Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

MHAGAMA AAGIZA NEEC KUFANYA TATHIMINI YA UHALISIA WA WANUFAIKA WA MIKOPO INAYOTOLEWA NA TAASISI ZA KIFEDHA

$
0
0
Na EmanuelMadafa,MichuziBlog,Mbeya 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri mkuu anayeshughulikia Sera,Bunge, Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama ameliagiza Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kufanya tathamini ya wananchi walionufaika na mikopo iliyotolewa kwenye Taasisi za kifedha ili kubaini idadi halisi ya wananchi hao.

Ametoa kauli hiyo hii leo (Oktoba 20, 2018) wakati akifungua maonesho ya Mifuko ya Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya kijamii yaliyofanyika katika viwanja vya Nzovwe Mbeya ambapo yalijumuisha wajasiliamali kutoka Wilaya 15 za Mikoa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.Amesema Lengo la kufanya tathimini hiyo ni kupata uhalisia wa wanufaika wa mikopo hiyo ili kuenenda sambamba na azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ambayo imekusudia kuifanya Tanzania kuwa Nchi ya viwanda na uchumi wa kati ifikapo Mwaka 2025.

Aliongezea kuwa, tathimini hiyo itasaidia kuondoa malalamiko kutoka kwa wananchi dhidi ya Serikali yao hususani wenye mtizamo hasi kuwa serikali haijafanya jambo lolote kuwawezesha kiuchumi.“Tathimini hii itasaidia kuwa na utaratibu mzuri wa kutunza takwimu sahihi zinazoonesha uhalisia wa wanufaika pia italeta chachu kwa kuhakikisha maonesho haya yanafanyika kwa mzunguko na kutoa fursa kwa wananchi wengi hasa maeneo ya vijijini kufahamu mifuko na programu za uwezeshaji nchini”.Alisitiza Mhagama

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Beng’i Issa aeleza kuwa ofisi yake itaendela kutekeleza kwa vitendo eneo la uwezeshaji wananchi kiuchumi na kuyachukua maagizo ya waziri ili kuhakikisha malengo yaliyoainishwa yanafikiwa.Naye Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe.Albert Chalamila alipongeza juhudi zinazofanywa na Ofisi ya Waziri Mkuu kuhakikisha wananchi wote wanawezeshwa kiuchumi na kujikwamua katika hali za umasikini na kuahidi kuendelea kuunga mkono juhudi hizo.

“Lazima tuendelee kuunga mkono jitihada za Ofisi ya Waziri Mkuu kwa vitendo na kuhakikisha changamoyo ya ajira kwa vijana inakomeshwa na kuwa na Taifa lenye maendeleo na wananchi wake”.Alisema Chalamila.Aidha, kaulimbiu ya maonesho ya Mwaka huu inasema “Vikundi vya Kifedha, Programu na Mifuko ya Uwezeshaji ni Chachu ya Maendeleo ya Viwanda”.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akisalimia wananchi walioshiriki katika maonesho ya Mifuko ya Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya kijamii (hawapo pichani) yaliyofanyika Oktoba 20, 2018. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akikata utepe wakati wa uzinduzi wa Programu ya malengo endelevu ya kuongeza ajira kwa vijana uliozinduliwa wakti wa maonesho hayo. 
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Beng’i Issa akihutubia wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Mifuko ya Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya kijamii yaliyofanyika katika viwanja vya Nzovwe Mbeya Oktoba 20, 2018
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akipokea maelezo ya nyaraka zilizoandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kutoka kwa Mkurugenzi wa mifuko ya Uwezeshaji (NEEC), Bw.Edwin Chrisant wakati wa maonesho ya Mifuko ya Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya kijamii yaliyofanyika katika viwanja vya Nzovwe Mbeya Oktoba 20, 2018 
Baadhi ya wananchi wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa maonesho hayo. 


“SERIKALI KUCHUKUA HATUA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZINAZOVIKABILI VYAMA VYA USHIRIKA WA AKIBA NA MIKOPO” -DKT TIZEBA

$
0
0
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akisisitiza umuhimu wa SACCOS nchini wakati akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Saccos Duniani hafla iliyofanyika katika viwanja vya kichangani Mkoani Iringa tarehe 18 Septemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, WK)
Sehemu ya wanachama wa vikundi vya akiba na mikopo wakifatilia hotuba ya Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) wakati akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Saccos Duniani hafla iliyofanyika katika viwanja vya kichangani Mkoani Iringa tarehe 18 Septemba 2018.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akisalimiana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Willium Vangimembe Lukuvi (Mb) mara baada ya kuwasili kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Saccos Duniani hafla iliyofanyika katika viwanja vya kichangani Mkoani Iringa tarehe 18 Septemba 2018.



Na Mathias Canal, WK-Iringa

Serikali kupitia Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania imeendelea kuchukua hatua stahiki katika kukabiliana na changamoto zinazovikabili vyama vya ushirika wa Akiba na Mikopo kwa ajili ya kuhakikisha kwamba vinaleta tija kwa jamii.

Hatua zilizochukuliwa na serikali ni pamoja na kuchukua hatua za kiutawala na kidola kwa baadhi ya viongozi na watendaji wa vyama vya ushirika wa Akiba na Mikopo waliojihusisha na wizi na ubadhirifu wa fedha katika vyama hivi, mfano; Alayabe SACCOS cha Karatu Mkoani Arusha, Mbinga Teachers SACCOS Mkoani Ruvuma na Ulanga Teachers SACCOS Mkoani Morogoro ambako baadhi ya viongozi na watendaji wamefikishwa mahakamani kwa vitendo vya ubadhirifu.

Vilevile, Kutengeneza mikakati ya kuhakikisha kwamba vyama vya ushirika wa Akiba na Mikopo haviendelei kutengeneza madeni yasiyokuwa na tija kwa jamii na kusaidia kuweka mikakati ya kupunguza madeni ambayo tayari yapo katika vyama vyetu vya ushirika wa Akiba na Mikopo.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Saccos Duniani iliyofanyika katika viwanja vya kichangani Mkoani Iringa tarehe 18 Septemba 2018.

Waziri Tizeba alisema kuwa serikali imeanza kufanya mawasiliano ya mara kwa mara na waajiri kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali kwa ajili ya kuwahimiza waone umuhimu wa kuwasilisha kwa wakati makato wanayokata kutoka katika mishahara ya watumishi waliokopa katika SACCOS ili fedha hizo ziweze kutumika kwa shughuli za maendeleo zilizokusudiwa.

Alisema pia, serikali itaendelea kuendesha mafunzo mbalimbali kwa viongozi, watendaji na wanachama wa vyama vya ushirika vya Akiba na Mikopo ili waweze kufahamu miongozo na taratibu mbalimbali za utendaji wa vyama hivi ili hatimaye viweze kuleta tija iliyokusudiwa kwa jamii inayozunguka.

Katika utafiti uliofanyika katika siku za hivi karibuni umebaini kwamba Tanzania ina jumla ya vyama vya ushirika vya Akiba na Mikopo 5640 kati ya vyama 55000 sawa na asilimia 10.3 ya vyama vya ushirika wa Akiba na Mikopo Duniani. Kwa mujibu wa utafiti huo, Tanzania ina jumla ya wanachama wapatao milioni moja na laki nane kwa SACCOS zote nchini kati ya wanachama milioni miambili (200) ya wanachama wote wa SACCOS sawa na asilimia 0.9 ya wanachama wa SACCOS zote Duniani. 

Dkt Tizeba alisisitiza kuwa Licha ya uchache wa wanachama wake ukilinganisha na idadi ya wanachama Duniani, SACCOS hapa nchini Tanzania zimeendelea kuwa msaada na mkombozi mkubwa katika kuondoa umasikini wa wanachama wa vyama hivi na jamii kwa ujumla wake.

Aidha, alisema Sekta ya ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) imeendelea kupanuka katika nchini kufuatia kuanzishwa kwa SACCOS nyingi katika maeneo ya mijini na vijijini hali ambayo imechangia kuongeza huduma ya kifedha kwa wananchi wa kawaida na hivyo kuleta tija kwa jamii.

Sambamba na hayo, alieleza kuwa uwepo wa maendeleo ya ushirika wa Akiba na Mikopo nchini umesaidia wanachama wengi kujijengea utamaduni wa kuweka akiba ya fedha mara kwa mara na kuwa na matumizi bora ya fedha wanazoweka akiba. Vyama vya ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) vimechangia kujenga tabia ya kujiamini na kuaminiana kifedha miongoni mwa wananchi wa kawaida na kujenga.

