Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live

Tanzania na China yasherekea miaka 50 katika sekta ya afya

0
0
Waziri Mkuu Mstaafu Salim Ahmed Salim, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu,Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dk. Augustine Mahiga, Balozi wa China Wang Ke pamoja na viongozi mbalimbali wakikata kike katika maadhimisho ya miaka 50 kati ya Tanzania na China katika Sekta ya Afya iliyofanyika Ubalozi wa China jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza katika sherehe za maadhimisho ya miaka ya 50 ushirikiano katika sekta ya afya kati ya Tanzania na China iliyofanyika katika Ubalozi wa China jijini Dar es Salaam.
Balozi wa China nchini Tanzania Wang Ke akizungumza katika sherehe za maadhimisho ya miaka ya 50 ushirikiano katika sekta ya afya kuhusiana na China kujihusiha katika masuala ya afya pamoja na ujenzi wa Hospitali uliofanyika Ubalozi wa China jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dk. Augustine Mahiga akizungumza  katika sherehe za maadhimisho ya miaka ya 50 ushirikiano katika sekta ya afya na ushirikiano kati ya Tanzania  na China katika masualaya kidiplomasia , sherehe hizo zimefanyika katika viwanja vya Ubalozi wa China jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi  Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Profesa Mohamed Janabi akizungumza kuhusiana na mchango wa China katika Taasisi hiyo katika maadhimisho ya miaka 50 kati ya Tanzania na China katika Sekta ya Afya yaliyofanyika Ubalozi wa China jijini Dar es Salaam
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akikabidhi zawadi Balozi wa China nchini  Tanzania Wang Ke ikiwa Serikali ya Tanzania kutambua mchango wa China  katika hafla ya sherehe zilizofanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akikabidhi zawadi Naibu Gavana wa Jimbo la Shadong Yuan Lini  ikiwa Serikali ya Tanzania kutambua mchango wa China  katika hafla ya sherehe zilizofanyika jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja kati ya Mawaziri pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu Salim Ahmad Salim. Picha na Chalila Kibuda

ZIARA YA MAKAMU WA RAIS KATIKA KIWANDA CHA KNAUF MKURANGA- PWANI

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Sululu Hassan akipata taarifa ya maendeleo ya uwekezaji wa kampuni ya KNAUF nchini kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu Tanzania, Bw. Zachopolous Georgions.
 Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa KNAUF Gypsum Afrika Mashariki, Zachopoulos Georgios wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya kiwanda hicho.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu akipokelewa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni mbunge wa Mkuranga, Abdalla Ulega  wakati alipowasili katika eneo la kiwanda Mkuranga
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu akiongea na uongozi ,wafanyakazi na wageni mbalimbali katika ziara hiyo
 Mkurugenzi Mtendaji wa KNAUF Gypsum Afrika Mashariki, Zachopoulos Georgios akielezea macheche kwa Makamu wa Rais juu ya kiwanda hicho.
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa KNAUF Gypsum Afrika Mashariki, Zachopoulos Georgios mara baada ya kumaliza kutoa maelezo ya kiwanda hicho. Baadhi ya wafanyakazi na wageni wakisubiri kumpokea, Mh.Makamu wa Rais wakati alipotembelea kiwanda cha KNAUF akiwa ziarani mkoani Pwani.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni mbunge wa Mkuranga, Abdalla Ulega akizungumza machache na Mkurugenzi Mtendaji wa KNAUF Gypsum Afrika Mashariki, Zachopoulos Georgios.
Eneo la kiwanda hicho. --- 

Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan, amefanya ziara katika kampuni ya kutoka Ujerumani ya KNAUF inayotengeneza jasi (Gypsum) na vifaa vingine vya kisasa vya ujenzi na kujionea uwekezaji inaoendelea kufanya wa kuzalisha bidhaa bora za ujenzi katika kiwanda chake kilichopo eneo la Mkuranga mkoani Pwani. 

Katika ziara hiyo ,Mh. Samia Suluhu Hassan,ambaye alikuwa katika ziara ya kutembelea mkoa wa Pwani,alisema serikali itaendelea kujenga mazingira mazuri ya uwekezaji ikiwemo kukabiliaana na changamoto ya umeme na kuwataka wawekezaji kutangaza bidhaa zao ili watanzania wajue kuwa bidhaa walizozoea kununua nje ya nchi sasa zinapatikana nchini. 

Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Bw.Zachopolous Georgions,alimweleza Makamu wa Rais, aliyeongozana na viongozi mbalimbali wa serikali katika ziara hiyo, kuwa hadi kufikia sasa kampuni tayari imewekeza zaidi ya shilingi bilioni 20/- na bado inaendelea kufanya uwekezaji, ili kuhakikisha bidhaa bora za ujenzi zinazalishwa hapa nchini ili kukidhi ongezeko la masoko yaliyopo sambamba na yaliyopo kwenye nchi jirani. Bw. Georgions, alisema kampuni hiyo imewekeza katika biashara ya jasi kanda ya Afrika Mashariki na imechagua, Tanzania kama makao yake makuu na ilianza rasmi shughuli zake nchini miaka mitatu iliyopita na tayari imeweza kuajiri watanzania kupitia uwekezaji wake. 

Mkurugenzi alisema kwa sasa kampuni inatengeneza jasi kutokana na mahitaji ya wateja wake na kwa kuanzia inatengeneza Gypsum zenye ukubwa wa milimita tisa hadi 12 ambazo ni nzuri katika kukinga nyumba dhidi ya moto na unyevu unaosababishwa na maji ya mvua. “Tunatumia teknolojia mpya ya utengenezaji wa jasi ambayo inawezesha matumizi ya chuma mahali ambako zamani zilikuwa zinawekwa mbao. 

Teknolojia hiyo tayari imeanza kutumika katika kiwanda cha Mkuranga pia tunatengeneza unga maalumu wa jasi ambao unaweza kutumika kwenye ujenzi hata wa nyumba za gharama nafuu”,alisema Georgions. Aliongeza kusema kuwa KNAF Tanzania pia ina mradi maalumu wa kufundisha vijana wa kitanzania kuhusu teknolojia mpya za ufungaji na utengenezaji wa jasi na wanapohitimu wanapatiwa vyeti vinavyotambulika dunia nzima katika sekta ya ujenzi vinavyowawezesha kufanya kazi katika nchi nyinginezo duniani KNAUF Tanzania, ni kampuni tanzu ya KNAUF yenye makao makuu Ujerumani, ikiwa na maeneo ya uzalishaji na ofisi za mauzo 150 katika nchi zaidi ya 60 ikiwa imeajiri wafanyakazi 26,000 duniani kote.

DAWASA Yawahakikishia Wakazi wa Dar es Salaam na Pwani Huduma Bora ya Maji

0
0
Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) imedhamiria kuendelea kuimarisha huduma zake katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano hasa katika ujenzi wa Viwanda kwa kuhakikisha kuwa huduma hiyo inafika maeneo ya Viwanda na kwa wananchi kwa kiwango kinachotakiwa.

Akizungumza katika kipindi cha mizani kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Afisa  Mtendaji mkuu wa Mamlaka hiyo Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kuwa wamejipanga kuhakikisha kuwa maeneo yote yanafikiwa na huduma ya maji safi na salama yakiwemo ya Viwanda na maeneo ya pembezoni  mwa Jiji la Dar es Salaam ambapo tayari hatua zimechukuliwa katika kutekeleza azma hiyo.

