Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1688 | 1689 | (Page 1690) | 1691 | 1692 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amemfukuza msimamizi wa ujenzi wa bandari ya Nyemirembe iliyopo wilayani Chato mkoani Geita kwa kukosa sifa na utaalam wa kusimamia ujenzi wa bandari hiyo na miundombinu yake na kuagiza aondolewe mara moja kwenye eneo hilo

  Hayo yamejitokeza wakati wa ziara ya Nditiye ya kukagua hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa bandari hiyo na miundombinu yake ambapo mkandarasi wa kampuni ya V.J Mistry & Co. Ltd amepewa jukumu hilo na Serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) ya kujenga bandari hiyo kwa gharama ya shilingi bilioni 4.128.

  Katika ziara hiyo, Nditiye amebaini kuwa msimamizi wa ujenzi wa bandari hiyo Bwana Pravin Rabadhia wa mkandarasi wa kampuni ya V.J Mistry & Co. Ltd, hana utaalamu, sifa wala vigezo vyovyote vya kusimamia mradi huo unaogharimu matumizi ya fedha nyingi zinazotokana na fedha za makusanyo ya kodi ya wananchi. Pia, alibaini uwepo wa Bwana Dipak Chaganlal, mfanyakazi wa kampuni hiyo ya mkandarasi aliyejitambulisha kwa Nditiye kuwa ana taaluma ya “storekeeper” akiwa msimamizi msaidizi wa mradi wa ujenzi wa bandari hiyo.

  Nditiye alielekeza msimamizi huyo aondolewe eneo la mradi wa ujenzi wa bandari ya Nyemirembe na mamlaka husika za vibali vya ajira, uhamiaji na mamlaka nyingine za manunuzi, bodi za makandarasi nchini zimchunguze taaluma yake, uraia wake, uhalali wake wa kufanya kazi ya kuwa msimamizi wa mradi huo kwa kuwa katika mahojiano nae akiwa kwenye eneo la mradi huo, wasimamizi hao wenye asilia ya kiasia hawakuweza kutoa maelezo yoyote ya kitaalamu kuhusu maendeleo ya ujenzi wa bandari hiyo.

  Nditiye ameelekeza kuwa kazi hiyo ya ujenzi wa bandari ya Nyemirembe isimame kwa muda wa wiki moja na amemtaka mkandarasi wa kampuni hiyo kufika na kuripoti ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita mara moja akiwa na wataalamu wanaohitajika kufanya kazi hiyo kuendana na matakwa ya mkataba husika na kuhakikisha kuwa wafanyakazi na vibarua wote wanalipwa fedha zao

  Ameongeza kuwa, Serikali haiwezi kuvumilia jambo hili kwa kuwa tayari imemlipa mkandarasi malipo ya awali ya asilimia 20 kuendana na makubaliano ya mkataba wa ujenzi huo yenye thamani ya shilingi milioni 800 katika kipindi cha miezi miwili iliyoishia ambapo hamna dalili yeyote ya mkandarasi ya kuonesha uwezo wa kujenga bandari hiyo kwa kuwepo na ukosefu wa vifaa na wataalamu kwenye eneo la mradi wa ujenzi wa bandari hiyo

  Naye Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel akiwa kwenye ziara hiyo amesema kuwa Serikali ya Mkoa wa Geita haiko tayari kufanya kazi na mkandarasi wa namna hii labda wakafanyie kazi zao nje ya Wilaya ya Chato na Mkoa wa Geita kwa kuwa Serikali imeifanya Wilaya ya Chato kuwa eneo la kimkakati la uwekezaji ili iweze kuhudumia mikoa ya Geita, Simiyu na Kagera. 
   
  “tunapata hamasa kubwa kwa kuona bandari ya Nyemirembe iliyokufa inafanyiwa kazi ili biashara ya usafirishaji wa mizigo na abiria ifanyike na tutumie fursa zilizopo kwa kuwa Serikali inabadilisha matumizi ya pori la akiba la Biharamulo na kuwa hifadhi ya taifa, hivyo ujenzi wa miundombinu kutainua fursa na kuleta watalii,”amesema Gabriel. Naye Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhandisi Mtemi Msafiri Simeon akiwa katika ziara hiyo alisema kuwa Chato ni kituo kikubwa cha uwekezaji, sekta ya utalii itatumia bandari hii. Bandari iwe ya kutosheleza abiria 200 hadi 300 na tuangalie namna ya kupanua eneo ili litoshe mahitai ya miaka 10 hadi 20 baadae

  Kaimu Meneja wa Bandari za Ziwa Victoria Bwana Morris Mtindichiusa amemweleza Nditiye kuwa, mkandarasi amesaini mkataba wa ujenzi wa bandari ya Nyemirembe na miundombinu yake ikiwemo gati la kupakia na kupakua mizigo, ujenzi wa jengo la abiria, ujenzi wa ghala la kuhifadhia mizigo, ujenzi wa mnara wa tanki la maji, ujenzi wa vyoo, jengola walinzi, jengo la kuhifadhia jenereta, uzio na mageti yake.

  Ameongeza kuwa mkandarasi ameanza kazi rasmi tarehe 2 Agosti, 2018 ambapo mkataba ulisainiwa tarehe 13 Juni 2018 na mkandarasi alikabidhiwa eneo la mradi tarehe 17 Julai, 2018. Mkataba huo ni miezi 12, hivyo ujenzi wa bandari ya Nyemirembe na miundo mbinu yake unahitajika kukamilika katika kipindi cha mwaka mmoja.

  Amefafanua kuwa bandari hiyo itakuwa na ghala la mizigo lenye uwezo wa kuhifadhi tani 3000 za mizigo na jengo la abiria litakuwa na uwezo wa kuchukua abiria 200 hivyo watazingatia maelekezo yaliyotolewa ili liweze kuchukua abiria 300. Pia, amesema kuwa kasi ya ujenzi wa bandari hiyo na miundombinu yake ni ndogo na hairidhishi kwa kuwa kwa kiasi cha fedha ambayo mkandarasi amelipwa alitakiwa awe amefikia asilimia 9 ya ujenzi badala ya asilimia 6 waliyofikia sasa. 
   
  Hivyo, ameahidi kuzingatia na kutekeleza maelekezo yalitolewa ya kumuondoa msimamizi wa mradi huo kwenye eneo la ujenzi wa bandari hiyo na kuhakikisha kuwa mkandarasi wa kampuni hiyo anafika ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chato kuripoti na kujitambulisha ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa kampuni hiyo inaweka msimamizi wa mradi mwenye utaalamu na ujuzi unaotakiwa


  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano 

  Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (kulia) akikagua maendeleo ya ujenzi wa bandari ya Nyemirembe iliyopo wilayani Chato, Geita. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel na wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo Mhandisi Mtemi Msafiri Simeon
  Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akimhoji mfanyakazi wa mkandarasi wa kampuni ya V.J Mistry & Co. Ltd Bwana Dipak Chaganlal (mwenye asili ya kiasia) kuhusu maendeleo ya ujenzi wa bandari ya Nyemirembe iliyopo wilayani Chato, Geita. Mwenye kofia nyeusi ni Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel
  Kaimu Meneja wa Bandari za Ziwa Victoria Bwana Morris Mtindichiusa akiandika maelekezo ya Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) kwa ajili ya ujenzi wa bandari ya Nyemirembe iliyopo wilayani Chato, Geita. Mwenye kofia nyeusi ni Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel 
  Wafanyakazi wa kampuni ya mkandarasi ya V.J Mistry & Co. Ltd wakiendelea na kazi mbali mbali za ujenzi wa bandari ya Nyemirembe iliyopo wilayani Chato, Geita wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Uchukuzi n Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (hayupo pichani) wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa bandari hiyo


  0 0

  Na Genofeva Matemu - JKCI

  Jumla ya wagonjwa 36 wamefanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua na bila kufungua kifua katika kambi maalum ya matibabu inayofanyika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).

  Upasuaji huo unafanywa na madaktari bingwa wa moyo wa Taasisi hiyo kwa kushirikiana na wenzao wa Shirika la Albalsam Care & Care la nchini Saudi Arabia ambapo wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa kufungua kifua ni 10 na bila kufungua kifua kwa kutumia mtambo wa Cathlab kwa njia ya kutoboa tundu dogo katika paja 26.

  Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu Bashir Nyangasa alisema wagonjwa waliofanyiwa upasuaji hali zao zinaendelea vizuri na wengine wameshatoka katika chumba cha uangalizi maalum na kurudi wodini kwa ajili ya kufanya mazoezi pamoja na matibabu.

