Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1725 | 1726 | (Page 1727) | 1728 | 1729 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Na Farida Ramadhani, WFM, Dodoma


  Serikali imesema kuwa vikundi vya Upatu havitasimamiwa chini ya Sheria mpya ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2018 (The Microfinance Act, 2018)kwa sababu havijihusishi na biashara ya huduma ndogo za fedha.

  Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) wakati akihitimisha hoja za mjadala waMuswada wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2018.

  Dkt. Mpango alisema Sheria hiyo itahusisha taasisi kama vile Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS), Taassi za huduma ndogo za fedha zisizopokea na zinazopokea amana na vikundi vya kifedha vya kijamii, wakopeshaji binafsi na asasi za kijamii.

  Alieleza kuwa Sheria hiyo pia inalenga kuwalinda wananchi wanaotegemea sekta ndogo ya fedha katika kuendesha maisha yao na shughuli za kiuchumi kwa ujumla na itasimamia na kudhibiti biashara ya huduma ndogo za fedha, kuwawezesha watumiaji na watoa huduma hiyo pamoja na kudhibiti changamoto zinazoweza kutokea katika sekta hiyo.

  “Madhumuni ya Sheria hiyo ni kuwatambua watoa huduma ndogo za fedha kwa lengo la kuwasimamia, kupata takwimu, kuwalinda na kuwawezesha watumiaji wa huduma ndogo za fedha”, alisema Waziri Mpango.

  Dkt. Mpango aliongeza kuwa Sheria hiyo imeweka utaratibu wa kuiwezesha Benki Kuu kutoa elimu kwa watumiaji wa huduma ndogo za fedha hususan vikundi vya kijamii kwa lengo la kunufaika na fursa zilizopo.

  Aliongeza kuwa wakati Benki Kuu itakapolazimika kusimamia Taasisi za huduma ndogo za fedha, taasisi hizo hazitatozwa fedha kugharamia majukumu ya Benki Kuu.

  Akizungumzia maoni wa wabunge kuhusu daraja la nne la Sheria hiyo linalohusu vikundi vya kifedha vya kijamii, wakopeshaji binafsi na asasi za kijamii, Waziri Mpango alifafafanua kuwa Sheria hii imebainisha kwamba kutaandaliwa kanuni na miongozo mahsusi kwa ajili ya kusimamia daraja hilo.

  “Sheria hii inaainisha shughuli mbalimbali zinazoweza kufanywa na mabenki na taasisi za fedha zinazoweza kusaidia katika kulea na kukuza watoa huduma wa daraja la nne. Miongoni mwa shughuli hizo ni pamoja na utoaji mikopo yenye msharti nafuu na elimu ya fedha”, alisema Dkt. Mpango.

  Alisema kuwa Serikali imejipanga kutenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa usimamizi wa daraja la nne. Mwongozo kwa ajili ya maandalizi ya bajeti ya 2019/20 umetoa maelekezo kwa Halmashauri zote kutenga fedha kwa ajili ya kazi hii.

  Aidha, baada ya Waziri Mpango kuwasilisha hoja hizo, Bunge lilipitisha Muswada wa Sheria hiyo ambao umeundwa baada ya kujitokeza changamotombalimbali zinazoikabili sekta ndogo ya fedha ikiwemo Taasisi za huduma ndogo za fedha kutoa mikopo kwa wananchi kwa vigezo na masharti magumu na hivyo kusababisha madhara kwa wananchi ikiwemo mali zao kuuzwa pasipo kufuatwa kwa taratibu za kisheria.
  Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Dkt. Adelardus Kilangi, akijibu hoja za wabunge wakati wa kuhitimishwa kwa mjadala wa Muswada wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha, bungeni, Jijini Dodoma. Walioketi kulia kwake ni Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb).
  Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akijibu hoja za Waheshimiwa Wabunge kuhusu Muswada wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha, bungeni Dodoma.
  Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) katikati, na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Adelardus Kilangi(kushoto) wakigonga meza kuashiria kuunga mkono hoja wakati wa kujibu hoja za Muswada wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha, bungeni Dodoma, kulia ni Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akifuatilia kwa makini hoja hizo
  Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), kushoto, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), kulia, wakiteta jambo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Adelardus Kilangi (katikati) wakati wa kujibu hoja za Muswada wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha, bungeni Dodoma.Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)

  0 0


  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Balozi Mpya wa Palestine Nchini Tanzania. Mhe. Hamdi.M.H.Abuali, alipofika Ikulu Zanzibar, leo kwa mazungumzo na kujitambulisha.tarehe 16/11/2018.(Picha na Ikulu)
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Balozi Mpya wa Palestine Nchini Tanzania Mhe. Hamdi M.H.Abuali, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha leo 16/11/2018, Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na mgeni wake Balozi Mpya wa Palestine Nchini Tanzania.Mr.Hamdi M.H.Abuali, baada ya mazungumzo yao alipofika Ikulu Zanzibar leo kujitambulisha.tarehe 16/11/2018.(Picha na Ikulu)
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na CEO wa Chuo Kikuu cha “Houkeland University Hospital” Mr.Eivind Hamsen, alipofika Ikulu Zanzibar na Ujumbe wake wa Madaktari Bingwa kwa mazungumzo,leo tarehe 16/11/2018.(Picha na Ikulu)
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Ujumbe wa Madaktari Bingwa kutoka Chuo cha “Houkeland University Hospital” kulia Mr. Eivind Hamsen -CEO,akiwa na ujumbe wake walipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo leo.tarehe.16/11/2018.(Picha na Ikulu)
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Ujumbe wa Madaktari Bingwa kutoka Norway Chuo Kikuu cha “Houkeland University Hospital” kulia Wairi wa Afya Zanzibar Mhe. Hamad Rashid Mohammed,anayefuata ni CEO Eivind Hamsen na John Wigum Dahil, wakifuatilia mazungumzo hayo wakiwa nje ya ukumbi baada ya mazungumzo yao leo Ikulu Zanzibar.terehe 16/11/2018.(Picha na Ikulu)
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Madaktari Bingwa kutoka Chuo Kikuu cha “Houkeland University Hospital” walipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo leo.tarehe 16/11/2018.(Picha na Ikulu)  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein amesema misaada mbali mbali iliyotolewa na Chuo Kikuu ‘Houkeland University Hospital’, imekwenda sambamba na dhamira ya muda mrefu ya Serikali ya kutoa huduma bora za tiba ya akili kwa wananchi wake.

  Dk. Shein amesema hayo leo Ikulu mjini Zanzibar, alipozungumza na ujumbe wa Madaktari wanne kutoka chuo kikuu cha ‘Houkeland University Hospital’ cha nchini Norway, ukiongozwa na Katibu Mtendaji Eivind Hamsen. Alisema kwa nyakati tofauti Serikali kwa kushirikiana na washirika wa maendeleo imekuwa ikifanya kila juhudi kuhakikisha inaimarisha upatikanaji wa huduma za tiba ya akili katika Hospitali yake iliopo Kidongochekundu mjini hapa na kuondokana na dhana iliyojengeka miongoni mwa jamii kuwa eneo hilo ni ‘jela’ ya wagonjwa hao.

  “Serikali imekuwa ikifanya kila juhudi kuimarisha Hospita hiyo, ili ionekane ni kituo cha tiba ya akili, sio tena jela ya wendawazimu kama ilivyokuwa ikitambulika mara baada ya kuanzishwa kwake”, alisema. Alisema juhudi hizo ziliambatana na uanzishaji wa sera mpya na sheria za uendeshaji wa hospitali hiyo, zikilenga kuleta mageuzi makubwa katika suala la upatikanaji wa huduma bora kwa wagonjwa.