 “Tumejipanga kuhakikisha kuwa  hata wananchi wasio na uwezo  wanafikiwa na huduma ya maji kwa njia ya mkopo ambapo tunawaunganishia maji na wanalipia kidogo kidogo hivyo mwananchi hatakuwa na sababu ya kukosa maji na hii ndiyo dhamira ya Serikali yetu;” Alisisitiza  Mhandisi Luhemeja.

Aliongeza kuwa Mamlaka hiyo pia ina miradi yakupeleka maji katika maeneo rasmi ya viwanda katika mkoa wa Pwani ambapo kuna miradi katika Wilaya za Kisarawe, Kibaha,Bagamoyo na Mkuranga ili kuchochea ujenzi wa uchumi wa viwanda.

Akifafanua Mhandisi Luhemeja amesema kuwa tayari  maeneo ya pembezoni yakiwemo Kiwalani, Ukonga, Salasala na Mbagala yameanza kunufaika na mpango wa kuhakikisha kuwa wananchi ambao hawajafikiwa na huduma hiyo wanafikiwa ili waweze kushiriki katika ujenzi wa uchumi na uzalishaji.

Akitolea mafano wa hatua zinazochukuliwa katika  kuimarisha huduma ya maji katika Wilaya ya Kigamboni Mhandisi Luhemeja amesema kisima cha Gezaulole kimeshafungwa pampu na mtandao  wa mabomba utawekwa ili maji yatakayozalishwa yasambazwe katika eneo hilo ikiwa ni hatua mojawapo yakuondokana na changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama

“ Upanuzi wa mfumo wa usambazaji maji kati ya Changanyikeni hadi Bagamoyo kwa ufadhili wa Benki ya Dunia unaendelea kwa kuongeza mtandao wa kusambaza maji ambao  utachangia kuondoa changamoto ya upotevu wa maji “,Alisisitiza Luhemeja.

Akizungumzia suala la watu binafsi kumiliki visima na kuuza maji Luhemeja amesema kuwa Mamalaka yake inachukua hatua madhubuti kuhakikisha kuwa maji hayo ni salama kwa matumizi ya wananchi  na si vinginevyo.

“Maji yanayosambazwa kwa wananchi lazima yakizi vigezo, DAWASA itapima maji hayo na kama hayakidhi vigezo basi visima husika vitafungwa ambapo kwa sasa tutasajili upya visima vyote vya watu binafsi wanaofanya biashara ya kuuza maji;’’Alisisitiza Luhemeja.
Kwa upande wa majitaka Mhandisi  Luhemeja amesema kuwa huduma hiyo inapanuliwa kwa kununua magari 20 ya kunyonya maji taka hali itakayopanua wigo wa huduma hiyo kwa wananchi na pia mifumo 9 ya majitaka imeanza kukarabatiwa ili kuweza kupokea na kutibu majitaka.

 Mamlaka hiyo imebuni mikakati mbalimbali ya kuimarisha utendaji  wake na huduma zake kwanza kwa kuanzisha kituo cha huduma kwa wateja, kuweka mikakati ya makusudi kuhakikisha kuwa wananchi wa pembezoni wanafikiwa na huduma ya maji, kuimarisha miundombinu, kuzuia uvujaaji wa maji, kuongeza mapato na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kutunza maji kupitia katika Kampeni maalum itakayoendeshwa katika shule za mikoa ya Dar es Salaam na Pwani ili kujenga utamaduni wa kulinda na kutunza maji na miundombinu.

DAWASA imekuwa ikiimarisha utendaji wake ili kuendana na azma ya Serikali kuhakikisha kuwa wananchi wanafikiwa na huduma ya maji safi na salama katika maeneo yao na kwa wakati.

Wasichana 600 kunufaika na kampeni ya kujiweka salama wakati wa hedhi ya taasisi ya Her Africa

0
0
Katika dhamira yake ya kuhakikisha Watoto wa kike wanapata elimu kuhusu umuhimu wa usafi katika kipindi vya hedhi, taasisi ya Her Africa imezindua kampeni ya kitaifa inayojulikana kama “Hedhi yangu, Furaha yangu” katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike ambayo huadhimishwa tarehe 11, Oktoba kila mwaka kama ilivyopangwa na Umoja wa Mataifa (UN).

Kupitia kampeni hii mifuko maalum itatolewa kwa wasichana ambao ndani yake kukiwa na mahitaji muhimu katika kipindi cha hedhi kama vile, paketi za pedi za kutumia mara moja na za kutumia zaidi ya mara moja, vitambaa laini vya kujisafishia, chupi na khanga mpya, sabuni ya kuogea pamoja na ya kufulia na dawa ya Dettol. 

Vifaa vinavyopatikana katika kifurushi hiki vimetolewa na wadau mbalimbali katika jamii kama msaada kutokana na jitihada kubwa zilizofanywa kupitia mitandao ya kijamii na taasisi ya Her Africa kufanya  uhamasishaji wa kulielezea tatizo na kutafuta kuungwa mkono kulipatia ufumbuzi.

Meneja Miradi wa Her Africa, Salha Kibwana amesema “Wanawake wengi na wasichana katika jamii zetu hupata changamoto kubwa katika kipindi cha mzunguko wao wa mwezi wa siku za hedhi, kutokana na kutoweza kumudu kununua pedi za kutumia, ukosefu wa elimu kuhusiana na hali hiyo, imani za mila ambazo zinawafanya wengi kuamini kuwa suala la hedhi halipaswi kuongelewa, ukosefu wa mazingira rafiki ya kujihifadhi mtu anapokuwa kwenye hali hiyo kama vile vyoo na maji safi ya kutumia. Changamoto hizo zote zinasababisha watumie vifaa vya kuwasitiri visivyofaa ambavyo vinaweza kuwasababishia kupata maradhi.”

Naye Zena Tenga, kutoka taasisi hiyo ya Her Africa, aliongeza kusema “Kampeni yetu hii imelenga kutoa elimu ya ufahamu kuhusiana na umuhimu wa usafi katika kipindi cha hedhi, kuwezesha kufahamu mzunguko wa siku za hedhi kwa mwezi kwa ajili ya kujiandaa, kujua dalili za kuingia kwenye siku za hedhi na mengineyo mengi.”

Kampeni hii imeungwa mkono kwa kiasi kikubwa na jamii, kampuni ya AIM Group Tanzania ilikuwa mstari wa mbele kuhakikisha inashiriki kukabili changamoto za hedhi kwa kutoa msaada wa pedi 144 na kugharamia mifuko maalum 14 yenye vifaa vya hedhi ambayo ilitolewa kama msaada kwenye kituo cha Watoto yatima cha Hiari.

