Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel Catalog



Channel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1692 | 1693 | (Page 1694) | 1695 | 1696 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Maneno haya yamesemwa na Mama Maria Nyerere, Mke wa Hayati Mwalimu Julius K. Nyerere mwasisi wa Taifa letu alipotembelewa na Viongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) TAIFA jana Oktoba 08/2018. 
  Viongozi hao kutoka Makao Makuu ya UVCCM ni Wakuu wa Idara Ndugu Hassan Bomboko (Uhamasishaji na Chipukizi), Peter Kasera (Organaizesheni, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa), Khamana Juma Simba (Vyuo na Vyuo Vikuu)
  Mama Maria Nyerere ameipongeza kazi kubwa inayofanywa na Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli na amewaomba Viongozi wote nchini, Vijana na wananchi kumuunga mkono na kufanya juhudi kwenye maeneo yao ili kusaidia kuijenga Tanzania Mpya.

  0 0

  Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akipokelewa na Watendaji wa Mkoa wa Manyara wakati alipowasili mkoani hapo kwa ajili ya kupata taarifa ya Elimu ya Mkoa huo. Naibu waziri huyo yuko Mkoani Manyara kwa ziara ya siku tatu ikiwa ni muendelezo wa ziara zake ambazo amekuwa akizifanya kukagua miradi ya Elimu inayotekelezwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na kuangalia hali ya Elimu katika mkoa husika.
  Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akitoa maelekezo kwa Viongozi na watendaji wa VETA Manyara wakati wa kukagua karakana inayotumika na wanafunzi wanaosoma kozi ya ufundi wa zana za kilimo (Agro Mechanics).

  Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akikagua maendeleo ya ujenzi wa karakana itakayotumiwa na wanafunzi wanaosoma kozi ya ufundi uwashi katika Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA Manyara.


  Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mheshimiwa William Ole Nasha amewataka viongozi kuanzia ngazi ya mkoa hadi vijiji nchini kote kuhakikisha wanafunzi wanaomaliza darasa la saba hawaondoki katika maeneo yao kwenda kufanya kazi za ndani wakati wakisubiri matokeo ya kuhitimu darasa la saba, kwani kufanya hivyo kunawaondolea fursa ya kuendelea na masomo pindi wanapofaulu.

  Ole Nasha ametoa agizo hilo mkoani Manyara wakati akizungumza na viongozi hao kuhusu hali ya Elimu mkoani humo ambapo amewataka kusimamia kwa ukaribu suala hilo ili kutokatisha ndoto za watoto hao na kwamba wale wanaofanya hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

  “Hakikisheni watoto wanaposubiri matokeo hawasafirishwi kwani wanapofika huko wanarubuniwa na waajiri hivyo hata matokeo yakitoka na kuonesha kuwa wamefaulu hawarejei kuendelea na masomo “alisisitiza Naibu waziri Ole Nasha.

  Kiongozi huyo ameendelea kuwasisitiza wazazi kuwa fursa za Elimu katika nchi yetu ni kubwa, ikizingatiwa kuwa Elimu msingi ni bure hivyo hakuna kisingizio tena kuwa mtoto hawezi kusoma.

  “wazazi msiwe sehemu ya kuchangia watoto wenu kwenda mjini kwa kuwa tu wanawatumia fedha kwa ajili ya matumizi bali hakikisheni mnawasimamia vyema watoto hao katika kipindi chote cha kusubiri matokeo na kuwapeleka shule pindi matokeo yanapotoka na kuonekana wamefaulu,” alisisitiza Naibu waziri Ole Nasha.Amewataka viongozi hao kutumia sheria kuhakikisha watoto wote wenye umri wa kuanza shule wanaandikishwa ili kutokuwa na wimbi kubwa la watoto wa mitaani wasiokwenda shule.

  Awali Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Arnold Msuya alimweleza Naibu waziri huyo kuwa mkoa kwa sasa una mwamko mdogo wa Elimu hasa katika jamii ya wafugaji hali inayopelekea wazazi kutowaandikisha shule watoto wenye umri wa kuanza shule

  Naibu waziri Ole Nasha pia ametembelea Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi stadi cha Mkoa Manyara na kuwataka kuboresha Mitaala yao ili mafunzo wanayoyatoa yaendane na wakati ikiwa ni pamoja na kukidhi mahitaji ya soko la ajira ili kuongeza fursa ya vijana kujiajiri pindi wanapomaliza masomo yao.

  Naibu Waziri huyo yuko mkoani Manyara kwa ziara ya kikazi kukagua miradi ya Elimu inayotekelezwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na kuangalia hali ya Elimu mkoani humo.

  0 0

  Mwanza, 9 Oktoba 2018: Washindi wa michuano ya Rock City Marathon 2018  wanatarajiwa kuondoka na zawadi zenye thamani ya zaidi ya sh milioni 30 pamoja na medali, imefahamika. Mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
  Akizungumza jijini Mwanza leo, Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mbio hizo zinazoratibiwa na kampuni ya Capital Plus International (CPI), Bw. Zenno Ngowi alisema pamoja na medali washindi wa kwanza wa mbio za kilomita 42 kwa wanaume na wanawake watajinyakulia sh. Mil 4 kila mmoja, sh.mil 2/- kwa washindi wa pili na sh. Mil 1/- kwa washindi wa tatu, huku washindi wanne hadi kumi nao pia wakiibuka na medali na pesa taslimu.
  Kwa upande wa mbio za  Kilomita 21, Ngowi alisema, pamoja na medali washindi wa kwanza kwa wanaume na wanawake watajinyakulia sh.  Mil 3/- kila mmoja, sh. Mil 1/-  kwa washindi wa pili na sh. 750,000/- kwa washindi wa tatu huku washindi wanne hadi wa kumi wakiibuka na  zawadi za pesa taslimu na medali kila mmoja.
   “Mbio za kilomita tano tunatarajia kwamba zitaongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza sambamba na baadhi ya wakuu wa mikoa kanda ya Ziwa ambao pia watajumuika na baadhi ya viongozi waandamizi wa mikoa hiyo wakiwemo wabunge, viongozi na wafanyakazi wa mashirika na makampuni mbalimbali yaani corporates pamoja na ndugu zetu wenye ualbino,’’alisema.
  Wadhamini watakaoshiriki katika mbio hizo ni pamoja na kampuni za Puma Energy Tanzania, Tiper, TANAPA, TTB, Nssf, Gold Crest, New Mwanza Hotel,  Cf Hospital, CocaCola, Metro Fm, Ef Outdoor,  Kk Security, Belmont Fairmount Hotel , Bigie Customs na Global Education Link.
  Alibainisha kuwa mbio za Km 5 zitahusisha watu wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino ambapo washindi kwa upande wa mashirika watapatiwa zawadi za utambuzi ikiwemo medali na vyeti vya ushiriki huku pesa zikielekezwa kwa washiriki wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino.
  Alisema washindi wa mbio za Kilomita tatu ambazo zipo mahususi kwa ajili ya wazee watapatiwa sh 250,000/- kwa washindi wa kwanza huku washindi wa pili wakipata sh 200,000/ na watatu  wakipatiwa sh 100,000/-pesa taslimu.
   “Kwa washindi wa mbio za kilomita mbili na nusu zitakazohusisha watoto wenye umri kati ya miaka 7 hadi 10 watapatiwa sh 50,000/-kila mmoja huku wa pili na watatu pia wakipatiwa pesa taslimu.’’ Aliongeza
  Bw Ngowi alivitaja vituo vinavyoendelea na usajili huo kwasasa kuwa ni pamoja na Igoma, Buzuruga, Airport Mwanza, Rock city mall, Chuo Kikuu cha Saut, Nyegezi Stand, Mwanza hotel, Nyamagana Stadium, Dampo pamoja na Nyakato.
  Alisema usajili huo pia utahusisha ofisi zote za riadha mikoa ya Geita, Simiyu na Shinyanga huku akiongeza : “Kwa upande wa Dar es Salaam Fomu za ushiriki pia zinapatikana katika jengo la SHAMO Tower, Mbezi Beach , jijini Dar es, Salaam ”



