika ujenzi wa Taifa kwa kulipa kodi, Mafunzo hayo yameandaliwa na MKURABITA.

   Mmoja wa wajasiriamali  waliopata mafunzo ya kujengewa uwezo ili waweze kurasimisha Biashara zao Bi. Sesilia Mwalyego akizungumza katika mafunzo hayo leo Mjini Njombe, Mafunzo hayo yameandaliwa na Ofisi ya Rais- MKURABITA yakilenga kuwajengea uwezo ili waweze kurasimisha Biashara zao.
   Mmoja wa wajasiriamali walionufaika na urasimishaji wa Ardhi Bw. Bahati  Mtitu akionesha jinsi alivyoiweza kupanua na kukuza shughuli  zake za ujasiriamali  baada kurasimisha ardhi na kupata hati zilizomuwezesha kukopa katika Taasisi za fedha
   Mafundi wakiendelea na kazi ya kuzalisha bidhaa mbalimbali katika Karakana ya Bw. Bahati Mtitu ambaye ni mnufaika wa Mpango wa Urasimishaji Ardhi uliomuwezesha kupata mikopo katika Taasisi za fedha
   Mjasiriamali huyo Bw. Bahati  Mtitu akionesha moja ya mashine alizobuni ikiwa ni sehemu ya kuimarisha Karakana yake ili iweze kuzalisha bidhaa na thamani za aina mbalimbali yakiwemo machepe na majembe.
   Mjasiriamali huyo Bw.Bahati Mtitu akionesha  moja ya kiwanja anachomiliki kutokana na urasimishaji ardhi ambapo ameweza kutumia hati hiyo kujipatia mkopo kutoka katika Taasisi za fedha.
   Mmoja wa wanufaika wa mpango wa urasimishaji Bw. Bahati Mtitu   ambaye pia ni mshiriki wa mafunzo hayo akionesha mfano wa milango inayozalishwa katika Karakana yake.
   Mjasisriamali huyo  Bw. Bahati Mtitu ambaye pia ni mshiriki wa mafunzo hayo akionesha baadhi ya Samani zinazozalishwa  katika Karakana yake.
  Mjasisriamali huyo Bw. Bahati Mtitu akionesha moja ya mashine katika karakana yake wakati Ujumbe wa MKURABITA ulipotembelea karakana yake iliyopo mjini Njombe.
  Meneja wa Benki ya NMB Mkoani Njombe Bw. Daniel Zaki akiwasilisha mada katika mafunzo yakuwajengea uwezo  wajasiriamali wa Halmashuri ya mji wa Njombe leo mjini humo.  (Picha zote na Frank Mvungi- Njombe)
  0 0

  Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imewahukumu wakulima wawili na mfanyabiashara mmoja kutumikia kif ungo cha miaka 20 gerzani baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na vipande vitano vya meno ya tembo na kuongoza uhalifu.

  Washtakiwa waliohukumiwa ni Amiri Fransis (44), mkulima Mkazi wa Tanga, Jairab Rashid (33), mkulima na Ibrahim Mkande (30) ambaye ni mfanyabiashara.

  Hukumu hiyo imesomwa leo Novemba 19 mwaka huu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya kuridhika na ushahidi wa mashahidi sita wa upande wa Jamhuri uliowasilishwa mahamani hapo pamoja na vielelezo vinne ikiwemo hati ya tathimini ya nyara za Serikali.

  Hakimu alisema washtakiwa walikuwa wanatuhumiwa na makosa mawili ya kuongoza mtandao wa kiarifu na kukutwa na nyara za Serikali, Mahakama imewakuta na hatia, ambapo watatumikia kifungo cha miaka 20 jela.

  Akisoma hukumu hiyo, hakimu Shaidi amesema, makosa haya ni makubwa sana, yanapelekea kuharibu utalii wa Taifa zima."Nyie ni wabinafsi sana m nataka kujinufaisha kibinafsi kwa Mali ambazo zinasaidia Taifa zima" amesema Hakimu Shaidi.

  Kabla ya kutolewa hukumu hiyo, Hakimu Shaidi aliuliza upande wa mashtaka kama walikuwa na lolote la kusema dhidi ya washtakiwa, ambapo wakili wa Serikali, Elizabeth Mkunde alisema hawana kumbukumbu zote za nyuma za washtakiwa, lakini ameiomba Mahakama kutoa adhabu Kali kwa washtakiwa ili iwe fundisho kwao kwa wengine ambao wanaingilia na kuharibu utalii wa Taifa.

  Katika kesi hiyo upande wa mashtaka uliwasilisha vielelezo ambavyo ni meno ya tembo, hati ya kukamatia mali, hati ya tathimini ya nyara hizo na maelezo ya onyo.Baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo, washtakiwa walisema hawajaridhika na hukumu hiyo na mbapo wanatarajia kukata rufaa, Mahakama Kuu.

  Katika kesi hiyo inadaiwa kati ya Januari 15 na 22, 2016, wakiwa maeneo ya mbali mbali ya Jiji la Dar es Salaam na Manyara washtakiwa waliongoza mtandao wa kiuhalifu kwa kupokea, kusafirisha na kuuza vipande vitano vya meno ya Tembo bila kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori.

  Pia inadaiwa Januari 22, 2016 washtakiwa wakiwa walikamatwa na vipande vitano ya vya meno ya tembo, vya uzito wa kilogramu 7.9, vyenye thamani ya USD 30,000 ambazo ni sawa na Sh milioni 65.6 bila kibali.

  Akizungumza nje ya mahakama, Baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi amesema, kwa upandw wa mashtaka wameridhishwa na hukumu ya Mahakama kwani uamuzi huo ni ushindi katika vita vya kupambana na Maliasili.

  0 0

  Shirika la Save The Children limekutana na waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga katika mafunzo ya siku moja kwa ajili ya kuwaeleza hali halisi ya mimba za utotoni katika mkoa wa Shinyanga ili waweze kuwa chachu ya mabadiliko katika jamii.

  Mafunzo hayo yamefanyika leo Jumatatu Novemba 19,2018 katika ukumbi wa Good Shepherd mjini Kahama, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Kahama,Anamringi Macha.

