Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1726 | 1727 | (Page 1728) | 1729 | 1730 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde akihutubia alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 53 ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) leo jijini Dodoma.Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya akizungumza alipokuwa akimkaribisha mgeni rasmi katika mahafali ya 53 ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) leo jijini Dodoma.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Ushauri la Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Dkt. Esther Ishengoma akizungumza katika mahafali ya 53 ya CBE leo jijini Dodoma.Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde akiteta jambo na Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Profesa. Emmanuel Mjema wakati wa mahafali ya 53 ya Chuo hicho leo jijini Dodoma.Kutoka kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde,Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Ushauri la Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Dkt. Esther Ishengoma na Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Profesa. Emmanuel Mjema wakimtazama mwanamke aliyekuwa akionyesha kipaji chake wakati wa mahafali ya 53 ya Chuo hicho leo jijini Dodoma.Mwanadada akionyesha kipaji chake cha kuchezea mpira katika mahafali ya 53 ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) leo jijini Dodoma.Baadhi ya wahitimu wa Shahada ya Uhasibu wakifurahia burudani kutoka kwa mwanadada aliyekuwa akionyesha kipaji cha kuchezea mpira katika mahafali ya 53 ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) leo jijini Dodoma.Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde akimkabidhi zawadi mmoja ya wanafunzi aliyeongoza katika taaluma alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 53 ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) leo jijini Dodoma.Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde akitoa tamko la kuwatunuku wahitimu wa ngazi Astashahada, Stashahada na Shada katika fani za Uhasibu, Biashara, Masoko na Ununuzi toka Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 53 ya Chuo hicho leo jijini Dodoma.Baadhi ya wahitimu wakitunukiwa shahada zao wakati wa mahafali ya 53 ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) leo jijini Dodoma. (Na: Mpiga Picha Wetu).

  0 0


  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Mtwara

  SERIKALI Kupitia Benki ya kilimo Tanzania(TADB) imetoa kiasi cha Shilingi Bilioni 2 kwa wakulima wa korosho wa mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma katika malipo ya kundi la kwanza la watu ambao wamehakikiwa kupitia vyama vya msingi na vyama vya ushirika.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 17, Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga, amesema TADB imeanza kulipa wakulima wote walioakikiwa katika mikoa tajwa kupitia vyama vyao vya Msingi na ushirika kwa kuhakikisha fedha hizo zinawafikia wakulima moja kwa moja kupitia akaunti zao.

  "zoezi la ulipaji limeanza jana na kwasasa tumewafikia wakulima zaidi ya 2168 kutoka mikoa mitatu tulionza nayo hivyo tunategemea kuendelea kulipa mpaka kufikia jumatatu tutakuwa tushalipwa wakulima wengi sana kama ilivyoagizwa na Rais Dk . John Pombe Magufuli kutaka fedha hizo ziende kwa wakulima moja kwa moja bila ya makato"amesema Waziri Hasunga.

  katika hatua nyingine Waziri wa Kilimo ametangaza kuwa jumla ya Tani 20 za korosho zimekamatwa kutoka ghala la mtu binafsi la Olam lililoko mkoani Mtwara ambapo zilikuwa zinahamishwa kwenda kwenye eneo la ununuzi wakati zikiwa ni za mwaka jana.

  amesema korosho hizo zilikabidhiwa katika Chama cha Msingi cha Mnyawi kwa lengo la kuchanganywa kinyemela na zile zinazopelekwa kwenye maghala makuu.“Jana (juzi) tulikamata tani 20 zilizokuwa zimepenyezwa katika vyama vya msingi, tusingependa lijirudie hivyo, wananchi wawe makini kuhakikisha korosho zinazoletwa katika vyama vya msingi ni zile za Watanzania ili korosho yetu peke yake iendelee kununuliwa na Serikali,” amesema Hasunga.

  Amesema korosho zitakazokamatwa kutoka nje au kuingizwa kinyemela kwenye vyama vya msingi zitataifishwa na wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.Jumanne wiki hii tani nyingine tisa zilikamatwa katika eneo la Newala baada ya kuingizwa kinyemela toka nchini Msumbiji.Aidha juzi pia yalikamatwa magunia 152 ya korosho katika Wilaya ya Nanyumbu yaliyoingizwa nchini kutoka Msumbiji.
  Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga,akizungumza na Waandishi wa Habari juu kiasi cha shilingi Bilioni mbili zilizotolewa katika awamu ya kwanza
  Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania(JWTZ) Luteni Jenerali , Yacoub Mohamedi akizungumza na waandishi wa habari leo Mkoani Mtwara juu ya Zoezi la ulipaji na ukusanyaji wa korosho. 
  Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga,akizungumza na Waandishi wa Habari juu kiasi cha shilingi Bilioni mbili zilizotolewa katika awamu ya kwanza
  Baadhi ya Malori yaliyopo katika Mkoani Mtwara kwa ajili kubeba korosho na kuzipeleka katika maghala Maalum yaliyotengwa. 
  WMajengo ya Bodi ya Korosho kama yanavyonekana kwa nje mkoani Mtwra ambapo kwa sasa macho na masikio ya wanahabari wanayaangazia hapo kujua mfumo mzima wa ulipwaji unakwendaje.

  0 0   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia upinde aliopewa na wazee wa kijiji cha Kilimarondo wilayani Nachingwea ikiwa ni ishara ya kumtakia ulinzi wakati wote anapotimiza majukumu yake ya kulitumikia taifa.  Alikuwa katika mkutano wa hadhara aliouhutubia kijijini hapo, Novemba 17, 2018.
  AAA
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia upinde aliopewa na wazee wa kijiji cha Kilimarondo wilayani Nachingwea ikiwa ni ishara ya kumtakia ulinzi wakati wote anapotimiza majukumu yake ya kulitumikia taifa.  Alikuwa katika mkutano wa hadhara aliouhutubia kijijini hapo, Novemba 17, 2018.
  AAAAAA
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akimsikiliza Mwenyekiti wa kijiji cha Mtua, wilayani Nachingwea, Anthony Makota   wakati  aliposoma taarifa kuhusu matatizo yanayokikabili kijiji hicho mbele ya   Waziri Mkuu ambaye alisimama kijijini hapo kuwasalimia wananchi, Novemba 17, 2018 . Kulia ni Mbunge wa Nachingwea, Hasan Masala. Picha na Ofisi ya Wazri Mkuu)

  0 0  Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Adm Mgoyi akipata maelezo kwa mwafunzi wa Kozi ya Uselemala Chuo cha VETA Mikumi Mariam Anderson wakati wa mahafali ya 21 ya Chuo hicho.
  Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Adam Mgoyi akizungumza katika mahafali ya 21 ya Chuo cha VETA Mikumi yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo hicho.
  Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki wa VETA Geofrey Sabuni akizungumza kuhusiana na mikakati ya VETA katika utoaji ujuzi kwa vijana katika kmahafali ya 21 ya Chuo cha VETA Mikumi yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo hicho.
  Aliyekuwa Mkuu wa Chuo cha VETA Mikumi Christopher Ayo akitoa salam kwa wahitimu ambao alikuwa nao wakati akihudumu cheo hicho katika chuo katika mahafali ya 21 ya Chuo cha VETA Mikumi yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo hicho.
  Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Mikumi Emmanuel Munuo akitoa taarifa ya chuo katika mahafali ya 21 ya Chuo cha VETA Mikumi yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo hicho.
  Mchoro wa Ramani waliochora wanafunzi wa kozi ya ujenzi katika Chuo cha VETA Mikumi.  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii Mikumi

  Serikali imejenga mazingira kwa vijana kupitia mapinduzi ya viwanda kwa serikali ya awamu ya Tano chini Rais Dkt John Pombe Magufuli ambapo ndio suluhisho ya vijana wenye ujuzi kutumika katika viwanda hivyo.

  Hayo aliyasema Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Adam Mgoyi katika mahafali ya 21 ya Chuo VETA Mikumi ,amesema kuwa mafunzo ya VETA ndio uwanja mpana katika soko la ajira kwa vijana kujiajiri au kuajiriwa.

  Amesema vijana waliohitimu ni zaidi 315 ambapo wanaenda katika soko la ajira hivyo wanaweza kujiunga katika vikundi na kuanza kuzalisha kile walichokipata kwa miaka waliosoma chuoni hapo. Wanachuo 315 wamehitimu mafunzo kwa ngazi ya (Level) II na III, kati yao wavulana walikuwa 209 na wasichana 106.

