Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46205 articles
Browse latest View live

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI NOVEMBA 15,2018

0
0

















BARAZA LA MADIWANI JIJINI TANGA LAAMUA SEHEMU ITAKAPOJENGWA HOSPITALI YA WILAYA.

0
0
MSTAHIKI Meya wa Jiji la Tanga Alhaj Mustapha Selebosi akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani 
 MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akipitia taarifa kwenye kikao hicho
MKURUGENZI wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji akizungumza katika kikao hicho
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Tanga akisikiliza kwa umakmini hoja mbalimbali kwenye kikao hicho
NAIBU Meya wa Jiji la Tanga Mohamed Haniu akipitia kabrasha wakati wa kikao hicho kulia ni Mstahiki Meya wa Jiji hilo Alhaj Mustapa Selebosi
 Diwani wa Kata ya Mnyanjani (CUF) Thobias haule akiuliza swali kwenye kikao hicho
 Diwani wa Kata ya Kirare

Baadhi ya madiwani wakiwa kwenye kikao hicho
 Mganga Mkuu wa Jiji la Tanga (CMO) Dkt Jery Khanga akifuatilia hoja mbalimbali kwenye kikao hicho akiwa na wataalamu wengine wa Halmashauri hiyo

BAADA ya mjadala wa muda mrefu hatimaye Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Tanga limeamua rasmi eneo la Mwakidila lililopo Kata ya Tangasisi kuwa sehemu sahihi ya ujenzi wa Hospitali ya wilaya Tanga ambao utagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 1.5

Awali hospitali hiyo ilitarajiwa kujengwa katika kata ya Masiwani ambapo tayari jengo la utawala la ghorofa moja lilikwisha jengwa ambalo linadaiwa kugharamia kiasi cha shilingi Milioni 700.Mjadala uliibuka ndani ya kikao hicho cha baraza hilo ambapo madiwani walipingana eneo gani linaweza kuwa sahihi kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali hiyo ambayo mchakato wake unadaiwa kuanza tangu mwaka 2005.

Akizungumza Mwenyekiti wa baraza hilo Mstahiki Meya Mustafa Seleboss alisema kweli yapo maeneo matatu yaliyotengwa kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo ambayo kila eneo linachangamoto zake huku akibainisha umuhimu wa hospitali hiyo kujengwa katika eneo hilo la Mwakidila.Aidha alisema Halmashauri imekwisha pokea kiasi cha shilingi Milioni 500 kati bilini 1.5 toka Serikali kuu kwa awamu ya kwanza ya ujenzi wa hospitali hiyo ambayo itaondoa sitofahamu ya kutokuwepo kwa Hospitali hiyo ndani ya Wilaya.

Seleboss alisema hakuna haja ya kuendeleza malumbano juu ya wapi Hospitali hiyo itajengwa huku fedha hizo zikiwa zimetolewa na Serikali kwa mashari ya utekelezaji wa haraka wa ujenzi wa hospitali hiyo ambayo itapunguza msongamano katika Hospitali ya Rufaa ya Bombo.“labda niwaeleze ukweli ndugu zangu madiwani plani ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya eneo la masiwani lipo palepale ila kutokana na mgogoro uliopo wa ardhi tunalazimika fedha hizo kuanza kujenga Mwakidila badala ya masiwani”Alisema Seleboss.

Hata hivyo aliwanasihi madiwani na wananchi wa kata ya masiwani ambao walitarajia kupata hospitali hiyo ya Wilaya kuwa ndoto hiyo haijafutika na itajemgwa Hospitali nyingine kwa kupitia fedha toka vyanzo vya ndani vya Halmashauri.“Tulikuwa na maeneo matatu ya mwakidila,masiwani na kihongwe lakini kutokana na changamoto ya maeneo hayo mawili ya kihongwe na masiwani tumeona ni bora mradi huu tuuelekeze mwakidila eneo lililopo karibu na barabara kuu ya Tanga-Pangani”Alisema.Awali akizungumzia mkanganyiko huo Diwani wa kata ya Duga Khalid Rashid(CUF) alisema hapingani na maamuzi ya baraza lakini jambo la msingi ni kuangalia gharama zilizotumiaka eneo la masiwani za ujenzi wa jengo la ghorofa moja la utawala kwa ajili ya Hospitali ya Wilaya.

Alisema ipo haja kwa Halmashauri kuwa makini juu ya taarifa za wataalamu ambao awali waliishauri Halmashauri kujenga Hospitali hiyo eneo la masiwani ambapo zaidi ya shilingi milioni 700 zimetumika katika ujenzi wa jingo la utawala.“Mstahiki Meya sipingi na wala sikatai hospitali hiyo kujengwa mwakidila lakini tuwe makini na wataalamu wetu tumewekeza fedha nyingi kwa nini hizi bilioni 1.5 zisiendeleze pale masiwani? lakini ni maamuzi ya baraza wacha tuyaheshimu”Alisema Rashidi.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Tanga Thobias Mwilapa alisema kumekuwepo na maneno ya fitina juu ya mradi huo wa Hospitali lakini jambo muhimu muafaka umefikiwa wa wapi itajengwa hilo ndio jambo la msingi.Alisema hakuna haja ya kulumbana hasa katika maswala ya msingi na maendeleo ya wanachi makubaliano ndio jambo muhimu ili pande zote mkubaliane kwa pamoja wapi hospitali hiyo itajengwa na lengo ni kumsaidia mwananchi katika swala la afya.

MAKAMU WA RAIS AFANYA ZIARA MERERANI,AZINDUA KIWANDA CHA KUCHENJUA MADINI YA GRAPHITE

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hasan amewataka wamiliki wa migodi na viwanda vya kuchenjua madini nchini kuzingatia haki na usalama wa wafanyakazi wao.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa Kiwanda cha Godmwanga Gems Ltd kinachotengeneza madini ya Kinywe (Graphite), Mererani Wilayani Simanjiro.

Makamu wa Rais ambaye yupo kwenye ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani Manyara.

“Pamoja na kuwekeza kupata pesa na kutoa ajira, kulipa kodi ni muhimu kuzingatia afya ya mfanyakazi kwa kumlinda kwa kumpatia vifaa vya usalama kazini pamoja na haki zao” alisema Makamu wa Rais.

Kiwanda cha Gomwanga Gem Ltd kinamilikiwa Mtanzania kwa asilimia 100%, kinazalisha tani 60 kwa siku na kimeajiri Watanzania 80 ambacho mpaka sasa kimezalisha tani 3730.

Kwa upande mwingine Waziri wa Madini Mhe. Angella Kairuki amesema kwa sasa Serikali imeweka zuio la kusafirisha madini ghafi mpaka yaongwezewe thamani hivyo amempongeza mmiliki wa kiwanda hicho kwa kuitikia maelekezo ya Serikali.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akionyeshwa namna madini ya Tanzanite yanavyotambulika na kuwekwa kwenye madaraja yake na Mtaalam wa Madini Bw. Jaffar Ally Mohamed wakati alipotembelea Ofisi ya Afisa Madini Mkazi Mererani. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongozana na Meneja wa Kampuni ya Godmwanga Gem Ltd Bw. Andrew Mbando (katikati) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Alexander Mnyeti (kulia) wakati alipotembelea kiwanda kinachomilikiwa na Mzawa kwa asilimia ambayo inachenjua madini ya Kinywe (Graphite). 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki kabla ya kuweka jiwe la msingi wa ufunguzi wa Kiwanda cha Godmwanga Gems Ltd kinachochenjua madini ya Kinywe (Graphite), Mererani wilayani Simanjiro mkoani Manyara.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka  jiwe la msingi la ufunguzi wa Kiwanda cha Godmwanga Gems Ltd kinachochenjua madini ya Kinywe (Graphite), Mererani wilayani Simanjiro mkoani Manyara.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipiga makofi mara baada ya akiweka  jiwe la msingi la ufunguzi wa Kiwanda cha Godmwanga Gems Ltd kinachochenjua madini ya Kinywe (Graphite), Mererani wilayani Simanjiro mkoani Manyara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Kiwanda cha Godmwanga Gems Ltd kinachochenjua madini ya Kinywe (Graphite), Mererani wilayani Simanjiro mkoani Manyara.

JUMIA TANZANIA YAZINDUA KAMPENI KUBWA YA MAUZO YA MWAKA ' BLACK FRIDAY'

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

MTANDAO wa Jumia Tanzania umezindua rasmi kampeni kubwa ya mauzo ya mwaka inayojulikana kama BLACK FRIDAY inayolenga kuwawezesha watanzania kufanya manunuzi kwa ajili nya msimu wa sikukuu za Krisimasi na mwaka mpya.

Black Friday imekuwa inafanya mauzo ya bidhaa tofauti kwa bei nafuu kutoka kwa wauzaji mbalimbali mtandaoni na kwa kupitia Jumia Tanzania itadumu kuanzia Novemba 16 hadi Desemba.Akizungumzia uzinduzi wa kampeni hiyo ya Black Friday, Meneja Masoko wa Jumia Tanzania Albany James amesema kuwa, kwa kawaida Black Friday imekuwa inafanyika kila mwaka ifikapo Novemba 23, lakini kwa mwaka huu itakuwa kila Ijumaa na itaanzia Novemba 23 mpaka Desemba 07 mwaka huu.

