Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1693 | 1694 | (Page 1695) | 1696 | 1697 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA) Dkt. Anold Mathias Kihaule, ameenza kazi kwa kukagua utendaji wa ofisi za Usajili za Mkoa wa Dar-es-salaam ambapo pamoja na mambo mengine amezungumza na wananchi na kutembelea ofisi ya Serikali ya Mtaa ambako huduma ya utoaji wa fomu na ugawaji wa Vitambulisho zinaendelea.

  Katika ziara hiyo Dkt. Kihaule aliyekuwa ameambatana na baadhi ya viongozi wa Mamlaka hiyo; amepongeza kazi nzuri inayofanywa na wafanyakazi wa NIDA na kusisitiza watumishi kuzingatia utoaji wa huduma unaozingatia viwango ili kuweza kupunguza malalamiko yasiyo ya lazima kwa wananchi.

  Aidha amewashukuru viongozi na Watendaji katika Serikali za Mitaa kwa kazi nzuri ya kuwahudumia wananchi kuhakikisha wanapata Vitambulisho vya Taifa na kuahidi kuendelea kuwapa ushirikiano katika kuhakikisha malengo ya Serikali yanafikiwa.

  Dkt. Anold Mathias Kihaule aliteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo akijaza nafasi iliyoachwa wazi na Ndg. Andrew W. Massawe aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Ajira na Walemavu.

  Pichani ni mmoja wa wakazi wa Kinondoni akimuelezea Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulish vya Taifa(NIDA), Dkt. Anold Mathias Khaule (wa pili kushoto) namna alivyopatiwa huduma katika ofisi ya Usajili Wilaya ya Kinondoni
  Mkurugenzi Mkuu wa NIDA akikagua fomu ya mmoja wa wananchi waliojitokeza kusajiliwa. Kutoka kulia ni Bw Dickson Mbanga Afisa Usajili wilaya ya Kinondoni na katikati ni Bw. Alphonce Malibiche, Mkurugenzi wa Idara ya Uzalishaji Vitambulisho vya Taifa.
  Mkurugenzi Mkuu NIDA akikagua sehemu ya kutunzia Vitambulisho vya Taifa katika ofisi ya Usajili wilaya ya Kinondoni. Kuli ni Afisa Usajili wilaya ya Kinondoni na wa kwanza kushoto ni Bw. Melkiory Ndofi Mkurugenzi wa Idara ya Fedha na Utawala.
  Mkazi wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Gift Emmanuel Nkya (aliyevaa nguo nyeusi) mwanafunzi wa mwaka wa kwanza chuo cha Biashara CBE, akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa NIDA alipotembelea kituo cha Usajili Kawe jijini Dar-es-salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Dkt. Anold Mathias Kihaule akiweka saini katika kitabu cha wageni ofisi ya Usajili wilaya ya Kinondoni wakati alipofanya ziara kukagua namna shughuli za Usajili zinavyofanyika kituoni hapo
  Mkurugenzi Mkuu wa NIDA (aliyevaa koti) akiingia kwenye ofisi ya Serikali Mtaa wa Mzimuni wakati wa ziara yake kukagua uendeshaji shughuli za Usajili Wilaya ya Kinondoni. Hapa alishuhudia utaratibu wa ugawaji fomu za Usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi na utaratibu wa kugawa Vitambulisho vya Taifa kupitia ofisi za Watendaji.


  0 0


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa mkoa wa Kagera katika kikao cha majumuisho ya ziara yake ya kikazi mkoani Kagera kwenye ukumbi wa ELCT, mjini Bukoba, Oktoba 9, 2018. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti, Naibu Waziri wa Kilimo, Dkt. Mary Mwanjelwa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Baadhi ya viongozi wa mkoa wa Kagera wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia kikao cha majumuisho ya ziara yake ya kikazi mkoani Kagera kwenye ukumbi wa ELCT, mjini Bukoba. Oktoba 9, 2018.  …………………

  *Ni kutokana na biashara za magendo zinazoendelea wilayani humo

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amechukizwa na biashara za magendo zinazoendelea katika wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera, hivyo amewataka viongozi wa wilaya hiyo wajipime wenyewe.

  Pia, Waziri Mkuu amemuagiza Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Kagera Bw. Adam Ntogha kumsimamisha kazi Afisa wa Forodha katika mpaka wa Mulongo Bw. Peter Mtei kwa tuhuma za kujihusisha na biashara za magendo. Ametoa agizo hilo jana (Jumanne, Oktoba 9, 2018) wakati akizungumza na viongozi wa mkoa wa Kagera katika kikao cha majumuisho ya ziara yake ya kikazi ya siku nne mkoani hapa kilichofanyika mjini Bukoba.

  “Biashara za magendo zinafanyika bila ya wao kuchukua hatua, mnatia aibu yaani hakuna kazi inayofanyika. Viongozi wa wilaya ya Kyerwa mjipime wenyewe, mialo mingi katika wilaya yenu inatumika kwa biashara ya magendo na butura.”

  Waziri Mkuu aliongeza kuwa katika mwalo wa Mulongo ulipo kwenye eneo ambalo Tanzania inapakana na nchi za Uganda na Rwanda, biashara za magendo na butura zinafanyika na hakuna kiongozi wanaochukua hatua. Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alimtaka Meneja wa TRA asiwahamishe watumishi wabovu kutoka kituo kimoja cha forodha na kuwapeleka kingine kwa kuwa huko wanakowapeleka wanakwenda kuendeleza biashara za magendo na kuikosesha Serikali mapato.

  Alitolea mfano mtumishi wa mamlaka hiyo Bw. Mtei ambaye alihamishiwa kituo cha Mulongo akitokea kwenye kituo cha Mtukura kilichopo katika mpaka wa Tanzania na Uganda kwa tuhuma za kuchua rushwa na kushirikiana na wafanyabiashara wa burura. Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema mtumishi huyo tayari alishapewa barua ya uhamisho kwenda katika kituo cha forodha cha Rusumo miezi minne iliyopita hadi sasa hajahama na anaendelea na biashara za magendo ambapo Agosti 5, mwaka huu anadaiwa kupitisha mzigo wa magendo uliobebwa kwenye gari aina ya fuso yenye za usajili T 957 AXF mali ya Erasto Muga.

  “Meneja TRA msimamishe kazi Bw. Mtei leo (jana) hatuwezi kuwa na watumishi wabovu alafu nyie mnawahamisha vituo ili wakaendelee kuharibu eneo lingine. Mnajua mkakati wa Serikali hii ni kudhibiti rushwa hivyo hatuwezi kuvumilia suala hili.” Kadhalika, Waziri Mkuu alimuagiza Meneja wa TRA wa mkoa wa Kagera Bw. Ntogha afanye ukaguzi kwenye vituo vyote vya forodha katika mkoa huo pamoja na kuongeza idadi ya watumishi na kudhibiti vitendo vya rushwa.

  0 0


  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  SERIKALI imezindua mfumo wa kitaifa wa uboreshaji upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kupitia mshitiri(Mzabuni binafsi).

  Mfumo huo maarufu kwa jina la Jazia unalenga kuongeza ufanisi wa upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vinavyokosekena Bohari Kuu ya Dawa (MSD) ili kuboresha upatikanaji wa bidhaa za afya katika vituo vya tiba.

  Mfumo huo umezinduliwa rasmi leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Ofisi ya Rais(TAMISEMI) Suleiman Jaffo ambapo amesema unakwenda kusaidia kuondoa changamoto ya kukosekana kwa dawa na vifaa tiba katika vituo vya tiba.

  "Mfumo huu wa uboreshaji upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kupitia mshitiri kutaongeza kasi ya upatikanaji dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara ili kupunguza muda wa kusubiri huduma na kupatikana kwa bidhaa za afya wakati wote,"amesema Jaffo.

  Ameongeza mfumo huo ambao umezinduliwa rasmi leo utakuwa ni wa nchi nzima na kutoa maagizo kwa mikoa yote nchini kujiunga na mfumo huo na ifikapo Oktoba 30 mwaka huu na tayari unatumika nchini kote.Amesema Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi madhubuti wa Rais Dk.John Magufuli moja ya vipaumbele vyake ni kuboresha sekta ya afya nchini kwa kuondoa changamoto zilizipo.

  "Hivyo mfumo huu unakwenda kumaliza tatizo la kukosekana kwa dawa katika vituo vya tiba,"amesisitiza.Amesema anatambua na kuthamini kazi nzuri ya MSD katika kusambaza dawa na vifaa tiba lakini mfumo huo utasaidia pale ambapo MSD wameshindwa kufikisha dawa au vitaa tiba hivyo.Ametoa maagizo kwa halmashauri zote nchini kuanzia sasa baada ya mfumo huo kuzinduliwa rasmi upatikanaji wa dawa katika vituo vya tiba uwe asilimia 98 na kuwataka wakurugenzi wa halmashauri kushiriki kikamilifu.