  Amesema vijana hao wanahitaji mazoezi ya kutosha ili kuweza kupambana na soko la ufundi katika Jumuia ya Afrika Mashariki hivyo ili waweze kuwa na vigezo hivyo walimu wanahitaji kuongeza nguvu za ziada kwa vijana hao hasa walioko bado katika masomo. Mgoyi aliwaasa vijana kutokuitegemea sana serikali katika kuwatafutia ajira na badala yake watumie fursa ya mafunzo walio pata VETA Kwenda kutengeneza kampuni na kujiajiri wenyewe na kuajiri wenzao.

  Aliwaasa vijana kutokuwa waoga katika katika kazi zao kwa yale walio fundishwa na kuwa wajasili ili waweze kuwaambia wateje na kuwaaminisha wateja ya kuwa wao ni bora, kwani wateja hawawezi kuwaamini kama wao watashindwa kuwaaminisha. Mkuu wa Wilaya huyo ameiomba VETA kuchangamkia fursa za uzalishaji mali kama wanavyofanya Jeshi ni katika ujenzi wa uchumi wa viwanda

  "VETA hatuna sababu ya kubaki nyuma kwa sababu wataalamu tunao na wanafunzi tunao wafundisha hawana tofauti yoyote na wale walioko katika secta zingine za uzalishaji"amesema Mgoyi

  Nae Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Mikumi Emmanuel Munuo amesema Chuo cha VETA Mikumi na Shirika la Plan International. Kwa mara nyingine tena, Chuo kiliingia mkataba na Shirika la Plan International kupitia ufadhili wa Jumuiya ya Ulaya (EU) kutoa mafunzo ya ufundi stadi kwa vijana 1651 ikiwa wavulana ni 741 na wasichana ni 910, Stadi kwa vijana walemavu 80 kati ya hawa wavulana ni 45 na wasichana ni 35 katika vijiji vilivyopo Mikumi .

  Amesema kozi walizozitoa kwa vijana wa vijiji mbalimbali kwa wenye mahitaji maalumu ni Umeme wa Majumbani, Ufundi Magari na Pikipiki, Udereva, Upishi na Mapambo, Uchomeleaji Vyuma, Ufundi Simu, Ushonaji, Useremala, Aluminium na Ujenzi wa Nyumba. Munuo amesema mradi huo uliamza kutoa mafunzo mwezi Oktoba, 2015 na kulimaliza kutoa mafunzo hayo mwezi Juni, 2018 kwa kuendesha kwa mfumo wa mafunzo nje ya Chuo (outreach) na uanagenzi ili kusaidia jamii na kuwafikia vijana wengi zaidi hasa wenye ulemavu.

  0 0

  NA MWAMVUA MWINYI,PWANI

  JESHI la polisi mkoani Pwani wanalishikilia lori dogo kwa tuhuma za kukutwa na korosho magunia 45 yenye uzito wa kilogramu 81 .

  Korosho hizo zinadaiwa zilikuwa zikisafirishwa kwenda kwenye chama cha msingi cha ushirika kinyume na agizo la Rais Dk John Magufuli kutaka korosho zote kusafirishwa na magari ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

  Kamanda wa polisi mkoani Pwani ,Wankyo Nyigesa alisema ,gari hilo linahisiwa kusafirisha korosho hizo kuwa hazijapatikana kihalali.Alieleza, tukio hilo lilitokea novemba 16 mwaka huu ambapo askari kwa kushirikiana na Mrajisi Msaidizi mkoa wa Pwani Angela Nalimi.

  "Gari hilo aina ya Canter lenye namba za usajili T 731DGG lilikuwa likizipeleka korosho hizo zikiwa kwenye magunia yenye nembo ya chama kikuu cha ushirika mkoa wa Pwani (CORECU) kwenda chama cha ushirika cha msingi cha Misugusugu wilayani Kibaha," alisema Nyigesa.Baada ya uchunguzi kukamilika watuhumiwa na gari lao watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili ikiwa watabainika walikuwa wanunuzi wasio ruhusiwa na serikali.
  Kamanda wa polisi mkoani Pwani ,Wankyo Nyigesa

  0 0


  0 0


   
   Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Idara ya Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole akipokea tuzo ya pongezi kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli, baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya CCM ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Gaudentia Kabaka katika Kongamano la Jumuiya hiyo , kumpongeza Rais Dk. Magufuli kutimiza miaka mitatau tangu aingie madarakani na pia kwa utekelezaji thabiti wa Ilani ya CCM, lililofanyika katika Ukumbi wa PTA, Temeke, Dar es Salaam, Novemba 17,2018. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Mwalimu Queen Mlozi.
    Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Idara ya Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole akisoma ujumbe ulioandikwa kwenye tuzo hiyo ya pongezi  kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli, baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya CCM ya Umoja wa Wanawake Tanzania(UWT) Gaudentia Kabaka katika Kongamano la Jumuiya hiyo , kumpongeza Rais Dk. Magufuli kwa utekelezaji wa Ilani ya CCM, lililofanyika katika Ukumbi wa PTA, Temeke, Dar es Salaam, Novemba 17,2018. 
  Katibu Mkuu wa UWT Taifa Mwalimu Queen Mlozi akishereheka pamoja na washiriki mbalimbali waliofika kwenye kongamano hilo lililofana kwa kiasi kikubwa,huku likihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama.
   
   Mwenyekiti wa Jumuiya ya CCM ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Gaudentia Kabaka akielekezwa jambo na Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo Mwalimu Mwalimu Queen Mlozi, katika Kongamano la kumpongeza Rais Dk. Magufuli kwa utekelezaji wa Ilani ya CCM, lililofanyika katika Ukumbi wa PTA, Temeke, Dar es Salaam, Novemba 17,2018.
  Baadhi ya  Washiriki wakishangilia wakati wa Kongangamano la Jumuiya ya Chama Cha Mapinduzi ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kumpongeza Mwenyekiti wao CCM, Rais Dk. John Magufuli kwa utekelezaji wa Ilani ya CCM, lililofanyika Novemba 17,2018 katika Ukumbi wa PTA, Temeke, Dar es Salaam.
   Baadhi ya Washriki mbalimbali wa Kongamano hilo 
    Baadhi ya Washriki mbalimbali wa Kongamano hilowakifurahia jambo huku wakiendelea kuangali yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo.
    Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Idara ya Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole alipokuwa akiwasili katika  katika Kongangamano la kumpongeza Rais Dk. Magufuli kwa utekelezaji wa Ilani ya CCM, lililofanyika katika Ukumbi wa PTA, Temeke, Dar es Salaam, Novemba 17,2018.
   Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Mwalimu Queen Mlozi akizungumza jamo kwenye kongamano hilo
   Baadi ya viongozi mbalimbali waliofika kwenye kongamano hilo la UWT
   Washiriki wakiserrbuka ukumbini

   Mwenyekiti wa Jumuiya ya CCM ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Gaudentia Kabaka akizungumza jambo.
   Meza kuu

   Mjumbe wa UWT Taifa,Spika Mstaafu Anne Makinda
   Mjumbe wa UWT Taifa,Naibu Spika wa Bunge Mh Tulia Ackson
    Mjumbe wa UWT Taifa,Waziri wa Madini Mh Angellah Kairuki
   Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Idara ya Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole akiteta jambo na Katibu Mkuu wa UWT Taifa Mwalimu Queen Mlozi.

   Mkuu wa Mkoa wa Kilimnajaro Anna Mghwira akizungumza kwenye kongamano hilo
   MKuu wa Wilaya ya Kisarawe,Jokate Mwegelo akizungumza jambo kwenye kongamano
   Katibu Mkuu wa UWT TAIFA Mwalimu Queen Mlozi akisalimiana na MKuu wa Wilaya ya Kisarawe,Jokate Mwegelo
   Washiriki wakishangilia wakati wa Kongangamano la Jumuiya ya Chama Cha Mapindizi ya Umoja wa Wanawake Tanzania(UWT) kumpongeza Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli kwa utekelezaji wa Ilani ya CCM, lililofanyika katika Ukumbi wa PTA, Temeke, Dar es Salaam.
  Mshiriki akifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri kwenye Kongamano.