Matukio Katika Picha Tamasha la Wajasiriamali wanawake Jijini Dodoma

$
0
0

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bi. Roida Andusamile akisisitiza kuhusu hatua iliyochukuliwa na Serikali katika kuwawezesha wajasiriamali wadogo kupata alama ya ubora wa bidhaa wanazozalisha ili kuchochea ujenzi wa uchumi wa Viwanda ambapo Serikali inalipa gharama hizo kwa wajasiriamali wadogo, hayo ilikuwa wakati wa Tamasha la Mwanamke Mjasiriamali linalofanyika Jijini Dodoma likishirikisha wajasiriamali wa hapa nchini na kutoka nchini Burundi.
Afisa Udhibiti Ubora wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Kanda ya Kati Bw. Sileja Lushibika akieleza hatua zinazopaswa kufuatwa na mjasirimali ili kupata alama ya ubora kwa mmoja wa wananchi waliofika katika Banda la Shirika hilo wakati wa Tamasha la Mwanamke Mjasiriamali linalofanyika Jijini Dodoma likishirikisha wajasiriamali wa hapa nchini na kutoka nchini Burundi.
Afisa Elimu, Habari na Mawasiliano wa Wakala wa Vipimo (WMA) Bw. Paulus Oluochi akizungumzia umuhimu wa kuzingatia vipimo kwa wajasirimali wakati wa kufungasha na kuzalisha bidhaa mbalimbali ili kuchochea dhana ya ujenzi wa uchumi wa Viwanda,hiyo ilikuwa wakati wa Tamasha la Mwanamke Mjasiriamali linalofanyika Jijini Dodoma likishirikisha wajasiriamali wa hapa nchini na kutoka nchini Burundi.
Afisa Elimu, Habari na Mawasiliano wa Wakala wa Vipimo (WMA)Bw. Paulus Oluochi akisisitiza kuhusu hatua zinazochukuliwa katika kuhakikisha kuwa wajasiriamali wote wanafikiwa na huduma za Wakala huo ili kutekeleza kwa vitendo matwakwa ya sheria ya vipimo na kanuni zake.
Afisa Vipimo wa Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) Bi. Zaidat Gharibu akionesha jinsi wanavyohakiki vipimo mbalimbali ikiwemo upimaji wa gesi yakupikia majumbani.
Sehemu ya mabanda ya wajasiriamali wanaoshiriki Tamasha la Mwanamke Mjasiriamali linalofanyika Jijini Dodoma likishirikisha wajasiriamali wa hapa nchini na kutoka nchini Burundi kama yanavyoonekana katika picha. Picha zote na Frank Mvungi MAELEZO, Dodoma

WAZIRI MKUU AAGIZA MRADI WA UMWAGILIAJI MPWAYUNGU UKAGULIWE

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na wananchi wa kijiji cha Mpwayungu wilayani Chamwino baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara kijijini hapo, Oktoba 20, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Bilinith Mahengeampeleke Afisa Kilimo wa mkoa Bw. Bernad Abraham  akakague mradi wa umwagiliaji wa Mpwayungu wilayani Chamwino ili kubaini waliohusika na ubadhilifu wa sh. bilioni 1.2 za mradi huo.

Alitoa agizo hilo jana jioni (Jumamosi, Oktoba 20, 2018) baada ya mbunge wa jimbo Mtera, Livingstone Lusinde kumuomba awasaidie kuhusu upotevu wa sh. bilioni 1.2 zilizotolewa kwa ajili ya mradi wa umwagiliaji ambazo matumizi yake hayajulikani.

Waziri Mkuu ambaye alikuwa katika ziara ya kikazi wilayani Chamwino, Dodoma alipokea ombi hilo la mbunge wakati akizungumza na wananchi wa Tarafa ya Mpwayungu, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mpwayungu.

Alisema mara baada ya Afisa Kilimo, Bw. Abraham kukamilisha ukaguzi wa mradi huo wa umwagiliaji apelekewe taarifa ili waliohusika na ubadhilifu wa kiasi hicho cha fedha wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alivunja kamati ya kusimamia huduma maji ya kijiji cha Mpwayungu na alimuagiza Mhandisi wa Maji wa wilaya ya Chamwino Bw. Godfrey Mbabaye aunde kamati mpya.

Waziri Mkuu alichua hatua hiyo baada ya kutoridhishwa na utendaji wa kamati hiyo ambayo ilishindwa kutekeleza majukumu yake ikiwemo ujenzi wa vituo vya kuchotea maji licha ya kukusanya sh. milioni 20 kwa mwezi, mradi huo unavituo vinne tu.

Alisema kitendo cha kamati hiyo kushindwa kuongeza kujenga vituo vingine vya kuchotea maji licha ya kukusanya fedha nyingi kwa mwezi kinasababisha malalamiko kutoka kwa wananchi ambao ndio wanufaika wa mradi huo.

Pia Waziri Mkuu alimuagiza mhandisi huyo aombe taarifa ya akaunti ya benki ya mradi huo ili kubaini katika mfuko wa mradi huo una fedha kiasi na ndipo aunde kamati mpya ya maji ambayo anatakiwa ashirikishe wanawake kwa kuwa wao ndio wahusika wakuu.

KUNAMBI ATOA ONYO KWA MTU YOYOTE ATAKAYEBAINIKA KULETA VURUGU NA KUKWAMISHA MPANGO MPYA WA URASIMISHAJI ARDHI

$
0
0
Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Bw.Godwin Kunambi akizungumza kwenye mkutaano wa hadhara na wananchi wa Mtaa wa Ndani na maeneo ya jirani uliokuwa unahusiana na mpango mpya wa urasimishaji ardhi.
Bi.Epifania Komba Afisa Mipango Miji akiwa na orodha ya majina
Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Bw.Godwin Kunambi akisisitiza jambo kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa Mtaa wa Ndani na maeneo ya jirani uliokuwa unahusiana na mpango mpya wa urasimishaji ardhi.
Baadhi ya wananchi wa Mtaa wa Ndani na maeneo ya jirani wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Bw.Godwin Kunambi wakati wa mkutano wa hadhara unaohusiana na mpango mpya wa urasimishaji ardhi.

Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Bw.Godwin Kunambi akimpa orodha Bw.Tahran Hoti ambaye ni mtendaji Mtaa wa Kata ya Mnadani
Bw.Afred Malenge akitoa changamoto za maendeleo ya shule ya Ndani kwa Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Bw.Godwin Kunambi wakati wa mkutano wa hadhara unaohusiana na mpango mpya wa urasimishaji ardhi

…………………..

Na.Alex Sonna,Dodoma

Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma ,Godwin Kunambi ametoa onyo kwa mtu yoyote atakayebainika kuleta vurugu na kukwamisha mpango mpya wa urasimishaji ardhi katika mitaa ya Kata ya Mnadani atachukuliwa hatua kali za kisheria

Bw.Kunambi huyo ametoa kauli alipokuwa kwenye mkutano wa hadhra na wananchi wa mtaa wa Ndani na maeneo ya jirani uliokuwa unahusiana na mpango mpya wa urasimishaji ardhi unaoendelea katika mkoa huo

Hata hivyo Kunambi amesema kuwa baada ya maagizo ya Mkuu wa Mkoa, Dk Binilith Mahenge aliyoyatoa siku za nyuma ya kutaka kuanza kwa mchakato wa kurasimisha ardhi katika maeneo ambayo hayakupimwa na yalikuwa na migogoro ya ardhi.” Wote mnakumbuka tulikuja hapa na mkuu wa mkoa (Dk Binilith Mahenge) na aliagiza kuanza kwa mchakato wa kurasimisha ardhi na kamati ziliundwa, lakini mchakato huu umeonekana kukwama katika mitaa mitatu ya Mbwanga, Mnadani na Ndanchi”alisema Kunambi

Aidha alisema kuwa kutokana na watu wachache ambao wanataka kutumia mpango huu kujinufaisha binafsi na kuibua mivutano isiyo na sababu hivyo ni lazima tuache siasa au kujipatia umaarufu kupitia changamoto za wananchi ”Baada ya mpango mpya kuanza, mtu yeyote atakayevuruga au kukwamisha mchakato huu na kuleta umaarufu kwa kupitia changamoto hizi za wananchi basi mahakamani kutakuwa nyumbani kwake,” alisema Kunambi

Kunambi amewataka wananchi kuhakikisha hawazirudishi kampuni mbili za urasimishaji ardhi zilizoingia kwenye mgororo, sambamba na moja aliyoidai kushindwa kazi katika maeneo mengi, alitoa orodha ya kampuni ambazo zimesajiliwa na serikali. ” Natoa orodha hii itakaa ofisi ya mtendaji mwananchi unahaki ya kutoa nakala, ila hakikisheni zile zilizochangia kukwamisha mchakato wa awali hazipewi kazi, Serikali inataka maeneo yenu yarasimishwe ili tulete miundombinu ya maji, umeme na huduma zingine za kijamii,” alisisitiza Kunambi

Kunambi alitumia nafasi hiyo kuwagiza watendaji wa serikali kuhakikisha wanaitisha mikutano ya wananchi isikapo Jumanne ili wachague kamati mpya ya watu saba kwa kila mtaa ambao ndio watakaosimamia suala hilo, huku akiwataka wananchi kuwa makini katika kuchangua wajumbe.