  “Tunafanya upasuaji wa kubadilisha valvu kwa wagonjwa ambao valvu zao hazifanyi kazi vizuri, kubadilisha mishipa ya moyo inayosafirisha damu kutoka mishipa mikubwa kwenda kwenye mzunguko wa moyo na kuziba matundu kwenye moyo kwa watu waliozaliwa na matundu hayo”,.

  “Katika kambi hii tumemfanyia upasuaji wa kupandikiza mshipa wa damu kutoka kwenye mguu na kuuweka kwenye moyo mgonjwa aliyekuwa na maradhi mawili ya moyo ambayo ni kuziba kwa mishipa ya damu na mlango mkubwa wa moyo”, alisema Dkt. Nyangasa.

  Dkt. Nyangasa aliwashauri wananchi wasingojee kuumwa ndio waanze kutafuta bima za afya bali wajenge mazoea ya kuwa na bima za afya kwani mwili ni kama gari linalopelekwa gereji mara kwa mara kwa ajili ya ukarabati vivyo hivyo mwili unatakiwa kufanyiwa uchunguzi wa afya mara kwa mara ili kuepuka vifo vya ghafla.

  Kwa upande wake daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu kutoka Shirika la Albalsam Care and Care la nchini Saudi Arabia Emad Bukhari aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuwekeza katika vifaa vya kisasa vya matibabu ya moyo.

  Dkt. Emad Bukhari alisema ,“Kuwepo kwa mashine hizi za kisasa, wataalam pamoja na huduma nzuri za kibingwa katika Taasisi hii, kumeifanya kutambulika kimataifa na hivyo kuzifanya taasisi zinazotibu magonjwa ya moyo Duniani kuja mahali hapa kutoa huduma kwa wananchi”, .

  Kambi hiyo ilienda sambamba na utoaji wa elimu pamoja na ubadilishanaji wa ujuzi wa kazi ambao umewajengea uwezo madaktari, wauguzi pamoja na wataalamu wa mashine za moyo.


  0 0


  Mwenyekiti wa Tume ya Madini Profesa Idris Kikula (kushoto) akielezea takwimu za leseni zilizotolewa na Tume ya Madini tangu kuanzishwa kwake kwenye mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika jijini Dodoma mapema tarehe 04 Oktoba, 2018. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya.
  Mwenyekiti wa Tume ya Madini Profesa Idris Kikula (katikati) akitoa ufafanuzi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya na kushoto ni Mkurugenzi wa Leseni na TEHAMA wa Tume ya Madini, Torece Ngole  Na Greyson Mwase, Dodoma

  Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa kati ya kipindi cha mwezi Mei hadi Septemba mwaka huu, Tume ya Madini, imetoa leseni 7879 ambazo maombi yake yaliidhinishwa kupitia kikao cha Tume kilichofanyika tarehe 25 Septemba, 2018 kilicholenga kujadili taarifa za Kamati za Tume na utendaji kazi katika kipindi cha mwezi Mei hadi Septemba, 2018.

  Profesa Kikula ameyasema hayo leo tarehe 04 Oktoba, 2018 kupitia mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika katika Ofisi za Tume ya Madini zilizopo jijini Dodoma.

  Akielezea kuhusu maombi ya leseni za madini 7879 yaliyoidhinishwa katika kikao cha Tume, Profesa Kikula alieleza kuwa ni pamoja na Leseni za Utafutaji wa Madini (Prospecting License – (PL) 263; Leseni Kubwa (Special Mining License – (SML) 03;(ziliidhinishwa ili kupelekwa kwenye mamlaka husika ambayo ni Baraza la Mawaziri) Leseni za Uchimbaji wa Kati (Mining License – (ML) 14 pamoja na leseni 1 ya Sihia (Transfer) ya uchimbaji wa Kati.

  Aliendelea kufafanua kuwa, maombi leseni za uchimbaji wa kati 14 yaliyopitishwa kuwa ni pamoja na kampuni za Dangote Industries Limited kwa ajili ya uchimbaji wa madini ya chokaa katika eneo la Mtwara; Nazareth Mining Investment Co Limited kwa ajili ya uchimbaji wa madini ya kinywe (graphite) katika eneo la Ruangwa mkoani Lindi na kampuni ya Sunshine Mining (T) Limited kwa ajili ya uchimbaji wa madini dhahabu katika eneo la Chunya mkoani Mbeya.

  Aliendelea kutaja kampuni nyingine kuwa ni pamoja na Said Seif Abdallah kwa ajili ya uchimbaji wa madini ya ujenzi katika eneo la Masasi mkoani Mtwara; Off Route Technologies (T) Limited kwa ajili ya uchimbaji wa makaa ya mawe katika eneo la Ileje mkoani Mbeya; leseni yenye ubia kati ya Shabani Daud Ibrahim, Andrew Bollen, Dunstan M. Mongi na Vedastus Mtesigwa kwa ajili ya uchimbaji wa madini ya dhahabu katika mkoa wa Geita.

  Maombi mengine yaliyopitishwa ni pamoja na leseni yenye ubia kati ya Jumbo Limited, na Ally Mbarak Mohamed kwa ajili ya uchimbaji wa madini ya kinywe (graphite) katika eneo la Ruangwa mkoani Lindi, Jacana Resources (Tanzania) Limited kwa ajili ya uchimbaji wa mchanga bahari (mineral sand) katika eneo la Temeke lililopo jijini Dar es Salaam na P. B. Mining Company kwa ajili ya uchimbaji wa madini ya fedha, dhahabu, shaba, zinki na galena katika eneo la Chunya lililopo mkoani Mbeya.

  Profesa Kikula alisisitiza kuwa, kikao hicho pia kilipitisha ombi la kubadili umiliki kutoka kwa Mbarouk Saleh Mbarouk kwenda katika kampuni ya M. B. Mining (T) Limited kwa ajili ya uchimbaji wa madini ya ujenzi katika eneo la Morogoro.

  Profesa Kikula aliendelea kutaja maombi ya leseni nyingine zilizopitishwa katika kikao hicho kuwa ni pamoja na Leseni za Uchimbaji Mdogo (Primary Mining License – (PML) 6313; Leseni za Uchenjuaji wa Madini (Processing License) 08 na leseni za Biashara ya Madini ambapo leseni kubwa (Dealers License) ni 557; na leseni Ndogo (Broker’s License) 720

  Katika hatua nyingine Profesa Kikula alisema kuwa, Mipango ya Ushirikishwaji wa Utoaji wa Huduma na Bidhaa kwa Wazawa katika Miradi ya Madini (local content plan) 19 ilipitishwa kati ya mipango 26 iliyowasilishwa kutoka katika kampuni mbalimbali za utafutaji na uchimbaji wa kati na mkubwa wa madini.

  Alielekeza waombaji leseni za madini kuwasilisha mipango yao kwa wakati ili iweze kupitiwa na kamati husika na kuwezesha leseni kutolewa mapema. Pia aliwataka waombaji wote wa leseni za madini kufuatilia leseni zao kwenye Ofisi za Madini zilizopo mikoani walikoombea leseni zao na kusisitiza kuwa orodha ya leseni zilizoidhinishwa inapatikana katika tovuti ya Tume.

  Wakati huohuo Profesa Kikula alisema kuwa Tume ya Madini imejipanga katika kuhakikisha kila mtanzania ananufaika ipasavyo na rasilimali za madini nchini
  Aliongeza kuwa, Tume imeweka mikakati ya kuwasaidia wachimbaji wadogo wa madini kwa kuwatengea maeneo kwa ajili ya uchimbaji madini na kuwataka kuunda vikundi na kusajiliwa kupitia viongozi wao hivyo kuwezesha upatikanaji wa leseni za madini na kufanya shughuli zao pasipo kikwazo chochote.

  “Sisi kama Tume ya Madini tunatambua mchango mkubwa wa wachimbaji wadogo wa madini na ndio maana tumekuwa tukifanya ziara katika maeneo ya wachimbaji wadogo na kutatua changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na migogoro; tunataka wafanye kazi katika mazingira salama kabisa,” alisema Profesa Kikula.

  Naye Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya akielezea mchango wa Sheria Mpya ya Madini alisema kuwa tangu kuanza kwa utekelezaji wa sheria mpya iliyoweka ongezeko la kutoka asilimia nne hadi sita za mrabaha na tozo la asilimia moja la kodi ya ukaguzi wa madini, makusanyo yameongezeka kutoka shilingi bilioni 194 hadi shilingi bilioni 301 kwa mwaka likiwa ni ongezeko la asilimia 55.