  Amesisitiza ni matumaini yake mfumo huo umekuja kumaliza tatizo la kukosekana kwa dawa na kama tatizo basi limepata tiba yake.Kikubwa ni kuhakikisha mfumo unasimamiwa vema kwa maslahi ya Watanzania wote.Ametumia nafasi hiyo kuzungumzia mikakati ya Serikali ya Awamu ya tano katika kuboresha sekta ya afya ikiwemo ya ujenzi wa hospitali za Wilaya na ujenzi wa vituo vya afya na lengo ni kuu ni kuboresha sekta ya afya nchini.

  Kwa upande wa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Grace Magembe amesema mfumo huo ambao umezinduliwa leo wao waliamua kuufanyia utafiti na kubaini utamaliza tatizo la kukosekana kwa dawa na vifaa tiba ndani ya mkoa huo."Kwetu sisi ni tofauti na mikoa mingine tuliamua kufanya utafiti kwanza na kubaini mahitaji halisi ya dawa na vifaa tiba.Hivyo leo tunaingia mkataba na wazabuni wetu tukijua mahitaji yetu,"amesema .

  Amefafanua wakati wa utafiti huo wamebaini mambo mengi kwani wamegundua kuna kampuni ambayo kazi yake ni vifaa vya umeme lakini ilipewa jukumu la kusambaza dawa.Amesema hivyo kupitia mfumo huo ambao umezinduliwa wapo makini kwa kuhakikisha wanaopewa jukumu la kusambaza dawa na vifaa tiba wamekidhi vigezo vyote na watalaam wa kada mbalimbali wameridhika.Amesema kwa Mkoa wa Dar es Salaam mzabuni binafsi ambaye amepewa jukumu hilo ni Bahari na Umoja ambao wameingia nao mkataba na kikubwa zaidi bei ambayo itatumika ni ile ambayo ipo sawa na bei ya MSD au chini.

  Kuhusu mfumo huo imeelezwa umejaribiwa kwa miaka minne katika mikoa ya Dodoma,Morogoro na Shinyanga tangu mwaka 2014.Mpango huo ulianzishwa na mradi wa ushirikiano wa nchi mbili kati ya Tanzania na Uswisi kupitia mradi wa Health Promotion and System Strengthening (HPSS) ambao pia unajulikana kama "Tuimarishe Afya Proejct" unaofadhiliwa na na Serikali ya Uswi
  si.

  Pia kwa muda mrefu usambazaji wa dawa na vifaa tiba nchini umekuwa ukifanywa na sekta ya umma pekee kupitia MSD lakini pamoja na juhudi zote za MSD kutokana na ukubwa a nchi wamekuwa wakisambaza dawa na vifaa tiba kati ya asilimia 50 hadi asilimia 60.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( TAMISEMI),Selemani Jafo akizungumza  na wadau mbalimbali wa afya katika  hafla ya uzinduzi wa mfumo wa mshitiri Kitaifa leo jiji Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( TAMISEMI),Selemani Jafo akizindua mfumo wa kitaifa wa uboreshaji upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kupitia mshitiri (Mzabuni binafsi) jana jijini Dar es Salaam.(kushoto) Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda.(Picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii).
   Sehemu ya wadau wa afya wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa mfumo wa Mshitiri Kitaifa jana jijini Dar es Salaam.
  Picha ya pamoja

  0 0


  0 0

  Na. Benedict Liwenga-TRA.

  WAFANYABIASHARA Mkoani Songwe wametakiwa kujitokeza kwa katika Kampeni ya Usajili na Elimu kwa Mlipakodi inayoendeshwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

  Kauli hiyo imetolewa leo na Afisa Kiongozi wa Kituo cha Huduma cha TRA mjini Tunduma wakati wa Kampeni ya Usajili na Elimu kwa Walipakodi mkoani hapo ambapo amewataka Wafanyabiashara kujitokeza kwa wingi kuweza kupatiwa huduma hiyo pasipo gharama yoyote.

  Bwana Mwita ameeleza kuwa, mwitikio wa wafanyabiashara katika kampeni hiyo ni mkubwa, ambapo wengi wa Wafanyabiashara ambao walikuwa hawana Namba ya Utambulisho ya Mlipakodi (TIN) wameshasajiliwa na kupatiwa TIN hizo.

  “Zoezi hili ni zuri na mwitikio wa watu ni mkubwa, niwaombe Wafanyabiashara waendelee kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kupatiwa TIN na elimu kuhusu masuala ya kodi”, alisema Mwita.

  Kwa upande wake Kiongozi wa msafara kutoka TRA Makao Makuu ambaye pia ni Afisa Mkuu Mwandamizi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Bi. Rose Mahendeka amesema kwamba, zoezi la usajili na utoaji elimu kwa mlipakodi litadumu mkoani Songwe kwa muda siku sita, ambapo wafanyabiashara wanahimizwa kuchangamkia fursa hiyo ili waweze kutatua kero mbalimbali zinazowakabili.

  “Kampeni hii katika Mkoa huu wa Songwe litadumu kwa muda wa siku sita na tayari tumeshaanza na maeneo mbalimbali kama vile Vwawa, Mlowo, Tunduma na baadaye tunaendelea na maeneo ya Mkwajuni, Ileje pamoja na Saza lengo ni kuwahamasisha wananchi hususan wafanyabiashara kuitikia wito wa kampeni hii”, alisea Mahendeka.

  Afisa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi toka TRA, Bi. Maya Magimba anafafanua kuwa, zoezi la utoaji huduma katika kampeni hiyo limeonekana kuwavutia wakazi wengi wa mjini hapo ambapo mpaka sasa hawajakumbana na changamoto yoyote kubwa.

  “Kwakweli mpaka sasa kampeni hii inaendelea vizuri na tumepata wateja wengi wenye uhitaji wa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi na tayari tumewasajuli na kuwapatia TIN zao lakini pia tumewapa elimu. Kuhusu changamoto katika kampeni hii ni chache sana ambapo hazijatukwamisha kuendelea na zoezi letu la kuwahudumia walipakodi wetu”, alisema Magimba.

  Kwa upande wao baadhi ya Wafanyabiashara katika Wilaya ya Momba mjini Tunduma wameeleza kufurahishwa na kampeni hiyo huku wakiiomba TRA kuendelea kuwapatia elimu kwani wengi wao walikuwa hawana elimu ya kutosha kuhusu masuala ya kodi na kuahidi kuwa mabalozi wa kuwahamisha wengine kulipa kodi kwa hiari.


  Kampeni ya Usajili na Elimu kwa Mlipakodi katika Mkoa wa Songwe inalenga kuongeza idadi ya Walipakodi wapya ikiwemo kuwapatia elimu wafanyabiashara kuhusu masuala mbalimbali ya kodi, ambapo mpaka sasa jumla ya wafanyabiashara zaidi 100 mkoani hapo wamesajiliwa na kupatiwa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) ambapo zoezi hilo bado linaendelea mpaka mwisho wa wiki hii.


  Afisa Mkuu Mwandamizi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bi. Rose Mahendeka (kushoto) akiwaeleimisha baadhi ya Wafanyabiashara wa Tunduma wakati wa Kampeni ya Usajili na Elimu kwa Mlipakodi inayoendelea Mkoani Songwe.

  Baadhi ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) (kushoto) wakiwasajili na kuwapatia elimu ya kodi Wafanyabiashara wa Tunduma wakati wa Kampeni ya Usajili na Elimu kwa Mlipakodi inayoendelea Mkoani Songwe.(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-TRA).

  0 0

  Mhe Mbarawa akiongozwa na wataalamu wa kampuni ya Sinohydro Corporation Ltd kuangalia mwamba unaotoa maji ardhini kwa kutumia camera maalumu. Picha na Vero Ignatus.
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Mbarawa akikagua urefu wa kisima katika kijiji cha Levolosi kata ya Kimnyaki akiwa ameambatana na wahandisi toka wizara ya maji na mamlaka ya maji safi na usafishaji jijinla Arusha AUWSA. Picha na Vero Ignatus


  Na. Vero Ignatus, Arusha

  Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof.Makame Mbarawa amelazimika kusitisha ziara kwa masaa mawili na nusu akisubiri kisima katika kijiji cha Levolosi Kata ya Kimnyaki Wilayani Arumeru kinachochimbwa kitoe maji kabla ya kwenda kusaini mkataba.

  Aidha Prof. Makame Mbarawa amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kumrudisha Wizarani mara moja Mhandisi wa Miamba Amir Msangi kwa uzembe wa kutoonekana kwenye eneo la mradi.

