Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1702 | 1703 | (Page 1704) | 1705 | 1706 | .... | 1897 | newer

  0 0


   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua  daraja la Chipanga wilayani Bahi, Oktoba 19, 2018. Wapili kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo, Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Bilinith Mahenge, Wanne kushoto ni Mbunge wa Bahi,   Omary Badwel na wapili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Athumani. 
  PMO_8937
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua daraja la Chipanga wilayani Bahi, Oktoba 19, 2018.  Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo na wapili kushoto ni Mbunge wa Bahi,   Omary Badwel. 
  PMO_8972
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akipata maelezo kutoka kwa Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Bahi, Kassim Kolowa  (kushoto) kuhusu vifaa vilivyopo kwenye chumba cha upasuaji cha Kituo hicho  wakati alipokitembelea, Oktoba 19, 2018. Wapili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Athumani. 
  PMO_08993
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na  Bibi Subi Mchome, ambaye ni mmoja wa wazazi waliojifungua salama katika wodi ya wazazi ya Kituo cha Afya cha Bahi  mkoani Dodoma, Oktoba 19, 2018. Wapili kushoto ni Mganga Mkuu wa Kituo hicho, Kassim Kolowa.
  PMO_9027
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mtalaam wa Maabara, Petronila Olomi  (kushoto) wakati alipotembealea Maabara ya Kituo cha Afya cha Bahi mkoani Dodoma, Oktoba 19, 2018. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) , Selemani Jafo na Wapili kushoto ni Mganga Mkuu wa Kituo hicho, Kassim  Kolowa.
  PMO_9040
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wagonjwa wa nje wakati alipotembelea Kituo cha Afya cha Bahi mkoani Dodoma, Oktoba 19, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  PMO_9061
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo orodha ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi ambao bado hawajahamia Bahi na wananishi mjini  Dodoma licha ya serikali kuwataka wahame, ili awachukulie hatua. Alikuwa katika kikao na Watumishi wa Halmashuri hiyo, Oktoba 19, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  PMO_9070
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Bahi kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa  wilaya hiyo, Oktoba 19, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  PMO_8865
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoka  katika moja kati ya nyumba sita za walimu alizozikagua katika Shule ya Sekondari ya Mpalanga wilayani Bahi, Oktoba 19, 2019. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Bahi, Mwanahamisi  Athumani. 
  PMO_08886
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiwasalimia wananchi baada ya kukagua ujenzi wa nyumba sita za walimu katika shule ya Sekondari ya Mpalanga wilayani Bahi, Oktoba 19, 2018. 
   

  0 0

  4
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars ambao walifika Ikulu jijini Dar es Salaam pamoja na Viongozi wa Shirikisho la Miguu la Tanzania TFF, BMT pamoja na Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo. 
  7
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Tanzania Taifa Stars mara baada ya kuzungumza nao Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha mstari wa Mbele ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe watatu kutoka kushoto, Waziri wa Mambo ya Nje Balozi Dkt. Augustine Mahiga watatu kutoka kulia akifatiwa na Leodgar Tenga Mwenyekiti wa BMT, kocha wa timu ya Taifa Emanuel Amunike Pamoja na Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao. Wengine ni Rais wa TFF Wallace Karia akiwa pamoja na Nahodha wa Timu ya Taifa Erasto Nyoni.
  8
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Nahodha wa Timu ya Taifa Erasto Nyoni mara baada ya kupiga picha ya pamoja na Timu ya Taifa Ikulu jijini Dar es Salaam.
  9
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Kipa wa Timu ya Taifa Aishi Manula mara baada ya kupiga picha ya pamoja Ikulu jijini Dar es Salaam.
  10
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Beki kisiki wa Taifa ya Tanzania Kelvin Yondani mara baada ya kupiga picha ya pamoja Ikulu jijini Dar es Salaam
  11
  Beki wa Timu ya Taifa Shomari Kapombe akijitambulisha mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
  13..13
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea zawadi ya Jezi ya Timu ya Taifa kutoka kwa Nahodha wa Timu hiyo Erasto Nyoni Ikulu jijini Dar es Salaam.
  14
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Nahodha wa Timu hiyo Erasto Nyoni mara baada ya kumkabidhi Jezi ya Timu ya Taifa.
  16
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwakabidhi Shilingi milioni 50, Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe pamoja na viongozi wa TFF ili zitumuke katika maandalizi ya mechi inayokuja ya kuwania kufuzi AFCON nchini Cameroon. Wengine katika picha ni Rais wa TFF Wallace Karia, Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao pamoja na Nahodha wa Timu ya Taifa Erasto Nyoni.
  15
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo mara baada ya kukabidhi Shilingi milioni 50 kwa TFF kwa ajili ya Maandalizi ya  Timu ya Taifa Ikulu jijini Dar es Salaam.PICHA NA IKULU

  0 0


  Wafanyakazi wa Jumuiya ya kuwasaidia na kuwaenzi wazee wasiojiweza (JUKWAUPE) wakiwa katika Kijiji cha Fumba kwa ajili ya kutoa msaada kwa wazee wasiojiweza wa kijiji hicho  Katibu Mkuu wa Jumuiya ya kuwasaidia na kuwaenzi wazee wasiojiweza (JUKWAUPE) Khamis Mussa Juma akimkabidhi msaada Mohammed Hassan Shoka.  Katibu Mkuu wa Jumuiya ya kuwasaidia na kuwaenzi wazee wasiojiweza Khamis Mussa Juma akimkabidhi msaada Fatma Shani Ameir.  Msaidizi Fedha wa Jumuiya ya kuwasaidia na kuwaenzi wazee wasiojiweza (JUKWAUPE) Ramadhan Ali Juma akimkabidhi msaada Maryam Mataka Mohammed.  Msaidizi Fedha wa Jumuiya ya kuwasaidia na kuwaenzi wazee wasiojiweza (JUKWAUPE) Ramadhan Ali Juma akimkabidhi msaada Amana Kombo Khamis wa Bweleo.  Mjumbe wa Jumuiya ya kuwasaidia na kuwaenzi wazee wasiojiweza (JUKWAUPE) akimkabidhi msaada Mwashamba Gharib Mkame katika hafla iliyofanyika Fumba.

  Picha Na Miza Othman Maelezo- Zanzibar.

  ……………………….

  Na Kijakazi Abdalla ,Maelezo

  JAMII imetakiwa kuwatunza na kuwaenzi wazee wasiojiweza ili wajione kuwa ni sehemu ya jamii inayohitaji matunzo na kuondokana na upweke baada ya mchango mkubwa waliotoa wakati wa ujana wao.

  Akizungumza katika hafla ya kuwafariji wazee wasiojiweza katika vijiji vya Fumba na Bweleo, Katibu wa Jumuiya ya Kuwasaidia Wazee wasiojiweza (JUKWAUPE) Khamis Mussa alisema wazee wanayokila sababu ya kusaidiwa kutokana na juhudi zao katika maendeleo ya Taifa .

  Alikumbusha kuwa malipo yanayotokana na kuwasaidia wazee ni makubwa mbele ya Allah na amewashauri wananchi kuwa karibu nao ili kujenga upendo na kujihisi kuwa bado wanathamani ndani ya jamii wanazoishi.

  Alisema kuwa lengo la kuanzisha jumuiya JUKWAUPE ni kutafuta misaada kutoka kwa wasamaria wema na kuifikisha kwa wazee hasa huduma muhimu za chakula, nguo na huduma ya afya.

  Alieleza kuwa Jumuiya hiyo imejikita zaidi kusaidia wazee wasiojiweza wenye umri kuanzia miaka 80 wanaoishi vijijini ambao mara nyingi wanashindwa kukidhi mahitaji yao ya lazima katika maisha.

  Sheha wa Shehiya ya Bweleo Mataka Ame Mataka aliishukuru jumuiya hiyo kwa msaada walioutoa na kuzitaka jumuiya nyengine kuiga mfano kama huo wa kuwasaida wazee kwani kutoa ni moyo .

  Aidha alizitaka Jumuiya nyengine zenye nia ya kutoa msaada hasa wa chakula na dawa kutoa taarifa katika taasisi husika kuhakikisha usalama wa msaada huo na kuepuka usumbufu wanapofika vijijini.

  “Kuna baadhi ya Jumuiya huenda katika vijiji kwa lengo la kutoa msaada lakini wanashindwa kufuata taratibu na hatimae kupata usumbufu usiowalazima,’’ alikumbusha Sheha Mataka.

  Wazee waliopatiwa msaada huo wameishukuru JUKWAUPE na kuwataka kuendelea kuwasaidia kila hali itakaporuhusu ili wajihisi kuwa bado wanajaliwa na kuthaminiwa.

  0 0   Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso akizungumza na wananchi wakati wa kukabidhi miradi ya maji ya Charambe na Kibonde maji Jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya hatua zinazochukuliwa katika kuimarisha huduma hiyo kwa wananchi.
  2
  Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso akikata utepe kuzindua miradi ya maji Charambe na Kibonde maji Jijini Dar es Salaam.
  3
  Afisa Mtendaji mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian  Luhemeja akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi miradi ya maji ya Charambe na Kibonde maji Jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya hatua zinazochukuliwa katika kuimarisha huduma hiyo kwa wananchi.
  4
  Sehemu ya washiriki wa hafla ya kukabidhi miradi ya maji ya Charambe na Kibonde maji Jijini Dar es Salaam wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso  ikiwa ni sehemu ya hatua zinazochukuliwa katika kuimarisha huduma hiyo kwa wananchi.
  5
  Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso akizindua mradi hou Wilayani Temeke Jijini Dar es Salaam.
  (Picha zote na DAWASA)
  ………………………..


  Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso ameikabidhi DAWASA miradi miwili ya majisafi na usafi wa mazingira yenye thamani ya milioni 500 na inahudumia wananchi wasiopungua 160,133 lengo likiwa kuwafikia wananchi 280,000 katika Wilaya ya Temeke.

  Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa, Naibu Waziri Mhe. Aweso amesema kuwa Serikali inaendelea na jitihada za kuimarisha huduma za maji katika Jiji la Dar es Salaam na maeneo mbalimbali hapa nchini ili kufikia malengo yaliyowekwa kufikia mwaka 2020.

  “Mradi  huu wa majisafi una uwezo wa kuzalisha lita laki 224,000 za maji kwa siku na utahudumia wakazi wa Charambe na Kibonde maji katika Manispaa ya Temeke ambapo wananchi wameanza kuunganishiwa huduma hii ya maji kupitia  Ofisi ya DAWASA Temeke”. Alisisitiza Mhe. Aweso

  Kuanza kwa mradi huu kunasaidia kuondoa changamoto ya upatikanaji wa maji katika maeneo hayo na kuchangia  katika kukuza shughuli za uzalishaji na maenedeo katika maeneo hayo.
  Kwa upande wa mradi wa kuchakata  majitaka Mhe. Aweso amebainisha kuwa mradi huo una uwezo wa kuchakata lita 50,000 za majitaka kwa siku ambapo mradi huo utasaidia upatikanaji  wa mbolea, maji kwa ajili ya umwagiliaji, pamoja na gesi.

  DAWASA imekuwa ikichukua hatua mbalimbali katika  kuimarisha huduma zake ikiwemo kudhibiti uvujaji wa maji na kuweka mtandao mpya katika maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma ya majisafi na salama.

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi.Dorothy Mwaluko akizungumza na Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu waliohudhuria kikao kazi kilichofanyika ukumbi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini Dodoma.
  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro (katikati mstari wa mbele), akifuatilia moja ya mada zilizowasilishwa katika kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu kilichofanyika ukumbi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini Dodoma.Kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi.Dorothy Mwaluko na kuli kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma Bw.Mathew Kirama.
  Baadhi ya Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu serikalin wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi.Dorothy Mwaluko (hayupo pichani) wakati akifunga kikao kazi cha watendaji hao kilichofanyika ukumbi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini Dodoma.
  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini Dodoma.

  …………………………………………………………………………………..

  Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu kutoka katika Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala, Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mashirika ya Umma wametakiwa kuhakikisha wanawahudumia vema watumishi wanaowasimamia ili kuwajengea ari ya utendaji kazi kwa watumishi hao.

  Wito huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Dorothy Mwaluko wakati akifunga kikao kazi cha siku mbili cha Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu serikalini kwa niaba ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro kilichofanyika ukumbi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini Dodoma.

  Bi. Mwaluko amewasisitiza Watendaji hao, kutojifanya miungu watu na badala yake wawahudumie watumishi wote kwa kuzingatia weledi, kauli nzuri na bila chuki ya aina yoyote. Bi. Mwaluko amewaelekeza watendaji hao, kuwahudumia vizuri Watanzania hususani wanyonge kama ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli anavyosisitiza mara kwa mara.

  Naye, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza na waandishi wa habari, amesema mkutano huo ulikuwa na lengo la kuwaelimisha watendaji hao masuala ya kiutawala na usimamizi wa rasilimaliwatu ili waweze kutimiza majukumu yao kikamilifu kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo ya kiutumishi. Dkt.Ndumbaro ameongeza kuwa, kupitia mkutano huo serikali imewasisitiza viongozi hao kuwajibika ipasavyo kwa umma na kwa watumishi walio chini yao.

  Aidha, Dkt.Ndumbaro amewataka viongozi hao kuwaelimisha watumishi wa umma walio chini yao kuhusu umuhimu wa kudai risiti pindi wanapofanya manunuzi ili kuiongezea serikali mapato yatakayoiwezesha kuongeza mishahara na kuboresha maslahi ya watumishi wa umma. Sanjari na hayo, Dkt. Ndumbaro amewashauri watumishi wa umma nchini kujiendeleza kitaaluma katika kada zao waliozoingiliwa katika utumishi wa umma ili elimu watakayoipata iwe na manufaa kwao na tija katika utumishi wa umma.

  Mkutano kazi huo ulihusisha jumla ya washiriki 456 kutoka katika Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala, Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mashirika ya Umma ambao walipata fursa ya kujifunza masuala mbalimbali ya kiutendaji, uendeshaji na usimamizi wa rasilimaliwatu kwa kuzingatia malengo,shabaha na vipaumbele vya kitaifa.

  0 0


   Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) akifafanua jambo wakati wa ziara yake ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano kwenye vijiji mbali mbali vya Wilaya ya Mkuranga. Wa pili kulia ni Mbunge wa jimbo hilo Abdallah Ulega na wa kwanza kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Mhandisi Peter Ulanga
  JPEG. NA. 2
  Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) akimsikiliza kwa makini Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega kuhusu ukosefu wa mawasiliano ya uhakika kwenye eneo hilo. Wa kwanza kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote Mhandisi Peter Ulanga
  JPEG. NA. 3
  Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (mstari wa mbele katikati) akikagua upatikanaji wa mawasiliano kwenye kata ya Mkamba Wilayani Mkuranga. Wa kwanza kushoto mbele ni Mbunge wa Jimbo hilo Abdallah Ulega
  …………………………………………………………………………….
  Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amefanya ziara ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano kwenye Wilaya ya Mkuranga iliyopo mkoa wa Pwani na kuahidi wananchi kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaongeza mawasiliano kwenye Wilaya hiyo ambayo ina viwanda vingi vyenye uwekezaji wa aina mbali mbali
  Amesema kuwa katika ziara yake amebaini kuwa yapo baadhi ya maeneo ambayo yanahitaji kuongezewa nguvu ili mawasiliano yaweze kufika eneo kubwa zaidi na kupeleka mawasiliano kwenye baadhi ya maeneo ambayo yana ukosefu wa mawasiliano kwenye Wilaya hiyo kwa kuwa mawasiliano ni maendeleo, uchumi na ulinzi na usalama.
  Amefafanua kuwa, “kimsingi mawasiliano yapo Mkuranga ila tunatakiwa kuongeza nguvu ili wananchi wapate mawasiliano. Tunahitaji wananchi wa Tanzania wawasiliane,” amesema Nditiye. Ameongeza kuwa minara iliyopo inaweza kuongezwa nguvu, kampuni nyingine zitafunga mawasiliano kwenye minara ya kampuni nyingine zilizopo na kujenga minara kwenye maeneo ambayo hayana mawasiliano kabisa.
  Nditiye amemshukuru Ulega na kuwapongeza wananchi wa Tanzania kwa kuonyesha uhitaji wa mawasiliano na wamegundua mawasiliano ni maendeleo yao, uchumi, ulinzi na usalama. Amesema kuwa karibu asilimia 60 ya eneo la Mkuranga halina mawasiliano na ameyataka makampuni ya simu yaliyojenga minara kwenye Wilaya ya Mkuranga kuongeza nguvu ya mawasiliano kutoka teknolojia ya 2G hadi teknolojia ya 4G.
  Naye Mbunge wa Jimbo la Mkuranga, Mhe. Abdallah Ulega ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi amesema kuwa Mkuranga haina mawasiliano ya uhakika, kuna shida kubwa sana ya mawasiliano.  “Tumefanya ziara ya kuja kuona hali halisi ya upatikanaji wa mawasiliano kwenye Wilaya ya Mkuranga ya upatikanaji wa mawasiliano ya uhakika, baadhi ya vijiji havina mawasiliano ya uhakika na wengine hawana mawasiliano kabisa na eneo hili lina wawekezaji wengi wa viwanda na mawasiliano yanawawezesha wananchi kutoa taarifa za masuala ya ulinzi na usalama”, amesema Ulega. Ameyataja maeneo hayo kuwa vijiji vilivyopo kwenye kata ya Mkuranga, Mpeko, Tengelea, Bupu, Kimanzichana, Kisegese, Mkamba, Lukanga, Magawa, Msonga, Dondo, Vikindu na kata ya Mbezi.
  Akijibu kiu ya wananchi waliojitokeza wakati wa ziara hiyo, Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Mhandisi Peter Ulanga akiwa kwenye ziara hiyo amesema kuwa UCSAF ilikuwa inaangalia Wilaya ya Mkuranga kwa muda na eneo lote la Mkuranga wataliangalia ili liweze kupata mawasiliano. “Serikali inaangalia mawasiliano kama dhana ya mkakati wa maendeleo ya wananchi kiuchumi, ndani ya kipindi cha mwaka mmoja tutakuwa tumefikisha mawasiliano ya uhakika kwenye vijiji vyote” amesema Ulanga. Ameongeza kuwa Mkuranga ina kata 25 na tumeona bado kuna matatizo ya mawasiliano ambapo katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2018/2019, UCSAF itapeleka mawasiliano kwenye kata 100 zilizopo kwenye maeneo mbali mbali nchini ambapo watatoa kipaumbele kwenye kata za Mkuranga ambapo kuna uwekezaji mkubwa
  Naye Meneja wa Kampuni ya Simu ya Vodacom wa Wilaya ya Mkuranga, Godfrey Kamage amesema kuwa, “tumepokea maoni ya wananchi na maelekezo ya Serikali, tutafikisha hili makao makuu ya Vodacom ili kuongeza nguvu ya mawasiliano kutoka 2G hadi 3G na yaweze kufika mbali zaidi,”.