  0 0

  Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara, Mwanaisha Ali Saidi (wapili kulia), akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa shindano hilo, nchini.
  Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang'ombe, akimkabidhi zawadi  mshindi wa tatu wa uandishi wa barua, Anna Malagi, kutoka Shule ya Umoja Primary and Nursery ya Mbeya katika hafla hiyo. Anayeshudia katikati ni Meneja Rasilimali za Shirika Macrice Mbodo. 
  Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang'ombe, akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili wa uandishi wa barua, Hajra Mustafa Kaniki, kutoka Shule ya Sekondari ya St. Mary's Mazinde Juu ya Lushoto, mkoani Tanga. Kushoto ni Meneja Rasilimali za Shirika Macrice Mbodo na wapili kushoto ni mwalimu wa shule hiyo, Josephine Mashare.  
  Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang'ombe (wapili kulia), akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa uandishi wa barua, Dorine John Massawe, kutoka Shule ya Sekondari ya Joyland Girls ya Same, mkoani Kilimanjaro. Kushoto ni mwalimu wa shule hiyo, John Lwanga na kulia ni Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara wa TPC, Mwanaisha Ali Saidi.
  Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang'ombe, akiwa katika picha ya pamoja na washindi watatu walioshinda shindano la uandishi wa barua, Anna Malagi (wapili kushoto), Hajra Mustafa Kaniki (wa tatu) na Dorine John Massawe. Kushoto ni Meneja Rasilimali za Shirika, Macrice Mbodo na kulia ni Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara, Mwanaisha Ali Saidi.  
  Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang'ombe (wapili kulia) na baadhi ya viongozi waandamizi wa shirika hilo, wakiwa katika picha ya pamoja na walimu, waliofuatana na  wanafunzi walioshinda shindano hilo. Kutoa kushoto ni Mwalimu John Mistry (wapili) kutoka Shule ya Umoja Primary and Nursery, Mwalimu John Lwanga (wa tatu) kutoka Shule ya Sekondari ya Joyland Girls ya Same, mkoani Kilimanjaro na Mwalimu Josephine Mashare (wa nne), kutoka Shule ya Sekondari ya St. Mary's Mazinde Juu ya Lushoto, mkoani Tanga.
  Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang'ombe akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani, jijini Dar es Salaam leo, ambapo washindi wa shindano la kimataifa la uandishi wa barua walizawadiwa zawadi mbalimbali pamoja na vyeti. Kushoto ni Meneja Rasilimali za Shirika Macrice Mbodo.

  Baadhi ya viongozi waandamizi wa Shirika la Posta wakiwa katika hafla hiyo. 
  Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari, wakifuatilia hafla hiyo. 
  Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika wakifuatilia hafla hiyo. 
  Mshindi wa kwanza wa uandishi wa barua, Dorine John Massawe, akiisoma barua yake iliyompatia ushindi wakati wa hafla hiyo. 
  Meneja Rasilimali za Shirika, Macrice Mbodo, akizungumza wakati akifafanua kuhusu masuala ya uandishi wa barua mbalimbali ambazo hadi sasa zinaendelea kuhudumiwa na shirika hilo. 
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Shirika la Posta, Elia Madulesi, akitoa matokeo ya washindi wa shindano la Kimataifa la uandishi wa barua, katika hafla hiyo. 

  0 0


   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia (WB) nchini Bella Bird aliyekutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2018.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo  na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia (WB) nchini Bella Bird na ujumbe wake walipokutana na kufanya nao mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2018.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na  Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia (WB) nchini Bella Bird na ujumbe wake walipokutana na kuzungumza Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2018.

  Picha na IKULU

  0 0


  Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike akisalimiana na Kamishna wa Utawala Gaston Sanga pamoja na viongozi waandamizi wa Jeshi la Magereza alipowasili katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwamvita Mkoani Mororgoro tarehe 9 Oktoba 2018.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Jacob Gideon Kingu akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike alipowasili katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwamvita Mkoani Mororgoro.
  Mdhibiti Mkuu wa Shirika la Magereza,Naibu Kamishna Afwilile Mwakijungu akitoa maelezo mafupi kuhusu Shirirka kabla ya mgeni rasmi kukaribishwa kufungua kikao.

  Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike akitoa maelezo mafupi kabla ya kukmkaribisha Katibu Mkuu wa Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Jacob Gideon Kingu kufungua kikao.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Gideon Kingu akisisitiza jambo kwa Wakuu wa Mikoa ya Kimagereza, Wakuu wa Magereza na Wakuu wa Miradi mbalimbali ambayo iko chini ya Shirika la Magereza, kabla ya ufunguzi rasmi wa Kikao.
  Wakuu wa Magereza wa Mikoa, Wakuu wa Magereza na Wakuu wa Miradi mbalimbali ambayo iko chini ya Shirika la Magereza wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Gideon Kingu.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Gideon Kingu (katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa juu wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara. Kulia kwa katibu mkuu ni Kamishna Jenerali Kasike, Kamishna wa Sheria na Utawala wa Magereza Uwesu Ngarama na Kamishna wa Miundo Mbinu na Uzalishaji Tusekile Mwaisabila. Kushoto kwa Katibu Mkuu ni Kamishna wa Utawa na Rasilimali watu Gaston Sanga, Kamishna wa Fedha na Mipango Gideon Nkana na Kamishna wa Huduma za Parol,Viwanda,Huduma za Jamii na Program za Urekebishaji Augustine Mboje.Waliosimama ni Manaibu Kamishna.
  Wakuu wa Magereza na Wakuu wa Miradi mbalimbali ambayo iko chini ya Shirika la Magereza wakiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi pamoja na viongozi wakuu wa Jeshi la Magereza nchini.Picha zote na Jeshi la Magereza Kitengo cha Habari

  0 0



  index
  Wakiongea kwa nyakati tofauti Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mh Martin Shigela na Naibu Waziri Mavunde wamewataka Vijana kuziunga mkono serikali za Muungano na SMZ kwa kazi kubwa inayofanywa ya kuwawekea Vijana mazingira wezeshi ya kisiasa,kiuchumi na kijamii.
  3
  Waziri wa Vijana,Utamaduni,Sanaa na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar(SMZ) Balozi Ali Abeid Aman Karume amewataka Vijana wa Tanzania kuwa mstari wa mbele katika kutetea na kulinda maslahi ya Taifa Tanzania ili kulifanya Taifa Tanzania liweze kustawi.
  2
  Balozi Karume kayasema hayo leo Jijini Tanga wakati wa Ufunguzi wa mdahalo wa Vijana katika kuelekea katika kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru ambapo amewasisitiza Vijana kuwa wazalendo na kudumisha Amani,mshikamano na Umoja kama ambavyo tuliaswa na waasisi wa Taifa Tanzania Hayati Baba Wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere na Hayati Abeid Aman Karume.