“Sasa hapa msifanye makosa kwenye kuchagua wajumbe wa kamati, mkiwachangua wala rushwa au madalali wa viwanja wanaweza kukwama tena kama awali, kwani kuna baadhi yalitaka kujipiatia viwanja kupitia ardhi zenu,” Kuhusu fedha walizotoa kwenye mchakato wa awami, Kunambi alisema fedha hizo ziko salama na kuwa zitatumika kwenye mpango mpya na kuonya mtu yeyote asithubitu kuchukua hata senti moja ya fedha hizo. Pia alisisitiza kuwa mwongozi wa gharama za kazi hiyo ni kati ya Sh 200,000-hadi Sh 250,000.

Kunambi alisema kuwa kuna kampuni ilisema ingefanya kazi hiyo kwa Sh 150,000, watu kama hawa wanatoa bei ndogo ili mvutia, lakini mujue watafidia fedha zao kupitia ardhi yenu wenyewe. Hivyo mnatakiwa kuwa kati ya kiwango kilichowekwa. Kwa upande wa baadhi ya wananchi walisema kuwa

mgogoro uliibuka baada ya kutokea kampuni moja ambayo ikitaka kufanya urasimishaji kwa Sh 250,000 na nyingine Sh 150,000 jambo ambalo liliwafanya wananchi kuwa na mashaka kuwa huwenda wanaibiwa

ZIARA YA DKT NDUGULILE KATIKA VIKUNDI VYA WANAWAKE WAJASIRIAMALI MVOMERO MOROGORO

$
0
0




Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongozana na Wananchi wa kijiji cha Wami Luwindo kilichopo Dakawa Wilaya ya Mvomero kukagua mradi wa skimu ya umwagiliaji uanondeshwa na Serikali ya kijiji hicho.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akipokea taarifa ya mradi wa skimu ya umwagiliaji uanondeshwa na serikali ya kijiji cha Wami Luwindo Dakawa Wilayani Mvomero kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya hiyo Bw. Frolence Laurent Kyombo.
Wajasiliamali wadogo kutoka vikundi vya mbalimbali vilivyopo wilayani Mvomero wakitoa maelezo kuhusu bidhaa wanazozalisha kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alipotembelea Wilaya hiyo jana kujionea kazi za vikundi hivyo wakati wa ziara yake ya siku tatu Mkoani humo.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikabidhi milioni moja kwa Mwenyekiti Skimu ya Umwagiliaji wa kijiji cha Wami Luwindo kilichopo Dakawa Wilaya ya Mvomero Bw. Juma Achumu kama mchango wa Wizara yake kuwezesha na kuamsha hari ya Wananchi kijiletea maendeleo.

Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

………………….

Na Mwandishi wetu Morogoro

Seriklai imeziagiza Mamlaka ya Udhiti Ubora Tanzania (TBS), Mamlaka ya Udhiti wa ubora wa Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) na SIDO kuwapa elimu Wanawake wajasiliamali wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro ili kuongezea thamani katika bidhaa zao kwa kuwapa wabunifu na kuhakikisha bidhaa zao zinakuwa vifungashio vyenye ubora ili ziweze kushindana katika soko na bidhaa nyingine.

Hayo yamesemwa mkoani Morogoro Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati alipotembelea vikundi vya wanawake wajasiliamali wa Wilaya ya Mvomero katika ziara yake Mkoani Morogoro kuangalia utoaji huduma za Afya na Maendeleo ya Jamii.

Pamoja na mambo mengine Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Ndugulile amesema ili wanawake hao waweze kufikia malengo yao na kukuza biashara yao lazima bidhaa ziwe na nembo ya biashara ambayo itatambulisha bidhaa zao na kusaidia kuvutia wateja.

‘’Wekeni nembo katika bidhaa zenu na serikali ya Wilaya iwasaidie ili muweze kuwa na viwanda vidogo vya uzalishaji mali jambo ambalo lipo pia katika Nchi zinazoendelea ambapo viwanda vidogo vimekuwa vikisaidia kuinua hali ya maisha ya wananchi mfano mkiongezea thamani bidhaa zenu na kuzipa nembo ya Movomero itakuwa bora zaidi’’. Alisisitiza Dkt. Ndugulile.

Naibu waziri huyo amewataka viongozi wa Wilaya Mvomero kutafuta namna ya kuwapa elimu ya kutengeneza vifungashio wajasiliamali wadogo hao ilikuweza kufikia hadhima ya serikali ya viwanda.

Wakati huo huo Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mvomero Bw. Florence Kyombo akitoa taarifa ya uwezeshaji wanawake kiuchumi ya Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF) na uhamasishaji wa wanawake kujiunga na vikundi vya kiuchumi Wilayani Mvumero alisema utoaji wa mikopo kwa wanawake utawezesha wananchi kuajiliwa, kuajili na kuongeza pato la familia.

Bw. Kyombo katika taarifa yake hiyo kwa Naibu Waziri wa Afya Dkt. Ndugulile alisema Wilaya yake kwa mwaka 2017/18 ilitoa mikopo kwa wanawake kiasi cha Tsh.84 kwa vikundi vya wanawake 44 vyenye wanaufaika 757 na vijana pia kiasi Tsh.57.4 milioni kwa vikundi vya vijana 15 vyenye wanufaika 184.

Akizungumzia kuhusu kikundi mlezi Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Jinsia kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Mboni Mgaza amesema kuwa dhana ya hiyo imeanzishwa na Wizara kwa lengo la kuwawezesha wanawake wajasirimali waliofanikiwa kuwasaidia wale ambao wanaanza ili kuinua katika biashara na ili wanawake kuweza kuinuka kiuchumi.

FAINALI ZA MASHINDANO YA VILABU VYA KODI ZAFANA

$
0
0
Na Veronica Kazimoto,Dar es Salaam

Fainali za mashindano ya vilabu vya kodi zilizoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), zimefanyika kwa mafanikio makubwa ambapo zawadi mbalimbali zimetolewa kwa Shule za Sekondari zilizoibuka na ushindi na baadhi ya wanafunzi waliofanya vizuri katika mashindano hayo.

Fainali hizo zilizofunguliwa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) zilifanyika jana katika Chuo cha Usimamizi wa Kodi (ITA) kilichopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Katika mashindano hayo, Shule ya Sekondari St. Joseph iliibuka mshindi wa kwanza kati ya shule 28 za Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani na kuzawadiwa runinga, kompyuta ya mezani, printa, saa ya ukutani, medali, ngao, na cheti.

Shule ya Sekondari Tumbi imeshika nafasi ya pili ambayo ilijinyakulia kompyuta ya mezani, printa, saa ya ukutani, medali, ngao, na cheti ikifuatiwa na Shule ya Sekondari Dar es Salaam ambayo ilipata ngao, kompyuta ya mezani, saa ya ukutani na cheti.

Kwa upande wa uwasilishaji mada zinazohusu masuala ya kodi, Shule ya Sekondari Zanaki iliongoza na kuzawadiwa kompyuta ya mezani, printa, saa ya ukutani, medali na cheti ikifuatiwa na Kerege ambayo ilijibebea printa, saa ya ukutani na cheti huku Shule ya Sekondari Misitu ikishika nafasi ya tatu na kuondoka na kompyuta ya mezani, ngao, na cheti.

Kwenye kipengele cha Ukusanyaji wa Risiti za Kielektroniki za EFD, walioibuka washindi ni Shule ya Sekondari Gerezani ambayo ilizawadiwa runinga, fedha taslimu shilingi 1,000,000, cheti na medali. Mshindi wa pili ni St. Joseph iliyojitwalia ngao, cheti na fedha taslimu shilingi 750,000 ikifuatiwa na Shule ya Sekondari Benjamini iliyopata ngao, cheti na fedha taslimu shilingi 500,000.

Aidha, Mwanafunzi Bora wa Mwaka huu katika fainali hizo, alikuwa ni Runi David kutoka Shule ya Sekondari Tumbi ambaye alijinyakulia laptop, ngao, medali na cheti.

Kilichofurahisha zaidi katika mashindano hayo ni ushiriki wa mwanafunzi mdogo kuliko wote mwenye umri wa miaka 12 Charles Denis kutoka Shule ya Sekondari Mbezi Inn ambaye alizawadiwa laptop, medali na kikombe cha chai kama motisha kwa wanafunzi wengine wenye umri kama wake kushiriki mashindano ya vilabu vya kodi.