  Akifungua mafunzo,Macha aliwataka waandishi wa habari kutumia kalamu zao kutoa elimu kwa jamii kuhusu madhara ya mimba na ndoa za utotoni.Alisema katika wilaya ya Kahama,halmashauri za Msalala na Ushetu zinaongoza kwa mimba na ndoa za utotoni kutokana na mila na desturi kandamizi,umaskini,tamaa za mwili,mazingira pamoja na maendeleo ya teknolojia ambapo simu za mkononi zimekuwa zikiongeza tamaa kwa wanafunzi.

  “Waandishi wa habari mna nafasi kubwa katika vita hii ya kutokomeza mimba na ndoa za utotoni kwa mnawafikia watu wengi zaidi kupitia habari zenu,Lazima wadau wote tushirikiane kutokomeza changamoto hizi ili watoto wetu wawe salama”,alisema.Aidha Macha aliwataka wananchi kuzingatia utawala wa sheria na kwamba serikali itaendelea kuwachukulia sheria watu wote wanaoshiriki kuwafanyia ukatili watoto.

  Kwa upande wake,Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima alisema lengo la kukutana na waandishi wa habari ni kufahamiana na kuwaeleza kuhusu shughuli zinazofanywa na shirika ili kufanya kazi pamoja kuhakikisha mimba na ndoa za utotoni zinatokomezwa mkoani Shinyanga.

  “Ili kufikia malengo yaliyokusudiwa,Save The Children imeona ni vyema kukutana na waandishi wa habari kwani tunaamini waandishi wa habari ni chachu ya mabadiliko katika jamii,hivyo tukiwaeleza hali halisi ya mimba na ndoa za utotoni mtaweza kuchukua hatua pia”,alieleza Malima.

  Alisema shirika hilo linatekeleza miradi mitatu mkoani Shinyanga ambayo ni mradi wa elimu,ulinzi wa mtoto na mradi wa kutokomeza mila na desturi kandamizi zinazochangia mimba na ndoa za utotoni.

  “Tunashirikiana na shirika la AGAPE kutekeleza mradi wa mradi wa kutokomeza mila na desturi kandamizi zinazochangia mimba na ndoa za utotoni katika halmashauri ya wilaya ya Kishapu kwenye kata 12 na shirika la KIWOHEDE kwenye kata 8 katika halmashauri ya Ushetu ambapo katika maeneo kiwango cha mimba na ndoa za utotoni ni kikubwa”,alisema Malima.
  Mkuu wa wilaya ya Kahama,Anamringi Macha akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari yaliyoandaliwa na shirika la Save The Children kwa ajili ya kukutana na kupanga mikakati ya kutokomeza ndoa na mimba za utotoni. Kushoto ni Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima - Picha zote na Kadama Malunde na Marco Maduhu- Malunde1 blog.
  Mkuu wa wilaya ya Kahama,Anamringi Macha akizungumza na waandishi wa habari wakati akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga yaliyolenga kukutana na wanahabari na kuwaeleza hali halisi ya mimba za utotoni katika mkoa wa Shinyanga ili waweze kuwa chachu ya mabadiliko katika jamii.
  Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima akielezea lengo la shirika hilo kutoa mafunzo kwa waandishi yaliyolenga kukutana na wanahabari na kuwaeleza hali halisi ya mimba za utotoni katika mkoa wa Shinyanga ili waweze kuwa chachu ya mabadiliko katika jamii.
  Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima akielezea lengo la mafunzo hayo.
  Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
  Mratibu wa mradi wa kutokomeza mila na desturi kandamizi zinazochangia mimba na ndoa za utotoni wa shirika la Save The Children,Mary Zebron akielezea miradi inayotekelezwa na shirika hilo ambayo ni elimu,ulinzi wa mtoto na mradi wa kutokomeza mila na desturi kandamizi zinazochangia mimba na ndoa za utotoni.
  Waandishi wa habari wakiwa ukumbini.
  Waandishi wa habari Malaki Philipo na Stephen Wang'anyi (kulia) wakiwa ukumbini.
  Mratibu wa mradi wa Ulinzi wa mtoto wa shirika la Save The Children,Alex Enock akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
  Mafunzo yanaendelea....Kulia ni Salim Yasin kutoka Huheso Fm akifuatiwa na Simeo Makoba wa Radio Faraja Fm na Marco Maduhu wa gazeti la Nipashe.
  Kushoto ni Mwandishi wa habari Paulina Juma kutoka Kahama Fm na Kadama Malunde wa Malunde1 blog wakiwa ukumbini.
  Kushoto ni Afisa mradi wa kuzuia mila na desturi kandamizi kutoka shirika la Save The Children,Msemakweli Bitagatcha na Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima wakiwa ukumbini.
  Mwandishi wa habari gazeti la Mwananchi,Shija Felician na Shaban Alley wa Star Tv wakifuatilia mada ukumbini.
  Mafunzo yanaendelea.
  Kushoto ni Mdhibiti Ubora wa miradi kutoka Save The Children Kanuty Munishi akifuatiwa Afisa mradi wa kutokomeza mila na desturi kandamizi zinazochangia mimba na ndoa za utotoni kutoka shirika la KIWOHEDE,Victor Reveta na Afisa mradi wa kutokomeza mila na desturi kandamizi zinazochangia mimba na ndoa za utotoni kutoka shirika la AGAPE ,Peter Amani wakiwa ukumbini. 
  Mratibu wa mradi wa kutokomeza mila na desturi kandamizi zinazochangia mimba na ndoa za utotoni wa shirika la Save The Children,Mary Zebron na Mtathmini na Ufuatiliaji wa miradi wa shirika la KIWOHEDE, Beatrice Freedom.
  Kushoto ni Mwandishi wa habari/Mkurugenzi wa Kijukuu blog,William Bundala akifuatiwa Greyson Kakuru wa TBC.
  Mratibu wa mradi wa kutokomeza mila na desturi kandamizi zinazochangia mimba na ndoa za utotoni wa shirika la Save The Children,Mary Zebron akitoa mada kuhusu madhara ya mimba na ndoa za utotoni.
  Kulia ni Afisa Habari halmashauri ya wilaya ya Ushetu,Emmanuel Shomary akifuatiwa na Afisa Maendeleo ya Jamii halmashauri ya Ushetu,Jovitus George wakifuatilia mada ukumbini.
  Kulia ni mwandishi wa habari wa ITV/Radio One Frank Mshana na Sumai Salum kutoka Divine Fm wakifuatilia mada ukumbini.
  Maafisa kutoka shirika la Save The Children,KIWOHEDE na AGAPE wakiwa ukumbini.
  Waandishi wa habari wakiwa ukumbini.
  Afisa mradi wa kutokomeza mila na desturi kandamizi zinazochangia mimba na ndoa za utotoni kutoka shirika la KIWOHEDE,Victor Reveta akielezea mafanikio ya mradi huo katika halmashauri ya Ushetu.
  Afisa mradi wa kutokomeza mila na desturi kandamizi zinazochangia mimba na ndoa za utotoni kutoka shirika la AGAPE ,Peter Amani akielezea mafanikio ya mradi huo katika halmashauri ya Kishapu.
  Kushoto ni Afisa Habari halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Robert Hokororo akiwa ukumbini,wengine ni waandishi wa habari.Picha zote na Kadama Malunde na Marco Maduhu- Malunde1 blog.

