Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

MAGAZETI YA LEO IJUMAA NOVEMBA 16,2018


MSHINDI WA GARI YA 'TBL KUMENOGA, TUKUTANE BAA' AKABIDHIWA GARI ALILOSHINDA

$
0
0
Meneja wa Udhamini na Mawasiliano ya Wateja wa TBL,David Tarimo (kulia) akimkabidhi ufunguo wa gari aina ya mshindi wa kwanza wa promosheni ya TBL Kumenoga Tukutane baa. Julitha Kilawe . Kushoto ni Meneja Matukio wa TBL, Angela Mritaba. Mshindi wa kwanza wa gari kupitia promosheni ya TBL Kumenoga Tukutane Baa Julitha Kilawe,(katikati) akionyesha ufunguo wa gari alilojishindia baada ya kukabidhiwa na Meneja wa Udhamini na Mawasiliano ya Wateja wa TBL,David Tarimo (kulia)mwingine pichani Kushoto ni Meneja Matukio wa TBL, Angela Mritaba.
Meneja wa Udhamini na Mawasiliano ya Wateja wa TBL, David Tarimo ( mwenye shati jeupe) akimfungulia gari na kumuelekeza jinsi linavyotumika Mshindi wa kwanza wa gari kupitia promosheni ya TBL Kumenoga Tukutane Baa Julitha Kilawe.

Na Mwandishi Wetu.
Mkazi wa jiji la Dar es Salaam na mfanyakazi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Julitha Kilawe, ambaye wiki iliyopita aliibuka mshindi wa gari mpya aina ya Renault KWID kupitia droo ya kwanza ya promosheni ya TBL Kumenoga, Tukutane Baa’ leo amekabidhiwa rasmi gari lake katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya TBL, Ilala jijini Dar es Salaam. Akiongea muda mfupi baada ya kukabidhiwa gari lake Julitha Kilawe, alisema “Ninayo furaha kubwa kwa kujishindia gari kupitia promosheni hii ya TBL Kumenoga tukutane baa, mpaka siamini macho yangu, naishukuru TBL kwa kuniwezesha kupata usafiri huu”. 

Kilawe alisema gari hilo atalitumia kwa usafiri wa kwenda kazini na shughuli nyinginezo za kifamilia na aliwataka wateja wa bia kuchangamkia promosheni hii kutoka TBL ambayo imelenga kuboresha maisha ya wateja wake. Akiongea wakati wa kumkabidhi zawadi hiyo, Meneja wa Udhamini na Mawasiliano ya wateja wa TBL, David Tarimo, kwa niaba ya kampuni ya TBL alimpongeza mshindi huyo na kutoa wito kwa wateja wote nchini kuendelea kuichangamkia promosheni hii ili kuweza kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo zawadi kubwa ya gari mpya aina ya Renault KWID.

 “Mshindi wetu wa kwanza kupitia promosheni hii ya TBL Kumenoga tukutane baa ameshapatikana na leo ndio amekabidhiwa rasmi gari lake. Natoa wito kwa wateja wetu popote walipo kuendelea kushiriki promosheni hii ya miezi mitatu bado kuna magari 2 kwa ajili yao na zawadi nyinginezo nyingi”, alisema Tarimo. Tarimo, aliongeza kuwa, promosheni hii inafanyika kwenye mabaa katika siku za mwisho wa juma yaani Ijumaa, Jumamosi na Jumapili kupitia bia za chapa za Safari Lager, Kilimanjaro Lager, Castle Lite na Balimi Extra Lager. Kwa upande wake, Meneja wa Ukuzaji wa Masoko wa TBL, Edith Bebwa, alisema promosheni inafanyika kwenye mabaa zaidi ya 5,000 nchini kote. “Wateja wetu wazidi kuitafuta bendera ya TBL Kumenoga, kwani ilipo bendera hii ndipo wateja na TBL wanapokutana katika promosheni.’ 

Alisema ili kuingia kwenye droo ya magari mapya ya ‘TBL Kumenoga, Tukutane Baa’ wateja watatakiwa kununua bia tatu kati ya Safari Lager, Kilimanjaro Lager, Castle Lite au Balimi Extra Lager kwenye promosheni ambapo watapatiwa kuponi yenye namba, kisha watatuma namba hiyo kwa meseji kwenda 15451, hii ni kwa wale wenye mitandao ya VODACOM, TIGO na AIRTEL. Kwa wateja wa mitandao mingine watatuma namba iliyo kwenye kuponi kupitia tovuti ya www.tblkumenoga.co.tz

JWTZ WAANZA UTEKELEZAJI WA AGIZO LA RAIS WILAYA YA NEWALA MKOANI MTWARA

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Newala, Mtwara

Mkuu wa Wilaya ya Newala Aziza Mangosongo leo amepokea ujumbe wa Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ )ambao umeanza kukagua Maghala yote ya kuhifazia korosho katika Wilaya hiyo kama ilivyoagizawa na Rais John Pombe Magufuli kufuatia Wafanyabiashara kutaka kuwalangua wakulima kwa kununua kwa bei isiyokuwa na Maslahi.

Ujumbe huo ambao ulipata nafasi ya kutembelea Maghala yote Makubwa ambayo yapo katika Wilaya yake hili waweze kuanza zoezi la kununua korosho kwa kuwalipa wananchi kupitia benki ya kilimo.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Newala mkoani Mtwara, Daniel Zenda amesema sababu kubwa ya kupungua kwa uzalishaji wa zao la korosho msimu huu ni kutokana na mvua iliyonyesha katikati ya msimu na kusababisha dawa ya Sulpher kushindwa kufanya kazi vizuri.

Akitoa muhtasari kwa vyombo vya habari jana mjini Newala juu ya shughuli zilizofanyika hadi sasa tangu serikali kutoa mwongozo wa ununuzi wa korosho, Zenda alisema propaganda zinaoenezwa kuwa upungufu wa uzalishaji umetokana na wakulima kutokupewa fedha za ushuru wa kusafirisha nje ( export levy) hazina ukweli wowote.

"Upungufu wa uzalishaji wa korosho haujasababishwa na kukosekana kwa fedha za export levy kama inavyoelezwa na baadhi ya wanasiasa badala yake mavuno yamepungua kwasababu mvua zilinyesha katikati ya msimu na kusababisha athari kwa dawa ya sulpher kushindwa kufanya kazi vizuri kwenye mazingira hayo," alisema Zenda.

Kwa mujibu wa Afisa masoko wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Tandaimba na Newala (TANECU), Juma Seleman, wanatarajia kupata tani 120,000 kwa msimu huu wa mwaka 2018/19 na kwamba zoezi la kukusanya kwenye maghala makuu kutoka vyama vya msingi linaendelea.

Alisema hadi sasa korosho iliyoingia kwenye maghala makuu ni tani 38,000 na bado zinaendelea kukusanywa kutoka vyama vya msingi na uvunaji unaendelea mashambani.Akizungumzia uamuzi wa serikali kununua korosho yote, Seleman alisema kama TANECU wanaunga mkono uamuzi wa serikali kupeleka fedha moja kwa mija kwa wakuoima bila kukatwa na kwamba wao wanaangalia kwanza maslahi ya wakulima hao kwani ndiyo kazi yao.

"Tayari utaratibu wa malipo umeshaanza kufanyika na pia utaratibu wa kuwatambua na kuwahakiki wakulima umeanza na tukimaliza haya tunaanza kuwalipa wakulima moja kwa moja kwenye akaunti zao," alisema Selema.

Alisema katika uhakiki wa wakulima wanashirikiana na vyama vya msingi vya ushirika wa wakulima ambapo taarifa zitapelekwa na kisha kila mkilima atakwenda kuhakiki kama taarifa zake ni sawa na baada ya hapo malipo yatafanyika.

Katika hatua nyingine Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) limeanza Operesheni Korosho kwa ukaguzi wa maghala na viwanda vya Korosho vilivyopo Newala likiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya hiyo, Aziza Mangosongo.Akizungumzia operesheni hiyo Zenda ambaye pia alikuwa kwenye msafara huo, alisema kikosi cha JWTZ kimetembelea maghala matatu na kiwanda kimoja kujionea shughuli zinazoendelea.