  Alisema tayari kuna mafanikio makubwa yaliofikiwa, katika upatikanaji wa huduma za tiba ya akili, huku mkazo ukielekezwa kukiimarisha zaidi. Katika hatua nyengine Dk. Shein alisema Zanzibar imepata mafanikio makubwa katika sekta ya Afya, kwa kuiimarisha Hospitali kuu ya Mnazi mmoja, Hospitali za Wilaya pamoja na vituo vya Afya Unguja na Pemba, kwa kuvipatia vifaa vya kisasa na mafunzo kwa madaktari wake.

  “ Kwa kushirikiana na washirika wa maendeleo tumeimarisha Hospitali kuu ya Mnazi mmoja na zile zilioko Wilayani, huduma mbali mbali zinapatikana kwa urahisi na bila ya malipo yoyote; kama vile MRI, watu wamekuwa wakitoka nje ya Zanzibar kufuta matibabu hapa”, alisema. Nae, Kiongozi wa ujumbe huo kutoka ‘Houkeland University Hospital’ COE Elvind Hamsen, alisema wameridhishwa na juhudi kubwa zilizochukuliwa na Serikali katika kuiendeleza Hospitali hiyo, sambamba na huduma bora zinazotolewa na wafanyakazi wake.

  Alisema Chuo hicho kitaendeleza ushirikiano uliopo ili kuimarisha upatikanaji wa huduma kwa maslahi ya jamii ya Wazanzibari. “Hatuhesabu kiwango gani cha fedha zimetumika, bali tunazingatia vipi upatikanaji wa huduma zitakavyoimarika”, alisema Hamsen. Aidha, kiongozi huyo alimhakikishia Rais wa Zanzibar kuwa Chuo hicho kitasaidia uanzishaji wa Hospital kuu ya kisasa, inayotarajiwa kujengwa katika eneo la Binguni, Mkoa Kusini Unguja.

  Chuo kikuu cha Houkeland University Hospital, kimekuwa na mradi wa kuisaidia Hospital ya Wagonjwa wa Akili, Kidongochekundu kupitia Nyanja mbali mbali ikiwemo kuboresha kitengo cha Pathology,ecology pamoja na kutoa mafunzo mbali mbali kwa watendaji katika masuala ya tiba ya akili.

  Wakati huo huo, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein amesema Zanzibar itaendelea kuimarisha ushirikiano uliopo kati yake na Taifa la Palestina, kwa maslahi mapana ya watu wa nchi mbili hizo. Amesema uhusiano na ushirikiano uliopo kati ya nchi mbili hizo ni wa muda mrefu, tangu enzi za muasisi wa Taifa hilo, Hayati Yasser Arafat, ukijikita katika nyanja za kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.

  Dk. Shein amesema hayo leo Ikulu mjini Zanzibar, alipozungumza na Balozi mpya wa Palestina nchini, Hamad M.H. Abuali, aliefika kujitambulisha. Alisema Serikali imeazimia kupanua wigo wa ushirikiano na Palestina katika nyanja za kiuchumi na kijamii, hususan kupitia sekta za Utalii, afya pamoja na biashara zitokanazo na kilimo. Alisema pamoja na Taifa hilo kupitia katika changamoto mbali mbali za kiusalama, tayari imepata mafanikio makubwa, hivyo ipo haja kwa nchi mbili hizo kushirikiana katika suala la mafunzo pamoja na kubadilishana wataalamu.

  Dk. Shein,aliwataka wananchi wa Palestina kujidhatiti na kuongeza juhudi katika harakati za kudai haki yao, kwa kuamini kuwa iko siku watafanikiwa. Nae, Balozi Abuali alimuahakikishia Dk. Shein azma ya Taifa hilo kuendeleza ushirikiano uliopo kati yake na Zanzibar, ili kuongeza kasi ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

  Alisema Palestina itafanya kila juhudi kuhakiksha kunakuwepo mafungamano mema kati ya nchi mbili hizo, ili kuona sekta zilizoainishwa zinakuwa chachu ya kuendeleza uchumi wa Zanzibar

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akiwa ameambatana na Mstahiki Meya wa jiji, Mamea wa Halmashauri na Madiwani wamefanya ziara Mkoani Morogoro kwenye Stand Mpya ya Mabasi ya Msamvu kujifunza namna stand hiyo imefanikiwa kuweka mazingira jumuishi kwa makundi yote wakiwemo wafanyabiashara na wasafiri.
  2
  RC Makonda amesema Dar es salaam ipo katika hatua ya ujenzi wa stand Mpya ya kisasa Mbezi Luis itakayogharimu zaidi ya shilingi Billion 50.9 ambayo itakuwa na ukubwa Mara nne ya Stand ya Msamvu ambapo itakuwa na uwezo wa kupokea Mabasi 500 kwa wakati mmoja.

  Aidha RC Makonda amesema Stand mpya ya Mbezi Luis itakuwa na Jengo la Abiria,Utawala, maegesho ya mabasi, shopping mall, Hotel,Taxi, Bajaji, Pikipiki, Bank, Petrol station, Apartment, ofisi za mabasi, sehemu ya wafanyabiashara, mama Lishe,Vyoo,kituo cha polis na sehemu ya kuhifadhi mizigo.

  Pamoja na hayo RC Makonda ameonyesha kufurajishwa na namna stand ya Msavu ilivyoweza kuweka utaratibu mzuri kiasi cha kuongeza mapato kutoka shilingi 350,000 hadi kufikia Shilingi Million 4.5 kwa Siku.
  3
  Kwa upande wa viongozi wa Mkoa wa Morogoro wameshukuru kupokea ugeni huo mzito na wamesema watafika Dar es salaam kujifunza mambo mengi ambayo Jiji hilo limepiga hatua na kupata sifa kubwa ndani Na nje ya nchi.

  0 0


  Pichani ni Msajili Mkuu-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati akiwa katika mazungumzo pamoja na Wahe. Majaji kutoka Mahakama Kuu Zhejiang iliyopo Jamhuri ya Watu wa China walipotembelea Ofisi ya Mhe. Msajili Mkuu, Novemba 16, 2018.  Na Lydia Churi – Mahakama

  Majaji watano kutoka Mahakama Kuu ya nchini China wameitembelea Mahakama ya Tanzania ili kujifunza namna mfumo wa utoaji haki wa Tanzania unavyofanya kazi na pia kubadilishana uzoefu kuhusu masuala yakisheria na utoaji haki.

  Majaji hao kutoka jimbo la Zhejiang la nchini China pia wameitembelea Mahakama ya Tanzania kwa lengo la kujifunza zaidi na kubadilishana uzoefu hasa kuhusu adhabu zinazotolewa na Mahakama kwa ajili ya kuirekebisha jamii.

  Akizungumza na Majaji hao, Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Katarina Revocati amewaambia kuwa Mahakama ya Tanzania ni chombo huru kinachotekeleza majukumu yake kwa uhuru pasipo kuingiliwa na Mihimili mingine. Akizungumzia adhabu zinazotolewa na Mahakama katika kuirekebisha jamii hasa zile za kifungo cha nje, Msajili Mkuu alisema adhabu hizo hutolewa kwa mujibu wa sheria na kwa vigezo mbalimbali ikiwemo kupunguza msongamano wa wafungwa magerezani na kufanya shughuli za uzalishaji ili kuisaidia jamii.