  0 0


  Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka akifunga mafunzo kwa wajasiriamali zaidi ya 700 wa Mjini Njombe yaliyoratibiwa na Ofisi ya Rais, Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) yakilenga kuwajengea uwezo wajasiriamali hao ili waweze kurasimisha Biashara zao. Hayo yamejiri leo tarehe 17/11/2018 Mjini humo.
  Sehemu ya Wajasiriamali hao zaidi ya 700 wa Mjini Njombe wakifuatilia hafla ya ufungaji mafunzo hayo iliyofanyika mjini humo ambapo Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Christopher Ole Sendeka alikuwa mgeni rasmi. Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo wajasiriamali hao ili waweze kurasimisha Biashara zao.
  Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) Bi. Seraphia Mgembe akizungumzia faida za mafunzo waliyopata Wajasiriamali zaidi ya 700 wa mjini Njombe yakilenga kuwajengea uwezo ili warasimishe Biashara zao na hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi.
  Mmoja wa wajasiriamali walinufaika na mafunzo yakuwajengea uwezo ili waweze kurasimisha Biashara zao Bw. Lucas Kawongo akifurahia cheti alichotunukiwa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe wakati akifunga mafunzo kwa wajasiriamali zaidi ya 700 wa Mjini Njombe.
  Mhasibu wa Mapato kutoka Halmashauri ya Mji wa Njombe Bw. George C. Mwasera akipokea cheti cha kuhitimu mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais- MKURABITA yakilenga kuwajengea uwezo wajasiriamali ili warasimishe Biashara zao.
  Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka akiwasili ukumbini kufunga mafunzo kwa wajasiriamali zaidi ya 700 yaliyoandaliwa na MKURABITA yakilenga kuwajengea uwezo wajasiriamali hao ili warasimishe biashara zao.
  Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka akifurahia jambo na Mratibu wa MKURABITA Bi. Seraphia Mgembe mara baada ya Mkuu wa Mkoa kufunga mafunzo kwa wajasiriamali zaidi ya 700 Mjini Njombe leo tarehe 17/ 12/ 2018. (Picha zote na MAELEZO, Njombe).

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Apongezwa kwa Kuwezesha Wanyonge

  Frank Mvungi- MAELEZO, Njombe

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amepongezwa kwa kuendelea kuwawezesha wajasiriamali kupitia Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) .

  Akizungumza wakati akifunga mafunzo ya siku 10 kwa wajasiriamali zaidi ya 700 wa Mjini Njombe Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Christopher Ole Sendeka amesema kuwa swala la urasimishaji Biashara kwa wajasiriamali ni takwa la Kisheria na pia ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ibara ya 58 ambapo Biashara zote zinatakiwa kuendeshwa katika mfumo rasmi na Serikali ya Awamu ya Tano imeweka mkazo mkubwa ili kuwainua wajasiriamali wanyonge.

  “ Nawapongeza MKURABITA na Halmashauri ya Mji wa Njombe kwa kufanikisha mafunzo haya kwa wajasiriamali yanayolenga kuwajengea uwezo ili waweze kurasimisha Biashara zao na pia kuanzishwa kwa Kituo Kimoja cha Urasimishaji Biashara hapa Njombe itakuwa ukombozi kwa wajasiriamali wetu”; Alisisitiza Ole Sendeka.

  Akifafanua Mhe. Ole Sendeka amesema kuwa kuanzishwa kwa Kituo cha Urasimishaji na Uendelezaji wa Biashara Mjini Njombe kumewashirikisha wadau kama MKURABITA, TRA, SIDO na Benki mbalimbali ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali kukabiliana na tatizo la Ongezeko la Biashara ndogo na za kati zisizo rasmi na ambazo zinakuwa kwa kasi.

  Aliongeza kuwa wananchi wote wanajukumu kubwa la kushirikiana na Serikali katika kutatua changamoto zilizopo katika maeneo yao hasa kwa wajasiriamali kuhakikisha kuwa wanatoa taarifa za wale wote wanaotaka kukwamisha juhudi za Serikali zinazolenga kuwainua.

  Kwa upande wake Mratibu wa MKURABITA Bi. Seraphia Mgembe amesema kuwa washiriki wa mafunzo hayo wamejengewa uwezo katika maeneo yafuatayo; Urasimishaji na Usajili wa majina ya Biashara, Upatikanaji wa leseni za Biashara na faida zake, utunzaji wa kumbukumbu za Biashara na umuhimu wake, huduma kwa mlipa kodi, Huduma za mifuko ya Hifadhi ya Jamii, Mbinu za Masoko.

  Aliongeza kuwa wajasiriamali wakirasimisha Biashara zao watakuza mitaji yao na kupanua masoko kwa kuwa watakuwa na uwezo wa kukopa katika Taasisi za fedha yakiwemo mabenki.

  Naye Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi. Ruth Msafiri amesema kuwa wajasiriamali wanapaswa kujenga utamaduni wa kurejesha kwa wakati mikopo wanayokopa katika kupitia Taasisi za fedha ili waweze kukuza Biashara zao.

  Pia alishauri Halmashuri kuangalia namna Bora yakuwawezesha wajasiriamali wanaoanza Biashra ili kuweka utaratibu utakaosaidia kukuza Biashara zao.

  Mafunzo yakuwajengea uwezo wajasiriamali yamefanyika Mkoani Njombe yakilenga kuwajengea uwezo ili waweze kurasimisha biashara zao na kuchangia katika kukuza uchumi. Wajasiriamali zaidi ya 700 wameshiriki katika mafunzo hayo ya siku 10.

  0 0


  Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle (wan nne kulia) akitoa maelekezo kwa mafundi wakati akikagua fitokombo (‘crankshaft’) mashine ya kuchonga vipuri vya injini za magari katika karakana ya TEMESA mkoa wa Mtwara wakati wa ziara yake mkoani humo kukagua utendaji kazi na kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wafanyakazi wa wakala huo.Wa pili kulia ni Kaimu Meneja wa TEMESA mkoa huo Rocky Sabigoro.
  Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle katikati akimpa maelekezo Mkuu wa Kivuko Kilambo Namoto ndugu Dhulkif Hamdan kulia wakati wa ziara yake ya kukagua usalama wa vivuko katika mikoa ya kusini. Kivuko cha MV. KILAMBO kinatoa huduma kati ya Kilambo na Namoto mkoani Mtwara.
  Abiria wa kivuko cha MV. KITUNDA kinachotoa huduma kati ya Kitunda na Lindi mjini wakimsikiliza kwa umakini mfanyakazi wa kivuko hicho wakati akiwapa elimu ya jinsi ya kuvaa boya la kujiokolea pindi inapotokea ajali ya maji.
  Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle katikati akitoa maagizo kwa Meneja wa TEMESA mkoa wa Lindi Mhandisi Grayson Maleko kulia wakati akikagua ujenzi wa jengo la abiria kusubiria kivuko (‘waiting lounge’) katika kivuko cha Lindi kitunda. Majengo hayo pamoja na vyoo yanajengwa pande zote mbili za kivuko na yanatarajiwa kumalizika hivi karibuni na kuanza kutumiwa na abiria wa kivuko hicho.
  Abiria wa kivuko cha MV. KITUNDA kinachotoa huduma kati ya Kitunda na Lindi mjini mkoani Lindi wakishuka kutoka kwenye kivuko hicho baada ya kuwasili kutokea Kitunda. Kivuko hicho kimekua msaada mkubwa kwa wakaazi wa maeneo hayo ambao kabla ya ujio wa kivuko walikua wakivuka kwa kutumia mitumbwi midogo ambayo ilikua ikihatarisha usalama wao kwa kiasi kikubwa.
  Kivuko cha MV. KITUNDA kikielea majini wakati kikikaribia maegesho ya Lindi Mjini kutokea Kitunda. Kivuko hicho kimekua msaada mkubwa kwa wakaazi wa maeneo hayo ambao kabla ya ujio wa kivuko walikua wakivuka kwa kutumia mitumbwi midogo ambayo ilikua ikihatarisha usalama wao kwa kiasi kikubwa.