  Waziri alitoa agizo hilo jana wakati alipotembelea Kijiji cha Levolosi, Kata ya Kimnyaki kujionea zoezi la uchimbaji wa visima vitatu na baada ya hapo alitia saini ya mkataba wa ujenzi wa mtandao mpya wa maji,mitambo ya kutibu maji safi ujenzi wa ofisi kuu ya AUWSA na ujenzi wa ofisi kuu ya AUWSA Kanda ya Kati wenye thamani ya Sh.bilioni 520.

  Prof.Mbarawa alisema serikali imeamua kuleta wataalam wake toka Wizarani ili wasimamie na kujifunza Teknolojia mpya ya uchimbaji visima vikubwa kwa ajili ya kuweza kufundiaha wenzao utaalam huo hapo baadaye.

  "Lakini cha kushangaza nimepata taarifa huyu Amir Msangi haonekani eneo la kazi na hivyo namwagiza mtaalam mwenzake Fatuma Mambo kumtaarifu Katibu Mkuu ili arudishwe Wizarani huyu na hapa aletwe mwingine atakayepata ujuzi huu,"alisema.Amesisitiza kuwa lengo kubwa la serikali ni kuwaleta wataalam hao ili kuhakikisha miradi ya maji inayotekelezwa inakuwa na ubora uliokusudiwa.

  Alisema kukamilika kwa mradi huo kutasaidia wananchi kupata maji kwa asilimia 95 ifikapo mwaka 2020.Aidha alisema miradi hiyo inatekelezwa na AUWSA kwa ufadhili wa serikali kupitia mkopo wa masharti nafuu toka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).

  Naye Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Arusha (AUWSA) Mhandisi Ruth Koya alisema mradi huo utakamilika Juni mwaka 2020 na wanatarajia Arusha itanufaika na mradi huo kwa kuwa ukosefu wamaji utakua historia.

  "Kwa kuanza tayari wakandarasi wameanza kusambaza mabomba ya maji taka nakuweka ya kisasa na makubwa yanayoendana na mahitaji ya sasa,lengo mazingira yawe safi na wananchi wapate huduma zamaji safi bila shida,"alisema

  Mhandisi Koya alisema zaidi ya wananchi 827,000 watanufaika na mradi huo ambao utazalisha maji lita milioni 200 kwa siku.Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya AUWSA, Dk.Richard Masika alisema ili miradi hiyo inayotekelezwa sasa iwe mfano na endelevu wamewapatia mafunzo Timu ya Menejimenti na watumishi wengine toka kwa wataalamu wa Jumuiya ya kusimamia mikataba ya Kimataita.

  "Ikukwepa gharama serikali tulimgharamia kuleta wataalam hawa toka nchi ya Switzerland"

  0 0

  Dar-es-Salaam, Tanzania – Wednesday, 10 October 2018:

  Letshego Bank Tanzania has expressed its commitment to serve Tanzanians especially, financially underserved micro and small entrepreneurs with simple and accessible financial solutions.

  The Bank’s newly appointed Chief Executive Officer Mr Thabit Ndilahomba said in Dar es Salaam yesterday that extending Letshego’s reach and enhancing the bank’s value proposition for customers, staff and other stakeholders is one of his priorities. “In line with Letshego Group’s regional strategy, Letshego Tanzania offers simple and accessible financial solutions that focus on the needs of individuals, as well as micro and small entrepreneurs,” he said.

  Thabit Ndilahomba, CEO Letshego Bank Tanzania added, “I am excited about the opportunities that my new role presents in delivering a strategy that not only enhances Letshego’s brand and reputation in Tanzania, but also stands to bring further value and benefits to one of our most important stakeholders, our customers,”

  “By increasing access to appropriate financial solutions and encouraging our customers to use their funds for productive purposes, Letshego aims to support the growth of economically active members in the local economy,” Formerly, the Chief Financial Officer FINCA, Mr Thabit plans to bring to his new role a valuable understanding and appreciation for the financial dynamics and performance of the business as a whole.

  On his part, Letshego’s Group CEO, Smit Crouse said Mr Thabit’s local experience gained from multiple growth sectors in Tanzania, as well as his financial skills and background position him well in delivering Letshego’s strategic ambition for Tanzania. “Letshego remains committed to Tanzania while progressing in its ambition towards providing solutions that create opportunity and flexibility for both individuals and small businesses, across Tanzania,” he said.

  Prior to joining Letshego, Thabit worked for FINCA Microfinance Bank where he held various senior positions including Chief Finance Officer and Chief Accountant. Thabit’s career also includes tenure with the RENCO Group, where he was Chief Accountant and Chief Financial Analyst. Thabit commenced his career as a Tax Assessor at the Tanzania Revenue Authority.

  Since taking up his role at the helm, Thabit Ndilahomba announced Letshego’s recent strategic partnership with Airtel Tanzania and Jumo, a savings option entitled ‘Timiza Akiba’. This innovative savings solution aims to promote a local savings culture by enabling customers to save money in their mobile wallets, incentivizing committed customers with rewards and interest, even on low account balances.

  Letshego in Tanzania has more than 240 employees, offering credit, savings and transactional solutions to individuals as well as small and micro entrepreneurs, with a special focus on affordable housing, education and health sectors.

  Letshego Bank Tanzania CEO Thabit Ndilahomba gestures as he makes presentation during launch of TIMIZA AKIBA (Past event). The recently appointed CEO is committed to extending Letshego’s reach and enhancing their value proposition for customers, staff and other valued stakeholders in Tanzania which is in line with Letshego Group’s regional strategy. (Photo by our Correspondent)


  0 0

  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (JWTZ) Jenerali Venance Mabeyo  akizungumza mara baada ya kutembelea mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa ya standard gaurge kutoka kituo cha Ilala hadi kituo cha Soga.

  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (JWTZ) Jenerali Venance Mabeyo akimsikiliza maelezo kutoka kwa Wafanyakazi wa kampuni iliyojenga reli ya mwendokasi ya Yapi Markez jijini Dar es Salaam kabla ya kuanza ziara ya kutembelea mradi wa ujenzi wa reli hiyo.
  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (JWTZ) Jenerali Venance Mabeyo  pamoja na baadhi ya wanajeshi wakiangalia jinsi mataaluma yanavyotengenezwa katika kituo cha Soga.
  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (JWTZ) Jenerali Venance Mabeyo  akizungumza na waandishi wa habari  katika kituo cha soga mara baada ya kutembelea na kukagua jinsi mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa standard george.
  Baadhi ya mataaluma kushoto yakiwa tayari kwa kutandikwa reli ya kisasa ya standard gaurge.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania(TRC) Masanja Kadogosa  akitoa maelezo kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (JWTZ) Jenerali Venance  Mabeyo wakati alipoembelea ujenzi wa reli ya kisasa ya standarge gaurge.
  Sehemu ya reli ambayo imekamilika.


  0 0

  Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na walemavu Mhe Jenista Mhagama (Mb) akizungumza jambo wakati akifungua kikao cha Mawaziri wa sekta za kilimo juu ya utekelzaji wa Mpango wa kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP II) leo tarehe 10 Octoba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-WK)
  Kutoka kushoto ni waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mhe Willium Lukuvu (Mb), Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) na Naibu waziri wa Fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijaji wakifatilia kwa umakini kikao cha Mawaziri wa sekta za kilimo juu ya utekelzaji wa Mpango wa kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP II) leo tarehe 10 Octoba 2018.
  Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akieleza umuhimu wa kuanza haraka utekelezaji wa ASDP II wakati wa kikao cha Mawaziri wa sekta za kilimo juu ya utekelzaji wa Mpango wa kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP II) leo tarehe 10 Octoba 2018.
  Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mhe Willium Lukuvu (Mb), akisisitiza jambo wakati wa kikao cha Mawaziri wa sekta za kilimo juu ya utekelezaji wa Mpango wa kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP II) leo tarehe 10 Octoba 2018. Mwingine ni Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba.
  Naibu waziri wa Fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijaji akieleza utayari wa ushiriki wa wizara yake wakati wa kikao cha Mawaziri wa sekta za kilimo juu ya utekelzaji wa Mpango wa kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP II) leo tarehe 10 Octoba 2018.
  Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na walemavu Mhe Jenista Mhagama (Mb) akizungumza jambo wakati akifungua kikao cha Mawaziri wa sekta za kilimo juu ya utekelzaji wa Mpango wa kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP II) leo tarehe 10 Octoba 2018.  Na Mathias Canal, WK-Dodoma

  Mawaziri wa wizara za sekta ya kilimo leo tarehe 10 Octoba 2018 wametuama kwa masaa kadhaa Mjini Dodoma katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kujadili kwa kina kuhusu maandalizi ya utekelezaji wa Mpango wa kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP II).

  Wizara washirika katika kutekeleza ASDP II ni pamoja na Wizara ya kilimo, Wizara ya mifugo na Uvuvi, Wizara ya Viwanda, Biashara, na Uwekezaji Wizara ya Maji, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi, na Ofisi ya Rais-TAMISEMI.