  Alisema Mahakama ya Tanzania imekuwa ikishauri matumizi ya adhabu mbadala ikiwemo kazi za nje badala ya adhabu za kifungo gerezani. Kupitia adhabu hizi, wafungwa watatumika pia kufanya kazi za uzalishaji mali na kuisaidia jamii.

  Kwa upande wao, Majaji hao kutoka nchini China wamesema wamefika nchini kujifunza mfumo wa utoaji haki unavyofanya kazi na hasa kuhusu adhabu zinazotolewa na Mahakama katika kuirekebisha jamii kwa kuwa mfumo huo pia hutumiwa na Mahakama zao.

  Kwa mujibu wa Majaji hao, China inazo fursa nyingi za kuwaendeleza wanasheria kitaaluma na hivyo wametoa wito kwa Mahakama ya Tanzania kutumia fursa hizo katika kuwaendeleza watumishi wake kama ambavyo nchi nyingine zimekuwa zikifanya.

  0 0
  *Ni kuanzia Julai hadi Oktoba mwaka huu, kwa msingi na sekondari

  *Waziri Mkuu aonya wanaoshiriki wizi wa mitihani

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kati ya Julai na Oktoba, mwaka huu, Serikali imetoa jumla ya sh. bilioni 83.2 ili kuimarisha usimamizi na uendeshaji wa shule nchini.

  Waziri Mkuu amesema, kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 38.6 zilipelekwa kwenye shule za msingi na shilingi bilioni 44.6 zilienda kwenye shule za sekondari ikiwa ni utekelezaji wa mpango wa elimumsingi bila malipo.

  Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Ijumaa, Novemba 16, 2018) bungeni mjini Dodoma wakati akitoa hoja ya kuahirisha mkutano wa 13 wa Bunge. Bunge limeahirishwa hadi Januari 29, 2019.

  “Katika kuimarisha usimamizi na uendeshaji wa shule nchini, Serikali inapeleka fedha za elimumsingi bila malipo moja kwa moja shuleni. Kwa mfano, katika kipindi cha Julai hadi Oktoba, 2018 shilingi bilioni 38.6 zilipelekwa katika shule za msingi na shilingi bilioni 44.6 kwenye shule za sekondari,” amesema.

  Amesema tangu kuanza kutekelezwa kwa mpango wa elimumsingi bila malipo, uandikishaji wa watoto wa darasa la awali na darasa la kwanza umeimarika na kwamba kumekuwepo na mwenendo mzuri wa ufaulu kwenye mitihani ya kumaliza darasa la saba.

  “Kumekuwepo na mwenendo mzuri wa ufaulu katika mitihani ya kumaliza darasa la saba, ambapo mwaka 2016 ilikuwa wastani wa asilimia 70 na mwaka 2018 ilikuwa ni wastani wa asilimia 78. Hali hiyo, imeongeza mahitaji mbalimbali, ikiwemo miundombinu katika shule zetu za msingi na sekondari,” amesema.

  Waziri Mkuu amesema katika kukabiliana na hali hiyo, Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa elimu inaendelea na mikakati ya ujenzi na ukamilishaji wa miundombinu muhimu ya shule.

  “Kwa mfano, kupitia programu ya Lipa Kulingana na Matokeo katika Elimu (EP4R), shilingi bilioni 53.4 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya shule za msingi na sekondari. Aidha, shilingi bilioni 9.2 zimeelekezwa katika uimarishaji wa miundombinu ya elimu kupitia programu ya kuboresha elimu ya shule za msingi (EQUIP-T),” amesema.

  Amesema Serikali itaendelea kuimarisha miundombinu na kuweka mazingira mazuri katika mfumo mzima wa elimu nchini kwa kushirikiana na wadau wote.

  Wakati huohuo, Waziri Mkuu amesema taasisi zote zinazohusika na usimamizi na uendeshaji wa mitihani ya taifa hazina budi kuhakikisha zinasimamia kikamilifu mitihani hiyo ili kuepuka udanganyifu.

  “Natambua kuwa mitihani ya taifa kwa darasa la nne, kidato cha pili na kidato cha nne inaendelea. Hata hivyo, katika kipindi cha hivi karibuni kumezuka matukio ya kuvuja kwa mitihani.”

  “Naziagiza taasisi zote zinazohusika na usimamizi na uendeshaji wa mitihani ya taifa kuhakikisha wanasimamia kikamilifu mitihani hiyo ili kuepuka udanganyifu. Itakapobainika kuwepo kwa udanganyifu wa mitihani, hatua stahiki zichukuliwe kwa mujibu wa sheria dhidi ya yeyote atakayehusika,” amesisitiza.

  hiki zichukuliwe kwa mujibu wa sheria dhidi ya yeyote atakayehusika,” amesisitiza. 
   
   WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa

  0 0

  Jonas Kamaleki, MAELEZO, Dodoma

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuri atakuwa Mgeni Rasmi katika Mkutano wa 21 wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Bonde la Mto Nile zilizopo kwenye Ukanda wa Maziwa Makuu.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dodoma, Waziri wa Maji, Prof. Makae Mbarawa amesema Mkutano huo utapitia utekelezaji masuala mbali mbali ya miradi, utapokea taarifa ya utendaji, hali ya ulipaji wa michango ya kila mwaka kwa nchi wananchama na tathmini ya watumishi wa Sekretarieti ya NELSAP.

  Mkutano huo ambao utafanyika Jijini Dar es Salaam Novemba 22, 2018 utawashirikisha mawaziri wa Maji na wawakilishi kuto nchi za Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Misri, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Sudan, Sudani ya Kusini na Uganda.Prof. Mbarawa amesema kuwa Mkutano huu utatanguliwa na vikao vya wataalamu ambavyo ni vya kiutendaji na vitaanza tarehe 20 hadi 21 Novemba, 2018 Jijini Dar es Salaam.

  “Ushirikiano wa Nchi za Bonde la Mto Nile ni wa muda mrefu, umeanza tangu miaka ya 1960 na ilipofika tarehe 22 Februari, 1999 nchi wanachama ziliunda Taasisi ya Mpito ya Bonde la Mto Nile iitwayo Nile Basin Initiative-NBI. Taasisi hii ilianzishwa Dar es Salaam, na sasa inaelekea kutimiza miaka 20,”alisema Prof. Mbarawa.

  Bonde la Mto Nile ni ukanda wote wa eneo la Bonde la Mto huo kuanzia Ziwa Victoria hadi Bahari ya Mediterania ambapo Tanzania iko sehemu ya juu ya Bonde la Mto Nile ambako Mto Mara, Simiyu na Mto Kagera inamwaga maji katika Ziwa Victoria ni sehemu ya Bonde hilo. Mto Nile ni mrefu sana Duniani kwa kuwa na urefu wa kilomita 6,695.

  Tanzania ni miongoni mwa nchi 10 za Bonde la Mto Nile zinazoshirikiana katika kusimamia na kuendeleza Raslimali za Maji za Bonde la Mto huo chini ya mwavuli wa NBI.