James amesema, tofauti na siku za kawaida za Black Friday kutakuwa na ofa nyingi zaidi na mapunguzo makubwa ya bei kwa bidhaa zote mpaka kufikia asilimia 70 na hii katika kuhakikisha wateja hawapitwi kunufaika na maununuzi ya bidhaa kutoka kwa wafanyabiashara tofauti wanaoaminika kwenye mtandao wa Jumia."Ukiachana na ofa na mapunguzo ya bei, kutwakuwa na vocha za bure za manunuzi kuanzia shilingi 5,000 mpaka 80,000, mauzo ya bidhaa ya muda mfupi katika siku (flash sales) na kuogesha zaidi Black Friday kutakuwa na 'Treasure Hunt' kila Ijumaa ambapo bidhaa itafichwa kwenye mtandao wa Jumia," amesema James.

"Mteja mwenye bahati atakayefanikiwa kuitafuta na kuipata atauziwa kwa bei yenye punguzo la asilimia 99, na baadhi ya zawadi zitakazokuwepo kuanzia Ijumaa hii ni luninga ya kisasa yenye ukubwa wa inchi 32 inayouzwa kwa shillingi 570,000 mtandaoni na itafichwa na kuuzwa kwa 5,700 kwa mteja atakayeipata, "amesema.Aidha, ameongeza kuwa lengo kuu la Jumia ni kuwawezesha watanzania kufanya manunuzi ya bidhaa mbalimbali kwa urahisi na haraka mahali popote naa muda wowote walipo na mteja atakayenunua bidhaa kupitia Jumia itakayozidi thamani ya 200,000 atapelekewa bure mpaka alipo kwa mkoa wa Dar es Salaam.

Kwa upande wa washiriki wa Black Friday, Kutoka kampuni ya Skymark Meneja wa Kampuni hiyo, Nishit Modessa amesema kuwa wameamua kushirikiana na Jumia Tanzania baada ya kuona ni wazo zuri sana baada ya kuletewa na wakaamua kutoa pikipiki ili wateja wa Jumia washindanie.

Miodessa amesema, huu ni mwanzo wa ushirikiano wao ila wanategemea kuendelea kushirikiana nao zaidi katika kuuza bidhaa zao ambazo ni pikipiki na bajaji kupitia njia ya mtandao.
 Meneja Masoko wa Jumia Tanzania Albany James  akizungumzia  uzinduzi  rasmi wa kampeni kubwa ya mauzo ya mwaka inayojulikana kama BLACK FRIDAY inayolenga kuwawezesha watanzania kufanya manunuzi kwa ajili nya msimu wa sikukuu za Krisimasi na mwaka mpya kupitia mtandao wa Jumia Tanzania, kulia ni Meneja Uhusiano wa Umma Jumia Tanzania Kijanga Geofrey.
 Meneja wa Kampuni ya Skymark Nishit Modessa akielezea ushiriki wao kwa mara ya kwanza katika mauzo makubwa ya mwaka yanayofanyika kupitia kampuni ya Jumia Tanzania na kuamua kushirikiana nao kwa kutoa pikipiki na wateja washindanie, Kushoto ni  Meneja Masoko wa Jumia Tanzania Albany James.

SERIKALI YASAINI MKATABA WA MKOPO NAFUU WA SHILINGI BILIONI 440.703 PAMOJA NA MSAADA WA SH. BILIONI 45 KUTOKA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA.

0
0

Na Grace Semfuko-MAELEZO.

Serikali kupitia Wizara ya Fedha imesaini mikataba mitatu na Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB ya kuipatia msaada na mikopo ya masharti nafuu yenye thamani ya dola za Kimarekani 156.59 ambazo ni sawa na shilingi Bilioni 358.236 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Mikataba hiyo ya Mikopo na Msaada imesainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Dotto James na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Dkt Alex Mubiru ambapo kwa upande wa mikopo Serikali ya Tanzania itailipa kwa kwa muda wa miaka 40 ijayo.

Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa njia ya kusafirisha Umeme wa Msongo Mkubwa wa 400kV kuanzia Nyakanazi Biharamuro Mkoani Kagera hadi Kigoma uliopata mkopo wa dola za Kimarekani milioni 123.39, Mradi wa kudhibiti Sumu Kuvu kwenye mazao ya nafaka ambao umepata dola milioni 33 zikiwepo dola milioni 20 za msaada na dola milioni 13 za mkopo huku Bajeti ya Serikali ya mwaka 2018/2019 nayo ikiongezewa mkopo wa masharti nafuu wa dola milioni 56 sawa na shilingi Bilioni 128.28.

Akizungumza wakati wa utiaji saini wa mikataba hiyo mitatu ya mikopo na msaada kati ya Tanzania na Benki ya maendeleo ya Afrika AfDB, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw.Dotto James amesema Serikali itahakikisha miradi hiyo inatekelezwa kama ilivyokusudiwa ili kuwaletea maendeleo Watanzania.

“Ndugu zangu hii ni hatua kubwa na nzuri kwetu watanzania, hizi sio fedha ndogo, ni fedha nyingi ambazo ni mkopo wa masharti nafuu pamoja na msaada kwenye eneo la kudhibiti Sumu Kuvu za nafaka, tutalipa mikopo hii kwa muda wa miaka 40” alisema Dotto James Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango.

Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Dkt Alex Mubiru amesema Benki hiyo inalenga kuimarisha maendeleo ya Watanzania kwani fedha hizo zinaingia moja kwa moja kwenye miradi ambayo itatumiwa na wananchi.

“Benki yetu ya Maendeleo ya Afrika AfDB inalenga kuimarisha maendeleo ya wananchi, tuna miradi mingi tunayofadhili kwa nchi za Afrika, kwa Tanzania pia tunayo miradi tunayoimarisha, lengo la mikopo na misaada hii ni koboresha maishaya watanzania” alisema Dkt Mubiru Mwakilishi Mkazi wa AfDB.

Zanzaibar ni miongoni mwa eneo litakalonufaika na msaada huo kutoka Benki ya AfDB kwa upande wa kudhibiti Sumukuvu kutoka kwenye mazao ya nafaka ambapo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bw.Ahmad Kassim Haji amesema watahakikisha wanalinda na kuhifadhi vizuri mazao yote ya nafaka na kwamba mradi huo utawawezesha kufanya shughuli hiyo kikamilifu.

Kwa Upande wake Mkemia Mkuu wa Idara ya Usalama wa Chakula kutoka katika Wizara ya Kilimo Bw. Clepin Josephat amesema Sumu kuvu ni fangasi hatari kwa uhai wa binaadamu kama watatumia nafaka zenye fangasi hao kwa ajili ya chakula.

“Sumu Kuvu ni hatari sana ,inaweza kusababisha Kansa ya Damu, Kansa ya Ini na magonjwa ambayo yanaua taratibu,watu wengi hawaielewi Sumu kuvu, sasa kupitia mradi huu tutaidhibiti kwa nguvu kubwa ili kulinda afya zetu” Alisema Bw Josephat.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango  Doto James (kulia) akiwa pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(AfDB) Alex Mubiru wakisaini mikataba ya makubaliano ya mkopo wa masharti nafuu wa  jumla ya Shilingi bilioni 440.703 pamoja na msaada wa Shilingi bilioni 45 ambapo fedha hizo zote zitatumika katika Mradi mkubwa wa umeme mkoani Kigoma, Bajeti Kuu ya Serikali, Kilimo pamoja na mambo mengine ya kimaendeleo.
 . Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango  Doto James (kulia) akizungumza na wanahabari (hawaonekani) pichani mara baada ya kusaini Mikataba hiyo ya mkopo wa masharti nafuu wa  jumla ya Shilingi bilioni 440.703 pamoja na msaada wa Shilingi bilioni 45 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) katika hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa wa Hazina jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Alex Mubiru 
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(AfDB) Alex Mubiru (kushoto) akizungumza na Wanahabari mara baada ya Benki hiyo kuikopesha Serikali ya Tanzania  jumla ya Shilingi bilioni 440.703 pamoja na msaada wa Shilingi bilioni 45 ambapo fedha hizo zote zitatumika katika Mradi mkubwa wa umeme mkoani Kigoma, Bajeti Kuu ya Serikali, Kilimo pamoja na mambo mengine ya kimaendeleo. 

POLISI WILAYA YA TABORA INAMSAKA ALIYESABABISHA TAHURIKI KWA KUTUMA MESEJI YA UONGO KUHUSU KUTEKWA WATOTO

0
0
NA TIGANYA VINCENT,RS TABORA

JESHI la Polisi Wilaya ya Tabora linaendelea kumtafuta mtu aliyesambaza ujumbe wa uongo juu ya kutekwa wa wanafunzi wawili wa Shule ya Msingi ChemChem uliosababisha taharuki kwa wananchi na kupelekea kuharibu mali za Polisi.

Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Tabora (OCD) John Mfinanga wakati akitoa ufafanuzi kwa Madiwani wa Manispaa ya Tabora kwenye kikao cha robo ya kwanza.Alisema ujumbe huo ulisababisha kuwepo na uvunjifu wa amani ambao ulitokana na baadhi ya raia kuanza kuwashambulia Polisi na mgari yao na kupelekea kupasuliwa vyoo.