Kwa upande wa jambo ambalo halikuwa la furaha lakini baadaye likageuka kuwa la shangwe ni pale mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Zawadi, Mariam Hussein aliyebubujikwa na machozi wakati akisimulia kukatazwa kushiriki mashindano hayo na mama yake mzazi, suala lililopelekea Mamlaka ya Mapato Tanzania kuahidi kumlipia gharama zote za kidato cha nne ikiwemo ada, jambo lililoibua furaha isiyo ya kifani kwa washiriki wa fainali hizo.

Fainali hizo zilizoshuhudiwa na Kamishna Mkuu wa TRA Charles Kichere ambaye ndiye aliyekabidhi zawadi mbalimbali kwa washindi, zilifungwa na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Richard Kayombo kwa kuwashukuru walimu, wanafunzi, majaji na kamati ya maandalizi kwa kufanikisha mashindano hayo.

"Napenda kuchukua fursa hii kumshukuru kila mtu aliyefanikisha mashindano haya wakiwemo wanafunzi, walimu, majaji na kamati nzima ya maandalizi ambayo imejituma kufanya kazi mpaka usiku ili kuhakikisha kuwa fainali hizi zinafanikiwa," alisema Kayombo.

Vilabu vya Kodi vilianzishwa na TRA mwaka 2008 na mpaka sasa kuna jumla ya vilabu 226 Tanzania Bara vikiwa na jumla ya wanafunzi 27,250 ambao ni wanachama hai wa vilabu hivyo.

Mashindano ya mwaka huu ni ya 11 kufanyika ambapo jumla ya shule 50 kutoka Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani zilishindanishwa na hatimaye shule 28 kati ya hizo zikafaulu kuingia kwenye fainali.

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere akiwakabidhi zawadi wanafunzi wa St. Joseph wakati wa fainali za mashindano ya vilabu vya kodi kwa Shule za Sekondari za Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani zilizofanyika katika Chuo cha Usimamizi wa Kodi (ITA) Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere akimkabidhi zawadi mwanafunzi mwenye umri wa mika 12 wa Shule ya Sekondari Mbezi Inn, Charles Denis wakati wa fainali za mashindano ya vilabu vya kodi kwa Shule za Sekondari za Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani zilizofanyika katika Chuo cha Usimamizi wa Kodi (ITA) Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere akimkabidhi zawadi mwanafunzi bora wa mwaka 2018 Runi David kutoka Shule ya Sekondari Tumbi wakati wa fainali za mashindano ya vilabu vya kodi kwa Shule za Sekondari za Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani zilizofanyika katika Chuo cha Usimamizi wa Kodi (ITA) Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere akimvisha mmoja wa wanafunzi ambaye shule yake iliibuka mshindi wakati wa fainali za mashindano ya vilabu vya kodi kwa Shule za Sekondari za Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani zilizofanyika katika Chuo cha Usimamizi wa Kodi (ITA) Jijini Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA TRA)

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI


WAZIRI MKUU AAGIZA KUBOMOLEWA KWA UZIO NA KUSITISHA UJENZI

$
0
0



Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa amemuagiza Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Bw. Godwin Kunambi kubomoa uzio wa mabati uliojengwa kwenye eneo la wazi lililotengwa kwa ajili ya kuchezea watoto na kusitisha mara moja shughuli za ujenzi kwenye eneo hilo. Pichani, Waziri Mkuu akimwonyesha Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi   ( wapili kushoto) ramani ya jiji la Dodoma inayoonyesha matumizi sahihi ya eneo  hilo, Oktoba 21, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_9573
Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa amemuagiza Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Bw. Godwin Kunambi kubomoa uzio wa mabati uliojengwa kwenye eneo la wazi lililotengwa kwa ajili ya kuchezea watoto na kusitisha mara moja shughuli za ujenzi kwenye eneo hilo. Pichani, mabati yakiwa yamezungushwa kwenye eneo hilo wakati Waziri Mkuu alipolitembelea, Oktoba 21, 2018.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
………………………………………………………………………………
*Ni baada ya kujengwa kwenye eneo la wazi na kuziba barabara
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Bw. Godwin Kunambi kubomoa uzio wa mabati uliojengwa kwenye eneo la wazi lililotengwa kwa ajili ya kuchezea watoto na kusitisha mara moja shughuli za ujenzi kwenye eneo hilo.

Uzio huo ambao mbali na kujengwa katika eneo la wazi lililotengwa kwa ajili ya kuchezea watoto kwenye mtaa wa Mji Mpya kata ya Madukani pia umeziba barabara ya tisa, hivyo kusababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa barabara hiyo.Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumapili, Oktoba 21, 2018) wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi jijini Dodoma, ambapo alitembelea eneo hilo na kuagiza libomolewe na lisalie kama inavyoonekana katika ramani na aliyeuziwa atafutiwe eneo lingine.

“Huu mji umejengwa kwa ramani, hamuwezi kubadili ramani kwa lengo la kumpa mtu eneo. Kwa nini mmeziba barabara ya tisa na huu mji unatambulika kwa barabara, sasa bomoeni hapa nataka barabara iendelee kutumika na eneo la kuchezea watoto libaki wazi,”Waziri Mkuu amemuagiza mkurugenzi wa jiji ahakikishe wanayatumia maeneo ya wazi kwa ajili ya kujenga sehemu za mapumziko ili kuwawezesha wananchi kupata maeneo ya kupumzika mara wanapomaliza kufanya shughuli zao za kikazi.

Amesema ni vema jiji likatenga ardhi na kupima viwanja kwa ajili ya matumizi mbalimbali yakiwemo ya biashara, makazi, taasisi, huduma za jamii, viwanda pamoja na maeneo ya wazi kwa ajili ya mapumziko. “Msifanye makosa kama yaliyofanyika Dar es Salaam.”Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Ardhi na Mipangomiji wa jiji la Dodoma, Bw. Joseph Mafulu alimuonyesha Waziri Mkuu ramani ambayo iliyotolewa na iliyokuwa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA) ambayo ilibadilisha matumizi ya eneo hilo na kumpa muwekezaji.
Baada ya Bw. Mafulu kuonesha ramani hiyo Waziri Mkuu alitoa ramani halisi ya jiji la Dodoma ambayo inaonesha eneo hilo ni la wazi na ni mahususi kwa ajili ya michezo ya watoto, hivyo alisisitiza kuwa litumike kama ilivyokusudiwa na si vinginevyo.

Kufuatia hatua hiyo, Waziri Mkuu aliwaonya watumishi wa halmashauri ya jiji la Dodoma kutorudia makosa yaliyofanywa na CDA na kwamba jukumu lao ni kuhakikisha wanayasahihisha makosa yaliyofanywa na mamlaka hiyo ili jiji liweze kupangika vizuri.Naye Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Bw. Kunambi aliahidi kuyafanyia kazi kikamilifu maelekezo yote yaliyotolewa na Waziri Mkuu na kesho (Jumatatu, Oktoba 22, 2018) ataandika barua kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa William Lukuvi kwa ajili ya kufuta hati ya eneo hilo na muwekezaji watampa eneo lingine.

Awali,Waziri Mkuu alizungumza na watumishi wa halmashauri ya jiji la Dodoma, ambapo aliwataka wabadilike na wasimamie vizuri rasirimali za umma pamoja na kuwahamasisha na kuwasisitiza wananchi wafanye kazi kwa bidii ili kufikia malengo maendeleo ya Taifa.

 Waziri Mkuu alisema mtumishi asiyeweza kufanya kazi kwa bidii anaweza kupata matatizo kwa sababu Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa Rais Dkt. John Magufuli imedhamiria kuwahudumia wananchi ipasavyo. Kadhalika, Waziri Mkuu aliwaagiza wakurugenzi wa halmashauri nchini pamoja na mameneja wasimamie vizuri utendaji kazi wa watumishi mbalimbali katika maeneo yao. Alisisitiza kuwa lazima watumishi wafanye kazi na matokeo yaonekane.

 Pia Waziri Mkuu alifungua ofisi kuu ya kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Makutupora na kisha alitembelea kiwanda cha kusindika zabibu cha Alko Vintage na kukagua uzalishaji wa mvinyo katika kiwanda hicho kilicho jijini Dodoma.