"Lengo kubwa la operesheni hii kwanza ni kuhakikisha korosho iliyopo kwenye maghala haitoki na hakuna korosho inayoingizwa kutoka nje ya nchi na kisha baadae wataanza kuzibeba na kuzipeleka kwenye kiwanda cha kubangua," alisema Zenda.Maghala yaliyotembelewa na timu hiyo ni pamoja na maghala mawili yanayomilikiwa na TANECU, ghala la Micronix System Limited lenye uwezo wa kuhifadhi tani 13,000 na ghala la Agrofocus ambayo yanamilikiwa na watu binafsi.

Aidha katika operesheni hiyo Zenda alisema DC Aziza kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi juzi Novemba 13 walifanikiwa kukamata zaidi ya tani tisa za shehena ya korosho iliyokuwa imeingizwa nchini kutokea Msumbiji.Alisema hali hiyo inatokana na uamuzi wa serikali kununua korosho kwa bei nzuri hivyo wafanyabiashara wasio na nia njema kutumia hiyk kama fursa ya kuingiza korosho za magendo kutafuta soko Tanzania.

"Mkuu wa Wilaya ya Newala na timu yake jana (juzi) walifanikiwa kukamata magunia 91 yenye uzito wa zaidi ya kilo 100 pamina na trekta moja lioilokuwa limebeba shehena hiyo na raia mmoja mtanzania ambaye ndiye mmiliki wa mzigo huo alikamatwa na yupo chini ya ulinzi," alisema.Alisema mara nyingi korosho huvushwa kwa mitumbi kutoka Msumbiji na kisha kupakiwa kwenye magari kuingia Tanzania kwa kuvuka mipaka isiyo rasmi.

Alisema waligundua mzigo huo iliingia kupitia mpaka wa Newala na Msimbiji na kisha kupelekwa kwenye Chama cha Msingi cha Masasi ambapo ulikuwa unapimwa ili uingie kwenye maghala yetu.

Katika hatua nyingine wakulima wilayani Newala wamempongeza Rais Dk. John Magufuli kwa uamuzi wake wa kutouza korosho kwa wafanyabiashara na badala yake serikali kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kununua kwa Sh. 3,300.

Masoud Mbelenje mkazi wa kijiji cha Moneka Kata ya Mtonya ambaye pia ni Diwani wa kata hiyo alisema wanafurahia uamuzi wa Rais Magufuli kwani amewaondolea tatizo la kila mara la kotokuwa na soko la uhakika licha ya kutumia gharama kubwa katika kilimo hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Newala AkiongozaUjumbe wa Kikosi cha Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Ambao wamefika Wilayani hapo kwa ajili ya kukagua Maghal ya Korosho hili waanze zoezi la ununuzi na kulipa fedha kwa wakulima kama ilivyoagizwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr . John Magufuli kuwa Korosho zote zitanunuliwa na jeshi .
Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakiwa ndani ya Ghala la Kiwanda cha Ubanguaji wa korosho Microfonix kilichopo Wilaya ya Newala Mkoani Mtwara
Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakiwa ndani ya Ghala la Agro focus kilichopo Wilaya ya Newala Mkoani Mtwara
Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakiwa ndani ya Kiwanda cha Ubanguaji wa korosho Microfonix kilichopo Wilaya ya Newala Mkoani Mtwara na kushuhudia zoezi la usafishaji wa korosho.

Wafanyakazi wa Kiwanda cha Ubanguaji wa Korosho cha Microfonix wakiendelea na kazi ya ubanguaji wa korosho na kusafisha katika Kiwanda hicho

MAWAZIRI WAKUTANA KUELEKEA UZINDUZI WA CHANELI YA RUNINGA YA UTALII

SERIKALI YAWAPANDISHA MADARAJA WATUMISHI WA UMMA 113,520 WALIOAJIRIWA TANGU MWAKA 2012

$
0
0
Serikali imewapandisha madaraja watumishi wa umma 113,520 walioajiriwa mwaka 2012 katika awamu tatu, ambapo ya kwanza walipandishwa vyeo Watumishi 28,049 waliokuwa wameidhinishiwa vyeo kabla ya zoezi la uhakiki wa watumishi hewa na uhakiki wa vyeti kuanzia mwezi Juni, 2016, awamu ya pili ilianza mwezi Novemba, 2017 na ilihusisha watumishi 59,967 ambao taarifa zao zilikuwa kwenye Mfumo Shirikishi wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS) kabla ya zuio na awamu ya tatu ilianza mwezi Aprili, 2018 na ilihusisha Watumishi 25,504 ambao barua zao zilikuwa hazijaingizwa kwenye Mfumo. 

Ufafanuzi huo, umetolewa Bungeni leo na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary M. Mwanjelwa (Mb) wakati akijibu swali la Mhe. Joram Hongoli (Mb) kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora lililohusu watumishi wa umma walioajiriwa 2012 kutopandishwa madaraja mpaka hivi sasa.

Dkt. Mwanjelwa amesema, watumishi walioajiriwa Mwaka 2012 walistahili kupandishwa madaraja kuanzia mwaka 2016/2017 kipindi ambacho Serikali ilikuwa ikifanya zoezi la uhakiki wa watumishi hewa na uhakiki wa vyeti, hivyo mara baada ya kukamilika kwa zoezi hilo Serikali ilianza kuwapandisha watumishi hao kwa awamu hizo tatu kwa kuzingatia vigezo stahiki na kuongeza kuwa watumishi wengine ambao wamekidhi vigezo wataendelea kukasimiwa katika bajeti ya mishahara ili waweze kupandishwa vyeo katika mwaka huu wa fedha 2018/2019. 

Aidha, Dkt. Mwanjelwa ameainisha kuwa, watumishi 31,188 walioajiriwa na TAMISEMI mwaka 2012, kati ya hao watumishi 15,320 wamepandishwa vyeo na kubadilishiwa mishahara, na watumishi 3,349 waajiri wao wamewapandisha vyeo lakini majina yao yapo UTUMISHI kwa ajili ya kupitia taarifa zao kabla ya kuwabadilishia mishahara na watumishi 1,064 waliopandishwa vyeo wamebainika kuwa na hoja mbalimbali ambazo waajiri wanapaswa kuzikamilisha na kurejesha majina yao UTUMISHI kwa ajili ya kuwaidhinishia mishahara, watumishi 4,552 hawapo tena katika Utumishi wa Umma na watumishi 6,903 bado hawajapandishwa vyeo ambapo Serikali inatarajia kuwapandishwa vyeo wakati wowote katika mwaka huu wa fedha 2018/19.

Suala la upandishwaji vyeo kwa Watumishi wa Umma linazingatia vigezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na utendaji kazi mzuri, kukidhi sifa zilizoainishwa katika Miundo ya Maendeleo ya Utumishi, uwepo wa nafasi wazi na bajeti iliyotegwa. Kwa mujibu wa Miundo ya Maendeleo ya Utumishi, mtumishi anapaswa kutumikia cheo kimoja si chini ya miaka mitatu kabla hajafikiriwa kupandishwa cheo. Aidha, iwapo mtumishi ameajiriwa kwa mara ya kwanza atapaswa kumaliza mwaka mmoja wa kuthibitishwa kazini kisha ndipo atumikie cheo hicho si chini ya miaka mitatu, hivyo kwa kuzingatia sifa mtumishi anaweza kupandishwa cheo baada ya miaka 3, 4, 5 au hata saba kutegemea na kukidhi vigezo stahiki.

IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
OFISI YA RAIS (UTUMISHI)
TAREHE 15 NOVEMBA, 2018.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary M. Mwanjelwa (Mb) akijibu swali la Mhe. Joram Hongoli (Mb) Bungeni leo, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora lililohusu upandishwaji wa madaraja kwa watumishi wa umma walioajiriwa mwaka 2012.