  Utekelezaji wake utachagizwa pia na Wabia wa maendeleo, Sekta binafsi, Taasisi zisizo za kiserikali, Wakulima, Wafugaji na Wavuvi.Mawaziri hao wakiongozwa na Mwenyekiti ambaye ni Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na walemavu Mhe Jenista Mhagama (Mb) wameridhia kwa pamoja kuanza haraka utekelezaji wa mradi huo wa ASDP II ambao utakuwa chachu ya ukuzaji wa uchumi kupitia kilimo.

  Majadiliano hayo yalijikita zaidi kujadili mapendekezo ya kikao cha makatibu wakuu wa wizara za sekta ya kilimo kilichofanyika tarehe 30 Agosti 2018 pia kujadili namna bora ya Uratibu wa ASDP II, na Mikakati ya kutafuta fedha za kugharamia utekelezaji wa ASDP II.

  Katika Mkutano huo Mwenyekiti ambaye ni Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na walemavu Mhe Jenista Mhagama (Mb) aliitaka timu ya ASDP II Taifa kueleza kwa kina mikakati ya kuboresha masoko ya mazao ya kipaumbele yaliyoainishwa katika utekelezaji wa ASDP awamu ya pili.

  Alisema kuwa kumekuwa na uhamasishaji mkubwa kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kulima pindi unapofika msimu wa kilimo lakini bado hamasa ya kutafuta masoko ni ndogo jambo ambalo linageuka karaha kwa wakulima nchi hivyo muarobaini wa kutafuta masoko ndio njia pekee ya kumkomboa mkulima.

  Kwa upande wake Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba akizungumza katika kikao hicho alisema kuwa “ Majira ya Nchi yetu tunaendeshwa na msimu wa kilimo hivyo tunapaswa kutekeleza mpango wa kuendeleza sekta ya kilimo kwa haraka ili kuendana na msimu” Alisema

  Aidha, alisema kuwa punde utekelezaji utakapoanza wafadhili wa mradi huo wanapaswa kupewa uhuru wa kuchagua eneo watakalosaidia ili kuongeza chachu na ufanisi wa haraka katika uwajibikaji. Naye Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijaji amewahakikishia mawaziri hao wa sekta za kilimo kuwa, wizara yake imejipanga vyema katika utekelezaji wa Mpango wa kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP II).

  “ Wengi wamezoea kuiita wizara yetu kama wizara ya madeni sasa tumejipanga vyema katika utekelezaji wa ASDP II kwani tunaamini kabisa kuwa ili kuwa na uchumi mzuri ulioimarika kwa wananchi na Taifa kwa ujumla tunahitaji kuwa na kilimo madhubuti “ Alikaririwa Dkt Kijaji

  ASDP II inalenga katika mnyororo wa thamani wa mazao ya kipaumbele na ikolojia ya kanda ya kilimo tofauti na utekelezaji wa ASDP awamu ya kwanza ambao ulifanyika nchi nzima na kuwa na miradi karibu sekta ndogo zote za serikali na vipaumbele na maamuzi ya uwekezaji wa Mamlaka za serikali za mitaa.

  Katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wa ASDP II Mazao ya kipaumbele yaliyochaguliwa kwa kilimo ni Mchele, Mahindi, Mtama/Uwele, Muhogo, Mboga/Matunda, Mazao ya Mbegu za mafuta (Alizeti, Ufuta, Nazi, Michikichi n.k) Pamba, Kahawa, Sukari, Korosho, Chai, Viazi mviringo na vitamu, Mikunde, Ndizi, na kwa Mifugo na Uvuvi ni Maziwa, Nyama (Ng’ombe), Mbuzi na Kondoo, Kuku, samaki na Mwani.

  Malengo ya ASDP II ni kuleta mageuzi ya sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ili kuongeza uzalishaji na tija, kufanya kilimo kiwe cha kibiashara zaidi na kuongeza pato la wakulima wadogo kwa ajili ya kuboresha maisha yao, usalama wa chakula na lishe.

  0 0


  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza na waandishi wa habari, kuelezea mipango na mikakati ya Benki hiyo katika mkutano uliofanyika kwenye hoteli ya Serena, Jijini Dar es salaam, Oktoba 10, 2018.
   
  Mkurugenzi Mtendaji Mpya wa Benki ya CRDB Ndugu Abdulmajid Mussa Nsekela amewahakikishia Wateja, Wanahisa  na Wadau wote wa Benki ya CRDB kuwa Benki hiyo ipo kwenye mikono salama na itaendelea kukua pamoja na kuzalisha faida kama ilivyotarajiwa. Bwana Nsekela aliyasema hayo katika Mkutano na Waandishi wa habari wenye lengo la kumtambulisha rasmi uliofanyika katika hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
   
  Akielezea kuhusu vipaumbele vyake, Ndugu Abdulmajid Mussa Nsekela alisema kuwa kwa kushirikiana na viongozi na wafanyakazi wa Benki hiyo, amedhamiria kufanya maboresho makubwa katika utoaji huduma kwa wateja kwa kutilia mkazo katika maeneo matano muhimu, ambayo ni uboreshaji wa mifumo na taratibu za  utoaji huduma, ili ziendane na mahitaji halisi ya wateja na soko, kuongeza weledi na umahiri wa wafanyakazi, kuwekeza kwenye teknolojia ya kisasa, kukuza biashara katika nyanja zote ili kuendana na kasi ya serekali ya awamu ya tano. Atahakikisha Benki inafanya vizuri na kupata faida zaidi ili kutoa gawiwo nono kwa wanahisa.   “Tutakuwa tukiboresha mara kwa mara taratibu za jinsi ya kupata na  kutumia huduma zetu. Tunataka upatikanaji na utumiaji wa huduma za Benki CRDB  uwe rahisi, huku tukiendelea kusizogeza huduma hizo karibu zaidi na wateja wetu” alisema Ndugu Nsekela.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay akitoa hotuba yake kabla ya kumkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Abdulmajid Nsekela, kuzungumza na waandishi wa habari, katika mkutano uliofanyika kwenye hoteli ya Serena, Jijini Dar es salaam, Oktoba 10, 2018.
   
  Akifafanua zaidi juu ya uboreshwaji wa huduma na mikakati ya Benki ya CRDB  katika eneo hilo muhimu, Ndugu Nsekela alisema kwa kipindi kifupi kijacho Benki ya CRDB  itajikita zaidi kwenye uwekezaji wa mifumo ya kidigitali (innovative products and services)  itakayowezesha kuwafikia wateja wengi zaidi, kwa urahisi zaidi, mahali popote walipo na hivyo kuwaondolea wateja wao ulazima wa kutembelea matawi ya Benki ya CRDB pindi wanapohitaji huduma. “Tutatumia fursa ya kuwa zaidi ya watanzania milioni 19.3 wanatumia simu za mikononi  kufanya miamala yao na kuwashawishi kutumia bidhaa zetu za SimBanking na SIMAccount ambazo nazo  hutoa huduma kama hizo” alisema.
   
  Akiongelea kuhusu mikakati ya kusogeza huduma kwa wateja, Ndugu Nsekela alisema Benki ya CRDB imejiwekea malengo ya kufikisha huduma katika wilaya zote nchini ifikapo mwaka 2022. Na wamejiwekea lengo la kuongeza Mawakala wake wa FahariHuduma katika kila kona ya nchi. Ndugu Nsekela alisema pia Benki hiyo pia ina mpango wa kuendelea kupanua wigo wa huduma zake nje ya nchi.
  Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa akizungumza jambo wakati akiongoza mkutano baida ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Abdulmajid Nsekela na waandishi wa habari, uliofanyika kwenye hoteli ya Serena, Jijini Dar es salaam, Oktoba 10, 2018.
   
  Akielezea kuhusu mahusiano baina ya Benki hiyo na Serikali na wadau wengine, Ndugu Nsekela alisema  kuwa  Benki ya CRDB inaitambua Serikali kama Mwanahisha wake na mdau mkubwa wa biashara. “Benki ya CRDB itaendela kuthamini mahusiano mazuri yaliyopo baina yake na Serikali na taasisi zake na tutaendelea  kubuni huduma na bidhaa mbalimbali mahususi kwa ajili ya kufikia mahitaji ya Serikali pamoja na wafanyakazi wake mmoja mmoja.
   
  Tunajivunia kuwa mmoja wa wadau wakubwa wa Serikali ili kwa pamoja tuweze kujenga uchumi wa nchi hususani katika kipindi hiki ambacho tunaelekea katika kujenga uchumi wa kati wa Viwanda,” alisisitiza Ndugu Nsekela.
   