Mfinanga alisema hadi leo ikiwa saa 30 zimeshapita hakuna mzazi aliyejitokeza kutoa taarifa juu ya kupotelewa na mtoto jambo linaonekana lilikuwa na uongo na lenye nia ya kuleta vurugu katika jamii.“Waheshimiwa Madiwani ni mzazi gani anaweza kukaa zaidi ya masaa 24 mtoto wake amepotea hatoi taarifa…tunamtafuta aliyesambaza meseji hiyo ili hatimaye tumfikishe anapostahili kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria” alisema.

Aliwataka Madiwani kusaidia kuwaelimisha wapiga kura wao wanapotoa taarifa ziwe za kweli ili zisisababishe taharuki na fujo katika jambo.Katika hatua nyingine Kamanda huyo wa Wilaya ya Tabora alisema Jeshi la Akiba Mgambo lipo kisheria na liko kwa ajili ya kusaidia majeshi mbalimbali yanapokuwa na uhitaji katika kutekeleza majukumu yao.

Alisema kama kuna miongoni mwao ambao sio waaminifu na wamekuwa wakiwaibia na kuwatesa wananchi ni vema wakatoa taarifa ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao kama waarifu.Mfinanga alisema uamuzi wa kulitumia Jeshi hilo la Akiba ulipitishwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya kwa lengo la kusaidia katika kukabiliana na vitendo vya uharifu katika maeneo mbalimbali na sio kwa lengo la kuwaumiza wananchi.

Awali baadhi ya Madiwani wa Manispaa ya Tabora walimtaka OCD kuachana na matumizi ya Mgambo hao kwa sababu ya baadhi yao kuwa wezi, vibaka na wanaoendesha vitendo vya unyanyasaji wa wananchi wanapokuwa katika Doria.Diwani wa Kata ya Isevya Ramadhan Kapera alisema hawawataki migambo kwa sababu ni wezi na wanachafua sifa ya Jeshi la Polisi la kulinda raia na mali zao.

Alisema kama Polisi ni wachache ni vema wakawatumia Jeshi la Wananchi wa Tanzania na Majeshi mengine katika kukabiliana na uhalifu katika Manispaa hiyo.Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Tabora Kitwala Komanya alisema kuwa baada ya kupata malalamiko kwa wakazi wa Tambuka Reli juu ya vitendo viouvu vinavyofanywa na baadhi ya Mgambo amekutana nao na kuwaonya.

Alisema Serikali haitasita kumchukulia hatua Mgambo na Polisi yoyote ambaye itabainika kuvunja Sheria ikiwemo kuiba mali za wananchi

TANZANIA YAPIGA HATUA KATIKA SEKTA YA BARABARA

0
0
Na. Vero Ignatus, Arusha

Serikali ya Tanzania imefanikiwa kuboresha ujenzi wa barabara kwa kutumia Teknolojia ya kuchanganya lami Kulingana na Mazingira husika katika kanda mbalimbali Nchini na ipo teyari kwa ajili ya uwekezaji kwa maendeleo ya uchumi wa taifa .

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Arusha Waziri wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano Mhandisi Isack Kamwele katika mkutano wa kimataifa Mhandisi amesema wakala wa barabara nchini Tanroads wameanzisha miongozo ya kuchanganya lami Kulingana na Mazingira ya hali ya hewa ya mikoa mbalimbali ili kuweza kujenga barabara imara zitakazoendana na mazingira husika.

Ameleza kuwa Tanzania kutokana na mikutano hiyo wameweza kufanikiwa kutengeneza Teknolojia mpya ya kuchanganya lami kutokana na mazingira na jiografia ya maeneo ambapo mfano lami inayojengwa Katavi itaendana na hali ya hewa ya Mazingira yake ili barabara zisiharibike na kudumu kwa muda mrefu hivyo kusaidia kukuza uchumi. Amewata wataalamu wa TANROADS kutofanya kazi Kwa mazoea na pia kuhakikisha wanatatua matatizo ya sehemu zao za kazi wasisubiri hadi mamlaka za juu kuwapangia majukumu yanayowahusu. 
Kwa upande wake Mkurugenzi wa TPA Deusdedit Kakoko akiongea kama mshiriki wa mkutano huo amesema kuwa mkutano huo umekuwa ni sehemu muhimu kwao kama mamlaka ya bandari wamejipanga kutumia mkutano huo kuboresha utendaji wao wa kazi.Kuangalia mabadiliko ya teknolojia ya usafirishaji na matumizi ya Tehama yatasaidia kuboresha na kubadilika kwa kwenda kwenye kizazi cha nne cha mapinduzi ya usafirisha duniani ambapo jambo hilo litaharakisha utoaji wa bidhaa katika bandari .

Kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Mapinduzi ya nne ya sekta ya usafirishaji yanayohusiana na mabadiliko ya kiuchumi katika nchi zinazoendelea.

GST YAAGIZWA KUANDAA RAMANI ZA MADINI NGAZI ZA MIKOA, WILAYA

0
0
*Biteko asema wachimbaji sasa kuchimba kwa uhakika


Na Asteria Muhozya, Dodoma

Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) imetakiwa kuandaa ramani zinazoonyesha madini mbalimbali katika ngazi ya Mikoa na Wilaya ili kuwapa nafuu watanzania wanaofanya shughuli za uchimbaji wa madini nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko baada ya kupokea taarifa ya Utafiti wa Jiokemia katika skeli kubwa na skeli ndogo (Geochemical Mapping for High and Low Density) uliofanyika nchi nzima kwa ushirikiano kati ya GST na Taasisi ya Jiolojia ya China.

Naibu Waziri Doto pia, ameitaka taasisi hiyo kuelekeza nguvu katika kuisaidia serikali katika kupata matokeo chanya katika shughuli za madini huku ikiongeza thamani ya kazi kutokana na utafiti huo na kuongeza kuwa, GST inaweza kutumia utafiti huo mkubwa kuandaa ramani za madini katika ngazi za Mikoa na Wilaya.

Akizungumzia manufaa ya tafiti huo kwa Tanzania, amesema baada ya muda si mrefu watanzania wanaofanya shughuli za uchimbaji watahamia katika uchimbaji wa uhakika na siyo wa kubahatisha kwa kuwa utafiti huo unaonesha mahali sahihi ambapo shughuli hizo zinaweza kufanywa.

Amesema mbali na shughuli za madini, utafiti huo pia unaweza kutumika katika sekta za kilimo, maji na ujenzi wa barabara kwa kuwa unawezesha kutambua aina ya udongo unaofaa kwa shughuli hizo. 

Kutokana na umuhimu wa utafiti na kazi iliyofanywa na taasisi hizo mbili, Naibu Waziri Biteko ametoa wito kwa Watanzania kuitumia taasisi ya GST katika shughuli za kitaalam ikiwemo kupata taarifa za utafiti zinazohusu sekta ya madini na kuongeza kuwa, sekta hiyo inao uwezo mkubwa wa kutekeleza wajibu wake.Aidha, Naibu Waziri Doto ametumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya China kutokana na ushirikiano huo iliyoutoa katika kutekeleza utafiti huo ambao umegarimu kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 4 na Laki Tano 

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jilojia ya China, Profesa Sun Xiaoming amesema kuwa taarifa ya utafiti iliyowasilishwa ni ya nchi nzima ya Tanzania na eneo la Mkoa wa Mbeya.Amesema utafiti huo umetoa matokeo ya jiokemia ya sampuli 71 nchini kote na sampuli 39 katika mkoa wa Mbeya na kuongeza kuwa utafiti huo utasaidia katika utekelezaji maendeleo ya shughuli za madini, kilimo na mazingira nchini.

Awali, akizungumza katika kikao hicho, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Mathias Abisai amesema kusudio la ujumbe huo ilikuwa ni kuhakiki kazi iliyofanyika na kuwasilisha ripoti. Ameongeza kuwa, ripoti hiyo itasaidia kwenye tafiti nyingine za madini ikiwemo maji na mazingira.

Ameongeza kuwa, mnamo Mwaka 2009 serikali ya China na Tanzania kwa kutumia taasisi zake za Jiolojia zilisaini hati ya makubaliano (MoU) kwa lengo la kuanzisha mradi huo wa miaka mitano ambapo kazi rasmi ya mradi ilianza mwaka 2013 na kukamilishwa mwaka 2018.

Naye, Kaimu Mtendaji Mkuu wa GST, Yokobeth Myumbilwa akileza malengo ya utafiti huo amesema kuwa ni kupata taarifa za utafiti wa jiokemia kwa ajili ya kuandaa kanzidata ambayo itaainisha uwepo wa taarifa zinazo ainisha uwepo wa aina mbalimbali za madini ,upangaji miji ,pamoja na taarifa hizo kuweza kutumika katika shughuli mbalimbali katika sekta za kilimo na mazingira.
 Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko, akionesha taarifa ya utafiti wa jiokemia uliofanywa nchi mzima na Taasisi ya Jiolojia ya Madini Tanzania (GST) kwa kushirikiana na Taasisi ya Jiolojia ya China. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia ya China Profesa Sun Xiaoming na Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Mathias Absai.
 Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Taasisi ya Jilojia ya China, Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), na Wataalam kutoka Wizara ya Madini na Tume ya Madini.
 Naibu Waziri Doto Biteko akimkabidhi Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia ya China, Profesa Sun Xiaoming Cheti cha kutambua mchango wake na kukamilika kwa utafiti wa Jiokemia uliofanywa nchini.
 Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia ya China, Profesa Sun Xiaoming (kulia) akitoa taarifa ya utafiti huo. Katikati ni Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko na kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu, Mathias Abisai.
 Sehemu ya Wataalam kutoka Taasisi ya Jiolojia ya China, Wizara, Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) na Tume ya Madini wakifuatilia kikao hicho.
 Mkurugenzi Mtendaji wa GST, Yokobeth Myumbilwa akizungumza jambo katika kikao hicho. 
 Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko akizungumza jambo (katikati). Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia ya China, Profesa Sun Xiaoming na kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu Mathias Abisai.
Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko akionesha Taarifa ya Utafiti wa Jiokemia iliyofanywa katika Mkoa wa Mbeya. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia ya China, Profesa Sun Xiaoming na kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu Mathias Abisai.