  0 0

  *Apatikana baada ya waliomteka kumtupa viwanja vya Gymkhana Dar
  *Waliomteka inadaiwa walikuwa wanaongea lafudhi ya South Afrika
  *MO mwenyewe awashukuru Watanzania kwa dua zao kwake

  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  MFANYABIASHARA maarufu Mohammed Dewji 'MO' aliyekuwa ametekwa akiwa katika Hoteli ya Collessium jijini Dar es Salaam hatimaye amepatikana akiwa mzima na mwenye afya njema.

  Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amethibitisha kupatikana kwa MO ambapo anasema yeye amemuona na amezungumza naye akiwa mzima na tayari ameungana na familia yake.

  Kamanda Mambosasa akifafanua zaidi leo jijini Dar es Salaam amewaambia Watanzania, MO alitupwa viwanja vya Gymkhana usiku wa kuamkia leo wa Oktoba 20 mwaka huu."Baada  ya kutekwa tarehe Oktoba 11,2018 gari ya watekaji iliendeshwa speed takribani dakika 15 na kuwekwa kwenye chumba akiwa amefunikwa  ili asiwatambue watekaji."

  Amesema kwa mujibu wa MO ni kwamba watekaji hao walikuwa wakiongea lugha za Afrika Kusini na hivyo inathibitisha waliomteka hawakuwa Watanzania na kinachoendelea Polisi nao wanaendelea kukamilisha taratibu za kiuchunguzi.

  Mambosasa amesema kuwa MO kwa siku zote ambazo alikuwa anashikiliwa na watekaji alikuwa kwenye mazingira magumu lakini wanashukuru amepatikana akiwa salama kwani kwa kipindi chote Jeshi la Polisi lilikuwa likihangaika kuhakikisha anapatikana na kweli amepatikana.

  Ameongeza kupitia upelelezi wao walipata taarifa MO ametupwa maeneo ya Gymkhana na hivyo baada ya kupata taarifa hizo yeye pamoja na maofisa wake wa upelelezi wamefika nyumbani kwa mfanyabiashara huyo ambaye ameungana na familia yake.

  Hata hivyo Mambosasa alimuomba MO kama hatojali kuzungumza ili Watanzania waweze kumuona na kumsikia ambapo alimpa nafasi ya kusalimia.Kwa upande wake MO amesema kuwa anawashukuru Watanzania wote na katika shukrani hizo ameanza kwa kumshukuru Rais Dk.John Magufuli na kisha akatoa shukrani kwa Jeshi la Polisi kutokana na jitihada zao za kuhakikisha anapatikana.

  "Ahsante wote na nawashukuru Watanzania wote ,nipo salama," amesema MO Dewji akiwa nyumbani huku Mambosasa akiwataka Watanzania kuendelea kuwa watulivu.Kwa kukumbusha tu Mo alitekwa Oktoba 10 mwaka huu saa 11 asubuhi baada ya kufika kwenye hoteli ya Collessium kwa ajili ya mazoezi ambapo kabla ya kushuka kwenye gari yake watekaji walimteka na kuondoka naye kwenye gari aina ya Toyota Suff na kisha kwenda kusikojulikana.

  Hata hivyo Polisi waliamua kuweka mikakati ya kuhakikisha MO anapatikana.Wakati wakiendelea na upelelezi wao jumla ya watu 27 waliwashikilia kwa mahojiano lakini hadi jana walikuwa wamebaki na watu nane.

  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro wakati anazungumza jana asubuh na waandishi wa habari alisema jeshi hilo halijalala tangu MO alipotekwa kwani wanaendelea kufuatilia na kukusanya taarifa ambazo zitafanikisha kupatikana kwake.

  IGP Sirro pia alionesha picha ya gari ambayo ilihusika katika tukio la kutekwa MO pamoja na risasi mbili ambazo zilikuwa eneo la tukio ambazo nazo walizichukua kwa ajili ya uchunguzi ambapo aliwahakikishia Watanzania jeshi lao la Polisi liko imara na linafanyakazi zake kwa weledi.
  Mfanyabiashara Mo Dewji amepatika. Waziri January Makamba amesema kuwa amemuona na kuongea nae kwa kirefu, ni mzima wa afya isipokuwa ana alama za kufungwa kamba mikononi na miguuni. Ameongeza kuwa, majira ya saa nane za usiku, watekaji walimtupa kwenye viwanja vya Gymkhana, Dar.


  0 0


  Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na viongozi wa mkoa wa Morogoro na baadhi ya watumishi wa Mkoa huo hawako pichani kuhusu madhumni ya kuanza ziara ya siku tatu mkoani humo pia kupokea taarifa ya masuala ya Afya na Maendeleo ya Jamii ya Mkoa jana huo.
  2
  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akitoa ufafanuzi wa hali ya maendeleo sekta Afya na Maendeleo ya Jamii ya Mkoa wa Morogoro kwa  Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile kabla ya Waziri huyo kuanza ziara ya siku tatu Mkoani humo .
  3
  Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Frank Jackob akitoa taarifa ya Mkoa wa Morogoro kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alipotombelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kupata taarifa ya Mkoa huo kabla ya kuanza ziara yake ya siku tatu  Mkoani humo.
  4
  Baadhi ya watumishi wa Mkoa wa Morogoro wakifuatilia kwa makini maelezo na maagizo ya Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alipotembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo kabla ya kuanza ziara ya siku tatu Mkoani humo.
  Picha Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
  ………………………………………………………………………..
   Na Mwandishi wetu- Morogoro
  Serikali imetaka  wazazi,walimu wakuu,watendaji wa kata na vijiji pamoja wale wote watakaousika na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto au kumpa mimba mwanafunzi kuwajibiswa kwa kusababisha watoto wa kike kushindwa kumaliza masomo yao na kusababisha wasichana walio mashuleni kushindwa kutimiza ndoto zao.                                                                                                          
  Hayo yalisemwa jana na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile alipofanya ziara Mkoani Morogoro kupata taarifa ya Mkoa huo kwa lengo la kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa masuala Afya na Maendeleo ya Jamii Mkoani humo.
  Akizungumzia hali hiyo Naibu Waziri Ndugulile alisema kiwango cha matukio haya ni kikubwa mno na kuagiza Mkoa huo kuanzisha Madawati ya Ulinzi na Usalama ya Wanawake na Watoto pamoja na vituo vya mkono kwa mkono (One Stop Centres) akisistiza kuwa haya ni maagizo ya serikali kama sehemu muhimu ya kupambana na vitendo vya ukatili nchini. 
  “Vituo hivi kwa nchi nzima ni kumi kwa hiyo akikisheni mnaanzisha Vituo hivi katika Mkoa wa Morogoro kwa kuwa ili ni agizo la serikali katika kuakikisha tunatokomeza vitendo vya ukatili”. Aliongeza Dkt.Ndugulile.
  Akisoma taarifa ya Mkoa huo kwa Naibu Waziri Ndugulile, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Frank Jacob alisema kuwa mkoa wa Morogoro una jumla ya matukio 2,555 ya mimba za utotoni akiyataja matukio 1,160 kuripotiwa kutoka Dawati la Polisi mengineyo 895 kulipotiwa katika vituo vya Afya, mashuleni na jamii.
  Aidha taarifa ya Mkoa kwa Naibu Waziri Ndugulile pia ilisema Mkoa wa morogoro una jumla ya kesi 268 zilizo mahakamani kuhusiana na vitendo vya ukatili lakini ni kesi 38 tu ambazo mashauri yake yametolewa hukumu lakini pia Mkoa huo una jumla ya matukio ya ukatili wa kijinsia 1,482 na kati ya matukio hayo watoto walioteandewa ukatili ni 819.
  Aidha taarifa ya hali ya mkoa kuhusiana na vitendo vya ukatili iliyotolewa kwa Naibu Waziri Ndugulile imeutaja mkoa huo kuwa na idadi ya watoto 43.5 elfu walio katika mazingira hatarishi yakipelekea uwapo wa mashauri  mbalimbali ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake  na watoto katika sehemu mbalimbali za mkoa huo.
  Naibu Waziri Ndugulile yupo Mkoani Morogoro kwa ziara ya siku tatu kuangalia hutoaji huduma za maendeleo ya Jamii lakini pia masula ya Afya ambapo alitembelea na kukagua makoa ya wazee funga funga, mradi wa umwagilia wa kikiji cha Wami Luiwindo Dakawa Wilayani Mvomero na kukagua hospitali za Mkoa na Wilaya.

  0 0


  Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack akiliangalia gari alilokabidhiwa kwa ajili ya Jeshi la Polisi wilayani Kishapu.
  Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack akitoa maelekezo na kumkabidhi funguo na kadi ya gari Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD) ya Kishapu, Emmanuel Galiyamoshi. Anayeshuhudia kushoto ni Alchelaus Mutalemwa.
  Sehemu ya maafisa wa Jeshi la Polisi wilayani Kishapu wakinyakua baada ya kushuhudia makabidhiano ya gari.


  Na Robert Hokororo, Kishapu

  Jeshi la Polisi Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga limepokea gari jipya kwa ajili ya matumizi ya shughuli zake kutoka mgodi wa almasi wa Mwadui.

