Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

WAHAMIAJI HARAMU 298 WAKAMATWA MKOANI TANGA

$
0
0

WAHAMIAJI haramu 298 wamekamatwa mkoani Tanga kutoka nchi mbalimbali ambao waliingia nchini kinyume cha kisheria na hivyo kujikuta mikononi mwa vyombo vya dola.

Hayo yalisemwa na Afisa Uhamiaji Mkoani Tanga Ali Dady wakati akizungumza na mtandao huo ofisini kwake kuhusu wahamiaji haramu waliokamatwa kwa kipindi cha kuanza Januari hadi Agosti mwaka huu.

Alisema mwezi January walikamatwa wahamiaji haramu 49 ambao walikuwa wametoka kwenye nchi mbalimbali ikiwemo Somalia,Kenya,Tanzania na China huku kwa mwezi February wakimatawa 77 kutoka nchi za Somalia,Ethiopia, Burundi,Uganda,Kenya na Paskistani.

Afisa Uhamiaji huyo alisema katika mwezi Machi na Aprili idadi yao uingiaji wa wahamiaji hao ulishuka ambapo Machi walikamatwa 18 na Aprili walikamatwa 26 huku mwezi Mei wimbi la ukamataji wao liliongezeka.

“Kwa mwezi Mei walikamatwa wahamiaji haramu 94 kutoka kwenye nchi za Ethiopia, Congo, China na Somalia huku mwezi June na Julai wakikamatwa wahamiaji 12 “Alisema.

Hata hivyo alieleza kwamba katika mwezi Agosti mwaka huu walimatwa wahamiaji haramu 22 kutoka nchi za Ethiopia,Kenya,Somalia na Tanzania ambao wamekuwa mawakala wa wahamiaji hao.

Alisema idadi ya wahamiaji kuingia mkoani Tanga imekuwa ikipungua kila wakati kutokana na kuwepo kwa ufuatiliaji sambamba na kuwekwa vizuizi kwenye maeneo mbalimbali

WATEJA WA TBL KUJISHINDIA MAGARI KUPITIA PROMOSHENI MPYA YA 'TBL KUMENOGA, TUKUTANE BAA'

$
0
0
Meneja wa Udhamini na Mawasiliano ya Wateja wa TBL,David Tarimo (kushoto) na Meneja wa Biashara na ukuzaji wa Masoko wa TB Group na ABInBev kanda ya Afrika Mashariki, Edith Bebwa, wakikata utepe wakati wa kuzindua promosheni ya 'TBL kumenoga, Tukutana baa wengine pichani ni mameneja wa chapa za vinywaji vya TBL.
Mameneja kutoka kitendo cha Masoko wa TBL wakipeperusha bendera wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo.
Meneja wa Biashara na ukuzaji wa Masoko wa TB Group na ABInBev kanda ya Afrika Mashariki, Edith Bebwa,akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi huo.
Meneja wa Udhamini na Mawasiliano ya Wateja wa TBL,David Tarimo akifafanua jambo wakati wa uzinduzi,wengine pichani ni Mameneja wa chapa za vinywaji vya TBL

RC MAKONDA AKUTANA NA WATENDAJI TPSF, WAWEKA MIKAKATI MADHUBUTI YA KUWASAIDIA WAFANYABIASHARA NA WAWEKEZAJI

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo ametembelea ofisi za Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania TPSF na kufanya mazungumzo ya kutafuta namna bora ya kuweka mazingira bora ya kibiashara ilikuondoa kero zinazowakabili wawekezaji na wafanyabiashara jijini humo.

Miongoni mwa mambo waliyoridhia kushirikiana ni pamoja na utoaji wa elimu ya biashara, usimamizi wa fedha pamoja na namna bora ya kutumia fursa ya 10% za mkopo zinazotolewa na serikali kwaajili ya vijana, Wanawake na walemavu ili fedha hizo ziwe na tija.

Aidha RC Makonda amezungumza ushiriki wa TPSF katika ziara ya Rais Dkt. John Magufuli jijini Dar es salaam ambayo tunaamini itakuwa fursa kubwa kwa sekta zote ikiwemo Biashara, uchumi, afya, elimu, miundombinu na maji ambapo amewahimiza kuitumia vizuri ziara hiyo ili kufikia ndoto ya Dar es salaam kuwa jiji la kibiashara.

Pamoja na hayo RC Makonda ameelezea mpango wa kuweka kitengo cha uwekezaji (one stop center) itakayohusisha watendaji kutoka taasisi za TIC, TRA, TBS, BRELA, Uhamiaji na wadau wote wanaohusika na biashara ilikuondokana na ukiritimba uliokuwa ukipelekea mianya ya rushwa kwa wawekezaji na mwisho wa siku wawekezaji kukata tamaa ya kuwekeza Dar es salaam.

Kwa upande wake mkurugenzi wa taasisi ya sekta binafsi Tanzania TPSF Bwana Godfrey Simbeye amemuahidi ushirikiano wa kutosha kwa RC Makonda katika masuala mbalimbali yanayolenga kuliboresha jiji la Dar es salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo ametembelea ofisi za Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania TPSF na kufanya mazungumzo ya kutafuta namna bora ya kuweka mazingira bora ya kibiashara ili kuondoa kero  Mkurugenzi wa taasisi ya sekta binafsi Tanzania TPSF Bwana Godfrey Simbeye
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akisalimiana na Mkurugenzi wa taasisi ya sekta binafsi Tanzania TPSF Bwana Godfrey Simbeye
alipowasili leo na kutembelea ofisi za Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania TPSF na kufanya mazungumzo ya kutafuta namna bora ya kuweka mazingira bora ya kibiashara ili kuondoa kero

MAJALIWA AHUTUBIA KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 25 YA MTANDAO WA VIKUNDI VYA WAKULIMA – MVIWATA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia katika Maadhimisho ya Miaka 25 ya Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, Oktoba 3, 2018.
 
Baadhi ya washiriki wa Maadhimisho ya Miaka 25 ya Mtandao wa Vikundi vya Wakulima (MVIWATA) wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, Oktoba 3, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Uswiss nchini, Florence Tinguely Mattli katika Maadhimisho ya Miaka 25 ya Mtandao wa Vikundi vya Wakulima (MVIWATA) kwenye uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro, Octoba 3, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa mkulima wa uyoga, Maria Shindika wa Mvomero (kulia) kabla ya kuhutubia katika Maadhidhimisho ya Miaka 25 ya Mtandao wa Vikundi vya Wakulima (MVIWATA) yaliyofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, Oktoba 3, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu unga na bidhaa mbalimbali zinaotokana na zao la soya kutoka kwa Julie Bwire wa Mvomero (kushoto) kabla ya kuhutubia katika Maadhimisho ya miaka 25 ya Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, Oktoba 3, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimina na Mlezi wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) na Mkuu wa Mkoa Mstaafu, Stephen Mashishanga wakati alipowasili kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kumwakilisha Rais, John Pombe magufuli katika Maadhimisho ya Miaka 25 ya MVIWATA, Oktoba 3, 2018. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Stephen Kebwe. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

*Asema zaidi ya wakulima wadogo 527,000 katika Mikoa 13 wamenufaika 


WAZIRIMKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetoa mikopo yenye thamani ya sh. bilioni 56.45 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya kilimo katika mikoa 13 hapa nchini.

Amesema mikopo hiyo imetolewa katika kipindi cha kuanzia Agosti 2015 hadi Septemba 2018, kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB).Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Oktoba 3, 2018) kwenye maadhimisho ya miaka 25 ya Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) mjini Mororogo.

Mikopo hiyo imewanufaisha wakulima wadogo zaidi ya 527,000 waliopo kwenye mnyororo wa thamani wa mazao ya kahawa, karafuu, mahindi, mbogamboga na mazao mengine.Amesema Serikali inatekeleza mipango mbalimbali kwa lengo la kutatua kero zinazowakabili na kuwawezesha wakulima wadogo kujikwamua kiuchumi kupitia kilimo. 

Amesema Juni 14, mwaka huu Rais Dkt. John Magufuli, alizindua Awamu ya Pili ya Programu ya Kuendeleza Kilimo hapa nchini (ASDP II) yenye lengo la kuboresha sekta ya kilimo.Waziri Mkuu amesema ASDP II inalenga kuhakikisha sekta ya kilimo inapewa kipaumbele stahiki ili iweze kuleta tija kwa wakulima wenyewe na Taifa kwa ujumla.

“Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuboresha sekta ya kilimo ikiwemo kutoa mikopo kwa wakulima wadogo; kuondoa baadhi ya tozo zenye kufifisha uzalishaji.” Pia kuweka mipango mizuri ya matumizi bora ya ardhi na kutafuta masoko pamoja na kuongeza thamani kwenye mazao ya kilimo ili kumuongezea tija mkulima.

Kadhalika, Waziri Mkuu ameongeza kuwa mchango wa wakulima wadogo umewezesha Taifa kujitosheleza kwa chakula na hata kuuza nje ya nchi mazao ya kilimo. Hivyo, Waziri Mkuu ametoa rai kwa viongozi na watendaji wa Serikali kujenga utamaduni wa kuhudhuria wa kukutana na kuzungumza na wakulima kuhusu mahitaji hayo.

“Tunafahamu kwamba wakulima mna changamoto nyingi zikiwemo za kisera, kirasilimali na kiutendaji kwenye masuala ya ardhi, masoko, mitaji na hata kero za tozo na ushuru.”Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameagiza Wakala wa Vipimo nchini (WMA) waendesha msako utakaowanasa wafanyabiashara wanaowaibia wakulima kwa njia ya udanganyifu wa kutumia vipimo visivyo sahihi.

Waziri Mkuu amesema mfanyabiashara yeyote atakayebainika kuwaibia wakulima kwa kutumia vipimo visivyo rasmi achukuliwe hatua za kisheria. 
“Utaratibu wa kutumia vipimo visivyo rasmi ambavyo vimepewa majina ya lumbesa, kangomba, umejileta mwenyewe na mengine mengi lazima ukomeshwe.”

Waziri Mkuu ameuagiza uongozi wa WMA kwa kushirikiana na halmashauri zote nchini wahakikishe mazao ya wakulima yanauzwa kwa kutumia vipimo rasmi ili wasiendelee kupunjwa.Akizungumzia kuhusu kero ya ardhi, Waziri Mkuu amesema Serikali itawapa wananchi ardhi inayotwaliwa kutoka kwa wawekezaji au wamiliki walioshidwa kukidhi masharti na yale yasiyoendelezwa kwa muda mrefu

SERIKALI YA MKOA DODOMA IMEWAVUA MADARAKA AFISA ELIMU HALMASHAURI CHEMBA NA KONDOA MJINI

$
0
0
Na.Alex Sonna,Dodoma

Serikali ya Mkoa wa Dodoma umewavua madaraka afisa elimu Halmashauri ya wilaya ya Chemba na afisa elimu Halmashauri ya wilaya ya Kondoa mji wameviliwa vyeo vyao.

Akizungumza na Waandishi wa habari Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk Binilith Mahenge leo amesema kuwa wamewavua pia madaraka watatibu wa Elimu ngazi ya kata watano.

Hatua hiyo inakuja baada ya shule za msingi zote katika wilaya ya Chemba na shule moja iliyopo wilay ya Kondoa mkoani Dodoma kwa tuhuma za kujihusisha na njama za udanganyifu zlizopelekea kufutiwa mitihani ya darasa la kutokana kutokana na udanganyifu.

Aidha amesema kuwa kutokana na udanganyifu huo pia waalimu wakuu wa shule tano waliobainika wazi wazi katika hatua za awali za uchunguzi kujihusi na njama hizi na ameagia Mamlaka za nidhamu kuwafungulia mashtaka wale wote waliohusika na tukio hilo.

“Waalimu wanne waliokuwa wasimamizi wa mitihani katika shule binafsi ya Kondoa integrity nao wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi,”,amesema Dk, Mahenge

Kuhusu kuwepo kwa taarifa kuwa Chemba na kondoa wamekuwa wakifanya vibaya katika mitihani hivyo kutumia njia hiyo ili waweze kufanya vyema, Ofisa Elimu Mkoa Maria Lyimo, alisema uchunguzi bado unandeea hivyo hawawezi kusema kuwa hi ndio sababu na mara uchunguzi utakapokamilika watatoa taarifa ya kina.

“Kwa sasa itoshe tu kupokea taarifa hiyo ya awali lakini bado tunaendelea na uchunguzi, hivyo taarifa kamili itakuja bada ya kukamilika kwa uchunguzi huo,”alisema Ofisa Elimu huyo.

Maria alizitaja kata ambazo waratibu Elimu wamevuruliwa madaraka kuwa ni pamoja na Farkwa, Kinkima, Bulemka, Chemba na Makamaka na walimu wakuu watano ni kutoka katika kata za Farkwa, Paranga, Chemba, Goima na Churuku .

Hata hivyo Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Maduka Keisy, amekanusha taarifa za kwamba kondoa na Chemba wamekuwa akifanya vibaya vipindi vyote vya mitihani bali matokeo yamekuwa yakibadilika badilika katika vipindi mbalimbali vya mitihani.

Bw.Keisy amesema kuwa huenda wakawa waliamua kutumia njama hizo kutokana na ushindani uliopo mana kwa mfano Kondoa katika mtihani wa darasa la Saba mwaka jana walishika nafasi ya kwanza kimkoa.

JALADA KESI TUHUMA ZA UHUJUMU UCHUMI INAYOMKABILI MSTAAFU WA TAZAMA LIPO KWA DPP

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii

UPANDE wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mstaafu wa Shirika la Mafuta Tanzania na Zambia (Tazama), Samwel Nyakirang'ani na wenzake 11, umeileza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa Jalada la keai hiyo lipo kwa (DPP), kwa ajili ya kulichambua na kulitolea maamuzi.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Patrick Mwita, ameeeleza hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba, kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.Mwita alidai jalada lipo kwa DPP kwa ajili ya kulichambuliwa na kulitolea maamuzi kwa kuangalia washtakiwa gani washtakiwe na washtakiwa gani waachiwe huru na pia itatoa maamuzi kama Mahakama ya Kisutu itapata mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo au itahamishiwa Mahakama ya mafisadi.

Ameongeza wapo katika hatua za mwisho za kukamilisha uchambuzi, hivyo wanaomba mahakama yako ipange tarehe nyingine, kwa ajili ya kutajwa.Baada ya kusikiliza hoja hizo, wakili wa utetezi, Alex Balomi ameutaka upande wa mashtaka kuongeza kasi ya ufuatiliaji wa kesi hiyo ili DPP aweze kutoa maamuzi haraka kwa sababu wateja wake wanaendelea kusota mahabusu.

Hakimu Simba ameutaka upande wa mashtaka kuharakisha zoezi la uchambuzi ili haki iweze kupatikana." Upande wa mashtaka mfuatilie kwa DPP kujua anamaliza lini kulipitia faili hili maamuzi yaweze kufanyika na haki iweze kupatikana" alisema Hakimu Simba.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 17, 2018. Mshtakiwa Nyakirang’anyi na wenzake katika kesi hiyo wanakabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kujiunganishia isivyo halali bomba la mafuta mali ya (TPA), Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Nyangi Mataro, mwalimu wa shule ya msingi Ufukoni na mkazi wa Kisiwani Mkajuni Kigamboni. Mfanyabaishara, Farijia Ahmed, mkazi wa Soko Maziwa Kigamboni, Malaki Mathias, mkazi wa Magogoni, Kristomsi Angelus, mkazi wa Soko Maziwa, Fundi Ujenzi Pamfili Nkoronko, mkazi wa Tungi Kasirati na Henry Fredrick, mkazi wa Tungi Kigamboni.

Wengine ni Audai Ismail ambaye ni mkazi wa Kibaha, Chibony Emmanuel, Roman Abdon, Amina Shaban na Zubery Ally.Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka matatu ya uhujumu uchumi kwa kujiunganishia isivyo halali bomba la mafuta, kinyume cha sheria ya Uhujumu uchumi.

DC NEWALA AAMURU MGANGA KUSIMAMISHWA KAZI BAADA YA MAMA MJAMZITO KUFARIKI KWA KUCHELEWA KUPATA HUDUMA

$
0
0

Na Mwandishi Maalum, Newala.
Mkuu wa Wilaya ya Newala Aziza Mangosongo ameagiza Mganga wa wodi ya wazazi katika Hospitali ya Wilaya hiyo Abdallah Kipeta kusimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi kufuatia tukio la kufariki mama mjamzito kutokana na uzembe wa kutompatia huduma za matibabu kwa wakat

Agizo hilo amelitoa jana, kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Newala, wakati akizungumza na watumishi wa Afya na Wajumbe wa Bodi ya Afya kwa lengo la kuwahimiza kufanyakazi kwa weledi na kuwahudumia wagonjwa bila ubaguzi.

