Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1694 | 1695 | (Page 1696) | 1697 | 1698 | .... | 1896 | newer

  0 0

  Kampuni ya simu za mkononi Airtel Tanzania inatarajia kutoa jumla ya TZS1.4 bilioni kama gawio kwa wateja wake wanaotumia huduma ya Airtel Money.

  Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wakutangaza hatua hiyo, Mkurugenzi wa Masoko na Airtel Money Bw. Isack Nchunda alisema kuwa gawio hili litatolewa kwa wateja wote wa Airtel Money pamoja na mawakala nchini kote ambao wamekuwa wakitumia huduma ya Airtel Money kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka ambayo ni miezi mitatu yaani (Junuari mpaka Machi mwaka huu).Airtel Money tumekuwa tukitoa gawio katika kila robo ya mwaka tokea mwaka 2015. Kwa robo hii, jumla ya 1.4 TZS bilioni zitatolewa kwa wateja wa Airtel Money pamoja na Mawakala. Wateja wa huduma ya Airtel Money pamoja na Mawakala watakuwa na Uhuru wa kuchangua jinsi ya kutumia fedha zao, alisema Nchunda.

  “Hii ni mara ya sita kwa kampuni ya Airtel kutoa gawio kwa wateja wote kupitia huduma yake ya Airtel Money. Kila mteja wa Airtel Money atapokea gawio hili tunalotoa kulingana na salio la Airtel Money ambalo anakuwa nalo kila siku katika akaunti ya Airtel Money. Mpaka sasa, kiasi cha bilioni 17 TZS Kimekwishatolewa kama gawio kwa wateja wa Airtel Money, aliongeza Nchunda.

  Sambamba na Kutoa Gawio tunapenda kuwafahamisha wateja wetu wote wa Airtel Money kuwa huduma yetu sasa imeboreshwa Zaidi. Sasa tumewapa uwezo Kurudisha Miamala endapo watatuma fedha kwa makosa . Kurudisha Muamala uliotumwa kwa makosa mteja anapiga *150*60# na kisha chagua akaunti yangu na kuchagua rudisha muamala. Pia wateja wa Airtel Money wanaweza kuhifadhi Kumbu kumbu ya namba wanazotumia mara kwa mara kutuma fedha au namba za Kampuni zinanazo tumika kulipa bili mbali mbali. Huduma hizi mbili ni maboresho muhimu sana kwa wateja wetu ambayo yatasaidia kupunguza kukosea miamala na kumfanya mteja aweze kutumia Airtel Money kwa urahisi Zaidi.

  Kwa upande wake, Meneja wa Airtel Money Ibrahim Malando alisema kuwa kuanzia sasa kila mteja wa Airtel Money ataweza kupata gawio lake kupitia akaunti yake ya Airtel Money na atakuwa na Uhuru wa aidha kutoa kwa matumizi yake au kutumia kwa kulipia bili mbali mbali kama kununua kifurushi, muda wa maongezi, LUKU na huduma nyingine nyingi.Mawakala wa Airtel Money watapokea gawio kupitia akaunti zao za Airtel Money kama kawaida na hivyo nawaomba waendelee kutoa huduma bora kwa wateja wetu ili waendelee kufurahia kupata gawio katika robo nyingine ya mwaka inayokuja, aliongeza Malando.

  Kulingana na Malando, Airtel Money imejidhatiti kuhahakisha kuwa inaendelea kutoa huduma bora ya kutoa huduma ya fedha kwa njia ya simu za mkononi na kuwa suluhisho kwa malipo ya biashara ya aina yeyote ile. Vile vile, kulingana na taarifa ya hivi karibuni toka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Airtel Money ndio huduma inayokuwa kwa kasi hapa nchini.

  Airtel Money ni huduma inayopatikana kwa urahisi sana na ubunifu wa hali ya juu. Ni kwa kupitia Airtel Money pekee ambapo mteja anaweza kutuma, kupokea na kutoa fedha bure na vile kufaidi mikopo ya papo kwa hapo ya Airtel Money Timiza. “Tunaendelea kuongeza mawakala kupitia usambazaji wa vioski vya Airtel Money na kuongeza Maduka ya Airtel Money Branch ambayo sasa tayari yanatoa huduma kama wakala wa kawaida na pia kama wakala mkubwa ambapo hadi sasa hivi tumeshafungua matawi (Airtel Money Branch) zaidi ya 400 yanayotoa wigo mkubwa zaidi wa mawakala nchini. Ni imani yetu tutaendelea kuwafikia wateja wengi zaidi kadri muda unavyokwenda.

  Airtel Money inawezesha malipo mbalimbali yakiwemo yale ya huduma za serikali ( e-government) ambayo wateja wanaweza kufanya hayo malipo popote kwa wakati mmoja. “Pia huduma ya Airtel Money imeunganishwa na mabenki zaidi ya 40 nchini ili kurahishishia wateja kufanya miamala mbali mbali kama vile kuhamisha pesa kutoka kwenye akaunti ya benki na kutuma kwenye akaunti ya Airtel Money muda wowote na sehemu yeyote ile”.
  Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando, akizungumza na waandishi wa habri, Dar es Salaam kuhusu gawio la Shilingi 1.4bilioni litakalo gawiwa wateja wa kampuni hiyo. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya Airtel Tanzania, Isack Nchunda.

  Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Isack Nchunda (katikati), akizungumza na waandishi wa habri, Dar es Salaam kuhusu gawio la Shilingi 1.4bilioni litakalo gawiwa wateja wa kampuni hiyo. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando na Meneja wa Airtel Money, Ibrahim Malando.

  0 0

  Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano wa Wakala wa Usalama na Afya Mahala Pa kazi (OSHA) Paul Gyuna kushoto akitoa elimu kwa mkazi wa Jiji la Tanga wakati alipotembelea banda lao kunakoendelea kuna kofanyika maonyesho ya Wiki ya Vijana Kitaifa kwenye viwanja vya Tangamano mjini hapa
  Mkaguzi wa Afya wa Osha Blandina Reubeni akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea banda lao

  Mkaguzi wa Afya wa Osha Blandina Reubeni akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea banda lao

  Mkaguzi wa Afya wa Osha Blandina Reubeni akimpima urefu mmoja wa wananchi waliotembelea banda lao

  Mkaguzi wa Afya (OSHA) Dkt Linda Katabari akimpima presha mkazi wa Jiji la Tanga ambaye alitembelea banda lao leo


  KUTOKUZINGATIWA kwa usalama na afya sehemu za kazi kunaweza kuleta athari kubwa ya kiuchumi kwa wafanyakazi kutokana na kwamba wanaweza kukumbana na majanga makubwa hali inayopelekea kuathiri shughuli zao na kila siku na kujirudisha nyuma kimaendeleo.

  Hayo yalisemwa leo na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano wa Wakala wa Usalama na Afya Mahala Pa kazi (OSHA) Paul Gyuna wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye viwanja vya Tangamano mjini Tanga kunakofanyika maonyesho ya Wiki ya Vijana Kitaifa.

  Alisema wanatumia maonyesho hayo ya wiki ya vijana ambao ndio nguvu kazi ya Taifa hivyo wamedhamiria kuwaeleza fursa wanazoweza kuzitumia ili kuweza kufanya kazi zao kwa ufanisi mkubwa wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku.

  “Tunaangalia Usalama na Afya kwenye maeneo yao ya kazi…tunaelewa wameajiriwa lakini kuna changamoto nyingi wanazopita kutokana na kwamba wengi hawaelewi kuhusiana na mambo ya usalama na afya na kutokujua jinsi ya kujikinga na madhara hivyo tumekuja kutoa elimu”Alisema.

  Alisema elimu wanayoitoa kwenye maonyesho hayo wanaamini wananchi wakishaijua wanaweza kujiepusha na athari za kazi hata ufanisi wa kazi utaongezeka na kuongeza kipato hatua itakayosaidia kuinua uchumi wao na jamii zinazowazunguka.