  0 0


  Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na wenye Ulemavu Mhe Jenista Mhagama akimkabidhi Meneja wa NSSF Kahama Ndugu Winston Mundigile Ufunguo wa Ofisi Ndogo alipofungua rasmi kituo cha uwezeshaji wananchi kiuchumi Mkoani Kahama. Taasisi mbalimbali zimepewa ofisi ndogo ili kutoa elimu na rasilimali nyingine ili kuwakwamua wananchi wa Wilaya ya Kahama Kiuchumi
  Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na wenye Ulemavu Mhe Jenista Mhagama akisalimiana na Baadhi ya Wafanyakazi wa NSSF Kahama katika Ofisi Ndogo ya NSSF alipofungua rasmi kituo cha uwezeshaji wananchi kiuchumi Mkoani Kahama. Taasisi mbalimbali zimepewa ofisi ndogo ili kutoa elimu na rasilimali nyingine ili kuwakwamua wananchi wa Wilaya ya Kahama Kiuchumi

  0 0


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary (kulia) wakimpongeza Mwanafunzi Halfani Abdallah Ngonde aliyemaliza Elimu ya Msingi katika Shule ya Nanjaru wilayani Ruangwa na ambaye aliibuka kuwa mwanafunzi bora wa Mkoa wa Lindi katika Matokeao ya Mtihani wa Darasa la Saba kwa mwaka huu. Waziri Mkuu alikuwa katika mkutano wa kuwapongeza walimu wa na baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi za wilaya ya Ruangwa ambayo imefanya vizuri na kuwa ya kwanza katika mkoa wa Lindi. Mkutano huo ulifanyika kwenye ukumbi wa Narung’ombe katika Halmashauri ya Ruangwa, Novemba 18, 2018. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0


  Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu kushoto akiwa na Zumbe wa Kitulwe Tibua Charles Nkuninga kulia wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye Tamasha la Bonde ambalo lilifanyika Kata ya Kicheba wilayani Muheza lililokwenda sambamba na maonyesho ya vitu mbalimbali vya asili ikiwemo vyakula
  Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu akizungumza wakati wa Tamasha hilo 
  Afisa Utamaduni wa wilaya ya Muheza Msafiri Charles Nyaluka akizungumza katika Tamasha hilo
   Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu akiingia kwenye Tamasha hilo 
  Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu kushoto akitazama bidhaa mbalimbali vinavyotengenezwa na wakima mama wa Kibondei wakati alipotembelea Maonyesho hayo wakati Tamasha la Bonde lililofanyika eneo la Kicheba wilayani Muheza
  MBUNGE wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu kulia akilakiwa na wananchi wa Kijiji Kicheba Kata ya Kicheba wilayani Muheza wakati alipokwenda kwenye Tamasha la Bonde. 
  Sehemu ya wananchi kutoka maeneo mbalimbali wakifuatilia Tamasha hilo 
  Ngoma ya Mdumangi ikiendelea kuchezwa 
  Ngoma ya Mdumange ikiendelea kuchezwa   MBUNGE wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu amewataka vijana wilayani humo kuacha kuvaa suruali na kuzishusha chini maarufu kama milegezo, mini sketi kwani kufanya hivyo kunapelekea kuondoa utamaduni wa kitanzania hususani za watu wa bonde kupotea badala yake wavae nguo za asili zenye heshima. 

  Kwani uvaaji huo wa nguo unapelekea kupoteza mila na tamaduni ambao uliopo huku akiwataka kubadilika kwa kuhakikisha wanavaa mavazi asili ambayo ni desturi kwa watanzania. 

  Hayo yalisemwa na Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu wakati wa Tamasha la Bonde ambalo lilifanyika Kata ya Kicheba wilayani Muheza lililokwenda sambamba na maonyesho ya vitu mbalimbali vya asili ikiwemo vyakula. 

  “Tamasha la Bonde linapaswa tuliendeleze kwa vizazi vya sasa na vijavyo waweze kujua tamaduni na mila zao ...lakini pia mambo ya mavazi badala ya kuvaa milegezo, mini sketi huku mavazi na desturi zetu vinapotea tuvae nguo za asili zenye heshima kwani bila kufanya hivyo mavazi na desturi vitapotea”Alisema Mbunge huyo .Mbunge huyo alisema pia ni muhimu tamaduni za kibondei kuhakikisha zinaendelezwa kila mwaka kupitia tamasha hilo kwa kuyafadili ili vijazi vya sasa na vijavyo viweze kujua mila zao huku akiwasisitiza wazee waliopo kutokuondoka nazo maana vijana wanaozaliwa wanaweza kuona mambo hayo hayawezekani. 

  Awali akizungumza katika Tamasha hilo Zumbe wa Kitulwe Tibua Charles Nkuninga alivitaka vizazi vitumie teknolojia ya sasa kuweza kuendeleza mila kwa kutumia mitandao ya kijamii ikiwemo Facebook, instragram, youtube na whatspp. “Lakin pamoja na mambo hayo lakini tamasha hili ni hatua moja linatupeleka mbele zaidi kwa sababu kitu ambacho ni changamoto tunatakiwa tukitatue uzoefu hata lugha kwani wapo baadhi ya vijana wengi hawajui lugha yao ya asili”Alisema 

  Naye kwa upande wake Mkuu wa wilaya Mstaafu Samweli Kamote alisema analifurahi tamasha hilo kwa maana malezi ya zamani waliokulia wao yanaanza kupotea yaliyokuwa yanalenga kwenye nidhamu,utii kwa vijana. Kamote alisema hivyo kufanyika kwa tamasha kila mwaka kunafufua ari ya kufanya mila na desturi zilizokuwa na malezi na maadili kwa vijana zinarudishwa kwani sasa utandawazi umetawala dunia vijana wanaharibika. 

  “Labda niwaambia kwamba tukiendeleza tamasha hili kila mwaka tutasaidia kurudisha nidhamu ya maadili kila mwaka na kutokusahau kupotea kwa lugha ambazo ndio msingi muhimu “Alisema.

  0 0
  Ndugu Alvaro Rodriguez Mwakilishi mkazi wa UN Tanzania amekamilisha uwepo wake wa siku2 Pangani kwa kishindo ikiwemo kutembelea Mbuga ya Saadani.Lengo ikiwa ni kuongeza nguvu kwa kazi kubwa anayofanya Raisi wa Jamhuru ya Muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli hapa Pangani.

  Ndugu Alvaro Rodriguez ameitanabaisha Pangani kuwa Wilaya rasmi ya kimkakati itakayokuwa na mashirikiano na UN Tanzania katika mikakati na masuala yote ya kimaendeleo.

  Pangani itakua wilaya pekee kwenye mpango wa “Youth Strategy 2030” ukiwa ni mpango kabambe wa vijana utakaoratibiwa na UN kuungana na mkoa wa Kigoma.

  Pangani kuwa wilaya rasmi itakayokuwa ya mfano katika kutekeleza na kituo rasmi cha utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG’s) ikiunganika na vijana 100 wa Pangani watakao patiwa mafunzo chini ya UN Tanzania na kuwa mabalozi(SDG Champions) na baadae kutoa elimu wilaya nzima.

  Ndugu Alvaro amejitolea rasmi kuwa Balozi wa wilaya ya Pangani na hasa akiahidi kila fursa atakayoiona na kila mdau wa maendeleo atakaezungumza nae ataitanguliza wilaya hii mbele.

  Aidha amepata ripoti inayoeleza nyanja mtambuka(sekta zote) kuhusiana na wilaya hii hasa alipokutanishwa na wakuu wa idara mbalimbali na hata madiwani wote na kuahidi kupeleka ripoti hii kwa taasisi zote 15 za UN hapa nchini ikiwemo Balozi mbalimbali ili kila mmoja aone ni wapi wanaweza kufanya jambo tokana na mipango na vipaumbele vilivyopo kwenye mipango yao.

  Pia ndugu Alvaro amezungumza na vijana wa Pangani kwenye mkutano mkubwa ulioandaliwa na kuahidi kutumia ushawishi wake kwa wadau mbalimbali ili wapatikane wanaoweza kufanya lolote kwa vijana hawa na zaidi akiwasihi kujishughulisha na kufanya kazi kwa bidii.