  Ndugu Nsekela alimalizia kwa kusema hali ya uchumi nchini inatoa fursa kubwa ya ukuaji kwa mabenki nchini huku akibainisha kuwa Benki ya CRDB itaendelea kutia mkazo katika kuhudumia wateja  Wakubwa, Wadogo na wa Kati pamoja na Biashara ya kilimo pamoja na kuwawezesha wawekezaji kwenye sekta ya viwanda ili kujenga Tanzania ya viwanda.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Abdulmajid Nsekela wakati wa mkutano na waandishi wa habari, uliofanyika kwenye hoteli ya Serena, Jijini Dar es salaam, Oktoba 10, 2018.
   
  Akizungumza katika Mkutano huo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB Ndugu Ally Laay alisema Bodi hiyo ina amini kuwa Ndugu Nsekela ni mtu sahihi kabisa wa kuongoza Benki ya CRDB na kuahidi kumpa ushirikiano wa kutosha.
  Ndugu Laay pia alitumia nafasi hiyo kumshukuru Dkt. Kimei kwa mchango wake kwa Benki ya CRDB kwa kipindi cha miaka 20 aliyoiongoza. “Ni kazi ngumu sana, lakini Dokta Kimei ameifanya kwa kujitoa na weledi wa hali ya juu sana,” alisema Ndugu Laay.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Abdulmajid Nsekela pamoja na Naibu Wakurugenzi wa Benki hiyo Dorah Ngariga wa Huduma Shirikishi (wa pili kulia) na Kushoto ni Esther Kitoka anayesimamia Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, wakati wa mkutano na waandishi wa habari, uliofanyika kwenye hoteli ya Serena, Jijini Dar es salaam, Oktoba 10, 2018.
   
   
   
   
   
   
   
   
   
   
   
   
   
   

  0 0

  Muanzilishi wa TESEApp Abdul Mombokaleo, akionyesha Tablet ambayo mwanafunzi anaweza kutumia katika kusoma katika mtandao wa TESEA ikiwa tayari imewekwa mtandao maalumu wa masomo ya sekondari (Kidato 1 – 4) na (kidato 5 – 6) akiwa na Mwenyekiti wa Taifa wa wamiliki wa shule na vyuo binafsi nchini (TAMONGSCO) Ndugu Charles Totera katika uzinduzi wa TESEApp.
  Muanzilishi wa TESEApp Abdul Mombokaleo, akionyesha Tablet ambayo mwanafunzi anaweza kutumia katika kusoma katika mtandao wa TESEA ikiwa tayari imewekwa mtandao maalumu wa masomo ya sekondari (Kidato 1 – 4) na (kidato 5 – 6) akiwa na Mwenyekiti wa Taifa wa wamiliki wa shule na vyuo binafsi nchini (TAMONGSCO) Ndugu Charles Totera katika uzinduzi wa TESEApp.

  Muanzilishi wa TESEApp Abdul Mombokaleo wa kulia akisalimiana na Mwenyekiti wa Taifa wa wamiliki wa shule na vyuo binafsi nchini (TAMONGSCO) Ndugu Charles Totera katika uzinduzi wa TESEApp.
  Muanzilishi wa TESEApp Abdul Mombokaleo akizungumza katika uzinduzi wa TESEApp.
  Baadhi ya wadau elimu na Walimu wa shule mbalimbali jijini Dar es Salaam wakifatilia kwa makini uzinduzi wa mtandao wa elimu wa TESEApp.


  Muanzilishi wa mtandao wa Elimu wa Tesea Abdul Mombokaleo amesema kuwa msingi wa kuanzishwa kwa mtandao wa Tesea ni kurahisisha upatikanaji wa marejeo(notes) kwa wanafunzi kujifunza na kupata elimu kwa kutumia teknolojia ya kisasa.

  Amesema mtandao huu utakuwa na marejeo(notes) zote za kutosha na ambayo yame hakikiwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania ili kusaidia wanafunzi kupata marejeo yanayotakiwa katika masomo yao.“mtandao huu hauchukui nafasi ya mwalimu bali utamsaidia mwalimu kuandaa masomo kwa urahisi kwani notes hizo zinafata mtaala wa serikali kwa kuwa na silabasi zote zinazotakiwa kwa mwanafunzi kujifunza awapo shuleni”. amesema Mombokaleo

  Amesema mtandao huo unaopatika kupitia simu za smartphone,laptop,tablet na computer za mezani na unaweza kupakuliwa kiurahisi na mwanafunzi kijisali na kuanza kutumia mtandao kwa gharama nafuu,na kupata masomo yote ya biashara,sayansi na elimu za dini ya kiislamu na kikristo pamoja na mitihani iliyopita (pastpapers).

  Kwa upande Mgeni rasmi katika uzinduzi huo Mwenyekiti wa taifa wa wamiliki wa shule binafsi nchini Charles Totera, amesema kuwa elimu inatakiwa kumsaidia mtu kuweza kutatua matatizo yake bila kusubiri msaada kutoka kwa mtu mwingine kwa uwezo wake wa kufikiri kutokana na elimu aliyonayo.

  Amesema kuwa Wizara ya Elimu iache kuwazawadia watu wano karirishwa katika elimu na badala yake kuwapa motisha watu wanakuja na ubunifu ambao unakuwa msaada kwa wengine kwani anafurahi kuona vijana wanatumia tekinolojia kufanya mambo ambayo ni msaada kwa Taifa.

  “Elimu ya kukaririsha wanafunzi inaua vipaji na kudumaza akili za wale ambao wanachukia kukariri napiga vita elimu ya kukariri haisadii mtu,nchi wala hata msomi mwenyewe”amesema Totera.Amesema kuwa mtandao huo utasaidia wanafunzi hasa wale ambao wanasoma wenyewe bila mwalimu na ambao hawana vifaa vya kujisomea kupitia mtando huo watapata elimu kamilifu na timilifu na kuwaasa walimu kuacha tabia za kukaririsha wanafunzi kwa ajili ya kufaulu mitihani.

  NAMNA YA KUPAKUA NA KUJIUNGA TESEApp
  1.Pakua TESEApp kutoka Google play (kupitia Android Devices)
  au App Store (kwa iOS Devices)
  2. Jiandikishe au jisajili kwa ajili ya kuingia (Sign Up)
  3. Chagua Kifurushi Unachohitaji


  4. Jifunze na Ufurahie

  0 0

   Mkurugenzi wa Tigo  Kanda ya Pwani, Joseph Mutalemwa  {Kulia}akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa {katikati}pamoja na Mratibu wa Tigo Fiesta 2918 , Pancras Mayalla almaarufu Askofu TZA katika Mkutano na waandishi wa habari kueleza maandalizi ya tamasha la Tigo Fiesta 2018 litakalofanyika uwanja wa Nang'wanda Jumapili hii pamoja na ofa mbali mbali za kampuni ya Tigo katika msimu huu ikiwemo mfumo wa  malipo kwa wakulima wa korosho kupitia huduma za Tigo Pesa.
  Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa {Katikati} akiongea na waandishi wa Habari {Hawapo Pichani} kuhusiana na fursa mbalimbali za biashara zinatazopatika katika mkoa huo kutokana na ujio wa tamasha la Tigo Fiesta 2018 - Vibe Kama Lote linalotarajiwa kufanyika siku  ya Jumapili ya wiki katika viwanja vya Nangwanda Sijaona. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Pwani, Joseph Mutalemwa na Mratibu wa Tamasha la Tigo Fiesta, Pancras Mayalla {almaarufu Askofu TZA}.


  Wateja wa Tigo kupata faida mara tatu kupitia promosheni za kusisimua

  Mtwara, Oktoba 13, 2018 – Huku msimu wa mavuno ya korosho ukiwa umewadia katika mikoa ya nyanda za juu kusini, wakaazi wa Mtwara na viunga vyake wanajiandaa kuvuna vibe kama lote kutoka kwa mastaa wa muziki wa bongo flava katika msimu unaoendelea wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote.

  Waandaaji Clouds Media Group, kupitia Katibu Kiongozi wa Kamati ya Maandalizi, Gardner Habash amewaalika wakaazi wa Mtwara waje kupumzika baada ya shughuli ngumu za kuvuna korosho kwa kusikiliza 100% vibe za nyumbani.

  ‘Kwa wafanya biashara, msimu waTigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote ni fursa ya kujiongezea kipato kwa kutoa huduma za usafiri, malazi, vinywaji na chakula na huduma nyingenezo zinazohitajika na maelefu ya mashabiki watakaojitokeza kushuhudia tamasha hili,’ Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Gelasius Byanakwa alisema.

  Kupitia shindano la Tigo Fiesta 2018 – Supa Nyota, wasanii wanaochipuka kutoka Mtwara watapata nafasi ya kuonesha vipaji vyao, na wale watakaofanya vizuri watapewa fursa ya kutumbuiza katika tamasha kuu la Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote linalotarajiwa kurindima siku ya Jumapili tarehe 14 Oktoba katika viwanja vya Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

  ‘Mbali na muziki, wateja wa Tigo pia wanaweza kuvuna hadi mara mbili ya thamani kwa vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia *147*00#. Promosheni ya Data Kama Lote itahakikisha kuwa mashabiki wanaweza kufuatilia habari na matukio yote ya msimu wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote; au kufurahia kuperuzi kwenye mtandao wenye kasi zaidi wa 4G+,’ Mkurugenzi wa Tigo, Kanda ya Pwani Joseph Mutalemwa alisema.