  Hata hivyo alisema pia licha ya kutoa elimu hiyo lakini wanatumia wiki hiyo kufanya upimaji wa afya, presha uzito na urefu na kutoa ushauri ili kuweza kuwasaidia kuondokana na matatizo wanayokutwa nay

  0 0


  Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi za Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi kabla ya kuanza ziara yake katika mkoa huo yenye lengo la kukagua shughuli za uchimbaji wa madini, kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wa madini tarehe 09 Oktoba, 2018.
  Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kulia) akisalimiana na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Katavi & Kapufi, Mahmood Yass (kushoto) kabla ya kuanza ziara yake katika mgodi huo uliopo katika eneo la Singililwa Wilayani Mpanda mkoani Katavi.
  Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akiangalia sampuli ya makinikia ya dhahabu katika Mgodi wa Dhahabu wa Katavi & Kapufi uliopo katika eneo la Singililwa Wilayani Mpanda mkoani Katavi.
  Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Katavi & Kapufi, Mahmood Yass (kulia) akimwonesha Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kushoto) moja ya mawe yenye madini ya dhahabu.
  Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akisalimiana na sehemu ya wafanyakazi wa Mgodi wa Dhahabu wa Katavi & Kapufi uliopo katika eneo la Singililwa lililopo Wilayani Mpanda mkoani Katavi.

  Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati) akiendelea na ziara katika Mgodi wa Dhahabu wa Katavi & Kapufi uliopo katika eneo la Singililwa Wilayani Mpanda mkoani Katavi.
  Mkaguzi wa Migodi kutoka Ofisi ya Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Katavi, Paul Veran (kushoto) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati) kwenye eneo yanapohifadhiwa makinikia ya dhahabu katika Mgodi wa Dhahabu wa Katavi & Kapufi uliopo katika eneo la Singililwa Wilayani Mpanda mkoani Katavi.
  Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa nne kulia) akikagua shughuli za uchenjuaji wa dhahabu zinazofanywa na wachimbaji wadogo katika machimbo ya dhahabu ya Mkwamba yaliyopo katika kijiji cha Kapanda Wilayani Mpanda mkoani Katavi.
  Sehemu ya wachimbaji wadogo katika machimbo ya dhahabu ya Mkwamba yaliyopo katika kijiji cha Kapanda Wilayani Mpanda mkoani Katavi wakifuatilia ufafanuzi uliokuwa unatolewa na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (hayupo pichani) katika machimbo hayo.
  Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akifafanua jambo alipokuwa akizungumza na wachimbaji wadogo katika machimbo ya dhahabu ya Mkwamba yaliyopo katika kijiji cha Kapanda Wilayani Mpanda mkoani Katavi (hawapo pichani).
  Mmoja wa wachimbaji wadogo katika machimbo ya dhahabu ya Mkwamba yaliyopo katika kijiji cha Kapanda Wilayani Mpanda mkoani Katavi, Fatuma John akiwasilisha kero yake kwa Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (hayupo pichani)  …………………

  Na Greyson Mwase, Katavi

  Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ameagiza Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Katavi, Mhandisi Giliard Luyoka, Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Afisa Usalama wa Wilaya, na Mwakilishi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhakikisha wanakuwepo wakati wa ufungaji na ufunguaji wa lakiri (seal) kwenye madini ya dhahabu ili kudhibiti utoroshwaji wa madini kwenye migodi.

  Ameyasema hayo leo tarehe 09 Oktoba, 2018 mara baada ya kumaliza ziara yake katika Mgodi Dhahabu wa Katavi & Kapufi uliopo katika eneo la Singililwa Wilayani Mpanda mkoani Katavi ikiwa ni sehemu ya ziara yake katika mkoa huo yenye lengo la kukagua shughuli za uchimbaji wa madini, kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wa madini.

  Katika ziara yake Nyongo aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Salehe Mhando, Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji wa Madini Mkoa wa Katavi (KATAREMA), William Mbongo, Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Katavi, Mhandisi Giliard Luyoka, Wataalam wa Madini, Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na waandishi wa habari.

  Alisema kuwa, ni kosa kubwa la kisheria kwa Afisa Madini Mkazi kufunga au kufungua lakiri (seal) pasipo kushirikisha Mkuu wa Wilaya, vyombo vya ulinzi na usalama na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kusisitiza kuwa iwapo itagundulika Serikali haitasita kuchukua hatua kali za kisheria.  Akielezea mikakati ya Serikali kupitia Wizara ya Madini kwenye usimamizi wa Sekta ya Madini Nchini, Nyongo alisema kuwa ni pamoja na uboreshaji wa Sheria ya Madini iliyolenga kuondoa mianya ya utoroshwaji wa madini nje ya nchi kwa kuzuia usafirishwaji wa madini ghafi nje ya nchi.

  Alisisitiza kuwa, Serikali inakaribisha wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi katika ujenzi wa mitambo ya kuchenjulia madini ndani ya nchi ili kuyaongezea thamani kabla ya kuuzwa nje ya nchi na kuongeza mapato.

  Wakati huohuo akizungumza katika machimbo ya dhahabu ya Mkwamba yaliyopo katika kijiji cha Kapanda Wilayani Mpanda mkoani Katavi yanayomilikiwa na William Mbogo, Naibu Waziri Nyongo alimtaka mmiliki wa leseni kuhakikisha anaandaa mikataba na kusaini pamoja na wachimbaji wadogo wanaoendesha shughuli za uchimbaji wa madini katika eneo hilo.

  Alisema kuwa, Serikali kupitia Wizara yake haipo tayari kushuhudia migogoro kati ya wawekezaji na wachimbaji wadogo wa madini pasipo suluhu inayotokana na ukiukwaji wa Sheria za Madini na kanuni zake.

  Katika hatua nyingine, Nyongo alimtaka mwekezaji huyo kutafuta mwekezaji mkubwa kwa ajili ya usimamizi wa shughuli za uchimbaji madini katika eneo husika iwapo anakosa uwezo wa kuendeleza kama leseni ya madini inavyomtaka.

  Aidha, alimwelekeza Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Katavi, Mhandisi Giliard Luyoka kuhakikisha anatafuta maeneo kwa ajili ya wachimbaji wadogo wa madini, ili waweze kuchimba katika mazingira mazuri huku wakifuata sheria na kanuni za madini.

  Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Nyongo aliwataka wachimbaji wadogo wa madini kuhakikisha wanalipa mrahaba na kodi mbalimbali Serikalini ili mapato yaweze kutumika kwenye uboreshaji wa sekta nyingine kama vile afya, elimu, maji na miundombinu.

  Awali mbali na pongezi, wakiwasilisha kero mbalimbali wachimbaji wadogo wa madini wanaoendesha shughuli za uchimbaji madini katika machimbo ya dhahabu ya Mkwamba yaliyopo katika kijiji cha Kapanda Wilayani Mpanda mkoani Katavi yanayomilikiwa na William Mbogo walieleza changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na mitaji midogo, vifaa duni pamoja maeneo rasmi kwa ajili ya uchimbaji madini.

  0 0

  Waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa Dr Hussein Mwinyi akiwa na baadhi ya maafisa wa jeshi la JKT kikosi cha 841 KJ Mafinga pamoja na mkuu wa JKT Tanzania Maj Gen SM Busungu wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye jengo la utawala la shule ya sekondari Kawawa wakati wa uzinduzi wa jengo hilo.
  Waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa Dr Hussein Mwinyi akiwa na baadhi ya maafisa wa jeshi la JKT kikosi cha 841 KJ Mafinga pamoja na mkuu wa jeshi ya JKT Tanzania Maj Gen SM Busungu wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Kawawa iliyopo Mafinga Mkoani Iringa.
  Waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa Dr Hussein Mwinyi akiwa na baadhi ya maafisa wa jeshi la JKT kikosi cha 841 KJ Mafinga pamoja na mkuu JKT Tanzania Maj Gen SM Busungu wakiwa kwenye picha ya pamoja
  Na hili ndio jengo la kisasa la utawala la shule ya sekondari ya kawawa lililofunguliwa na waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa Dr Hussein Mwinyi
  NA FREDY MGUNDA,IRINGA.  WAZIRI wa ulinzi na jeshi lakujenga taifa Dr Hussein Mwinyi ameupongeza uongozi wa shule ya sekondari yaKawawa kwa ujenzi wa jengo la kisasa la utawala ambalo litachangia katika ufanisi bora wa kazi kwa walimu na wafanyakazi wote wa shule hiyo.