NHC YAWATAKA WALIOPEWA HATI KWENYE MRADI WA SAFARI CITY KUANZA UJENZI ILI HUDUMA ZIWAFIKIE

$
0
0
Mkurugenzi wa shirika la nyumba la taifa Dkt.Maulidi Banyani akiwa na Kaimu mkurugenzi wa Auwsa Mhandisi Humphrey Mwiyombela wakikabidhiana hati ya kiwanja na kibali cha ujenzi wa ofisi za AUWSA kwenye eneo la Safari City nje Kidogo ya jiji la Arusha Picha na mahmoud ahmad wa globu ya jamii Arusha.



Na Ahmed Mahmoud Arusha

Shirika la taifa la Tafa (NHC)Limewataka wale wote walikabidhiwa hati za viwanja walivyopewa katika la eneo la Safari City lililopo kata ya Mateves nje kidogo ya jiji la Arusha kuhakikisha wanaendeleza maeneo yao ili kuhakikisha huduma muhimu za umeme na maji zinasogezwa katika mji huo mpya.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya Hati ya umiliki wa eneo na kibali cha ujenzi kwa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira(AUWSA) iliyofanyika katika kata ya matever jijini hapa Mkurugenzi wa shirika la nyumba la taifa(NHC)Dkt.Maulidi Banyani amesema kuwa shirika hilo katika kuhakikisha linafikia malengo ya kusogeza huduma zake kwa jamii ya watanzania wa vipato vyote na kupunguza gharama za ujenzi kuendana na mazingira.

Ameeleza kuwa limeingia makubaliano na AUWSA na kuwapatia eneo lenye ukubwa wa squaremita elfu 13 kwa ;lengo la ujenzi wa ofisi kuu ya kanda,Karakana,Bohari na Kituo cha Taarifa za mita hatua hiyo itasaidia kupunguza tatizo la maji katika eneo hilo baada ya mamlaka hiyo kuonyesha nia ya kusogeza huduma hiyo kupitia mradi huo.

Kwa upande wake Kaimu mkurugenzi wa AUWSA Mhandisi Humphrey Mwiyombela amelishukuru shirika la nyumba kwa kuwapatia eneo hilo nakuhaidi kujenga jengo lenye ukubwa wa ghorofa sita litakalotumika kama ofisi kuu ya kanda ambalo litafungwa mitambo maalumu ya kupokea taarifa za mbali mbali katika mtandao wao wa huduma za maji.

Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Auwsa Dkt Richard Masika amesema kuwa ujio wa mamlaka ya maji katika eneo hilo la safari City litakuwa ni mkombozi kwa jamii inayozunguka katika eneo hilo na maeneo ya jirani kwa kuwa kutakuwa na mtandao mabomba ya maji wawenye teknolojia mpya na hivyo kuondoa tatizo la maji katika eneo hilo na kuwa kituvu cha mradi huo wa billion 520 kwa kuboresha mawasiliano.

“sio tu kwamba tunaboresha mji wa Arusha bali tunapunguza changamoto ya msongamano na kila mwananchi anayo fursa ya kukimbilia kwenye eneo hilo kwa lengo la kupata huduma muhimu za maji sanjari na kuwa kwenye makazi bora nampongeza sana mwenyekiti wa bodi na mkurugenzi wa Shirika la nyumba kwa kuteuliwa kwao na kuwataka ushirikiano wao uendelee”alisema

Aidha katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega ambaye pia ni mjumbe wa Bodi ya Auwsa amesema kuwa ujio wa mradi huo ni faraja kwa mkoa huo na kuendelea kupanuka na kuondoa msongamano katika jiji la Arusha

Amezitaka taasisi zingine zikiwemo za serikali kama Polisi,Tarura Tanesco na idara ya Zimamoto kuiga mfano wa AUWSA kuja kuchukuwa maeneo kwa ajili ya ofisi na hivyo kuboresha makazi ya jiji la Arusha na kusogeza huduma kwa wananchi sanjari ambao wamekuwa na changamoto ya kutafuta huduma hiyo katikati ya jiji pekee hali inayowawiya vigumu pindi kunapotokea mahitaji ya huduma zao.

VODACOM TANZANIA FOUNDATION YAKABIDHI VIFAA VYA KULINDA MAISHA YA WATOTO NJITI HOSPITALI YA RUFAA DODOMA

$
0
0

Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (kulia) akizungumza wakati makabidhiano ya mashine ya kusaidia kupumua kwa Watoto njiti ilivyotolewa na taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation kwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma ili kusaidia kupunguza vifo vya Watoto Njiti. Kushoto ni Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation Rosalynn Mworia, Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel, Doris Mollel (kati).

Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation Rosalynn Mworia, akikabidhi mashine ya kusaidia kupumua kwa Watoto njiti kwa Waziri wa Madini Angellah Kairuki (wa pili kulia) na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayesimamia Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na walemavu Anthony Mavunde (kulia) katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma ili kusaidia kupunguza vifo vya Watoto Njiti. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel, Bi Doris Mollel.
Afisa Muuguzi Msaidizi kutoka Kitengo cha kuhudumia Watoto Njiti Constancia Mankupe akielezea kwa vitendo namna mashine ya kusaidia kupumua kwa Watoto njiti inavyofanya kazi, mashine hii ni mojawapo kati ya vifaa tiba vyenye thamani Sh 25 m vilivyotolewa na taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation vilivyokabidhiwa kwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma ili kusaidia kupunguza vifo vya Watoto Njiti. Kulia kwake ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayesimamia Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na walemavu Anthony Mavunde na Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel, Doris Mollel.

MKIWAENDEKEZA WATOTO MTATENGENEZA “BOMU”- POLISI

$
0
0
Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha

Imeelezwa kwamba tabia ya wazazi kutoa ahadi ya zawadi kwa kila wanachofanya watoto wao ni kibaya na kinawajengea mazingira magumu watoto hao baadae hasa pindi hali ya uchumi inapobadilika.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto mkoa wa Arusha Inspekta Happyness Temu wakati alipokuwa anafafanua aina za malezi katika kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa hewani kila siku Asubuhi katika kituo cha Redio cha Triple “A” kilichopo jijini hapa.

Inspekta Happyness alisema kwamba, baadhi ya wazazi wamekuwa na tabia ya kutoa ahadi ya fedha au vitu kwa watoto wao kwa nia ya kutoa hamasa ili wafanye vizuri aidha katika masomo au shughuli zozote hali ambayo kimalezi si sahihi kwani inaweza kusababisha mtu kuwa tabia tofauti pindi atakapokuwa mkubwa.

“Tabia hii inawafanya watoto wanapokuwa kwenye malezi wawe na matumaini kwamba kila kizuri wanachofanya lazima mwishoni kiendana na zawadi na hivyo mtoto anasababishiwa tamaa, mfano ukimaliza ugali wote nakununulia keki”. Alisema Inspekta Happyness.

Alisema pindi anapokuwa mtu mzima hali hiyo itamuathiri kwa kuwa atakuwa anataka kupewa asante ya kitu au fedha kutoka kwa kila atayemhudumia mara baada ya kumaliza kazi kitu ambacho si sahihi.

Alisema pongezi kwa mtoto sio lazima iendane na kuahidiwa na kupewa kitu au fedha bali inaweza kufanyika kwa njia ya maneno tu na ikamridhisha kwani si kila wakati mzazi unaweza ukawa na uwezo ule ule kiuchumi kuna wakati unashuka au mtoto anakuwa mikononi mwa walezi wengine ambao uwezo wao ni mdogo.

Akifafanua juu ya aina ya malezi alisema kwamba yapo ya aina tatu ambayo ni malezi ya kimabavu; ambapo mzazi au mlezi anaweka sheria ambazo atataka zifuatwe bila kutoa nafasi ya kumsikiliza mtoto.“Hali hii inasababisha mtoto asiweze kuwa na mazingira huru ya kujifunza kitu chochote kipya zaidi ya kile atakachoelekezwa katika mazingira ya ndani kwa kuwa atakuwa anaogopa kugusa hata Redio au TV, lakini pia anakosa kujiamini na wakati mwingine analazimika kuwa muongo pindi anapokwenda kinyume kwa kuogopa kupata kipigo”. Alifafanua Inspekta Happyness.