  0 0


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu usindikaji wa kahawa yenye viwango vya juu kutoka kwa Mkurugenzi wa Kiwanda cha kahawa cha AMIMZA kilichopo Bukoba, Bw. Amiri Hamza (wapili kushoto) wakati alipotembelea kiwanda hicho, Oktoba 9, 2018. Watatu kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage na wapili kulia ni Naibu Waziri wa Kilimo, Dkt. Mary Mwanjelwa. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea kiwanda cha kisasa cha kusindika kahawa cha AMIMZA cha mjini Bukoba Oktoba 9, 2018. Wapili kushoto ni Mkurugenzi wa kiwanda, Amiri Hamza na kushoto ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage. Wapili kulia ni Naibu Waziri wa Kilimo, Dkt. Mary Mwanjelwa . Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  Wachimbaji wa visima wameaswa kufuata sharia ,kanuni pamoja na taratibu ziliziowekwa na bodi ya Bonde la Wami/Ruvu ili kulinda vyanzo vya maji katika kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama.

  Hayo ameyasema Katibu Tawala Msaidizi wa Huduma za maji Mkoa wa Dar es Salaam , Elizabeth Kingu wakati akizungumza na wadau wa uchimbaji wa Visima uliondaliwa na Bodi ya Bonde la Wami/ Ruvu uuliofanyika jijini Dar es Salaam.

  Kingu amesema kuwa sharia zilizowekwa lazima zifuatwe kwa wachimbaji kuhakikisha wanakuwa na vibali kutoka katika bonde ambao ndio wasimamizi wa vyanzo vya maji.

  Amesema kuwa vyanzo vya maji vinahitaji kudhibitiwa kw kuhakikisha kila mtu anafuata sheria ya kufanya kazi ikiwa ni lengo moja ya kutoa huduma kwa wananchi.

  Nae Afisa wa Maji wa Bonde la Wami/ Ruvu Mhandisi Simon Ngonyani amesema kuwa kumekuwa na uchimabji holela wa visima huku wengine wakiwa hawana hata leseni kutoka bonde. Amesema kuwa baada ya kikao hicho watafanya operesheni ya kuangalia visima hivyo kwa wenye visima na vibali ya uhalali pamoja Ankara zao kama wanalipa.
  Katibu Tawala Msaidizi wa Huduma za maji Mkoa wa Dar es Salaam Elizabeth Kingu akizungumza wakati akifungua mkutano wa wachimbaji visima ulioondaliwa na Bonde la Wami/Ruvu uliofanyika jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali za Maji, Utafiti na Tathimini wa Wizara ya Maji, Hosea Sanga akizungumza kuhusiana wizara ya maji ilivyotoa mamlaka ya katika bonde katika usimamizi wa vyanzo vya maji.
  Afisa wa Maji wa Bonde la Wami/Ruvu akitoa mada kwa wachimabji wa visima kuhusiana na sheria za uchimbaji visima hivyo pamoja na mamlaka ya Bonde katika utoaji wa vibali vya uchimbaji  katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.
   Baadhi ya wadau wa uchimbaji visima wakiwa katika mkutano huo leo jijini Dar es Salaam.

  0 0


  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly kulia akielezea mipango ya mamlaka hiyo wakati wa ziara ya ugeni kutoka KFW ya nchini Ujerumani kutembelea mradi wa maboresho ya huduma ya maji safi Jijini Tanga
  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly  katikati akionyesha kitu ugeni kutoka KFW ya nchini Ujerumani  wakati wa ziara yao ya kutembelea mradi wa maboresho ya huduma ya maji safi Jijini Tanga.kulia ni Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi
  Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi akizungumza wakati wa ziara hiyo kushoto ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly
  Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi kulia akifirahia jambo na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maji Mijini kutoka Wizara ya Maji -Dodoma Mhandisi Lydia Joseph kushoto wakati wa ziara hiyo

  Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi  akilakiwa na watumishi wa mamlaka hiyo mara baada ya kuwasili eneo la Mowe
  Wageni hao wakishuka kwenye eneo la kusafishia maji Mowe Jijini Tanga  wakati wa ziara hiyo
  Wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumaliza ziara hiyo

  MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) imenufaika na ruzuku ya zaidi ya Shilingi bilioni 1.2 baada ya kutimiza masharti ya mkopo wa zaidi ya shilingi Bilioni 3 toka katika benki ya CRDB ya utekelezaji wa huduma ya Maji safi Jijini Tanga.

  Ruzuku hiyo hutolewa na Benki ya watu wa Ujerumani (KFW) kutokana na Mamlaka husika kutimiza vema masharti ya mkopo huo ikiwa pamoja na zoezi zima la marejesho huku likizingatiwa suala la utekelzaji wa mradi uliopewa fedha hizo.

  Hayo yalibainishwa  na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly wakati wa ziara ya ugeni kutoka KFW ya nchini Ujerumani kutembelea mradi wa maboresho ya huduma ya maji safi Jijini Tanga.

  Alisema mkopo huo umewasaidia kuongeza uwezo wa usambazaji wa maji hasa katika maeneo yaliyokuwa na mgawo wa maji bila sababu yaliyochangiwa na udogo wa vipenyo vya mabomba yaliyokuwa yanapeleka maji kwenye maeneo hayo.

  “Kama nilivyoonyesha kwamba tumeongeza bomba kubwa la nchi 8 kwa ajili ya kuongeza mgawanyo wa maji kwenye eneo la Neema na kwengineko na kuwepo kwa usambazaji mkubwa kwenye maeneo hayo lakini pia tumejenga mtandao wa km 60 kwa kutumia mkopo huo na ruzuku tuliyopewa”Alisema

  Aidha alisema hivi sasa wamejipanga kuendelea kudumisha ubora wa huduma zao ili kuhakikisha wananchi wanaowahudumia wanaendelea kupata huduma bora ya maji katika maeneo yao.

  Alisema mbali ya ubora wa huduma hizo za maji lengo kuu ni kuhakikisha wanapokuwa wageni wahisani waweza kupata mrejesho na taswira nzuri kwa mamlaka ili waendelee kupata moyo wa kuwasaidia.

  Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maji Mijini kutoka Wizara ya Maji -Dodoma Mhandisi Lydia Joseph alisema fedha hizo zinalenga katika miradi inayojenga inalengo la kutoa uzoefu kwa mamlaka za maji zinazoingizwa kwenye mfumo huo ili
  ziweze kupata uzoefu wa kuwekeza badala ya kuishia kutoa huduma pekee.

  Alisema mamlaka nyingi zimekuwa na lengo la kutoa huduma ya maji kwa wananchi kwa miundombinu iliyojengwa na serikali tangu zamani hivyo kutokana na ongezeko la watu na mahitaji yao Mamlaka zinatakiwa kupanua huduma zao.

  Mhandisi Lydia alisema mbali na huduma pia mamlaka hizo za maji zinatakiwa kuboresha miundombinu ambayo inahitaji uwezeshwaji kutokana na serikali kuwa na mambo mengi ya kufanya hivyo wakati mwengine huelemewa na uwekezaji jambo ambalo limepelekea kushindwa kuendana na kasi ongezeko la watu.

  “Kwa maana hiyo Mamlaka zetu kama zitapata mikopo na zikijenga uaminifu zinaweza kupata miradi kama hiyo na zaidi ya hiyo huku zikijijengea morali kwa mamlaka zenyewe hasa kwenye uwekezaji na Serikali ikatoa sapoti ”Alisema Mhandisi Joseph.