  Mwisho ameahidi kurudi Pangani January 2019 akiwa na team ya wadau wa awali watakao kuwa wamepatika na kutimiza yatakayokuwa yamefanikishwa kwa kipindi hicho na kuzindua mafunzo kwa vijana ya malengo ya maendeleo endelevu(SDG’s)

  Amehitisha kwa kumshukuru DC Pangani Mh.Zainab Abdalah kwa namna alivoiunganusha wikaya hii na anavyojutuma kwa ajili ya Pangani na kumpongeza kwa mapokezi na maandalizi yote kwenye ugeni huu unaoenda kufungua milango ya Pangani.
  #pangaimpya
  #panganiyenyemalengo

  0 0


  Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Masikio, Pua na Koo wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Edwin Liyombo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu upasuaji wa kupandikiza vifaa vya kusaidia kusikia kwa watoto 10 ambao umefanywa na wataalam wa Muhimbili kwa kushirikiana na mtaalam kutoka nchini Misri.
  Watoto waliopandikizwa vifaa vya kusaidia kusikia wakiwa wodini baada ya kupatiwa huduma hiyo.
  Pichani ni baadhi ya watoto waliopandikizwa vifaa hivyo.

  Dkt. Liyombo akiwaeleza waandishi wa habari jinsi vifaa vya kusaidia kusikia vinavyofanya kazi baada ya mwezi mmoja.

  …………………………

  Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imepata mafanikio makubwa baada ya kufanya upasuaji wa kupandikiza vifaa vya kusaidia kusikia kwa watoto 21 ndani ya miezi 17 ukilinganisha na watoto 50 waliopandikizwa vifaa hivyo miaka 15 iliyopita nchini India.

  Kila mwaka Serikali ilikuwa ikipeleka wagonjwa nchini India kwa ajili ya kupandikizwa vya vifaa vya kusaidia kusikia na hadi kufikia mwaka 2016, wagonjwa 50 tu walikuwa wamenufaika na huduma hiyo.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Masikio, Pua na Koo wa Muhimbili, Dkt. Edwin Liyombo amefafanua kwamba hospitali hiyo itavunja rekodi kwa kuwa hadi sasa tayari wagonjwa 21 ndani ya miezi 17 kuanzia Juni mwaka 2017 hadi Novemba 2018 sawa na asilimia 42 wamepatiwa matibabu tofauti na wagonjwa 50 waliopelekwa India katika kipindi cha miaka 15 iliyopita kuanzia 2003 hadi 2016.

  Dkt. Liyombo amesema mwaka 2003 Serikali ilianza kupeleka wagonjwa nchini India kwa ajili ya kupandikizwa vifaa vya kusadia kusikia na kwamba idadi ya wagonjwa imekuwa ikiongezeka. Dkt. Liyombo amesema kwamba gharama ya kutoa huduma hiyo kwa mgonjwa mmoja katika Hospotali ya Taifa Muhimbili ni Tshs. 37 milioni wakati India kwa mgonjwa mmoja ni Tshs. 80 milioni hadi Tshs. 100 milioni.

  “Kwa sasa gharama za kupandikiza kifaatiba cha kusaidia kusikia kwa mgonjwa mmoja ni Tshs. 37 milioni, gharama hii ni kubwa kwa mgonjwa mmoja kwani kifaa cha usikivu pekee yake kinagharimu Tshs. 31 milioni kwa mgonjwa mmoja, huku upasuaji ukigharimu Tshs. 6 milioni,” amefafanua Dkt. Liyombo.

  Dkt. Liyombo amesema kwamba hadi sasa Serikali imetumia jumla ya Tshs. 777 milioni kupandikiza vifaa vya kusaidia kusikia kwa watoto 21 na kwamba kama wageenda nje kutibiwa watoto hao wangeigharimu Serikali Tshs. 2.1 bilioni hivyo wataalam wa Muhimbili wamefanikiwa kuokoa Tshs. 1.323 bilioni.

  Amesema wataalam wa Muhimbili kuanzia tarehe 12 hadi 16 Novemba, 2018 kwa kushirikiana na daktari Bingwa wa Upasuaji wa Magonjwa ya Masikio, Pua na Koo, Prof. Lobna El Fiky kutoka Chuo Kikuu cha Ain Shams nchini Misri-wamefanikiwa kufanya upasuaji kwa watoto 10 waliozaliwa na matatizo ya kutosikia. “Napenda kuwaambia kwamba sisi wataalam wazalendo tumefanya upasuaji kwa watoto 10 sisi wenyewe kwa zaidi ya asilimia 95 hivyo tunaendelea kujiimarisha,” amesema Dkt. Liyombo.

  Naye Veronika Kiundo, Mkazi wa Mkoa wa Tanga ambaye mtoto wake amepandikizwa kifaa cha kusaidia kusikia katika hospitali hiyo amesema kwamba anaishukuru Serikali kwa kumwezesha mtoto wake kupatiwa matibabu hayo. Mama huyo amesema kwamba alianza kugundua mtoto wake ana tatizo la usikivu baada ya mwaka mmoja na nusu. “Baada ya kugundua nilimpeleka hospitali ya mkoa na baadaye walinipatia rufaa ya kuja Muhimbili,” amesema mama huyo.

  0 0   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akizungumza jambo wakati akifungua kikao cha Mawaziri wa Sekta za uchumi walipokutana kujadili utekelezaji wa Programu ya pamoja ya ujenzi wa uchumi wa viwanda katika ukumbi wa mikutano wa Waziri Mkuu Bungeni Jijini Dodoma, Novemba 17, 2018.
  ????????????????????????????????????
  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Joseph Kakunda (Mb) akielezea utekelezaji wa Wizara yake wakati wa kikao hiko walipokutana kujadili utekelezaji wa Programu ya pamoja ya ujenzi wa uchumi wa viwanda, Jijini Dodoma.
  ????????????????????????????????????
  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) akisisitiza jambo wakati wa Kikao hiko cha Mawaziri wa Sekta za kiuchumi walipokutana kujadili utekelezaji wa Programu ya pamoja ya ujenzi wa uchumi wa viwanda, Jijini Dodoma.
  ????????????????????????????????????
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa (Mb) akielezea umuhimu wa kila Wizara kutekeleza majukumu kwa haraka ili kutimiza malengo wakati wa Kikao hicho.
  ????????????????????????????????????
  Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Sekta Binafsi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Ezamo Maponde akiwasilisha mada kwa Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Sekta za Kiuchumi walipokutana Jijini Dodoma.
  ????????????????????????????????????
  Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mwita Waitara (Mb) akichangia mada wakati wa kikao hicho.
  ????????????????????????????????????
  Baadhi ya Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Watendaji Wakuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi wakimsikiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama walipokutana kujadili utekelezaji wa Programu ya pamoja ya ujenzi wa uchumi wa viwanda Jijini Dodoma.
  ????????????????????????????????????
  Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Prof. Faustine Kamuzora akielezea jambo kwa Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Watendaji Wakuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi wakati wa kikao hicho. (Kulia) ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, TAMISEMI Dkt. Zainabu Chaula. (Kushoto) ni Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Joseph Buchweshaija.
  ????????????????????????????????????
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akiteta jambo na baadhi ya Mawaziri (kushoto) ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Eng. Isack Kamwelwe, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Joseph Kakunda, Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango na Watendaji Wakuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi mara baada ya kumaliza majadiliano ya utekelezaji wa Programu ya pamoja ya ujenzi wa uchumi wa viwanda, Jijini Dodoma.PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU
  ……………….


  Mawaziri wa sekta za uchumi wamekutana Jijini Dodoma kujadili utekelezaji wa Programu ya pamoja ya Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda.

  Akizungumza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ambaye alikuwa Mwenyekiti wa mkutano huo alisema kuwa Programu ya ujenzi wa uchumi wa viwanda imejikita katika kuweka mazingira wezeshi ya biashara na uwekezaji nchini kwa lengo la kuvutia sekta binafsi na kuongeza fursa za ajira.

  “Programu hiyo itakuza uchumi na ujenzi wa viwanda kwa kufuata misingi na kanuni za kibiashara zinazokubalika kimataifa, ikiwakama nyenzo muhimu katika kuhakikisha viwanda vitakavyoanzishwa vinakuwa chachu ya maendeleo hapa nchini,” alisemaMhagama.