  0 0


  Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Sokoine Dkt. Jumanne Shija akizungumza katika kikao cha tahimini ya utendaji kilichohusisha wataalam wa MHN pamoja na wataalam wa hospitali hiyo.
  Baadhi ya wataalam wa Hospitali ya Taifa Muhimbili pamoja na wataalam wa Hospitali ya Sokoine wakimsikiliza Kaimu Mganga Mfawidhi katika kikao hicho.
  Daktari Bingwa wa magonjwa ya kike na uzazi kutoka MNH Geofrey Marandu akielezea jambo katika kikao hicho.
  Katibu wa hospitali hiyo Boniface Lyimo akitoa neno la shukrani wakati wa kikao hicho.
  Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Sokoine akiwa katika picha ya pamoja na watalaam wa afya wa Idara ya Upasuaji mara baada ya kuanzishwa kwa idara hiyo kufuatia ushauri uliotolewa na wataalam wa MNH.


  Watalaam wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MHN) ambao walikua wakitoa huduma za afya kwa njia ya mkoba katika Hospitali ya Rufaa mkoa wa Lindi SOKOINE wamehitimisha huduma hiyo leo kwa kuwahudumia zaidi ya wagonjwa 1103 na kufanyia upasuaji wagonjwa 47.Maeneo ambayo wataalam wa Muhimbili wamehudumia kwa kushirikiana na wataalam wa Hospitali ya Sokoine ni upasuaji, magonjwa ya kike na uzazi, meno, macho,watoto, magonjwa ya mfumo wa mkojo, magonjwa ya dharura, Radiolojia pamoja na magonjwa ya ndani.

  Mbali na kutoa huduma hizo lakini pia watalaam wa Muhimbili wamewajengea uwezo kiutendaji wataalam wa hospitali hiyo pamoja na kuleta mabadiliko ikiwemo kuelekezwa jinsi ya kanzisha idara na kuzisimamia ili kuleta ufanisi katika utoaji huduma.Akizungumza katika kikao cha tathimini ya utoaji huduma, Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Sokoine Dkt. Jumanne Shija amesema kuanzishwa kwa idara mbalimbali kutaleta mabadiliko makubwa katika kutimiza majukumu yao kuanzia ngazi ya chini mpaka ya juu.Hivyo amewataka watumishi wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Lindi kukubali mabadiliko ili kufikia malengo ya utoaji huduma bora.

  ‘’Hospitali hii ni ya rufaa, wananchi wanaitegemea katika kupata huduma hivyo lazima tutoe huduma bora na zenye viwango vya juu na yote yatafanikiwa endapo kila mmoja atatimiza wajibu wake’’.amesisitiza Dkt. Shija.Kwa upande wake Daktari Bingwa wa magonjwa ya kike na uzazi kutoka MNH Geofrey Marandu amemsihi kiongozi wa hospitali hiyo kutowaonea aibu watumishi wanaokwamisha maendeleo ya hospitali.
  Ameto wito kwa watumishi hao kutumia fursa zinazojitokeza ili kupata ujuzi Zaidi.

  Mara baada ya kumaliza kutoa huduma katika hospitali ya Rufaa mkoa wa Lindi wataalam hao wataelekea Hospitali ya Ligula Mtwara kwa ajili ya kutoa huduma na kuwajengea uwezo wataalam wa hospitali hiyo.

  0 0


  Madaktari bingwa wa masikio, pua na koo pamoja na wataalam wengine wakiwa katika picha ya pamoja na watoto 10 waliopandikizwa vifaa vya kusaidia kusikia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Wataalam hao leo wamewaona watoto hao wodini ili kujua maendeleo ya afya zao baada ya kupandikizwa vifaa hivyo. Kutoka kulia ni Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Masikio, Pua na Koo kutoka Misri, Prof. Lobna El Fiky, Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Masikio, Pua na Koo, Dkt. Edwin Liyombo wa Muhimbili (aliyembeba mtoto) Kushoto ni mtaalam wa vifaa vya kusaidia kusikia kutoka Misri, Mohamed El Disouky na mtaalam wa usikivu, Fayaz Jaffer na wengine ni wazazi wa watoto hao. Wazazi wa watoto hao wametoka mikoa mbalimbali nchini ikiwamo Kilimanjaro, Songea na Tanga. Hadi sasa idadi ya watoto waliopandikizwa vifaa hivyo imefikia watoto 21.
  Watoto waliopandikizwa vifaa vya kusaidia kusikia wakiwa wodini baada ya kupatiwa huduma hiyo.
  Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Masikio, Pua na Koo kutoka Misri, Prof. Lobna El Fiky akifuatilia maendeleo ya mtoto aliyepandikizwa vifaa vya kusaidia kusikia na wataalam wa Muhimbili kwa kushirikiana na wataalam kutoka Misri. Kushoto ni Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Masikio, Pua na Koo, Dkt. Edwin Liyombo wa Muhimbili. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji wa Muhimbili, Dkt. Sufiani Baruani. Wengine ni wataalam wa magonjwa ya masikio, pua na koo.
  Mmoja wa wazazi wa watoto waliopatiwa huduma hiyo akizungumza na Prof. Lawrence Museru wa Muhimbili kuhusu maendeleo ya afya ya mtoto wake. Kushoto ni Prof. Lobna El Fiky.

  0 0


  Mhandisi Barton Komba wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), (aliyesimama mbele), leo akitoa maelezo ya maendeleo ya mradi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere kwa Wajumbe wa Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar walipofanya ziara ya mafunzo.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Lawrence Thobias (kulia mbele waliosimama), akiielezea Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar namna ya uendeshaji, ukusanyaji na mgawanyo wa mapato kwa mujibu wa sheria, wakati ilipotembelea Jengo la Tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere.
  Mhandisi Barton Komba wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), (aliyenyoosha mkono) akitoa ufafanuzi kwa Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar leo ilipotembelea Jengo la Tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere.
  Wajumbe wa Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakimsikiliza Mhandisi wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Bartyon Komba akitoa maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Jengo la Tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, walipotembelea leo.
  Wajumbe wa Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakimsikiliza Mhandisi wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Bartyon Komba akitoa maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Jengo la Tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, walipotembelea leo.

  ………………………………………………………………………..

  Na Mwandishi Wetu

  WAJUMBE wa Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi la Zanzibar imekiri kujifunza mambo makubwa katika ujenzi wa jengo la Tatu la Abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TB3), imeelezwa.

  Mwenyekiti wa Kamati hiyo, ambayo ilikuwa na ziara kwenye jengo hilo na Mhe. Mohammed Said (Mwakilishi wa Mpendae), amesema ujenzi wa jengo hilo ni fundisho tosha kutokana na kwenda kwa kasi tangu ujenzi wake uanze Juni 2013, tofauti na ujenzi wa jengo la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Amani Abeid Karume umechukua takribani miaka 10 tangu mwaka 2009 lakini hadi sasa lina asilimia 39 pekee.

  Mhe. Said amesema TB3 ni jengo la kisasa kutokana na miundombinu yake ambayo mingi inaendeshwa kwa mifumo maalum, ikiwemo sehemu ya mizigo, ambayo inaendeshwa kupitia hatua tano.

  “Katika ziara hii tumefarijika sana kwani tumejifunza mengi wenzetu walivyoweza kuufikisha mradi huu, kwa kweli tumechukua yote na tutakwenda kuishauri serikali namna bora ya kuendeleza ujenzi wa majengo na viwanja vya ndege kwa ujumla,” amesema Mhe. Said.

  Hali kadhalika, Mhe Said amesema mbali na kutembelea jengo hilo, pia wamepata maelezo mazuri ya kiutendaji katika uendeshaji, ukusanyaji na mgawanyo wa mapato kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), na wataishauri serikali namna bora ya kudhibiti mapato.

  Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Bw. Lawrence Thobias, ameishukuru kamati hiyo kwa kuichagua TAA kuwa sehemu yake ya mafunzo, kwa kuwa imezoeleka wengi wanaotaka kujifunza lazima waende nje ya nchi.

  Bw. Thobias amesema TAA ikiwa ni moja ya taasisi za serikali chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, imekuwa ikijiendesha kwa kufuata sheria na taratibu za ukusanyaji wa mapato za serikali.

  Akiwasilisha maendeleo ya mradi wa jengo la tatu la abiria, mmoja wa wasimamizi kutoka Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Burton Komba amesema hadi kufikia Oktoba 31, 2018 umefikia asilimia 85.53 na unatarajiwa kukamilika Mei 2019.

  Mhandisi Komba amesema ujenzi wa jengo hilo ambalo litahudumia abiria milioni sita kwa mwaka, umehusisha eneo la maegesho ya ndege lenye mita za mraba 227,000 lenye uwezo wa kuegesha ndege 19 za Daraja C kwa wakati mmoja zikiwa kwenye madaraja na eneo lisilokuwa na madaraja.

  “Pia eneo hili linaweza kuegesha ndege za daraja E 11 mfano wa hii Dreamliner ya ATCL Boeing 787 na Boeing 777, ni eneo kubwa,” amesema.

  Pia amesema kumejengwa maegesho ya magari mchanganyiko yasiyopungua 2075 kwa wakati mmoja; barabara za kuingia na kutoka eneo la jengo; uzio wa usalama, mifumo ya maji taka nay a mvua; ujenzi wa matanki ya kuhifadhia maji yenye ujazo wa lita milioni 2.26; kituo kikubwa cha umeme (33Kv); usimikaji wa jenereta saba zenye uwezo wa KvA 2000 kila moja; ujenzi wa mifumo ya kujaza mafuta kwenye ndege na kusimika mifumo ya mawasiliano na usalama.


  0 0

  NA Estom Sanga- DSM

  Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika,Dr. Hafez Ghanem amefanya ziara katika mtaa wa Mamboleo,halmashauri ya wilaya ya Temeke jijini DSM na kukutana na Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF.

  Akizungumza na Walengwa hao baada ya kukagua bidhaa wanazozitengeneza kama njia mojawapo ya kukuza kipato chao, Dr. Ghanem amesema jitihada waliyonyesha Walengwa hao ya kuuchukia Umaskini ,itaendelea kuungawa mkono na Benki hiyo ya Dunia ambayo amesema ni rafiki mkubwa wa Serikali ya Tanzania.

  Dr.Ghanem ametoa rai maalum kwa Walengwa hao wa TASAF kutumia fursa hiyo kuongeza uzalishaji mali na kutumia mazingira mazuri ya kujiletea maendeleo kwani amesema ni dhahiri kuwa serikali ya Tanzania inawajali na imeonyesha utayari wa kuboresha maisha ya wananchi. Aidha Makamu huyo wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika ambaye aliambatana na Mkurugenzi Mkazi wa Benki hiyo Bi. Bella Bird, amesisitiza kuwa taasisi hiyo kubwa ya fedha Duniani itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania kufadhili Mpango huo wa Kunusuru Kaya Maskini kutokana na mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha utekelezaji wake.

  Akizungumza kwenye Mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bw. Ladislaus Mwamanga ameelezea mafanikio makubwa ambayo Mfuko huo umepata tangu kuanzishwa kwake takribani miaka 18 iliyopita hususani katika nyanja za elimu,afya,maji, na uchumi. Bw. Mwamanga amesema mafanikio makubwa yaliyopatikana yametokana pia na usimamizi wa Karibu wa viongozi wa Serikali katika ngazi zote za utekelezaji ambapo wamekuwa wakiwahamasisha wananchi kutumia vizuri fursa hiyo ili waweze kuinua kiwango chao cha maisha na kutokomeza umaskini kwa kasi kubwa zaidi.

  Benki ya Dunia pamoja na taasisi nyingine za Kimataifa imekuwa ikichangia fedha kugharamia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambao kwa sasa unahudumia takribani kaya Milioni Moja na Laki Moja Tanzania Bara, Unguja na Pemba,Mpango ambao umekuwa chachu ya maendeleo kwa Kaya za Walengwa .Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika,Dr. Hafez Ghanem (watatu kulia) akiangalia bidhaa zinazozalishwa na kuuzwa na Walengwa wa TASAF katika eneo la Mamboleo,Temeke kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato.
  Baadhi ya walengwa wa TASAF wa Mtaa wa Mamboleo-Temeke jijini DSM wakiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa WB kanda ya Afrika Dr. Hafez Ghanem na viongozi wengine akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Ladislaus Mwamanga kulia kwa Makamu huyo wa Rais wa WB.
  Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika, Dr. Hafez Ghanem akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi ambao wazazi wao wako katika Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na serikali kupitia TASAF.
  Makamu Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika,Dr.Hafez Ghanem,akivishwa skafu alipowasili kwenye mtaa wa Mamboleo,wilayani Temeke jijini DSMalipokutana na Walengwa wa TASAF.

  0 0

   Mkurugenzi Mkuu Tume ya Nguvu za Atomiki Nchini Profesa Lazaro Busagala akizungumza na Meneja Mredi kutoka Jumuiya ya nchi za Ulaya Genevieve Liz pamoja na wageni wengine alioonhozana nao. 
  Denis Mwalongo Mkuu wa Idara ya Mionzi, mashine za kuhakiki vifaa vya mionzi katika mwili wa binadamu akiwaonuesha wageni hao kutoka Umoja wa Ulaya jambo 
  Dkt Wilbroad Muhogora mwenye (shati la draft) Mtafiti wa Tume akifafanua jambo kwa wageni kutoka Umoja wa Ulaya pamoja na, waandishi wa habari

  Na, Vero Ignatus Arusha 

  Umoja wa Ulaya (EU) umerithishwa na ujenzi wa maabara ya kisasa ya Tume ya Nguvu za Atomiki (TAEC) ikiwemo uwekaji wa vifaa vyenye thamani ya zaidi ya sh, bilioni 2.3. 

  Akizungumza mara baada ya kutembelea maabara hiyo, Meneja Mradi na Usalama wa Masuala ya Mionzi, kutoka EU, Genevieve Lizin alisema umoja huo umerithishwa na kazi nzuri ya uwekaji vifaa uliofanywa na serikali. 

  Alisema Umoja huo umeamua kutoa vifaa hivyo kwaajili ya kudhibiti masuala ya mionzi ndio maana wametoa ili kudhibiti masuala ya mionzi katika nchi za Afrika. "Maabara hii ni ya kisasa na hakuna mfano wake katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla hivyo tumeridhika na kazi waliyofanya Taec katika zoezi la uwekaji vifaa ambavyo sisi tumevitoa "

  Naye Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo, Profesa Lazaro Busagala alisema serikali imetoa Sh, bilioni 2.3 kwaajili ya ujenzi wa maabara ya kisasa ya Tume ya Nguvu za Atomiki (TAEC) kwa lengo la kuhakikisha maabara hiyo inatoa huduma bora za kisasa za masuala ya mionzi kwa nchi za Afrika. 