  Pia, Mkurugenzi wa Leseni na TEHAMA kutoka Tume ya Madini, Torece Ngole akielezea mikakati ya Tume katika kukabiliana na changamoto ya migogoro kwenye uchimbaji wa madini inayosababishwa na wachimbaji wadogo kwa kuvamia maeneo yenye leseni kubwa, alisema kuwa Tume imeshaanza kutenga maeneo kwa ajili ya wachimbaji wadogo na kusisitiza kuwa mpaka sasa imeshatenga maeneo 74

  Alisisitiza kuwa Tume imekuwa ikiwaelimisha wachimbaji wadogo kuhusu sheria na kanuni za madini na kusisitiza kuunda vikundi ili waweze kupatiwa maeneo na leseni za uchimbaji madini.

  0 0

  Na Stella Kalinga, Simiyu

  Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu amefanya ziara mkoani Simiyu Oktoba 03, 2018 na kuzungumza na viongozi wa mkoa huo, ambapo ameeleza kuwa moja ya malengo ya ziara yake ni kufahamu Mipango na Fursa za Uwekezaji zilizopo mkoani Simiyu, ili aweze kuzungumza na wawekezaji nchini Kenya kuwekeza mkoani humo.

  Balozi Kazungu amesema nchi ya Kenya ndiyo inaongoza kuwekeza nchini Tanzania ukilinganishwa na nchi nyingine za Afrika ambapo hadi sasa imewekeza takribani dola za Kimarekani bilioni 1.6 hapa nchini.“ Nimekuja hapa ili tufahamiane vizuri, nijue mipangilio yenu, fursa za uwekezaji ziko wapi ili tuweze kuzungumzana wenzetu wakaja kuwekeza, Kenya ni nchi inayoongoza kwa kuwekeza nchini Tanzania, hadi sasa imewekeza takribani dola bilioni 1.6 ” alisema Balozi Kazungu.

  Aidha, ameomba ushirikiano kati ya Tanzania na Kenya uendelee kuimarishwa kwa lengo la kuzifanya nchi hizi kuwa shina la viwanda na uwekezaji na kuwa wanufaika wa soko la pamoja la Afrika hali itakayochangia kuimarisha uchumi wa nchi hizo.Pamoja na ushirikiano katika masuala ya uwekezaji na viwanda Balozi Kazungu amesisitiza masuala ya ujirani mwema, upendo na ushirikiano wa kindugu baina ya nchi hizo mbili.

  Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka amesema Serikali mkoani humo inakaribisha sekta binafsi na iko tayari kutoa ardhi bure kwa wawekezaji walio tayari kuwekeza Simiyu katika maeneo yanayojibu mahitaji ya mkoa na nchi kupitia malighafi zinazolishwa ndani ya mkoa na ndani ya nchi.

  “Kwa mtu aliye tayari kujenga kiwanda kinachojibu mahitaji yetu kama mkoa hasa kitakachutumia malighafi tulizonazo mfano atakayewekeza kwenye viwanda vya kusindika nyama, viwanda vya kutengeneza bidhaa za ngozi, pamba na yeyote atakayewekeza kwenye viwanda vyenye malighafi inayozalishwa hapa nchini, tutampa ardhi bure” alisema.

  Mtaka amemweleza Balozi Kazungu kuwa mkoa huo pia uko tayari kutoa ardhi bure kwa wawekezaji walio tayari kuwekeza kwenye ujenzi wa vyuo ikiwemo vya ufundi na utalii ili kuwajengea vijana ujuzi .

  Naye Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amesema mafanikio ya Mkoa huo yanayopelekea kufanya vitu vikaonekana ikiwa ni pamoja na kuwa na Mwongozo wa Uwekezaji ni ushirikiano uliopo kati ya viongozi, watendaji, wadau mbalimbali wa maendeleo ikiwepo Taasisi za Serikali na binafsi, sekta binafsi, madhehebu ya dini pamoja na wananchi.

  Mkurugenzi wa Kiwanda cha kuchambua Pamba cha Alliance Ginnery kilicjopo Bariadi, Bw. Boaz Ogola ambaye ni Mwekezaji kutoka nchini Kenya amemweleza Balozi kuwa Tanzania ni nchi yenye amani na mahali sahihi kwa uwekezaji, hivyo akatoa wito kwa Mhe. Balozi kuwaalika Wafanyabiashara kutoka Kenya kuja kuwekeza Simiyu na Tanzania kwa ujumla.
  Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) akimkabidhi Nakala ya Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Simiyu Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu, wakati wa ziara yake mkoani humo, Oktoba 03, 2018.
  Kutoka kulia Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini, Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka, Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu na Mkurugenzi wa Kiwanda cha kuchambua Pamba cha Alliance Ginnery kilichopo Bariadi, Bw. Boaz Ogola wakiteta jambo, wakati wa ziara ya Balozi huyo mkoani Simiyu, Oktoba 03, 2018.
  Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Simiyu , Mjini Bariadi wakati wa ziara yake mkoani humo, Oktoba 03, 2018.
  Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu ( wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa mkoa wa Simiyu mara baada ya kuhitimisha ziara yake mkoani Simiyu, Oktoba 03, 2018.

  Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka(kulia) , mara baada ya kuwasili Mjini Bariadi wakati wa ziara yake mkoani humo, Oktoba 03, 2018.

  Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka(kulia) akisalimiana na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu, mara baada ya kuwasili Mjini Bariadi wakati wa ziara yake mkoani Simiyu, Oktoba 03, 2018.

  Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu, akisalimiana na Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini mara baada ya kuwasili Mjini Bariadi wakati wa ziara yake mkoani Simiyu, Oktoba 03, 2018.

  0 0


  0 0  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Ubelgiji hapa nchini Peter Van Acker Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa wa Ubelgiji hapa nchini Peter Van Acker mara baada ya kupokea Hati zake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Norway hapa nchini Elisabeth Jacobsen Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Norway hapa nchini Elisabeth Jacobsen Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Balozi wa Norway hapa nchini Elisabeth Jacobsen kabla ya kuanza mazungumzo mara baada ya kupokea Hati zake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Norway hapa nchini Elisabeth Jacobsen Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Sweden hapa nchini Anders Sjoberg Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Sweden hapa nchini Anders Sjoberg mara baada ya kupokea Hati zake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Sweden hapa nchini Anders Sjoberg mara baada ya kupokea Hati zake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Palestina hapa nchini Hamdi Abuali Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Palestina hapa nchini Hamdi Abuali Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Palestina hapa nchini Hamdi Abuali mara baada ya kupokea Hati zake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Kuwait hapa nchini Mubarak Mohammad Alsehaijan mara baada ya kupokea Hati zake Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Kuwait hapa nchini Mubarak Mohammad Alsehaijan mara baada ya kupokea Hati zake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga mara baada ya kupokea Hati za Utambulisho kutoka kwa mabalozi wa nchi tano watakaowakilisha nchi zao hapa nchini, Ikulu jijini Dar es Salaam.

  0 0


  Na Ripota Wetu,Globu ya jamii.

  UONGOZI wa Shule ya Msingi Misray iliyopo wilayani Kondoa wameishukurua benki ya TPB kwa kuwasaidia kuwajengea vyumba viwili vya madarasa,ofisi za walimu pamoja na samani zake.

  Umesema msaada huo sasa utaondoa changamoto kubwa ambayo walimu na wanafunzi wa shuleni hapo walikuwa wanaupata ikiwemo ya kukatisha masomo pindi mvua inaponyesha.

  Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Misray Veronica Gabriel ametoa shukrani hizo mbele ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Ashatu Kijaji pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya TPB Dk.Edmund Mndolwa.

  Ambapo makabidhiano ya msaada huo yalifanyika shuleni hapo na mgeni rasmi alikuwa Dk.Kijaji ambaye ndiye aliyekabidhi kwa uongozi wa shule hiyo.Mwalimu Gabriel amesema kuwa wanatoa shukrani kwa uongozi wa benki hiyo na kuahidi msaada huo wa majengo watautunza pamoja na samani zote ambazo zimetolewa."Napenda kuwahakikishia uongozi wa Benki ya TPB kuwa huu msaada umesaidia kutatua tatizo la uhaba wa majengo duni yaliyooezekwa kwa nyasi na ilitulazimu kukatisha masomo pindi mvua inaponyesha.