  Aliongeza kuwa Serikali imedhamiria kutekeleza kwa vitendo azma ya ujenzi wa uchumi wa viwanda ili kufikia malengo ya dira ya Taifa ya maendeleo ya kuiwezesha Tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo 2025.
  Hata hivyo, Waziri Mhagama alieleza kuwa Programu hii ya pamoja inatokana na kutegemeana kwa mipango na mikakati ya kisekta katika kufikia malengo ya Serikali kwa pamoja.

  Aidha, alitoa rai kwa kila mmoja kuhakikisha sekta anayoiongoza inatoa mchango stahiki katika kufikia azma ya Serikali kwa kuweka malengo yanayotekelezeka kwa wakati na kufanya mapitio ya sera, sharia na kanuni.
  “Niwaombe wote mliopo hapa kuhakikisha mnatimiza wajibu kwa kutekeleza Programu hii ya ujenzi wa uchumi wa Viwanda ikiwa njia ya uhakika katika kuhakikisha rasilimali za Taifa zinatumika kwa manufaa ya nchi na kuweza kuongeza fursa za ajira kwa Watanzania” alisisitiza Mhagama.

  Kwa upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango amewahimiza Mawaziri kutekeleza yaliyopo kwenye kitabu cha mwongozo wa mazingira bora ya biashara hapa nchini “Blue Print”, ili kuendelea kuboresha zaidi masuala ya biashara na uwekezaji.

  Naye, Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera na Uratibu, Prof. Faustine Kamuzora alisema kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu imekuwa ikiratibu program hiyo katika taasisi za Serikali kulingana na majukumu yao.
  “Kila wizara iandae mpango mkakati na namna bora yakufanikisha utekelezaji wa program hiyo kwa kushauriana na wadau wa sekta binafsi ambao ni wadau muhimu”, Alisema Kamuzora.

  Pia, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Godfrey Mwambe alisema kuwa ni vyema kila Wizara na Taasisi zikajitathimini katika kutekeleza mikakati waliyonayo ili kuvutia wawekezaji na ujenzi wa viwanda kwenye maeneo ya msingi.

  “Tunataka kuona viwanda vya hapa nchini vinakuwa ni soko la mazao yanayozalishwa moja kwa moja na wakulima” alisema Mwambe.

  0 0  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.) akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo) pichani kuhusu ziara ya ujumbe wa Makampuni 7 makubwa ya uwekezaji kutoka Uturuki itakayofanyika nchini kuanzia tarehe 18 hadi 24 Novemba, 2018. Ujumbe huo utatembelea mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Simiyu kwa ajili ya kuangalia fursa za uwekezaji katika ujenzi wa viwanda vya nguo, kiwanda cha kuongeza thamani bidhaa za kilimo, ujenzi wa maduka makubwa na hoteli za kimataifa. Mkutano huo na waandishi wa habari ulifanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam tarehe 18 Novemba, 2018. 
  Sehemu ya wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakinukuu taarifa kutoka kwa Mhe. Dkt. Ndumbaro (hayupo pichani) 
  Sehemu nyingine ya wanahabari wakiwajibika 
  Waandishi wa Habari wakifuatilia taarifa kuhusu ziara ya ujumbe wa Makampuni ya uwekezaji kutoka Uturuki iliyokuwa ikitolewa na Mhe. Dkt. Ndumbaro (hayupo pichani) 
  Balozi wa Uturuki nchini, Mhe. Ali Davutoglu (kushoto) akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Jestas Nyamanga (katikati) pamoja na Afisa kutoka Ubalozi wa Uturuki wakifuatilia mkutano kati ya Dkt. Ndumbaro na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) 
  Mkutano ukiendelea 
  Mwandishi kutoka Gazeti la Nipashe, Bw. Gwamaka akimuuliza swali Dkt. Ndumbaro (hayupo pichani)
  Balozi wa Uturuki nchini, Mhe. Davutoglu nae akizungumza wakati wa mkutano huo kuhusu ziara ya ujumbe kutoka Uturuki huku Mhe. Dkt. Ndumbaro akisikiliza
  Sehemu ya Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na JNICC wakimsikiliza Balozi Davutoglu (hayupo pichani) 
  Awali Bw. Hassani Mwamweta, Afisa Mambo ya Nje akieleza utaratibu kuhusu mkutano kati ya Mhe. Dkt. Ndumbaro na waandishi wa habari kabla ya mkutano huo kuanza. 
  Mhe. Naibu Waziri Dkt. Ndumbaro pamoja na Mhe. Balozi Davutoglu na wajumbe wengine akiwemo Bw. Nyamanga wakimsikiliza Bw. Mwamweta (hayupo pichani) akitoa utaratibu wa mkitano kabla ya mkutano kuanza 
  Kabla ya kushiriki mkutano na waandishi wa habari Mhe. Dkt. Ndumbaro alikutana na Balozi wa Uturuki nchini Mhe. Davutoglu 
  Mhe. Dkt. Ndumbaro akizungumza na Mhe. Balozi Davutoglu 
  Mhe. Dkt. Ndumbaro akimweleza jambo Mhe. Balozi Davutoglu huku mara baada ya kumaliza mkutano kati yake na waandishi wa Habari. Pembeni ni Bw. Nyamanga, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika 
  Mhe. Dkt. Ndumbaro akiagana na Mhe. Balozi Davutoglu 
  Mhe. Balozi Davutoglu akibadilishana mawazo na Bw. Nyamanga, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika pamoja na Bw. Mwamweta mara baada ya mkutano kati ya Dkt. Ndumbaro na waandishi wa habari kumalizika

  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ameipongeza Serikali ya Uturuki kwa kuendelea kuimarisha ushirikiano na Serikali ya Tanzania hususan katika kukuza biashara, uwekezaji na utalii.

  Mhe. Dkt. Ndumbaro ametoa pongezi hizo wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam tarehe 18 Novemba 2018 kuhusu ziara ya ujumbe wa Makampuni 7 makubwa ya uwekezaji kutoka Uturuki.

  Mhe. Dkt. Ndumbaro alisema kuwa, ziara ya ujumbe huo nchini ambayo itafanyika kuanzia tarehe 18 hadi 24 Novemba 2018 ni mwendelezo wa jitihada za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Uturuki na wadau mbalimbali katika kutekeleza diplomasia ya uchumi ambayo pamoja na mambo mengine inalenga kwenye kutafuta na kuleta wawekezaji wenye nia ili wawekeze katika maeneo mbalimbali hapa nchini kwa lengo la kukuza uchumi na kuinua kipato cha wananchi.

  Akielezea ziara hiyo, Dkt. Ndumbaro alieleza kuwa, ujumbe wa wawekezaji kutoka Makampuni hayo ya Uturuki hapa nchini utatembelea mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Simiyu. Alisisitiza kwamba ujumbe huo umechagua mikoa hiyo kwa malengo mahsusi ya kuwekeza katika sekta ya viwanda ikiwemo Kiwanda cha nguo, kiwanda cha sukari, kiwanda cha saruji, kiwanda cha vifaa vya ujenzi, kiwanda cha kuongeza thamani bidhaa na uwekezaji kwenye sekta ya nishati kwa mkoa wa Simiyu. 

  Aidha, kwa mkoa wa Dodoma ujumbe huo una nia ya kuwekeza katika ujenzi wa maduka makubwa (shopping malls), ujenzi wa majengo mbalimbali (real estate) na ujenzi wa hoteli zenye hadhi ya kimataifa. 

  “Tunaishukuru kwa dhati kabisa Uturuki kwani imekuwa nchi ya kwanza kutekeleza azma ya Serikali ya kuhamia Dodoma kwa kuonesha nia thabiti ya kuwekeza kwenye sekta mbalimbali mkoani humo ikiwemo maduka makubwa ya biashara (shopping malls) na hoteli za kimaifa zenye hadhi ya nyota tano” alisema Dkt. Ndumbaro.

  Mhe. Dkt. Ndumbaro aliongeza kusema kuwa, ushirikiano kati ya Tanzania na Uturuki umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka kutokana na jitihada zinazofanywa na Serikali ikiwemo kusainiwa kwa mikataba mbalimbali ya ushirikiano, kuboreshwa kwa mazingira ya uwekezaji na biashara hapa nchini na ufunguzi wa Balozi. Alieleza kuwa, kutokana na jitihada hizo Kampuni nyingi za Uturuki zimeonesha nia na shauku ya kuwekeza na kufanya biashara hapa nchini.