Alisema aina ya pili ni malezi ya Kidemokrasia ambapo wazazi hutumia muda mwingi kujenga mahusiano kwa watoto wao lakini pia wanaweka sheria na kuwaambia faida zake kama zitafuatwa na hasara zake kama zitavunjwa.“Watoto wanaolelewa katika hatua hii wanakuwa na uthubutu wa kufanya jambo jema lakini pia huwa wanakuwa na uwezo wa kutathmini zuri na baya na kisha kufanya maamuzi sahihi”. Alisema Inspekta Happyness.

Aidha alisema kwamba aina ya tatu ni malezi huru ambapo wazazi wanaweka sheria kwa watoto wao lakini hawazifuatilii hivyo wanatoa mwanya mkubwa kwa watoto kuwa huru zaidi.Katika hatua hii watoto wanaweza kujiingiza katika makundi mabaya bila hata mzazi kujua kwa kuwa anakuwa mbali nao na ni rahisi kumtetea mtoto wake kwa lolote baya kwa kuwa hajawahi kumshuhudia au kusikia.

Jeshi la Polisi mkoani hapa kupitia Dawati la Jinsia na Watoto limekuwa likitoa elimu juu ya vitendo vya unyanyasaji na ukatili kupitia mikutano ya hadhara, nyumba za Ibada na Redio mbalimbali kwa lengo la kuwaelimisha wananchi ili washiriki moja kwa moja kutoa taarifa na kusaidia kutokomeza vitendo hivyo.
Pichani ni Mkuu wa Kitengo cha dawati la Jinsia na Watoto mkoa wa Arusha,Inspekta Happyness Temu.

Article 0

$
0
0
NA YEREMIAS NGERANGERA,NAMTUMBO

Athmani Amani mkazi wa kijiji cha Naikesi kata ya kitanda wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma anawaomba watanzania kumsaidia fedha za kugharimia matibabu ya mtoto wake Shaziri Athmani (12) anayesumbuliwa na tatizo la moyo kuwa mkubwa.

Mtoto Shaziri Athamani ni mwanafunzi wa darasa la nne shule ya msingi Naikesi iliyopo kata ya Kitanda wilayani Namtumbo awali alikuwa anasumbuliwa na kuvimba miguu hali iliyokuwa inamkosesha masomo yake darasani mara kwa mara kuanzia mwaka 2016.

Mwaka huo huo mwezi septemba baba yake alilazimika kumpeleka Hospitali ya Mkoa Songea kuangalia tatizo la kuvimba kwa miguu ya mtoto huyo na baada ya kupata vipimo wakashauriwa kuenda Hospitali ya Peramiho .

Bwana Athamani alidai kuwa hakuwa na fedha za kumpeleka mtoto peramiho kwa kipindi hicho na badala yake alirudi naye nyumbani Naikesi kwenda kuuza mifugo lakini fedha hizo hazikumwezesha kukidhi mahitaji ya kumtibu mwanae katika Hospitali ya Peramiho baada ya kufika katika Hospitali hiyo na kumaliza fedha yake yote aliyokuwa nayo katika vipimo pekee .

Baada ya kupatiwa vipimo na kubaini Tatizo la mwanae alirudi na mwanae mpaka kijijini kwake kujipanga upya kwa ajili ya matibabu ya mwanae na kujitahidi kwa kile anachokipata anunue dawa kwa ajili ya mwanae huyo.

Pamoja na jitihada hizo hali ikaendelea kuwa sio nzuri na ndipo alipolazimika kufanya kazi za kulima mashamba ya watu ili apate fedha za kumtibu kijana wake na mwaka huu mwezi oktoba alimpeleka kijana wake huyo peramiho na baada ya kufika peramiho na kupatiwa vipimo alishauriwa na madaktari kumpeleka mtoto huyo Hospitali ya Muhimbili Dar es salaam.

Hata hivyo mzazi huyo aliomba msaada vyombo vya habari kumsaidia tatizo lake ili aweze kuchangiwa na wasamaria wema ampeleke mtoto wake muhimbili ambapo vyombo vya habari vilimsaidia na aliweza kusaidiwa michango iliyomwezesha kumfikisha kijana wake muhimbili na kupatiwa matibabu ya awali.

Anawashukuru Watanzania wote waliomchangia kijana wake na kuweza kupata matibabu ya awali lakini anawaomba waendelee kumchangia kwani kila baada ya miezi mitatu anatakiwa kumpeleka kijana wake huyo hospitalini hapo na yeye hana uwezo wa wa fedha za kumpeleka hospitali kijana wake huyo mara kwa mara muhimbili zaidi ya kuwategemea wasamaria wema .

Kijana huyo baada ya kupata matibabu ya awali ameanza kuonesha hali ya matumaini tofauti na ilivyoawali kabla ya kumpeleka Muhimbili kwa matibabu ya awali alisema mzazi huyo.
Athmani Amani mkazi wa kijiji cha Naikesi kata ya kitanda wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma anawaomba watanzania kumsaidia fedha za kugharimia matibabu ya mtoto wake Shaziri Athmani (12) anayesumbuliwa na tatizo la moyo kuwa mkubwa.

ZANZIBAR KUADHIMISHA SIKU YA TAKWIMU AFRIKA.

$
0
0
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar 16.11.2018

Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeandaa Mdahalo mkubwa utakaofayika Novemba 19, kwa lengo la kuongeza uelewa wa Wananchi juu ya umuhimu wa Takwimu katika maendeleo ya Taifa.

Mtakwimu Mkuu wa Serikali Mayasa Mahfudh Mwinyi aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake Mazizini kuhusu shamrasharma za maadhimisho ya siku ya Takwimu Afrika.

Amesema Takwimu zina umuhimu mkubwa katika kupanga maendeleo ya Taifa hivyo wananchi wanapaswa kujua kwa undani wake ili kutoa mashirikiano kwa ofisi hiyo.Amesema Ofisi ya Takwimu itaendelea na jukumu lake la kufanya Tafiti katika nyanya mbalimbali ikiwemo za kiuchumi, kimaendeleo na kijamii na kuishauri Serikali na Taasisi binafsi kuhusu mwelekeo wa kiuchumi.

Aidha amezishauri Taasisi za Serikali na binafsi kuzitumia Takwimu zinazotolewa na ofisi hiyo ili zipige hatua mbele kimaendeleo na kukabiliana na changamoto zao.Alisisitiza wadau wote wanaotaka kufanya tafiti rasmi kwenda katika Ofisi yao kuomba ushauri wa kitaalamu ili Takwimu watakazozipata katika tafiti zao ziwiane na Takwimu ya Ofisi yake.

“Ili kuepuka mgongano wa Kitakwimu nawaomba Wadau wote wanaofanya Tafiti basi waje ofisini tuwasiliane kuboresha Takwimu badala ya takwimu hizo kugongana” alisisitiza Mtakwimu Mkuu.Mbali na kilele Mtakwimu Mayasa alielezea mambo watakayoyafanya ikiwa ni pamoja na kutoa msaada katika nyumba za kulelea watoto Mazizini ambapo Jumapili kutakuwa na Mchezo wa Mpira wa Miguu kati ya Ofisi ya Mtakwimu na Ofisi ya Mdhibiti Mkuu wa Serikali.

Awali Mtakwimu Mwandamizi kutoka Ofisi ya Mtakwimu Abdulmajid Jecha alisema kulingana na Takwimu za uwezekano wa umri wa kuishi kwa Mzanzibari ni miaka 67.Alisema miaka hiyo imeongezeka kutokana na uimarishwaji wa huduma za Afya Zanzibar na matumizi madogo ya ulevi ikiwemo Pombe kwa Wanzanzibari.