"Nimesikitishwa sana na kifo cha huyu mama, alikuja hapa nesi akawa anahangaika kupiga simu lakini kila mganga anayepigiwa anasema siyo zamu take, sasa yule alitekuja alikuwa amechekewa sana had I mama yule akafa.

Sasa huyu mama aliyekua ameacha kichanga eti ndiyo mnachangachanga vihela kukinunulia maziwa, kufanya hivyo ndiyo kutarudisha uhai was huyu mama? Naagiza Mkurugenzi mwandikie barua ya kumsimamisha kazi huyu Daktari halafu nipate nakala Mara moja, kama mlizoea kubebana Mimi kwangu hapana, sins mbeleko wala shuka", alisema Mkuu Hugo was wilaya.

" Hospitali hii inachangamoto nyingi sana, haina dawa, mashuka huku waiguzi hawajali wagonjwa, imefikia hatua hata bombs ya sindano mgonjwa anaambiwa hakuna, anaambiwa akanunue kwenye duka la dawa hapo nje, na hili duka lipo bize kwelikweli, vipi mna ubia nalo?" Alisema na kuhoji.

"Inasikitisha kuona kwamba huduma zinazorota kwenye hospitality hii, mkiulizwa mnasema hakuna pesa, lakini pesa za kulipana safari na semina mnapeana, sasa mnazipata wapi", alihoji.

Alisema  kitendo cha wauguzi kutowajali wagojwa na kuwatolea kauli mbovu na ukosefu wa dawa kimesababisha wagonjwa wengi kutojitokeza kwenda kupata huduma za afya na hivyo kufanya mapato ya hospitali hiyo kushuka  tofauti na ilivyokuwa zamani.

"Hospitali hii sasa inaonekana mnajali pesa badala ya utu, mgonjwa akitoka nchi jirani ya Msumbiji  mnamkimbilia kwa sababu mnamuna atawapa rushwa, lakini akitoka Mnyambe au Kitangale hamumjali, hii tabia lazima ikome kabisa", alisema Mkuu huyo wa Wilaya.

Mkuu huyo wa Wilaya alihitimisha kwa kutoa mwezi mmoja kwa uongozi wa hospitali hiyo kujenga choo kilichoboka kwenye wodi ya wazaxi ambapo sasa wagonjwa kwenye wodi hiyo wanajisaidia nje.

pia ametoa agizo kwa Mganga Mkuu wa hospitali hiyo Chitopela Chitopela kuhakikisha mapungufu yaliyojitokeza katika hospitali hiyo yanafanyika kazi hususani kutumia fedha nyingi katika kununua dawa na vitendea kazi.

DKT. ABBASI AHIMIZA VIONGOZI WA MKOA WA SIMIYU KUTANGAZA NA KUTETEA MAGEUZI YANAYOFANYWA NA SERIKALI

$
0
0

 
Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, akitoa mada ya umuhimu wa mawasiliano ya kimkakati mbele ya viongozi mbalimbali wa mkoa wa Simiyu. Kwenye wasilisho lake amesisitiza kutangaza na kutetea mageuzi yanayofanywa na Serikali ya amamu ya tano.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mheshimiwa Anthony Mtaka pamoja na viongozi wengine wa mkoa huo waliohudhuria kikao cha uwasilishaji wa mada iliyohusu umuhimu wa mawasiliano ya kimkakati katika kutangaza ahadi za serikali.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji wa Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, mheshimiwa Anthony Mtaka (katikati) na Katibu Tawala wa mkoa huo Jumanne Sagini.

DKT SHEIN AZINDUA MFUMO WA KUIMARISHA USALAMA KATIKA MJI WA ZANZIBAR WAFANYIKA

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt,Ali Mohamed Shein akibonyeza kitufe kuashiria Uzinduzi wa mradi wa Mfumo wa kuimarisha usalama katika mji wa Zanzibar uliofanyika katika Ukumbi wa Idrisa Abdull Wakil Kikwajuni mjini Zanzibar. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt,Ali Mohamed Shein akitoa hatuba ya Uzinduzi wa mradi wa Mfumo wa kuimarisha usalama katika mji wa Zanzibar uliofanyika katika Ukumbi wa Idrisa Abdull Wakil Kikwajuni mjini Zanzibar. 
Makamanda pamoja na Wananchi mbalimbali waliohudhuria katika Uzinduzi wa mradi wa Mfumo wa kuimarisha usalama katika mji wa Zanzibar uliofanyika katika Ukumbi wa Idrisa Abdull Wakil Kikwajuni mjini Zanzibar. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ Haji Omar Kheir akitoa hotuba ya makaribisho kwa Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa mradi wa Mfumo wa kuimarisha usalama katika mji wa Zanzibar uliofanyika katika Ukumbi wa Idrisa Abdull Wakil Kikwajuni mjini Zanzibar. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt,Ali Mohamed Shein katikati akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali katika Uzinduzi wa mradi wa Mfumo wa kuimarisha usalama katika mji wa Zanzibar uliofanyika katika Ukumbi wa Idrisa Abdull Wakil Kikwajuni mjini Zanzibar. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt,Ali Mohamed Shein kushoto akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt,Abdalla Juma Sadalla(MABODI)Mara baada ya kuasili katika Uzinduzi wa mradi wa Mfumo wa kuimarisha usalama katika mji wa Zanzibar uliofanyika katika Ukumbi wa Idrisa Abdull Wakil Kikwajuni mjini Zanzibar. PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

TCRA YAKUTANA NA VIONGOZI SHINYANGA,YAWATAKA WAMILIKI WA VING'AMUZI NA VISIMBUZI KUHESHIMU SHERIA

$
0
0
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) imesisitiza juu ya umuhimu wamiliki wa ving'amuzi na visimbuzi vinavyorusha matangazo yake hapa nchini kuheshimu sheria na kuhakikisha wana leseni zinazowaruhusu kuonesha chaneli za ndani bure badala ya kuwatoza wananchi fedha yoyote.

Hali hiyo imebainishwa leo Oktoba 3,2018 mjini Shinyanga kwenye semina ya siku moja iliyoendeshwa na Mamlaka hiyo kwa viongozi mbalimbali wa serikali, mashirika ya umma na asasi za kiraia mkoani Shinyanga.

Semina hiyo ililenga kuwapa uelewa viongozi hao juu ya sababu za TCRA kufungia baadhi ya ving’amuzi kurusha chaneli za ndani baada ya kubaini vimekiuka masharti ya leseni zao ambapo hata hivyo lengo ni kumwokoa mtumiaji wa ving’amuzi na visimbuzi kutotozwa gharama kubwa.

Mtoa mada katika semina hiyo, Mhandisi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Francis Mihayo alisema lengo la mamlaka hiyo ni zuri ambalo limezingatia sheria za mawasiliano nchini.Mihayo alisema maamuzi yaliyochukuliwa na TCRA kuagiza kuondolewa kwa chaneli za ndani kwenye baadhi ya ving’amuzi na visimbuzi vya makampuni ya DSTV, AZAM TV na Zuku TV ambavyo havikuwa na leseni ya kurusha chaneli za ndani umelenga kusimamia sheria zilizopo.

Alisema ving’amuzi vilivyozuiliwa vinapaswa kuheshimu sheria za nchi na kwamba vituo vilivyoshinda tenda ya kuonesha chaneli za ndani zipatazo nane ndizo zinazopaswa kuonesha chaneli hizo na si vituo vingine.Alifafanua kuwa baada ya kuhama kutoka kwenye analojia kuja digitali, serikali iliweka sheria na taratibu ambazo zinatakiwa kufuatwa ili jamii iendelee kunufaika na uhabarishwaji pasipo kurudishwa nyuma na gharama kubwa.

"Kuna kitu kinaitwa FTA (hii ni ya kurusha Maudhui Bila kulipia) na vipindi vya kutolipia ni Vipindi vya Kijamii ikiwemo taarifa ya Habari, vinapaswa kuwa Bure.Na kuna mfumo wa (Subscription by payment) pay TV yaani watumiaji wanapata vipindi vya TV kwa kulipia, na hivi vipindi ni vile ambavyo si vipindi vya kijamii.