“Tumejitoa kusaidia kukabili changamoto hii kwa kuwa wanawake wengi na wasichana katika jamii wanapata shida wakati wa kipindi cha mzunguko wa siku zao za hedhi kwa mwezi, kutokana na kutoweza kumudu gharama za vifaa vya kuwasitiri, ukosefu wa elimu hiyo na imani potofu kuwa suala la hedhi ni mwiko kuongelewa hadharani. Wakati umefika sasa wa kuunganisha nguvu na kuunga mkono watu binafsi na taasisi ambazo zimejitoa kupambana kuondoa changamoto hizo.”alisema Ritha Tarimo kutoka kampuni ya AIM Group.
 Moja ya mwanzilishi wa mradi wa " Her Africa" akizungumza na wanafunzi wa kike kutoka shule ya primary St Joseph kuhusu elimu hedhi kabla ya kutoka msaada wa mifuko maalum kwa wasichana hao yenye vitu muhimu vya kutumia wakatika wa kipindi cha hedhi.
Wanafunzi  kutoka shule ya msingi ya St Joseph wakionesha mifuko maalum waliyopokea kutoka kwa "Her Africa" yenye vitu muhimu vya kutumia wakatika wa kipindi cha hedhi. Her Africa imeanzisha kampeni ya "Hedhi yangu, Furaha Yangu" ambayo inatarajia kuwafikishia wasichana 600 mifuko hiyo maalum yenye vifaa vya hedhi.

TADB, YARA kuendelea kuchagiza tija katika uzalishaji wa kilimo

0
0
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imekubaliana na Kampuni YARA Tanzania kuendelea kuchagiza tija katika uzalishaji katika mazao ya kimkakati ya kilimo hapa nchini.

Dhamira hiyo ya kuwasaidia wakulima imewekwa wazi wakati wa kikao cha pamoja kati ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine na Meneja Mkuu wa YARA Tanzania, Bw. William Ngeno kilichofanyika katika Ofisi za YARA jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika kikao hicho, Bw. Justine amesema kuwa Benki ya Kilimo imejidhatiti kuwasaidia wakulima wadogo wadogo nchini kwa kuchagiza uzalishaji ili kuongeza kipato kwa wakulima hao.“Tumedhamiria kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka  kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kuongeza kipato kwa wakulima wadogo nchini,” alisema.

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa YARA Tanzania, Bw. William Ngeno alisema kuwa uhakika wa mbolea bora na viuatilifu vya uhakika ni muhimu katika kuongeza tija na uzalishaji hali itakayochochea kuongeza kipato cha mkulima nchini.Aliongeza kuwa matumizi ya pembejeo bora ni msingi katika mapinduzi ya kilimo kama inavochagizwa na TADB.

“Matumizi bora ya pembejeo yanasaidia kuongeza tija katika kilimo hivyo kuleta uhakika wa mavuno kwa wakulima wadogo wadogo” alisema.
 Meneja Mkuu wa YARA Tanzania, Bw. William Ngeno (kushoto) akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine (kulia) wakati walipokutana kuzungumzia mikakati ya kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo nchini. Wengine pichani ni maofisa kutoka TADB na YARA Tanzania.
 Meneja wa Utafiti wa Udongo wa YARA Tanzania, Bw. Peter Assey (kulia) akitoa maelekezo ya namna wanavyofanya utafiti wa udongo ili kubaini mbolea sahihi kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo hapa nchini. Wanaomsikiliza ni Meneja wa Wakulima Wadogo kutoka TADB, Bw. Joseph Mabula (kushoto), Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine (katikati) na Meneja Mkuu wa YARA Tanzania, Bw. William Ngeno (wapili kulia)
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine na timu yake wakiangalia namna mbolea inavyofungwa tayari kwenda sokoni.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine (kulia) akizungumza wakati wa ukaguzi wa shughuli za uzalishaji wa mbolea unaofanywa na Kampuni ya YARA Tanzania. Pichani ni Meneja Mkuu wa YARA Tanzania, Bw. William Ngeno (kushoto), Meneja wa Wakulima Wadogo kutoka TADB, Bw. Joseph Mabula (wapili kushoto) na Meneja wa Utafiti wa Udongo wa YARA Tanzania, Bw. Peter Assey (kulia).
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine (wa pili kushoto) akisikilza maelezo kuhusu aina ya mbolea zinazozalishwa na Kampuni ya YARA Tanzania. Anayetoa maelezo hayo ni Meneja Mkuu wa YARA Tanzania, Bw. William Ngeno (kushoto). Wengine pichani ni Meneja wa Wakulima Wadogo kutoka TADB, Bw. Joseph Mabula (wapili kulia) na Meneja wa Utafiti wa Udongo wa YARA Tanzania, Bw. Peter Assey (kulia).

Airtel Tanzania yatoa msaada kwa kituo cha yatima Morogoro

0
0
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kupitia kitengo chake cha huduma kwa wateja imetoa msaada wa vitu mbali mbali kwa kituo cha yatima cha Mgolole Orphanage Center, Morogoro.

Msaada huo ni pamoja na vitanda, neti, magodoro, deep freezer, chupa za chai, hot pot, sukari, sahani, sabuni, nepi, pampers na toy za watoto vyote vikiwa na thamani ya TZS 18 milioni.

Kutoa kwa msaada huo ni muendeleo wa kampuni ya Airtel Tanzania kupitia programu ya Airtel Tunakujali ambapo wafanyakazi wa kampuni hiyo kukubali kutoa sehemu ya mshahara wao ili kusaidi huduma za kijamii na hasa kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

Akiongea mara baada ya kutoa msaada huo kwa kituo hicho cha Mgolole cha Morogoro, Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja Airtel Tanzania Adriana Lyamba alisema muda mrefu wafanya kazi wa Airtel kupitia Airtel tunakujali imekuwa ikitembelea na kusaidia vituo mbali mbali vya yatima ikiwa ni pamoja na kuwapa misaada mbali mbali.

Leo ni siku yenye furaha sana kwetu zote kwani mayatima ni sehemu ya Jamii yetu na ni muhimu kuwapa upendo pamoja na kuwafariji. Hiki ambacho tumekuja kutoa leo hapa  ni kidogo lakini nina uhakika kitagusa mioyo yenu lakini zaidi ni kujua tuko pamoja nanyi na tunawajali sana, alisema Lyamba.

Naomba kutoa pongezi za dhati kwa wafanyakazi wenzangu wa Airtel kwa kukubali kutoa sehemu ya kipato chao na leo tumeweza kufika hapa. Lakini zaidi napongeza uongozi wa kampuni yetu kwa kukubali na kuridhia programu yetu hii hapa ya Airtel Tunakujali ambayo imekuwa ikituleta karibu na Jamii inayotuzunguka, alisema Lyamba.

Tunayo furaha kuweza kuwafikia watoto hawa ambao wako kwenye kituo hiki na dhamira yetu ni kuendelea kugusa maisha ya watoto wanaoishi kwenye mazingira mangumu na kuwafanya wajisikia kuwa sehemu ya familia ya Airtel, aliongeza Lyamba.

Kwa upande wake, Makamu Mama Mkuu wa kituo cha Mgolole Sista Valeria Mnyanzaga alisema ni furaha kwa kampuni kubwa ya Airtel kuguzwa na maisha ya watoto wanaoishi kwenye kituo hiki na hatimaye kuja kutoa msaada na kutuunga mkono.
 Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja Airtel Tanzania Adriana Lyamba (kulia) akikabidhi msaada kwa Makamu Mama Mkuu wa kituo cha yatima cha Mgolole, Morogoro. Airtel Tanzania kupitia mradi wake wa Airtel Tunakujali walitembelea kituo hicho pamoja na kutoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye dhamani ya TZS 18 milioni mwishoni mwa wiki.
 Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja Airtel Tanzania Adriana Lyamba (kulia) akikabidhi msaada wa dogoro kwa Makamu Mama Mkuu wa kituo cha yatima cha Mgolole, Morogoro. Airtel Tanzania kupitia mradi wake wa Airtel Tunakujali walitembelea kituo hicho pamoja na kutoa msaada wa vitu mbali mbali vyenye dhamani ya TZS 18 milioni mwishoni mwa wiki. Kati kati ni Meneja wa Kitengo cha huduma kwa wateja Airtel Tanzania Deogratius Hugo. 