BARAZA LA KILIMO TANZANIA LAWAFUNDA WANACHAMA WAKE KUHUSU UONGOZI NA UTAWALA BORA

0
0
 Mkufunzi kutoka Baraza la Kilimo Tanzania Dkt Freddy Gamba akisisitiza jambo wakati akitoa mafunzo ya Uongozi na Utawala bora kwa wanachama wa Baraza la Kilimo Tanzania, ambapo wanachama hao wanatarajia kunufaika na mafunzo hayo kwa siku mbili yanayofanyika Dar es Salaam, huku lengo kuu ikiwa ni kuwajengea uwezo kiutendaji wanachama wa baraza katika taasisi wanazoziongoza. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Kilimo Tanzania Bi Janeth Bitegeko akisisitiza jambo kwa wanachama wa Baraza la Kilimo wanaoshiriki semina ya siku mbili ya Uongozi na Utawala bora, mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo zaidi wa kiutendaji wanachama wa Baraza la Kilimo Tanzania ambao ni viongozi katika taasisi wanazoziongoza.
 Afisa Sera kutoka Baraza la Kilimo Tanzania Bi Neema Nyamubi na baadhi ya wanachama wa Baraza la Kilimo Tanzania wakifuatilia kwa makini mafunzo ya Uongozi na Utawala bora, mafunzo hayo ya siku mbili yanayofanyika Dar es Salaam yanaratibiwa na Baraza la Kilimo Tanzania.
 Baadhi ya wanachama wa Baraza la Kilimo Tanzania ambao wanatoka kwenye Taasisi za TAMPRODA, SECO,  SUWA Farmers Association, Agri link Tanzania na Morogoro Rural Agro Dealers  Association, wakifuatilia mafunzo ya Uongozi na Utawala bora, mafunzo hayo ya siku mbili yanayofanyika Dar es Salaam yameratibiwa na Baraza la Kilimo Tanzania.
 Mwenyekiti wa taasisi ya Morogoro Rural Agro Bw Michael Mpembwa akijadili jambo na washiriki wenzake na wa semina ya uongozi na uatawala bora, mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo wa kiutendaji wanachama wa baraza la kilimo Tanzania.
Afisa Uhamasishaji Maendeleo ya wanachama na Uhusiano Kimtandao kutoka Baraza la Kilimo Tanzania Bw Khalid Ngasa na washiriki wengine wa semina ya siku mbili ya Uongozi na Utawala Bora, Semina hiyo imelenga katika kuwajengea uwezo zaidi wa kiutendaji wa wanachama wa Baraza la Kilimo Tanzania ambao ni viongozi katika taasisi wanazoziongoza.

MAANDALIZI YA JESHI KUANZA UBANGUZI WA KOROSHO KIWANDA CHA BUCO, LINDI

0
0

WAZIRI KIGWANGALLA AITEGA BODI YA WADHAMINI YA TaFF

0
0
Na Lusungu Helela-Dodoma.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameiagiza Bodi ya pili ya Wadhamini ya Mfuko  wa Misitu Tanzania (TaFF) isimamie utekelezaji wa uanzishwaji wa  mradi wa viwanda  vya kusindika, kuchakata  na kufungasha asali katika mikoa inayofuga nyuki ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo na kujenga uchumi wa viwanda

Waziri Kigwangalla ametoa agizo hilo   wakati alipokuwa akizindua  Bodi ya pili ya Wadhamini ya Mfuko wa Misitu Tanzania uliofanyika leo jijini Dodoma.

Kufuatia agizo hilo, Waziri Kigwangalla ameiambia Bodi hiyo kuwa pamoja  na utekelezaji wa maagizo mengine aliyowapatia, suala la uanzishwaji viwanda vya kusindika, kuchakata na kufungasha asali na bidhaa nyingine zitokanazo na ufugaji nyuki katika mikoa ya Tabora, Kigoma, Katavi, Rukwa, Songwe na Mbeya liinapaswa kupewa uzito wa  juu kiutekelezaji.

Waziri Kigwangala ameongeza kuwa ni azma ya Serikali ya awamu ya tano kuifikisha Tanzania katika uchumi wa  kati ifikapo 2025 na kuwa suala hilo lina  umuhimu mkubwa  kwa wafugaji wa nyuki na uhifadhi mazingira..

Ameongeza kuwa endapo suala hilo la viwanda litafanikiwa , itasaida  kuchochea jamii  kuwa mstari wa mbele  kulinda misitu badala ya sasa jamii kujikita kwenye ukataji  miti ovyo hali inayotishia nchi kugeuka kuwa  jangwa kama hatua za haraka hazitachukuliwa. 

Amesema kiwango cha  ufugaji nyuki kwa mikoa inayofuga  si cha kuridhisha kwa vile wafugaji walio wengi  wamekuwa wakifuga kwa mazoea jambo ambalo wafugaji walio wengi kuamua kuachana na shughuli hiyo na kugeukia uchomaji mkaa pamoja na kujiingiza kwenye   shughuli za uharibifu mazingira.

Waziri Kigwangalla amesema uanzishwaji wa viwanda hivyo vitasaidia jamii kuwa na  kipato mbadala hali itakayopelekea wananchi  kuanza kuona umuhimu wa kulinda na kuhifadhi misitu.

"Mkianza kuwekeza upande wa magharibi  ambapo kuna zaidi ya asilimia 60 ya misitu yote hapa nchini wananchi, wakiwemo Nzega, Sikonge, Uyui, Tanganyika, Mlele, Mpanda na Kaliua hawatakubali kuona mtu au kikundi cha watu kinaharibu misitu.

 "Nataka kuona mapinduzi makubwa kwenye ufugaji nyuki kwa kuiwezesha jamii  kuwa na  mizinga ya kisasa ili iweze kufuga nyuki  kisasa na hatimaye wapeleke kwenye viwanda wakajifunze kufungasha kisasa, ili ipate bei kubwa, na mwisho wa siku wataona faida ya kuwa na misitu.


Wakati huo huo, Waziri Kigwangalla ameitaka Bodi hiyo isimamie utekelezaji wa uhuishaji wa misitu ya kijiji pamoja na ile ya Halmashauri ambayo tayari imeharibiwa kwa kuanza kupanda miti ya  asili pamoja na kuanzisha mashamba mapya ya miti.

Naye, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe, Constantine Kanyasu ameitaka Bodi hiyo isimamie utekelezaji wa upandaji miti kwa vile mikoa kama Shinyanga hali ya uharibifu misitu inatisha,

Ameongeza kuwa kama hatua za makusudi hazitachukuliwa itafika kipidi ambacho akina mama wa vijijjini watakuwa wakitembea umbali wa kilomita 200 kwa ajili yua kutafuta kuni

Awali, Kaimu Katibu ,Mkuu wa Wizara hiyo, Lucius Mwenda amesema tangu kuanzishwa kwa Mfuko huo umekuwa ukisaidia sana kwenye uhifadhi licha ya kuwa mfuko huo umekuwa na changamoto ya uhaba wa watumishi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi hiyo Prof. Romanus Ishengoma amemhakikishia Waziri Kigwangalla kuwa Wajumbe wa Bodi watafanya kazi kwa weledi na utaalamu wa hali ya juu na kuanza na suala la uanzishwaji wa viwanda vitavyowasaidia wafugaji nyuki nchini.
 Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza  na Wajumbe wa  Bodi ya pili ya Wadhamini  ya Mfuko wa Misitu Tanzania  pamoja na sekretarieti ya Bodi hiyo wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo iliyofanyika jijini Dodoma. 
 Mwenyekiti wa  Bodi ya pili ya Wadhamini  ya Mfuko wa Misitu Tanzania, Prof. Romanus Ishengoma akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Romanus Ishengoma  mara baada ya Waziri Kigwangalla  kuzindua  Bodi hiyo jijini Dodoma.
 Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Wizara hiyo,  Mhe. Constantine Kanyasu ( kushoto)  wakimkabidhi kabrasha Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Misitu Tanzania,  Prof. Romanus Ishengoma (kulia) ikiwa ni ishara ya kumkabidhi majukumu ya kuusimamia Mfuko huo wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo uliofanyika leo jijini Dodoma.
 Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Wizara hiyo,  Mhe. Constantine Kanyasu (kushoto)  wakimkabidhi kabrasha Mjumbe  wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Misitu Tanzania, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa  (kulia) ambaye pia  ni Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki  wakati  Waziri Kigwangalla alipokuwa akizindua wa Bodi hiyo jijini Dodoma. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Wizara hiyo,  Mhe. Constantine Kanyasu (kushoto)  wakimkabidhi kabrasha Mjumbe  wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Misitu Tanzania, Tuli Msuya (kulia)  wakati  Waziri Kigwangalla alipokuwa akizindua wa Bodi hiyo jijini Dodoma
Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Wizara hiyo,  Mhe. Constantine Kanyasu (kushoto)  wakimkabidhi kabrasha Mjumbe  wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Misitu Tanzania, Prof, Dos Santos Silayo (kulia) ambaye pia  ni Mtendaji  Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)  wakati  Waziri Kigwangalla alipokuwa akizindua wa Bodi hiyo jijini Dodoma. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt. Hamisi Kigwangalla(katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Wajumbe wa  Bodi ya pili ya Wadhamini  ya Mfuko wa Misitu Tanzania  pamoja na sekretarieti ya Bodi hiyo wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo iliyofanyika jijini Dodoma. Wengine ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu(wa tatu kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Prof. Romanus Ishengoma (wa tatu kulia). 
                     ( Picha zote na  Lusungu Helela-MNRT) 