  Akizungumza wakati wa kuzindua jingo hilo la utawala waziri Mwinyi alisema kuwa jengo limejengwa kwa viwango ambavyo serikali ya awamu ya tano inataka na jingo hilo linaviwango vinavyotakiwa.“Kwa kweli nisiwe mchoyo wa fadhila jengo hili limejengwa kwa kuzingatia ujenzi unaotakiwa na lina ramani ambayo itadumu kwa miaka mingi na itakuwa auheni kwa wafanyakazi kufanya kazi zao kwenye jengo hili” alisema Mwinyi

  Waziri Mwinyi aliwataka wafanyakzi wa shule hiyo kuhakikisha wanalitunza jengo hilo pamoja na miundo mbinu yake kwa ajili ya vizazi vingine. Awali akisoma risala kwa waziri Mwinyi mkuu wa shule hiyo Meja Erenest Sikaponda alisema kuwa jengo hilo la utawala limejengwa kwa shilingi 222,591,000 na kufanikiwa kuokoa kiasi cha shilingi 103,360,000 kwa kuwa hapo awali BOQ ilikuwa inaonyesha kuwa gharama za jengo ni shilingi 325,951,000.

  Kupungua kwa gharama hizo ni kutokana na ubunifu,matumizi mazuri ya rasilimali,nidhamu katika matumizi ya fedha,nguvu kazi ya vijana ambao baadhi yao walikuwa mafundi na gari kubwa la kusombea mchanga,kifusi na mawe msaada huo ulitoka katika kikosi cha 841kj Mafinga” alisema Maj Sikaponda Maj Sikaponda aliwashukuru wadau mbalimbali ambao walitoa msaada wa hali na mali kusaidia ujenzi wa jengo hilo la kisasa la utawala ambalo litakuwa msaada mkubwa kwa wafanyakazi wa shule hiyo.

  “Mheshimiwa waziri tunapenda kuwashukuru wadau wafuata TANROAD mkoa wa Iringa kwa msaada wa kifusi cha kujaza msingi kwa trip mia,kampuni ya kichina inayojenga barabara ya Mafinga Igawa kwa msaada wa tripu moja ya kokoto ya ujazo wa Mita 15 za mraba,Clement 
  Sangale saruji mifuko 20, na Beruto Kaboda alitoa mbao 2×3 Arobain” alisema Maj Sikaponda

  Aidha Maj Sikaponda alisema kuwa jengo hilo la kisasa la utawala linakabili na changamoto ya ukosefu wa samani kutokana na ufinyu wa bajeti hivyo walimuomba waziri kuwasaidia kuzipata samani hizo.Tumalizie kwa kumshukuru mkuu wa JKT Tanzania pamoja na bodi ya shule kwa usimamizi mzuri wa mipango ya maendeleo ya shule hii.

  Kwa upande wake mkuu wa JKT Tanzania Maj Gen SM Busungu liwapongeza viongozi waliosimamia ujenzi wa jengo hilo hadi lilipofikia na kuhakikisha linajengwa kwenye ubora unaotakiwa.Maj Gen SM Busungu alimuomba
  waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa DR Mwinyi kwenda kuwaombea samani RA ambazo walizitaifisha kutoka bandarini ambazo maarufu kama samani za makonda ili ziweze kutatua changamoto hiyo katika jengo hilo la utawala.

  Akijibu ombi hilo la mkuu wa majeshi ya JKT waziri Mwinyi alisema ataenda kuwaomba TRA kwa kuwa wote wanaitumikia serikali moja.

  0 0

  Baadhi ya watendaji kutoka idara za Mahakama, Polisi na viongozi wa vijiji, kata na mitaa kwenye halmashauri ya mji Kasulu mkoani Kigoma wahimiza umuhimu wa kuimarisha ulinzi ili kupunguza madhila kwa watu wenye ualbino, sambamba na kuelimisha jamii zaidi kuhusiana na masuala ya ualbino ili kuondoa dhana potofu, dhidi ya watu wenye ualbino ambayo imejangeka miongoni mwa baadhi ya wananchi.

  Pia jamii kukumbushwa kuhusiana na maadili mema, sambamba na kuhakikisha watendaji hao wanazingatia maadili yao ya kazi katika kuwahudumia wananchi.

  Maazimio hayo yamefikiwa baada ya watendaji hao kupatiwa elimu kuhusu ualbino, maadili na amani, iliyotolewa na mashirika ya CEFA Tanzania, GNRC Tanzania na Under The Same Sun, ambayo kwa pamoja yanatekeleza mradi wa Haki Yetu.
   John Richard, Afisa Mawasiliano wa Mradi wa Haki Yetu, akizungumza na baadhi ya watendaji wa kata, maafisa kutoka idara ya Mahakama na Polisi kwenye halmashauri ya mji Kasulu, mkoani Kigoma kuhusiana na utekelezaji wa mradi wa Haki Yetu.

   Faustine Gwassa, Naibu Meneja wa Mradi wa Haki Yetu akichokoza mada wakati wa mafunzo kwa baadhi ya watendaji wa kata, maafisa kutoka idara ya Mahakama na Polisi kwenye halmashauri ya mji Kasulu,mkoani Kigoma. 
  Joyce Mdachi, kutoka shirika la GNRC akifundisha umuhimu wa maadili na amani kwa baadhi ya watendaji kata, maafisa kutoka idara ya Mahakama na Polisi kwenye halmashauri ya mji Kasulu, mkoai Kigoma.

  0 0

  *Amuagiza mkuu wa wilaya afanye uchunguzi kubaini zinapokwenda

  WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Bw. Jabir Shekimweri afanye uchunguzi kuhusu matumizi ya sh. milioni 70 zinazotelewa kila mwezi na Serikali kwa ajili ya kununulia dawa kwenye wilaya hiyo.

  "Kilichokuwa kinasemwa na wabunge bungeni nilidhani sicho, nikasema nakuja niyasikie mwenyewe. Kweli wananchi hawaridhiki nimeona. Sasa mkuu wa wilaya shughulikia hili jambo ili kubaini fedha za dawa zinakwenda wapi.”

  Alitoa agizo hilo jana jioni (Jumatano, Oktoba 10, 2018) wakati akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa shule msingi Mpwapwa, ambapo alipokea malalamiko ya wananchi juu ya ukosefu wa dawa. Dawa pekee wanazopewa ni za kutuliza maumivu tu.

  Waziri Mkuu alisema lengo la Serikali kutoa fedha hizo kila mwezi ni kuhakikisha kwamba wananchi wote wanapata huduma za afya popote walipo badala ya kusafiri umbali mrefu kwenda makao makuu ya wilaya.

  "Kila mwezi Serikali inatoa zaidi ya sh milioni 70 kwa ajili ya kununulia dawa kwenye wilaya hii ya Mpwapwa. Pia kuna fedha za mfuko wa afya sh. milioni 60 pamoja na fedha za matokeo mazuri ya afya sh. milioni 300 kwa mwaka, shida ya dawa haitakiwi kuwepo hapa.”
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Mpwampwa, kwenye ukumbi wa chuo cha uwalimu Mpwapwa mkoani Dodoma, Oktoba 10, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mpwampwa Paul Mamba Sweya, kwenye ukumbi wa chuo cha uwalimu Mpwapwa mkoani Dodoma, Oktoba 10, 2018.
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwahutubia wananchi wa Wilaya ya Mpwapwa kwenye uwanja wa Chazugwa mkoani Dodoma, Oktoba 10, 2018. 
   Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega, akizungumza na wananchi wa Mpwapwa katika uwanja wa Chazugwa mkoani Dodoma, Oktoba 10, 2018.
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa na mkewe Marry, akikagua shamba la korosho la Magereza wilayani Mpwapwa Dodoma, Oktoba 10, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


  0 0

  Itakuwa benki ya kwanza ya nchini kuwa na kadi ya visa ya YUAN malipo ya kabla.
  Wafanyabiashara wanaotembelea Uchina mara kwa mara na wanafunzi kufaidika wanaosafiri kwenda China.