NAIBU WAZIRI-IGENI UTARATIBU WA KILA MTOTO KUWA NA MLEZI WAKE KATIKA VITUO VYA KULELEA WATOTO YATIMA

0
0
NA TIGANYA VINCENT.

VITUO vya kulelea na kutunza watoto yatima na wale walioko kwenye mazingira hatarishi nchini vimetakiwa kuiga utaratibu wa Kituo cha Shirika Masista wa Upendo wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora wa kumwekea kila mtoto mdogo mlezi na mwangalazi wake wa karibu wakati wote ili kuwafanya wasijione wapweke.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Daniel Ndumbaro mara baada ya kutembelea Kituo cha Shirika Masista wa Upendo la Jimbo Kuu Katoliki Tabora kinacholea watoto yatima na wale waliokuwa wakiishi katika mazingira magumu na wazee wasijiweza kwa ajili ya kuwapa sukari, maziwa ya watoto wachanga na ‘pampas’ na kuwakuta wakitumia utaratibu wa kila mtoto kuwa na mlezi wake.

Alisema utaratibu unaotumiwa na Kituo hicho wa kumwakea mtoto mlezi na mwangalizi wake wa karibu ambaye siye Sista ni njia nzuri ya kuwasaidia watoto kutojiona kama yatima kwa kuwa wapweke na kuisi yule ndiye mzazi wake.Aidha Naibu Waziri huyo alilipongeza Shirika hilo kwa malezi na huduma nzuri wanazotoa kwa watoto hao na wazee wasijiweza jambo ambalo limefanya waishi kwa furaha na ushirikiano miongoni mwao.

Alisema kazi inayofanywa na Shirika hilo ni nzuri na kubwa ambayo kimsingi ilikuwa ifanywe na Serikali lakini wao wameamua kwa upendo wao kuwalea na kuwatunza watoto ambao wamepoteza wazazi wao na wazee wasijiweza ambao wametelekezwa na ndugu zao.

Dkt. Ndumbalo aliongeza kuwa Serikali itaendelea kutoa ushirikano kwa kadiri itakavyowezekana kwa Shirika hilo na mengine ambayo yanatunza watoto walioko katika mazingira hatarishi na wazee wasiojiweza ili nao wajione kuwa ni Watanzania sawa na wengine.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Daniel Ndumbaro akisalimia wazee  leomara baada ya kutembelea Kituo cha Shirika Masista wa Upendo la Jimbo Kuu Katoliki Tabora kinacholea watoto yatima na wale waliokuwa wakiishi katika mazingira magumu na wazee wasijiweza  kwa ajili ya kuwapa  sukari, maziwa ya watoto wachanga na ‘pampas’ na kuwakuta wakitumia utaratibu wa kila mtoto kuwa na mlezi wake. 
 Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Daniel Ndumbaro akimsalimia Mzee Lucas Simon(kushoto)  leo mara baada ya kutembelea Kituo cha Shirika Masista wa Upendo la Jimbo Kuu Katoliki Tabora kinacholea watoto yatima na wale waliokuwa wakiishi katika mazingira magumu na wazee wasijiweza  kwa ajili ya kuwapa  sukari, maziwa ya watoto wachanga na ‘pampas’ na kuwakuta wakitumia utaratibu wa kila mtoto kuwa na mlezi wake.
 Kaimu Mama Mkuu wa Shirika la Masista wa Wamisionari wa Upendo wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora Sisita Emmanuella MC (kushoto) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Daniel Ndumbaro(katikati) leo mara baada ya kutembelea Kituo cha Shirika Masista wa Upendo la Jimbo Kuu Katoliki Tabora kinacholea watoto yatima na wale waliokuwa wakiishi katika mazingira magumu na wazee wasijiweza  kwa ajili ya kuwapa  sukari, maziwa ya watoto wachanga na ‘pampas’ na kuwakuta wakitumia utaratibu wa kila mtoto kuwa na mlezi wake.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Daniel Ndumbaro akikabidhi maziwa na sukari kwa Masisita mara baada ya kutembelea Kituo cha Shirika Masista wa Upendo la Jimbo Kuu Katoliki Tabora kinacholea watoto yatima na wale waliokuwa wakiishi katika mazingira magumu na wazee wasijiweza  kwa ajili ya kuwapa  sukari, maziwa ya watoto wachanga na ‘pampas’ leo.

NAIBU WAZIRI HASUNGA AFUNGA TAMASHA LA UTAMADUNI WA MTANZANIA

0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utaliii, Mhe. Japhet  Hasunga akizungumza na  Athumani Issa wakati alipotembelea nyumba ya kabila la Wamwela katika kijiji cha Makumbusho wakati wa   kufunga tamasha  la utamaduni wa mtanzania inayowakilishwa na jamii za mkoa wa Lindi lililofanyika kwa muda wa siku nne katika  kijiji hicho  jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utaliii, Mhe. Japhet  Hasunga akiwasaidia akina Mama wa kabila la Wamwela  kutwanga nafaka  wakati alipotembelea nyumba ya kabila la Wamwela katika kijiji cha Makumbusho wakati wa   kufunga tamasha  la utamaduni wa mtanzania inayowakilishwa na jamii za mkoa wa Lindi lililofanyika kwa muda wa siku nne katika  kijiji hicho  jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Maliasili na Utaliii, Mhe. Japhet  Hasunga akipewa kibuyu chenye  pombe na Halima Abdallah ambacho kimekuwa kikitumiwa na kabila hilo kunywea pombe  wakati alipotembelea nyumba ya kabila la Wamwela katika kijiji cha Makumbusho wakati wa   kufunga tamasha  la utamaduni wa mtanzania inayowakilishwa na jamii za mkoa wa Lindi lililofanyika kwa muda wa siku nne katika  kijiji hicho  jijini Dar es Salaam 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utaliii, Mhe. Japhet  Hasunga akiangalia baadhi ya mabaki ya samaki aina ya nguva aliyekutwa amekufa kando kando mwa bahari ya Hindi mkoani Lindi wakati alipotembelea mabanda  kabla ya   kufunga tamasha  la utamaduni wa mtanzania inayowakilishwa na jamii za mkoa wa Lindi lililofanyika kwa muda wa siku nne katika  kijiji hicho  jijini Dar es Salaam 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utaliii, Mhe. Japhet  Hasunga (katikati) akiwa na Mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi wakiwa wameongozana na   Wakurugenzi pamoja na Wazee wa kabila la Wamwela wakati kutembelea nyumba ya kabila la Mwela katika kijiji cha Makumbusho  kabla ya kufunga tamasha  la utamaduni wa mtanzania inayowakilishwa na jamii za mkoa wa Lindi lililofanyika kwa muda wa siku nne katika  kijiji hicho  jijini Dar es salaam 
Baadhi ya vikundi vya ngoma vikitumbuiza wakati wa  kufunga tamasha  la utamaduni wa mtanzania inayowakilishwa na jamii za mkoa wa Lindi lililofanyika kwa muda wa siku nne katika kijiji cha Makumbusho    jijini Dar es salaam .                              ( PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA)   


TCRA YAENDELEA KUWAKUMBUSHA UMMA KUHUSU MATUMIZI SAHIHI NA SALAMA YA MITANDAO YA KIJAMII

0
0

Italia yaiahidi Afrika Ushirikiano wa kiuchumi

0
0

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Italia na Afrika wameazimia kukuza na kuimarisha Ushirikiano katika nyanja mbalimbali, hususan biashara na uwekezaji kwa ajili ya maendeleo ya kweli barani Afrika.