  " Kwa kweli ilikuwa changamoto kubwa sana .Tunatoa rai kwa taasisi nyingine kutoa misaada kama hii kwa ajili ya kuondoa changamoto zilizopo,"amesema.Kwa uoande wake Dk.Mndolwa amesema wao kama taasisi ya fedha inayohudumia jamii wameguswa na matatizo hayo na ndio maana walipopokea naombi kutoka kwa uongozi wa shule hiyo wakaona ni vema wakasaidia.

  "Tumetoa msaada huu baada ya kushuhudia mazingira magumu ambayo watoto hawa walikuwa wanakabiliana nayo kutokana na kukosa majengo ya madara." Hawa watoto wetu sote na ni jukumu letu kama wazazi kuona umuhimu wa jambo hili la kuwasaidia kwani hawa watakuwa viongozi wetu wa baadae.Ujenzi umegharimu Sh.Milioni 63 ,"amesema Dk.Mndolwa.

  Kutokana na msaada huo shule hiyo imefanikiwa kutatua changamoto ya tatizo la madarasa,ofisi ya walimu na samani zake baada ya benki hiyo kusaidia.


  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Ashatu Kijaji akipiga makofi wakati wa uzinduzi wa jengo la darasa katika Shule ya Msingi Misray wilayani Kondoa.Majengo hayo yamejengwa na Benki ya TPB
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya TPB Dk.Edmund Mndolwa wa kwanza kulia pamoja na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Ashatu Kijaji anayefuata wakiwa pamoja na viongozi wa ngazi mbalimbali na walimu wakati wa kukabidhiwa kwa majengo mawili ya madarasa, ofisi na samani kwa shule ya msingi Misray.
  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Ashatu Kijaji akiwa pamoja na viongozi wa benki ya TPB na wanafunzi wa Shule ya Msingi Misray wilayani Kondoa baada ya kukabidhiwa msaada wa majengo mawili ya madarasa,ofisi za walimu na samani zake

  0 0

  Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi, akiweka sahihi kwenye kitabu cha wageni alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jijini Dar es Salaam, mapema leo tarehe 04/10/2018.
  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CGF) Thobias Andengenye (wa pili kushoto) akitoa maelezo ya utendaji kazi wa Jeshi hilo kwa Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam mapema leo tarehe 04/10/2018.
  Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi, akifuatilia kwa karibu maelezo aliyokuwa akiyatoa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji CGF Thobias Andengenye, alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam, mapema leo tarehe 04/10/2018.
  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CGF) Thobias Andengenye akisalimiana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi, alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam mapema leo tarehe 04/10/2018.
  Kamishna wa Operesheni Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CF) Billy Mwakatage akisalimiana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi, alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam mapema leo tarehe 04/10/2018.
  Picha ya Pamoja, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CGF) Thobias Andengenye (wa kwanza kushoto) akiwa na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi, pamoja na Kamishna wa Operesheni (CF) Billy Mwakatage (wa kwanza Kulia), mara baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo, Jijini Dar es Salaam mapema leo tarehe 04/10/2018. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)

  0 0

  MTANDAO wa Elimu Tanzania (TEN/MET) umetoa kauli na kulaani vitendo vya udanganyifu kwenye Shule za Msingi nchini, vilivyofanywa na baadhi ya  watendaji wa elimu hadi kusababisha Baraza la Mitihani Tanzania kufuta matokeo ya Darasa la Saba kwa baadhi ya shule. 

  Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania, Bi. Cathleen Sekwao alisema kitendo kilichofanywa na watendaji hao waliopewa dhamana ya kusimamia elimu ni sawa na kuhujumu juhudi kubwa za Serikali na wadau wengine wa elimu zinazofanyika kuinua kiwango cha elimu nchini. 

  Alisema kitendo cha wanafunzi hao kufutiwa matokeo ya mitihani kimewaathiri wanafunzi kisaikolojia na hisia na kuwapotezea uwezo wao wa kujiamini katika kufanya mitihani mingine, licha ya kwamba walioshirikishwa hawakuwa na uwezo wa kupinga wanachoelekezwa na walimu au viongozi katika jambo hilo. 

  “Ikumbukwe kuwa mtoto wa Darasa la Saba hana uwezo wa kupinga anachoelekezwa na viongozi au walimu wake hivyo huamini kila anachoambiwa afanye ni chema bila kujua madhara yake ya baadae. Ni dhahiri kuwa kitendo cha kufutiwa matokeo ya mitihani kimewaathiri watoto hao kisaikolojia na kihisia na hivyo kuwapotezea uwezo wao wa kujiamini katika kufanya mitihani mingine na safari yao ndefu ya kutimiza ndoto zao,” alisema Bi. Sekwao. 

  Alipongeza uamuzi uliofanywa na Serikali kupitia Baraza la Mitihani kuwafanya warudie mitihani ni jambo jema, inaonesha dhahiri kwamba kuna nia ya kuwapa fursa watoto hao. Pamoja na hayo alishauri muda uliotolewa wa kurudia mitihani hiyo ni mdogo kuwawezesha watoto hao kujiandaa na kujijenga kisaikolojia ili kuwa tayari kufanya mtihani mwingine. 

  “…Tunapendekeza kuwa angalau wapewe mwezi mmoja wa kujiandaa na kujengwa kisaikolojia…Mtandao unaipongeza Serikali kwa kuweza kubaini kitendo hiki cha hujuma na kuchukua hatua za awali. Ni matarajio yetu kuwa uchunguzi utakapokamilika wale wote waliohusika watachukuliwa hatua stahiki za kisheria na kinidhamu ili iwe fundisho kwa umma,” alisisitiza Bi. Sekwao.

  Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bi. Cathleen Sekwao (kushoto) akitoa kauli ya mtandao huo kupongeza Serikali kupitia Baraza la Mitihani kufuta matokeo ya darasa la saba kwa baadhi ya shule kwa ile kuonekana uwepo wa mchezo mchafu kuchezea mitihani hiyo. Kulia ni Meneja Programu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (Ten/Met), Bw.Nicodemus  Shauri Eatlawe. 

  Meneja Programu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (Ten/Met), Bw.Nicodemus  Shauri Eatlawe (kulia) akitoa ufafanuzi kwa wanahabari kuhusiana na kauli ya mtandao huo juu ya kufutwa kwa matokeo ya mitiani darasa la saba. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa REPSSI nchini Tanzania, Edwick Mapalala na Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bi. Cathleen Sekwao wakifuaatilia.

  Mkurugenzi wa REPSSI nchini Tanzania, Edwick Mapalala (kushoto) akizungumza kwenye mkutano huo wa TEN/MET na waandishi wa habari. Kulia ni Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bi. Cathleen Sekwao akifuatilia. 

  Afisa Programu wa TenMet, Bi. Alistidia Kamugisha (kushoto) akichangia hoja katika mkutano huo na wanahabari. Kulia ni Bi. Edwick Mapalala.

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Mtwara Evod Mmanda amemuagiza Afisa Ushirika wa Halmashauri hiyo Hamidu Ndagu kuwasilisha ofisnini kwake mara moja taarifa za maandishi juu wa tuhuma za viongozi wa Chama cha Msingi cha ushirika Madimba AMCOS kutuhumiwa kughushi Nyaraka na kufanikisha kufanya miamala ya kifedha katika taasisi za Kibenk bila kufuata taratibu za makubaliano na wajumbe wa ushirika huo.
  Mkuu huyo wa wilaya ametoa agizo hilo akizungumza na wanachama wa AMCOS hiyo ya Madimba baada ya kupata taarifa ya uwepo wa migogoro iliyo pelekea wanachama kuwafukuza viongozi na wajumbe wote wa bodi ya ushirika huo ambapo amemtaka Afisa ushirika kuwasilisha maelezo ya kina juu ya hatua alizo chukua kufuatilia shuala hilo kwa kuwa vyama vyote vya msingi vya ushirika vipo chini yake.