  0 0

  Serikali imejipanga kuhakikisha miradi ya maji hapa nchini inatekelezwa kwa kasi kubwa kwa majiji unafikia asilimia 95 ambapo miji ya wilaya asilimia 90 na vijijini kwa asilimia 85 ifikapo mwaka 2020 ambapo kwa jiji la Arusha inatekeleza mradi mkubwa wa maji utakaozalisha lita million 200 kwa siku kwa gharama ya billion 520.

  Aidha Serikali imepanga kutekeleza Mradi mkubwa wa maji hapa nchini utakogharimu kiasi cha Trilion 1.1 sawa na dola za kimarekani million 500 kwa watanzania wamesubiria maji hivyo watakaopata nafasi ya kusimamia mradi huu kuutekeza kwa ufanisi na kwa wakati.

  Akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea visima vya maji katika kijiji cha Levolosi kata ya Kimnyaki wilaya ya Arusha dc na kutiliana saini Waziri wa maji na umwagiliaji Prof.Makame Mbarawa amesema kuwa serikali itaendelea kuhakikisha miradi hiyo inaondoa adhaa ya maji kwa watanzania

  Amesema kuwa jiji la Arusha kwa sasa linazalisha maji lita million 45 kwa siku wakati mahitaji yanayotosheleza kwa siku ni lita million 94 ndio maana serikali ikaliona hilo na ikaandaa mradi mkubwa uakapo kamilika utazalisha lita million 200 kwa siku ambao utaondoa tatizo la maji kwa jiji la Arusha na kuwa historia.

  “Jiji la Arusha kwa sasa kuna upungufu mkubwa wa maji ambapo serikali inakuja na mradi huu mkubwa kwa kuchimba visima 56 tunajenga mfumo wa kusafisha maji na mfumo wa kusambaza maji na mfumo wa kusafisha maji taka na wakandarasi wapo kazini”alisema Prof.Mbarawa.

  Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji (AUWSA) Mhandisi Lucy Koya Alisema kuwa Wakandarasi wanaendelea na kazi ikiwamo utandazaji wa mabomba ya maji taka na kuondoa uvujaji wa maji machafu barabarani kwa kuondoa mabomba ya zamani na kutandika mapya makubwa kutoka na mahitaji ya sasa.

  Amesema kuwa mamlaka hiyo imeongezewa eneo la kata 8 za wilaya ya Arusha dc na tunaishukuru serikali yetu kwa kuona changamoto ya upungufu wa maji na kutuletea mradi huu mkubwa wa billion takribani 520 mkopo nafuu kutoka benki ya maendeleo ya Afrika.

  Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Auwsa Dkt.Richard Masika alisema kuwa bodi yao imejipanga kuhakikisha miradi hiyo inajengwa kwa ufanisi na kwa viwango ndio maana wamepeleka watumishi wa sekta ya utawala kwenye mafunzo ya kusimamia miradi mikubwa kuweza kujifunza ili teknojia hii ibaki nchini na kuboresha weledi ili kupitia mafunzo hayo kujua thamani ya mradi na kuondoa gharama.

  Amesema kuwa mafunzo hayo yatasaidia kuongeza na kusimamia mradi huu kwa ufanisi na weledi na hatutarajii mradi huu ukashindwa kusimamiwa kwa muda uliopangwa na chini ya ubora ila najua utasimamiwa kwa kuangalia ubora na thamani ya mradi na kujengwa kwa muda uliopangwa .

  0 0



  Sehemu ya Washiriki wakiwa katika Mafunzo hayo.
  Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, Mhe. Salvatory Bongole (aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Mahakimu na Wajumbe wa Mabaraza ya Kata wanaoshiriki katika Mafunzo ya siku tatu, Oktoba 08, 2018 hadi Oktoba, 10, 2018.
  Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora, Mhe. Salvatory Bongole (katikati) ambaye pia alikuwa Mhe. Mgeni rasmi wa Mafunzo hayo, akiwa katika picha ya pamoja na Wanasheria wa Manispaa ya Tabora (waliosimama).

  ……………………….

  Na Aisha Abdallah, Mahakama Kuu Tabora

  Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora, Mhe. Salvatory Bongole amefungua rasmi Mafunzo ya Mahakimu na Wajumbe wa Mabaraza ya Kata mkoani humo yanayolenga kuwajengea uwezo wa kuyasimamia mabaraza ya kata katika utekelezaji wa majukumu kwa mujibu wa sheria.

  Akifungua Mafunzo hayo mapema Oktoba 08, katika Ukumbi wa Katibu Tawala, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mhe. Bongole aliwaelezea washiriki wa mafunzo hayo kuwa ni muhimu kwa sababu yataleta uelewa wa pamoja kati ya Mahakama na Mabaraza ya Kata juu ya mamlaka ya Mahakama na Mabaraza katika utoaji haki.

  Aidha katika hotuba yake ya ufunguzi,Mhe. Jaji Mfawidhi huyo pia alisisitiza kuhusu umuhimu wa kumsikiliza mtu kabla ya kutoa maamuzi na kuwaasa wanasemina kuyatekeleza mambo yote watakayojifunza katika semina hiyo. “Kama sehemu ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Mahakama suala la ushirikishwaji wa Wadau limepewa kipaumbele ili tuweze kufanikisha huduma ya utoaji haki”, alisema Mhe. Jaji Bongole.

  Katika semina hiyo, Mahakama imewashirikisha Wanasheria kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora na Halmashauri ya Manispaa-Tabora kama viongozi wa Mabaraza ya Kata. Mafunzo hayo ya siku tatu yameandaliwa na Mahakama ya Tanzania na kuendeshwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA).

  Washiriki ni Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo kutoka Tabora Mjini, Urambo, Nzega na Igunga pamoja na wajumbe wa Mabaraza ya
  Kata na Wanasheria wa Halmashauri ya Manispaa na wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora

  0 0

  Na Mwandishi wetu, Kondoa

  WAKULIMA wa Mbaazi na Choroko hapa nchini wanatarajia kuondokana na adha ya mazao yao kukosa soko baada ya wawekezaji kadhaa kujitokeza kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya kuchakata mazao hayo katika mikoa ya Arusha, Dodoma, Dar es Salaam na Morogoro.

  Kauli hiyo ya matumaini kwa wakulima hao imetolewa wilayani Kondoa mkoani Dodoma na Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omari Mgumba, wakati akitoa salaam kwenye Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Jimbo la Kondoa, ambapo Mbunge wa Jimbo hilo, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, aliwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya chama hicho kwa kipindi cha miaka 3 ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano.

  " Kilimo kinategemewa na zaidi ya asilimia 65 ya watanzania, lakini zao la mbaazi limekuwa na matatizo ya soko ndio maana Serikali imeamua kuchukua hatua kwa kuwahamasisha wawekezaji kujenga viwanda vya kusindika mazao hayo hapa hapa nchini, jambo ambalo limeanza kutekelezwa" alisema Mhe. Mgumba

  Alisema hivi sasa viwanda vitatu vya  kuchakata mbaazi vinajengwa mkoani Arusha, Dar es Salaam na Morogoro katika eneo la Mtego wa Simba, huku kiwanda kimoja na kusindika choroko kikijengwa mkoani Dodoma.

  Alisema kuwa lengo la hatua hizo ni kujibu kero ya muda mrefu ya wakulima wa mazao hayo katika mikoa ya Manyara, Arusha, Dodoma na maeneo mengine yanayolimwa mazao hayo  kukosa soko la uhakika kwa kuongeza thamani ya mazao hayo hapa hapa nchini.

  "Ukiongeza thamani ya hizi mbaazi unapanua soko katika dunia badala ya kutegemea soko moja tu la nchini India, ambapo sasa mbaazi zitauzwa nchi mbalimbali zikiwemo nchi za kiarabu, Ulaya na Marekani" Alisisitiza Mgumba.