Hali hiyo ni tafauti kidogo kwa Tanzania Bara ambapo Makadirio ya kuishi ni miaka 66.“Sababu zinazofanya Makadirio ya kuishi kwa Wazanzibari kuwa juu ukilinganisha na Bara ni uimarishwaji wa huduma za Afya kwa mfano kupungua kwa Malaria ikilinganishwa na Bara lakini hata Ulevi ambao ni chanzo cha magonjwa Zanzibar ni kidogo ukilinganisha na Bara ” alibainisha Abdulmajid Jecha

Hivyo Jecha alishauri watu wazidi kuzitumia Takwimu sahihi zinazotolewa na Ofisi hiyo ili kujipangia mipangilio yao ya maendeleo.Kila ifikapo November 18 ni siku ya Takwimu Afrika ambapo kwa Zanzibar itaadhimishwa November 19 katika viunga vya Ofisi hiyo Mazizini, ili kufikisha ujumbe kwa wananchi wengi.
Mtakwimu Mkuu wa Serikali Mayasa Mahfudh Mwinyi akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake Mazizini kuhusu shamrashamra za maadhimisho ya siku ya Takwimu Afrika.

KONGAMANO LA WAHITIMU WA CHUO KIKUU MZUMBE LAFANA

$
0
0
 Rais wa Baraza la Wahitimu Chuo Kikuu Mzumbe, Ludovick Utoh, akizungumza katika mkutano uliowakutanisha wahitimu wa waliosoma chuoni hapo. Picha zote Kajunason/MMG - Morogoro.  Spika wa Bunge mstaafu, Anne Makinda, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano uliowakutanisha wahitimu wa waliowahi kusoma Chuo Kikuu Mzumbe.  Makamu Mkuu Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka, akizungumza katika mkutano uliowakutanisha wanafunzi waliowahi kusoma na kuhitimu katika chuo hicho. Makamu Mkuu wa Chuo Taalum, Prof. Ganka Nyamsogoro, akizungumza katika mkutano huo.   Baadhi ya washiriki wa mkutano huo.  Baadhi ya washiriki wa mkutano huo.  Mwenyekiti wa Baraza Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Mathew Luhanga, akimkabidhi cheti cha shukrani Spika wa Bunge mstaafu, Anne Makinda, wakati wa mkutano uliowakutanisha wahitimu waliowahi kusoma chuoni hapo. Kulia ni Makamu Mkuu wa chuo hicho, Prof. Lughano Kusiluka.  Rais wa Baraza la Wahitimu Chuo Kikuu Mzumbe, Ludovick Utoh, akipokea cheti cha shukrani kutoka kwa Mwenyekiti wa Baraza chuo hicho, Prof. Mathew Luhanga.        Wahitimu wa mwaka 2018 wakipokea vyeti vyao vya ubora kutoka Mwenyekiti wa Baraza Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Mathew Luhanga.  Mwenyekiti Baraza Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Mathew Luhanga, akimkabidhi cheti cha shukrani Meneja Mawasiliano Chuo Kikuu Mzumbe, Sylvia Lupembe, wakati wa kusanyiko la wahitimu waliohitimu chuoni hapo.  Makamu Mkuu Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Lghano Kusikula, akimpongeza Meneja Mawasiliano Chuo Kikuu Mzumbe, Sylvia Lupembe, wakati wa mkutano uliowakutanisha wanafunzi waliohitimu miaka ya nyuma chuoni hapo pamoja na wahitimu wa mwaka 2018.

WANACHAMA WA BARAZA LA KILIMO TANZANIA WATAKIWA KUZINGATIA WELEDI KATIKA UTENDAJI.

$
0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la kilimo Tanzania Bi Janeth Bitegeko akifunga semina ya siku mbili iliyoandaliwa na Baraza la Kilimo kwa ajili ya kuwajengea uwezo wanachama wa Baraza la Kilimo, ambapo miongoni mwa taasisi zilizoshiriki semina hiyo ambayo ni wanachama wa Baraza la Kilimo ni pamoja na TAMPRODA, SECO, SUWA Farmers Association, Agri link Tanzania na Morogoro Rural Agro Dealers Association, ambapo pamoja na masuala mengine amewataka wanachama hao kuhakikisha wanazingatia uongozi wa utawala bora pamoja na kuimarisha mawasiliano kiutendaji.mafunzo hayo ya siku mbili yamefanyika Dra es salaam.
Mkufunzi kutoka Baraza la Kilimo Tanzania Dkt Freddy Gamba akisisitiza kuhusu umuhimu wa watendaji kuzingatia mawasilaino sahihi, lakini kuzingatia uongozi wenye ueledi wakati wa kutekeleza majukumu yao, mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Baraza la Kilimo Tanzania yaliwahusisha wanachama wa Baraza la Kilimo yaliyokuwa yakilenga kuwafundisha uongozi na utawala bora.
Mwakilishi wa Taasisi ya Agri Link Tanzania ambayo pia ni mwanachama wa Baraza la Kilimo Tanzania Bw. Zephaniah Mugittu akiwaeleza wajumbe namna mafunzo hayo ya uongozi na utawala bora aliypoyapata yatakavyomsaidia kiutendaji, pamoja na masuala mengine ameushukuru uongozi wa Baraza la Kilimo kwa kuandaa mafunzo hayo kwa wanachama wake.
Afisa Uhamasishaji Maendeleo ya wanachama na Uhusiano Kimtandao kutoka Baraza la Kilimo Tanzania Bw Khalid Ngasa ( wa kwanza kulia )na washiriki wengine wa semina ya Uongozi na Utawala Bora, watendaji hao wameambiwa kuhakikisha wanazingatia mawasiliano sahihi katika ufanyaji kazi wao, bila kuathiri utendaji kazi wa taasisi.
Afisa Sera kutoka Baraza la Kilimo Tanzania Bi Neema Nyamubi ( kati kati ) na baadhi ya wanachama wa Baraza la Kilimo Tanzania wakifuatilia kwa makini mafunzo ya Uongozi na Utawala bora, Mkufunzi wa Semina hiyo amewataka wanachama hao kuhakikisha wanatambua umuhimu wa kuwa na wajumbe wa bodi wenye uelewa wa sekta husika wanayofanyia kazi, mafunzo hayo ya siku mbili yaliratibiwa na Baraza la Kilimo Tanzania.

MEYA MANISPAA YA IRINGA AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA KUOMBA NA KUPOKEA RUSHWA

$
0
0

Na Francis Godwin,Iringa

TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) imemfikisha mahakamani  Mstahiki Meya wa halmashauri ya manispaa ya Iringa Alex Kimbe kupitia chama cha demokrasia na maendeleo ( CHADEMA)  makosa mawili ya jinai kuomba na kupokea rushwa .

Kaimu kamanda wa takukuru mkoa wa Iringa Mweli Kilimali akizungumza leo na vyombo vya habari ofisibni kwake alisema kuwa meya huyo alipokea kiasi cha shilingi milioni 2 kutoka kwa mteja wao .

Alisema kuwa tukio la kukamatwa meya huyo lilitokea Novemba 15 mwaka huu majira ya saa 12 jioni katika Hotel ya Gentle Hills mjini Iringa .Kuwa meya huyo ambae ni diwani wa kata ya Isakalilo aliokea pesa hizo kinyume na kifungu cha 15 (1) (a) cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11/2007.

Alisema meya Kimbe alipokea fedha hizo za mtego wa rushwa akiwa kwenye gari yake aina ya nadia yenye rangi ya Marron ikiwa na namba za usajili T 456 CKD iliyokuwa imeegeshwa katika eneo la kuegesha magari kwenye hoteli hiyo .“ Maafisa wa takukuru waliweza kumfuatilia meya huyo kwa muda mrefu na hivyo kuweza kumkamata akiwa amekwisha pokea fedha hizo za mtego kutoka kwa mtoa taarifa wao “

Kilimali alisema kuwa awali walipokea taarifa ya kuwepo kwa ushawishi wa  kutoka kwa meya huyo kwenda kwa mmoja kati ya wakandarasi wanaoendesha tenda katika Manispaa ya Iringa ili muda ukiisha apate nafasi ya kupata tenda husika .Hivyo meya huyo alimuomba mtoa taarifa rushwa na shilingi milioni 10 na baada ya mtoa taarifa kujitetea hatokuwa na uwezo wa kutoa fedha hizo mtuhumiwa alikubali kupokea shilingi milioni 2.