  0 0


  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kuku Project Bw. Geofrey Kayenga akifungua Semina kwa ajili ya ufugaji wa kisasa wa kuku kwa wafugaji na ambao wanahitaji kuanza na wanaofuga kuku, alisema kuwa lengo kubwa la semina hiyo ilikuwa ni kuhamasishana na kubadilishana ujuzi wa ufugaji wa kuku kwa ujumla na kuwapa njia za kisasa za ufugaji wa kuku, Chuo cha Ustawi wa Jamii Jijini Dar es Salaam.
  Bi. Beatrice Kanemba Meneja Mawasiliano wa Kuku Project, akielezea kwa ufupi juu ya Kuku Project ambapo ilianza mwaka 2014, alisema kuwa malengo yao yalikuwa ni kuona sekta ya ufugaji inakuwa rasmi,watu kufanya ufugaji kama biashara,kutumia teknolojia ya mitandao ya kijamii kutoa elimu ya ufugaji wa kuku ili kuwafikia watu wengi zaidi. aliongeza kuwa baadhi bidhaa walivyonavyo ni pamoja na Vifaa vya kisasa vya ufugaji na vifaranga wa iana zote ya kuroirer pamoja na ushauri wa ufugaji wenye tija na usimamizi wa mabanda na masoko ndani na nje ya nchi. 
  Bw. Deusdedit Nestory, Mkuu wa Kitengo cha Kuku Manispaa ya Kinondoni akielezea mikakati ya Serikali kupitia Wizara ya Kilimo na Ufugaji ambapo pamoja na kuhimiza wananchi kufanya shughuli zao kwa vikundi ili kuwarahisishia kupata mikopo na kufanya kazi kwa urahisi lakini pia wanatoa elimu ya ufugaji wa kuku kwa wananchi kuanzia ngazi ya Kata lengo likiwa ni kuboresha sekta ya ufugaji wa kuku.
  Daktari wa Mifugo wa Kuku Project Dkt. Shukuru akielezea namna wanavyotatua shida mbalimbali hasa za magonjwa ya kuku lakini pia kutoa ushauri wa kitaalam ili mfugaji asiweze kupata hasara hasa katika ufugaji wake.
  Baadhi ya watu mbalimbali walifika katika semina hiyo wakiendelea kufuatilia masomo mbalimbali juu ya ufugaji wa kuku wa kisasa.
  Mmoja wa wafugaji aliyefika katika Semina hiyo akielezea matarajio yake na namna atakavyo nufaika na Kuku Project. 
  Mmoja wa washiriki katika Semina hiyo akielezea namna alivyoelewa kuhusiana na ufugaji wa kuku kwa kutumia vifaa vya kisasa na wenye tija kwa washiriki wengine. 
  Mwendesha Semina hiyo Bi. Zainab Muharami kutoka Kuku Project akielezea zaidi baadhi ya mambo yanayohusiana na Kuku Project.
  Afisa Mikopo wa Kuku Project Sigbeth Fraden akielezea taratibu za kupata mkopo kupitia Platinum Credit ambapo kwa sasa wanatoa mikopo kwa ajili ya ufugaji wa kuku kwa watumishi wa umma na mipango ya kuanza kuwapa mikopo hiyo kwa watu binafsi bado inaendelea.
  Mfugaji wa mda mrefu Mama Anna Mfinanga akielezea namna Kuku Project ilivyomsaidia na alivyofaidika nayo kutoka katika ufugaji mpaka kutaftiwa masoko sehemu mbalimbali ikiwemo ya mayai. 

  Meneja Utendaji wa Kuku Project Bw. Goodluck Kilango, akielezea namna watu wanaweza kufanikiwa zaidi katika ufugaji wa kuku na pia kuwataka vijana waweze kuwa wafugaji kwa sababu ufugaji unalipa, mwisho aliwashukuru wadau wote waliofika katika semina hiyo ya ufugaji iliyoandaliwa na Kuku Project.
  Wafanyakazi wa kuku Project pamoja na wananchi mbalimbali waliofika katika semina ya ufugaji wa kuku wakiwa katika picha ya pamoja.(Picha zote na Fredy Njeje)

  0 0

  Na Estom Sanga-DSM 

  Wadau wa Maendeleo na menejimenti ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF- wamekutana jijini DSM kwenye Ofisi Ndogo za Mfuko huo Kujadili pamoja na mambo mengine maandalizi ya zoezi la kufuatilia utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini litakalofanyika mwanzoni mwa mwezi ujao. 

  Utaratibu huo wa kufuatilia utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini hufanyika mara mbili kwa mwaka na hujumuisha Maafisa wa Serikali na wadau wa Maendeleo wa ndani na nje ya nchi ambao hupata fursa ya kutembelea baadhi ya maeneo na kukutana na Walengwa na Viongozi wa Maeneo ya Utekelezaji wa Mpango. 

  Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF imekuwa ikitekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini –PSSN- ulioanza mwaka 2012 katika baadhi ya Halmashauri za Wilaya kwa majaribio na kisha kutekelezwa nchini kote kufuatia mafanikio ya majaribio yaliyofanyika katika wilaya za Bagamoyo, Kibaha, Chamwino na Mbarali mkoani Mbeya. Kwa sasa Mpango huo unanufaisha Kaya takribani Milioni Moja na Laki Moja Tanzania Bara ,Unguja na Pemba ambako walengwa hupata ruzuku ya Masharti hususani katika nyanja za elimu na afya na ile isiyokuwa ya Masharti kwa lengo la kuboresha maisha ya walengwa . 