  Awali kabla ya mkuu wa wilaya kuchukua maamuzi ya kumuagiza afisa huyowa ushirika, Alitoa nafasi kwa Wanachama wa Ushirika kueleza sababu zilizo pelekea kuchukua maamuzi ya kuwafukuza kwenye uongozi viongozi wote wa Bodi ambapo wamedai chanzo ni mwenyekiti wa ushirika huo (Bashiru Lyakuti) kutokuwwa na maelezo ya kutosha kila wanapo mhoji juu wa taarifa za ushirika ambapo amekua akiwajibu kuwa hana uelewa wa masuala ya ushirika.
  Aidha wanachama hao wamedai kuwa sababu nyingine ni mwenyekiti huyo kumsimamisha kazi katibu Mkuu wa AMCOS hiyo kwa tuhuma za kuto kuwa na ushirikiano na viongozi wenzakee hadi kufikia kufanya miamala ya kifedha kwenye taasisi za kifedha bila kujadiliana na wajumbe wenzake(Kughushi), jambo ambalo limepingwa vikali na katibu mkuu huyo Ablari Rashidi.Kufuatia hali hiyo ya sintofahamu mkuu wa wilaya hiyo ya Mtwara Evod Mmanda akamuagiza Afisa ushirika wa halmashauri hiyo kuandaa Taarifa ya Kina kueleza mchakato mzima na hatua ambazo amesha zichukua kudhibiti suala hilo kuhakikisha halijitokezi tena katika msimu huu wa Kerosho ambao tayari umeanza.

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania Bw.Richard Mayongela akiongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC Bw. Geoffrey Mwambe walipotembelea uwanja wa ndege wa tatu wa Mwalimu Julius Nyerere kukagua maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo ambao unajengwa na Serikali kwa gharama ya zaidi ya shilingi Bilioni 560 za kitanzania, ujenzi huo ulianza Mwezi Juni 2013 unatarajia kukamilika mwezi mei 2019 (Picha na Grace Semfuko)
  Jengo jipya la tatu la Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere linavyoonekana kwa mbele likiwa limelamilika kwa asilimia 82 ya ujenzi wake, jengo hilo linagharimu zaidi ya shilingi bilioni 56 za kitanzania na linatarajia kukamilika ujenzi wake Mei 31 mwaka 2019
  Jengo jipya la tatu la uwanja wa mwalimu Julius Nyerere likiwa katika hatua mbalimbali za umaliziaji wa ujenzi wake, Jengo hilo la tatu linatumia zaidi ya shilingi Bilioni 560 za kitanzania na lilianza kujengwa Mwezi juni 2013 na kutarajiwa kumalizika mwezi Mei 2019


  Na Grace Semfuko-MAELEZO.

  Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), kinatambua kuwa miezi michache ijayo Serikali kwa kukamilisha ujenzi wa majengo na ufungaji wa mitambo ya kisasa kukidhi mahitaji ya teknolojia ya kimataifa, jengo la tatu (terminal 3) Uwanja wa Kimataifa Julius Nyerere( JNIA) ni ukurasa mpya wa fursa za kuongeza kasi ya uwekezaji hapa nchini.

  Mkurugenzi Mkuu wa TIC, Geoffrey Mwambe alitembelea eneo la Ujenzi na kupokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Anga Tanzania ( TAA), Richard Mayongela kwa ziara ya kutambua zaidi mapya ya jengo la tatu ili kumpa nafasi ya kujenga vishawishi kwa wawekezaji kuhusu manufaa ya chombo hicho kinachokamilika wakati tayari tatizo la foleni ya magari toka uwanjani huo kuingia jijini umeisha baada ya barabara la juu kukamilika katika maungo ya barabara za Mandela toka Bandarini na Nyerere itokayo JNIA. 

  TIC ni taasisi ya Serikali, imekuwa ikifanya juhudi za kufafanua kwa wawekezaji fursa zilizopo Tanzania kwa lengo la kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje nchi , na hivyo kukamilika kwa ujenzi wa uwanja huo na kuwa chombo chenye kila hitaji la abiria wa anga katika dunia ya sasa, utaongeza idadi ya wawekezaji kwa sababu ya huduma mpya hizo. “Huduma yetu usafiri wa anga inabadilika kabisa” amesema Mkurugenzi Mkuu TAA, Mayongela.

  Mayongela amesema kukamilika kwa uwanja huo mpya jengo la tatu kutaondoa kabisa msongamano wa abiria uliopo uwanja wa pili (Terminal 2) uliojengwa miaka 34 iliyopita, ambao kwa wakati huo ulilenga kuhudumia abiria Milioni 1.5 na sasa umezidiwa kwa kuhudumia abiria hadi milioni 2.5 kwa mwaka, kutokana na ongezeko la abiria nahatimaye kusababisha kuzidiwa kwa uwanja huo.

  Uamuzi wa kujenga kituo cha pili (Terminal 2) ulioazimiwa na serikali mwaka 1984 ulitokana na kuwepo kwa ongezeko la abiria kituo la kwanza (Terminal 1) kilichojengwa mwaka 1956, ambapo kituo kilikuwa na uwezo wa kuhudumia abiria laki tano tu, hatua iliyosababisha Serikali kujenga uwanja huo wa pili ambao nao kwa sasa umelemewa na abiria wengi.

  “Ujenzi wa uwanja huu ni mkombozi mkubwa kwetu Watanzania katika kuboresha Sekta ya anga,uwanja wa ndege tunaoutumia sasa ulijengwa mwaka 1984 ,ni miaka 34 mpaka sasa kwa hiyo utaona ni jinsi gani tulivyo bize kuhudumia abiria kwa idadi iliyolengwa mwaka huo kwa sasa watu tumeongezeka na hivyo Serikali imefanya jambo la msingi sana kujenga uwanja huu” Alisema Mkurugenzi Mkuu TAA. 

  Hata hivyo, vituo viwili vilivyopo, Uwanja huo JNIA bado vilikuwa na mapungufu ya mahitaji ya kisasa kwa dunia inayobadilika kila siku kiteknolojia, na Mkurugenzi Mkuu wa TIC ameelezwa huduma sasa zitakuwa na viwango vya kuhudumia kila aina ya makundi ya watu maarufu na kituo sasa kitaweza kupokea aina yoyote ya ndege pasipo kuhofia ubora ama ukubwa wake.

  Kadhalika, naye Bw. Mwambe amekiri na kufurahishwa na hatua za uboreshaji wa usafiri wa anga uliofikiwa na taifa na kuongeza kuwa kukamilika kwa uwanja huo kutasaidia kuongezeka kwa tija kwenye uwekezaji, kwani abiria na mizigo ya wawekezaji itahudumiwa kwa usafiri wa anga.

  “Usafiri wa anga una uhusiano mkubwa na kuimarisha uwekezaji Nchini,wawekezaji wengi wanaingia nchini kupitia usafiri wa anga,wanakuja na kuleta vifaa vya uwekezaji kwa kutumia usafiri wa aina mbalimbali ukiwepo usafiri huu wa anga,kwa hiyo kukamilika kwa uwanja huu kutatusaidia sisi kuimarisha sekta ya uwekezaji Nchini na ndio maana nimekuja kuangalia maendeleo yake” Alisema Bw.Geoffrey Mwambe Mkurugenzi Mtendaji wa TIC.

  “Abiria wa kigeni akitua Tanzania kitu cha kwanza atakachokutana nacho ni Sura ya Nchi ambayo inatambulishwa na uwanja wa ndege mzuri, sisi Tanzania Tupo Vizuri! Napenda kuishukuru Serikali ya awamu ya tano ya Rais Magufuli kwa kuimarisha miundombinu, tumeona hivi karibuni Rais akizindua barabara ya juu ya Mfugale,tunaona kasi ya ujenzi wa Reli ya Standard Gauge, Ujenzi wa uwanja huu na mengineyo mengi,kwetu sisi TIC tumefarijika kwani wawekezaji sasa watapata urahisi wa usafirishaji” Alisema Mwambe, Mkurugenzi Mtendaji wa TIC.

  Jengo hilo jipya la tatu la uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, litahusika na ndege za kimataifa tu na litahudumia Abiria milioni 6 kwa mwaka, na kuwa na uwezo wa kuhudumia abiria hata 2,800 kwa saa kwa wanaoingia na kutoka, na pia utahudumia ndege kubwa 19 na Ndege ndogo 11 zinazoingia na kutoka Nchini kwa wakati mmoja.

  Ujenzi wa Jengo la tatu (Terminal 3) JNIA ulioanza Juni, 2013 na utakaogharimu jumla ya Shilingi Bilioni 560 unakabidhiwa rasmi mamlaka husika tayari kwa kuutumia Mei, 2019 ukiwa katika viwango vyote vya kimataifa na kwa sasa wajenzi wanasema kazi ilyosalia ni ndogo ya asilimia 17.