  Gari hilo aina ya Nissan Hilux lenye thamani ya sh. milioni 80 limepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack ambaye alikabidhi jeshi hilo.

  Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya gari hilo yaliyofanyika wilayani humo Mhe.Telack aliushukuru mgodi kwa msaada huo. Telack ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa alisema kuwa gari litawezesha shughuli za Polisi kufanyikaa kwa ufanisi.

  Aliwaomba wasichoke kuendelea kuisaidia Kishapu pamoja na kushirikiana na Serikali ya wilaya hiyo kwani wao pia ni sehemu ya jamii hiyo. Aidha alilitaka jeshi hilo kulitumia gari hilo walilokabidhiwa kwa matumzi yaliyokusudiwa ya kulinda wananchi ili waendelee kuwa na imani nalo.

  0 0


   Ujenzi wa mradi wa maji wa Chipingo-Mkaliwata, wilayani Masasi katika mkoa wa Mtwara ukiendelea.
  1
  Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akitoa msisitizo kwa Jumanne Mackenzie, mkandarasi kutoka Kampuni ya Singilimo Enterprises Ltd akamilishe mradi wa maji wa Makong’onda, uliopo katika Wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara.
  3
  Mkurugenzi Mtendaji wa MANAWASA, Mhandisi Nuntufye David akiwa na Waziri wa Maji,  Makame Mbarawa kwenye chanzo cha maji cha Mbwinji.
  4
  Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akitoka kukagua chanzo cha maji cha Kisimani Newala kilichopo katika Wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara.
  5
  Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akikagua maendeProfesaleo ya ujenzi wa mradi wa maji wa Chipingo-Mkaliwata, wilayani Masasi katika mkoa wa Mtwara
  ………………………
  Serikali imewekeza takribani kiasi cha Shilingi Bilioni 45 kwenye miradi ya maji mkoani Mtwara kwa lengo la kufikisha huduma ya maji mkoani humo kwa asilimia 100.
  Akizungumza akiwa ziarani katika Wilaya ya Masasi, Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa Ilani ya Chama cha Mapinduzi inataka ifikapo mwaka 2020 upatikanaji wa huduma ya maji nchini uwe kwa kiwango cha asilimia 95 mijini, asilimia 90 kwenye miji mikuu ya wilaya na asilimia 85 vijijini.
  Profesa Mbarawa amesema ili kufikia lengo hilo mpaka sasa Serikali imetenga Shilingi Bilioni 45 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji 37 kwenye mkoa wa Mtwara pekee, ambapo mpaka sasa imeshalipa kiasi cha Shilingi Bilioni 25 na Shilingi Bilioni 20 iliyobaki italipwa kwa kadiri hati za malipo zitakapokuwa zinafika wizarani.
  Amezungumza hayo mara baada ya kukagua miradi ya maji ya Makong’onda, Chipingo-Mkaliwata na kutembelea chanzo cha maji kinachotumiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Masasi-Nachingwea (MANAWASA).
  Profesa Mbarawa amesema kwa sasa mkoa wa Mtawara una jumla ya miradi 37 inayotekelezwa na 4 kati ya hiyo imekamilika, mingine ikiwa katika hatua mbalimbali za utekelezaji na kuahidi itakamilika kwa wakati ili kumaliza tatizo la upatikanaji wa maji kwa wakazi wa mkoa huo.
  Amesisitiza kuwa maeneo mengi Mtwara kuna vyanzo vya maji vya kutosha, ukiacha Wilaya ya Nanyumbu ambapo upatikanaji wa vyanzo vya uhakika ni chanamoto. Kikubwa kinachotakiwa ni usimamizi mzuri wa wakandarasi waliopewa kazi na wahandisi wanaosimia ujenzi wa miradi hiyo na kutunza vyanzo vya maji vilivyopo viweze kuwa endelevu.
  Vilevile, Profesa Mbarawa amesema suluhisho la tatizo la maji katika Wilaya ya Nanyumbu ni ujenzi wa mabwawa, na hivi karibuni wataanza ujenzi wa mabwawa matatu kama mpango wa muda mfupi, wakati mpango wa muda mrefu ni kutumia mradi wa Makonde kwa kujenga matenki ya maji kwa ajili ya kusambaza maji katika wilaya hiyo.
  Aidha, amekuwa Waziri wa Maji wa kwanza kufika Kijiji cha Mkwaya na kuwatoa hofu ya upatikanaji wa maji baada ya kumtaka mkandarasi kutoka Kampuni ya Singilimo Enterprises Ltd awe amekamilisha mradi wa Makong’onda ifikapo mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu, vinginevyo atamfukuza endapo atashindwa kuukamilisha.
  Wakazi wa Kijiji cha Mkwaya kilichopo Kata ya Makong’onda wamesema kukamilika kwa mradi huo kutaleta faraja kubwa kwa kuwa huduma ya maji inapatikana, ila kiwango chake bado hakitoshelezi mahitaji.


  0 0


  0 0  Kundi la Rostam linalowashirikisha wasanii wawili Roma na Stamina jana walipanda jukwaani kuimba pamoja na msanii Maua Sama wimbo unaotamba kwa sasa ujulikanao kama IOKOTE kwenye Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote lililofanyika uwanja wa Majengo mjini Moshi.

  Tukio hilo liliwafanya mashabiki walipuke kwa shangwe kwa namna wasanii wote watatu walivyokuwa wakiiimba kwa pamoja na kufanya kionjo cha aina yake na kwa ubunifu mkubwa.Hii ilitokea kabla Maua hajashuka jukwaani ndipo Rostam walipovamia jukwaa na kuimba wote, Na mara baada ya kuimba wimbo huo, wakamalizia kuimba wimbo mwingine walioshirikishana uitwao Kibamia.

  Tamasha hili likiwa limemaliza mkoa wa sita usiku wa kuamkia jana, baada ya kupita mikoa ya Morogoro,Rukwa,Iringa,Songea,Mtwara na Kilimanjaro.
  Wasanii mbalimbali walinogesha tamasha hilo wakiwemo Weusi, Chege, Nandi, Me. Blue,Chin Beez, WhoZu, Rosa Ree, Mavoko na wengine.

  Kwa upande wa shindano la kutafuta wasanii wenye vipaji Tigo Fiesta Supa Nyota, msanii anayechipukia, Samson Msweta maarufu kama Samson Classic aliibuka kidedea na atauwakilisha mkoa Kilimanjaro kwenye fainali za Tigo Fiesta Supa Nyota mwaka huu jijini Dar es salaam.

  Nao Wadhamini wa Tamasha hilo Kampun ya Tigo, Mkurugenzi wa Kanda ya Kaskazini, Nancy Bagaka alisema ‘Mbali na muziki, wateja wa Tigo pia wanaweza kuvuna hadi mara mbili ya thamani kwa vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia *147*00#. Promosheni ya Data Kama Loteitahakikisha kuwa mashabiki wanaweza kufuatilia habari na matukio yote ya msimu wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote; au kufurahia kuperuzi kwenye mtandao wenye kasi zaidi wa 4G+,’ Bagaka alisema.

  Wateja wote wa Tigo pia wanaweza kuvuna hadi TSH 10 millioni, zawadi za kila wiki za TSH milioni moja, ama zawadi za kil asiku za TSH 100,000 kwa kushiriki katika shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo. Ushiriki katika shindano hilo unapatikana kwa kutuma neno MUZIKIkwenda 15571 au kwa kutembelea tovuti ya http://tigofiesta.co.tz
   
   Tamasha hilo litaendelea jumapili hii kwenye uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga

  Wenyewe wanajii ROSTAM,Roma na Stamina wakionesha umahiri wao wa kughani kwenye jukwaa la tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote lililofanyika uwanja wa Majengo mjini Moshi usiku wa kuamkia jana.
  Msanii Rapa Rosa Ree akiimba kwa staili ya kufokafoka kwenye Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote lililofanyika uwanja wa Majengo mjini Moshi usiku wa kuamkia jana.
  Mmoja wa wasanii mahiri anaekuja kwa kasi katika anga za muziki wa kizazi kipya Maua Sama akitumbuiza mbele ya wakazi wa jiji la Tanga waliojitokeza kwa wingi katika tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote lililofanyika uwanja wa Majengo mjini Moshi usiku wa kuamkia jana.

  Msanii Richie Mavoko akiimba mbele ya mamia ya washabiki na wapenzi wa tamasha la Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote lililofanyika uwanja wa Majengo mjini Moshi usiku wa kuamkia Jana.
  Msanii Nandy akionesha jinsi gani anaweza kuteka mashabiki kwa namna alivyokuwa anaimba nao kwenye Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote lililofanyika uwanja wa Majengo mjini Moshi usiku wa kuamkia Jana.
  Msanii Nandy akionesha jinsi gani anaweza kuteka mashabiki kwa namna alivyokuwa anaimba nao kwenye Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote lililofanyika uwanja wa Majengo mjini Moshi usiku wa kuamkia Jana.

  0 0

  *Atangaza msako mkali kuwasaka watekaji,agusia walivyotaka kuchoma gari kupoteza ushahidi 
  *Silaha ya kivita,bastola zakutwa ndani ya gari ya watekaji ,atoa onyo kali


  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  JESHI la Polisi nchini limesema baada ya mfanyabiashara maarufu Mohammed Dewji 'MO' kupatikana, kwa sasa linaendelea na uchunguzi na msako mkali kuwakamata watekaji.