  Awali, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango na Mbunge wa Jimbo la Kondoa, Dkt. Ashatu Kijaji alimweleza Naibu Waziri huyo wa Kilimo kwamba Wilaya ya Kondoa ina wakulima wengi ambao wanahitaji kuboreshewa mazingira yao ya kilimo ili waweze kujikwamua kiuchumi

  "Watu wanasema Kondoa ni vijijini kwa asilimia 100 lakini kwa kasi tunayokwenda nayo, baada ya miaka 5 Jimbo hili litakuwa miji mitupu katika kata zote 21 na kitakacho tuvusha kwenda kwenye miji hiyo ni kilimo" alisisitiza Dkt. Kijaji

  Mbaazi imekosa soko katika miaka mitatu mfululizo ambapo bei hiyo ilishuka kutoka  shilingi 2,500 na 3,000 kwa kilo mwaka 2015 na kufikia bei ya shilingi 250 hadi 300 kwa kilo jambo linalowakatisha tamaa wakulima huku wafanyabiashara na baadhi ya wakulima wakiwa na shehena ya zao hilo kwenye maghala wakisubiri kupanda kwa bei.
  Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omari Mgumba, akitoa salaam kwenye Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Jimbo la Kondoa, ambapo Mbunge wa Jimbo hilo, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, aliwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya chama hicho kwa kipindi cha miaka 3 ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano, katika Jimbo la Kondoa, uliofanyika katika Kata ya Pahi, Wilayani Kondoa.

  0 0

  Katibu Mtendaji wa Sekretariet ya SADC Dkt. Stergomena L. Tax na Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Bw. Laurean Rugambwa Bwanakunu wamesaini mkataba wa makubaliano ya MSD kuwa mnunuzi Mkuu wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwa ajili ya nchi 16 wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). 

  Hatua hii inafuatia uteuzi wa serikali ya Tanzania kupitia Bohari ya Dawa (MSD) ulifanywa wakati wa mkutano wa SADC wa mawaziri wa Afya wa nchi wanachama, uliofanyika mwezi Novemba, 2017 nchini Afrika Kusini. 
   Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Bw. Laurean Bwanakunu amesema tangu wakati huo hadi sasa wamekuwa wakishirikiana na na Sekretarieti ya (SADC) kuandaa rasimu ya mpango wa utekelezaji wa manunuzi ya pamoja yaani SADC Pooled Procurement Services (SPPS). 

   Amesema kulingana na mpango huo, uratibu wa manunuzi unaanza rasmi tarehe leo, tarehe 9/10/2018, kupitia mkataba wa makubaliano yaani Memorandum of Understanding (MoU) kati ya MSD na Sekretarieti ya SADC. 
   Bwanakunu ameongeza kuwa MSD itakuwa na majukumu ya kupokea mahitaji ya manunuzi ya dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kutoka kwa nchi hizo 16 za Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), kununua dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara, kusimamia takwimu na taarifa za dawa pamoja na kusimamia Kanzidata (Database) ya dawa za nchi hizo. 

   Ameongeza kuwa MSD itasimamia bei elekezi ya dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara, kusimamia mfumo wa manunuzi kwa njia ya mtandao kwa nchi zote wanachama, kutoa huduma za kitaalam na kupanga bei elekezi. MSD pia itaanzisha kitengo maalumu ndani ya kurugenzi ya manunuzi kwa ajili ya kazi hii ya ununuzi wa dawa, vifaa tiba ba vitendanishi vya maabara kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya SADC tu. 

   Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Sekretariet ya SADC Dkt. Stergomena L. Tax ameeleza kuwa Tanzania kuwa mnunuzi mkuu wa dawa kwa nchi za Ukanda wa SADC ni heshima kubwa kwa Taifa, kuaminiwa kwa huduma bora, uwezo na kukidhi vigezo vya kitaalamu katika mnyororo wa ugavi. 

   Makubaliano hayo yameshuhudiwa na Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye amesema kwamba SADC imeipa Tanzania heshima kubwa na kuichagiza MSD kuhakikisha inatekeleza majukumu yake vizuri ili isionekane kuwa SADC ilifanya makosa kuichagua Tanzania.
  Katibu Mtendaji wa Sekretariet ya SADC Dkt. Stergomena L. Tax na Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Bw. Laurean Rugambwa Bwanakunu wakisaini mkataba wa makubaliano ya MSD kuwa mnunuzi Mkuu wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwa ajili ya nchi 16 wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) makao makuu ya MSD jijini Dar es salaam Oktoba 9, 2018
  Katibu Mtendaji wa Sekretariet ya SADC Dkt. Stergomena L. Tax na Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Bw. Laurean Rugambwa Bwanakunu wakibadilishana nyaraka baada ya kusaini  mkataba wa makubaliano ya MSD kuwa mnunuzi Mkuu wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwa ajili ya nchi 16 wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) makao makuu ya MSD jijini Dar es salaam Oktoba 9, 2018 
  Katibu Mtendaji wa Sekretariet ya SADC Dkt. Stergomena L. Tax na Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Bw. Laurean Rugambwa Bwanakunu wakionesha nyaraka za mkataba wa makubaliano ya MSD kuwa mnunuzi Mkuu wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwa ajili ya nchi 16 wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) makao makuu ya MSD jijini Dar es salaam Oktoba 9, 2018
  Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akipeana mikono na Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Bw. Laurean Rugambwa Bwanakunu baada ya hafla hiyo fupi makao makuu ya MSD jijini Dar es salaam Oktoba 9, 2018

  0 0









  Kamishna Msaidizi na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Barnabas Mwakalukwa akinyanyua juu moja ya bunda la Dola za Kimarekani zilizokamatwa leo kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), zikisafirisha isivyo halali na raia wa Sudan Kusini Bi. Nada Zaelnoon Ahamed na Bw. Mohamed Belal, raia wa Syria.
  Jumla ya Dola za Kimarekani 70,000 sawa na Tsh. milioni 156 za Kitanzania zikiwa zimekamatwa leo kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), zikisafirishwa na Raia wawili wa Syria Bw. Mohamed Belal na Bi. Nada Zaelnoo Ahamed raia wa Sudan Kusini kwa kutofuata taratibu.
  Bi.Nada Zaelnoon Ahamed (38) Raia wa Sudan Kusini (katikati mwenye ushungi) akiwa mbele ya waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa Jengo la Pili la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), baada ya kukamatwa na dola 60,000 za Kimarekani na Paundi 3410 za Sudan.

  Raia wa Syria, Bw. Mohamed Belal (31) mwenye fulana nyeupe akiwa mbele ya waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa Jengo la Pili la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), baada ya kukamatwa na dola 10,000 za Kimarekani, ambazo hakuzitolea taarifa kwa Maafisa wa Forodha wa kiwanjani hapo.
  Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Paul Rwegasha (kushoto) akimsikiliza Kamishna Msaidizi wa Polisi, Barnabas Mwakalukwa (aliyesimama) alipokuwa akitoa maelezo kwa waandishi wa habari leo ya kukamatwa kwa Raia wawili wa Sudan Kusini na Syria waliokuwa wakisafirikisha fedha taslim milioni 156 bila kufuata sharia.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (wa pili kulia) akisisitiza jambo kwenye mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) uliofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Jengo la Pili la abiria la Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), wakati walipokamatwa Raia wawili wa Syria na Sudan Kusini wakisafirisha mamilioni ya fedha bila kufuata taratibu.