  Aidha alishukuru Umoja wa Ulaya kwa kutoa vifaa vyenye thamani ya Sh, bilioni 11.5 vilkvyofungwa kwenye maabara za Tume hiyo ambavyo vimetolewa na Umoja wa Ulaya (EU).Alisema serikali kwa awamu ya kwanza imetoa Sh, bilioni 1 huku fedha nyingine Sh, bilioni 1.3 kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa maabara hiyo ya kisasa ambayo itaweza kutumiwa na watu mbalimbali nchini na nchi za Afrika 

  "Tunamshukuru Rais John Magufuli kwa kuwezesha maendeleo ya nchi yanasonga haswa katika kuhakikisha tume hii inapata maendeleo na kuchangia fedha katika mfuko huu serikali "Katika maabara hiyo kutakuwa na uhakiki wa vifaa vya kupimia mionzi, chumba cha mionzi mikali kwaajili ya kupikia vyuma kwa njia ya kupiga picha kwa kutumia mionzi pamoja na chumba cha kutumia mionzi kwaajili ya shughuli nyingine ambamo kitasimikwa kifaa cha kupima viasili vya mionzi vilivyopo mwilini mwa binadamu. 

  Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na Mashine ya kupima mionzi iliyoko ndani ya Mwili wa binadamu (whole body counter), mashine ya kuhakiki vifaa vya mionzi , Secondary standard dosimetry laboratory ( SSDL)

  Mashine ya kupima viasili vya mionzi kwenye mazingira , maji na hewa TXRF, mashine ya kupima mionzi kwenye vyakula aina ya Hyper pure Germanium detector. Sambamba na mashine ya kupima mionzi kwa wafanyakazi wanaofanya kazi kwenye mazingira ya vyanzo vya mionzi inayoitwa Harshaw 6600.

  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii, Mtwara

  WAZIRI wa Kilimo Japhet Hasunga, amesema serikali imeshaanza uhakiki wa wakulima wanaodai malipo ya korosho ambapo jumla ya vyama vya msingi 35 vimeshahakikiwa na malipo yameanza kufanyika.

  Hayo aliyasema jana mkoani Mtwara wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu opereshe korosho inayoendelea katika mikoa inayolima korosho kuhakikisha wakulima wote wanauza korosho zao kwa serikali kwa bei ya Sh. 3,300.

  "Tulitenga vyama 50 vya awamu ya kwanza na ndani ya siku mbili tumehakiki taarifa za wakulima kwenye vyama 35 kwa kuangalia majina yao, kiasi cha korosho walichoingiza kiasi cha fedha wanazotakiwa kulipwa na taarifa za akaunti zao na hivi ninavyoongea tayari wameanza kulipwa kuanzia sasa kupitia akaunti zao binafsi," alisema Hasunga.

  Alitaja halmashauri ambazo vyama vyao vimehakikiwa kuwa ni pamoja na Halmashauri ya Newala (5) Wilaya ya Newala (5) Wilaya ya Masasi (5) Nanyumbu (2) Lindi (5) Tunduru Ruvuma (5).Kuhusu malipo ya kitaasisi ikiwemo ushuru wa halmashauri alisema inaanda mwongozo wa kuangalia namna ya kuwalipa na kwamba malipo yatafanyika baada ya korosho kubanguliwa na kuuzwa.

  "Ili kulipa malipo ya makato yote lazima tujue tumeuza korosho kwa bei gani kisha kama ni asilimia zinakatwa kulinga na bei tuliyouzia," alisisitiza.Makato hayo ya kitaasisi huwa yanalipwa kwa Halmashauri ambayo huchukua asilimia tatu ya bei elekezi, wasafirishaji wa korosho, watunza maghala pamoja na vyama vikuu vya ushirika ambavyo hukata Sh. 53 katika kila kilo moja ya korosho kwaajili ya vifungashio.

  Hasunga yupo mikoa ya kusini tangu siku moja tu baada ya kuteuliwa kwenye nafasi hiyo ili kujionea zoezi la uingizaji korosho kwenye maghala na kuhakikisha kuwa hazitoki na kuuzwa baada ya serikali kuweka msimamo wa kununua korosho zote za wakulima nchini.

  Alisema kwasababu serikali ndiyo mnunuzi wa korosho hivyo inalazimika kulipa tozo ambazo walikuwa wanalipa wanunuzi wengine."Kwa agizo la Rais fedha zote zitapelekwa kwa wakulima bila makato yoyote kwasababu tunaangalia wakulkma kwanza na wengine watalipwa baadae" alisema.
  Waziri wa Kilimo , Japhet Hasunga akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu utaratibu wa kutoa Malipo ya korosho kuanzia leo Novemba 17 mwaka 2018 kama ilivyoagizwa na Rais Dr.John Pombe Magufuli.
  Baadhi ya Wanafunzi wakiwa wametoka kuokota korosho katika Mashamba ya shule kwa ajili ya kukusanya ziende kuuzwa kwenye Maghala.

  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii,Newala ,Mtwara.

  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Newala, Mussa Chimae amesema tangu kutangazwa kwa operesheni korosho ofisi yake kwa kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Newala wamezunguka  Wilaya nzima kutoa elimu kuhusu nini kifanyike kupitia agizo la Rais Magufuli kuwa Serikali itanunua Korosho yote nchini.

  Akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo ofisini kwake Wilayani Newala Chimae amesema kuwa  wamezunguka kwa wananchi kutoa elimu juu ya namna zoezi hilo litakavyoendesha ikiwa ni pamoja na kuwataka watendaji wa vijiji na kata kusimamia zoezi hilo kwa makini hili kusitokee malalamiko yoyote.
  "Sambamba na zoezi la uhakiki wa taarifa za wakulima pia tumetoa maagizo kwa watendaji wa mitaa na kata kusimamia zoezi la uingizaji wa korosho kwenye maghala na kuhakikisha kuwa hakuna korosho inayoingia kutoka nje ya mitaa au kata zao ili kudhibiti korosho za magendo zinazoingizwa kutoka nchi jirani," alisema Chimae.

  amesema kuwa Halmashauri ya Newala ni moja ya Halmashauri zinazopakana na nchi jirani ya Msumbiji ambapo kwa upande wa majirani zetu kwa sehemu nao wanalima zao la Korosho hivyo wamejipanga kwa kila namna kwa kushirikiana na Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) Kuwa hakuna korosho kutoka nchi jirani itakayopenya nchini kupitia milango ya Wilaya hiyo.

  amesema kuwa tayari askari wa JWTZ Wamejipanga katika Maghala na wameimarisha ulinzi kwa kukagua na kulinda korosho hili isije mtu akatokea akatia doa wilaya yake kwa kufanya vitu tofauti na maagizo ya Rais.

  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Newala, Mussa Chimae akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu  Mafanikio yaliyopatikana katika Wilaya hiyo kwa kipindi hiki cha Miaka Mitatu ya Serikali ya  awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli

  Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya Habari wakimsikiliza
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Newala, Mussa Chimae
  Jengo la Utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Newala linavyoonekana kwa nje


  0 0


  Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Mtwara

  Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ametaka watendaji wa Bodi ya Korosho na Waendesha maghala kusimamia kwa weledi ubora wa korosho ili fedha za serikali zinazotolewa kwa ajili ya kununua korosho za wakulima katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma zitumike ipasavyo.

  Waziri Hasunga ameyasema hayo tarehe 16 Novemba 2018 wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.