  Akizungumza mchana huu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Simon Sirro amewaambia Watanzania leo kupitia vyombo vya habari kuwa MO yupo salama na kwa sasa wao ndio uchunguzi kama umeanza upya kubaini watekaji na lazima wapatikane aidha wakiwa hai au wamekufa.

   Amesema wametoa taarifa za tukio hilo kwa nchi jirani,hivyo waliohusika na utekaji huo wajue hawana pa kukimbilia kwani kokote watakaoenda watapatikana tu.

  Pia amesema watekaji hao baada ya kumtupa mfanyabiashara huyo katika viwanja vya Gymkhana barabara ya ya Ghana jirani na Ubalozi wa Denmark walitaka kulichoma moto gari waliyoitumia yenye namba za usajili T 314 AXX lakini kwenye vioo vya pembeni kukiwa na namba za usajili AGX 404 MC yenye rangi ya blue nyeusi na ufito wa rangi ya shaba kwa chini kwa lengo la kupoteza ushahidi lakini hawakufanikiwa.

  "Jeshi la Polisi linaendelea na msako kuhakikisha waliokuwa wamemteka mfanyabiashara huyo wanapatikana," amesema IGP Sirro na kusisitiza Jeshi la Polisi litahakikisha linafanikiwa kuwapa wahusika wa tukio hilo.

  NAMNA MO ALIVYOPATIKANA 

  IGP Sirro amesema kutokana na tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara huyo maarufu Alhamisi ya Oktoba 10 mwaka huu ,anaufahamisha umma kuwa MO amepatikana akiwa mzima wa afya usiku wa kuamkia Oktoba 20 baada ya kutekelezwa na watekaji eneo hilo la Gymkhana.

  Amesema taarifa za awali zinaeleza kuwa baada ya kutekwa mfanyabiashara huyo alifungiwa kwenye nyumba ambayo bado haijajulikana na kufungwa miguu na mikono huku wakimziba macho.

  Ameongeza uchunguzi wa awali umebaini kuwa watekaji hao walitumia gari aina ya Toyota Surf yenye namba za usajili T 314 AXX lakini kwenye vioo vya pembeni ilikuwa na namba AGX 404 MC yenye rangi ya blue nyeusi.

   ATOA PONGEZI KWA SERIKALI, MO ,WANANCHI

  Wakati huo huo IGO Sirro ametoa pongezi kwa Serikali,vyombo vya ulinzi na usalama, familia ya Mohamed Dewji ,waandishi wa habari na wananchi wote kwa ushirikiano mkubwa walioutoa katika kipindi chote ambacho mfanyabiashara huyo alikuwa ametekwa kwa jitihada walizofanya hadi kufanikiwa kumpata.

  "Ninawaomba muendelee kushirikiana nasi kwa kutupatia taarifa zitakazowezesha kupatikana kwa watuhumiwa wote wa tukio hili ili wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.Bahati nzuri watuhumiwa wamelitelekeza gari walilotumia kutekeleza azma yao mita chache kutoka eneo alipotelekezwa mfanyabiashara huyo.

  " Ukaguzi wa kina wa gari hilo umefanyika na umewezesha kupatikana kwa bunduki aina ya AK 47 moja na risasi zake 16 ,bastola aina ya Glock 19 ikiwa na risasi 13, bastola aina ya P.Bereta ikiwa na risasi 3 na Gas Pistol 4.5 mm.Nitaendelea kuwapa taarifa kadri maendeleo ya upelelezi yatakavyokuwa yakipatikana,"amesema Sirro.

  NAMNA MO ALIVYOOMBA MSAADA WA ASKARI

  IGP Sirro pia amesema taarifa za kupatikana kwa MO zilitolewa na  askari wa getini katika eneo hilo la  Ghykhana  baada ya MO kumuomba askari huyo kutoa taarifa kwa  familia yake ndipo walipofika eneo hilo.

  "Baada ya kuja katika eneo hilo ndipo walipotujulisha Polisi na hivyo tukafika eneo la tukio na kujiridhisha kupatikana kwa mfanyabiashara huyo Dewji."Ilikuwa saa saba usiku  maeneo ya Gymkhna  gari iliyohusika na utekaji huo lilitelekezwa aina ndani yake likiwa na mfanyabiashara Mohamed Dewji," amesema.


  MAZUNGUMZO KATI YAO NA MO

  Pia IGP Sirro amesema baada ya kufanya mazungumzo na Mo Dewji amewaeleza waliomteka walikuwa wanazungumza lugha ya kingereza na mmoja lugha ya Kiswahili cha hovyo.

  Kwa mujibu wa kamanda sirro amesema Mo aliwaeleza kuwa baada ya kumteka walitaka atoe fedha ambapo aliwaeleza yeye alikuwa hana hela na badala yake aliwaeleza awape namba za simu za baba yake.

  Amesema hata walipopewa na za simu za baba yake hawakumpigia kwani  waliogopa mtego wa Polisi.

  ATOA ONYO KALI

  Wakati huo huo IGP Sirro  ametoa onyo kali kwa kikundi cha baadhi ya watu ambao wanaingilia utendaji kazi  wa Jeshi la Polisi kupitia mitandao ya kijamii.

  " Kuna kikundi ambacho chenyewe kipo kwa ajili ya kuingili majukumu ya Polisi.Jamani Polisi wanafanya kazi usiku kucha tena wakipita kukagua katika kila eneo na kwamba wenyewe wamelala na wake zao lakini kazi yao kuingilia kazi za Polisi."amesema  Sirro na kuwaonya wenye tabia hiyo kuacha mara moja.
    Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Simon Sirro alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari kutika viwanja vya Gymkhana,jijini Dar kuhusiana na tukio la kupatikana Mfanyabiashara Mohammed Dewji a.k.a MO

  0 0

  Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

  WANANCHI wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma wameelezwa kuwa wana kila sababu za kuhakikisha wanakuwa na afya bora na salama, kwani afya ni muhimu na afya ni mtaji mkubwa katika maisha ya binadamu.

  Pia wamehimizwa kupima afya zao kwa lengo la kutambua iwapo wamepatwa na maambukizi ya UKIMWI au laa, kwani kwa atakaepatwa na ugonjwa huo ataanza kutumia dawa ya ARV  na hivyo ataishi maisha marefu.

  Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Kizigo wakati akizungumza na wananchi kuhusu kampeni inayoendelea ya  kupambana  na UKIMWI na kujenga jamii yenye uelewa na furaha.

  Kizigo amesema mbele ya wananchi kuwa Serikali ilianzisha kampeni ya Furaha Yangu iliyozinduliwa kitaifa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kwa Mkoa wa Ruvuma ilizinduliwa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu Agosti  31 mwaka huu 2018

  "Wilaya ya Namtumbo tumeendelea na kampeni hii ikiwa na lengo kuu la kuongeza kiwango cha upimaji wa VVU hasa kwa wanaume na wananchi kwa ujumla. Hadi juzi Oktoba 18 mwaka huu wa 2018 Wilaya ya Namtumbo walipima wanaume 873 na 16 walipatikana na VVU ambao kati yao 13 wameshaanza dozi (ARVs)," amesema.

  Ameongeza kuwa Wilaya ya Namtumbo wameendeleza jitihada hizo kwa kuanzisha ligi ya mpira wa miguu iitwayo Laigwanani Supwr Cup ambapo Laigwanani ni neno la kimasai linalomaanisha Kijana na lengo ikiwa ni kuhamasisha vijana kujitokeza kupima, kujitambua afya zao na watakaokutwa na VVU kuanza dozi mapema.

  Mkuu huyo wa Wilaya amewaambia wananchi hao kwa watakaobainika kuwa na virusi vya UKIMWI dawa zipo na wataishi miaka mingi na kwamba anajua vijana wanaogopa kupima kwa kuhofia njia ambazo wamezipitia.

  Amewashauri wananchi kujitokeza na kupima afya na watambue afya ni mtaji muhimu katika maisha na ndio maana wilaya ya Namtumbo imeona umuhimu wa kampeni hiyo ya kuhamasisha kupima UKIMWI ikaendelea na lengo ni kihakikisha afya za wananchi zinakuwa salama.

  Pia amewashauri kwa wale ambao hawapo ndani ya ndoa wawe waache kujihusisha na ngono zembe na wasubiri hadi watakapoingia kwenye ndoa au wawe na wakishindwa basi wawe na mpenzi mmoja na wawe wanatimia mpira ili kujikinga na maambukizi.

  Kizigo ameongeza ni vema vijana wakatambua wao ni Taifa la leo na kesho na hivyo kujilinda kwa kuwa na afya njema ni jambo la msingi kwani wakiwa na afya njema watakuwa na fursa ya kujituma kwa ajili ya maendeleo yao ,wilaya,mkoa na taifa kwa ujumla.
   
   Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Sophia Kizigo akisalimiana na mmoja wa Marefa watakaokuwa wakichezesha Ligi hiyo ya mpira miguu iitwayo LAIGWANANI SUPER CUP, Lengo ikiwa ni kuhamasisha vijana kujitokeza kupima, kujitambua afya zao na watakaobainika kuwa na maambuziki ya VVU wataanza dozi mapema.

   Pichani Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Sophia Kizigo akisalimiana na baadfhi wachezaji wa timu walioshiriki  ligi ya mpira wa miguu iitwayo LAIGWANANI SUPER CUP, Lengo la kuanzishwa kwa Ligi hiyo ni kuhamasisha vijana kujitokeza kupima, kujitambua afya zao na watakaobainika kuwa na maambuziki ya VVU wataanza dozi mapema.
  Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Sophia Kizigo akikabidhiwa taarifa kutoka kwa Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo,kabla ya kuanza kwa mchezo wa Ligi ya mpira wa Miguu iitwayo LAIGWANANI SUPER CUP.