  BancABC Tanzania ambayo ni kampuni tanzu ya Atlas Mara na ambao imeorodhesha kwenye soko la hisa la London, imepiga hatua nyingine kwenye soko kwa upande wa ubunifu kwa kuja na kadi ya malipo ya kabla – YUAN pre-paid Visa card, ambayo itawawezesha kufanya malipo kwa kwa fedha za China. Kwa sasa BancABC Tanzania inazo kadi 5 za malipo ya kabla ambazo zinapatikana kwa fedha ya USD, Tanzania, Uingereza, Ulaya na Afrika Kusini.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutambulisha kadi hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Digitali BancABC Silas Matoi alisema kuwa China imekuwa ni kati ya nchi mashuhuri kwa maswala ya biashara duniani ambapo pia wafanyabiashara wadogo na wakubwa pamoja na wanafunzi kutoka nchini Tanzania wamekuwa wakitembelea kwa wingi ndio maana BancABC ikaamua kuja na kadi ya malipo ya kabla ya YUAN ili kutoa suluhisho hasa pale wanapokuwa wanahitaji fedha ya China.

  Kadi ya YUAN ni kadi maalum ambayo inawafanya watumiaji waweze kupata fedha za Uchina kwa thamani ile ile ambayo imewekwa kwenye kadi yake na hivyo itapunguza sana changamoto za kubadilisha fedha ambazo wafanyabiashara na wanafunzi wamekuwa wakikumbana nazo pale wanapohitaji fedha za Uchina wakiwa China au popote pale duniani, alisema Matoi.

  Matoi aliongeza kuwa ‘Kadi ya YUAN imeundwa kwa umakini mkubwa kwa mfumo salama wa chip na PIN wenye teknolojia ya hali ya juu ambayo inatumika duniani kote na hivyo kuondoa tatizo la kuibiwa. YUAN kadi pia ina huduma ya kupokea ujumbe mfupi wa maneno na hivyo kumfanya mmliki kupata taarifa zote kwa kila muamala au malipo anayofanya kwa kutumia njia ya mtandao.

  YUAN kadi haina na makato yeyote ya mwezi na hivyo kuwa na gharama nafuu kwa wateja wetu, alisema Matoi huku akiongeza kuwa mzazi mwenye motto ambaye yuko masomoni China anatakiwa kuweka fedha kwenye akaunti ya motto wake yenye fedha za Uchina na papo hapo salio litaonekana kwenye kadi ambayo motto anamiliki.

  Alisema kuwa BancABC Tanzania ilishinda tuzo ya VISA mwaka 2016 kwa kuongoza kwenye huduma ya malipo ya mtandaoni na mpaka sasa hivi bado inashikilia tuzo hiyo. ‘Tuzo ya VISA tuliweza kushinda kutokana na kuwa na kadi zetu za malipo ya kabla ambazo zimejenga imani kwa wateja wetu pamoja na watumiaji wengine’, aliongeza Matoi.

  Hakuna haja ya kuangaika wapi unaweza kutumia kadi ya YUAN kwani inapatikana maasaa 24 kwa siku saba za wiki kwenye ATM za Visa milioni 2.7 duniani kote na kwenye maduka 46 ya reja reja ulimwenguni kote huku kwa Tanzania ikipatikana kwenye ATM za Visa 400 na maduka yayokubali kadi ya Visa 1000.

  Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kitengo cha Wateja Binafsi na Wanafanyabiashara Joyce Malai BancABC alisema kuwa kuzindua kadi hiyo ni hatua nyingine kubwa kwa benki hiyo kuendelea kutoa huduma bora na zenye kutoa suluhisho kwa wateja. YUAN kadi bali na kuokoa muda kwa wateja wetu lakini pia inaondoa matumizi ya fedha yasiokuwa ya lazima kwani mteja anaweza kutumia kiasi kile tu ambacho kimehifadhiwa kwenye akaunti yake. 

  Malai aliongeza kuwa kutokana na huduma bora na nafuu ambazo benki BancABC imekuwa ikizitoa, benki hiyo ilishinda tuzo ya Best Emerging Bank – East Africa kwenye tuzo za The Banker, East Africa Awards 2017. Imekuwa ni moja ya lengo letu sisi kama benki kuendelea kushinda tuzo mbali mbali kuja na huduma zenye ubunifu wa kuwa suluhisho kwa wateja wetu, alisema Malai.
   Mkuu wa Huduma za Kidigitali wa Benki ya BanABC, Silas Matoi (kulia), na Mkuu wa Wateja Binafsi na wateja wafanyabiashara wa kati na wadogo, Bi. Joyce Malai, wakionyesha mfano wa kadi ya ATM ya fedha za kichina wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa kadi hiyo jijini Dar es Salaam jana.
   Mkuu wa Huduma za Kidigitali wa Benki ya BanABC, Silas Matoi (kulia), akizungumza katika hafla ya ya uzinduzi rasmi wa kadi ya ATM ya fedha za kichina ya Visa  jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkuu wa Wateja Binafsi na wateja wafanyabiashara wa kati na wadogo, Bi. Joyce Malai.

  0 0


  0 0


  The Tanzania Revenue Authority’s Director for Taxpayer Services and Education Mr Richard Kayombo explaining tax issues in relation to investments environment in various sectors in Tanzania during the Swedish Business delegation seminar held in Dar es Salaam.

  The Tanzania Revenue Authority’s Director for Taxpayer Services and Education Mr Richard Kayombo explaining tax issues in relation to investments environment in various sectors in Tanzania during the Swedish Business delegation seminar held in Dar es Salaam.

  The Tanzania Revenue Authority’s Director for Taxpayer Services and Education Mr Richard Kayombo explaining tax issues in relation to investments environment in various sectors in Tanzania during the Swedish Business delegation seminar held in Dar es Salaam. Centre is a Senior Investment Manager at Swedfund Ms Audrey Obara and right is a Director and co-founder MTI Investment Dr. Neema Mori.

  Some Swedish Business delegation listening to the Tanzania Revenue Authority’s Director for Taxpayer Services and Education Mr Richard Kayombo (not in picture) during a seminar held in Dar es salaam.


  Veronica Kazimoto,Dar es Salaam

  The Tanzania Revenue Authority (TRA) has provided tax education and explanations on tax matters in relation to investments environment in various sectors in the country.

  Speaking to the Swedish Business delegation during a seminar held in Dar es Salaam, TRA’s Director for Taxpayer Services and Education Mr. Richard Kayombo said that, Tanzania tax laws grant various tax incentives in order to make it possible for investors to be encouraged to invest in specific sectors but also give them relief to bring in capital goods and Technology for the benefit of industrialization agenda that is key for the 5th phase government.

  The reliefs are embedded in the various tax laws that include the East African Customs Management Act, VAT Act 2014 and the Income Tax.

  “Among the incentives granted include Common External Tariffs which applies to all imported goods into the region with three rates of 0%, 10% and 25% depending on the type of goods, harmonized East African Community tariffs of zero rate for imports of raw materials, capital goods, replacement parts, inputs for agriculture, animal husbandry, fishing, livestock and pharmaceuticals medicaments,” Mr Kayombo said.

  He added that, “Other incentives under corporate tax include a reduced rate from normal 30% to 25% charged for three years to newly listed companies with the Dar es Salaam Stock Exchange (DSE), 20% for a new entity dealing in manufacturing of pharmaceuticals and leather products and 10% rate for corporations investing in a plant for assembling Motor Vehicles, tractors and fishing auto boats”.