  Wateja wote wa Tigo pia wanaweza kuvuna hadi TSH 10 millioni, zawadi za kila wiki za TSH milioni moja, ama zawadi za kil asiku za TSH 100,000 kwa kushiriki katika shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo. Ushiriki katika shindano hilo unapatikana kwa kutuma neno MUZIKIkwenda 15571 au kwa kutembelea tovuti ya http://tigofiesta.co.tz.

  Watakaoshusha vibe kama lote mjini Mtwara ni pamoja na kundi la Rostam (Roma and Stamina), Fid Q, Zaid na Weusii (Joh Makini, Niki wa Pili na G-Nako) ambao walikonga mioyo ya wapenzi wa muziki mjini Iringa. Wengine ni wasanii a bongo flava Mesen Selekta na Foby, wakongwe Chegge, Barnaba na Mr Blue, pamoja na akina dada Ruby na Lulu Diva.

  TIketi za Tigo Fiesta 2018 – Mtwara zinapatikana kwa bei punguzo ya TSH 5,000 kupitia Tigo Pesa Masterpass QR kwa kupiga *150*01#, kuchagua namba 5 (lipia bidhaa), na kuchagua namba 2 (lipa kwa Masterpass). Tuma kiasi husika cha TSH 5,000 kwenda namba ya Tigo Fiesta 78888888.

  Tamasha la Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote tayari limezuru mikoa ya Morogoro, Sumbawanga na Iringa, na linatarajiwa kutembelea mikoa ya Singida, Songea, Moshi, Tanga, Muleba, Kahama, Mwanza, Musoma, Arusha na Dodoma, huku fainali ikiwa Dar es Salaam.


  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe, akifungua kongamano la siku moja la ajira binafsi  mjini Morogoro , lililoandaliwa na Taasisi ya WICOF inayojishughulisha na masuala ya kijamii hususani, walemavu na  watoto  mkoani humo .
  Washiriki wa kongamano hilo.

  Kongamano likiendelea.  Mtoa mada Mogani Isdori akitoa mada kuhusu ulipaji kodi.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo akipunga mkono wakati akitoa mada kuhusu matumizi ya mitandao.
  Mwanachuo cha Jordan cha mjini Morogoro, Aviva Chrispin akiuliza swali.
  Mjasiriamali, Neema Heri akitoa ushuhuda wa mafanikio yake.
  Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo SUA, Dk.Suleiman Rashid akitoa mada kuhusu umuhimu wa vifungashi kwenye Tangaza na kuongeza thamani ya bidhaa.
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akizungumza katika kongamano hilo akizungumzia umuhimu wa vifungashio na kuongeza thamani ya bidhaa.
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka  akiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi wa kongamano hilo, DC Mchembe pamoja na watoa mada.

  Mjasiriamali, Sara Ngonyani akitoa mada.

  Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Mwajabu Dhahabu, akihutubia.

  Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe, akimkabidhi zawadi ya saa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya WICOF, Mwajabu Dhahabu akimkabidhi zawadi ya picha baba yake Mzee Dhahabu.
  Picha ya pamoja.


   
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo, akiwa katika picha ya pamoja na vijana walioshiriki katika kongamano hilo.

  Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa masuala ya wanawake waliohudhuria kongamano hilo.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo, akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya WICOF, Mwajabu Dhahabu.

  Na Dotto Mwaibale, Morogoro

  WANAWAKE nchini wametakiwa kuthubutu, kuwa wavumilivu na wabunifu ili waweze kuinuka kiuchumi.

  Mwito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe mjini Morogoro juzi wakati akifungua kongamano la siku moja la ajira binafsi lililoandaliwa na Taasisi ya WICOF inayojishughulisha na masuala ya kijamii hususani, walemavu, watoto na wazee   mkoani Morogoro.

  "Ili mjikomboe kiuchumi mnatakiwa kuthubutu, kuwa wavumilivu nawabunifuna uiunga katika vikundi vya ujasiriamali muweze kupata mikopo nakufanyashughuli mbalimbali za biashara" alisema Mchembe.

  Alisema dhana ya  50 kwa 50 kati ya wanaume na wanawake si kuosha vyombo bali ni mwanamke kuweza kufanya kazi za uzalishaji mali kama wanavyofanya wanaume na kumiliki ardhi.

  Akizungumza wakati akitoa mada katika kongamano hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo aliwataka wanawake hao kutumia mitandao ya kijamii kwa maufaa badala ya kuitumia kwa masuala yasiyo na tija.

  "Jamani wanawake wenzangu tutumie simu zetu kwa ajili ya maendeleo, kama kupeana taarifa, kutafuta masoko ya bidhaa zetu na si vinginevyo" alisema Mgongo.

  Akitoa zawadi ya pekee katika kongamano hilo alisema kwa kutambua umuhimu wa mtoto wa kike Shule ya John The Baptist Girls High School imetangaza fursa ya kusomesha bure wanafunzi  watatu wa kidato cha kwanza na watatu wengine hadi cha nne kwa mwaka 2019.

  Alisema anachotakiwa kufanya mwanafunzi ni kufika shuleni hapo siku yoyote ndani ya mwezi wa oktoba 2018 kwa ajili ya kufanya mtihani wa kuchuana na kuwa fursa hiyo imetolewa na Mfuko wa Ndibalema John Mayanja Memorial Scholarship.

  Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Mwajabu Dhahabu alisema kuwa kongamano hilo lenye lengo la kuwajengea uwezo ajira binafsi watoto wa kike ni la kwanza tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo mwaka jana.

  Alisema kufanyika kwa kongamano hilo ni maandalizi ya kuelekea katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani yatakayofanyika hivi karibuni.s

  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka akizungumza katika kongamano hilo alisema serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk.John Magufuli imeweka mazingira mazuri ya kuwasaidia wajasiriamali na kuwa imetenga fedha  kwa ajili ya kuwakopesha hivyo akato mwito kwa wajasiriamali hao kuongeza thamani ya bidhaa zao kwa kuziweka katika vifungashio vilivyobora. 

  Katika hatua nyingine Mtaka aliipongeza kampuni ya Trumark kwa kazi kubwa inayoifanya ya kuwasaidia vijana  kuzitambua fursa za maendeleo na akatoa mualiko kwa wajasiriamali hao kwenda Simiyu kwenye maonyesho ya viwanda vidogo vidogo (SIDO) yatakayofanyika kuanzia Oktoba 23 hadi 28.

  Kongamano hilo lilihitimishwa kwa makundi mbalimbali pamoja na watoa mada kupata zawadi na vyeti vya ushiriki.   0 0


  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Kongamano la Wadau wa Mnyororo wa Ugavi wa Dawa- Tanzania (Tanzania Health Supply Chain Summit 2018) linalofanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. Mwenyekiti wa Kongamano la Wadau wa Mnyororo wa Ugavi wa Dawa- Tanzania (Tanzania Health Supply Chain Summit 2018) Bw. Mavere Tukai akizungumza machache wakati akitoa neno la utangulizi katika Ufunguzi wa Kongamano la Wadau wa Mnyororo wa Ugavi wa Dawa -Tanzania linalofanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam.
  Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI, Dkt. Zainabu Chaula akitoa shukrani zake za pekee kwa waandaaji wa Kongamano la Wadau wa Mnyororo wa Ugavi wa Dawa- Tanzania (Tanzania Health Supply Chain Summit 2018) linalofanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile na Mwenyekiti wa Kongamano la Wadau wa Mnyororo wa Ugavi wa Dawa- Tanzania (Tanzania Health Supply Chain Summit 2018) Bw. Mavere Tukai.


  Washiriki wa Kongamano la Wadau wa Mnyororo wa Ugavi wa Dawa- Tanzania (Tanzania Health Supply Chain Summit 2018)
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (katikati) akizungumza na wanahabari mara baada ya kufungua Kongamano la Wadau wa Mnyororo wa Ugavi wa Dawa- Tanzania (Tanzania Health Supply Chain Summit 2018) linalofanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Bwana Laurean Bwanakunu (kulia) akielezea jinsi mfumo wao wa utoaji wa Dawa. 
   
  Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 
   
  Serikali imepiga marufuku kwa madaktari kuwaandikia wagonjwa dawa kwa majina ya kibiashara badala yake watumie majina ya asili (Generic name). Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile wakati akifungua mkutano wa Kongamano la Wadau wa Mnyororo wa Ugavi wa Dawa- Tanzania (Tanzania Health Supply Chain Summit 2018) linalofanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam. 
   