Mawaziri hao walifikia azimio hilo wakati wa mkutano wa pili wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Italia na Afrika uliofanyika Farnesina, Italia tarehe 25 Oktoba 2018 na kuhudhuriwa na Mawaziri wa zaidi ya nchi 40 akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb). 

Mawaziri hao walikutana kwa madhumuni ya kujadili kwa pamoja changamoto zinazohusu usalama, uhuru, amani, demokrasia na namna wadau wa Italia (wenye viwanda, Wafanyabiashara, wanazuoni na taasisi zisizo za kiserikali) watakavyoweza kushiriki katika kukuza uchumi barani Afrika hasa katika sekta ya uwekezaji na biashara. 

Katika hotuba yake kwenye mkutano huo ambao ulifunguliwa na Rais wa Italia, Mhe. Sergio Mattarella, Mhe Waziri Mahiga alisisitiza suala la amani kuwa ni muhimu kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi barani Afrika. Aidha, alieleza umuhimu wa Jumuiya za Kikanda katika kusuluhisha migogoro mbalimbali inayotokea kwenye Bara la Afrika. Katika hilo, alijulisha jitihada zinazofanywa na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) katika kusuluhisha mgogoro nchini Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Sanjari na mkutano huo, Waziri Mahiga alipata fursa ya kufanya mazungumzo kwa nyakati tofauti na Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia, Mhe Enzo Moavero na Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Ufadhili wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Bw. Gilbert F. Houngbo.

Kwenye mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia, Viongozi hao walikubaliana kuwa, kuandaliwe Hati ya Makubaliano (MoU) kati ya Tanzania na Italia ya kufanya majadiliano ya mara kwa mara yenye lengo ya kukuza ushirikiano katika sekta mbalimbali ikiwemo biashara, uwekezaji, utalii, elimu na utamaduni.

Kuhusu mazungumzo na Rais wa IFAD, wawili hao walikubaliana kuimarisha ushirikiano wa Tanzania na Mfuko huo kwenye maeneo makuu mannne ambayo ni Huduma za kifedha kwa wakulima wadogo, kuwajengea uwezeo vijana ili waweze kufanya kilimo kama sehemu ya ajira, kuboresha sekta ya mifugo pamoja na masuala ya lishe bora. 

Aidha, Rais wa IFAD alimuahidi Mhe Waziri kuwa mfuko huo utaendelea kushirikiana vizuri na serikali ya Tanzania hata kwenye miradi inayoendelea ikiwemo Programu ya Miundombinu ya masoko, uongezaji wa thamani na kuwawezesha wakulima wadogo wa vijijini kifedha (Marketing Infrastructure, Value Addition and Rural Finance-MIVRAF). Madhumuni ya programu hiyo ni kupunguza umasikini na kuharakisha ukuaji wa uchumi vijijini ili kuboresha kipato na usalama wa chakula kwa jamii ya watu wa vijijini.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar Es Salaam, Tanzania
29 Oktoba 2018 


IGP SIRRO AKUTANA NA KIKOSI MAALUM KINACHOPAMBANA NA UHALIFU WILAYANI BIHARAMULO

0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akizungumza na askari wa kikosi maalum cha kupambana na matukio ya uhalifu na wahalifu katika eneo la Midaho wilayani Biharamulo mkoani Kagera leo 29/10/2018 wakati akiwa safarini kuelekea wilaya ya Ngara mkoani humo kwa ziara ya kikazi. Picha na Jeshi la Polisi.
 
Askari wa kikosi maalum kinachopambana na matukio ya uhalifu na wahalifu kama wanavyoonekana Pichani wakitekeleza majukumu yao katika eneo la Midaho wilayani Biharamulo mkoani Kagera leo 29/10/2018. Picha na Jeshi la Polisi.

MGANGA MKUU SINGIDA APEWA WIKI MBILI KUBORESHA AFYA MAKAZI YA WAZEE

0
0
Na ANTHONY ISHENGOMA

Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile amemuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida kuhakikisha wazee wasiojiweza wanaoishi Makao ya Wazee ya Taifa Sukamahela wanapatiwa vyandarua kwa ajili ya kujikinga na Malaria.

Naibu Waziri Ndugulile ametoa agizo hilo alipotembelea makao hayo yaliyoko nje kidogo ya mji mdogo wa Manyoni kujionea hali halisi ya maisha ya Wazee wasiojiweza.

Dkt. Ndugulile ametoa muda wa wiki mbili kwa Mganga Mkuu Mkoa kutekeleza jambo hilo na kutaka mrejesho wa utekelezaji wa agizo hilo.“Hili ni kosa ambalo siwezi kulisamehe tuna vyandarua vingi vya kutosha sioni sababu wazee hawa kulala kwenye vyumba bila vyandarua, nawapa wiki mbili kuhakikisha kila mzee analala kwenye chandarua.,” Aliagiza Dkt.Ndugulile.

Pia Dkt. Ndugulile amewataka watendaji wa Idara ya Afya wa Zahanati ya Sukamahela iliyopo katika eneo la makao ya Wazee hao kuhakikisha wanakuwa na dawa za kutosha hasa zile maalumu kwa ajili magonjwa ya Wazee.Makao ya Wazee Sukamahela pamoja na mambo mengine yanayowakabili na upungufu wa chakula, na wamekili kuchoshwa na ulaji wa aina moja ya mboga hivyo kutoa ombi lao kwa Naibu Waziri kutatua changamoto hiyo.

Naibu Waziri Ndugulile amehaidi kushughulikia suala la ukarabati wa majengo chakavu ya yaliyopo katika Makazi hayo.Kwa nyakati tofauti wazee waishio katika makazi hayo wamelalamikia ukosefu wa umeme katika makazi hayo, dawa za magonjwa ya ukoma na vifaa vidogo vidogo kwa ajili ya usafi na kilimo cha mbogamboga pamoja na miundo mbinu chakavu ya vyoo.Aidha Dkt.Ndugulile amesema serikali inakusudia kufunga baadhi ya vituo na kuvipanga kikanda ili iweze kudumisha huduma kwa wazee wasiojiweza lakini kugeuza makazi yatakayofungwa kuwa nyumba salama kwa ajili kupambana na vitendo vya kikatili.