  ABIRIA wawili Raia wa Sudan Kusini na Syria leo wamekamatwa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) wakisafirisha fedha taslim dola 70 za Kimarekani sawa na shilingi milioni 156 za Kitanzania na paundi 3410 za Sudan bila kufuata taratibu.

  Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa Jengo la Pili la abiria la JNIA, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi, Barnabas Mwakalukwa alimtaja Raia wa Sudan Kusini Bi. Nada Zaelnoon Ahamed (38) mwenye hati ya kusafiria namba P01563534 amekamatwa saa 10:00 jioni akiwa eneo la ukaguzi wakati akiingia ndani tayari kusafiri kwa ndege ya Shirika la Ndege la Kenya (KQ 485) akielekea Nairobi.

  Hatahivyo, Afande Mwakalukwa amesema abiria huyo mbali na fedha hizo za Kimarekani pia amekamatwa na paundi za Sudan 3410, ambazo zote kwa pamoja alishindwa kutoa taarifa ya fedha alizokutwa nazo kwa mujibu wa sheria ya utakatishaji fedha ya mwaka 2006 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2012.

  Pia alimtaja Bw. Mohamed Belal (31), Raia wa Syria mwenye hati ya kusafiria namba 003-16L096876 aliyekuwa akisafiri kwa ndege ya Shirika la ndege la Ethiopia (ET 864) kuelekea Syria kupitia Addis Ababa amekamatwa na dola za kimarekani 10,000 sawa na Tsh. milioni 20 za Kitanzania, ambazo naye alishindwa kuzitolea taarifa. “Watuhumiwa wote wawili wamezuiwa na hawawezi kuendelea na safari zao kwa ajili ya uchunguzi zaidi na hatua za kisheria zilizopo,” amesema Afande Mwakalukwa.

  Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela amewapongeza maafisa usalama wa JNIA kwa kufanya kazi kwa weledi na uadilifu pamoja na kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama katika kuhakikisha wasafiri, wadau na maeneo yote ya viwanja vya ndege yanabaki salama na vitendo vya kiuhalifu havina nafasi katika viwanja hivyo. Bw. Mayongela amesema pamoja na watumishi hao kufanya kazi katika wakati mgumu kutokana na baadhi ya abiria kuwa watata kila wanapotaka kutekeleza wajibu wao kwa mujibu wa sheria na kanuni.

  Ametoa wito kwa wadau, wasafiri na wafanyakazi wote kushirikiana na maafisa usalama, vyombo vya ulinzi na usalama katika kutoa taarifa stahiki ili vitendo vya kiuhalifu kama hivi visipate nafasi kwenye viwanja vya ndege kwani ndio vinatoa taswira ya nchi. “Viwanja vya ndege visitumike kama uchochoro wa kupitisha nyara za serikali, dawa za kulevyia, fedha haramu au matukio yeyote yanayoashiria uvunjifu wa Amani au uvunjaji wa sheria za nchi,”

  Pia aliongeza “Niombe wananchi na vyombo vya usalama kufanya kazi kwa weledi kwa sababu wasipofanyakazi kwa weledi matukio kama haya yangeweza kupata nafasi na kuharibu taswira ya nchi, kwa ujumla mwisho wa siku inaharibika, kwani nia yetu na lengo letu ni zuri ni kuhakikisha hatutumiki kwa namna moja au nyingine kufadhili au kuwezesha shughuli za kiuhalifu zifanyike katika maeneo yetu”.

  Amesema na hii ni moja ya ushahidi maafisa usalama wanapata mafunzo na kujengewa uwezo wa kuwa na vifaa vya kisasa kwani vitu mbalimbali vimekuwa vikigundulika kupitia mashine za ukaguzi, na pia kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama, hivyo ametoa wito watu wasidhubutu tena kujaribu kwa namna yeyote ile akidhani viwanja vya ndege wamelala, kwani ulinzi na usalama unaendelea kuimarika.

  Kwa upande wake Meneja wa Forodha wa Kituo cha JNIA, Bw. Njaule Mdendu amesema abiria wote wanaosafiri au kuwasili endapo wanakiasi kikubwa cha fedha za kigeni kuanzia dola 10,000 za Kimarekani sawa na Milioni 10 za Kitanzania anapaswa kutoa taarifa Idara ya Forodha kwa kuwa ni matakwa ya sheria ya mwaka 2006 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2012 na kanuni za mwaka 2016, na asipofanya hivyo ni kosa la jinai

  Bw. Mdendu amesema abiria wanapaswa kuchukua fomu maalum akieleza utambulisho wake na kiasi cha fedha anachoingia nacho au kutoka nacho, na fomu atazipata kwenye ofisi zote za forodha za mipakani kwenye viwanja vya ndege, mipaka ya ardhi na majini endapo atakuwa akitumia usafiri wa barabara au majini.

  “Hizi fomu pia zipo kwenye tovuti ya Mamlaka ya Mapato Tanzania na akishajaza anawasilisha ofisi za Forodha na kiasi cha fedha anachosafiri au kuwasili nacho na afisa atazihakiki na akiridhika ataruhusu aendelee na safari yake, na napenda kuwatoa hofu watu kuwa fedha zao hawanyang’anyi baada ya kutoa taarifa na ataondoka nayo, lakini endapo usipotoa taarifa ni kosa na inaadhabu yake kulingana na kiasi cha fedha ulichokutwa nacho, hivyo tuwaombe abiria kutimiza matakwa ya kisheria, kwani watu wamekuwa wakifanya makosa bila kujua sheria,” amesema.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila akifungua semina ya uraghibishaji na uhamasishaji wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kwa viongozi wa mkoa na Wilaya kwenye ukumbi wa halmashauri wa Benjamin Mkapa Jijini Mbeya.Kulia ni Ofisa mpango toka Wizara ya Afya Osca Kaitaba na mwisho ni Mkuu wa Wilaya ya Kyela Bi.Claudia Kitta.
  Ofisa Mpango toka Mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Osca Kaitaba akifafanua jambo kwenye mkutano huo


  Na.WAMJW,Mbeya


  Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele yameleta mahangaiko pamoja na athari kwa jamii wa Mkoa wa mbeya ikiwepo ulemavu

  Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Mkoa wa MbeyaSerikali Mkoani Mbeya imesema kuwa nchi zilizo katika Ukanda wa kusini mwa Jangwa la Sahara ambazo zinakabiliwa na tatizo la magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele zimeathiri sehemu kubwa ya jamii Mkoani hapa na kuleta mahangaiko kwa wananchi pamoja na ulemavu.

  Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila wakati wa ufunguzi wa semina ya uraghibishaji na uhamasishaji wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kwa viongozi wa Serikali wa Mkoa na wilaya mkoani hapa.Alisema Magonjwa hayo yamekuwa yakiathiri zaidi wananchi na kiasi kikubwa yakipunguza uwezo wa wananchi katika shughuli za uzalishaji na ujenzi wa Taifa.


  “Magonjwa haya, pamoja na kusababisha usumbufu mkubwa kwa waathirika pia yanaongeza matumizi ya rasilimali chache tulizonazo katika kuyakabili “alisema Mkuu huyo mkoa.

  Aidha,Chalamila alisema kwamba uwepo wa magonjwa hayo umefanya watoto kutokuwa na mahudhurio mazuri mashuleni kutokana na muda mwingi kuwa wanaumwa.Hata hivyo alisema kuwa jambo la kutia moyo ni kwamba Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na wadau wamekuwa wakitoa Kingatiba za kukinga magonjwa haya katika mkoa wa Mbeya.