  Under the Value Added Tax (VAT), Mr Kayombo pointed some incentives including zero rate for all exports, exemptions of various items as provided in the respective tax laws that include exemption of imported machinery by local manufacturers and processors of vegetable oil, Textiles, pharmaceuticals, hides and skins and leather manufactured in Tanzania Mainland. On the other hand, he assured the Swedish Business delegates that, as a way fighting corruption, the Authority has a fully-fledged department responsible for staff ethics and integrity so that taxpayers may be treated fairly and with respect.

  “The department conducts both proactive and reactive anti-corruption functions to ensure that TRA staff do not engage in corruption practices that not only deny government its due revenue but damages trust and relationship between the revenue administration and taxpayers. Kayombo further gave assurance to the investors on the availability of redress mechanisms on tax issues that should give Taxpayers comfort whenever they have disputes on tax matters. The mechanism starts with the Regional Managers across the Country, then to the respective Commissioners and finally to the Commissioner General.

  He went on to elaborate that “should a taxpayer remain unsatisfied with the internal redress mechanism, he is free to escalate the matter by appealing to the Tax Appeal Board and then to the Tax Appeals Tribunal which all ensure and guarantee good Governance and transparency”, he added. Mr. Richard Kayombo finally took this opportunity to call upon more and more foreign Investors to come and invest in Tanzania since the Government is taking all the necessary measures to improve the investment climate in the country as well as tax systems aiming at reducing the cost of doing business by both current and prospective investors.

  The Swedish business delegation was led by Ambassador Dr. Wilbrod Slaa the Tanzanian Ambassador to Sweden and the Ambassador of Sweden to Tanzania Mr. Anders Sjoberg. On his part, Ambassador Dr. Slaa expressed his gratitude to the Swedish Investors for coming all the way to Tanzania to seek the abundant opportunities for which the 5th phase Government is determined to welcome and support in order to realize the industrialisation agenda.

  On the other hand, the Swedish Ambassador to Tanzania Mr. Anders Sjoberg showed his appreciation to Ambassador Slaa for his tireless effort in persuading and supporting investors to come to Tanzania as well as the readiness of the Government of Tanzania in welcoming investors from Sweden and other parts of the world which was vividly expressed through representation by various Government Departments and Ministries to explain and clarify issues to investors.

  0 0

  Na Estom Sanga -TASAF

  Menejimenti ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii - TASAF imekutana na Wadau wa Maendeleo kujadili masuala mbalimbali ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaohudumia takribani kaya Milioni Moja na Laki Moja nchini kote.

  Akitoa taarifa katika kikao hicho, Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bwana Ladislaus Mwamanga amesema hatua kubwa imepigwa katika utekelezaji wa Mpango huo huku akiishukuru Serikali na Wadau wa Maendeleo kwa kuendelea kutoa msaada muhimu katika kufikia mafanikio hayo.

  Aidha Bwana Mwamanga amesema msaada wa Serikali na Wadau wa Maendeleo unaoendelea kutolewa umeusaidia kwa kiwango kikubwa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii – TASAF kuandaa kwa ufanisi Awamu ya Pili ya Mpango huo inayotarajiwa kuanza hapo mwakani.

  Amesema maandalizi hayo yanazingatia kwa kiwango kikubwa maelekezo ya Serikali yanayosisitiza umuhimu wa walengwa kufanya kazi za uzalishaji mali ili hatimaye waweze kuondokana na umaskini na kuboresha maisha yao.

  Bwana Mwamanga amesema TASAF imekuwa ikitiwa moyo na namna Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wanavyoendelea kutumia fursa hiyo muhimu ya kujumuishwa kwenye Mpango kwa kuzingatia masharti ya Mpango huo.

  Vikao vya pamoja kati ya menejimenti ya TASAF na Wadau wa Maendeleo hufanyika kwa lengo la kuona namna shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini zinavyotekelezwa ili kukidhi matakwa na maagizo ya serikali ya kuhakikisha kuwa kero ya umaskini miongoni mwa walengwa inatokomezwa. 
   Wajumbe wa kikao cha menejimenti ya TASAF na Wadau wa maendeleo wakifuatilia mjadala kwenye kikao chao cha kila mwezi kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa TASAF.
   
  Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Ladislaus Mwamanga (mbele) akiongoza kikao cha wadau wa maendeleo na menejimenti ya TASAF.


  0 0


  Wakaazi wa Itundu mjini Songea wakiangalia simu mbalimbali kwenye duka la Tigo lililopo mtaa huo. Katika msimu huu wa Tigo Fiesta wateja wa Tigo wanapata bonasi ya hadi GB 2 baada ya kununua simu aina ya Tecno S2, R6 na ZTE-KISS 3 katija maduka yote ya Tigo nchini.  Mtoa Huduma wa Duka la Tigo mtaa Itundu mjini Songea Neema Sammy akimkabidhi mteja, Otimary Kapinga simu na tiketi aliyojishindia kwenda kuona tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote kesho mara baada ya kununua simu leo

  Mtoa Huduma wa Duka la Tigo mtaa Itundu mjini Songea William Nombo akimkabidhi mteja, Jordan Maneno simu na tiketi aliyojishindia kwenda kuona tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote kesho mara baada ya kununua simu aina ya Tecno R6.
  Mtoa Huduma wa Duka la Tigo mtaa Itundu mjini Songea Water Newton akimkabidhi mteja, John Komba simu na tiketi aliyojishindia kwenda kuona tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote kesho mara baada ya kununua simu leo aina ya Tecno S2
  Wateja wa Tigo walionunua simu aina ya Tecno S2 Tecno R6 na ZTE-KISS 3 wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kupewa zawadi zao za tiketi kuhudhuria tamasha la Tigo Fiesta litalofanyika kesho uwanja wa Majimaji.

  0 0


  Mkuu wa Kitengo cha Wateja wadogo na wa kati wa benki ya NMB, Omari Mtiga (kushoto) akimkabidhi moja ya jezi Mwenyekiti wa klabu ya gofu Lugalo Brigedia Jenerali mstaafu, Michael Luwongo zilizotolewa na NMB ikiwa ni sehemu ya udhamini wa Mashindano ya Mchezo wa Golf ya Mkuu wa Majeshi nchini yanayotarajia kufanyika Oktoba 13 katika viwanja vya Lugalo Dar es Saalam.

  BENKI ya NMB imedhamini Mashindano maalum ya Mchezo wa Golf ya Mkuu wa Majeshi nchini yanayotarajia kufanyika Oktoba 13 na kushirikisha wachezaji wa gofu kutoka klabu mbalimbali nchini.

  Udhamini uliotolewa ni wa shilingi milioni 26 pamoja na vifaa mbalimbali zikiwemo jezi zitakazo tumika katika mashindano hayo vimekabidhiwa jana jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Kitengo cha Wateja wadogo na wa kati wa benki ya NMB, Omari Mtiga katika viwanja vya Lugalo.Kukabidhiwa kwa udhamini huo ni mwendelezo wa Benki ya NMB kudhamini na kusaidia shughuli anuai za michezo hususani ya Jeshi la wananchi.

  Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mara baada ya kukabidhiwa kwa udhamini huo, Makamu Rais wa Umoja wa Klabu za Golf Tanzania, Luteni Canali David Luoga alisema mashindano hayo yanatarajia kushirikisha wachezaji kutoka vilabu mbalimbali vya golf Tanzania na makundi ya wachezaji wakiwemo watoto.Alisema mashindano hayo ambayo yatafanyika kwa siku moja pekee na kufunguliwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama (JWTZ), Jenerali Venance Mabeyo washindi watajipatia fedha taslimu pamoja na vikombe.

  Aliongeza kuwa mashindano hayo yatakuwa na mvuto wa pekee kwa kile kushirikisha viongozi waandamizi mbalimbali kutoka Serikalini waliostaafu na awaliopo madarakani.