  Dkt. Ndugulile amesema imefika wakati serikali imebidi kutoa tamko hilo kwasababu Madaktari wengi wamekuwa wakikiuka miongozo wa utoaji matibabu uliotolewa na wizara ya afya. "Katika mfumo wa utoaji wa huduma za afya, tunamtaka daktari aandike kwa jina la asili ili mfamasia akatafsiri aina ile ya dawa tulizonazo kwenye akiba yetu za dawa tulizonazo, ubora wa dawa za Tanzania ni za kiwango cha juu kabisa, tuwaambie wa Tanzania waache zile dhana potofu akisikia zile zinazotoka," amesema. 
   
  Amesema kinachotokea kwasasa katika hospitali nyingi unakuta madawa ni mengi ila hayatumiki wanaishia kwenda kununua nje wakati angeandika kwa jina halisi angepatiwa. Amewataka wafamasia na waganga wafawidhi wa hospitali zote nchini kuhakikisha wanatoa orodha ya dawa zote walizonazo kila mwanzo wa wiki ili kuwawezesha watoa dawa kufahamu dawa walizonazo ili kuondoa adha kwa wananchi kuandikiwa dawa ambazo hazipo.
   
   Nae Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI, Dkt. Zainabu Chaula amesema kuwa ni vyema madaktari wakazingatia maagizo yale yote ambayo yamekuwa wakitolewa na viongozi. Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Bwana Laurean Bwanakunu amesema kuwa wao wamejipanga na wanaakiba ya kutosha ya dawa hivyo ni vyema wahusika kufuata utaratibu ili wanunue na wapelekewe kwa wakati muafaka. 
   
  Kongamano la Wadau wa Mnyororo wa Ugavi wa Dawa- Tanzania (Tanzania Health Supply Chain Summit 2018) linawakutanisha wadau wote wa masuala ya afya kutoka nchi nzima.

  0 0


   

  *Yaelezwa kuna madereva wamekimbia na funguo za mabasi kusikojulikana

  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
   
  BADALA ya raha sasa karaha!Ndivyo unavyoweza kuuzungumzia usafiri wa mabasi ya mwendo kasi katika Jiji la Dar es Salaam ambapo wananchi wa Jiji hilo wamelalamikia unyanyasaji unaofanywa na watoa huduma wa usafiri huo.

  Wakati watumiaji wa usafiri huo wakioneshwa kuchoshwa na usafir inavyoendesha, kwa upande wa uongozi wa DART umedai mradi huo unahujumiwa na baadhi ya watu wasiokuwa na nia njema kwao.

  Hata hivyo kutokana na changamoto za usafiri huo leo asubuhi wananchi wa Kimara waliamua kuonesha hisia zao kwa kufunga barabara huku wakidai wamechoshwa na namna ambavyo huduma hiyo inatolewa.Wameiomba Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam kuingilia kati kumaliza changamoto na adha ya usafiri wanayoipata huku wengine wakesema usafiri huo ni mateso kwao.

  Wameiambia Michuzi Blog kuwa mabasi hayo yamekuwa yakiwapita watu vituoni na hakuna sababu za msingi za kufanya hivyo na matokeo yake kusababisha watu kujazana na hiyo ni hatari kwani inaweza kusababisha maafa.

  WATENDAJI UDART WAJITETEA 

  Kwa upande wa Watendaji wanaosimamia Usafiri wa Mabasi ya Mwendo wa haraka(UDART) kupitia Meneja Mawasiliano wao Deus Bugaiywa amesema kinachotokea kwenye mradi huo 
  wanahisi kuna hujuma zinazonywa kwa lengo la kukwamisha huduma ya usafiri kwa wananchi.

  Amesema kutokana na hali hiyo kwa sasa kuna uchunguzi maalumu unafanywa kwa lengo la kubaini ukweli.Kuhusu kilichotokea leo asubuhi na kusababisha adha kubwa ya usafiri kwa wakazi wa Dar es Salaam na hasa wa Kimara amesema imetokana na kitendo cha madereva wawili kuchukua funguo za mabasi mawili ya mita 18 na kukimbia kusikojulikana."Kawaida mabasi huanza kutolewa saa 10 alfajiri ili kwa ajili ya kuanza kutoa huduma ya kusafirisha wananchi.Lakini leo asubuhi muda huo ulipofika walikuja madereva wawili na kisha kuchukua mabasi mawili na kisha kwenda kuziba njia.

  "Baada ya hapo wakakimbia kusikojulikana na wakati wanachukua funguo hizo walikuwa wamevaa makoti marefu na kufunika sura zao.Hivyo bado wanaendelea kufuatiliwa ili kuwabaini na ndio maana tunahisi kuna hujuma zinaendelea,"amesema Bugaiywa.Ameongeza hata madai ya kuwa wamegoma kwasababu ya kutolipwa mshahara nalo halina ukweli kwani wamekuwa wakilipwa mshahara kama kawaida.

  MAKONDA KUTINGA KITUO CHA KIMARA 

  Wakati huohuo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amewaagiza watendaji wote wanaosimamia Usafiri wa Mabasi ya Mwendo wa haraka (UDART) kukutana nae kesho saa 12:30  asubuhi eneo la kituo cha Mabasi (Kimara Bus Terminal) .Makonda amesema lengo anataka kufahamu kwanini hakuna hatua madhubuti walizochukuwa kumaliza kero za wananchi na  hafurahishwi hata kidogo na namna mradi wa mabasi ya mwendo wa haraka unavyoendeshwa .

  Amesema hata matarajio ya Rais Dk. John Magufuli yalikuwa ni kuona changamoto ya muda mrefu ya usafiri inageuzwa kuwa historia kupitia mradi huo lakini imekuwa tofauti na matarajio hayo."Hatuwezi kuvumilia kuona wananchi wanateseka wakati Serikali yao ipo kwaajili yao, kesho lazima hili liishe ili wananchi wasafiri pasipo usumbufu kama Serikali yao inavyotaka". amesema Makonda

  0 0

  Na: Sylvester Raphael

  Taasisi mpya ya Agri Thamani Foundation iliyoanzishwa kwa lengo kuu la kuboresha lishe Mkoani Kagera na kuongeza ushirikishwaji wa wanawake na vijana katika kuongeza Mnyororo wa thamani kwenye Sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi imetiliana saini na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera katika Mkataba wa Makubaliano ili kuanza utekelezaji wa shughuli zake ifikapo Novemba Mosi, 2018.

  Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Taasisi ya Agri Thamani Foundation ambaye ni mzawa wa Mkoa wa Kagera Bi Neema Lugangira mara baada ya kutiliana saini kwenye Mkataba wa Makubaliano na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Bw. Nesphory Bwana alisema kuwa aliamua kuanzisha Taasisi hiyo kutokana na Mkoa wa Kagera kuwa na kiwango kikubwa cha watoto wenye udumavu na utapiamlo kutokana na kutopata lishe bora na stahiki.

  “Nimeamua nianzishe Taasisi ambayo itausaidia Mkoa wetu wa Kagera hasa kuondoa udumavu kwa watoto kwani ukiangalia haraka utaona kuwa Mkoa wa Kagera kila zao linakubali kustawi lakini watoto hawapati lishe bora jambo ambalo linapelekea kudumaa kwao na mtoto akiwa na udamavu hawezi kuwa na kiwango kizuri cha akili hata kukua kwake kunaathirika.” Alieleza Bi Neema.

  Bi Neema alieleza kuwa ili kufanikisha suala la kuondoa udumavu Kagera kwanza ni kuongeza ushiriki wa Wanawake na Vijana katika kuongeza Mnyororo wa Thamani katika Sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi ambapo alitolea mfano katika kwenye kilimo kuwa Kagera kuna Mazao mengi lakini huenda akina mama hawajui namna bora ya kuongeza mnyororo wa thamani kwenye mazao hayo lakini pia hawajui maana ya kufanya kilimo baishara ili kuingiza kipato na kuongeza ajira kwa vijana.

  “Tutajikita katika Kilimo Biashara kwa kuongeza ushiriki wa wanawake na vijana katika kuhakikisha wanaongeza thamani ya mazao mfano mama anayelima viazi lishe afundishwe namna ya kukausha viazi hivyo na kuchanganya na mazao mengine na kutengeneza unga bora wa lishe, kwanza mama huyo watoto wake hawawezi kupata udumavu, pili atakuwa amejua namna bora ya kutunza unga wa viazi lishe badala ya kutunza viazi vyenyewe ambavyo mwisho wa siku vinaharibika.” Alifafanua Bi Neema

  Bi Neema anasema kuwa Mkoa wa Kagera umebarikiwa kila zao kukubalika na wananchi wa Kagera wanalima mazao yote, masoko ya mazao hayo yapo lakini tatizo mazao hayo hayalimwi katika mfumo wa kuyaongezea Mnyororo wa Thamani yanapelekwa sokoni hivyo hivyo jambo ambalo linapelekea Mkulima kunyonywa lakini wakulima hanufaiki na mazao hayo kwani watoto wao utawakuta na udumavu kutokana na kutopata lishe bora.