CITI FOUUNDATION NA TAMFI WAZINDUA AWAMU YA TATU YA TUZO ZA WAJASIRIAMALI

0
0

Mtendaji mkuu Citi bank Tanzania joseph Carasso akizungumza. Mwingine ni wmenyekiti wa bodi ya Tamsi Joel Mwakitalu

Kwa mara ya tatu mfululizo, CITI Foundation ikishirikiana na Shirikisho la Asasi zinazotoa huduma ndogo za fedha (TAMFI), jana wamezindua awamu ya tatu ya tuzo za wajasiriamali za CITI (CITI Micro entrepreneurship Awards – CMA).Tuzo hizi zinalenga kutambua mchango mkubwa wa wajasiriamali kwenye kuinua uchumi wa familia zao na jamii zinazowazunguka.

Kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu wa Citibank Tanzania, Bw. Joseph Carasso, tuzo za CITI zimeshamiri na katika kipindi cha miaka miwili iliyopita kumekuwa na mafanikio makubwa kwa wajasiriamali wadogo na walio wabunifu.
Washiriki katika uzinduzi
Watu walionufaika katika msimu uliopita wakizungumza umuhimu wa tuzo hizo

Mtendaji huyo alisema CITI inaamini kuwa wajasiriamali wadogo wenye ubunifu ndio wajasiriamali wakubwa wa kesho. Tunawathamini sana.Tuzo za wajasiriamali za CITI (CMA) zimekuwa alama kubwa ya utendaji wa kazi za Citi Foundation kwa zaidi ya muongo mmoja.

Tangu mwaka 2005, wakati zilipoanzishwa nchini Marekani tuzo za CITI, zimelenga kuleta mageuzi ya kiuchumi na fursa kwa wajasiriamali katika nchi zaidi ya nchi thelatini duniani kote.Hapa nchini katika awam,u ya tatu , CITI itatoa zaidi ya shilingi milioni 70 kwa washindi kumi na sita. Na tuzo hizi zitaweka alama na kutoa motisha kwa wajasiriamali na asasi zinazotoa huduma ndogo za fedha.
waandishi wa habaria wakirekodi tukio
Mtendaji wa TAMFI Terry akielezea hafla ya uzinduzi wa tuzo

waandishi kazini

Malengo ya Citi Foundation ni kufanikisha kuainisha huduma za fedha jumuishi na kuchangia Maendeleo endelevu (Sustainable Development Goal (SDG) 8,), ambayo pamoja na mambo mengine yanaainisha ajira zenye staha kwa wote.Akielezea zaidi, Bw Carasso, alisema kwamba tuzo hizi pamoja na kuinua viwango vya huduma za fedha jumuishi nchini zinasaidia mjasiriamali mmoja mmoja kuinua viwango vya maisha vya familia zao na jamii zinazowazunguka na Taifa kwa ujumla.

Hii inalenga moja kwa moja malengo ya SDG 9.3 ambalo linalenga kuongeza idadi ya wajasiriamali wadogo katika nchi zinazoendelea pamoja na huduma za kifedha katika mnyororo wa thamani na masoko.Naye Mwenyekiti wa Bodi ya TAMFI, Bw Joel Mwakitalu, alisema kwamba “tuzo hizi ni chachu kwa wajasiriamali na wanachi kwa ujumla na kwamba kukopa na kurejesha katika biashara ni ufunguo wa maendeleo ya ki-uchumi.”

Aliongeza kwamba “kwa miaka miwili iliyopita, zaidi ya wajasiriamali 30 wamenufaika na tuzo hizi. Wajasiriamali hawa walipita katika mchujo uliokuwa na vigezo vya urejeshaji wa mikopo kwa muda uliopangwa, ukuaji wa biashara, ubunifu katika biashara, uzalishaji wa ajira, na bishara endelvu. Miongoni mwa wajasirimali waliofaidika na fedha hizo walikuwepo katika hafla ya uzinduzi kwa msimu wa 2018/19.

Wajasiriamali hawa waliopita kwenye mashindano haya walipata Zaidi ya Shillingi Milioni 140 ambazo tafiti zinaonyesha kuwa asilimia kubwa ya pesa hizi za tuzo zimeziwekeza kwenye biashara zao.” Tuzo hizi zitazingatia maeneo ya kijiografia, jinsia, na sekta za uchumi. Biashara itakayoshindanishwa ni lazima iwe endelevu, inaleta mabadiliko katika maisha ya mjasiriamali na jamii inayomzunguka. Kutakuwa na mshindi wa jumla na mshindi kutoka taasisi inayotoa huduma ndogo za fedha.

VIGEZO VYA TUZO

Wajasirimali wadogo wenye mafanikio ni lazima wawe wale ambao kwa juhudi binafsi wamesababisha mabadiliko makubwa katika shughuli zao, katika jamii na familia zao.


Maombi ya ushiriki yatachambuliwa kwa kuangalia yafuatayo:

Ukuaji wa kibiashara: Mjasirimali anatakiwa kuelezea historia ya biashara, ikoje kwa sasa, ilianza linin a ilianzishwaje, mapato na ukubwa wa mauzo wakati ananza na sasa na kiasi kinachouzwa kwa mwezi. Kwa sasa kuna matawi mangapi ukilinganisha na wakati alipoanza au kama utoaji huduma huo umetanuliwa au kubadilishwa.

Kutambua msukumo ulioletwa na biashara hiyo kwa biashara nyingine na faida ambazo wanunuzi au wateja wamezipata kutokana na kukua kwa biashara na kama biashara hizo zipi ndani ya jamii, nje ya wilaya au mbali zaidi.Uzalishaji wa ajira: je biashara imepanda kutoka kuwa na ajira ya mtu mmoja na kuajiri watuw engi wakiwemo wale ambao si wa familia moja.Watu wangapi waliajiriwa wakati wa kuanza na sasa wapo wangapi. Je jinsia katika ajira zikoje.

Uendelevu: je uendeshaji wa biashgara hiyo unaenda sawa na gharama zake, je imesajiliwa au inafikiriwa kusajiriwa?Je inategemea mafanikio ya mjasirimali au inajitegenmea na endelevu kwa kuzingatia msiungi uliowekwa?Ubunifu: je ni kitu gani kinafanywa tofauti ili kuifanya biashara kuwa na mafanikio?Je inatoa bidhaa adhimu? Je wameanzisha mawasilino ya Tehama au uhifadhi wa nishati ili kuendelezwa kwa ufanisi?

Nidhamu ya kifedha: je mshiriki ameonesha nidhamu ya fedha na hasa katika uwekaji wa akiba, urejeshaji wa mikopo na uwekezaji. Hapa anatakiw akuleta taarifa kamili inayohusu mikopo na akiba na historia yake.Manufaa kwa familia: Ni kwa namna gani biashara hiyo imeleta athari chanya kwa jamii. Je mafanikio ya biashara hiyo imewezesha kuboresha makazi, huduma za afya, elimu kwa watoto, afya na kadhalika. Onesha na mifano.

Naibu Waziri Dkt Kijaji Mgeni Rasmi Mahafali ya 11 ya Chuo Cha Kodi

0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 11 ya Chuo cha Kodi yatakayofanyika Novemba 17 chuoni hapo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkuu wa Chuo hicho Profesa Isaya Jairo amesema katika mahafali hayo Naibu Waziri atakabidhi zawadi kwa wanafunzi 14 waliofanya vizuri katika maeneo mbalimbali.

Profesa Jairo amesema kuwa wahitimu kwa mwaka huu ni 359 na idadi imekuwa ikiongezeka kila kila mwaka kutokana na ubora wa elimu wanayoitoa.
Amesema mikakati ya Chuo ni kuwa Chuo Kikuu kutokana na mahitaji ya Kodi na kuwa Chuo pekee kinachotoa utaalam wa kodi katika Afrika Mashariki.

Profesa Jairo amesema wahitimu 74 watatunukiwa Cheti cha Uwakala wa Forodha cha Afrika Mashariki pamoja na wahitimu 33 watatunukiwa cheti cha Usimamizi wa Forodha na Kodi, wahitimu 142 stashahada Usimamizi wa Forodha na Kodi, wahitimu 95 shahada ya Usimamizi wa Forodha na Kodi, wahitimu 95 wengine shahada ya uzamili katika Kodi na wahitimu 15 Postgraduate Diploma.