Lakini kumekuwa na kuchanganya mambo ambapo Ving'amuzi huwalipisha watu na kwenye vipindi vya kijamii ambavyo vilipaswa kuonyeshwa bure kwenye ving'amuzi vyote.Pia vipindi vya kijamii vilipaswa kutoonueshwa kwenye madishi ya satellite ambazo ni zakulipiwa moja kwa mpja kwani ni kukiuka masharti ya leseni yao",alisema Mihayo.

Awali mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akifungua semina hiyo amewataka viongozi wote waliohudhuria sheria hiyo kufikisha kwa wananchi elimu watakayoipata ili waelewe na waache kuilalamikia mamlaka ya TCRA wakidai haitendi haki.Alisema lengo kuu la serikali ni kuhakikisha masharti ya leseni waliyopewa wamiliki wa ving’amuzi na visimbuzi yanaheshimiwa na kwamba kuwatoza wananchi malipo kwa chaneli zinazopaswa kuoneshwa bure ni kosa la kisheria.

“Ni vyema tukawa wanafunzi bora ili tuweze kuelewa masuala mengi yanayohusu sekta hii, kwani sisi sote ni wadau wakubwa wa sekta hii, ama kwa taarifa zetu kutangazwa kupitia vituo vya utangazaji au sisi wenyewe tuna visimbuzi majumbani mwetu kwa ajili ya kufuatilia na kusikiliza taarifa mbalimbali,”

“Ndugu washiriki maelezo yaliyotolewa kwa watoa huduma wa ving’amuzi vya AZAM, DSTV na Zuku yameangalia maslahi mapana ya taifa ikiwa ni pamoja na kumlinda mtumiaji wa mwisho kwa siku za mbeleni,” alieleza Telack.

Pia alisema iwapo TCRA wasingechukua hatua waliyoichukua hivi sasa watoa huduma hawa wangelazimisha huduma hii kwenye majukwaa yao na kuanza kupandisha bei taratibu kama wanavyotaka na hatimae wananchi wangeshindwa kumudu tozo zinazotozwa kila mwezi.

Kwa upande wao washiriki wa semina hiyo walishukuru kwa kupatiwa elimu iliyotolewa ambapo hata hivyo walichangia hoja mbalimbali na kuiomba TCRA kusimamia kwa ukaribu zaidi sheria zake ili wananchi watendewa haki badala ya kuumizwa kwa gharama za ving’amuzi wanazotozwa kila mwezi ambapo wameomba ikiwezekana gharama za sasa zipunguzwe kidogo.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Zainab Telack akifungua semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA kwa viongozi mbalimbali wa serikali, mashirika ya umma na asasi za kiraia mkoani Shinyanga kwa ajili ya kuwapa uelewa viongozi hao juu ya sababu za TCRA kufungia baadhi ya ving’amuzi kurusha chaneli za ndani baada ya kubaini vimekiuka masharti ya leseni zao.Picha zote na Suleiman Abeid -Malunde1 blog
Mhandisi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Francis Mihayo TCRA Makao Makuu jijini Dar es Salaam akitoa mada wakati wa semina ya siku moja iliyoendeshwa na Mamlaka hiyo kwa viongozi mbalimbali wa serikali, mashirika ya umma na asasi za kiraia mkoani Shinyanga kwa ajili ya kuwapa uelewa viongozi hao juu ya sababu za TCRA kufungia baadhi ya ving’amuzi kurusha chaneli za ndani baada ya kubaini vimekiuka masharti ya leseni zao.

Kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga,Albert Msovela na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Zainab Telack wakisikiliza mada ukumbini.

Wakuu wa wilaya mkoani Shinyanga wakiwa ukumbini.
Viongozi mbalimbali wakifuatilia mada ukumbini.
Viongozi mbalimbali wa mkoa wa Shinyanga wakiwa katika ukumbi wa mikutano ya ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga.
Muandaaji wa vipindi vya TCRA kwenye vyombo vya habari vya Maadili na kizazi kipya (MAKIKI),Terry Gbemuu maarufu Mama Terry akiwa ukumbini.








Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Meshimiwa Zainab Telack akizungumza wakati wa semina hiyo.


DKT TIZEBA AIPONGEZA MVIWATA KWA KUWAUNGANISHA WAKULIMA NCHINI

$
0
0
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akitoa salamu za Wizara ya kilimo mbele ya Mgeni rasmi ambaye ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa (Mb) kwenye Maadhimisho ya miaka 25 ya mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (MVIWATA) Leo tarehe 3 Octoba 2018 katika uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro. (Picha Zote Na Mathias Canal-WK)
Baadhi ya wakulima wakifatilia Maadhimisho ya miaka 25 ya mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (MVIWATA) Leo tarehe 3 Octoba 2018 katika uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro
Naibu Waziri wa kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa (Mb) kwenye Maadhimisho ya miaka 25 ya mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (MVIWATA) Leo tarehe 3 Octoba 2018 katika uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro.
Waziri wa kilimo Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Dkt Bashiru Ally mara baada ya kuwasili kwenye Maadhimisho ya miaka 25 ya mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (MVIWATA) Leo tarehe 3 Octoba 2018 katika uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro.

Na Mathias Canal-WK, Morogoro


Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba (Mb) ameupongeza mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (MVIWATA) tangu kuanzishwa kwake mwaka 1993 kwa kuwa dira na Muungano wenye sauti moja yenye mshikamano na mafanikio makubwa kwa wakulima nchini.


Waziri Tizeba ametoa pongezi hizo Leo tarehe 3 Octoba 2018 wakati akitoa salamu za Wizara ya kilimo mbele ya Mgeni rasmi ambaye ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa (Mb) kwenye Maadhimisho ya miaka 25 ya mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (MVIWATA).


Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Dkt Bashiri Ally, Waziri Tizeba alisema kuwa kipindi cha miaka 25 MVIWATA imekuwa mtandao wenye dhamira chanya kwa kuwaunganisha wakulima wadogo kwa kutetea maslahi yao na kujenga mikakati ya pamoja ya kujikwamua kijamii, kiuchumi na kiutamaduni.


Aliitaka MVIWATA kuwa inapaswa kusimamia zaidi maslahi ya wakulima nchini kwa kuwa wahusika wakuu na wamiliki wa mfumo wa uzalishaji na kuwa sehemu ya mfumo wa maamuzi ya masuala yahusuyo maisha ya wakulima wadogo hususani mfumo wa uzalishaji na rasilimali ardhi.


Dkt Tizeba aliwahakikishia wananchama hao zaidi ya 2000 walioshiriki katika kongamano hilo la siku tatu kuwa wakulima wanapaswa kueleza changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwa ni pamoja na kuzitafutia ufumbuzi wa haraka iwezekanavyo.


Naye, Mkurugenzi Mkuu wa Mtandao wa wakulima Tanzania (MVIWATA) Ndg Stephen Ruvuga akisoma risala ya maadhimisho hayo ameipongeza serikali katika kujenga uchumi wa Taifa katika kuimarisha sekta ya kilimo nchini.


Alisema kuwa kwa kutambua hilo na hususani katika matumizi ya fedha za umma aliongeza kuwa kunapaswa kuongeza msisitizo katika usimamizi wa matumizi ya fedha za umma na kuongeza ukusanyaji wa mapato.


Alisema kuwa pamoja na jitihada kubwa za serikali za kuimarisha sekta ya kilimo wakulima kwa ujumla bado wanachangamoto mbalimbali ikiwemo swala la ardhi, bei ya Mazao na soko la uhakika na mitaji ya uwezeshaji wakulima.

WAZIRI MPINA AAPA KUTOENDELEA KUTUMIA MABILIONI KUAGIZA BIDHAA ZA SEKTA ZA MIFUGO NA UVUVI NJE YA NCHI

$
0
0

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akitoa hotuba yake ya uzinduzi wa Dawati la Sekta Binafsi la kusaidia sekta za mifugo na uvuvi linaloundwa kwa ushirikiano kati ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), ASPIRES kwa kushirikiana na SAGCOT, USAID pamoja na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji jijini Dodoma jana.Walioketi kushoto kwake ni Katibu Mkuu Mifugo, Profesa Elisante Ole Gabrieli, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Kilimo, Mifugo na Maji, Mahmoud Mgimwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega.