  "Kama unavyofahamu klabu yetu ya mchezo wa golf inashirikisha pia viongozi mbalimbali waandamizi kutoka Serikalini waliostaafu na wengine bado wapo madarakani nao tunatarajia watashiriki katika mashindano haya...hivyo yatakuwa na mvuto wa kipekee," alisema Luteni Canali Luoga.
  Mkuu wa Kitengo cha Wateja wadogo na wa kati wa benki ya NMB, Omari Mtiga (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi ya Shilingi milioni 26 Mwenyekiti wa klabu ya gofu Lugalo Brigedia Jenerali mstaafu, Michael Luwongo (katikati) zilizotolewa na NMB kudhamini Mashindano maalum ya Mchezo wa Golf ya Mkuu wa Majeshi nchini yanayotarajia kufanyika Oktoba 13 katika viwanja vya Lugalo Dar es Saalam.

  0 0

  Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo leo tarehe 11 Octoba 2018 wakati akizungumza kwenye kongamano maalumu la muelekeo wa siku ya chakula Duniani katika ukumbi wa mihadhara (MLT 9) katika Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo-SUA Mkoani Morogoro. (Picha Zote Na Mathias Canal, WK)

  Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kongamano maalumu la muelekeo wa siku ya chakula Duniani katika ukumbi wa mihadhara (MLT 9) katika Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo-SUA, Mkoani Morogoro. Leo tarehe 11 Octoba 2018
  Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi shahada za awali Chuo kikuu cha Sokoine Bi Suzan Agustino wakati alipowasili kushiriki kongamano maalumu la muelekeo wa siku ya chakula Duniani katika ukumbi wa mihadhara (MLT 9) katika Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo-SUA Mkoani Morogoro. Leo tarehe 11 Octoba 2018
  Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Kushoto) akikagua Shamba la mafunzo ya Mazao ya kipaumbele (Pamba, Kokoa, Kahawa, Chai, Katani, Miwa na Matunda kabla ya kushiriki kongamano maalumu la muelekeo wa siku ya chakula Duniani katika ukumbi wa mihadhara (MLT 9) katika Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo-SUA Mkoani Morogoro. Leo tarehe 11 Octoba 2018.

  Na Mathias Canal, WK-Morogoro

  Utamaduni wa kula aina fulani ya chakula kwa aina moja tu ni miongoni mwa mambo yanayowafanya wananchi kukumbwa na njaa pindi kinapokosekana aina ya chakula kile walichokizoea.

  Moja ya matatizo makubwa katika jamii ni pamoja na wananchi kuamini katika utamaduni wa aina moja ya chakula jambo ambalo halipaswi kutiliwa mkazo kwa namna yoyote.

  Hayo yamebainishwa na Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba Leo tarehe 11 Octoba 2018 wakati akizungumza kwenye mdahalo wa kuelekea siku ya chakula Dunia ambayo hafla ya kilele chake itafanyika Mjini Tunduma Mkoani Songwe tarehe 16 Octoba 2018.

  Katika mdahalo huo ulioandaliwa na Shirika la chakula na kilimo la umoja wa mataifa umoja wa chakula Duniani (FAO), Mpango wa chakula wa umoja wa Mataifa (WFP), Benki ya Kimataifa ya Maendeleo ya kilimo (IFAD) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine, Waziri Tizeba alisema kuwa katika kipindi hichi Kilimo cha kujikimu sio mjadala serikalini na nchi kwa ujumla bali serikali inaendelea na juhudi za makusudi kusisitiza kilimo cha biashara ili wananchi waondokane na umasikini  wa kipato.

  "Na katika hali ya kawaida endapo utekelezaji wa mpango wa kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP II) ukitekelezwa ipasavyo nchi ya Tanzania kabla ya kufikia mwaka 2025 itafikia uchumi wa kati" Alikaririwa Dkt Tizeba na kuongeza kuwa

  " Ni lazima tusisitize wakulima kushughulika na kilimo biashara ili waweze kumudu elimu bora, afya bora na kila kitu"

  Alisema kuwa njaa haijalishi kile kinachozalishwa bali njaa ni umasikini unaosababishwa na kutokuwa na uwezo wa kupata chakula kwani kuna uwezekana mwananchi asizalishe chakula lakini akawa na uwezo wa kununua chakula chochote anachotaka.

  Alisema kuwa serikali imeanza mkakati madhubuti wa kuimarisha masoko ya mazao mbalimbali ndani ya nchi sambamba na kuimarisha masoko ya nje ambapo katika Mpango wa kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP II) muhimili wa tatu ni kuboresha masoko.

  “ Ndugu zangu sio kwamba hatuna chakula wakati mwingine chakula kipo lakini watu hawali vizuri kutokana na mila na tamaduni zetu za kiafrika ambapo kwa wakati wote wanawake ndio wapishi na wanaume kusalia kuwa wahemeaji (Kununua).

  Kwa upande wake Naibu Makamu wa Mkuu wa Chuo cha Sokoine cha Kilimo (Utawala na Fedha) Prof Yonika Ngaga ametoa pongezi kwa waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba kwa kukubali kushiriki mdahalo huo ambao mjadala mkubwa ulihusu kujadili namna bora ya kutatua changamoto ya njaa nchini Tanzania na Barani Afrika kwa ujumla wake


  0 0

  BENKI ya TIB Corporate washeherekea wiki ya huduma kwa wateja kwa kutembelea wateja wake.

  Leo Oktoba 11 benki hiyo wamewatembelea Shirika la Reli Tanzania (TRC) na Shirika la Bima la Taifa (NIC) ikiwa ni kwaajili ya kuwashukuru pamoja na kujitadhimini jinsi ya utoaji wa huduma kwa wateja wao.

  Akizungumza na wafanyakazi wa benki hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa amewashukuru wafanyakazi wa benki hiyo kwa kuwaona wamhimu katika kuendeleza gurudumu serikali ya viwanda hapa nchini kwa utunzaji wa fedha.

  Nae Mkurugenzi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Sam Kamanga amewashukuru kwa kuona nchango wa shirika hilo pia pia amewaasa kujitangaza zaidi ili kuondoa mkanganyiko uliopo katika jina la benki hiyo.


  Mkurugenzi mkuu wa benki ya TIB Corporate Frank Nyabundege akizungumza na wafanyakazi wa beki ya TIB Corporate jijini Dar es Salaam leo ikiwa ni kusheherekea wiki ya huduma kwa wateja ambayo hufanyika kila mwaka ifikapo Oktoba.
   Mfanyakazi wa benki ya TIB Corporate  akizungumza na wafanyakazi wa benki ya TIB Corporate hawapo pichani jijini Dar es Salaam leo ikiwa ni kusheherekea wiki ya huduma kwa wateja.
  Wafanyakazi wa benki ya TIB Corporate wakimkabidhi ua Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa baada ya kutembelewa ofisini kwake na wafanyakazi wa TIB Corporate jijini Dar es Salaam leo ikiwa ni sehemu ya kuwashukuru wateja wa benki hiyo katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja.

  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa  akifurahia jambo mara baada ya kutembelewa na wafanyakazi wa benki ya TIB Corporate jijini Dar es Salaam leo.
  Wafanyakazi wa benki ya TIB Corporate na mfanyakazi wa malaka ya reli Tanzania wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa hayupo pichani mara walikpomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.
  Wafanyakazi wa benki ya TIB Corporate wakiwamkabidhi Mkurugenzi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Sam Kamanga mara baada ya kumtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo ikiwa ni kwaajili ya kushaherekea pamoja na kujitathimini katika wiki ya huduma kwa wateja ambapo benki hiyo imeadhimisha mwaka huu kwa kuwatembelea wateja wake mahali walipo.


  Mkurugenzi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Sam Kamanga mwenye miwaniakizungumza na wafanyakazi wa benki ya TIB Corporate jijini Dar es Salaam leo  ikiwa ni adhima ya benki hiyo kuwatembelea wateja wake.
  Mfanyakazi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) akizungumza na wafanyakazi wa benki ya TIB Corporate jijini Dar es Salaam leo  mara baada ya kuwatembelea ofisini kwao.
     Picha za pamoja za wafanyakazi  wa benki ya TIB Corporate.