  “Takwimu zinaonesha kwamba kutoka mwaka 1990 hadi mwezi Septemba mwaka 2018 jumla ya Kampuni 48 za Uturuki zimewekeza Tanzania. Uwekezaji huo unathamani ya Dola za Kimarekani milioni 324.46 na umezalisha ajira 3,455 kwa Watanzania katika maeneo mbalimbali” alisema Dkt. Ndumbaro.

  Akizungumzia biashara kati ya Tanzania na Uturuki, Mhe. Dkt. Ndumbaro alieleza kuwa imeimarika kwa kiasi kikubwa katika miaka ya hivi karibuni ikilinganishwa na miaka kadhaa iliyopita.

  Mhe. Dkt. Ndumbaro alieleza kuwa awali Tanzania ilikuwa ikiingiza zaidi bidhaa kutoka Uturuki kama zana za kilimo, bidhaa za ujenzi, nguo na bidhaa mbalimbali za plastiki. Hata hivyo, mwaka 2017 kumekuwa na mabadiliko makubwa kwa Tanzania kuuza zaidi bidhaa zake Uturuki kama pamba, mbegu za mafuta, korosho na tumbaku kuliko Uturuki ilivyouza bidhaa zake Tanzania. 

  “Kwa mfano wakati bidhaa zilizouzwa Tanzania kutoka Uturuki zikiwa na thamani ya shilingi bilioni 6.091 tu, Tanzania iliuza bidhaa Uturuki zenye thamani ya Shilingi bilioni 154.749. Mabadiliko haya chanya yamechochewa na sababu mbalimbali ikiwemo juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki na Sekta Binafsi ya Tanzania kuchangamkia fursa mbalimbali za masoko zinazojitokeza Uturuki” aliongeza Dkt. Ndumbaro.

  Mhe. Naibu Waziri alisema kuwa ujumbe wa Makampuni hayo makubwa kutoka Uturuki ni fursa muhimu kwa Tanzania hususan kwenye mikoa ambayo yameonesha nia ya kuwekeza. Aliongeza kuwa uwekezaji utakaofanywa na Makampuni hayo utatoa fursa kubwa kwa Watanzania ambapo inakadiriwa takribani ajira 1,400 zitatolewa na Makampuni hayo.

  Kabla ya kuelekea Dodoma na Simiyu kwa ajili ya kuendelea na ziara, wawekezaji hao, watafanya mkutano na wadau muhimu wa masuala ya uwekezaji jijini Dar es Salaam ambao ni; Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Chama cha Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Wakulima (TCCIA), Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji Tanzania (EPZA), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

  Mkutano kati ya Dkt. Ndumbaro na Waandishi wa Habari ulihudhuriwa pia na Balozi wa Uturuki hapa nchini, Mhe. Ali Davutoglu ambaye nae alisisitiza nchi yake kuendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala mbalimbali ikiwemo uwekezaji, utalii na biashara ili kuzililetea maendeleo nchi hizi mbili.

  Imetolewa na:
  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
  Dar es Salaam.
  18 Novemba 2018


  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza Bibi Niachia Kalembo kutoka kijiji cha Mtimbo wilayani Nachingwea ambaye ni mmoja wa wazazi waliojifungua katika Kituo cha Afya cha Mkowe wilayani Ruangwa wakati alipotembelea kituo hicho, Novemba 18, 2018  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa amembeba mtoto aliyezaliwa katika kituo cha Afya cha Mkowe wilayani Ruangwa na Bibi Asia Abdallh (kushoto) wakati alipotembelea wodi ya wazazi katika Kituo hicho Novemba 18, 2018.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mtambo wa utakatishaji vifaa vya upasuaji katika Kituo cha Afya cha Mkowe wilayani Ruangwa, Novemba 18, 2018.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi khanga Muuguzi wa Kituo cha Afya cha Mkowe wilayani Ruangwa, Grace Nanguka ikiwa ni zawadi ya watumishi wote wa Kituo hicho wakati alipokagua ujenzi na ukarabati wa Kituo hicho, Novemba 18, 2018.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Walimu na baadhi ya wanafunzi wa Shule za Msingi za wilaya ya Ruangwa kwenye ukumbi wa Narung’ombe, Novemba 18, 2018. Kulia ni Mkewe Mary, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi na wapili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Ruangwa, Hashim Ngandirwa.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwaametembelea kituo cha afya cha Nkowe na kuwataka wananchi wakilinde na kukienzi kwa kuwa ndio mkombozi wao kiafya.Amesema kwa sasa wananchi hao hawana sababu ya kulipa nauli kwenda Ruangwa kufuata huduma za vipimo na matibabu katika hospitali ya wilaya hiyo.

  Waziri Mkuu ametembelea kituo hicho cha afya leo (Jumapili, Novemba 18, 2018) akiwa katika ziara yake ya kikazi Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.Ametaja baadhi ya huduma zinazopatikana kwa sasa kwenye kituo cha Afya Nkowe ambazo awali hazikuwepo kuwa ni pamoja na upasuaji, maabara, mama na mtoto.
  “Rais Dkt. John Magufuli anataka kila Mtanzania apate huduma za afya karibu na makazi yake ili asilipe nauli au kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya.”

  Waziri Mkuu amesema amefurahishwa na huduma zinazotolewa kituoni hapo, ambapo amewataka watumishi waendelee kuwahudumia wananchi vizuri.Baadhi ya wagonjwa waliolazwa katika kituo hicho cha afya wameishukuru Serikali kwa kuboresha huduma za afya nchini, ambapo kwa sasa wanatibiwa karibu na makazi yao. Awali, Mganga Mfawidhi wa kituo hicho, Dkt. Paul Mbinga alisema kituo hiko kinahudumia jumla ya wakazi 5,264 wa kata ya Nkowe pamoja na wananchi wa kata za jirani za Chienjele, Nandagala, Likunja na Mnacho. 

  Alisema baada ya kukamilika kwa mradi huo wananchi sasa wanapata huduma ambazo walikuwa wanalazimika kuzifuata katika hospitali ya wilaya zikiwemo za upasuaji, damu salama, maabara, kujifungua, kulaza wagonjwa na kuhifadhi maiti.Dkt. Mbinga alisema mradi wa ujenzi wa kituo hicho cha afya uliogharimu sh. milioni 500 umepunguza gharama kwa wananchi zinazoambatana kwenda kutibiwa katika hospitali ya wilaya ambayo ipo umbali wa kilomita 20. “Mradi huu umeimarisha mifumo ya huduma kwa watoto, wazee, watu wenye ulemavu na vijana.

  Baada ya Waziri Mkuu kutembelea kituo hicho cha afya, alikwenda kukagua ujenzi wa gereza la wilaya ya Ruangwa pamoja na mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi ya askari Magereza wa gereza hilo.


  IMETOLEWA NA:

  OFISI YA WAZIRI MKUU,JUMAPILI, NOVEMBA 18, 2018.

  0 0

  Na. Vero Ignatus, Arusha

  Mamlaka ya mawasiliano Nchini kanda ya kaskazini imeendesha semina ya siku moja kuhusu huduma za utangazaji kwa chanel zinazotazamwa bila kulipia 

  Akizungumza katika semina hiyo Mkuu wa Kanda ya Kaskazini Francis Msungu amesema leo ngo kuu la serikalini kuwataka watoa huduma kujenga miundo mbinu ya Minara hapa nchini na hii itapelekea watanzania wengi watapata ajira. Katika semina hiyo iliyojumuisha viongozi mbalimbali wa serikali ngazi ya mkoa washiriki kuweza kuuliza maswali nje ya mada yanayohudu vifaa vya mawasiliano, simu, tekevisheni pamoja na radio.

  Mamlaka hiyo ya Mawasiliano iliweza kutoa ufafanuzi kwamba maduka yanayouza vifaa vya mawasiliano vya eletroniki wauzaji wake wanatakiwa kuwa na leseni kutoka mamlaka ya mawasiliano sambamba na ile ya biashara.Msungu amesema kuwa mafundi wanaotengeneza simu za mkononi wanapaswa pia kwa mujibu wa sheria wawe na kibali kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Nchini.