FARAJI MAJIMOTO AIBUKA MSHINDI WA TIGO FIESTA SUPA NYOTA MKOA WA TANGA

$
0
0


Meza ya Majaji ikijadili jambo wakati wa shindano la kusaka vipaji la Tigo Fiesta Supa Nyota mkoa wa Tanga, Toka kushoto ni Mecky Manyanga, Adam Mchomvu, Stamina na Moko Biashara.
IMG_20181021_145845
Jaji Mkuu wa shindano la kusaka vipaji Tigo Fiesta Supa Nyota 2018, Adam Mchomvu akimnyanyua mkono juu mshindi wa shindano hilo toka Tanga, Faraji Majimoto maarufu kama Rai Mc, kwenye kinyang’anyiro kilichofanyika leo kiwanja cha Tangamano Tanga. Faraji ataingia kwenye fainali itakayofanyika Dar es salaam mwezi ujao.
IMG_20181021_140622
Faraji Majimoto RAI MC akifanya yake kwenye steji
IMG_20181021_143930
Sehemu ya umati uliohudhuria kwenye shindano la kusaka vipaji vya kuimba la Tigo Fiesta Supa Nyota kiwanja cha Tangamano, Tanga

DC MURO ATEMBELEA NA KUKAGUA UJENZI WA KITUO CHA AFYA MBUYUNI

$
0
0



Imma Msumba, Arumeru.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mh.Jerry Muro amefanya ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua Ujenzi wa Kituo cha Afya cha Mbuyuni kilichopo katika Halmashauri ya Arusha Dc  ambacho Serikali imetenga fedha Milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa Maabara na Nyumba ya Mtumishi wa kituo hicho pamoja na kufanya ukarabati wa majengo yaliyokuwepo kwa lengo la kuwapa wananchi huduma bora za afya na kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi. 
 IMG-20181021-WA0010
IMG-20181021-WA0013
Dc Muro akikagua ujenzi wa Kituo hicho ameleza kuwa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya Afya kwa kuimarisha huduma za Afya na kujenga vituo vyenye hadhi vijijini.
 IMG-20181021-WA0006
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi hiyo ya Ujenzi wa Kituo hicho Ndg.Leskara Olerangai Ambaye pia ni Diwani mstaafu wa kata ya Oljoro ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli kwa  kuwezesha kutoa fedha kwa wakati huku akimpongeza Dc Muro kwa jitihada zake anazozifanya ili kuhakikisha ujenzi una kamilika kwa wakati.

AJALI YA GARI YAUA WATUMISHI WATANO WIZARA YA KILIMO NA CHAKULA

$
0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

WATUMISHI watano wa Wizara ya Kilimo na Chakula wamefariki dunia leo asubuhi baada ya gari waliyokuwa wakisafiria kupata ajali wilayani Manyoni mkoani Singida.

Taarifa ya Katibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo ambayo ameitoa leo kwa vyombo vya habari amesema kuwa Wizara yao imepatwa na msiba wa watumishi wake watano.

Amesema watumishi hao waliopata ajali leo asubuhi wilayanu Manyoni mkoani Singida, walipokuwa safarini kuelekea Mwanza kikazi.

Amewataja watumishi hao waliofariki ni Stella Ossano (39), Esta Mutatembwa (36), Abdallah Mushumbusi (53), Charles Somi na Erasto Mhina (43)

"Miili ya marehemu ipo njiani kuja Hospitali ya Mkoa wa Dodoma leo Oktoba  21, 2018.Mungu azilaze roho zao mahala pema peponi, Amina," amesema Katibu Mkuu kwenye wizara hiyo.
Baadhi ya wananchi wakitazama namna ajali hiyo ya gari yenye namba za Usajili STK 8925 ikiwa imepta ajali eneo la Njirii Manyoni. Ambapo Gari ndogo, ya Wizara ya Kilimo na Chakula, iliyokua imebeba Wataalam wane pamoja na Dereva Wote wamefariki papo hapo. Wanaume watatu, na wanawake wawili. Miili imehifadhiwa katika Hosptal ya Wilaya Manyoni. Mwenyezi Mungu Awarehemu
Baadhi ya Maofisa wa Polisi wakitazama gari yenye namba za Usajili STK 8925 ikiwa imepta ajali eneo la Njirii Manyoni. Ambapo Gari ndogo, ya Wizara ya Kilimo na Chakula, iliyokua imebeba Wataalam wane pamoja na Dereva Wote wamefariki papo hapo. Wanaume watatu, na wanawake wawili. Miili imehifadhiwa katika Hosptal ya Wilaya Manyoni. Mwenyezi Mungu Awarehemu.

CHAMA CHA MAPINDUZI KUWACHUKULIA HATUA KALI WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA WASIO SOMA MAPATO NA MATUMIZI

$
0
0
Katika Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM Kata ya Mtoni Wilaya ya Temeke Mkoa wa Dar es salaam Ndg. Humphrey Polepole Katibu Mwenezi wa CCM amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitawachukulia hatua kali Wenyeviti wa Serikali za Mitaa wanaotokana na CCM wasio soma mapato na matumizi kwa wananchi kwa mujibu wa Sheria.

Akifafanua suala hilo Ndg. Polepole ameeleza kuwa kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa wa Mwaka 2019 CCM inahitaji watu watakao kuwa Viongozi wa wananchi kupitia CCM wenye sifa nzuri kwenye mitaa yao, amekemea suala la urafiki, undugu na upangaji wa safu katika mchakato wa kuwapata viongozi wa wananchi na amewataka Viongozi wa CCM na Viongozi wa Serikali ngazi zote kuwa na ushirikiano kwa lengo la kuwaletea maendeleo wananchi kwa haraka.

“Wapo wenyeviti wa Serikali za Mitaa wa CCM wasio soma mapato na matumizi…watu jeuri… wanafanya nini kwenye Chama chetu..? hawa hatuendi nao hadi mwaka 2019…kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mwakani tunataka watu wenye sifa nzuri” amesisitiza Ndg. Polepole

Aidha Ndg. Polepole ametumia mkutano huo kusisitiza kuhusu suala la  Viongozi wa Serikali hususani wakuu wa Wilaya kuendeleza utaratibu wa kusikiliza wananchi na utolewaji wa mikopo ya Halmashauri bila riba kwa makundi ya kina Mama, Vijana na Watu wenye ulemavu ili kuwawezesha wananchi kiuchumi na kutatua shida na changamoto zao kwa haraka.

Huu ni muendelezo wa vikao vya ujenzi na uimarishaji wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kuhakikisha dhana ya Chama imara, Serikali imara inadhihirika.
 Katibu Mwenezi wa CCM Ndg. Humphrey Polepole akizungumza Katika Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM Kata ya Mtoni Wilaya ya Temeke Mkoa wa Dar es salaam

DC Kinondoni aahidi kutatua kero ya barabara inayokwenda Kliniki ya Heameda, Mengi ashangazwa na maajabu ya Dk.Mwandolela

$
0
0

VIONGOZI wa ngazi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es  Salaam wamepongeza uongozi wa Kliniki ya Heameda iliyopo Bunju B ambayo imekuwa ikitoa huduma za matibabu ya moyo kwa wananchi wa wilaya hiyo na maeneo mengine huku ukiahidi kushughulikia kero ya ubovu  barabara inayoelekea kwenye kliniki hiyo ambayo imetajwa kutoa mchango mkubwa kuokoa maisha ya Watanzania.

Hayo yamesemwa jana na ujumbe wa Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni kupitia Mkuu wake wa Wilaya Daniel  Chongolo na Mganga Mkuu wa halmashauri hiyo Dk.Christowell Mande wakati wa uzinduzi rasmi wa Kliniki ya Heameda ambapo mgeni rasmi alikuwa Mwenyekiti wa Kampuni za IPP Reginald Mengi.

Akizungumzia Kliniki hiyo Chongolo amesema Serikali inathamini mchango wa kliniki hiyo kwa kutoa huduma kwa wananchi wa Kinondoni na hasa walioko maeneo hayo ambayo hayana vituo vingi vya afya.Pia amejibu kuhusu ombi kero ya barabara inayoingia kwenye  kliniki hiyo kwa kuahidi kuishughulikia mara moja kwa kuitengeneza.

Kwa upande wa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Dk.Mande amesema Serikali inatambua na kuthamini mchango wa sekta binafsi katika kutoa huduma za afya na iko tayari kufanya kazi na kliniki hiyo.

"Tunawakaribisha muda wowote kufanya kazi katika dhana ya PPP.Kikubwa ambacho tunaweza kueleza hapa ni kwamba tunathamini mchango wenu na tunaomba tuedelee kushirikiana katika kuwahudumia Watanzania,"amesema.

Wakati huo huo mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Kliniki ya Heameda Dk.Reginald Mengi amesema kijana wa Kitanzania Dk.Hery Mwandolela ambaye ndio mmikili wa Kliniki hiyo amefanya maajabu makubwa na anastahili kuwa mfano wa kuigwa.

"Nimefurahi kwani tulionana miaka 23 iliyopita ukiwa mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Kibaha ukiwa huna kitu lakini leo umefanya jambo kubwa sana ndani ya nchi yetu.Nitoe mwito kwa vijana wengine kuiga mfano huu kwa kuthubutu.Ukisema neno na ukaliamini linatokea, na kila wakati ukiwa a kauli mbiu ya I can, I must ,I will ...kila kitu kinawezekana,'"amesema.