  Alisema kuwa baada ya wananchi katika maeneo mbalimbali kusikia kuwa serikali imeanza kuwalipa wakulima wa korosho yamejitokeza matukio ya kuwepo kwa korosho chafu zilizotunzwa kwenye maghala tangu msimu wa mwaka jana 2016/2017 zikiwa hazipo katika ubora unaotakiwa wa daraja la kwanza ilihali korosho za madaraja mengine hazijaanza kununuliwa.

  “Nadhani wanafanya hivi ili wafaidike na hela za serikali, jambo hili hatuwezi kukubaliana nalo kwani tayari tumeshakamata Tani 20 za korosho chafu kutoka kwenye ghala la Olam za Chama cha Ushirika cha Mnyawi Amcos kilichopo Nanyamba pamoja na Mbembaleo Amcos ambapo gunia tano za korosho chafu zimepatikana” Alisema

  Aidha, Mhe Hasunga alisema kuwa Kuna watu wameanza kuingiza korosho zao kutoka nchi jirani baada ya kusikia kuwa Tanzania inanunua korosho kwa bei nzuri huku akisisitiza kuwa watanzania wanapaswa kushirkiana na vyombo vya dola kutoa taarifa za wahalifu wanaoingiza korosho kinyume na sheria.

  Alisema, kuruhusu korosho za nje ya nchi zitaharibu soko ikiwa ni pamoja na kuhatarisha amani ya wananchi waliyonayo katika maeneo yote yanayolima korosho.“Tutailinda mipaka yetu na kuilinda korosho yetu ambayo tunayo” Alisisitiza Mhe Hasunga

  Kuhusu kuanza malipo kwa wakulima Mhe Hasunga alisema kuwa tayari vyama 35 vimekwisha hakikiwa na serikali imeanza kulipa fedha zinazostahili.Serikali imeshanunua Tani 738.7 huku wakulima wakinufaika na fedha zao ambapo taratibu zingine zinaendelea kwa ajili ya kuhakiki na kukamilisha malipo kwa wakati katika vyama vingine.

  “Vyama vilivyohakikiwa ni 35 lakini mpaka sasa kati ya hivyo vyama 6 vimeshaingiziwa fedha ambavyo ni Mtama Amsos, Kitomiki Amcos, Mnazimoja Amcos, Mtetesi Amcos, Chamana Amcos na Msafichema Amcos”

  Waziri Hasunga aliongeza kuwa mpaka kufikia jana jioni (Tarehe 16 Novemba 2018) tayari wanachama 2348 walikuwa wamelipwa kupitia njia ya benki huku akisisitiza kuwa serikali ilianza kwanza na mkulima ambapo hatua itakayofuata itakuwa ni kuwalipa wachuuzi sambamba na walinda ghala.Wakulima wanaendelea kulipwa fedha zao ambapo kilo moja ya koroshwa inanunuliwa kwa shilingi 3300 fedha ambayo inaenda moja kwa moja kwa mkulima bila kukatwa kiasi chochote cha fedha.
  Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb)

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameishukuru Serikali ya China kwa kuunga mkono jitihada za maendeleo zinazofanyika nchini hivi sasa chini ya uongozi wa Serikali ya awamu ya tano. 

  Ametoa shukrani hizo jana jioni (Ijumaa, Novemba 16, 2018) alipokutana na Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Watu wa China, Bw. Cai Dafeng ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma. “Tunaishukuru Serikali ya China kwa sababu tumepokea misaada na mikopo ya gharama nafuu na kuendeleza miradi mbalimbali kama vile mradi wa umeme wa Kinyerezi, awamu ya pili ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa Zanzibar,” alisema. 

  Alisema Serikali ya China imekuwa pia na mahusiano ya muda mrefu na Serikali ya Tanzania na hasa kwenye sekta ya afya ambapo kuna wanafunzi wengi wa Kitanzania ambao wako China wakisomea udaktari na masuala ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA). “Tuna mahusiano mazuri kwenye sekta ya afya na sasa hivi tuna madaktari 20 ambao wanasoma huko na wengine wanasomea masuala ya TEHAMA. Pia tuna mahusiano mazuri baina ya Bunge la Tanzania na China,” alisema. 

  Waziri alisema Tanzania imejipanga kuinua uchumi wake kupitia ujenzi wa viwanda na sekta nyingine kama utalii kutokana na vivutio vilivyopo nchini kama vile Mlima Kilimanjaro, mbuga za wanyama za Serengeti na visiwa vya Zanzibar. “Nimefurahi kusikia kuwa hivi karibuni tutapata idadi kubwa ya watalii kutoka China,” alisema. Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Watu wa China, Bw. Cai Dafeng alisema amefurahishwa na jinsi Serikali ya awamu ya tano inavyoendelea kubadili hali ya uchumi wa nchi na maisha ya Watanzania chini ya uongozi wa Dkt. John Pombe Magufuli. 

  Alisema China itaendelea kuiunga mkono Tanzania kwenye masuala ya kiuchumi na haiko tayari kuona ikiingiliwa masuala yake ya ndani na mataifa kutoka nje. Akizungumzia kuhusu masuala ya uwekezaji baina ya Tanzania na China, Bw. Cai alisema China itaendelea kuyahimiza makampuni ya nchi hiyo ili yawekeze zaidi nchini Tanzania kwenye maeneo mbalimbali kama vile ujenzi wa bandari ya Bagamoyo. “China inataraji kuongeza uwekezaji kwenye kilimo, nishati na miundombinu,” alisema. 

  Kuhusu elimu, Bw. Cai alisema Serikali ya nchi hiyo inaangalia uwezekano wa kuanzisha masomo ya lugha ya Kichina katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ili Watanzania wengi zaidi waweze kujifunza lugha hiyo. Kuhusu afya, alisema China itaendelea kutuma madaktari wake ili waje kutoa huduma kwa Watanzania na inatamani kuona mahusiano baina ya mtu mmoja mmoja kutoka nchi hizo mbili ikiendelea kukua.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Watu wa China Cai Dafeng, ofisini kwake Mlimwa jijini Dodoma Novemba 16, 2018. 
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akutana na Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Watu wa China Cai Dafeng, ofisini kwake Mlimwa jijini Dodoma Novemba 16, 2018. 
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mahagama, akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Watu wa China Cai Dafeng, ofisini kwa Waziri Mkuu Mlimwa jijini Dodoma Novemba 16, 2018. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

  0 0

  Meneja wa TCRA Kanda ya Kaskazini Fransis Msungu akiongea kwenye semina iliyowashirikisha watendaji wa kata na mitaa waalimu wakuu kutoka halmashauri za jiji na wilaya ya Arusha sanajri na wakuu wa vituo vya polisi wilayani hapa iliyofanyika kwenye hotel ya Golden Rose jijini hapa picha zote na mahmoud ahmad arusha.
  Muwasilishaji kutoka mamlaka ya mawasiliano nchini Tcra Janny Kaaya akitoa mada wakati wa semina ya watendaji wa kata na mitaa waalimu wakuu na wakuu wa vituo vya polisi walioshiriki semina hiyo kwenye hotel ya Golden Rose jijini hapa picha na mahamoud ahmad wa globu ya jamii arusha
  Katibu tawala wa wilaya ya Arusha mjini David Mwakiposa akifunga semina hiyo iliyowashirikisha Halmashauri za jiji la Arusha na wilaya ya Arusha iliyofanyika kwenye Hoteli ya Golden Rose jijini hapa picha na mahmoud ahmad wa globu ya jamii Arusha.

  ……………….