Katika mahafali hayo Naibu Waziri Kijaji atatoa vyeti kwa wahadhiri waliofanya tafiti na kuchapishwa katika majarida mbalimbali ya Kitaaluma.
Mkuu wa Chuo Cha Kodi Profesa Isaya Jairo akizungumza na waandishi habari kuhusiana na mahafali 11 ya Chuo hicho yatakayofanyika Novemba 17 mwaka huu katika viwanja vya Chuo hicho jijini Dar es Salaam.

TIGO YAZINDUA PROMOSHENI YA ‘JIGIFTISHE’ AMBAPO SHILINGI MILIONI 600 ZITATOLEWA KWA WATEJA NA KUWAFANYA MAMILIONEA MSIMU HUU WA SIKUKUU

0
0

Mkuu wa Masoko wa Tigo, Tarik Boudiaf (kushoto), Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo, Hussein Sayed (wa pili kushoto), Balozi waTigo Lucas Mkenda almaarufu Joti (katikati), Meneja Mawasiliano Woinde Shisael (wa pili kulia) pamoa na Mkuu wa Bidhaa za Tigo Pesa, James Sumari (kulia) wakizindua promosheni ya Jigiftishe itakayowapa wateja wa Tigo fursa ya kushinda hadi TSH 50 milioni katika msimu huu wa sikukuu.


Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo, Hussein Sayed (kushoto), Meneja Uhusiano wa Tigo Woinde Shisael (kati) pamoja na Balozi wa promosheni ya Tigo Jigiftishe, Lucas Mkenda almaarufu Joti (kulia) wakizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa promosheni ya Jigiftishe itakayowapa wateja wote watakaotumia huduma za Tigo katika msimu wa sikukuu fursa ya kushindania jumla ya shilingi 600 milioni.


Wateja watakaoongeza salio au kuweka Pesa Kwenye Tigo Pesa au Kutumia huduma yoyote ya Tigo watapata nafasi ya kushinda zawadi nono za hadi TSH milioni 50!

Dar es Salaam, 15 Novemba 2018; Tigo Tanzania - kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali, itawezesha wateja wake kuwa mamilionea baada ya kuzindua promosheni kubwa zaidi itakayogawa kiasi cha TSH milioni 600 katika msimu huu wa sikukuu.

Promosheni hiyo ya kipekee ya ‘JIGIFTISHE’ kutoka Tigo katika msimu huu wa Krismasi na Mwaka Mpya itawafanya zaidi ya wateja 450 kuwa mamilionea ndani ya siku 45, kutokana na kutumia huduma za Tigo pekee. Ni rahisi na hakuna kujiunga kwenye promosheni hii.

‘Wateja wa Tigo watakaoweka pesa kwenye akaunti zao za Tigo Pesa, kuongeza salio au kununua simu janja kwenye maduka yote ya Tigo au kutumia huduma zozote za Tigo katika kipindi hiki cha sikukuu watapata fursa ya kujishindia TSH milioni 1 kila siku au TSH milioni 10 kila wiki. Pia kutakuwa na zawadi kubwa za TSH milioni 15, TSH milioni 25 au TSH milioni 50 zitakazotolewa mwishoni mwa promosheni hii ya JIGIFTISHE!’ Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Akibainisha vigezo vya ushiriki katika promosheni hiyo ya JIGIFTISHE, James Sumari, Mkuu wa Bidhaa za Huduma za Tigo Pesa wa Tigo alisema kuwa ili kupata fursa ya kushinda, wateja wa Tigo wanahitaji kununua kifurushi chochote kwa njia yoyote (ikiwemo kupitia *147*00#, *148*00# au kuongeza muda wa maongezi kwa njia ya kielektroniki, kadi au kupitia Tigo Pesa) au kufanya miamala ya Tigo Pesa kupitia *150*01# katika msimu huu wa sikukuu.

‘‘Ni rahisi sana! Hakuna kufanya kitu chochote maalum ili uweze kushinda. Unachohitaji kufanya ni kuendelea kutumia huduma au kununua bidhaa za Tigo ili upate nafasi ya kuwa milionea!” Woinde alisisitiza. Kila muamala utakaofanyika utampa mteja nafasi moja ya kushiriki katika droo, na wateja wanaweza kutazama nafasi zao za kushinda kwa kupiga *149*22#. Kadri unavyofanya miamala zaidi ndivyo unavyojiongezea nafasi za kushinda.

Promosheni hii ya JIGIFTISHE itakayojaza mifuko ya wateja na manoti na kubadilisha maisha yao inathibitisha kuwa Tigo ndio mtandao unaotoa huduma bora zaidi za kidigitali kwa wateja wake na kuwawezesha kufurahia msimu huu wa sikukuuu huku wakimaliza au kuanza mwaka mpya kwa mtindo tofauti.

‘Hii ndio njia yetu ya kuwashukuru wateja wetu wote kwa kuendelea kutumia huduma zetu bora, zenye kasi ya juu na rahisi. Tunachukua fursa hii kuongeza tabasamu katika nyuso za wateja wetu,’ Woinde alisema.

Tayari wateja wa Tigo wanafurahia unafuu na urahisi wa kutumia huduma bunifu za Tigo kama vile kufanya miamala ya Tigo Pesa (kutuma na kupokea pesa ikiwemo kutoka mitandao mingine na benki), kulipia huduma mbali mbali kama vile LUKU, kufanya manunuzi kutoka kwa wafanyabiashara tofauti, kukamilisha malipo ya Kiserikali na pia kufurahia huduma bora za maisha ya kidigitali kwenye mtandao mkubwa zaidi wa 4G nchini.

CBA BANK NA VODACOM WAFANYA PROMOSHENI YA PILI YA SHINDA NA M-PAWA IKIWA NI MOJA YA JITIHADA ZA KUHIMIZA WATANZANIA KUWEKA AKIBA NA KULIPA KWA WAKATI.

0
0
Mkurugenzi Idara Wateja binafsi na Masoko wa Benki ya Biashara Afrika CBA Julius Konyani(katikati), na muwakilishi kutoka Vodacom Tanzania Noel Mazoya, katika katika uzinduzi rasmi wa Promosheni iliyopewa jina la Shinda na M-PAWA. ilifatwa na kutangazwa kwa washindi 400 waliongezewa mara mbili ya salio lao, na watu 30 zaidi waliochukua mikopo na kulipa kwa wakati walijishindia 100,000 tshs kila mmoja.

CBA Bank na Vodacom wamefanya promosheni ya pili ya Mpawa iliyoibua washidi wengine 200 walioweka amana na Mpawa , Ambao watajishindia mara mbili ya kiasi walichohifadhi kwenye Mpawa.

Promotion hii ilizinduliwa tarehe 8 mwezi wa kumi na moja, Draw ya leo inafanya idadi ya washindi kuwa 430, Ambapo washindi 400 wamejishindia mara mbili ya amana zao walizohifadhi kwenye Mpesa, na washindi 30 ambao walikopa na kurejesha kabla ya wakati wamejishindi Shilingi TZS 100,000/= kila mmoja. 
 
Jumla ya washidi 1296 wanategemea kupatikana katika kipindi hiki cha wiki sita za kampeni. Zawadi kubwa zitakazotolewa kwenye droo kubwa wiki ya sita zitakua ni kitita cha Milioni 10 taslimu na Bajaj tano.

Promosheni hii inaonyesha jitihada za CBA Bank na Vodacom kuleta muamko wa kifedha na kuhimiza Watanzania kuwa na tabia ya kuweka akiba. Akizungumza wakati wa uzinduzi kutoa zawadi kwa washindi wa droo ya kwanza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa CBA Julius Konyani alisema “M-PAWA ni bidhaa inayoendelea kuleta mapinduzi ya kimaendeleo kwa Watanzania hasa wale wamiliki wa biashara ndogo wanaoweka akiba na na kupata riba na Pia kupata mikopo inayowasaidia katika kuendeleza na kukuza biashara zao”.

Promosheni hii ya Shinda na M-PAWA itaendeshwa kwa muda wa wiki sita kuanzia Novemba 2018 hadi nusu ya Desemba 2018.

Meneja Masoko wa Vodacom Huduma za kifedha Noel Mazoya alisema “Wateja watakaoomba mkopo na kurudisha mapema watakuwa na nafasi ya kuopoa zawadi ya shilingi 100,000 kwa wateja 15 kila wiki na Jumla ya wateja 96 watashinda kwa wiki sita. 
 
Tunajenga utamaduni wa kuhimiza Watanzania kuchukua mikopo ili kuwawezesha kukuza biashara zao. Hata hivyo hatuwahimizi tu wateja wakope, lakini pia kurudisha mikopo mapema. Hii itawapa wateja fursa ya kuomba tena mkopo na kuongeza kiwango wanachoweza kukopa” alisema haya wakati wa tukio la droo ya kwanza lililoshuhudiwa na Bodi ya bahati nasibu Tanzania pamoja na watendaji wengine wa CBA.

Mpawa ni Huduma inayotolewa kwa ushirikiano wa Bank ya CBA na Vodacom, Huduma hii inawewezesha wateja kuweka fedha kwenye Mpawa na Kupata Riba/faida. CBA imekuwa mmojawapo ya benki inayowekeza nchini ambapo kuptia huduma hii imefanikiwa kuwafikia wateja zaidi ya milioni saba, wakiwa ni wateja wadogowadogo ambao wanahifadhi kiwango cha kati ya shilingi 1000/= na 3000/=. Viwango ambavyo mfumo wa kibenki wa kisasa usingeweza kuwahudumia, Huduma hii ya mpawa imeifikia jamii kubwa ambayo haipo kwenye mfumo rasmi wa kifedha (Financial Inclusions). 
 