  0 0

  Na Veronica Kazimoto -Dar es Salaam

  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere amefungua fainali za mashindano ya kumi na moja (11) ya vilabu vya kodi katika Shule za Sekondari za Mikoa ya Dar es salaam na Pwani yaliyofanyika leo katika Chuo cha Usimamizi wa Kodi (ITA) jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza wakati akiwahutubia wanafunzi na wageni waalikwa, Kichere amesema lengo la mashindano hayo ni kuwafundisha wanafunzi uzalendo na kukuza uelewa wao juu ya masuala mbalimbali ya kodi ili waweze kuelewa umuhimu wa kulipa kodi kwa hiari. "Haya mashindano yanafanyika kama sehemu ya kujenga uzalendo kwa wanafunzi wetu ili waweze kuelewa umuhimu wa kulipa kodi na hatimaye waweze kulipa kodi kwa hiari maana tunasema samaki mkuje angali mbichi," alisema Kichere.

  Ameongeza kwa kusema kuwa, "Sisi Mamlaka ya Mapato Tanzania tunasema kwamba elimu ndio kitu muhimu sana kwasababu watu wakielewa umuhimu wa kulipa kodi, tutakusanya kodi nyingi zaidi ambazo hutumika katika kuboresha huduma mbalimbali za jamii kama vile utoaji wa mikopo ya elimu ya juu, utoaji wa elimu bure, uboreshaji wa miundombinu ya elimu ikiwa ni pamoja na ujenzi wa madarasa, mabweni, nyumba za walimu na ununuzi wa vifaa vya maabara na kufundishia."

  Aidha, Charles Kichere amebainisha kuwa, Mamlaka ya Mapato ya Tanzania kwa kushirikiana na taasisi nyingine za serikali inafanya mpango wa kuingiza mtaala wa somo la kodi kuanzia Shule za Msingi hadi vyuoni ili kujenga uzalendo wa kulipa kodi kwa hiari nchini. Mamlaka ya Mapato Tanzania ilianzisha vilabu vya kodi mwaka 2008 na mpaka sasa kuna jumla ya vilabu 226 Tanzania Bara vikiwa na jumla ya wanafunzi 27,250 ambao ni wanachama hai wa vilabu hivyo.

  Mashindano ya mwaka huu yameshindanisha jumla ya shule 50 kutoka Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani ambapo shule 28 zimeingia fainali zikiwa zimegawanyika katika makundi mawili, shule 18 zinashindana katika kujibu maswali wakati shule 10 zinashindana kuwasilisha mada mbalimbali zinazohusu kodi. 
  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere akiwahutubia wanafunzi na wageni waalikwa wakati wa ufunguzi wa fainali za mashindano ya vilabu vya kodi kwa mwaka 2018 wa Shule za Sekondari za Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani uliofanyika katika Chuo cha Usimamizi wa Kodi (ITA) Jijini Dar es Salaam.
  Jopo la majaji likifuatilia na kutoa alama kwa makundi ya wanafunzi wanaojibu maswali mbalimbali yanayohusu kodi wakati wa fainali za mashindano ya vilabu vya kodi kwa mwaka 2018 yaliyofanyika katika Chuo cha Usimamizi wa Kodi (ITA) Jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya Wanafunzi wa shule za Sekondari za Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi ambaye alikuwa ni Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (hayupo pichani) wakati wa fainali za mashindano ya vilabu vya kodi kwa mwaka 2018 yaliyofanyika katika Chuo cha Usimamizi wa Kodi (ITA) Jijini Dar es Salaam.
  Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Zanaki Salma Mtanda akiwasilisha mada kuhusu mapato yatokanayo na uwekezaji wa rasilimali wakati wa fainali za mashindano ya vilabu vya kodi kwa mwaka 2018 yaliyofanyika katika Chuo cha Usimamizi wa Kodi (ITA) Jijini Dar es Salaam.
  Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Zanaki Salma Mtanda akiwasilisha mada kuhusu mapato yatokanayo na uwekezaji wa rasilimali wakati wa fainali za mashindano ya vilabu vya kodi kwa mwaka 2018 yaliyofanyika katika Chuo cha Usimamizi wa Kodi (ITA) Jijini Dar es Salaam.


  0 0  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akizungumza na Watendaji Wakuu wa Wizara na Taasisi zake katika kikao cha kujadili masuala mbalimbali ya utendaji kazi kwa kipindi cha mwezi Agosti hadi Oktoba, 2018. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam leo. Kulia kwa Waziri Lugola ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali, Jacob Kingu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati meza kuu) akifuatilia kwa makini taarifa ya Jeshi la Polisi iliyokua inasomwa na Kamishna wa Polisi Jamii, Musa Ali Musa (kulia), kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Polisi nchini, katika kikao kilichokua kinajadili masuala mbalimbali ya utendaji kazi kwa kipindi cha mwezi Agosti hadi Oktoba, 2018. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto meza kuu ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali, Jacob Kingu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali, Jacob Kingu akizungumza katika Kikao cha Watendaji Wakuu wa Taasisi za Wizara hiyo, kilichokuwa kinajadili masuala mbalimbali ya utendaji kazi wao kwa kipindi cha mwezi Agosti hadi Oktoba, 2018. Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Katibu ni Waziri wa Wizara hiyo, Kangi Lugola. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati) akimtaka Kamishna wa Polisi Jamii, Musa Ali Musa (kulia), amfafanulie jambo baada ya kuwasilisha taarifa ya Jeshi hilo katika kikao kilichokua kinajadili masuala mbalimbali ya utendaji kazi wa Taasisi za Wizara hiyo kwa kipindi cha mwezi Agosti hadi Oktoba, 2018. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto meza kuu ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali, Jacob Kingu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akifurahi jambo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali, Jacob Kingu, katika kikao cha Watendaji Wakuu wa Taasisi za Wizara yao (hawapo pichani), kilichokua kinajadili masuala mbalimbali ya utendaji kazi kwa kipindi cha Mwezi Agosti hadi Oktoba, 2018. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0


  Halmashauri za Wilaya ya Msalala, Shinyanga (Shinyanga)  Nyang'hwale (Geita), Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji) na Wadau wa Maendeleo ambao ni ACACIA Mining PLC (kupitia Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu) wamesaini hati za makubaliano ya kisheria kutekeleza  Mradi wa Pamoja wa Maji ujulikanao kama JOINT WATER PARTNERSHIP PROJECT (JWPP). 
  Akizungumza jana wakati wa kutia saini makubaliano hayo (Legal Agreement) kijiji cha Ilogi halmashauri ya Msalala, Katibu Mkuu Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo amesema katika mradi huo sehemu kubwa ya fedha za mradi zimetolewa na Serikali kupitia wizara ya maji na ACACIA Bulyanhulu Gold Mine Ltd ambapo pia halmashauri hizo tatu zinachangia kiasi cha fedha kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za mradi huo kutoka katika makusanyo yake ya ndani. 
  Mradi huu utanufaisha jumla ya vijiji kumi na nne (14) kutoka katika Halmashauri za Wilaya tatu ambapo kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga  vijiji viwili ambavyo ni Mwenge na Mahando vitanufaika na mradi huo.
  Kwa upande wa Halmashauri ya wilaya ya Nyang'hwale vijiji 6 ambapo ni Nyugwa, Mwamakiliga, Izunya, Kharumwa, Kafita na Lushimba vitanufaika kupitia mradi huo na kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Msalala  pia ni Vijiji 6 ambavyo ni Kakola Na. 9, Lwabakanga, Bushing'we, Kakola, Bugarama na Ilogi.
  Profesa Mkumbo amesema Utekelezaji wa Mradi huu umegawanyika katika Awamu mbili. 
  Awamu ya kwanza ambayo inahusisha utandazaji wa bomba kuu la kusafirisha maji kutoka bomba kuu la KASHWASA katika Kijiji cha Mhangu (Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga) hadi Tanki la kuhifadhia maji katika kijiji cha Ilogi (Halmashauri ya Wilaya ya Msalala) Bomba hili kuu la kusafirisha maji yaani Mhangu - Ilogi. 
  Amesema Transmission Main ni la chuma na lina urefu wa kilimita 58.5 na vipenyo kati ya milimita 110 hadi milimita 400; zikiwemo bomba za matoleo kuwezesha usafirishaji wa maji kwenda kwenye vijiji 14 vitakavyonufaika na mradi huo. Utekelezaji wa shughuli za Mradi katika Awamu ya Kwanza umekwishaanza.
  Amesema Awamu ya pili ya Mradi itahusisha ujenzi wa matanki mapya 11 ya maji yenye ujazo kati ya lita 45,000 hadi lita 900,000 pamoja na utandazaji wa bomba za mfumo wa usambazaji maji katika vijiji vyote 14 vilivyotajwa hapo juu. Utekelezaji wa shughuli za Mradi Awamu ya pili bado haujaanza.
  Kuhusu Mkandarasi wa Utekelezaji wa Shughuli za Mradi Awamu ya Kwanza,amesema, utekelezaji wa shughuli za mradi kwa Awamu ya Kwanza unafanywa na Mkandarasi, Kampuni ya Kichina inayoitwa M/s. Beijing Construction Engineering Group (BCEG) Co. Ltd ambapo muda wa mkataba ni miezi kumi na mbili (12). 
  Mkumbo pia amebainisha kwamba Msimamizi wa Shughuli za Ujenzi wa Mradi Awamu ya Kwanza ni Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza (MWAUWASA), na kwamba awamu ya Kwanza ya Utekelezaji wa Shughuli za Mradi huu inatarajiwa kugharimu jumla ya Shilingi za Kitanzania Bilioni 13,860,873,200.
  Mchanganuo wa uchangiaji wa Serikali pamoja na Wadau wa ACACIA Bulyanhulu Gold Mine Ltd katika gharama za mradi kwa upande wa serikali Wizara ya Maji na Umwagiliaji imechangiaTSH 4,000,000,000/=, Halmashauri ya Wilaya ya Msalala TSH 600,000,000/=,Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale TSH 600,000,000/= na Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga TSH 40,000,000 na  ACACIA Bulyanhulu Gold Mine Ltd USD 2,000,000.
  Wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo akitia saini hati za makubaliano hayo (Legal Agreement) kutekeleza  Mradi wa Pamoja wa Maji ujulikanao kama JOINT WATER PARTNERSHIP PROJECT (JWPP). Wa kwanza kulia ni Meneja Mkuu wa Migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi,Benedict Busunzu. 
   Viongozi wa ACACIA na Serikali wakitia saini hati za makubaliano hayo (Legal Agreement).
  Viongozi wa ACACIA na Serikali wakielekea katika kijiji cha Ilogi halmashauri ya Msalala ambapo bomba la maji litapita.
  Katibu Mkuu Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo akishiriki kuchimba mtaro katika eneo la Kijiji cha Bushing'we halmashauri ya Msalala ambapo bomba la maji litapita.
  Meneja Mkuu wa Migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi,Benedict Busunzu akishiriki kuchimba mtaro katika eneo la Kijiji cha Bushing'we halmashauri ya Msalala ambapo bomba la maji litapita.
  Katibu Mkuu Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo akizungumza baada ya kusaini hati za makubaliano ya kisheria kutekeleza  Mradi wa Pamoja wa Maji ujulikanao kama JOINT WATER PARTNERSHIP PROJECT (JWPP). 
  Meneja Mkuu wa Migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi,Benedict Busunzu akizungumza baada ya kusaini hati za makubaliano ya kisheria kutekeleza  Mradi wa Pamoja wa Maji ujulikanao kama JOINT WATER PARTNERSHIP PROJECT (JWPP). 
  Mkuu wa wilaya ya Kahama,Anamringi Macha akizungumza.