  Ndiyo maana tumeshauri wananchi kupitia viongozi kwamba unapopeleka kutengeneza simu yako kabla hujampa mtu kuitengeneza hakikisha je anacho kibali kinachomruhusu kufanya hiyo shughuli hiyo?
  Unapokwenda dukani kununua kifaa chako cha mawasiliano radio, televisheni ni haki yako kujua je huyu anayeniuzia ametathimishwa kufanya hiyo kazi?

  Amesema lengo kubwa la Mamlaka kuwataka watu hawa kuwa na leseni ni kumlinda mtumiaji wa hizo huduma(mlaji).Unapoenda kununua kifaa chako hakikisha umepewa risiti na sasa risiti hiyo imeongezewa kazima iwe na Efd ya TRA, lazima uwe na garantiii kama kunatokea lolote uweza kufidiwa kile kifaa na kupatiwa kingine hiyo ndiyo nia njema ya serikali kuweka huo utaratibu. Alisema

  Amesema baadhi ya mafundi wanapotengeneza vifaa vya wateja wao asilimia kubwa wanabadilisha namba tambulishi na kupewa namba ya mtu mwingine ambapo amesema hilo ni tatizo.Kwa usalama wa nchi hili swala la msingi sana najua namba ya simu kitamvulishi ni kitambulisho muhimu kwa watumiaji wa simu hivy kuweni makini, hata vocha mnapozitumia msizitumie hovyo. Alisema

  Msungu amewashauri wananchi kunua Madishi ya setilite badala ya kununua antena za kawaida hii itasaidia kuto kununua vingamuzi vingi. Katika semina hiyo muwezeshaji injinia Jan Kaaya amefundisha kuhusu masharti ya urushaji wa Maudhui. Amesema Masharti ya Leseni yananawataka watoa huduma kuhakikisha maudhui yao yanatazamwa bila Malipo.

  Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Arusha Dc akifungua semina hiyo Gabriel Daqqaro amesema viongozi walio hudhulia Mafunzo haya ni vema zaidi kutumia Mafunzo hayo kuwafundisha wananchi. 

  Moja ya washiriki katika semina hiyo Mwalimu mkuu Salei Bi. Miminini Payema ameiomba mamlaka ya Mawasiliano ifanye mawasiliano kufanya Mazungumzo na Wamiliki wa DSTV ili kupata chanel za ndani Bure. 
  Wapili kutoka kulia ni Katibu Tawala David Mwakiposa wa wilaya ya Arusha akibadilishana mawazo na Kaimu mkurugeni wa jiji la Arusha Valentine Makuka pamoja na Mkuu wa wilaya Arusha Gabriel Daqqaro
  Washirili wa warsha hiyo wakiendelea kufuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiendelea 
  Mkuu wa Kanda ya Kaskazini TCRA Francis Msungu

  Muwezeshaji wa Warsha hiyo Injinia Jan Kaay (TCRA) akiendekea kutoa elimu kwa washiriki.
  Wakwanza kulia ni mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro ndiye akiyefungua warsha hiyo ya siku moja ya watumishi na viongozi mbalimbali wa serikali mkoani Arusha katika ukumbi wa Goldenrose.
  Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo wakiendelea kufuatilia kwa makini

  0 0

  Kamishna wa Bima Nchini, Dkt. Baghayo Saqware amefanya mazungumzo na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Prof. Mussa Juma Assad yaliyolenga kukuza ushirikiano wa usimamzi wa sekta ya bima na ukaguzi wa hesabu za serikali.

  Akizungumza na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali mwishoni mwa wiki, Dkt. Saqware alisema Mamlaka ya Usimamizi wa shughuli za Bima (TIRA) imefanya mabadiliko madogo ya sheria ya bima Na. 10 ya Mwaka 2009 katika kifungu cha 133, kinachotaka majanga yote ya yapewe kinga na makampuni ya Bima yaliyosajiliwa na Mamlaka, na kuomba Ofisi ya CAG kuweka utaratibu wa ukaguzi wa utekelezaji wake kwenye miradi ya serikali.

  “Ndugu CAG, mabadiliko haya yanataka majanga yanayotokana nauendashaji wa shughuli zote za kiuchumi na kijamii kukatiwa bima na
  makampuni yenye usajili nchini, ndiyo sababu serikali imeona ni vematushirikiane katika kuhakikisha taasisi zetu zinakidhi matakwa ya
  sheria hii” alisema Dkt. Saqware.

  Serikali ya Awamu ya Tano inatekeleza miradi mingi na mikubwa yakimkakati hivyo ni fursa adhimu kwa kwa sekta ya bima kushirikikikamilifu katika kuhakikisha miradi hii inapatiwa kinga dhidi ya
  majanga yanayoweza kuathiri na kuchelewesha utekelezaji wa Miradihiyo
  .
  “Uchumi wetu hautakuwa dhabiti ikiwa tutaendelea kuruhusu kinga zabima za miradi hiyo kwenda kunufaisha makampuni ya nje ya nchi, hii
  ndiyo sababu Mamlaka imeishauri Serikali kufanya mabadiliko ya sheriaili kuimarisha soko la bima la ndani na kuzuia utoroshwaji wa fedha”,
  aliongeza Dkt. Saqware.

  Pamoja na kuombaOfisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu zaSerikali kusimamia utekelezaji wa sheria hii, ili taasisi za ummazinunue bima kutoka makampuni ya ndani, Dkt. Saqware alimpitisha Prof.
  Assad katika mabadiliko mengine ya sheria ya Bima.

  Mabadiliko hayo ni pamoja na kuzuiwa kwa ulipaji wa bima za mizigoinayoingizwa nchini kwa kampuni za bima za nje ya nchi, ambapo Taasisiya Bima nchini (IIT) kwa kushirikiana na Mamlaka imeandaa mfumo wakieletroniki unaotumika kulipia bima za mizigo yote inayoingizwanchini kwa kutumia makampuni ya ndani.

  Kwa upande wake Prof. Assad alisema ni muda muafaka kwa uongozi waMamlaka kuonana na ofisi yake ili kujadili namna ya utekelezaji wamabadiliko ya sheria, kwani kazi za udhibiti na ukaguzi wa hesabu zaserikali unahitaji utayari wa wadau mbalimbali katika kuifanikisha.

  “Niseme tu, nimefurahi kupata maelezo ya namna gani sekta ya bimaimejipanga kudhibiti mianya ya upotevu wa raslimali za nchini, naninawahakikishia kuwa ofisi yangu iko tayari kushirikiana nanyi katikakuhakikisha mashirika na taasisi za serikali zinakuwa mfano wa kuigwakatika utekelezaji wa sheria hii, alisema Prof. Assad.

  Mabadiliko haya ni sehemu ya jitihada za Mamlaka ya Usimamizi waShughuli za Bima kuendelea kutekeleza vipaumbele vya serikali katika
  ukuaji wa sekta ya bima na kuhakikisha inakuwa na mtaji wa kutoshakuhimili majanga kwa kiwango kikubwa.

  0 0


  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Watu wa Jamuhuri ya China Mhe. Cai Defeng, alipowasili Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo wa Rais wa Zanzibar leo tarehe 18/11/2018


  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Ujumbe wa Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Watu wa Jamuhuri ya China, Ikulu Zanzibar, akitambulishwa na Makamu Mwenyekiti wa Bunge Mr. Cai Defeng katikati.
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Watu wa Jamuhuri ya China Ikulu Zanzibar,kulia Makamu Mwenyekiti wa Bunge la China Mr. Cai Defeng na Ujumbe wake walipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo leo,18/11/2018
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Watu wa China Mr. Cai Defeng alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo.akiwa na Ujumbe wake

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Watu wa Jamuhuri ya China na Ujumbe wake na Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, baada ya mazungumzo yao Ikulu Zanzibar.tarehe 18/11/2018

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na mgeni wake Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Watu wa Jamuhuri ya China Mr. Cai Defeng akimuonesha mandhari ya visiwa vya Zanzibar wakiwa nje ya ukumbi wa mkutano baada ya mazungumzo yao Ikulu Zanzibar.leo tarehe 18/11/2018.(Picha na Ikulu

older | 1 | .... | 1726 | 1727 | (Page 1728) | 1729 | 1730 | .... | 1898 | newer