Naibu Waziri Ndugulile yupo mkoani Singida kufuatilia utekelezaji wa masuala ya Afya, Ustawi na Maendeleo ya Jamii.
Naibu Waziri wa Afya ,Maendeleo yaJamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na Wazee waishio Makao ya Wazee Sukumahela Wilayani Manyoni wakati wa ziara take inayoendelea Mkoani Singida.
Naibu Waziri wa Afya ,Maendeleo yaJamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua Jiko kinapoandaliwa chakula cha Wazee waishio Makao ya Wazee Sukumahela Wilayani Manyoni wakati wa ziara take inayoendelea Mkoani Singida

SACOSS NCHINI ZAASWA KUENDELEA KUTOA ELIMU YA USHIRIKA KWA WANACHAMA

0
0

Mwenyekiti wa Bodi ya Magereza SACCOS, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Mbaraka Semwanza akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kufungua rasmi Mkutano Mkuu wa sita wa Mwaka wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara ulifanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma.
Meza Kuu wakifuatilia ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa sita wa Mwaka wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara.
Mjumbe wa Mkutano Mkuu akitoa hoja ya kuthibitisha notisi kabla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa sita wa Mwaka wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara.
Mlezi wa Magereza Saccoss ambaye ni Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akitoa neno kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi Kaimu Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini, Bw. Philemon Chilewa.
Kaimu Mrajis wa Vyama vya Ushirika Nchini Bw. Philemon Chilewa akitoa hotuba ya ufunguzi kwa niaba ya Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini kwenye Mkutano Mkuu wa sita wa Mwaka wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa sita wa Mwaka wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara wakisikiliza hotuba ya Mgeni rasmi kama inavyoonekana katika picha.
Mlezi wa Magereza Saccoss ambaye ni Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akiagana na Mgeni rasmi Kaimu Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini, Bw. Philemon Chilewa baada ya ufunguzi wa Mkutano huo.
Kaimu Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini, Bw. Philemon Chilewa(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara(waliosimama). Walioketi(wa tano toka kulia) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(wa tatu toka kulia) ni Mwenyekiti wa Bodi ya Magereza Saccos, SACP. Mbaraka Semwanza(wa tatu toka kushoto) ni Kamishna wa Fedha na Utawala, Gaston Sanga mara baada ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Tano unaofanyika kwa siku moja Mkoani Dodoma.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike ambaye pia ni Mlezi wa Magereza SACCOS nchini akisalimiana na Wajumbe mbalimbali ambao ni Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza alipowasili kwenye Ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma tayari kwa Mkutano Mkuu wa sita wa Mwaka wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara. Mkutano huo unafanyika kwa siku mbili kuanzia leo Oktoba 29 – 30, 2018 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Magereza SACCOS, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Mbaraka Semwanza(kulia) akimuongoza Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(katikati) ambaye pia ni Mlezi wa Magereza SACCOS kuingia ukumbini tayari kwa Mkutano Mkuu wa sita wa Mwaka wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara(kushoto) ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi la Magereza, Gaston Sanga. Picha zote na Jeshi la Magereza





Na Lucas Mboje, Dodoma

VYAMA vya ushirika nchini vimetakiwa kuendelea kutoa elimu ya ushirika mara kwa mara kwa wanachama wake ili kujenga uelewa wakutosha kuhusu sheria, kanuni na masharti mbalimbali ya ushirika.

Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa sita wa mwaka wa Chama cha Ushirikia wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza nchini, Kaimu Mrajisi wa Vyama vya Ushirika nchini, Bw. Philemon Chilewa ametoa rai hiyo kwa vyama vya ushirika nchini kuendelea kutoa elimu ya ushirika kwani ni muhimu katika uendeshaji wa shughuli za chama.

Amesema kuwa elimu ya ushirika isitolewe tu kwa watendaji na viongozi wa chama bali itolewe kwa wanachama wa ushirika ili wajue uendeshaji wake na kunufaika na huduma zitolewazo na chama. “Vyama vingi vya ushirika hapa nchini vimekufa kwa kukosa elimu ya ushirika, niwaombe sana wasimamizi wa ushirika muendelee kutoa elimu kwa wanachama”. Amesisitiza Kaimu Mrajis Chilewa.

Aidha, Kaimu Mrajis Chilewa amewaasa Magereza SACCOS pamoja na Saccos zote nchini kufanya shughuli zake kwa kufuata sheria ya ushirika pamoja na kuheshimu na kusikiliza maoni ya wanachama kwani wao ndo wenye mali.

Ameongeza kuwa kwakuwa Mkutano huo utahusisha uchaguzi wa mjumbe mmoja wa Bodi, Bw. Philemon Chilewa pia amewaasa wajumbe wa Mkutano huo kuwa makini katika uchaguzi huo kwa kuchagua mtu mwenye weledi na mwenye mapenzi ya dhati na ushiriki wao ili aweze kutimiza majukumu yanayokusudiwa.

Awali, akimkaribisha Mgeni rasmi katika Mkutano huo, Mlezi wa Magereza Saccos, ambaye ni Kamishna Jenerali wa Magereza nchini – CGP Phaustine Kasike amesema kuwa idadi ya wanachama imeongezeka hadi kufikia wanachama zaidi ya 13,000 ikiwa na mtaji wa zaidi ya bilioni 20 hivi sasa.

Pia, Mlezi wa Magereza Saccos, CGP Kasike ameongeza kuwa pamoja na changamoto za mabadiliko ya kiuchumi, kumekuwa na ushindani mkubwa wa Taasisi za kifedha katika kutoa huduma za mikopo kwa wanachama.

Chama cha Ushirikia wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza nchini kilianzishwa mwaka 2005 kwa lengo la kupunguza umasikini na kuinua hali ya maisha ya watanzania hususani watumishi wa Jeshi la Magereza.

Mwakyembe Aagiza Wamiliki na Wahariri wa gazeti la Tanzanite Kujieleza

0
0
Na mwandishi wetu, Dodoma.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (Mb), amesema habari iliyochapishwa na gazeti la kila siku la Tanzanite la leo Jumatatu tarehe 29 Oktoba, 2018 lenye habari zenye tuhuma za kisiasa dhidi ya Viongozi kadhaa, haziakisi msimamo wa Serikali na ameagiza mmiliki na Bodi ya uhariri ya gazeti hilo waitwe mara moja Idara ya Habari (MAELEZO) kujieleza kuhusu msingi wa habari hiyo.

Dkt. Mwakyembe ametoa ufafanuzi huo leo mchana, mara baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuelezea kushtushwa kwake na mwenendo wa gazeti hilo kuchapisha habari zinazoibua tuhuma za kisiasa dhidi ya baadhi ya Viongozi nchini, wakiwemo Wabunge na kusababisha taharuki kubwa katika jamii.

Gazeti la Tanzanite linatolewa na kampuni ya CZ Information and Media Consultant LTD ya Dar es Salaam na leo katika toleo lake Na. 254 limeandika katika ukurasa wake wa mbele  habari yenye kichwa kinachosomeka “Vigogo 14 hatari kwa nchi watajwa” ambayo inawataja viongozi kadhaa wa kisiasa na wafanyabiashara.

MTANZANIA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 23 NCHINI UINGEREZA KWA KUMUUA MKEWE

0
0

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

MTANZANIA Kema Salumu (39) amehukumiwa kifungo cha miaka 23 baada ya kukutwa na hatia ya kumuua mkewe Leyla Mtumwa (35) wakiwa nyumbani kwao huko Haringey Uingereza mapema April mwaka huu.

Mahakama imeeleza kuwa chanzo cha tukio hilo ni Salumu kuwa na wivu wa kimapenzi kwa mkewe mara baada ya kutoka na rafiki zake usiku.

Imeelezwa kuwa mapema Machi 30 Salumu aliandaa mpango kabla ya kwenda jikoni na kuchukua kisu na kumjeruhi Leyla kwa kumchoma kisu mara 49 katika maeneo ya kichwa, shingo, mwili na mikono huku kijana wao wa miaka 12 akishuhudia na kupiga kelele akimzuia baba yake.