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina( wa tano kutoka kushoto walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Serikali na taasisi mbalimbali wadau wanaounda Dawati la Sekta binafsi la kusaidia sekta za mifugo na uvuvi nje ya ofisi ya Dawati hilo jijini Dodoma, nyuma ya jengo la Bunge jana . Waliosimama nyuma ni wataalam wa dawati hilo.
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akitia saini kitabu cha wageni kwenye ofisi mpya ya Dawati la Sekta Binafsi la kusaidia sekta za mifugo na uvuvi linaloundwa kwa ushirikiano kati ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), ASPIRES kwa kushirikiana na SAGCOT, USAID pamoja na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji jijini Dodoma jana. Kushoto kwake anayeshuhudia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Kilimo TADB, Japhet Justine, Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega.




· Aunda dawati maalum kusaidia sekta binafsi.
· Assisitiza “We can, We Must, We Will”


Na John Mapepele, DODOMA


WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amesikitikishwa na kitendo cha Tanzania kutumia takribani sh. bilioni 100 kila mwaka kuagiza samaki, maziwa na nyama kutoka nje ya nchi licha ya Tanzania kuwa na ng’ombe milioni 30.5 na samaki tani milioni 2.7 walioko kwenye maziwa, mito na bahari bidhaa ambazo zingeweza kuzalishwa nchini na kuleta ajira na kujenga uchumi wa Taifa.

Mpina ametoa kauli hiyo jana jijini Dodoma wakati wa akizindua Dawati la Sekta Binafsi la kusaidia sekta za mifugo na uvuvi linaloundwa kwa ushirikiano kati ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), ASPIRES kwa kushirikiana na SAGCOT, USAID pamoja na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ambapo amesema Serikali ya awamu ya tano haitakubali tena hali hiyo iendelee.

Mpina alisema kutokana na changamoto zilizopo wizara yake imeona kuna umuhimu wa kuunda dawati hilo ili kuunganisha na kuweka daraja baina ya wizara na sekta binafsi, daraja ambalo kwa sasa ni kama limevunjika ili kutoa suluhisho la changamoto zinikazoikabili sekta binafsi katika biashara na uwekezaji kwenye sekta hizo hali itakayoamsha na kuvutia uwekezaji katika mashirika ya Serikali ya NARCO na TAFICO.

“Tumechoka kuona wawekezaji wa Business Plan, michoro , vikao na mawasilisho kibao lakini uwekezaji hakuna, tumechoka kuona nchi yetu inageuzwa kuwa soko la viwanda vya nje vya mazao ya mifugo na uvuvi huku sehemu kubwa ya malighafi ikitokea nchini,tumechoka kuona ajira za watanzania zikipelekwa nje ya nchi, pia Serikali kukosa mapato”alisema Waziri Mpina.

Hivyo Dawati hilo litawaunganisha wadau katika mabenki na Taasisi za fedha ndani na nje ya nchi na kutoa suluhisho la kiutawala na kifedha katika viwanda na maeneo mengine ya wawekezaji.Pia litahusisha maafisa wabobezi kwenye masuala ya Sekta Binafsi, masuala ya kibenki na biashara.

Mpina alisema Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020 ibara ya 25 a-q na ibara ya 27 a-p inaiagiza Serikali kufanya mageuzi katika sekta ya mifugo na uvuvi ili kuongeza uzalishaji, thamani na masoko ya uhakika,mipango ya Serikali kutekeleza majukumu hayo yameainishwa katika ASDPII,FYDPII.

Aliongeza kuwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli, wakati wa kampeni za uchaguzi za mwaka 2015 na hata baada ya kuchaguliwa ameahidi kufanya mageuzi makubwa katika sekta za mifugo na uvuvi ambapo pia katika vikao na mikutano mbalimbali ameonyesha kutokuridhishwa na yanayoendelea katika sekta ya mifugo na uvuvi.

“Mhe Rais amekuwa akihoji mara kwa mara kwanini tuagize samaki nje ya nchi, wakati tuna bahari, maziwa na mito yenye raslimali nyingi?? Kwa nini tuagize viatu na nyama kutoka nje wakati tunayo mifugo mingi inayotuzunguka?? Kwa nini tumekuwa na viwanda vingi ambavyo havifanyi kazi maswali haya ya Mheshimiwa Rais ni maagizo na maelekezo kwa Wizara yangu ni lazima yapate ufumbuzi”alisema Mpina.

Hivyo Waziri Mpina akasisitiza kuwa maagizo na maelekezo yote ya Rais Dk. Magufuli ni lazima yapatiwe majibu ya vitendo kabla ya kumalizika kwa awamu ya kwanza ya uongozi wake mwaka 2020.“Tunaapa kutokushindwa na Mwenyezi Mungu atatusaidia. ‘Leaders must be willing to sacrifise for the sake of the vision,for the sake of their people, for the sake of the National’.Pia tunakumbuka maneno mazuri ya Mwandishi wa Dk. Reginald Abraham Mengi katika kitabu chake cha I can, I must, I will the Spirit of Success hivyo hivyo na sisi We can, We Must, We Will. Hatutashindwa” alisisitiza Mpina.

Kwa upande wake Katibu Mkuu- Mifugo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Elisante Ole Gabriel alisema wazo la kuundwa kwa dawati hilo limeasisiwa na Waziri Mpina na kwamba wao kama watendaji wakuu wa wizara watasimamia kikamilifu kuhakikisha matokeo ya haraka yanapatikana kutokana na kuanzishwa kwa dawati hilo na kuwezesha mchango wa sekta ya mifugo katika pato la taifa kuongezeka kutoka asilimia 6.9 mwaka 2017.

Naye Katibu Mkuu- Uvuvi, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Rashid Tamatama changamoto kubwa iliyokuwa inakabili ukoaji wa sekta hiyo ni mikopo hali iliyochangia sekta hiyo kuchangia asilimia 2.2 katika pato la taifa hivyo kuanzishwa kwa dawati hilo kutasaidia kuinua sekta hiyo na kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Kilimo TADB, Japhet Justine aliwawakishia kuwa kwa sasa wavuvi na wafugaji wanakopesheka hivyo kupitia dawati hilo ni dhamira mageuzi ya haraka yatapatikana.Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kuendeleza Kilimo Nyanda za Juu Kusini (SAGCOT), Geofrey Kirenga kwa sasa taasisi hiyo itaongeza wigo wa kusaidia sekta za mifugo na uvuvi kutokana na kuwepo mipango madhubuti ya kusaidia sekta hizo.


Mratibu wa Mradi wa ASPIRES, Prof. David Nyange kuanzishwa kwa dawati hilo ni fursa kwao kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kufikia uchumi wa viwanda kupitia sekta za mifugo na uvuvi.

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS OKTOBA 4,2018

TTCL YAMUONGEZA MSANII MAN FONGO TAMASHA LA RUDI NYUMBANI KUMENOGA

$
0
0

Mkuu wa Biashara Mkoa wa Dar es Salaam wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Bi. Mary Kinabo (kushoto) akisaini mkataba leo Dar es Salaam na msanii wa muziki aina ya singeli, Man Fongo (kulia) ili msanii huyo kushiriki katika kampeni kubwa ya Rudi Nyumbani Kumenoga inayoendelea mikoa yote ya Tanzania. Anayeshuhudia kulia ni mwanasheriaa wa TTCL, .Wasanii wengine wanaaonogesha kampeni hiyo ni pamoja na Asley Isihaka maarufu kama Dogo Asley na Shilole ‘Shishi Baby’. 
Mkuu wa Biashara Mkoa wa Dar es Salaam wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Bi. Mary Kinabo (kushoto) akibadilishana mkataba na msanii wa muziki aina ya singeli, Man Fongo (kulia) mara baada ya kuusaaini ili msanii huyo kushiriki katika kampeni kubwa ya Rudi Nyumbani Kumenoga inayoendelea mikoa yote ya Tanzania. Anayeshuhudia kulia ni mwanasheriaa wa TTCL. Wasanii wengine wanaaonogesha kampeni hiyo ni pamoja na Asley Isihaka maarufu kama Dogo Asley na Shilole ‘Shishi Baby’. 
Mkuu wa Biashara Mkoa wa Dar es Salaam wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Bi. Mary Kinabo (kushoto) akimpongeza msanii wa muziki aina ya singeli, Man Fongo (kulia) mara baada ya kuusaini mkataba ili msanii huyo kushiriki katika kampeni kubwa ya Rudi Nyumbani Kumenoga inayoendelea mikoa yote ya Tanzania. Anayeshuhudia kulia ni mwanasheriaa wa TTCL. 
Mkuu wa Biashara Mkoa wa Dar es Salaam wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Bi. Mary Kinabo (kushoto) pamoja na msanii wa muziki aina ya singeli, Man Fongo (kulia) wakionesha mkataba mara baada ya msanii huyo kushiriki katika kampeni kubwa ya Rudi Nyumbani Kumenoga inayoendelea mikoa yote ya Tanzania. Anayeshuhudia kulia ni mwanasheriaa wa TTCL. 
Sanii wa muziki aina ya singeli, Man Fongo (kulia) akizungumza mara baada ya kusaini ili kushiriki katika kampeni kubwa ya Rudi Nyumbani Kumenoga inayoendelea mikoa yote ya Tanzania. 
Mkuu wa Biashara Mkoa wa Dar es Salaam wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Bi. Mary Kinabo na Man Fongo wakizungumza. 
Afisa Masoko Mkuu wa Shirika la mawasiliano Tanzania (TTCL), Laibu Leornad (kushoto) akizungumza katika hafla hiyo.