Akiwa mahakamani Mwendesha mashtaka upande wa jamhuri Restuta Samson alisema hamakamani hapo jana kuwa Kimbe anashitakiwa makosa hayo mawili likiwemo la kuomba rushwa ya shilingi milioni 10 kutoka kwa Nance Nyalusi kama zawadi baada ya kupata zabuni ya kukusanya ushuru stendi kuu ya mabasi mjini Iringa .Kuwa mshitakiwa alifanya kosa hilo kinyume na sheria kwa meya kuomba zawadi hiyo kutoka kwa mzabuni huyo .

Wakati shitaka la pili ni mshitakiwa amefikishwa mahakamani hapo kwa kosa la kupokea rushwa kutoka kwa Nance Nyalusi .Hata hivyo mshitakiwa huyo aliweza kukana makosa yote yanayomkabili kuwa si ya kweli na kwa kuwa upande wa wakili wa jamhuri katika kesi hiyo uliieleza mahakama hiyo kuwa upelelezi bado haujakamilika na hauna pingamizi juu ya dhamana ya mshitakiwa .

Hakimu wa mahakama hiyo Liad Chamshana alisema hamaka yake inamtaka mshitakiwa kusaini dhamana ya maadishi ya shilingi milioni 10 pamoja na kuwa na wadhamini wawili mashariti ambayo yalitekelezwa na mshitakiwa kuachiwa kwa dhamana .

Akizungumza nje ya mahakama na waandishi wa habari wakili anayemtetea Kimbe Lutebuka Samson Antony alisema kuwa kosa la kwanza linalomkabili mtaja wake ni kudhaniwa kuomba rushwa huku kosa la pili ni la kudhaniwa kupokea rushwa kesi hiyo itatajwa tena Desemba 5 mwaka huu .
Kimbe akiwashukuru waliofika Mahakamani leo.
 Meya Alex Kimbe akifikishwa Mahakamani na Maofisa wa TAKUKURU leo
Meya Alex Kimbe akiwa Mahakamani leo

MAKAMU WA RAIS AFANYA ZIARA BABATI MJINI MKOANI MANYARA LEO

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameutaka Uongozi wa mkoa wa Manyara kutumia sheria za mazingira kulinda vyanzo vya maji. Makamu wa Rais ameyasema hayo leo mjini Babati akiwa kwenye ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo.

“Tumieni sheria ya mazingira inayotaka kuwe na mita 60, hii itasaidia kulinda na kutunza vyanzo vya maji, washirikisheni wataalam wa mazingira katika hili” alisema Makamu wa Rais. Leo katika ziara yake wilayani Babati, Makamu wa Rais ametembelea kiwanda cha mbolea Minjingu, amezindua jengo la Ofisi ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (BAWASA), kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara, kuweka jiwe la msingi wa ujenzi wa mtandao wa barabara Babati pamoja na kuhutubia wananchi wa Babati mjini katika uwanja mpira wa Kwaraa.

Katika hotuba yake kwa wakazi wa Babati mjini Makamu wa Rais amesema ziara yake ilianzia Mererani wilayani Simanjiro ambapo ameshuhudia ongezeko la ukusanyaji mapato pamoja na viwanda vya kuongeza thamani ya madini yetu. Pia amesisitiza kwa wananchi kufuata sheria na taratibu zilizowekwa kwani kufanya hivyo kutapunguza migogoro mingi haswa ya ardhi. Makamu wa Rais ameziomba taasisi za maji katika mji wa Babati kuangali mpya tozo wanazowatoza wananchi kwani ni kubwa.

Kwa upande mwingine Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISENI Selemani Jafo amesema Serikali inajenga hospitali mpya 67 ndani ya mwaka mmoja, vituo vya afya 350 ndani ya miezi 18, shule za sekondari 89 kongwe zinafanyiwa ukarabati, kwa upande wa miundo mbinu zaidi ya kilomita 6 kati ya 10 za mtandao wa barabara Babati mjini zimekamilika.

Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Manyara ndugu Alexander Mnyeti amesema wamekuwa wakijitahidi kutatua migogoro mbali mbali hatua kwa hatua na wameweza kusimamia miradi kwa ubora unaotakiwa “Pesa za miradi zinaenda sehemu husika na hii ndio imetupa sifa ya kuwa mkoa wa pili Kitaifa katika mbio za mwenge za mwaka huu”.

Nae Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini Mhe. Pauline Gekul pamoja na mambo mengine alikishukuru Chama cha Mapinduzi kwa kumpokea na kumpa nafasi ya kukitumikia chama hicho kama Mbunge.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wanachi waliojitokeza kwa wingi nje ya geti la kiwanda cha Mbolea Minjingu mkoani Manyara. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo la Ofisi ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (BAWASA), wengine pichani ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo, Mwenyekiti wa Bodi ya BAWASA  Dkt. Elibarick Olomi (kushoto) na Mkurugenzi wa BAWASA Mhandisi Idd Yazid Msuya, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Manyara Mzee Simon Lulu na Mkuu wa mkoa huo Mhe. Alexander Mnyeti (Kulia). 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la mtandao wa barabara za lami katika mji wa Babati, kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mganga Mfawidh wa Hospitali ya Mkoa wa Manyara Dkt. Catherine Magali pamoja na Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Damas Kayera wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa hospitali ya rufaa ya mkoa huo. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  akihutubia wananchi wa Babati Mjini kwenye uwanja wa mpira Kwaraa, Babati mkoani Manyara.
Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini Mhe. Pauline Gekul akihutubia wananchi wa jimbo lake kwa mara ya kwanza kwa tiketi ya CCM mbele ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye uwanja wa mpira Kwaraa, Babati mkoani Manyara. 

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MAKAMU WA RAIS WA BENKI YA DUNIA KWA UKANDA WA AFRIKA HAFEZ GHANEM IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Kanda ya Afrika Hafez Ghanem mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Bella Bird Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Kanda ya Afrika Hafez Ghanem kabla ya kuanza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Kanda ya Afrika Hafez Ghanem Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Kanda ya Afrika Hafez Ghanem Ikulu jijini Dar es Salaam aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mara baada ya mazungumzo yake na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Kanda ya Afrika Hafez Ghanem watatu kutoka kushoto Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Bella Bird wapili kutoka kushoto akifatiwa na Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako. Wengine katika picha ni Waziri wa Mambo ya Nje Balozi Dkt. Augustine Mahiga pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi.
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Kanda ya Afrika Hafez Ghanem akizungumza na wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Kanda ya Afrika Hafez Ghanem mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja  na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Kanda ya Afrika Hafez Ghanem mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Bella Bird wapili kutoka kushoto akifatiwa na Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako. Wengine katika picha ni Waziri wa Mambo ya Nje Balozi Dkt. Augustine Mahiga , Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi pamoja na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu. Mstari wa nyuma wakwaza kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, Katibu Mku Wizara ya Fedha Doto James, Balozi Zuhuru Bundala pamoja na wageni wengine. 

 PICHA NA IKULU

AZAM FC WAOMBA KURUDI TENA TAIFA, MECHI SIMBA NA YANGA

$
0
0
VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL)  klabu ya Azam FC, imehamishia rasmi Uwanja wa Taifa mechi zake za nyumbani itakazocheza na Simba na Yanga kwenye Ligi Kuu  msimu huu.

Katika barua iliyoandikwa jana kuelekea Bodi ya Ligi Tanzania Bara (TPLB) na nakala yake kutumwa kwenye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imeeleza kuwa sababu kubwa ya Azam FC kufikia uamuzi huo ni kuwapa nafasi mashabiki wengi kushuhudia mechi hizo kutokana na udogo wa Uwanja wa Azam Complex.

“Uongozi wa Azam Football Club unaomba ofisi yako tukufu kurejesha mechi zetu za Ligi Kuu za nyumbani zinazohusisha timu za Simba na Yanga zichezwe katika Uwanja wa Taifa msimu huu 2018/2019 badala ya kuchezwa Uwanja wa wetu wa Azam Complex,” ilieleza barua hiyo.

Ikieleza sababu za kufikia uamuzlidai kuwa; “Hii ni kutokana na uwezo mdogo wa uwanja wa Azam Complex kuingiza mashabiki na wi huo, barua hiyo iliyoandikwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amini ‘Popat’, iatazamaji.”