  0 0  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge wakati alipozungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Chamwino kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Oktoba 20, 2018.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Halmshauri ya wilaya Chamwino kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa wilaya hiyo, Oktoba 20, 2018. (Picha na Ofisi ya waziri Mkuu)
  Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Oktoba 20, 2018.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisoma majina ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino ambao hawaishi kwenye Kituo chao cha kazi cha Chamwino badala yake wanaishi jijini Dodoma. Alikuwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri hiyo kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Chamwino, Oktoba 20, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Vumilia Nyamoga ordha ya watumishi ambao hawaishi kwenye kituo chao cha kazi cha Chamwino na badala yake wanaishi jijini Dodoma. Alikuwa katika mazungumzo na watumishi wa Halmashauri hiyo kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Oktoba 20, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
  Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino wakimshangilia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wakati alipowasili kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo kuzungumza na watumishi hao, Oktoba 20, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  *Ni wale washio nje ya kituo, wawe wamehamia ifikapo Desemba 15


  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwaametoa siku 25 kwa watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Chamwino wanaoishi nje ya kituo chao cha kazi wawe wamehamia.

  Pia amemkabidhi Mkuu wa wilaya hiyo Bibi Vumilia Nyamoga orodha ya watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Chamwino ambao wanaishi nje ya kituo cha kazi kwa hatua zaidi. Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumamosi, Oktoba 20, 2018) wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri ya wilaya na ofisi ya mkuu wa wilaya ya Chamwino.

  “Ifikapo Desemba 15 mwaka huu watumishi wote wawe wamehamia katika kituo chao cha kazi. Sheria ya utumishi inamtaka mtumishi aishi katika maeneo ya kituo cha kazi.” Waziri Mkuu amesema lazima watumishi wote wa umma wafuate sheria, kanuni na taratibu za utumishi na atakayeshindwa kuhamia atakuwa amejiondoa kwenye utumishi.

  Kadhalika, Waziri Mkuu amewataka watumishi wa halmashauri hiyo kwa kushirikiana na wakuu wa idara na madiwani watambue vyanzo vyote vya mapato. Amesema baada ya kuvitambua wasimamie utaratibu wa ukusanyaji kwa njia ya kielekroniki ili kuiwezesha halmashauri kupanga miradi na kuitekeleza kupitia fedha za ndani.

  Pia Waziri Mkuu amekagua barabara za mitaa katika mji wa Chamwino zenye urefu wa kilomita 3.5 zinazojengwa kwa kiwango cha lami na kuweka jiwe la msingi la ujenzi huo. Baada ya kukagua barabara hizo, Waziri Mkuu alikagua ujenzi wa miundombinu ya majengo ya kituo cha Chamwino na kisha kuzungumza na wananchi waliofika kituoni hapo.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali zote mbili, yaani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na Dkt. Ali Mohamed Shein zinaamini kuwa vyama vya Ushirika ni njia muhimu sana ya kuzalisha ajira hususan kwa wanawake na vijana.

  Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa Uzinduzi wa Ushirika wa Mamlaka Saccos uliofanyika katika ukumbi wa Abdul Wakiil, Baraza la Wawakilishi la Zamani Kikwajuni, Zanzibar.Ushirika wa Mamlaka Saccos ulianza na wanachama 55 na mpaka sasa wakati wa uzinduzi wake una wanachama 250 pamoja na mambo mengine Ushirika huo umeshatoa mikopo bila riba shilingi milioni 93 kwa wanachama 133.

  Makamu wa Rais aliwapongeza wanaushirika huo kwa kusema “Ni wazo zuri sana kama mtalisimamia na kulitekeleza ipasavyo kwa haika mtajikomboa kiuchumi na kubadilisha kwa kiasi kikubwa hali zenu za maisha”Makamu wa Rais aliendelea kusema kuwa Binafsi anaamini sana katika ushirika tena ushirika wa kuweka na kukopa kwani ni moja ya njia sahihi ya kujikomboa kiuchumi.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewaomba wananchi wa Zanzibar kupinga kwa nguvu zote masuala ya udhalilishaji na ukatili kwa wanawake na watoto na kuwataka watoe ushirikiano na Serikali katika mapambano dhidi ya udhalilishaji pia aliwahimiza wananchi hao kutunza mazingira kwa faida ya sasa nay a baadae.

  Wakati huohuo Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto Mhe. Moudline Castico amewataka wanachama wa Saccos hiyo kufanya kazi kwa bidii na si kwa mazoea.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akiwa ameshikilia bango lenye maneno ya uzinduzi wa Ushirika wa Mamlaka Saccos kama ishara ya uzinduzi rasmi, kushoto ni Mwenyekiti wa Ushirika Ndugu Mohammed Khamis Ali. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akionyesha picha yake aliopewa kama zawadi wakati uzinduzi wa Ushirika wa Mamlaka Saccos kama ishara ya uzinduzi rasmi, wengine pichani ni Waziri wa Kazi Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto Mhe. Moudline Castico (kulia) kushoto ni Mwenyekiti wa Ushirika Ndugu Mohammed Khamis Ali. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ushirika wa Mamlaka Saccos kwenye ukumbi wa Abdul Wakiil, Baraza la Wawakilishi la Zamani, Kikwajuni, Zanzibar. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ushirika wa Mamlaka Saccos kwenye ukumbi wa Abdul Wakiil, Baraza la Wawakilishi la Zamani, Kikwajuni, Zanzibar. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