  “Hii ni kutokana na lengo la Serikali ya awamu ya tano ambalo ni kudhibiti magonjwa haya na hivyo kupunguza gharama kwa wananchi kwa kugawa kingatiba hizo”Alisisitiza Chalamila

  Akielezea zaidi Chalamila alisema Mkoa wa Mbeya walikuwa wanakabiliwa na magonjwa yote matano ambayo ni minyoo ya tumbo kichocho, matende na mabusha katika wilaya zote ila kwakuwa na usimamizi na uhamasishaji nzuri mkoa wake hivi sasa wamepunguza magonjwa hayo na hivyo kuwataka viongozi wa mkoa na Wilaya zake kuzidi kuhamasisha na kuelimisha zaidi wananchi kujitokeza kumeze kingatiba ili kutokomeza magonjwa hayo.

  Alisema kwa upande wa ugonjwa wa Trakoma kwa wilaya za Kyela, Chunya na mbarali, ugonjwa wa usubi upo kwa wilaya za rungwe, Kyela na busokelo.Kwa upande wake ofisa mpango kutoka Mpango wa Kudhibiti Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele Wizara ya Afya Oscar Kaitaba alisema semina hiyo imejumuisha wajumbe kutoka halmashauri tatu za mkoa wa Mbeya ambazo ni Rungwe, Kyela, Busokelo.Aidha Kaitaba alitaja wajumbe hao kuwa wakuu wa wilaya, wakurugenzi,waweka hazina wa Wilaya, waganga wakuu waratibu pamoja na maafisa usalama wa wilaya

  0 0

  Benki ya Dunia imeahidi kuwekeza zaidi nchini Tanzania katika Sayansi na  Teknolojia ili kuongeza kasi ya maendeleo ya kiuchumi  kwa lengo la kuisaidia Tanzania kukuza uchumi wa viwanda na kuondoa umasikini  kwa wananchi wa wake.
  Hayo yameelezwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango, alipofanya mkutano na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Bw. Hafez Ghanem, katika mikutano ya mwaka ya Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Mjini Bali Indonesia.                     
  Dkt. Mpango amesema kuwa Benki ya Dunia imeamua kuwekeza katika teknolojia kwa kuwa ni eneo sahihi linaloweza kukuza uchumi wa Taifa kwa zaidi ya mara mbili kutokana na tafiti zilizofanywa na Benki ya Dunia.
  “Kimsingi Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia amefurahia ajenda za maendeleo za Tanzania kuhusu kujenga uwezo wa rasilimali watu katika kukuza uchumi wa viwanda na ameahidi kuanza kwa kuwekeza zaidi kwa watoto wenye umri mdogo ili mipango ya maendeleo ya nchi iwe endelevu”, alieleza Dkt. Mpango.
  Aidha Waziri Mpango alimueleza Makamu wa Rais wa Benki hiyo kuwa Tanzania imeweka  mikakati  mbalimbali ya kujenga uchumi wa viwanda utakaotumia malighafi za ndani ili kuongeza ajira kwa wananchi walio wengi.
  Kuhusu umuhimu wa Sekta Binafsi katika maendeleo ya nchi Waziri Mpango alisema Makamu wa Rais Bw. Ghanem, ameahidi kuwekeza zaidi katika miradi ya pamoja kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP), kwa kuiwezesha Serikali ya Tanzania na wadau wengine kwenda kupata mafunzo yatakayoongeza ujuzi wa utekelezaji wa miradi hiyo katika nchi zilizofanya vizuri katika eneo hilo ili kuongeza ufanisi wakati wa utekelezaji wa miradi hiyo.
  Kwa upande wake Kamishna na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere, amesema kuwa mfumo wa dunia ya sasa unazitaka nchi kujitegemea kimapato hivyo TRA itaendelea kuongeza nguvu ya ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa  kuwa Benki ya Dunia imeahidi kuboresha miundomibnu ya ukusanyaji mapato kwa nchi ya Tanzania.
  Waziri Mpango ameiomba Benki ya Dunia iendelee kuisaidia Tanzania kwa kutoa rasilimali fedha katika kuwezesha miundombinu ya kukuza uchumi ikiwemo ya miradi ya nishati ya umeme, ujenzi wa reli kwa kiwango cha Kimataifa (SGR), na miradi ya maji.
  Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia ameahidi kutembelea Tanzania mwanzoni mwa mwaka ujao ikiwa ni juhudi za kuendeleza ushirikiano wa kimaendeleo kati ya benki hiyo na Tanzania.
  Mikutano ya mwaka ya Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), inaendelea mjini Bali Indonesia ambapo imewakutanisha wadau wa masuala ya fedha wakiwemo Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu kutoka nchi mbalimbali Dunia kujadili Sera na misaada inayotolewa na Taasisisi hizo.
   Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), akiwa na Waziri wa Fedha na Mipango wa  Zanzibar Dkt. Khalid Salum Mohamed, muda mfupi kabla ya Mkutano na Makamu wa Rais wa  Benki ya Dunia (WB) Bw. Hafez Ghanem, katika mkutano wa mwaka wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na WB,  Mjini Bali, Indonesia.
   Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na ujumbe wake  na Makamu wa Rais wa  Benki ya Dunia (WB) Bw. Hafez Ghanem na ujumbe wake katika mkutano wa mwaka wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na WB mjini Bali, Indonesia.
   Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb)  (wa pili kushoto) akielezea miradi ya maendeleo ambayo inahitaji fedha ili iweze kuchochea uchumi ikiwemo miradi ya Nishati ya Umeme na ujenzi wa miundombinu ya Reli ya Kisasa kwa kiwango cha Kimataifa – SGR alipofanya Mkutano na Makamu wa Rais wa  Benki ya Dunia (WB) Bw. Hafez Ghanem, katika mkutano wa mwaka wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na WB Mjini Bali Indonesia.
   Makamu wa Rais wa  Benki ya Dunia (WB) Bw. Hafez Ghanem (katikati) akieleza nia ya Benki yake ya kuwekeza kwenye mafunzo ya Miradi ya pamoja kati ya Sekta Binafsi na Sekta ya Umma Mjini Bali Indonesia alipofanya Mkutano na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb)  (hayupo pichani).
  Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar Dkt. Khalid Salum Mohamed(kulia) akizelezea miradi ya kukuza utalii ambayo inahitaji fedha ili kuweza kuchochea maendeleo wakati wa Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia (WB) Bw. Hafez Ghanem, katika mkutano wa mwaka wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na WB, Mjini Bali Indonesia.

  0 0



















  0 0

  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly kulia akielezea mipango ya mamlaka hiyo wakati wa ziara ya ugeni kutoka KFW ya nchini Ujerumani kutembelea mradi wa maboresho ya huduma ya maji safi Jijini Tanga
  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly katikati akionyesha kitu ugeni kutoka KFW ya nchini Ujerumani wakati wa ziara yao ya kutembelea mradi wa maboresho ya huduma ya maji safi Jijini Tanga.kulia ni Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi 
  Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi akizungumza wakati wa ziara hiyo kushoto ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly 
  Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi kulia akifirahia jambo na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maji Mijini kutoka Wizara ya Maji -Dodoma Mhandisi Lydia Joseph kushoto wakati wa ziara hiyo 
  Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi akilakiwa na watumishi wa mamlaka hiyo mara baada ya kuwasili eneo la Mowe 
  Wageni hao wakishuka kwenye eneo la kusafishia maji Mowe Jijini Tanga wakati wa ziara hiyo 
  Wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumaliza ziara hiyo 


  MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) imenufaika na ruzuku ya zaidi ya Shilingi bilioni 1.2 baada ya kutimiza masharti ya mkopo wa zaidi ya shilingi Bilioni 3 toka katika benki ya CRDB ya utekelezaji wa huduma ya Maji safi Jijini Tanga.