  Kufuatia utekelezaji wa Mpango huo wa Kunusuru Kaya Maskini, Walengwa wa Mpango huo wameonyesha mabadiliko makubwa hususani katika uboresha ya makazi ,uanzishaji wa miradi ya kiuchumi huku suala la mahudhurio ya wanafunzi wanaotoka kwenye Kaya hizo shuleni na kwenye vituo vya afya yakiboreshwa zaidi. 

  Serikali kupitia TASAF kwa sasa iko katika maandalizi ya Awamu ya Pili ya utekelezaji wa Mpango huo ambayo mkazo maalum utawekwa kwa Walengwa kufanya kazi na kuibua miradi itakayowaondolea kero kwa kushirikiana na Wataalamu walioko kwenye maeneo yao huku pia mkazo mkubwa ukiwekwa kwenye shughuli za uzalishaji mali ili waweze kukuza uchumi wao na hivyo kupunguza umaskini .
  Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bw.Ladislaus Mwamanga (katikati) akimsikiliza kiongozi wa Shughuli za TASAF katika Benki ya Dunia Bw. Mohamed Muderis (mwenye miwani).
  Wadau wa Maendeleo na Menejimenti ya TASAF (picha ya juu na chini wakiwa katika mkutano wa kujadili utekelezaji wa Shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini jijini DSM.
  Menejimenti ya TASAF akiwa katika mkutano na Wadau wa Maendeleo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Mfuko huo kujadili masuala ya utekelezaji wa shughuli za Mfuko huo jijini DSM.

  0 0

   Benki ya Exim Tanzania leo imezindua rasmi kampeni yake inayofahamika kama ‘Deposit Utokelezee na Exim’ ikiwa ni muendelezo wa benki hiyo kuwahamasisha watanzania kujenga tabia ya kujiwekea akiba zaidi.

  Kampeni hiyo iliyozinduliwa jijini Dar es Salaam leo inawawezesha wateja wa benki hiyo kupata viwango vya riba vya kuvutia hadi asilimia 10.5 ikiwa watafungua akaunti ya amana maalum (fixed deposit) au kuweka kwenye akaunti zao za amana maalum kiasi kisichopungua Sh 50m/- kabla ya Desemba 31 mwaka huu..

  "Kampeni hii inalenga kukuza utamaduni wa kujiwekea akiba miongoni mwa watanzania. Kwa kuzingatia viwango vya ushindani tunavyowasilisha kupitia kampeni hii, wateja wetu watakuwa na uwezo wa kunufaika na riba ya hadi 10.5% kwenye amana zao, " Alisema Kaimu Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo na wa kati wa Benki ya Exim Bi Agnes Kaganda wakati hafla fupi ya uzinduzi wa kampeni hiyo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

  Kampeni hii inakuja ikiwa ni mwendelezo wa mkakati wa benki hiyo katika kusimamia ustawi wa wateja unaofahamika kama 'Exim kazini leo, kwa ajili ya kesho' (Exim at Work Today, for tomorrow) unaoendana na dira na muelekeo wa benki hiyo. Ni kampeni inayothibitisha nia ya benki ya Exim katika kutafuta kesho iliyo bora kwa wateja na jamii inayoizunguka.

  Bi Kaganda aliongeza, "kama benki, tunaahidi kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya wateja wetu, ili kuhakikisha wanakua na ustawi mzuri sasa na hata baadae. Kupitia akaunti zetu za muda maalum (Fixed deposit) mteja anaweza kuongeza kiasi kikubwa cha pesa huku akiwa na uhuru wa kuchagua aina ya muda anaotaka. Tunaamini kwamba kesho yako bora inaanza leo.’’

  Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1997, Benki ya Exim imefanikiwa kujitanua maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi ambapo kwasasa ina matawi yake kwenye mikoa 13 nchini ikiwa ni pamoja na mikoa ya Dar es Salaam, Zanzibar, Tanga, Morogoro, Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Mwanza, Shinyanga, Kigoma, Iringa, Mbeya na Mtwara. Pia matawi yake yapo kwenye nchi za Comoros, Djibouti na Uganda.


  Kaimu Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo na wa kati wa Benki ya Exim Bi Agnes Kaganda (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na kampeni mpya ya benki hiyo inayofahamika kama ‘Deposit Utokelezee na Exim’ leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni muendelezo wa benki hiyo kuwahamasisha watanzania kujenga tabia ya kujiwekea akiba zaidi. Wengine ni pamoja na Mkuu wa Kitengo cha wateja wakubwa (corporate) wa benki hiyo Bw Shrikant Ganduri (kushoto) na Mkuu wa Hazina na Masoko ya Fedha wa benki hiyo Bw Arafat Haji
  Mkuu wa Hazina na Masoko ya Fedha wa benki hiyo Bw Arafat Haji (Kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na kampeni mpya ya benki hiyo inayofahamika kama ‘Deposit Utokelezee na Exim’ iliyozinduliwa leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni muendelezo wa benki hiyo kuwahamasisha watanzania kujenga tabia ya kujiwekea akiba zaidi. Wengine ni pamoja na Kaimu Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo na wa kati wa Benki ya Exim Bi Agnes Kaganda (katikati) na Mkuu wa Kitengo cha wateja wakubwa (corporate) wa benki hiyo Bw Shrikant Ganduri.

  0 0

  MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesema ipo katika mchakato wa kuweka elimu ya kodi katika mitaala ‘syllabus’ ya elimu nchini ili wanafunzi waanze kufundishwa maana ya kodi tangu wakiwa wadogo.

  Hatua hiyo inatokana na kuwapo kwa uelewa mdogo katika masuala ya kodi ambao unachangia kwa kiasi kikubwa wafanyabiashara wengi hasa wanaoanzisha biashara kuona ulipaji kodi ni mzigo. Akizungumza katika mafunzo ya kodi kwa wafanyabiashara wadogo na wakati, Afisa Elimu Mkuu kwa Mlipakodi kutoka TRA, Rose Mahendeka alisema mchakato huo unatarajiwa kukamilika hivi karibuni.

  Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Taasisi ya The Tanzanian Associate kwa kushirikiana na Kampuni ya Abel and Fernandes Communications, yalilenga kuwakuelimisha jamii kuhusu masuala ya kodi. Aidha, Mahendeka alisema bado kuna changamoto ya baadhi ya wafanyabiashara kutoelewa umuhimu wa kulipa kodi pamoja na kuweka kumbukumbu za mapato na matumizi katika biashara zao.

  “Wafanyabiashara wengi hawana uelewa wa kodi ila tupo katika mchakato wa kuweka elimu ya kodi katika mitaala ya elimu waanze kupata wakiwa wadogo kabisa kule mashule ili waanze kupata uelewa wakiwa wadogo kabisa kwamba nini maana ya kodi, inahusu nini na jinsi gani kodi inalipwa Tanzania, tunaamini kwa njia hiyo watu wengi wataelewa,” alisema.

  Naye Mshauri wa masuala ya Kodi, Petro Francis alisema ni muhimu sana kwa wafanyabiashara wa ngazi zote kuelewa maana ya kodi na umuhimu wa kulipa kodi. “Jamii inapaswa kufahamu kwamba kodi ndio chanzo kikuu cha mapato ya serikali, hivyo bila kodi huduma za kijamii haziwezi kupatikana, huduma za hospitali, barabara na madaraja, zinachangiwa kwa kiasi kikubwa na kodi kutoka kwa wananchi wake,” alisema. Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Abel & Fernandes Communications, Fatma Fernandes alisema sheria za kodi zipo ila wajasiriamali wengi wanashindwa kuelewa namna kufanya ili kulipa kodi kwa wakati.

  Wakati Mwanzilishi wa Taasisi ya The Tanzania Associates, Lucy Minde alisema wameandaa mafunzo hayo ili kuhamasisha watu wajifunze umuhimu wa kulipa kodi na kuzingatia sheria za biashara ili wasipate shida pindi wanapoanzisha biashara. Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo Kwigaya Mito alisema mfanyabiashara ni muhimu kujua ni wakati gani alipe kodi, wakati gani apate msamaha wa kodi na wakati gani aenende vizuri na sheria za kodi kwani kodi ni muhimu kwa maendeleo ya nchi.

  Naye Fahad Rajab ambaye pia ni mfanyabiashara alisema mafunzo hayo yamemfungua upeo lakini pia amejua kodi si kuionewa. “Vijana tunapofanya biashara huona kama kodi ni mzigo, ila ukielimishwa na kupata ushauri, unaona kodi ni sawa na inatusaidia kuongeza pato la Taifa na kuleta maendeleo kiujumla,” alisema. 
  Afisa Elimu Mkuu kwa mlipa kodi kutoka TRA, Rose Mahendeka akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafunzo ya kodi kwa wafanyabiashara yaliyoandaliwa na Taasisi ya The Tanzania Associates kwa kushirikiana na Kampuni ya Abel & Fernandes Communications kwa lengo la kuwajengea wafanyabiashara uelewa wa kisheria kuhusu umuhimu wa kulipa kodi.
  Mmoja wa washiriki wa mafunzo ya kodi kwa wafanyabiashara, Kwigaya Mito akichangia mada katika warsha iliyoandaliwa Taasisi ya The Tanzania Associates kwa kushirikiana na Kampuni ya Abel & Fernandes Communications kwa lengo la kuwajengea wafanyabiashara uelewa wa kisheria kuhusu umuhimu wa kulipa kodi.
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Abel & Fernandes Communications, Fatma Fernandes akizungumza katika warsha iliyoandaliwa na Taasisi ya The Tanzania Associates kwa lengo la kuwaelimisha wafanyabiashara wa kati na wadogo kuhusu sheria za kodi na umuhimu wa kulipa kodi.
  Mshauri wa masuala ya Kodi, Petro Francis akichangia mada katika warsha iliyoandaliwa Taasisi ya The Tanzania Associates kwa kushirikiana na Kampuni ya Abel & Fernandes Communications kwa lengo la kuwajengea wafanyabiashara uelewa wa kisheria kuhusu umuhimu wa kulipa kodi.
  Mwanzilishi wa Taasisi ya The Tanzania Associates, Lucy Minde akichangia mada katika warsha iliyoandaliwa taasisi hiyo kwa kushirikiana na Kampuni ya Abel & Fernandes Communications kwa lengo la kuwajengea wafanyabiashara uelewa wa kisheria kuhusu umuhimu wa kulipa kodi.

  0 0  Je Taa za Gari lako zina ukunguZimepauka?Kupelekea hupati Mwanga wa Kutosha wakati wa Usiku?Na Ushafikiria Kununua Taa Nyingine? Kama Ni NDIO Basi sasa huna Haja ya Kuwaza Kununua TAA NYINGINE 


  Nasafisha na kuzirudisha kwenye Hali yake ya upya lakini Ukipata muonekano amaizing na Kupata mwanga wa Kutosha Wakati wa Usiku na gari lako kuongezeka thamani  Kwa Gharama nafuu kabisa ya Shilingi Elfu 35 tu Nakufuata Popote Ulipo kwa Dar Es Salaam Na Taa zako zinarudi kwenye Upya Kabisa  Nipigie Simu 0712 390200 sasa Nije Kukuhudumia

  0 0

  Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Mtwara Dkt. Lobikieki Kissambu (kulia) akizungumzia ujio wa wataalam wa afya kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, kushoto ni Daktari Bingwa kutoka Muhimbili Innocent Mosha.
  Baadhi ya wagonjwa wakisubiri kupatiwa huduma katika hospitali hiyo mapema hii leo.
  Watoa huduma katika Idara ya magonjwa ya dharura wa hospitali ya Ligula wakielekezwa na Daktari kutoka Muhimbili namna ya kumuhudumia mgonjwa ambaye amezidiwa.
  Daktari Bingwa wa magonjwa ya macho kutoka Muhimbili Judith Mwende (kushoto) akiangalia maendeleo ya mgonjwa wa macho ambaye alifanyiwa upasuaji wa macho mwezi wa tatu mwaka huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. 
  Mtaalam wa kupima usikivu kutoka MNH, Sista Theresia Uisso akimuelekeza mgonjwa namna ya kuishi kulingana na tatizo linalomkabili, kushoto ni Madaktari wanafunzi wakifuatilia.
   