  0 0


   Waziri wa Madini Angellah Kairuki na mgeni wake Waziri wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) Martin Kabwelulu (wa pili kushoto) wakimsikiliza Mtaalam Mwelezi  Martin Sezinga Akiwaonesha mashine mbalimbali zinazotumiwa katika hatua mbalimbali za uzalishaji na uchenjuaji wa madini ya dhahabu katika mgodi wa mfano wa Lwamgasa.
  PICHA 2- BUSOLWA
  Waziri wa Madini Angellah Kairuki (kushoto) na Waziri wa  Madini wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Martin Kabwelulu wakiteta jambo baada ya kutembelea mgodi wa Busolwa Mining Ltd unaomilikiwa na Mtanzania, mkoani Geita
  PICHA 3 KONGO TANZANIA
  Meneja wa Mgodi wa Busolwa Mining Ltd, Flex Adoph akimweleza jambo Waziri wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Martin Kabwelulu (katikati) wakati alipotembelea katika mgodi huo kujifunza namna mmiliki wa mgodi huo alivyotoka katika uchimbaji mdogo hadi kuwa mchimbaji wa Kati lakini pia kujifunza namna mgodi huo unavyofanya shughuli zake za uchenjuaji na uzalishaji wa madini ya dhahabu. Anayeshuhudia ni Waziri wa Madini Angellah Kairuki.
  PICHA 5 B
  Waziri wa Madini wa  Angellah Kairuki na Mgeni wake Waziri wa Madini wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Martin Kabwelulu (Wa tatu kushoto) wakiangalia madini ya Dhahabu yanayozalishwa na kuchenjuliwa katika Mgodi wa Nsangano Gold Mine mkoani Geita walipoutembelea mgodi huo.
  PICHA 5, A, B
  Waziri wa Madini Angellah Kairuki na mgeni wake Waziri wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Martin Kabwelulu pamoja na ujumbe walioambatana nao wa Mkoa wa Shinyanga wakiangalia namna shughuli mbalimbali za uzalishaji wa madini ya Almasi  katika Mgodi wa Almasi Mwadui (WDL) zinavyofanyika.
  PICHA 8
  Waziri wa Madini Angellah Kairuki na Waziri wa Madini wa Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo (DRC) Martin Kabwelulu wakiangalia Kitabu kinachotunza uzalishaji wa madini ya Almasi katika Mgodi wa Almas Mwadui (WDL) Kitabu hicho kina kumbukumbu za uzalishaji wa tangu mwaka 1958. Anayeshuhudi ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,  Zainab Tellack.
  PICHA 9
  Sehemu ya mitambo mbalimbali katika Mgodi wa Mfano wa Lwamgasa. Mgodi huo umejengwa na Wizara ya Madini kupitia Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) kwa lengo la kutoa elimu ya uchimbaji wenye tija kwa wachimbaji wadogo, kutoa huduma na elimu kuhusu uchenjuaji  sahihi wa dhahabu. Mgodi huo umejengwa mkoani Geita.
  PICHA 10
  Waziri wa Madini Angellah Kairuki, mgeni wake  Waziri wa Madini wa Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo uongozi wa Mkoa wa Shinyanga, Wilaya ya Kishapu na uongozi wa mgodi wa Almasi Mwadui wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuutembelea mgodi huo.
  …………………………………………………………………………………
  Asteria Muhozya na Rhoda James, GEITA
   Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Madini imeanza kufanya mazungumzo na nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ili iweze kujenga Kiwanda cha Kuchenjua madini ya Colbat nchini.
   Hayo yalibainishwa Oktoba 19, mkoani Geita  na Waziri wa Madini wa Tanzania Angellah Kairuki wakati wa kuhitimisha ziara ya siku Nne ya  Waziri wa Madini wa Kongo (DRC), Martin Kabwelulu aliyoifanya nchini kwa mwaliko wa Waziri Kairuki.

  Kairuki alisema kuwa, nchi ya Kongo ndiyo mzalishaji mkubwa wa madini ya Colbat duniani ambapo asilimia 70 ya madini hayo duniani yanazalishwa nchini humo.Aliongeza kuwa, kwa sasa nchi hiyo inayo changamoto ya kusafirisha madini hayo yakiwa ghafi ikiwemo ukosefu wa umeme wa kutosheleza kwa ajili ya ujenzi wa viwanda hivyo.

  “Tumekubaliana kuendelea na mazungumzo  na Kongo ili shughuli za uchenjuaji na uyeyushaji wa madini hayo ufanyike nchini  kwa kuwa tumeshaanza kuwekeza kwenye Vinu/viwanda  vya Kuchenjua na kuyeyusha madini mbalimbali. Hivyo, tunataka wayasafirishe makinikia ya Colbat hapa na tuyachenjue hapa,” alisisitiza Kairuki.

  Akizungumzia matumizi ya madini hayo, Kairuki alisema kuwa, madini ya Colbat yanatumika kutengeneza betri na vihifadhi nishati (capacitor) ambazo zinahitajika sana hususan, kwenye magari yanayotumia umeme.bali na makubaliano ya ujenzi wa kiwanda hicho, pia Waziri Kairuki alisema kuwa nchi hizo zimekubaliana masuala kadhaa ikiwemo kuendelea kubadilishana uzoefu wa usimamizi wa sekta ya Madini ili kuweza kunufaisha wananchi hasa wale wanaozunguka maeneo ya migodi.

  “Nchi ya Kongo DRC imefurahishwa na hatua za Mkoa wa Geita kwenye usimamizi wa mapato yatokanayo na madini pia mchango wa migodi kwa maendeleo ya wananchi wanaozunguka mgodi,”alisema Kairuki.
  Vilevile, alisema kuwa nchi hizo zimekubaliana kuboresha mahusianao ya kimkakati ambapo Kongo imeahidi kuiunga Mkono Tanzania katika masuala ya Mashtaka dhidi ya makampuni za uwekezaji.

  Pia, alisema Kongo imeahidi kukitumia Chuo Cha Madini Dodoma (MRI) kupata mafunzo mbalimbali yanayohusu sekta ya madini yanayotolewa kituoni hapo;
  “Kongo imepanga kuja kujifunza mfumo mpya wa utoaji wa leseni za madini (cadaster) ambao umebuniwa na kusanifiwa na watanzania,” alisema Kairuki.
  Kairuki aliongeza kuwa, nchi hizo zimekubaliana kuendelea kuboresha mifumo ya udhibiti utoroshaji wa madini yanayotoka Kongo na Tanzania kwa manufaa ya nchi zote mbili.

  Aidha, Waziri Kairuki alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji wa Kongo wenye nia ya kuwekeza nchini kwenye migodi, viwanda vya uchenjuaji, uongezaji thamani madini (ukataji, unga’rishaji).“Lakini pia tumewakaribisha kutumia bandari yetu kupitisha madini yao pamoja na kukubaliana kuwa na Mining Forum kati ya nchi hizi mbili tu ukiachia Forum nyingine ambazo tumelenga kuziandaa na kushirikisha wadau kutoka nchi mbalimbali,” alisema Kairuki.
  Aidha,  alisema nchi hiyo imeahidi kurudi nchini  katika kipindi kifupi kijacho kwa ajili ya kujifunza zaidi kuhusu namna Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST)  inavyofanya kazi zake za utafiti na maabara.

  Kwa upande wake, Waziri wa DRC, Martin Kabwelulu alisema atawatuma Wataalam wake kurudi nchini kwa ajili ya kujifunza mfumo mpya wa utoaji wa leseni za madini (cadaster) wa Tanzania na kuongeza ni mfumo mzuri ambao utaliwezesha taifa hilo kusimamia vema rasilimali madini na kuhakikisha kwamba zinawanuifaisha wananchi wake.

  Pia, alisema kuwa nchi hiyo inao ukosefu wa umeme wa kutosha jambo ambalo linafanya nchi hiyo kusafirisha madini hayo nje yakiwa ghafi ikiwemo madini ya Colbat na dhahabu na kuongeza kuwa, Rais wa nchi  hiyo, Joseph Kabila katika ujumbe wake amemweleza kuwa, anataka madini yote ya Kongo yasafirishwe kupitia Tanzania.

  “Tunataka tusafirishe madini yetu kupitia bandari ya Tanzania. Lakini pia nimeona njia ya kupitishia madini yetu kupitia reli ya Kati ya Kigoma –Dar es Salaam ni fupi sana,” alisema Kabwelulu.Akizungumzia mabadiliko ya Sheria ya Madini yaliyofanywa nchini humo hivi karibuni, alisema nchi hiyo iliamua kubadili sheria yake kutokana na kutokunufaika kabisa na rasilimali hiyo hususan kwa wananchi wanaozungukwa na  rasilimali hizo na kuongeza kuwa, sheria ya sasa inapigania zaidi maslahi ya nchi na wananchi wake.

  “Nafurahi nimepokelewa vizuri sana Tanzania, nimejifunza mengi kweli hii ni nchi rafiki. Sisi tunao uzoefu wa miaka mingi kwenye sekta hii lakini bado hatujanufaika kabisa,” alisema Kabwelulu.Naye, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Luhumbi alisema kuwa, amemwomba Waziri wa Madini wa Kongo kujenga kiwanda cha Colbat nchini kwa kuwa nchi hiyo iko jirani sana na mkoa huo na kwamba mkoa huo umejipanga kwa mazingira ya uwekezaji mkubwa.

  Akiwa nchini, Waziri Kabwelulu alipata fursa ya kukutana na Menejimenti ya Wizara ya Madini na Taasisi zake ambapo pande zote zilibadilishana uzoefu wa namna zinavyosimamia sekta ya madini, ikiwemo masuala ya uchimbaji mdogo wa madini.Aidha, Waziri Kabwelulu na mwenyeji wake Waziri Kairuki walitembelea Mgodi wa Mfano wa Lwamgasa ambao umejengwa mahsusi kupitia Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) unaosimamiwa na wizara. Lengo la mgodi huo ni kutoa elimu kwa wachimbaji wadogo kuhusu uchimbaji sahihi  na uchenjuaji bora wa madini dhahabu. Pia, walitembelea migodi ya Wachimbaji wa Kati inayomilikiwa na watanzania ya Buswola  Mining Ltd na Nsangano Gold Mine mkoani Geita kujifunza walikotokea katika uchimbaji mdogo hadi kuwa wa Kati na pia walitembelea mgodi wa Almasi wa Mwadui (WDL) mkoani Shinyanga.

  Ziara ya Waziri Kabwelulu nchini ililenga katika kubadilishana uzoefu na utaalamu katika masuala ya uendelezaji na usimamizi wa Sekta ya Madini ikiwemo kuimarisha zaidi ushirikiano  uliopo baina  ya hizo mbili, kuangalia fursa za ushirikiano wa kibiashara na kiuwekezaji kupitia rasilimali madini madini, kubadilishana uzoefu kuhusu Mabadiliko ya Sheria  za  Madini yaliyofanywa na nchi hizi mbili hivi karibuni pamoja na kudumisha undugu na urafiki baina ya nchi hizo mbili.

older | 1 | .... | 1702 | 1703 | (Page 1704) | 1705 | 1706 | .... | 1897 | newer