  0 0

  NA MWAMVUA MWINYI, PWANI 

  KAMANDA wa polisi mkoani Pwani (ACP) Wankyo Nyigesa ameweka bayana, askari wa usalama barabarani hawataona muhali kuchukua hatua dhidi ya mabasi ya abiria yatakayojaza abiria pamoja na yanayokalisha abiria waliozidi kwenye ndoo za lita 20. 

  Aidha ameyaasa ,magari ya watoto wa shule mengi ni machakavu hivyo ameelekeza wayapeleke yakaguliwe kabla ya kubeba wanafunzi . 

  Akitoa rai hiyo kwa waandishi wa habari, Nyigesa alisema ,haiwezekani madereva wakakiuka sheria za usalama barabarani kwa makusudi wakitegemea kutoa faini bali wanachotakiwa ni kufuata sheria zilizopo. 

  Aliwataka ,abiria na jamii kutoa ushirikiano kwa askari hao kwa kutoa taarifa ama kuyafichua magari ya abiria yanayojaza abiria kupita kiasi ili wayachukulie hatua ikiwemo kupigwa faini. 

  Nyigesa alieleza, magari ya watoto wa shule mengi ni machakavu hivyo ameelekeza wayapeleke yakaguliwe kabla ya kubeba wanafunzi . Aliwataka, waendeshaji wa vyombo vya moto kutii sheria, na kwamba magari yao yatakaguliwa yawapo ndani ya mkoa huo. 

  “Magari ya watoto yaliyo mengi hayana mikanda sasa ni jukumu lao kujikaguwa kabla hawajakaguliwa na kukamatwa , “Hakuna polisi atakayemuonea aya dereva wala hatutaona muhali katika suala hili la kudhibiti ajali”alisisitiza Nyigesa. 

  Kamanda huyo alieleza, kila mmoja atii sheria bila kushurutishwa

  Kamanda wa polisi mkoani Pwani (ACP) Wankyo Nyigesa, akizungumza na wanahabari (hawapo pichani)

  0 0


  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa , MNEC Theresia Mtewele aliyeshika Ilani ya chama cha mapinduzi akiwa sambamba na diwani wa kata ya kitwiru Baraka Kimata ,MNEC Mussa Mwakitinya na mkurugenzi wa TAEDO Kenani Kihongosi ambaye pia ni mwenyekiti wa vijana wa ccm mkoa wa Iringa (UVCCM) akielezea jinsi ilani ya CCM inayotekelezwa kwa kutoa elimu mbalimbali ikiwapo elimu ya wajasiliamalia ambayo ilitolewa siku hiyo katika kata ya kitwiru kwa wananchi wote waliojitkeza Kutoka kusho ni mkurugenzi wa TAEDO Kenani Kihongosi ambaye pia ni mwenyekiti wa vijana wa ccm mkoa wa Iringa (UVCCM),diwani wa kata ya kitwiru Baraka Kimata,Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa , MNEC Theresia Mtewele aliyeshika Ilani ya chama cha mapinduzi akiwa sambamba na ,MNEC Mussa Mwakitinya na diwani wa kata ya nduli Bashir Mtove wote hao walihudhuria utoa elimu wa wajasiliamali wa kata ya Kitwiru


  NA FREDY MGUNDA,IRINGA.


  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Taifa anayewakilisha vijana, MNEC Theresia Mtewele, amewataka wajasiriamali wa mkoani Iringa kuwa na ubunifu kwenye biashara zao,kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha za kibiashara ili kukuza mitaji yao pamoja na kujiunga katika vikundi ili waweze kupatiwa mikopo itakayowasaidia kujikwamua kiuchumi.

  Akizungumza wakati wa ufunguaji wa mafunzo ya ujasirilimali yaliyoratibiwa na Diwani wa Kata ya kitwitu, Baraka Kimata na kutolewa na taasisi ya TAEDO, MNEC Mtewele alisema wajasariliamali wengi wamekuwa hawakopesheki kwa sababu hawajajiunga katika vikundi.

  “Ili kuendana na sera ya Serikali ya viwanda wajasiriliamali hawana budi kujiunga katika vikundi vidogo ili kupata mikopo itakayowasaidia kuanzisha viwanda vidogo jambo ambalo litawasaidia kuongeza kipato na ajira kwa watu wengine,” amesema.

  MNEC Mtewele aliwataka wajasiriamali wa Iringa kuwa wabunifu katika biashara zao ili kuweza kufanikiwa zaidi “ili mjasiriliamali aweze kufanikiwa lazima awe na nidhamu na fedha anayopata na si kuitumia hovyo kwani itasababisha kuyumba kwa biashara na hatimaye kufilisika”

  Kwa upande wake Diwani Kimatha, alisema aliamua kutoa mafunzo hayo bure kwa wananchi wake ili kujikwamua kiuchumi na kujijengea ajira kuliko kusubiri kuajiriwa.Kimata alisema lengo la kufanya hivyo ni kuwakwamua wananchi wake kiuchumi ikiwa pamoja na kuunga mkono jitihada za Mh.Rais John Pombe Magufuli juu ya Tanzania ya viwanda huku akiwashauri viongozi wenzie kutumia nafasi za uongozi kwa kuwasaidia wanaowaongoza.

  Nao baadhi ya wananchi wa kata ya kitwiru mkoa wa Iringa wamemshukuru diwani wa kata ya Kitwiru Baraka Kimata kwa kuwasaidia kupata mafunzo ya ujasiriamali, huku wakiahidi kuunga mkono sera ya Tanzania ya viwanda kwa kufungua viwanda vidogo vidogo mara baada ya mafunzo hayo .

  Hayo yamesemwa na baadhi ya wananchi wa kata ya kitwiru katika semina ya mafunzo ya ujasiriamali inayolenga ufugaji wa kuku na utengenezaji wa bidhaa mbalimbali , ambapo wamemshukuru diwani wa kata huyo kwa kitendo cha kugharamia mafunzo hayo kwao ,huku wakiahidi kuunga mkono sera ya Tanzania ya viwanda mara baada ya kumaliza mafunzo hayo.

  0 0  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama eneo lililoandaliwa kwa ajili ya ujenzi wa Mradi wa Kuzalisha Umeme katika Maporomoko ya Mto Rufiji- Stieglers Gorge wakati alipotembelea eneo hilo Oktoba 4, 2018. Kushoto kwake ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani. 
  Eneo litakapojengwa tuta la kukinga maji katika Mradi wa Kuzalisha Umeme  kwenye Maporomoko ya Mto Rufiji- Stieglers Gorge ambalo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alilitembelea, Oktoba 4, 2018.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa tawi la reli litakalounganisha Stesheni ya Fuga katika reli ya TAZARA na eneo utakapojengwa Mradi wa Umeme wa Moporomoko ya Mto Rufiji – Stieglers Gorge wakati alipotembelea Stesheni hiyo, Oktoba 4, 2018. Kushoto ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani na kushoto kwa Waziri Mkuu ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kanda ya Tanzania wa TAZARA, Fuad Abdallah.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka wa Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kushoto) kuhusu ujenzi wa tawi la reli litakalounganisha Stesheni ya Fuga katika reli ya TAZARA na eneo utakapojengwa Mradi wa Umeme wa Maporomoko ya Mto Rufiji – Stieglers Gorge wakati alipotembelea eno hilo Oktoba 4, 2018. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kanda ya Tanzania wa TAZARA, Fuad Abdallah. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiksalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo wakati alipowasili kwenye eneo utakapojengwa Mradi wa Umeme katika Maporomoko ya Mto Rufiji – Stieglers Gorge, Oktoba 4, 2018. Kulia ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani na wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Stephen Kebwe. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kutembelea eneo la ujenzi wa Mradi wa Umeme wa Moporomoko ya Mto Rufiji – Stieglers Gorge, Oktoba 4, 2018.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kanda ya Tanzania wa TAZARA, Fuad Abdallah wakati alipotembelea Stesheni ya TAZARA ya Fuga kukagua ujenzi wa tawi la reli hiyo litalounganisha steheni hiyo na eneo utakapojengwa Mradi wa Umeme wa Maporomoko ya mto Rufiji – Stieglers Gorge, Oktoba 4, 2018.  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema uamuzi wa Serikali ya awamu ya tano wa kujenga mradi wa kuzalisha umeme kwenye maporomoko ya mto Rufiji, Stiegler’s Gorge utasaidia sana kudhibiti uharibifu wa mazingira nchini.

  Akizungumza baada ya kutembelea eneo utakapojengwa mradi huo, leo (Alhamisi, Oktoba 4, 2018), Waziri Mkuu amesema umeme utakaotokana na maji, utazalishwa kwa gharama nafuu na utakuwa wa uhakika zaidi.