Pia ameguswa na ubovu wa barabara ya kuingia kwenye kliniki hiyo ambapo amesema atachangia ujenzi wa barabara hiyo baada ya Mkuu wa Wilaya kueleza kwamba ataishughulikia.

Awali Mkurugenzi wa Kliniki ya Heameda ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya moyo Dk.Hery Mwandolela amesema Kliniki yao ilianza mwaka 2010 ikiwa na wafanyakazi wawili na walikuwa kwenye vyumba viwili vya kupangisha lakini sasa kuna wafanyakazi 30 ina miliki jengo kubwa na vifaa vya kisasa.

"Heameda Kliniki imefanikiwa kufikia malengo iliyojiwekea ikiwemo kutoa huduma bora za kisasa kwa asilimia 95 na tumetoa huduma za matibabu kwa wagonjwa 13000 tangu tulipoanza tena kwa ufanisi mkubwa.Pia watalaamu wao wametoa elimu ya afya na upimaji kwa wafanyakazi wa taasisi binafsi na za Serikali.Baadhi ya taasisi hizo ni BoT,Tanesco,CRDB, TTCL,Tantrade ,NBC,NMB, Cocacola, na Vodacom ambao wote waliendelea kupata huduma bora na bado ni wateja wetu,"amesema.

Dk.Mwandolela pia amesema wameweza kuendesha uchunguzi wa afya bure kwa wananchi  katika Kliniki yao Julai mwaka huu kwa kuwahudumia wananchi wa Dar es salaam na sehemu nyingine.Huduma hiyo ilitolewa na madaktari bingwa kutoka India kwa kushirikiana na madaktari bingwa wa hapa nchini ambapo jumla ya wanachi 521 walipata huduma.

Amefafanua kati ya hao 72 walikuwa na shinikizo la damu bila kujua , 16 walikuwa na kisukari,wanaume nane waligundulika na satarani ya tezi dume na wananchi 89 walikuwa na matatizo ya macho.

Dk.Mwandolela amefafanua kwa kuzingatia ubora wa kimataifa Heameda Kliniki ina matarajio ya muda mfupi na ya muda mrefu ambapo amesema matarajio ya muda mfupi ambayo ni ndani ya mwaka mmoja ni kuendelea kuboresha huduma kwa wagonjwa wa nje kwa kukamilisha vipimo vyote muhimu na kuboresha huduma za dharura.

Wakati matarajio ya muda wa kati ambayo ni ndani ya miaka miwili ni kuanzisha huduma za kulaza wagonjwa , upasuaji na kulaza wagonjwa mahututi (ICU), kuanzihsha kozi fupi kwa madaktari za kufundisha kwa vitendo jinsi ya kufanya na kutafsiri kwa usahihi vipimo muhimu  vya moyo yaani Echo, ECG, ABPM,Holter na TMT kwani vipimo hivyo ni muhimu sana katika kuchunguza magonjwa ya moyo na kuokoa maisha ya mgonjwa.

"Madaktari wengi nchini hata walio katika daraja la ubingwa hawana ujuzi wa kufanya tafsiri sahihi ya vipimo hivyo.Pia kuweka mashine za CT Scan  kwa ajili ya moyo na magonjwa mengine.

Wakati matarajio ya muda mrefu ni kumalizia ujenzi kwa sehemu iliyobakia , kufungua chuo cha mafunzo ya kada mbalimbali za afya kwa kiwango cha Stashahada(Diploma), na hapo baadae kuwa chuo kikuu cha afya.

Kuhusu lengo lao kuu amesema ni kuifanya kliniki hiyo kuwa hospitali bora ya kuokoa maisha Watanzania hasa wenye magonjwa ya moyo.Pia kutoa huduma nzuri za afya kwa wananchi.Kuhusu maono yao ni kuwa na hospitali kubwa yenye hadhi ya juu nchini Tanzania na kimataifa.

Amefafanua kuwa Kliniki ya Heameda ilianzishwa rasmi Oktoba 20 mwaka 2010 baada ya kusajiliwa rasmi kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za nchi yetu chini ya wizara  ya Afya.Kliniki hiyo ina watalaam waliobobebea katika fani ya magonjwa ya moyo na fani nyingine mbalimbali za afya kwa  ufanisi na weledi wa hali ya juu.

Kuhusu changamoto Dk.Mwandolela amesema ubovu wa miundombinu  hasa barabara inayoingia hospitalini hapo imekuwa kero kubwa kwa wagonjwa na wafanyakazi hasa katika msimu wa mvua na tayari taarifa hizo wameshazifikisha kwenye mamlaka husika kwa hatua zaidi.

Changamoto nyingine ni ukubwa na ugumu wa gharama za uwekezaji hasa kwa kutuma mikopo  inayotolewa na benki za biashara zinazotoza riba kubwa badala ya kutumia benki za uwekezaji zenye riba nafuu.

Ametumia nafasi hiyo kuwaomba vijana wa kitanzania kuiga mfano wake lakini pia kuamini kwenye falsafa iliyobebwa na kauli mbiu iliyojikita kwenye kuamini katika kuweza huku akitoa ombi kwa Dk.Mengi awe mlezi wao ili waweze kutumia kipawa na ujuzi alionao kufanikisha ndoto na malengo ya kliniki yao.
 Mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Kiliniki ya Heameda Dk.Reginald Mengi akikata utepe kuashiria kuzinduliwa rasmi kwa Kliniki hiyo leo jijini Dar es Saalam.Anayeshangilia mmiliki wa kliniki hiyo ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo Dk.Hery Mwandolela
 Mwenyekiti wa Kampuni za IPP Media Dk.Reginald Mengi (katikati) akiwa pamoja na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo Dk.Hery Mwandolela(kulia) na kushoto Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo wakiangalia ujumbe uliopo kwenye jiwe la msingi ikiwa ni ishara ya kuzinduliwa rasmi kwa Kliniki ya Heameda ambayo ni maalum kwa ajili ya kutoa huduma ya matibabu ya magonjwa ya moyo.

 Mkuu wa Wilaya Kinondoni jijini Dar es Salaam Daniel Chongolo akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kliniki ya Heameda iliyopo Bunju B jijini Dar es Salaam ambapo ameahidi kutatua kero ya barabara inayoelekea kwenye kliniki hiyo
 Mmiliki wa Kliniki ya Heameda ambaye pia ni Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo Dk.Hery Mwandolela akizungumza wakati wa uzinduzi wa kliniki hiyo leo jijini Dar es Salaam
 Mwenyekiti wa Kampuni za IPP Dk.Regenald ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa Kliniki ya Heameda akiwa kwenye picha ya pamoja
 Mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Kliniki ya Heameda iliyopo Bunju B jijini Dar es Salaam Dk.Reginald Mengi akikabidhi cheti maalum kwa Dk.Isaac Maro kwa kutambua mchango wake  katika kliniki hiyo.
Mwenyekiti wa Kampuni za IPP Dk.Reginald Mengi(kushoto) aliyekuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa Kliniki ya Heameda iliyopp Bunju B jijini Dar es Salaam akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo(kulia) leo.Katikati ni Mmiliki wa kliniki hiyo Dk.Hery Mwandolela

VIONGOZI BORA HUANZIA SHULENI

$
0
0
SHULE ya sekondari ya Imperial kwa mara ya kwanza imesheherekea 
mahafali ya kwanza ya kidato cha nne mahafari yaliyofanyika jana Oktoba 20,2019.

Akizungumza Katika mahafali hayo Spika wa Bunge mstaafu, Anne Makinda  alisema kuwa shule zinajukumu la kuwaandaa vijana kuwa Viongozi Bora kwani waliowengi hutokea shuleni.

Pia alizindua kampeni maalum ya Shule hiyo inayotambua mchango wa viongozi mbalimbali katika kuhamasisha uongozi bora, alisema wanafunzi wanaoaminishwa kuwa wanaweza kuwa viongozi bora tangu wakiwa wadogo hujenga tabia ya wao kujilinda na kujichunga wenyewe.

Mbali na kusifia mandhari nzuri ya shule hiyo Anne alisema anaamini Viongozi wazuri watatoka shuleni hapo, na kuwasihi wazazi kutohangaika kuwapeleka watoto wao mbali ili hali kuna shule kama Imperial yeye viwango vya kimataifa. 

Kwa Mujibu wa Mkuu wa Shule hiyo bwana Lincolin Mashanda, alisema nayo Imperial Sec School imejiandaa kuzalisha Viongozi hao wa Kesho katika fani na nyanja mbalimbali katika ubora kwa kuzingatia, maadili mema na kwa  kuhamasisha hilo kuanzia Shuleni hapo. 