CBA Bank na Vodacom zitaendelea kuwekeza nchini na wanatoa wito kwa wateja wote wa Vodacom/Mpesa kuweka hela zao katika kibubu chao cha mpawa ambacho ni salama na benki yao mkononi mwao, Pia wanaweza kukopa kiwango chochote kati ya shilingi 1000 mpaka laki tano.

WAZIRI WA MAJI MHE. PROFESA MAKAME MBARAWA (MB) AVUNJA MIKATABA YA WAKANDARASI WA MIRADI YA MAJI YA LINDI NA KIGOMA

0
0
Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa (Mb) akiwa na Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) ofisini kwake jijini Dodoma kuhusu kuvunja mikataba ya Wakandarasi wanaotekeleza miradi ya Maji ya Mkoani Kigoma na Lindi.


Waziri wa Maji Mhe. Profesa Makame Mbarawa (Mb) amevunja mikataba miwili inayohusu kandarasi ya ujenzi wa miradi ya maji kwa kampuni mbili za kimataifa. 

Kampuni hizo ni Overseas Infrastructure Alliance (India) Pvt. Ltd yenye mkataba Na. ME-011/2011-2012/W/05 iliyokua inatekeleza Mradi wa Majisafi na Usafi wa Mazingira wa Lindi mjini na kampuni ya Spencon Services Ltd yenye mkataba Na. ME-011/2011-2012/W/05 iliyokua inatekeleza Mradi wa Majisafi na Usafi wa Mazingira wa Kigoma mjini. Mikataba hiyo imevunjwa kutokana na uzembe wa wakandarasi hao kuchelewa kukamilisha miradi.

Profesa Mbarawa amefafanua kuwa mikataba ya wakandarasi hao imevunjwa kutokana na kufilisika kifedha na kusababisha kukosa uwezo wa kumalizia kazi ndogo iliyokuwa imebaki na kukamilisha miradi hiyo, kulikopelekea wananchi wa maeneo hayo kutopata huduma ya majisafi na salama kwa muda mrefu kinyume na matarajio ya Serikali hivyo kuvunjwa kwa mikataba.

Amesema hatua hiyo inatokana na miradi hiyo kuchukua muda mrefu kukamilika pamoja na juhudi za viongozi wa juu wa Serikali, akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa pamoja na Waziri mwenyewe kwa nyakati tofauti.

Mkandarasi wa mradi wa maji wa Lindi mjini kampuni ya Spencon Services Ltd ilipaaswa kukamilisha mradi toka Tarehe 17 Machi, 2015 kwa mujibu wa mkataba wa awali ikashindwa na kuongezewa muda hadi Tarehe 1 Desemba, 2015 lakini mpaka kufikia leo mradi huo haujakamilika. Naye mkandarasi wa mradi wa maji Kigoma mjini kampuni ya Overseas Infrastructure Alliance (India) Pvt. Ltd ilipaswa kukamilisha Tarehe 17 Machi, 2015 kwa mujibu wa mkabata wa awali, na ikaongezewa muda hadi Tarehe 23 Desemba 2015. Mradi huo haujakamilika mpaka sasa ukiwa umefikia asilimia 87 ya utekelezaji.

Profesa Mbarawa amesema kumekuwa na tabia iliyokithiri ya uzembe wa kuchelewa kukamilika kwa miradi ya maji katika maeneo mbalimbali nchini na kwa sasa Wizara ya Maji imeamua tabia hiyo ikome, na wakandarasi wote wenye tabia hiyo watachukuliwa hatua na wasitarajie kupata kazi yoyote katika miradi ya maji.

Pamoja na kuvunja mikataba ya wakandarasi hao, Serikali itachukua hatua zote za kinidhamu ili iwe fundisho kwa wakandarasi wengine wenye tabia kama hizi, na kusimamisha fedha za matazamio (retention money) ambazo zilikuwa zilipwe kwa wakandarasi hao baada ya kukabidhi mradi, sasa zitumike kwa ajili ya kumalizia kazi zilizobaki kwenye miradi hiyo.

Profesa Mbarawa amekiagiza Kitengo cha Manunuzi cha Wizara ya Maji kufanya uchunguzi wa kina kwa wakandarasi kwa lengo la kujua uwezo wao na kazi walizokwishazifanya ili waweze kujiridhisha na uwezo wao kabla ya kupewa kazi. Pia, ameagiza wakandarasi wasipewe kazi zaidi ya mbili kwa wakati mmoja, kwa kuwa jambo hilo linachangia utendaji wao kusuasua na kutaka wapewe kazi nyingine baada ya kumaliza kazi walizonazo kwa viwango vinavyokubalika.

Aidha, ameagiza wakandarasi wote watakaoharibu kazi za miradi ya maji kwa kuzifanya kinyume na makubaliano ya mikataba wachukuliwe hatua za kisheria na wasipewe tena kazi katika miradi ya maji.

ASILIMIA 30 SAWA NA KAYA MASKINI 6,048 HAZIJAFIKIWA -TASAF

0
0

Kamati ya kusimamia ofisi ya viongozi wakuu wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar na mkurugenzi mtendaji wa mfuko wa maendeleo ya jamii Ladislaus Mwamanga (mwenye suti ya rangi ya ugolo) na baadhi ya viongozi mkoani Pwani na halmashauri ya Kibaha Vijijini, wakipatiwa maelezo wakati walipotembelea kilimo cha bustani huko Disunyara Kibaha Vijijini. (picha na Mwamvua Mwinyi)


Naibu waziri ,ofisi ya makamu wa pili Rais wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mihayo N’hunga akizungumza wakati wa ziara ya kamati ya kusimamia ofisi ya viongozi wakuu wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar iliyofanyika Kibaha Vijijini Mkoani Pwani. (picha na Mwamvua Mwinyi)
…………………………………………….
 
NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA
MKURUGENZI wa mfuko wa maendeleo ya jamii -TASAF, Ladislaus Mwamanga amesema, bado zipo kaya maskini 6,048 sawa na asilimia 30 Tanzania Bara na Visiwani, ambazo hazijafikiwa katika utekelezaji wa mpango kunusuru kaya maskini . 

Aidha , wale ambao wameshanufaika awamu ya kwanza ya mpango huo watafanyiwa tathmini, na wameandaa mkakati wa kuwapima kwa vigezo vya kuwa na hali nafuu kwa utaratibu ili watoke na wapishe wengine.

Akiweka bayana juu ya masuala hayo, wakati wa ziara ya kamati ya kusimamia ofisi ya viongozi wakuu wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar iliyofanyika Kibaha Vijijini Mkoani Pwani, alisema maeneo ambayo hayakufikiwa ,utekelezaji utaanza mwezi april 2019 ,ili kukamilisha maeneo yote nchi nzima 16,048.#

Mwamanga alisema vijiji,sheia na mitaa 10,000 wameshavifikia hadi sasa .
Alifafanua, kuna kaya maskini ziliachwa kwenye mpango kwa sababu mbalimbali nao wataingizwa kwenye mfumo thabiti ili kuwa na rekodi sahihi kwa nchi nzima.
Hata hivyo ,alisema kaya ambazo zina wazee na wenye ulemavu wataendelea kuwasaidia ili kukidhi mahitaji yao ya msingi. 

Akizungumza baada ya kupokea taarifa hiyo, Naibu waziri ,ofisi ya makamu wa pili Rais wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mihayo N’hunga alisema, serikali ipo katika hatua za mwisho za kisera kutatua changamoto ya muda mrefu kwa kaya ambazo hazikujumuishwa katika mpango . 

Alifafanua ,kaya hizo hazikuweza kujumuishwa kutokana na kutofanyiwa dodoso na baadhi ya walio fanyiwa dodoso kukataa mpango kwa madai kwamba hauna manufaa kwao.

N’hunga alisema, kupitia madodoso hayo ,serikali ikajumuisha watu hao kwenye mpango kupitia changamoto hizo ,kuboresha sera na utaratibu uliopo ili kupunguza changamoto hiyo Bara na Visiwani kwa lengo la kuwafikia watanzania maskini katika ngazi ya sheia,kata, mitaa na vitongoji . 

Hata hivyo alieleza dhamira ya serikali zote mbili kufikia april 2019 kaya zilizopo kwenye vijiji,sheia na kata ambazo hazijafikiwa waweze kufikiwa .
Katibu tawala msaidizi mkoani Pwani ,Abdulrahman Mdimu alisema, wanakabiliwa na changamoto ya baadhi ya kaya maskini katika vijiji 86 ,mitaa 33 kutofikiwa kutokana na upungufu wa raslimali fedha .

Alitaja changamoto nyingine ni baadhi ya walengwa kukataa kuingizwa kwenye mpango kwa madai serikali haiwezi ikatoa fedha bure ,mitazamo hasi wakidhani kuwa kaya ikitambuliwa ni maskini ni kufedheheka.