  Amesema kwa vile umeme utakaozalishwa katika mradi wa Stiegler’s Gorge utakuwa wa bei nafuu na hivyo kuwa rafiki kwa wananchi wa kipato cha chini, utatumika kama nishati mbadala kwa kuni na mkaa  ambao umechangia sana kwenye uharibifu wa mazingira hasa ukataji miti.

  Waziri Mkuu Majaliwa amewaomba viongozi wa Serikali na vyama vya siasa wawaelimishe Watanzania kuwa mradi wa Stiegler’s Gorge una faida kubwa kwa Taifa kiuchumi na hauna athari za mazingira na badala yake utayaboresha.

  Amewahakikishia Watanzania kuwa mradi huo utajengwa na utakamilika katika muda uliokusudiwa ambao ni miezi 36 kuanzia siku mkandarasi atakapokabidhiwa kazi hiyo.

  Akizungumzia usalama katika eneo la mradi, Waziri Mkuu amesema viongozi wa mikoa ya Morogoro na Pwani wahakikishe kwamba wanaweka ulinzi wa kutosha kuanzia sasa na wakati  ujenzi utakapoanza ili kuzuia hujuma  na vitendo vya wizi na udokozi vinavyoweza kuvuruga kasi ya ujenzi wa mradi.

  Amesema vifaa vitakavyoletwa na mkadarasi lazima vilindwe na wajenzi watakaoshiriki katika ujenzi wa mradi wahakikishiwe usalama wao na mali zao.

  Amewataka wananchi pia washiriki katika ulinzi kwa kutoa taarifa  kwa vyombo vya dola kuhusu watu wenye mienendo inayoweza kuzorotesha ujenzi wa mradi huo kwani jukumu la ulinzi si la polisi peke yao.

  Kuhusu ajira kwa vijana wanaotoka katika maeneo yanayozunguka mradi, Waziri Mkuu amesema utaratibu utawekwa ili vijana wenye sifa wapewe nafasi ya kushiriki kwenye usaili na ikibidi watafanyiwa mchujo kwenye maeneo yatakayofikiwa na wengi. 

  Aliwaasa wote watakaobahatika kupata ajira ya kushiriki katika ujenzi wa mradi huo wawe waadilifu na wachapakazi ili kulinda heshima ya vijana wa Kitanzania na kuwashawishi wajenzi wa mradi kuajiri vijana wengine zaidi.

  Kuhusu Wizara ambazo zinaguswa na maandalizi ya ujenzi wa miundombinu inayohitajika katika ujenzi wa mradi wa Stiegler’s Gorge, Waziri Mkuu ameagiza wizara hizo zishirikiane ili kuhakikisha kwamba kila Wizara inatimiza majukumu iliyopangiwa kwa wakati.

  Wizara ambazo tayari zimeanza kuweka miundombinu wezeshi kwa mradi huo ni pamoja na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inayosimamia ujenzi wa barabara na tawi la reli itakayounganisha eneo la mradi na stesheni ya  Fuga katika reli ya TAZARA kazi ambayo imeanza na Waziri Mkuu wenyewe aliikagua.

  Wizara ya maji nayo tayari imetimiza jukumu lake la kupeka maji katika eneo la mradi wakati wizara ya nishati imepeleka umeme. Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja na Wizara ya Kilimo nazo zipo kwenye eneo la mradi kutimiza majukumu yote yanayozigusa.

  Awali, Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani aliishukuru Serikali kwa kukubali kutoa fedha ambazo zimesaidia sana katika ujenzi wa miundombinu ya maandalizi ya ujenzi wa mradi.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  ALHAMISI, OKTOBA 04, 2018.

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Golobu ya Ja Jamii
  NDOA  za utotoni zimeendelea kuwa kikwazo kwa maendeleo ya mtoto wa kike ambapo takiwmu za hali ya watu na afya nchini kwa mwaka 2015/2016 zinaonyesha asilimia 36 ya wanawake umri wa  miaka 25-49 wamepata watoto kabla ya kufikisha umri wa miaka 18.
  Hayo aliyasema  Mchumi na Mratibu wa Mpango kazi wa Kitaifa wa kutokomeza Vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake na watoto kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Seto Ojwando katika mdahalo wa Wadau uliofanyika katika Chuo cha Ustawi Jamii jijini Dar es Salaam.
  Amesema tafiti za afya na uzazi na viashiria vya malaria  TDHS 2015/2016  zinaonyesha kuwa mwanamke mmoja kati ya 10 wenye umri wa miaka 15 hadi 49 wamekeketwa  huku mikoa ambayo inaongoza katika ukeketaji huo ni Manyara  asilimia 58, Dodoma asilimia 47, Arusha 41, Mara asilimia 32 pamoja na Singida asilimia 41.
  Ojwando amesema katika tafiti hiyo ya TDHS ya 2015, 2016 Mikoa  inayoongoza kwa mimba za utotoni ni Katavi asilimia 45,Tabora asilimia 43, Dodoma asilimia 39, Mara asilimia 37 pamoja na Singida asilimia 34.
  Amesema kuwa nia ya kukuatana na wadau pamoja na wasomi katika Chuo cha ustawi wa jamii ni sehemu ya utekelezaji wa mapango kazi wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto  na mpango wa vietndo vya ukatili dhidi ya watoto ulianza 2017  ikiwa ni lengo kupunguza vitendo vya aina zote ukatili dhidi ya mwanamke na watoto kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2022.
  Nae Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii Dkt.Zena Mabeyo amesema kuwa kama wazalishaji wa wataalam wanawajibu kutoa rasilimali watu  itakayotumika kwa ajili ya kustawisha jamii katika kuondokana na mimba za utotoni, ukeketaji pamoja na vitendo vya aina yeyote vya ukatili.
  Amesema kuwa serikali imekuwa mstari wa mbele wa kupigania masilahi ya watoto wa kike hivyo jamii inahitaji kuchukua hatua katika kuwalinda watoto wa kike kufikia malengo yao.
  Mtoa mada katika mdahalo huo Mhadhili wa Chuo cha Ustawi wa Jamii Leah Omary  amesema kuwa watoto wa kike wanahitaji kupewa ulinzi pamoja na wazazi kukaa na familia zao.
  Maazimio ya mdahalo huo yatapelewa katika kilele cha maashimisho ya siku ya kimataifa ta ya mtoto wa kike yatakyofanyika Oktoba 11 jijini Dar es Salaam.  
   Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii Dkt. Zena Mabeyo akifungua madahalo wa kitaifa wa kutokomeza ukeketaji ,Mimba na Ndoa za Utotoni uliofanyika katika Chuo hicho jijini Dar es Salaam.
   Mhadhili wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Leah Omary akitoa mada katika madahalo wa kitaifa wa kutokomeza ukeketaji ,Mimba na Ndoa za Utotoni uliofanyika katika Chuo hicho jijini Dar es Salaam.
   Mchumi na Mratibu wa Mpango kazi wa Kitaifa wa kutokomeza Vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake na watoto kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Seto Ojwando akizungumza katika mdahalo wa kuhusiana na seriakli kuchukua hatua mimba za utotoni, ndoa z utotoni pamoja na ukeketaji
   Mhadhili wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Zachayo Shigongo akitoa maada kusiana na malezi ya watoto katika madahalo wa kitaifa wa kutokomeza ukeketaji ,Mimba na Ndoa za Utotoni uliofanyika katika Chuo hicho jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wadau katika mdahalo huo wa kujadili na kutokomeza ukeketaji ,Mimba na Ndoa za Utotoni uliofanyika katika Chuo hicho jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Majaji wa shindano la Fiesta Super Nyota 2018 mkoani Rukwa, wakiongozwa na Jaji Mkuu, Adam Mchomvu (mwenye miwani), wakijitambulisha mbele ya washiriki na wageni mbalimbali waliofika kushuhudia kupatikana wa nyota wapya wa muziki wa kizazi kipya. wengine toka kulia ni Afisa Michezo Manispaa ya Rukwa, Adam Evarist, Afisa Utamaduni wa Manispaa ya Rukwa, Charles Kiheka na kushoto ni The Baton A ambaye alikuwa mshindi wa Tigo Fiesta Supa Nyota mwaka jana.
  Washiriki wakiwa kwenye mchujo wa mwisho uliotoa washindi wawili ambao watapanda kwenye jukwaa la Tigo Fiesta kesho uwanja wa Nelson Mandela Sumbawanga na kupata mshindi mmoja.
  Moja kati ya washindi wawili wa Tigo Fiesta Supa Nyota mkoani Rukwa, Robby Gitaa akionyesha uwezo wake wa kuimba na kupiga gitaa kwenye shindano la kutafuta vijana wenye vipaji vya muziki mkoani humo leo.
  Moja kati ya washindi wawili wa Tigo Fiesta Supa Nyota mkoani Rukwa, Tigani Tozi akionyesha uwezo wake wa staili ya kufokafoka kwenye shindano la kutafuta vijana wenye vipaji vya muziki mkoani humo leo.