  Watoa huduma wa Hospitali ya Ligula wakiwasajili wagonjwa ambao wamejitokeza kupata huduma za afya katika hospitali hiyo.


  Madaktari Bingwa wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo wameanza kutoa huduma za afya katika Hospitali ya Rufaa mkoa wa Mtwara, Ligula ikiwa ni moja ya mkakati wa MNH wa kuwajengea uwezo wataalam wa afya wa hospitali za rufaa za mikoa nchini ili kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda kutibiwa Muhimbili.

  Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Ligula Dkt. Lobikieki Kissambu amesema wataalam hao watatoa huduma katika maeneo mbalimbali ikiwemo upasaji, magonjwa ya mfumo wa mkojo, magonjwa ya kike na uzazi, meno, macho, watoto, magonjwa ya koo, pua na masikio, maabara pamoja na magonjwa ya ndani.Amesema ujio wa wataalam hao utasaidia kupunguza gharama ambayo hospitali imekua ikitumia kusafirisha wagonjwa wanaopata rufaa kwenda Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi.

  Kwa mujibu wa Mganga Mfawidhi kwa mwezi hutoa rufaa kwa wagongwa 10 hadi 20 hivyo hutumia takribani shilingi milioni 300 kwa mwaka kwa ajili ya kusafirisha wagonjwa hao.‘’Wataalam hawa kutoka Muhimbili watatusaidia kuwajengea uwezo wataalam wetu hasa ukizingatia hospitali ya Ligula ina upungufu mkubwa wa Madaktari Bingwa mpaka sasa hospitali hii ina Daktari Bingwa mmoja tu, lakini pia ujio huu utatusaidia kupunguza gharama za kusafirisha wagonjwa ambao wanapata rufaa ya kwenda kutibiwa Muhimbili. Amesema Mganga Mfawidhi.

  Hata hivyo amesema katika kukabiliana na ukosefu wa Madaktari Bingwa hospitali hiyo imewapeleka shule Madaktari watatu ambao wanasomea ubingwa katika upasuaji, mifupa pamoja na koo, sikio na pua. Kwa upande wake Daktari Bingwa wa magonjwa ya kike na uzazi kutoka Muhimbili Geofrey Marandu amesema mbali na kutoa huduma za afya lakini pia watawajengea uwezo watalam hao na kuhakikisha huduma hizo zinakua endelevu.

  ‘’Mbali na kuwahudumia wagonjwa pia tutakaa kwenye idara zao ili kuona changamoto zinazowakabilli na namna ya kuzishughulikia’. amesema Dkt. Marandu.

  Kufuatia ujio wa Madaktari Bingwa wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili pamoja na wataalam wengine takribani wananchi elfu mbili wanatarajiwa kupata huduma za afya.Madaktari Bingwa wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo wameanza kutoa huduma za afya katika Hospitali ya Rufaa mkoa wa Mtwara, Ligula ikiwa ni moja ya mkakati wa MNH wa kuwajengea uwezo wataalam wa afya wa hospitali za rufaa za mikoa nchini ili kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda kutibiwa Muhimbili.

  Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Ligula Dkt. Lobikieki Kissambu amesema wataalam hao watatoa huduma katika maeneo mbalimbali ikiwemo upasaji, magonjwa ya mfumo wa mkojo, magonjwa ya kike na uzazi, meno, macho, watoto, magonjwa ya koo, pua na masikio, maabara pamoja na magonjwa ya ndani.

  Amesema ujio wa wataalam hao utasaidia kupunguza gharama ambayo hospitali imekua ikitumia kusafirisha wagonjwa wanaopata rufaa kwenda Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi.Kwa mujibu wa Mganga Mfawidhi kwa mwezi hutoa rufaa kwa wagongwa 10 hadi 20 hivyo hutumia takribani shilingi milioni 300 kwa mwaka kwa ajili ya kusafirisha wagonjwa hao.

  ‘’Wataalam hawa kutoka Muhimbili watatusaidia kuwajengea uwezo wataalam wetu hasa ukizingatia hospitali ya Ligula ina upungufu mkubwa wa Madaktari Bingwa mpaka sasa hospitali hii ina Daktari Bingwa mmoja tu, lakini pia ujio huu utatusaidia kupunguza gharama za kusafirisha wagonjwa ambao wanapata rufaa ya kwenda kutibiwa Muhimbili. Amesema Mganga Mfawidhi.

  Hata hivyo amesema katika kukabiliana na ukosefu wa Madaktari Bingwa hospitali hiyo imewapeleka shule Madaktari watatu ambao wanasomea ubingwa katika upasuaji, mifupa pamoja na koo, sikio na pua. Kwa upande wake Daktari Bingwa wa magonjwa ya kike na uzazi kutoka Muhimbili Geofrey Marandu amesema mbali na kutoa huduma za afya lakini pia watawajengea uwezo watalam hao na kuhakikisha huduma hizo zinakua endelevu.

  ‘’Mbali na kuwahudumia wagonjwa pia tutakaa kwenye idara zao ili kuona changamoto zinazowakabilli na namna ya kuzishughulikia’. amesema Dkt. Marandu.Kufuatia ujio wa Madaktari Bingwa wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili pamoja na wataalam wengine takribani wananchi elfu mbili wanatarajiwa kupata huduma za afya.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu ujenzi wa bweni lenye uwezo wa kulaza wanafunzi 80 kutoka kwa Mkuu wa Shule ya Mnacho wilayani Ruangwa, David Mwakalobo wakati alipokagua ujenzi wa bweni hilo Novemba 19, 2018 . Kulia kwake ni Mkuu wa wilaya ya Ruangwa, Hashim Mgandirwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa bweni lenye uwezo wa kulaza wanfunzi 80 katika shule ya Sekondari ya Mnacho wilayani Ruangwa, Novemba 19, 2018. Wapili kulia ni Mkuu wa Shule hiyo, David Mwakalobo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waganga na Wanguzi wa Zahanati ya Nandagala wilayani Ruangwa kabla ya kukagua ujenzi wa majengo ya Zahanati hiyo Novemba 19, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsalimia mtoto Hamza Abdulrazak aliyepelekwa na Mama yake Mzazi, Mariam Liwena (wapili kushoto) katika Zahanati ya Nandagala wilayani Ruangwa kwa matibabu, Novemba 19, 2018. Watatu kushoto ni Ajira Mpoka na mwanae Naifat Arifa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa chumba cha upasuaji katika Zahanati ya Nandagala wilayani Ruangwa, Novemba 19, 2018. Kushoto ni Mganga Mfawidhi wa Zahanati hiyo, Abubakar Abbas Rugwa.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Zahanati ya Nandagala wilayani Ruangwa Novemba 19, 2018. Kushoto kwake ni Mkuu wa wilaya ya Ruangwa, Hashim Mgandirwa, kushoto ni Mganga Mkuu wa wilaya ya Ruangwa, Dkt. Mahela Njile na kushoto ni Mganga Mfawidhi wa Zahanati hiyo, Abubakar Abbas Rugwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  ………………………………………………………………………………