Kamati hiyo ilitembelea pia ,mradi wa kutoa ajira ya muda -uvunaji wa maji ya mvua katika zahanati ya Disunyara kata ya Kilangalanga na kilimo cha bustani ,ambapo kaimu mratibu TASAF halmashauri ya Kibaha Vijijini Halima Bira, alisema mpango huo umekuwa mkombozi katika jamii . 

Halima alisema ,mpango huo ulianza kutekelezwa 2012 na jumla ya kaya 7,250 zilitambuliwa na kati ya hizo kaya 5,600 kutoka vijiji 45 ziliandikishwa kwenye mpango. 

Shuhuda wa utekelezaji wa mpango wa TASAF ,huko Disunyara Athumani Shabani alisema,ameweza kusomesha watoto ,wameibua miradi na wazee wananufaika kupitia mradi huo

MSHINDI WA NYUMBA ALIA KWA UCHUNGU KUFUATIA USHINDI WA BIKO

0
0

Mkurugenzi Mkuu wa Biko, Charles Mgeta wa pili kutoka kulia akimkabidhi hundi ya sh milioni 20 na nyumba iliyopo Kigamboni mshindi wao Prisca Msuya wa katikati aliyeibuka kidedea kwenye droo kubwa iliyochezwa juzi Jumatano. Wengine ni Afisa Leseni wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Catherine Lamwai kushoto akifuatiwa na Kajala Masanja Balozi wa Biko pamoja na Meneja Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Tuntufye Mwambusi. Picha na Mpigapicha Wetu.

Mkurugenzi Mkuu wa Biko, Charles Mgeta akimkabidhi hundi ya sh milioni 20 na nyumba iliyopo Kigamboni mshindi wao Prisca Msuya aliyeibuka kidedea kwenye droo kubwa iliyochezwa juzi Jumatano. Picha na Mpigapicha Wetu.

Mshindi wa nyumba na sh milioni 20 wa Biko, Prisca Msuya wa Mbezi jijini Dar es Salaam, amelia kwa uchungu mbele ya waandishi wa habari wakati anakabidbiwa hundi ya ushindi wake wa fedha na nyumba kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) iliyopo Kigamboni, huku akishuhudiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Biko, Charles Mgeta.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, mama huyo ambaye ni mjasiriamali mdogo wa duka, alisema kitu kinachomliza ni kushinda nyumba na sh milioni 20 kutoka Biko, huku akitokea kwenye maisha duni ya kuishi kwenye chumba na sebule. 

“Siamini macho yangu kwamba kweli nimeshinda nyumba kutoka Biko, maana maisha yangu ya nyuma anayajua Mungu, ingawa tangu Biko inaanza nilikuwa namuomba Mungu ili niweze kushinda zawadi za juu ikiwamo sh milioni 10, jambo ambalo Mungu amenitimizia mara mia moja. “Kwakweli namshukuru sana Mungu kwa zawadi hii pamoja na kuwaombea Biko katika mtazamo wao wa kuleta utajiri kwa watu wake, hivyo Watanzania wote naomba tucheze Biko kwa sababu ndio michezo halali unaoweza kutoa mamilioni pamoja na nyumba,”Alisema. 

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Biko, Charles Mgeta, alisema mchezo wao umeanzishwa kwa lengo moja la kuwakwamua Watanzania, wakiwamo wadau wa kubahatisha, akisema kila mtu anapoibuka na ushindi anazunguukwa na watu wanaotumia ushindi huo kuboresha maisha yao kwa pamoja. “Leo hii tunamkabidhi dada Prisca fedha na nyumba, ila tunaamini wapo watoto wake, mume na ndugu ambao kwa namna moja ama nyingine watakuwa wamekwamuliwa na mchezo wetu wa Biko. 

“Tunaomba Watanzania wote waendelee kucheza Biko ili wapate nafasi ya kushinda zawadi zetu maana kucheza ni rahisi ambapo namba ya Kampuni ni 505050 na kumbukumbu ni 2456, huku wanaocheza sana ndio wenye nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi kutoka kwetu Biko,”Alisema. 

Akizungumzia mchezo wa Biko, Afisa wa Leseni wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Catherine Lamwai, alisema Biko ni mchezo halali unaofuata sheria, kanuni na taratibu zote, huku akisema uwapo wake una manufaa makubwa kwa jamii pamoja na serikali kwa ujumla. 

“Mtu yoyote anayeshinda Biko lazima kuna sehemu yake ya ushindi inaenda kwa serikali kama kodi, huku Biko nao kama Kampuni wakikatwa kodi hivyo kuchangia kwenye pato la Taifa, hivyo Watanzania waendelee kucheza ili wapate ushindi,”Alisema. 

Naye Meneja Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Tuntufye Mwambusi, alisema mshindi wa Biko hajapata nyumba tu, ila nyumba bora inayofaa kukaliwa na binadamu wenye ndoto kama Prisca. “Hii ni fursa adhimu ambayo imeenda kwa mshindi wa Biko, ambapo ameshinda nyumba kutoka Biko, huku tukipewa fursa pana ya kutoa nyumba zetu kama NHC kwenda kwa washindi jambo ambalo ni la kizalendo linalofanywa na watu wa Biko, hivyo kwa niaba ya menejimenti ya NHC nafikisha pongezi kwao huku nikiwataka Watanzania wote wacheze Biko bila kuchoka ili washinde fedha na nyumba kwa ajili ya kubadilisha maisha yao,” Alisema. 

Bahati Nasibu ya Biko ni mchezo unaotoa nafasi kubwa ya ushindi ambapo mbali na kushinda nyumba, pia zawadi za papo kwa hapo zinaendelea kutolewa kuanzia sh 5000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na sh 1,000,000 huku Jumapili hii zawadi ya mamilioni au nyumba zikitarajiwa kwenda kwa washindi katika droo kubwa ya Jumapili hii.

ALIYEKUWA MBUNGE WA TEMEKE ABDALAH MTOLEA AOMBA KUJIUNGA NA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

0
0
Wakati tarehe ya mwisho ya kupokea viongozi wa upinzani wanao omba kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ikifika leo hii, Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Temeke kwa tiketi ya Chama cha CUF Abdalah Mtolea amejivua uanachama wa CUF na kujiuzuru Ubunge wa Jimbo la Temeke, huku akieleza chanzo kikiwa migogoro isiyoisha katika Chama cha CUF kwa zaidi ya miaka miwili sasa. Tukio la kujivua uanachama wa CUF na kujiuzuru ubunge lilitokea ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wakati akichangia hoja katika mjadala uliokuwa unaendelea mapema leo.

Ndugu Abdalah Mtolea jioni ya leo ametangaza nia yake ya kuomba kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) akieleza msingi wa uamuzi huo ukiwa umejengwa katika ukweli kwamba wengi ya wapiga kura wake wamemshauri kujiunga na CCM.

Akizungumza katika kikao cha waandishi wa habari, watumishi na baadhi ya wanachama wa CCM katika Ofisi ya Makao Makuu ya CCM Jijini Dodoma, Ndugu Mtolea ameeleza sababu zinazopelekea kuomba kujiunga na CCM na kuwa amevutiwa na Mageuzi makubwa ya Kiuongozi na kazi nzuri inayofanywa na CCM na Serikali yake chini ya Ndugu John Pombe Joseph Magufuli Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kikao hicho cha waandishi wa habari, watumishi na baadhi ya wanachama wa CCM kimehudhuriwa pia na Kamaradi Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa CCM ambaye amemwelekeza kwenda katika tawi lililo karibu na makazi yake Wilayani Temeke, Jijini Dar es Salaam ili afuate utaratibu wa kuomba uanachama wa CCM.



Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM
Ndugu Bashiru Ally akizungumza jambo wakati wa kikao cha Watumishi na baadhi ya Wanachama wa CCM,kushoto aliyekubwa Mbunge wa Temeke kwa Tiketi ya CUF Ndugu Abdalah Mtolea
  Ndugu Bashiru Ally Katibu Mkuu wa CCM na kushoto na aliyekubwa Mbunge wa Temeke kwa Tiketi ya CUF Ndugu Abdalah Mtolea Wakifurahia Jambo
Kikao cha Watumishi na Baadhi ya Wanachama wa CCM na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Bashiru Ally Kakurwa ambacho kilipata bahati ya kupokea kauli ya Ndugu Mtolea kuomba kujiunga na CCM.

MKUU WA JESHI LA MAGEREZA AKUTANA NA RC NJOMBE KABLA YA KUHITIMISHA ZIARA YAKE

0
0
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini (CGP) Phaustine Kasike akielezea malengo ya ziara yake ya kikazi mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe alipotembelea Ofisi za Mkoa huo.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akikagua mashamba ya chai ya Gereza Njombe kabla ya kuhitimisha ziara yake, leo Novemba 15, 2018.
Mkuu wa Jeshi la Magereza, CGP. Phaustine Kasike akiagana na baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi Mkoani Njombe ambao waliongoza msafara wa Kamishna Jenerali katika vituo vyote alivyotembelea Mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Christopher Ole Sendeka (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(wa pili toka kulia) pamoja na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Njombe. Wa pili toka kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Njombe, Bw. Erick Shitindi ( Picha na Jeshi la Magereza).
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Christopher Ole Sendeka akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini (CGP) Phaustine Kasike alipotembelea Ofisi za Mkuu wa Mkoa kabla ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi, leo Novemba 15, 2018.
Viewing all 46205 articles
Browse latest View live




Latest Images