Aidha imeelezwa kuwa awali alikana kufanya mauaji hayo kwa kusema kuwa alikuwa anajilinda na baadaye Septemba akakiri kufanya mauaji hayo.

Salum Kema amekuwa akiishi Uingereza kwa miezi sita tangu waoane na Leyla  na baadaye kumuua papo hapo kwa kisu.

FID Q NA JUX WAACHA VIBE LA TIGO FIESTA MUSOMA

0
0
Wasanii Fid Q na Jux usiku wa kuamkia jana waliacha alama ya Vibe la Tigo Fiesta  kwenye uwanja wa Karume mjini Musoma.

Wasanii hao kwa wakati tofauti wakiwa kwenye steji waliweza kuteka hisia za mashabiki waliofurika uwanjani hapo. Msanii Fid Q ndiye aliyefungua pazia la Tigo Fiesta mjini Musoma mkoani Mara, Kwa mkoa huo wasanii wanaopendwa zaidi ni wa mtindo wa kufokafoka (Hip Hop) ndipo Fid Q alipopewa jukumu la kuanza na kuamsha shangwe kubwa na hasa alipomaliza kwa wimbo wake ujulikanao kama FRESH.
 
Nae Juma Jux ambaye ni "Fundi" wa nyimbo Laini aliweza kuwaimbisha mashabiki mwanzo hadi mwisho aliposhuka kwenye jukwaa hilo kwa nyimbo zake JUU, ZAIDI na UTANIUWA na nyingine nyingi kwa kweli huyu ndio msanii aliyeweza kuimba na mashabiki kwa pamoja.

Tamasha hilo linatarajiwa kuendelea mjini Muleba ijumaa hii kwenye uwanja wa Zimbihire.


 Msanii Fareed Kubanda maarufu kama Fid Q akiwa kwenye jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote lililofanyika uwanja wa Karume mjini Musoma usiku wa kuamkia jumatatu.








MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AITAKA WCF KUENDELEA KUWABANA WAAJIRI KUJISAJILI

0
0

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MAKAMU wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameuagiza uongozi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), kuendelea kuwafuatilia waajiri ambao bado hawajajisajili ili waweze kufanya hivyo.
Makamu wa Rais alitoa wito huo leo Oktoba 29, 2018 alipotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonesho ya viwanda Mkoa wa Pwani kwenye viwanja vya CCM-Sabasaba, Picha ya Ndege Mkoani humo.
Alisema viwanda vimeongezeka nchini na kwamba huduma za WCF zitahitajika sana kwa wakati huu na hivyo kuutaka uongozi wa Mfuko, kuhakikisha unaendelea na ufuatiliaji kwa waajiri wa zamani na wapya ambao bado hawajajisajili na kuwasilisha michango kwenye Mfuko watekeleze takwa hilo la kisheria ili mfanyakazi anapoumia aweze kupata haki yake ya fidia.
“Waajiri wao muwabane wajisajili na mfuko na waweze kuwasilisha michango ili Mfuko uendelee kuwa na uwezo wa kulipa fidia, pale watoto wetu (wafanyakazi) wanapokatika vidole au kuumia waweze kupata haki zao.” Alisisitiza.
Katika hatua ya kuimarisha Hifadhi ya Jamii, Tanzania, Serikali ilianzisha Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi kwa mujibu wa kifungu namba 5 cha sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi, kipengele cha 263 kilichofanyiwa marejeo mwaka 2015 ili kuhakikisha kila mfanyakazi Tanzania Bara kutoka sekta ya umma na binafsi anapata fursa ya kuwekewa bima na mwajiri wake ili anapopata majeraha au magonjwa awapo kazini basi aweze kufidiwa kwa mujibu wa sheria.
Katika hatua nyingine, WCF imekuwa miongoni mwa taasisi zilizotunukiwa vyeti vya shukrani kwa kuwezesha maonesho hayo kufanyika. 
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi unashiriki maonesho hayo ya kwanza ya viwanda kufanyika Mkoani Pwani ambapo waajiri, wafanyakazi na wananchi wamekuwa wakipita kwenye banda la Mfuko huo kupata elimu kuhusu shughuli za Mfuko.
 Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi cheti cha shukrani Mkurugezni Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw.Masha Mshomba kutokana na Mfuko huo kuwa miongoni mwa taasisi zilizowezesha kufanyika kwa maonesho ya kwanza ya viwanda Kibaha kwenye viwanja vya Sabasaba-Picha ya Ndege Mkoani Pwani, Oktoba 29, 2018.  
 Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo.
 Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, alipotembelea banda la Mfuko huo.
Bw. Mshomba (wapili kushoto), akimsikilizia kwa makini Mwenyekiti Mtendaji wa IPP., Dkt. Reginald Mengi, mmoja wa waajiri wakubwa hapa nchini, wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya makampuni mbalimbali (waajiri), kwenye maonesho ya viwanda Kibaha kwenye viwanja vya Sabasaba, Picha ya Ndege Oktoba 29, 2018.
Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipeana mkono na Mkurugenzi wa Huduma za Fedha na Uwekezaji, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw.Bezil Ewala, alipotembelea banda la Mfuko huo. Wapili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Mshomba.
 Wananchi wakipatiwa maelezo na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa WCF, Bw. Sebera Fulgence walipofika kwenye banda la Mfuko huo.
 Mgeni rasmi katika picha ya pamoja na wawezeshaji wa maonesho hayo.
Kikundi cha ngoma cha JKT

MAGAZETI YA LEO JUMANNE OKTOBA 30,2018

0
0
















TTGA WATAMBUA MCHANGO WA WAONGOZA WATALII WALIOOKOA MTOTO WA FARU

0
0

Mwenyekiti wa Chama cha Waongoza Utalii Nchini (TTGA) Khalifa Msangi. Picha na Vero Ignatus
Edward Mfaume miongoni ya waliookoa mtoto Faru juzi asiuwawe na simba. Anafanya kampuni ya Kiboslope, akipokea cheti kutoka kwa Mwenuekiti wa Bodi ya TTGA Christopher Nzela. Picha na Vero Ignatus
Juma Rajabu Sumbi ni miongoni mwa wale waliookoa mtoto wa Faru mwaka jana Moru,Ni Freelencer kwa sasa anawafanya nyingi za Tawisa. simba. Anafanya kampuni ya Kiboslope, akipokea cheti kutoka kwa Mwenuekiti wa Bodi ya TTGA Christopher Nzela. Picha na Vero Ignatus
Wakwanza kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Waongoza Utalii Nchini (TTGA) Khalifa Msangi. Haji Mbuguni Mjumbe wa kamati ya Mazingira Na mahusiano (TTGA) pamoja na Juma Rajabu Sumbi ni miongoni mwa wale waliookoa mtoto wa Faru mwaka jana 2017.Picha na Vero Ignatus
Pichani anaonekana Simba akimshambulia mtoto wa Faru,juzi ngorongoro, guides waliweza kumuokoa, TTGA wametambua mchango wao mkubwa wamefanya matukio yote mawili kuwapongeza guides na kuwapa vyeti. Picha kwa hisani ya TTGA.