WAANDISHI WASHINDA TUZO ZA HABARI ZA MAJI...MWAKYEMBE ATOA NENO

$
0
0

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WAZIRI wa Habari,Sanaa ,Utamaduni na Michezo Dk.Harson Mwakyembe amekabidhi tuzo za Habari za Maji kwa waandishi mahiri wa masuala ya uwajibikaji kuhusu usimamizi wa rasilimali za maji.

Tuzo hizo zimeandaliwa na Shirika la Shahidi wa Maji kupitia Programu ya Uhakika wa Maji kwa kushirikiana na Shirika la Water Witness International,WaterAid pamoja na Journalist Enviromental Association of Tanzania(JET).

Tuzo hizo ambazo zimekabidhiwa kwa waandishi hao zinajulikana kama Tuzo za Habari za Maji kwa waandishi hao mahiri wa masuala ya uwajibikaji kuhusu usimamizi wa rasilimali za maji.Waliokabidhiwa tuzo hizo ni Mwandishi Nuzulack Dausen (Kundi B) ambalo lilihusu Uandishi mahiri wa habari za maji kwa uhakika wa maji.

Mwandishi mwingine aliyepatq tuzo ni Sylvester Domasa(Kundi B) ambalo lilihusu Mwandishi mahiri wa habari aliyetumia taarifa za mradi wa uhakika wa maji kuleta mabadiliko.Pia Mwandishi Amina Semagongwa (Kundi C) ambalo lilihusu Mwandishi mwenye umri mdogo

Akizungumza Waziri Mwakyembe amesema tuzo hizo zitaleta chachu kwa waandishi kuandika habari za maji.Kuhusu mjadala ambao ulizungumzia waandishi kutoandika habari za maji,amesema changamoto kubwa ni waandishi kutokuwa na ari ya kufanya tafiti na hiyo inatokana mazingira duni ya kufanya kazi waandishi na hivyo mkakati wa Wizara yake ni kuinua taaluma ya habari ikiwa pamoja na kuboresha maslahi ya waandishi.

"Ukame wa habari za maji katika vyombo vya habari kuna sababu nyingi ambazo zinachangia na kubwa ni ari ya kufanya kazi za tafiti kwenye vyombo vya habari." Hakuna ari ya kufanya tafiti kutokana na mazingira yaliyopo katika tasnia ya habari na ndio maana tumeandaa sheria ya huduma ya kupata habari ambayo itasaidia kuondoa changamoto,"amesema Dk.Mwakyembe.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maji Juma Uweso amesema tuzo hizo ni chachu kwa waandishi kujikita katika kuandika habari zinazohusu rasilimali ya maji.Pia amesema maji ni muhimu katika kufikia dira maendeleo ya Taifa na kwamba moja ya jukumu ni kulinda vyanzo vya maji.Ameongeza rasilimali za maji zimeendeleea kupungua mwaka hadi mwaka na hiyo inatokana na kuongezeka kwa idadi ya watu, mabadiliko ya tabianchi na uwepo wa shughuli za kibinadamu.

"Sote tunafahamu kuwa sekta ya maji inapaswa kupewa kipaumbele na kila mmoja wetu na Serikali itaendelea kupambana na changamoto zilizopo.Pia amesema kuna changamoto ya uelewa kuhusu maji na hivyo mkakati wa Wizara ni kutumia vyombo vya habari kuelemisha umma.Hivyo amesema tuzo za maji zitatoa nafasi ya kuongeza uelewa wa Watanzania kuhusu sekta ya maji na kuomba waandishi wa habari kuendelea kushiriki kwenye tuzo hizo.

Amewapongeza Mashahidi wa Maji kwa kuandaa tuzo ambazo zimekuja wakati muafaka.Wakati huo huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo amesema changamoto kubwa iiyopo ni kwamba maji bado ni shughuli za Serikali.Amesema hivyo Serikali imekuwa ikihamasisha sekta binafsi kushiriki katika shughuli za maji na kwa sasa kuna mpango mkakati unaandaliwa kwa ajili ya kuhakikisha sekta binafsi zinashiriki katika shughuli za maji.

Pia amesema habari za maji zinaandikwa sana na anakumbuka hivi karibuni aliulizwa maswali 500 ndani ya saa moja kuhusu maji wakati anazungumza kwenye moja ya luninga nchini.Amesema waandishi wanaandika sana habari za maji na hasa zinazohusu usambazaji lakini zile za kulinda rasilimali maji ndio hazijapewa kiuambele.“Ili habari iandikwe kuna namna yake.Habari za maji zinaandikwa kila siku.Mfano Profesa Kitila Mkumbo akinywa maji si habari ila nikinywa maji yaliyochanganyika na kinyesi hiyo itakuwa habari,"amesema.

Ameongeza kuwa “Pia ili iwe habari lazima kuwe na mgogoro kidogo na kwa hapa nchini bado hatuna migogoro inayoibuliwa katika eneo la maji,”amesema.Naye Mratibu wa Shirika la Shahidi wa Maji matarajio ya shirika hilo ni kuona idadi kubwa ya waandishi wa habari wanashiriki na kushinda tuzo hizo.

 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dk.Harson Mwakyembe (kushoto) akimkabidhi zawadi mshindi wa habari za maji,Nuzulack Dausen katika hafla iliyofanyika jana  jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii).
 Waziri  wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dk.Harson Mwakyembe akizungumza na wadau mbalimbali wa maji katika hafla ya tuzo  za habari za maji zilizotolewa jana jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo akizungumza katika hafla ya tuzo za maji jana jijini Dar es Salaam.
 Sehemu ya wadau mbalimbali wa maji wakiwa katika hafla ya tuzo za waandishi wa habari za maji jana  jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dk.Harson Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na wageni waalikwa na washindi wa tuzo hizo.

DKT.CHAULA:HAKIKISHENI VITUO VYA AFYA VYOTE NCHINI VINA HATI MILIKI

$
0
0

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Zainabu Chaula akikagua ukarabati na ujenzi wa chumba cha upasuaji katika kituo cha afya cha Mabamba kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma katika ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya ukarabati na ujenzi wa vituo vya afya nchini leo Mkoani Kigoma.
Jengo la Wodi ya wazazi lililopo katika kituo cha afya cha Mabamba kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Zainabu Chaula akikagua ukarabati na ujenzi wa miundombinu ya kituo cha afya cha Mabamba kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma katika ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya ukarabati na ujenzi wa vituo vya afya nchini leo Mkoani Kigoma.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Zainabu Chaula akikagua ukarabati na ujenzi wa chumba cha upasuaji na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Bw. Rashid Mchatta (katikati) wakikagua chumba cha upasuaji katika kituo cha afya cha Mabamba kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma katika ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya ukarabati na ujenzi wa vituo vya afya nchini leo Mkoani Kigoma.



Na. Angela Msimbira OR-TAMISEMI KIGOMA


Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Zainabu Chaula amewaagiza viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kuhakikisha vituo vyote vya afya vinapatiwa hati miliki.

Dkt. Chaula ameyasema hayo alipokuwa akikagua ukarabati na ujenzi wa kituo cha afya cha Mabamba kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo, Mkoani Kigoma katika ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya ukarabati na ujenzi wa vituo vya afya nchini leo Mkoani Kigoma.