Mashanda amesema 
"Yapo mambo kadhaa ambayo yanamfanya mtu awe kiongozi bora, mambo haya yakianza kuzoeshwa mapema huwa tabia na muongozo kwa vijana wetu..

Mashanda alikinukuu Kituo cha utafiti na mafunzo ya uongozi cha Dale Carnegie cha jijini New York nchini Marekani kinachosema katika utafiti wao wamegundua kwamba kinachomfanya mtu awe kiongozi bora sio suti wala sura bali uwezo na nia ya dhati katika kuamsha ari, kuwawezesha unaowaongoza, kuwafanya wajiamini na kuwapa motisha watu unaowaongoza.

Kiongozi bora ni yule anayeweze Kuyakabili Matatizo au Changamoto
Kiongozi bora ni yule ambaye ana ujasiri wa kutosha wa kukabiliana na kila aina ya changamoto inaweza kujitokeza kwa busara."

"Dunia ya leo imejaa changamoto za kila aina. Kila kukicha kuna jipya na gumu zaidi. Taswira ya uingozi bora inamjenga kijana kujiamini na kujilinda hivyo kuwa sababu ya yeye kukabiliana na changamoto mbalimbali za ujana kwa matumaini."

"Kiongozi bora lazima awe muaminifu. Uaminifu unaanzia kwenye kuwa mkweli. Na hii nitabia inayoanza utototoni."

"Kiongozi bora ni yule mwenye uwezo wa kusimamia ahadi yake na jitihada anazofanya kutimiza ahadi yake."

"Kiongozi bora lazima ajiheshimu. Na dhana ya kujiheshimu ni pana. Hii ni pamoja na kuheshimu wazazi wako, ndugu, jamaa  marafiki na watu wote. Unapojiheshimu, inakuwa rahisi kuongoza wengine."
:Kiongozi bora huwa anakiu ya kujifunza zaidi na ni mtafiti. 
Kiongozi bora ni Mtendaji
Yote niliyoyataja hapo yanafundishika."

:Sasa pamoja na masomo mengine Imperial secondary school inamuandaa mwanafunzi wake katika mazingira ya kuyatambua haya na kuyafanyia kazi mapema kipindi awapo shuleni. '

Alisema 'Tunaamini ugeni wa  mama Anne S..Makinda katika mahali yetu utaongeza tija na hamasa kwa kile tulichokuwa tukiwaandaa nacho wanafunzi wetu.
Mgeni Rasmi ambaye ni Spika wa Bunge Mstaafu Anne Makinda  akizungumza katika mahafali ya kwanza ya kidato cha nne Imperial Secondary School (ISS) yaliyofanyika jana Msolwa Chalinze.
 Mgeni Rasmi ambaye ni Spika wa Bunge Mstaafu Anne Makinda akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kusheherekea Mahafari ya kwanza ya kidato cha nne.


 Baadhi ya wahitimu wa kidato cha nne wakiwa katika picha ya pamoja.
 Mgeni Rasmi ambaye ni Spika wa Bunge Mstaafu Anne Makinda akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa kidato cha nne.
 Wahitimu wa kidato cha nne wakizungumza wakati wa kusheherekea mahafari yao ikiwa ni wakwanza tangu kuanzishwa kwa shule hiyo. 
 Mgeni Rasmi ambaye ni Spika wa Bunge Mstaafu Anne Makinda akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu pamoja na wazazi wao katika mahafali ya kwanza ya kidato cha nne.

WANACHAMA 15 KUTOKA VYAMA VYA UPINZANI WAHAMIA CCM

$
0
0
WANACHAMA 15 wa vyama vya siasa vya upinzani wilaya ya Temeke wamejiunga na chama cha Mapinduzi CCM jijini Dar es Salaam leo.

Wanachama waliohama vyama vyao na kujiunga na CCM ni aliyekuwa katibu CHADEMA kata ya chang'ombe Abduli Kheri, Mwenyekiti CHADEMA Kata ya toangoma John Matugura, aliyekuwa katibu CHADEMA kata ya Temeke na katibu na mwenyekiti wa Bavicha wilaya ya TemekeChales Gahu, Afisa uchaguzi CHADEMA katibu mwenezi ACT WazalendoSteven Shekumkae.

Mwanachama CHADEMA Saidi Mohamed Ngaola,Mwenyekiti CHADEMA kata ya Kurasini James Nyaki, Mwanachama CHADEMA Mahamudu Saidani, Katibu mwenezi CHADEMA kata ya MtoniThomas Elia, Mwanachama CHADEMA Juma Said, Mwenyekiti Vijana Chama cha ACT Wazalendo KelvinAbiud ,Wanachama wa ACT Wazalendo Editha Bunjoro (Mama Kelvini,) Taifa baraza la wadhamini CHADEMA,Katibu kata CUF Toangoma Ally Mbonde,Renaty Lipambile Mwenyekiti CHADEMA wilaya ya Temeke na diwani wa kata ya mtoni Bernard Mwakyembe.


Wakizungumza mara baada ya kurudisha kadi za vyama vyao wanachama hao wamesema kuwa hawajanunuliwa bali wanaunga mkono juhudi za Rais John Pombe Magufuli baada ya kuona utekelezaji wake.

Akizungumza wakati wa kuwapokea katika chama cha Mapinduzi CCM katibu Mwenezi wa chama cha Mapinduzi CCM, Humfrey Polepole jijini Dar es Salaam leo amewakaribisha katika kwenye chama Tawala CCM.

Amesema kuwa utaratibu wa kupata kadi zao za Chama cha mapinduzi watazipata kwenye mashina wanakoishi kama utaratibu ulivyopangwa na Chama cha Mapinduzi.

Pia Polepole amesema kuwa Wanawake wa chama cha mapinduzi watanufaika na mikopo isiyona riba kwani chama kimechoka na mikopo kutoka sehemu nyingine na yenye riba.
 Baadhi ya wanachama kutoka vyama vya upinzani wilaya ya Temeke wakiwa mbele mara baada ya kupkelewa katika chama Cha Mapinduzi CCM jijini Dar es Salaam leo.

 Mwanachama mpya akifungwa skafu ya CCM.
 Wanacham wapya wa CCM wakirudisha kadi zao za vyama walikokuwa.

WAZIRI WA UJENZI, MHANDISI KAMWELE AKAGUA UJENZI BARABARA SITA DAR-KIBAHA

$
0
0

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Injinia Patrick Mfugale (kulia) akimwelezea Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Issack Kamwele (katikati) maendeleo ya mradi wa ujenzi wa barabara sita kutoka Dar es Salaam hadi Maili Moja Kibaha unaojengwa na fedha za Serikali kwa gharama ya takribani zaidi ya shilingi bilioni 140. Waziri Mhandisi Kamwele alitembelea kukagua maendeleo ya mradi huo na miradi mingine ya Tanroads iliyopo jijini Dar es Salaam. Mradi wa ujenzi wa barabara sita unatarajiwa kukamilika mwezi wa kwanza 2020.

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Injinia Patrick Mfugale (kushoto) akimwelezea Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Issack Kamwele (kulia) maendeleo ya mradi wa ujenzi wa barabara sita kutoka Dar es Salaam hadi Maili Moja Kibaha unaojengwa na fedha za Serikali kwa gharama ya takribani zaidi ya shilingi bilioni 140.
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi Julius Ndyamukama (aliye nyoosha kidole) akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Issack Kamwele alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara sita kutokea Dar es Salaam hadi Mail Moja Kibaha. 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe pamoja na msafara wake wakitembelea mradi wa barabara sita unaoendelea eneo la Kimara Dar es Salaam hadi Mail Moja Mkoa wa Pwani.
Ujenzi wa barabara sita kutokea Dar es Salaam hadi Mail Moja Kibaha ukiendelea. Eneo hili unajengwa ukuta kuzuia maji ya mto kuingilia barabara hizo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe akipata maelekezo ya ujenzi wa barabara sita kutoka kwa wataalam wa Tanroads.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe akizungumza na wananchi akiwa katika ziara ya kukagua ujenzi wa barabara sita kutokea Dar es Salaam hadi Mail Moja Kibaha. Katika ziara hiyo Waziri Kamwelwe aliwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa Serikali ya Rais John Pombe Magufuli katika jitihada za kumaliza msongamano wa magari kuingia na kutoka Dar es Salaam. 
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe aalipozungumza nao katika ziara ya kukagua ujenzi wa barabara sita kutokea Dar es Salaam hadi Mail Moja Kibaha.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe akizungumza na wananchi akiwa katika ziara ya kukagua ujenzi wa barabara sita kutokea Dar es Salaam hadi Mail Moja Kibaha. Katika ziara hiyo Waziri Kamwelwe aliwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa Serikali ya Rais John Pombe Magufuli katika jitihada za kumaliza msongamano wa magari kuingia na kutoka Dar es Salaam. 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya MECCO, Abdukadri Budjet (wa kwanza kushoto) mara baada ya kukagua ujenzi wa barabara ya Mbezi-Goba-Wazo Hill yenye urefu wa kilometa 5 inayojengwa na kampuni ya MECCO.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe akizungumza na wanahabari mara baada ya kukagua ujenzi wa barabara ya Mbezi-Goba-Wazo Hill yenye urefu wa kilometa 5.
Muonekano wa kivuko cha waenda kwa miguu eneo la njia panda Kawe kituo cha Bondeni jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Injinia Patrick Mfugale (katikati) akifafanua jambo kwa  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Issack Kamwele (wa pili kushoto) alipokagua maendeleo ya daraja la Mlalakuwa jijini Dar es Salaam, linalojengwa na Serikali kwa takribani ya shilingi bilioni 4.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (kulia) akitoa maelekezo kwa wahandisi wa kampuni ya KIKA (kulia) wanaojenga Daraja la Mlalakuwa eneo la JKT jijini Dar es Salaam alipokagua mradi huo.
Sehemu ya ujenzi wa Daraja la Mlalakuwa eneo la JKT jijini Dar es Salaam ukiendelea.