  0 0


    Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mbunge wa Kongwa ambaye ni Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, wakati akiwasili Wilayani Kongwa kwenye ziara ya kikazi mkoani Dodoma, Oktoba 11, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  PMO_3509
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimuangalia mtoto Magreth Laurent wa Shule ya Saint Francis Kongwa , akizungumza kuwakilisha watoto katika siku ya mtoto duniani, kabla ya kuzungumza na watumishi wa Halmashari ya Kongwa kwenye ziara ya kikazi mkoani Dodoma, Oktoba 11, 2018. 
  PMO_3569
  Mbunge wa Kongwa ambaye ni Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Kongwa kwenye ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Wilayani Kongwa Dodoma, Oktoba 11, 2018.
  PMO_3591
  PMO_3605
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Kongwa, kwenye ukumbi wa Halmashauri Wilayani hapo, kwenye ziara ya kikazi mkoani Dodoma, Oktoba 11, 2018. 
  PMO_3612
  PMO_3523
  Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wakati akizungumza nao akiwa kwenye ziara ya kikazi mkoani Dodoma, Oktoba 11, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Na: WFM,  Mjini Bali Indonesia
  African Export Import Bank (Afreximbank) ya Misri, imeonyesha nia ya kuipatia Tanzania mkopo wa zaidi ya Shilingi trilioni moja (dola za Marekani zaidi ya milioni 500) kwa ajili ya kutekeleza miradi ya kipaumbele hasa ya miundombinu ya reli na kujenga vituo vya biashara (SEZ and Industrial parks).
  Hayo yalibainishwa mjini Bali Indonesia, na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango baada ya Mkutano na Makamu wa Rais wa Afreximbank Bw. Amr Kamel,  uliofanyika  wakati wa mikutano ya mwaka  ya Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) ikiendelea.
  Waziri Mpango, alisema kuwa Afreximbank imethibitisha kuwa ipo tayari kutoa mkopo wa  dola za Marekani milioni 125  (takribani Shilingi bilioni 285.9) kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha Kimataifa  (SGR),  kipande cha Morogoro hadi Makutupora mkoani Dodoma.
  “Afreximbank wanania pia ya kutoa  dola milioni 400 (takribani Sh. Bilioni 914.9) ambazo wanaweza kutukopesha kwa ajili ya kugharamia miradi ya miundombinu itakayorahisisha biashara kati ya Tanzania na nchi jirani na Bara la Afrika kwa ujumla,  ili kuchochea kasi ya ukuaji wa biashara katika nchi hizo kwa lengo la kuondoa umasikini”, aliongeza Dkt. Mpango.
  Alisema kuwa kwa kuwa tayari Tanzania ilikuwa na mkakati wa kufungua vituo vya biashara katika mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara na mikoa mingine, suala la mkopo huo ni fursa kubwa kwa  maendeleo ya nchi, hivyo jambo hilo litafanyiwa kazi kwa kushirikiana na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji  na Sekta Binafsi, ili Taifa liweze kunufaika na fedha ambazo benki hiyo ipo tayari kuzitoa.
  Aidha, amesema kuwa  katika majadiliano na benki hiyo kuna umuhimu wa kuangalia namna ya rasilimali fedha ambazo Benki Kuu za nchi mbalimbali za Afrika zimekuwa zikiwekeza nje ya Bara hilo, ili ziweze kuwekezwa kwenye benki za Afrika kama Afreximbank ili kuleta maendeleo kwa haraka katika Bara hilo.
  Vile vile benki hiyo imeikaribisha Tanzania kushiriki mkutano wa biashara utakaofanyika mwezi Desemba mwaka huu mjini Cairo Misri, ambapo kwa upande wa Tanzania ni fursa kwa Makampuni ya umma na binafsi kutangaza bidhaa mbalimbali zinazozalishwa kwa lengo la kukuza biashara ndani ya Bara la Afrika.
  Makamu wa Rais wa Afreximbank Bw. Amr Kamel, alisema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi za kimkakati kwa kuwa ina mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi jirani, hivyo Afreximbank imeamua kusaidia miradi mbalimbali ya ujenzi wa miundombinu ili kuharakisha maendeleo ya nchi ya Tanzania na nyingine.
  Waziri Dkt. Mpango ameishukuru Benki hiyo kwa kuisaidia Tanzania katika mkakati wa kufikia uchumi wa kati unaotegemea viwanda ifikapo mwaka 2025, hivyo kuwa Taasisi yenye tija si tu kwa maendeleo ya Tanzania lakini pia kwa Bara la Afrika.
  Imetolewa na :-
  Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  Wizara ya Fedha na Mipango
  Bali, Indonesia
  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto), akizungumzia miradi ya miundombinu ikiwemo ya Reli ya Kisasa kwa kiwango cha kimataifa, katika kuchochea maendeleo ya kiuchumi, wakati wa Mkutano na Makamu wa Rais wa Afreximbank Bw. Amr Kamel, uliofanyika Bali Indonesia, kulia ni Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. John Rubuga.
  Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. John Rubuga, na Afisa Mwandamizi wa Wizara hiyo Bw. Elias Shosi, wakimsikiliza kwa makini Makamu wa Rais wa Afreximbank Bw. Amr Kamel, alipokuwa akizungumzia maamuzi ya benki yake kuikopesha Tanzania zaidi ya Shilingi trilioni moja wakati wa mkutano uliofanyika Bali, Indonesia.
  Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. John Rubuga, na Afisa Mwandamizi wa Wizara hiyo Bw. Elias Shosi, wakimsikiliza kwa makini Makamu wa Rais wa Afreximbank Bw. Amr Kamel, alipokuwa akizungumzia maamuzi ya benki yake kuikopesha Tanzania zaidi ya Shilingi trilioni moja wakati wa mkutano uliofanyika Bali, Indonesia.
  Meneja wa Afreximbank Kanda ya Afrika Mashariki Bw. Kudakwashe Matereke, akieleza jambo wakati wa Mkutano kati ya Makamu wa Rais wa Afreximbank Bw. Amr Kamel na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hawapo pichani), mjini Bali Indonesia wakati wa mikutano ya mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa – IMF.
  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) na Makamu wa Rais wa Afreximbank Bw. Amr Kamel, wakipeana mkono baada ya kumalizika kwa mkutano kati yao uliofanyika mjini Bali Indonesia wakati wa mikutano ya mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa – IMF.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango)

  0 0


  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Kamishna Diwani Athuman wakizungumza na Maofisa Wakuu wa Polisi waliopo Makao Makuu ya Polisi wakati wa kikao cha kuweka mikakati ya kuzuia na kupambana na rushwa. 
  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Kamishna Diwani Athuman (kushoto) wakati Mkurugenzi huyo na ujumbe wake walipotembelea Makao Makao Makuu ya Polisi na kufanya kikao na Maofisa Wakuu wa Polisi kwa lengo la kuweka mikakati ya kuzuia na kupambana na rushwa. Wengine ni Naibu Mkurugenzi Mkuu Brigedia Jenerali John Mbungo na Kamishna wa Utawala na Raslimali watu Albert Nyamhanga. (Picha na Jeshi la Polisi).
  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Kamishna Diwani Athuman wakiwa katika picha ya pamoja na Maofisa na Viongozi wengine baada ya kumaliza kikao kwa lengo la kuongeza kasi katika kuzuia na kupambana na rushwa. 
  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Kamishna Diwani Athuman baada ya kumaliza kikao na Maofisa Wakuu wa Polisi Makao Makuu ya Polisi kwa lengo la kuongeza kasi katika kuzuia na kupambana na rushwa. (Picha na Jeshi la Polisi)

  0 0  Watalii wakiwa kando ya Mto Mara katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ,eneo la Kogatende wakishuhudia tukio kubwa la kuhama kwa Makundi Makubwa ya Nyumbu wakivuka mto kutoka Hifadhi ya Masai Mara nchini Kenya kuingia Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
  Kundi la Nyumbu likijiandaa kuvuka Mto Mara katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

  Nyumbu wakivuka Mto Mara kuingia katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti .
  Baadhi ya Watalii wamelazimika kuongeza siku za kukaa katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa ajili ya kushuhudia tukio hilo la aina yake ambalo hutokea kila mwaka .
  Kundi kubwa la Nyumbu likiwa katika maandalizi ya kuvuka Mto Mara kuingia Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

  Magari yaliyobeba Watalii yakiwa yameegeshwa kando ya Mto Mara kusubiri tukio la kuvuka kwa Makundi ya Nyumbu katika Mto Mara kuingia Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
  Mamba wakiwa Mto Mara katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakiwa katika mawindo ya Mnyama Nyumbu wakati akivuka.