  Aidha, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Bw. Nesphory Bwana alimshukuru Bi Neema kuwa na wazo na akaamua kulifanyia kazi wazo hilo ili lifanye kazi katika Mkoa wa Kagera ambako yeye ni mzaliwa. “Ungeweza kuanzisha Taasisi kama hii lakini ukaipeleka mikoa mingine lakini wewe uliona uusadie Mkoa wako, kwaniaba ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera nakushukuru sana.” Alitoa Shukrani Bw. Nesphory.

  Pia Bw. Nesphory alimhakikishia Bi Neema kuwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera ipo tayari kushirikiana naye ili kupunguza kiwanngo cha udumavu katika Mkoa wa Kagera. Vile vile Bw. Nesphory alimuomba Bi Neema kushirikiana na Mkoa katika kuelimisha wananchi wa Mkoa wa Kagera kuhusu Sera ya Ushiriki wa Watanzania (Local Content) katika miradi mbalimbali inayoyekelezwa au inayotarajiwa kutekelezwa mfano Mradi wa Bomba la mafuta, na Mradi wa Mapori ya Biharamulo Burigi na Kimisi (BBK) kuwa Hifadhi za Taifa.

  Hapo awali Mkoa wa Kagera ulishaanza kuchukua hatua za kupambana na utapiamlo na udumavu wa wtoto ambapo aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu mwezi Machi 2018 alizindua Kampeni ya kila kaya kuwa na angalau miche mitano ya matunda kuzunguka nyumba ili watoto wapate matunda aina mbalimbali kwaajili ya lishe bora na kuhamasisha ulaji matunda hayo.

  Aidha, Mkuu wa Mkoa huyo Mstaafu Mhe. Kijuu aliziagiza Taasisi zote za Serikali na zisizokuwa za Serikali kuhakikisha zipanda miche ya matunda katika maenneo ya Taasisi hizo. Pia alitoa wito kwa baadhi ya Taasisi hizo kugharamia uanzishwaji wa vitalu vya miche ya matunda ili kuigawa miche hiyo kwa wananchi ambao hawana uwezo wa kuinunua ili wapewe bure kuipanda katika kaya zao.

  Kitakwimu Katika Mkoa wa Kagera Asilimia 39.1% ya wanawake kati miaka 15 hadi 49 wana upungufu wa damu, Asilimia 57.2% ya watoto chini ya miaka mitano wana upungufu wadamu, na Asilimia 41.7% ya watoto chini ya miaka mitano wana udumavu. Aidha, Kitaifa Mkoa wa Kagera unashika nafasi ya nne katika mikoa kumi ya mwanzo inayoongoza kwenye udumavu wa watoto wenye umri chini ya miaka mitano Rukwa ikiongoza na asilimia 56.3% na Mkoa wa Dar es Salaam ukiwa kwa asilimia 14.6% (Kwa Mujibu wa “Tanzania Demographic and Health Survey” 2015/2016)

  Bi Neema Lugangira anasema kuwa fursa za kuboresha lishe zipo katika Mashirika mengi ya Kimataifa lakini mpaka atokee mtu au Taasisi itakayokuwa na malengo thabiti ya kutekeleza miradi kama hiyo na ikaleta matokeo chanya kwenye eneo husika kama yeye na Taasisi yake anavyolenga kufanya.

  Taasisi mpya ya Agri Thamani Foundation ilianzishwa Mwezi Julai 2018 na Bi Neema Lugangira ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Mlezi wake ni Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Kayanza Peter Pinda. Aidha, Taasisi hiyo inatarajia kuanza kutekeleza majukumu yake rasmi mwezi Novemba 2018 baada ya kutiliana saini katika Mkataba wa Makubaliano na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Oktoba 10, 2018 na ofisi za Taasisi hiyo zitakuwa Makao Makuu ya Mkoa wa Kagera.
   Bi Mwasham Msabaha Mkurugenzi Mtendaji  wa Taasisi ya Agri Thamani Foundation akisaini Mkataba wa Makubaliano
   Bi Neema Lugangira Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Taasisi ya Agri Thamani Foundation Akimsikiliza Kaimu Katibu Tawala Bw. Nesphory Ofisini Kwake
   Bi Neema Rugangira Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Taasisi ya Agri Thamani Foundation akisaini Mkataba wa Makubaliano
   Bi Neema Rugangira Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Taasisi ya Agri Thamani Foundation na Kaimu  Katibu Tawala Mkoa Bw. Nesphory Bwana  Wakisaini Mkataba wa Makubaliano.
   Bi Neema Rugangira Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Taasisi ya Agri Thamani Foundation na Kaimu  Katibu Tawala Mkoa Bw. Nesphory Bwana Wakipeana Mikono Baada ya Kusaini Mkataba

   Kabla ya Kusaini Mkataba wa Makubaliano.
   Kaimu  Katibu Tawala Mkoa Bw. Nesphory Bwana  akisaini Mkataba wa Makubaliano Pamoja Bw. Isaya Tendega Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Uchumi na Uzalishaji.
   Kaimu  Katibu Tawala Mkoa Bw. Nesphory Bwana  akisaini Mkataba wa Makubaliano.
  Picha ya Pamoja

  0 0

  Muandaaji wa Muziki nchini Tanzania, Producer Pancho Latino almaarufu Mafia ambae alifanya kazi kwenye studio mbalimbali  aliyefariki jana kwa  kuzama kwenye maji kwenye kisiwa cha Mbudya Dar es Salaam anatarajia kuzikwa Wilayani Gairo, Morogoro. Kwa mujibu wa taarifa iliyoandikwa na Msanii Fid Q katika ukurasa wake wa Twitter imesema kuwa Marehemu  Pancho Latino itahitimishwa siku ya Jumamosi nyumbani kwao. Ibada itaanza saa 4 asubuhi, na baadae wataaga mwili wa marehemu na maziko yatafanyika saa nane mchana. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Lugalo kwa uchunguzi zaidi.

  0 0

  Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

  MTENDAJI Mkuu wa Wakala wa Usafiri wa Mabasi yaendayo kasi jijini Dar es Salaam(DART) Mhandisi Ronald Lwakatare amepewa onyo kwa kile kinachoelezwa kushindwa kutekeleza majukumu yake.

  Onyo hilo limetolewa leo na Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Suleiman Jafo ambapo pia amemtaka Mhandisi Lwakatare kujieleza kwanini ameshidwa kumsimamia mtoa huduma Udart.

  Waziri Jafo mbali ya kutoa onyo hilo ametoa maagizo kwa Naibu Waziri wake Joseph Kakunda kufanya kikao ambacho kitamjumuisha Mtendaji mkuu wa Dart pamoja na mtoa huduma Udart ili kubaini changamoto zilizopo ambazo zinasababisha usafiri huo kuonekana kero kwa wananchi.

  Amefafanua usafiri wa mabasi ya mwendo kasi ni usafiri uliokuwa wa nema kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam ambao wengi wao walikuwa wanatumia zaidi ya saa tatu kutoka Posta hadi Kimara.

  "Leo hii kupitia usafiri huu wanatumia takribani dakika 40 hadi 45, hivyo hatuwezi kuacha huduma ziendele kudorola kwa kiasi hichi.Lazima ufumbuzi upatikane ili wananchi wafurahie huduma za usafiri huo,"amesisitiza Jafo.

  Wakati huo huo Waziri Jafo amemtaka Katibu Mkuu wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Mhandisi Mussa Iyombe kufanya uchunguzi katika ofisi ya Dart ili kuona kama wapo watendaji ambao wanakwamisha huduma hiyo.

  0 0


  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam , Paul Makonda akizungumza na Wakazi wa Kimara mara baada ya kutembelea kituo cha Mabasi ya Mwendokasi na kujionea kero na changamoto za mradi huo na kuahidi kwenda kuzungumza na Waziri wa Tamisemi, Suleimani Jaffo ili kulitafutia ufumbuzi wa haraka.
    Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam , Paul Makonda  akitembelea eneo la kituo na kujionea Changamoto zilizopo
    Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam , Paul Makonda , akifungua geti lililofungwa  eneo la Kimara Mwisho Wananchi wasipite na kuamuru litumike kuanzia leo ili kiupunguza kero kwa Wananchi
   Wananchi waliokuwa wamefurika eneo la Kimara kusubiri Mabasi ya Mwendokasi asubuhi ya leo.
   Abiria wakiwa wamebanana  ndani ya basi la Mwendokasi  kutokana na uchache wa mabasi
   Wakazi wa Mbezi na Kimara wakiwa wamejazana kumsikiliza mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam eneo la Kimara Mwisho


older | 1 | .... | 1693 | 1694 | (Page 1695) | 1696 | 1697 | .... | 1897 | newer