Tigo Pesa na Google team waungana kuwezesha Watanzania kulipia maudhui au application yoyote inayopatikana Google Play Store

$
0
0



Je umewahi kutaka kununua muziki, cinema, apps au vitabu kwa kusoma kwenye mtandao wa Google Play Store lakini ukashindwa kufanya hivyo kwa sababu hukuwa na kadi ya benki?

Tangu Juni yam waka huu, kampuni inayoongoza kwa maisha ya kidigitali nchini, Tigo imeingia makubalino na Google kuwapa wateja uwezo wa kulipia maudhui ya mtandaoni kutoka Google Play Store kwa njia ya Tigo Pesa.

Huduma hii inayowezeshwa na Bango inawawezesha wateja 7 milioni wanaotumia huduma ya kifedha ya Tigo Pesa kulipia maudhui au application yoyote inayopatikana Google Play Store kwa kutumia akaunti yao ya Tigo Pesa.

‘Tigo customers using Android smartphones or tablets can now make one-off, in-app or subscription payments for content on Play Store in a simple and convenient way from anywhere in the country through their active Tigo Pesa wallets. This gives our customers the added convenience that enables them to download and enjoy online content from Google Play Store as they seamless enjoy our transformational digital lifestyle services through Tanzania’s biggest and fastest 4.5G network,’ Tigo’s Chief Officer for Mobile Financial Services, Hussein Sayed said in Dar es Salaam today.

This solution seamlessly combines Google Play with the Tigo Pesa purchase experience that Tigo customers are used to when paying for goods and services. Customers go through the same steps they would normally do to purchase content on the Play Store, and under the payment options choose Tigo Pesa. They then follow a few simple steps to link their Google profile to their Tigo Pesa account, create and enter a new 6-digit passphrase which will be used for all Play Store purchases.

Mahir Sahin, Africa Director for Android Partnerships, Google, said: “We are very excited to partner with Tigo to offer this innovation which enables Tigo Pesa customers to make payments in the Google Play Store directly. This will give millions of Tanzanians who do not have credit cards access to the full depth of content on Google Play.”

‘Tigo is at the helm of digital lifestyle transformation, with Tigo Pesa leading the innovation in mobile financial services by being the first mobile money wallet in Tanzania to enable Google Play Store content purchases. This proves that Tigo Pesa is a fully-fledged mobile financial service offering customers more and better digital payment solutions,’ Hussein added.

With so many Tanzanian’s preferring to use their mobile device to pay for goods and services, Tigo has now empowered them to purchase their favorite content on the world’s leading app store through Tigo Pesa.

VIONGOZI BORA HUANZIA MASHULENI-ANNE MAKINDA

$
0
0
SHULE ya sekondari ya Imperial kwa mara ya kwanza imesheherekea mahafali ya kwanza ya kidato cha nne mahafari yaliyofanyika jana Oktoba 20,2019.

Akizungumza Katika mahafali hayo Spika wa Bunge mstaafu, Anne Makinda  alisema kuwa shule zinajukumu la kuwaandaa vijana kuwa Viongozi Bora kwani waliowengi hutokea shuleni.

Pia alizindua kampeni maalum ya Shule hiyo inayotambua mchango wa viongozi mbalimbali katika kuhamasisha uongozi bora, alisema wanafunzi wanaoaminishwa kuwa wanaweza kuwa viongozi bora tangu wakiwa wadogo hujenga tabia ya wao kujilinda na kujichunga wenyewe.

Mbali na kusifia mandhari nzuri ya shule hiyo Anne alisema anaamini Viongozi wazuri watatoka shuleni hapo, na kuwasihi wazazi kutohangaika kuwapeleka watoto wao mbali ili hali kuna shule kama Imperial yeye viwango vya kimataifa. 

Kwa Mujibu wa Mkuu wa Shule hiyo bwana Lincolin Mashanda, alisema nayo Imperial Sec School imejiandaa kuzalisha Viongozi hao wa Kesho katika fani na nyanja mbalimbali katika ubora kwa kuzingatia, maadili mema na kwa  kuhamasisha hilo kuanzia Shuleni hapo. Mashanda amesema "Yapo mambo kadhaa ambayo yanamfanya mtu awe kiongozi bora, mambo haya yakianza kuzoeshwa mapema huwa tabia na muongozo kwa vijana wetu.

Mashanda alikinukuu Kituo cha utafiti na mafunzo ya uongozi cha Dale Carnegie cha jijini New York nchini Marekani kinachosema katika utafiti wao wamegundua kwamba kinachomfanya mtu awe kiongozi bora sio suti wala sura bali uwezo na nia ya dhati katika kuamsha ari, kuwawezesha unaowaongoza, kuwafanya wajiamini na kuwapa motisha watu unaowaongoza.

Kiongozi bora ni yule anayeweze Kuyakabili Matatizo au ChangamotoKiongozi bora ni yule ambaye ana ujasiri wa kutosha wa kukabiliana na kila aina ya changamoto inaweza kujitokeza kwa busara.""Dunia ya leo imejaa changamoto za kila aina. Kila kukicha kuna jipya na gumu zaidi. Taswira ya uingozi bora inamjenga kijana kujiamini na kujilinda hivyo kuwa sababu ya yeye kukabiliana na changamoto mbalimbali za ujana kwa matumaini."

"Kiongozi bora lazima awe muaminifu. Uaminifu unaanzia kwenye kuwa mkweli. Na hii nitabia inayoanza utototoni.""Kiongozi bora ni yule mwenye uwezo wa kusimamia ahadi yake na jitihada anazofanya kutimiza ahadi yake."

"Kiongozi bora lazima ajiheshimu. Na dhana ya kujiheshimu ni pana. Hii ni pamoja na kuheshimu wazazi wako, ndugu, jamaa  marafiki na watu wote. Unapojiheshimu, inakuwa rahisi kuongoza wengine.":Kiongozi bora huwa anakiu ya kujifunza zaidi na ni mtafiti. Kiongozi bora ni Mtendaji
Yote niliyoyataja hapo yanafundishika."

:Sasa pamoja na masomo mengine Imperial secondary school inamuandaa mwanafunzi wake katika mazingira ya kuyatambua haya na kuyafanyia kazi mapema kipindi awapo shuleni. 'Alisema 'Tunaamini ugeni wa  mama Anne S..Makinda katika mahali yetu utaongeza tija na hamasa kwa kile tulichokuwa tukiwaandaa nacho wanafunzi wetu.
 Baadhi ya wahitimu wa kidato cha nne wakiwa katika picha ya pamoja.
Mgeni Rasmi ambaye ni Spika wa Bunge Mstaafu Anne Makinda  akizungumza katika mahafali ya kwanza ya kidato cha nne Imperial Secondary School (ISS) yaliyofanyika jana Msolwa Chalinze.
 Mgeni Rasmi ambaye ni Spika wa Bunge Mstaafu Anne Makinda akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kusheherekea Mahafari ya kwanza ya kidato cha nne. 
 Mgeni Rasmi ambaye ni Spika wa Bunge Mstaafu Anne Makinda akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa kidato cha nne.
 Mgeni Rasmi ambaye ni Spika wa Bunge Mstaafu Anne Makinda akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu pamoja na wazazi wao katika mahafali ya kwanza ya kidato cha nne.

MAGAZETI YA LEO JAMATATU OKTOBA 22,2018

Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images