Pichani anaonekana mtoto wa Faru aliyekuwa amezama kwenye matope serengeti Moru mwaka jana 2017 akaokolewa baada ya kuonwa na guides, wakawaita Rengers. Picha kwa hisani ya TTGA



Na. Vero Ignatus Arusha





Chama cha Waongoza Watalii Tanzania(TTGA) kimetoa vyeti kwa Madereva 12 waongoza watalii waliofanikiwa kumuokoa mtoto wa Faru asiuwawe na Simba katika Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa Ngoro ngoro na Hifadhi ya Taifa Serengeti.
 
Akizungumza katika hafla hiyo mwenyekiti wa TTGA Khalifa Msangi amesema kuwa waongoza watalii wa Tanzania wapo vizuri sana kwa kuwa ndio sekta inayoongoza katika kuingiza fedha za kigeni hapa nchini na kuchangia pato la Taifa (GDP).

Msangi amesema Waongoza watalii wana mchango mkubwa wa kuiletea taifa maendeleo kwa kuwa wakifanya kazi kwa Uzalendo,na kujituma basi ni wazi kuwa wanapelekea Idadi ya watalii nchini.

Aidha amesema Chama hicho kimeamua kuwapa Vyeti kama Ishara ya kutambua mchango uliofanywa na Madereva hao kwa kutambua kuwa mnyama faru ni mnyama Adimu na yupo mbioni kutoweka duniani.

“Kwanza tuwapongeze Madereva hawa kwa kazi kubwa ya Kizalendo walioifanya na madereva hawa wanastahili pongezi kwanza kwa kuhataraisha maisha yao na Wageni, ili tu kuweza kuokoa mtoto huyo wa faru ambaye mama yake alishamua kukimbia kutokana na kundi la samba,wamesfanya jambo la kizalendo sana”alisema Msangi.

Msangi amesema Madereva sita waliweza kumnusuru mtoto wa faru katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngoro ngoro na namna bora ya kuwaongezea madereva wengine sita mnamo mwaka 2017 waliweza kumnusuru mtoto wa faru ambaye pia alititi katika tope katika hifadhi ya taifa ya Serengeti.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya TTGA Christopher Nzela amewataka Waongoza watalii nchini watambue kuwa wao ni Mabalozi wa nchi na waendelee kuuza nchi vizuri kwa kuwa kwa kufanya hizo wataweza kusaidia Juhudi za kuongeza Idadi ya watalii nchi kama Serikali inavyotamka kila siku.

Kwa Upande wao baadhi ya madereva waliotunikiwa Vyeti akiwemo Edward Mfaume na Juma Sumbi wameiomba serikali kupitia Mamlaka za Hifadhi zilizopo nchini kutambua kuwa wao sio Maadui zao bali ni wafanyakazi wenzao hivyo kuomba ushirikiano wa dhati kwa kuwa rasilimali zilizopo zipo kwa Ajili ya kunufaisha Taifa.

Hata hivyo wameongeza kuwa Madereva wa Utalii wamekuwa wakifika kila mahali tofauti na Wafanyakazi wa hifadhi kwa kuwa wapo wachache na Waongoza watalii kuwa wengi hivyo kufika kila mahali ndio maana matukio hayo huwakuta Waongoza watalii na sio Askari wa Wanyamapori (Rangers).

HATUWEZI KUENDELEA KUAGIZA SUKARI WAKATI TUNA UWEZO WA KUFANIKISHA UZALISHAJI-DKT TIZEBA

0
0
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa Bodi ya Sukari Tanzania (SBT) hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Mjini Dodoma, jumatatu tarehe 29 Octoba 2018.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa Bodi ya Sukari Tanzania (SBT) hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Mjini Dodoma, jumatatu tarehe 29 Octoba 2018.

Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akimkabidhi muongozo wa utendaji kazi Mwenyekiti wa Bodi ya sukari Tanzania Bi Mwamini Juma Malemi kwenye uzinduzi wa Bodi ya Sukari Tanzania (SBT) hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Mjini Dodoma, jumatatu tarehe 29 Octoba 2018.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania Prof Kenneth Michael Kitundu Bengesi akizungumza kwenye uzinduzi wa Bodi ya Sukari Tanzania (SBT) hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Mjini Dodoma, jumatatu tarehe 29 Octoba 2018.


Na Mathias Canal-WK, Dodoma


Serikali imeipa changamoto Bodi ya sukari nchini kutekeleza majukumu yake kwa weledi ikiwa ni pamoja na kusisitiza kuhuisha uzalishaji wa sukari kwa wingi ili kuondokana na uagizaji wa sukari kutoka nje ya nchi.

KaMpuni mbalimbali za uzalishaji wa sukari nchini zimeitikia wito wa Serikali wa kuongeza uzalishaji wa sukari ili nchi iweze kujitegemea kwa bidhaa hiyo pendwa kwa matumizi ya nyumbani na viwandani na ziada jambo litalopelekea Bodi ya sukari kusimamia majukumu yake ipasavyo ili kuondokana na uagizaji wa sukari nje ya nchi.

Kauli hiyo imetolewa leo jumatatu tarehe 29 Octoba 2018 na Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa Bodi ya Sukari Tanzania (SBT) hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Mjini Dodoma.

Waziri Tizeba amemtaka Mwenyekiti wa Bodi ya Sukari nchini Bi Mwamini Juma Malemi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania Prof Kenneth Michael Kitundu Bengesi Kudhibiti sukari inayoingia nchini pasina utaratibu huku akiwataka kusimamia kwa weledi ufanisi katika uongezaji wa uzalishaji wa sukari nchini.

Aidha, Dkt Tizeba alisema kuwa ufungashaji wa sukari kwenye ujazo wowote ule kwa kutumia vifungashio vya aina yoyote kama vile mifuko yenye nembo ya SUPER FINE lazima uzingatie Sheria ya Sukari Namba 26 ya Mwaka 2001 ambayo inazuia ufungashaji wa sukari bila kupata idhini ya Bodi ya Sukari Tanzania.Alisema kuwa kwa mujibu wa Sheria hiyo ni marufuku kufungasha au kuuza sukari nyeupe kwa kuwa sukari hiyo ni kwa ajili ya matumizi ya viwandani kama malighafi na sio kwa ajili ya matumizi ya kawaida majumbani.

Alisisitiza kuwa Mtu yeyote atakayebainika kuvunja Sheria hiyo ya Sukari, atawajibika kulipa faini ya kiasi cha fedha kisichopungua Shilingi Milioni Kumi (10,000,000) au kifungo cha miaka mitatu (3) jela au vyote kwa pamoja.“Kuna watu wanaolipa kodi ili wazalishe sukari lakini inapoingia sukari ambayo imepenya kinyemela hata ulinganifu wa soko madukani unakuwa mdogo kwa kuwa wanaoingiza bila utaratibu wanauza kwa kiasi cha chini kwa kuwa hawana uchungu wa kulipa kodi”

“Na hili sio jambo la hiara Bodi ni lazima isimame kidete kubaini mianya yote ya wafanyabiashara wanaoingiza sukari bila utaratibu” Alikaririwa Dkt Tizeba.Kuhusu sukari ya viwandani (Industial Sugar) Dkt Tizeba alisema kuwa, wafanyabiashara wamekuwa wakiomba kiwango kikubwa cha kibali cha uagizaji wa sukari lakini serikali ikihakiki kupitia kodi waliyolipa inakuwa haifanani na kiasi kilichoagizwa.

Viewing all 46206 articles
Browse latest View live




Latest Images