  0 0

   The University of Dar es Salaam, College of Information and Communication Technology, Head of Computer Science and Engineering Department, Dr. Honest Kimaro (2ndR) speaks during a ceremony to award full PEPFAR scholarships for the two-year Master of Science in Data Science to UDSM-CoICT students. With him are Ms. Meredith C. Falion, PEPFAR Political and Private Sector Associate (Right), Mr. Stephen Chacha, The Data Collaborative for Local Impact (DCLI) Country Program Coordinator (2ndL) and Tanzania Data Lab (dLab) Director of Research and Innovation, Mr. Agapiti Manday (1stL).
   Mr. Stephen Chacha, The Data Collaborative for Local Impact (DCLI) Country Program Coordinator (2ndL) speaks during a ceremony to award full PEPFAR scholarships for the two-year Master of Science in Data Science to UDSM-CoICT students. With him are Ms. Meredith C. Falion, PEPFAR Political and Private Sector Associate (Right), the University of Dar es Salaam, College of Information and Communication Technology, Head of Computer Science and Engineering Department, Dr. Honest Kimaro (2ndR) and Tanzania Data Lab (dLab) Director of Research and Innovation, Mr. Agapiti Manday (1stL).
  Ms. Meredith C. Falion, PEPFAR Political and Private Sector Associate (Right), The University of Dar es Salaam, College of Information and Communication Technology, Head of Computer Science and Engineering Department, Dr. Honest Kimaro (2ndR),  Mr. Stephen Chacha, The Data Collaborative for Local Impact (DCLI) Country Program Coordinator (2ndL) and  the Tanzania Data Lab (dLab) Director of Research and Innovation, Mr. Agapiti Manday (1stL) in a group photo with PEPFAR Scholars during a ceremony to award them with full PEPFAR scholarships for the two-year Master of Science in Data Science at UDSM-CoICT.

  0 0
  0 0

  Kwa masikitiko makubwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo anatangaza kifo Cha Dada yake mpendwa Bi Mwajuma Gambo kilichotokea Jana tarehe 04/10/2018 kwenye Hospital ya Muhimbili  jijini Dar Es Salaam. 

  Mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi (kesho) tarehe 06/10/2018 Saa 6 Mchana kwenye makaburi ya MCHIKICHINI Ilala Dar Es Salaam. 

  Msiba upo nyumbani kwao Kariakoo mtaa wa Mheza Karibu na Shule ya Sekondari ya Benjamini Mkapa. 

  Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi-AMEN
  Bi Mwajuma Gambo enzi za uhai wake.

  0 0

  Katibu Tawala wa mkoa wa Rukwa, Bernard Makali(katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo kuelekea Tamasha la Tigo Fiesta litakalofanyika siku ya Ijumaa mkoani humo, Wengine kwenye picha ni Mkurugenzi wa Tigo Nyanda za Juu Kusini , Henry Kinabo (kushoto) na Msanii wa Bongo Fleva Nandy.
  Mkurugenzi wa Tigo Nyanda za Juu Kusini , Henry Kinabo akizungumza na waandishi wa habari leo kuelekea Tamasha la Tigo Fiesta litakalofanyika siku ya Ijumaa uwanja wa Nelson Mandela wilaya Sumbawanga. Wengine kwenye picha kulia  ni Katibu Tawala wa mkoa wa Rukwa, Bernard Makali, Msanii  Msanii wa Bongo Fleva Nandy na Mwisho kulia ni Katibu Tawala Msaidizi Idara ya Utawala, Winnie Kijazi  na kushoto Msanii, Nikki wa Pili
  Katibu Tawala wa mkoa wa Rukwa, Bernard Makali(katikati)akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wwafanyakazi wa Tigo na wasnii wataopanda leo kwenye jukwaa la Tigo Fiesta uwanja wa Nelson Mandela.
   
   


  SUMBAWANGA KUONJA VIBE KAMA LOTE LA TIGO FIESTA 2018

  Onesho hilo latua Sumbawanga an ofa tatu za kusisimua

  Sumbawanga, Oktoba 5, 2018 – Baada ya mafanikio ya ufunguzi wa msimu wa Tigo Fiesta 2018- Vibe Kama Lote mjini Morogoro, sasa ni zamu ya Sumbawanga na viunga vyake kufurahia vibe lote katika msimu mkubwa zaidi wa muziki na utamaduni nchini uliowasili mjini hapo na promosheni tatu kabambe, fursa za kibiashara kwa wakaazi wote pamoja na ahadi ya vibes moto moto kutoka kwa 100% wasanii wa nyumbani.

  Pazia la onesho hilo litakalofanyika katika viwanja vya Mandela mjini Sumbawanga litafunguliwa na wasaanii wanaochiopuka waliofanya vizuri katika shindano la kusaka vipaji la Tigo Fiesta 2018 – Supa Nyota. Wasanii wa kike Nandy na Maua Sama pia watakuwepo kukongo nyoyo za mashabiki, wakati wasanii wa hip-hop Fid Q, Bil Nas na kundi la Weusi linaloundwa na Joh Makini, Niki wa Pili pamoja na G-Nako nao watafunika onesho hilo. Mashabiki wa muziki pia wategemee kupata vibes za uhakika kutoka kwa wasanii wa bongo fleva Chegge, Jux, Whozu, Nedy Music, Barnaba na Marioo..

  Mdhamini mkuu wa msimu huu, kampuni ya Tigo imewakumbusha mashabiki wote wa muziki mjini Sumbawanga kufurahia promosheni zake tatu murwa katika msimu hii wa vibes. ‘Data Kam Lote inawapa wateja hadi mara mbili ya vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*0#. Hii itawawezesha wateja wa Tigo kufurahia msimu huu wa vibes kupitia mtandao wa kasi ya juu zaidi wa Tigo 4G+,’ Mkurugenzi wa Tigo, Kanda ya Kusini Henry Kinabo alisema.

  Tigo pia inatoa punguzo kubwa la bei kwa tiketi za tamasha la Tigo Fiesta 2018 zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa Masterpass QR. Kwa Sumbawanga, tiketi zitakazonunuliwa kwa mfumo wa Tigo Pesa Masterpass QR zitagharimu TSH 5,000 pekee badala ya TSH 7,000 kwa watakaonunua kwa pesa taslim, Wateja wanapaswa kupiga *150*01# na kuchagua 5 (lipia huduma) kisha kuchagua namba 2 (lipa Masterpass QR) na kutuma kiasi husika kwenda namba ya Tigo Fiesta 78888888.

  Wateja wa Tigo pia watapata faida zaidi kupitia shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo Trivia linalotoa zawadi za kila siku za TSH 100,000, zawadi za kila wiki za TSH 1 milioni, simu janja za mkononi zenye thamani ya TSH 500,000 kila moja, pamoja na donge nono la TSH milioni 10 kwa mshindi wa jumla. Kushiriki wateja wanapaswa kutuma neno MUZIKI kwenda 15571 au kutembelea tovuti ya http://tigofiesta.co.tz na kuchagua Trivia.

  Katibu Tawala mkoa wa Rukwa, Bernard Makali alielezea shukrani zake kwa waandaji kutoa fursa ya kuuitangaza wilaya hiyo akisema kuwa itaibua fursa nyingi zaidi za biashara na kujiongezea kipato kwa wakaazi. 

  Huu ni mwaka wa 17 wa tamasha la muziki na kitamaduni la Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote ambapo mwaka huu linashirikisha 100% wasanii wa nyumbani watakaozuru mikoa 15 ya nchi ikiwemo; Morogoro, Sumbawanga, Iringa, Singida, Songea, Mtwara, Moshi, Tanga, Muleba, Kahama, Mwanza, Musoma, Arusha na Dodoma, huku kilele kikifanyika Dar es Salaam.

older | 1 | .... | 1688 | 1689 | (Page 1690) | 1691 | 1692 | .... | 1897 | newer