Aidha barua hiyo pia ilieleza changamoto walizopata kwenye mechi za kwanza zilizofanyika msimu uliopita ndani ya uwanja huo, wakidai kuwa idadi kubwa ya mashabiki walikosa fursa ya kutazama mechi hizo mbili dhidi ya Simba na Yanga jambo ambalo si zuri kwa maendeleo ya mpira wa miguu.

Azam FC ikiutumia kwa mara ya kwanza uwanja wake kwenye mechi hizo mbili, iliweza kutoka suluhu dhidi ya Simba kabla ya kupoteza kwa mabao 2-1 walipocheza na Yanga, bao la matajiri hao likifungwa na Shaaban Idd nay ale ya Yanga yakifungwa na mshambuliaji, Obrey Chirwa, aliyehamia Azam FC wiki iliyopita na beki wa zamani wa Azam FC, Gadiel Michael.

MAZOEZI YA PAMOJA MAJESHI YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI YAWAPA UTAYARI WA KUKABILIANA NA MAJANGA MBALIMBALI

$
0
0

WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt Hussein Mwinyi akizungumza wakati akifunga kufunga mazoezi ya ya mafunzo ya Ushirikiano Imara mwaka 2018 ya Kijeshi kwa vikosi vyanchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwenye eneo la Mlingano wilayani Muheza mkoani Tanga ambayo yalikuwa na malengo ya kukabiliana na vitendo vya kigaidi,uharamia,majanga na kujenga uchumi imara katika nchi
Waziri wa Ulinzi wa Kenya Balozi Raychelle Omamo akitoa salamu kwenye ufungaji huo wa mafunzo
Mkuu wa Majeshi nchini Jenerali Venance Mabeyo akizungumza katika halfa ya ufungaji wa Mafunzo hayo yaliyifanyika kwenye eneo la Mlingano wilayani Muheza Mkoani Tanga
WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt Hussein Mwinyi kushoto akiwa na Waziri wa Ulinzi wa Kenya Balozi Raychelle Omamo
Vikosi mbalimbali vikipita mbele ya mgeni rasmi leo

MAJESHI ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yapo imara kupambana na vitendo vya uvunjifu wa amani katika nchi wanachama baada ya kuhitimisha mazoezi ya pamoja yaliyozikutanisha nchi hizo mkoani Tanga .

Hayo yameelezwa na Waziri wa Ulinzi Dr Husein Mwinyi wakati wa kufunga mazoezi hayo ambayo yalikuwa na malengo ya kukabiliana na vitendo vya kigaidi,uharamia,majanga na kujenga uchumi imara katika nchi wanachama.

Aidha Dkt Mwinyi alisema kumekuwepo na ufanisi wa hali ya juu wa utayari wa kukabiliana na majanga kama hayo hivyo jukumu lipo kwa vikosi hivyo kujiamini na kutumia mbinu walizopata ili kuzisaidia nchi zao. “Tunaimani sasa baada ya mazoezi haya kwanza vikosi vyetu vitakuwa imara zaidi lakini ni wakati wa kuanza kupambana na matukio kama hayo si kwa nchi mojamoja bali kwa kushirikiana zaidi”Alisema Dr Mwinyi.

Mazoezi hayo yalizikutanisha nchi zote wanachama ikiwa pamoja na Tanzania ambae ni mwenyeji,Kenya,Uganda,Rwanda na Burundi huku Sudani kusini haikufika kutokana na sababu zilizo juu ya uwezo wao. Kwa upande wake Waziri wa Ulinzi toka Nchini Kenya Balozi Rachael Omamo alisema mbali ya kubadilishana uzoefu katika Nyanja ya kiusalama bali mazoezi hayo yanajenga mahusiano bora kwa Nchi zote wanachama.

Alisema Vikosi hivyo vinahitaji kujitathmini zaidi na kuitumia fursa hiyo kujiimarisha katika Nyanja zote ili kuweza kukabiliana na majanga yanayozikabili nchi hizo. “Majeshi yetu yanatakiwa yavute soksi ili kujiweka imara na mambo mbalimbali yanayozikabili nchi zetu lakini lazima tushirikiane kwa kila hali na kufanya hivi tunaweza kufanikiwa na kuwa sehemu salama”Alisema Balozi Omamo.

Naye kwa upande wake Mkuu wa Majeshi Nchini Jenerali Venance Mabeyo alisema mazoezi hayo yanajenga hasa kufahamiana katika vikosi hivyo na ndio msingi wa kufanikiwa katika mapambano dhidi ya majanga kwa nchi wanachama.

Alisema ni mazoezi yaliyoviongezea uwezo vikosi hivyo hasa na mapambano ya kigaidi,uharamia na majanga mbalimbali na hiyo ndio azma ya mazoezi hayo ambapo bado nchi za Afrika zinakabiliwa na changamoto ya mapambano hayo.

“Unajua lazima tujifunze mbinu za ugaidi na uharamia lakini lazima tufahamu watu wanaofanya matukio kama haya ni vikundi vidogovidogo ambavyo si rasihi kuvitambua na umoja wetu kupitia mazoezi haya lazima tutafanikiwa”Alisema Jeneral Mabeyo.

Jenerali Mabeyo mbali na hayo pia alizungumzia mwanajeshi wa Tanzania aliyeuwawa katika Nchi ya Demokrasia ya Congo akiwa katika majukumu ya kulinda amani alisema ni kweli na ni mapambano ya kawaida dhidi ya waasi hao.

Alisema ni ajali ya kawaida hasa kwa vikosi hivyo vinavyolinda amani katika nchi mbalimbali hapa Duniani na inaweza kutokea sa yoyote hivyo jukumu kubwa lililopo mbele ni kusahihisha makosa hayo.

“Ni tatizo na tunasahihisha lakini si jambo kubwa sana ni swala la kawaida katika maeneo ambayo wanajeshi wetu wapo kwa ajili ya kulinda amani katika nchi hiyo ya Congo”Alisema.

Alisema wanajeshi wa Tanzania wapo nchini humo kusaidia kupamba na waasi kwa ajili ya kurudisha amani ambayo inaonekana kuyumba na jambo hilo husababishwa na vikosi vya waasi ambao wanapamba na majeshi ya Serikali.

BODI YA WAKURUGENZI YA TANESCO YARIDHISHWA NA UBORA WA MITA ZINAZOZALISHWA NCHINI

$
0
0
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco) Alexander Kyaruzi kulia akiangalia mchakato wa utengenezaji wa mita katikati ni Meneja Mwandamizi wa Usambazaji na huduma kwa wateja wa shirika hilo Theodory Bayona  na kushoto ni Mkurugenzi wa Kiwanda cha cha Inhemeter
 Mkurugenzi wa Kiwanda cha cha Inhemeter kushoto akisisitiza jambo kwa  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco) Alexander Kyaruzi
Mkurugenzi wa Kiwanda cha cha Inhemeter kulia akimueleza jambo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco) Alexander Kyaruzi
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco) Dkt Alexander Kyaruzi  katika akiwa kwenye picha ya pamoja kulia kwake ni Mjumbe wa bodi ya Shirika hilo Balozi James Nzagi  na kushoto ni kwake ni Mjumbe wa Bodi hiyo Gilay Shamika

Bodi yaWakurugenziya TANESCO imesema inaridhishwa na Ubora wa mita zinazozalishwa hapa nchini kwani zinaviwango sawan amita zinazo zalishwa njeya nchi.

Hayo yalibainishwa leo wakati wa ziara iliyofanywa na Bodi yaWakurugenzi hiyo katika kiwanda cha Inhemeterna Baobab Energy System vilivyopo mjini Dar es salaam, Mwenyekiti wa Bodi yaWakurugenziya TANESCO Dkt. Alexander Kyaruzi amesema kuwa dhumuni kubwa la ziara hiyo ni kukagua na kujiridhisha na ubora wa mita na uwezo wa viwanda hivyo katika kukidhi mahitaji ya TANESCO na REA.