  Na Ahmed Mahmoud Arusha

  Mamlaka ya mawasiliano Tanzania(TCRA)imewataka wale wote wenye kuuza bidhaa za mawasiliano ikiwemo simu za mkononi,Radio na Runinga kuhakikisha wanajisajili kwao ili wananchi wapate huduma zilizo sahihi na kuondoa malalamiko kutopata huduma stahiki

  Akizungumza kwenye semina ya huduma za utangazaji kwa channeli zinazotazamwa bila malipo iliyowashirikisha watendaji wa mitaa,Kata, Wakuu wa vituo vya polisi,waalimu wakuu wa shule sanjari na watumisha wa idara za serikali wilayani hapa Meneja wa mamlaka hiyo Mhandisi Fransis Msungu amesema kuwa hapa Arusha mamlaka hiyo imebaini kuwa wafanyabiashara wengi wana leseni za biashara lakini za mamlaka hiyo wengi wao hawana.

  Amesema kuwa maswali mengi yalioelekezwa kwa mamlaka hiyo imeonyesha mafundi wa simu na maduka mengi hayana leseni za mamlaka hiyo hivyo kutoa wito kwao kuangalia na kujisajili haraka kwao ili kuweza kumlinda mlaji.

  “Nawasihi wote kuhakikisha wanajisajili haraka kwao ili kuwezakuondoa malalamiko yanayotolewa na walaji kwa mamlaka yetu utaona hapa Arusha kuna maduka 40 yenye leseni zetu mengi yaliopo bado hayajasajiliwa sanjari na mafundi wa simu”alitanabaisha Msungu.

  Kwa Upande wake Katibu Tawala wa wilaya ya Arusha David Mwakiposa amesema kuwa mbali na malalamiko mbali mbali yaliotolewa na washiriki wa mkutano huo suala zima ni mashirikiano kati ya Tcra na wadau mbalimbali na semina hiyo imefungua milango kwa wananchi kwani elimu itawafikia walengwa ambao ni wananchi.

  Amesema kuwa semina hiyo inatakiwa kuwa endelevu na watendaji wamejipanga kuhakikisha kuwafikishia wananchi kwenye maeneo yao na tutarajie kuondoa changamoto mbali mbali zinazo wakabili wananchi hususani ya wizi wa mtandao.

  “Natoa rai kwa TCRA kuhakikisha changamoto mbali mbali zinazoelekezwa kwao kuzitafutia ufumbuzi ili kuondoa kero na adha wanayokutana nayo wananchi katika maeneo mbali mbali hapa nchini tunashukuru sana sisi tumepata uelewa wa masuala haya ya channel zisizolipiwa na tunaahidi kutoa elimu kwa wananchi”alisema Mwakiposa

  Aidha Baadhi ya washiriki mbali mbali walioshiriki katika semina hiyo wamepata uelewa ila wakaitaka Tcra kuenda mbele zaidi katika suala zima la utoaji wa elimu kwa wananchi sanjari na kutatua changamoto mbali mbali wanazokutana nazo walaji wa mamalaka hiyo.

  0 0   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) selemani Jafo akiwa na viongozi wenzake wakishiriki na wananchi kushusha vifaa vya ujenzi kutoka katika meli kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali kisiwa cha Ukara.
  2
  .Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) selemani Jafo akitoa maagizo viongozi wa Mwanza.
  3
  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela akizungumza mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) selemani Jafo
  4
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) selemani Jafo akiwa na viongozi mbalimbali wakielekea kisiwa cha Ukara.
  ……………..


  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) selemani Jafo amekemea mila ya wafiwa kutakaswa kwa kufanya tendo la ndoa na mtu mwingine ili kuondoa mkosi kwenye kisiwa cha Ukara kwa kuwa wanaweza kupata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi(VVU) na ugonjwa wa Ini.

  Waziri Jafo amekemea tabia hiyo inayoendelea kisiwani humo kwasasa baada ya watu wengi kufiwa na wenza wao kutokana na ajali ya kivuko cha MV. Nyerere kilichozama miezi michache iliyopita na kupoteza watu wengi.

  Katika ziara yake maalum ya utekelezaji wa agizo la Rais Dk. John Magufuli la ujenzi wa majengo yenye hadhi ya hospitali katika eneo la Ukara, Waziri Jafo amesema zoezi hilo limeanza rasmi leo na kuagiza ujenzi huo ukamilike ndani ya miezi mitatu. Amesema amepata taarifa kwamba wafiwa wanafanya mapenzi na watu wengine ili watolewe mikosi kitendo ambacho ametahadharisha kwamba kinaweza kusababisha maafa makubwa kisiwani humo kutokana na watu wao kuambukizwa nagonjwa yakiwepo gonjwa la UKIMWI na Ugonjwa wa Ini yaani Hepatitis B.

  Jafo amewataka wale ambao bado hawajafanya kitendo hicho cha kutakaswa wasijaribu kabisa kwani kinaweza kusababisha maafa makubwa kisiwani humo.

  Naye, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela amemuhakikishia waziri Jafo kwamba watasimamia ipasavyo ujenzi huo na kukamilika ndani ya miezi mitatu ili adhima ya Rais Magufuli ya kuwasaidia wananchi wa Ukara katika sekta ya afya iweze kutimia.

  0 0


   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa Nachingwea wakati  alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Nachingwea kwa ziara ya kazi wilayani humo, Novemba 17, 2018.  Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Nachingwea, Rukia Muwango. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)  
  PMO_0104
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Nyamatula wilayani Nachingwea akiwa katika ziara ya kazi wilayani humo, Novemba 17, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua gwaride wakati wa sherehe za uzinduzi wa Jeshi USU la Wanyapori na Misitu iliyofanyika Fort Ikoma Serengeti mkoani Mara.
  4
  Jeshi USU la Wanyamapori na Misitu likipita kwa ukakamavu mbele ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) wakati wa sherehe za uzinduzi wa jeshi hilo zilizofanyika Fort Ikoma Serengeti mkoani Mara.
  5
  Jeshi  USU la Wanyamapori na Misitu likionyesha picha za Viongozi wakubwa wawili Mwalimu Julius K. Nyerere (kulia) kama ishara ya mpambanaji wa kusimamia rasilimali zetu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kama mtekelezaji katika kuhakikisha rasilimali zetu zinalindwa na kufaidisha Wananchi wa Tanzania  na picha za wanyama zinaashiria wanyama wakubwa watano ambao ndio kivutio zaidi duniani na wamekuwa kwenye hatari ya kutoweka wakati wa sherehe za uzinduzi wa jeshi hilo zilizofanyika Fort Ikoma Serengeti mkoani Mara.
  6
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi bendera Mkurugenzi Mkuu wa Hifahi za Taifa (TANAPA), Dkt. Allan Kijazi kama ishara ya uzinduzi na kuanza kufanya kazi rasmi kwa jeshi la USU leo wakati wa sherehe za uzinduzi wa Jeshi  USU la Wanyapori na Misitu iliyofanyika Fort Ikoma Serengeti mkoani Mara. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

  0 0

   Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete  akiwatunuku wahitimu wa shahada mbalimba mapema leo katika Mahafali ya 48 ya chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (UDSM)  leo Jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali katika Mahafali ya 48 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo .(Picha na Emmanuel Massaka MMG)
   
  Wahitimu wa Shahada mbalimbali wakifurahia mara baada ya kutunukiwa rasmi katika Mahafali ya 48 ya chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam.

older | 1 | .... | 1725 | 1726 | (Page 1727) | 1728 | 1729 | .... | 1898 | newer