Amesema kuwa Serikali imetumia gharama kubwa katika ujenzi wa miundombinu ya afya nchini, hivyo Mamlaka za Serikali za Mitaa hazinabudi kuhakikisha zahanati na vituo vyote vya afya nchini vinakuwa na hati miliki.

“Viongozi wamekuwa wakitoa maagizo kuhusu uwepo wa hati miliki kwa majengo ya Serikali lakini bado baadhi ya watendaji wa Mamlaka husika hawatekelezi maagizo hayo, hivyo nawaagiza viongozi wote wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha kila Zahanati, Kituo cha afya kinakuwa na Hati Miliki.” Anasisitiza Dkt. Chaula.

Akiongelea kuhusu ukusanyaji wa mapato Dkt. Chaula amesema kuwa kila kituo cha afya kinatakiwa kufunga mifumo ya kielektroniki ili kuongeza mapato kwenye vituo vya afya.“Sijaridhishwa na hali ya ukusanyaji wa mapato katika Zahanati na vituo vya afya kwa kuwa mapato bado nimadogo ukilinganisha na huduma zinazotolewa ukizingatia kuwa Serikali imeweza kukarabati na kujenga miundombinu ya afya nchini, hivyo nawaagiza Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha wanasimamia ukusanyaji wa mapato katika vituo hivyo” Anasema Dkt. Chaula

Naye Mganga Mfawidhi wa Wilaya ya Kibondo Dkt.Sebastian Pima amesema kuwa ujenzi na ukarabati wa awamu ya kwanza umetekelezwa katika kituo cha Afya cha Mabamba na kugharimu shilingi milioni 500.Dkt. Pima ameyataja majengo yaliyojengwa kuwa ni wodi ya kinamama yenye uwezo wa kuchukua vitanda vine (4), Kliniki ya baba, mama na mtoto, nyumba ya mtumishi, chumba cha kuifadhia maiti, chumba cha upasuaji, chumba cha kufulia, maabara na ukarabati wa jengo lazamani la wodi ya wazazi.

Aidha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Zainabu Chaula yupo kwenye ziara ya kikazi kukagua maendeleo ya ukarabati na ujenzi wa vituo vya afya nchini na tayari ameshatembelea Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko na Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma.

WANAOSHAWISHI WAKULIMA WA KOROSHO KUKATAA MFUMO WA STAKABADHI GHALANI MKOANI PWANI WAPEWA ONYO

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI,MKURANGA

SERIKALI Mkoani Pwani, imetoa onyo kwa watu ama vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS ) wanaoshawishi wakulima kukataa mfumo wa stakabadhi ghalani pamoja na kupeleka korosho kwenye maghala makubwa na badala yake wanawarubuni kuuza kwa mtindo wa kangomba .

Aidha umetoa wito ,kwa wadau mbalimbali kujenga ghala la Kibiti ili yaweze kupewa leseni ya kutumika katika msimu ujao wa ukusanyaji na ununuzi wa korosho .Akifungua mkutano wa wadau wa zao la kibiashara la korosho ,wilayani Mkuranga ,mkuu wa mkoa huo ,mhandisi Evarist Ndikilo alisema ,yeyote aliyejipanga kukataa mfumo huo ni mhujumu uchumi na biashara hiyo haikubaliki.

Alisema, kuwa na maghala machache ni mpango wa serikali hivyo hawatakuwa na nafasi ya kutumia maghala ya vichochoroni ambayo yameshasababisha changamoto nyingi msimu uliopita ."Tunazijua Amcos ambazo zilitutia doa ,tuwajua majina na mipango wanayoyafanya ,nawataadhalisha kabisa ,hatutaki tuharibu sifa yetu tena "tutamnyakua mmoja baada ya mmoja "

Ndikilo pia alikemea, baadhi ya wanunuzi wa korosho waache kuhujumu uchumi kwa kushinda minada kisha kushindwa kulipia kwa wakati na makubaliano ya mkataba na kuanzia sasa hawatawachekea wanunuzi wa aina hiyo."Msimu huu unaokuja hatutaki utani ,tumechoka kuwa kichwa cha wendawazimu ,kila mmoja anufaike mnunuzi na mkulima bila kumyanyasa mkulima " alibainisha.

Alielezea ,tangu wameanza kutumia mfumo huo msimu wa mwaka 2015/2016 waliuza tani 8,800 ,mwaka 2016/2017 tani 13,300 na msimu wa 2017/2018 tani 20,650 hivyo kila msimu umekwenda ukiongezeka kwa uzalishaji.


Kwa mujibu wa mkuu huyo wa mkoa ,bei nayo imepanda mwaka hadi mwaka kwa mwaka 2015/2016 ilikuwa sh.2,900 kwa kilo ya korosho kwa daraja la kwanza,ambapo 2017/2018 korosho daraja hilo iliuzwa kwa sh. .3,800 na kuongeza mapato .Ndikilo alifafanua ,haikuwa rahisi kufikia malengo hayo kwani wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya maghala madogo,yasiyo na ubora na kuathirika kwa ubora wa korosho katika msimu uliopita na uhaba wa magunia .

Hata hivyo ,alitaka magunia ya mkoa yasiangukie kwa watu asiowaaminifu ili kuendelea kulinda korosho ya mkoa huo .Awali meneja uratibu huduma ,kutoka bodi ya usimamizi wa stakabadhi za maghala ,Temu fidelis alisema kuna maghala mawili yaliyosajiliwa likiwemo la Mkuranga ambalo litakuwa na uwezo wa kuhifadhi tani 15,000 za korosho na litahifadhi korosho za wakulima kutoka Mkuranga ,Mafia ,Kibiti ,Rufiji .

Alitaja ghala jingine ni la Tanita wilayani Kibaha ambalo litahifadhi tani 5,000 za korosho kutoka Kibaha ,Kisarawe ,Bagamoyo na Chalinze ,na maghala hayo yataendeshwa na mwendesha ghala .Katibu tawala msaidizi uchumi na uzalishaji ,Shangwe Twamala aliwasihi ,wakulima wa mkoa wa Pwani wasirudi nyuma ili kupata manufaa.

Nae kaimu naibu mrajis -uthibiti kutoka tume ya maendeleo ya ushirika Tanzania ,Collins Nyakunga alibainisha , mwaka jana walifanya uchunguzi na kubaini kuna uhuni unafanywa na baadhi ya AMCOS ikiwemo kufanya ubabaishaji na kusababisha hasara .

Alisema ,chama cha ushirika kinaendeshwa kwa mujibu wa sheria na mtendaji anaajiriwa kama mwajiri mwingine na ukiona unashindwa kutekeleza majukumu yako acha kazi nafasi hiyo apewe mwingine.
Mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo akifungua mkutano wa wadau wa zao la kibiashara la korosho ,wilayani Mkuranga

 Baadhi ya washiriki kwenye mkutano wa wadau wa zao la kibiashara la korosho ,wilayani Mkuranga ,Mkoani Pwani .(picha na Mwamvua Mwinyi )
 Kaimu naibu mrajis -uthibiti kutoka tume ya maendeleo ya ushirika Tanzania ,Collins Nyakunga akitolea ufafanuzi jambo wakati wa mkutano wa wadau wa zao la kibiashara la korosho ,wilayani Mkuranga ,mkoani Pwani.
 Katibu tawala msaidizi uchumi na uzalishaji ,Shangwe Twamala akizungumza jambo katika mkutano wa wadau wa zao la kibiashara la korosho ,wilayani Mkuranga ,Mkoani Pwani.(picha na Mwamvua Mwinyi

SERIKALI YAWATAKA WAFUGAJI NYUKI KUFUGA KISASA

$
0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

SERIKALI imewataka wafugaji nyuki nchini kuendesha ufugaji wao kwa njia za kisasa utakaowawezsha kuzalisha mazao yenye ubora na thamani kwa ajili ya kujiongezea kipato.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga wakati wa maadhimisho ya siku ya kitaifa ya kutundika mizinga nchini iliyofanyika Novemba 03, 2018 Kalambo mkoani Rukwa katika shamba la nyuki Nawima lililopo katika Msitu wa Mto Kalambo.