  Ruzuku hiyo hutolewa na Benki ya watu wa Ujerumani (KFW) kutokana na Mamlaka husika kutimiza vema masharti ya mkopo huo ikiwa pamoja na zoezi zima la marejesho huku likizingatiwa suala la utekelzaji wa mradi uliopewa fedha hizo.

  Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly wakati wa ziara ya ugeni kutoka KFW ya nchini Ujerumani kutembelea mradi wa maboresho ya huduma ya maji safi Jijini Tanga.

  Alisema mkopo huo umewasaidia kuongeza uwezo wa usambazaji wa maji hasa katika maeneo yaliyokuwa na mgawo wa maji bila sababu yaliyochangiwa na udogo wa vipenyo vya mabomba yaliyokuwa yanapeleka maji kwenye maeneo hayo.“Kama nilivyoonyesha kwamba tumeongeza bomba kubwa la nchi 8 kwa ajili ya kuongeza mgawanyo wa maji kwenye eneo la Neema na kwengineko na kuwepo kwa usambazaji mkubwa kwenye maeneo hayo lakini pia tumejenga mtandao wa km 60 kwa kutumia mkopo huo na ruzuku tuliyopewa”Alisema

  Aidha alisema hivi sasa wamejipanga kuendelea kudumisha ubora wa huduma zao ili kuhakikisha wananchi wanaowahudumia wanaendelea kupata huduma bora ya maji katika maeneo yao.Alisema mbali ya ubora wa huduma hizo za maji lengo kuu ni kuhakikisha wanapokuwa wageni wahisani waweza kupata mrejesho na taswira nzuri kwa mamlaka ili waendelee kupata moyo wa kuwasaidia.

  Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maji Mijini kutoka Wizara ya Maji -Dodoma Mhandisi Lydia Joseph alisema fedha hizo zinalenga katika miradi inayojenga inalengo la kutoa uzoefu kwa mamlaka za maji zinazoingizwa kwenye mfumo huo iliziweze kupata uzoefu wa kuwekeza badala ya kuishia kutoa huduma pekee.

  Alisema mamlaka nyingi zimekuwa na lengo la kutoa huduma ya maji kwa wananchi kwa miundombinu iliyojengwa na serikali tangu zamani hivyo kutokana na ongezeko la watu na mahitaji yao Mamlaka zinatakiwa kupanua huduma zao.

  Mhandisi Lydia alisema mbali na huduma pia mamlaka hizo za maji zinatakiwa kuboresha miundombinu ambayo inahitaji uwezeshwaji kutokana na serikali kuwa na mambo mengi ya kufanya hivyo wakati mwengine huelemewa na uwekezaji jambo ambalo limepelekea kushindwa kuendana nakasi ongezeko la watu.

  “Kwa maana hiyo Mamlaka zetu kama zitapata mikopo na zikijenga uaminifu zinaweza kupata miradi kama hiyo na zaidi ya hiyo huku zikijijengea morali kwa mamlaka zenyewe hasa kwenye uwekezaji na Serikali ikatoa sapoti ”Alisema Mhandisi Joseph.

  0 0


  Ngoma ya Kabila la wamaasai wakiimba katika Tamasha la Urithi Festival lililozinduliwa Jijini Arusha Katika uwanja wa Shekhe Amri Abeid .Picha na Vero Ignatus.
  Baadhi ya washiriki wakila ugali wa asili na mlenda katika tamasha la urithi festival katika uwanja wa shekh Amri Abeid Jijini Arusha na Vero Ignatus.
  Katibu mkuu Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Suzan Mlawi akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Arusha katika Tamasha la Urithi Festival lililozinduliwa mkoani Arusha. Picha na Vero Ignatus
  Katibu mkuu Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Suzan Mlawi akiwa katika moja ya banda wanalotengeneza vitu vya asili. Picha na Vero Ignatus.
  Kutoka katikati ni Katibu mkuu wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Suzan Mlawi, kulia kwake ni Mkurugenzi mkuu wa Makumbusho ya Taif a Profesa Audix Mabula ambaye pia ni Mwenyekiti wa maandalizi ya Tamasha la Urithi, akifuatiwa na Katibu tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kwitega. Picha na Vero Ignatus.
  Kushoto ni Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa Profesa Audix Mabula, Katibu Mkuu wizara ya habari michezo michezo na Utamaduni Suzan Mlawi wakiwa katika moja ya banda uwanjani hapo. Picha na Vero Ignatus.

  Ngoma ya asili ya Wakina mama kutoka kabila la Kimeru. Picha na Vero Ignatus
  Hawa nao wakinamama kutoka kabila la Kimaasai walipamba Tamasha hilo la Urithi na utamaduni mkoani Arusha katika uwanja wa Shekh Amri Abeid. Picha na Vero Ignatus.




  Na.Vero Ignatus ,Arusha

  Kila mwaka mkoa unatakiwa kutenga fungu kwaajili ya kuandaa tamasha la urithi na utamaduni itakayochangia kuzaa zao jipya la utalii na kupanua wigo wa vivutio vya utalii nchini.

  Hayo yamesemwa na Katibu mkuu wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Suzan Mlawi katika uzinduzi wa Tamasha la Urithi lililozinduliwa Jijini Arusha katika uwanja wa Shekh Amri Abeid na kushirikisha makabila mbalimbali mkoani hapo.Ameeleza kuwa Taifa lisilo na utamaduni ni taifa lililokufa, sambamba na kupoteza rasilimaliza husika kwani utamaduni ni kuvutio kibwa cha utalii.

  "Tusipoenzi na kuzitunza tamaduni hizo utu wetu rasilimali zetu zitapotea, kwani utamaduni wetu ni kivutio kikubwa cha utalii"alisema Katibu Suzan Kwa upande wake Katibu tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kwitega amesema asilima 80%wageni wanaoingia nchini wanatembelea Mkoani hapo kutokana na vivutio vilivyopo mkoani Arusha kupitia vya utalii Maonyesho hayo yamehusisha wadau kuonyesha mambo burudani,ngoma za asili,vyakula vya asili,mavazi ya asili ,utalii na tamaduni za Mtanzania bila kuvunja sheria .

  Tutapata nafasi nzuri za kuona tamaduni mbalimbali za kuona mambo mbalimbali, mavazi, vyakula, michezo ya asili.alisema Kwitega.Mkurugenzi mkuu wa Makumbusho ya Taif a Profesa Audix Mabula ameipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kubuni wazo hilo zuri, kwa kutambua na kuthani, kutafiti na kuhifadhi vitu vya asili kwa manufaa ya Watanzania na kwa vizazi vijavyo.

  Ikumbukwe kuwa septemba 15 Tamasha la Urithi Festival lilizinduliwa rasmi Jijini Dodoma na Makamu wa Rais Samia Suluhu likiwa na kauli mbiu isemayo "Urithi wetu Fahari yetu"Maonyesho hayo yamehusisha wadau mbalimbali kuonyesha mambo burudani,ngoma za asili,vyakula vya asili,mavazazi ya asili ,utalii na tamaduni Kuhifadhi tamaduni zetu nzuri Tamasha hilo la urithi litafungwa tarehe 13 octoba na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika uwanjawa Shekh Amri Abeid Arusha.

older | 1 | .... | 1692 | 1693 | (Page 1694) | 1695 | 1696 | .... | 1897 | newer