Alisema kwani kwasasa uhitaji wa Mita umekua mkubwa kutokana na uhitaji wa umeme kwa wananchi wa Vijijini na Mjini, pamoja na maboresho yanayofanywa na Shirika yakubadilisha mita za wateja wa zamani ambao walifungiwa mita miaka 10 iliyopita na sasa wanahitajika kuwekewa mita mpya.

Aidha aliongeza kwa kusema kuwa mahitaji ya Mita kwa TANESCO ni mita Laki tatu kwa mwaka, hivyo Bodi hiyo imeridhika kuona viwanda hivyo vina uwezo wakuzalisha mita laki 5 kwa kila kiwanda, kiwango ambacho kitakidhi mahitaji ya TANESCO na REA .

MHANDISI LUHEMEJA AZUNGUMZIA MAFANIKIO YA DAWASA KATIKA MIAKA MITATU YA DKT JOHN POMBE MAGUFULI

$
0
0
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya MajiSafi na MajiTaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumzia mafanikio ya miaka mitatu ya Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ikiwemo makusanyo ya maduhuli kwa mwaka 2014/15 yameongezeka kutoka wastani wa shilingi bilioni 2.9 na kufikia bilion 10.5 kwa mwezi kwa mwaka 2018 leo Jijini Dar es Salaam.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Katika mafanikio ya miaka mitatu ya Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli makusanyo ya maduhuli ya Mamlaka ya MajiSafi na MajiTaka Dar es Salaam (DAWASA) kwa mwaka 2014/15 yameongezeka kutoka wastani wa shilingi bilioni 2.9 na kufikia 10.5 kwa mwezi kwa mwaka 2018.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Habari maelezo leo Jijini Dar es Salaam, Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kuwa Kwa hivi sasa makusanyo yameongezeka hadi kufikia Shilingi bilioni 10.5 kwa mwezi kwa mwaka huu 2018 huku lengo letu na mikakati ni kufikia makusanyo ya Shilingi bilioni 12 kwa mwezi.

Mhandisi Luhemeja amesema, kwa upande wa ukusanyaji wa mapato haya yanatokana na mauzo ya huduma za maji na majitaka katika eneo la DAWASA, ambalo ni jiji la Dar es salaam na miji ya Kibaha na Bagamoyo

Ameeleza kuwa, mpaka sasa katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya awamu ya tano, miradi mikubwa iliyokamilika ni pamoja na upanuzi wa mtambo wa Ruvu juu, ujenzi wa tenki la Kibamba na ulazaji wa mabomba makuu ya kusafirisha maji.

Mhandisi Luhemeja amesema, kufuatia kukamilika kwa miradi mbalimbali , maji yanayozalishwa yameongezeka na kufikia lita milioni 502 kwa siku wakati mahitaji ya maji kwa siku ni lita milioni 554, na Serikali imejipanga kumaliza tatizo la Maji Dar es Salaam ifikapo mwaka 2020 kwa upatikanaji wa huduma za maji katika jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani kufikia asilimia 95 kwa maji safi na asilimia 30 kwa maji taka.

Amesema, Katika miaka hii mitatu ya Serikali ya awamu ya tano miradi mingine inayotekelezwa ni pamoja na ile ya kufikisha huduma katika maeneo ambayo hapo awali yalikuwa na changamoto ya upatikanaji wa maji kwa kutumia fedha za ndani.

Sehemu kubwa ya jiji inapata maji, ambayo hayakuwa na huduma sasa yamefikiwa kwa mfano maeneo ya Segerea, Kinyerezi, Kipawa, Ukonga, Changanyikeni, Goba, Mivumoni, Salasala, Madale kwa Msuguri, kwa Mbonde, Misugusugu, Kiwalani, Miti Mirefu na baadhi ya maeneo ya Kigamboni", amesema Mhandisi Luhemeja. 

Mhandisi Luhemeja amesema kuwa, mafanikio haya yanakuja baada ya ufanisi katika utekelezaji wa miradi mbalimbali iliyopelekea kuongezeka kwa maji yanayozalishwa pamoja na kuimarika kwa utendaji kazi kunakozingatia usimamizi mahiri wa utoaji huduma bora.

“Katika kuhakikisha kuwa maji yalioongezeka yanawafikia wananchi wengi zaidi hasa katika maeneo ambayo zamani hayakuwa na mtandao wa mabomba, miradi mbalimbali mikubwa na midogo imetekelezwa, miradi hiyo inahusisha ujenzi wa matenki ya maji matano yenye ujazo wa kati ya lita milioni 5.0 na 6.0 pamoja na ulazaji wa mtandao wa mabomba”, amesema.

Matenki hayo yamejengwa katika maeneo ya Changanyikeni, Salasala,Wazo, Mabwepande na Bagamoyo na katika maeneo yote ya miinuko ili kuwezesha maji kufika katika maeneo mengi Zaidi kwa msukumo mzuri na mradi huo umetekelezwa na serikali kupitia mkopo wa masharti nafuu kutoka benki ya Exim ya India na upo katika hatua za ukamilishwaji.

Mhandisi Luhemeja amesema kilometa 176 za mtandao chakavu wa maji zimebadilishwa na hivyo kuchangia kupungzua kiwango cha maji yanayopotea, kwa ujumla kiasi cha kilomita 500 za mabomba mapya zzimelazwa mitaani ili kuweza kugawa maji kwa uwiano mzuri zaidi na kufanya mamlaka kuwa na mtandao wa Kilomita 3,000 kutoka 2,500 zilozokuwepo 2015. 

Ili kuboresha huduma na kufikia lengo la kufikishia asilimiaa 95 ya wananchi ndani ya eneo la huduma ya DAWASA maji safi, bora na ya gharama nafuu kuna miradi imendelea kutekelezwa ambapo kuna mradi wa Chalinze III, Kibamba-Kisarawe , Chalinze Mboga, Mlandizi - Manelomango, Kilindoni- Mafia, Mkuranga na miradi mipya inayolenga kufikia watu wenye kipato waishio katika maeneo yasiyo na huduma ya maji.

Miradi mitatu mikubwa ya kisasa ya uchakataji majitaka inatarajiwa kujengwa hivi karibuni ikiwa ni sehemu ya kufikishwa asilimia 30 ya huduma ya majitaka. Pia miradi midogo ya uchakataji majitaka ipatao 50 itejengwa kuhakikisha kuwa wananchi wa ngazi zote wanafikiwa na huduma bora ya majitaka.
Mkurugenzi wa idara ya habari maelezo Tanzania Dr. Hassan Abbas akimkabidhi kitabu cha nchi yetu kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya MajiSafi na MajiTaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja leo Jijini Dar es Salaam.

Matukio Katika Picha Bungeni Leo

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango akihitimisha hoja baada ya Muswada wa Sheria ya Huduma za Fedha wa mwaka 2018 baada ya kupitishwa na Bunge leo jijini Dodoma. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akiwasilisha tamko kuhusu mashindano ya pili ya riadha ya wanawake nchini yatakoyofanyika Dar es Salaam kuanzia tarehe 24 na 25/11/2018 leo Bungeni jijini Dodoma Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiteta jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Huruma Mkuchika(kushoto) wakati wa kikao cha tisa Mkutano wa 13 wa Bunge leo jijini Dodoma. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Hanang’I, Mhe. Mary Nagu(kushoto) wakati wa kikao cha tisa Mkutano wa 13 wa Bunge leo jijini Dodoma Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza akiteta jambo na Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Dotto Biteko(kulia) wakati wa kikao cha tisa cha Mkutano wa 13 wa Bunge leo jijini Dodoma. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenyeulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akifuatilia hotuba ya hitimisho la hoja ya muswada wa sheria ya huduma za fedha ya mwaka 2018 wakati wa kikao cha tisa Mkutano wa 13 wa Bunge leo jijini Dodoma. Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano, January Makamba. Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo toka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Yusuf Singo (katikati) akibadilishana mawazo na Mbunge wa Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete (kulia) na Mbunge wa Same Magharibi, Mhe. Dkt. David Mathayo David. Baadhi ya wageni wa Mhe. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe wakitambulishwa Bungeni leo jijni Dodoma. Wageni hao ni wanafamilia ya Clouds Media ambao wapo jijini Dodoma kwa ajili ya Tamasha la Fiesta
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>