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwaamewataka wananchi kwenye Kata ya Mnacho wilayani Ruangwa washirikiane kujenga mabweni katika shule ya sekondari Mnacho ili kuwaondolea wanafunzi adha ya kutembelea umbali mrefu kwenda shuleni hapo.

  Ameyasema hayo leo (Jumatatu, Novemba 19, 2018) wakati alipotembelea shule hiyo kwa ajili ya kukagua mradi wa ujenzi wa bweni, ambalo ujenzi wake unagharimu sh. milioni 92.4 ikiwa ni mchango uliotolewa na wadau wa elimu.

  “Bweni hili likikamilika litawapunguzia wanafunzi kutembea umbali mrefu kuja shuleni hususani wanaoishi vijiji vya mbali kwa sababu wataishi hapa, jambo ambalo litachangia kuongeza ufaulu wa watoto wetu.” Kadhalika, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi waishio katika Kata hiyo na za jirani washirikiane na kuanzisha mradi wa ujenzi wa mabweni mengine kwa kuwa hilo moja lililojengwa na wadau halitoshi kulingana na idadi ya wanafunzi.

  Amesema yeye yuko tayari kuendelea kuwaunga mkono wananchi hao kwenye mipango yao yote ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Kata yao, lengo likiwa ni kuhakikisha mikakati ya Serikali ya kuboresha huduma za jamii inatimia. Hata hivyo, Waziri Mkuu amewataka wananchi hao washirikiane na walimu kufuatilia maendeleo ya taaluma kwa watoto wao shuleni na kujiridhisha kama wanafanya vizuri darasani na iwapo watabaini changamoto waweze kuzitatua kwa pamoja.

  Akisoma taarifa ya ujenzi wa bweni hilo, Mkuu wa shule ya sekondari Mnacho, Mwalimu David Mwakalobo amesemma ujenzi wa bweni hilo lenye uwezo kulaza wanafunzi 80 ulianza Septemba 19, 2018 na unatarajiwa kukamilika Januari, 2019. “Kutokana na idadi ya wanafunzi waliopo shuleni bweni hili litakidhi mahitaji ya kuwalaza wanafunzi wa kike tu. Tunaendelea kuwaomba wahisani waendelee kutusaidia ili tupate bweni lingine kwa ajili ya kuwalaza wanafunzi wa kiume.”

  Mwalimu Mwakalobo amesema iwapo watafanikiwa kuwa na mabweni ya kuwalaza wanafunzi wote 334 shuleni hapo yatawasaidia katika kutatua changamoto ya utoro na mdondoko wa kitaaluma kwa wanafunzi kwa sababu wengi wanatoka mbali. Pia mradi wa ujenzi wa mabweni utasaidia walimu kuwa karibu na wanafunzi wakati wote, hivyo kupata muda mwingi wa kuwasaidia wanafunzi kimasomo kwa sababu watakuwa wanaishi shuleni. “Mradi huu pia utapunguza wanafunzi wengi wa kike kupata ujauzito.”

  Ameongeza kuwa uwepo wa mabweni shuleni hapo utaongeza ari ya wanafunzi kupenda shule tofauti na hali ilivyo sasa kwa sababu wengi wanalazimika kutembea muda mrefu kwa kuwa wanatoka vijiji vya mbali, jambo linalowafanya wasipende shule.

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii .

  CHAMA cha Waajiri Tanzania (ATE) wamefanya mkutano mkuu wa kwanza wa wanawake katika uongozi kwa mwaka 2018 uliombatanisha mahafali ya pili ya programu ya mwanamke wa wakati ujao (Female Future Programme). 

  ATE wamefanya mkutano huo wakishirikiana na Shirikisho la vyama vya waajiri nchini Norway (NHO) wenye lengo la kuwajengea uwezo wanawake kwa ajili ya kushika nafasi za juu za uongozi na kuwapa uwezo wa kuingia kwenye bodi mbalimbali na kushiriki katika maamuzi.

  Akifungua Mkutano huo, Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira ma Wwtu wenye Ulemavu Jenista Mhagama amesema mkutano huu mkubwa wa mwaka wa uongozi kwa wanawake unaenda samamba kabisa na juhudi za nchi yetu katika kuhakikisha idadi ya wanwake kwenye nafasi zao za juu za uongozi inazidi kuongezeka pia wanawake kuwa na idadi kubwa ya uwakilishi katika bodi za wakurugenzi za makampuni mbalimbali. 

  "Serikali ya awamu ya tano imeendelea kusimamia na kuhakikisha kunakuwa na uwiano mzuri wa viongozi wanawake ndani ya serikali na jumuiya mbalimbali , makampuni ya kibiashara nchni na katika kufanikisha hili serikali imeanzisha mpango mkakati wa kitaifa kwa ajii ya maendeleo ya usawa wa kijinsia ambapo upo kwenye dira ya maendeleo ya Taifa 2025"amesema Jenista. 

  Jenista amesema, programu hiyo ni fursa kwa wanawake wa wakati nujao na mafunzo hayo wakiyatumia vizuri yatawasaidia kuendesha maisha katika nyanja mbalimbali, kazini, nyumbani, kwenye jamii na kwa kizazi kijacho. 

  Amesema, kwa mwaka 2017 idadi ya wanawake katika bodi mbalimbali za taasisi za serikali iliongezeka na kufikia 117 kutoka 114 kwa mwaka 2014 ikilinganishwa na wanaume ambapo walipungua toka 526 mwaka 2014 hadi 352 mwaka 2017, aidha katika miaka hiyo idadi ya wanawake majaji imeongezeka na kufikia 39 kati ya majaji 95, wakati mwaka 2012 majaji wanawake walikuwa 34 kati ya 97.