  Mnyama Pundamlia wakiwa upande wa pili mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ,tunaweza sema ni kama wako hapo kwa ajili ya mapokezi ya Nyumbu wanarudi kutoka katika Hifadhi ya Masai Mara nchini Kenya.
  Eneo la Mto Mara ambapo Watalii wakingojea tukio la kuvuka kwa Makundi ya Nyumbu.  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini .

  Hifadhi ya Taifa ya Serengeti iliyopo Mkoani Mara,imeendelea kuwa maarufu Duniani na kuvutia watalii wengi zaidi kutoka maeneo mbalimbali ya Dunia kwa ajili ya kujionea tukio la kila mwaka la kuhama kwa Makundi makubwa ya Nyumbu kutoka Hifadhi ya Masai Mara nchini Kenya na kuingia Serengeti.

  Tukio hili ambalo hutokea kuanzia mwezi Julai na wageni kulipa jina la “Great Wildebeest Migration” mwaka huu linatajwa kuvutia watalii wengi zaidi huku wengine wakilazimika kuongeza siku za kukaa katika Hifadhi ya Serengeti wakingojea kushuhudia tukio hilo.

  Michuzi blog imeshuhudia Msururu wa Magari ya kubeba watalii yakiwa na wageni kando ya Mto Mara kusubiri kujionea hali inavyokuwa wakati wanyama hao wakivuka kwa makundi kutoka upande mmoja wa mo kuingia Hifadhi ya Serengeti.

  Eneo la Mto Mara ambapo Wanyama hawa wamekuwa wakivuka linatajwa kuwa na Vivuko 10 hali inayochangia waongoza watalii kufuata mwenendo wa Nyumbu kwa sababu si rahisi kufahamu wapi wataelekea kuvuka jambo ambalo hutumia zaidi ya saa 5 hadi 7 kungojea tukio hilo.

  Tukio la misafara ya makundi ya wanyama hao kuhama na kurudi hubadilika kila mwaka kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na kiwango cha maji katika mto mara hata hivyo limeendelea kuwa kivutio kikubwa kwa wageni .

  Kivutio kikubwa katika misafara ya wanyama hao ambao wamekuwa wakiondoka nchini kila mwaka kuanzia mwezi mey na kurudi kuanzia mwezi julay ni namna wanavyovuka mto mara na jinsi wanavyokabiliana na wanyama wengine ndani ya mto huo wakiwemo Mamba

  0 0


  0 0


  Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba akizungumza mara baada ya kushuhudia utiaji saini hati ya makabidhiano ya ukopeshaji wa matrekta kwa vyama vya ushirika vya msingi katika Ukumbi mdogo wa Mikutano Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo (SUA) Mjini Morogoro leo tarehe 11 Octoba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, WK)
  Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa Benki ya Maendeleo ya kilimo (TADB), Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba Ndg Marco Mtunga na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Prof Damian Gabagambi wakionyesha hati ya makabidhiano ya ukopeshaji wa matrekta kwa vyama vya ushirika vya msingi katika Ukumbi mdogo wa Mikutano Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo (SUA) Mjini Morogoro leo tarehe 11 Octoba 2018.
  Naibu Waziri wa kilimo Mhe Omary Mgumba akizungumza mara baada ya kushuhudia utiaji saini hati ya makabidhiano ya ukopeshaji wa matrekta kwa vyama vya ushirika vya msingi katika Ukumbi mdogo wa Mikutano Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo (SUA) Mjini Morogoro leo tarehe 11 Octoba 2018.
  Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali mara baada ya kushuhudia utiaji saini hati ya makabidhiano ya ukopeshaji wa matrekta kwa vyama vya ushirika vya msingi katika Ukumbi mdogo wa Mikutano Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo (SUA) Mjini Morogoro leo tarehe 11 Octoba 2018.

  Na Mathias Canal-WK, Morogoro


  Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba leo tarehe 11 Octoba 2018 ameshuhudia utiaji saini hati ya makabidhiano ya ukopeshaji wa matrekta kwa vyama vya ushirika vya msingi.


  Katika hafla hiyo iliyofanyika katika Ukumbi mdogo wa Mikutano katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo (SUA) Mjini Morogoro Waziri Tizeba amesisitiza matrekta hayo kutumika ipasavyo kwenye sekta ya kilimo ili kuongeza tija kwenye uzalishaji wa kilimo nchini jambo litakalokuwa na manufaa kwa mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.


  Taasisi ambazo zimeshirikiana kufanikisha utiaji saini huo ni Bodi ya Pamba ambayo ipo chini ya wizara ya kilimo, Benki ya Maendeleo ya kilimo-TADB, Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) na Tume ya Maendeleo ya ushirika.


  Dkt Tizeba alisema kuwa Vyama vya ushirika vya msingi vinapaswa kuongeza juhudi katika kilimo ili kuakisi kulipa gharama za mkopo ambao ni asilimia 20 ya mkopo wote katika kipindi cha miaka mitatu huku asilimia zingine 80 zikilipwa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo-TADB.


  Utiaji huo wa saini hati ya makabidhiano ya ukopeshaji wa matrekta 300 kwa vyama vya msingi vya ushirika unajili wakati ambapo hivi karibuni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa alimkabidhi Waziri wa kilimo Dkt Charles Tizeba jumla ya matrekta 500 ya Ursus kwa ajili ya kukopeshwa kwenye  vyama vya ushirika vya msingi ili wakulima kunufaika na tija katika kilimo hususani zao la Pamba.


  Akizungumza mara baada ya kushuhudia utiaji saini Dkt Tizeba alisema kuwa sekta ya kilimo nchini bado inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo tija ndogo inayosababishwa na matumizi madogo ya pembejeo, huduma duni za ugani na matumizi ya zana duni za kilimo ambapo wakulima wengi wanatumia majembe ya mkono au kutumia maksai wakati wa kulima.


  “Katika kilimo cha Pamba msimu wa mwaka 2017/2018 ushahidi unaonyesha wakulima walichelewa kuanza kuandaa mashamba kwa sababu Maksai wakati wa kiangazi wanadhoofu sana,” Alikaririwa Dkt Tizeba na kuongeza kuwa


  “Mara mvua inaponyesha hawawezi kulima mpaka majani yawe mengi ndio wapate nguvu za kuanza kulima, hali hii inaondoa uwezekano wa wakulima kutumia teknolojia mpya katika kilimo kama vile kilimo hifadhi ambacho kimedhihirika kuongeza tija zaidi ya mara mbili” 


  Tizeba alisema mtazamo wa mpango huo ni kuunganisha nguvu za mkulima mmoja mmoja ili kuharakisha kuleta maendeleo yao ambapo utatekelezwa kwa kutumia sehemu ya fedha zinazolipwa AMCOS kama kamisheni ya kusimamia ununuzi wa pamba ambapo matarajio ni kukusanya Bilioni 6 kama uzalishaji wa pamba utafika kilo milioni 400 kwa mwaka.


  Alisisitiza kuwa Bodi ya Pamba pamoja na Tume ya Maendeleo ya ushirika zinapaswa kufuatilia kwa karibu hatua zote mwenendo wa ufanyaji kazi wa matrekta hayo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa punde yanapoanza kufanya kazi yawe yanafanyiwa marekebisho ya mara kwa mara.

older | 1 | .... | 1694 | 1695 | (Page 1696) | 1697 | 1698 | .... | 1896 | newer