Jumla ya mizinga 100 imetundikwa katika kuazimisha siku hiyo na kufanya idadi ya mizinga katika shamba hilo kufikia 362. Awali shamba hilo lilikuwa na mizinga 262 ikuhudumiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).

Hasunga amesema ufugaji nyuki ni fursa kwa vile mazao yake hutumika kama chakula na dawa lakini pia malighafi viwandani na soko lake la ndani na nje ni la uhakika ukilinganisha na bidhaa yoyote inayozalisha nchini.“Asali yetu inagombewa katika soko la dunia, muhimu kwetu kuzingatia uzalishaji wenye tija na kuacha tabia ya kukata miti na badala yake tulinde na kuhifadhi misitu yetu ambayo nyuki hutegemea katika uzalishaji wa mazao yake,” amesema Hasunga.

Kwa wake Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo amewataka wananchi kuchangamkia fursa ya ufugaji nyuki na kuwataka kuachana na shughuli za uchomaji mkaa na kujikita katika shughuli za kujiongezea kipato pasipo kuathiri misitu kama shughuli za ufugaji nyuki.Wakati huo huo Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo amewataka wananchi kuungana katika vikundi na kujenga viwanda vidogo vidogo na vikubwa katika maeneo mbalimbali ili Serikali iwasaidie.

“TFS inashirikiana na Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF) katika kuwajengea uwezo wafugaji nyuki, jiungeni katika vikundi, andikeni maandiko mlete TaFF tuwape ruzuku zitakazowawezesha kuanzisha viwanda vya kuchakata mazao ya nyuki, masoko tunayo na serikalikali kila mwaka inatumia takribani sh. milioni 100 katika kuhakikisha inalinda ubora wa bidhaa zake za Nyuki,” amesema Prof.Silayo.

Ameongeza Serikali ina mashamba darasa ya nyuki 154 (manzuki) yenye jumla ya mizinga 11,012 na tayari imeanza ujenzi wa viwanda vya uchakatati mazao ya nyuki katika mikoa ya Singida,Tabora pamoja Iringa huku upembuzi yakinifu unaendelea katika Mkoa wa Katavi.

Katika hatua nyingine, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Allen Richard amesema Idara yake itahakikisha inafuatilia na kuona ni wafugaji wangapi wanatumia mizinga ya kisasa na kuwaelimisha wale wote wanaotumia mizinga ya asili kuachana nayo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Japhet Hasunga (kulia) akitundika mmoja kati ya mzinga 100 waliyotoa wakala wa huduma ya misitu (TFS) katika msitu wa Mto kalambo wenye Hekta 42,000.
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kulia) baada ya kutundika mmoja wa mizinga ya nyuki 100 iliyogawiwa kwa viku

DK.MWAKYEMBE AWATEMBELEA NAFASI ART SPACE,AWAPONGEZA KWA KUTIMIZA MIAKA 10

$
0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

WAZIRI wa Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo Dk.Harrson Mwakyembe amewapongeza Nafasi Art Space kwa kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake huku akielezea namna ambavyo wamekuwa wadau muhimu katika kukuza na kuendeleza sanaa za aina mbalimbali nchini.

Dk.Mwakyembe amewatembelea Nafasi Art Space katika ofisi zao zilizopo Mikochen B jijini Dar es Salaam akiwa ameambatana na Katibu Mtendaji ww Baraza la Sanaa Tanzania(BASATA) Godfrey Mngereza pamoja na viongozi wengine wa ngazi mbalimbali wakiwamo pia wa TAFCA.

Akiwa hapo Dk.Mwakyembe alipata nafasi ya kuelezwa historia ya Nafasi Art Space, mipango na mikakati ndani miaka 10 ya mwanzo.Mchoraji mahiri ambaye pia ni Mwalimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mmoja ya wajumbe wa bodi na mwalinzi wa Nafasi Art Space Profesa Elias Jengo, alitumia nafasi hiyo kueleza mafanikio ya uwepo wao.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Nafasi, Rebecca amemueleza Waziri Mwakyembe kuwa Nafasi Art Space imefanikiwa kuipeleka mbele sanaa ya Tanzania na mkakati wao ni kuendelea zaidi ya hapo."Mkakati na malengo yetu ni kuipeleka sanaa mbele zaidi na kuongeza fursa na vipato vya wasanii kupitia sanaa," amesema.

Pia amezungumzia namna ambavyo wasanii wananufaika kwa studio za kufanyia kazi, mafunzo mbalimbali, nafasi ya kukutana na wasanii wenzao kupitia Nafasi Art Space.Pia fursa ya kukutana na wapenzi wa sanaa wanaoweza kuthamini kazi zao.Kuhusu mambo ambayo yamefanyika katika kuadhimisha miaka 10 ,Rebecca amesema Septemba mwaka huu wameshiriki shughuli mbalimbali za kijamii.

"Nafasi kwa mwezi wote wa Septemba tumeshiriki mambo mbalimbali ikiwemo kwenda mashuleni,hospitalini na maeneo ya soko." Tumeshiriki shughuli za kufanya usafi na mwisho kabisa tukawa na tamashaa kubwa na la aina yake ambalo lilifanyika hapa kwetu ambapo hakukuwa na kiingilio,"amesema.

Hata hivyo baada ya kupata maelezo mbalimbali Dk.Mwakyembe ameshuhudia maonesho ya kazi za wasanii.Ameshuhudia michoro mbalimbali ya wasanii mahiri ambao wamebobea katika sanaa ya uchoraji wakiwamo Paul Ndunguru, Masoud Kibwana, Mwandale “Big Mama” Mwanyekwa, Cloud Chatanda, Amani Abeid, Safina Kimbokota, Fred Halla, Nathan Mpangala, and others.

Pamoja na yote hayo Dk.Mwakyembe amefanya mazungumzo na Ofisa wa Sanaa ya michezo wa Nafasi Kwame Mchauru.Akizungumza na wajumbe wa bodi, wasimamizi, wafanyakazi na Nafasi Art Space Dk.Mwakyembe amewahakikishia kuwasaidia katika kuendeleza sanaa nchini.Pia amewapongeza Nafasi kwa mchango ambao wanautoa katika kuendeleza sanaa na kwamba ushirikiano na uhusiano kati ya Wizara na Nafasi utaendelea kukua na kuimarika siku hadi siku.

Pia Dk.Mwakyembe amesema amefurahishwa na Nafasi katika kukuza utamaduni na utambulisho wa taifa wa Tanzania, kusaidia wasanii vijana katika elimu zao na maendeleo, na kufanya kazi pamoja kutumia sanaa kama chombo cha kuboresha jamii.



Waziri wa Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo Dk.Harson Mwakyembe akiangalia moja ya kazi ya uchongaji vinyago iliyofanywa na wasanii waliopo Nafaso Art Space baada ya kuwatembelea kwa lengo la kuwapongeza kwa kutimiza miaka 10

RAIS DKT SHEIN AKUTANA NA UJUMBE WA MASPIKA WA MABUNGE NCHI ZA JUMUIYA YA MADOLA BARANI AFRICA.

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge la Rwanda Mhe.Edda Mukabagwiza akiwa miongoni mwa ujumbe wa Maspika wa Mabunge ya Nchi  za Jumuiya ya Madola Barani Afrika walipofika Ikulu Mjini Zanziobar leo
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Ujumbe wa  Maspika wa Mabunge ya Nchi  za Jumuiya ya Madola Barani Afrika unaoongozwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia Mwenyekiti wa Maspika kutoka Nchi za Wanachama wa Jumuiya ya Madola Mhe.Job Ndugai (wa pili kulia),walipofika Ikulu Mjini Zanziobar leo,
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed SheiN akibadilishana mawazo na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia Mwenyekiti wa Maspika kutoka Nchi za Wanachama wa Jumuiya ya Madola Mhe.Job Ndugai wakati alipoongoza ujumbe wa Maspika wa Mabunge ya Nchi  za Jumuiya ya Madola Barani Afrika walipofika Ikulu Mjini Zanziobar leo,[Picha na Ikulu.] 04/10/2018.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiagana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia Mwenyekiti wa Maspika kutoka Nchi za Wanachama wa Jumuiya ya Madola Mhe.Job Ndugai baada ya mazungumzo na Ujumbe wa  Maspika wa Mabunge ya Nchi  za Jumuiya ya Madola Barani Afrika,ulipofika Ikulu Mjini Zanziobar leo,[Picha na Ikulu.] 04/10/2018.
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images