  “Programu hii kwangu ni fursa kwenu na mafunzo haya mkiyatumia vizuri yatawasaidia kuendesha maisha katika Nyanja mbali mbali: kazini, nyumbani, kwenye jamii na kwa kizazi chetu kijacho” aliongeza Waziri Jenista. 

  "Nawapongeza Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa mafanikio haya makubwa ya kutoa mfunzo kwa Wanawake 25 kutoka makampuni 16 katika Awamu hii ya pili ya Programu hii ya Mwanamke wa Wakati Ujao kwani imekuwa ni sehemu ya kuongeza Wanawake wengi zaidi katika nafasi za uongozi na uwakilishi katika Bodi za Wakurugenzi katika Taasisi mbalimbali," 

  Naye Mkurugenzi wa ATE, Dkt. Aggrey Mlimuka alisema kuwa katika Awamu ya Pili ya Programu ya Mwanamke wa Wakati ujao ATE wameweza kutoa mafunzo kwa Wanawake 25 kutoka kampuni na Taasisi 16.

  “Tumetoa mafunzo haya kwa kushirikiana na Chuo cha Mafunzo ya Uongozi Afrika Mashariki na Kusini (ESAMI) na katika awamu hii ya Pili ya mafunzo jumla ya wanawake 25 kutoka katika makampuni na Taasisi 16 ambayo yamefadhili mafunzo haya yaliyokuwa na sehemu kuu tatu ambazo ni Uongozi, Ufanisi katika Bodi na Ufanisi katika utekelezaji wa majukumu mahali pa Kazi” 

  Hivyo basi napenda kutoa wito kwa makampuni, Taasisi, Mashirika ya Kiserikali na Binafsi kuendelea kuunga mkono programu kwa kuleta wafanyakazi wengi zaidi ili waweze kupatiwa mafunzi haya kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

  Dkt. Mlimuka aliongeza kuwa Programu ya Mwanamke wa Wakati Ujao imelenga hasa kujenga uwezo Wanawake katika kuongoza kwenye Nafasi za juu na kuleta matokeo makubwa katika kampuni na taasisi zao pasipo kuathiri majukumu yao Binafsi. 

  “Programu ya Mwanamke wa Wakati ujao ina Malengo Makuu matatu ambayo ni Kupata Wanawake wengi Zaidi kwenye nafasi za juu za uongozi, kwenye hatua za kufanya maamuzi na pia kwenye Bodi Mbalimbali za Wakurugenzi, Pili ni kuwahamasisha na kuwapa changamoto viongozi wanawake kufanya kazi kwa juhudi na malengo makubwa ili kuhakikisha wanapata matokeo chanya kwenye makampuni na taasisi zao wanazoziongoza na Tatu ni Kutengeneza Jukwaa kubwa la Wanawake kwa ngazi zote kuka pamoja na kubadilishana uzoefu kuhusiana na uongozi” Alifafanua Dr. Mlimuka. 

  Akitoa salamu zake Mwenyekiti wa ATE Bi. Jayne Nyimbo alisema kuwa Mkutano huu Mkuu wa Uongozi kwa Wanawake uliobeba kauli mbiu ya wenye kauli mbiu isemayo “Uongozi wenye Ufanisi kwa Mazingira yanayobadilika Kibiashara” ni moja ya mkakati wa Programu ya Mwanamke wa wakati ujao wa kuhakikisha inawaleta pamoja wanawake na kuwawezesha kukua kiuongozi. 

  “ATE tukiwa ndio wawakilishi wa waajiri wote nchini furaha yetu ni kuona wanachama wetu ambao ni taasisi na makampuni mbalimbali wanakuwa na Viongozi wanawake wenye uwezo mkubwa lengo likiwa kuongeza uzalishaji wa taasisi zao na taifa kwa ujumla” Alisema Jayne Nyimbo. 
  Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira ma Wwtu wenye Ulemavu Jenista Mhagama akizunguzma wakati wa 
  mkutano mkuu wa kwanza wa wanawake katika uongozi kwa mwaka 2018 uliombatanisha mahafali ya pili ya programu ya mwanamke wa wakati ujao (Female Future Programme).
  Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Nchini (ATE) Dkt Aggrey Mlimuka akizzungumza na waandishi wa habari wakati wa 
   mkutano mkuu wa kwanza wa wanawake katika uongozi kwa mwaka 2018 uliombatanisha mahafali ya pili ya programu ya mwanamke wa wakati ujao (Female Future Programme).
  Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira ma Wwtu wenye Ulemavu Jenista Mhagama akitoa cheti kwa moja ya wahitimu Arafa wakati mkutano mkuu wa kwanza wa wanawake katika uongozi kwa mwaka 2018 uliombatanisha mahafali ya pili ya programu ya mwanamke wa wakati ujao (Female Future Programme).
  Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira ma Wwtu wenye Ulemavu Jenista Mhagama akitoa cheti kwa moja ya wahitimu Bahati Minja wakati mkutano mkuu wa kwanza wa wanawake katika uongozi kwa mwaka 2018 uliombatanisha mahafali ya pili ya programu ya mwanamke wa wakati ujao (Female Future Programme).
  Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira ma Wwtu wenye Ulemavu Jenista Mhagama akitoa cheti kwa moja ya wahitimu Sophia Said Mwema wakati wa mkutano mkuu wa kwanza wa wanawake katika uongozi kwa mwaka 2018 uliombatanisha mahafali ya pili ya programu ya mwanamke wa wakati ujao (Female Future Programme)
  Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira ma Wwtu wenye Ulemavu Jenista Mhagama akiwa katika picha ya pamoja na Sekretarieti ya Chama cha Waajiri Nchini (ATE)  mkutano mkuu wa kwanza wa wanawake katika uongozi kwa mwaka 2018 uliombatanisha mahafali ya pili ya programu ya mwanamke wa wakati ujao (Female Future Programme).
  Wadau wakiwa wanaendelea na mkutano mkuu wa kwanza wa wanawake katika uongozi kwa mwaka 2018 uliombatanisha mahafali ya pili ya programu ya mwanamke wa wakati ujao (Female Future Programme)

older | 1 | .... | 1727 | 1728 | (Page 1729) | 1730 | 1731 | .... | 1897 | newer